Hii ni nini?

msaada

Watu wa Mungu, hii Dunia ina mambo mazito na ya ajabu sana. Mpaka nimeamua kuwashirikisha jambo hili maana yake ninahitaji msaada wa Maombi kutoka kwenu nikiamini katika Kanisa hili mpo Watumishi wenye vipawa mbalimbali mlivyokirimiwa na Roho Mtakatifu.

Ninaye mdogo wangu wa kike ambaye katika familia yetu ni wa Mwisho kuzaliwa. Katika historia ya maisha yake toka ameanza shule ya msingi mpaka kidato cha nne hakuwahi kuwa na tatizo lolote na alikuwa akimpenda sana Mungu.Zaidi ya kumpenda Mungu niligundua ndani yake kulikuwa na karama za Kipekee na za tofauti sana.

KUANZA KWA TATIZO.

Tatizo lake lilikuja kumuanza baada ya kuingia mwaka wa kwanza katika chuo cha IFM.Tatizo hili lilimpelekea mpaka aka – Discontinue chuo hicho kabla ya kujiunga tena upya katika Chuo cha St,Jordan Morogoro ambapo yupo mpaka sasa.

TATIZO LIKO NAMNA GANI?

Ni vigumu kueleza kwa ufasaha kinachomsibu huyu Dada,kutokana na kwamba yeye mwenyewe anafika sehemu anashindwa aeleze kwa namna gani ili aweze kueleweka.Ila kuna baadhi ya vitu katika maelezo yake mengi ambayo amekuwa akinipa nilijaribu kuvidaka.

1.) Anasema imekuwa ikimtokea mara nyingine akiwa njiani akitembea anajikuta anakutana na Mtu mwingine mwenye sura na mfano wake yeye.Kwa maana nyingine wanakuwa wapo wawili wakitazamana na kushangaana each other.

2.) Experience nyingine aliyonayo, ni kwamba inaweza ikatokea akamfikiria mnyama au ndege fulani, na ghafla akajikuta amebadilika kuwa huyo Mnyama/ndege (Siwezi kuelezea kwa namna gani ila ndio maelezo ambayo amenipatia)

3.) Pia mara nyingine anaweza kuwa anatembea barabarani then akijiangalia anajikuta nyama zote za mwili zimemwacha na Mishipa ya damu ikionekana wazi wazi (Ni hali ambayo inamuogopesha sana sana ikimtokea)

Hizo ni baadhi tu, ila ni mauza uza mengi sana ambayo amekuwa akikutana nayo na anafikia sehemu kushindwa kuelewa yupo katika ulimwengu upi.

Yupo ndugu yangu ambaye alimpeleka kwa Madaktari wa Psychology, na wengine wa akili, wapo ambao walisema tatizo lake ni la ugonjwa unaitwa BIPOLA, but toka kipindi chote hicho dawa alizopewa hazijamsaidia chochote na yeye anasema anaendelea kuteseka. Wapo baadhi ya madaktari walikiri kuwa hilo tatizo kwao ni geni na walikiri kuwa Option iliyobakia ni maombi tu.

Kwa kweli dada yangu huyu toka tatizo hilo limuanze ni kama moyo wake umefungwa kabisa, ukaribu na Mungu haupo tena. Kuna kipindi alishawahi niambia kuwa akilala amekuwa akijikuta yupo na waarabu wakimuongelesha kiarabu. Nakumbuka kipindi hicho baada ya kunieleza hivyo nilichukua hatua ya kumpeleka kwenye maombi na kweli mapepo yalidhihirika yakatoka. Ila tatizo hilo nililolieleza hapo juu ndio linanipa shida kuelewa ni nini kinamsibu huyu dada. Maana linampelekea sometimes anakuwa kama mtu anayetaka kuchanganyikiwa.. In short anasoma chuo katika mazingira Magumu sana na hana uhakika kama atafanikiwa kumaliza salama.

Please, Yeyote ambaye anajua amekirimiwa karama za Kiroho kuweza kumfungua mtu mwenye tatizo kama hili au yeyote anayemjua Mtumishi anayeweza kuwa na mzigo wa kumfungua mtu katika tatizo la namna tuwasiliane.

