Je mtu aliyeokoka aweza kupoteza wokovu tena?

kupotea

Wapendwa Bwana Yesu asifiwe! naomba ufafanuni wa kina katika mada tajwa hapo juu!

Ahsanteni,

Erasto.R Mazengo,
  
Advertisements

191 thoughts on “Je mtu aliyeokoka aweza kupoteza wokovu tena?

 1. Mjema,

  Nfikuru baada ya kupotea muda mrefu ulitakiwa ufyatilie kwanza tumefika wapi ndipo yseme unachosema.

  Mada hii imeshahamia kwingine panaitwa Hapo Bwana ajapo.

  Hata hivyo, vitu vingi ulivyosema mlishasema sana.

  Sasa unaposema kuwa Yesu akirudi anatuletea uzima wa milele huo kwangu naona ni upofu wa maandiko na kutanguliza wazo la kufikirika zaidi.

  Yaani wewe mpaka sasa hujui kuwa uzima wa milele upo unasubiri Yesu akirudi ndo aulete? Hii ni ajabu sana!
  Anyway, mimi uzima wa milele ninao hata sasa! Wewe endelea kuusubiri!

  Neno atakayevumilia hadi mwisho ndiye atakayeokoka mmelisema sana. Hebu sasa tuliangalie kwa kuwauliza swali hili : Waliokuwa wanaambiwa hivyo ni akina nani na huo wakati unaosemwa unawahusu akina nani na itakuwa lini?
  Hebu hiyo story yote kisha unipe majibu!

  Ukipomjibu yule aliyesema ameokoka lakini anadumbuliwa na nguvu za giza nilijua kuwa baadae utakuja tu useme mambo fulani kama ulivyosema hapa.
  Ndio maana hujaona nimechangia chochote.

  Point si kuokoka duniani, bali ni ufahamu wa huyo anayedai kusumbuliwa na nguvu za giza yuko hatua ipi katika process ya wokovu.
  Anaweza kusema ana miaka kumi lakini kumbe ni mchanga kabisa anayehitaji maziwa.

  Ishu si miaka ila how much unaijua kweli ili ikuweke huru kwelikweli.

  Nenda mada ilikohamia tafadhali!

 2. Sungura,

  1.Mathayo24:13-“atakayevumilia hata mwisho ndiyo atakayeokoka”

  2.Waebrania 11:13 “Hawa wote wakafa katika imani, wasijazipokea zile ahadi, bali wakaziona tokea mbali na kuzishangilia, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya nchi”.

  3.1kor 15:26- ” Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti. ”

  Rafiki, Wokovu ni mpaka mwisho wa pambano; Hata babu zetu walitazamia ahadi za hizo hadi wanaenda kaburini hawajaipata na Adui wa mwisho ni mauti.Kama Yesu alivyoishinda ndiyo ahadi yake kwa wale watakaovumilia hadi mwisho wa wakati.

  Hata hivyo; nimekuwa mvivu kuchangia mada hii maana kwa sababu nilishajua kuwa tunatofautiana mitazamo ambapo, wewe Sungura & Co. mnatazama mibaraka/Merits za kumpokea Yesu kama Wokovu na ambao ninyi wenyewe mmekiri kuwa UNAPOTEZEKA i.e kusema umeokoka Past na Present sio lazima uwe umeokoka in Future. Kwa maneno mengine Sungura umedai kuwa Wokovu unapotezeka na sio lazima kuwa wewe unayesema kuwa umeokoka eti uwepo mbinguni.Hata hapa SG, yupo mwenzenu anayesema ameokoka miaka 10 iliyopita, lakini anakiri kuwa nguvu za giza zinamsumbua… ajabu kweli.. na bado amekaririshwa… ” NIMEOKOKA..” na hapo umbandui ukitaka ugomvi mwambie hujaokoka.

  Kwa Upande wetu mimi & Siyi tunaamnini kuwa wokovu haupotezeki na ili kusema nimeokoka ni mpaka mwisho wa pambano Yesu ajapo ambapo hata waliolala ndio kwanza watasema Wameokoka kwa kuwa dhambi na muasisi wake sehtani watatoeshwa milele na Mauti haita kuwepo tena milele.

  Sungura, Yesu akija mara ya pili sio kwamba anakuja kutupa zawadi ( Zawadi itatolea Yesu atakapokuja Mara ya Tatu baada ya Miaka 1000-yaani mauti & Uzima wa milele) kama unavyodai Sungura bali anakuja kutupa WOKOVU usiopotezeka kwani Neno la Mungu linasema:

  1kor 15:26- ” Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti. ” NA

  Waebrania 9:28-….hali kadhalika Kristo alitolewa kama dhabihu mara moja tu ili azichukue dhambi za watu wengi; naye atakuja tena kwa hao WAMTAZAMIAO KWA WOKOVU….

  Suala la PAST,PRESENT… FUTURE linakosa mashiko kwani umeshaonyesha kuwa wapendwa wanaosema kuwa wameokoka Jana na Leo sio lazima wawemiongoni waliokoka Kesho…..

  Ushauri wangu-Badala ya kuwafanya watu wawe na kiburi kuwa wameshamaliza pambano leo ni bora Wautazamie Wokovu uliotajwa Ebr9:28

  Ubarikiwe.

 3. Siyi,

  Maelezo yako kuhusu maandiko yanatakiwa yawe kwenye sphere ya neno la Mungu.
  Acha kuongea maneno bwerere halafu unarahisisha tu kwa kusema hayo ni maneno yako wakati yametoka katika muktadha wa neno la Mungu!

  Mimi nitahayari na nini, wakati wiki mbili sasa nakungoja hufiki? Wewe njoo na kila unachojua na ulichonacho utanikuta!

  Siku ya mwisho ni kufufuliwa wala si kuokolewa!

 4. Sungura,
  Kama ni maelezo yangu, wewe ni nani hata uniwekee mipaka ya kusemanini na nini nisisseme? Kama kweli ingekuwa kwenye mstari wa Biblia, hiyo ndiyo ingekuwa hoja. Lakini ni kwenye maelezo yangu kumbe!! aaaa!!, Pole bwana.
  Akili yako huenda ndiyo ngumu kuelewa. maana tangu mwanzo nilikuuliza utofautishe kati ya kukokalewa na kunyakuliwa. Madude uliyonipa, yalinitia kichefuchefu tu. Sikuamini kuwa haya nayo yametoka kwa Sungura.
  Sasa tusiende kokote.Nataka tujadili maana ya WOKOVU tu basi. Na hili tutaliangalia kuanzia Agano la Kale hadi Jipya. . Hapo ndipo tutaona kama ulikuwa sahihi ama la!! Huna haja ya kutahayarika kijana. Wewe ngoja, nakuletea dondoo.
  Siyi

 5. Siyi,

  Utaniita vyovyote utakavyo, lakini ukweli ni ukweli hauwezi kushindwa na uongo.

  Ni vigumu sana, in fact haiwezekani kuipinga mistari iliyojaa kwenye biblia inayosema tumeokolewa, na tunaokolewa.

  Lakini pia wewe siyo slow learner tu, bali ni mgumu kabisa wa kuelewa hata ukirudia kusoma kitu mara ishirini.

  Unachoniambia nimechemka ni wagumu wa kuelewa tu kama wewe wanaweza wakashindwa kukielewa na kunilipukia kwa pupa kuwa nimechemka.

  Kasome tena labda safari hii utaelewa.

  Nimekwambia kwenye maelezo yako ( siyo maelezo ya biblia) umeongeza maneno “siku ya mwisho”

  Wala sijakwambia kuwa umeongeza neno siku ya mwisho kwenye mstari wa Yoh6:37

  Au hujui maana ya neno maelezo yako!

  Basi fanya zoezi la kuwa quick learner labda itakusaidia.

  Ngoja niongeze na mengine:

  Kwenye maelezo ya Yesu hapo hajaongelea suala la kuokolewa siku ya mwisho, ila ameongelea suala la kufufuliwa siku ya mwisho.

  Na hao watakaofufuliwa siku hiyo ni wale ambao tayari wana uzima wa milele ndani yao.
  Sijui wewe umelitoa wapi hilo la kuokolewa siku ya mwisho!

  Nafikiri ni kule kusoma mstari huku ukiwa na mapokeo fulani hivyo kushindwa kuona inachosema na kuona unachodhani.

  Kwenye hiyo sura hakuna neno kuokolewa siku ya mwisho, ila kuna neno kufufuliwa si ya mwisho!

  Siyi, wewe hauko makini na ni mpotoshaji!

  Prove me wrong!

 6. Brother Siyi,

  Nakungoja tu maadam utakuwa umejitenga na hiyo miungu yako. Yesu anakupenda, njoo kwake.

 7. Sungura,
  Nitakuja tu. Mimi na wewe kasi hatufanani. Hata namna ya kusoma mapachiko, mimi huwa naenda slowly but sure!! Wewe huwa unaenda tuuu fasta na hatimaye unaishia kutoelewa au kutoka na maana isiyo sahihi. Hili nimeligundua kuwa, wewe huwa uko fasta sana kusoma mapachiko ya watu ndiyo maana huwa unaondoka kappa!! Kwa mfano, umeniambia nimepotosha Yohana 6:37 inayosema, kuwa, “Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe”. Sasa hiyo phrase ya uliyoiongeza wewe –“siku ya mwisho” kwenye aya hiyo, uliitoa wapi? Umeangalia vizuri kweli kwenye pachiko langu hilo kuna makosa hayo uliyoyabaini wewe?? Hebu rudia tena kulipitia!! Nakushauri uwe unasoma polepole ili uelewe. Vinginevyo, utazidi kuwa mbishi tuuu kumbe mwenye tatizo ni wewe mwenyewe!!
  Kuhusu wokovu usiopotezekea, wewe subiri. Nakuja tu. Mimi huwa sibahatishi kama wewe. Nitakupa na references zote. Wokovu ni kuchagua. Ni kuamua kaka. Hauji kama ajali!! Wenzio tulishaamua kuchagua!! Wale wanaomfuata Kristo kwa ukamilifu, ndio watakaookolewa. Hakuna mtu anayemfuata Kristo bila ya ukamilifu bado akaendelea na sifa ya kuwa mfuasi waKristo. Akina Yuda, hawakuwa wafuasi wa Kristo, japo kwa macho walionekana hivyo. Kuna wengi leo Siku za Sabato huenda kanisa wakijidai kama wakristo ni “.. watu waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo” Yuda 4. Watu wa namna hii huwezi kuwaita wafuasi wa Kristo japo wamo ndani ya kanisa. Wala huwezi kusema kuwa wana wokovu na siku ya mwisho, watapoteza wokovu kwa maana hawamfuati Kristo kwa ukamilifu. Wale ni waasi kabisa hata Kristo hazitambui ibada, sadaka na huduma zao wanazodhani ni za kiimani. Mungu yuko makini mno. Huwezi kuwa vuguvugu kwake. Mungu ni Moto. Kamwe hatakuwa Moto na Baridi. Wala hatakuwa baridi. Hivyo usidanganyike kuziruhusu hekima za kibinadamu (ambazo ni upuuzi mbele zake), ziapply kwenye neno la Mungu!! Utaishia hewa tu!! Wewe kaa mkao wa kula. Jiandae kuunywa mchuzi wa mbwa ungali wa moto!!
  Siyi

 8. Siyi,

  Ivi mbona hufiki, kila wakati unaniambia tu unakuja?

  Mbaya zaidi kuna kitu unataka kutupotosha kwenye kitacha ulichonukuu , cha Yoh 6:37.

  …whoever comes to me, I will never send him away. Kwenye huo mstari hakuna neno ‘siku ya mwisho’

  Lakini wewe kwenye maelezo yako unasema hivi; ..ukimwendea kwa ukamilifu wote siku ya mwisho huwezi kupotea”

  Halafu huwa nakwambia kuwa unabisha kitu ambacho hata nafsi yako inakusuta, bt unanikatalia. Ona tena hiki kitu kwenye sentensi yako.

  Umesema kuwa “ukimwendea kwa ukamilifu…”. Hii ni condition ya namna ya kumwendea. Kwa hiyo ukimwendea si kwa ukamilifu unapotea.

  Na kutembea kwa ukamilifu ukiwa ndani ya Yesu ni ku-exercise imani katika Yesu. Ukiacha kufanya hivyo unakuwa umepotea na kutokuwa miongoni mwa wale atakaowafufua siku ya mwisho!

  Kwa hiyo siku ya mwisho ishu si kupatikana wala kupotea, ispokuwa ni kufufuliwa. Na huko kufufuliwa kunawahusu wale tu ambao walishakuwa mali ya Yesu tayari!

  Tumia neno la haki kihalari!

 9. Mjema,
  Endelea kutuombea kwa umoja wetu. Mungu anatupenda sote.
  Neema ya Bwanaikufunike.
  Siyi

 10. Ziragora,
  Nina habari njema kwako-kukuletea habari za Mungu asiyejulikana kwako ambaye unamwabudu! Nitakuja!
  Siyi

 11. Sungura,
  Acha mbwembwe rafiki yangu. Mimi nilikwambia kuwa, Sodzo na Soteria, ulichemka kaka!! Ndiyo maana hutaki kuileta hapa. Na wanaSG wajue wote kuwa, kwa fafanuzi zako hizo za SOdzo na Soteria, uliwadanganya na hivyo huna budi kuwaomba radhi. Inabidi ufanye hivyo kabisa. Maana ulisema kitu ambacho huwezi kukithibitisha –uwongo, uzushi na heresy tupu!!
  Wokovu wanaoufundisha akina Siyi, nilikwambia kuwa ni wokovu usiopotezeka. Yesu alisema, “Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe”- Yohana 6:37. Yesu tunayemwabudu sisi, ukimwendea kwa ukamilifu wote, siku ya mwisho huwezi kupotea. Kama ninyi akisa Sungura mna yesu wenu anayeweza kupoteza mtu, endeleeni na yesu wenu huyo, wa kwetu sisi hapotezi!

  Baada yaw ewe kushindwa kabisa kutetea source ya definitions za Sodzo na Soteria, mimi nitakuletea muda si mrefu. Endelea kuningoja.
  Siyi

 12. Wote;

  ” Yesu…akawafunulia akili zao wapate kuelewa na Maandiko…” Luka 24:45

  Mungu na atusaidie.

 13. Ndugu Siyi,

  Hoja iko, kwani sitachoka kukwambia uachane na miungu yako.
  Wewe unawaza hoja ni kuandika mingi?

  Asante.

 14. Siyi,

  Kunapotokea chance ya kuongea maneno matupu nakuona unavyochonga kwa wingi wa meneno.

  Ni kitu cha ajabu sana kung’ang’ania kupewa tofauti ya kunyakuliwa na kuokolewa. Je kweli kwamba hujui au unajaribu kufanya trick za kifarisayo?

  Kunyakuliwa ni kitendo cha kanisa kutwaliwa Yesu ajapo mawinguni. Ambapo walioaga dunia na kulala ktk Bwana watafufuliwa kwanza ili kumlaki Yesu mawinguni.

  Kuokoka ni kile kitendo cha kutolewa/ kuhamishwa toka katika ulimwengu wa giza na kuingizwa ktk ulimwengu wa nuru kwa mtu anayempokea Yesu.

  Siyi nakwambia tena kuwa dhana ya once saved always saved uliyoing’ang’ani kwa kusema kuwa ndio msimamo wetu ni kukosa uungwana.

  Maana ya hiyo dhana ni kwamba mtu akishaokoka hawezi kupoteza huo wokovu no matter what.
  Ambapo kimsingi na wewe unasimamua hiyo kuwa mtu akishaokolewa ameokolewa.

  Sisi kwa uwazi kabisa tumekwambia kuwa mtu anaweza akapoteza wokovu pale anapoasi, kama ambavyo Yuda katuonya katika Yuda 1:5

  Hebu na wewe weka hapa msimamo unaousema ni Mungu ambao uko tofauti na wa kwetu. Tuonyeshe ambapo Mungu kasema mtu hawezi kupoteza wokovu !

  Suala la Sozo na Soteria nshakwambia msimamo wangu kwenye ukurasa wa Huko Bwana ajapo!

 15. Sungura,
  Tangu siku ile nilikuuliza tofauti ya kuokolewa na kunyakuliwa, lakini uliingia mitini. Leo tena nakuona hoja hiyohiyo uliyokimbia kuijibu, bado unaijengea hoja!! Kama si ufedhuli ni nini kaka!! Jibu hoja tafadhali.
  Nashukuru kama nini mna msimamo wenu tofauti na msimamo wa Mungu. Maana mnasema, “Sisi msimamo wetu ni kwamba mtu akiokoka anaweza poteza wokovu wake”. Mungu ana msimamo wake. Jaribuni kujitathimini kama mko sahihi na mtazamo wenu huo!!
  Nilikwambia utoe rejea na siyo fasili ya Sodzo na Soteria, lakini unakimbia na kulalama weee. Najua unafahamu ulichokifanya ndio maana unapiga chenga!!
  Hutuwezi kuwa tunabashiri suala la wokovu kaka. Inabidi tuelewe maana ya WOKOVU kwanza, in relation to Christ. Ndiyo maana nikakwambia utupe rejea ya Sodzo na Soteria ili tuanzie hapo. Na kama ungekuwa muungwana, ungesema tu mbashala kabisa ni wapi ulikosea/ulituuzia mbuzi kwenye gunia ili tusaidiane maana sisi sote ni watu tu. Binadamu tu wenye mapungufu tena makubwa. Ni kwa neema tu ndiyo maana tumestahili tusichostahili.
  Mimi nakungoja ujibu hoja zangu;
  a. Leta rejea za Sodzo na Soteria with their meaninds
  b. Eleza/tofautisha kati ya kuokolewa na kunyakuliwa.
  NB: Kipengele (a) ndiyo cha muhimu zaidi kukijibu.
  Nakungojeni
  Siyi

 16. Ziragora,
  Tangu mwanzo uliishiwa hoja. Nikakuona kumwa umeishiwa hoja kabisa. Hata sasa, ilmradi unaandika tu basi. Lakini huna chochote unachoandika rafiki yangu. Naomba umsaidie Sungura kutoa rejea ya Sodzo na Soteria.
  Nataka tuanzie hapo kwanza na si kuuziana porojo mnakokufanya!
  NAwangoja!!
  Siyi

 17. Siyi,

  “Ndio maana hata waliokufa wakiwa wakamilifu kabisa, saa inakuja kristo atawafufua ili kuwatoa katika vifungo vya mauti, ili wasife tena. Huko ndiko kuokolewa anakokuzungumzia Siyi”

  Yes, huko ndiko kuokolewa anakokuzungumzia Siyi, lakini siko kuokolewa inakokuzungumzia biblia.
  Hicho kitendo biblia inakiita kunyakuliwa.

  Kusema kwamba huko ndo kuokolewa kwa maana ya kutolewa katika ulimwengu wa giza na kuingia ulimwengu wa nuru ni upofu mkubwa wa kutokujua maandiko.

  Halafu Siyi vitu vingine is just common sense.
  Unaposema siso tunaogelea katika dhana ya Once daved always saved, nafikiri ni kukosa umakini.

  Tafsiri ya hii dhana kwa Kiswahili ni sawa na kusema kuwa mtu akisha okoka hawezi poteza wokovu wake.

  Sisi msimamo wetu ni kwamba mtu akiokoka anaweza poteza wokovu wake.

  Ninyi mnaamini kuwa ukishaokoka wokovu huo haupotezeki.

  Sasa hebu tumia common sense hapo kujua kati ya sisi na ninyi nani yuko kwenye dhana ya Once saved always saved?

  Wewevnfo uko under hiyo heresy, in case kama ulikuwa hijui!!

 18. Siyi,

  Lile unalozusha tuliisha limaliza baadaye ukakwamia mu sabato. Hapa sasa mada unaigeuza dini. Msiwe wa kugeuzageuza mambo ili muonekane mna maarifa ya ujanja. Unapodhaifuka unakimbilia sabato, unapogongwa unakimbilia dini. Wewe unalifahamu dini langu kweli? Ukimuona hata mwengine anaeimbaimba dini, dhebebu, … fafamu kama ni yeye ndiye aliye ndani, kwani umevijuaje? Hivi unapojisahaulisha kama hapa ni kanisani na kusema isiyokweli ukihalalisha uongo unajisikia umeokoka? Kwani anaeruhusiwa jadili juu ya wokovu siyo muongo bali aliyeokoka!!! Usijiite aleyeokoka bali ujiite bumubishi na muongo.

  Asanteni.

 19. Ziragora,
  Naona na wewe umeanza kumenya mbuga. Mada siyo usabato. Na wala hatufanyi mchezo hapa rafiki. Hoja ni kwamba, je, kama wewe Ziragora, unasema umeokoka -una wokovu tayari. Je, wokovu huo unaweza kupotezeka? Kama ni ndiyo, je Yuda Iskariote naye aliokoka halafu akapoteza wokovu wake? Acha kubweteka kijana!!
  Mimi na wewe tunatofautina hapo tu. Mimi naamini kuwa, wokovu ni mchakato. Ili mtu afikie hatua ya kusema NIMEOKOKA, sharti awe amefikia hatima ya mchakato huo -yaani ametwaliwa mbinguni. Ndio maana hata waliokufa wakiwa ni waaminifu kabisa, saa inakuja Kristo atawafufua ili kuwatoa kwenye vifungo vya mauti ili wasife tena!! Huko ndiko kuokolewa anakokuzungumzia Siyi.
  Na wewe Ziragora unajidai huioni hiyo hoja japo iko wazi sana. Sababu ni udini na udhehebu uliowakaa. Na utawagharimu mno msipoangalia mapema maana doctrine hiyo ya “Once Saved Always Saved” ni heresy ambayo hamjawahi kuiona!! Ila kwa vile hamuielewi, na hamtaki kuiellewa, mimi nawaombea tu.
  Mngekuwa na hoja mngeijibu hiyo hoja yangu Biblically. LAkini kwa vile sasa, udini umewakaa, mtakufa kibudu msipoangalia.
  Wenu Siyi

 20. Siyi,

  Huwezi mfwata Yesu namna ulivyo. Au uko Yuda!!! Kwani kidogo tu atavunja vile visabato vyako, na utaanza mhukumu. Ya kwanza achana na vihekalu vidogo vidogo, ya pili umfwate Yesu. Usiifanye mzaha Siyi, utajikuta siku moja jehanum! Hebu fikirini, waliyokuwa kikwazo kwa Yesu kila siku siyo hawo wote waliodhani wanazitimiza sheria za Mungu? Mungu wetu ni Roho wala siyo Sabato. Sasa wewe tafuta mapema mbingu ya mungu sabato utakoyoingia. Huoni jinsi umegeuza mada ili uilazimishe iwe sabato?

 21. Sungura,
  Ha ha ha ha ha!!! To be paid is not to be saved!! Wuuuu!!!
  Kaka nilijibu mapachiko kama mawili matatu hivi (tar. 15 hadi 17). Bado hayajaruhusiwa. Nayaona yanasubiri moderations!!. Kabla sijajibu maswali yako uliyoniuliza, naomba unitofautishie kati ya;
  1. Kunyakuliwa na kuokolewa.
  2. Wale watakaonyakuliwa na wale watakaolipwa sawasawa na kazi zao, tofauti yao ni nini? Kila kundi litakuwa sehemu gani?
  3. Swali la Sodzo na Soteria, linahitaji rejea tu. Kwa maneno mengine, ulisoma wapi ili na mimi Siyi nikajiridhishe hapo?
  NB: Kama nilionekana kukutusi sana, wewe nisamehe tu rafiki yangu. Sikuwa na lengo la kutukana mtu. Naamini niliandika with a little irritations!! Huu nao ni udhaifu ambao sharti niushinde. Ndiyo safari yenyewe ya kiimani kaka. Nakungoja ujibu maswali yangu kwanza, ili nilete mwitiko kwa maswali yako fasta.
  Ubarikiwe sana.
  Nakungoja
  Siyi

 22. Siyi,

  Sikuwa nimeona comment yako ya tar. 13 kwa sababu na ya kwangu ya mwisho ilikuwa ya tarehe hiyoyo. Bila shaka zilikuwa moderated muda mmoja.

  Naona umeniita majina yote unayoona yanapendeza moyo wako kuniita. Well, hiyo siyo shida kwangu hata kidogo.

  Ninachosikitika tu ni kwamba unatumia paragrafu ndefu kuni-insult mimi badala ya kuongea substance inayohusu mada jadiliwa.

  Umekazia sana kuniambia nimekwama, sasa labda nioneshe nimekwama wapi.
  Lakini usije ukadhani kukujibu maswali yako kwa style unayotaka wewe ati ni kukwama, labda wew ndo utakuwa umekwama kuelewa.

  Kuna kitu kimoja kiko sensitive nakiona katika uelewa wako, hata Mjema pia.

  Mko na hii pre-conceived concept kuwa wokovu hauwezi kuwa wokovu mpaka tuwe tumewekwa mbali na hii dunia ambayo shetani yumo ndani yake.

  Kifikra ya kimantiki na kudhanika inaonekana ni dhana sahihi. Lakini katika mantiki ya uwezo wa Mungu ni dhana dhaifu sana maana inajaribu kuuhoji uwezo wake na kupingana na kile ambacho maandiko yamesema.

  Hebu imagine, kuna maandiko ya kutosha tu yanayosema ‘ Tumeokolewa’, lakini kwa sababu ya hiyo pre-conceived concept, Siyi/ Mjema anasema ‘no, hapo biblia inamaanisha kitu kingine. Maana hiyo dhana inamwambia kywa hicho kitu hakiingii akilini.

  Maandiko yanaposema ‘naye alituokoa…’ hiyo dhana inamwambia kuwa hapo yatakuwa yanamaanisha kitu kingine, maana bado tuko duniani.

  Lakini kwa nini dhana hii imepata nguvu?

  Ni kwa sababu ya kutojua maana halisi ya neno ‘Kuokoka’ kuwa katika lugha ya kimaandiko(biblia) lilitumikaje, hasa katika lugha za asili za maandiko.

  Ni sawa na biblia inaposema “kwa kupigwa kwake sisi tuliponywa” halafu unamwambia mgonjwa kwamba ‘wewe ulishaponywa’ lazima awe anauelewa uweza wa Mungu ili akubali hiyo kauli. Vinginevyo angependa umwambie kwa kupigwa kwake wewe utapona, hiyo ndo itaendana na ufaham wa mtu asiyejua uweza wa Mungu.

  Ndicho nikionachacho katika akili ya Mjema na Siyi. Madamu wao walishaaminishwa kwamba huwezi ukasema umeokoka wakati bado uko kwenye dunia ambayo umo. Na hili kwa mantiki ya kibinadamu, na kwa kutokujua kuwa neno wokovu ni collective ni sahihi kabisa kuing’ang’ania.

  Lazima sasa hawa ndugu niwaulize swali hili ” NINI MAANA YA KUOKOKA MNAYOJUA NINYI(Siyi na Mjema)

  Siyi najua unajua kuwa kanisa litanyakuliwa, na kutakuwa na harusi ya mwanakondoo. Baada ya hiyo harusi kutakuwa na utawala wa miaka elfu moja.
  Hebu niambie wakati wa huo utawala walionyakuliwa watakuwa wapi?

  Ivi inaposema biblia kuwa atakayevumilia hadi mwisho ndiye atakayeokoka, hilo neno ‘ ndiye atakayeokoka’ maana yake ni ndiye atakayetolewa duniani?

  Je, isemapo ‘aaminiye na kubatizwa ndiye atakayeokoka’ maana yake ni ndiye atakaetolewa duniani au atakaenyakuliwa?

  Siyi, unataka nini nifanye kuhusu neno SODZO na SOTERIA? Maana unataka nikupe rejea. Hebu iweke sawa unachotaka kuhusu hilo.

  It never says that he is coming soon to save, but it says ‘ am coming soon with ma reward to pay each one according to what he has done’. (Rev 22:12)

  To be paid is not to be saved!

  N

 23. Ziragora na Sungura,
  Inaweza kuwachukua muda mrefu kuelewa somo hili , lakini ukweli wake hautabadilika. Hakuna cha usabato wala umasalia. Kinachozingatiwa hapa ni utii wa neno wa neno la Mungu. Tusipokubali kukifuata kile Kristo alichokifanya pale msalabani, tusitarajie chochote kwa baadaye!! Tukipumbazika kuwa tumeokoka tukaduwaa eti na kutofanya lolote kwa ajili ya wokovu wetu, hatima yetu ni uangamivu milele. . Hatuna budi kuiacha dunia na mambo yake yote kwa ajili ya kile alichokifanya Kristo ili hatimaye tupate uzima wa milele. Enzi za Kristo akiwa duniani, Petro alihoji swali kama hilo,
  ” …Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata; tutapata nini basi?”
  Petro hakuuliza kuwa tumeshapata nini kwa kuacha familia zetu, kazi zetu nk. Aliuliza, kwa future tense, TUTAPATA nini basi???
  Jibu la Kristo nalo lilikuwa yakinifu kweli; “Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli”. mtt 19:27-28.
  Yesu aliwaambia, wataketi kwenye ufalme wake baadaye. Siyo sasa!! Sasa hivi, (tuliotambua ukombozi wa Kristo)tunajitahidi tu kuiacha ndunia na mambo yake kwa njia ya nguvu za RM. Hatima ya kuviacha vyote hivi, ni uzima wa milele. Lini? BAADAYE!!
  Mbarikiwe.
  Siyi

 24. Sungura,
  Nilikwambia umekwama rafiki. Nimekuona umemwuliza Mjema kuwa mtu anaweza kupoteza ukombozi?? Sijui atakujibuje!! Lakini ngoja tumsubiri. Mimi navyoona hizi athari za mafundisho yenu ya kizushi ndani ya makanisa yenu. Alichokifa Kristo msalabani, alikifanya kwa dunia nzima. Na wala hakitakuja kubadilika hata siku moja. Nipende nisipende Kristo alishafanya. Kilichobaki ni mimi tu kukikubali kile alichokifanya pale msalabani basi.
  Matokeo au malipo ya kukikubali na kukifuata kile alichokifanya Kristo, ndio huo wokovu. Kwa kukusaidia zaidi, fuatilia hilo fundisho lenu la NIMEOKOKA< NIMEOKOKA, limeingia lini ndani ya ukristo. Jaribu kulifuatilia. Huenda utapata msaada kwa hilo.
  Nakungoja ujibu maswali yangu.
  Siyi

 25. Ziragora na Sungura,
  Inaweza kuwachukua muda mrefu kuelewa somo hili , lakini ukweli wake hautabadilika. Hakuna cha usabato wala umasalia. Kinachozingatiwa hapa ni utii wa neno wa neno la Mungu. Tusipokubali kukifuata kile Kristo alichokifanya pale msalabani, tusitarajie chochote kwa baadaye!! Tukipumbazika kuwa tumeokoka tukaduwaa eti na kutofanya lolote kwa ajili ya wokovu wetu, hatima yetu ni uangamivu milele. . Hatuna budi kuiacha dunia na mambo yake yote kwa ajili ya kile alichokifanya Kristo ili hatimaye tupate uzima wa milele. Enzi za Kristo akiwa duniani, Petro alihoji swali kama hilo,
  ” …Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata; tutapata nini basi?”
  Petro hakuuliza kuwa tumeshapata nini kwa kuacha familia zetu, kazi zetu nk. Aliuliza, kwa future tense, TUTAPATA nini basi???
  Jibu la Kristo nalo lilikuwa yakinifu kweli; “Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli”. mtt 19:27-28.

  Yesu aliwaambia, wataketi kwenye ufalme wake baadaye. Siyo sasa!! Sasa hivi, (tuliotambua ukombozi wa Kristo)tunajitahidi tu kuiacha ndunia na mambo yake kwa njia ya nguvu za RM. Hatima ya kuviacha vyote hivi, ni uzima wa milele. Lini? BAADAYE!!
  Mbarikiwe.
  Siyi

 26. Sungura,
  Nilikwambia umekwama rafiki. Nimekuona umemwuliza Mjema kuwa mtu anaweza kupoteza ukombozi?? Sijui atakujibuje!! Lakini ngoja tumsubiri. Mimi navyoona hizi athari za mafundisho yenu ya kizushi ndani ya makanisa yenu. Alichokifa Kristo msalabani, alikifanya kwa dunia nzima. Na wala hakitakuja kubadilika hata siku moja. Nipende nisipende Kristo alishafanya. Kilichobaki ni mimi tu kukikubali kile alichokifanya pale msalabani basi.
  Matokeo au malipo ya kukikubali na kukifuata kile alichokifanya Kristo, ndio huo wokovu. Kwa kukusaidia zaidi, fuatilia hilo fundisho lenu la NIMEOKOKA< NIMEOKOKA, limeingia lini ndani ya ukristo. Jaribu kulifuatilia. Huenda utapata msaada kwa hilo.
  Nakungoja ujibu maswali yangu.
  Siyi

 27. Siyi,

  Si hivyo vihekalu vidogo vidogo unavyoita sabato na masabato?
  Ukiwa pamoja na mafarisayo na waandishi , nawe utasema Yesu asulubiwe kwani hakuheshimu sabato, wala hakunawa mikono….. Kwani inaonekana wokovu wako si rohoni. Sasa, pengine mwili yako ndo itaenda mbinguni na roho yako ife!!!

 28. Ok Mjema,

  Unataka tuwaambie watu kile ambacho wewe unasema au kile ambacho biblia inasema?
  Neni linasema tumeokolewa kwa neema, Yesu anasema tunapisali tumwombe Mungu atuokoe na mwovu, wewe unasema tuwaambie watu wataokolewa in future!

  Vipi kuhusu hili, je mtu anaweza akapoteza ukonbozi wake? Hebu toa jibu nikusikie.

  Halafu buo mstari uko kitabu gani unaosema Mungu si kigegeu atuokoe halafu kesho tupoteze wokovu? Nipe huo tafadhali!

  Hayo maswali uliyoniuliza hebu jaribu hata jumuuliza mwalimu wa biblia wa kisabato ambaye anaweza akasema ukweli bila kuwa biased uone atajujibu nini. Maana naona unashindwa kuelewa kitu chepesi sana.

  Ukishindwa kufanya hivyo, basi fanya hili jingine hata kwa kugoogle; tafuta nini maana ya Wokovu(Salvation), utakuwa umejifanyia favour kubwa sana.

  Unajaribu kuilazimisha akili ikupe mantiki ya kuokoka leo, kama ambavyo Nicodemus alivyojaribu kuilazimisha impe mantiki ya neno kuzaliwa mara ya pili. Hakuweza hata kidogo, zaidi ya kukubali mantiki aliyompa Yesu ambayo ni mantiki tu mtu anapoamua kuamini.

  Acha nikujibu hili ambalo nalo jibu lake liko wazi sana basi tu.
  Wokovu nitaupoteza tu ikiwa nitaamua kuasi, just kama walivyoamua kufanya wale walioangamia jangwani!

  Soma na haya maandiko; Hebrews 2:2-3, na ile Yuda verse 5 unayoifaham!

  Mjema, wewe ile sala ya Bwana huwa unaisalije pale kwenye ‘utuokoe na yule mwovu’?

  Mtu aliyeshinda huwa haji kuokolewa, huwa anapewa taji ya ushindi!!
  Yesu ajapo mara ya pili haji kutuokoa, anakuja kutupatia reward!

 29. Lwembe,
  Kama tulishakombolewa mara moja tu, je kuokolewa kuko mara ngapi???!! Naomba ujibu swali hili tafadhari with Biblical refences. Kwa maneno mengine, Kristo alishafanya yote mpaka sasa –kukomboa na kuokoa? How? Kama jibu ni ndiyo, unafikri bado ana haja ya kurudi tena kama alivyoahidi? Kuja kufanya nini sasa? Kama sivyo, unamaanisha nini kusema hivyo? Hebu nipe utofauti wa kuokolewa tukiendelea kuwa kwenye vita, majanga, ibilisi na malaika zake na kule kuokolewa kwa kuwekwa mbali na taabu zote akiwemo ibilisi!! Tafadhali nifafanulie hizo maana mbili za wokovu kiimani!!
  Zaidi ya hapo, nakuona unachomeka mafundisho ya umizimu, umizimu mtupu!! Mara Yesu alienda kuhubiri mizimu!! Mara dunia hii inatutunzia wokovu!! Sasa ni nani anayewatunzia wokovu hapa duniani? Ni dunia yeyenyewe au kuna kiumbe anayewatunzia? Haya ndiyo matatizo yanayowafanya kuimba nyimbo za NIMEOKOKA, NIMEOKOKA ilihali bado sana. Mwasema mu matajiri, hamhitaji chochote, mwaona n.k. kumbe mu vipofu, uchi na wanyonge mnaohitaji msaada wa Kristo ili kuushinda ulimwengu mfae kwa mavuno, mavuno ya baadaye.
  Tunawaombea sana, maana hatuoni nuru kwenu japo mwadai kuwa mko nuruni.
  Siyi

 30. Sungura,
  Nilijua tu!! You are very cunning brother!! Cunning indeed!! Very deceitful!! Ajabu safari hii umekwama sasa!! Kimsingi umekwama kabisa!! Nilitarajia utajikongoja kujibu hata hoja moja tu!! Naona zimekutoa jasho na kuziita upuuzi ee!! Hakuna hoja iliyokushinda kuijibu usiite upuuzi, ujinga, na blaablaa!! That is how you are my brother!!
  Zaidi ya hapo, huenda huwa unameza mazimamazima yale unayofundishwa na walimu wako wa uongo. Kama si hivyo, naomba rejea ya Sodzo = wokovu kwa Kiebrania na Soteria = wokovu Kigiriki. Naomba hizo rejea uthibitishe. Mwambie na Lwembe, Haule wakusaidie kukupatia hizo rejea!! Kama hakuna jambo lolote la wokovu lisilohusiana na kifo cha Kristo huku bado unasema kuwa waisrael kutoka Misri, ule nao ulikuwa ni wokovu kwao, je, kipindi hicho kulikuwa na kafara ya kristo?? Acha ufidhuli kijana!! Nilikwambia umekwama!!
  Na usifikiri Mungu kuwa huwa anafikiri kidogo kama wewe. Mungu ana utaratibu maalumu. Yeye ni Alfa na Omega. Alipanga kuwaijia baadaye wale watakaomwamini. Wajapokutwa hai, wajapokutwa walishalala, Kristo atakuja kuwaokoa wote! Kama angekuwa anachomoa kila anayemwamini, kusingekuwa na haja ya YEYE kurudi tena!! Kufanya nini kama kila anayemwamini anamchomoa kimyakimya mbinguni? Acha hila bro. Kama sisi akili zetu zina shida, basi zenu zina shida marudufu!!
  Usipotubu na kujiangalia upya, Usipowaomba msamaha hao uliowakosesha kwa muda mrefu hadi sasa, mauti inakuotea mlangoni.
  Ghairini, ghairini mkatubu. Mbona mwataka kufa (milele), enyi marafiki?? Ghairini tafadhali!!
  Siyi

 31. Mjema,
  Ubarikiwe mjoli. Sifa na utukufu kwa YEYE aliyetuita kutoka gizani na kuingia katika Nuru yake ya ajabu. Ujasiri uliouonesha Bwana atakujazi. Kazi uliyoifanya Mjema, is more exceeding! Exceeding indeed!! Usichoke kaka. Kikubwa kama ulivyosema, tuendelee kuwaombea marafiki zetu hawa. Ipo siku Bwana atawafungua!
  Kazi kubwa, umeifanya aise!! Naona umewafunga kamba shingoni hawa marafiki zetu –Sungura, Lwembe, Haule & Co. Wanang’ang’ana kufundisha fundisho la wokovu unaopotezeka!!!????????? Yaani hata watu nao hawashtuki jamani!! Ndume zimeng’ang’ana kabisa ooh kuna past, present …. Ha ha ha haa!! Kazi umeimaliza kijana ktk hili. Blesssed indeed, indeed!! Amina.
  Neema ya Bwana ikufunike daiama. Amina.
  Siyi

 32. sungura,

  Mzee wa nyakati! Mbona hujatafakari aya pacha ya “..utuokoe na yule mwovu” yaani “..usitutie majaribuni..”?

  Hebu twambieni wenzetu,majaribu yamekwisha?

  Halafu ikiwa kila siku unaomba “..utuokoe na yule mwovu” mbona ni ishara kuwa bado tu. Ingekuwa mmeshaokoka msiendelea kuiomba iyo aya “..utuokoe na yule mwovu” inhli hali bado mwovu bado yupo mtaendelea kuomba hadi mwisho wa wakati, na nikwa wale tu,watakaovumilia. Uangalieni wokovu kwa mantiki ya umilele na sio ule unaopotezeka!

  Usisahau kutafakari na kujibu maswali yangu, ili unisaidie.

  Tufunguliwe akili, Tuelewe na maandiko.

 33. Dah, Lwembe,

  Nilikuwa sijaiona hiyo katika sala ya Bwana kutoka kwenye hiyo angle ‘ utuokoe na yule mwovu’ Dah, kumbe tunaokolewa na mwovu! Hii ni wakati uliopo!

  Big up!

 34. sungura &co,

  Umejibu vyema!mnafundisha wokovu unaopotezeka!! Sasa ndo hapo hasa mkanganyiko unapoanzia, kumbe kusema kuwa “nimeokoka” leo haimaanisi kuwa nitakuwa nimeokoka mwisho wa siku Yesu ajapo. !

  Ona sasa mnafundisha wokovu unaopotezeka!. Sisi tunahimiza wokovu wa kudumu.Ndio hapo hasa tunapokinzana,uwezi kusema kuwa nimeokoka,nimeokoka! Wakati unajua kuwa haiwezi kuwa hivyo milele!

  Sio sahihi kufundisha wokovu wa kuunga,unga. Vipande,vipande,kuchomea,chomea, (piece meals).waambieni watu wautazamie wokovu (in future terms) ambapo mtu aupatapo hawezi kamwe kuupoteza! Huu ndio Wokovu hasa wakuwaimiza watu, sio kuwapumbaza pumbaza kwa maneno kuwa wameokoka na huku mwajua hasa kuwa kuna uwezekano wa kuupoteza!

  Sungura, ndio hapo hasa tunasema ili biblia isipingane, kuwa leo umeoko lewa na kesho waweza poteza wokovu izo aya unazosema kuwa zinasema tumeokoka na tunaokoka zipatane na tutaokoka. Na sio km mnavyodai ninyi kuwa tumeokoka,tunaokoka na Tunawezaokoka. Zingatia neno-tunawezaokoka-lina uwezekano wa kupoteza wokovu. Kuhusu Lenda na sisi na siyi, nimekuwa nikikumbusha mara kwa mara kuwa sio wasabato wote wanaosema hakuna kuokoka duniani! Kama ilivyo sio wajumapili wote wanaosema kuokoka ni duniani! Wote tunaendelea kujifunza.

  Mstari wa kuthibitisha ilo ni: Mungu sio kigeugeu hata hatuokoe halafu kesho tupoteze wokovu.mkono wake haukupunguka hata asiweze kuokoa.

  Ninachoamini, ni mtazamo tu tunatofautiana, wakati ninyi mnaupa uzito jana na leo, sisi tunahimiza mwisho wa pambano-kesho!

  Sungura, kumbe na wewe wajua kuwa ingawa leo wakiri kuokoka, kesho waweza usiokoke!wokovu unaopotezeka ajabu kweli.msimdhalilishe Mungu hayupo hivyo!

  maswali: 1.ni nini kinachookoka jana na leo(past.present),na nini kinaokoka kesho-future?

  2.ni nini kinachosababisha mtu kupoteza wokovu?

  3.Sungura, hv unaposema umeokoka unafikiri wewe na watu wanaokutazama mnafikiri kuhusu past&present tu au zaidi future-Yesu ajapo?.

  Ni kweli,tunaokolewa kwa neema, na ndio maana Neema iyo mwisho wake ni Yesu ajapo, siku hasa ya wokovu usiopotezeka!

  TUFUNGULIWE AKILI, TUELEWE NA MAANDIKO.YESU TUSAIDIE!

 35. Siyi, Mjema & co,

  Waliangukiaje tena mautini, humo walimotolewa ilhali wakiwa ni waliookolewa?

  Kama tulivyoona kwamba tulikombolewa mara moja tu, na kwa kukombolewa huko Tukaokolewa na Hukumu ijayo hapo Tulipohesabiwa Haki. Nako Kuhesabiwa Haki maana yake ni kurejeshewa Haki ya kuuendea Mti wa Uzima, ile iliyoondolewa kule Edeni, Mwa 3:22 “… na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala, akaishi milele” ndipo ktk Kuhesabiwa Haki tunapewa uwezo wa “kuuona Ufalme wa Mungu”, ule Mti wa Uzima, na kuianza safari ya kuuendea, tukiwa tumepewa na jinsi kamili ya kuufikia; huku ndiko Kuzaliwa Mara ya Pili!

  Nako kurejeshewa kwetu Haki ya Uzima wa Milele, si kukiondoa kifo au mateso ya jinsi ya mwili km kuumwa nk, haya yanaendelea kuwepo kwa kuwa yanaambatana na dunia iliyolaaniwa ambayo sisi tu sehemu yake, maana hii miili ilifinyangwa kutoka ktk huo udongo; lakini arabuni ya ukombozi wa miili, ndio huo uponyo wa kiUngu tuliopewa “kwa kupigwa kwake”, na mamlaka juu ya hali zote zenye kufisha tuliyo nayo ktk Jina la Bwana Yesu Kristo!

  Pia ieleweke kwamba ni ktk Kuhesabiwa Haki ndipo sisi husajiliwa ktk Jeshi la Kristo “kuipigania Imani! Hii ni vita ya kiroho tunayokutana nayo ktk Hatua hii ya Pili ya Utakaso, hapo tunapoianza safari ya kuuendea ule Mti wa Uzima, ni vita kali sana! Naye Mungu, ktk hatua hii hutupa mafunzo na silaha za kukabiliana na onslaught hiyo, Efe 6:10-11 “… mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.” Ni vita ya HILA inayohitaji uweza na nguvu za Mungu kushinda!!!

  Neno la Mungu ndilo pekee linaloweza kuifunua Hila, basi humo ktk Ghala ya silaha za Mungu, ili kupambana na hila hizo, anasema, “16 zaidi ya yote mkiitwaa NGAO YA IMANI, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. 17Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na UPANGA WA ROHO ambao ni neno la Mungu; 18kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho…”

  Siyi, hii ni hatua ya “combat”, yale mapambano ya mtu na mtu ktk vita! Si tulisoma kule kwamba kuna ambao majina yao hayajaandikwa ktk Kitabu cha Uzima, hawa ndio vyombo vya Shetani. Shetani anaweza kuigiza vipawa vyoote kasoro Upendo. Anaweza kuwa nabii au mwalimu au malaika wa nuru, au chochote kile ktk nyanja za dini, tena akawa na mafanikio makubwa sana, basi jeshi lote hilo limejipanga ktk Hatua hii kuhakikisha kwamba HATUVUKI kuufikia huo Mti wa Uzima; “12Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.”!

  Kwamba hii ndio Hatua ya HATARI kuliko zote, ninaamini sote tunalifahamu hilo. Hata ktk michango ya ndg Mjema na Siyi jambo hili limejionesha wazi na limekuwa ndilo kikwazo kwao wanapoitazama vita jinsi ilivyo kali, halafu eti mtu mwingine anakwambia kuwa yeye ameokoka na vita hiyo inayoendelea, naye akiwa frontline kama Uria, haiwaingii akilini kabisa! Jambo la Imani huwa haliingii akilini!!

  Katika Hatua hii, kwa kutindikiwa Imani, kundi kubwa la hao “… waitwao ni wengi” litaangushwa na kurudishwa mautini, majina yao yakifutwa ktk Kitabu cha Uzima! Yuda Iskariote, jina lake lilikuwemo ktk kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, yaani unapoongelea Wokovu, basi jina lako kuwemo ktk kitabu hicho si jambo dogo. Yuda alihesabiwa Haki, Akatakaswa lakini akajichafua, AKAFUTWA jina lake! Akina Anania na Saphira, walithubutu kumdanganya RM, ile KUFURU, kama ambavyo leo hii Cults zinavyotuingiza wengi wetu ktk kufuru; mtumishi anawaaminisha watu kwamba yeye ni “Adamu wa Pili, Mungu wa Majeshi”, kusanyiko zima linaitikia Amina! Wengine wanaoongozwa kuhamisha koma ktk Maandiko wakiyaondoa ktk maana yake ili kukidhi mafundisho yao, na kusanyiko linaitikia ‘Amina’, huku wakijua fika kwamba kuongeza au kupungu ktk Neno la Mungu ni Kifo! Mafundisho yote yasiyotokana na Neno la Mungu yanaishia kukutia matatani!

  Israeli walipokuwa ktk hatua hii, Shetani aliwatengenezea “ndama wa dhahabu”, wakamwabudu, wakapotea kusanyiko loote! Mungu akiisha kutuokoa kutoka ktk dunia ya uharibifu, alituketisha hapo juu na kutukabidhi Neno lake la Thamani, hilo lenye Kututakasa kikamilifu; tumepewa ili lituongoze ktk maisha yetu mapya. Nuru ya Kuhesabiwa Haki huongezeka Nguvu ktk Utakaso. Yaani tunapoliishi hilo Neno, ndilo linalomshinda Shetani, hilo ndilo Ngao iwezayo kuizuia hiyo mishale ya moto inayorushwa kutoka kila kona! Kama ambavyo Mungu hakutushurutisha kuipokea Injili, alitungojea ktk uamuzi tutakaoufanya kisha yeye akaja juu ya huo; hata ktk hatua hii, akiisha kutukabidhi hilo Neno, lililojaa Maarifa, uamuzi wa kuambatana nalo ni wetu, yaani tukiwa ni wale kondoo!

  Katika Utakaso ndio kuna Kuchafuliwa! Mungu ni Mtakatifu, hakuna mchafu anayeweza kumsogelea, wala hakuna sala au chochote unachoweza kufanya ili Mungu akupokee; Yeye anaiangalia Damu ya mwanawe tu, unapokoshwa ktk hiyo, ndipo Mungu humuona Kristo na si wewe! Naye Kristo akiwa ni Neno lake, ndio kusema ukiambatana na Neno, ndipo unapokuwa chini ya Damu yake, umefichwa hapo, na si kelele za ” Nakumwagia Damu ya Yesu ikulinde…” nk, au mafundisho ya dini yanayoikataa hiyo Damu, maana kama Maandiko yanasema Kristo alishuka Kuzimu akazihubiri roho zilizo kifungoni, mafundisho yenu yakikufundisha kulikanyaga Neno hilo, yakakuambia si hivyo, ndiko kukufuru kunakopelekea jina lako KUFUTWA ktk Kitabu cha Uzima!!

  Hivyo twafahamu kwamba Damu ndiyo inayoutunza wokovu wetu, kila siku TUNAOSHWA tope tulilorushiwa na Shetani, ndio ile Ngao ya Imani, “Baba yetu uliye mbinguni, …. utusamehe makosa yetu … Na usitutie majaribuni, lakini UTUOKOE na yule mwovu..” MT.‬ ‭6‬:‭10-13; sala na maombi kila wakati, ule ukuhani tuliopewa: Kut 29:38-39 “Basi sadaka utakazozitoa juu ya madhabahu ni hizi … Mwana-kondoo mmoja utamchinja asubuhi; na mwana-kondoo wa pili utamchinja jioni. 43Nami nitakutana na wana wa Israeli hapo, na hiyo Hema itafanywa takatifu kwa utukufu wangu.” Hema, ile miili yetu, ikiisha kutakasika Mungu hushuka akutane nasi, akituhakikishia uwepo wake ktk vita inayoendelea, yeye aliye Mkombozi na Mwokozi na Jemadari wetu, atupaye kushinda vita hiyo ktk yeye!‬‬

  Hii ndiyo jinsi TUNAYOOKOLEWA KILA SIKU humo vitani!!!‬‬ Nao uhakika wa kuokolewa huko mbele Bwana ajapo uko ktk kuokolewa leo hii, ukipotea leo, kama wale Israeli waliopotea huko jangwani, basi Bwana ajapo ni lazima atakukosa!! Ni HASARA iliyoje!!!

  Gbu!

 36. Mjema,

  Yes, mtu anaweza akapoteza wokovu! It is as simple as that.

  Nawe nithibitishie kwa kifupi tu vinginwvyo.

  Nini maana ya Wokovu ndugu mjema?

  Ona huu mstari: For with the heart one believes and thus has righteousness, and with the mouth one confesses thus has Salvation (Rom 10: 10).
  Mjema hii sentensi iko katika wakati fani?

  Tunaposema wokovu katika past, present, na future tense, simply tunasema ilichosema biblia. Na tumekuonesheni mistari ya kutosha inayosema tumeokolewa Na inayosema tuliokolewa, unataka nini cha zaidi?

  Mimi naona tu kwamba au hujui maana ya neno Wokovu au hutaki kujua maana ya neno hilo.

  Ivi wewe na Siyi mmesoma shule tofauti na Lenda, au yeye ni msabato masalia. Maaba naona kudogo ana uwezo wa kuyaona mambo ktk ukweli wake.

  Anyway, hata sishangai kwa nini hujamtaja wakati mnapongezana, ila umempongeza Siyi tu. Japo mnapongezana kwa kazi ambayo pupa.

  Wewe ulisema wokovu ni uzima wa milele, lakini Siyi kasema wokovu ni glorification, mambo ambayo kibiblia ni uongo.

  Kuna wakristo wakisikua neno kutakaswa kifikra wanalihusisha na kumwagiwa kimiminikafulani, na wajua ni hivyo.
  Lakini ukiwapeleka katika maana halisi kwa lugha za asili ndipo hukuta maana ya kutakaswa ni kutengwa, tofauti kabisa
  na picha waliyokuwa nayo.(huu ni mfano)

  Mjema, picha mliyonayo ta maana ya neno Wokovu, ni ta kufikirika tu, nendenu kwenye original writings za biblia mtajua maana ya wokovu!

  By grace we are saved!

 37. Siyi,

  Mimi huwa sikimbii mjadala, tutakwenda mpaka wote mtakapoamua kuacha.

  Umeongea kwa namna ya masikitiko sana wakati ukimjibu Haule, amvayo mtu asiyejua anaweza akafikiri kuwa unaongea kitu cha maana sana.

  Lakini acha nikuoneshe kitu ambacho kimejificha kati ya mistari.

  Nilikwambieni maana halisi ya neno wokovu ni Sodzo kwa Kiebrania, na Soteria Kigriki.
  Ndani yake kuna kukombolewa, kuponywa magonjwa, kusamehewa dhambi, n.k.

  Kukombolewa ni kutolewa katika ufakme wa giza na kuingizwa ktk ufalme wa nuru.

  Sasa wewe unadai unaongelea wokovu unaohusiana na kifo cha Kristo na ss ati tunaongelea wokovu unaohusiana na kuponywa magonjwa na kunasuliwA na maadui hapahapa duniani.

  Siyi kifo cha kristo ndo kinachohusiana na kuponywa magonjwa hapa duniani, ndicho kinahusiana na kukombolewa hapa duniani, hakuna jambo moja katika neno wokovy ambalo halihusiani na kifo cha Kristo.

  Kukombolew, kuponywa, kusamehewa dhambi, kote huko kunahusiana na jifo cha kristo. Na hayo mambo yote kwa ujumla wake ndo yanaitwa SODZO/SOTERIA kwa hizo lugha za asili, au Wokovu kwa lugha yetu.

  Kama msingi wa kifo cha kriso kwa wokovu ni Yesu kututoa duniani, basi ingekuwa tu mtu anapomwamini basi anatolewa duniani.

  Ivi Siyi kwa ufahamu wako mtu anapoambiwa yuko dhambini maana yake huwa ni nini hasa? Je bi kwamba huyo mtu yuko kwenye hii universe au je mtu huyo yuko kwenye kutumikishwa na shetani?

  Kwa nini usiende na wewe kwenye lugha za asili ukaupate huu ukweli kuliko kung’ang’ana tu mantiki ya kiakili uliyonayo!

  Ukiongelea kuwa hatima ya Wokovu ni kutwaliwa kutoka kwenye hii dunia ya sasa, ni kweli iko hivyo. Lakini ujue hiyo ni hatima au hitimisho la jambo.

  Na Mungu hatutou hapa duniani ati ili kusudi tuwe mbali na shetani. Anatutoa kwa sababu anataka kuiteketeza hii dunia halafu afanye nyingine ambayo tutaishi humo.

  Jambo ambalo unanishangazeni kabisa ninyi watu, ni kuikataa mistari inayotamka kuwa tumeokolewa, na kujaribu kulazimisha kuwa inamaanisha kitu kingine.

  Something must be wrong with u guys!

 38. siyi,

  mzee wa “Take heed! Take heed!”

  Ongera sana kwa uvumilivu kwa walimu wa aina hii,ht ivyo you have done a great job!mbegu ulizopanda hazitapotea bure! Hata km sio kina sungura, lwembe& co, waliochagua kuwa mbegu iyo kuangukia njiani,miambani na kwenye magugu, wapo wengi,waliona mioyo inayotaka kujifunza na kubadili misimamo yao,wataelewa na wata “take heed!take heed” kwa kuwa wao ni udongo mzuri.

  Hata ivyo, tusisahau kuwasemea rafiki zetu hawa kwa Yesu,ili hatimaye, “wafunguliwe akili,waelewe na maandiko”

  Congratulation Mjoli!!

 39. sungura &co,

  Naona baada ya kazi zito vijana wananawa mikono.

  Nami nawaacha na swali hili(km umesha lijibu nijulishe ulipojibu):

  Qz:Je,ninyi mliookoka (ile ya past&present) mnaweza msiwepo mbinguni(future)?

