Kushinda tamaa ya mwili!

ndoa01

Amani ya Bwana iwe nanyi enyi nyote,

Nini uzoefu wako  uliyeoa au kuolewa? Unaweza sema kitu gani hapa kwa dhati ili ufundishe vijana?

JE TUNAOA/OLEWA ILI KUTULIZA/KUSHINDA KABISA TAMAA YA MWILI AU KWA KUA kiakili, kiumri, kijamii, kifamilia, kimpango wa maisha binafsi, ni wakati umefika kufanya ivyo?Imeandikwa…1Wakorinto. 7:1-9…. Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe.Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake. Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali mkewe.Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha kwa kusali; mkajiane tena, Shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu.Lakini nasema hayo, kwa kutoa idhini yangu, si kwa amri.Ila nipendalo ni kwamba watu wote wawe kama mimi nilivyo; walakini kila mtu ana karama yake mwenyewe itokayo kwa Mungu, huyu hivi, na huyu hivi. Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, Ni heri wakae kama mimi nilivyo. 9 Lakini ikiwa HAWAWEZI KUJIZUIA, na waoe; maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa

NOTICE pia mstari wa 9-ktk Kiingereza..NIV…”But if they CANNOT CONTROL themselves, they should marry, for it is better to marry than to burn with passion.

Si ni kweli hapo Paul anashauri, kama mambo yanakushinda, basi oa/olewa?

Si ni ukweli pia amesema kua kama unaweza kuji control, basi fanya tu na kazi ya Bwana na maisha?

–ES

Advertisements

23 thoughts on “Kushinda tamaa ya mwili!

 1. ALELUYAAAAA… Wapendwa nawasalimu katika jina la YESU KRISTO.. nina swali ni muda gani wa vijana kuoa na kuolewa kiumri ktk kibiblia

 2. Wapendwa nina swali; Ni kwa namna gani Mwanadamu anaweza kuachana na tabia sugu katika maisha yake hasa zile zmbazo haziipendezi jamii?

 3. ck Lwembe points zako zimenifungua sana.
  Siri kubwa naiona vijana hawana NENO ndio maana wanayumbishwa .ukijua kuwa ni Roho mwenyewe atawakutanisha (Isaya 34:16) na kazi ya kuchunguza si yako hautataabika.
  Exodus 33:14 “my Presence will go with you and you will find rest”.
  Mungu atusaidie tudwell in His Presence na tuliishi na kutafakari NENO lake na sio mapokeo.

 4. Jamani wandugu ni kweli kabisa kuwa hatupaswi kuzitegemea akili zetu wenyewe, bali Mungu ndiye jibu lako, Jamani tuendelee kujifunza katika bwana japo kukosoana ni vizur kwani uta ijuaje kweli uking’ang’ania unayosema bila kupokea mawazo ya wengine?

 5. Amina ndg Stephen!

  Unajua ndg yangu kuna tofauti kubwa sana kati ya ‘hadithi za kizee’ na ‘hadithi za uongo’; naona unaendelea kuyachanganya mambo tena!!

  ‘Hadithi za kizee’ huwa zimejaa mafunzo, hizo husaidia kuwafikisha wachanga ktk uelewa wa mambo kwa kadiri ya maisha yetu ya kila siku, na hilo huwezekana kutokana na hekima ya wazee, wameona mengi!!!

  2Tim 4:4 uliyoinukuu, haizungumzii ‘hadithi za kizee’ bali ‘hadithi za uongo’ kama hii yako, isiyo na rejea ya Maandiko, unayoifundisha ya kuchunguza wachumba. Hicho kifungu kinasema hivi, “Nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo.” Basi, “hadithi ya kuchunguzana wachumba” ni ya uongo maana hakuna mahali Biblia inalifundisha hilo, huku ndiko kuzitegemea akili zako mwenyewe!

  Hata huyo mtumishi wa Ibrahimu, inaonesha kwamba hujayaelewa yaliyoandikwa. Elieza HAKUMCHUNGUZA Rebeka, bali alimuomba Mungu ampatie mke mwema kwa ajili ya mwana wa bosi wake, na si haya mambo uliyoyaandika! Mtu kakutana naye kisimani, kamchunguza lini kama hizo si hadithi za uongo unazoleta? Nimekwambia Mungu ndiye mwenye kuzichunguza tabia zetu, na ndiye aliyemleta Rebeka kisimani na kumvuvia Elieza jinsi ya kumtambua, hayo ni mambo ya IMANI kaka!!!! Mtafute Mungu kwanza na hayo mengine utaongezewa, hata mchumba wa kumuoa, Mungu ndiye anaye ujua ubavu wako halisi, msubiri yeye! Mit 3:5 “Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe”!!!!!!

