Ndoa Njema!

ndoanjema

Amani ya Bwana iwe nanyi enyi nyote, 

Imeaminika na hata kusisitizwa sana kua, ukipata Mke/Mume mwema tu au ukipatia Ndoa tu, yaani wewe mambo yako safi na umefanikiwa kweli kweli. Napenda ufundishe kitu hapa ili  tupeane maarifa na ufahamu wa mambo kwa Ukweli wa dhati kabisa wa Neno na pia  uhalisia wa maisha ya Ndoa kwa kujibu swali la kichwa cha mada na mengine yatakayoambatana na swali hili la msingi…’’’ JE NDOA NJEMA INATOKANA NA KITU KUPATA KITU CHEMA TU AU KUNA MENGINE YAAMBATANYO?

Kuna maandiko kadhaa hapa ya kuongoza Tafakari yako:

Imeandikwa: Mithali.18:22…Apataye MKE apata KITU CHEMA; Naye ajipatia kibali kwa Bwana

Imeandikwa: Mithali. 19:14  “Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; BALI MKE MWEMA NA MENYE BUSARA  mtu hupewa na BWANA”

Imeandikwa:  Mithali.14:1….Kila MWANAMKE ALIYE NA HEKIMA  hujenga nyumba yakeBali aliye MPUMBAVU huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.

Maswali ya nyongeza kwa lile la msingi la mada:

….Mke amesemwa ni Kitu Chema au Mwema, Je ni aina gani ya Mwanamke huyo? Yukoje? Anafanyaga nini spesheli kuzidi wengine mpaka awe chema/mwema? Ana nini yeye kwani?

….. Mke amesemwa kua anaweza kua Mwanamke mpumbavu, huyu naye flavors zake zikoje? Anafanya nini au ana tabia zipi hata aitwe mpumbavu maana anainyuka nyumba yake mwenyewe? Dah! Aisee! Yaani anaibamiza nyumba yake mwenyewe!

….Na mwenye Hekima na Busara anafanyaga nini naye? Ana tabia zipi practically? Vitu gani anafanyaga ukiviona live unajua aaa, ok, thas it gold over there?

….Na Pengine swali changamoto zaidi, Unajuaje Mke/Mume mwema/Mwenye hekima na busara?  Maana naona hakuna uwezekano wa kumfahamu kabla ya ndoa maana kufahamu fulani ana hekima/busara/mwema ni function ya time baada ya kuishi kwa pamoja!

…. Na kwa kua si rahisi kujua hekima/busara/uwema wake hadi muishi pamoja, sasa ktk kuchumbia inabidi tu kwenda kwa imani au kujilipua lolote na liwe maana sasa hufanyeji? Kwa kua ni mpaka uishi naye kwanza na hilo haliwezekani mpaka umuoe kwanza!

…. Au ktk Urafiki, Uchumba unawezajua kwa hakika u- mwema, mwenye hekima na busara? Kweli? Bila kuishi naye kwanza? Real? Hakuna ku-act ili uingie kati kwanza?

…..Vipi maswala ya shekeli, kukosa kipato, hayachangii kweli kufanya  au kutofanya uwema/hekima/busara ushari au yenyewe ndio chanzo tena cha vurumai?

 Press on.

Edwin Seleli

Advertisements

9 thoughts on “Ndoa Njema!

 1. Siyi,
  Sina hakika kama unjua hasa maana ya Dhambi.
  Nini tofauti kati ya dhambi na makosa?
  Yawezekana unampinga Lwembe bila kujua.