  Jibu:Kwa majibu miliyotoa hadi sasa kwa swali hili lililobeba mada ya mjadala jibu ni NDIYO-ikimaanisha kuwa hawa wanaoamini wameshaokoka sio lazima wawepo mbinguni!kuna uwezekano wa kupoteza wokovu.hii kwa mtu anaefikiri ni kwmb,wokovu walionao watu hawa haujakamilika au upo hatarini kwani adui angali akiwashambulia. Hii ndio mantiki ya majibu yenu,na mwenye akili anajua mbivu vs mbichi.

  Sisi, tutaendelea kuamini kuwa, wateule watakao sema TUMEOKOKA, ni wale tu waliompokea na kumwamini Mungu ktk maisha ya sasa na wataendelea kujua wako vitani ambapo imani yao ujaribiwa na wataendelea kuvumilia hadi mwisho,ndio hatimaye wokovu!Na saa iyo i karibu kuliko pale walipo amini.Na niwakati huo pekee ambapo kamwe hawawezipoteza wokovu. Yaani, Mtu akishaokoka hawezi kamwe kupoteza Wokovu,kwani the war is over forever ana ever.!

  Tusamehane kwama tumekwazana kwa njia moja au nyngne ila ni ktk kujifunza!

  Ombi langu: “… Tufunguliwe akili, tuelewe na maandiko…”.

 40. Siyi,

  Hukuhitaji kuongea ujinga wote huo uliouongea kwenye hiyo comment yako kwangu. Hizo ni kelele za mfa maji.

  Ati leo ndo unajaribu kujinasibu kuwa nanyi wasabato mwatenda miujiza. Kwani wewe ili ujye kuwa sisi hutenda miujiza tulikutangazia kuwa Siyi sis huwa tunatenda miujiza, si miujiza tutendayo ilitutambulisha yenyewe?

  Kumbe leo ndo unajua kuwa miujiza nayo ni part ya wanaomfuata Kristo kiusawasawa, mbona sasa ulikuwa unaiponda?

  Kwa kifupi umeongea vitu vya kipuuzi tu, ambavyo kwa mtu yeyote mwenye common sense lazima avipuuze. Kwa mantiki hiyo navipuuza.

  Umesema tutakufa kibudu, wow, hii nimeipenda sana!
  Mnyama aliyekufa kibudu maana yake amekufa bila kuchinjwa.

  Kwa hiyo wewe ambaye hutakufa kibudu utachinjwa?

  Anyway, nafikiri mpaka hapo kwa ujumla kazi tumeimaliza kwa habari ya wokovu. Tumempinga shetani vya kutosha, naye ametukinbia!

  Mungu akusaidie rafiki!

 41. Mjoli Haule,
  Mimi nashukuru kwa vile hata wewe umekuwa ni mmoja wao!! Kumbuka, nilitangulia kusema, HAMTATUELEWA KWA SASA!! Mtatuita kwa majina yote, -walimu wa wajinga, wapuuzi, wapumbavu, wazushi, wapinga kristo n.k. Hata Yesu Wayahudi hawakumwelewa. Walifikiri ni mtu aliyekuwa anapingana na kaida za imani zao na taratibu zao za dini, naam hata mafundisho yao ndiyo maana mara nyingine, walimwambia “anakufuru” Masikini hao, hawakumwelewa!! They looked the popular side!! Walisahau kuwa, siku zote, Mungu hajawahi kuwa kwenye popular side!!!
  Mwisho, mkipenda tuishie hapa kwenye huu mjadala, ni vyema. Lakini tambueni kuwa, mafundisho ya uongo, muda si mrefu yatadhihirika!! Walioko ndani ya cage ya ibilisi, muda si mrefu watatambua lakini watakuwa wamechelewa!! Kama ni mipasho tumepeana sana. Nafikiri yatosha sasa!!Na Mungu atusamehe sote kwa hilo.
  Akina Siyi, wanaamini kuwa, wao walishakombolewa kwa damu ya thamani ya Kristo. Hawadaiwi chochote kwa makosa na dhambi zao kusamehewa!! Yesu alishalipa!! Wanachodaiwa akina Siyi, ni ile nia na dhamira ya dhati ya kumfuata huyo rafiki yao aliyewalipia deni – Kristo. Kwa maneno mengine, wanajukumu la kuukulia wokovu –kufa kila siku katika ulimwengu wa dhambi na kuhuishwa katika ulimwengu wa roho –sanctification!! Yesu aliuita mchakato huu kama kukua kwa ngano ambako ndani yake huwa kuna magugu!! Ngano itakapokomaa, itasubiri mvunaji -Kristo.
  Ninyi endeleeni na kuokoka sasa hivi. Maana ninyi, mmeshindwa kabisa kutofautisha kati ya kuponywa maradhi, kuponywa na maadui, n.k. kwa hapahapa dunini (japo Biblia imetumia neno lilelile -kuokoa) na ile ya kuokolewa kwa maana ya kutolewa duniani. Na hii imekuwa isivyo bahati, maana nimekuwa nikizungumzia habari za wokovu unaolenga kifo cha Kristo, huku nikibishana na watu wanaolenga maana ya mtu kuponywa, kunasuriwa n.k. na maadui akiwa duniani. Ni Mambo mawili, yenye uhusiano wa namna Fulani maana yametumia neno moja, lakini hatima zake ni tofauti. Moja ya duniani ambayo ibilisi ameemphasize zaidi . Na nyingine ya mbinguni inayopigwa vita nap engine watu kukana kabisa kuwa haipo. Nafikiri hapa ndipo penye mtanziko!! Hakuna namna ya kufanya isipokuwa, kila mmoja akafanya kadri Mungu wake anavyomuongoza. Mimi nilishakombolewa, nakua kiimani na hatimaye, namgonja Kristo aje anitoe kwenye ulimwengu huu wa shida. Kurudi kwa kristo kuwatoa wateule wake duniani, ndio msingi mkuu wa maana ya WOKOVU uliogharimu maisha ya Kristo. Bila kurudi kwake, dhana hii ya wokovu (wa kuwatoa watu wake dhambini na kuwaingiza kwenye maisha ya milele), itakuwa haijakamilika. Hii ndiyo sababu kuu ya kurudi kwake Kristo.
  Bwana awabariki
  Siyi

 42. Mjema,

  Unauliza swali kitoto eh!

  Majibu ya swali lako hujayaona kwenye michango tuliyotoa, au ulikuwa husomi?
  Acha kutu- opinionate, jibu la swali lako tulishalitoa muda mrefu sana.

  Unaposema wokovu ni mchakato unaelewa maana yake lakini, au unaongea tu kwa vile imekuwa kawaida kwa waswahili kutumia neno mchakato?

  Hatima ya mchakato ni tofauti na mchakato wenyewe. Kama unajua wokovu ni mchakato, mbona sasa unasema hatima ya mchakato ndo mchakato wenyewe?

  Mchakato ni kitu unachokiishi, kwa hiyo sisi tunauishi wokovu.

  Halafu unaposema wokovu wetu wa Sodzo napo nakuona hata hujielewi. Sodzo ni neno la Kiebrania lenye maana ya Wokovu kwa Kiswahili.
  Wewe endelea kusubiri kuokoka mbinguni, sisi wokovu ni sasa!!

 43. Kaka siyi

  Mimi,Sina sababu ya kujibu maswali yako,ila ingekuwa heri kwako ukichukua ushauri huu,kamwendee Mbuzi ukajifunze jinsi ya kula chakula na kucheua upate kujua jinsi ya kula neno la Mungu kwa njia kutafakari(Meditate)

  Lakini ukibaki unadhani unajua na kumbe haujui na hautaki uonekani haujui, Endelea kuwa mwalimu Mkuu wa wajinga.maana ndio njia ikupasayo

  Sikubaliani na wala sina patano na mtu au watu ambao wanajiita wakristo lakini kumbe ni wapinga Kristo wakipotosha ile kweli iletayo utauwa.

  Niwashukuru Mr Lwembe na Kaka Sungura wamepika na kutulisha vitu vitakatifu Bwana Yesu awabariki na kuwaongeza kulijua neno lake maana mmetutafakarisha neno la Mungu aliye hai,
  Biblia inasema na vitabu vikafunguliwa na majina yao yakaandikwwa ktk kumbukumbu jinsi walivyolitafakari lile neno.

  Mjoli Haule

 44. sungura,lwembe,ziragora & CO.

  Jibuni maswali yangu hapo juu, A & B. Itawasaidia kuelewa Wokovu.

  Nawasubiri!

 45. Lwembe,
  Mimi naendelea kukungoja nione unataka kutuambia nini hasa kuhusu wokovu. Nakusubiri.
  Siyi

 46. Siyi, Mjema & co,

  “PRESENT TENSE”-LEO -(Yesu Kristo ni yeye yule jana, LEO…)- TUNAOKOLEWA.

  Baada ya kuutazama Wokovu ulioleta Ukombozi wetu, ambao kwao Tuliokoka na Hukumu ijayo, nasi kuingizwa ktk Nguvu ya Kufufuka kwake, TUKAHESABIWA HAKI KWA IMANI!

  Israeli, wakiisha Kukombolewa kwa damu, waKaokolewa kutoka ktk mikono ya Wamisri. Tukaona kwamba Kuokolewa kwao kuliambatana na kuyatimiza maagizo waliyopewa wakiidhihirisha Imani iliyowaingiza ktk Kuhesabiwa Haki, dhihirisho la majina yao kuandikwa ktk Kitabu cha Uzima.

  Tazama, ulikuwa umejikabidhi kwa miungu ya kipagani, maisha yako yote ukiwa umeyatoa kwa miungu. Kisha siku moja akawafikia Mwinjilisti Musa, mzee wa miaka 80, mkononi ana fimbo tu; akawambia “Mimi” amenituma kuja kuwatoa ktk utumwa na mateso mliyonayo chini ya utawala huu wa dhambi! Hebu liwazie jambo hilo, kwamba Musa wanamjua vizuri sana, yule kijana mwenye nguvu na hodari mwenye maarifa yote ya kijeshi, na elimu ya kutukuka; akiwa ktk kilele hicho alimkimbia Farao, sasa leo anatembelea fimbo, eti ndiyo kaja kututoa kutoka mkono wa chuma unaotushikilia, (wakiyawazia yale majeshi ya Farao dhidi ya huyu mzee mwenye kifimbo), njaa itakuwa imemchanganya hadi imemtoa pangoni huyu mzee!

  Mungu hadhihirishwi kwa liturgia, bali kwa Injili inayoambatana na Miujiza ambayo hawakuwahi kuiona wala kuisikia ktk maisha yao yote ya kuitumikia miungu ya Litugia, na alipomaliza mahubiri, Israeli ikayaamini yote!

  Hatua ya pili waliyoipitia Israeli, kulingana na Mpango wa Mungu wa Wokovu, wakiisha kuwa wamehesabiwa Haki, ilikuwa ni Kutakaswa. Tukumbuke kwamba, Kuhesabiwa Haki humtukia mtu pale anapoiamini Injili. Yaani unaweza kuhudhuria mkutana wa Injili leo, ukayaona matendo makuu ya Mungu, ukaamini katikati ya mkutano huo, Mungu anakuhesabia Haki papo hapo! Kwahiyo tunaweza kusema kwamba jambo la Kuhesabiwa Haki ni instantaneous, yaani jambo la ‘papo kwa papo’!

  Israeli wamechafuka kwa zaidi ya miaka 400, basi ili kuwarejesha ktk mkondo wa kiUngu, kule kuwatakasa, Mungu aliwatayarishia Torati, na kuwapitisha ktk njia yake akiwalea kuyakulia mambo mapya ya uhuru ktk Yeye.

  Pia tukumbuke kwamba utumwa ni wa mwilini, pale roho zinapokuwa zinamilikiwa. Israeli waliokolewa kutoka utumwa huo, na ktk hatua hii ya pili, wakiwa wamerejeshewa uhuru wao, watesi wao wakiwa wameangamizwa, vita ilihamia rohoni; Shetani ni king’ang’anizi, tena ni hodari! Mungu huwa haingilii Uhuru wa maamuzi, anauheshimu sana, mpaka wewe mwenyewe umruhusu awe ndiye mwamuzi wa mambo yako, ndiyo ile asili ya kondoo ambayo hupatikana ktk kulisikiliza na kulitii Neno lake, hilo liiumbayo Imani yake ndani ya hao waliolipokea.

  Basi licha ya kuyaona mambo makuu Mungu aliyowatendea, akijidhihirisha kwao kwa Nguzo ya Moto iliyowaongoza usiku, na ktk Wingu mchana, na wao wenyewe kuwa mashahidi wa kuipokea arabuni ya wakovu wao, rejea ambayo ilipasa iwapeleke mbele zaidi; lakini washawishi miongoni mwao (kumbuka kwamba walipotoka huko Misri hawakuchujwa, walikuwa ni mixed multitude), wakawatia baridi, kusanyiko likapoa; na mwishoni wakajirudisha kwa miungu ya kipagani waliyotoka nayo huko Misri, wakajitengenezea mungu wa ndama wa dhahabu kwa mikono yao wenyewe na kisha wakamuabudu; na huo ukawa ndio mwisho wa safari yao ya wokovu, imani ikiwa imekwisha kuondolewa kwa ibada ya kipagani, ndipo bila imani ni vigumu kumfikia Mungu huyo ambaye ndiye Wokovu wao; Majina yao YAKAFUTWA kutoka ktk Kitabu cha Uzima, Kut 32:33 “BWANA akamwambia Musa, Mtu ye yote aliyenitenda dhambi ndiye nitakayemfuta katika kitabu changu.”!!!!

  Basi bila imani kila jambo huwa gumu, hata ilipofika wakati wa kuingia ktk nchi ya Ahadi, pale Kadesh Bania, Hes 13, pakawa ndicho Kiti cha Hukumu kwao, imani yao ikiingizwa ktk mizani, ikaonekana kusanyiko lote la waabudu ndama wa dhahabu liko utupu, wanaogopa mpaka mijusi. Kizazi chote kilifia jangwani huko kusiko na Ufufuo, isipokuwa watu waili tu waliojikabidhi kwa Mungu, wale kondoo!

  Ibada zina hatari kuliko tunavyoziwazia, maana zinawakilisha vita vya kiroho, Biblia inasema Shetani anarusha mishale ya moto, na ktk hili twafahamu kwamba Israeli walipaswa wamsikilize na kumngojea Musa ktk kila jambo maana yeye ndiye aliyekuwa Sauti ya Mungu kwao; nao waliposita ktk hilo, tumewaona akina Kora wakiinuka kumpinga Musa ktk jitihada ya vita ya kiroho kuwagombea Israeli, mpaka akina Miriamu wakapigwa ukoma, lakini kwa ile ibada ya ndama wa dhahabu, Ngao ya Imani ikawadondoka, mishale ya moto ikawapata na wote wakafa kiroho!

  UKIFUTWA JINA ktk Kitabu cha Uzima, mambo yako yanakomea hapo, licha kwamba waliendelea kula manna na baraka nyinginezo, ilikuwa ni kuzisogeza siku tu, wakiisubiri Mauti waliyoichagua!

  Waliangukaje tena mautini walimotolewa ilhali wakiwa ni waliookolewa?

  Tutalitazama hilo zaidi …

  Gbu!

 47. “PRESENT TENSE” – LEO – TUNAOKOLEWA.

  Ktk kuendelea, kuna jambo moja ambalo ni la muhimu sana kulijua ili kupata ufahamu sahihi kuhusu Wokovu, licha ya jambo la majina kuwa yameandikwa ktk Kitabu cha Uzima, lakini tunaona pia kuhusishwa kwa mnyama kondoo.

  Mungu ktk Hekima yake, alimchagua kondoo kuwa kielelezo cha wanaye. Kama tulivyosoma kuhusu Mwana-Kondoo aliyechinjwa huko ilipowekwa misingi ya dunia, pia, tunaona watu wake wakifananishwa na mnyama huyo, Yn 10:27 “Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata.”

  Sifa moja ya kondoo ni kwamba, akipotea, huwa hawezi kujisaidia, hana uwezo wa kujiokoa, hawezi hata kunusa harufu ya hatari kama simba anapomnyatia! Kondoo humuhitaji mchungaji wake wakati wote, furaha na nguvu ya kondoo iko ktk kuwa karibu na mchungaji wake; “Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.” Zab.‬ ‭23‬:‭4. ‬‬

  Basi hii ndiyo sifa ya mkristo, yeye huhesabika kama kondoo ktk sifa hiyo. Macho yake na moyo wake vyote humtazama Mchungaji wake, yule aliyemkomboa, humtegemea ktk kila jambo; ndiyo ile Imani kamilifu kwa Mchungaji wake!

  Baada ya kuliongeza jambo hili ktk Msingi wa Wokovu, sasa nitaendelea tuitazame ile hatua ya Present Tense, Tunayo okolewa Leo.

  Gbu!

 48. Sungura,
  Unachekesha na kwa upande mwingine unatia huruma. Huelewi. Mwenye kuishiwa ni wewe!! Angalia una viporo vingapi vya maswali ambayo nakukumbusha kila leo lakini hutaki kujibu??? Na unajidai kujiaminisha kuwa uko sahihi, subiri!! Maneno haya, yatakuja kutimia maishani mwenu, na mtakuwa mmechelewa sana.
  Usijivunie miujiza ya uongo rafiki yangu!! Na nikwambie, sisi wasabato tunatenda miujiza tena hujawahi kuona!! Ila kwa sababu wewe hujui, huwezi kuelewa!! Kama unataka kulithibitisha hilo, huna haja ya kumuita mch. wa kisabato ili akutendee muujiza uone mbashala. Wewe muite mtu mdogo tu kama Siyi na wewe (au mch.wako) kwenye tukio lolote la kutenda muujiza. Mungu atakayejibu siku hiyo kwenye tukio hilo, ndipo atakuwa Mungu wa kweli. Tafuta mgonjwa, au mtu wa aina yeyote ili mimi na wewe (au mchu. Wako) tukutane kwa ajili ya maombi. Mungu atakayetenda siku hiyo, wakati huo, na awe Mungu wa kweli!!. Hakuna haja ya kuandikia mate rafiki yangu!! Usidanganyike!! Kama tumejaa maneno yasiyo na nguvu, jaribu kufanya nililokwambia uone!!
  Tunatenda miujiza, japo miujiza, hatuifanyi kuwa ndiyo msingi mkuu wa imani yetu. Hasha!! Na kama unaimani inayotegemea miujiza, kuwa ndiyo ikutambulishie imani ya kweli, nakupa pole!! Pamoja na Biblia kukuonya kuwa mwangalifu kwa miujiza, umefumba macho na kukumbatia miujiza tu!! Pole sana. Sisi wasabato tuna akili hai. Tuko makini mno!! Nilikwambia, huwa hatubahatishi kitu rafiki! Nashangaa unaiita advance hii!!! Mbona chekechea tu rafiki? Ha ha ha ha !! Kwako advance eee!!!
  Na ndiyo maana nilikwambia, wewe/ninyi bado sana. Mko nyuma zaidi ya mkia wa mbuzi. Siwatukani wala sijivuni!! Nawaambia ukweli. Mtakufa kibudu!! Wokovu hamuujui japo kwa viburi vya kipumbavu, mnajiadai eti mmeokoka, tena bado mkiwa duniani!! Fanatics. Kama jambo hili dogo tu la kuokoka linawachanganya, mtajuaje habari za Musa kwenda mbinguni? Sasa kama hakwenda, aliyeoneokana mlimani alikuwa ni mzuka au? Jibu sasa mtalaamu!
  Akili zenu, zimesheheni mapambio tu yaliyojaa ufedhuli mtupu ndio maana hamuwezi kuelewa lolote kuhusu Biblia. Kama kuitetea imani tu umeshindwa, unatarajia nini rafiki?? Si heri ukawe mganga wa kienyeji?? Usidanganyike kijana, mbingu ni ya watu wanaoishi sawasawa na neno/sauti ya Mungu. Kinyume na hapo, ni kupoteza muda na rasilimali. Lazima tujigambe, maana hatubahatishi. Wokovu ni kuchagua kijana. Sisi tulishachagua. Ninyi mnaimba liturujia!!
  Ni kweli sisi ni watu wa Biblia. Ukitaka kututisika, gusa Biblia. Ukitaka kujua misingi mikuu ya imani yetu, soma Biblia! Tunaweza kukitetea kile tunachokiamini kwa ujasiri popote na wakati wowote with biblical references!! Biblia tunaijua kwa kiasi kikubwa kaka (japo siyo wote). Kwa hilo, hatuna budi kumshukuru Mungu. Ukiona msabato anabahatisha (kwa vile huwa hawakosi), jua ni mchanga au mdumavu! Walio hai, hutembea na Kristo kila aendako!! Na kama kuiamini Biblia unasema ni heresy, show me from the bible what type of heresy we have!! Hata mimi siwaambii wala siwalazimishi muwe wasabato. Kazi yangu ni kusema kile Biblia inachokisema. Mtu akikipokea, mimi sipati faida yoyote! Ukifa dhambini, hata Mungu hana hasara rafiki!! Kama aliua mabilioni wakati wa Nuhu na Sodoma, sembuse Sungura na heresy wenzake!! Mtakaufa tu msipojali!!
  Wokovu, ni baadaye!! Sasa hivi tumekombolewa tu!! Tuko safarini!! Safari ya kiimani, ni full of vionjo vya matatizo, majaribu, nk. Na Mungu huyaruhusu haya wakati mwingine ili atukomaze kufikia hatua ya kukomaa tayari kwa kuvunwa! Wakati wa mavuno, ni baadaye. Sasa hivi, kama mimea, tulishapandwaa shambani, tunamea ndani ya Kristo (japo wengine wanapitia changamoto), lakini hatima ya haya yote, ni kuvunwa. Na hii ndiyo dhana sahihi ya mchakato wa wokovu.
  Kama ninyi mna mungu anayewavuna mkiwa hapagapa duniani, nawapa pole sana. Nina uhakika huyo, atakuwa ni ibilisi mwenyewe. Poleni sana.
  Siyi

 49. wana SG,

  Tumeongea mengi sana! Ila swali la msingi linabaki kuwa:

  A: Je,mtualiyeokoka(ile ya kikwenu SODZO-past.present) anaweza kupoteza wokovu tena (future)?

  B: Yaani kwa maneno mengne,wewe,sungura,lwembe,ziragora,edwini n.k uliyeokoka jana na leo unaweza usiwepo mbinguni?

  Tafadhali jibu: 1.NDIYO 2.HAPANA 3.SIJUI.

  Kumbuka swali A na B ni sawa na hivyo majibu yake ni sawa.

  Yeyote atakaye tafakari maswali haya na mantiki yake iliopo atajua endapo kuna wokovu duniani au la!

  Wokovu ni mchakato na hatima yake ni mwisho wa vita!

  Mbarikiwe nyote.

 50. Siyi,

  Sasa naona dozi imekuzidia, huelewi hata unachoongea bali unajiongelea tu.
  Ulidhani ni rahisi kupiga teke mchokoo, na kwa vile hukusikia wakati nakuonya hayo ndo matokeo yake.

  Huna tena cha maana unachoongea, bali unalopoka tu. Njia ya muongo huwa ni fupi. Wewe kama umeishiwa cha kusema nyamaza tu, tutaelewa kuwa umeishiwa.
  Hatukuwa tunajadili ili tukufanye uache usabato wako. Balu tulitaka ujue ukweli ulivyo ili usiendelee kudanganya watu.

  UnakimbIlia kusema tutakataliwa pamoja na kutenda kwetu miujiza, lakini ni kwa sababu ninyi hamna uwezo ndani yenu wa kutenda miujiza yoyote. Ni kama madebe tupu, kazi yake kupiga kelele za maneno tu.

  Unatakiwa uelewe kuwa miujiza ni part ya imani katika Kristo, alisema tutafanya zaidi ya yale aliyofanya yeye, koz yeye alikuwa anaondoka.

  Miujiza katika imani yetu itaendelea kufanyika na imani bado tutailinda. Sisi ndo wale walioupindua ulimwengu.

  Hii haikuwa shule ya a,b, c, d, bali ilikuwa advanced level , ambayo kimsingi imekushinda. Uwezo wako wa kuelewa ni mdogo.

  Unataka tukwambie Musa alijwebdaje mbinguni. Tutakwambiaje jambo ambalo halipo? Biblia imesema Musa alikufa. Hilo suala na kuonekana kwake mlima wa ugeuko halimaanishi kuwa alikwenda mbinguni.

  Aliyekwenda mbinguni ni yule tu aliyeshuka toka mbinguni.

  Akili yako haiwezi kuwaza above sabato na vyakula najisi. Ndio maana kwa ujinga uliokolea unadhani Yesu kaleta pumziko la mwili. Kwa hiyo nwili wako na nafsi yako hupumzika J’mos tu. Pole sana.

  Wasabato mmejaa maneno mengiii lakini nguvu ni sifuri.
  Huu ufalme tunaotumikia hauko katika neno tu, bali ni katika nguvu pia.

  Wewe usipoukubali huu Wokovu ambao umethibitishwa na kudhihirishwa leo, wala hautapenya kuiingia mbingu kama unavyojigamba.

  Sidhani hata kama huwa unachukua muda kujitathmini kama yko sawa ktk kile unachoamini, au kazi yako ni kuona tu akini Ziragora ndo hawako sawa.

  Mimi sina shida na usabato wako, shida yangu ni jinsi ambavyo wasabato hujifanya mnajuwaaaa, lakini ukija kuwaangalia ujuaji wenu uko kwenye heresy.

  Siyi, barudia tena, hatuko hapa kukung’ang’aniza uokoke, ila tuko hapa kuhakikisha humdanganyi mtu. Wewe endelea na usabato wako, utajijua mwenyewe.

  Tumekuthibitishia kuwa wokovu ni sasa, tumekwambia wokovu ni kukombolewa, kusamehewa dhambi, kuponywa, yaani ni kutolewa katika ulimwengu wa giza na kuhamishiwa ulimwengu wa nuru.

  Halafu unamakizia kwa kusema tuombeane, sijui kwa Mungu yupi sasa,maana inaonekana wa kwetu na wa kwenu ni tofauti.

  Kama umeishiwa cha kusema, omba tukomee hapa, lakini habari ndo hiyo.

 51. Sungura
  Mimi hapa bro Sungura!!
  Si nuru ndogo peke yake, bali ni mtu wa nuru kubwa na ndogo. Huwezi kuvielewa hivi kwa sasa!! Ndiyo maana, wewe huwezi kuelezea Musa aliendaje mbinguni, japo unakiri kuwa alikuwepo kwenye ugeuko. Nilikuomba uthibitishe!! Na nilikuuliza, ujibu namna alivyoenda mbinguni. Lakini hukujibu na badala yake ukucheka tu!! Utabaki kucheka tu kama Kayafa!! Hutaelewa!!
  Kama unafikiri Haule kafanya uchambuzi wa maana, nawangoja nyote msaidiane naye kujibu maswali na changamoto nilizokupeni. Hadi mnatia huruma rafiki zangu. Mnatia aibu kabisa. Acheni niwaambie hivyo tu. Ninasikitika sana. Watu wanaomjua Mungu, tena wanaojiita kuwa ni wasomi wa Maandiko, hawawezi kusema maneno kama haya,
  “Kama ulidhani kuwa unaweza kumkimbia shetani kwa kwenda kuishi mbinguni, imekula kwako, maana tunatakiwa kumshinda tukiwa duniani”.
  Utaendaje mbinguni bila ya kumshinda ibilisi? Na kwa vile kwenye nchi mpya na mbingu mpya hakutakuwa na masumbufu ya vilio, maradhi na taabu zote, je, Yesu atakuwa ametukimbiza/kutupokonya kutoka kwa ibilisi? Very Fanatic!!
  Na kuhusu mambo ya mwilini na ya rohoni, mtakesha hamtaelwa msipojishghulisha kuyafahamu. Mnajidai kuyajua kumbe hamyajui hata chembe. Hata chembe!! Ni watupu kama nini!! Maana msingekuwa watupu, dhamiri zenu zisingekuwa tofauti na mnachokitenda!! Imani yenu, isingekuwa tofauti na jinsi mlivyo!! Mngekuwa watu wa rohoni, mngemjua Mungu aliye Roho. Na kama mngelimjua Roho, mngelilijua Neno ambalo lilitoka kwake. Msingemhuzunisha kwa kueneda tofauti na alivyosema –Biblia. Ndio maana nawaambia ninyi SIYO WATU WA ROHONI, acheni kutudanganya hapa!! Hamuwezi kuwa watu wa rohoni (kisima cha Neno), halafu mkaenenda tofauti na neno. Ndiyo maana nawaambia, hamtaweza kuelewa maana ya pumziko la kimwili, kiakili na kisaikolojia bila ya kuijifunza Biblia kwa umakini. Mtaishia kucheka tu!! Na mtashangaa sana siku ya mwisho Kristo atakapowaambia, SIKUWAJUA, ONDOKENI KWANGU NINYI MTENDEAO MAOVU.
  Mbinguni, hatuendi kwa sababu tunamkimbia Ibilis. Tutaenda kwa sababu Yesu ametukomboa na tumeishi sawasawa na Neno lake. Wanaoishi kinyume na neno la Mungu, wajaposema wameokoka, wajapotenda miujiza mingi ya kuwapumbaza, wajaponena kwa lugha zisizoeleweka, wajapolia wakati wa kuomba, wajapokanyaga ardhi kwa kishindo wakati wa kuomba, n.k., mbele za Kristo, watu hao wote, wanajulikana kama ni watenda maovu!!
  Najua akili zenu ni nzito kuelewa. Na hamtaeelewa kirahisi kwamba inakuwaje, kutoa pepo, kuombea watu wakapona, kunena kwa lugha n.k. yakawa ni matendo maovu hadi Kristo aseme “sikuwajua” –Mtt 7:21-23?? Hamtaelewa!! Ndiyo maana na ninyi eti mko makini kudanganywa wakati huko mliko, mlishadanganyika tayari!! Kwa vile sasa hivi hamjaliaona hilo, hamtaelewa!! Mtaelewa mtakapofunuliwa!! Mtaelewa mtakapojinyenyekeza kujifunza neno la Mungu. Kristo atawafunulia!!
  Tuombeane sana!!
  Siyi

 52. Bro, Haule
  Nakushukuru kwa mtazamo wako pia. Maana una huo uhuru wa kutoa mtazamo na mawazo kadri uwezavyo. Hiyo ni haki yako itumie. Sijui kama kweli mimi ni mtaabishaji. Huenda kweli nisijue maandiko kwa kiwango ulicho na wewe. Na hilo lisikupe shida!! Ipo siku nitakuwa mkomavu kimaandiko kama wewe.
  Aidha, pamoja na uchanga wangu kimaandiko, sina uhakika kama nilichanganya habari za dunia na mji mtakatifu baada ya miaka elfu!! Sina uhakika kama nilichanganya!! Huenda hukunielewa tu kwa vile umesema sijakomaa kimaandiko. Jaribu kunisoma tena ili upate concept!! Vinginevyo (wewe kama mwalimu), utanipa sifuri kumbe nilistahili kupata 80.
  Kaka Haule, kama mimi ni kipofu kweli, siyaoni mafungu yanayosema kuwa tumeokolewa tukiwa hapahapa duniani, wewe hujayaona maswali niliyowaulizeni hapo juu? Ulijaribu kuyajibu hata kidogo??!! Mimi nina wasiwasi na wewe ktk ufuatiliaji wa michango hapa SG. Unaibuka na falsafa za ajabu sijui zinakotoka. Ona ufidhuli huu ulioandika hapa, “Siyi na Jamaa zake kuna roho inatenda kazi ndani yao kwa kuwa wao ni mataifa hawajaokoka na wanakana hakuna kuokoka,unaiona hiyo roho ya mpinga Kristo inavyotenda kazi ndani yao”.
  Wewe unafikiri mataifa ni akina nani? Una uhakika kuwa Siyi na wenzake wamekana hakuna kuokoka??? Hebu thibitisha!! Mimi nina wasiwasi na cheti chako cha ualimu hapa!! Huenda wewe ni mwalimu wa kipindi cha mama Sitta!! Mwalimu wa C. Programu!! Kwa nini??
  Angalia ufidhuli na kujichangnya kwingine ulikokuandika hapa, “Kwa wale watoto wachanga(mnao ukulia wokovu) linganisheni haya maandiko Uf 20:7-10 vs Uf 21:1-5 na anachokifundisha ile roho ya mtabihishaji Siyi kama kuna sehemu shetani anaukaribia mji Mtakatifu Jerusalem mpya…kwa kweli ni roho ya upotofu imetamalaki hapa”.
  Sasa, wewe umekataa kuwa ibilisi hataukaribia mji mtakatifu. Lakini aya hiyohiyo uliyonukuu mwenyewe, inakuthibitishia hilo kuwa atauzunguka mji mtakatifu kwa ajili ya mashambuli dhidi ya watakatifu!! Sasa, unaweza kukizunguka kitu bila kukikaribi mwalimu?? Hebu soma ulichonikunuu mwenyewe…
  “Ufunuo20.7-10
  Na hiyo miaka elfu itakapokwisha, Shetani atafunguliwa, atoke kifungoni mwake;
  naye atatoka kuwadanganya mataifa walio katika pembe nne za nchi, Gogu na Magogu, kuwakusanya kwa vita, ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari.
  Wakapanda juu ya upana wa nchi, wakaizingira kambi ya watakatifu, na mji huo uliopendwa. Moto ukashuka kutoka mbinguni, ukawala.
  Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele.”
  Kwa vile wewe ni mwalimu mzuri, kwa mujibu wa Ufunuo 21.1-5
  uliyonukuu, hebu nitofautishie kati ya;
  1. Kambi ya watakatifu na Mji Mpya.
  2. Yerusalemi Mpya na Mbingu mpya na nchi mpya.
  Mwisho, umesema kuwa mbingu na nchi za sasa zitakusanywa kama kurasa. Vyema kabisa!! Na umesema kuwa sisi tutaendelea kuishi hapahapa duniani ukimsupport Sungura. Je, hiyo mbingu mpya na mpya na nchi mpya, zitaitwa dunia pia? NB: Kumbuka zile za kwanza zilishakusanywa kama kurasa!!!!
  Safari hii nakuomba ujibu mapema pachiko hili kabla mchuzi haujapoa!! Nakungoja mwal Haule.
  Siyi

 53. Siyi,

  Nafahamu sitakukwepa kwani hata Yesu alilaumiwa kutoheshimu Sabato. Yesu namfahamu kama Njia na Kweli na Uzima. Hapo ndipo nilipo. Lakini kwa miungu ile yako siko. Ukiisha abudu siku anamtiya wapi Yesu. Pia kinachoshangaza ni kwamba unadai kuwa kwa upande wa Yesu !!!
  Acha ile miungu uje na shahuku yako katika kumtumikia Yesu. Imeandikwa kila goti lipigwe na ulimu ukiri kama Yesu ni Bwana. Haleluya!!!

  Wewe tu acha kubahatisha, endelea na mada jinsi ilivyo.

 54. Haule,

  Asante sana kwa facts ambazo umekuwa ukichangia ktk mada hii.

  Nathamini ana mchango wako.

  Ubarikiwe

 55. Siyi, mzee wa nuru ndogo,

  Umenichekesha sana tena leo. Nilikushauri mapemaa kwamba usipige teke mchokoo, utaumie vibaya.

  Kwa sababu umekosa mahali pa kudhika katika neno halisi la Mungu, umeamua kuleta na ile akiba ambayo yenyewe huwa ni ya wasabato tu ili ijaribu kukusaidia kulinda upotofu wa imani yenu. Hiyo nuru ndogo yako ndio itapotelea kabisa kwenye hii nuru kubwa tuliyonayo sisi.

  Sihitaji kukuambia zaidi jinsi ulivyodhihirisha kuwa biblia huijui, ila unajua tu vitu vichache ambavyo hutumiwa ku-defend upotofu wenu.

  Uchambuzi wa ndugu Haule juu ya kujichanganya kwako unatosha kabisa kukupa aibu itakayokufanya uone utubu ukitaka.

  Kama ulidhani kuwa unaweza kumkimbia shetani kwa kwenda kuishi mbinguni, imekula kwako, maana tunatakiwa kumshinda tukiwa duniani.

  Jesus who lives in us is coward ati ashindwe kumshinda shetani mpaka asubiri twende mbinguni ndo tupate huo ushindi.

  Yerusalem mpya haitaelea angani, itakuwa duniani au kwenye nchi ambayo inaitwa mpya.

  Tena acha kujifocha majanini, na kupaza sauti ati Sungura ameanza kuelewa tofauti ya Salvation na Safety. Nani alikuwa haelewi jati yangu na wewe, na mpala sasa bado huelewi tu.

  Ulipomwambia Ziragora akaribie kwenye pumziko la kimwili, kiakili na kisaikolojia ati ndio pumziko la sabato nikazidi kutambua jinsi ninavyohangaika na vuvuzela.

  Ndio maana unasisitiza mno katika wokovu wa kimwili (Safety) wakati wenzio tunaongelea wokovu wa kiroho ( Salvation).

  Ilikuwa inanisumbua kidogo kwamba ujasiri wa kuikanyagakanya mistari aliyokupa ndugu Haule inayosema tumkwisha okolewa kwa neema uliutoa wapi!

  Mambo yenu ninyi ni ya kimwilimwili tu( machanical) wakati huko Mungu alishatutoa.

  Yesu anaongelea pumziko la rohoni kutoka kwenye mizigo ya dhambi wewe unaongelea pumziko la kimwili, kiakili na kisaikolojia tena la siku moja tu ya Jumamosi. Ikiisha J’mosi unarudia tena zigo lako.

  Hivyo hivyoo, tunapoongelea wokovu (Salvation) ambao ni kutolewa katika nguvu za giza, wewe unaongelea Safety ambayo ni kutolewa sehemu ya hatari physically.

  Ndio maana unang’ang’ana na suala la kutolewa duniani physically kwa kunyakuliwa ati huko ndiko kuokoka.

  Biblia inasema saa ya wokovu ni sasa, lakini wasabato kwa kutumia kitu kinachoitwa nuru ndogo mnasema wokovu ni mbinguni.

  Mtaendelea kuchanganyikiwa mpaka mtakapokuvali kujua kweli ya Kristo..

  Na hautafanikiwa kudanganya mtu hapa!!

 56. Bro Sungura unayo kazi kweli……. kuwatupia mbwa vitakatifu.
  Huyu ndugu Siyi nimemngundua hajui maandiko na Zaidi sana ana roho ya kutahabisha inayomuongoza.Ndio ni Mtahabishaji…

  Ona kwa kusudi maalum anachanganya Kuishi miaka elfu duniani na Bwana Yesu(Ufunuo20) na Mji Mtakatifu Yerusalem Mpya(Ufunuo 21)
  Wakati anajua fika kuwa Mji Yerusalem Mpya utatelemka wakati Mbingu na nchi hii ya sasa itakuwa imekunjwa kama karatasi na shetani amesha hukumiwa kwa kutupwa ziwa la moto(Ufunuo 20:10)

  Kaka Sungura nakushauri ujichunge na hii roho,kumbuka huyu jamaa hajaokoka(Mataifa)yuko mwilini kwa hiyo amefungwa nira shingoni…..lijamu mdomoni….. hatamu ameshika bwana yake shetani
  hana hiyari ya kuchagua njia wala mwendo, maana yuko mwendo mdundo kuelekea ziwa la moto ndio maana anashindwa na dhambi na anadhani sisi wote tuna nira ya shetani anasahau kuwa sisi tumesha chukua nira ya Kristo na mizigo yote tumemkabidhi Bwana Yesu.nira yake laini na mzigo wake mwepesi tuna raha nafsini mwetu.

  Nilipoandika maandiko haya hapa 09/05/2014 at 3:40 PM

  Efeso 2.1-10 
  “Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu;
  ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi; ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine. Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda;
  hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema.
  Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu;
  ili katika zamani zinazokuja audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu sisi katika Kristo Yesu.
  Kwa maana MMEOKOLEWA kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.
  Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.”

  Tazama Bro Sungura
  Huyu ni kipofu wa namna gani! hata asiye ona kuwa tulikuwa wafu kwa sababu ya Dhambi na sasa tumehuishwa na kuokolewa kwa neema na bado tupo hapa duniani, toka wafu mpaka kuuwika(kufukuka)na kuketi pamoja naye ktk ulimwengu wa roho.Tuko huko haleluya.

  Siyi na Jamaa zake kuna roho inatenda kazi ndani yao kwa kuwa wao ni mataifa hawajaokoka na wanakana hakuna kuokoka,unaiona hiyo roho ya mpinga Kristo inavyotenda kazi ndani yao.

  Tuwaombee kwa Bwana Mungu anafadhiri atakaye kumfadhiri….anarehemu yeye atakaye kumrehemu.vinginevyo tujihadhari na Mbwa(mataifa) Fil 3:2

  Kwa wale watoto wachanga(mnao ukulia wokovu) linganisheni haya maandiko Uf 20:7-10 vs Uf 21:1-5 na anachokifundisha ile roho ya mtabihishaji Siyi kama kuna sehemu shetani anaukaribia mji Mtakatifu Jerusalem mpya…kwa kweli ni roho ya upotofu imetamalaki hapa.

  Ufunuo20.7-10
  “Na hiyo miaka elfu itakapokwisha, Shetani atafunguliwa, atoke kifungoni mwake;
  naye atatoka kuwadanganya mataifa walio katika pembe nne za nchi, Gogu na Magogu, kuwakusanya kwa vita, ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari.
  Wakapanda juu ya upana wa nchi, wakaizingira kambi ya watakatifu, na mji huo uliopendwa. Moto ukashuka kutoka mbinguni, ukawala.
  Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele.”

  Ufunuo 21.1-5
  “Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.
  Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.
  Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.
   Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.
  Na yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya.”

  Kama anavyofundisha Bro Sungura tangu mwanzo kusudi la Mungu sisi binadamu tukae ktk Nchi(Dunia)itabaki hivyo ndio maandiko.

  Mjoli Haule

 57. Ziragora,
  Nikutakie Sabato njema rafiki. Karibu kwenye raha ya mapumziko ya kimwili, kiakili na kisaikolojia-pumziko la Sabato.
  Huwezi kuupata wokovu bila ya kuwa Msabato halisi hasa kama uliwahi kusikia habari za Sabato na Bwana wa hiyo Sabato. Na hii miongoni mwa vipengele vya njia nyembanyemba iendayo uzimani. Nayo ina watu wachache tu, wanaoiona. Walio wengi, hawaioni huku wakidanganyika kuwa eti wana wokovu!!
  Hakuna wokovu kwa watu walio nje ya Amri za Mungu ikiwemo na Sabato. Pigeni porojo zooote, lakini huu ndio msimamo wa mbingu wa siku zote.
  Sabato njema nyote.
  Siyi

 58. Siyi,

  Kwa nini sasa unatatizika? Si hiyo ukosefu wa wokovu ndio inakutatiza? Unapokuwa na Mungu anaeitwa sabato, Yesu, Bwana wa sabato atakupiga teke.

  Asante

 59. Sungura,
  Ni kweli Musa alikufa. Na Biblia inaonesha kuwa alitwaliwa mbinguni. Soma Yuda 9. Japo aya hii haioneshi moja kwa moja kuwa Musa alitwaliwa mbinguni, sisi wasabato tuna kitu kinachoitwa Roho ya Unabii a.k.a (nuru ndogo) inayotuthibitishia kuwa Musa alitwaliwa mbinguni
  “Moses passed through death, but Michael came down and gave him life before his body had seen corruption. Satan tried to hold the body, claiming it as his; but Michael resurrected Moses and took him to heaven. Satan railed bitterly against God…but Christ did not rebuke His adversary,…He meekly referred him to His Father, saying, “The Lord rebuke thee” Early Writings, p. 164.
  Sisi huwa hatubahatishi kiasi hicho kaka. Lakini zaidi ya hapo, wewe jiulize, umewahi kusikia kaburi la Musa lilipo kwa sasa? Nafurahi na wewe umekiri kuwa Musa alionekana kwenye ugeuko pale mlimani. Sasa swali la kujiuliza, aliendaje mbinguni?
  Hata mimi sikusema kuwa tutaishi mbinguni milele. Nilichosema ni kwamba, hatutaishi duniani. Hatutaikanyaga ardhi ya dunia hii tena!! Ninachojua ni kwamba, baada ya miaka elfu, makao aliyoenda kuyaanda Kristo (mji mtakatifu-Yerusalem), utashuka chini. Ukishuka chini, sisi hatutatoka kwenye mji huo kuishi duniani. Isipokuwa tutaishi ndani ya mji huo milele na Kristo. Kama wewe unaelewa tofauti, leta hoja kwa vigezo!!
  Aidha, mimi nashukuru tu kwa kujifunza kwako kumbe kunakusaidia. Sasa umepiga hatua nyingine ya kuelewa Safety na Salvation pamoja na mizizi yake!! Hatua kubwa hiyo mwanaume. Plz, nenda zaidi ya hapo!! Pamoja na kuziita shalom mind hoja zangu, nafikiri ungezipongeza maana zinakuongezea vitu vizuri vya wokovu japo, hutaki kukiri hivyo!! Pole sana.
  Na msingi wa Yesu ni kuwatoa watu duniani (kwenye dhambi). Duniani ndiyo kuna dhambi rafiki. Ndimo alimo ibilisi na malaika zake anayewafanya watu watende dhambi tangu mwanzo. Ibilisi alipoasi mbinguni, kulichafuka, ndiyo maana walimfukuza. Akashuka duniani (sehemu iliyokuwa salama) nako kukachafuka. Na kwa sababu ya upendo wa Mungu kwa wanadamu, Yesu alikufa ili atutoe kwenye hiyo hatari –dunia. Hata baada ya mji mtakatifu kushuka duniani baada ya miaka elfu, shetani alionekana kutaka kuushambulia tena mji. Moto ukashuka ukamlamba!! Ndipo tutaendelea kuishi ndani ya mji ule na Kristo wetu milele na milele.
  Hii ndiyo concept sahihi ya wasabato kuhusu wokovu!! Wokovu hauwezi kukamilika ktk maisha yetu kama bado tutaendelea kuwepo kwenye dunia hii. Mchakato ulishaanza (ukombozi), hatima yake bado, nayo muda si mrefu itafika.
  Hatima ya wokovu, ni maisha yasiyo na mashambulizi ya ibilisi. Life in absence of the Devil beside you!!
  Ubarikiwe

 60. Siyi,

  Musa alikufa, tena baada ya kumkosea Mungu, lakini Henoko alitwaliwa kwa sababu ya ukamilifu wake.

  Na hatusomi popote kuwa Musa alitwaliwa mbinguni kama Henoko na Eliya. Na havari za Musa zinakuja kuonekana tena katika mlima wa ugeuko.
  Unaweza kuthibitisha kwenye maandiko kuwa Musa alitwaliwa kama Henoko?

  Yes, maisha yetu ya milele hayatakuwa mbinguni bali ni duniani. Kama nasema uongo thibitisha hapa uongo wangu.

  Nafikiri hujui tofauti ya root word ‘SAVE’ inayozaa noun ‘SALVATION’ na ‘SAVE’ inayozaa noun ‘SAFETY’.
  Kimsingi maana ya wokovu unayohangaika nayo(Kutolewa sehemu ya hatari kuja sehemu salama) siyo maana ya Salvation, ispokuwa ni maana ya Safety.
  Ndio maana unang’ang’ana na suala la kutoka duniani kwenda mbinguni ndio wokovu,ati kwa sababu shetani hawezi kuweko huko mbinguni tutakakokuwa.
  Wahat a shallow mind is that!
  Ivi unaelewa suala la miaka elfu baada ya kanisa kuwa limenyakuliwa, ivi unaelewa suala la shetani kuizunguka kambi ya watakatifu, hayo mambo yatatokea tukiwa mbinguni au duniani?

  Nafikiri wewe bado uko kwenye gereza la shetani, ndio maana akili yako haiwezi kuelewa kuwa maana ya Salvation ni kutolewa katika ufalme wa giza na kuingizwa katika ufalme wa mwana wa Pendo lake.

  Na hutaelewa maana akili yako imejaa magugu ya mapokeo, kama tu walivyo wasabato wengi.

  Kuzaliwa kwa Yesu Ktisto kulikuwa kwa ajili ya kuwaokoa watu na dhambi zao, si kuwatoa watu duniani. Hiyo kazi alishaifanya akamaliza na akaondoka.

  Msingi wa Wokovu ni kuwatoa watu dhambini, si kuwatoa duniani kama wasabato mnavyodai.

  By grace we are saved!

 61. Ziragora,
  Sishangai kukuona ukijikongoja kwa maneno machache yasomaana. Sina udini, udhehebu wala nini!! Nina dini ya Kristo pekee!! Nimeamua kuwa na dini ya Kristo tu kwa sababu yeye ndiye mwenye mbingu. Nataka kuja kuishi na Kristo siku zote. Sehemu alipo Kristo, daima ibilisi hatakuwepo!
  Kafara ya Kristo haikuwa ya kuwaokoa watu na kuwaacha tena kwenye ulimwengu huu wa dhambi!! Hasha!! . Mji anaoutuandalia Kristo, sheatni hatakuwepo kule! Changamkeni tu!! Acheni kupigwa changa la macho!!

 62. Sungura,
  Acha uchuro rafiki yangu. Jibu swali usipige chenga. Hoja ilikuwa ni kwamba, wewe ulikataa kwenda mbinguni siyo kuokoka; nikakuuliza kuwa, kama kwenda mbinguni, siyo kuokoka, walifanyaje? Kwa upande wa pili, katika maisha yao, walikuwa wachaji Mungu sana. Katika uchaji Mungu wao huo, nako kulikuwa ni kuokoka? Mtu anaweza kuokoka mara ngapi katika maisha yake? Je, kwa mfano hao wengine ambao hawakwenda mbinguni kama vile akina Ibrahimu, Isaka, Yakobo,Yusufu nk, nao wakati wa uhai wao kwa vile walikuwa ni wachaji Mungu, nao waliokoka? Na kama kwenda mbinguni siyo kuokoka,wao wokovu wao umeishia makaburini mwao? Haya ni miongoni mwa maswali ambayo wewe Sungura, uliyakimbia mbashala (live). Lwembe yeye akasarenda nusu, japo kwa shingo upande ya kuleta utatu wa wokovu –past, present na future!! Namsubiri naye ajibu kwa maswali ya mifano hiyo hapo juu!
  Bro. Sungura, kwa taarfia yako, aya za kuokoka in future ziko nyingi kuliko za past na present. Acha kudanganyika wewe!! Na kama kuna kuokoka duniani, thibitisha hilo kwa kujibu maswali hayo in relations to your personal interpretive verses of past and present!!
  Na hata kama hatutaishi mbinguni, NAOMBA UELEWE kuwa, kamwe, hatutaishi duniani tena!!! Soma vizuri na wewe maandiko. Acha ubishi wa kijinga kaka!! Kama unasoma Biblia inakwambia kuwa tutakuja kuishi tena duniani, nenda uvae miwani, macho yako yatakuwa na shida kama siyo akili yenyewe!!!
  Ubarikiwe
  Siyi

 63. Siyi,

  Nilikwanbia acha kupiga teke mchokoo, ila ulijifanya mjuajiiiii.
  Sasa badala ya kuongea sense unalalama tu, oh umetuuliza swala la Henoko, na Musa hatujakujibu lakini tumeongeza swali juu yake, n.k!

  Just use yo common sense, siwezi kujibu swali ambalo maelezo yake hayako sawa. Badala ya kueleza todauti ya wokovu wetu na wa akina Henoko lazima unithibitishie kwanza ni wapi biblia imesema Henoko au Musa aliokolewa.

  Halafu bajua jinsi maandiko yanayosema tumeokolewa/tuliokolewa/tunaokolewa yanavyokutesa, unatamani yasomeke vingine.

  Na kwa taarifa yako, yenyewe yako mengi kuliko yaliyo ktk future tense, pole sana.

  Teba mimi sitishwi na kuweka kwako msisitizo kuwa wewe hujaokoka, nami nakuhimiza kabisa kuwa acha, maana inakuhusu wewe.

  Ambacho nilishasema siwezi kukuacha ydanganye watu ni kule kuwaambia kuwa hakuna kuokoka duniani.

  Ulianza ukakataa kuwa Isarael kutoka Misri haukuwa wokovu kabla ya kufika Kanaan, tukakuthibitishia kuwa biblia imesema ulikuwa wokovu.

  Ukasena waliofika Kanaan hao sasa ndo waliokoka maana wasingerudi Misri(utumwani) tena. Lakini tukakukumbusha juwa baada ya hapo Israel waliwahi kwenda utumwani Babeli hata Misri tena.

  Ulisema hatua ta nwisho ya mchakato wa wokovu ati inaitwa Glorification, tukakwambia kuwa biblia inasema tayari sis tumeshatukuzwa na Kristo.

  Nafikiri ni nduguyo Mjema akasema kuwa kuokolewa ni kule kupata uzima wa milele, ambayo ati hatua ya mwisho kabisa.
  Naye hakukumbuka kuwa uzima wa milele ni huku kumjua Mungu na Yesu kristo, ina naama uzima huo tayari tuko nao ndani yetu.

  Ukasema tena kuwa Mungu haokoi na kukiacha kitu katika hatari, kitu ambacho ni kweli. Maaba alituokoa kutoka kati ulimwengu wa giza(hatarini ) na kutuingiza katika ufame wa nwaba wa pendo lake( usalamani), nasi tunalindwa na yule mwovu. Kama huko si kuwa salama ni nini? Au wewe unataka ukaishi mbinguni ndipo ujue uko salama?

  Nakukumbusha kuwa hatuendi kuishi mbiguni Siyi, baada ya kunyakuliwa na kula harusi ya mwanakondoo tutarudi duniani, na maisha yetu ya milele hayatakuwa mbinguni, soma vizuri maandiko.

  Siyi mnataka nini kama si ubishi tu wa kijinga na kiburi cha dini!!!

  Mambo mengi unayasema tu kwa fikra zako za kibinadamu, kisha ubajiamisha kuwa iko hivyo.

  Rudi kwenye maandiko ujifunze vizuri neno wokovu/kuokoka lilitumikaje itakusaidia angalao hata kule kujua kuwa neno hilo limetumika katika nyakati tatu, angalao kama nduguyo Lenda alivyojaribu kuelewa hizo nyakati, japo anazikiri na kuzionesha kwenye maandiko huku akiteswa na udanganyifu wa pando la dini yenu kuwa wokovu ni baadaye(future tense pekee).

  Saa ya wokovu ni sasa!!!

 64. Siyi, acha uoga!

  Hakuna lugha ngumu unayoiongea, ninachokiona kwako ni uoga wa kusahihishwa tu, na ndio unao kuvuruga!

  Kwanza nilikuona umeuona Utatu wa Wokovu, zile tenses tatu:Tumeokolewa, Tunaokolewa na Tutaokolewa. Hatua iliyobakia ilikuwa ni ndogo sana, huo Utatu kuwa Mmoja! Ukibaki ktk hizo tenses utaishia ktk fanatism, maana tense mojawapo ikisimama kipekee hukupeleka huko kama ninavyokuona jinsi inavyokutoa ktk Maandiko!

  Ole wao, hao walimu wako, kwa kuwa wameuondoa ufunguo wa maarifa, wamekuacha unazunguka kama pia; bali ukitulia uyasikilize Maandiko, utarudishiwa ufunguo!!

  Acha kutaharuki, tulia niyamalizie hayo uliyonituma nikajifunze!

  Gbu!

 65. Mjema,

  Asante kwa maswali yaliyoambatana na maelezo.

  Umeniuliza maswali matano, ktk maswali hayo kuna ambayo majibu yake yako ktk sehemu hii tunayoiendea sasa, kwahiyo ningekuomba uyaangalie huko na iwapo kuna mapungufu yoyote, basi nitafurahi tuyatazame sote upya!

  1. Kuhusu nini/kipi kinachookolewa PAST, kipi PRESENT na FUTURE;
  Nitajibu kinachookolewa Past kama hivi:
  Mwa 1:26 “Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu …”; Huyu ndiye aliyekombolewa huko alikochinjwa Mwana-Kondoo, kwani huyo ni sehemu ya Mungu ambayo asingeiacha ipotee! Basi kwa kafara hiyo, wote ambao majina yao yameandikwa ktk Kitabu cha Uzima cha Mwana-Kondoo, huyo aliyechinjwa kwa ajili yao, WALIOOKOLEWA kutoka mautini na hivyo hawafi tena (1Yn 3:14 “Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mautini kuingia uzimani”), tangu huko ilikotolewa Sadaka hiyo kwa ajili yao, kilichokuwa kimebakia ni wao kupelekewa Habari ya Ukombozi wao kwamba Deni yao ya Dhambi IMELIPWA, ndipo kwa Habari Njema hiyo iliyoshikamana na Nguvu ya Wokovu ambayo ndiyo ile IMANI, nafsi, yule Adamu wa Mwa 2:7 “BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai”, zilitoka zikawa HURU na UTUMWA wa Dhambi!

  Nalo jambo hili la wao KUOKOLEWA huko nyuma ungeweza kulifananisha na jambo hili tunalotangaziwa leo hii, likifanywa hai kwa tukio lililotokea miaka 2000 iliyopita nasi tukitangaziwa kulipata huko lilikotokea licha ya kwamba hatukuwepo huko, bali hulipokea leo hii! 1 PET‬ ‭2‬:‭24‬ “… na kwa kupigwa kwake mliponywa.” Sio mnaponywa au mtaponywa, hapana, MLIPONYWA hukoooo miaka 2000 iliyopita!!! Ni mambo ya rohoni, mwilini ni vigumu kidogo kueleweka, lakini maadamu tunajifunza, tutapanda darasa!!!