  Hata hiyo Matt 19:10, haizungumzii kuwachunguza wachumba, bali Ndoa na Talaka!!!

  Hivi kuna gumu gani la kueleweka kuhusu mambo ya Yakobo? Mwa 29: 17 “Raheli alikuwa mzuri wa umbo, na mzuri uso. 18 Yakobo akampenda Raheli akasema, Nitakutumikia miaka saba kwa kumpata Raheli, binti yako mdogo.” Au ndg yangu unaposema kumchunguza mchumba una maana ya kuuchunguza uzuri wa sura na umbo la unayetaka kumuoa kama alivyofanya Yakobo? Au wewe unaposoma Maandiko hayo yanasomeka tofauti na hivyo yalivyoandikwa kiasi kwamba unamuona Yakobo akimchunguza Raheli tabia? Haya mambo yote anayeyasimulia ni RM, ndiye aliyezichunguza tabia za Raheli na kuzisoma siri za moyo wa Yakobo na kisha kutusimulia!!!

  Unaniomba tulifuate Neno, haya Neno ndilo linatuambia Yakobo alimpenda Raheli, huyo aliyekuwa “mzuri wa umbo, na mzuri wa sura”; na wewe unatutahadharisha kwamba, “leo watu wanakosea wanaangalia sura”; Je tumfuate nani, wewe unayeponda kuangalia sura au Neno linatutonesha kuhusu uzuri wa sura????

  Acha mambo ya uongo, jambo la kwanza ni sura na umbo, (hata kama binti hujamuona, lakini taswira ya matamanio yako si unayo, Mungu huiangalia hiyo), halafu ndio unasikilizia!!! Huwezi kumuomba Mungu usichokijua, utakuwa mnafiki tu! Hata maelezo yako nayaona yamejengeka ktk msingi wa kubahatisha. Naona hatua inayofuata utawashauri vijana wanaotaka wachumba wapitishe maombi yao kwa mchungaji ili awachagulie wenye tabia nzuri!!!

  Lakini kijana wa kikristo aliyezaliwa mara pili, huyo ambaye amejazwa RM huyo mwenye kuzichunguza tabia, ana haja gani ya kuanza kutumia akili zake ktk jambo la uchumba? Au wanajazwaga RM siku za ibada tu? Kuwa na Nia ya Kristo maana yake nini, si ni kuongozwa na Kristo! Kama alimuongoza Elieza akampata Rebeka, si ataniongoza nami leo niliye mwana, kwa uhakika zaidi ili furaha yangu iwe kamili!!!? Au Mungu amebadilika siku hizi? “Yeye ni yule yule, jana, leo na hata milele”!

  Bado ninaamini kwamba jambe la kumchunguza mchumba latokana na ‘Kutokuamini’ na ni mtego wa Ibilisi unaowatesa vijana wengi, ndio maana nikasema ni la kihuni!

  Stephen, rudi kwenye hivyo vifungu ulivyovinukuu, visome pole pole, vitakujenga sana; hata ukiturudia hapa utatusisitizia Utakatifu ili tuwe tofauti ktk kuishinda kwetu tamaa ya mwili!!

  Gbu!

