Unyenyekevu ni sababu ya kukuwa Kihuduma!

huduma

Salom WANA WA Mungu,

Miaka ya hivi karibuni zimezaliwa huduma za Kikristo ambazo zimejaa majaribu ya kiburi kwa watumishi wa Mungu.

Huduma hizi zenye nguvu zimekuwa zikiinuka na kuzaliwa kila iitwapo leo, labda tujiulize kidogo kama zatoka kwa mwanzilishi MUNGU MWENYEWE au kuna chanzo kingine nyuma ya pazia?

Hatari ninayoiona ni kuleweshwa na nguvu hiyo kwa watumishi wa Mungu, Ambazo wamekuwa wakijaribu kuanzisha funuo mbalimbali japo ipo nje ya neon /au hakuna mfananisho wa neon, mfano kula majani, kutembea na vichupa vya mafuta, vitambaa, maji nk . nimelitafakali jambo hili nikaona ni rahisi kwa mtumishi anayetumiwa sana na Mungu kulewa na kile afikiriacho kuwa ni nguvu na mafanikio yake mwenyewe.  Na ni mara nyingi watu weengi sana wanakuwepo kumhakikishia umaarufu wake ktk ibada zake na vyombo vya habari.  Kwa kuiona miujiza aifanyayo, watu hufurahia kumheshimu kama vile ni mungu mdogo “wametushukia kwa mfano wa wanadamu!”  (Mdo 14:11).  Fedha na nafasi ya heshima huja kirahisi, na mara huanza kufikiria na kuamini kwamba baraka za Mungu ni kwa ajili yake.

Hivyo imekuwa changamoto kwa watumishi hawa na ni hatari kwa kuwa huwa tayari kwa anguko kubwa. Tumeshuhudia watumishi wengi kwa hili jambo la kukosa unyenyekevu limekuwa sababu ya kuanguka kwa wengine. Maanguko haya kuwa siyo kwa ajili ya mafanikio ya huduma yenye nguvu, bali hutokea kwa kukosa mafanikio hayo.  Kwa sababu watumishi wengine wamekuwa wanatamani mno kutumiwa na Mungu kwa namna kubwa au kwa sababu wanatamani sana kule kuonekana na watu kama watumishi wenye nguvu kubwa wanaighoshi kweli. Nyakati nyingine wanaanza kuinakili miujiza au kufanya mambo zaidi ya maandiko.  Wanakuwa wako tayari kuridhika na uongo na hata kuongeza jambo ambalo siyo halisi badala ya, kwa unyenyekevu kumtegemea Mungu kwa matendo ya kweli.  Jinsi inavyohuzunisha na ilivyo janga kubwa sana siku hizi.

Katika kuhudumu katika huduma yenye nguvu, tusije tukasahau ya kwamba nguvu yote ni ya Mungu na hivyo utukufu wote ni wake YEYE MUNGU.  Wakati wale sabini na wawili waliporudi kutoka kwenye huduma, walitoa ripoti kwa Yesu, “Bwana hata pepo wanatutii kwa jina lako” (Lk 10:17).  Yesu alifurahi pamoja nao.  Halafu akawapa onyo “Lakini msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii; bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni”  (Mstari 20).  Alikuwa anawaambia, “Msijiinue kwa yale mliyoyatenda kwa ajili ya Mungu, bali furahini kwa yale Mungu aliyowatendea.”  Unyenyekevu ni jambo muhimu. Hivyo basi imekuwa ni changamoto kwa watumishi, na hata kwetu sote tuwe makini kuwikia sauti ya Mungu na kuelewa kwamba yote tuyanyayo ni kwa utukufu wake Mungu na si kwa ajili ya kuinua nafsi zetu kwa kitambo kidogo na kukosa yoote milele.

Nawabariki nyoote

Amen

Anthony

Advertisements

3 thoughts on “Unyenyekevu ni sababu ya kukuwa Kihuduma!

 1. solomon unatakiwa kuokoka, kujazwa roho mtakatifu na kutembea vizuri na Mungu katika uzuri wa utakatifu pasipo michanganyo, hapo roho mtakatifu atakupa uwezo wa kutofautisha huduma hii ni mtu na hii ni Mungu. Wakati mwingine utatambua kwa mwenendo wa huduma kwa kipimo cha neno la Mungu.

  Pili: Mtumishi ni mtu yeyote aliyeokoka na kuendelea kuyaishi maisha ya kumwishia Mungu.

  Ubarikiwe.

 2. habari ndugu zangu,
  nimefurahi sana kwa maada nzuri,N aomba kuuliza maswali mawili
  1.Je nitatambuaje kwamba hizi huduma zatoka kwa mwanzilishi MUNGU MWENYEWE au kuna chanzo kingine nyuma ya pazia?
  2.nini maana ya kuwa mtumishi?