  Swali na 2-4 Ninayaacha kwanza

  5. Ni nini tofauti kati ya Wokovu na Ukombozi?
  Wokovu ni ule Uamuzi wa kuilipa gharama ya Mauti yaani Ukombozi. Kwahiyo ndani ya Wokovu ndimo mna mchakato mzima unaoukamilisha Uamuzi huo, unaoanza na Ukombozi unaopelekea KUOKOLEWA kwa hao waliokombolewa.

  Kuhusu hayo unayonikumbusha, ninakushukuru sana, lakini tuendelee kuyaangalia Maandiko yanachokifunua huenda yakatupa Ufahamu ulio bora zaidi!

  Asante, &
  Gbu!

 66. Sungura,
  Naomba nipige ndege wawili kwa jiwe moja (nijibu pachiko zako mbili kwa yangu moja tu) tena dogo.
  Ukisema hujaelewa, napo sioni shida kwangu maana nakujua kwa kiasi Fulani. Na ninapenda nikwambie kuwa, mbinguni hakuna atakayeasi, maana kinyonge hakitaingia huko. Kama na sisi Biblia ingesema kuwa tutaokolewa kama watu wa enzi za Nuhu, Lutu, Israel n.k. na kisha wakaendelea kubaki duniani(sehemu shetani alipo), uwezekano mkubwa wa kuja kuasi tena hata kwetu, ungekuwepo!! Ndiyo maana ninyi akili zenu kwa vile bado zimefungwa, hamuwezi kuona tofauti hiyo. Kwa ujasili kabisa wa kutokuelewa, mnanunukuu aya za Biblia kuhalalia upuuzi huo!! Na msipoangalia, mtaendelea na ubishi huohuo baadaye mtakuja kufa kibudu vijana!! Angalieni sana. Mungu hana kigeugeu na wala hana pande mbili, tatu saba nk. Msidanganyike!!
  Wokovu wa awamu hii ni tofauti sana na ule wokovu wa zamani kama mnavyouita!! Safari hii, destination yake, ni mbinguni, sehemu ambako ibilisi hayupo. Kwa maneno mengine, WOKOVU aliouleta Kristo, bila ya kutupeleka mahali pa salama ambapo shetani na malaika zake hawapo, WOKOVU huo haujakamilika. Ndiyo maana Yesu alitoa ahadi…NITARUDI TENA NIWAKARIBISHE KWANGU, … Sehemu Kristo alipo. Vinginevyo, kwa kifo chake msalabani, angesema nimemaliza, asingeahidi tena.
  Lakini watu mnaojidai mnaona kumbe vipofu tena wa kutupwa, mambo haya hamtayaelewa; ni mpaka mmefunuliwa!! Ndio maana mnasema, wokovu siyo kwenda mbinguni!! Kwa maneno mengine, mnakana kuwa YEsu hatarudi tena!! Mnafikiri kauli za namna hiyo kama si za ibilisi ni za nani??? Niliwauliza, kama hata duniani watu wanaokoka, je, akina Ibrahimu, Henoko, Eliya, Musa nk. nao waliokoka? Badala ya kujibu, mnarudisha maswali yaleyale kana kwamba hamjayaelewa!! Acheni usanii huo!!
  Nawapa pole sana marafiki zangu. Sisi akina Siyi, tumeshautambua ukombozi wa Mungu, na tunasafiri kiimani tukimgonja Kristo ili aje atutoe kwenye dhiki!! Tuko kwenye dhiki maana bado tuko duniani –hatujaokoka, Yoh 16:33. Waliokoka, hawakai kwenye dhiki bro!!
  Safari hii, WOKOVU ni beyond human imaginations bro!! Yohana anasema sikio halijawahikusikia, jicho halijawahi kuona, ulizi kuonja….. yaani beyond zaidi ya beyond!! Ni tofauti na Israel kwenda kanaani, kutolewa babeli nk.
  Kama wewe wokovu wako ni wa duniani, nakupa pole sana.
  Siyi

 67. Naam kaka Haule,
  Nilitarajia watu kunishangaa sana maana wamekaririshwa mambo ya ajabu kweli. Biblia hii ukiisoma kama gazeti, utaishia kuwa na uelewa tenge na hatimaye utapotea pamoja na jitihada zote ulizodhani kuwa ni za kiimani!! Ndani ya Biblia, kaka Haule, hakuna fumbo!! Hakuna aya yoyote inayooelezea mambo tata!! Sisi wenyewe tu na wachungaji, walimu na waingilisti wetu ndiyo huwa tunajikoroga!! Wale wanaoisoma kama gazeti, wakisoma aya inayosema “msinyimane….”, wengine huitumia kuhalalisha uzinzi. “akupigaye shavu la kulia, mgeuzie na la kushota….” Kweli wengine hufanya hivyo. Halikadhalika, na baadhi yetu wanaoosoma “waliokolewa”, humaanisha kuponywa kijumla japo mtu mhusika aweza kufa, kuugua tena n.k. Wanamfanya Mungu kuwa UNPERFECT na mambo yake kuwa UNPERFECT!! Ukiwaambia acheni uzinzi, wanakunukulia aya ya Biblia inayosema, “msinyimane”. Very Fanatic!!
  Watu wa namna hiyo, huwa hakuna namna ya kuwasaidia isipokuwa kuwaombea tu.
  Nakusubiri na interpretation ya mbwa wa Agano Jipya kaka.
  Ubarikiwe na Bwana.
  Siyi

 68. Kwako Siyi.

  Kuna upuuzi umeusema muda mrefu sana tumekunyamazia, sasa naona unazidi kuusema tu.

  Umesema Mungu hawezi kuokoa kisha akaangamiza. Huo ni uongo,ni wazo la kufikirika kwa kuangalia upande mmoja tu wa Mungu kuwa ni mwenye rehema.

  Ona gapa: ” .. God having saved the people out of the land of Egypt, He destroyed those who did not believe”. (Yuda :5) Au biblia ya kwako inasomekaje hapo?

  Halafu ivi biblia imesema kuwaHenoko, Musa ba Eliya waliokolewa? Ningependa nami nione hiyo sentensi!

  Umekuita kule kukiri kwetu kuokoka kuwa ni kuwa ‘fanatic’.
  Ok, inawezekana kabisa. But nani fanatic wa kwanza kati yetu na biblia iliyosema maneno kama haya: ” He is the one who saved us, and called us with a whole calling… (2Tim 1:9)

  Siyi hebu kubali kuelewa maana ya neno Wokovu/Kuokoka kibiblia, na lilivyotumika katika muktadha wa kimaandiko. Usikomee tu kujua kuokoka ni kutoka sehemu ya hatari na kuwa sehemu salama.
  Unatakiwa kujua huko kutoka sehemu ya hatari na kuwa sehwmu salama ni kupi hasa, yaani hatarini ni wapi na salamani ni wapi!

  Ukifanya hivyo utapumzika kupiga teke mchokoo.

 69. Mjema,

  Ninachotaka ujue ni kuwa hakuna kitu chochote hapa unachonifundisha wala ukweli wowote unaonipa kwa habari ya kuokoka. Hilo lielewe kabisaaa, wala usijifariji. Nakijua vema ninachokitetea hapa.

  Kuna sehemu nahisi umejichanganya, au hujui tunachojadili hapa. Lakini ili nijiridhishe acha nikuulize maswali mafupi.

  Kuokoka kiroho ni kupi?
  Lakini kama wafia dini japo kimwili walikufa ila kiroho waliokoka, waliokokaje wakati kumbe kuokoka ni mpaka kufika mbinguni, na tunajua mtu akifa haendi mbinguni mpaka unyakuo?

  Halafu hakuna wokovu wa kikwetu na wa kikwenu, wokovu ni mmoja tu huo ambao kwa kiebrania unaitwa SODZO na kiyunani unaitwa SOTERIA. Wewe nilisikia umeenda chuo cha biblia, inakuwaje hujui haya maneno?

  Maswali uliyouliza majibu yake yako kwenye mada ya tulikojadili maana ya kuokoka, kayacheki huko.

  Ila jibu la swali la mwisho jibu ni kama ifuatavyo:
  Kuokolewa toka kwenye meli ni sawa na kile kitendo cha Petro kuokolewa na Yesu alipotembea juu ya maji na kuanza kuzama.

  Sasa na wewe jiulize kama Yesu alikuwa amekuja kumwokoa Petro na kule kuzama baharini au alikuwa amekuja kumtoa ktk utumwa wa shetani ambako ndiko kuokoka ambako sisi tunakuongekea.

  Hilo ndo jibu!

 70. Siyi,

  Ni kitu gani unachosema tumeelewa, kwamba na Mjema tumemwelewa?

  Hakuna chochote kuntu kwa habari ya kuokoka ambacho mnaweza kuongea kikaleta maana, mmedanganywa ile mbaya na mmefungwa kwa sababu ya ujinga uliojaa akilini mwenu.

  Wewe ulikataa kuwa Israel kutoka kwao Misri biblia imesema waliokolewa na wakaangamizwa walioasi.
  Mjema akaje akakubali maana aliliona andiko hilo katika kitabu cha Yuda, lakini akasema ati lugha iliyotumika hapo haina maana ya kuokoka.

  Imagine baadae Mjema anasema kufika Kanaan ndo ilikuwa kuokoka kwa vile wasingeweza sasa kurudi tena Misri.
  Anashindwa kuelwa kuwa baada ya hapo Israel walikwenda utumwani Babeli wakitokea hukohuko Kanaan.

  Ndiposa muelewe tunachowaambia kuwa wokovu alooleta Yesu si kwenda Mbinguni bali ni kutolewa katika utumwa wa shetani. Ni wokovu wa rohoni.

  Siyi nilikushauri ujifunze vizuri lugha, vinginevyo utaishia kulaumu kuwa hujajibiwa maswali yako. Siwezi kukujibu kama unavyotaka wewe.

  Na Lwembe kakufafanulia zaidi neno “escape”

  Kama kuna jambo linanifanya mpaka nihisi kuwa inawezekana kabisa usabato nao ni ‘cult’ ni vile mnavyolazimisha kupindisha maneno kila tunapowapa mistari inayosemea kuokolewa in past tense.

  Huwezi hata ukathibitisha kimaandiko kuwa kwenda mbinguni ndio kuokoka.

  Usishindane na ukweli wa maandiko.

 71. Kaka Siyi

  Angalia maandiko haya ya “Mdo 2:47” na fumbo la roho ya dini na fundisho lake,

  “wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa WAKIOKOLEWA.”

  Kwa fumbo la roho ya dini yako unatuambia tuone pameandikwa WAKIKOMBOLEWA na sio wakiokolewa,

  Niliposoma hili bandiko lako………….. jioni hii,
  Nikamtafakari Mbwa aliyeandikwa ktk agano jipya

 72. Lwembe,
  Umejitahidi sana kuelezea habari za kuokoka duniani!! Hadi nashangaa mimi na rafiki yangu Mjema, kwa nini hamtuelewi?? Tunazungumza lugha gani iliyo ngumu kueleweka kwenu? Nahisi mnatakiwa kutofautisha usalama tunaoupata baada ya kumwamini Kristo na usalama tutakaoupata baada ya kutwaliwa zetu mbinguni. Hiki ndicho kiambaza ambacho nini mnakichanganya sana.
  Shortly;
  Matokeo ya uasi wa wazazi wetu wa kwanza, hatuwezi kuyakwepa kwa sasa -kifo cha kimwili. Kipo na tutaendelea kufa hadi Kristo atakapokuja kukikomesha! Na mnajua kabisa kuwa, kifo hiki, ni matokeo ya huo uasi ambao na sisi (kama vizalia vya waasi -Adamu na Hawa), tumeathiriwa, ndio maana bado tunakufa tena kwa njia mbalimbali i.e maradhi, ajali, uzee tu, kunyongwa n.k. Zaidi ya matokeo haya, kilikuwa ni kifo cha kupotea milele -kutokuwa na Mungu daima tofauti na ulivyokuwa mpango wake toka mwanzo!!
  Mpango wa ukombozi ulipofanyika, haukulenga kutuokoa na kifo cha kimwili. Ulilenga kutuokoa ili tuwe karibu/tuishi na Mungu milele. Ili tuishi milele, wale wanaoupokea huo mchakato awali wa ukombozi, ndio wanaoathiriwa na cheche kiduchu katika hali zao za kimwili (i.e kuponywa maradhi, kuacha dhambi n.k.) japo kifo cha kimwili(gereza la mauti) kinawangoja. Ndiyo maana nawaambieni, Mungu hawezi kuokoa mtu (kwa maana ya kumfanya awe salama kimwili na kiroho) ilhali bado yuko chini ya athari/matokeo ya dhambi –kifo. Hapa ndipo mmepigwa changa la macho!! Na hamtaki kuelewa/kukubali kuwa mmeingia mkenge!! Mungu hawezi kuokoa nafsi ambayo bado inaweza kupitia masaibu mengi. Huko siyo kuokolewa, bali ni kuponywa tu, kwa maana kwamba, unaweza kuugua/kuasi tena. Yule aliyeokolewa na Mungu, hawezi kufa kifo cha namna yoyote ile (kimwili au kiroho). Hawezi!! Mungu ana uataratibu maalumu katika utendaji wake wa mambo. Ili mchakato ukamilike, daima huwa na hatua mathubuti. Huwezi kusema/kutumia neno NIMEKAMILISHA jambo, ilhali bado uko hatua ya kwanza ya mchakato. Kwa Mungu havitoki vitu nusunusu wapendwa. Mungu hutoa vitu vilivyo kamili. “ na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka” –Yakob 1:17. Huwezi kusema uko kariakoo ilhali ndio umepanda gari la kwenda huko tena uko kituoni mbezi, kimara, ubungo au mbagara!! Watakucheka sana na hata Mungu atakushangaa sana. Hivyo wapendwa, kwa mantiki kama hizo, hatuwezi kutumia neno NIMEOKOKA!! Mngesema mmekombolewa, hapo mngeeleweka vyema sana na watu wangefahamu kuwa, bado mna safari (ya kiimani), ili mje MUOKOLEWE baadaye!! Maana pamoja na kuwa mmekombolewa, wenye uamuzi wa kutaka kuokolewa baadaye, ni ninyi wenyewe!!
  Lwembe na Co (kana unavyoitumia kuturejelea sisi), WOKOVU wa mwanadamu aliye hai ni long process wapendwa!! Mungu alishaukomboa ulimwengu mzima kwa njia ya mwanaye. Wale watakaoutambua na kuufuata ukombozi huo, ndio watakaookolewa!!. Sasa hivi, tumekombolewa tu, kuokoka bado!! Kusema hivi, haina maana kwamba akina Siyi na Mjema, hawaujui wokovu! Hasha!! Wokovu tunaujua sana ndiyo maana tunapoteza muda mwingi kuwafundisheni na ninyi ili muujue, maana mnachoking’ang’ania siyo wokovu bali ni maluweluwe na danganya toto tu!! Ni danganya toto kwa sababu, inampumbaza muumini (yule aliyeutambua ukombozi), na kumfanya aduwae, aendelee ktk dhambi na kutofanya chochote kwa ajili ya waokovu wake wa baadaye, maana anaamini kuwa, akiwa mwenye dhambi hivyohivyo, eti yuko salama!! Huo ni uongo wa ibilisi wa kuwapoteza yumkini hata walio wateule!! Take heed!!
  Ndiyo maana kwa kipindi cha nyuma, niliwauliza kuwa, akina Adamu hadi kizazi cha Yakobo (Israel) ambao walikombolewa kwa damu za wanyama; nao waliokoka? Kama waliokoka, unawezaje kuutofautisha wokovu wao na ule wa akina Henoko, Eliya na Musa ambao walichukuliwa mbinguni? Nasikitika hadi leo, maswali ya namna hii hayakujibiwa hadi leo, japo watu wameng’ang’ana na kauli mbiu, nimeokoka, nimeokoka; very fanatic!!
  Wokovu, unahusisha kusalimisha katika hali zote –kimwili na kiroho. Wanaosalimika kimwili tu, hao huwa wameponywa na dhahama za muda/kitambo tu. Wale walio salama kiroho, ni wale walioutambua ukombozi –kafara ya Kristo, japo kifo cha kimwili na masaibu ya dunia hii bado yanawangoja. Wajapokufa leo kwa kifo cha kimwili, watakuja kuishi milele na Kristo. Na waliookolewa, ni wale walio salama kimwili na kiroho. Duniani, huwezi kuwa salama kimwili na kiroho!! Huo ndio udanganyifu mnaoung’ang’ania wapendwa!! Tutakuwa salama kimwili na kiroho-tutaokolewa tutakapofika mbinguni, sehemu ambayo, hakuna kilio, maumivu ya aina yoyote na wala kifo hakitakuwepo tena huko!!
  Kwimbila guru kumala amimbo!!
  Siyi

 73. Ziragora,
  Hata wengine wasioelewa kama wewe, nao waliendelea kunishangaa kama unavyofanya wewe. Hata mimi nami nakushangaa. Mimi sina vidhehebu rafiki rangu. Nina imani ya Kristo ndani yangu tu! Nina imani utakuja kunielewa baadaye. Shetani ni mjanja sana. Na kama hujamwelewa, yeye huchukua sehemu kubwa ya ukweli (99%) na na kisha kuichanganya na uongo (1%). Sasa ni ngumu sana kumwelekeza mtu aione hiyo moja zaidi ya 99 alizo nazo. Na ameteka watu wengi sana kwa mtindo huo!! Nao wanaamini kuwa wako sahihi. Hiyo ndiyo kazi kubwa!!

  Saa inakuja mtatuelewa tu. Mambo yatakapowachanganyia, mtakuja kukumbuka haya tuyasemayo mimi na Mjema. HAtari ni kwamba, mnaweza kuzinduka mkiwa mlishachelewa tayari. Hasara iliyoje!!
  Changamkeni marafiki zangu. Tunawapenda sana, hatutaki mpotee!! Tunazidi kuwaombea tu!
  Siyi

 74. Lwembe,

  Nashukuru kwa kuendelea kutuelewesha kuhusu “kuokoka hapa dunian tungali vitani” uenda tutaelewa! Hata ivyo,wakati unaandaa wokovu kwa wakati uliopo na ujao naomba ujibu maswali yafuatayo kutokana na hoja zako unazofafanua?

  1.Ni nini\kipi kinachookolewa PAST,kipi PRESENT na FUTURE.

  2.Je,mtu anaweza kuokoka PAST na PRESENT ila akapoteza Wokovu kwa mtazamo wa FUTURE?

  3.Ikiwa “ukiamini na kubatizwa umeshaokoka” vipi kuhusu kina akani na kora agano la kale,na Yuda agano jipya,unawaelezeaje?

  4.Ni kweli kuwa,Mungu aliandaa mpango wa Wokovv tangu kuumbwa misingi ya ulimwengu na yeye ni yule yule Jana, Leo na Milele, sasa wewe,Lwembe ulikuwepo tangu kuumbwa misingi ya ulimwengu ili uhusikane na iyo past.

  5.Ni nini tofauti kati ya Wokovu na Ukombozi?

  Mwisho:

  Nataka nikukumbushe kuwa baada ya kuamini na kubatizwa, ni hatua ya kwanza tu,katika mduara wa wokovu-kwa maana ile ya umilele, ni sharti uilinde na kuvumilia na iyo imani ambayo ujaribiwa km dhahabu,ndipo utakapookoka!

  Hata,Paulo anatukumbusha kuwa, kumwamini na kubatizwa Yesu sio mwisho,lazima tuvumilie kama mkulima avumiliaye msimu mzima akitazamia mavuno.pia yeye anasema,sio kwamba amefika ila anapambana ili hatimaye aipate mede ya ushindi.!

  Lwembe, ni kweli kuwa Mungu anaweza kutunasua toka ktk hatari fulani “KIMWILI” kama ilivyokuwa kwa Israel, toka Misri-ambao baadae aliwaangamiza kwa kuwa hawakuwa tayari kuurithi wokovu wa kiroho. Ila mpendwa uwezi kuegemea kwenye nguzo hii ya mchanga ukadai upo salama.

  Vivyo hivyo, wapo waliopoteza Wokovu Kimwili, Ila Wokovu wa Kiroho-ni washindi na zaidi ya washindi

  Karibu,Mtumishi.

 75. Siyi, Mjema & co,

  KUOKOKA kunakotokana na UKOMBOZI:

  Kimsingi, tunauchunguza ule UTATU wa KUOKOKA ili tupate uelewa kamili wa jambo hili la WOKOVU ulioleta UKOMBOZI wetu.

  PAST TENSE – JANA – (Yesu Kristo ni yeye yule JANA…)
  Ktk kulifikia jambo hili la KUOKOKA, tulilitazama jambo la Kuanguka kwetu, ili kubaini TUMEOKOLEWA kutoka jambo gani. Nayo Maandiko yakatuambia, Rum 5:12 “… kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi”; chimbuko la shida hii tunaliona hapa, Mwa 2:17 “… matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.”

  Matunda ya mti huo yaliliwa kama tunavyosoma ktk Mwa 2:6, nayo Dhambi iliyoongazana na Mauti vikawafikia, kama Mungu alivyolihukumu kosa hilo; hivyo Hukumu ya Kifo ikawafikia na kuwashikilia wao na vizazi vyao vyote.

  Lakini pia tumeona kwamba licha ya jambo hili kufanyika hapo Mwa 2:6, Injili imetufunulia jambo jingine lililofanyika huko nyuma, hapo ilipokiwekwa misingi ya dunia, linalohusiana na hili Kosa na Hukumu yake, Mungu akituonesha kwamba aliyajua yote kabla hata hayajatendeka ktk mwili; ndipo AKATUKOMBOA HUKO NYUMA, mapema, akailipa Gharama ya HUKUMU YAKE JUU YA WANAWE, yeye mwenyewe kupitia huyo “… Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia”

  Twasoma pia, kuwa huko alikochinjwa huyo Mwana-Kondoo, majina ya waliokombolewa kwa tendo hilo, yaliandikwa ktk Kitabu chake cha Uzima, yaani hao aliowaona wakiupokea Ukombozi huo; wale ambao hawakuupokea, majina yao hayakuandikwa, kwahiyo hawahusiki na Ukombozi huo, na hivyo wao ni “dugu moja na Mauti”! Ufu 13:8 “Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia.”

  Kutoka Andiko hili ndio tunafahamu kwamba Wokovu ni kwa waliokombolewa, hao ambao majina yao yameandikwa ktk Kitabu cha Uzima; Dan 12:1 “… na wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile.” Nako kuandikwa kwa majina ktk kitabu hicho ni kulingana na jambo la kwamba, hapo Mungu alipotuangalia kimbele, aliwaona wakiipokea Habari Njema ya Wokovu wao wanaoitiwa, jambo ambalo lilikidhi kigezo cha wao kuandikwa majina yao, yaani wakiwa ndio hao walioitwa, Mt 22:14 “Kwa maana waitwao ni wengi …”

  Basi jambo hili, kivuli chake unaweza kukiona kwa Israeli walipoitwa kutoka Misri, wakiisha kukombolewa kwa damu, wakaondoka Misri, wakiwa ni hao WALIOOKOLEWA, ile Hatua ya Kwanza, kule Kuhesabiwa Haki kwa kumwamini Mungu walipouitikia wito wake, haijalishi mazingira au adui ana nguvu kiasi gani, Mungu huilinda Ahadi yake ukimwamini; nalo kundi lote likabatizwa ktk bahari ya Sham kuwa wa Musa; na walipoibuka kutoka ktk tumbo la bahari, walikuwa ni mashahidi wa wokovu wao, kule Kuokoka kulikotokana na wao kumuamini Mungu alipowapa neno hilo; ndio unawaona wakiingia ktk roho na kumshangilia Bwana, Kut 15:1- “Ndipo Musa na wana wa Israeli wakamwimbia BWANA wimbo huu wakanena, na kusema, Nitamwimbia BWANA, kwa maana ametukuka sana … BWANA ni nguvu zangu, na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu.”!

  Ndio kusema, Kanisa, sisi waaminio wa leo, kwa kule kuiamini Injili tuliyohubiriwa, iliyotudhihirishia jinsi tulivyo wenye dhambi na wenye kustahili Hukumu, ikatuonesha na jinsi ya kuikimbia Hukumu hiyo kupitia huyo Mwana-Kondoo wa Sadaka aliyetupatia Mungu, Yn 1:29 “… Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!”; Basi, kwa Kuziungama dhambi zetu, tulizitua hapo miguuni pa Kristo, yule Mwana-Kondoo aichukuaye dhambi ya ulimwengu, akauchukua uzinzi wetu, hiyo mauti, ndipo ukamilifu wa huko kubadilishana mizigo, ni lazima uwe huko mautini, Kristo aliyefufuka huwezi kumsogelea, ndio maana unazamishwa huko chini ya maji ikiwa ni ishara ya kufa na kuzikwa pamoja naye, kama israeli walivyobatizwa wawe wa Musa, ndivyo nasi twabatizwa kwa Jina la Bwana Yesu Kristo ili tuwe wake, huyo aliyetununua kwa damu yake, inayotukosha na kutupa Uzima wa Milele alionao yeye, naye kubaki na mauti yetu, Rm 6:5-6: “Kwa maana kama tulivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika tutaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake”; huku ndiko Kuokoka inakokufundisha Biblia; Mk 16:16 “Aaminiye na kubatizwa ataokoka”, ni kwa huyo aliyefufuliwa kutoka mautini!

  Ndipo kulingana na lile jambo la Majina kuandikwa, twafahamu kwamba kuipokea kwetu Injili, yaani kule Kuiamini, ndio udhihirisho wa majina yetu kuwa yaliandikwa ktk Kitabu cha Uzima. Nao uthibitisho wa kiMaandiko wa jambo hili unaweza kuusoma ktk Lk 10:20 baada ya wale 70 kurudi wakifurahia matendo makuu yaliyofanyika ktk huduma yao, kumbuka kwamba na Yuda Iskariote alikuwa miongoni mwao: “Lakini, msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii; bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni.”

  Basi, kwa kadiri utakavyolitazama jambo hili la Kuokoka na hayo majina kuandikwa, utaona kwamba IMANI ndiyo kigezo cha kwanza ktk kutimia kwa mambo haya. Ili ufike ktk kumuamini Mungu ktk anachokuahidi au kukufunulia, ni lazima Imani iwe imepandwa moyoni mwako kwanza, nayo IMANI, Maandiko yanatuambia kwamba huja kwa kusikia, na kusikia huja kwa neno la Kristo. Hivyo twaweza kusema kwa uhakika kwamba Imani imewekwa ndani ya Injili.
  Lakini Imani ni nini? Heb 11:1: “… imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.”
  Ndipo Imani ikiisha kujengeka, zile Ahadi tulizozipokea ktk MATARAJIO hubadilika na kuwa HAKIKA na BAYANA, hata ikiwa ni Ahadi ya “Kuokoka” kama hiyo tunayoiona ktk Mk 16:16; hii ndiyo sababu pekee ambayo unawaona wakristo wakikiri KUOKOKA leo hii, kwani Tumaini husubiri hayo yatakayo patikana huko mbele, lakini Imani hukupatia hayo sasa hivi, hata huo Wokovu!

  Basi, kwamba Mungu alimtoa Mwana-Kondoo huko ilipowekwa misingi ya dunia, akatukomboa kutoka mautini, naye Kristo akaja kulidhihirisha jambo hilo; basi Habari Njema za Kukombolewa kwetu zilipotufikia, ndio unatuona tukikutangaza Kukombolewa kwetu hapo tulipomwambia bwana jela alifungue lango nasi kutoka nje tukiwa huru, TULIOOKOLEWA kutoka Hatia na Adhabu ya Dhambi hivyo tu SALAMA, tukiwaacha mautini jeshi zima la hao ambao majina yao hayajaandikwa ktk Kitabu cha Uzima, kama wale Wamisri waliofia baharini!!

  Hii ndio ile Hatua ya Kwanza, KUHESABIWA HAKI KWA IMANI, kule “Kupewa Moyo Mpya wa Nyama” ule wa jiwe tukiuacha huko mautini! (Eze 36:26)

  Tutaiendea sehemu ya pili ya ule Utatu wa Kuokoka tuitazame “Present tense” -TUNAOKOLEWA.

  Gbu!

 76. Siyi, Mjema & co,

  Neno “escape” lina maana hizo hizo za ‘toroka’, kumponyoka adui’, pamoja na ‘kuokoka’, kutegemeana na maudhui ya unachokisema; ndio maana kutokea mwanzo nilisema ninalitazama jambo la KUOKOKA ktk mantiki ya UKOMBOZI wa zile nafsi kutoka katika Hukumu!!!

  Kwahiyo, naona nimalizie lile somo uliloniambia nikajifunze, ambavyo ninaamini kwamba niliyoyaona huko yatasaidia kuwainua kiufahamu kiasi kwamba hata hayo maswali yako yatayeyuka!

  Uwe na subira kidogo, utauelewa tu Wokovu ni nini kwa hapa duniani!

  Gbu!

 77. Brother Siyi,

  Hivi umekataa kuacha hivyo vihekalu vyako vidogo vidogo? Utaangamia wewe . Usilete mzaha ndani ya maneno ya Mungu. Hivi sabato zako zinakutania wapi na wokovu? Toka kule ulipo, ni pabaya tu, ni kuangamia tu!!! Unasema una uhakika na wokovu bila kujua wokovu ni nini? Ukiwekwa pamoja na maandishi na mafarisayo, utasema kama Yesu atundikwe kwani ameivunja sabato!!!! Njooni chini ya msalaba uokolewe, kaka!!!

  Mungu akuwezashe.

 78. Sungura & Lwembe,
  Naona mmenielewa vyema. Na hata Mjema mmemwelewa vyema pia. Na niliwashauri tangu mwanzo kuwa, msiisome Biblia akama gazeti. Mungu hajawa mpumbavu wa kuokoa halafu aangamize baadaye. Mungu habahatishi wapendwa.
  Nilidhani kuwa mngejibu maswali yangu kwa mchanganuo maridhawa, jambo ambalo halikufanyika.
  Hoja za Sungura nilizijibu vyema sana . NA hata Mjema naye kafanya vivyohivyo!! Nilitarajia kuwaona mkirespond kwenye maswali niliyowaulizeni. Mf. Kama secape ina maana ya kuokoka, Je, Kristo amekuwa mwizi kiasi cha kutuponyoa mikononi mwa ibilisi? Hawezi kutuokoka tu kwa nguvu na uweza wake hadi atuiibe -atuponyoe??
  Badala ya kujibu maswali na hoja zangu za kimaandiko, mmekimbilia kutoa porojo ndeefu zisizo na maana.
  Kama kweli ni waungwana, nawaomba mjibu maswali yangu kwa ufasaha!!
  Nawangoja!
  Siyi

 79. Sungura,

  Majibu ya hoja zako haya hapa:

  1.umesema safari ya waisrael toka misri hailandani na yetu toka dumian kwenda mbinguni! AU kanaani na mbinguni tofauti!

  Jibu:Kaka,mlandano ninaouongelea ni ule wa Neno la kingereza , “similar” na sio “identical”! Kwani wewe umewatazama kimwili na ukasahau kiroho!

  Fikiri kuhusu Yesu vs Kondoo waliokuwa wanatolewa kafara kabla ya kifo chake, upo mlandano ambapo kondoo alimwakilisha Yesu. This is “similar” but not “identical”.

  Umesahau kuwa kimwili vs kiroho vinakwenda pamoja. Mungu daima utaka tuwe huru kimwili ili tuwe huru kiroho! Usisahau hilo!

  Mlandano ninaouongelea ni huu:

  1.Israel walikuwa watumwa kwa Farao-misri,sisi tulikuwa watumwa kwa shetani-duniani

  2.Mungu alimtumia Musa kuwatoa israel kwa farao,Mungu amemtumia Yesu kututoa ktk makucha ya iblisi Tena yapo mengi ya kufanana kati ya Musa vs Yesu mfano,kuzaliwa na maisha yao ya utumishi.

  3.waisrael walitembea Jangwani yenye dhiki,leo tunatembea ktk dunia ambayo Yesu alisema,ni njia nyembamba,tena kunayo dhiki!

  4.Musa alikufa kabla ya kuwafikisha Israel Kaanani,Yesu imempasa kufa kabla ya zawadi yetu kwenda mbinguni.

  5.Yesu alikuwepo na kanisa Jangwani akimfariji Musa, Musa akiwa na Elia walimtokea Yesu ktk upweke na kumtia Moyo.

  6.Musa aliwatangulia waisraeli kwenda sio kaanani bali mbinguni, Yesu ametutangulia mbinguni kuandaa makao.

  7.Waisrael wengi hawakufika nchi ya kaanani,kwa sababu ya ukaidi wao,Yesu ametabiri njia ni nyembamba na watakaoiweza wachache.

  8.waisrael jangwani walipitia magumu ili kujaribiwa imani zao,vivyo ivyo nasi imani zetu ujaribiwa.

  Na mengne unaweza kuendelea!

  Hoja2:umeuliza ni wapi imeandikwa kuwa tunasafiri kwenda mbingu mpya na nchi mpya!

  1Pet2:11 Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho.

  Fil3:20-” Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo.

  Ufu21,22-inaeleza habari za mbingu mpya na nchi mpya,

  Hoja3:umesema Mungu akuwaokoa waisirael na Jangwa bali na utumwa!

  Ni kweli kwa mtazamo wa kimwili ila kiroho walipaswa pia kuwa huru, kwani bbdo wengn wao walivamani utumwa wa kimwili.kwa iyo kuokoka ni mpaka pale walipo ingia kaanani ambapo kamwe hawawezi rudi\waza misri.

  Zingatia hili:Jangwa ni mapatito kuuelekea Wokovu kama ilivyo duniani kuliko na dhiki, Yesu anasema tujipe moyo,yeye ameushinda ulimwengu!

  Hoja4:Je,Musa alipokufa,aliwatangulia Waisrael Kaanani.

  Jibu:Ndio,tena sio kaanani ya duniani bali ile halisi ya mbinguni.

  Hoja5:umesema kwamba nabishana na Yuda1:5.

  La hasha! Ukiongelea Wokovu kimwili-mtazamo hafifu ni kweli unachosema Lakini ukiongelea Wokovu kiroho-mtazamo sahihi,haupo sawa. na sisi hapa na wenzangu tunasisitiza wokovu kiroho,ambao uo tunaweza kudai kuwa umetimia pale tu,tutakapo wekwa mbali na dhiki na adui yaani mbinguni.

  Wako wafia dini ambao hawakuokoka kimwili yaani waliuwawa lakini Wameokoka.

  Na nyie, msiwasisitizie watu wokovu wa kimwili bali wa kiroho.

  Hebu ni kuulize sungura, huko kanisani kwenu,hakuna wagojwa wa saratani,ukimwi au hata walio kufa kwa malaria.Je,hao hawajaokoka kimwili? Kiroho Je,wameokoka?

  Asante kwa kujibu swali langu kwako kuhusu,Je, wale walioangamizwa Jagwani mfano,Akani na Kora,wataingia mbinguni?

  Swali hili lililenga kukutoa katika mtazamo wa kimwili tunaopambana nao hapa SG na kutaka ufikiri wokovu kwa maana ya kiroho, ukiweza kuwaza ivyo hutapata shida ya msisitizo tunaokupa hapa.

  Hata ivyo, Umejibu kwa mashaka,kwamba, uenda, Yesu alipozihubiri Roho zilizopo kuzimu waliamini na kutubu.!!

  Mh,hapa napo utazua mjadala, rafiki, wafu hawajui neno lolote! Usilete habari za maisha baada ya kifo.Itafakari biblia kwa ujumla wake!

  Hata,ivyo tusiongelee ilo la wafu,ninachotaka kusema kwenye jibu lako hapo juu ni:

  Nadhani umeshaelewa dhana ya kuokoka mnayoisisitiza nyie ni ya kimwili,hafifu,isiyo na uhakika,na iyo hasa, ndiyo muihubiriyo,tofauti nasi, tunaojua kuwa iyo ya kimwili ni given,wala sio ya lazima (kwani wapo waliopoteza iyo ya kimwili ila ni washindi na zaidi ya washindi) ukiipata ya kiroho ambayo kilele chake ni Yesu ajapo umeipata halisi!

  Sasa mpendwa hebu nijibu maswali yafuatayo:

  1.Je, mtu aliyeokoa ile ya kikwenu sodzo(past &present) anaweza kupoteza tena Wokovu (future)? Zingatia Yuda1:5.(swali hili sio geni kwako).

  2.katika wokovu wa sodzo unaofundisha hapa SG,ni nini kinachookolewa past,kipi kinachookolewa present na kipi future?

  3.kunatofauti gani kati ya Wokovu aliotuletea Yesu na ule ambao wanadamu wenzetu wanaweza kutufanyia.mfano.utasikia taarifa ya habari kwamba, “kati ya watu 80,waliozama kwenye ajali ya meli,ni watu 7 pekee WALIOOKOLEWA”!!

  Karibu mjoli!

 80. Siyi & Mjema,

  Kulingana na hatua tuliyoifikia ktk mjadala huu, yaani hapo tulipoyaendea yale maneno mawili “Redeemed na Saved” kuyachunguza, ninaamini kwamba kwa sehemu ufahamu wetu umeinuka, kwahiyo napenda kukushauri ndg yangu Mjema, jaribu kuisoma michango hiyo kwanza ili ujipandishe ktk ufahamu, kuliko hivi ambavyo unayarudia tuliyoyaacha, kule kunukuuu vifungu vya Maandiko bila Maarifa, kwani sasa tunalitazama suala la KUOKOKA ktk mantiki ya WOKOVU uliouongoza UKOMBOZI huo uliompeleka Kristo msalabani; hatuzungumzii uponyo au escape na mambo mengine madogo madogo ambayo kesho yanaweza kujirudia ktk mzunguko wake kulingana na yanavyotumika!

  Sote tumeona, kulingana na Maandiko, jinsi ambavyo neno KUOKOKA linavyojifunua katika namna tatu, zile tenses: 1. Kuokolewa – huko nyuma, 2. Kuokoka – sasa hivi, na 3. Tutaokolewa – huko mbele. Basi, huu ndio UTATU wa Kuokoka; Nao Wokovu haukamiliki pasipo huo Utatu uliojengwa juu ya Msingi wa UKOMBOZI!

  Agano Jipya ndilo linaloifunua Siri ya Wokovu, ile Injili ya mitume, ndipo kutoka humo tunafahamu kwamba: Sote tunakabiliwa na HUKUMU ya kifo, ile Mauti! Rum 5:12 “… kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi.” Hii ndiyo hali yetu, na sote tunakabiliwa na Mauti, kule kutengwa na Mungu milele kunakoishia jehanum ya moto!

  Je, kuna yeyote kati yetu anayeweza kuikimbia Hukumu hiyo? Mwenye dhambi hawezi kujiokoa wala kumuokoa mwingine, yaani mauti haiwezi kuikoa mauti; ni Uzima pekee unaoweza kuiokoa mauti!!! Nao Uzima twafahamu kwamba u na Mungu, ni huo pekee unaoweza Kutukomboa kutoka ktk Mauti inayotushikilia. Nao uzima hukaa ndani ya damu, nayo Damu ya Kristo, iliyomwagwa msalabani, twajua kwamba hiyo ni Damu ya Mungu kulingana na maumbile, kwani damu ya mtoto hutoka kwa babaye. Hivyo, tumenunuliwa kutoka Mautini kwa gharama ya Uhai wa Mungu; ndio kusema hali yetu ni zaidi ya Adamu; kwani sisi, juu ya vichwa vyetu, tuna thamani ya Damu ya Mungu, hiyo iubebao ule Uhai wa Mungu, yaani ile Pumzi na ndio maana kwa jambo hilo tunakuwa ni viumbe vipya kwa Pumzi hiyo inayotufufua kutoka mautini ilikotununua!

  Maandiko ndiyo yanayotufunulia UKOMBOZI wetu, jinsi yake. Mungu huwa hafanyi mambo yake kiholela bali kwa Utaratibu kamili. Ktk jambo hili la Ukombozi, Mungu ameziweka Sheria zake huko ktk Law 25. Huko twaona Ukombozi huwahusu ndugu tu, ni ndugu wa karibu pekee anayeweza kumkomboa nduguye aliye utumwani kwa kuilipa gharama iliyomuingiza ktk utumwa huo, ambayo kwetu sisi ilikuwa ni kifo, huko kutengwa na Mungu milele, pale Adamu na mkewe walipoliacha Neno la Mungu, hilo lililokuwa ndio Uzima wao, na kukipokea Kifo badala yake! Rm 7:14 “… bali mimi ni mtu wa mwilini, nimeuzwa chini ya dhambi” na kuwa chini ya hukumu ya kifo, Eze 18:4 “Tazama, … roho ile itendayo dhambi itakufa.” Nao mshahara wa dhambi twafahamu ni mauti!

  Kutoka jambo hili ndio tunauona huo Uamuzi wa Kutukomboa. Ndipo gharama iliyohitajika ni UHAI ulio nje ya stahili ya Adhabu hiyo, na hakupatikana ndugu yeyote wa karibu yetu, yaani ndg wa karibu wa Adamu na Hawa huko Edeni, zaidi ya Mungu mwenyewe!

  Pia ni vizuri tufahamu kwamba, kwa vile stahili ya Kukombolewa kwetu ilihitaji uhai ulio safi wa jamaa ya karibu, ambaye tumeona alikuwa ni Mungu mwenyewe, nao wakati kulingana na Programu yake ya kutukomboa ukiwa bado, ndipo kwa tendo hilo la kumchinja huyo mwana kondoo kwa ajili yao, nayo damu yake ikiwa ni hafifu ya Gharama iliyostahili, iliwapasa waendelee ktk jambo hilo mpaka hapo Malipo stahili yatakapofanywa, ndio hizo kafara za wanyama zilizoendelea kwa ajili hiyo, kila wakati wakikombolewa ili kupokea Rehema KWA KULITIMIZA jambo hilo, yaani humchinja kondoo huyo akiwa ni badala ya wao waliopaswa kufa kifo cha huyo kondoo, kila walipoingia dhambini!

  Basi kwa kifupi tunaweza kusema kwamba Ukombozi ulifanywa tangu misingi ya dunia ilipokuwa ikiwekwa, Ufu13:8 ” … Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia”; hili latuonesha kwamba Mungu katika Hekima na Uwezo wake, aliyaona yote yatakayotendeka huko mbele, jinsi ya dhambi itavyoingia na kutumiliki, ndipo akayashughulikia kimbele, na kuyakamilisha yote, haswa huo Ukombozi. Ndipo kinachoendelea leo hii ni udhihirisho wa hayo yote, kuanzia huko Edeni, kwamba Mungu alimchinja kondoo yule akiwa ni kivuli cha yule Mwana-Kondoo aliyechinjwa tayari huko misingi ya dunia ilipokiwekwa, nao ukamilifu wake kulingana na Sheria ya Dhambi na Mauti ulitimia hapo Kristo aliposulubiwa, akilidhihirisha lile lililofanyika huko nyuma.

  Basi ni vizuri sote tukajifikisha ktk ufahamu kwamba kulingana na hali yetu baada ya Anguko, nasi sote kuzaliwa ktk Dhambi, ndipo haiwezekani kwa yeyote KUOKOKA na Hukumu ya Jehanum bila hiyo Fadhila ya Mungu, aliyeutoa Uhai wake na KUTUKOMBOA!

  Basi sasa, ikiwa hamjachoka na mikeka, nitahitimisha niliyoyaona kuhusiana na jambo hili, kwa kukutazama KUOKOKA kunakotokana na UKOMBOZI.

  Asanteni kwa leo, &

  Gbu!

 81. Mjema,
  However, Kanaan na mbinguni ni vitu viwilo tofauti. Israel walikuwa wanaenfa Kanaan siyo mbinguni.

  Jibu pia maswali yangu.
  Thank u.

 82. Mjema,

  Umeniuliza swali ambalo jibu lake hulijui just kwa sababu kuna mpindo kwenye ufaham wako.

  Yuda mstari wa tano inasema kuwa japo Yesu aliwaokoa kutoka Misri lakini aliwaangamiza jangwani.
  Waliangamizwa kwa sababu waliasi. Sasa ukiniuliza kama watakuweko mbinguni nakushangaa.

  Lakini ninazidi kushangaa umepata wapi ujasiri wa kuikatalia biblia ilichosema kwenye hicho kitabu cha Yuda, ndio maana nikakufananisha na mtu ambaye amesema mouoni meake kuwa hakuna Mungu.

  Huo ndo ukweli wenyewe kuwa Mungu wetu huokoa na kuangamiza. Kwa hiyo kama ulikuwa hujui angalao sasa unajua.

  Bt kumbuka Bwana Yesu alipokata roho alienda kuzihubiria roho zilizokuwa kuzimu. Inawezekana Akani na Kora walimpokea Yesu.

  Saa ya wokovu ni sasa.

 83. Mjema,

  Tena unaposema kuwa safari ya Israel inalandana na sisi kusafiri kwenda mbingu mpya na nchi mpya nao ni uongo unaoweza kusemwa tu na mtu asiye makini.

  Wapi tumeambiwa kuwa tunasafiri kwenda kwenye mbingu mpya na nchi mpya?

  Na kwa kuwa kuokoka kwao ilikuwa ni kule kufika Kanaan kama unavyodai, kwa hiyo waliokufa jangwani bila dhambi walikuwa wakikata roho wanaenda Kanaan?

  Na una uhakika kuwa Musa alikufa bila dhambi, kilichosababisha afe kilikuwa cha sawa mbele za Mungu, au ndio huko kusema fikra zako ukidhani kuwa unasema ilichosema biblia?

  Unatakiwa kuona kuwa wokovu wa Isareal toka Misri ulikuwa wa kutoka kwenye utumwa wa Farao wala si utumwa wa shetani, kwa hiyo ulikuwa wokovu wa kimwili kabisa.
  Wokovu wetu ni wa kutoka utumwa wa shetani (Dhambi) ambayo ilisababishe tuwe chini ya hofu ya kifo, kwa hiyo wenyewe ni wokovu wa kiroho.

  Hata ukiamua kuamini kuwa Israel waliofika Kanaan ndio waliookoka, huku ukiamini kuwa kuokoka ni kutolewa mahali ambapo shetani yupo (yaani duniani),unatakiwa kujibu hili: kwani Kanaan shetani hakuweko?

  Ndiposa inakuja point amesema Lwembe kuwa Israel waliokolewa kutoka kwenye mikono ya Farao, (yaani kuwekwa nje ya mikono ya Farao), wala Mungu hakuwa amekwenda kuwaokoa kutoka kwenye safari ya jangwani.
  Kwa hiyo tangu ile dakika walipotolewa kwenye mikono ya shetani walikuwa wameokolewa.
  ———————

  Comment yangu ya kwanza hapo ina makosa fulani ya sarufi niiliandikia kwenye simu, bila shaka utaelewa nilichosema.
  Ila paragrafu ya mwisho inatakiwa kusomeka hivi;

  Huwa sipendi kulumbana na mtu nwenye akili pumbavu inayokataa kuukubali ukweli wa biblia ulio wazi,tena kwa kulazimisha kama hivi.

  Ni hayo tu!

 84. Sungura,

  Ubarikiwe,kukosa neno la kuniita bali umeniita mpumbavu!! Neno ilo sio nzuri hata km umeliita sio tusi!!.

  Ninachokiamini wote tupo njia moja tu,tunachotofautiana ni mtazamo tu! Short term vs Long term views.

  Ni ajabu km Mungu wenu Anaokoa halafu Anahangamiza!! Ni bora tu angewaacha wafie misri.Haileti maana Mjoli!

  Hebu sasa nikuulize swali moja tu.Tafadhali uwe mkweli,

  1. Wale walio angamizwa kwenye Jangwani kwa sababu ya manung’uniko-ambao unadai wameokoka-mfano, kina Akani, Je watakuwepo mbinguni?

  Nivumilie na Upumbavu wangu. Tafadhali nijibu mjoli.

  Asante!

 85. Mjema,
  Sina namna nyingine ya kukuita zaidi ya kukuita mpumbavu (nafikiri unajua upumbavu siyo tusi)

  Biblia ndio imesema Israel kutoka kwao Misri walikuwa wameokoka, halafu wewe kwa sababu ya ujinga tu wako tu wa kuelewa maana ya maandiko.

  Hebu irekebishe sasa biblia useme wewe ilitakiwa isemeje kama unaona kusema kwayo kuwa Israel walioangamia jangwani walikuwa wameokoka imekosea.

  Tofautisha kabisa neno Sodzo/soteria na hiyo concept mnayosema sijui ya Calvin. Sodzo siyo concept bali ni neno la asili ambalo limetumika likimaanisha wokovu. Nakushangaa unapoliita concept.

  Hebu sema wewe nini maana ya kuokoka!!

  Halafu kinawakwaza nini ña kuokoka kwetu, ninyi kama hamtaki endeleeni kusubiri ya kwenu mnayoijua.

  Mnataka tuamini mawazo yenu badala ya kile biblia imesema,kama huo si upumbavu na uzandiki ni kitu gani.

  Mkikuta mstari unasema tumeokolewa au tunaokolewa huo mnazema umekosewa au hauna maana hiyo,ila mkikuta mstari unasena tutaokolewa(wajati ujao) huo ndo mnasema uko sawa.

  Huwa sipendi kulumbana na mtu nwenye pumbavu inayokataa kuukubali ukweli wa biblia jlio wazi,tena kwa kulazimisha kama hivi.

 86. Sungura,

  Baada ya kutafakari aya ulizoomba kuhusu kuokoka hapa duniani, napenda nikurudishe kwenye hadithi ya waisrael toka misri ambayo inalandana sana na safari yetu toka duniani kwenda mbingu mpya na nchi mpya. Mtazamo wa Wokovu mnaoeleza ninyi hauleti maana kuwa, Mungu alipowatoa tu Misri,waisrael walikuwa WAMEOKOKA inli hali walikuwa wangali jangwani.

  mpendwa, Ikiichukulia Yuda1:5-isemayo kuwa baada ya Mungu kuwaokoa Israel toka Misri aliwaangamiza tena wale wasioamini, itachekesha ukisema,wale waisrael walipaswa kudai wameokoka wangali jangwani. Jambo ambalo si kweli. waliookoka ni wale tu walio waliokufa bila dhambi,Jagwani. Mfano-Musa,na wale tu walioingia kaanani wakiwa hai.sio wale walioangamizwa kama Akani,n.k

  Dhana iyo ni sawa na kusema “mtu aliyeokoka anaweza kupoteza tena wokovu” jambo ambalo si sahihi.

  Mifano mingine ni:

  1.Mke wa Lutu-sio sahihi kusema kuwa ameokoka ingawa malaika waliwatoa Sodoma&Gomora.kwa mtazamo wako Sungura,hata mke wa Lutu ameokoka!!

  2.Yuda-ingawa alikuwa mteule wa Yesu,hatuwezikusema ameokoka.never!!

  Sungura, Wokovu mnaofundisha ninyi ni ule wa kumpokea Yesu kisha kuangamia hapa Jangwani\duniani.Sisi tunausisitiza ule wa mwisho wa pambano.kati ya uovu na wema.

  Jambo hili ni sawa na wanafunzi wa fomu four, mmoja anasoma kwa kufocus mtihani wa Taifa na mwingne anasoma akifocus mtihani wa mock. Jiulize ni yupi atakayefaulu vizuri na hatimaye kwenda A-level.

  Rafiki Mifano yote hii inaonyesha- wote hawa, Mke wa Lutu, Waisrael walo angamizwa jangwani na Yuda , hawakuvumilia hata mwisho-kwa kuilinda Imani,na hivyo Hawakuokoka!!Math14:13.

  Sungura,

  Dhana ya SODZO unayoing’ania tulishakwambia ni man-made, J.Calvin dogma.usilazimishe tuifuate,sio ya kibiblia.

  Karibu tena.

 87. Mjema,

  Nimefurahi sana kukuona tena, habari za huko chuoni?!

  Kulingana na mchango wako, naona huko chuoni wamefuta uelewa wote uliokuwa nao kabla hujaenda huko na wamekujaza mambo yasiyoeleweka kabisa kwa kadiri ya Neno la Mungu, ndio maana umekuja na mizaha!!!

  Haya, chukua ile Biblia yako ile uliyoinunua kwa wale “wala nguruwe”, kisha fungua kitabu cha Kutoka 6:6 Mungu anasema hivi:
  “Basi waambie wana wa Israeli, Mimi ni YEHOVA, nami nitawatoa ninyi mtoke chini ya mizigo ya Wamisri, nami NITAWAOKOA na utumwa wao, nami nitawakomboa kwa mkono ulionyoshwa, na kwa hukumu kubwa.”

  Baada ya hapo Misri yote iliingia ktk Hukumu, nchi nzima iliingia ktk vilio vya kufiwa kasoro wana wa Israeli tu ndio waliookoka na pigo hilo la mauti, lakini utimilifu wa ahadi waliyopewa ulikuwa bado, kama unavyowaona hapa Farao alipowainukia tena, Kut 14:5-
  ” Ni nini jambo hili tulilotenda, kwa kuwaacha Waisraeli waende zao wasitutumikie tena? 6Akaandalia gari lake, akawachukua watu wake pamoja naye; 7tena akatwaa magari mia sita yaliyochaguliwa, na magari yote ya Wamisri, na maakida juu ya magari hayo yote. 8Na BWANA akaufanya moyo wake Farao mfalme wa Misri kuwa mgumu, naye akawafuata wana wa Israeli; kwa sababu wana wa Israeli walitoka kwa ujeuri. 9Wamisri wakafuata nyuma yao, farasi zote na magari yote ya Farao, na askari zake wenye kupanda farasi, na jeshi lake, nao wakawapata hali wamepanga pale karibu na bahari, karibu na Pi-hahirothi, kukabili Baal-sefoni. 10Hata Farao alipokaribia, wana wa Israeli wakainua macho yao, na tazama, Wamisri wanakuja nyuma yao; wakaogopa sana; wana wa Israeli wakamlilia BWANA. 11Wakamwambia Musa, Je! Kwa sababu hapakuwa na makaburi katika Misri umetutoa huko ili tufe jangwani? Mbona umetutendea haya, kututoa katika nchi ya Misri? 12Neno hili silo tulilokuambia huko Misri, tukisema, Tuache tuwatumikie Wamisri? Maana ni afadhali kuwatumikia Wamisri kuliko kufa jangwani.”

  Unawaona hao, wanatofauti gani na wewe unayejiona panzi mbele ya dhambi, hilo jeshi kubwa la Shetani? Imani yako imetoweka, mambo yote umeyasahau, unatamani kurudi utumwani kwa Tumaini la Uongo hilo lisilokuwepo, kwani ajapo Kristo hatuhitaji tena kuwa na imani, maana hiyo ndiyo inayotupeleka kwake, sasa kama huna hiyo leo ilipomwagwa utaipata wapi itakapoondelewa? !! Bali Mungu huyatimiza yote aliyoyaahidi watu wake:
  “13Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa BWANA atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele.”
  Umeelewa Mjema! Mambo yote hutendeka kwa ajili ya Utukufu wa Mungu, hata hizo Ahadi zake ni kwa ajili hiyo.
  “26BWANA akamwambia Musa, Nyosha mkono wako juu ya bahari, ili maji yarudi tena juu ya Wamisri, juu ya magari yao, na juu ya farasi zao. 27Musa akaunyosha mkono wake juu ya bahari, na kulipopambazuka, bahari ikarudi kwa nguvu zake; Wamisri wakakimbia mbele yake; na BWANA akawakukutia mbali hao Wamisri kati ya bahari. 28Yale maji yakarudi yakafunikiza magari na wapanda farasi, hata jeshi lote la Farao lililoingia katika bahari nyuma yao; hakusalia hata mtu mmoja.”

  Jitahidi kaka, unapoisoma Biblia yako, jaribu kukiangalia kwanza kinachoongelewa, maana ya neno “Kuokoka, au Kuokolewa, au Wokovu huwa inabeba maana kulingana na mantiki inayofunuliwa katika vifungu hivyo individually, usiwe mtu wa mtazamo mmoja, tena ulio finyu, mpaka unaishia kuikosa hata maana ya jambo na hivyo kubakia kama mpagani uliyejitayarisha kuipinga Injili kwa nguvu zako zote, kwa kutetea jambo lisilo na maana ktk Ufalme wa Mungu!

  “30Ndivyo BWANA ALIVYOWAOKOA Israeli siku ile mikononi mwa Wamisri; Waisraeli wakawaona Wamisri ufuoni kwa bahari, wamekufa.”

  Je, hiyo Kut 6:6 imewatimilia au la? Wamisri waliowatia utumwani wangalipo au la?

  Yaamini Maandiko, na si masomo yenu, utapotea dogo, maana kazi ya mapepo ya dini kukushawishi ufanye confession; basi kama ambavyo kwa kukiri mtu hupata Wokovu na kwa kukiri kwamba hakuna Wokovu duniani mtu HUUPOTEZA Wokovu wake!!!

  Fikiri, Chukua Hatua!

  Gbu!!

 88. Duh, Siyi!

  Nakuona unavyolipandisha ghorofa lako juu ya hako “kamsingi”; angalia lisije likakuporomokea kama la TB Joshua, hahahahaha….!! Hata hivyo, ninawapa pole wote walioguswa na msiba huo, Bwana awe faraja kwao ktk wakati huu mgumu!

