UTISHO WA KUFUFUKA!!

msalaba
MAANDIKO: YOSH. 5: 1 (YOSH. 2: 1 – 24)

Mojawapo ya ahadi toka kwa Mungu wetu tunayemtumikia, ni pamoja na kutuma utisho wake mbele yetu (utisho wa Mungu wetu) huwa unatangulia daima mbele na kumfadhaisha adui yetu sana. Kutoka 23: 27 – 30

– Kwa kweli Yesu Kristo ni tishio, kwa wakuu wa dini ni tishio kwa Wafalme ni tishio, kwa mapepo na wachawi ni tishio, kwa wasomi ni tishio, kwa matajiri ni tishio, kwa askari ni tishio, kwa magonjwa na wafu ni tishio, nasi tunatakiwa kulijua hili na kulikiri daima hata tunapoona wengine wakiogopa na kukata tamaa kutokana na vitisho vya adui. Hes. 14: 6 – 9.

– Mpaka leo duniani kote, kufufuka kwa Bwana Yesu ni tishio kwa imani nyingine zote ambazo waanzilishi wake na umaarufu wao hatimaye waliishia kaburini na hawakutoka kamwe hadi sasa ilibaki mifupa tu makaburini na nyama zao zikawa chakula cha mchwa!!.

– Askari waliopewa kulilinda kaburi la Yesu, saa anafufuka walikipata cha moto!! Soma waliyoyakuta. Math. 28: 1 – 4, 11 – 15.

– Habari hii ya kufufuka kwa Yesu imeenea dunia nzima na adui hata anapojaribu kuifunika kamwe hataweza, Yesu amefufuka na huu ndiyo ukweli, ndiye aliye na mamlaka juu ya kifo na siyo nabii au mtume mwingine yeyote, na kwa kweli huu ndiyo ushindi mkubwa sana wa Wakristo wa kweli.

Ukitaka kujua kuwa Kristo ni tishio; soma
(a) Marko 5: 1 – 15
(b) Yohana 11: 43 – 53 n.k. 2

Kama ilivyokuwa katika nyakati za Joshua, ambapo watu wa Yeriko mioyo yao ilikuwa imeyeyuka na hofu ya Mungu kuiangukia Nchi ile; ndivyo ilivyo dunia hii ya sasa tunayoishi, pamoja na dini nyingi kujikakamua lakini viongozi wao wanajua kuwa Yesu Kristo ndiye nabii pekee aliye tishio, ambaye kaburi halikuweza kumshika, na habari zake zinaposhuhudiwa mahala popote kwa usahihi, zina uwezo wa kuwaondoa watu wa aina yoyote katika utumwa wao!!.

Hakuna imani katika nabii yeyote leo hii hapa duniani iliyo na uwezo wa kumweka mtu huru zaidi ya imani ya Yesu Kristo.

– Kama Joshua, hakuna sababu ya Kanisa kuishi kwa hofu hata kama dunia hii ingefanya vituko vyake; bado tutaishi, tutakula, tutavaa, tutajenga, watoto wetu watasoma, watafanya kazi na biashara nzuri; Bwana amekwisha ondoa uvuli wanaojivunia.

– Tunatamba kwa sababu mwanzilishi wa imani yetu hayumo kaburini, amefufuka, yu hai milele na milele, anajipigania, anasema, anatembea, anaishi, anazo funguo zote za mauti na za kuzimu, Wana wa Sayuni hatuna sababu ya kujikunyata!!

– Hakuna roho ya nguvu tena kwa shetani dhidi yetu. Ona alivyo tishio huyu Mwanaume!! Luka 11: 37 – 41

Joshua alipata ushindi sana sababu ya ufahamu huu, adui zangu Mungu ametuma utisho kwao, na mioyo yao tayari imeyeyuka!!
Bwana tusaidie

Na
REV. L.M. Mwizarubi

Advertisements

5 thoughts on “UTISHO WA KUFUFUKA!!

  1. pasipo kufuffuka yesu kungekuwa hamna maana ya yeye kuja duniani kilele cha huduma yake ni kufufuka ndio maana kabla au baada yake hakuna mwingine aliyefufuka kama yeye

  2. kweli hakuna jina la kufanana na jina hili linalalo pita majina yote jina hili linapotajwa na watu waliolitumaini hakuna kitu cha kusimama mbele ya jina hili liwe ni pepo,uchawi,,nguvu yoyote ya giza vyote vinapiga saluti mbele ya jina hili ndio maana hata watu wa dini pamoja na misimamo yao yanapowafika shingoni wanakimbilia kwa Yesu Mungu akubaliki mtumishi wa Mungu kwa kutukumbusha

  3. Nikweli Mtumishi, ubarikiwe sana. Kwakweli kila nilitajapo jina la kristo na kuitafakari injili yake, napata amani ya ajabu mno moyoni mwangu mpaka najishangaa kwa machozi!!. Ni furaha ya ajabu mno inayoniugua kama niko ulimwengu mwengine hivi. Jina la yesu liinuliwe juu…juu..juu…sana sana sana!!!. Pasaka njema watumishi wa Mungu.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s