 2. Lwembe,
  Nashukuru kwa kunielewa kaka isipokuwa kwa maelezo yangtu ya mwisho yaliyokuchanganyeni. Napenda nikuulize kuwa, UNALIJUA NENO LA MUNGU KWA UJUMLA WAKE? Najaribu kukubashiria jibu kuwa, “HAPANA”. Sasa kama ni hapana, hebu mwangalie Daudi na Mathayo wanavyosema, “Ni nani awezaye kuyatambua makosa yake? Unitakase na mambo ya siri. Umzuie mtumishi wako asitende mambo ya kiburi, Yasinitawale mimi. Ndipo nitakapokuwa kamili, Nami nitakuwa safi, sina kosa lililo kubwa. Maneno ya kinywa changu, Na mawazo ya moyo wangu, Yapate kibali mbele zako, Ee Bwana, Mwamba wangu, na mwokozi wangu” – Zab. 19:12-14.
  ” Basi Yesu akijua mawazo yao, akawaambia, Kila ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, hufanyika ukiwa; tena mji au nyumba yo yote ikifitinika juu ya nafsi yake, haitasimama” -Matt 12:25.
  Kadiri unavyomjifunza Mungu kila saa, ndipo utakavyozidi kugundua hata baadhi ya udhaifu ambao hapo awali haukujua kuwa ni shida katika maisha yako ya Ukristo. Aidha, binadamu tuna asili ya dhambi (tumezaliwa na asili ya uovu) toka kwa wazazi wetu wa kwanza. Kwa sababu hiyo, ndiyo maana tuna vita (vya wema vs uovu) kuanzia na nafsi zetu wenyewe hadi wenzetu.
  Kuacha kwa dhambi moja, hufungua njia ya kuacha dhambi nyingine kama ilivyo kuruhusu kosa moja, huruhusu utendaji wa kosa lingine. Tunapomkaribia Mkristo aliye JUA LA HAKI, ndipo huwa uovu na makosa yetu huwa bayana zaidi kuliko mtu asiyejishughulisha kumtafuta au kumkaribia Mungu. Kwa mkristo wa kawaida anayetaka kwenda mbinguni, ni lazima aumie tu anapoona kuwa bado ana udhaifu wa hapa na pale kadri anavyomkaribia Mungu siku zote. Maumivu hayo, humfanya amlilie Mungu ili apewe nguvu ya kuyaacha hayo madhaifu. Na hii ndiyo stage ya SANCTIFICATION kama unakumbuka kaka Lwembe.
  Ubarikiwe nsana rafiki yangu.
  Kwa unyenyekevu wote
  Siyi nduguyo…

 3. edwini,

  Naona umekimbia bunge la EA (kwanini ndoa nyingi leo zina migogoro?) sasa umeingia kwenye Bunge la Katiba (ndoa njema). Yaani umebadili from hasi (-ve) to chanya (+ve).

  Km ulikuwa makini kwenye bunge la EA ungeshaelewa mengi ya uliyouliza hapa. Ulipaswa tu uyabadili ktk mtazamo chanya unaotaka. Hata hvyo usijali tutajuzana.

  Zingatia yafuatayo:
  1.mke mwema au ndoa njema ujengwa na kanuni tulizo kwambia kwny mada ileee! .Pia soma mithali 31.utajua anavyo act/flavor zake.
  -mke mpumbavu ni kinyume chake.mfano. biblia inasema ni mgomvi.

  2.pesa haina nafasi kwny ndoa njema. Kwani leo ipo kesho haipo. Wenye ndoa njema uzingatia- kuutafuta ufalme wa Mungu kwanza na mengne ni zidisho tu.-pia kumbuka Mungu alipo mpa adam na hawa ndoa njema hakuwapa pesa. Ila alikidhi tu mahitaji yao.

  …Itaendelea….

 4. Siyi,

  Ninakushukuru kwa maelezo mazuri uliyonipatia ukinielewesha jinsi ya kuufikia Utakatifu ili niwe nisiye tenda dhambi.

  Kwa kiasi kikubwa nimeyafuatilia hayo uliyonielekeza, kuanzia na Law 11:44 hadi Matt 6:33, nikajisikia Utakatifu kabisaaaa!!!

  Lakini niliporudi kumalizia kuyasoma maelezo yako, hilo fungu la mwisho, hapo unaponiambia,
  “”Maisha ya Mkristo yeyote, ni kujiona unapungua kila saa kadri unavyozidi kumkaribia Mungu. Pamoja na dhambi zetu tuzitendazo kila saa aidha kwa kusikia, kuona, kuwaza, kuhusika kabisa au dhambi za shirika …”
  Hapa ndipo umenivuruga tena, maana huko juu nilikuwa NISIYE TENDA DHAMBI, lakini huku mwisho unaniambia maisha yangu ni ya KUTENDA DHAMBI!!!