 6. Bwana yesu asifiwe ndugu ck lwembe
  mpendwa umeeleza mambo mengi bila uthibisho wa neno la Mungu yaani kunukuu vifungu kwenye biblia bila kufanya hivyo hizo zinaitwa hadithi za kizee (2timotheo 4:-4) hapa tunaongea mambo ya kujenga si ya kubomoa mambo ya ndoa yaliwachanganya hata wanafunzi wa Yesu mpaka wakasema kama ni hivi haifai hata kuoa soma (mathayo 19:10) sasa tunaposema mda wa kuchunguza tuna maana hii kwa ni nini watu wana weka vigezo utavionaje vigezo kama hutakuwa na mda wa kuchunguza kwa nini biblia inasema huyu alikuwa dhaifu wa macho na huyu alikuwa mzuri ndugu lwembe ujue ulikuwepo uchunguzi mpaka wakatofautisha usilete mambo ya kuwakosesha watu wanaotaka kujifunza sasa naanza kwa mtumishi wa ibrahimu aangalia mambo aliyo chunguza (1).alichunguza tabia ya utii (2).ukalimu (3)mchapa kazi soma (mwanzo 24:-14) leo watu wanakosea wanaangalia sura nije kwa yakobo wewe unafikili angekuwa ana tabia mbaya mda wa miaka saba uchumba usinge bakia hata labani alipombadilshia mke hata yule raheli angeweza kukataa mimi nimeshudia mabinti wenye msimamo wanapochumbiwa wanapowambia vijana ngoja niombe pale wanaposema waombe wanatumia hekima wanataka wapate mda wa kuchunguza kipindi kinapokuwa kilefu unashanga kumbe kijana alikuwa anataka kwa tamaa za mwili hana mbele wala nyuma mwisho ule uvumilivu unamshinda unakuta kaenda kuchumbia mwingine sili inafichuka unasikia yule kijana kachumbia zaidi ya sehemu moja ukiona kijana ana halaka jiulize ni kwa mapenzi ya Bwana au ni shetani haya mambo ya yanahitaji uongozi wa Roho mtakatifu pamaja na maombi mpaka amani ya kristo iamue moyoni mwako pia mpendwa lwembe ujue biblia hajaandikwa kama unanavyo dhani biblia imeandikwa kwa kifupi ujue hata mtumishi wa ibrahim pamoja na uchunguzi,vigezo vyake bado hata yeye alichunguzwa akahojiwa alijuana naye vipi mpaka anaeleza ushuhuda wake soma (mwanzo 24:-33…54) pia soma (Yohana 21:-25) naomba tulifuate neno la Bwana sio mambo ya vichwani balikiwa na Bwana ameni

 7. Ndg yangu Stephen,
  Shalom!

  Kujifunza mambo ya Mungu kunahitaji unyofu! Nao unyofu hujumuisha pamoja na kuyakubali makosa yetu, na kupokea yaliyojidhihirisha ktk Neno la Mungu na si kuyafukia tuliyochapia!!

  Jambo uliloulizwa na ndg Eucalyptos ni jepesi sana, tena lilikuwa na maana ya kuufungua ufahamu wako ili majibu yako yanayoendana na Neno la Mungu yawe na faida kwetu sote tunaolifuatilia jambo hili katika kujifunza. Lakini badala ya kujibu, naona umeleta ngonjera, ukiendelea kutufundisha Mapokeo!

  Kwa kifupi jambo la kuchunguzana uchumba ni la kihuni na HALIPASWI kuwapo makanisani mwetu!!! Hii ni kutokana na ukweli kwamba Hakuna aliyewahi kumchunguza mchumba aliyemchumbia kwa nia ya kuzijua tabia zake kama mnavyofundisha.

  Hata Yusufu katika kumchumbia Mariamu, hakukaa kumchunguza tabia kama mnavyotaka kutuaminisha. Maana rahisi ya uchumba ni kumchagua unayetaka kumuoa, mkiridhiana, basi posa hupelekwa ili kumfunga binti huyo asiposwe na mwingine, na kisha mwanaume hujitayarisha katika shughuli ya kuoa. Sasa kwa suala la Yusufu, hebu jaribu kuwaza kama ungekuwa ndio wewe ungefanyaje? Umemposa binti ambaye amekuhakikishia kuwa hajamjua mwanaume yeyote yule. Ukiwa ktk kujitayarisha kwa mahali na yapasayo, siku hiyo unapompelekea mahitaji, mkiwa mmeketi faraghani, anakuambia, “Mpenzi Steve,” nawe unamtazama usoni, macho yake yale makubwa, yanakuchanganya akili kidogo, yanaonesha yana furaha, lakini pia yana ukungu wa mashaka, unaitika ,”Naam, kipenzi!” kisha anakupa mkasa wa Malaika Gabriel na kwamba utarajie kulea mimba!!!

  “Mimba!!!” Yusufu lazima alipotea mlango wa kutokea, kama si mkono laini wa Mariamu uliomshikilia, na sauti nyororo iliyomhimiza kuwa na subira, ndipo na akili ikamrudia akatulizana angalau, na kuondoka hapo akiwa mwenye mawazo mengi sana. Kwamba hivi kweli huyu binti anataka kunifanya mimi bwege kiasi hiki, anisukumizie mimba isiyo yangu; Lah, balaa gani hili yaani kumpenda imekuwa nongwa! Ah, acha nisubiri nione kama ni utani au kweli! Biblia ilsema Yusufu alikuwa ni mtu mwenye Haki, basi kusubiri kwake hakukuwa kwa ajili ya kuisoma tabia ya Mariamu, la hasha, bali kuyaona matokeo ya taarifa aliyopewa! Tumbo lililpoanza kuvimba, ndipo alipoamua kumuacha binti huyo aliyempenda, na akingali anampenda, ndio sababu alitaka kumuacha kimya kimya!!!!