– Daniel J-
Advertisements

41 thoughts on “Hii ni nini?

 1. pole ndugu Daniel pia mpe mdogo ako polen
  swala la kufunguliwa ni mhitaji kwamba ameandaje moyo wake,maana ukiangalia yesu alipokuwa anaponya watu hakuponya tuu bali anaangalia iman ya mtu mwenyewe,na injili tulionao kwa sasa ni injili ya Yesu ya yeye kushnda mauti
  akatukabidhi ufunguo wa kufungua na kufunga math 18:18 lakin pamoja na hayo andalio la moyo ni wa mwanadamu tafsiri yake ni kwamba umejaanda kupona au unamashaka(unaamini) bali jawabu mungu pekee ndo anaetoa, maana yake ukisha amini ndipo miujiza yako yanatokea ingawaje ametupa mamlaka luka 10:19

  mpendwa daniel mungu pekee ndo anaweza kutoa majibu ya hitaji lakin ukwali ni kwamba kutakuwa na mtu aliendaliwa kwa ajili ya mujiliza ya kila mtu utajuaje?

  Rud magotin muulize Mungu birika lake litakuwa wapi nae Mungu atakupa maelekezo
  Yesu atusaidie sana atupe na nguvu zaidi

  mbarikiwe wote

 2. kissa,

  Usijali.tupo pamoja. Tufanye kesho jumatano, tar 30/04/14. Mimi nimekubali. Hebu kesho turushe makombora ya maombi kwa rafiki yetu huyo.

  Hata mimi nilitegemea mtoa mada,angekuwa wa kwanza kuchagua siku ya mfungo ila yupo kimya. Sijui hajaona kinachoendelea hapa? AU hatuamini?

  kissa tulianzishe, unajua kuna wakati Mungu ujibu maombi ya watu wake yanayoelekezwa kwa wenye shida hata km walengwa hao hawajui kinachoendelea. Pia haina haja ya kuwa nae pamoja ili Mungu atende. Yatamfikia huko huko alipo. Maombi upenya sehemu isiyopenyeka, na usafiri kwa kasi na umbali usiofikika kibinadamu.

  Twende kazi, kesho mfungo. Hakuna kula kwa ajili ya mwenzetu uyo.

  “IT BEGIN WITH YOU”

 3. Mbona kimya watumishi wa Mungu tupange basi siku ya maombi wakati ulio kubalika ni sasa.

 4. sawa kabisa tufanye hivyo j5 au cku yoyote tujulishane ili tuweze kufunga na kuomba kwaajili ya hili saula.mimi niko tayari

 5. Tomas Majinge,

  Ubarikiwe.Tunahitaji Imani na Ujasiri km wako. Nakuunga mkono mtumishi. Kwa kuwa km hatutafanya ivyo-kumsaidia uyo dada yetu, uwepo wetu hapa SG ni bure. Tupange siku ya maombi ya kufunga. Km itawafaa wote tufanye Jumatano ijayo tar 30/04/14. Ni mapendekezo yangu tunaweza kupanga siku nyingne.

  Tuchukue hatua ya imani wanaSG.

 6. Kabla ya yote ningependa mbali na kutoa ushauri,ningependa wanna strict gospel kama kuna waliotayari kumsaidia ndugu yet Daniel .j naomba tuungane kuliombea swala hili kwani tatizo la ndugu yetu lina tuhitaji.Tukubaliane kuombea ukombozi wa dada huyu kwa maombi ya kufunga.Pili napenda kukutia moyo ndugu Daniel.j kuwa shida ya Dada yako inawezekana kwisha.navyoona mimi shida kubwa iliyopo ni kuwa ndugu yako ametengwa na Mungu ama wa hofu au wa kukata tamaa. Ninakushauri usikbilie kumchukua yeye kama yeye kwanza ukakimbilia kwenye huduma za ukombozi .Unachotakiwa kufanya ni tafuta kikundi cha maombi uwashirikishe shida hii anatakiwa kwanza arudi katika hali ya kumpenda Mungu no hatua ya kwanza ya kufunguliwa
  Ombeeni jambo hili kwanza

