MTUME na NABII kama si MTUME au NABII!

kanisa

Amani ya Bwana iwe daima nanyi enyi nyote,

On Serious note, tupeane shule hapa kwa maswali yafutayo:

Ana sifa/characters gani za nje-Matendo na Maneno-Kazi zinazotoka au jidhihirisha toka kwake hata tukiona tunajua hakika huyu ana huduma izo na yule fake au kujitutumua/kujiinua na mbwembwe tu, hamna lolote?

Kwa nini Mtu akiwa na huduma izi kizazi cha leo, anapenda sana ajulikane kuliko alipokua anafanya huduma ya Ushuhudiaji Mtaa kwa Mtaa, Shemasi, Mze wa Kanisa, Kutembelea Wagonjwa na Wafungwa kwa Neno, kusafisha Kanisani-jengoni, Kusimamia kamati ya mazishi, kuoa na kuolewa hapo Church kwakwe nk?

Kwani Huduma izi, Mtu anakuja kupewa na Mungu baadaye anapoukulia Wokovu au pale pale anapompata Master? Why Mtu anakaa ktk Wokovu kwa miaka na tunafahamiana au tunamjua kisha baadaye ghafla tunasikia yeye ni Mtume na Nabii au Nabii/Mtume?, ni fix au kweli tu kua kuna kitu kimeshushwa ghafla somewhere in life time ya mhusika ingawa juzi tulimfahamu sana si kiivyo?

Na kwa nini Mtu tunamuona/fahamu kabisa kua pale alipo anafanya kazi ya Uchungaji lakini hajiiti/itwi Mtume na Mchungaji au Nabii na Mchungaji lakini inapendelewa combination ya Mtume na Nabii? why?

Vipi Mtume akiwa huduma yake ni Mjini/Jijini tu ila maporini, machakani, upaganini, kizani ambako hakuna Kanisa wala Injili, hakanyagi, tukimponda-pinga, kosoa, sahihisha, kataa, kemea,vunja nk- kua ni mjanja tu, tunakosea?

Dah! Press on,

Edwin Seleli

Advertisements

12 thoughts on “MTUME na NABII kama si MTUME au NABII!

 1. Haleluya
  Karama/uduma za rohoni alizitoa Bwana/Roho mtakatifu.
  Kuzipima karama/uduma kama nizakweli tunamuitaji Roho kutuambia nani ni nabii/mtume wa kweli au wa uongo,na ziad tunaitaji kujua majukumu ya kila mtumishi mwenye huduma/karama usika kwani mgawanyo wa karama/uduma ndiyo unamfanya mtumishi kuwa mkuu au lah Mungu umtukuza yule amtakaye,sasa kama majukumu ya mtume na nabii yanamfanya kuonekana kuwa mkuu kwenye nyumba ya Bwana mtakuwa mnatumia akili ya shetan kupingana na watumishi wa Mungu,

 2. MTU AKIJIITA MTUME NA NABII, TAYARI HUYO NI KRISTO WA UONGO NI YESU PEKEE ALIYEWEZA KUBEBA SIFA ZA MTUME WAKATI HUO HUO NABII.
  HIZI NI KARAMA AMBAZO ROHO MTAKATIFU HUZITOA SI MTU KUJIPA.

  MITUME WALITEULIWAJE? MUNGU HUWACHAGUA, HAWAJICHAGUI NA KUJIPA MAJINA, BALI KIBARAZA KILIKAA.

  MATENDO 1:24-25
  “KISHA WAKAOMBA, WAKASEMA, WEWE, BWANA, UJUAYE MIOYO YA WATU WOTE, TUONYESHE NI NANI ULIYEMCHAGUA KATIKA HAWA WAWILI, SHIKE MAHALI KATIKA HUDUMA HII NA UTUME HUU, ALIOUKOSA YUDA, AENDE ZAKE MAHALI PAKE MWENYEWE.”