  Nimeuona mchango wako kwa Sungura pamoja na maswali yake, ni changamoto nzuri, maana hayo ni maswali ya haki; lakini majibu ya Sungura, nayo pia ni ya haki! Basi shida iko wapi? kwa kadiri nilivyolifuatilia jambo hili, shida ninayoiona ni ya UFAHAMU tu, kuhusu Wokovu na Kuokoka, yaani kujua kwamba Kuokoka siyo Wokovu ingawa Wokovu unajumuisha kuokoka! Ni ktk mkanganyiko kama huu ndio namuona Sungura akisema kwamba “”neno wokovu limetumika past, present na future”” lakini ktk uhalisi, ni neno KUOKOKA ndilo limetumika ktk tenses hizo, ambazo kwazo ndio Wokovu unatafsirika kwa mkristo baada ya ile hatua ya Ukombozi kufanyika pasi yeye kujua, maana, kama Maandiko yanavyokiri, “Wafu hawajui neno lolote”, ndivyo tulivyokuwa huko dhambini tulikoshikiliwa na Mauti!

  Basi tukiijua ile application ya hizo namna tatu zihusuzo KUOKOKA, tutakuwa tumejiweka ktk nafasi nzuri zaidi kiufahamu hata kuyafaidi matunda ya Wokovu, yale maziwa na asali!!!

  Jambo la kwanza, tunapozungumzia Kuokoka kunakohusiana na Wokovu, ni muhimu sana kupata kujua Tunaokolewa kutoka jambo gani; Wizi wa fungu la kumi, au njaa, au majambazi, au mafuriko, au kifo, au Dhambi, ama ni nini hasa tunachookolewa nacho????

  Labda ngoja niendelee kidogo, tuuangalie zaidi ule UAMUZI wa Kutukomboa, na matokeo yake, ili kulibaini jambo hilo kulingana na Maandiko.

  Uamuzi huo wa Kutukomboa ulifanyika baada ya jambo la sisi kuingizwa utumwani, au kifungoni, au mautini, kupitia dhambi kujitokeza na hivyo kumlazimu Mungu, kutokana na kutupenda kwake, aufikie Uamuzi huo na kisha autimize kwa kuilipa hiyo gharama ambayo ni Damu ya Mwana-Kondoo, akiichukua yeye Mauti iliyotustahili sisi, na kuturejeshea tena Uzima wa Milele ambao tuliupoteza hapo tulipoingia Mautini; Ufu 13:8 “… Mwana-Kondoo aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia”

  Basi, ikiwa gharama ya Ukombozi wetu ililipwa huko ilipowekwa misingi ya dunia, ndio kusema kwamba mambo yote yalifanyika huko kwanza, Dhambi na Ukombozi, kabla hata ya sisi kuzaliwa ktk miili hii hapa duniani! Nao udhihirisho wa hayo yaliyofanyika, ndiko kusulubiwa kwa Kristo ili kuimwaga hiyo Damu, iibebayo hiyo gharama, ambayo kwayo twasafika hapo tunapokombolewa, Mauti ikituachilia kutoka ktk makucha yake kwa kumiminwa kwa hiyo Damu!

  Tunaweza kuliona jambo hili jinsi linavyojifunua tunapoyarejea yaliyojiri huko Misri, kwa Israeli, hao wateule wa Mungu, walipokuwa utumwani, Kut 6:6
  “Basi waambie wana wa Israeli, Mimi ni YEHOVA, nami nitawatoa ninyi mtoke chini ya mizigo ya Wamisri, nami nitawaokoa na utumwa wao, nami nitawakomboa kwa mkono ulionyoshwa, na kwa hukumu kubwa.”

  Kutoka kifungu hiki cha Maandiko, tunaweza kuyaona mambo haya matatu ktk uhalisi wake:
  1. Salvation au Wokovu: Mungu anawatangazia Israeli Uamuzi alioufikia wa kuwatoa chini ya mizigo ya Wamisri, na kuwaokoa ktk utumwa. Ahadi ya Mungu ni tangazo la Uamuzi alioufikia kuhusu jambo hilo, nawe ukiwa ktk hali ya utumwa, basi tangazo hilo huwa ni Habari Njema kwako, huo Wokovu wako, kule kurejeshewa uhuru ulioupoteza.

  2. Redemption au Ukombozi: ” … nitawakomboa kwa mkono ulionyoshwa, na kwa hukumu kubwa.” Ili Ahadi hiyo iweze kuwatimilia, inahitajika Ukombozi ufanywe kwanza ndipo kuwa Huru kwao kutoka utumwa na hiyo mizigo kuwezekane. Misri yote iliingia ktk Hukumu kubwa, unaweza kuyasoma mapigo yaliyoipata, ikiwa ni hukumu juu yao kulingana na ukaidi wao, bali mapigo hayo hayakuwa ndio “malipo kwa ajili ya Ukombozi” wa Israeli!

  HUKUMU ilikuwa juu ya Misri yote kama nchi, na Israeli walikuwamo humo Misri. Pigo la mwisho, ambalo ndilo Hukumu ya mdhambi, ni Mauti, Kut 11:1 “BWANA akamwambia Musa, Liko pigo moja bado, nitakaloleta juu ya Farao na juu ya Misri.” Ndio kusema Mauti ilipaswa iifunike Misri yoote, bila kubagua, maana Mungu ni mwenye haki, ndipo ktk Hukumu hiyo asingeweza kuwabagua Israeli ambao pia walikuwa ni wadhambi, maana hilo lingemfanya asiwe mwenye Haki. Basi ili awaokoe ktk Hukumu hiyo, ilimbidi awape jinsi ambayo uovu wao utalipiwa, jinsi hiyo ilikuwa ndicho kile kivuli cha yule Mwana-Kondoo aliyechinjwa, nayo ishara hiyo ndiyo pekee kupitia kwayo wangepona! Kut 12:5-7:”Mwana-kondoo wenu atakuwa hana ila, mume wa mwaka mmoja; … na kusanyiko lote la mkutano wa Israeli watamchinja jioni. Nao watatwaa baadhi ya damu yake na kuitia katika miimo miwili na katika kizingiti cha juu, katika zile nyumba watakazomla.” Hivyo, damu ya mwana kondoo ndiyo iliyokidhi hiyo gharama kwa kiwango cha Ukombozi wao ktk wakati huo.

  3. Saved au Kuokoka: Kwahiyo kutoka jambo hili, ndipo tunafahamu kwamba Ukombozi uliofanywa unahusu kutuondoa ktk HUKUMU! Basi ktk siku ile ambayo Misri yote iliingia ktk kilio kwa Hukumu hiyo, ni Israeli pekee ndio WALIOOKOKA na Hukumu hiyo kupitia ile kafara ya mwana-kondoo waliyemla na damu yake kupakwa juu ya miimo ya milango ya nyumba zao ili kuwa ishara ya kukombolewa kwao kutoka Hukumu hiyo hapo ‘Malaika wa Kifo’ alipopita!

  Kimsingi tunapozungumzia wao Kuokoka, ni ktk mtazamo wa kuitazama Hukumu iliyopita juu ya nchi, haswa tunapoyatazama matokeo. Lakini kwa hakika Kuokoka kwao hakuko ktk matokeo ya Hukumu hiyo bali ktk kuupokea Wokovu waliokirimiwa, kwa kuyatii maagizo yanayoupasa Wokovu huo kama yalivyoelekezwa. Kama siku ile kuna Muebrania ambaye hakushiriki hilo jambo, yaani hakuupokea huo Wokovu, na hivyo kuishia kutokupaka hiyo damu, basi ni dhahiri kwamba nyumba yake ilikuwa ktk kilio pamoja na Wamisri kwa kukumbwa na Hukumu hiyo!

  Kwahiyo tunaweza kuona hapo kwamba Israeli walipoipokea Habari Njema ya Wokovu wao, kwanza iliwaondoa kutoka ktk Hukumu iliyoifunika nchi yote, ndiko huko kuokolewa kwao, ambako ilikuwa ndio arabuni yao ya ile Ahadi ya “kutolewa kwao chini ya mizigo ya Wamisri, na kuokolewa kwao kutoka utumwani!” Basi kwa wao kuinuka na kumchinja yule mwana kondoo wa kiwango kilichohitajika, na kumla na kuipaka damu yake kama ilivyoagizwa, hii ilikuwa ni kuutangaza Wokovu uliowafikia, ambao ulibeba gharama ya Mauti itakayoiangukia nchi na uhuru wao kutoka utumwani ktk namna zote tatu, zile tenses:
  1. Past: Walipoipokea Ahadi, yaani Kuyaamini hayo aliyoyasema Mungu – waliokolewa; ndiko huko kuokoka au Kuhesabiwa Haki kwa Imani.
  2. Present: Walipoinuka kuyatimiza hayo yaliyoagizwa, ikiwa ni ishara ya kuupokea huo wokovu; Walitakasika kwa hayo.
  3. Future: Ile Hukumu iliyopita juu ya Misri, ilijidhihirisha kuwa ndio arabuni ya wokovu wao kamili kama ulivyoahidiwa; ndiko huko Kutukuzwa kwao, yaani Uwepo wa Mungu, ule Utukufu wake, ukijidhihirisha kuwepo kati yao!

  Nitapose tena hapa kidogo ili niwapeni nafasi ya kutafakari, na kama kuna lolote lililo tenge, basi tuliangalie kwa pamoja.

  Gbu!

 89. Mjema,

  Kweli umedandia.

  Hebu nismbie, wapi biblia inasema hakuna kuokoka duniani?

  Tafuta original translation uniambie hapo ambapo biblia unayosema kuwa ina udhaifu wa lugha imesema Israel waliokoka, hiyo unayodhani ina lugha sahihi imesemaje.

  Kinachowasumbua ninyi Mjema ni kutojua maana ya wokovu (Sodzo)
  Matokeo yake mnashindana mpaka na maandiko.

  Wokovu (Sodzo) ni zaidi ya kwenda mbinguni. Ni neno la jumla nilishawaamnia.

  Unashangaa Mungu kuokoa na kuangamiza wakati unajua hata malaika walipoasi aliwashusha. Naona unamwangalia Mungu kwa upande mmoja tu wa wingi wake wa rehema.

  Haya, nangoja majibu!

 90. haleluyah,

  Kumbe bado mjadala huu unaendelewa!, nimekosa mambo mengi kweli.Mbarikiwe.

  Samahani kwa kudandia.

  Sungura,

  Waisrael walipotoka Misri walikuwa bado hawajaokoka!

  Sababu:Mungu awezi kukuokoa halafu ukaangamia.-Ingawa biblia inasema ivyo ambapo ni udhaifu wa lugha.ukitafuta mantiki ya kuokoka halafu kuangamia, utachekesha watu.

  Kumbuka kati ya walioanza safari naweza kusema 99% hawakufika Kaanani.Halafu kumbuka yafuatayo:

  1.Walililha kurudi Misri-walikumbuka sufuria za nyama walizokula misri.

  2.Walimnung’unikia Musa au Mungu kwa ugumu wa mapito ya Jagwani.

  Na kumbuka safari ya Israel toka Misri-Kanaani ni snerio nzuri kuelezea safari yetu toka duniani-kwenda mbinguni.

  Na hayo yote mawili hapo juu ndiyo yanayo likumba kanisa,na ndio maana twasema duniani hakuna kuokoka,tunaukulia wokovu.

  Utasemaje umeokoka na wakati upo Jangwa la Dunia hii ndugu yangu Sungura.

  Fikiri, chukua hatua

 91. Siyi,

  Unataka tuufanye huu mjadala kwa Kiingereza au?

  Pili, umeandika kurasa ndefu sana kea sababu inabidi uweke maneno mengi sana kujitetea.

  Kwa hiyo umeelewa sasa kwamba neno wokovu ni collective kama nilivyowahi kukwambia wakati ule naeleza maana ya Sodzo/Soteria?

  Umeelewa sasa kwamba kusamehewa dhambi ni Sodzo, kutolewa kwenye ufalme wa giza ni Sodzo, kukombolewa ni Sodzo, n.k?

  Lakini pia nakushangaa unavyogombana na biblia, halafu tuhuma unazitups kea akina Sungura.
  Siyi iliyosema maana ya neno wokovu ni biblia siyo sisi, hatujiiti wala hatuimbi kuea tumeokoka, bali biblia ndio inayotuita na kusema hivyo.

  Maswali uliyoniuliza kuhusu hiyo mistari ya wakati ujao, nilishakwambia kuwa neno wokovu limetumika past, present na future. Ulinibishia lakini sasa umeyaona nwenyewe,kiasi kwamba unataja kuleta dhana yenye mtazamo ws kwamba biblia inajipinga kwa kule kutumia wakati uliopita,uliopo,na ujao.
  Siyi, wemye lugha yao hivyo ndivyo walivyolitumia neno wokovu, wewe mdandiaji unajifanya kujua kuliko wao.

  Jifunze vizuri lugha, neno “escape” nenda kalisome vizuri kisha uone maana yake kama halitoshi kutumika kuonyesha hali ya kutoka sehemu ya hatari kwenda sehemu salama.

  Siyi, lakini hujajibu suala la msingi sana. Nilikutaka useme kama kile kitendo cha Israel kutolewa Misri waliokoka au haikuwa kuokoka. Nijibu hilo wala usikwepe.

  Kisha punguza maneno , go strait to the point.
  Unaongea maneno mengi kiasi cha kufanya mambo ya msingi yafichike.

  Njoo!

 92. Lwembe,
  Dhana ya Sungura ya mtu kupoteza wokovu si sahihi. Alipaswa aseme hivi; Mtu aliyeanza mchakato wa wokovu/aliyemwamini Yesu anaweza kurudi nyuma. Mtu aliyeokoka, ni mtu aliyefikia ukamilifu na alikuwa glorified. Sasa atapotezaje tena wokovu? Huyo mtu hapotezi wokovu ila hurudi nyuma kiroho/kiimani. Angesema hivi, hoja yake isingekuwa na mjadala. Maana hakuna aliyeenda mbinguni halafu akatamani kurudi duniani. Ukishadidia uongo huu wa huyu jamaa (Sungura), nazidi kukushangaa sana. Ngoja nione na wewe utakavyoleta mwitiko kwenye hoja za kuokoka nilizompatia Sungura hapo juu; maana si kwa Sungura peke yake.
  Aidha, nikushukuru kwa kupekuapekua kwenye maana ya kukomboa (to redeem) na kuokoa (to save). Sipingani na fafanuzi (maana/definitions) za maneno hayo mawili ulizotoa. Ninachokuomba ni kuthibitisha tu kuwa, kama ulitumia Kamusi, ni kamusi ipi? Taja tu. Najua unayo na ulirejea. Naomba unipatie hiyo rejea ili inisaidie mimi na wenzangu (wasomaji).
  Uamuzi wa kumkomboa mwanadamu ni kweli upo na ulifanyika baada tu ya Adamu kuanguka dhambini. Ni kweli kuwa, ulifanyika kabla ya ukombozi. Maelezo haya najua kwa nini umeyaleta. Barabara yako naiona ileee!! Ngoja nikutazame kwanza unakoelekea!!
  Zaidi ya hapo, tafsiri ya huo UAMUZI, sipingani nayo wala sikubaliani nayo isipokuwa umenionesha hiyo rejea (Kamusi/Biblia) sahihi ya kiimani. Na kwa sababu hiyo, kwa sasa nisingependa kuzungumzia chochote juu ya definition yako hiyo, hadi utakapoleta hapa hiyo rejea. Na katika faiwa tanzu (subsidiary definitions) za WOKOVU, kimsingi Sungura nimempatia baadhi ya aya ulizozitoa hapo. Jaribu kushirikiana naye kuzijibu hizo huenda mtapata uelewa kuwa, tunapomwamini Yesu na kusafiri kiimani huku siko kuokoka, bali ni michakato tu. Kuokoka ni THE FINAL OF THE WHALE PROCESSES –hatua ya mwisho ya kutwaliwa na Kristo. Biblia iko clear kwa hilo, endapo utaisoma kwa uangalifu tu.
  Na katika hatua hii ya tatu naona umesema na kukiri wazi kuwa huko ni kuokoka!! Angalia Sungura atakumeza!!! Unamsaliti hivihvi kaka!! Tena peupe hivihviv!! Angalia sana maana yeye kakataa kuwa destination ya Wokovu SIYO KUOKOKA!!. Nina imani baada ya kupitia mikeka mirefu niliyomwandikia Sungura, kuna baadhi ya hoja humo, zimejibu hoja zako hapa. Jaribu kupitia huko kwanza ili ukikamilisha uchambuzi wako wa UAMUZI wa UKOMBOZI, najua utakuja na mambo mengine mazuri zaidi.
  Zaidi ya hapo, mimi nikushukuru tu kwa pachiko zuri lenye uchokozi ndani yake.
  Ubarikiwe sana
  Siyi

 93. Sungura,
  Mwendelezo……

  Sasa na wewe nakuomba utanzue ukinzani za dhana hizi akilini mwako
  Nami nakuuliza, unawezaje kuyafasiri maandiko haya kukaidi neno la Mungu??

  Mathayo 10:22 Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.
  Mathayo 24:13 Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.
  Mathayo 24:22 Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo.
  Marko 16:16 Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.
  Luka 21:36 Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu.
  Yohana 10:9 Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho.
  Swali; Huyu anayevumilia, anavumilia wakati gani? Akiwa ameshaokoka au akishavulia ndiyo ataokoka??

  Mathayo 19:25 Wanafunzi waliposikia, walishangaa mno, wakisema, Ni nani basi awezaye kuokoka? Marko 10:26 Nao wakashangaa mno, wakimwambia, Ni nani, basi, awezaye kuokoka?
  Swali; wakati wanajiuliza swali hili, wao walikuwa walishokoka au walikuwa bado?

  Marko 13:13 Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kusaburi hata mwisho, ndiye atakayeokoka.
  Marko 13:20 Na kama Bwana asingalizikatiza siku hizo, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule aliowateua amezikatiza siku hizo.
  Matendo ya Mitume 15:1 Wakashuka watu waliotoka Uyahudi wakawafundisha wale ndugu ya kwamba, Msipotahiriwa kama desturi ya Musa hamwezi kuokoka.
  Matendo ya Mitume 16:30 kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka?
  Matendo ya Mitume 16:31 Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako.
  Matendo ya Mitume 27:20 Jua wala nyota hazikuonekana kwa muda wa siku nyingi, na tufani kuu ikatushika, basi tukakata tamaa ya kuokoka.
  Warumi 10:9 Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.
  Warumi 10:13 kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka.
  Warumi 11:26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake.
  Waebrania 12:25 Angalieni msimkatae yeye anenaye. Maana ikiwa hawakuokoka wale waliomkataa yeye aliyewaonya juu ya nchi, zaidi sana hatutaokoka sisi tukijiepusha na yeye atuonyaye kutoka mbinguni;
  Matendo ya Mitume 15:11 Bali twaamini kwamba tutaokoka kwa neema ya Bwana Yesu vile vile kama wao.
  Matendo ya Mitume 16:31 Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako.
  Warumi 10:9 Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.
  Wokovu Lini? Baadaye

  Mimi naona umeshanielewa. Maana mimi nasema, wokovu ni mchakato unaoanzia na kumwamini Yesu, kutembea/kukua ktk imani na destination yake ndiyo hiyo kutolewa duniani. Bila ya hii destination ya kutolewa duniani kuifikia, huwezi kusema kuwa umeokoka. Utakuwa unatudanganya kweupe na sisi hatutakubali, maana Biblia tunaisoma vizuri chini ya ungozi wa nguvu za kiungu na tunaielewa vyema. Wasabato wazuri kimaandiko, wanaamini kuwa, ili mtu afikie hatua ya kusema AMEOKOKA, ni hadi afike hatua ya mwisho ya wokovu. Sungura (kama ungekuwa mwanamke), huwezi kuitwa biological mother, ni mpaka umebeba mimba, ukashikwa na utungu wa kuzaa na hatimaye ukazaa. Ukibebea mimba tu na kuumwa utungu halafu usizae mtoto, huwezi kuitwa mama. Hatua hii ya mwisho, ndiyo inayodetermine sifa ya jina lako- mama mzazi. Huu unaweza kuwa ni mfano dhaifu, lakini najua unanielewa. Watu watang’amua wenyewe.
  Wewe umesema, wokovu ni kumwamini Yesu, kukua katika imani basi. Huu ndio wokovu. Kwenda mbinguni SIYO kuokoka (utanisahihisha kama nimekuelewa vibaya). Umesema kwenda mbinguni ni kunyakuliwa!! Unajua maana ya kunyakuliwa ( to rapture)?? Kama kazi ya Yesu ya kuokoa iliishia msalabani, kwa nini alisema kuwa anaenda kutuandalia makao ya kutukaribisha kwake??? Au ni ubishi tu usio na sababu? Maana mara nyingine unakana mambo uliyoyasema wewe mwenyewe na kudai hujasema. Unataka uthibitisho!! Eti nakusingizia ooh, wewe hujasema hayo, ooh, kama nilisema kweli show me!!! Nakunuu maaana umetaka hadi nikuoneshe japo mimi sikutaka kufika huko…
  “Ndio kusema Paul hakuwa anasema hayo maneno kwa warumi huku akiwa bado yuko chini ya dhambi yeye mwenyewe. Ni mjinga tu ndo anaweza dhani hivyo.” 02/07/2014 at 6:51 PM
  “Ati unaniambia unajitahidi kujionesha kuwa umekubaliwa na Mungu. Hpo napo nimeona ni kwa jinsi gani hujui maana ya huo mstari. Mtu aliyekubaliwa na Mungu si mtu ambaye yuko chini ya dhambi tena, maana huo mstari unakwambia kuwa huyo ni mtu aliekubaliwa/aliyepata kibai mbele za Mungu. Huwezi kuwa umepata kibali mbele za Munu na hapohapo ukawa tena chini ya dhambi, hizo ni falme mbili tofauti.” 07/07/2014 at 12:56 AM
  “Ivi kama gereza limefunguliwa na wewe mfungwa umeruhusiwa kutoka, ukishatoka unaendelea tena kuwa mfungwa? Na kama jibu ni kwamba huendelei kuwa mfungwa maana yake unakuwa huru. Ukiwa huru maana yake ni nini kama si kuwa mbali na hatari? Kuwa mbali na hatari uliyokuwemo maana yake ni nini kama siyo kuokoka?” 01/08/2014 at 3:20 AM

  Sasa Ona ulivyojichanganya hapa rafiki hebu soma hapa;
  “Nilikwambia moja ya kipengele au package ya wokovu ni kusamehewa dhambi, wewe unaniambia kuwa ati nimesema kuwa ukiokoka hutendi dhambi. Hili nadhani umelipinda hivyo ili utafute mwanya wa kuniambia kuwa kama ukiokoka huwewzi tenda dhambi mbona Isreal walitenda dhambi jangwani! Nimekuona. Na nimekuona jinsi ambavy umelirukia tuu neno ‘wokovu ni mchakato’ bali kufikiri sana ni nini maana yake hasa. 30/08/2014 at 1:27 AM
  Haya sasa kana tena!!! Uongo wangu uko wapi? Kati ya mimi na wewe mzushi ni nani?
  Na kama unataka hata aya inayoonesha kuwa waliofika kanaani kuwa waliokoka, kimsingi unachekesha sana. Nikuulize, kwani safari ya kutoka Misri destination yake ilikuwa ni jangwani au Kanaani? Najua jibu lako, litakuwa ni jangwani, maana ukisema kanaani, utakjipinga mwenyewe. Maana kwa mawazo yako, Israel wakati wakiwa Jangwani, waliokoka. Ufidhuli mkubwa!! Na utapotea Sungura kwa sababu ya negative pre-conceived ideas towards me. Angalia sana kijana!!
  NB; 1. Kumbuka swali langu nililokuulizeni tofauti ya kuishi dhambi na kutenda dhambi!!
  2. Hoja ya kutawadha ni wewe uliyeisema. Mwanafunzi sikuelewa. Naomba ufafanuzi wake. Ingekuwa hoja tofauti kabisa nah ii, usingeitolea mfano.
  Nakungoja
  Siyi

 94. Sungura,
  Nadhani umenielewa japo unaonekana kunilalamikia kuwa naongopea mara nyingine. Kimsingi mnahitaji neema kubwa sana. Mnahitaji kuombewa.
  Na nikwambie kabisa kuwa, destination ya kitu kinachoitwa wokovu, ni kutolewa duniani. Na hilo si uongo kama unavyouita. Kama wewe ni mkristo usiyeitazamia mbingu mpya na nchi mpya, una isivyo bahati, waswali wa zamani, walisema, una bahati mbaya kweli!! Na kwa mawazo yako, bado unajiaminisha kuwa tunaokolewa bado tukiwa hapahapa duniani. Ufidhuli mtupu!! Kumbuka kuwa shetani hajafa!! Tunapookolewa halafu tukaendelea kubaki duniani, unafikiri mashambulizi yake (shetani) dhidi yetu, yataisha? Na Biblia unapoisoma inakueleza hivyo kweli?
  Yesu ni mwokozi wa watu na dhambi zao. Kiingereza wanatumia neno from their sins!! Dhambi ziko wazi? Nani alileta dhambi? Je, hivi huwa unasoma historia za baadhi ya watu walioishi dhambini, halafu wakawa wenye haki, Mungu aliendelea kuwaacha dhambini-duniani? Na hata hao waliokufa wakiwa wenye haki wakazikwa, je Biblia husema kwa vile walikuwa ni wenye haki, ndiyo safari zao ziliishia hapo? Kama hazijaishia hapo, kwa nini waje kutolewa duniani-kufufuliwa siku ya mwisho? Unaponinyoshea kidole cha mwenda wa zimu, angalia vidole hivyo vinavyokurudia wewe mwenyewe!!! Vingapi? Zidisha mara kimoja kinachonielekea mimi, uatapata jibu kaka.
  Nina wasiwasi kama nguvu ya kumshinda ibilisi inaitwa WOKOVU. Hii nayo ni mpya kabisa. Naomba msingi wa kimaandiko zaidi ya fungu ulilotoa maana haliendani na maana hiyo. Wokovu ni kitu kingine kabisa na chapeo, japo zinahusiano kwa kiasi Fulani. Aya ulizozileta, nilikupa assignment mwanzoni kabisa, ukakimbia. Naona na sasa hivi umezileta tena. Nami napenda kukupatia mrejesho wake kwa namna nyingine japo maana ni ileile huenda autanielewa. Here we go;
  -(NAYE ALITUOKOA KATIKA NGUVU ZA GIZA, AKATUHAMISHA NA KUTUINGIZA KATIKA UFALME WA MWANA WA PENDO” WAKOLOSAI 1:13
  Maana yake;
  Neno “alituokoa” limetumika kumaanisha kufunguliwa gereza; kukombolewa hasa kwa wale walioitambua kafara ya Kristo pale msalabani!! Haina maana kwamba, wameshaepukana na mashambulizi ya ibilisi. Ukisoma Kolos. 1:13 hadi 15, inakupatia picha sahihi ya sentensi nzima. Inasema, “Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake; ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi; naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote”.
  Jambo linalozungumziwa hapa kaka Sungura, ni jambo la kuhesabiwa haki kwa njia ya imani katika Kristo Yesu. Kumbuka mtu aliyehesabiwa haki kwa imani, anaweza kupata matatizo mengi naam hata kifo (chenye matumaini) ndani ya imani hiyo. Mtu aliyeokoka, hawezi kupatwa na shida, mateso, dhiki, kifo n.k. Paulo anasema, “Sasa nayafurahia mateso niliyo nayo kwa ajili yenu; tena nayatimiliza katika mwili wangu yale yaliyopungua ya mateso ya Kristo, kwa ajili ya mwili wake, yaani, kanisa lake”-Kolos. 1:24. Ukiendelea kusoma, Paulo anasema, lengo la mateso hayo, ni kuikamilisha kazi ya utume aliopewa na Mungu kwa ajili ya kanisa lake. Akishaikamilisha, baadaye aje aokolewe.
  -“LAKINI WEMA WAKE MWOKOZI WETU MUNGU, NA UPENDO WAKE KWA WANADAMU, ULIPOFUNULIWA, ALITUOKOA.” TITO 3:4)
  Hata hapa hoja ni ileile kaka Sungura. Ni kuzaliwa mara ya pili na siyo kuwekwa salama kwa maana ya kutofikiwa na mabaya. Soma vyema kuanzia mstari 4- hadi 6 inasema, “Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, alituokoa; si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu; ambaye alitumwagia kwa wingi, kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu”.
  Ili unielewe zaidi,
  NB: Karibia Biblia zote za Kiingereza zimetumia neno “APPEARED” kama linavyosomeka -But after that the kindness and love of God our Saviour toward man APPEARED. Sasa jiulize, how comes, since when na in what grounds the meaning of ‘Save’ is equal to the meaning of ‘appear’? Sungura, wewe ni mwanafunzi mzuri wa Biblia, lakini nashangaa hata huelewi mambo rahisi kiasi hiki. Sijui ni ushabiki wa dini, dhehebu au nini. Yaani hata sielewi, kwa nini huelewi!!! Mungu atusaidie sote rafiki yangu.
  -“MKIOKOLEWA NA UHARIBIFU ULIOMO DUNIANI KWA SABABU YA TAMAA” 2 PETRO 1:4
  Maana yake
  Petro ametumia neno “mkiokolewa” kwa maana ya kuponywa-kukua katika Kristo, kuukulia wokovu. Mkiokolewa, kwa maana ya kuacha dhambi moja baada ya nyingine. Isome vizuri tena, “Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa. Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa, na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu saburi, na katika saburi yenu utauwa, na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo. Maana mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele, yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda, kwa kumjua Bwana wetu Yesu Kristo”-2Petro 1:4-8. Mchakato wa kufikia destination ya wokovu, kujumlisha/kuongeza mema na kutoa mabaya katika maisha ya muuminni.
  NB: Asilimia kubwa ya Biblia za Kiingereza, zimetumia neno “escape” kwenye nafasi ya “okoa”. Kwani sasa, kwa wewe unayejua maana ya okoa, hivi ni sawa na maana ya escape ambalo kwa Kiswahili ni toroka au ponyoka? Yaani hadi tunafikia hatua ya kumpa ibilisi mamlaka ya kumshinda Kristo kiasi kwamba, Yesu hawezi kuwaaokoa watu wake kutoka mikononi mwa ibilisi isipokuwa kwa kuwatorosha au kuwaponyosha!!! Yaani Yesu anamwogopa ibilisi?!! Aibu hii rafiki!! Ni aibu kwa sababu, una very BAD concept ya kwamba, kunyakuliwa siyo wokovu!! Na kunyakuliwa (to rapture) ni kutorosha au kuponyosha watu kwa siri. Na unapozidi kuwa na concept ya ajabu kiasi hicho, kimsingi unazidi kuiinua bendera ya ibilisi zaidi ya ile ya Kristo japo hujui, na hutaki kujua!! Rafiki, sina msaada mwingine zaidi ya kukwambia ukweli kabla hujachelewa!!

  -“SASA KUMEKUWA WOKOVU NA NGUVU….” UFUNUO 12:10
  Maana yake,
  Yohana ametumia “sasa kumekuwa wokovu” kwa maana kwamba, baada ya ibilisi (enzi zile akiitwa Lucifer) kuasi mbinguni, ugomvi ulitokea kati yake na Mungu –Kristo. Ibilisi alipokaribishwa duniani, mbingu zinatangaza wokovu kwa wanadamu, wokovu ambao ungepatikana kwa njia ya Kristo. Uone upendo wa Mungu ulivyo wa ajabu kwetu. Shetani anakimbizwa mbinguni, na isivyo bahati anadondokea duniani na kuwashambulia viumbe wapenzi wa Mwenyewzi Mungu –wanadamu. Bado Yesu anamfuatilia na huko duniani kuendeleza mapambano. Vita kuu ilishaisha – kufa na kufufuka kwa Kristo. Kilichobaki, ni sisi kukiona kile alichokifanya Kristo pale msalabani na kuishi kwa hicho. Kukitambua na kukiishi kwacho ndiyo kazi kubwa kubwa inayohitaji uangalifu na umakini mkubwa; maana pamoja na Yesu kutukomboa, bado kuna watu watafia dhambini kwa sababu ya uchaguzi mbaya kama alioufanya Adamu bustanini Edeni.
  Haya hii haimaniishi kuwa wokovu unaozungumziwa ni wokovu wa akina Sungura wa kusema nimeokoka ilhali bado uko vitani. Malaika alimaanisha mchakato wote wa wokovu ambao hatuwezi kusema nimeokoka bila ya kufikia destination yake –kutolewa kwenye sayari dunia sehemu ibilisi na malaika zake walipo. Dunia ni si sehemu salama. Ndio maana Mungu aliijaza maji hapo zamani (gharika), kwa sababu ya kazi za ibilisi kwa watu. Na Mungu ameahidi kuiteketeza tena dunia kwa moto. Ingekuwa sehemu salama baada ya kifo cha Kristo, Mungu asingeahidi kuiteketeza tena kwa moto.

  -*2Tim1:9 -12 Ambaye ALITUOKOA akatuita kwa mwito mtakatifu,
  Maana yake
  Aya hizi hazina maana tofauti na Kolos. 1:13-15. Mtu aliyeokolewa, hapati taabu tena. Hasumbuliwi wala kusukwasukwa na upande wa yule adui. Vinginevyo hiyo siyo maana dhahiri ya “kuokoa” kwa maana ya kutoa eneo la hatari na kuweka sehemu salama. Paulo angemaanisha asingesema haya aliyoyasema hapa; “Basi usiuonee haya ushuhuda wa Bwana wetu, wala usinionee haya mimi mfungwa wake, BALI UVUMILIE MABAYA PAMOJA NAMI KWA AJILI YA INJILI, kwa kadiri ya nguvu ya Mungu; ambaye alituokoa akatuita kwa mwito mtakatifu, si kwa kadiri ya matendo yetu sisi, bali kwa kadiri ya makusudi yake yeye na neema yake. Neema hiyo tulipewa katika Kristo Yesu tangu milele, na sasa inadhihirishwa kwa kufunuliwa kwake Mwokozi wetu Kristo Yesu; aliyebatili mauti, na kuufunua uzima na kutokuharibika, kwa ile Injili; ambayo kwa ajili ya hiyo naliwekwa niwe mhubiri na mtume na mwalimu. KWA SABABU HIYO NIMEPATIKANA NA MATESO HAYA, WALA SITAHAYARI; KWA MAANA NAMJUA YEYE NILIYEMWAMINI, NA KUSADIKI YA KWAMBA AWEZA KUKILINDA KILE NILICHOKIWEKA AMANA KWAKE HATA SIKU ILE”-2Timothy 1:9-12. Paulo anachokiongea hapa ni ule msaada wa kututia nguvu aufanyao Kristo kwa wale waliompokea. Msaada ambao ataendelea kuutoa kwa watu wake hadi atakapokuja kuwaokoa –kuwatoa duniani na kuwapeleka sehemu salama-mbinguni.

  -NA HIVYO MNAOKOLEWA, IKIWA MNAYASHIKA SANA MANENO NILIYOWAHUBIRI ISIPOKUWA MLIAMINI BURE” 1 WAKORINTHO 15:2
  Maana yake
  Paulo anasema -mnaokolewa akimaanisha ‘mnakua katika Neema-mnaukuulia wokovu’ endapo mtaishi sawasawa na injili niliyowahubirini. Na hatima ya kukua katika Neema –ukamilifu katika Kristo, anaufafanua katika mistari ya mwisho ya sura hiyo ya 1 wakorintho 15:50’s. Ili watu wafikie hatua hii ya kutukuzwa pamoja na Bwana wao, Paulo anawasisitiza “Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana siku zote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana” aya ya 58.
  Wanaotikisika, ni wale walio kwenye vishindo vya ibilisi. Wale ambao bado wanaendelea kuitenda kazi ya Mungu. Na Paulo anawaambia kuwa, kazi/taabu yao katika utumishi huo si bure. Kuna uzima wa milele. Aliyeokoka, haahidiwi uzima wa milele maana anao tayari. Wale ambao walishamwamini Kristo tu na wanaendelea kukua katika imani, ndio wenye ahadi ya uzima wa milele.
  -We believe it is through the grace of our Lord Jesus that we are saved, just as they are.” Acts 15;11
  Maana yake;
  Ukiangalia tafsiri za Biblia angalao zinazoaminika kwa kiasi Fulani, zinasema kama vile tafsiri ya Kiswahili ilivyo.
  But we believe that through the grace of the Lord Jesus Christ WE SHALL BE SAVED in the same manner as they.”-NKJV
  But we believe that WE SHALL BE SAVED through the grace of the Lord Jesus, just as they will.”-RSV
  But we believe that through the grace of the Lord Jesus Christ WE SHALL BE SAVED, even as they.- AKJV
  Bali twaamini kwamba TUTAOKOKA kwa neema ya Bwana Yesu vile vile kama wao.-SUV
  Nadhani ya kwako kaka Sungura, ni suala la tafsiri tu.

  Inaendelea…..

 95. Siyi, ndugu yangu!

  Mambo ya Sabato na Eva kula tunda ni kati ya hayo Mafumbo ya Mungu; nitayaacha kidogo ili tulitazame kwanza jambo la Wokovu ambalo tukilipokea ktk stahili yake, basi Mafumbo yote ya Mungu atayafumbua pamoja na mafumbo ya Shetani, vyote vitakuwa wazi ili tupate Kukamilika maana bila ya hivyo hatuwezi kuwa Kamili, na Ukamilifu ndio unaohitajika haswa ktk wakati huu tunapomgojea Kristo; ACHA UOGA!

  Ulinipa ushauri huu kuhusu suala la KUOKOKA:
  “Na hili huwezi kulielewa vyema, ni mpaka umekaa chini ukamlilia Mungu akuongoze kwenye uelewa sahihi wa somo maalumu liitwalo – KUHESABIWA HAKI KWA IMANI, ndani ya Biblia. Kuna kuwa redeemed na baadaye kuwa Saved!! Jifunze zaidi!!”

  Sikumlilia Mungu, maana Neno lake tumekwisha kupewa, hivyo nikakaa chini “nijifunze zaidi” kutoka hilo tulilopewa! Nimeupenda sana ushauri wako kwani umenifanya nirudi huko nyuma ya jambo hili ili nipate kulijua kwa undani zaidi. Rejea niliyoitumia ni Biblia ya KJV, na ilipobidi nilitumia kamusi ili kuipata maana ya maneno kama ulivyonishauri.

  Ninategemea kwamba nawe utakuwa ni yule aliyefanya maamuzi magumu ya kuiacha Biblia yako iiongoze dini yako, na si dini yako ndio iiongoze Biblia!

  Kwanza kuhusu swali lililoulizwa ktk mada hii, kimsingi mimi nakubaliana na Sungura kwamba mtu aliyeokoka asipokuwa makini anaweza kufika mahali akakupoteza kuokoka kwake. Mfano halisi ni Yuda Iskariote au akina Anania na Saphira; maana kulingana na Maandiko twafahamu kwamba yeyote atakayeiamini Injili na kubatizwa ataokoka!

  Baada ya hapo, sasa nataka niyarejee yaliyojiri ktk mchango wako, kuhusu “Kuokoka” kulingana na kile Biblia inachofundisha. Nimeyafuatilia yale maneno mawili, “Redeemed na Saved”, juu ya hilo, nimeona kwamba haya maneno yanazaliwa kutoka neno “Salvation”, hili ndilo neno mama ya hayo. Nitaanza na neno “Redeemed” kwamba ndilo jambo linalotokea kwanza kama ulivyosema; neno hilo linatokana na neno Redeem ambalo tafsiri yake rahisi ni kama hivi:
  Redeem = Kukomboa kwa malipo.
  km. a. Kukomboa kutoka ktk kifungo kwa kulipa malipo
  b. Okoa, ponya, opoa, fanya huru tokana na hatari, utumwa, kifungo, maumivu, mauti, dhambi na matokeo yake, kwa njia ya kafara (ikiwa ndiyo malipo) kwa ajili ya huyo mwenye dhambi

  Kutoka maana hizi chache tunaweza kusema kwa uhakika kwamba, tulikombolewa na Mungu kwa malipo ya kule kutolewa kafara kwa Kristo pale msalabani; hili tunalijua hivyo baada ya kuwa limefanyika hivyo ktk uhalisi wake. Lakini, ni muhimu sana pia kujua kwamba, UAMUZI WA KUTUKOMBOA ndio uliotangulia kufanyika kabla ya ukombozi huo kufanywa kwa huko kuilipa hiyo gharama ya ukombozi!

  Ndipo ni vizuri tuuangalie kwanza huo UAMUZI uliotangulia kufanywa, maana huu ndio msingi halisi wa jambo hili, na ndio kiini. Nao Uamuzi huu ndio unaoitwa SALVATION au WOKOVU, ambamo ndani yake ndimo mna Ukombozi unaopelekea Kuokolewa au Kuokoka kwa hao waliokusudiwa jambo hilo. Wokovu unajumuisha matendo ya ukombozi na michakato yake kama Kuhesabiwa Haki, Kutakaswa, Neema, Msamaha, Ondoleo la dhambi, Kutukuzwa, nk. Nao Wokovu huo hutafsirika kwa mkristo ktk namna tatu:

  1. Mkristo AMEOKOLEWA kutoka Hatia na Adhabu ya Dhambi hivyo yu SALAMA! (Lk 7:50; 1Kor 1:18; 2Kor 2:15; Efe 2:5,8; 2Tim 1:9)

  2. Mkristo ANAOKOLEWA kutoka tabia na kutawaliwa na Dhambi.
  (Rm 6:14; 8:2; 2Kor 3:18; Gal 2:19-20; Phi 1:19; 2:12-13; 2Th 2:13)

  3. Mkristo, hapo Bwana atakaporudi, ATAOKOLEWA kutoka ktk shida na mapungufu yote ya mwili ambayo ni matokeo ya dhambi na laana ya Mungu juu ya dunia hii iliyo dhambini (Rm 8:18-23; 1Kor 15:42-44), na kufanywa kuwa mwenye kumfanania Kristo kikamilifu (Rm 13:11; Ebr 10:36; 1Pet 1:5; 1Yn 3:2).

  Wokovu huo ukiwa ni kwa Neema kupitia Imani, ni zawadi ya bure isiyohitaji jitihada yetu wala malipo yoyote kutoka kwetu, ndipo wapaswa kupokelewa kwa shukrani! (Rm 3:27-28; 4:1-8; 6:23; Efe 2:8)

  Hebu nipose kidogo kwanza, nikupe nawe nafasi ya kuyatafakari haya machache, kisha nitaendelea tuzidi kuuchunguza huo “Uamuzi wa Kutukomboa.”

  Asante!

 96. Ny friend Siyi,

  Kuna mambo ambayo huwa yanaitwa uendawazimu ukiyafanya, nayo ndio unayojaribu kuyafanya hapa bwana Siyi.
  Unasema mtu huwezi kusema umefika mwisho wa safari wakati ndo uko mwanzo wa safari. Ni kweli kabisa huwezi kufanya hivyo. Lakini ninachojiuliza ni hiki kwamba kwani nani kasema kuwa ameshafika safari?

  Si umekazia mwenyewe kusema kuwa wokovu ni mchakato, na mimi nimekukubalia kuwa ni kweli. Na nikakwambia kuwa ni mchakato ambao tunauishi. Ukisema kuwa wokovu ni mchakato halafu ukasema kuwa kile kitendo cha kufika unakokwenda ndio wokovu, na sawa na kufika Ubungo unatoka Moro halafu ukasema kuwa kile kitendo cha kufika Ubungo ndio safari yenyewe. Huo ni uenda wazimu!
  Lazima uelewe uhalisia wa wokovu kwamba tunaokolewa kutoka wapi. Kwa mawazo yako ninavyokuona unajaribu kujiaminisha kuwa tunaokolewa kutoka duniani kwa maana ya kutolewa kwenye hii sayari, kitu ambacho ni uongo.
  Tunaokolewa kutoka dhambini siyo kutolewa duniani. Atairwa jina lake Yesu, ndiye atayewaokoa watu wake na dhambi zao. Dhambi siyo hii sayari, dhambi ni mfumo wa maisha ya uovu.

  Unaposema si vyema hata kidogo kutumia neno ‘nimeokoka’ unapingana na nani sasa, si unapingana na biblia? Siyo sisi tunaosema kuwa tumeokoka, bali ni biblia ndo inayotuambia hivyo kuwa tumeokoka, nasi twakubaliana na biblia kuwa tumeokoka.
  Ndiyo hiyo mistari inayosema ‘tumeokolewa kwa neema, Kanisa liliongezeka kutokana na wale waliokuwa wanaokolewa.

  Unawezaje kupingana na maandiko kama haya :

  -(NAYE ALITUOKOA KATIKA NGUVU ZA GIZA, AKATUHAMISHA NA KUTUINGIZA KATIKA UFALME WA MWANA WA PENDO” WAKOLOSAI 1:13

  -“LAKINI WEMA WAKE MWOKOZI WETU MUNGU, NA UPENDO WAKE KWA WANADAMU, ULIPOFUNULIWA, ALITUOKOA.” TITO 3:4)

  -“MKIOKOLEWA NA UHARIBIFU ULIOMO DUNIANI KWA SABABU YA TAMAA” 2 PETRO 1:4
  -“SASA KUMEKUWA WOKOVU NA NGUVU….” UFUNUO 12:10
  -*2Tim1:9 -12 Ambaye ALITUOKOA akatuita kwa mwito mtakatifu,

  -NA HIVYO MNAOKOLEWA, IKIWA MNAYASHIKA SANA MANENO NILIYOWAHUBIRI ISIPOKUWA MLIAMINI BURE” 1 WAKORINTHO 15:2

  -We believe it is through the grace of our Lord Jesus that we are saved, just as they are.” Acts 15;11
  Wokovu ni moja ya silaha anazotakiwa kuvaa mkristo ili apigane na ibilisi, inaitwa chapeo(helmet) ambayo inavaliwa kichwani(Efeso 6:17)
  Wewe Siyi unayedai wokovu siyo duniani kinyume kabisa na biblia inavyosema sijui nini kimejaa kichwa chako.
  Unakana kitu ambacho ni moja ya silaha ya kumshinda shetani. Na shetani tunapambana naye na kumshinda hapahapa duniani wala si mbinguni.

  Nakuwa kama naongea na mtu ambaye ufahamu wake umegandamana katika kuelewa mambo hata mepesi kabisa, kwa nini huwezi tu kuiona mantiki hii ndogo kuwa kama wokovu ni mchakato basi lazima uuishi huo mchakato maana ndo unaokupeleka kwenye destination. Nje ya huo mchakato unaoitwa wokovu huwezi hata kufikia destination yako. Wokovu siyo hiyo destination, bali ni mchakato (chombo) unaaokupeleka kwenye destination. Usikariri tu kusema kuwa ni mkosa kusema umeokoka , maana kwa kufanya hivyo unapingana hata na unachokikiri mwenyewe.

  Siyi unajua umezidiwa kuelewa hata na Lenda ambaye ni msabato mwenzio, yeye alishaelewa kuwa neno wokovu kwenye biblia liko katika Past, Present, na Future. Wewe umeng’ang’ana na future peke yake, na matokeo yake ukifika kwenye andiko ambalo lina past au present unapata shida sana, kiasi kwamba unatamani maandiko yote yangetuma future.
  Mantiki iliyo kichwani mwako ya neno kuokoka kwa sehemu kubwa siyo ya kibiblia, siyo ya neno Sodzo, bali una picha ya mindset ya kawaida kabisa ambayo ni hekima ya dunia tu ya mtu wa mwilini.

  Nahisi nahangaika na mtu mwenye akili ndogo sana katika kulielewa hili! Anyway, ngoja nikuvumilie, u never know!!

  Unasema mtu aliyeokoka hana vita tena maishani mwake, this is very fanny, na hiyo mentality ndo inayowatesa sana wasbato kwa habari ya wokovu. Huo ndio uongo ambao mnadanganywa Siyi? Mtazamo ulionao juu ya kitu kinachoitwa wokovu hauko sahihi.

  Sikia, Israel pamoja na kuokolewa kutoka Misri walipigana vita za kutosha tu jangwani, na waliozembea hawakufika hata nchi ya ahadi. Na ndio maana nimesema kuwa mtu anaweza akapoteza wokovu wake.
  Usijifanye kama vile hatujajadili nini maana ya wokovu, ndio maana nilikwambia kuwa hii mada wewe imekutupa nje, maana unayoyajadili ni yale ambayo tulishayajadili kwenye mada ya Kuokoka duniani.

  Hakuna cha tone la shetani wala nini,biblia inasema tumeokolewa au ya kwako haijasema hivyo Siyi? Kama ni tone la shetani ninyi ndo mko nalo ambao mnakinzana na ukweli wa maandiko.
  Siyi unawezaje

  Nionyeshe kauli yangu ambayo nilisema kuwa aliyeokoka hawezi kujikwaa, mbona unazidi tu kuniambia kuwa ninakinzana na kaulia zangu za mwanzo? Show me!!
  Vinginevyo acha maneno ya kuchombeza yasiyokuwa na ukweli bhana, hiyo ni tabia ya uswahiliswahili ambayo haifai kwenye mambo muhimu kama haya.
  Nionyesheandiko linalosema kuwa Israel waliofika mwisho wa safari (yaani nchi ya ahadi) ndio waliookoka. Na hapa ndipo nitaumbuka vibaya mno Siyi, maana unasema mawazo yako ukifikiri kuwa umesema biblia.
  Wewe unaposema kuwa Kaleb na Joshua hao ndio tungesema kuwa waliokoka, bilblia inasema wao ndio waliingia kati ya waliokuwa wameokolewa toka Misri.
  Hebu sema, Israel walikombolewa kwa kitu gani huko Misri?

  Siyi, hebu acha mzaha bwana, ni aibu kubwa sana kuniambia eti ninaishia kuwa na maana tenge, maana tenge ipi unayoisemea, kama si kuleta upuuzi tu kwenye jambo makini kama hili!!
  Huwezi kunifundisha wewe namna ya kusoma biblia, wakati mtu mwenyewe unashindwa kuelewa mambo ya kawaida kama haya.
  Suala la kutawadha sintalijadili sasa hivi hapa, siyo mahali pake!

  Nakungoja Siyi!!

 97. Mjoli, Haule,
  Ninavyokuona umetumia uwezo wako mkubwa wa akili kumjibu Siyi. Hajaambulia chochote ndugu yangu. Umesema
  1. “Kuna sheria ya mwilini(Torati) na kuna sheria ya roho wa uzima
  (sheria yaKristo)Injili”
  Bado sijakuelewa. Ni sheria zipi hizo? Unaweza kuzitofautisha mtumishi?
  2. “Kuna sheria Dhambi(Rum7) na kuna sheria ya uhuru(Rum8)”
  Bado sijakuelewa. Unaweza kuzitofautisha?
  3. “Kuna sheria ya mume Rum 7:1-4”
  Bado sijakuelewa. Sheria hizi ziko nje ya amri 10 au?
  4. “nilimaanisha kuna Mw 1:29-30;9:3-4 na kuna Kumb 14”
  Hii habari ya vyakula, inahusianaje na Rumi 7 na 8? Au kwa vile leo tuna nyama, je hatupaswi kula mboga na matunda? Hebu jaribu kufafanua rafiki yangu, maana naona umeniacha kabisa!!
  5. “Tuseme na kutenda kama watu tutakaohukumiwa kwa sheria ya uhuru Yak 2:12”
  Je, sheria ya uhuru ni tofauti na amri kumi? Au ni sheria zinazosemwa kwenye Yakob 2: 11 (Kwa maana yeye aliyesema, Usizini, pia alisema, Usiue. Basi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekuwa mvunja sheria)???
  Nakungoja mtumishi
  Siyi

 98. Bro Siyi……..Nilimaanisha

  Kuna sheria ya mwilini(Torati) na kuna sheria ya roho wa uzima
  (sheria yaKristo)Injili

  Kuna sheria Dhambi(Rum7) na kuna sheria ya uhuru(Rum8)

  Kuna sheria ya mume Rum 7:1-4

  nilimaanisha kuna Mw 1:29-30;9:3-4 na kuna Kumb 14

  Tuseme na kutenda kama watu tutakaohukumiwa kwa sheria ya uhuru Yak 2:12

 99. Sungura,
  Kwanza, Mimi nashukuru tu kama umenipa heshima ya kujadili mada hii. Nimetambua hiyo heshima yako. Aidha, nimetambua pia heshima SG moderators kuendelea kuyaruhusu mapachiko yangu yawafikie wengi. Mungu awabariki kwa jitihada na umoja wenu. Kazi yenu si bure!!
  Pili, Baada ya kusema hayo, nipende kusema kuwa, ndani ya mada, huwa zinaibuka mada nyingine ndogondogo ambazo ni vigumu sana kuziepuka wakati wa mjadala. Ukiwa mhafidhina wa mijadala, utakuwa mtwana wa fikra maana huwezi kuzungumzia mti, usipohusisha na matawi yake. Halikadhalika, huwezi kuzungumzia HABARI YA KUPOTEZA WOKOVU bila kuangalia chanzo, upatikanaji na hatima yake. Kwa mantiki hiyo, nachelea kusema kuwa mimi najadili nje ya mada, japo naheshimu mawazo yako pia.
  Tatu, hata mimi siku ile, nilisema hivyohivyo kuwa, pamoja na kwamba hizo huduma za maombezi kanisani zipo, haina maana kwamba kila mdhambi hulazimika kwenda mbele kuombewa. Hata mimi siku ile nilisema kuwa, kwa sasa hatuna makuhani wanadamu isipokuwa Kristo pekee. Ukitenda dhambi ya kukusudia au kwa isivyo bahati, nenda magotini omba msamaha wa dhambi hiyo na damu ya Kristo (kwa njia ya Imani), itakkusafisha na uovu wote. Hivyo kwenda kanisani au kutoenda kanisa kutubu, ni uchaguzi tu wa mtu mwenyewe. Na namna zote hizi za toba (ile ya binafsi na ile ya mbele za kadamnasi), Mungu anazitambua.
  Nne, hata mimi sitaki watu waniamini maana sina mbingu ya kuwapeleka. Ni vyema wakamwamini mwenye mbingu –Kristo Yesu pekee. Nilichokuwa nakileta kwenu siku ile ni kile mnachodhani mnakiona kumbe hamkioni. Naam, hata sasa mwaendelea kudai kuwa mnaona kumbe ni vipofu mnaohitaji msaada. Lakini kwa vile hamtaki kushikwa mkono na wenye macho, hatuna kuwaacha hadi hapo mtakapotambua kuwa mlikuwa ni vipofu. La msingi ni kwamba, angalieni msichelewe!!!!
  Tano, Sungura, naamini ulinielewa tangu mwanzo nilipozungumzia habari wa wokovu – nikitoa maana ya Justification by Faith, Sanctification na hatimaye Glorification. Napenda kurudia maelezo yangu kuwa, UNAPOANZA SAFARI, HUWEZI KUSEMA UMESHAFIKA MWISHO WA SAFARI. Itakuwa ni kioja kwa mtu kusema niko Dar es Salaam ilhali yuko Mikese kama anatokea Morogoro. Kama unaishi Dar es Salaam, nina imani ulishawasikia watu wakiongopea wenzao wanapoongea na simu, “Niko ubungo, kumbe bado yuko kimara n.k.” Na watu humshangaa sana mtu huyo!! Huo ni UONGO na ndicho mnachokifanya ninyi akina Sungura, kuendelea kuipumbaza akili kuwa mmeshafika kumbe masikini bado. Na kwa sababu bado, si vyema hata kidogo kutumia neno nimeokoka ilhali bado uko kwenye mchakato tu. Unapoanza kazi, huwezi kusema kuwa umeshaimaliza. Hutaeleweka kwa watu!! Watakucheka sana!! Ndiyo, maana Siyi (na wengine walio makini katika hili), hatusemi tumeokoka na badala yake tunasema tumehesabiwa haki kwa imani kwa njia ya kumwamini Kristo aliyetukomboa (redeemed us) kwa damu yake. Tunasamehewa yote ya kale na kuwa wapya. Tunapokuwa tumekombolewa sasa, tunabaki na jukumu la kuishi sawasawa (sanctification) na ukombozi huo ili siku ya mwisho tuokolewe (saved). Na kwa wale wanaomkiri Kristo na kufa papo hapo kama vile yule mwizi msalabani, mgonjwa mahututi n.k. hao hupata tiketi ya moja kwa moja ya ufufuo wa kwanza. Wale wanaoendelea kuwa hai, mchakato wa wokovu, unaanza pale mtu anapomwamini Kristo. Anapotambua kafara yake msalabani-ukombozi. Baada ya hapo mtu huwa ni mumini, mfuasi, mtume nk wa Kristo anayeukulia wokovu. Ndiyo maana anaitwa ‘msafiri wa kwenda mbinguni’-Kolos. 3:1-4. Msafiri bado anaweza kukutana na vita, mapambano na dhahama nyingi njiani, naam hata kukata tamaa endapo hatakuwa beneti na Kristo. Ndiyo maana Paulo anasema, tunayaweza yote katika yeye anayetutia nguvu-Filip 4:13. Bila msaada wa Kristo, safari ya imani hatuiwezi. Mtu aliyeokoka, hana vita tena vinavyomkabili maishani mwake. Yuko eneo salama huyo. Haguswi na ibilisi tena kwa namna yeyote ile. Ndiyo maana sisi tunasema, hii ndiyo hatua ya Glorification. Kwa hiyo kaka Sungura, tofauti ni hiyo ndogo tu na inabidi uielewe vyema. Shetani huweka tone dogo tu la uongo kwenye kweli nyingi. Na watu huwa ni vigumu sana kubalibaini tone hilo, hasa linaposemwa na watu wakubwa (viongozi) wanaoaminika kwa watu wengi. Hatari sana hiyo kaka!! Ila nashukuru kwa vile umeanza kutambua na kukubali mwenye kuwa muumini, mfuasi wa Kristo, msafiri wa kwenda mbinguni nk (ninyi kwa kutokujua mnamuita aliyeokoka), anaweza kujikwaa –kutenda dhambi tofauti na kauli zako mwenyewe za hapo awali. Nina imani hata Mjoli Haule, atashtuka kidogo kukuona Sungura umekiri hivyo. Hiyo nayo ni hatua nzuri. Tuzidi kuombeana sana marafiki zangu, ili hatimaye tusipotee kabisa. Itakuwa hasara iliyoje!! Mungu atusaidie sana!!
  Sita, naomba unieleze maana ya “kutenda dhambi” na “kuishi dhambini”!! Je, mtu anapotawadha, ni ishara ya kufanya nini? Ni kuoga mwili mzima au? Je, kauli ya Kristo ya kutawadha mikono, kichwa na miguu ilimaanisha nini? Kuoga mwili mzima au sehemu tu” Je, wanafunzi waliobatizwa upya na Paulo katika Mdo 19:1-6, hao nao walitawadha au walioga upya?
  Saba, kwa habari ya Musa kuwatoa Israel Misri, nafikiri ulinielewa vyema, japo mfa maji haachi kutapatapa. Umesema, “Kitendo cha Israel kufika Kanaan hakikuwa ndio wokovu, hicho kilikuwa ni destination ya huo mchakato(wokovu)”. Umechanganya madesa kweli hapa. Kwa mujibu wa Biblia, wale waliofika mwisho wa safari, ndio waliokoka. Walipoanza safari, walikombolewa tu utumwani. Waliofika, ndio waliokoka. Na hata kipindi kijacho, Biblia inasema, wale watakaovumilia hadi mwisho, ndio watakaokoka – Mathayo 10:22, Mathayo 24:13. Agano la Kale linatambua mashujaa wa imani waliotoka Misri hadi Kanaani walikuwa ni wawili tu – Joshua na Kalebu. Hawa ndio leo tungesema, waliokoka. Kumbuka, mwanzoni nilikupeni kanuni za kuisoma Biblia. Lakini hukuonekana kukubaliana nazo. Na badala yake, ndiyo unaishia kuwa na maana tenge kiasi hiki kaka. Tafadhari zirejee zile kanuni. Zitakusaidia sana kuielewa Biblia unapoisoma.