  Akisha funguliwa katika hili ndipo utamshauri na kumpeleka kwa maombi ya ukombozi huko atafanyiwa maombezi.Nionavyo mimi kuna majini au mapepo ama yanamfuatilia au pengine yamesha mwingia na yamefanya mkataba naye kwa vitisho
  Atakavyoweza kuwa amefunguliwa akarudi kwenye kumpenda Mungu atafunguka kuweza kueleza yote anayoyaona au sikia au kutana nayo.hii ni sehemu muhimu sana katika huduma ya kumweka huru MTU na pia ni hakikisho pekee LA tatizo kutojirudia tena.Tokea hapo ndugu yako ataweza kumpa YESU maisha yake na ataweza kutembea kwa ushindi
  Naomba unitumie jina lake nitakuwa nikimwombea.namba Yangu ya simu ni 0754865366.barikiwa

 7. poleni sana Soma Isaya 43:26 Anasema Unikumbushe natuhojiane ukisoma katoka Warmi 8:19 kwa maana viumbe vyote vinatazamia kwa shauku nyingi: toa neno *VIUMBE* wekaneno *UHAI* Na ukidoma Warumi 8:11 Lakini ikiwa Roho wake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kroisto Yesu katika wafu ataihuisha na miiliyenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu. Soma kwa makini huo ndo ushindi

 8. lwembe,

  Asalaam alykum,

  Inawezekana hoja uliyoiibua, wivu wa kihuduma/utumishi/madhehebu ina ukweli kwa upande mmoja ila pia hoja za wapendwa, kucrush hoja ya kumwambia mwenye matatizo, “njoo huku.., nenda kule kwa…” nayo pia ina ukweli wake kwa upande mwngne.ni mtazamo wangu km ifuatavyo,

  1.Bila shaka hoja yako imejengeka kweny ukweli kuwa Mungu ameweka wengne kuwa mitume,wengne manabii,wengne huduma za uponyaji,miujiza n.k. Kama apendavyo Roho.

  -Hata hivyo tujiulize kuwa Je, Mungu ni maskini ht agawe karama hizi kwa wachache tu?? je, inaleta picha kuwa muanzisha mada, ndg Daniel J, kuwa ktk makanisa anayoyafahamu karibu nae, au alipo uyo dada mgonjwa kuwa hakuna mwny karama za hao watumishi wenye majina makubwa ht mpaka aelekezwe,au ht wakati mwingne asafiri umbali mrefu na kwa gharama kubwa kufuata izo huduma. Kwangu haileti picha, km hakuna wenye karama hizo kwny makanisa ya karibu,basi ni bora yakafungwa tu.

  -ktk makanisa yote nadhani Mungu amegawa karama hizo kwa ajili ya huduma. Kinachotokea leo kuna, i)wapo lakini hawavumi îi)wenye karama hizo lakini hawajijui,hawazitumii,au wanazitumia kidogo sana. Kama ujuavyo karama zisipotumika hatimaye ufa! Ninachotaka kukwambia ni kuwa wapo wakina T.B.joshua wengi tu ikiwa watu watasimama ktk huduma na kuzitumia karama zao. Kinachotakiwa tu ni Imani tu km punje ya haradali

  2.mimi nadhani siku hz watu wanafuata majina ya watumishi badala ya kufuata huduma. Km mtu angetaka huduma isingekuwa vigumu kuipata kwa watumishi walio karibu nae badala ya hao wenye majina makubwa.

  3.Hali hii ya kufuata majina ya watumishi badala ya huduma naweza kuifananisha na Paulo alipowakemea watu, kwani ni wanajiita , “sisi ni wa Paulo, Sisi niwa Apolo…” ambapo alivunja kiambaza icho kwa kuwaelekeza kwa Yesu.

  4.Pia Yesu aliwalaumu sana wanafunzi wake kwa kushindwa kuwahudumia wagonjwa kwa kukosa kwao Imani ktk huduma.na wanafunzi walikiri kutokuweza/kuamini kwao.