  Angalia ulichokifundisha huko nyuma hata kikanivutia: “”Mtu yeyote anayeishi sawasawa na sheria ya Mungu, yaani HATENDI DHAMBI…”” halafu linganisha na hiki ulichokitamatisha ktk kuufikia huo Utakatifu huko kuwa USIYE TENDA DHAMBI:
  “” Pamoja na dhambi zetu tuzitendazo kila saa…””

  Hebu nifafanulie zaidi hali hii mpya ambayo mtakatifu anatenda dhambi kila saa halafu anakuwa hatendi dhambi!!!

  Ubarikiwe!!!

 5. Seleli,
  Naona hukunielewa, ndiyo maana umeelea kaka. Niliandika nikiwa na uelewa wa mawazo hayo yote uliyojaribu kuyadokeza hapo! Niliandika Kikristo, kwa Mkristo ili usomwe na Mkristo. Kama Baba na Mama yangu walikuwa wana ndoa njema ilhali hawakuwa/au siyo Wakristo, hii ni kutokana na kwamba, Mungu aliwachukulia katika hali yao hiyo ya kutomjua, “Basi, zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hazioni; bali sasa anawaagiza watu wote wa kila mahali watubu” – Matendo ya Mitume 17:30. Kwa wewe uliye na ufahamu sasa wa kila kitu kumhusu Mungu, Mungu atakutendeeni accordingly. Ndiyo maana kuna hatari kubwa sana kwa mtu kuijua sheria ya Mungu na asiifuate kuliko asiyeijua kabisa. Ni rahisi kiasi hicho tu kaka.
  Ubarikiwe

 6. Lwembe
  Ha ha ha ha!! Nimefurahishwa sana na maelezo yako ya kifalsafa. Niende moja kwa moja kwenye swali lako la kutaka kujua namna ya kuufikia utakatifu ili Mungu atusitawishe katika mambo yetu yote (ukizingatia hoja yetu ya kupata mke/mume mwema). Najibu kifupi kwa maelezo haya machache tu
  Tuliumbwa kwa mfano na sura ya Mungu mwanzo 1. Kama tuliumbwa kwa jinsi hiyo, hivyo tangu mwanzo tuliumbwa ili tuakisi tabia ya utakatifu wa Mungu, maana Mungu ni mtakatifu. Hata baada ya anguko la mwanadamu dhambini, bado Mungu ameendelea kuwa na wito huo kwetu wa kututaka kuwa watakatifu kama YEYE alivyo “Kwa kuwa mimi ni Bwana, Mungu wenu; takaseni nafsi zenu basi; iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu; wala msitie uchafu nafsi zenu kwa kitu kitambaacho cha aina yo yote, kiendacho juu ya nchi”- Lawi 11:44, na “kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu” – 1 petro 1:16. Tunapokuwa watakatifu, daiama huwa tunakuwa upande wa Mungu, na YEYE hufanya makazi katikati yetu “12 Nami nitakwenda kati yenu, nami nitakuwa Mungu wenu, nanyi mtakuwa watu wangu”- Lawi 26:12. Kumbuka kuwa nilisema kuwa tunapoyafanya mapenzi ya Mungu yaani sheria ya Mungu inapokuwa ndani yetu, ndipo Mungu atatusikia. Lakini zaidi ya hapo, atakuwa katikati yetu, atakuwa kwetu pia “Maana hili ndilo agano nitakaloagana na nyumba ya Israeli Baada ya siku zile, asema Bwana; Nitawapa sheria zangu katika nia zao, Na katika mioyo yao nitaziandika; Nami nitakuwa Mungu kwao, Nao watakuwa watu wangu” – Ebran 8:10. Swali la kujiulizqa sasa, ni je, tunawezaje kuifikia hali hii ya utakatifu? Yafuatayo ni miongoni mwa mambo yanayomfanya mtu kuufikia utakatifu.
  1. Jitenge na uovu/waovu. 1 Wathesalonike 5:22 jitengeni na ubaya wa kila namna, 2 Wathesalonike 3:6 Ndugu, twawaagiza katika jina la Bwana Yesu Kristo, jitengeni nafsi zenu na kila ndugu aendaye bila utaratibu, wala si kwa kufuata mapokeo mliyoyapokea kwetu. Kwa maneno mengine, Fanya urafiki na Mungu, Yohana 15:14 Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo.
  2. Soma Biblia(Kumbukumbu la Torati 27:10 Basi isikize sauti ya Bwana, Mungu wako, ufanye maagizo yake na amri zake nikuagizavyo leo) na kuomba (Yohana 15:7 Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa) kila saa kama inawezekana; kesha!!
  3. Weka tumaini lako kwa Bwana Mungu katika mambo yako yote(Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.-matt 6:33) n.k.