  Hivyo kaka Sungura, ni vyema ukaelewa kuwa, tumekombolewa kwa damu ya Yesu. Tumehesabiwa haki kwa njia ya imani. Watakaokubali kuishi sawasawa na Neema hiyo, wakavumilia hadi mwisho, ndio watakaokoka!! Lini?? Baadaye -siku Yesu atakaporudi!
  Ubarikiwe sana
  Siyi

 100. Mjoli Haule,
  Ubarikiwe sana kaka kwa kurejea tena. Nashukuru kama unatufuatilia na Sungura (mzee wa logic) kwenye mjadala huu. Umeandika Kiingereza, ngoja mimi niandike Kiswahili tu, maana kiingereza changu ni kile cha akina Kayumba. Hivyo badala ya watu kusoma na kumakinika juu ya hicho nilichoandika, wataanza kuvunja mbavu kwa kiingereza changu kibovu… Huo ndio ukweli kabisa. Ila usingekuwa unajua Kiswahili, basi ningeandika hichohicho kibovu. Nina imani kwa neema ya Kristo, ungeelewa tu.
  Mimi umenichanganya au niseme umeniacha hoi njia panda kabisa. Kwani Warumi 7 inazungumzia nini kilicho tofauti na Warumi 8, ambacho wakristo wanapaswa kukiacha kile cha warumi 7 na kukifuata kile cha warumi 8? Kwa maneno mengine, ni mapokeo yepi yaliyoko kwenye warumi 7 ambayo, waumini hawapaswi kuyafuata leo? Ni wakati gani tulikuwa warumi 1, 2, 3, 4, 5, 6, 7, na hadi leo unasema tuko warumi 8? Je, tutafika lini warumi 9, 10…nk.? Au ulimaanisha nini rafiki kwa kusema hayo hapo juu? Naomba unisaidie tafadhali!!
  Nakungoja!!
  Siyi

 101. Siyi,

  Kwanza nikwambie jambo moja kuwa nimekupa heshima kubwa sana kukubalia kujadili nje ya mada. Wewe kulingana na unachoamini haukutakiwa kujadili hii mada. Lakini kwa vile hukulion sana hilo ulijiingiza ukajikuta unatulazimsha kujdili kitu ambacho mada imekiacha nje.

  Pili, mambo uliyosema ya kwenda kutubu kanisani na kuitwa mbele, na kuomba toba wakati wa maombi kanisa ni typical religious, na yamejaa mentality ya mfumo wa agano la kale wa kiibada( kwenda kufanya kila kitu Hekaluni). Hili agano jipya ambalo ni bora zaidi, hekalu ni mimi mwenyewe, so yote hufanyika ndani yangu.
  Usibebe dhambi toka nyumbani kwako hadi kanisani , it could be too late!!

  Tatu hayo mawazo ati ya kuja siku moja kukulaumu kuwa ulikuwa nasi hukutuambia futa kabisa, Siyi nakijua vizuri ninachokiamini na kukikiri, naam nimeokoka!
  Hata kama ungetaka tukuamini tusingekuamini, so huhitaji hata kutambia kuwa hutaki tukuamini!

  Tatu, nimekuambia mara nyingi sana kuwa wewe huwa unadhani kunyakuliwa ndiko kuokoka, ndio maana ukikutana na sentensi inayosema tumeshaokoka, eg tumeokolewa kwa neema, unapata shida sana kukubaliana na hiyo mistari.

  Umekiri vema kuwa wokovu ni mchakato au safari ukishaanza kuisafiri ndio maana yake umeokoka. Kama kunyakuliwa ndio kuokoka, basi kusema kwako kuwa waliokufa wamefika safari yao ni kusema uongo, maana hata wao wanasubiri kunyakuliwa.

  Wokovu tunauishi, ni maisha yanayoendelea ndio maana tunasema ni mchakato. Kama wewe unasema kuwa wokovu ni mchakato halafu unasema hujaokoka, basi huuishi huo mchakato maana yake wewe uko nje ya huo mchakato( wokovu)

  Mimi sijui nini kigumu kwako kuelewa hili suala, maana si suala gumu kulielewa hata kwa akili tu. Nafikiri kuna mapokea yameweka cementi kwenye ufahamu wako.

  Siyi kile kitendo cha kutolewa tu sehemu ya hatari /dhambini /utumwani /gerezani mwa shetani/ kwenye ulimwengu wa giza ndicho wokovu wenyewe, hakisubiri mpaka ufike unakopelekwa ndipo kiitwe wokovu.

  Which means, aliyekutoa huko alikutoa kwa kumshinda aliyekuwa anakushikilia, si kwamba ulitoroka kwa hiyo unakaa kwenye safari (wokovu) kwa hofu kwamba uliyemtoroka atakufuatia na kukukamata tena.
  Farao alidhani Israel wametoroka, hivyo akaamua kuwafuatia kwa nyuma, bila shaka unajua kilichompata, maana alitambua kuwa hawakutoroka, bali aliyewachukua alimshinda kwanza yeye!

  Siyi kuna tofauti kubwa sana kati ya kutenda dhambi na kuishi dhambini, sisi hatukuwa watenda dhambi, bali tulikuwa tunaishi kabisa humo. Tuliposamehewa siyo maana kwamba hatuwezi tukajikwaa, tunaweza, lakini tulishatoka kwenye kuishi humo. Kumbuka kauri hii’aliyekwisha kuoga, haogi tena, bali hutawadha’

  Nilikwambia moja ya kipengele au package ya wokovu ni kusamehewa dhambi, wewe unaniambia kuwa ati nimesema kuwa ukiokoka hutendi dhambi. Hili nadhani umelipinda hivyo ili utafute mwanya wa kuniambia kuwa kama ukiokoka huwewzi tenda dhambi mbona Isreal walitenda dhambi jangwani! Nimekuona. Na nimekuona jinsi ambavy umelirukia tuu neno ‘wokovu ni mchakato’ bali kufikiri sana ni nini maana yake hasa.

  Wokovu hauwi mchakato wa au safari ya kufika mbinguni, bali ni mchakato wa kuufikia utimilifu wa kristo. Siyi kuna watu mimi naamini wataingia mbinguni hata kuwa wameuishi huo mchakato. Kuna watu wanamkiri kristo wakiwa karibu na kukata roho.

  Biblia haijipingi wewe ndo huielewa, uko so closed, bila shaka unajua mambo ya closed questions na open questions kwenye mambo ya research.

  Kuokolewa siyo kutolewa duniani , bali ni kutolewa kwenye gereza la ulimwengu wa giza, ndo kitu hasa Yesu alidhihirishawa ili akifnye, na alikifanya kwa hicho kifo chake. Siku ya mwisho unayoisema Yesu haji kututoa gerezani, bali anakuja kutuchukua kwenda mbinguni. Na kwenyewe hatuendi kuishi, bali tunaenda kula bata tu kisha tunarudi duniani. Dunia ndio sehemu alipotengenezewa mwanadamu kuishi, siyo mbinguni( Ihope hiyo siyo ngumu)

  Siyi acha uongo, Musa hakutumwa kwenda kuwaweka Israel huru na utumwa wa Farao, alitumwa kwenda kuwatoa Misri, na alifanya hivyo. Na ndo hapo nikakwambia kuwa hicho kitendo cha kutolewa kwao Misri ndicho biblia inasema Israel waliokoka. Lakini walioshindwa kuushi huo mchakato wa wokovu walifia jangwani. Ndio maana niliwahi kukuambia suala la kuukulia wokovu. Sasa huwezi ukakulia kitu ambacho hauko naccho.

  Kitendo cha Israel kufika Kanaan hakikuwa ndio wokovu, hicho kilikuwa ni destination ya huo mchakato(wokovu)

  Tofautisha kati ya wokovu na hatima ya wokovu!

  Ndiposa nikarudi kwenye mada nikasema, mtu anaweza kupoteza wokovu wake, kama wale Isreal walivyoupoteza na kujikuta hawawezi kufika kwenye hatima ya safari yao , yaani nchi ya ahadi!!

  Siyi, tunaishi wakovu, naam tumeokoka!!!!

 102. Bro Siyi………

  Are you struggling in Romans 7 or are you walking in victory in Romans 8?
  Chapter 8….. Paul talks about is the power of the indwelling Spirit to set us free
  from the flesh. Something happened to Paul that needs to happen in all of us

  Mjoli Haule

 103. Sungura,

  Nashukuru kwa vile umekiri kuwa huwa huendi kanisani kutubu. Hata mimi sikubishii kwa hilo. Kama unafikiri mungu atakutuma kwenda kuzimu, subiri, utaenda tu. mungu wako huyo atakutuma tu.

  Aidha, hata mimi sikuchora mstari kuwa kwenda kanisani ni kwa ajili ya kutubu tu. Hasha! Ielewe kuwa, kwenda kanisani, ni kwenda kumwabudu Mungu. Kutubu ni sehemu ya maombi ya ibadani, ndiyo maana watu huitwa mbele kuombewa na wachungaji. Lakini toba kama toba, unaweza kuifanya popote na bila yeyote yule kumhusisha isipokuwa wewe na Mungu wako tu. Ndani ya Biblia kuna mifano mingi ya watu waliotubu wenyewe tu, na wale walioenda mbele ya kadamnasi kutubu. Zote ni toba na Mungu anazikubali. Ukidakia kipande kimoja cha sentensi na kujidai ndo umeona ilhali u kipofu, huko ni ishara ya kuishiwa rafiki yangu. Wewe leta hoja za kimaandiko. Porojo sina muda nazo kaka!!

  Aidha, naomba uelewe kuwa, siko hapa kumshambulia mtu yeyote. Nashambulia uongo uliomo ndani ya vichwa vyenu!! Na kwa vile umesema unaniuliza maswali mepesi, nami nitakupatia majibu mepesi pia;

  Swali 1.
  “…shida unayopata ni ipi kuhusu cc na kuokoka, je ni kule kukiri kwetu kuwa tumeokoka, au ni kule sisi kuwa si wasabato/tusiosali J’mosi?

  Jibu jepesi
  Mimi sina shida na ninyi. Sina ugomvi na ninyi. Ninyi ni marafiki zangu tu!! Na kwa vile ni marafiki zangu, ninawapenda sana. Ndiyo maana naumia sana ninapowaona mna uelewa wenye nasaba za kishetani huku mkifikiri kuwa mko sahihi!! Naumia sana kwa kweli!! Kwa nini?? Nataka kwenda na ninyi mbinguni. Sitaki kwenda peke yangu. Na kwa sababu ninawapenda, sina budi kuwaambieni japo, najua mtanichukia sana mwanzoni kwa sababu ya kutonielewa. Saa ipo mtakuja kunielewa kabisa.

  Aidha, kukiri kwenu kwamba mmeokoka, mimi sina tatizo nako, isipokuwa mnapaswa kukiri kwa ufasaha wa lugha ya Maandiko. Mkisema mmeokoka kwa maana ya kuwa wafuasi au waumini wa Kristo, mwafanya kosa kubwa. Na hilo sharti mimi ndugu yenu ninayewapenda sana, niwaambie. Maana nisipowaambia, mkipotea, mtakuja kulalamika, ohh Siyi wewe ulikuwa pamoja nasi, mbona hukuturekebisha kwa kauli zetu hizo za kiudanganyifu? Kimsingi, nitatahayarika!! Ili niyakwepe hayo yote, sharti niwaambie ili kama ni kubadilika, mbadilike kungali mlango wa rehema haujafungwa kwenu! Habari za kuokoka vs kumkiri Kristo, siku ile nilisema sana na hata kwa Lwembe hapo juu, nimesema pia. Rejea tafadhali.

  Kuhusu ninyi kutokuwa wasabato, sidhani kama linanihusu pia. Maana kuwa msabato ni kufanya uamuzi kati ya mtu mwenyewe na Mungu wake. Ninachokifanya mimi ni kukuelekezeni tu. Sabato ndiyo ishara kwa watu wa Mungu. Mungu hana ishara nyingine yoyote kwa watu wake, ni Sabato tu. Haina maana kwamba nashadidia amri moja tu. Hasha! Ninachosema ni kwamba, huwezi ukasema kuwa wewe ni mfuasi wa Kristo, mtu unayempenda Kristo huku ulishaikataa ishara yake – Sabato. Huo ni uongo usiovikwa hata vazi lolote. Hivyo, ninyi ndg zangu, mna hatari za aina mbili (kwa mujibu wa swali lako), kutotumia maneno sahihi ya Biblia huku mkidanganyika hamna dhambi ilhali hata ile ishara (Sabato) ya kuonesha kuwa ninyi ni wafuasi au waumini wa Kristo, nayo mmeikataa. Makosa mnayoyafanya kwa sasa (japo hamuelewi na itawachukua muda mrefu kuelelwa), ni hayo mawili- unafiki, yaani ninyi ni zaidi ya watu waasi. Samahani kwa lugha kali!!

  Swali 2
  Unadhani tukiacha kukiri kuwa tumeokoka ndo tutakuwa hatujaokoka?

  Jibu jepesi
  Mnachopaswa kufanya ni kubadilisha kauli na kuipokea/kuikubali ishara ya Mungu – Sabato. Badala ya kusema hivyo, mnavyosema sasa (kama swali 2 hapo juu), mnapaswa kusema kuwa, ninyi ni Waumini/wafuasi wa Kristo. Ni wasafiri/wapitaji tu hapa duniani. Maskani yenu ni mbinguni. Na mtafika mbinguni, safari yenu ya kiimani itakapokamilika kwa kila mmoja. Nasema hivyo kwa sababu baadhi yetu, wameshakufa wakiwa wakamilifu, wengine watakufa kabla ya Kristo kurudi na wengine watakutwa hai. Kristo atakaporudi, wakamilifu wote waliokufa, na watakaokutwa hai, wanyakuliwa kumlaki Bwana hewani. Kristo atawaondoa duniani na kuwapeleka mbinguni. Kwa hiyo mchakato wa wokovu unaanza pale tunapomwamini/kumkiri Kristo na utakamilika pale Yesu atakapotutoa duniani na kutupeleka mbinguni. Kwa sasa hatuwezi kusema kuwa tumeokoka ilhali bado tuko duniani, maana bado tuko kwenye mchakato na wengine hawajauanza hata huo mchakato wenyewe.

  Mimi sitaki mniamini. Napendekeza muiamini Biblia tu. Biblia inasema Yesu ni mwokozi wa watu kutoka kwenye dhambi zao!! Mathayo 1:21 Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.
  Wewe Sungura unakataa kuwa Yesu haji kuokoa wadhambi!! Duu, tumwamini nani kati ya wewe na Mungu?

  Na kama majibu yangu ya Waisrael umeyapata vyema, sasa na wewe jitathimni hicho unachokiamini kama kiko sahihi. Wewe unasema waliokoka, na kuokoka unakokusema, ni kutotenda dhambi. Je, hayo waliyoyafanya jangwani wakadumu miaka 40, hayakuwa dhambi? Je, unaweza kubatilisha usemi wako sasa kuwa mtu aliyemkiri Kristo, bado ni mdhambi huyo anayehitaji utakaso wa kila saa ili afikie ukamilifu? Je, umekubali sasa kuwa wokovu ni mchakato na si wimbo wa kilokole ‘nimeokoka, nimeokoka’? Mimi nakuonesha tu, mwenye kufanya uamuzi sahihi, ni wewe mwenyewe. Nina imani unaelewa maana una uwezo mkubwa sana wa kiakili. Hata nashangaa kwa nini hulioni jambo jepesi kama hili!!

  Aya ulizoninukulia, nilishazijibu mwanzoni kabisa mwa mjadala huu. Unataka tena nirudie au? Kama unataka nizirudie, jibu pia zile nilizokupeni mimi ili uoneshe kama Biblia inajipinga au la!!

  Kimsingi nakubaliana na wewe kuwa, kifo cha Kristo ndiyo msingi na kiini cha wokovu wetu. Pamoja na kiini hicho kuwepo, bado kuna masharti kwa wale watakaookolewa siku ya mwisho. Vinginevyo, dunia nzima (waovu na wema), kifo cha Kristo kingewaokoa wote. Lakini kwa vile kuna masharti, hatuwezi kusema kuwa hatuna dhambi, tumeokoka (saved), ilhali bado tunavunja sheria za Mungu, tunaweza kukutana na changamoto mbaya za ibilisi n.k.. Kile alichokifanya Kristo hakina tofauti na kile alichokifanya Musa kwa wana wa Israel (kwa maana ya kawaida japo Kristo huwezi kumlinganisha na mwanadamu). Kazi ya Musa ilikuwa ni kuwaweka huru Israel kutoka mikoni mwa utumwa wa Farao. Wenye kuupokea uhuru huo, walikuwa ni Waisrael na wamisiri baadhi. Kifo cha Kristo, kilituweka huru mikononi mwa shetani. Wenye kuupokea uhuru huo, ni sisi wayahudi na wamataifa wote. Kuukubali uhuru huo, sharti tukubaliane na kile anachosema katika maandiko yake. Mimi ninachoelewa kama ilivyokuwa kwa Musa, Yesu alituredeem kwanza, halafu kama tutakubaliana na masharti ya uhuru huo, atakuja kutusave kutupeleka mbinguni. Kuna haja ya wewe kujifunza habari za Mkombozi (Redeemer) na Mwokozi (Saviour). Jifunze kwanza ili ugundue sehemu tunayobishania saana.

  Naishia hapa kwa leo.

  Siyi

 104. Lwembe,
  Rafiki yangu kipenzi
  Naomba ieleweke kwamba, mimi sipingi wokovu. Na hili nililisema tangu mwanzoni mwa mjadala huu. Ninachowaonesha ambacho ninyi hamkioni, ni KUOKOKA au KUMKIRI/KUMWAMINI KRISTO?? Hiki ndicho mnakichanganya na hamtaki kuelewa. KUOKOKA na KUMWAMINI/KUMKIRI KRISTO, hivi ni vitu viwili tofauti japo kuokoka, kunategemea kuamini kwanza. Kumkiri Kristo, ndiyo hatua ya kwanza kabisa ya wokovu. Hatua ya pili ni safari ya imani hiyo/kumkiri huko. Hatua ya mwisho, ndio huo utimilifu wa wokovu –yaani kutolewa duniani, kutolewa kwenye mazingira ya dhambi japo sisi tunaweza kufikia hatua ya kutokuwa na dhambi. Haina maana tunapofikia hatua ya kutokuwa na dhambi, tunakuwa tumeokoka; isipokuwa, tutakuwa tumefikia hatua ya ukamilifu tu tukiwa na asilimia 100 za kumgonja Kristo atukaribishe nyumbani kwake kusikokuwa na dhambi, siku atakaporudi. Kristo alikuja kutengeneza njia/daraja la kututoa kwenye dunia ya dhambi na kutupeleka sehemu isiyo na dhambi. Na hii ndiyo maana ya jina lake. Na hili huwezi kulielewa vyema, ni mpaka umekaa chini ukamlilia Mungu akuongoze kwenye uelewa sahihi wa somo maalumu liitwalo – KUHESABIWA HAKI KWA IMANI, ndani ya Biblia. Kuna kuwa redeemed na baadaye kuwa Saved!! Jifunze zaidi!!
  Kuna haja kubwa ya ninyi rafiki zangu kujifunza maana ya KUPONYWA na KUOKOKA. Abimeleki hakuokolewa, isipokuwa aliponywa!! Tafsiri nyingi za kiingerezazimetumia maneno “ReDEemed” na “SaVEd”. Ili uelewe, huna haja ya kwenda kusoma theolojia. Wewe chukua hata kamusi tu, zitakusaidia kuelewa. Huwezi ukawa unachanganya mambo rahisi kiasi hiki, kama unavyosema hapa “Mkristo anapojazwa RM ndipo wokovu wake huwa kamili. Yaani RM anapojaa ndani ya moyo wako, hapo ndipo yule mtu wa ndani hukamilika.”
  Haya ni maelezo ya upotovu kabisa!! Nayaita ya kipotovu kwa sababu yanampumbaza mtu asiwe na lolote la kujishughulisha hasa kwenu ninyi marafiki zangu mnaonena kwa lugha zisizoeleweka hata kwa ninyi wenyewe kwa kisingizio cha kujazwa RM!!! Lwembe, mtu anapojazwa RM, ukamilifu wa wokovu kwake huwa bado, japo katika safari ya imani, huwa ni mtu aliyepiga hatua kubwa kiimani-kuukulia wokovu. Wokovu kwake mtu huyo, alishauanza mchakato tu lakini ukamilifu BADO!! Hayuko salama huyo bado!! Anaweza kuugua, anaweza kuteswa na mikono ya ibilisi, kufa au kuuliwa kama tunavyoona kwa Mitume baada ya pentekoste!! Pamoja na kujazwa RM, bado waliendelea kukamilishwa ktk Kristo. Soma historia za utumishi wao vizuri. Walipokamilika (walipogongwa mhuri wa Mungu), wengi wao walilala na tumaini, naam baadhi yao (kama Paulo) walidiriki kutangaza kuwa “Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake” – 2 tim 4:7-8. Kaka Lwembe (Sungura na wengine, ambao naamini kuwa mnasoma hii pia), pamoja na jitihada hizi zote za mitume, bado walibakiza ngwe moja ya WOKOVU – kunyakuliwa (au kuondolewa duniani).

  Kama ni habari za kuponywa, mitume waliponywa sana. Baadhi yao Mungu aliwaponya kimiujiza mno tena mbashala(live) kabisa. Mf. Yohana. Kama angekuwa Lwembe na Sungura, mngesema Yohana aliokoka!!! Fanatics!! Wapendwa, duniani, tunamwamini/kumkiri Kristo, tunakamilishwa, na hatimaye, tunaokolewa kutoka duniani. Kuokolewa ni hatua ya mwisho ya wokovu, baada ya hizo mbili za mwanzo. Nayo (kuokolewa), haiwezi kuja kwetu halafu bado tukaendelea kuwepo hapahapa duniani!! Hatuwezi kubaki tunaimba kuwa haya ni mambo ya rohoni peke yake kana kwamba hakuna kilichofunuliwa kwetu!! Mambo ya rohoni, hayapingani na neno la Mungu. Yale yanayodaiwa kuwa ni ya rohoni lakini huwezi kuyapata popote ndani ya Biblia, huo ni uchawi na mazingaombwe yaliyovikwa vazi la kikristo. Mtu yeyote akikufundisheni hivyo, jueni kuwa hiyo ni Luciferian doctrine!! Hakuna udini hapo, usidanganyike!
  Naona unanichangamsha, ngoja nizidi kukuchangamsha na wewe pia!!

  Kuhusu suala la sabato; kimsingi umesema vizuri. Hata mimi sifundishi sabato kama inavyofundishwa na baadhi ya wasabato. Samahanini wasabato wenzangu mnaosoma hii!! Huwa najitahidi kuionesha Sabato kwa mujibu wa Biblia peke yake. Ukienda kwa baadhi ya wasabato, sabato huwa wanaisimplify sana kana kwamba, ni kitu kinachotunzwa kutegemeana na mazingira ya mtu!! Baadhi yao (wachache sana) nimewasikia kwa masikio yangu wakipotosha ukweli huo. Amri za Mungu, Neno la Mungu huhitaji utii bila ya kuangalia mazingira! Mungu aliposema, ‘usizini’, hakuna sababu za mazingira zitakazokufanya uzini halafu uwe na kisingizio cha kipuuzi kiasi hicho. Hali kadhalika na kwa sheria zingine zote. Hivyo kaka Lwembe, watu wengine huniita falisayo, japo siko kwenye ufalisayo hata kidogo. Siku zote nitasimama kwenye kile kifundishwacho na Biblia na si dhehebu!! Kwa hiyo, usiwe na wasiwasi Lwembe kwa hili na mengine ambayo huwa tunajadili. Niko Bible based tu.

  Aidha, mimi nilitarajia kuwa ungenipatia utondoti yakinifu unaojibu maswali yangu niliyokuulizeni siku ile. Naona umejaribu kubabia tu hapa. Sasa kama siku zile za mwanzo hazifanani na zile zingine, je, una ushahidi wa kibiblia kuthibitisha tofauti hiyo au ni mawazo yako tu? Kwa Wakristo tulio wengi, tunaamini kuwa Yesu ndiye aliyeumba vyote. Au siyo? Kama ni kweli, je alikosea hata YEYE aliposema, “
  Je! Saa za mchana si kumi na mbili- Yoh. 11:9? Au Mungu alipowaambia Israel kufanya kazi kwa muda wa siku 6 na ya 7 ni Sabato(kutoka 20:8-11), alimaanisha nini? Sabato zilipofika, na manna isishuke kutoka mbinguni, ilikuwa ni baada ya miaka elfu sitasita? Au unataka tena nikupatie saa za usiku? Hebu jaribu kuangalia aya nyingi zinazoonesha ufanano wa saa za mchana na usiku ndani ya Biblia.

  Na kama Sabato haina “ikawa jioni, ikawa asubuhi siku ya saba”, je unataka tukae tustarehe tuuu siku zoote baada ya siku sita kwa sababu hiyo? Kama Yesu na YEYE (aliye muumbaji wa vyote), angekuwa na nadharia tete uliyonayo hiyo, huoni kuwa angewasaidia wayahudi kwenye utunzaji wa sabato ili kuunga mkono hoja yako ya utunzaji wa sabato? Kwa nini na yeye alifanya vilevile kama alivyofanya wakati wa agano la kale? Na kama siku ya Saba haina majira kama zilivyo siku ya kwanza, pili na ya tatu, je huoni kuwa kuziita majina siku hizi sawa na majina ya siku zingine zenye majira, ni kukiuka maandiko sasa? Una ushahidi wa Kibiblia, kulithibitisha hilo ili na mimi nijifunze kwako? Nami nakutia moyo usilete udini kwenye suala la Sabato. Liko wazi mno kaka. Acha kabisa hadithi zako za Eva kulala (kula tunda) na nyoka hapa!!!

  Niko makini sana na dini!! Nikipotea, nitakuwa nimeamua mwenyewe tu.
  Ndiyo maana nimeamua kubaki na Mungu. Kubaki na sauti yake tu.

  Nawaombea nyote! Siku ipo, Mungu atawafungua.

  Siyi

 105. Siyi inaendlea …

  Ona biblia inchosema:

  2Tim1:9 -12 Ambaye Alituokoa akatuita kwa mwito mtakatifu, …
  – Inasema alituokoa, Siyi anasema hatujaokoka!

  *Tito3:4-5 Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, Alituokoa; si kwa sababu ya matendo ya haki ….
  – Inasema alituokoa ,Siyi anasema hatujaokoka

  Efeso 2: 8 -Kwa maana Mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; …
  – Inasema tumeokolewa kwa Neema, Siyi anasema hatujaokoka!

  Siyi mpaka hapo unataka nikuiteje kama si mjinga?

  Swali lako la kwanza: Maelezo yangu yamekujibu kuwa akija haji kutoa watu dhambini bali kuwatoa duniani watu aliokwisha kuwatoa utumwani mwa shetani, maana kuishi duniani (planet earth) siyo maana yake kuwa utumwani mwa shetani au dhambini.

  Swali lako la pili: Uhusiano wa unyakuo na kifo cha kristo upo. Na uko hivi; kifo cha kristo ndo kilichowatoa utumwani mwa shetani ( ulimwengu wa giza) wale ambao kristo atakuja kuwanyakua ( na hao ndo waliokolewa kwa neema, huko kutolewa utumwani mwa shetani)

  Ndio maana nilikuambia kuwa hii mada umeingilia tu ilikuwa haikuhusu, maana badala ya kujadili suala la kma mtu anaweza akapoteza wokovu wake, umetulazimisha tujadili suala la kama mtu anaweza kuokoka duniani, wakati hiyo mada tulishaijadili sana.

  Nakuona pia kingine kinachokupa shida ni suala la uhusiano wa mtu aliyeokokoka kuwa na dhambi. Na hilo nalo kwa vile unatafuta mantiki yake kwa mtazamo wa kiakili unajikuta umekwama kabisa kuelewa.
  Ngoja leo nisiliongelee kwanza hilo.

  Biblia imesema tumeokoka, hivyo nasi twakiri hivyo!

 106. Siyi,

  Maneno kama haya ya mimi naelekea kuzimu hata tusiyapotezee muda kujibizana, na sioni shida kwenda kuzimu kama Mungu atanituma huko, wewe wala usipate shida.

  Ni kweli tupu kuwa huwa siendi kanisani kutubu, ila wewe ndio huenda kanisani kutubu (old testament concept). Kama kwa kufanya kwangu hivyo unadhani kuwa huwa nakosea, just nioneshe ni wapi mitume wanatufundisha kuwa tukitaka kutubu twende kanisani.

  Unajua ulivyo mjinga japo unadhani u mwerevu, huoni tofauti ya kutbu na kwenda kanisani. Hata hiyo sala aliyowafundisha Yesu wanafunzi wake hakuwaambia wawe wanaenda kanisani kuisali.

  Hasira hukaa kifuani pa mpumbavu, mimi siyo miongoni mwa hao wapumbavu ambao wanabeba hasira kutoka walipo hadi kanisani ili wakatubu huko.

  Hebu niambie leo umetenda dhambi ngapi, na je unasubiri mpaka kesho au Jumatano ifike ukienda kanisani ndo ukazitubu?

  Kama una akili nzuri ya kufikiri nadhani mpaka hapo utakuwa umeelewa kuwa huwa hatuendi kanisani kutubu.

  Ask God to have mercy on u not me, nafikiri hayo majibu yangu kuhusu suala la kwenda kanisani kutubu yanakutosha, sihitaji hata kujibu kila neno jepesi ulilojaza katika hiyo paragrafu.

  Na leo ngoja nikuulize swali jepesi, shida unayopata ni ipi kuhusu cc na kuokoka, je ni kule kukiri kwetu kuwa tumeokoka, au ni kule sisi kuwa si wasabato/tusiosali J’mosi?
  Unadhani tukiacha kukiri kuwa tumeokoka ndo tutakuwa hatujaokoka?

  Maana nakuona badala ya kuzama kwenye kuongelea ni kwa jinsi gani haiwezekani kuokoka ukiwa duniani (kama ambavyo wewe unaamini), unazama kwenye kutushambulia sisi kule kukiri kwetu kuwa tumeokoka.

  Siyi hata kama hutaki kujifunza, lakini lazima nikwambie tena na tena kuwa Yesu akija haji kuokoa wadhambi, hiyo kazi alishaifanya. Akija anakuja kuchukua walioukubali wakovu. Tatizo kubwa ambalo litakutesa sana ni ideology mbaya uliyonayo kuhusu nini maana ya kuokoka.

  Ivi Siyi unataka tukuamini wewe na mawazo yako au tuamini ambacho biblia inasema? Biblia inasema Israel waliokoka kwa kile kitendo cha kutolewa Misri, wewe unasema huo siyo wokovu wakati biblia inasema huo ulikuwa wokovu, na ndo Sodzo yenyewe.
  .p.t. o

 107. Siyi,

  Kuhusu sabato ndg yangu jitahidi ktk ufahamu, hapa hatuzungumzii mafundisho ya kisabato au ya kikatoliki au ya kilokole nk bali tunazungumzia kile Biblia inachokifunua ktk kutufundisha hii mila na desturi mpya. Ndipo kutoka hilo, yapime mafundisho ya dhehebu lako kuona kama yako sawa na hicho. Hayo ndio Maarifa!!!

  Nilikuambia kuhusu hiyo siku moja ya Mungu kuwa ni sawa na miaka elfu, si kwamba hilo ni korokoro langu, hapana, hilo ni Neno la Mungu “Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja.” (‭2 PET.‬ ‭3‬:‭8‬)

  Ukijaribu kulichanganya Andiko hili na mafundisho yenu kuhusu sabato, utaishia kuchanganyikiwa kama ninavyokuona! Kila utakapozihesabu hizo siku za Mungu ili uzioanishe na sabato yenu mliyojitengenezea, ni sawa na kulitia maji gari la petroli! Uongo huwa haufiki mbali, mwisho wake ni kuyakataa Maandiko ili kuficha aibu na hivyo kuendelea kujishusha chini zaidi ndani ya lile shimo reeeefu!

  Pia, ukizitama kwa makini siku hizo saba za uumbaji, utaona kwamba hata siku zenyewe pia zimeumbwa! Na katika kuumbwa kwake hazifanani! Zile siku tatu za mwanzo Mungu alizitenganisha kwa Nuru na Giza. Kwahiyo hauwezi ukazileta katika kipimo cha masaa 24 ziwe sawa na hizi tatu ambazo zimetenganishwa kwa mianga ya jua na mwezi kufanya mchana na usiku.
  “Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza. Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja.” (‭MWA.‬ ‭1‬:‭3-5‬ SUV)

  Ktk siku ya nne ndipo jua linakuja:
  “Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndiyo dalili na majira na siku na miaka; (‭MWA.‬ ‭1‬:‭14‬ SUV)
  Unaona? Hizi siku haziko sawa!!!!

  Haya, Sabato ndio kabisaaaaaa; haina ikawa jioni wala asubuhi ni back into eternity! Hapa ndipo unapopaswa usikilize vizuri ili uelewe tunakuambia nini.

  Mungu si kiumbe cha wakati, yeye ni wa milele yaani Eternal, asiye na Mwanzo wala Mwisho, kama mchoro wa duara ulio kamilika, hauwezi ukapaona ulipoanzia wala kuishia! Katika zile siku sita alizofanya kazi, ina maana alijiondoa katika mzunguko huo yaani aliukata ndipo akauingiza wakati; kama vile Kristo alivyozaliwa na kuyatimiza yote yaliyompasa katika wakati uliopangwa, na akiisha kumaliza akasema “anarudi” kwa babaye huko ktk Eternity! Basi ktk siku ya saba, Mungu asingepumzika kama mwanadamu aliye kiumbe cha wakati, yeye alirudi ktk Eternity ktk siku hiyo ya saba, ndio maana haina majira!!! Naye mkristo aliyezaliwa mara pili huingia huko aliko Mungu, ktk hiyo Sabato, ndipo mahangaiko ya kumtafuta Mungu kwake hukoma, maana yuko naye fulltime hana mchana wala usiku! Unamuona yule mtu wa rohoni mambo yake? Huyo ndiye mwenye kumuabudu Mungu, maana saa zote yupo naye hapo, Mungu alishuka mpaka huku chini kumtafuta, “Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.” (‭YN.‬ ‭4‬:‭23‬ SUV)

  Unatafutwa Siyi, fungua macho hayo, uyaone mambo matamu ya wokovu!

  Dini si mchezo kaka, zinaweza kukutia uzezeta wa kiroho usioutegemea, ukabaki unafunga kwa komeo banda la kuku wakati mwemwe kisha ondoka nao wooooote!!!!!!

  “Sabato” njema!

 108. Siyi,
  (Ninaendelea…)

  Labda pia utakuwa huijui sawa sawa hata hali ya mwokovu, kwamba ni vipi haswa anakuwa Ameokoka hapa duniani, haswa huu upande wa pili, yaani huku Agano Jipya? Mkristo anapojazwa RM ndipo wokovu wake huwa kamili. Yaani RM anapojaa ndani ya moyo wako, hapo ndipo yule mtu wa ndani hukamilika. Huyu unayemuona mmoja huwa ni wawili, mmoja wa duniani, huyo wa kufa; na mwingine wa mbinguni, wa kuishi, huyu aliyezaliwa kwa Roho wa Mungu. Amina! Akiwa ktk mwili wake huyo atakufa; lakini ktk nafsi yake yeye amevuka mauti na kuingia Uzimani. Akiwa ktk mwili wake wa nyama, ana mawasiliano na dunia kwa zile hisi tano; kuona, kunusa, kugusa, kusikia na kuonja; katika roho ana mawasiliano na Mungu kupitia RM.

  Malaika wa Mungu huwatembelea na kuongea nao, wakiwa wametumwa na Mungu ili kuwafunulia yaliyofungwa, na kuwaletea ujumbe kutoka kwa Mungu, kama unavyomuona Danieli au Paulo mtume nk. Hivi ndivyo mambo yalivyo ktk Ufalme wa Mungu, kile kipeo cha Wokovu wetu.

  Kimsingi jambo la wokovu ni la rohoni ambalo hudhihirika ktk mwili, hapo tunaposherekea Ushindi tulioupata huko rohoni. Nao Ushindi hudhihirisha “Nguvu” tulizonazo. Nazo Nguvu zote, ziwe za kichawi, au uganga, au za dini kama hizi zinazokushikilia, na hata Nguvu za Mungu, zote hupatikana ktk ulimwengu wa roho. Na kuingia katika ulimwengu huo, ni lazima uwe initiated, yaani ufunzwe, sawa na kuingizwa jandoni au kufundwa, kulingana na milki unayoingizwa! Nao wokovu maana yake ni kuingizwa ktk ulimwengu wa roho ktk Kristo Yesu aliye Mshindi, ndio maana sisi huukiri ushindi huo tulionao ktk ulimwengu huo ambao wewe Siyi hujauingia, wewe bado uko hapa chini ukitumikishwa na dini, maana mwenye nguvu hutawala kulingana na mipaka ya milki yake, hata dini!

  Basi, Injili unayohubiriwa, ndiyo “Nguvu” pekee iwezayo kukutoa humo ulimoshikiliwa na hizo nguvu za dini, zikiyatawala maisha yako kinyume na mapenzi ya Mungu. Injili ni ya rohoni, humo ndani yake ndimo ilimohifadhiwa Nguvu ya Mungu, Efe 3:8-10 “… nalipewa neema hii ya kuwahubiri Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika; na kuwaangaza watu wote wajue habari za madaraka ya siri hiyo, ambayo tangu zamani zote ilisitirika katika Mungu aliyeviumba vitu vyote; ili sasa, kwa njia ya kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho.”

  Umeiona Nguvu ya Mungu iliyokabidhiwa Kanisa kupitia Injili ya Kristo? “… Amka, wewe usinziaye, Ufufuke katika wafu, Na Kristo atakuangaza.” Efe 5:14

  “Nguvu” ndg yangu hutumika ktk kuyabadili mazingira hapo inapolazimu. Mazingira ya dunia baada ya Anguko, iligubikwa na dhambi, yaani mauti, chini ya utawala wa Shetani, ndio hizo falme na mamlaka, na wakuu wa giza, na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho; unaona, wanaitawala dunia kutoka ktk ulimwengu wa roho! Kwahiyo huwezi kuipindua mamlaka hiyo ya mauti ukiwa ktk ulimwengu huu wa mwili, huu unafaa kwa dini tu ambazo hukuingiza ktk hisia za utakatifu kwa kukufanya kuwa mwenye mfano wa utauwa, usio na “Nguvu” ya kulibadilisha jambo lolote lile, kwani “nguvu” ya mauti ni hodari wa kushikilia watu!

  Basi, kama nilivyowahi kukuambia, kwamba ni katika wokovu ndipo tunaposajiliwa kuipigania Imani, vita hivi vinapiganiwa huko ktk ulimwengu wa roho, ni vita vya kiroho. Nasi tukiwa na hiyo Silaha komesha, ule Upanga wa Roho, ambao ni Neno la Mungu, ambaye ndiye Kristo; naye akiisha “… kuwapokonya nguvu zao hao pepo watawala na wakuu; aliwafanya kuwa kitu cha fedheha hadharani kwa kuwaburuta kama mateka katika msafara wa ushindi wake” (Kol‬ ‭2‬:‭15‬) [“And having spoiled principalities and powers, he made a shew of them openly, triumphing over them in it.”]; Je, bado tu hauoni ni kwanini tunasherekea Ushindi tukingali vitani???

  Changamka kaka!!!

  Juu ya korokoro la sabato, nitali explain punde tu, vuta subira!

  Gbu!

 109. Siyi,

  “Kwa kuwa BWANA awaridhia watu wake, Huwapamba wenye upole kwa wokovu.” (‭ZAB.‬ ‭149‬:‭4‬)

  Inashangaza sana jinsi ambavyo unashindwa kuuona wokovu tulioletewa hapa duniani, wakati maelezo yake yamejaa Biblia nzima, yaani almost kila Andiko utakalolichukua linazungumzia jambo hilo!

  Narudia tena, yale “makorokoro” niliyoyajaza kichwani mwangu; kwamba unakuwa ni huyo aliyeokoka, hapo unapokuwa Umehesabiwa Haki, kisha Ukatakaswa, na mwisho Ukatukuzwa – huko Kujazwa RM, yaani kuwa “Sealed In” (The Kingdom of God), ukiifikia hatua hii, Mungu huwajibika mpaka kwa mapungufu yako, maana wewe ni subject wa Ufalme wake; hii ndiyo Habari Njema ya wokovu!!!

  Nilikuonesha mfano wa Daudi, lakini hukuambulia chochote, haya, mtazame na huyu mwingine aliye sehemu ya hili korokoro ninalokuhadithia, huyo aliye kivuli chetu, ilivyokuwa kwake alipoingia ktk mapungufu, Mwa ‭20‬:‭1-18‬:
  “Ibrahimu akaondoka huko kwenda nchi ya kusini, akakaa kati ya Kadeshi na Shuri, naye akatembea katika Gerari. Ibrahimu akamnena Sara mkewe, Huyu ni ndugu yangu. Basi Abimeleki mfalme wa Gerari akapeleka watu akamtwaa Sara. Lakini Mungu akamjia Abimeleki katika ndoto ya usiku, akamwambia, Umekuwa mfu wewe kwa sababu ya mwanamke huyu uliyemtwaa, maana ni mkewe mtu. Basi Abimeleki alikuwa hakumkaribia, akasema, Ee Bwana, Je! Utaua hata taifa lenye haki? Je! Hakuniambia mwenyewe, Huyu ni ndugu yangu? Na mwanamke mwenyewe naye alisema, Huyu ni ndugu yangu. Kwa ukamilifu wa moyo wangu, na kwa kuwa safi mikono yangu, nimefanya hivi. Mungu akamwambia katika ndoto, Nami nimejua ya kwamba kwa ukamilifu wa moyo wako umefanya hivi, ndipo nami nikakuzuia usinitendee dhambi, kwa hiyo sikukuacha umguse. Basi sasa umrudishe mwanamke kwa mtu huyo, maana yeye ni nabii, naye atakuombea, upate kuishi. Bali usipomrudisha, fahamu ya kwamba kwa hakika utakufa wewe na watu wote ulio nao.”

  Unauona Wokovu ulivyo mtamu Siyi? Hakuna Hukumu juu yao waliompokea Kristo! Oh, sijui mimi nafuata Amri ya Nne kama alivyotufundisha nabii wako Ellen; jibu ni kama lile la kwa Abimeleki, Nenda kwa Petro mtumishi wangu akakuombee, akubatize kwa jina la Bwana Yesu Kristo upate Ondoleo la dhambi zako upate kuishi, vinginevyo fahamu kwa hakika umepotea!

  Kwanini iko hivi, Mungu amelifanya jambo hili kuwa hivyo kutokana na Thamani ya Damu ya Mwanae, iliyoulipia udhaifu wangu kabla hata sijautenda, na hivyo kwa Neema kunirejeshea utakatifu nilioupoteza! Hii ndiyo Siri ya Wokovu, ambayo Shetani haijui.

  “Ibrahimu akamwomba Mungu, Mungu akamponya Abimeleki …”!
  Bado unayo nafasi ya kuokoka na Hukumu iliyo mbele yako, kama utajishusha na kuwa mwenye upole ili BWANA akupambe kwa wokovu!

  Ngoja nipose hapa kidogo, uyatafakari hayo, kisha nikuunganishie na hicho kipande kilichobakia!

 110. Sungura,
  Bwana akubariki sana. Hata mimi huwa najitahidi tu kukujibu, lakini kimsingi, unachosha. Mbaya zaidi, unafikiri unaelewa sahihi habari za wokovu kumbe unaelekea kuzimu tu. Na unataka kukokota hata watu wengine waelekee kuzimu huko unakoenda wewe!! Nami kama kazi yangu ilivyo (kuweka wazi uongo wa ibilisi uliofunikwa kwa vazi la kikristo), sitaona haya kukushughulikia hadi pumzi yangu ya mwisho. Mungu nisadide!!
  Kama kweli wewe ni mkristo unayetaka kwenda mbinguni, huwezi kusema haya “Kwanza nataka ujue kuwa siendagi kanisani kutubu mimi, hiyo huwa mnafanya ninyi ambao hamjui mnachofanya, but bado mnapapasa”.
  Sasa wewe ukiudhiwa na mtu yeyote, kwa vile hasira nayo tu ni sawa na uuaji mbele za Mungu, huwa unafanyeje rafiki at the end? Je, hata Yesu naye alipowafundisha mitume wake namna ya kusali akisema, “utusamehe makosa yetu kama na sisi tuwasamehevyo wanaotukosea…”, alikosea? Kama dhambi huishia pale mtu anapomwamini Yesu, je, wakati Yesu anawafundisha hayo wanafunzi wake, walikuwa bado hawajamwamini? Sungura, usipoangalia, utapotea kwa kujifanya kichwa ngumu!! Maana kama hutubu, ina maana dhambi kama hizo zinakaa!! No repent, no remission of sins!! Kwa hiyo wewe, una dhambi zisizotubiwa! Na unataka watu wakufuate na imani ya ajabu kiasi hiki, hakika yake nyote mtatumbukia shimoni!! Oh God, have mercy on Sungura! Tusaidie sote, tuamke usingizini! Maana ibilisi yuko kazini! Bila ya msaada wako, Siyi, Sungura, Lwembe, Seleli, Mary, Tumaini, Mjema, Mabinza, Mhina, Milinga, Deo, Yusha, Magreth, Ziragora, Ditu na wengine wengi, tutapotea!! Ee, Mungu tusaidie!
  Kama bado unashikilia msimamo tenge wa kuokoka ukiwa duniani, wewe endelea nao!! Lakini ujue kuwa, hakuna usalama hapo. Dhana ya kuokoka ukiwa hapa duniani, ndiyo hii inayowafanya mtamke hadharani kuwa hamna dhambi! Hamtubu dhambi! So, kwa maneno mengine, hamumhitaji Kristo anayekuja kuokoa wadhambi! Maana ninyi siyo wadhambi! Na Kristo anakuja kwa wadhambi. Tayari ninyi ni kundi na lile linalomgonja Kristo. Na kama wewe kwa sasa si mkosaji, mdhambi n,k, nakupa pole maana Kristo (Yule mwokozi) haji kwa ajili yako. Labda kama una kristo mwingine rafiki! Na inavyoonekana, wewe unaelewa kuwa, mchakato wa wokovu wa Kristo uliishia msalabani! Nami ngoja nikuulize maswali ya kichokozi japo huna tabia ya kujibu;
  1. Kama Kristo kwa kufa msalabani aliwaokoa watu(aliwaweka salama), kwa nini atakuja kuwaokoa watu walio salama? Je, falsafa ya mtu mzima kuhitaji tabibu, wewe umeipata wapi? Au wapi ulishaona aliye salama anapewa msaada?anaokolewa?
  2. Je, kifo cha Kristo, hakina sehemu yoyote kwenye unyakuo(japo siyo wa siri) wa kanisa lake?
  Nilijua tu kuwa sehemu hii (ya mavazi yasiyofaa, pete, nywele nk) ungeleta hoja. Nashangaa kuniambia nithibitishe japo naongelea wasabato wenzangu!! Usishangae! Ni wasabato tena baadhi tu (wale vichwa ngumu kama wewe), niliowatolea mfano japo sikumaanisha kwa wasabato peke yao. Narudia tena kusema, hata kama wewe ni msabato usiyeenenda sawasawa na Biblia (msabato jina), mapachiko yangu yanakuhusu pia kama wale waj2. Tujitahidi kufanya matengenezo ya dhati, vinginevyo, tutaishia kuitwa wasabato tu.
  Sungura, kuhusu hoja hii ya mavazi na mapambo, rejea mazungumzo yangu ya Lwembe juu ya nywele. Lwembe si msabato. Na hoja ilimgusa. Mpaka leo kama hajafanya matengenezo, anahitaji msaada mwingine tu. Kama na wewe unahitaji kupona juu ya ufidhuli ulioingia ndani ya ukristo, nitakupatia tu. Na wewe jiandae kunieleza kwa nini unafikiri kuwa ni sahihi kuendeleza dhambi za kuvaa vimini, kata K, suruali kwa akina mama, pete n.k.? Na tutaomba ukurasa mpya wa mada kwenye blog ili uwe tofauti na mada hii. Get ready!
  Sungura, sidhani kama kweli ni mimi ambaye sina umakini au ni wewe mwenyewe!! Suala la mtu kumkiri na kumkana Kristo, tulishalijadili zamani kama ilivyo dhana ya wokovu (fasili yake). Nashangaa tena kukuona unataka nijadili/niseme chochote tena on the same thing. Sijui, huenda sijalielewa swali, unataka nini hasa!! Waweza kuliuza kwa namna nyingine ili nami nipate kukuelewa unataka nifanye nini zaidi ya kile nilichokwisha kukifanya huko nyuma.
  Swali la Israel kuwa waliokoka ama la!! Nafikiri litakuwa ni swali lenye jibu zuri la kukusaidia uelewe kama uko sahihi na msimamo wako huo wa kuokoka mtu akiwa duniani!!
  Kwanza, ngoja niseme kuwa Israel kutolewa Misri –waliokoka (japo sikubaliani na dhana hii); kwa ajili ya kukusaidia uelewe. Twende kazi…
  Kama Israel waliokoka rafiki, walitolewa kwenye ibada za sanamu za Misri na kuitwa kwenda kumwabudu Mungu pekee, ni akina nani waliofika mlimani wakatengeneza ndama wa shaba? Unakubuka ni mara ngapi Israel walimnung’unikia Musa na Mungu? Ni mara ngapi Mungu aliwatia miononi mwa maadui pindi uasi wao ulipozidi? Je, walipomrudia kwa kulia, kufunga na kuomba –kutubu, Mungu hakuwasikia? Safari ya kwenda Kanaani kutokea Misri, ilikuwa ya siku ngapi? Kwa nini walidumu jangwani kwa miaka yote 40? Na kama hiyo haitoshi, Kanaani walifika watu wangapi waliotoka Misri? Kwa nini? Kama waliokoka, (hawakuwa na dhambi tena) ilikuwaje wakafanya hayo yote?
  Sungura, mawazo ya sisi tumeokoka kama waisrel kutolewa Misri-Kanaani ndiyo mliyo nayo mlio wengi!! Na isivyo bahati, mmesahamu kuwa, wokovu wenu bado haujakamilika maana hamjaivuka bahari ya shamu, jangwa, milima na maadui njiani. Na hii ndiyo kazi ya ibilisi- kutupotosha yumkini hata wateule. Mara nyingi tumedanganika kuwa tumeshaokolewa, hatuna dhambi, n.k., hivyo hatuna haja ya kufanya lolote–(kuendelea na safari ya kiimani). Na akina Siyi wakiwaambia, wanaonekana kuwa ni wapuuzi, wajinga, maamuma, washenzi na wasio na akili timamu!
  Kristo anatushangaa sana kila siku tunapojidai kuwa hatuna dhambi. Ni ajabu sana tunapokuwa wanafiki mbele zake bila ya hiana. Rehema na neema yake, bado vinatungoja. Sauti yake bado inaendelea kusikika ikisema, “Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu. Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi. Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona. Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu. Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi. Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa” – Ufunuo 3:15-22.
  Siyi

 111. Siyi,

  Ivi wewe lini ujinga utaisha akilini mwako? Umeongea maneno mengiiiii ya kitoto na yenye kuchefua. Ivi uliamua kuandika kile ambacho wewe unafikir tu au?
  Inahitaji uvumilivu mkubwa sana hata kutumia huu muda wangu kukujibu. Lakini nilishakwambia kuwa siko hapa kukulazimisha kuokoka hiyo si kazi yangu. Ila niko hapa kuhakikisha kuwa sikuachi ukapotosha kweli ya Kristo kwa kule kuamini kwako fundisho la uongo.

  Kwanza nataka ujue kuwa siendagi kanisani kutubu mimi, hiyo huwa mnafanya ninyi ambao hamjui mnachofanya, but bado mnapapasa.

  Wewe hata ukiamua kusema kabisa wazi kwamba unatutukana tuliooka, hainipi shida yoyote, lakini cha msingi unachotakiwa kufanya ni kuthibitisha kuwa hakuna kuokoka hapa na utuambie tunaenda kuokokea wapi.

  Na sioni sababu kwa nini nikae narudia kukwambia kitu kilekile. Wewe ni mjinga tu kama mjinga mwingine ambaye haijui siri ya kristo ila anajua tu maandiko pasipo kujua kweli iliyo ndani ya hayo maandiko.
  Ungekuwa na akili timamu usingeendela kulazimisha kuwa maana ya kuokoka ni kutolewa duniani. Na kama hiyo ndo ingekuwa maana yake basi Yesu kama jina lake lilivyo, kwamba ni mwokozi angeshatuondoa hapa duniani, maana kazi ya kuokoa alishaimaliza akaenda na kuandaa makao. Sijui unaposema anakuja tena kuokoa ni lini hiyo, maana harudi tena msalabani. Safari yake inayofuata anakuja kunyakua/kuchukua kanisa.

  Maneno kama haya si yanatoka kwenye moyo wa mtu aliyejaa ujinga wa kweli ya Mungu ndani yake! Ona ‘’ Wameendelea ktk uasi wakilivunja neno la Mungu (k.v. kuvaa vimini, kuvaa pete, kusuka na kukari nywele, kuvaa vibode, kuvaa suruali n.k.) wakifikiri kuwa, kumwamini Yesu tu yatosha!”
  Unachotaka kuniambia hapo ni kwamba kuvaa vimini, kuvaa pete,n.k ni dhambi. Just prove it! (japokuwa unaongelea wasabato wenzio)

  Siyi kadri ambavyo nimezidi kusoma makala yako nazidi kuona tu kwamba umeongea maneno mengi ya kipuuzi ili kujificha tutoke kwenye mantiki nzima ya mada. Kwa hiyo nimeamua kufupisha hivi: kabla sijakujibu maswali ambayo uneniuliza, shughulika kwanza na hili ambalo nililiweka wazi sana kwako.
  Najinukuu ‘’ Tena kwa kukupa majibu direct to the topic, ni kwamba mtu aliyeokoka anaweza akaupoteza wokovu.

  Kumkiri Yesu ni hiari ya mtu na kumkana ni hiari ya mtu. Maana kama kwa kumkiri na kumwamini mtu anapata wokovu na kwa kumkana na kutomwamini mtu anapoteza wokovu ’’
  Na jingine hili hapa nilikuuliza lakini kwa sababu ya kukosa umakini umeandika ukurasa mreeefu ukilazimisha kujibu comments zangu zote ndani ya comment moja. Hiyo nayo ni aina fulani mbovu sana uandishi.

  Hili hapa ‘’ Kwani Israel hawakuokolewa Misri, au hicho kitendo cha kutolewa kwao Misri kilikuwa nini kama siyo wokovu, justification au?

  Please jibu haya mambo ili mjadala tuupeleka kama watu wenye akili timamu!
  Lakini kitu ambacho kinanichefua sana juu yako Siyi ni vile unavyoongea vitu vingine kana kwamba ndo tunaanza kuvijadili wakati tuanelekea au tumetimza mwaka kabisa tulishavichambua. Kwa mfano: tulichukua muda mwingi sana kuchambua maana ya neon KUOKOKA kutoka kwenye neon SODZO na SOTERIA, Lkini ulivyo mtu wa ajabu bado unatulazimisha turudi kwenye jambo hilohilo. Ndo maana niliwahi kuwaambieni kuwa mnaongea maneno yaleyale kwa style zilezile.

  Anyway, shughulikia hivyo vitu viwili hapo juu kwanza!