  Hivyo rafiki,hoja za wapendwa binafsi naziangalia kwny angle iyo sijui wewe.

 9. Nashukuru sana kwa Mawazo yenu Wapendwa woote mliochangia hapo Juu. Mungu awabariki sana, na katika kuchambua maoni yote hapo juu, kwa kuwa niko mbali na muhusika mwenyewe, kwa kuanza nitawatafuta hao walio karibu naye kwanza,yaani CASFETA wakae nae chini kwanza,wamuhoji pia waone wanaanzia wapi kumpa huduma ya kiroho.

  Kuna ambao wameuliza baadhi ya maswali.Kwa mfano kuna mtu ameuliza Je, amempa Bwana Yesu maisha yake?

  – Katika maelezo yangu nimeeleza kuwa alikuwa akimpenda sana Mungu hapo awali. Sidhani kama mtu anaweza akampenda Mungu ki kweli kweli bila kuokoka.

  – Kuhusu kufanyiwa sala ya Toba, kama nilivyoeleza awali ni kwamba kwa sasa Moyo wake unakuwa kama umefungwa. Kuna utofauti mkubwa uliopo, kwa jinsi alivyo sasa na alivyokuwa zamani. Kwa sasa anakuwa ni mzito sana kusikia habari za Mungu (Ninavyoona hapa,Kufunguliwa kunahitajika kwanza).

  Mungu Awabariki!!
  Daniel J.

 10. i feel sor 4 her bt hakuna linaloshindikana kwa MUNGU aendelee kuwa na imani thn acache maombi na maombozi ktk makanisa ya kiroho

 11. Wapendwa, Sungura, Milinga, Tumaini, Seleli na Siyi,

  Kimsingi maelezo yenu yanayozikataa Huduma kwa kisingizio cha kuinuliwa watumishi badala ya Kristo, yamejengeka ktk ushindani mlionao wenye wivu wa kuyalinda makusanyiko yenu kuliko Fundisho la kiBiblia!!!

  Na kama msukumumo wenu hautokani na hayo niliyoyasema hapo juu, basi mtakuwa bado ni watoto wachanga ktk Imani, na hivyo mnapaswa kupuuzwa kwa hizo kauli zenu!

  Ktk huduma zote zinazofahamika kwa masuala ya kuombea wagonjwa au kukemea mapepo na utajirisho, ukiacha huduma ya Siloamu, huduma nyinginezo zote huyafanya mambo hayo kwa jina la Yesu! Vipawa hivyo walivyonavyo watumishi hao hutumika ktk jinsi ya Fundisho la Biblia kama Injili inavyoagiza. Labda mkitujuza tofauti kuhusu hizo huduma mnazoziona zinajitukuza, labda wagonjwa wakiponeshwa kwa jina la nabii au mtume au askofu nk, basi hao wapaswa kuepukwa kwani hawana tofauti na waganga wa kienyeji!

  Lakini kutukuzwa mnakokulalamikia ninyi si ktk namna hiyo, bali umaarufu wa majina ya watumishi ndio unao wakwaza. Na kwa vile kukwazwa kwenu ni kwa kinafiki, ndio kumewaongoza kuleta malalamiko yasiyoendana na Injili licha ya kuonekana yanastahili!

  Kulingana na malalamiko yenu, mlipaswa mtuoneshe japo mtumishi mmoja aliyemtukuza Kristo, kiasi kwamba jina la huyo mtumishi likafutika na kuwa replaced na jina Yesu!

  Vitabu vyote ktk Biblia, HAKUNA hata kimoja kilichopewa jina la Yesu, hata cha Ufunuo kina jina la Yohana!!!! Basi tusemeje, kwamba hao watumishi wamejitukuza?