  Mfano wa Yakobo uliouleta, uko nje ya muktadha wa jambo unalolifundisha, hilo ambalo ni mapokeo. Miaka saba aliyotumikia Yakobo haikuwa kwa ajili ya kumsoma Raheli tabia, sijui unatoa wapi mambo yako haya!
  Mwa 29:15-20 “Labani akamwambia Yakobo, Kwa sababu wewe ni ndugu yangu, basi, je! Unitumikie bure? Niambie mshahara wako utakuwa nini? Labani alikuwa na binti wawili, jina la mkubwa ni Lea, na jina la mdogo ni Raheli. Naye Lea macho yake yalikuwa dhaifu, lakini Raheli alikuwa mzuri wa umbo, na mzuri uso. Yakobo akampenda Raheli akasema, Nitakutumikia miaka saba kwa kumpata Raheli, binti yako mdogo. Labani akasema, Afadhali nikupe wewe kuliko mtu mwingine; kaa kwangu. Yakobo akatumika miaka saba kwa kumpata Raheli. Ikawa machoni pake kama siku chache tu kwa vile alivyompenda.”

  Mapenzi siyo mchezo! unapoambiwa “ukiwaka tamaa” usidhani ni utani. wanakwambia ukipenda, maji utayaita “mma”!!! Huyo hapo Yakobo akitumika miaka saba, akiiona kama ni siku chache tu!!!! Mambo yakuchunguzana unayaona ktk vifungu hivyo? Hayapo, ni mambo yenu ya kufikirika tu mnayowaharibu nayo vijana. Nao wanaanza kuchunguzana ktk wasiyoyajua na kuishia ktk uasherati! Roho Mtakatifu ndiye azichunguzaye tabia zetu!

  Binti anapochumbiwa, maana yake anaambiwa kwamba kuanzia saa ya uchumba huo, anapaswa sasa aanze safari ya kumfanania mumewe, ndio maana ya yeye kuwa “ubavu”; huwezi kuchukua ubavu wa kenge ukaupachika kwa Adamu ukafaa, haiwezekani!!!

  Kanisa ndilo lililo mfano bora katika jambo hili la kuchumbiana. Angalia hapa linapochumbiwa, 2Kor 11:2 “Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi.” Jaribu kuangalia ni lini uliposwa, muda wote huu tangia Injili ilipotufikia ndipo tulipoposwa. Hata sasa tungali tukiendelea kumfanania Kristo Mume wetu, tukijiweka tayari kwa Arusi! Ni hawa tu wanaoweza kuoana ktk Shwari ya Neno la Mungu, tamaa zao zikijituliza ktk ndoa yao iliyo ndani ya Mapenzi ya Mungu, na si kutumia akili huku tukijidhanisha kwamba RM ndiye katuongoza tuchunguzane kwa miaka miwili mpaka wanawake wanaanza kuzeeka bado mnachunguzana tu; mwisho, Oh, nimeota ndoto yule rafiki yako ndiye anayepaswa awe mke wangu!!

  Ubarikiwe tunapo endelea na Changamoto za Injili!

 8. naomba kuongeza mfano kama nilivyo ombwa na ndugu eucalyptos mtu mwingine ambaye uchumba wake ulidumu kwa miaka saba ni Yakobo soma mwanzo 29:-15..20 naomba niseme kipindi cha uchumba jambo la muhimu kuangalia ni je mchumba wako ana upendo kutoka moyoni au anakutaka kwa tamaa ya mwili maana kama ni kwa tamaa ya mwili ujue ndoa ni agano lililokusudiwa kuishi maisha yote ambayo mungu atawapa soma sifa za upendo ktk (1wakolinto 13:-4..8) leo kwa kukosa upendo ,uvumilivu,kuhesabu mabaya.ndoa zinavunjika kipindi cha uchumba kikiwa kilefu hata kama kuna tabia imejificha utajua sasa ukiingia unajua mapungufu yote utajua njinsi utakavyo chukuliana naye uchumba sio ndoa ukiona huwezi unalusiwa kuvunja pia naomba niongeze kitu kingine haya yafanyike baada ya kumpa Yesu maisha yaani kuokoka na biblia inasema usifungiwe nira na mtu asiye amini sawasawa soma (2wakolinto 6:-14..15)leo kwa tamaa watu kwa tamaa,na haraka za kuolewa hata kama ungemshauri wanakataa mimi kuna binti tulikuwa tunasali kanisa moja la wokovu akachumbiwa na kijana wa dini nikamwambia biblia inakataa kufungiwa nira na mtu asiye amini yule binti akakataa leo anajuta,analia,mimi niseme vijana simameni kwa Bwana Mungu anajua mawazo anayowawazia ni mema si mabaya ya kuja kujuta maishani MUNGU AWABALIKI WOTE AMEN