 112. Lwembe,
  Duuu!! Na wewe rafiki yangu, una makorokoro kweli umeyajaza kwenye kichwa chako. Kwan unataka kuniambia kuwa juma moja la uumbaji ilikuwa ni miaka elfu 7?? Can you prove that bro?? Kama Sabato ni baada ya miaka elf 6 then elfu 7 ndiyo Sabato, je, wale wote walioishi katika agano la kale na tukawaona wanatunza Sabato, walitunza sabato za miaka elfu 7? Je, hata Yesu naye alitunza Sabato ya miaka elfu 7? Zingatia aliishi duniani kwa miaka isiyozidi 34!! Na una uhakika kuwa hakuna aya inayosema kuwa Mungu hupumzika kila sabato? Ukiuchanganya unabii na literal meanings, utaishia hewa rafiki!!
  Sabato haijaanzia jangwani rafiki yangu. Sabato ilianzia bustanini Edeni. Vizazi vyote vya Adamu, vilitunza Sabato. Mpaka kufikia kwa Ibrahimu (myahudi kwa kwanza), hata kabla ya kizazi chake (vitukuu vyake) kupelekwa utumwani, Sabato ilitunzwa. Ndiyo maana leo, kile Wayahudi walichopewa na Mungu ili kukifiksha kwa mataifa mengine, sherti tukifanye, vinginevyo tutapotea tu maana wokovu unatoka kwa wayahudi kaka.

  Hoja ya kuokoka, angalia utakinzana na Sungura japo anaweza asikuambie hapa moja kwa moja!!. Kama hata ukiokoka, unasema bado mtu unakuwa katika hatari na mashambulizi, zaidi, huoni kuwa kutumia neno “UMEOKOKA” ni sawa na kufuru?? Sasa utaokokaje kama bado uko kwenye hatari zaidi??? Lwembe na ndg yangu, Sungura, akili zenu Mungu atazifungua na wala siyo Siyi!!
  Nashukuru kwa vile umeorodhesha mafundisho mengi ambayo wewe mwenyewe ulshindwa kuyathibitissha Kimaandko enzi zile. Tafsri yenu ya mtu kuokolewa kwa sheria, sijui mnaipata wapi!! Anyway, heri niyi. Sisi akina Siyi, tutaokolewa kwa NEEMA tu japo sheria na neema huwezi kuzitenganisha!! Kwa maelezo mengine, huwezi kudanganyika kuwa, Unampenda Yesu huku ni mvunja sheria!! Fanatic!!

 113. Sungura
  Tunaendelea…
  Aidha, kuhusu kile kimfanyacho mtu kutenda dhambi ni dhambi yenyewe!! Nami ngoja nikuulize swali, Kile kilichomwangusha mwanadamu bustanini Edeni, kilikuwa ni nini? Shetani au dhambi iliyokuwa ndani yake mwanadamu huyo? Na kama dhambi inakaa ndani, nani aliiweka humo? Mungu au Shetani? Nakusubiri.

  Sungura, sasa nimekuelewa vyema kuwa, tatizo lako kumbe liko hapa…!! Ona unavyosema, “Yesu akirudi haji kuokoa, anakuna kunyakua waliotayari. Kuokoka siyo kutolewa duniani, bali ni kutolewa katika mikono ya shetani na kulindwa na Mungu.
  Dunia haikuumbwa kwa ajili ya shetani na wala shetani hakuanza kuwepo duniani baada ya anguko, amekuwepo hata kabla ya anguko akiwa mwovu hivyohivyo. Sasa kwa nini ushindi wa maisha ya wokovu usiwezekane duniani ambamo shetani anaishi wakati nguvu ya kufanya hivyo imo ndani yetu!!!!”
  Mmmh!! Sasa hebu nijibu maswali haya machache na Ziragora wako!!
  1. Unaweza kueleza maana na tofauti iliyopo kati ya wokovu na unyakuo? Yesu ni mwokozi au mnyakuzi wa watu?
  2. Wale ambao hawajamwamini Yesu (ninyi mnakuita kuokoka), wanalindwa na nani kwa sasa? Shetani au Mungu?
  3. Shetani hajaanza kuwepo duniani kabla na baada ya anguko la nani? La kwake au la mwanadamu? Unataka kusema kuwa shetani aliumbwa akiwa muovu tayari tangu mwanzo? Au kwa maelezo mengine, Mungu alijitengenezea tatizo mwenyewe kwa kumuumba shetani?
  4. Kama uwezo wa kushinda na hadi kupata wokovu uko ndani yetu, je, Kifo cha Kristo msalabani kilikuwa bure kwa vile tunaweza kumshinda shetani sisi wenyewe?

  Nawangoja wewe na Ziragora pamoja na yeyote atakayekuwa na mtazamo kama wenu. Nawaombea maana naona mko mbali sana vijana!!
  Mungu atusaidie sote.
  Siyi

 114. Sungura,
  Samahani kwa kuchelewa kujibu mapachiko. Nilikuwa busy kweli rafiki.
  Wewe nisamehe bure!!
  Nimekuona umecheka sana, ngoja nikufuatilie nione kilichokuchekesha!!
  Naona unafanya mchezo na Mungu. Nilipokupa mfano wa Ibrahimu na Isaka, nilitaka utafakari. Mungu alitoa hizo kanuni za kutoa kafara akijua kabisa kuwa, kulikuwa na masikini, wafugaji, wafanyabiashara na wakulima. Na miongoni mwa masuala yaliyohusisha kafara, kubwa zaidi lilikuwa ni kwa ajili ya toba. Kafara na sadaka ni vitu viwili tofauti. Sadaka watu walipeleka chochote, lakini kafara kwa ajili ya toba, ilikuwa ni lazima kitu chenye kiwe cha kumwaga damu bila ya kujali kuwa muhusika alikuwa ni mfanyabiashara, mkulima au masikini wa kutupwa. Soma vizuri historia ya kile kiitwacho KIVULI CHA KRISTO katika agano la kale. Ninachotaka uzingatie hapa ni hiki;
  Biblia imetumia maneno SADAKA YA KUTEKETEZWA (Sucrifice offerings -) katika dhana ile tunayoiita sisi leo kuwa ni kafara. Ni kafara kwa sababu zilikuwa ni sadaka zilizohusisha umwagaji wa damu ili mtu apate ondoleo la dhambi-“ Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo” – Ebr. 9:22. Sasa inabidi uangalie kwa makini SADAKA zilizokuwa kafara na SADAKA zilizokuwa dhabihu tu. Neno KAFARa, mara nyingi katika Biblia ya Kiswahili lilitumika kwa matoleo ya unga wa kuvukiza uvumba madhabuhuni. Natambua kuwa kulikuwa na aina nyingi sana za sadaka ikiwemo na sadaka ya kuteketezwa (sacrifice offering- (The Guilt Offering (Lawi. 5.14- Lawi.6.7)) ambayo leo tunaiita kafara. Na hii ndiyo concern yangu kubwa. Hakuna mtu aliyeenda kutoa sadaka ya namna hii aliyetoa sadaka za matunda, k.v. maembe, mahindi, mikate, andazi nk. Wote walitoa sadaka za kuteketezwa bila ya kujali mtu alikuwa mfugaji ama la! Wafugaji walitoa sadaka za wanyama na masikini walitoa sadaka za njiwa. Ndiyo maana nilikwambia usome Biblia kwa umakini mikubwa. Ukiisoma kama gazeti la mwananchi, utaishia kuuliza maswali hayo uliyouliza ya tofauti kati ya sadaka na kafara!!
  KAtika ufun 5:2 umesema kuwa, “So, angepatikana mtu, malaika, au yeyeote angetumwa huyo badala ya mwanae pndwa.” Hizi ndizo fallacies unatengeneza hapa. Hatuwezi kamwe kutumia sababu za namna hii katika kujadili mambo ya Mungu. Ni mambo ambayo Mungu hajayafanya, sisi hatuwezi kuyajengea misingi ya kutumbaza kuendelea kujificha kwenye uasi. Mungu atatuadhibu tu!
  Umeuliza habari za Mungu kutobadilika. Sijui unataka nieleze nini maana najua unajua, ila unauliza. Kwani Paulo anaposema “Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele”.- Waebrania 13:8, wewe binafsi huwa unaelewa nini?” Au huwa unaelewa nini nabii Malaki anaposema, “Kwa kuwa mimi, Bwana, sina kigeugeu; ndio maana ninyi hamkuangamizwa, enyi wana wa Yakobo”.-Malaki 3:6? Shortly, nikwambie kuwa, Mungu na Neno lake (Sheria yake), hajabadilika. Na hatabadilika kamwe. Jinsi alivyowaua waasi wa sheria zake ktk agano la kale, ndivyo atakavyowaua waasi wa sheria zake agano jipya. Kama wewe unamlazimisha Mungu kukubaliana na wewe huku ukijidanganya kuwa uko salama, nakupa pole sana. Mungu anahitaji UTII wa neno lake tu mara baada tu unapomwamini! Ukiasi, usitarajie lolote mbali na uangamivu rafiki!
  Kuhusu suala la kuokoka ukiwa hapa duniani, sidhani kama utaelewa sasa. Nimetumia muda wangu mwingi sana kukuelimisha habari za jambo hili. Mjema naye kakueleza kwa marefu na mapana. Kinachokuponza, ni mapokeo rafiki yangu. Unga wa ndele!! Na hili ni kwa sababu huelewi mchakato wa kitu kinachoitwa “WOKOVU”. Unafikiri, kuokoka ni kuimba kama chiriku, “nimeokoka, nimeokoka”!! Kama huko ndiko kuokoka, kuanzia leo huna haja ya kuwa unaenda kanisani kuomba msamaha ya wa makosa unayoyatenda kwa fikra, macho, masikio, mdomo na pengine hata kimwili kabisa. Kwa nini? Kwa sababu, mtu aliyeokoka, hana dhambi. Na kwa sababu hana dhambi, ilhali uko kwenye ulimwengu wa dhambi, ina maana humuhitaji Masihi aje akutoe ulimwenguni maana huna sababu ya kutolewa humo – maana huna dhambi!! Na kwa sababu umeokoka (huna dhambi), humuhitaji Mwokozi, maana Kristo alikuja kwa wenye dhambi!! Na wala huhitaji msaada wake wa Roho Mtakatifu wa kukukamilsisha maana huna mapungufu – kwa sababu umeokoka (huna dhambi). Na hata hujiulizi kwa nini utakufa tu pamoja na kwamba “UMEOKOKA”!!! Kama kweli huna dhambi, na kifo ni matokeo ya dhambi, kwa nini ufe ilhali huna dhambi(umeokoka) rafiki? Hivi mpaka hapa huoni kuwa kudai umeokoka ilhali uko duniani, is a very stupid concept?? Na wewe unaiimba kila siku, “nimeokoka, nimeokoka” Samahani, sina maana ya kuwatukana wote wanaotumia kauli mbiu hii, hasha. Ninawapenda na kuwaheshimu nyote. Shida yangu ni kwa nini hamuoni uongo huu uliojificha ndani ya kapeti na ninyi mmeukumbatia tu? Aidha, siyo ninyi peke yenu, ninaamini kuna baadhi ya wasabato nao wasioelewa wenye mtazamo huu wa kijinga!! Wameendelea ktk uasi wakilivunja neno la Mungu (k.v. kuvaa vimini, kuvaa pete, kusuka na kukari nywele, kuvaa vibode, kuvaa suruali n.k.) wakifikiri kuwa, kumwamini Yesu tu yatosha!! Concept ya “Once Saved Always Saved” itawapoteza wengi sana wasipokuwa makini kusoma Biblia zao vizuri!! Tusipokuwa na jitihada zozote za kutambua kile allichokifanya Kristo pale msalabani, hakika tutapotea milele. Na wala Yesu hakusema kuwa tunapomwamini, tuimbe nyimbo za “tumeokoka, tumeokoka, au tunampenda Yesu, tunampenda Yesu”. Hasha. Alichokisisitiza kwa wote wamwaminio(wampendao), ni KULISHIKA NENO LAKE. Kuishi sawasawa na neno lake – kuzishika amri zake!! Na hii ndiyo dalili na ishara pekee kwa wote wanaompenda na wanaomgonja Kristo kwa mara ya pili.
  Kuhusu siku ya sabato kuwa niliitoa wapi?!!! Niseme kuwa niliitoa ndani ya Biblia. Mungu alipumzika siku ya Jumamosi, Yesu alipumzika siku ya Jumamosi na hata mitume wake wote walipumzika siku ya jumamosi. Nukuu uliyoitoa ya Yoh. 5:17 inayosema, “Akawajibu, Baba yangu anatenda kazi hata sasa, nami ninatenda kazi.” Kilichokuwa kinawasumbua wayahudi, ni namna ya kuitunza hiyo Sabato na siyo Sabato yenyewe. Na wewe nakuona unachanganya vitu hivi viwili, Sabato yenyewe na Utunzaji wake. Na waj2 wengi sana, wanaidefine Sabato kama utunzaji wake ulivyo. Nataka niwaambie kuwa, hivi ni vitu viwili tofauti japo vina uhusiano. Sabato iko palepale na inatakiwa kutunzwa na kila mtu. Nayo inapaswa kutunzwa siku ya jumamosi – siku ya sabato tu na si vinginevyo.

  Suala linalowasumbua walio wengi, naam hata baadhi ya wasabato, ni namna ya kuitunza hiyo Sabato. Wengi hufikiri kwenda siku ya jumamosi kanisani ndiyo njia pekee ya kutunza sabato, hasha!! Na wengine hufikiri kuwa, hawawezi kufanya lolote siku ya Sabato, hii nayo siyo kweli!! Wapendwa, utunzaji wa sabato, unapaswa kufanywa kama utunzaji wa amri zingine unavyofanywa. Unapaswa uanzie ndani ya fikra na moyo wa mtu mwenyewe. Kinachoonekana kwa nje, sharti kiwe ni matokeo ya kile kilicho ndani ya fikra na moyo wa mtu. Kwa kulitambua hilo, inabidi tujifunze ni mambo gani ambayo Mungu huyafanya hata siku ya Sabato kama Kristo alivyofanya. Kristo aliyafanya hayo kwa sababu aliyajifunza kutoka kwa Baba yake. “Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda; kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vile vile”.-Yoh 5:19.
  Wayahudi hawakuelewa jinsi Mungu alivyowataka waitunze sabato ndiyo maana walikuwa wanakinzana na Masihi kwa sababu wao walikuwa wameshaingiza desturi na tamadun zao kwenye suala zima la utunzaji wa sabato. Ndiyo maana hadi leo, utawasikia waj2 wanadai, aaah!! Wasabato Bwana, hawapaswi kutembea zaidi ya umbali wa kurusha jiwe siku ya sabato!! Ukimwuliza, umesoma aya gani kwenye Biblia inayosema hivyo, hana!! Ni mapokeo anayoyasikia kwa wahubiri wake kanisani na yeye kuzitumia bila ya kuzifanyia utafiti wowote. Wapendwa, kama utunzaji wa Sabato Mungu angeufanya kama baadhi ya watu wanavyofkiri, leo ng’ombe wasingepelekwa malishoni sku ya sabato, wagonjwa wangekufa sana mahospitalini siku ya sabato na watangazaji wa vyombo vya habari vya dini sku ya sabato, nao wangefunga vituo vyao hivyo. Na kama ingekuwa hivyo, Mungu asingeruhusu jua kuwaka siku ya Sabato, angeondoa ulinzi wake kwa watu sku ya sabato, mapepo yasingeondolewa siku ya sabato, waliojeruhika siku ya sabato wasingepata huduma hadi sabato iishe, Yesu angetembea umbali wa kurusha jiwe tu siku ya sabato n.k. Kwa mawazo yangu, hii sabato ya namna hii ndiyo ingekuwa mzigo. Lakini sasa tunapojifunza suala la utunzaji wa sabato, tunaliona kuwa siyo mzigo hata kidogo. Siku ya Sabato ni ya kutofanya kazi zetu zote. Ni sku ya kustarehe kabisa kama Mungu alivyostarehe. Baadhi ya mambo ambayo yako kwenye utunzaji wa Sabato ambayo Mungu mwenyewe na mwanaye wanaonekana kuyatenda siku ya Sabato, sisi hatuna budi kuyafanya pia pale yanapotokea kama emergencies!! Tunahitajika kujifunza kuelewa tu.

  Inaendelea…

 115. Sungura & Lwembe,
  Wajoli wa Bwana, nimewaona. Nitakuja na majibu yenu stahiki kabisa. Nimetingwa na majukumu tu kidogo. Mniwie radhi kwa kuchelewa kujibu mapachiko yenu. Maana nina siku mbili tatu tu tangu niyaone. Vuteni subira tafadhari. Muda si mrefu naja!!
  siyimnn

 116. Siyi,

  Nimekuona unamwambia ndugu Ziragora eti hubahatishi katika suala la wokovu, we ni muongo mwenye kudhani tukuamini kwa sababu ya wingi wa maneno yako.

  Kama hubahatishi, mbona unachanganya hata jambo dogo linaloitwa kuingia mbinguni ukidhani huko ndiko kuokoka?

  Kitu ambacho kimekupiga chenga kabisa ni kule kudhani kuwa kunyakuliwa na kuingia mbinguni ndio kuokoka. Huwezi kutofautisha kati ya kuokoka na kunyakuliwa au kuingia mbinguni.

  Tena kwa kukupa majibu directo to the topic, ni kwamba mtu aliyeokoka anaweza akaupoteza wokovu.
  Kumkiri Yesu ni hiari ya mtu na kumkana ni hiari ya mtu. Maana kama kwa kumkiri na kumwamini mtu anapata wokovu na kwa kumkana na kutomwamini mtu anapoteza wokovu .

  Yesu akirudi haji kuokoa, anakuna kunyakua waliotayari. Kuokoka siyo kutolewa duniani, bali ni kutolewa katika mikono ya shetani na kulindwa na Mungu.
  Dunia haikuumbwa kwa ajili ya shetani na wala shetani hakuanza kuwepo duniani baada ya anguko, amekuwepo hata kabla ya anguko akiwa mwovu hivyohivyo. Sasa kwa nini ushindi wa maisha ya wokovu usiwezekane duniani ambamo shetani anaishi wakati nguvu ya kufanya hivyo imo ndani yetu!!!!

  Hatuhitaji muda wowote wa kuja kujua kama akina Siyi walikuwa wanasema ukweli , ‘we already know’ kwamba akina Siyi wanasema uongo na kukana ukweli kwa mapokeo ya uongo.

  Kwani Israel hawakuokolewa Misri, au hicho kitendo cha kutolewa kwao Misri kilikuwa nini kama siyo wokovu, justification au ?

 117. Siyi,

  Kuokoka nilikuambia ni hali ya kuwa juu ya hatari zote pamoja na kifo. Sasa unielewe vizuri, sisemi kwamba eti ukiokoka hatari zinakwisha, hapana, hatari zinaongezeka zaidi, maana sasa hata marafiki wanakutenga! Vipepo vyote ulivyokuwa kipenzi chao, kuanzia vya dini mpaka vya umalaya, sasa unakuwa adui yao! Vinakuzunguka tayari kukushambulia; vita inakuwa ni kali saana, kuokoka siyo kuwa ktk picnic!

  Watazame Sauli mfalme, aliyejivika mavazi first class ya kivita, na Daudi kijana mdogo mchunga kondoo, anayetembea na manati ya kuwindia njiwa; ni yupi kati ya hawa aliyekuwa ktk hatari ya kuangamia mbele za Goliath? Kwa akili na jicho la kawaida ukiwatazama wawili hao ni lazima tu umwambie Daudi arudishe vyombo nyumbani, hawezi kufaulu ktk Amri Kumi za Mungu, amwachie Sauli, yeye anayajua mambo ya Sheria na Kafara zake na Sheria za Maadili, na Sabato Muhuri wa Mungu, tena anayajua mpaka ya ‘rohoni’ km yule mwivi pale msalabani kwamba hakuingia ktk Ufalme wa Mungu siku ile aliposulubiwa Kristo, wala Kristo hakuwatembelea hao roho walio kifungoni maana alikuwa kaburini, na wafu hawajui neno lolote, mpaka unabii wa Daniel utakapotimia watakapoamshwa kutoka mavumbini; hapo atakapo kuja “Mungu Mwana”; yaani Sauli alijivisha makorokoro ya kivita mengi saana mpaka akashindwa kuhuika akapigane na Goliath, na wala kuyavua hataki!

  Akina Goliath leo hii wamejaa kila kona, wanasubiri wakati muafaka. Hali itakayowakuta akina ‘Sauli’ wa leo itakuwa mbaya kuliko iliyomkuta Sauli siku hiyo, maana Sauli kwa yale Mafuta aliyotiwa, ingawa alikuwa chini sana ktk kiwango cha kumfanania Mungu, bali kwa yale mafuta aliweza kuuona Wokovu wa Israeli ndani ya kile kitoto Daudi! Ndio maana unamuona akimvulia makorokoro yake yote yampasayo mfalme, huyo jemadari apasaye kuyaongoza majeshi yake vitani, akiuvua ufalme, akimpa Daudi; yaani alipofika Goliath, ndipo alipojiona kwamba yu mtupu, miungu yake yote aliyoitegemea haikumfaa kitu, HAKUNA ANAYEWEZA KUHESABIWA HAKI KWA SHERIA!

  Daudi aliyakataa makorokoro ya mfalme aliyeukataa wokovu kwa kuyatumainia hayo makorokoro; yalikuwa ni najisi na ndio kisa cha huzuni iliyowafika ktk siku waliyodhani itakuwa ya shangwe maana kwa yale makorokoro waliamini watashinda vita waliyoishabikia!! Kwani kila walipoambiwa waupokee wokovu wawe salama, yale makorokoro waliyojivisha yaliwaambia usalama wao vitani utategemea kuyakariri hayo madude! Wokovu sio hadithi ndg yangu, ujasiri unaouona kwa Daudi ndio uhalisi wa Wokovu!

  Iwapo inakuchukua umri wako kutoka humo katika gereza lililofunguliwa milango utoke, basi hiyo ni dalili kwamba hauuoni mlango wa kutokea ambao ni Kristo, ndio maana ungali unazizunguka hizo selo ukitangaza kuhusu Mlango uliofunguliwa maisha yako yote unayoendelea nayo humo gerezani, changamsha akili hiyo kaka, kimbia kungali kweupe!!!

  Ubarikiwe!

 118. Siyi,
  Umenifurahisha saana, yaani uko ngangari kinoma kama yule kipofu waliyemdanganya kwamba anaona, naye kwa kujitutumua akasema anaona; ilipofika saa ya kuinuka kuondoka, akakomaa akainuka kama mtu mwenye kuona, akaishia kutumbukia kwenye bwawa la maji machafu!

  Kila unapokutana na neno “Amri”, naona ufahamu wako umegotea ktk “Amri Kumi”, hizo zilizokuja na sabato, hata umejifikisha ktk uelewa kwamba zinatumika mpaka huko mbinguni!

  Sabato unayoiona mbinguni inamhusu Mungu tu, kama alivyoitamka, alipumzika yeye siku ya saba baada ya siku sita za kufanya kazi njema! Hakuna mahali ktk Biblia panapoonesha kwamba Mungu anapumzikaga kila siku ya saba; tena basi siku moja ya Mungu ni miaka elfu. Pia elewa kwamba Adam aliumbwa ktk siku ya sita, na Sheria inatutaka tufanye kazi siku sita na ya saba ndio tupumzike, basi kwa kadiri utakavyozihesabu siku za Adam, sabato yake haiwezi kuwa hiyo Jumamosi, au ikawa sawa na ya Mungu. Msijijazie mioyoni mwenu makorokoro yasiyo na faida!

  Israeli walipokuwa Misri waliiabudu miungu ya kimisri, hawakuwa na sabato. Sabato kwa binadamu inaanzia huko jangwani ktk urahisi wa kuzihesabu siku kulingana na hali yao hapo walipopewa hizo Amri na Hukumu zake, akiwatoa kutoka ktk Upagani waliouzoelea, na sasa akiwaingiza ktk mfumo mpya. Hivi kama hawa watu walikuwa na hizo Amri, walifikaje kumtengeza yule mungu wa ndama wa dhahabu? Mfano wake waliutoa wapi, na kiu ya kumtengeneza ilitoka wapi? Vilitoka ktk elimu na mazoea ktk hizo ibada za huko Misri kama nanyi!
  “Basi sasa mcheni BWANA, mkamtumikie kwa unyofu wa moyo na kwa kweli; na kuiweka mbali miungu ambayo baba zenu waliitumikia ng’ambo ya Mto, na huko Misri; mkamtumikie yeye BWANA.” (‭YOS.‬ ‭24‬:‭14‬)

  Huu ndio udhihirisho wa ukweli wa sabato kuanzia huko jangwani ktk hesabu ya siku za ki Misri kulingana na ufahamu wa siku waliokuwa nao kwa kadiri ya siku za ibada za kipagani walizokuwa wakizifanya! Unaweza kukuta kwamba siku hiyo waliyoifanya kuwa sabato huenda ina uhusiano na miungu ya kipagani ya Misri! Kwahiyo kulihusisha jambo la Sheria, hiyo sabato msiyoielewa, na wokovu ni kujivuruga akili yako na kuukomaza moyo wako kuwa mgumu kama jiwe na kuishia kuyakosa mambo yaliyo rahisi!
  Sungura amekuonesha jinsi Kristo alivyoliweka wazi jambo hili la sabato kuhusiana na Mungu, “Akawajibu, Baba yangu anatenda kazi hata sasa, nami ninatenda kazi” Yn 5:17. Andiko hili linathibitisha jinsi ambavyo sabato ni kwa ajili ya binadamu, Mungu akimpa pumziko la lazima la mwili huyo aliyezaliwa na kukulia utumwani, ndio maana unaliona katika AMRI likiambatana na Hukumu!!!

  Sabato ni Agizo la Mungu ktk hizo Amri, lakini hesabu ya siku ktk maana ya Jumapili hadi Jumamosi, Mungu hakujihusisha nayo, ndio maana tunawambia kuwa Jumamosi ni siku ya sabato sawa, lakini katika hesabu za Kiyahudi, ambayo Mungu hana tatizo nayo kwani hata sabato yenyewe amewapa wao wapumzike na kumuabudu, kwa AMRI!

  Lakini kwa waliookolewa kutoka ktk kitanzi cha Sheria, wao wanaongozwa na AMRI Mpya ambayo wao wenyewe hawana uwezo wa kufaulu ktk kuitii, ndipo huwalazimu kufa kwanza pamoja na Kristo ktk Ubatizo wa maji mengi kwa Jina la Bwana Yesu Kristo, ili kupata Ondoleo la Dhambi ambalo humpa fursa RM kuwafufua ktk utu mpya anaouongoza yeye ndani yao, ambaye ndiye mwenye uwezo wa kuitii hiyo Amri Mpya, Upendo, ambao ni Mungu, na HAUNA HUKUMU maana Kristo alikwisha kuhukumiwa; Yn 5:24 “Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani.”

  Huyu mtu aliyepita kutoka huko Mautini, huko kwenye mafundisho ya dini, akiisha kuingia Uzimani ndiye tunaye muongelea katika lugha rahisi kwamba, AMEOKOKA!!!!!

 119. Siyi inaendelea …..

  Kuna swali lingine nakunukuu: ”Kama uko duniani tayari unasema mtu ameshaokoka, unafikiri Yesu atakuja kufanya nini sasa?”

  Jibu ni jepesi mno; anakuja kunyakua walioupokea wokovu wake!

  Siyi mbona unaongea mambo ya kitoto katikati ya kikao cha watu wazima rafiki yangu?
  Ona ulichosema hapa ”Alichokifanya Yesu kwetu ni kutufungulia lango la gereza tu. Wenye uamuzi wa kutoka ndani au la ni sisi wenyewe!!
  Una matatizo ya utambuzi wa mambo eh, au nyeusi na yeupe kwako zote ni nyeusi?

  Ivi kama gereza limefunguliwa na wewe mfungwa umeruhusiwa kutoka, ukishatoka unaendelea tena kuwa mfungwa? Na kama jibu ni kwamba huendelei kuwa mfungwa maana yake unakuwa huru. Ukiwa huru maana yake ni nini kama si kuwa mbali na hatari? Kuwa mbali na hatari uliyokuwemo maana yake ni nini kama siyo kuokoka?

  We vip bwana, mbona unakuwa kama mtu asiyefikiri, au kwa sababu umekariri mapokeo yanayokwambie kuwa lazima useme hakuna kuokoka duniani?
  U even don’t see the logic out of examples u give!!!

  Kama wewe mpaka sasa hujamaliza safari ya kutembea toka gerezani basi bado mfungwa, bado ni mtumwa, na uelewe aliyeamuru gereza lifunguliwe si waibu ake tena kuja kukukokokta toka huko gerezezani. Yeye akirudi anakuja kuchukua waliohuru, walio mbali na hatari ya ufungwa, hao ndio waliokoka.

  Siyi ivi una akili kweli kichwani mwako, nani alikwambia Mungu hupumzika siku ya Jumamosi?
  Ivi unakumbuka maneno ya Yesu kwa mafarisayo walipomwambia kuwa hapaswi kufanya kazi siku ya sababo? ”Aliwaambia Baba yangu yu afanya kazi hata sasa”
  John 5:17 – In his defense Jesus said to them, “My Father is always at his work to this very day, and I too am working- NIV)

  Utaendelea kuwa mjinga usipofika wakati ukaelewa nini kilikuwa kinafanyika aano la kale na nini kinafanyika katika agano jipya. Ndio maana hili ni la kale na hili ni jipya. Naona unatamani ungeishi kipindi cha la kale, bahati mbaya sana hizo zama hazikuwa zako.

  Yesu ibada zake alikuwa anakwenda kufanyia milimani, hekaluni alikuwa anakwenda kufafuta kilichopotea. Ilikuwa ni lazima awafuate hukohuko wanakokusanyika ili akawapae habari njema.

  Usinitie moyo mimi, jitie moyo mwenyewe, maana mimi simtafuti Mungu, bali Mungu yuko ndani yangu anaishi. Wewe ndo unahangaika kumtafuta, sijui utampata lini!!

  Wewe unayedhani umetii sheria za Mungu, mbona bado unaendlea kutembea kutoka gerezani, hata wokovu wenyewe huuhjui, Unatii sheria zipi sasa za jipya au kuukuu?

  Mwisho; mimi nimekwambia kuwa kinachomfanya mtu atende dhambi ni dhambi yenyewe, hutaki unataka niseme kuwa kinachomfanya mtu atende dhambi ni shetani. Halafu ati unajiita msomi mzuri wa biblia!!
  Soma hapa kisha uniambie kama kinachomfanya mtu atende dhambi siyo dhambi yenyewe. (Roman 7: 20 – Now if I do what I do not want to do, it is no longer I who do it, but it is sin living in me that does it.)

  Habari ndo hiyo mzee, Yesu ni mwokozi kwa sababu anaokoa!

  Kama unategemea unyakuo bila kuokoka,
  basi utaona makoti tu ya walionyakuliwa!

 120. Kuna swali lingine nakunukuu: ”Kama uko duniani tayari unasema mtu ameshaokoka, unafikiri Yesu atakuja kufanya nini sasa?”

  Jibu ni jepesi mno; anakuja kunyakua walioupokea wokovu wake!

  Siyi mbona unaongea mambo ya kitoto katikati ya kikao cha watu wazima rafiki yangu?
  Ona ulichosema hapa ”Alichokifanya Yesu kwetu ni kutufungulia lango la gereza tu. Wenye uamuzi wa kutoka ndani au la ni sisi wenyewe!!
  Una matatizo ya utambuzi wa mambo eh, au nyeusi na yeupe kwako zote ni nyeusi?

  Ivi kama gereza limefunguliwa na wewe mfungwa umeruhusiwa kutoka, ukishatoka unaendelea tena kuwa mfungwa? Na kama jibu ni kwamba huendelei kuwa mfungwa maana yake unakuwa huru. Ukiwa huru maana yake ni nini kama si kuwa mbali na hatari? Kuwa mbali na hatari uliyokuwemo maana yake ni nini kama siyo kuokoka?

  We vip bwana, mbona unakuwa kama mtu asiyefikiri, au kwa sababu umekariri mapokeo yanayokwambie kuwa lazima useme hakuna kuokoka duniani?
  U even don’t see the logic out of examples u give!!!

  Kama wewe mpaka sasa hujamaliza safari ya kutembea toka gerezani basi bado mfungwa, bado ni mtumwa, na uelewe aliyeamuru gereza lifunguliwe si waibu ake tena kuja kukukokokta toka huko gerezezani. Yeye akirudi anakuja kuchukua waliohuru, walio mbali na hatari ya ufungwa, hao ndio waliokoka.

  Siyi ivi una akili kweli kichwani mwako, nani alikwambia Mungu hupumzika siku ya Jumamosi?
  Ivi unakumbuka maneno ya Yesu kwa mafarisayo walipomwambia kuwa hapaswi kufanya kazi siku ya sababo? ”Aliwaambia Baba yangu yu afanya kazi hata sasa”
  John 5:17 – In his defense Jesus said to them, “My Father is always at his work to this very day, and I too am working- NIV)

  Utaendelea kuwa mjinga usipofika wakati ukaelewa nini kilikuwa kinafanyika aano la kale na nini kinafanyika katika agano jipya. Ndio maana hili ni la kale na hili ni jipya. Naona unatamani ungeishi kipindi cha la kale, bahati mbaya sana hizo zama hazikuwa zako.

  Yesu ibada zake alikuwa anakwenda kufanyia milimani, hekaluni alikuwa anakwenda kufafuta kilichopotea. Ilikuwa ni lazima awafuate hukohuko wanakokusanyika ili akawapae habari njema.

  Usinitie moyo mimi, jitie moyo mwenyewe, maana mimi simtafuti Mungu, bali Mungu yuko ndani yangu anaishi. Wewe ndo unahangaika kumtafuta, sijui utampata lini!!

  Wewe unayedhani umetii sheria za Mungu, mbona bado unaendlea kutembea kutoka gerezani, hata wokovu wenyewe huuhjui, Unatii sheria zipi sasa za jipya au kuukuu?

  Mwisho; mimi nimekwambia kuwa kinachomfanya mtu atende dhambi ni dhambi yenyewe, hutaki unataka niseme kuwa kinachomfanya mtu atende dhambi ni shetani. Halafu ati unajiita msomi mzuri wa biblia!!
  Soma hapa kisha uniambie kama kinachomfanya mtu atende dhambi siyo dhambi yenyewe. (Roman 7: 20 – Now if I do what I do not want to do, it is no longer I who do it, but it is sin living in me that does it.)

  Habari ndo hiyo mzee, Yesu ni mwokozi kwa sababu anaokoa!

  Kama unategemea unyakuo bila kuokoka,
  basi utaona makoti tu ya walionyakuliwa!

 121. Siyi,

  Nimecheka sana!

  Unajua ulivyoanza kusema kuwa una wasiwasi kama huku niliko hata biblia huwa tunasoma, ukaongeza na maelezo mengi mengi hapo mbele yake, nilidhani kuwa kuna kitu cha maana sana umeongea. Nilipokuta unaniuliza swali kuhusu Ibrahim na Isaka nilicheka kweli.

  Ni mamuma tu ndiye anaweza akadhani kuwa swali nililouliza kuhusu kama Kaini na Habili waliagizwa watoe sadaka za wanyama, kuwa ni swali lisilo na maana. Ulitakiwa kulitafakari kwanza ndipo ujibu, naamimi jibu lako lingekuwa tofauti na ulilonijibu.

  Hebu jiulize tena: Je Ibrahim alikuwa mkulima au mfugaji, na je Kaini alikuwa mfugaji au mkulima? Na kisha ujiulize kama sadaka ya mazao iliruhusiwa kutolewa mbele za Mungu.

  Hebu jaribu kusoma Mwa 4: 2b ili uone Kaini alikuwa anafanya kazi gani , na Habili kazi gani. Then, ujiulize sasa kwamba ingekuwaje mkulima atoe sadaka ya ng’ombe wakati alichonacho ni mazao?
  Halafu angalia Habili hakutoa tu wanyama, bal wazaliwa wa kwanza, tena walionona.

  Ukiwa na akili iliyo sawasawa unaweza gundua kuwa kosa la Kaini yawezekana ni kutoa mazao kwanza ambayo si malimbuko, halafu yawezekana yalikuwa na hitilafu.

  Wewe uliyemsomi mzuri wa biblia kuliko sisi wengine, nani alikwambia kwamba Kaini na Habili walitoa kafara mpaka uifananishe na ile ya Ibrahim kumtoa Isaka?
  Au wewe biblia yako imesema Kaini na Habili walitoa kafara?
  Unaelewa toafauti ya kafara na sadaka ( sacrifice and offering)?

  Kuna kiswali umeniuliza sidhani kama ulitegemea nitakijibu lakini: Kwamba kwa nini Mungu hakutuma hata malaika badala ya mwanae mpendwa?

  Siyi uliyemsomi mzuri wa biblia kama unavyojipiga kifua, ungekuwa umesoma kitabu cha Ufunuo 5: 2 …., ungeshagundua kuwa Mungu alimtuma mwanae kwa kuwa hakupatikana mbinguni wala duniani wa kujitokeza kukifungua kitabu, ndipo ikabidi amwachile mwanae wa pekee.
  So, angepatikana mtu, malaika, au yeyeote angetumwa huyo badala ya mwanae pndwa.

  Kuna kitu hapa nakunukuu ”Jinsi alivyofanya ktk agano la kale, ndivyo atakavyofanya na sasa. Bado hajabadilika.”
  Hebu fafanua, ni kitu gani alichokifanya katika agano la kale atakifanya hivyo hivyo katika hili agano jipya?

  P.T.O

 122. Ziragora,
  Nilishaamua kutobahatisha kabisa kwenye suala la wokovu. Sijali hata mtu wa imani yangu akinena kinyume na andiko, nampatia za kwake. Sibahatishi kaka. Na kila siku naenda magotini nikimlilia Mungu nisibahatishe kwenye suala la wokovu. Na nina imani sibahatishi. Nina uhakika na hicho ninachokiamini!! Biblia nimeisoma na ninaendelea kuisoma, bado haijabadilika. Inaendelea kuniambia kuwa niko sahihi. Napita kwenye nyayo zilezile za wenye haki waliotangulia. Mungu anisaidie safari niimalize vizuri.
  Ni kweli mpango wa Mungu ni kuwaokoa wanadamu wote. Shida iliyopo, si wote wanaoupokea wito huo wa kuokolewa!! Ndiyo maana hata Yesu mwenyewe, alisema, waitwao ni wengi, lakini wateule ni wachache tu. Mungu hataokoa watu walioamua kufuata madanganyao kisa walikuwa wengi kwa idadi. Kipindi cha nyuma hakufanya hivyo na hata kipindi kijacho, hatafanya hivyo pia.
  Kuna makundi mawili tu ya watu duniani. 1. Wenye Haki na 2. Waovu. Sasa jifunze wenye haki ni akina nani!!Jitahidi kuangalia sifa za wenye haki halafu ulinganishe na zile za waovu. Makundi yote haya yako bayana ndani ya Biblia. Kama unaisoma Biblia mstari kwa mstari, nina imani utakuwa umekumbana nazo. Zirudie tena!! Habari za kwenda mbinguni siyo lelemama kaka!! Acha kudanganyika kabisa. Bado nazidi kukuonya kuhusu jambo hili ungali una nafasi ya kutubu!! Fanya haraka usije ukachelewa.
  Mungu akubariki sana

 123. Sungura,
  Rafiki sidhani kama huko uliko kama huwa mnasoma Biblia kiuhalisia. Nina wasiwasi. Huenda uko kwenye zile injili za miujiza tu na utajirisho!! Injili za kuwapatia watu reliefs za kimaisha wakiwa hapa duniani!! Injili dhaifu na potofu kwa mujibu wa barabara ya kuelekea mbinguni. Historia inatuambia kuwa, wote tunaowasoma leo ndani ya Biblia kuwa mifano mizuri kwetu, hawakuwa na injili za namna hiyo. Zingalie vizuri rafiki! Unaweza kufikiri unajua na kusikitikia wengine kumbe wewe ndiyo unapaswa kusikitikiwa zaidi. Nasema haya kwa uchungu sana, nikijua kabisa kuwa, bado una uelewa mdogo sana wa Biblia. Kwa nini?
  Angalia miongoni mwa maswali unayouliza; “Ivi, Mungu alikuwa amewaamuru Kaini na Abel watoe dhabihu za wanyama? Hebu nioneshe hilo agizo Siyi”
  Nami nakujibu kwa aya; “Isaka akasema na Ibrahimu baba yake, akinena, Babangu! Naye akasema, Mimi hapa, mwanangu. Akasema, Tazama! Moto upo, na kuni zipo, lakini yuko wapi mwana-kondoo kwa sadaka ya kuteketezwa? ”- Mwanzo 22:7.
  Wewe unafikiri Isaka alijuaje kama yeye na babaye walikuwa wanaenda kutoa sadaka ya kafara? Kwani kuna sehemu ulishasoma Ibrahimu alionekana kumfundisha mwanaye mfumo wa utoaji kafara kiasi cha kumfanya aulize maswali ya namna hiyo? Ukipata majibu ya hapa, yapeleke wa Adamu na wanae basi.
  Swali
  “Na ni nini kinakufanya uone kuwa kosa la Kaini llikuwa ni kule kutoa matunda ya mazao badala ya wanyama, angetoaje wanayama wakati yeye alikuwa ni mkulima na Abeli ndo alikuwa alikuwa mfugaji?”
  Mwitkio
  Wewe unafikiri kwa nini hata waisrael walilazimika kupeleka mnyama, njiwa nk (kitu chenye damu), kwa ajili ya kafara ya toba? Wewe unafikiri hawakuwepo akina Kaini enzi za Israel? Walipofanya kinyume na maagizo ya Mungu nini kiliwatokea? Soma historia kaka!! Mimi nakuona unamchezea Mungu!!
  Swali
  “Kwa nini usione kuwa Kaini hakutoa kilicho kizuri toka kwenye mazao yake, maana hata Abeli hakutoa mnyama yeyote, bali alitoa wazaliwa wa kwanza tena walionona?”
  Mwitiko
  Sasa kama unafahamu baadhi ya taratibu Mungu alizowapa, kwa nini unauliza maswali ya kipuuzi rafiki? Na kwa nini ilikuwa ni mpaka wanyama wa uzaliwa wa kwanza tu??? Tena walionona tu?? Kama na matunda nayo ya kwanza yangekuwa deal, kwa nini Mungu aliyakataa? Hii inakupa implication gani kuhusu kile alichokuja kukifanya Mungu baadaye katika yoh 3:16? Wewe unafikiri Mungu alishindwa kutoa hata malaika mmoja tu akawafilia wanadamu? Kwa nini ilikuwa ni mpaka mwanae pekee? Tafakari juu ya hili, itakufanya uone ubaya na gharama ya dhambi!! Usicheze na dhambi!! Kama hutatii kile Mungu anachoagiza katika neno, usitarajie rehema/neema yoyote kuipata kutoka kwake. Jinsi alivyofanya ktk agano la kale, ndivyo atakavyofanya na sasa. Bado hajabadilika.
  Swali
  “Unamsubirije Kristo wakati umesema wokovu duniani hajaukamilisha ataukamilisha mbinguni, unamsubirije ambaye unakana kuwa bado hajakuokoa kwa neema yake?”
  Mwitiko
  Kama uko duniani tayari unasema mtu ameshaokoka, unafikiri Yesu atakuja kufanya nini sasa? Hivi unajua kilichojificha juu ya hiyo concept ya kuokoka ukiwa duniani? Hebu jifunze kuhusu hilo na ujaribu hata kuwaulizia mashahidi wa yehova. Watakwambia habari za marejeo ya Kristo na hatima ya kila mtu. Kama na wewe umekula unga wa ndele kiasi hicho, leo nakunywesha unga wa lele uzinduke!! Alichokifanya Yesu kwetu ni kutufungulia lango la gereza tu. Wenye uamuzi wa kutoka ndani au la ni sisi wenyewe!! Hii ndiyo tofauti ya kuwa mkristo na mpagani japo wote wamefiwa na Kristo. Wale wanaogundua kuwa lango limefunguliwa (wanaomwamini Yesu), ndio wanaofanya mchakato wa kutoka. Na kutoka ndani ndiyo UKRISTO wenyewe!! Huu ndio ufuasi wenyewe halisi!! Ni mchakato kaka. Ni vizuri ukaielewa kazi aliyokuja kuifanya Kristo na mipaka yake. Hili litakusaidia sana. Na ili ujue, jisomee historia ya kafara za agano la kale na maana zake. Jifunze mipaka ya zile kafara, utaelewa kile alichokifanya Kristo pale msalabani. Tofauti na hivyo, utaendelea kuwa mbishi nami sitashangaa maana nakuona historia huielewi!!

  Na kama pumziko hilo la moyoni ndio mwisho wa yote, wewe endelea kujifariji! Kama pumziko la rohoni ndiyo Sabato, basi Mungu asingekuwa na sababu ya kupumzika siku moja mwishoni mwa juma na kuiita Sabato maana kwake siku zote zilikuwa ni sabato. Na wala asingehangaika kuwaambia Israel kuimbuka na kuitakasa siku ya sabato – kutoka 20:8-11. Aidha, asingewaambia kuwa Sabato ni utambulisho wake kwa watu walio wake –ezek. 20:20. Hata Yesu mwenyewe uliyemnukuu akituambia tujifunze kwake, asingeenda siku ya sabato akaabudu kama siku zote zilikuwa ni sabato kwake, maana yeye hakuwa na dhambi hivyo, hakuwa na mzigo wowote wa kupumzishwa!! Hata mitume waliomshuhudia uso kwa macho, nao wangeendelea kwenye ufidhuli huohuo unaoutetea kaka. Lakini hawakufanya hivyo. Nami nikutie moyo kuwa, jitahidi kumtafuta Mungu; hakuna usalama huko uliko? Bila utii wa sheria za Mungu hakuna wokovu!! Short and clear!! Yesu hakusema kuwa mtu akimpenda, aimbe barabarani kuwa ‘nampenda Yesu’ au ajiite kuwa ameokoka, hasha!! Yesu alisema, mkinipenda, mtazishika amri!! Kama wewe unazivunja tena kwa makusudi kiasi hicho, usitarajie lolote tofauti na uangamivu milele.
  Hoja yako nyingine
  “Siyi mimi najua kinachomfanya mtu kutenda dhambi ni dhambi yenyewe, sijui kwa nini hutaki kuelewa huo ukweli. Labda wewe una jibu tofauti, wunaweza sema”
  Mwitiko
  Ukisema hivyo, utakuwa unadelete uwepo wa shetani na kazi zake!! Au kwa lugha nyingine, shetani unambatiza jina la kutokuwa kiumbe na kumfanya kuwa ni dhambi!! Unakifanya kitwendwa kuwa mtenda!! Pole sana. Na huo ndi miongoni mwa upotovu unaoushikilia rafiki yangu. Angalia sana!! Nakuona umenyaka mate ya theolojia ya kuchukulia maana za neno la Mungu kwa mujibu wa mujibu wa muktadha na wakati uliopo!! What a Heresy!!
  Hoja yako
  Thibitisha basi kuwa Adam, Abraham, Isaka, na Yakobo walikuwa wanasali siku ya sabato (Jumamosi)!!!!!!!
  Mwitiko,
  1. Hili nilishajibu muda mrefu sana. Na sikuanzia kwa Adamu tu. Nilianzia kwa Mungu mwenyewe, Adamu na hao wengine wengi waliofuata. Je, ni kweli waliitunza Sabato ya siku ya Saba? Kwa maelezo zaidi, rejea hapa; https://strictlygospel.wordpress.com/2013/03/18/ukweli-ni-kwamba-yesu-aliitangua-torati/ Soma comments zangu na za lenda za tarehe M. J. N. Siyi says: 18/03/2013 at 8:59 AM , M. J. N. Siyi says: 20/03/2013 at 10:07 AM , M. J. N. Siyi says: 20/03/2013 at 10:54 AM , lenda says: 20/03/2013 at 4:25 PM , M. J. N. SIYI SAYS: 20/03/2013 AT 8:54 PM , M. J. N. Siyi says: 25/03/2013 at 7:56 AM . Ikiwezekana ili upate mtiriko mzuri, soma mjadala mzima maana si mrefu. Una komments 70’s. Kuna watu waliokuwa wabishi kama wewe, utawaona wanakiri ukweli wa Sabato!!
  Ubarikiwe

 124. Brother Siyi,

  Nashukuru tena kwani hukudharau mwito wangu..

  Nataka tu uelewe kama kutofahamu kwa mtu kuna madhara mengi na moja wapo ni kupoteza lengo ya mada yenyewe. Nashangaa kwa nini wokovu imeambatanishwa na unachokiita “sabato” bila kutafakari. And you say “You must re-look the Scripture”. Dan!!!! Do you think you are sahihi na yale unayoyatamka au unakurupuka tu kama parrot? Hiyo homework nakupa wewe: “read carefully scriptures from Genesis to Revelation, utaelewa”. Tunachotaka ni kwamba watu wengi waokoke, si kama unavyosema eti wachache tu. Hiyo siyo lengo ya Jesus, Yeye anataka wote waokoke. Kama Ndugu Siyi hatapenda wokovu asije akadanganye kama Jesus alitaka aokowe wachache.

  Be blessed.

 125. Dah, Siyi,

  Yaani kuna vitu unaongea vinanisisimua sana, maana vinaonesha ni kwa kiasi kikubwa sana uko ‘ignorant wa kile Yesu alikuja kufanya katika ujumla wake. Lakini pia unaonekana kipofu hata kwa mambo ambayo yako peupe mno. Kweli wewe umeshikwa na fundisho nyonge mpaka ukashikika, unaitafuta mantiki ya agano jipya sura ya mwilini kabisa na hivyo unajikuta umetupwa mabli sana.

  Ivi, Mungu alikuwa amewaamuru Kaini na Abel watoe dhabihu za wanyama? Hebu nioneshe hilo agizo Siyi.
  Na ni nini kinakufanya uone kuwa kosa la Kaini llikuwa ni kule kutoa matunda ya mazao badala ya wanyama, angetoaje wanayama wakati yeye alikuwa ni mkulima na Abeli ndo alikuwa alikuwa mfugaji?

  Kwa nini usione kuwa Kaini hakutoa kilicho kizuri toka kwenye mazao yake, maana hata Abeli hakutoa mnyama yeyote, bali alitoa wazaliwa wa kwanza tena walionona?

  Unamsubirije Kristo wakati umesema wokovu duniani hajaukamilisha ataukamilisha mbinguni, unamsubirije ambaye unakana kuwa bado hajakuokoa kwa neema yake?

  Anyway, kuna swali la msingi sana umeniuliza, na jibu la hilo ndio hasa msingi wa tofauti ya agano la kale na agano jipya. Umeniuliza tofauti ya kupumzika rohoni na kupumzika mwilini.

  Sikia hapa Yesu anachokitangaza:

  -28 Come unto me, all ye that labour and are heavy laden, and I will give you rest.

  29 Take my yoke upon you, and learn of me; for I am meek and lowly in heart: and ye shall find rest unto your souls.

  30 For my yoke is easy, and my burden is light.(Matthew 11:28-30King James Version (KJV))

  Yesu anawaita watu waliolemewa na mizigo. Inawezekana kabisa hapa napo wayahudi walimshangaa maana anaita wajtu awapumzishe wakati hawakuwa na mizigo yoyote mabegani mwao.

  Basi kama raha inayosemwa kumbe wataipata nafsini/rohoni mwao, basi huo mzigo wanaotakiwa kuupeleka kwa Yesu ili awapumzishe ni wa huko nafsini ambako raha itapatwa.
  Kitu ambacho kinaweza kukaa rohoni au nafsini mwa mtu kikafanyika mzigo, basi hicho kitakuwa ni zao la shetani ambalo ni dhambi.
  Na Yesu anampumzisha mtu kwa kumsamehe dhambi zake, hivyo mtu anaposamehewa dhambi zake (mzigo)nafsi yake inaburudika, hiyo burudani ndiyo raha au pumziko lenyewe la rohoni, na ndiyo sabato yenyewe

  Na hapa ndipo mantiki ya sabato kutoka agano la kale kuja jipya imewachenga kabisa akina Siyi. Maana meng’gang’gana na siku ya sabato badala ya sababto yenyewe. Ndio maana mwandishi wa kitabu cha Waebrania anasema kuwa imebakia raha ya sababto kwa watu wa Mungu (Ebra 4:1-)

  Pumziko la mwili ni kule kutofanya kazi yoyote (muscle work) kama ambavyo Israel walikuwa hawafanyi kazi katika siku ya sabato. Na ndiyo ninyi akina Siyi mmeng’ang’ana nayo na mnadhani mmepatia kweli, lakini kumbe mnafanya out of ignorance. Mna-apply agano kuukuu ambalo limeshatoweshwa.

  Mungu leo hakai kwenye siku ya sabato, bali anakaa kwenye sabato yenyewe.

  Ni kitu kingine nikwambie, katika agano jipya hakuna siku maalum ya ibada, bali siku zote ni ibada. Suala la siku nzima kufanya ibada ni taratibu za dini tu, ambapo mkiamua kushinda au kutoshinda kanisani hata haimsumbui chochote Mungu. Ibada kwa mwamini inafanyika ndani yake 24/7 .

  Siyi mimi najua kinachomfanya mtu kutenda dhambi ni dhambi yenyewe, sijui kwa nini hutaki kuelewa huo ukweli. Labda wewe una jibu tofauti, wunaweza sema.

  Alichomaanisha Paul katika Rum3:31, soma tu vizuri tena na tena hiyo mistari utakielewa.

  Halafu Siyi elewa kitu kimoja kwamba kunukuu andiko siyo hoja, hoja ni maana halisi ya hilo andiko na matumizi au ‘applicability’ yake katika wakati au majira tunayoongelea.
  Agano ambalo Paul analiita kuwa ni kitu kikuukuu nalo limo ndani ya biblia, lakini ‘applicability/ validity yake ilishakwisha.

  Thibitisha basi kuwa Adam, Abraham, Isaka, na Yakobo walikuwa wanasali siku ya sabato (Jumamosi)!!!!!!!

 126. Ziragora,
  Hata mimi nakushukuru kwa michango yako bro. Kikubwa, tuombeane sana. Wokovu ni issue. Si mchezo kabisa. Kuimngia mbinguni ni issue kaka.Si kama watu wanavyodanganyana hapa nimekuwa nikiwaona kwa muda mrefu. Mungu ameweka pande mbili tu. Uzima na Mauti. Na daima wale wanaoangukia uzimani, wamekuwa ni wachache sana kwa mujibu wa historia ya Biblia. Hata hapa SG, wale wanaoelekea uzimani, ni wachache sana na kwa isivyo bahati, wamekuwa wakieleweka kwa watu wachache pia.
  Ninawahahakishia kuwa, mtakuja kugundua baadaye sana kuwa Siyi na wenzake, walikuwa sahihi kabisa. Lakini angalieni msingundue huku mkiwa mmeshachelewa!!! What a sad!! Tuombeane. Mbingu si mchezo kama wengi wanavyofikiri. You must re-look the Scripture!!
  Ubarikiwe Ziragora

 127. Ndugu Sungura, Siyi , Lwembe, …

  Bwana Yesu asifiwe!

  Kinachosumbua watu wengi ni kusoma Biblia juu juu na kufwata bila kuchunguza walimu wanaowafundisha ndani ya makanisa ya kuonekana kwa macho.
  Ni vizuri kutafakari Neno la Mungu jinsi lilivyoooo, wala si kusoma gazeti ambazo wamoja wanaconnect ku Biblia; hiyo ni uasherati.

  Ubarikiwe ndugu Lwembe. Nafikiri utaeleweka vigumu kama ukiambia watu wasiotofautisha imani na wokovu. Hawo watu hawajue kama Imani ni mbegu. Hiyo mbegu inaweza komaa ao inaharibika. Lakini Wokovu ni mavuno. It’s the last step. Ndio maana nafasi nyingi Biblia inasema kama anaeamini ataokolewa hapo ikitia wokovu katika future. Hivi mtu anapoleta confusion kati ya imani na wokovu ataendelea jifariji kama ameokoka mpaka ile siku ya kiama ambapo atajikuta jehanam. Asante kwa ufafanuzi na tafakari za Neno jinsi lilivyo. Press on my brother. Uwaambie kama kuna steps nyingi katika kuukomalia ukristo na ya mwisho ni kutumbukia ndani ya wokovu. Ukiisha upata kweli kweli hakuna anaeweza kukunyang’anya tena.

  Ndugu Siyi,
  Asante kwa kujivunia unayodhania imani unayo. Jithahidi uufikie wokovu kamili na Mungu akuwezeshe. Yesu akusaidie usikwamie kwenye sabato, siku ya sabato na masabato. Hayo siyo maneno ya wokovu ndugu yangu.Wewe tu angalia msalaba na uufikie wokovu; ukiisha ufikia utaisikia moyoni mwako. Hiyo ndiyo lengo yetu sisi sote.

  Ndugu Sungura,
  Mungu akubariki. Umesema vizuri sana. Mtu yeyote akitaka fahamu Neno la Mungu inafaa afahamu agano zote Mungu alizofanya na wanaadamu tangu Adamu wa kwanza hadi Adamu wa pili(wa mwisho). Hivyo vipindi vyote havihitaji ushabik. The bible is clear, lakini watu wanajithahidi kabisaaa ku create vihekalu vdogo vidogo ndani yao wakiamini tule tunabii na tafsiri zinazosindikiza biblia wakidhani biblia haijitoshelee. Mungu awasaidie warekebike.

  Nawashukuru kwa michango yenu, mbarikiwe sana.