  Maandiko yanatufundisha kwamba Kristo atakuwa ndani yetu akijidhihirisha, tena akasema dunia haitalitambua hilo. Je, nanyi ndugu zangu hamlitambui hilo? Hamjaula mwili wake wala kuinywa Damu yake? 
  “Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake. (YN. 6:56)
  Au hamuujui huo mwili wake kuwa ni nini?
  “Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya Neno la uzima; (1 YOH. 1:1 )!!!!
  Je, kujulikana kwa Paulo, ktk jinsi hiyo aliyotukuka, ndio tuseme amejitukuza kuliko Bwana wake? Tazama anachokikiri hapa, “… alipoona vema kumdhihirisha Mwanawe ndani yangu, ili niwahubiri Mataifa habari zake; …” (GAL. 1:16)

  Kristo anapojidhihirisha ndani ya watumishi wake huwa hayaondoi majina yao kwa ushuhuda, maana hao ni mali yake, amewanunua kwa Damu yake na sasa amewadai kutoka mikono ya Shetani aliyekuwa akiwashikilia! Ukisikia mpeleke mgonjwa wako kwa nabii Seleli, kwa watu wa dunia, kwao jambo hilo huwa ni sawa na umaarufu wa mganga wa kienyeji, nao huja kwa imani hiyo wakitegemea kupokea kutoka kwa huyo nabii; lakini kwa wakristo ni tofauti, wao humfuata huyo ktk kuutafuta udhihirisho wa Kristo; ndipo wangehangaika kwenda kwenye huduma hii na ile ili tu wamfikie huyo mwenye kumdhihirisha Kristo kwa uhakika; wakiitafuta dalili ya Kristo ndani ya mtumishi (2 KOR. 13:3)!

  Au ninyi mnapomwelekeza mwenye shida kama hii iliyomfika ndg yetu huyu, huwa mnamuelekezaje hadi awafikie? Mnamwambia, panda basi la kawe ushukie Biafra utaona ubao umeandikwa kanisa la Yesu?? Au muhudumu wenu anaitwa Yesu Kristo??? Au unamwambia aje Kanisa la Wasabato wa Adventist? Hilo ndilo jina la Yesu?? Au Karismatiki, au TAG au EAGT au Kwa Mwakasege nk haya ndio Yesu?

  Mtu anapomwelekeza mwingine afike anapoweza kusaidiwa, ni lazima mtambue kwa kiwango chake kama ambavyo nanyi mlipo, hapo ndipo kila mmoja wetu anaamini kwamba Kristo anadhihirishwa, na hivyo kuwa na ujasiri wa kumuelekeza nduguye aliye ktk shida!!!

  Kristo hudhihirika ndani ya watumishi wake; alikuwa ndani ya Petro, Paulo na mitume wote, akijidhihirisha, “Kazi hizi nizifanyazo …” Kama ambavyo leo hii yupo tena ndani ya watumishi wake akiendelea kuzifanya kazi hizo. Maana imeandikwa kwamba ishara hizo wanazozifanya zitaambatana na waaminio, hao wenye kuula Mwili wake na kuinywa Damu yake; ndipo wakiwa ni hao, utukufu wote humrudia Kristo kwa mkristo na kwa mpagani, yeye humtukuza mtumishi; nalo jambo hilo lastahili kuwa hivyo ili kuzibaini tofauti, mafuta yakijitenga na maji!!!

  Mimi niliwategemea mje na hoja safi za kuzibainisha huduma alizoelekezwa, mtupe hayo mapungufu mnayoyajua ambayo yanauondoa uwezekano wa Kristo kudhihirishwa ktk huduma hizo. Angalieni, mimi ninamkataza asiende Siloamu kwa sababu huduma hiyo inakiri kwamba Shetani alikwisha kufa tangu 2008; na kwa mtazamo wa kawaida ktk nuru ya Maandiko inaonesha kuwa huyo dada atakuwa na shida ya pepo, basi kama unaambiwa huyo anayekusumbua alikwisha kufa ilhali anajidhihirisha kwako, hilo linapaswa likuoneshe kuwa ukikanyaga mguu wako ktk huduma hiyo, utaongezewa na mapepo ya dini kama hayo yanayojitambulisha kuwa yenyewe ni “Adamu wa pili Mungu wa majeshi”!! Huku ndiko kujiinua. Haya nanyi tupeni sababu kuhusu hizo huduma!!!

  Mbarikiwe!!!