 9. Kutokana na mchango wa Stephen, mimi naomba kujua yule Isaka alikuwa na muda gani wa kumchunguza mwenzi wake kabla hajamuoa, vilevile mifano mingine walau mitatu tofauti na wa Yusufu na Mariamu. Hili ni somo limekuwa likifundishwa saana juu ya “muda wa kuchunguzana”; Ninaomba kujua kuchunguzana huko kunasaidia nini na baada ya kujua hizo weakness unazitibu ama “unamtelekeza” huyo mwenzi? Je kama mmechunguzana, mkaingia kwenye ndoa, hakutakuwa na “ambayo hayakuonekana kwenye kuchunguzana”.

 10. Hii ni kwa Wote mliochangia hapo juu

  HOSEA 4: 6 .. Watu wangu wanaANGAMIZWA KWA KUKOSA MAARIFA,NA KWA KUWA UMEYAKATAA MAARIFA NA MIMI NIMEKUKATAA USIWE KUHANI WANGU

  MITHALI 24:3-6 inasema KW HEKIMA NYUMBA HUJENGWA, KWA NENO LA MAARIFA HUTHIBITIKA NA KWA UFAHAMU vyumba vyake hujazwa na kupabwa na vitu vya thamani.

  MITHALI 14: 1…MWANAMKE MPUMBAVU HUBOMOA NYUMBA YAKE KWA MIKONO YAKE….

  NINACHOTAKA KUSEMA NINI?

  HOSEA ANASEMA KUKOSA MAARIFA TUNAANGAMIZWA,MITHALI INASEMA HEKIMA,MAARIFA NA UFAHAMU NDIYO VINAVYOJENGA NYUMBA. MITHALI TENA INASEMA UPUMBAVU VIKIKAA KWA MWANAMKE UTAMHARIBIA NYUMBA YAKE

  ukienda kwenye kamusi Neno MAARIFA (knowlegde) linasema the FACTS OR INFROMATIONS ABOUT SOMETHING PERSON ACQUIRED THROUGH BEING TRAINED,TOUGHT OR GAINED BY EXPERIENCE’

  Neno UFAHAMU (understandings) linasema ABILITY TO COMPREHED OR TO GRASP SOMETHING IN YOUR MIND WHEN YOUR TRAINED, TOUGHT OR EXPERIENCED

  Neno HEKIMA(wisdom) IS ABILITY TO APPLY WHAT YOU HAVE KNOWLEGDE/UNDERSTAND

  kwa maana hiyo UKITAKA KUWAMSHINDI KATIKA NDOA (MAANA HUU NI UWANJA WA VITA VYA KIROHO) LAZIMA UTAFUTE MAARIFA (MAFUNDISHO NA NENO LINALOZUNGUMZIA HABARI YA NDOA TU NA NAMNA YA KUISHI NA MKE AU MUME, NAMNA YA KUTII AU KUPENDA)

  KWA FAIDA TU SI KATIKA NDOA TU UKIONA BIASHARA,KAZI,WATOTO WANKUSUMBUA TAFUTA MAARIFA (KNOWLEGDE) ILI UWE NA NENO KWA WINGI KATIKA HEKIMA YOTE…KUMBUKENI USIPOJUA JAMBO FULANI UNAKUWA MJINGA WA HILO JAMBO(SHETANI ATATUMIA KUKUTESA HADI UIJUI KWELE YAANI UTAIFAHAMU KWELI NA HIYO KWELI ITAKUWEKA HURU KABISA

  OMBI LANGU KWENU NI KUWA WAGALATIA 5:22-26 IWE NDIYO AJENDA YA KUDUMU KATIKA MAOMBI YAKO KWA MUNGU KUWA AKUPE TUNDA LA ROHO