  Maisha ya Mkristo yeyote, ni kujiona unapungua kila saa kadri unavyozidi kumkaribia Mungu. Pamoja na dhambi zetu tuzitendazo kila saa aidha kwa kusikia, kuona, kuwaza, kuhusika kabisa au dhambi za shirika, bado Mungu huguswa sana lile hitaji letu la moyoni la kutaka kumkaribia na kujitenga na uovu wote. Inawezekana kuishi maisha matakatifu. Wapo watu ndani ya Biblia, walioishi maisha ya namna hiyo.

 7. Nzala Michael Siyi,

  Naomba kuuliza, nimeuliza MAMBO gani na umeandika nini? Unaweza rudia kusoma uliyoandika WEWE kisha sema umeandika nini HASWA? dah! aisee!

  Kwamba ukifuata mapenzi ya Mungu, utapata ndoa safi, Mungu atakupa kitu safi, nauliza ivi/niiweke ivi…Baba na Mama yako walioana wakiwa ktk Imani au bado hata ukazaliwa? kama walikua bado, was that ndoa au la? walifuata mapenzi ya Mungu, devo hata wakaishi pamoja kwa miaka hadi leo na ndimo humo ulitokea?

  Press on

 8. Siyi,
  Kimsingi, naweza kusema umeyaelewa vizuri saaana maswali au changamoto aliyoileta Seleli. Nasema ni changamoto kwasababu anajaribu kuupata ukweli wa jambo hili badala ya kujiridhisha na mistari ya Biblia tusiyoielewa, kisha tukajifanya kwamba tumeielewa, huku tukiliendea jambo hilo la ndoa kwa namna yetu wenyewe ktk pose ya Biblia, ule Unafiki!!!

  Maelezo ya Seleli, na maswali yake, ktk ukamilifu wake, ninayaona yamejengeka ktk msingi wa vifungu vya Biblia alivyovinukuu, ambavyo kwa uhakika ni Neno la Mungu lenye kutimilka pasi upungufu wowote ule kwa wanae kwa kadiri alivyolitamka. Shughuli au changamoto, ni huko kututimilia kwa hayo yaliyonenwa, je inakuwaje???? Yaani bila fiks, hebu tuelezane kiukweli, inakuwaje? Kwanza unajuaje kuwa huyu ndiye yule aliyenenwa ktk Maandiko, Eliezar aliwekaga vigezo, je sisi tunao ubavu wa kuweka vigezo, au ndio vile vigezo vyetu vya kulazimisha tukiisha kuvutiwa na kabinti?

  Lakini, nilipoyatazama zaidi hayo ya Seleli katika kioo cha haya uliyoyaleta, kulingana na vifungu ulivyovirejea na kuvijengea hoja, nimepata mwanga zaidi ktk jambo hili, haswa kule kumjua kuwa huyu ndiye yule aliyenenwa au niliyeahidiwa! Ngoja ninukuu sehemu ya maelezo yako ambayo ninaamini yanaliweka wazi hili jambo:
  “”Mtu yeyote anayeishi sawasawa na sheria ya Mungu, yaani hatendi dhambi, daima Mungu atasikia maombi yake na atapata mwenza mzuri na mwema tu hata kabla ya kuanza kuishi naye. Lakini ukiwa mvunja sheria za Mungu (hata kama unavunja moja tu), Mungu hatasikia maombi yako kabisa. “Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo” – Yohana 9:31. Mithali 28:9 Yeye aligeuzaye sikio lake asiisikie sheria, Hata sala yake ni chukizo.””