 12. Yesu Ndo Dawa. Mi Napenda Kwanza Ampokee Yesu , Maana Chanzo Cha Mapepo Mengi Kuwaingia Watu Ni Dhambi, Ktk Uzoefu Wa Huduma Nimegundua Wengi Wanaweza Kuombewa Lkn Kama Hajampokea Yesu Tatizo Linarudi. Kwa Hiyo Aokoke Kwanza Na Akae Chini Ya Mafundisho Ya Kweli Hilo Tatizo Dogo. Edwin Seleli

 13. Nimekuona Seleli,
  Nimekuona Tumaini,
  Nimekuona Milinga.

  Dini inatesa sana mindset za watu!

 14. Sungura, Tumain and Milinga,

  Ndio maana mwanzo nilisema juu kule ivi..”’, Tafadhari sana, tusitukuze/pamba sana directly au indirectly, technically or tactfully, madhehebu/dini/mtu fulani, iyo haifai hata kidogo..Yeye hana budi kupungua ili Yesu aongezeke na kwamba kwa kila neno na tendo, tufanyayo, acha Yesu ainuliwe na awe focus ya maombi na hamu zetu kutaka afunguliwe”

  Mambo ya kusema sijui mlete kwa fulani au yule, ni utoto na udhihirisho wa effects za kukaliwa kama miungu wadogo na viongozi wa dini/kiroho, mbovu sana iyo kitu na tendency.

  Press on

 15. Daaah!thnx Sungura& Millinga mmenena vyema!inashangaza na kuckitisha kila m2 njoo kwa flani njoo kwa flani!Mimi nilitegemea kuckia njoo kwa Yesu bt c njoo kwa flani!hebu wapendwa 2muinue Yesu badala ya kuwainua wa2 na madhehebu ye2!kwanza kila m2 ana haki sawa mbele za Mungu!Ukiwa kama mtoto wa Mungu unahaki zote mbele za Baba yako ndiyo maana anasema ombeni neno lolote kwa jina la Yesu ata2patia!so hakuna aliyenahaki zaidi mbele za Mungu kuliko mwenzake!wote 2nahaki sawa!hata wewe unahaki sawa za kuomba mbele za Mungu akakuckia na kujibu sawa sawa na haja ya moyo wako!hii mambo njoo kwe2,nenda kwa flani hii mambo ni ku2kuzana badala ya kumpa cfa na u2kufu kamanda mwenyewe JESUS.

 16. Mpendwa Dan,

  Poleni kwa changamoto hiyo. Pamoja na yote hayo uliyoshauriwa hapo juu, nukuu ya maneno ya Yesu naomba ikusadie. Nayo ni: “……..MAMBO MENGINE …..HAYAWEZEKANI ILA KWA KUFUNGA NA KUOMBA….”

  Usiweke Imani kwa watu wala mtu awaye yote hapa duniani. Maandiko yanasema, “………..Amelaaniwa amtegemeaye mwanadamu…….”

  Usiende kwa mtu wala kanisa au huduma yoyote bali nenda kwa Yesu kwa Imani. Maandiko yanasema, “…..ukiwa na imani kama punche ya ulezi utauambia mlima huo ung’oke nao utatii…….”

  Siyo kwamba nakukataza kwenda kwenye kanisa fulani au kwa mtu fulani kama ulivyoshauriwa hapo juu. Mimi ninakushauri hasa uweke tumaini lako kwa Kristo Yesu. Wahubiri hawa wanaovuma hapa Bongo ni kama Punda tu aliyembeba Yesu siku ile anaingia Yerusalem. Je, watu walimtukuza Punda au walimtukuza Mpanda Punda? Je, kama Yesu angekuwa hajapanda mwanapunda, huyo punda angetandikiwa khanga na matawi ya miti? No!!

  Kwa hiyo mtazame Yesu tu naye atamponya dada yako. Funga na kuomba kwa Imani. Usiende kanisa lolote linalosifika hapa Bongo kama Roho wa Mungu hajakusukuma kufanya hivyo. Omba kwanza upate mwelekeo wa Imani na RM atakusaidia kukuelekeza ni wapi Mungu ameweka mlango wa kutokea.
  Ubarikiwe.