 3. Thobias Mosha,

  Ha ha ha ha .. Mitume na Nabii wa leo ”’hawana uwezo wa kuponya mafua acha ukoma”, kweliiiiiiiiiiiiiii, tena wapo wapo tu na mishe mishe town, shekeli looking from their Kondoo and kujenga Kingdoms zao

  Press on

 4. anaweza kuwa mtume na nabii kwa kujiweka yeye mwenyewe ila matukio ya utumishi ndio yanaamua mitume wa siku hizi wengi wapo mijini na hata hawana uwezo wa kuponya mafua acha ukoma na mengineyo usitishwe na majina makubwa

 5. “Maana “UNABII ” haukuletwa po pote kwa mapenzi ya Mwanadamu, bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu. (2 Petro 1:21)…..Jambo la ajabu ni kwamba asilimia kubwa ya hao wanaojiita manabii na mitume wa sikuhizi hata neno la Mungu hawalijui vya kutosha!!. Sasa hapo utaona jinsi watu wanavyopotoshwa kwa kupenda Miujiza badala ya kupenda neno la Mungu. Mimi napita tu jamani, mbarikiwe na bwana.

 6. Kw uelewa wangu, karama za huduma sawasawa na EFESO4:11, zipo ndani ya mtu tangu alipokuwa agent wa Shetani, tofauti na Karama saidizi kama vile Kunena kutafsiri Lugha, Neno la Maarifa na Hekima, uponyaji n.k ambazo huja baada ya mtu kuwa Agent wa Mnazareth. Hivyo, hizi karama za huduma mtu anapokuwa jna lake limehamishwa kutoka ktabu cheusi kuja kile kipya na safi cha uzima, anaanza kuzitumia hizo karama kwa upande wa YESU na Injili yake, mfano: amaye mambo mengi hufanyika vyema kirahisi na kwa haraka akiwepo, na ambaye ni mwanzilishi wa vikundi mbalimbali wakati hajampa Yesu maisha, labda tuseme mhuni anayeanzisha magenge ya uporaji n k yaan yeye anakuwa mwanzlish na kiongozi huku akitafuta wanachama wengi zaidi, huyu akiongoka huwa mwanzilishi mzuri sana wa vyama vya kitume, fellowship ktk maeneo mbalimbali, n.k huyu hivyo ni mtu mwenye karama ya UTUME, ambaye alipokuwa katika mikono ya ibilisi alitumia kufanya utume wa ibilisi, MTUME hatulii mahali pamoja huzunguka zunguka kuhakikisha habari njema inawfika wote na pia hupenda sana kutoa nafasi za kujaribu ili kuinua vipawa vya waamini, mtu ambaye yuko stationery na aliye kalia huduma zote tunapata shida anapojinadi kuwa yeye ni mtume, maana amekosa sifa Msingi za kitume!
  Pia tuseme labda mtu ni muongeaji sana kila maada anependa agusie na kutia neno lake ,huwa mara nyingti mhubiri anapomuongokea Kristo. nakadhalika na kadhalika