 128. Siyi,

  Naona mafundisho yenu, kulingana na maelezo yako, yameutawala sana moyo wako kiasi kwamba unashindwa kabisa kuipokea Injili! Hebu itazame kauli yako hii ulipomjibu ndg Haule kuhusu wokovu, ni kauli ya mtu asiyeipokea Injili kabisa, yaani mtu mwenye mfano wa utauwa tu:
  “” Kama ukishamkiri Kristo (wewe unasema kuokoka), ndiyo kuwa salama, kwa kweli unadanganyika sana kaka. Kimsingi tunapomkiri Kristo, ndipo huwa tunatangaza mashambulizi makali ya ibilisi dhidi yetu kuliko ilivyokuwa hapo nyuma. Acha mchezo kaka.””

  Siyi, Mungu hamuogopi Shetani! Shetani anaweza kuuua mwili tu!

  Woga wako wa vita ni halali, maana hujafikia kuwa Jeshi la Mungu, wewe bado ni mgambo wa dini, basi anapokutokezea Goliath lazima uzimie! Shetani anaijua vita kama unavyomuona kamanda wake Goliath, basi mnapotangulizana wanamgambo, ndipo yeye hunguruma tu na kuwasambaratisha, na mwishowe huwakalia na kuwapa mafundisho ya kufisha zaidi ambayo huwafanya kuwa jeshi lake tiifu bila ninyi kulijua jambo hilo, mkidhani mnamtumikia Mungu!

  Jambo la kwanza analokufanyia ni kuiondoa ile hofu ya Mungu inayokujengea imani inayotawaliwa na upendo kwa Mungu, ikiondolwe hiyo uoga huibadili na kukaziwa na mafundisho yasiyo na tija kama hilo linalo kuhakikishia kuwa huwezi kuokoka hapa duniani!

  Unajua Siyi, inawezekana kabisa kwamba inakuwia vigumu kuelewa maana kamili ya wokovu kutokana na mazingira. Yaani unaweza kuwa kiroho umekulia ndani ya banda kama kuku wa kizungu, kwa hiyo hujui hata inachukua nini kumkamata panzi, kama kuku wa kienyeji!

  Najua jinsi mnavyojitoa kwa mafundisho yenu, lakini mafundisho hayo hayana Mafuta! Mwisho wa siku mtabakia kuwa ni wale wanawali walioikosa Karamu! Mafuta hayatolewi mbinguni bali hapa duniani hapo unapoijia Injili. Ukiyakosa Mafuta hapa duniani, basi mbingu ni hadithi tu! Mafuta ndiyo yanayo kuhakikishia mbingu, ndiko huko KUOKOKA tunakokusema. Unapotiwa Mafuta ndipo unapotiwa Muhuri wa Ukombozi, kwamba wewe HAUTAPOTEA kamwe!!!

  RM ndiye Muhuri wa Mungu, Efe 4:30 “Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi.” (EFE. 4:30). Ku seal kitu, yaani kukitia muhuri, ni kukifunga. Na hauwezi kukifunga chochote kile iwapo huna kifungio! Kuni hufungwa kwa kamba zinapokuwa tayari kubebwa, nyumba hufungwa kwa kufuli, hapo unapotaka kuwazuia wasio husika kuingia ndani; naye Mkristo anapokuwa tayari kwenda vitani hufungwa na RM, RM ndiye anayepasisha ubora wa kilicho ndani yetu, hicho alichokitoa kwa Kristo na kutuletea, basi. Yeye hukikagua ili kuona kama ni halisi, ile Injili ya mitume, ndipo hukutia Muhuri, Ishara ya kazi iliyokamilika, ile aliyoziinua zile Huduma Tano kuifanya, ili “Kuwakamilisha Watakatifu, ule Mwili wa Kristo”!!!

  Basi kama hilo Kanisa ndilo mwili wa Kristo, jambo au wazo la kwamba Kristo anaweza kupotea linaonesha jinsi ambavyo hujaielewa Injili, uko mbali sana huko porini; na hii inatokana na kulishwa matango mwitu kwa wingi mpaka damu imevilia!!!

  Sasa, RM akija kukukagua kisha akayakuta madude yasiyoeleweka kama hayo mliyonayo ninyi: Sheria za maadili, mara Sabato ndio Muhuri wa Mungu, sijui vyakula najisi, wanawake walionyolewa nywele zao nk, RM hawezi kupasisha zigo kama hilo, anamuachia Lusifa akutie muhuri wake, ile chapa ya mnyama, nawe kuanzia hapo unakuwa Mali yake, na mafundisho mengine yenye kuupinga wokovu unaletewa na yanakuwa matamu sana!

  Kama nilivyowaambia jamaa zako, mambo ya wokovu kwenu ninyi ni magumu kueleweka kutokana na kuondoka kwenu kwenye Msingi wa Neno la wakati wenu lile la Kuhesabiwa Haki kwa Imani na Utakaso, hapo mlipo wafuata walimu na manabii wa Uongo; nayo matunda yake ndiyo huu ukakasi tunaouona kwenu! Hebu ona kichekesho hiki, kwamba “Yesu ameingia patakatifu pa patakatifu huko mbinguni, ili kutuombea, hiyo mnayoiita ‘Kazi Maalumu’ mwaka 1844″; fundisho hili mmelishwa baada ya fundisho lenu la awali kwamba Yesu atarudi mwaka huo kugonga mwamba! Sasa fundisho hili linatofauti gani na fundisho la Katoliki linalowaelekeza wajoli wake kumuomba “Bikira wa Milele, Maria Mtakatifu Mama wa Mungu, utuombee”! Nao walipoona wanazidi kuonekana wapagani kwa kumuomba mtu aliyekufa, wakaongeza Uongo mwingine wa kufisha zaidi, mwaka 1950 wakatangaza kwamba “Mwili wa Maria umepalizwa mbinguni”!!!!

  Lakini Neno la Mungu halivurugiki kwa chochote kile, maana limejengwa ktk Msingi wa Imani, ambayo ndiyo inayotuingiza ktk wokovu! Hakuna Uongo unaoweza kulivuruga Neno la Mungu. Neno la Mungu ni Imara tena linatenganisha nafsi na roho! Ndipo kwa hilo Neno, hao walimu na manabii wenu wa Uongo, watasimama Hukumuni wahukumiwe kwanza, ndipo makundi yao yawafuate tena huko wanakopelekwa; kama ambavyo akina Paulo watasimama Hukumuni, kama alivyosimama Mungu mwenyewe Hukumuni ktk Kristo ili aihukumu dhambi kulingana na Utakatifu wake! Basi kama Paulo alimdhihirisha Kristo, ndio kusema alikwisha kuhukumiwa pamoja naye na sasa ni mtawala pamoja naye baada ya Kushinda; tena kwa lile Neno anaendelea kuwahukumu mataifa hata sasa, ndio maana unayaona makundi makubwa yaliyohukumiwa tayari, yakiwa yamekatiliwa mbali kutoka lile Shina lenye Uzima wa Milele, Kristo!

  Kaka Injili ni tamu sana, na ina kona nyingi sana za kumpoteza asiye husika, mfuate Paulo kama anavyomfuata Kristo ili upone, punguza kujua kusiko na tija, kuna Uzao Mpya wa watu wa Mungu, amefanya uumbaji mpya kupitia Kristo, Adamu wa Pili. Uzao huu mpya ni wa watu wa rohoni licha ya wewe kuwaona ktk mwili, ninaamini jambo hili ndilo linalokuchanganya, unashindwa kumuona Mungu akiumba upya; bado umekwama katika Juma la kwanza la uumbaji! Ephesians 4:24 ” Mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli”

  Umeelewa Siyi? Umekwamia kwa Adamu wa Kwanza, huyo aliyeanguka, na uzao wake wote kuirithi adhabu ya kifo. Dhambi ilikuwa ni sehemu ya maisha yake mpaka alipoletewa Kivuli cha Wokovu, ile Torati, yaani Agano la Kale, ili angalau limsogeze aifikie Njia iliyo SALAMA!. Basi ile halisi ikiisha kufika kivuli kina kazi gani tena? Ndio maana ilipobadilika Sheria na mambo yake yalibadilika pia, hayo yanayoifanya hiyo kuwa Sheria; ndipo unaisikia Siku Mpya hiyo inayoitwa Siku ya Bwana, ambayo huko nyuma ilikuwa ni hiyo Sabato; mtume Yohana anaijua vizuri siku hiyo, Ufu 1:10 “Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana…” Haleluyaaaaa, umeiona Siyi siku hiyo ya Bwana? mambo yamebadilika kaka, Mungu si mchezo, kawaacha stendi!!!!

  Nakutakia Jumamosi njema!!!!

 129. Sungura,
  Nafurahi kukuona unaendelea.
  Kinachonisikitisha (sidhani kama ni mimi peke yangu), ni jinsi unavyoamini!! Pengine nakuangalia kwa upande mwingine kama mtu unayejibu (ukiwa na sababu zako hidden) ili kuona mimi nitasemaje!! Anyway haya ni miongoni mwa mawazo yangu juu yako ninaposoma majibu/mirejesho yako.
  Siku ile nilikuuliza, Kwa nini kuna dhambi? Angalia jibu ulilonipa.. “Hii iko hivi; nje ya sheria dhambi imekufa (haipo). Kwa hiyo kinachomfanya mtu atende dhambi ni dhambi yenyewe”.
  Nilivyokuelewa ni hivi; Uwepo wa sheria, ndio unaosababisha uwepo wa dhambi!! Kwa hiyo hatuwezi kuwa na dhambi kama sheria haipo. Kwa maneno mengine, dhambi ni mtoto wa sheria. Nimekuelewa kuwa, Mungu alikosea sana kuwapatia wanadamu sheria, maana kwa kufanya hivyo, alisababisha matatizo makubwa. Mmmh!Anyway, nikuulize maswali nililokuuliza siku ile, ‘Je, muumini (au wewe mwenyewe) huwa hatendi dhambi?’ Sheria inapokufa(inapoondoka), kwa mtu nini kinatokea? Mkristo/mtu anawezaje kuwa na dhambi (inayomfanya kutenda dhambi nyingine) kama sheria imekufa kwake? Naomba unieleze, Paulo alimaanisha nini katika Warumi 3:31 Basi, je! Twaibatilisha sheria kwa imani hiyo? Hasha! Kinyume cha hayo twaithibitisha sheria.

  Mimi naona unataka kurefusha mjadala kwa mambo yanayoeleweka. Kama Paulo alikuwa anazungumza kwa Present na Past tense, nafsi ya kwanza umoja , pili, tatu n.k. mambo ambayo unafikiri yanakupa ruhusa ya kuendelea kwenye uasi, keep on bro!! Kama Paulo aliamini tu ndo akafikia ukamilifu, basi atakuwa alimaanisha hivyo. Lakini kama wokovu ni mchakato, evaluate yourself!! Otherwise, utapotea aisee!!
  Kwa mujibu wa jibu ulilonukuu Rumi 7:14 na 8:2, naomba unitajie mifano michache ya hizo sheria tafadhali.
  Kwa habari ya siku ya Sabato kuwa ni application tu ndiyo inamatter, sadaka za Kaini zingematter mbele za Mungu pia. Kama siku siyo deal mbele za Mungu, basi YEYE, Mwanaye, mitume wake n.k. wangelifahamu hilo. Kama unaihalalisha Biblia kwa mawazo yako tu, jiangalie sana rafiki. Uko hatarini sana. Maana kama unaijua maana ya Sabato kiasi hicho halafu ukapotea, what a sad my fried!!
  Naendelea kuomba jibu la uhakika kwa swali hili;
  “ Waweza kutofautisha kati ya kupumzika mwilini na kupumzika rohoni??” Tell me please!!
  “Nithibitishie kimaandiko hiki ulichosema, nakunukuu ‘’ Na kukusanyika J2 kusali kama siku maalumu ya ibada, ni kuvunja sabato pia. Lakini kama utakusanyika j2 kwa ibada za kawaida kama zile za siku nyingine za wiki (j3, j4, j4, nk), ukasali halafu ukaenda kazini, hiyo si dhambi. Ukiifanya j2 kama siku maalumu ya ibada, hapo ndiyo wafanya kosa kwa Mungu.”
  Mwitiko
  Nadhani hapa huhitaji references za kibiblia. Najua unafahamu kabisa kuwa, ratiba ya maombi kwa mkristo yeyote yule ni mara tatu kwa siku (Asubuhi, Mchana na Jioni). Wengine huenda zaidi ya hapo. Ndani ya wiki (siku 7), kuna siku moja ambayo muumini hapaswi kuomba mara tatu tu. Siku nzima anapaswa kusali na kujifunza ukuu wa Mungu. Hii ndiyo Sabato. Nayo iko so specific ndani ya Biblia-siku ya 7 ya juma. Ukifanya siku nyingine tofauti, hutakuwa na tofauti kati ya yule aliyepeleka matunda kama dhabibu mbele za Mungu badala ya mnyama. Alizingatia hiyohiyo mantiki unayoisema wewe. Mungu hakuikubali mantiki yake. Na wewe Sungura kama una mantiki ya kusali (siku nzima) siku ya kwanza ya juma tofuati na Sabato(siku ya 7), wewe nenda tu tuone kama Mungu huyo ataikubali mantiki yako pia. May be, you are so exceptional bro.!!
  Kuhusu kazi kama ibada, ni lazima utasema ni upuuzi tu maana nilinukuu aya za Biblia. Kwa hiyo hata mwenye Biblia naye hana tofauti na mimi (mpuuzi). Tangu lini Lucifer alimpongeza Mungu kwa maneno yake? Kama huangalii vizuri, hata wewe watembea njia ileile… Pole sana!!
  Na kama akina Siyi hatuitunzi Sabato isipokuwa siku, hebu niambie tofauti iliyopo kati ya kutunza Sabato na kutunza siku!! Nakusubiri.
  “Siyi nipe andiko unalosema ullitoa lenye kuthibitsha hata maneno yako (‘Haipaswi hata watu kufikiri mawazo yao mengine tofauti na utakatifu wa ibada tu kama Mungu anavyoagiza).
  Andiko la Isaya 58:13 halina hayo maneno yako niliyoyaweka kwenye mabano.”
  Mwitiko
  Mimi nasema inayo. Tena nakuongezea na aya inayofuata ili uione vizuri; Haya soma tena Isaya 58;
  13 Kama ukigeuza mguu wako usihalifu sabato, usifanye anasa yako siku ya utakatifu wangu; ukiita sabato siku ya furaha, na siku takatifu ya Bwana yenye heshima; ukiitukuza, kwa kutokuzifanya njia zako mwenyewe, wala kuyatafuta yakupendezayo, wala kusema maneno yako mwenyewe;
  14 ndipo utakapojifurahisha katika Bwana; nami nitakupandisha mahali pa nchi palipoinuka; nitakulisha urithi wa Yakobo baba yako; kwa maana kinywa cha Bwana kimenena hayo.
  Sasa kama bado unabisha, je, wewe huwa unasema maneno bila ya kufikiri/kuwaza????
  Na wadhambi huwapigi mawe kwa sababu hujaambiwa kama vile ambavyo hujaambiwa kuchinja!!! Basi hakuna haja ya kuendelea kuhoji kitu ambacho hujaambiwa (huenda hata kusoma bado). Endelea katika nuru iyohiyo ulinayo. Ukipotea haya, ukipona, Amina!!
  Mwisho naona bado unaendelea kuuliza swali lilelile huku jibu ukiwa ushalitoa mwenyewe. Kifupi, mimi nimeamua kumfuata Kristo kwa uhalisia wake. Nimeamua kutobahatisha katika jambo lolote linalohusu wokovu wangu. Na ninamwomba Mungu anisaidie sana nisipotee. Mpaka sasa, niko njia sahihi, namgonja Bwana anikaribishe nyumbani kwake. Naendelea kuvipiga vita. Na kwa sababu amenifundisha kutokuwa mbinafsi, nawakaribisha na ninyi akina Sungura na wengine. Lakini kama mtaendelea kuitii miili huku mkizisingizia roho zenu, mtapotea hakika. Nawaombea tu.

 130. Siyi,
  Nakushangaa sana kuniambia ati nimeumbuka, kwa lipi? Ishu siyo siku ya sabato kuwa J’mosi, bali ni application na mantiki ya sabato.
  Hata sihitaji kuongea mengii, just prove to me kuwa Ibrahim, Isaka, hata Adam alikuwa anasali J’mosi. Nipe hayo maandiko.
  Na nilishawahi kukutaka ufanye hivi tena, lakini hukufanya.

  Narudia tena kukwambia kuwa tofautisha sabato na siku ya sabato. Sabato ni pumziko, siku ya sababto ni ya kupumzika. So unaponiuliza kwani sabato ilianza kwa wana wa Israel sijui kama unasoma between the lines au unaongea tu.

  Hujui maana ya kupumzika rohoni na mwini unaponiuliza ‘’ Waweza kutofautisha kati ya kupumzika mwilini na kupumzika rohoni??
  Nithibitishie kimaandiko hiki ulichosema, nakunukuu ‘’ Na kukusanyika J2 kusali kama siku maalumu ya ibada, ni kuvunja sabato pia. Lakini kama utakusanyika j2 kwa ibada za kawaida kama zile za siku nyingine za wiki (j3, j4, j4, nk), ukasali halafu ukaenda kazini, hiyo si dhambi. Ukiifanya j2 kama siku maalumu ya ibada, hapo ndiyo wafanya kosa kwa Mungu.

  Hicho unachosema nimekinukuu nusu hivyo hujakielewa, maelezo yake yapo paragrafu iliyofuata, wala halikuwa swali. Maswali yalifuata chini zaidi.

  Na ulichojibu kwenye swali la kutaja kazi moja ambayo si kumwabudu Mungu kwa aliyezaliwa mara ya pili, ni upuuzi tu. Nami nakupuuza kama huo upuuzi wako!

  Narudia kukwambia tena hiyo uliyoiona kuwa ni ‘fallacy’ kuwa ninyi akina Siyi hata hamwitunzi sabato mnayosema mnaitunza, bali mnatunza siku ya J’mos.
  Siyi nipe andiko unalosema ullitoa lenye kuthibitsha hata maneno yako (‘Haipaswi hata watu kufikiri mawazo yao mengine tofauti na utakatifu wa ibada tu kama Mungu anavyoagiza).
  Andiko la Isaya 58:13 halina hayo maneno yako niliyoyaweka kwenye mabano.

  Kwamba kwa nini mimi siwapiga mawe wakosa na sichinji kafara; ni kwa sababu mimi sikuwahi kuambiwa kuwapiga mawe wakosa, wala sikuwahi kuambiwa kuchinja kafara. Labda wewe nithibitishie kuwa niliwa kuambiwa.

  Mimi nilikuuliza uniambie kama uko chini ya utawala wa shetani, lakini wewe unanijibu kuwa Yesu alikusamehe ya mwanzo – so what?
  Lini sasa wewe utaupata uzima wa milele Siyi?

 131. Siyi inaendelea….

  Uliniuliza hili swali ” Nini kinachomfanya mtu atende dhambi? Ni kwa sababu sheria zipo au ni kwa sababu gani? Kwa nini kuna dhambi?”

  Hii iko hivi; nje ya sheria dhambi imekufa (haipo). Kwa hiyo kinachomfanya mtu atende dhambi ni dhambi yenyewe.

  Jingine hili hapa ”Kama wale wote wanaomwamini Kristo wako huru; je kwao sheria haina nafasi katika maisha yao ya sasa?”
  Jibu: Sheria ipi?

  Siyi ukitaka kujua nini Paul alikuwa anamaanisha soma tu vizuri alivyoshift kutoka past tense kuja present tense kwa kuangalia kuanzia Rum 7:13 on.
  Ivi anaposema katika verse 7:14 kuwa ‘ bu I’m unspiritual sold into slavery to sin” unaona nini hapo, kwamba mtume Paul mpaka hiyo dakika alikuwa bado ameuzwa chini ya utumwa wa dhambi?
  If yes, then niambie, alitoka lini sasa kwenye huo utumwa wa dhambi?

  Swali jingine: ”Naomba unifahamishe maana na mifano ya sheria ya Roho wa uzima. Je, ina tofauti yoyote na ile aliyoisema Paulo katika War. 7:14? Kama ni ndiyo/siyo, kivipi?”

  Kwenye Rumi 7:14 imesema torati asili yake ni ya rohoni
  Kwenye Rum 8:2 imesema sheria ya Roho wa uzima..
  Sheria ya Roho wa uzima ni kule kuhesabiwa haki kwa njia ya neema kupitia kumwamini Yesu Kristo, na sheria ya torati ni kule kuhesabiwa haki kwa njia ya matendo ya mwilini kabisa.
  Hiyo ndiyo tofauti about the two mentioned laws.
  Najua umeuliza hili na kuliweka hivyo ukiwa na lengo ndani yake,
  karibu!

 132. Sungura,
  Nashukuru kwa mwitiko wako japo umekwepa kujibu maswali yangu. Yaonekana uliisoma post yangu ukiwa umechoka sana (usiku wa manane!!). Nakusihi uirudie tena maana kuna maswali mengine umeuliza, majibu yake yapo humohumo kwenye hiyo Post.
  Kwanza namshukuru Mungu kwa vile umetambua na kukiri ukweli wa Biblia kuwa, Sabato ya Biblia/Mungu ni J’mosi. Na zaidi ya hapo, ingekuwa tofauti, ungeyajibu maswali yangu niliyokuulizeni kwa habari ya watu kusali siku zingine kama nako ni kutunza sabato ama la. Ni dhahiri kuwa, ukweli huo, umekuumbua rafiki. Umekwepa kwa makusudi tu na kuanza kupiga porojo nyiingi kana kwamba hatujawahi kuzijadili hapa blogoni. Mf. Wa porojo ulizoleta.
  “Siyi, ivi kabla ya Musa hajaambiwa na Mungu awaambie wana wa Israel wasifanye kazi siku ya sabato, je kule nyuma walikuwa wanafanya kazi siku ya sabato au ilikuwaje.”
  Mwitiko
  Kwani sabato ilianzia kwa wana wa Israel? Mada hii tulishajadili hapa na wewe ukachangia. Anyway, pole bwana. Sabato haikuanzia kwa wana wa Israel. Ilianzia bustanini Eden. Kabla Mungu hajamwambia Musa awaambie Waisrael kutunza Sabato, waisrael walikuwa utumwani, hivyo hawakujua kuwa utunzaji wa Sabato ulikuwa ni mojawapo ya Sheria za Mungu ambazo hata baba zao (akina Ibrahimu, Isaka nk) walitunza Sabato.
  Angalia porojo nyingine uliyoleta rafiki…”
  Ivi, ikiwa agano la kale lilikuwa kivuli cha agano jipya,sabato maana yake ilikuwa ni pumziko la mwilini. Leo agano jipya si kivuli tena bali ni halisi, maana yake pumziko hilo si la mwilini tena bali la rohoni. Sasa rohoni huwa kuna kazi gani ambazo zinatakiwa kupumzikwa J’mos na siku zingine zinaendelea?”
  Mwitiko
  a. Waweza kutofautisha kati ya kupumzika mwilini na kupumzika rohoni?
  b. Biblicaly, ninapoitunza sheria kiroho, haina maana kuitunza kimwili? Kwa mf. Hivi ninapozini kimwili, kiroho huwa niko salama au kinyume chake?
  Swali lingine…
  “Siyi, hebu niambie tena: Maana ya kutunza sabato ni kukusanyika J’mos kusali, na maana ya kuivunja sabato ni kukusanyika J2 kusali”.
  Mwitiko
  Ni zaidi ya kukusanyika tu jmos. Na kuivunja Sabato ni zaidi ya kukusanyika j2. Unaweza kwenda kusali jmosi still ukavunja sabato. How? Endapo utatenda lolote lisilopaswa kutendwa siku ya sabato. Lipi hilo? Yapo mengi. Machache; Rejea. Kutoka 20:8-11, Isaya 58:13-14 n.k. Na kukusanyika J2 kusali kama siku maalumu ya ibada, ni kuvunja sabato pia. Lakini kama utakusanyika j2 kwa ibada za kawaida kama zile za siku nyingine za wiki (j3, j4, j4, nk), ukasali halafu ukaenda kazini, hiyo si dhambi. Ukiifanya j2 kama siku maalumu ya ibada, hapo ndiyo wafanya kosa kwa Mungu.
  Aidha, sielewi uliponinukuu nusu hapa ulitaka kumaanisha nini??? Hebu angalia.. “Siyi kwa maelezo yako haya ”kuna siku moja maalumu ndani ya juma, ambayo ni maalumu (takatifu) kwa Mungu tu – siku nzima. Haipaswi kuchanganywa na kazi yoyote ile tofauti na kumwabudu Mungu tu. Haipaswi hata watu kufikiri mawazo yao mengine tofauti na utakatifu wa ibada tu kama Mungu anavyoagiza,”.
  Mwitiko
  Hapa sina jawabu maana sijui unataka niseme nini. Na kimsingi mimi sikutoa maelezo tu yanayoelea hewani. Nilikupatia na aya inayosupport maelezo hayo japo hapa hukuinukuu kwa makusudi. Sikusema mimi, ila nilinukuu kile Mungu anachotaka watu wake wakifanye pamoja na kwamba baadhi yao (kama akina Sungura), wanaweza wakakiona kama hakina maana, japo kwa Mungu kina maana.
  “Hebu nitajie kazi moja ambayo si kumwabudu Mungu kwa mtu aliyezaliwa mara ya pili. Au hata maana ya kuabudu hujui ila unadhani unaijua. Hauna tofauti na mwislam anayesubiri kuwa mtakatifu wakati wa mfungo.”
  Mwitiko
  Huenda kweli nikafanana na mwislamu. Nisikatae tu. Inabidi nijihoji pia. Ni kweli kuwa, kufanya kazi ni sehemu ya ibada kwa mfuasi wa Kristo. Mtu asiyefanya kazi, ni mvunja sheria particulary ya Sabato – “Fanya kazi siku sita”. Ndiyo maana wale wote wanaoliitia jina la Bwana, wanapaswa kuwa vielelezo vya utendaji bora wa kazi makazini kwao. Kinyume na hapo, ni sawa na waasi.
  Aidha, kuna kazi nyingi zinazofanywa na watu wanaotunza sheria rohoni, huku miili yao ikifanya kinyume na kilicho rohoni. Watu wanaoifuata miili japo husema kuwa ni watu wa rohoni. Watu walao nguruwe, wanywao pombe, wezi, wazinzi, wavunja sabato ya siku ya 7, nk. Na ukiwauliza, watakwambia kuwa wao wako rohoni japo miili/nafsi zao, zinatenda kimwili. Kimsingi, matendo ya namna hii kwa watu hawa huwa siyo ibada. Ni machukizo. Uvunjaji wa amri ya 3.
  “Yaani mpaka hapo wewe naona hutunza tu siku wala huwa hutunzi sabato, maana kuna tofauti kati ya sabato na siku ya sabato. in fact hata siku ya sabato na yenyewe huwa hamuitunzi”.
  Mwitiko
  Sina uhakika na hicho unachokisema, kwa sababu huishi na mimi. Aidha ningependa utofautishe Sabato na Siku ya Sabato!! Halafu mwishoni, ukajenerolaizi kuwa in infact, hatuitunzi na hiyo Sabato!! Hii nayo ni fallacy rafiki yangu. Hao unaowaona hawaitunzi, ni wasabato kwa jina tu. Kama unakumbuka, wito wangu siku ile, nilikwambia kuwa, ni heri kuwa mfuasi wa neno la Mungu zaidi kuliko kuwaangalia watu wengine wanafanya nini.
  “Ati unasema haipaswi hata watu kufikiri mawzo yao mengine tofauti na utakatifu! Hebu niambie hayo mawazo mengine ambayo ni tofauti na utakatifu ambayo siku zingine unaweza kuyafikiria”.
  Mwitiko
  Kwanza si mimi niliyesema hivyo. Ni Biblia/Mungu. Nilinukuu Biblia rafiki yangu. Unachopaswa kufikiri siku ya Sabato, jifunze Mungu alifikiri nini siku hiyo katika mwanzo 2.
  “Nimekuuliza unionyeshe mahali ambapo biblia imekataza kuwapiga mawe wadhambi. Yesu hakuwahi kukataza kupiga mawe wadhambi!”
  Mwitiko,
  Kwani mimi nilisema alikataza? Wewe usiyepiga mawe wadhambi, Biblia imekukataza kufanya hivyo? Kama ni hapana, kwa nini leo hupigi mawe wadhambi rafiki yangu? Au nikuongezee hoja, ni wapi wewe umesoma kuwa Biblia imesema “Sasa msichinje kafara za wanyama”. Na kama hakuna, kwa nini wewe leo huchinji? Kama hili linaeleweka vyema kwako, ugumu wa hilo la kwanza, uko wapi?
  “Halafu maneno ”sheria za kafara na sheria za maadili” yatumie tu unapoongea na wasabato wenzako, hakuna hayo maneno kwenye biblia, ila yako kwenye dini yenu”.
  Mwitiko
  Ok, anyway nitatumia sheria za maagizo badala ya sheria za kafara. Na nitatumia Amri kumi badala ya sheria za maadili.
  “Siyi, huwezi kunidanganya rafiki yangu huwezi. Kwa kifupi hujui maana ya sheria ya dhambi na mauti, kama ambavyo hujui maana ya sheria ya Roho wa uzima iliyo katika kristo Yesu. Unaleta fafanuzi ya dini yako ndo unataka kuniambia kuwa ndiyo maana ya sheria ya dhambi na mauti na sheria ya Roho wa uzima!! Acha upuuzi huo Siyi”.
  Mwitiko
  Kimsingi hata mimi siwezi kudanganya mtu. Na nikigundua kuwa nimedanganya (bila kujua), nitakuomba radhi mara moja. Sijui kudanganya rafiki yangu. Usiwe na shaka. Na wala hakuna upuuzi wowote. Fikra zako tu.
  Na kama mimi sielewi maana ya sheria ya roho wa uzima na sheria ya dhambi, nilitarajia unijibu maswali yangu niliyokuuliza kwenye hii hoja. Badala ya kujibu,umeleta porojo na shutuma rafiki yangu. Sidhani kama wanaume wenye busara kama wewe wanaweza kufanya hivyo.
  “Unataka kuniambia wewe mpaka dakika hii hujatubu, au umejiongelea tu hata hujui unachosema. Siyi are u still under devil’s kingdom or what? Answer me please!”
  Mwitiko
  What a sad!!! What more should I tell you? Nilikwambia kuwa, nilipoamini, Yesu alinisamehe yote ya mwanzo. Nilipompokea, mtu mmoja anapenda kusema, nikaingia ndani ya karakana/gereji (yaani kanisa lake), ndipo alianza kunirekebisha/kunitengeneza. Na ili niirejee hali ya upya (hali ya utakatifu), matengenezo hayo sharti yachukue muda. Ndiyo maana nikasema kuwa, uongofu ni mchakato mrefu rafiki yangu. Kiuhalisia, maisha ya dhambi huwa hayakomi mtu anapomwamini Yesu, bali hukoma kadri mtu anavyokua kiimani ndani ya Kristo. Ndiyo maana nilikwambia kuwa, mimi Siyi sijaridhika na kiwango changu cha uanafuanzi ndani ya Yesu. Ndiyo maana nakufa kila siku kama Paulo.
  Yote ninayokwambia kwa sasa yanaweza kutokuwa na maana, lakini baadaye yatakuwa na maana tu. Nakungoja tena.
  Siyi

 133. Siyi,

  Ujinga ni sifa na upumbavu ni sifa ambayo hupimwa kulingana na anachosema mtu katika uwanja fulani wa ufahamu wa jambo.

  Nasikitika umeandika sana for nothing kwa kweli, japokuwa pole yako kwa mkeka mrefu nimeipokea.

  Nianze na sabato:

  Kwanza usipate shida, ni kweli kabisa ya sabato waliyokuwa wanapumzika Israel ni siku ya J’mos. Hiyo wala usiipotezee muda kuielezea.

  Nilipokuuliza “Ivi kusali J’mosi ndo kutunza sabato na kufanya ibada J’pili ndo kuvunja sabato?” Ulinijibu a big ‘NDIYO’

  Lakini baadae nilipokuuliza kama wewe J2 hushinda kama mpagani umeleta longolongo nyingi.
  Kama kusali J2 ni kuvunja sabato, basi Yesu aliivunja.

  Lakini kama utakana jibu lako la ndiyo kubwa, basi ujue kusali J2 si kuvunja sabato kama ulivyokuwa umesema.

  Siyi, ivi kabla ya Musa hajaambiwa na Mungu awaambie wana wa Israel wasifanye kazi siku ya sabato, je kule nyuma walikuwa wanafanya kazi siku ya sabato au ilikuwaje.

  Ivi, ikiwa agano la kale lilikuwa kivuli cha agano jipya,sabato maana yake ilikuwa ni pumziko la mwilini. Leo agano jipya si kivuli tena bali ni halisi, maana yake pumziko hilo si la mwilini tena bali la rohoni.
  Sasa rohoni huwa kuna kazi gani ambazo zinatakiwa kupumzikwa J’mos na siku zingine zinaendelea?

  Siyi, hebu niambie tena: Maana ya kutunza sabato ni kukusanyika J’mos kusali, na maana ya kuivunja sabato ni kukusanyika J2 kusali.

  Siyi kwa maelezo yako haya ”kuna siku moja maalumu ndani ya juma, ambayo ni maalumu (takatifu) kwa Mungu tu – siku nzima. Haipaswi kuchanganywa na kazi yoyote ile tofauti na kumwabudu Mungu tu. Haipaswi hata watu kufikiri mawazo yao mengine tofauti na utakatifu wa ibada tu kama Mungu anavyoagiza,”

  Ni kwamba, una safari ndefu sana ya kujua siri ya Kristo na maana ya agano jipya, hivyo nikiuita kuwa ni mjinga wala usilalame.

  Hebu nitajie kazi moja ambayo si kumwabudu Mungu kwa mtu aliyezaliwa mara ya pili. Au hata maana ya kuabudu hujui ila unadhani unaijua. Hauna tofauti na mwislam anayesubiri kuwa mtakatifu wakati wa mfungo.
  Yaani mpaka hapo wewe naona hutunza tu siku wala huwa hutunzi sabato, maana kuna tofauti kati ya sabato na siku ya sabato. in fact hata siku ya sabato na yenyewe huwa hamuitunzi.

  Ati unasema haipaswi hata watu kufikiri mawzo yao mengine tofauti na utakatifu! Hebu niambie hayo mawazo mengine ambayo ni tofauti na utakatifu ambayo siku zingine unaweza kuyafikiria.

  Unajua tunaongea kutoka kona tofauti sana, ni kama analogia na digitali vile.

  Siyi punguza porojo, huongei na maamuma, bali na mtu anayefuatilia kwa makini.
  Nimekuuliza unionyeshe mahali ambapo biblia imekataza kuwapiga mawe wadhambi. Yesu hakuwahi kukataza kupiga mawe wadhambi!

  Halafu maneno ”sheria za kafara na sheria za maadili” yatumie tu unapoongea na wasabato wenzako, hakuna hayo maneno kwenye biblia, ila yako kwenye dini yenu.

  Siyi, huwezi kunidanganya rafiki yangu huwezi.

  Kwa kifupi hujui maana ya sheria ya dhambi na mauti, kama ambavyo hujui maana ya sheria ya Roho wa uzima iliyo katika kristo Yesu.

  Unaleta fafanuzi ya dini yako ndo unataka kuniambia kuwa ndiyo maana ya sheria ya dhambi na mauti na sheria ya Roho wa uzima!! Acha upuuzi huo Siyi.

  Unataka kuniambia wewe mpaka dakika hii hujatubu, au umejiongelea tu hata hujui unachosema.
  Siyi are u still under devil’s kingdom or what? Answer me please!

  Swali la kama wewe hapo ulipo ni mwenye dhambi umeliletea blablaa. Lakini ulivyojibu kumenifanya nigundue kuwa kumbe naongea na mtu wa mwilini tu, asiyeweza kuyatambua mambo haya ya rohoni.

  Sikia rafiki, wewe kama una dhambi tubu, anasema tukitubu anatusamehe. Na akishatusamehe hatuwi tena chini ya dhambi zetu.

  Ati unaniambia unajitahidi kujionesha kuwa umekubaliwa na Mungu. Hpo napo nimeona ni kwa jinsi gani hujui maana ya huo mstari.
  Mtu aliyekubaliwa na Mungu si mtu ambaye yuko chini ya dhambi tena, maana huo mstari unakwambia kuwa huyo ni mtu aliekubaliwa/aliyepata kibai mbele za Mungu.

  Huwezi kuwa umepata kibali mbele za Munu na hapohapo ukawa tena chini ya dhambi, hizo ni falme mbili tofauti.

  Wito uliotupa, mimi binafsi nauona ni wa kitoto sana ambao unafaa ukawape watu wenzako wa mwilini.

  Nitaendelea….

 134. Sungura,
  Asante rafiki kwa mchomozo wako.
  Huenda kweli mimi ni mjinga!! Inabidi nijifikirie sana. Kwa nini uniite mjinga? Hivi kweli mimi ni mjinga? Ujinga wangu uko wapi? Nimefanya nini cha kijinga? Haya ni baadhi ya maswali ambayo nilifundishwa kuyatafakari pale ninapokutana na tusi lolote kabla sijajibu chochote juu ya tusi hilo. Nikijichambua mwenyewe na kujiona kuwa siyo mjinga, nilichokisema siyo cha kijinga, na wala hakina ujinga wowote ndani yake, huwa nampuuza tu aliyenitusi (nampotezea) na kisha huendelea na mambo yangu. Kwa nini? Kwa sababu daima naelewa kuwa, mtu asiyetaka kujifunza lolote na kwa vyovyote, hata mwalimu wake humuona kama ni mjinga fulani tu anayepoteza muda. Matokeo ya mtihani, ndiyo hubaini nani ni mjinga haswaa kati ya mwalimu na mwanafunzi!! Hata mimi, najua iko siku Sungura (huenda na wengine kama wapo), atakuja kuamini ni nani alikuwa mjinga kati yangu na yeye/wao. Kwa sasa, rafiki yangu Sungura,, hili lisikupe shida. Hebu tuendelee kuziona busara zako ulizoandika sasa.
  Ninaanza kwa kukunukuu, “Ukisoma Warumi sura ya 6, utagundua Paul alikuwa anaelezea jinsi dhambi ilivyomtawala mtu kwa sababu ya uwepo wa sheria, na jisnsi sasa waliomwamini Yesu wamewekwa huru mbali na hiyo dhambi”.
  Maswali
  1. Nini kinachomfanya mtu atende dhambi? Ni kwa sababu sheria zipo au ni kwa sababu gani? Kwa nini kuna dhambi?
  2. Kama wale wote wanaomwamini Kristo wako huru; je kwao sheria haina nafasi katika maisha yao ya sasa?

  Siyi ni mtu wa imeandikwa tu. Porojo yeye hawezi. Naomba unithibbitishie kutoka rejea yoyote ile (hata ya kanisani kwenu), inayosema kuwa, Paulo alikuwa anachanganya tu nafsi na njeo wakati wa kusimulia/kufundisha injili na wala yeye injili aliyokuwa anaihubiri, haikumhusu maana alikuwa tayari kashaokoka .n.k. Naomba hizo rejea tafadhali. Otherwise, naomba ukiri kama ni mtazamo/uelewa wako tu rafiki.
  Swali la nyongeza,
  Naomba unifahamishe maana na mifano ya sheria ya Roho wa uzima. Je, ina tofauti yoyote na ile aliyoisema Paulo katika War. 7:14? Kama ni ndiyo/siyo, kivipi?
  Again here we go bro. Sungura, “Au wewe kuna mahali kwenye hiyo mistari umeona Paul anasema kuwa dhanbi itakoma ndani wakati tukinyakuliwa?”.
  Jibu
  Kwa mujibu wa warumi 7:14 (torati/sheria asili yake ni rohoni); kama sheria inakaa moyoni/rohoni, na kisababishi cha dhambi umesema kuwa ni sheria, je, unataka kuniambia kuwa Yesu atakuja kutuokoa na dhambi hivyohivyo kwa sababu sheria imo ndani yetu? Au sijakuelewa rafiki? Hebu njoo tena kwa lugha ya moja kwa moja… si unajua sisi akina Siyi… tena!!! Huenda sijalielewa swali!!
  Aidha, nizidi kukubali kuitwa mjinga tu tena sana hasa pale ninapoisema kweli ya Biblia. Ukiniita mpuuzi, sitatahayari hata kidogo. Naama hata kama ungeenda zaidi ya hapo ukaniita “mpumbavu”. Bado ningeshangilia tu. “Maana hekima ya dunia hii ni upuzi mbele za Mungu. Kwa maana imeandikwa, Yeye (ibilisi) ndiye awanasaye wenye hekima katika hila yao” – 1 Wakorintho 3:19. Ili nikujibu vizuri, ni vyema nilinukuu kwanza swali lako,
  “Ivi kusali J’mosi ndo kutunza sabato na kufanya ibada J’pili ndo kuvunja sabato?
  Jibu lake. Ni NDIYO. Tena ndiyo hiyo inaweza isijitosheleze kabisa bila ya kukupatia maelezo kidogo.
  Biblia, kuanzia mwanzo hadi ufunuo, imesema Sabato ni J’mosi. Hiyo ndiyo siku ya Saba ya wiki kwa mujibu wa Biblia/Mungu. Kuanzia Adamu hadi Yohana wa Ufunuo, waliitunza Sabato ya siku ya Saba ya juma kwa mujibu wa Biblia. Ndani ya Biblia, hakuna hata aya MOJA inayounga mkono watu kusali j’pili kama siku takatifu ya ibada. Wale wooote wanaosali j’pili, kimsingi wanafuata sheria/maagizo ya wanadamu na siyo ya Mungu. Na kile wanachokitafuta wakijitetea kwa hekima za dunia hii ambazo ni upuuzi mbele za Mungu, watakiona tu wasipotubu mapema.
  Zaidi ya hapo, unaweza kuwa msabato wa siku wa j’mosi lakini kama huenendi sawasawa na Neno la Mungu kwa ujumla wake, wewe ni muasi vilevile. Kushika Sabato ya siku ya Saba halafu ukavunja sheria nyingine, haikusaidii kitu rafiki.
  Kwa ufupi, naweza kukuthibitishia aya nyingi tu ndani ya Biblia na vitabu vingine vya kihistoria ukweli wa Siku ya Sabato (jumamosi). Na kama huo nao ni ujinga, acha niendelee kuitwa mjinga kwa huo ukweli na mwingine niliokwishasema huko nyuma. Na wito wangu kwako, jitahidi kuwa mfuasi wa neno la Mungu zaidi kuliko madhehebu. Utakapolitii neno la Mungu na kulifuata, utunzaji wa Sabato (na sheria zingine) utakuja automatically kama matokeo ya utii wako kwa sauti ya Mungu.
  Hapa nakunukuu tena, “Kwa hiyo wewe J’pili huwa husali unashidaga kama mpagani tu kwa sababu siku hiyo ukisali unakuwa umevunja sabato?”
  Jibu
  Kwani malaika wa mbinguni hawakuwa wanasali siku zingine (zile sita) kabla ya siku ya Saba wakati wa juma la uumbaji? Hivi Yesu alipowaambia wanafunzi wake “kesheni….” kwa maana ya salini kila saa/siku, aliwaambia wazifanye Sabato saa/siku zote za juma? Au Yesu hakuwa anasali siku zingine isipokuwa siku ya Sabato tu? Kama alikuwa anasali, je, alizifanya sabato pia siku hizo (alizokuwa akisali)? Acha kudanganyika rafiki yangu Sungura. Pamoja na kusali siku zote, kuna siku moja maalumu ndani ya juma, ambayo ni maalumu (takatifu) kwa Mungu tu – siku nzima. Haipaswi kuchanganywa na kazi yoyote ile tofauti na kumwabudu Mungu tu. Haipaswi hata watu kufikiri mawazo yao mengine tofauti na utakatifu wa ibada tu kama Mungu anavyoagiza, “Kama ukigeuza mguu wako usihalifu sabato, usifanye anasa yako siku ya utakatifu wangu; ukiita sabato siku ya furaha, na siku takatifu ya Bwana yenye heshima; ukiitukuza, kwa kutokuzifanya njia zako mwenyewe, wala kuyatafuta yakupendezayo, wala kusema maneno yako mwenyewe; ndipo utakapojifurahisha katika Bwana; nami nitakupandisha mahali pa nchi palipoinuka; nitakulisha urithi wa Yakobo baba yako; kwa maana kinywa cha Bwana kimenena hayo” Isaya 58:13-14. Bwana ameahidi Baraka tele naam uzima wa milele kwa wale wote watakaoliskia neno lake.

  Swali lako lingine…
  “Tena je, mwalimu wako ndo kakufundisha hivyo kwamba kazi ya Neema ni kutusaidia kutopondwa mawe tukitenda dhambi?”
  Jibu
  Ni zaidi ya kutopondwa mawe. Maana unaweza kupondwa mawe na usife. Siyo mwalm aliyenifundisha, bali ni Mungu kwa njia ya neno lake. Amenifundisha kuwa, kazi ya neema (rehema kwa mtu asiyestahili), ni kunitoa kwenye cage ya dhambi (mauti) na kuniingiza kwenye uzima wa milele. Kuwepo kwa neema/rehemu hiyo, hakunifanyi niendelee kuvunja sheria. Nikiendelea kutoutendea haki huo msamaha wa dhambi (neema/rehema), nitakuwa sijaifahamu vyema kazi ya neema. Nikiendelea kuifanya siku ya j’pili kama siku ya ibada kinyume na sheria za mtoa neema, mtoa neema atanirudisha tu tena ndani ya cage ya dhambi(mauti), maana bado nitakuwa sijatambua kuishi sawasawa na sheria zake licha ya msamaha alioutoa kwangu. Ni rahisi kiasi hicho, huna haja ya kudanganyika rafiki!
  Swali lako…
  “Lini biblia ilikuagiza kuwa mtu akitenda dhambi usimpige mawe?”
  Jibu
  Ha ha ha haa!! Kama haijakataza, wewe bado unapiga mawe wadhambi kama fundisho la kiimani? Unazijua sifa za wale wanaopaswa kuwapiga mawe wadhambi? Ukiwa na sifa za hao wapiga mawe, hata wewe leo unaweza kupiga mawe mtu kama utamuona ametenda dhambi. Ngoja nikupeleke kwenye sifa za wapiga mawe ili na wewe ujitathimini uone kama una sifa za kupiga mawe watu… Yohana 8:7 Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, YEYE ASIYE NA DHAMBI MIONGONI MWENU na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe.
  Sasa tafakari ni akina nani waliompeleka huyo mwanamke kwa Yesu? Je, walikuwa ni wapagani, waumini tu wa kawaida au baadhi yao walikuwa ni viongozi wa dini? Utapata jawabu.
  Zaidi ya hayo, nazidi kukuona kuwa u mtu unayehitaji kujifunza zaidi Biblia kama alivyo Siyi. Kwa nni? Nakunukuu, “Kusema kwako kuwa sheria ambayo haiwezi kututawala ni sheria ya kupondwa mawe kwa mdhambi, unamaanisha kuwa shria ya dhambi na mauti yenyewe inaendelea kututawala. Sijui hilo hayo manrno umeyatoa wapi”.
  Mwitiko..
  Kwa muumini wa kawaida tu, hawezi kuchanganya haya mambo kama ulivyofanya wewe hapa. Wewe unafikiri, hata kwa sasa, ili mtu aonekane ametenda dhambi, huwa anavunja sheria zipi? Sheria za kafara au za maadili? Kama wewe unatawaliwa na sheria ya kupondwa mawe, ina maana bado unatoa kafara za wanyama rafiki? Kifo cha Kristo bado hakijawa na effect yoyote kwako? Kama hutoi kafara, na unasema kuwa sheria hiyo ya kafara (kupondwa mawe) bado inakutawala, … unachekesha kweli rafiki!! Hebu jifunze basi mambo haya, maana mmmh!!
  Kwa ufupi, kilichoondolewa msalabani, ni mauti ya milele kwa mdhambi iliyokuwa imemkabili tena bila ya kupata hata fursa ya kuomba msamaha. Kwa maneno mengine, kile alichokifanya Mungu kwa Adamu na mkewe bustanini Edeni baada ya anguko lao dhambini, kilikuwa ni kielelezo tu ya kile kilichofanyika msalabani. Adamu na Mkewe hawakuomba msamaha japo Mungu aliwapa fursa ya kufanya hiyo. Kimsingi hawakutubu tofauti na kurushiana lawama tu. Upendo na rehema visingekuwa tabia ya Mungu, Mungu angewaangamiza papo hapo baada ya wao kula tunda. Maana kabla hawajaasi, aliwaambia, “… hakika mtakufa…”. Rehema za Mungu zinawafanya waendelee kuishi hata baada ya kula tunda. Zaidi ya hapo, Mungu alitaka watafakari na kuona kama wangejutia/kutubu jambo ambalo halikufanyika. Ndivyo ilivyo leo kwa wadhambi (mimi na wewe Sungura), Mungu bado anaendelea kutupa fursa ya kutubu. Na tusipotubu na kuisikia sauti yake kwa njia ya neema yake aliyoifunua kwetu, tutarajie uangamivu tu.
  Ukisema kuwa sheria hii haikutawali, kimsingi kwa tafsiri hiyo uliyo nayo, nikwambie kuwa, unajichanganya sana rafiki. Hebu soma tena aya hiyo, “(Rom 8:2 -For the law of the Spirit of life in Christ Jesus hath made me free from the law of sin and death)” na Rom 6 : 14(For sin shall no longer be your master, because you are not under the law, but under grace)
  Tafsiri sahihi ya aya hizo;
  Kwa ufupi, sheria ya maadili (amri 10) inapokaa ndani ya moyo wako, kimsingi hutakuwa mtumwa wa dhambi tena. Ndani ya moyo ndimo dhambi huanzia. Unajisi (wa mawazo, matendo n.k.) huanzia ndani ya moyo wa mtu. Ndiyo maana Mungu kupitia kinywa cha Suleimani, anasema, “Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima” – Mithali 4:23. Moyo unapokuwa salama, hutawaza mabaya/dhambi. Huu ndiyo uhuru anaouzungumzia Paulo kwa wale walio ndani ya Kristo kikwelikweli (siyo kwa jina tu). Kwa wale walio ndani ya Kristo, sheria hii ya uhuru Mungu alishaiandika, ndani ya mioyo yao tayari. Paulo analiita kuwa ni agano la milele. “Hili ni agano nitakaloagana nao baada ya siku zile, anena Bwana, Nitatia sheria zangu mioyoni mwao, Na katika nia zao nitaziandika; Dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena kabisa.” Ebr 10:16, 17. Hivyo wale wenye walio na sheria ya Mungu ndani ya mioyo yao, hutawaona wamevunja Sabato ya siku ya Saba wala amri nyingine yoyote, maana sheria ya Mungu inakaa ndani yao. “Maana hili ndilo agano nitakaloagana na nyumba ya Israeli Baada ya siku zile, asema Bwana; Nitawapa sheria zangu katika nia zao, Na katika mioyo yao nitaziandika; Nami nitakuwa Mungu kwao, Nao watakuwa watu wangu” Ebr 8:10. Ukiwaona wanavunja, jua kuwa ni wakristo jina tu. Kwa hiyo kaka Sungura, huwezi kusema sheria iko ndani yako huku unalivunja neno la Mungu hadharani au kwa siri. Hiyo ni kufuru kubwa sana rafiki. Wapaswa kutubu!
  Swali lako la mwisho
  “Siyi hebu nijibu hili swali; dakika hii unaposoma na kunijibu una dhambi au hauna?”
  Jibu
  Soma Ebr. 8:10b. Unafikiri ni lini Mungu ataziandika sheria zake ndani ya Mioyo ya watu wake? Alishaziandika, anaziandika au ataziandika? Lini sasa???? Mungu huanza kuziandika sheria zake ndani ya mioyo ya watu wake pale wanapompa Kristo maisha yao. Na kwa vile mchakato wa uongofu (sanctification) ni wa taratibu, wapo waliofikia kiwango cha kutokuwa na dhambi kabisa na wapo walio kwenye mchakato wa uongofu na wale ambao bado kabisa hawajauanza. Kwa vile umeniuliza mimi, napenda kukwambia kuwa, mpaka sasa kila ninapojitathimini kabisa ndani ya moyo wangu, huwa najiona bado nina safari ndefu ya kwenda. Nasema hivyo kwa sababu kuna yale ninayokosea (kwa wenzangu na kwa Mungu) kama mwanadamu ama kwa kujua au la; yote haya huwa ni makosa mbele za Mungu. Yanahitaji kutubiwa kila saa. Mara nyingine, mawazo mabaya hunijia halafu nikayakemea kwa jina la Yesu; lakini haya nayo tayari huwa ni dhambi mbele za Mungu zinazohitaji kutubiwa. Mara nyingine hata nasahau kuwaombea watu wengine, maadui zangu na marafiki zangu, hizi nazo ni dhambi zinazohitaji kutubiwa. Kwa ufupi, kila siku najiona mpungufu rafiki yangu. Ndiyo maana najitahidi kila siku, kujionyesha kuwa nimekubaliwa na Mungu, kama mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, akitumia kwa halali neno la kweli -2 Timotheo 2:15.

  Na huu ndiyo ungekuwa wito wangu kwako Sungura, Haule na wengine wote; ya kwamba, tujitahini kujionyesha kama tunaenenda sawasawa na Neno la Mungu huku tukiachilia mbali hoja za kidhehebu na udini, mambo ambayo hayana wokovu ndani yake. Utiifu wetu kwenye Neno la Mungu ndiyo utakaotupeleka mbinguni na wala si dini wala dhehebu. Naomba nieleweke hivyo.
  Ubarikiwe Sungura na wengine na poleni kwa mkeka mrefu kiasi.
  Siyi

 135. Siyi,

  Ni hivi, hilo swali ulilotuuliza ni la kipuuzi. Na linakuonesha jinsi usivyojua hata usivyojua mifumo ya usomaji na uandishi wa simulizi. Yawezekana hujasoma Fasihi au ulisoma lakini ukabaki mjinga.

  Hilo swali ulishaniuiliza kwenye mada ningine inayohusu wokovu nikakujibu, lakini kwa sababu wewe unajdili huku ukiwa unajiaminisaana kuwa unachoamini kiko sahihi, kwa hiyo huwa hujadli kwa ajili ya kujifunza ili ubadilike ndio maana hata majibu yakinifu huwa huyaoni tunapokujibu.

  Ni mjinga tu wa Fasihi ndiye anayeweza kudhani kuwa Paul wakati anaongea hayo maneno alikuwa bado yuko chini ya dhambi.
  Huna tofauti na mwislam mwenye kuchukua aya ya 1Kor 15:15 (Moreover we are even found to be false witnesses of God, because we testified against God that He raised Christ, whom He did not raise,), na kuhitimisha kuwa sisi ni mashahidi wa uongo.

  Just kwa sababu ni mjinga wa kanuni za usomaji hakujua kuwa alitakiwa asome nini kimesemwa katika aya za mwanzo. Nawe Siyi ni mmojawapo wa watu wa namna hiyo.

  Ukisoma Warumi sura ya 6, utagundua Paul alikuwa anaelezea jinsi dhambi ilivyomtawala mtu kwa sababu ya uwepo wa sheria, na jisnsi sasa waliomwamini Yesu wamewekwa huru mbali na hiyo dhambi.
  Ndipo Paul kufika kwenye Rum 7:7b katika kuendelea kwake kuchambua hilo suala anabadili mtindo wa usimulizi kutoka kwenye nafsi ya kwanza wingi kuja kwenye nafsi ya kwanza umoja( yaani anajiweka hapo yeye mwenyewe) akielezea katika wakati uliopita jinsi dhambi ilivyoiteka hiyo fulsa ya uwepo wa sheria na kuzalisha tamaa mbaya ndani yake.( Verse 8)

  Na kufikia mstari wa 14, anaendelea kumwelezea huyo mtu aliyetawaliwa na dhambi katika nafsi ya kwanza lakini katika wakati uliopo.

  Ndipo kufikia sura ya 8 ya Warumi Paul anakiweka wazi kitu ambacho kimeharibu sheria ya dhambi na mauti, ambacho ni ile sheria ya Roho wa uzima iliyo katika Kristo Yesu. Na kama una akili unajua kabisa kuwa hiyo sheria ya Roho wa uzima haikuanza kufanya kazi kwa Paul wakati amefika Rumi, bali ilianza kufanya kazi ndani yake tangu siku Anania alipoweka mkono juu yake.

  Au wewe kuna mahali kwenye hiyo mistari umeona Paul anasema kuwa dhanbi itakoma ndani wakati tukinyakuliwa?

  Ndio kusema Paul hakuwa anasema hayo maneno kwa warumi huku akiwa bado yuko chini ya dhambi yeye mwenyewe. Ni mjinga tu ndo anaweza dhani hivyo.

  Upuuzi mwingine nimeouona unaendelea nao, unamwambia Haule kuwa hajamjua Mungu kwa sababu anavunja sabato na kusali siku nyingine ya jua.

  Sina namna nyingine ya kukuita Siyi, zaidi ya kukuita mjinga wa kweli ya Mungu.

  Ivi kusali J’mosi ndo kutunza sabato na kufanya ibada J’pili ndo kuvunja sabato?
  Kwa hiyo wewe J’pili huwa husali unashidaga kama mpagani tu kwa sababu siku hiyo ukisali unakuwa umevunja sabato?

  Tena je, mwalimu wako ndo kakufundisha hivyo kwamba kazi ya Neema ni kutusaidia kutopondwa mawe tukitenda dhambi?
  Lini biblia ilikuagiza kuwa mtu akitenda dhambi usimpige mawe?