  TABIA ZA UPENDO 1 WAKORINTHO 13:4-8

  KUNA MTUMISHI WA MUNGU ANAITWA MYLES MUNROSE NILIPOANZA KUYAFUATILIA MAFUNDISHO YAKE KUHUSU NDOA KANIBADILISHA SANA NAMNA AMBAVYO NILIKUWA SIJUI

 11. Ni kweli Paulo anasema kwa ajili ya tamaa, lakini ukisoma vizuri maandiko yanaonyesha ndoa ni kusudi na ni mpango wa Mungu, hivyo na liwe hilo kusudi linakuingiza katika ndoa na si tamaa, tofauti yake ni kwamba ukiingia kwa kusudi utaangalia mambo kama vile muda mhubir 3:1, mwenzi halisi marko 10:6 n.k lakini anaeoa kwa ajili ya tamaa atajichukulia tu yeyote na mwisho wake unakuwa majuto

 12. inamaana wanaume wote ndio wana sifa bora ya kuwa mume? ndoa zote zinavunjika sababu wanawake wanakua hawana sifa ya mke mwema? wanaume ndio wamesimama kwenye mstari sahihi katika suala la ndoa? mimi hiyo nakataa nawashauri mabinti msichoke kumuomba mungu ili muweze kusikia sauti yake watawafuata wanaume weengi sasa bila kupeleka iyo hoja mbele za Mungu. mtawakubali ambao hamjatoka kwenye mbavu zao. Maana nao watakuja na maneno mazuri sana. napia watawaambieni. HUYU SASA NI MFUPA WA MIFUPA YANGU NA NYAMA YA NYAMA YANGU. Kwamaana shetani naye huja kama malaika wa nuru. Namalizia kwa kusema Mungu hana upendeleo lolote unaloliona ni hitaji kwako mwambie yeye aliyekuumba. Mungu awabariki

 13. Mabinza chenga nyingi kama Mess!Umesema hakuna andiko linalosema m.mke aombe mume nami nikakuuliza kuhusu bangi,cgara,naongezea na zile wanazojidunga au nusa mateja mstari gani kwenye bible unazitaja na kuzikataza?na huko binti kukaa na ku2lia mbele za Bwana na kusubiri ndipo kufanyeje?

 14. kwanza kabisa niwapongeze wote mliochangia moja niungane na wote waliosema mwenye kutafuta ni mme sio mke tunaona hata baba wa imani wakati ulipofika wa kijana wake kupata mwenzi anatuma mtumishi kumtafuta soma (mwanzo 24:1…66) shida za mabinti wengi leo hawana sifa kama za mke wa isaka ndio maana hata ndoa nyingine zinavunjika kwa sababu baada ya kuoana mwenza anakosa sifa hizi wakati wa uchumba ama mda wa kuchunguzana ulikuwa mdogo kwa haraka ya tamaa ya kupata mwenzi halaka mimi nashauli mwe na kipindi kilefu cha uchumba ili mchunguzane kamaYusuph mme wa mama yake na Yesu mariam alipochunguza mpaka akataka kumacha mariam mpaka akahakishiwa na Roho mtakatifu kuwa mimba aliyo nayo ni kwa uwezo wa roho mtakatifu zifa zenyewe ni hzi kwa wale ambao hamsomi biblia 1.uwe mtu wa kazi sio mvivu 2.uwe na heshima ya moyoni sio ya kujionyesha kwa baathi ya watu kama vingozi wa dini ukiwa na hiyo itakutagaza hata kupata mwenzi 3.uwe mtii na mnyenyekevu kwa leo niishie hapo ni mimi ngulo mjoli wa Bwana Yesu

 15. Mpendwa Kissa,
  Kwanza nisamehe tu kwa kuchelewa kurudi kwako kama ulivyotarajia. Kusema kweli mimi pia natamani sana kujifunza ili kuliweka Neno la Mungu likae kwa wingi ndani yangu.