  Basi ndio kusema, kuomba kwetu tunakokufanya ili Mungu atupatie wake au waume kulingana na Neno lake, licha ya shauku yetu, bado kusikilizwa kwa maombi yetu hayo kutategemea kikamilifu hali ya utakatifu wetu, je, tu watakatifu, yaani HATUTENDI DHAMBI????? Kwahiyo hata kumjua kuwa huyu ndiye niliyeahidiwa itategemea kikamilifu hali yako ya utakatifu, huko kuwa kwako USIYE NA DHAMBI; ukiwa huna dhambi ndio utayajua hayo yooote kuhusu mwenza wako, vinginevyo tutegemee rehema ya Mungu kwa upande mmoja, na usingizi wa shetani kwa upande mwingine, kwamba kalala na hatuoni ili atuwashie!

  Jambo linalonisumbua sasa hivi, baada ya kuyasoma maelezo yako Siyi, ni hili la mtu kuwa “Hatendi Dhambi”, ambalo ndio ufunguo wa mafanikio yetu ktk kujenga uhusiano imara na Mungu wetu; je, tunawezaje kuifikia hali hiyo, ili tuishi tukiwa “Hatuna Dhambi” kiasi kwamba kama angeletwa yule “Magdalene” wenu mzinzi mbele yetu leo hii, kisha Kristo akatuambia kuwa “Asiye na Dhambi awe wa kwanza kumrushia jiwe…”; nadhani atakapoinua kichwa chake safari hii hatamuona yule mwanamke bali rundo la mawe lililomfunika!!!

  Hebu nipe jinsi ya kuifikia hali hiyo ya kuwa huna dhambi; na je, wako watu wasio na dhambi hapa duniani, haswa leo hii? Maana imeandikwa, 1 Yoh 1:8 “Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.”!!!!!!

  Ubarikiwe!

 9. Seleli,
  Ha ha ha ha. Kwanza, una uzoefu na hiki unachokifundisha au? Halafu mbona umeuliza maswali kana kwamba huna imani rafiki yangu? Waseja si utawaogopesha kuoa/kuolewa sasa!!!

  Kwa kiasi fulani (kiubinadamu) hoja zako zina msingi. Lakini tukienda kiroho, zinapwaya kaka. Kama kweli wewe ni kijana, uliyetulia, unayempenda Mungu, hutumii akili na macho kumpata wa kumpenda, bali unamwachia Mungu kwa asilimia kubwa, utajutaje baada ya kuoa/kuolewa? Kamwe, haitakuja kutokea, labda kama Bwana ana makusudi Fulani juu yako.
  Biblia inasema, “Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia”- 1 Yohana 5:14. Msisitizo wangu hapa ni phrase hii “tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake”. Kwani mapenzi ya Mungu ni yepi? Biblia inasema, “Kuyafanya mapenzi yako, Ee Mungu wangu, ndiyo furaha yangu; Naam, sheria yako imo moyoni mwangu”- Zaburi 40:8. Kijana yeyote anayeishi sawasawa na sheria(neno) za Mungu, Mungu hatampa jiwe wakati ameomba mkate wala hatapewa nyoka wakati ameomba samaki (Luka 11:11). Mbingu hufurahia mno zinapomuona Seleli anaishi sawasawa na neno la Mungu, naam hudiriki hata kumuita ndugu/mzazi wa Kristo. “Kwa maana mtu ye yote atakayeyafanya mapenzi ya Mungu, huyo ndiye ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu”- Marko 3:35. Mtu yeyote anayeishi sawasawa na sheria ya Mungu, yaani hatendi dhambi, daima Mungu atasikia maombi yake na atapata mwezi mzuri na mwema tu hata kabla ya kuanza kuishi naye. Lakini ukiwa mvunja sheria za Mungu (hata kama unavunja moja tu), Mungu hatasikia maombi yako kabisa. “Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo” – Yohana 9:31. Mithali 28:9 Yeye aligeuzaye sikio lake asiisikie sheria, Hata sala yake ni chukizo.

  Ukimwabudu Mungu sawasawa na anavyotaka, ukaacha hisia na mitazamo yako, Mungu kwa hakika atakupatia mke/mume mwema mno. Bwana hupendezwa sana na watu waaminifu siku zote.

  Nilikuwa nadokeza tu ndugu yangu Seleli.
  Wakatabahu!!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s