 3. Antony,

  Ubarikiwe kwa Ukweli mtupu!

  Na pia imeandikwa,”Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake”1pet5:6

  Pia, imeandikwa “kabla ya anguko utangulia kiburi”.Mithali 16:18-19 …

  Na tena imeandikwa,”ajikwezae atadhiliwa, naye ajidhilie atakwezwa”.Luk 14:11.

  Tukumbuke kuwa Roho ya kiburi/kujikweza inatoka kwa shetani. Hebu tuone mifano hii.

  Wakati huo akiwa ni malaika wa nuru/lusifa, kwa sababu ya uzuri na mamlaka aliyopewa na Mungu. Shetani aliona Mungu ajampa cheo alichokuwa anakitaka. Nae kwa kiburi cha moyo wake alisema hv:

  “12 Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa! 13 Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini. 14 Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu.” Isa14:12-14.

  Hapa tunaona kiburi cha moyo wake shetani alitaka kujikweza na: KUFANANA NAE ALIYE JUU-yaani kutoka malaika mpaka kuwa Mungu per se. je huku sio kujikweza? Tafadhali zingatia maneno NITAFANANA NAE ALIYE JUU ..Isa14:14 yanamaana sana. Utaona hapa chini.

  Je, ni nini matokeo ya shetani kutaka kujikweza. Haya hapa:

  Isa14:15-“Lakini utashushwa mpaka kuzimu; Mpaka pande za mwisho za shimo.”.

  ADAM NA HAWA!

  -jamii ya wanadamu pia imeanguka dhambini kwa sababu iyo iyo ya kutaka kujikweza hata KUFANANA NAE ALIYE JUU/MUNGU km tulivyoona ktk Isa14:14. Hebu tuone nini kilitokea pale edeni!

  Nyoka wa zamani aitwae Ibilisi na Shetani. Uf. alimwaidi Hawa kuwa kuvunja agizo la Mungu la kutokula ule mti wa ujuzi wa mema na mabaya kutawafanya adam na hawa wawe Mungu/kufanana nae aliye juu, jambo ambalo lilimfanya nae ashushwe kutoka mbinguni!. Hebu tusome .

  Baada ya majibizano ya muda mfupi shetani alimdanganya Hawa kwa kumwambia :

  Mwanzo3:4-5 ” Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, 5 kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi MTAKUWA KAMA MUNGU, mkijua mema na mabaya.”

  Zingatia maneno: …. nanyi MTAKUWA KAMA MUNGU…. ni hali ile ile ya kujikweza na kiburi alichokuwa nayo lusifa kwa kutaka kufanana nae aliye juu! Kila mmoja anajua nini kilitokea kwa adam na hawa baada ya kuvunja agizo la Mungu. Udanganyifu ulioje kwa watumishi wa Mungu Lusifa, adam na hawa. Kwa kujikweza kwao hakika walidhiliwa. Hadi leo mimi na wewe tunashiriki adha za moyo wa kiburi wa wazazi wetu.

  Kiburi na kujikweza ndio dhambi ya kwanza kutokea mbinguni na edeni na ndio maana ktk vitu saba alivyovitangaza Mungu kuwa ana vichukia cha kwanza ni kiburi.

  “Kuna vitu sita anavyovichukia BWANA; naam, viko saba vilivyo chukizo kwake. Macho ya KIBURI, ulimi wa uongo…” mithali 6:16-19.

  Hivyo basi ht leo ukiona mtumishi wa Mungu aliyekaramiwa uwezo wa Mungu {iwe ni mhubiri,muimbaji,mwalimu, mwinjilisti n.k} amekengeula na amekosa unyenyekevu na kujawa na kiburi na kujikweza! Ujue tu amenaswa na hila ya yule mwovu na amekuwa wakala wake kuendeleza kile kilicho asisiwa mbinguni then pale eden na ht leo kinaendelea.yaani pale tunapopokea sifa,heshima na utukufu anaostahili Mungu kupitia huduma zetu, ndio yale yale ya ” KUFANANA NAE ALIYE JUU” yaani kuwa miungu watu kitu ambacho ni kinyume na Amri ya kwanza ktk amri kumi za Mungu, isemayo , “usiwe na miungu mingine ila mimi”. kutoka20:1-3

  Unyenyekevu ni matokeo ya uwepo wa RM + kuvaa silaha zote za Mungu {Efeso6} katika maisha ya mtu wa Mungu. Tumpokeeni uyo atatunyenyekesha.

  Mtumishi wa Mungu, ili udumu ktk huduma yako anachotaka Mungu ni hiki:

  Mika 6:8. “Na BWANA anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako!”

  Watumishi wa Mungu, tubadilike. Unyenyekevu unalipa!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s