 17. E bwana eh,

  Hebu tuacheni kutumikia madhehebu. Yesu kama ni Yesu kweli ni Yesu popote pale. Siyo lazima kwenye dhehebu lenu.

  Kila mtu ‘njoo kwetu, nenda kwa fulani, nenda kule’ kwani ni wapi ambapo Yesu wa kweli hafanyi kazi kama yupo?

  Habari ndo hiyo!

 18. Fika ktk hema la kuabudia la NGURUMO YA UPAKO ,kawe utakutana na watumishi watakuhudumia na tatizo lako litakwisha km co kutoweka kabisa.

 19. KAMA UPO DAR MPELEKE ZOE MINISTRIES TABATA SEGEREA UKIFIKA SEGEREA STAND WAULIZE HATA DEREVA BODABODA WANAPAFAHAMU NI HUDUMA YENYE MIUJIZA YA KUTISHA ISIYOFIKIRIKA KWA MACHO YA KIBINADAMU ATAFANYIWA MAOMBI YA UKOMBOZI

 20. niliwai kusikia kuhusu tatizo hili mara nyingi huwa kuna watu wanautaaram wa kutengeneza majini yenye sura na maumbile kama binaadam kabisa.lakini dawa yake ni kufanyiwa ukombozi na yeye kuamini kwamba yupo mungu mwenye uweza wa kutoa ivo vi2.

 21. shetan mwongo sana lakin amewekwa chini ya miguu yetu hivyo tunamamlaka dhidi yake .

 22. Bwana Yesu asifiwe. Huyo dada atakuwa ana jinni mahaba ndio anatabia hiyo yakuvaa sura za watu. Nakuomba umpeleke Arusha Radio Safina atafunguliwa na sasaivi watumishi wa hapo wanafundisha kuhusu somo hili la jinni mahaba.www.radiosafina.org

 23. Bwana yesu asifiwe. Kwa upeo wangu mdogo hayo ni mapepo hakuna kingine. Namshauri mpeleke kwa mzee wa upako kwa maombezi au kanisa lolote la kiroho kwa ajili ya maombezi. Naamini atafunguliwa.

  Sent from Samsung Mobile

 24. Pole sana ni mambo ya ajabu tena yasiyofikrika, na kihalisia si jambo dogo, ila ukweli MUNGU MWENYEZI yupo, na mtumainie yeye. Kama hatua zote ulizoshauliwa hapo juu tatizo halitaisha mwone pia T B JOSHUA wa Nigeria. Tazama Emmanuel TV

 25. Kama yuko hapo chuoni aonane na hao CASFETA, maana itakuwa ni rahisi sana kwao kumsaidia coz wako nae hapo.

  Na uzuri wametoa namba zao hapo juu.

  First aid ya kiroho inatakiwa kuanza hivyo, hatua zingine zitafuata kama italazimika!

  Bless u!

 26. pole sana kwa hilo tatizo, ilaomba unipigie kwa namba hii ili nisaidie maana nimewahi kukutana mtu mwenye tatizo kama hilo na leo ni mzimna wa afya 0717577474, apostle Emanuel

 27. mh! jmn kna watu wana mapito! mpaka naogopa but Mungu wetu ni mkuu na muweza, km mpo Dar es salaam mpelekeni kwa pastor katunzi, nina iman atamsaidia… polen sn

 28. naomba mawasiliano yake,mimi nina vipindi vya dini vya radio hapa mbeya hivyvo watumishi ni wengi sana wanaweza kumsaidia ktk maombi.plz naitwa mbulinyingi.0713016203 nipigie

 29. Shalom, Luka 1:37 “kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu. Ndugu usiliangalie tatizo likaimeza nguvu ya Mungu ndani yako, yeye huwa hashindwi na jambo lolote. Tatizo la mdogo wako ni kwamba ameibiwa na kufungwa katika magereza za kipepo. Kama umeokoka na Yesu Kristo yu aishi ndani yako waweza mfanyia maombi na akafunguliwa kabisa. Soma Isaya 42:22 Roho Mtakatifu atakufunulia hiki nilichokiandika hapo juu.

