Usiyaone matatizo ya kiuchumi kama Kikwazo – Mwl Mwakasege

mwakasege

Shalom,

Tunajua unataka uwe na uchumi mzuri. Hii ni kwa mwanadamu yeyote bila kujali mahali alipo,awe anafanya kazi au hata kama hafanyi kazi.

Kuanzia leo na siku kadhaa zitakazofuata,tutajitahidi kukushirikisha misingi kadhaa iliyomo katika biblia,ambayo tunaamini itakusaidia uwe na uchumi mzuri. Msingi wa kwanza ni huu:Badilika unavyoamini juu ya uchumi,utabadilika unvyosema juu ya uchumi,na hali yako ya uchumi itabadilika vivyo hivyo.

Tunaamini ya kuwa; mtu akibadilika anavyoamini atabadilika pia anavyosema;na hali yake ya maisha itabadilika vivyo hivyo.
Jambo hili tunalipata tunaposoma kitabu cha Mithali 23:7 ya kuwa; “Maana aonavyo nafsini mwake,ndivyo alivyo.”
Tafsiri nyingine ya mstari huu inasema;”maana awazavyo nafsini mwake ndivyo alivyo.” Tasfiri nyingine ya mstari huu inasema;”maana aaminivyo nafsini mwake,ndivyo alivyo.” Mstari huu unataka tujue ya kuwa maisha ya mtu alivyo ni matokeo ya awazavyo au aaminivyo au afikirivyo(mindset), nafsini mwake.

Ulivyo kimaisha kwa nje ni matokeo ya msimamo wako wa kimawazo ndani yako. Kwa ulivyo kiuchumi,ni matokeo ya msimamo wako kimawazo(mindset),ulionao ndani yako juu ya uchumi.

Wapelelezi 10 walileta habari mbaya walipotoka kuipeleleza Kaanani,kwa vile waliamini mioyoni mwao ya kuwa “majitu” waliyoyakuta Kaanani yalikuwa kikwazo na pingamizi kwao.Wapelelezi wawili (Yoshua na Kalebu),waliona hayo “majitu” pia lakini mioyoni mwao waliamini tofauti. hawakuyaona majitu kama kikwazo bali waliyaona kama fursa kwao ya kutatua tatizo hilo ili waweze kula.

Soma habari hii katika kitabu cha hesabu 13:32,33 na Hesabu 14:9,28
Matokeo ya tofauti hizo kuwaza na kuamini,kuliamua hatma ya baadaye ya uchumi na maisha yao.Wapelelezi 10 waliishia kulalamika na kushindwa kwenda Kaanani. Na wale wawili (Yoshua na Kalebu) waliweza kwenda Kaanani na wakawa na maisha mazuri.

Wazo tunalokufikirisha siku hii ya leo ni kwamba;Usiyaone matatizo ya kiuchumi yanayokuzunguka kama kikwazo,bali yaone fursa ya kuyatatua ili iwe njia mojawapo ya kuongeza kipato chako. Kumbuka wanaolalamika wanapoona matatizo,wanajipofusha fikra szao wasiona fursa za kimaendeleo katika matatizo hayo.

Mungu awabariki.

Christopher & Diana Mwakasege(Mana Ministry)

Advertisements

26 thoughts on “Usiyaone matatizo ya kiuchumi kama Kikwazo – Mwl Mwakasege

 1. Neno la Mungu ni taa na mwanga maishani mwetu. Na tubadilifikra zetu vijana tuuone ushindi. Amen

 2. (aonavyo nafsini mwake ndivyo alivyo) ninapo soma ujumbe ambayo Mungu Baba yetu anayoweka ndani mwako ; roho yangu inakuwa inajazwa matumaini na kusadiki sana maneno ya Mungu. kwa iyo nina omba iyo upako kwa Mungu mara mbili.

 3. Bwana asifiwe napenda sana Mungu anisidie nimjue vizuri nisianguke kwemye dhambi naombeni mniweke kwemye maombi

 4. Mungu wa Mbinguni akubariki kwa somo njema limenitoa sehemu moja kwenda sehemu nyingine ya juu kabisa.

 5. Hakika Mungu ni mwema sana kwani hili neno limenipa nguvu sana yakutoka katika mawazo ya kujiwazia vibaya kila wakati lakini kwa sasa namshukuru Mungu nimepata mwanga wa ushindi nimetambua kuwa yote yawezekana ukimtegemea Mungu pekee ubarikiwe sana mwalimu

 6. Ameni !!!!!!!!!!!!!!!!hii ni siri ya ajabu sana,nilikua na maswali mengi sana kuhusu uchumi wangu,asante kwa sehemu Mungu ameongea na mimi kupitia wewe,Barikiwa sana Baba,nikipata muendelezo wake ingekuwa vizuri,Huduma njema!

 7. asante mtumishi wa MUNGU kwa kunifikishia ujumbe huu.natumaini nitaufanyia kazi na MUNGU aliyembinguni atatenda jambo katika uchumi wa family na kanisa kiujumla

 8. Soma hili ni la baraka sana kwangu Mungu akutie nguvu mtumishi nami anisaidie kuweka kwenye matendo ninacho jifuza humu!

 9. nimebarikiwa naomba Mungu aniongoze vyema na kunipa hekima zaidi katika uchumi wangu -ubarikiwa mtumishi wa Bwana

 10. somo ni zuri sana linatusaidia litatusaidia sana vijana wa Tanzania hasa tunaohitimu vyuo vikuu kupata maarifa ya kutatua changamoto zinazotukabili.

 11. Amen,
  somo limenijenga na kuzifungua fikra zangu. Kwa hakika nasubili ukurasa ufuatao. Ubarikiwe mtumishi

 12. kwel mwalimu kufikiri fikiri sana vikwazo na pupa kunapunguza uwezo wa kuona mbali.na spid ya mafanikio

 13. Katika walimu wanaonsaidia na kulisha kiroho changu we we ni mmoja wao ubarikiwe MTU wa Mungu nasubiri page nyingine

 14. amen mtumishi mwakasege: somo limeishia pazuri maana ni mahali ambapo nilitaka sasa nikae nianze kusoma vizuri nashangaa limeisha bado nina maswali mtumishi

 15. MAFUNDISHO NI MAZURI, NA NI KWELI KWAMBA MAFANIKIO KATIKA MASHAKA HAYAPO HATA KIDOGO. DAUDI KWA SAULI ALIONESHA UJASILI NA IMANI, AKAISHI HATA KUWA MFALME. OLE WEWE ULIYE KAMA SAULI KWA DAUDI, MAANA NEEMA YA SAULI SIO YA WEWE. USHINDI UPO KWANI TULIYENAYE NI MSHINDI.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s