 7. Salele haya yaitabiriwa na yameandikwa kwenye biblia, manabii wa uongo wengi watatokea, wengi wengi sio wachache. Nakubaliana na ndugu John hapo juu anayejikweza, anayedharau wengine na kujiona yeye ndiye pekee au yuko juu, anayependa pesa wote hawa ni manabii wa uongo. Na kwa siku za leo sioni haya kusema yawezekana kabisa asilimia 98 ya manabii ni waongo, hiyo 2% nimeiacha tu lakini nayo sidhani kama wapo wakweli kufikisha kiwango hicho.
  Hawana wanachoweza tabiri lakini wanatumia psychological manipulation kudanganya watu. Ni nabii yupi aliwahi lionya taifa kwa majanga yanayokuja, au hata kusema tu kwa neema zilizoko mbele. Manabii waleo wanahangaika na human psychology ambayo hatima yake hubaki kuwa tata usipofanikiwa unaambiwa hunaimani ya kutosha, ukifa na ugonjwa unaambiwa hakuamini sawasawa. Hata hao wa utajirisho ni nani aliyetajirikia kwake ajitokeze tumuone, siongelei kuwa na nyumba, gari, biashara au kakiwanda uchwara, ninamaanisha mtu kuwa tajiri. Maana hivyo hata wasiokuwa kwa manabii wanapata na kuzidi hivyo. Manabii waleo ni kama tawi jingine tu la kisiasa wa kitanzania, wahangaika na kutafuta mali tu na hawana wanacho fanya kwenye ufalme wa Mungu.
  Wamejaa kujikweza tu na kudharau wengine ilihali maisha na mwenendo wao hauwatofautishi wengine kama wanasiasa, wa wachoyo, wabinafsi na ndio maana hawana ujasiri wa kuwasema viongozi wanaofanya mambo kiholela kwa maslahi binafsi maana siku wakisema yatawatokea puani.

 8. PRAISE THE LORD

  Kwa Mungu hakuna huduma ndogo ,zote ni kubwa na hutenda kazi kwa ushirikiano, ni sawa sawa mwili na viungo vyake, jinsi utakavyoifanya kazi ya mungu kwa bidii ndipo huduma yako huonekana kubwa kwa uaminfu.

 9. ilianza kama utan na sasa iko serious kabisa. eti kwamba kuna grades kwenye utumishi! eti kwamba nabii yuko juu ya wote! eti kwamba anafuatia mtume, halafu mchungaji, mwalimu ndipo makanjanja wainjilisti!!!UKITAKA KUJUA KWAMBA HUYO NABII NI MUONGO UKIONA ANASISITIZIA UKUBWA AMA CHEO WAKATI YESU ALISEMA ANAYETAKA KUWA MKUBWA NA AWE MDOGO WA WOTE! NIMECHAGUA KUWA MDOGO WA WOTE ILIMKRISTO ATUMIKE NDANI YANGU KWA UAMINIFU

 10. Naungana na Annastellah kwa mawazo yake. Lakini tukumbuke pia kuwa hizi ni siku za mwisho, na haya yote yalitabiriwa kuwa siku za mwisho watazuka manabii wa uongo, nao tutawatambua kwa matendo yao. Manabii wapendao pesa kuliko kumpenda Mungu, wenye kujisifu, wasiopenda kukemea dhambi. Mimi kwa ufahamu wangu wa dini tangu nilipopata akili, ninapoona mtumishi yoyote hakemei dhambi kanisani, huyo nina mashaka naye, maana sio kazi aliyoitiwa. Dhambi ndio suala la kwanza kukemewa sio kupiga brashi!! Waumini wa leo ni kukimbilia miujiza ya pesa kwa hao mitume wa sasa, nguvu zao kubwa ni kuwatajirisha watu na kuwajaza mambo ya dunia, maana tunaambia kila kitu kitapita lakini neon la mungu halitapita kamwe. sasa kama Nabii hakemei dhambi ama hana ratiba ya kuwaleta watu kwa Yesu, lazima uweke ???? kwenye huduma yake.
  Tunaomba wao wanaotoa huduma hizi watusaidie kujibu.

 11. Da! mtumishi umeongea la maana sana minatoa wito kwa mitume na manabii watusaidie kujibu haya maswali. maana asilimia kubwa ya mitume na manabii wa kizazi hiki ni waongo kabisakabisa. sikatai mitume wapo na manabii wapo kwa matunda yao tunawagundua na wala hawajitangazi tukonao makanisani wengine wako chini ya wachungaji wanafanya kazi ya Mungu bila misifa na wengine ni wachungaji lakini wanahuduma hizo tunawagundua bila wenyewe kujitangaza. lakini nyie nnao jinadi na kujisifia nawaonea huruma sana maana mmesha pata thawabu zenu hapa hapa duniani.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s