  Nikwamba, sisi kama sisi hatuna jinsi ya kuwasaidia hawa mabinti zetu, ila mwenye uwezo huo ni Mungu tu, yeye kasema wenye mizigo “alete kwangu name nitamsaidia”. Ki ukweli ni kwamba, tunatakiwa kukaa ndani ya Neno la Mungu, kuiishi mifano iliyomo humo na kuielewa methali yake. Tufuate maelekezo ya Neno la Mungu na si vinginevyo. Kumuomba Mungu, Kusali na kushukuru ndilo kusudi liletalo suruhisho katika mambo yetu, lakini si kila jambo linaombwa na kukubalika na Mungu mwenyezi, kinachokubaliwa kila tukiombacho ni kile kilicho katika NENO! Mojawapo ya makusudi ya Mungu kutupatia tuyaombayo ni kutufurahisha, lakini furaha inayokusudiwa na Mungu ni ile ya kweli na kamilifu. Biblia inasema katika Yh. 16:24 kwamba, 24Mpaka sasa hamjaomba jambo lo lote kwa Jina Langu. Ombeni nanyi mtapewa, ili furaha yenu ipate kuwa kamili.’’

  Unajua, Mungu si muongo wala haongopewi, ili mwanamke apate ndoa toka kwa Bwana, ni lazima awe na sifa za kuwa “MKE MWEMA” ili atakayepewa mke wa jinsi hiyo , ajue kwa moyo wake na si kwa akili zake kuwa, amempata kwa Bwana, maana mke mwema hupatikana kwa Bwana! Lakini jiulize kwanza kuwa kwanini Binti kuombewa ama kuomba Mme? Kuomba ama kuombewa ili kupata hilo si vibaya, lakini mwombaji kwanini afikie hapo?

  Biblia inasema, kila wakati Mungu hulichunguza Neno lake ili apate kulitimiza. Kwenda kuombewa ama kwenda mbele za Bwana kuomba upewe Mme kwa akili ni sawa,ila kufanya hivyo ni kama kumaanisha kuwa, Binti huyo atakuwa anajaribu “kuwaacha wazazi wake” na kwenda kutafuta mme, Unaona?! Lakini kujiandaa na kufanya hivyo my anaweza kuona kuwa si vibaya, maana huo ni “UBINADAMU” tu, na ubidamu ni ubatiri maana ni matunda yatokanayo na Akili! Imeandikwa katika Meth. 16:1 kuwa, Maandalizi ya moyo ni kazi ya mwanadamu bali jawabu hutoka kwa Mungu, sasa ili jawabu lije, Mungu huliangalia Neno lake. Lakini ukisoma katika Mwz. 2:18-24 utaona kwamba, Binti kwenda yeye mbele za Bwana ili kupata Mme, ni kuwa kinyume na mistari hiyo niliyoitaja! Ni kutaka awe ameumbwa kwanza kabla ya mme, ni kudai atafutiwe ubavu wake, wakati mwenye ubavu ni mwanamme na mwanamke ni kutokana na mwenye ubavu, kwa kawaida mwenye chake ndiye hukidai!

  Tukienda mbele kidogo katika hilo, na kusoma ile Mwz. 2:22 inasema, “22Kisha BWANA Mungu akamfanya mwanamke kutoka kwenye ule ubavu aliouchukua kutoka kwa huyo mwanaume, akamleta huyo mwanamke kwa huyo mwanaume.” Unaona? Unadhani kwanini? Mme ndiyo mhitaji, anahitaji msaidizi, si vema awe peke yake! Na katika ule mstari wa 23, mwanamme baada ya kukitambua kile kilicholetwa mbele yake ili kijibu hitaji lake alisema, 23…… “Huyu sasa ni mfupa wa mifupa yangu na nyama ya nyama yangu, ataitwa ‘mwanamke,’ kwa kuwa alitolewa katika mwanaume”. Na kutambua huko kwa Adamu kukampa kibali cha yeye kutafuta Mke (amtafute kwa Bwana). Tazama mstari wa 24 unasema, “24Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe nao watakuwa mwili mmoja”. Sasa, Binti anahitaji nini na anacho kigezo kipi kwa mjibu wa Neno la Mungu, hata aende mbele za Mungu kuomba Mme?

  Ukimsiliza Paulo naye kuna pahala kasema, “…..ili kuepuka zinaa kila Mtu na awe na MKE wake…” na hapo hajasema ili kuepuka zinaa ila MWANAMKE na awe na mmewe, kwa nini? Kwasababu maandiko hayaelekezi mwanamke atafute mwenyewe wa kumuoa! Mwisho kabisa nimalizie kwa kusema tu kwama, Yule anayesema kuwa bangi haijakatazwa kwa kuandikwa ndani ya Biblia atakuwa hajaelewa!
  Makatazo na yaliyokubaliwa yote ndiyo yanaifanya Torati, na torati haiwezi kuwa torati kama hakuna hukumu! Biblia inasema, “…..macho wanayo lakini hawaoni…” kwanini? ILI WAPOTEE! Kwanini wapotee? Ndiyo, KWAKUWA HAWAKUKUSUDIWA! Sasa, ngojea mpaka uione imeandikwa “acha Bangi” ndiyo uache!

