UAMINIFU!!

uaminifu

Asifiwe Mungu Baba

Katika Mwana na Roho Mtakatifu Amen.

Wapendwa awali ya yote kwanza nipende kumshukuru sana Mungu kwa neema yake juu yetu na kwa uzima na afya hii tuliyo nayo ambayo kwa namna moja ama nyingine kwangu imekuwa ndiyo mtaji mkuu katika kumuishia Mungu, haleluya.

Ingawa sijajua kwa upande wako waitumiaje neema hii ya uzima na afya alokujaalia Mungu lakini hilo libaki kama lilivyo maana Mungu zaidi ndiye ajuaye ya sirini mwa moyo wa mwanadamu basi kila mtu kama alivyo na aseme na moyo wake.

Watu wa Mungu aliye hai; imenipasa kusema nanyi katika siku hii ya leo jambo moja tu dogo lakini lenye nafasi kubwa sana katika kuishi kwetu ambalo kwa namna moja ama nyingine kule kuonekana kwake kuwa dogo pengine kunaweza kutufanya tukawa ni wenye kulidharau sana.

Limenenwa kwa sana masikioni mwetu, limesemwa kwa sana machoni petu na tumehubiriwa sana katika ibaada na makusanyiko yetu ya kila siku lakini pengine kwa wingi wa kusemwa sana kuhubiriwa sana halijapata nafasi ndani ya mioyo yetu hivyo nalo huja na kuondoka kana kwamba ni tusi kwetu hata lisipate kuheshimiwa na kuthaminiwa.

UAMINIFU, neno hili ni dogo kwa udogo wake katika muundo wake kwanzia matamshi na kiuandishi wake lakini lililo kuu sana lenye maana kubwa na lili pana sana kwanzia Rohoni na Mwilini pia.

Mtu alitendaye neno hili sawa sawa na kabisa na jinsi maana yake ilivyo basi ni kwamba ameipata nyongeza iliyo kuu sana zaidi ya kule kuishi kwake, uhai wake, na vingine vyoote alivyo navyo mtu huyo.

Ndugu Uaminifu ni Roho kama zilivyo roho zingine za Upole, Wema, Huruma, Unyenyekevu, Utulivu, Upendo, Uvumilivu, n.k

Pamoja na hayo yoote UAMINIFU ni roho ambayo ikienda sawa sawa na roho zingine zote basi hakuna jambo baya ambalo mwanadamu anaweza kulitenda kwa mwingine kwa sababu ile roho ya uaminifu i hai kwake hivyo na hizo zingine zote zinakuwa hai ili kutenda kazi sawa sawa na mapenzi ya Mungu.

Kwa nini? Kwa sababu MUNGU ndiye yeye aliye UAMINIFU hivyo na mtu uwapo mwaminifu katika roho unakuwa mwaminifu katika mwili mwili pia na hivyo ubaya kwako mwenyewe na kwa mwingine hutaufanya. Amen?

Jifanyie uaminifu basi wewe ndugu yangu usiwatende mabaya wengine naam na Mungu atatajwa kwako vyema wala hautakuwa tukano la Mungu mbele ya wapumbavu wasema hapana Mungu ila uovu tu. Sema Amen

Ufanyie uaminifu mwili wako ukivitenga viungo vyako vyote kwa ajili ya Mungu na ndipo mabaya yote yatakuwa mbali nawe ili Mungu apate kunenwa vyema kwa kukumiliki kwake. Sema Amen

Mfanyie uaminifu mwenzio ili yeye amuone Mungu katika maisha yako nawe upate kuwa alama ya uwepo wa Mungu duniani katika mwili. Sema Amen

Yafanyie uaminifu maisha yako ukitamani kukosa pamoja na Mungu kuliko kupata pamoja na shetani ili kuifurahia dunia. Sema Amen.

Yafanyie uaminifu mahubiri uyapatayo kila siku toka kwa watu wa Mungu mbali mbali ili yapate kukubadilisha kimaisha. Sema Amen.

Mfanyie uaminifu Mungu upate kudumu ukitenda mema ili wewe uwe sehemu ya utukufu kwake na watu waseme Mungu wako anastahili sifa kwa aina ya kuishi kwako. Sema Amen.

Maana imenenwa iweni “waaminifu” hata kufa.

Mungu awabariki

Awape nguvu kutenda uaminifu.

Amen

–Mwamfupe Anyisile

Advertisements

9 thoughts on “UAMINIFU!!

  1. Ubarikiwe Sana mtumishi, hapa Mungu amesema na mimi moja kwa moja, ni ne o lente nguvu za roho wa Mungu.. Naomi nasema AMINA

  2. nimebarikiwa sana kwa kunifundisha yale sikujua Mungu wa amani akubariki

  3. Inapokuja isues of faithfullness and intergrity hapo ndipo napoamin hakuna atakae mwona mungu kwa matendo ya sheria!! ¶ its just by bgrace!!!!!!”!

  4. Ubalikiwe kwa kuleta hoja hii ukweli moja ya dhambi itakayo wapeleka wengi motoni ni hii mfano (1),kukosa uaminifu katika zaka (2).kukosa uaminifu kwa habali ya kukusanyika pamoja yaani kuhudhulia ibada(3). kukosa uaminifu ktk kunena yaani leo watu ni waongo,wasingiziaji (4) ,kukosa uaminifu kwa wachumba,wenzi wetu nk kweli Mungu atusaidie

  5. Amina mtumishi wa Mungu uaminifu ni jambo muhimu na nigumu ukijaribu kwa akili zako. ila tunayaweza yote katika yeye atutiae nguvu

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s