 30. Daniel Pole, sana, Dada yetu so sorry plz.

  Pamoja na nia njema ya kutaka apone, tafadhari sana, tusitukuze/pamba sana directly au indirectly, technically or tactfully, madhehebu/dini/mtu fulani, iyo haifai hata kidogo.

  Tuwe na Mind ya Yohana Mbtz hii..Yeye hana budi kupungua ili Yesu aongezeke na kwamba kwa kila neno na tendo, tufanyayo, acha Yesu ainuliwe na awe focus ya maombi na hamu zetu kutaka afunguliwe.

  Press on

 31. Daaah!Pole sana bt mimi jibu langu simple!hakuna awaye yeyote duniani anayeza kutatua tatizo lake icpo kuwa kamanda mmoja 2 ambaye ni kamanda wa makamanda Jesus Christ.Yeye ndiyo kimbilio le2 haijalishi unamzigo kiac gani hata kama umeteswa namna gani just mkimbilie huyu kamanda wa makamanda Jesus!Nenda kwake ukiwa umenyoosha mikono juu ya kwamba umechoshwa na shida na taabu unazozipata na kumwamini Yeye ya kwamba ata2a mizigo uliyokuwa nayo na kufutilia mbali shida na taabu unazopitia!napita tu!

 32. Mtumishi pole sana kwa tatizo la mdogo wako ningependa kukuuliza je mdogo wako ameokoka?

 33. Daniel J,

  Pole rafiki kwa majanga,

  Wala usijiulize ni nini hiki? jibu lipo wazi. Nguvu za giza zimemtumikisha.

  -Hata hivyo hasihofu kwani, Msaada wake u katika Bwana, na Nguvu za kutoka mautini zina Yehova Bwana. Zab121:2, 68:20.

  Daniel, sio mpaka uelekezwe kwa mtu mwingne hata wewe unaweza kumrejesha uyo dada kwa Yesu. chukua hatua ya imani na Yesu atatenda.

  Au hata hapo Morogoro alipo, atafute wacha Mungu walipo na wa Muombee kwa Imani, na huko kumwombea kvampa afya.

  Pia, chukua muda kuhojiana nae kuwa kuna mkataba gani amefunga na shetani au kitu gani cha shetani alicho nacho maishani kwake! Dhambi. iridhi, ushirikina n.k. Na awe radhi kuikiri kwa jina na kutubu. Pia, mshauri adumu ktk sala na ibada pamoja na watakatifu wengne.

  Ni lazima awe na muda wa kufunga na kuomba, kwani “namna iyo haiwezekani bali kwa kufunga na kuomba.”Mathayo 17:21. Hivyo, siku utakayopanga kufunga na kuomba, shirikisha wanaSG tujumuike pamoja.

  Nami pia nawiwa kusema kuwa: Kwa jina la Yesu uyo binti amefunguliwa milele. Na aenende pamoja na Yesu nae asitende dhambi tena. amen.

  Pamoja.

 34. Poleni kwa mahangaiko hayo.Mwambie dada atutafute CASFETA hapa chuoni Jordan ili tuweze kumsaidia kwan Yesu hashndwi!
  YOTE YANAWEZEKANA

  0757405325 au 0658902515

 35. Poleni kwa shida hyo. Je huyo dada amemkabidhi Yesu maisha yake? Mwambie atutafute CASFETA hapa chuon Jordan tutamsaidia. unaweza kumpa hii no. 0757405325

 36. Ninakushauri kwenda naye katika Huduma yoyote ya Kiroho ambayo upo karibu nayo ili aweze kufanyiwa Ukombozi huyo mtu. Binafsi napendekeza Nenda naye Efatha Ministry kama upo Dar iwe MWENGE au kama upo Morogoro ni Nanenane. Nina uhakika atafunguliwa na atakuwa huru.
  Kinachohitajika kwake huyo si Uponyaji ni Ukombozi ndo maana nakusisitiza kumpeleka kwa mtumishi ambaye Neema ya Ukombozi amepewa na BWANA YESU. Maana kinachomtesa huyu mtu ni mapepo aina ya majini.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s