  Ninacho weza kuwashauri mabinti na wanawake wenye kuhitaji ndoa wakae na kutulia mbele za bwana, yeye anajua ubavu uliofanyizwa binti ama mwanamke Yule, ni wa kutoka kwa nani na mwenye ubavu huo yuko wapi, bwana atakupeleka, na mwenye ubavu wake akikuona tu uta msikia akisema tena kwa sauti kuu kuwa, “HUYU SASA NI MFUPA WA MIFUPA YANGU NA NYAMA YA NYAMA YANGU,……….” Namyi mtaishi ndoa yenye furaha, maana ni mpango wa Mungu wetu tufurahi kwa ukamilifu!

  “Ufahamu ni chembe ya Uhai!”

 16. mtumishi wa Mungu mabinza nasubiri kwa hamu utumegee ufahamu kuhusu wanawake kupata wenza bila kuomba.

 17. So Mabinza mwanamke anampataje mwanaume wa kwel?kama kwenye biblia hakuna!vp kuhusu kuvuta bangi au cgara ni wapi wamekataza kukamua mimea hiyo aliyoiumba Mungu ni wapi kwenye Bible wametaja bangi na cgara hazifai kuvuta?So kama vp wa2 2le bangi na cgara kama kawa au waonaje Mpendwa Mabinza?

 18. asante ndugu yangu mabinza naomba unisaidie. Kweli sijaona mwanamke kwenye biblia akitafuta mwenza au akiomba kwa bwana. Sasa tuwashaurije mabint zetu jinsi ya kuwapata wenza. naomba nisaidie ili nipate ufahamu niwafundishe mabinti maana mimi naumia sana kuona ndoa za wakristo zikivunjika ovyo. Kama yangu iliyovunjika nikiwa na umri wa miaka 28 tu.

 19. Maombi ambayo Mungu hujibu, pamoja na mambo mengine, ni lazima kuomba lile ambalo linaendana name Neno LA Mungu.

  Watu wengi husema tu kuwa, Neno linssema TUKIOMBA LOLOTE KWA JINA LAKE TUTAPEWA! ni kweli hivyo ndivyo Neno linavyosema. Lakini waombaji hawataki kujiuliza kuwa, hilo “jambo lolote” linalosemwa na Biblia ndo ni lolote tu hata kama halimo ndani ya Neno?

  Hivi katika Biblia ni yupi kati ya mwanamme na mwanamke anayepaswa kuomba Mwenza kwa Bwana ama mwenye kwenda kutafuta mwenza no yupi? Ni wapi pameandikwa katika Biblia Mwanamke aombe ama aombewe ili kupata Mme?

  Kama papo, basi kazana tu katika kuomba kwa Imani utapokea, LA hapapo utakesha!

  “Ufahamu ni chembe ya uhai”

 20. Kuwa na moyo wa subira na uvumilivu chaguo lako liko ila msikilize kwanza mungu

 21. mm nashindwa kuelewa kabisa?kuna wakati naomba ,nafunga na nakuwa nipo safi kabisa namuomba mungu anipe mume lakini ndo kwanza wananifata waume za watu na wanaume wa kiislam,yani mpaka nimekata tamaa nimeamua kuacha kabisa hata kuomba mume.
  naomba mnishauli nifanyaje?

 22. bwana Yesu asifiwe. kwakweli nimependa mada hii ubarikiwe mtumishi wa Mungu. ila nilikuwa napenda kuongezea kuwa mtu kabla hajaingia kwenye ndoa aombe na amsikilize Mungu anasema nini juu ya huyo mwenza wake kwakufanya hivyo talaka kwa wakristo hazita kuwepo. kinyume na hapo ita tugharimu sana. mimi nilikaa kwenye ndoa miaka sita tu tukaachana na mume wangu sasa niliapa kifo kitatutenganisha siwezi kuolewa tena kunawakati hata namkosea Mungu kwa kuwaza hata tamaa huwa inanijia muda fulani. Je ningetulia na kuomba kwa bidii si nilazima Mungu angenipa ambaye tusinge achana hadi kifo. sasa imenigharimu maisha yote nitakua bila mume. Ushauri wangu kwa vijana mtafuteni Mungu kwa bidii maana baraka za Mungu hazichangamani na huzuni.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s