  Kusema kwako kuwa sheria ambayo haiwezi kututawala ni sheria ya kupondwa mawe kwa mdhambi, unamaanisha kuwa shria ya dhambi na mauti yenyewe inaendelea kututawala. Sijui hilo hayo manrno umeyatoa wapi.

  Sikia, kisichonitawala ni sheria ya dhambi na mauti wala siyo sheria ya kupondwa mawe. Hiyo sheria ya kuponda mawe haijawahi kumtawala mtu.(Rom 8:2 -For the law of the Spirit of life in Christ Jesus hath made me free from the law of sin and death)

  Ona anavyosema hapa: Rom 6 : 14(For sin shall no longer be your master, because you are not under the law, but under grace)

  Siyi hebu nijibu hili swali; dakika hii unaposoma na kunijibu una dhambi au hauna?

  Siyi ni aibu wewe kumwambia Haule achangamke,

  Hujui tu, wewe ndo uko gizani!

 136. Kaka Haule,
  Nimekuona rafiki. Nimekusoma vizuri.
  Nami naja hivi;
  Kwanza, watu hawaokoki wanapokufa. Hiyo nayo ilikuwa ni imani potofu ya kukupeleka motoni tu rafiki kama hiyo uliyo nayo sasa. Najua unaona kama nakukejeli/kukutusi kama hutaangalia vizuri. Kumbe la! Najaribu kukuonesha kile usichokiona sasa japo wadhani unakiona ndg yangu. Twende taratibu tu kwa upendo na kheri kama ndg ndani ya Kristo..
  Pili, Kama ukishamkiri Kristo (wewe unasema kuokoka), ndiyo kuwa salama, kwa kweli unadanganyika sana kaka. Kimsingi tunapomkiri Kristo, ndipo huwa tunatangaza mashambulizi makali ya ibilisi dhidi yetu kuliko ilivyokuwa hapo nyuma. Acha mchezo kaka. Paulo mnapomsoma pasi na umakini mkubwa, kwa hakika mnapotea ndugu zangu. Sina uhakika kama na wewe Haule umefikia hata (angalau) kiwango cha Paulo na Petro, wafuasi wa Kristo. Mf. Paulo anasema;
  “Na sisi, kwa nini tumo hatarini kila saa? Naam, ndugu, kwa huku kujisifu kwangu niliko nako juu yenu katika Kristo Yesu Bwana wetu, ninakufa kila siku”. _ 1 Korinth 15:30-31 (cf. Rom. 7)

  Sasa, niambie Paulo alikuwa anakufa kila siku….!! Kila siku anapambana na dhambi! Kumbuka huyu ni mfuasi wa Kristo. Alishampokea Yesu na yote ya kwanza akasamehewa/yakafutwa. Alishaanza safari mpya ya kiimani, lakini bado anapambana na dhambi – anakufa kila siku katika mwili wa dhambi. Paulo angekuwa na falsafa uliyo na wewe pamoja na marafiki zako wengine, falsafa ya “Once Saved Always Saved”, Paulo asingesema maneno hayo. Aidha, ili kukuthibitishia hili, Paulo hakuwa anasema maneno yake mwenyewe. Alikuwa anafundisha fundisho la Kristo alilolitoa kwa wafuasi wake.Yesu alisema;

  “Akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate” – Luka 9:23. Kaka Haule, mtu anapomwamini Yesu, bado hajaokoka. Badala yake, huingia kwenye vita vikali zaidi vya kiroho kuliko ilivyokuwa kabla/hajaamini. Katika Injili ya Mathayo, Yesu aliiweka vizuri kauli hii;

  “Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona. Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake? Kwa sababu Mwana wa Adamu ATAKUJA katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake” – Mathayo 16:24-27.

  Yesu mwenyewe hakuwaambia wanafunzi wake kuwa “kwa vile mlishaniamini, tayari mmekwishaokoka”. Hakusema hivyo. Bali alitoa mwelekeo wa safari ya imani na miisho yake. Yesu anawaambia ATAKUJA….kumlipa kila mtu… Hii ndiyo konsepti sahihi ya wokovu kaka Haule. Tunapomwamini Kristo kwa sasa, kimsingi tunaanza safari mpya ya kiimani tu kuuelekea uzima aliouahidi Kristo mwisho wa wakati.

  Hiyo maana unayoipata kwenye 2Pet2:21-22, kimsingi unailazimisha tu ikubaliane na mtazamo wako. Maana mafungu hayasemi kuwa mtu akishamwamini Yesu, tayari maeshaokoka. Yuko huru na salama ilhali yuko duniani. Aya hizi hazisemi hivyo kaka. Hebu tuzione sote,
  “Maana ingekuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa.
  Lakini imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli, Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaa-gaa matopeni”.
  Aya hizi zinatoa onyo kwa wale wanaorudi kuwa hai katika ulimwengu wa mwili (wasiokufa kila siku) ilhali ni waumini. Wale wasioweza kuubeba msalaba wa Kristo kila siku. Wale walioijua kweli halafu wasiiishi, hao ndiyo wako hatarini maana ingekuwa heri wasingeijua kweli. Kwa ufupi, maisha ya kumwamini Kristo, ni maisha ya vita muda wote hadi Yesu atakapokuja kutokoka – kututoa duniani.

  Tatu, Ukisema kuwa waumini wa Kristo hawapaswi kutenda dhambi, wasema vyema kabisa. Adamu naye hakupaswa kukiuka sheria za Mungu bustanini. Lakini unajua kilichotokea baadaye. Yohana aliyeishi na Kristo anatushauri kwa kuzingatia hali yetu ya kibinadamu kuwa, “Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki” 1 Yohana 2:1. Wito wa Mungu kwa wanadamu wote, ni kutozivunja amri zake. Cha ajabu, hawa wanadamu walishauzwa kwenye zizi la ibilisi (dhambi). Wana asili ya dhambi. Wana mawazo yaliyo najisi muda mwingi. Kama Mungu angeamua kuwatupilia mbali mara, nadhani hata wewe leo usingekuwa hai. Neema ya Mungu inatulinda tu ndg yangu ili tupate kutubu (kufa kila siku ktk mwili wa nyama) na kisha tuwe hai ktk roho. Na huku ndiko kuenenda ktk roho unakokusema kaka ktk Gal 5.16 -18.

  Nne, Unapokuwa kwenye Frekwensi moja na Kristo ukiwa bado duniani, haina maana kwamba uko salama kaka. Bado shetani atakuandama tena kila dakika. Na mimi sishabikii kuwa, kuandamwa huko ndiko kukuangushe. Hasha!! Ninachosema ni kwamba, Haijalishi uko karibu na Kristo kiasi gani, maadamu upo duniani, tarajia majaribu ya shetani au tests kutoka kwa Mungu mwenyyewe. Vita hiviepukiki kaka. Amani na tumaini la ushindi ktk mapambano hayo, tunalipata katika wafili 4:13. Ukisema umeokoka (uko salama) ilhali uko kwenye uwanja wa vita, hata ndege watakucheka. Na kwa kukwambia ukweli tu, hakuna ukamilifu nje ya njia sahihi. Huko ni kudanganyana tu. Mtu asipoamua kumfuata Kristo kila aendako, hakika yake ni uangamivu tu. Na mtu asikudanganye kuwa eti ukiwa msabato, m-EAT, mlutheri, nk ndiyo utaenda mbinguni. Kuna imani moja tu kama alivyo Mungu mmoja ambaye na Baba wa wote wanaomkiri na kumfuata hatua kwa hatua. Nikwambie tu kuwa, kuna baadhi ya watu wanaosali jmosi lakini watachomwa moto tu. Kwa nini? Kwa sababu walibweteka kwa kuitwa wasabato na hivyo kuendelea kwenye uovu fulani uliokuwa umezoeleka kwao na kuuona kama ni sehemu ya maisha yao ya kila siku. Binafsi sikuiti ili uwe msabato. Nakuita ili uwe mfuasi halisi wa Kristo. Uifuate Biblia. Mfuate Mungu rafiki yangu. Nadharia za wanadamu (in relation to the Bible) zitakupoteza hakika!!

  Tano, sheria ya Mungu inapokaa ndani ya mioyo yetu, huko ndiko kumpendeza Mungu. Hakuna kitu kingine kinachomfurahisha Mungu kama hicho-kuishi sawasawa na sheria yake ya upendo. Na kimsingi tunapoishi kiroho, ina maana tunaishi kwa kufuata sheria sheria za Mungu zilizo mioyoni mwetu tayari. Hatuongozwi na mwili, bali roho. Kwa hiyo, kwa maneno mengine, kuishi kiroho, ni kuishi kwa kufuata sheria za Mungu kwa msukumo wa moyoni ambako sheria/torati yake hukaa. Unapoishi kinyume na kile kilichomo moyoni(torati/sheria ya Mungu), kimsingi wewe ni muasi. Hata kama unajitahidi sana kushika amri zote lakini ukajikwaa ktk moja, bado wewe ni muasi. Ndiyo maana hata wewe kaka Haule, nasikitika kukwambia kuwa, bado hujamjua Mungu, maana bado sheria ya upendo haipo moyoni mwako. Unavunja sabato ya Mungu, na kusali siku nyingine ya jua. Sasa utajiitaje mkamilifu katika upotovu rafiki yangu? Kama maagizo ya torati yalishatimia ndani yetu, na kwamba tunapaswa kuishi kiroho( kwa kufuata kile kilichowekwa ndani yetu automatically), kwa nini bado unaufuata mwili kama kweli sheria ya Mungu iko ndani yako? Kama si uongo/kudanganyana ni nini hicho?

  Sheria ambayo haiwezi kututawala tena, ni ile sheria ya mwilini (sheria ya kupondwa mawe kwa mdhambi). Sheria inayotutawala sasa, ni ile iliyo ndani ya mioyo yetu (sheria ya Mungu ya maadili). Sheri ambayo ukiivunja, unaonekana mkosaji pamoja na kwamba hautapondwa mawe (kwa maana uko chini ya neema). Mimi nakushauri kuachana na falsafa za kidini/kidhehebu na kimtazamo. Acha neno liseme lenyewe. Msikilize Mungu na si wanadamu.

  Nami nakungoja ili tusemezane kungali ni mchana. Maana usiku waja, ambao Siyi hutamsikia tena akisema habari njema za wokovu. Changamka ndg yangu.
  Ubarikiwe pia
  Siyi

 137. Asante Kaka Siyi……
  Unajua Mimi na Wewe tuko ktk frikwensi mbili tofauti

  Mimi nilishaishi maisha bila wokovu(kuzaliwa kwa mwili) ambayo wewe wayaishi sasa na
  kungoja kuokoka ukisha kufa,
  Nilikuwa mkristo kwa kuzaliwa, Nilikuta wazazi wana dini yao nami nikawemo humo.
  Sasa injili ya wokovu ikanizukia……..Nuru imeniangazazi,Naijua kweli nayo imeniweka huru,kwa hiyo kuna shida kubwa ya kuelewana Mimi na Wewe si ndogo kwa kweli…….Lakini twende kazi

  Umeandika mengi kaka Siyi kwa leo tuanze na hili……..
  Tafakari haya maandiko yako halafu linganisha na maandiko yanavyotufundisha
  na kutuhekimisha,Uone ulivyopotoshwa au unavyopotosha.

  Bro Siyi…..umeandika
  Pamoja na kwamba kwa njia ya kumwamini Kristo tunaweza kuponywa magonjwa, hii haina maana kwamba hatutaugua tena!! Tunaweza hata kufufuliwa katika wafu, hii haina maana kwamba, hatutakufa tena. Na baadhi yetu tunapomwamini Yesu, huachana na dhambi k.v. za ulevi, uzinzi, nk lakini baadaye (kwa vile bado tuko vitani), hujikuta tukianguka na kurudia matapishi. Tukisema kuwa tumeokoka katika hali hii, kimsingi tunaidhalilisha kazi ya Kristo

  Haya ni majibu ya Maandiko…….si yangu

  2Pet2:21-22
  Maana ingekuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa.
  Lakini imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli, Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaa-gaa matopeni.

  Wewe Bro Siyi….haya maandiko hayakuhusu kwa kweli…si ndivyo….utakubaliana nami
  kwa hilo hakuna shaka hata kidogo kwa hayo maandishi yako.

  Unapingana na Roho Mtakatifu&Neno kwa mafundisho yako…..walimu wa uongo walizungumzwa kwenye 2Pet2:1-14.
  Waliookoka hawaruhusiwi kuanguka na kurudia matapishi….si unaona tofauti yetu waliookoka
  na wasio okoka……..Tuliokoka tunapewa onyo ingekuwa heri tusingeijua njia ya haki,
  Kaka Siyi…..unaona jinsi gani ulivyo chini sana.hakuna injili ya kweli kwako inayonifanya kuwa mtauwa.

  Waliokoka maandiko yanawaambia hivi….

  Gal 5.16 -18
  Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.
  Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.
  Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria.

  Sio watu wote wanaoshindwa na dhambi,haya maandiko si yako,wenyewe ni hawa….

  Jn3.8 Upepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho.

  Bro Siyi aliyezaliwa kwa mwili ni mwili…..ndivyo ilivyo…..unayarudia matapishi sawa rudia……….

  Ukipokea Wokovu utaisikia hiyo brodikasti ya Roho Mtakatifu ya kwenenda kwa roho……maana utakuwa katika network/frikwensi moja naye,Jaza kiriba mafuta kabla ya Bwana harusi kuja….maana yangu zaliwa mara ya pili(okoka)……. Ndio toka huko kati yao……Tatizo unadhani kuwa hakuna wakamilifu……Sikia wito huu wa Bwana

  Yesu akamwambia, Ukitaka kuwa mkamilifu, enenda ukauze ulivyo navyo, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate.”Math19:21

  Bro acha huu utajiri wa dini/madhehebu

  Bro Siyi torati ni ya rohoni asili ya ni Roho Mtakatifi na imetoka kwa Mungu amabaye ni ROHO…….Soma vizuri huo mstari Rum7:14b

  Tulikuwa watu wa mwilini, na kuuzwa chini ya dhambi.
  Torati inamtawala mtu anapokuwa hai ……Lakini sisi tuliompokea Bwana Yesu tuliifia torati kwa njia mwili wake Kristo….hili torati itimie mwilini mwetu
  Rom7:4-5 Kadhalika, ndugu zangu, ninyi pia mmeifia torati, kwa njia ya mwili wa Kristo, mpate kuwa mali ya mwingine, yeye aliyefufuka katika wafu, kusudi tumzalie Mungu matunda. Kwa maana tulipokuwa katika hali ya mwili, tamaa za dhambi, zilizokuwako kwa sababu ya torati, zilitenda kazi katika viungo vyetu hata mkaizalia mauti mazao.

  Yesu alichukua adhabu yetu mwilini mwake kwa sababu nyingi moja wapo ni hii ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho.

  maandiko yanaandika Kolosai3:3
  Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu.
  Sasa kwa kufuatana na Rum 7:1 sheria(torati) haiwezi kututawala,
  Kwa hiyo tunavifisha viungo vyo mwili kwa uweza ya RM,Ambavyo hapo kale nasi tulitembea ktk hivyo tulipoishi ktk dhambi,Tunamshukuru Mungu kwa Yesu kristo aliyetuandika huru,Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili ile sheria ya uhuru uliyo ndani yake kristo imetuacha huru mbari na sheria ya dhambi na mauti.

  Mungu kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili.

  Basi …….Bro Siyi kwa sasa sina nafasi pande hizi za SG….Niko na shughuli nyingi zia Kanisa/Taifa/Familia nitakuja siku chache zijazo tutafakari hayo unayoyatetea yamkini kwa mapenzi ya Mungu mkuu na Mwokozi wetu Yesu Kristo utafunguliwa

  Barikiwa

 138. Kaka Haule,
  Siko kwa ajili ya kumjaribu mtu. Hasha!!
  Huwa napenda sana kuuliza maswali kwa sababu naamini kwa kiasi Fulani huwa najibu maswali yangu kwa kuwauliza watu maswali ambayo kwa kiasi fulani (japo kidogo) huwafanya watafakari zaidi, badala ya kushikilia misimamo yao waliyonayo. Na hata kwako pia, ninajibu kwa mtindo huohuo…
  Umesema kuwa, waliambiwa watu (waumini wa enzi hizo) waliokuwa chini ya sheria-agano. Kimsingi mimi sipingani na wewe. Ninachotaka ukione ni kile anachokisema Paulo aya ya 14 “Kwa maana twajua ya kuwa torati asili yake ni ya rohoni; bali mimi ni mtu wa mwilini, nimeuzwa chini ya dhambi”. Sasa kama tulitoka kwa Bosi wetu wa kwanza (torati ya rohoni) na kuuzwa kwa bosi mwingine (mauti), kwa nini tuseme kuwa tuko salama (kimwili) ilhali rohoni hatujarejeshwa (torati haijaandikwa tena ndani ya mioyo yetu? – Waebrania 8:10). Kama Paulo alikuwa muumini tayari, mhubiri injili kwa leo tungemwita mchungaji, je, andiko hili (Warumi 11:27 Na hili ndilo agano langu nao, Nitakapowaondolea dhambi zao), lilikuwa limetimia kwa Paulo na waumini wengine? Kama ni ndiyo how na kwa nini Paulo aseme maneno hayo? Kama jibu ni hapana, yalikuja kutimia lini, hayakutimia kabisa au yatatimia lini?

  Nimekuwa pamoja nanyi kwa muda kitambo sasa. Nimewasikia sana mkisema akina Siyi, Mjema nk ni watu wa mwilini, maana ni washika sheria za mwilini. Swali lingine la nyongeza hapa, kama torati asili yake ni ya rohoni, huoni kuwa Mungu huwa anawashangaa sana mnapowadharau akina Siyi wanaoshika sheria ya Mungu ambayo asili yake ni ya rohoni? Ninyi mnashika nini basi ambacho hakiko chini ya agano (torati)? Je, ni nani aliye wa mwilini kati yetu na ninyi? Au huwa mnasema kuwa ni watu wa rohoni ilhali hamjui maana ya kuwa mtu wa rohoni kwamba ni kuwa mshika torati?

  Sura ya nane ya Warumi 8, Paulo anatoa wito wa watu kuishi kwa mujibu wa Maisha ya tangu mwanzo (maisha ya watu waliyoishi torati ikiwa ndani ya mioyo yao). Ameonesha gharama (kifo cha Kristo) iliyotolewa kwa ajili ya kuturejesha kwenye maisha hayo baada ya kuteseka sana katika utumwa wa dhambi. Kwa maana wale watakaoishi kwa kufuata mfumo huo wa rohoni (torati ikiwa ndani), ndiyo watoto wa Mungu “Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu” – Rumi 8:14.

  Na ili tufikie hatua ya kuishi kiroho, sharti kuna process-safari ya kiimani. Mabadiliko haya kwa walio wengi huchukua muda mrefu sana. Wengine wanapomwamini Yesu, huacha pombe, nguruwe, uzinzi nk (dhambi zinazoonekana kwa macho) na baadaye huenda zaidi ya hapo (kuacha dhambi zisizoonekana kw macho i.e wivu, husuda, mawazo mabaya, hasira n.k.) ili kufikia hatua ya utakatifu kuanzia ndani ya moyo wa mwanadamu. Mabadiliko yote haya, huhitaji muda na rasilimali zingine nyingi. Pamoja na kwamba kwa njia ya kumwamini Kristo tunaweza kuponywa magonjwa, hii haina maana kwamba hatutaugua tena!! Tunaweza hata kufufuliwa katika wafu, hii haina maana kwamba, hatutakufa tena. Na baadhi yetu tunapomwamini Yesu, huachana na dhambi k.v. za ulevi, uzinzi, nk lakini baadaye (kwa vile bado tuko vitani), hujikuta tukianguka na kurudia matapishi. Tukisema kuwa tumeokoka katika hali hii, kimsingi tunaidhalilisha kazi ya Kristo. Kristo akituokoa hatuwezi kuendelea kuteseka na matokeo ya dhambi kaka Haule. Kwa vip? Kwa sababu tutakuwa tumetoka ndani ya gereza(dunia). Yesu amekuja kutufungulia gereza la dhambi. Ili tuweze kuokolewa, ni mpaka tulione lango lililofunguliwa(tumwamini Yesu). Na tukishaliona, tuamue kutoka ndani ya gereza hilo (mchakato). Tukifanikiwa kutoka(kufikia ukamilifu), Yesu atatuijia na kutukaribisha kwake. Kwa sasa hatuwezi kusema kuwa tumeokoka ilhali bado tuko ndani ya gereza la mauti (dunia). Tutakapotoka nje ya gereza hili, mbingu zitashuhudia, malaika watashuhudia, wanadamu watashuhudia na hata sisi wenyewe tutashuhudia na kukiri kama Paulo alivyokiri baada ya safari yake ndefu ya kiimani kufikia ukamilifu, “Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake” 2 timothy 4:7-8. Isivyo bahati, Paulo alilala kama akina Ibrahimu akiingojea ile ahadi. “Hawa wote wakafa katika imani, wasijazipokea zile ahadi, bali wakaziona tokea mbali na kuzishangilia, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya nchi” – Waebrania 11:13.
  Sasa hivi tulishaanza safari ya kutoka gerezani (tu wageni juu ya nchi). Hatujaokoka bado. Tutaokoka tukifika nyumbani. Jambo la kutia moyo ni kwamba, tumekaribia nyumbani. Tujipe moyo rafiki!

  Hii ndiyo safari ya kiimani.
  Nakungoja kwa makala uliyosema
  Ubarikiwe

 139. Bro Siyi
  unauliza unataka kufahamu au kutujaribu….kwani wewe ni mjaribu!!1
  …..au ni kweli kuwa haujui/hufahamu na hivyo hii andiko Rm.7:15-20 lime kuua kabisa kiasi huamini kuwa hakuna wokovu duniani!

  Hujui hata Paul alikuwa anawazungumzia watu gani!!!!!!?

  ameandika………..
  Rm.7:1
  Ndugu zangu, hamjui (maana nasema na hao waijuao sheria) ya kuwa torati humtawala mtu wakati anapokuwa yu hai?

  Hii sura ni mahususi sana kwa ajili ya wale Waakovu walioshi ktk sheria ya torati kabla ya kuokoka(kuoshwa na damu ya Yesu,walifungwa na agano), hata kama kwa kiasi sisi mataifa inatuhusu.(Nitakuja kueleza baadaye inavyotuhusu sisi mataifa)

  Kwani wewe Siyi linakuhusu nini agano la Yakobo nawe ni mzabibu mwitu!!!!?

  Maswali yote ya Rm.7:15-24 na swali analojiuliza Paul nani atamuokoa na mwili wa mauti(nguvu ya dhambi)

  Ujauona!!!? mstari wa Rm.7:25 akipata jibu“through Jesus Christ our Lord.”

  Sura ya 8 ina majibu ya tatizo la nguvu ya dhambi ktk mwili iliyoonyeshwa ktk sura ya 7

  Rm.8:1-4
  Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.
  Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.
  Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili;
  ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho.

  Rm.7:6Bali sasa tumefunguliwa katika torati, tumeifia hali ile iliyotupinga, ili sisi tupate kutumika katika hali mpya ya roho, si katika hali ya zamani, ya andiko.

  God fulfills His promises through Jesus Christ; He liberates His people and fulfills the law in Himself. The solution to the sin capacity problem rests in the work of Christ on the cross and the gift of the indwelling Holy Spirit

  Jn.5.24
  Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani.

  Eph.1:13-14
  Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi aliye Mtakatifu.Ndiye aliye arabuni ya urithi wetu, ili kuleta ukombozi wa milki yake, kuwa sifa ya utukufu wake.

  Vipi!!
  Bro Siyi……unauliza maswali yenye majibu sura inayofata,
  msipende kutumia mistari ya kukata tamaa ndiyo mnayokazania kuwa wokovu haupo duniani mpaka uwe umekufa.

  Mungu akipenda…..
  Nitakuja kujibu maswali yako kwa yale ninayofahamu.

  Barikiwa.

 140. Sungura, Lwembe, Seleli and your company as well
  Kama kuokoka ni kuondolewa dhambi, Je, Paulo alikuwa ameondolewa au bado unapomsoma Warum 7:15-20?
  Je, tunaweza kuwa tunaokoka kila siku pindi tunapoondolewa dhambi tulizozotenda kwa kujua au kutokujua?

 141. Inaendelea….

  Mjema,

  Sasa, mwangalie huyo aliye Jeshi la Mungu. Mungu hahitaji marundo ya watu ili aitimize Azma yake, wokovu wa watu wake! “Daudi akaongea na watu waliosimama karibu, akisema, Je! Atafanyiwaje yeye atakayemwua Mfilisti huyo, na kuwaondolea Israeli aibu hii? Maana Mfilisti huyu asiyetahiriwa ni nani hata awatukane majeshi ya Mungu aliye hai?” (1 SAM. 17:26) Daudi ndiye “Majeshi ya Mungu aliye hai”!

  Inachukua kumjua Mungu, ule Moyo wake, ndipo jambo la wokovu wako linapoweza kuwa halisi, vinginevyo unakuwa unaongelea mambo usiyoyajua kama hayo majeshi yaliyojikunyata, hayana tena hata uwezo wa kupiga zile ‘kelele za vita’; zile silaha za ukweli, zenye kufikiwa rohoni, walijidhania wanazo; kumbe masikini ni watupu, kilicho hai ndani yao ni ile Nia ya kuyapinga yote yaliyo Kweli ya Mungu, hiyo ndiyo roho wanayopewa “Mgambo wa dini”! Mtazame kaka yake Daudi, huyo aliye ktk hao mgambo wa Sauli; hapo ningemchukulia Daudi kwamba ni Mpentekoste mdogo, nao kaka zake ndio hao Wakatoliki, Wasabato na makundi yote yenye kuupinga wokovu: “Naye Eliabu, mkubwa wake, alisikia hapo alipoongea na watu; na hasira yake Eliabu ikawaka juu ya Daudi, akasema, Mbona wewe umeshuka hapa? Na kondoo wale wachache umemwachia nani kule nyikani? Mimi nakujua kiburi chako, na ubaya wa moyo wako; …” (1 SAM. 17:28)

  Unawaona! Unapowaambia Habari Njema za Wokovu, huo unaokuingiza ktk Ufalme wa Mungu hapa duniani, huo unaoziwezesha zile Ishara halisi kufuatana nawe, wao hukuona ni mwenye kiburi cha Uzima, tena huenda mbele zaidi wakakuambia kuwa unayafanya hayo kwa pepo, yaani una roho mbaya, kama kauli ya Eliabu juu ya Daudi, huyo aliyepakwa Mafuta, ilivyokuwa, ndivyo ilivyo hata leo hii, Roho wa Mungu mwenye kuzifanya hizo Ishara, wao humwita ‘pepo’, ile KUFURU!!!

  Haya, iangalie hiyo final encounter, usikilize kwa makini Unabii anaotolewa Goliathi, labda utakuonesha kwa sehemu jinsi Mungu alivyouficha wokovu usitambulikane kwa mgambo!
  “Mfilisti akamwambia Daudi, Njoo huku kwangu; nyama yako nitawapa ndege wa angani na wanyama wa mwituni. Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la BWANA wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana. Siku hii ya leo BWANA atakuua mkononi mwangu, nami nitakupiga, na kukuondolea kichwa chako, nami leo nitawapa ndege wa angani na wanyama wa nchi mizoga ya majeshi ya Wafilisti, ili kwamba dunia nzima wajue ya kuwa yuko Mungu katika Israeli. Nao jamii ya watu wote pia wajue ya kwamba BWANA HAOKOI kwa upanga wala kwa mkuki; maana VITA NI VYA BWANA, naye atawatia ninyi mikononi mwetu.” (1 SAM. 17:28, 44-47)

  Daudi anavijua vita katika utoto wake kuliko hao manabii na mitume na makusanyiko yao waliyoyapindisha na kuyoondoa katika Imani, kama hilo la Sauli anayetegemea mafunzo yake ya mwilini kuvipiga vita vya rohoni!

  Umeelewa Mjema? Daudi hajasema kwamba yeye ndiye atakaye muua huyo Mfilisti, anasema “BWANA atakuua mkononi mwangu”!!! Huyo hapo ameokota mawe matano, 5 ni namba ya Neema, nayo Neema hiyo kwa Israeli ndiyo huyo Daudi!! Tazama hiki anachokionesha Isaya huko nyuma, akiizungumzia siku yetu ya leo, akiutazama huo wokovu uliojivingirisha katika Neema, 53:5 ” 5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.” Unaona, yooote ameyafanya Kristo, wewe pokea tu ndg yangu, legeza shingo hiyo!!!

  Petro pia, kwa Roho yule yule aliyeutoa unabii huu kwa Isaya, analirejea Neno hilo katika kutimia kwake na sasa akiniandikia mimi Lwembe leo hii, ninapoujia wokovu, akinirudisha huko nyuma ili niungane na Sadaka iliyotolewa kwa ajili yangu na kisha niyapokee kwa shukurani yoooote niliyokirimiwa kabla ya misingi ya ulimwengu kuwekwa, ule Wokovu wangu. Ndio huu udhihirisho ninaouishi leo hii, kwamba ninapoumwa, basi mimi hulirejea lile Neno la wokovu wangu, na kuupokea uponyaji wangu uliofanyika miaka elfu mbili iliyopita; 1Pet 2:24 “… na kwa kupigwa kwake mliponywa.” Sio tutaponywa, hapana Tuliponywa huko nyuma katika siku ile alipopigwa; yaani niliponywa kabla sijazaliwa!!!!! Kilicho bakia kwangu ni kuupokea uponyaji; vivyo wokovu, niliokolewa kabla ya misingi ya ulimwengu kuwekwa na sasa ninaupokea tu leo hii, na kuyafaidi matunda ya kazi ya Bwana; yaani sipigani vita ila nakusanya spoils!!!!.

  Mjema, maana rahisi ya wokovu ni kule kuondolewa dhambi zangu, sio kusamehewa, hapana, KUONDOLEWA!! “24 Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti …” Basi dhambi zangu zikiisha kuchukuliwa na Yeye, mimi nabakia na Utakatifu wake, huo anaonipa hapo anapozichukua dhambi zangu, ndiko huko kuwa hai kwa mambo ya haki nikitolewa kutoka kundi la wafu wanaoukataa wokovu, nikurejea kwa Mchungaji na Mwangalizi wa roho zetu!

  Nako kurejea huko ndio ile Raha na Burudisho mlivyovikataa!!!

  Gbu!

 142. Mjema
  Asante kwa kuyapokea maelezo yangu kuhusu wokovu!

  Hata hivyo, naona hujayaelewa vizuri ktk kina chake! Ninaona hivyo kutokana na comment zako haswa kuhusu “Mgambo wa dini”. Nilikuambia kuwa ktk Jeshi la Mungu HAKUNA “mgambo” humo, sasa unaponiambia kuwa Mungu atawatumia hao walio “mwilini” ktk vita ya kiroho, ndipo nimegundua kuwa hata Jeshi la Mungu lenyewe hulijui sawa sawa!

  Mfano wa David na Goliath ulioutumia ni mzuri sana iwapo tu unalijua Jeshi la Mungu likoje, maana mfano wako huo unayaonesha majeshi yote mawili; Mgambo wa dini na Super Jeshi la Mungu katika hayo makabiliano ya kivita!

  Sauli alipomuasi Mungu alibakia na dini. Alikuwa ni jemadari wa hilo jeshi lake ambalo kwa kuikosa ile Nguvu ya Mungu, walibakia kuwa “Mgambo wa dini” licha ya wao kujidhania kuwa ni Jeshi la Mungu! Unajua, mara nyingi sisi hujiaminsha ktk kuyajua mambo ya Mungu, hata kujiona tu sehemu yake, kwa kuyaamini mafundisho ya makusanyiko yetu ambayo kwa kuyapokea, ndani yetu hujengeka Nia ya kuyakataa yote yanayotofautiana nayo, hata ikiwa ni Neno la Mungu; ndipo macho yetu ya kiroho hupofuliwa kwa ridhaa yetu wenyewe!!!
  “Na watu wote na watoza ushuru waliposikia hayo, waliikiri haki ya Mungu, kwa kuwa wamebatizwa kwa ubatizo wa Yohana. LAKINI, MAFARISAYO NA WANA-SHERIA WALILIPINGA SHAURI LA MUNGU JUU YAO, KWA KUWA HAWAKUBATIZWA NAYE.” (LK. 7:29, 30).
  Dini yao iliwazuia kuupokea wokovu, wakabaki huko nje wakiendelea kuupinga kwa gharama ya nafsi zao, kama ilivyo leo hii!

  Jeshi la Sauli lilipotoka kwenda vitani, walijiamini kwamba wanao uwezo, ile Nguvu, maana waliamini kwamba wao ni Jeshi la Mungu, kama ambavyo nasi makundi yetu, hayo yanayo ukataa Wokovu yalivyo leo hii! Basi, Israeli wote nao walikuwa nyuma ya jeshi lao, ndio maana unamuona Daudi akitumwa kuwapelekea chakula huko, waliamini kwamba Mungu atawapa Ushindi, maana wao ni waokovu wake, kwa falsafa ya dini yao!

  Kijana Daudi alipotumwa huko kambini kwao, aliwakuta wakitoka kwenda vitani, “Daudi akaondoka asubuhi na mapema, … akafika penye magari, wakati lile jeshi walipokuwa wakitoka kwenda kupigana, wakipiga kelele za vita.” (1 SAM. 17:20)

  Unawaona! Wanapiga kelele za vita!! Hata Daudi alipowaona aliridhika kwamba hao ni Jeshi la Mungu; hata wewe Mjema, usingewaza tofauti! Wamefanya ibada zote, wamejikaririsha vifungu vyote vya Sheria, bila ufahamu, na sadaka za kuteketeza wametoa, tena sabato ile walikesha hekaluni kwa mambo hayo!! Hao hapo wanapiga kelele za kumpokea Kristo, wanasema ndiye Jemadari wao, wameoshwa kwa Damu yake, wamejaa Nguvu zake! Tena ungezisikia kelele zao, ungedhania wananena kwa lugha kama wanavyojikaririsha uongo!

  Lakini, ilipowadia ile final showdown, kelele na tambo zao vyote vikatoweka, huyo Mungu waliyedhani wanamuabudu na kumtolea sadaka zao akawa ni mungu wa hadithi, aliyewakirimia intellectual faith iliyowafikisha ktk kiwango cha kuwa “mgambo wa dini” tu: hawajawahi kumwamini Mungu mioyoni mwao! Mungu anafikiwa kwa Imani tu, nayo Imani hukaa moyoni; “Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.” (MK. 16:17, 18); Halelluyaaaaaa!!!

  Alipowatokea yule pepo anayeitwa Goliathi, akawashushia matusi na kejeli, “… watu wote wa Israeli walipomwona yule mtu wakakimbia, wakaogopa sana.” (1 SAM. 17:24). Unawaona hao mgambo waliojidhania kuwa ni Jeshi, wanasema, Ishara hizo zilikwisha na mitume, wakasema Yesu alituambia tutatoa pepo akija mara ya pili kutuchukua, wakanukuu vifungu vya Maandiko bila Maarifa huku wakikimbia!

  Hivi unajua kuwa hata mtume Paulo, hapo alipokiitwa Sauli, naye pia alikuwa ni mgambo wa dini?!!!!

  Inaendelea….

 143. Hahahahahaha…..! Haule, nakuona ulivyopanda juu, juuuu sana ambako kunguru wa dini hawezi kufika, akijaribu mbawa zitamnyofoke; huko Heavenly places in Christ Jesus, huko kwenye pumziko, ile Sabato, katika ile raha yetu, tuliyopewa, kile kiburudisho cha ule uchovu wa kubeba madude ya dini tuliyobebeshwa huko utumwani!!!!

  Na kwa huyo aliyeikataa hiyo raha, ule wokovu wenye kuburudisha; huyo asiyetaka kulisikia neno hilo:
  “Kwa sababu hiyo neno la BWANA kwao litakuwa hivi, amri juu ya amri, amri juu ya amri; kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo; ILI WAENDE NA KUANGUKA NYUMA, NA KUVUNJWA, NA KUNASWA, NA KUCHUKULIWA.”

  Hahahaha….. spiritually wamechukuliwa na mizimu, down into the abyss, no wonder hawana uwezo wa kusikia wala kuelewa chochote!!

 144. Mjema,
  Binafsi sijaelewi haja yako ni nini!
  kuniwekea maneno mdomoni kana kwamba ya kwangu,

  Ni vema mtazamo wako ulinganishe na neno la Mungu linasema nini,Maandiko niliyoandika ktk post zangu ni neno la Mungu,nilijibu kulingana na maswali/yaliojiri,
  siwezi kujibu unavyotaka wewe najibu kulingana na neno la Mungu,

  Wapi mimi niliandika wokovu ninaoamini mtazamo wake hakuna
  kutakaswa/kutukuzwa umepata ujasiri huo!

  Mimi siwezi kuchagua/kutafsiri maneno ya Mungu kama vile unavyofanya wewe kuwa wokovu baada ya kufa.

  ndio maana tuliangalia hizo tense kupitia maandiko tukaona kuwa ni hekima ya kibinadamu tu.

  Sikubaliani na mtazamo ulionichagulia,huo utofauti unaouona ni wa kwako unaopingana na maandiko/neno la Mungu

  Umeandika….

  “Utofauti wetu wa mtazamo upo hivi:
  Wenu: Wokovu= Kumpokea/Kumkiri/Kuwamini Yesu
  Wetu: Wokovu= Kumwamini Yesu(kuhesabuwa haki)+Kutakaswa + Kutukuka.
  Kama mpo makini mtaona utofauti wetu!!”

  Usiweke mawazo yako yawe ya kwangu,usilishe watu sumu,
  kwa sehemu ninayaelewa maandiko vizuri.

  Kuna watu hawa watatu kwenye maandiko-wewe upo kundi lipii!!unanishangaza!
  1.Mtu(mwanadamu) wa tabia ya asili
  huyu kwake mambo ya Mungu kwake ni upuuzi

  2.Mtu(mwanadamu) wa tabia ya mwilini
  Wakati mwingi umepita kwake na bado anahitaji kufundishwa
  mafundisho ya kwanza ya neno la Mungu,kwamba anahitaji maziwa

  Imeandikwa….
  Kwa maana kila mtu atumiaye maziwa hajui sana neno la haki, kwa kuwa ni mtoto mchanga.

  3.Mtu wa rohoni
  Hafundishwi na mtu,huyatambua yote anahifahamu nia ya Bwana
  Roho wa kweli anamuongoza ktk kweli yote,

  Wanaongozwa na Roho wa Mungu hao ndio wana wa Mungu,
  Hao hawakupokea roho wa utumwa iletayo hofu,wewe unayo hofu

  …Ngoja tuangalie maandiko ninayoamini ya kutukuzwa na kutakaswa
  kunaanza hapa na baadaye milele,Kwa maana tuliokolewa kwa taraja;

  imeandikwa…..
  Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita,
  hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hao AKAWATUKUZA.Rm8:30

  unaona maandiko hayo siyo yangu

  Unakumbuka jibu la Bwana kwa Kefa…kwamba sisi tumeacha vyote(LK18:29-30/MK10:30)….

  Huyo Roho ututamani kiasi chakuona wivu………. na utujalia neema ile iliyozidi.

  Angalia mifano hii michache….
  *Kumb28:1Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani;

  *Josh3:7Bwana akamwambia Yoshua, Hivi leo nitaanza kukutukuza mbele ya Israeli wote, wapate kujua ya kuwa mimi nitakuwa pamoja na wewe, kama nilivyokuwa pamoja na Musa.

  Josh4:14 Siku ile Bwana alimtukuza Yoshua mbele ya macho ya Israeli wote; nao wakamcha, kama walivyokuwa wakimcha Musa, siku zote za maisha yake.
  2Sam5:12 Akajua Daudi ya kwamba Bwana amemweka imara awe mfalme juu ya Israeli, na ufalme wake ameutukuza kwa ajili ya watu wake, Israeli.

  Bro Mjema….huyo ndiye Mungu aokoaye
  1Ny:29:12 mkononi mwake mna uweza na nguvu,tena mna KUTUKUZA na kuwezesha

  Mjema….Walio mpokea Yesu are presently glorified positionally, but one day in heaven we will be glorified in the fullest sense(MWILI/NAFSI/ROHO)

  No Christian will miss out on this labda Mkristo jina/Ukristo wa kurithi toka kwa baba/babu…..mimi siwezi kuacha dini/dhehebu ya babu na baba.

  Hivi kweli mimi siamini utakasao ….tuangaliea haya maomb/duai ya Paul
  Waliompokea/Amini wanatakaswa….

  (1Thes5:23-24)Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo,Yeye ni mwaminifu ambaye awaita, naye atafanya.

  Ngoja tuone haya maandiko kama tuko vitani hatuwezi kuokoka vinginevyo maandiko hayana maana yoyote tunajilisha upepo na kupiga ngumi hewani

  Rm8:31,35-39

  *Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu?
  *Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?
  *Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa.
  *Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.
  *Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo,
  wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.

  Bro…..
  Tukiona ahadi za Mungu hatusiti na kutokuamini….. Tunapata nguvu kwa imani tukijua kuwa mkono Mungu una uweza na Yeye ndiye utufanya imara ktk Kristo Yesu, Anatuwezeshwa kwa uweza/ nguvu na kuwa na saburi pamoja na furaha haki na amani ktk Roho Mtakatifu

  Bro Mjema
  Tuliokolewa/Tunaokolewa/Tutaokolewa……..Ndio maandiko

  (kuoshwa/kutakaswa/kuhesabiwa haki/kutukuzwa)kunaanzia hapa duniani, Ulimwengu wote Utajua/Unajua kwamba Bwana yupo pamoja nao hao walioamini injili ya Mungu hata kama hawataki kuamini wataamini zile kazi zinazitendwa.

  Umemuona Joshua/David/Job walitukuzwa toka hapa duniani,maandiko yanesema ili watu wote wajue kwamba Mimi(Mungu)nipo pamoja nanyi. Tukitii na kutunza maagizo yake anaanza kukutukuza hapa hapa dunia na kisha milele ktk ufalme wa Bwana Lk18:29-30.

  Imeandikwa hivi………..
  Naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii;Ambaye tuna maneno mengi ya kunena katika habari zake(tunaoamini wokovu ni sasa); na ni shida kuyaeleza kwa kuwa mmekuwa wavivu wa kusikia(nyie msioamini wokovu sasa).”Ebr5:9,11”msisitizo ni wangu

  Sioni Heri kwako…….Lakini ngoja nikuache na imani/hekima yako ya kujipigania nafsi yako.maandiko yapo wazi lakii mjema huyaoni,mara naamini wokovu ila mtazamo tunapishana,kwakweli hatupishani isipokuwa wewe unapishana na maandiko ya nenl la Mungu

  1Cor15:1-2Basi, ndugu zangu, nawaarifu ile injili niliyowahubiri; ambayo ndiyo mliyoipokea, na katika hiyo mnasimama,na kwa hiyo MNAOKOLEWA; ikiwa mnayashika sana maneno niliyowahubiri isipokuwa mliamini bure.

  Ps 27:1The Lord is my light and my salvation; Whom shall I fear? The Lord is the strength of my life; Of whom shall I be afraid?

  Ps 46: 1 God is our refuge and strength, A very present help in trouble. 2 Therefore we will not fear, Even though the earth be removed, And though the mountains be carried into the midst of the sea; 3 Though its waters roar and be troubled, Though the mountains shake with its swelling. Selah

  Wenye roho ya hofu/woga wote tafadhari Soma Zab 46 yote hiyo vita hamtaigopa tena
  maana neno la Mungu ni upanga linatenganisha nafsi na roho.ni moto ni nyundo.

  Bwana alifanya njia pasipo na njia,anafanya njia pasipo na njia,atafanya njia pasipo njia,isipokuwa woga/hofu na kutaka kuelewa nguvu za shetani ili upigane naye vita hili hali kuna silaha umepewa za kujilinda unaziacha unavaa silaha za woga.Na woga/hofu inawangusha ,wanaanguka kwa ukiri wa maneno ya vinywa vyao

  Mr Mjema ningali na mengi ya kunena ….Rehema ya Mungu na izidi kwetu

  Amen

  Mjoli Haule

 145. Lwembe,
  Noted!
  ………..

  Mjema na wenzako, mmedanganywa na mkadanganyika kwelikweli kuhusu wokovu.

  Kumbe hata uzima wa milele huujui!! Uzima wa milelel hauko mbinguni, bali tuko nao hapa duniani tayari.

  Nao ni huu ”wakujue wewe Mungu pekee wa kweli na Kristo uliyemtuma” (Yoh 17:3)

  Swali: Tunamjua huyu Mungu pekee wa kweli?
  Tunamjua Kristo aliyetumwa na yeye?
  Jibu: Mimi namjua. Kwa hiyo kwa kuwa kumjua ndio uzima wa milele, basi ninao!
  Wewe nafikiri unasubiri ukamjue mbinguni, endelea kusubiri!

  Kama Petro alipookolewa toka majini akawekwa kwenye mtumwi alikuwa salama, na alhali mtumbwi uliendelea kuwa baharini, basi ni sahihi kabisa kwamba tulio katika Kristo Yesu tuko salama kabisa (tumeokoka) japokuwa bado tuko duniani.

  Petro alipowekwa kwenye mtumbwi alikuwa na hiari ya kujirushia kwenye maji au kuendelea kukaa kwenye mtumbwi ili abaki salama. Haukuwa wajibu wa Yesu kumlazimisha Petro abaki kwenye mtumbwi, bali wajibu wa Petro mwenyewe. Lakini shetani kama angetaka kumtoa Petro mkono mwa Yesu kumrudisha majini, asingeweza!

  Kama una akili umeelewa.

  Kuhusu suala la Yuda, jibu langu ni hivi; Inawezekana Yuda siku Kristo akitudi akanyakuliwa kumlaki. Labda wewe kama unakithibitisho kwamba hatanyakuliwa unioneshe.

  Mpaka mtakapoelewa maana ya Neono ‘WOKOVU’ Kibiblia linamaanisha nini huo ndio wakati pekee mtaelewa tunachojadili hapa.

  Mnajaribu kuelewa neno wokovu kwa mantiki ya lugha ya kwenu, na ndipo mnajikuta mmepotea kweli. Ona swali ulilomuuliza Edwin kuwa mtu anaokokaje akiwa vitani?

  Nami nakuuliza wewe kwa mantiki hiyohiyo:
  Je, anayehitaji wokovu ni mateka au askari anayepigana vita?

  Nafiki na hapa kama una akili umeelewa matumizi ya neno Wokovu!

 146. edwin,

  Acha mikwara mtumishi! Habari ndo iyo.

  Naona umepotea siku nyingi,take this warm up kabla sijakupeleka msituni:

  Jibu hili kama una ubavu: Mtu anaokokaje akiwa vitani?

  Zingatia: baada ya kumwamini Yesu unatakiwa kuilindi imani iyo yenye thamani na inayojaribiwa kila siku,mahali,saa na sekunde. Ni wale tu wanaovumilia na kuistaimili majaribu hayo hadi MWISHO NDIO WATAKAOKOKA!

  Hizo,past na present tenses za kuokoka. ni hatua tu za kuukulia wokovu mpaka pale mtu anapotengwa milele na adui,either during death or jesus second advent. Thats all.

  Swali2: kuokoka ile ya kikwenu/kipentekoste/J.Calvin ya mdo2:47 iliwahusisha anania na safira,ila Mdo5,mambo yaligeuka wakapoteza wokovu unaodai upo mdo2. Uoni udhaifu wa hoja yako kupitia tukio hili?

  Karibu Mjoli.

 147. Lwembe,

  Asante kwa habari njema kuhusu Wokovu ulioueleza. Hat hivyo nina haya kwa ajili yako;

  Mungu amevichagua vitu vinyonge ili haviaibishe vilivyo hodari. Hivyo basi, hao unaowadharau katika Jeshi la Mungu kwamba eti ni Migambo tu wanaweza kutumiwa na Jemedari Mkuu Yesu na wakawa washindi hata zaidi ya hao wana Jeshi wenye vyeo vya juu kabisa. Think of Daudi vs Goliath.

  Nina Imani kuwa utapitia michango yangu kwa haule na Sungura hapo juu kwani hoja zako more or less zimejibika.

  Angalizo: Tunajaribiwa kila siku, na tunapagwa kuipigania Imani na Kuilinda hadi mwisho (kulala mauti/Yesu ajapo) ambapo hakuna kujaribiwa tena ndipo tutataposema Tumeokoka.

 148. Sungura;

  Maswali yako ni haya;

  1 Petro alimuomba Yesu atembee juu ya maji, Yesu akamkubalia. Lakini alipoanza kuzama alipiga kelele akimuomba Yesu amwokoe.

  Swali: Yesu alimwokoa au hakumwokoa?
  Swali: Na kama alimwokoa, walijikuta hawako baharini au waliendelea kuwa baharini lakini wako salama?

  2.Ivi wokovu ni kwa ajili ya walioko duniani au walioko mbinguni?

  Majibu:

  1.Yesu alimwokoa Petro dhidi ya kuzama ILA baada ya hapo hawakuwa hatarini tena kwani walikuwa ndani ya meli.

  Rafiki, kuokolewa kwa Petro katika tukio hili, hakuna uhusiano wowote na kile tunachokisisitiza hapa-Wokovu kwa maama ya Uzima wa milele.Wala alichokitaka Yesu wanafunzi wajifunze katika tukio hilo sio kuwa anajua kuokoa dhidi ya kuzama baarini bali kuwaokoa dhihi ya uhaba wa Imani yao ambayo Petro hakuwa na uzoefu nayo kwani hata baada ya tukio hilo siku nyingi baadae bado halikuwa hajaokoka kwani halikosa Imani dhidi ya kifo cha Yesu na kufufuka kwake.

  Sungura, hebu nikupe mifano mingine ya baharini;

  1. Agano la Kale: Kumbuka Yona alipokimbia kazi ya Mungu Ninawi badala yake akapanda meli kwenda Tarshishi. Baada ya dhambi yake iyo Mungu alileta dhoruba iliyosababisha atupwe baharini.Mungu alipomwokoa kupitia samaki aliyemmeza, Je unataka kusema kuwa Yona aliokolewa kwa maana ya uzima wa milele au ya kawaida tu. Ni na maana hii kuwa, Mungu alimwokoa yona kama anavyoweza kumwokoa mtu yeyote ataambaye hajawahi kusikia habari zake kabisa!

  2.Siku moja wanafunzi wa Yesu walipokuwa wanasafiri baharini, Yesu akiwa amelala fofofo? kulitokea dhorura na hivyo wanafunzi wake wakaogopa sana. Wakamwednea Yesu wakitaka hawaokoe. Yesu aliwaokoa dhidi ya ile dhoruba. Lengo la tukio hilo haikwa tu kuwa Yesu anajua kuokoa dhidi ya dhoruba ya bahari bali zaidi sana kutaka wakue katika imani.

  sasa nawe nikuulize swali: Je, Yuda ambaye alikuwa miongoni mwa waliookolewa dhidi ya dhoruba hiyo, ( yaani ALIOKOLEWA au AMEOKOLEWA) Je, leo hii yupo katika walio na rekodi ya watakao urithi uzima wa milele ( ATAOKOLEWA) Yesu ajapo.

  Wapendwa, tuutazame wokovu kwa maana ya Umilele na sio ya kawaida. Wokovu kwa maana ya Umilele inahitaji Kuilinda Imani inayojaribiwa kila siku hata mwisho wa wakati.

  Jibu2: Watu wanaokolewa TOKA duniani KWENDA Mbinguni na uzoefu huu uwa kamili pale tu mtu anapotolewa nje ya dunia yenye dhiki,adha, njaa, majaribu na kila aina ya atari

 149. J.Haule & Sungura,

  Poleni wajoli kwa kusubiri itikio letu kwa hoja zenu kuhusu wokovu. Pia hongereni kwa kumtafuta Bwana kwa bidii na kuchukuliana nasi. Ni muda tangu tuwe hewani hata hivyo ni majukumu ya maisha yaliyobana kwa muda.

  Sungura, nimeiona kiu yako kujibu aya za Haule kwenye pakicho lake la tarehe 09/05/2014 at 3:40 PM. Nami napenda kusema machache yafuatayo;

  Wapendwa, ni ukweli kuwa biblia ina aya zenye nyakati tofauti katika kuuelezea wokovu yaani : ALITUOKOA, AMETUOKOA na ATATUOKOA. Pia katka mada fulani mlijaribu kuzifafanua akiwemo mjoli Sungura. Ila ndg zangu hebu tutafakari kidogo juu ya nyakati hizi;

  1.Ninachotaka kuwakumbusha ni kuwa tunachotofautiana ni mtazamo tu, na sio kwamba tunaupinga wokovu. la hasha!!. Utofauti wetu wa mtazamo upo hivi:

  Wenu: Wokovu= Kumpokea/Kumkiri/Kuwamini Yesu

  Wetu: Wokovu= Kumwamini Yesu(kuhesabuwa haki)+Kutakaswa + Kutukuka.

  Kama mpo makini mtaona utofauti wetu!!

  Wapendwa,hatua ya kwanza ya kumwamini au kumpokea kristo yaweza kuwa jambo la siku moja. Hata hivyo, hatua ya pili ya utakaso ni endelevu tangu mtu anapompokea Yesu hata mwisho wa pambano au kujaribiwa kwa Imani ambayo ni siku ya kifo chake au siku hajapo Yesu-Kutukuka.

  Haule, Sungura, hapo mlipo ninyi mnapitia utakaso na mnatakiwa kuilinda imani iyo hata mwisho ndipo mtakapookoka. Imani ni sawa na dhahabu inayotakaswa kila siku na mtu hapaswi kujikinahi kiimani hawapo katika mchakato huo mpaka pale imani yake inapokuwa imesafishwa na kuwa safiii.

  2.Wokovu una maana mbili, ya kawaida na ya kiroho. Ni kweli mtu anapoponywa anaweza kudai kuwa Mungu amemwokoa katika ugonjwa huo ( Maana ya kawaida), Lakini SIO kiashiria kuwa ataingia mbinguni (maana ya kiroho). Kwani Kuhusu kuponywa sio mpaka mtu awe amemokea Yesu ndo anusuriwe dhidi ya ugonjwa/ajali au hatari nyingine yeyote ile. Pia mtu mcha Mungu anapopoteza maisha kwa ugonjwa/ ajali au hatari nyingine yeyote ile haina maana kuwa hajaokoka! mtu anaweza kufa kwa maradhi na bado siku ya Gloryfication akapata kibali cha kuingia jiji la Jerusalemu ya mbinguni.

  Hivyo basi, tense za : ALITUOKOA na AMETUOKOA sio ishara kuwa ATATUOKOA. Sisi mtazamo wetu ni kuwataka mtazame ATATUOKOA ambayo ndiyo hasa kilichomleta Yesu na kinachotutofautisha sisi tunaomjua Yesu na wasiomjua Yesu.

  Elewani hivi; ALITUOKOA na AMETUOKOA ni kile Yesu alichokwisha kukifanya kwa ajili ya watu wote ( waliompokea na wasiompokea) Ila ile ya ATATUOKOA ni kwa wale waliopitia tanuu la utakaso na kuvumilia hata mwisho hatimaye kutukuka.

  Hiyo ndiyo maana, msijekujivunia ALITUOKOA na AMETUOKOA kama kina wana wa Israeli toka Misri-Jangwani na kukosa ATATUOKOA kwa kushidwa kufika Kanaani. Ndivyo iliyokuwa pia kwa Yuda aliyemsaliti Yesu.

  3.Ubarikiwe kukiri kuwa tupo vitani, tena vila isiyo “lele mama” na sio juu ya damu na nyama. Hata hivyo, sijakupata / sijatosheka ufafanuzi wako wa : ” Ni kwa jinsi gani mtu anaweza kuokoka akiwa vitani?” tafadhali ni fahamishe zaidi.

  Halafu haule, hakuna anaye mtukuza shetani au anaye tangaza Injili ya woga hapa. Ni ukweli usiopingika kuwa ili umsinde adui ni sharti uelewe jinsi nguvu zake zilivyo hasa na hivyo ujipsnge vilivyo kumkabili. Watu wengi watapotea kwa kushndwa kujipanga dhidi ya adui.

  Swali kwako: Je, unajua kuwa mtu anaweza kutendewa ile ya ALITUOKOA na AMETUOKOA na hakaikosa ile ya ATATUOKOA? Tafakari.

  Habari ndo iyo na ubarikiwe.

 150. Ajabu kabisa!

  Nini Mnaongea hapa Siyi/Mjema/Lenda na the like Kuhusu jambo kubwa na tukufu sana ili la Kila Mwanadamu kabla hajatoa ulimi nje, ahakikishe ana Wokovu ndani? MNASEMAJE eti? Kwamba nini ? What?

  Press on

 151. “”Swali: Yesu alimwokoa au hakumwokoa?
  Swali: Na kama alimwokoa, walijikuta hawako baharini au waliendelea kuwa baharini lakini wako salama?””

  Maswali kama haya ndiyo yanayoiamsha tafakari ndani ya mioyo minyofu!

  Kwa mfano, huwa mara nyingi tunaitukuza “Damu” iliyomwagika pale Kalvari kwamba ndiyo iliyotuokoa, jambo ambalo huturejesha huko kwenye Torati pasi ufahamu, ndio maana akina Siyi inawawia ugumu kuukubali wokovu na hata kuijua Neema!

  Bali Kweli ya Injili ni kwamba TUNAOKOLEWA KWA NEEMA na si Damu; Damu HUUTUNZA wokovu tuliokirimiwa, hutusafisha na kutuacha tulio Safi!! Neema ndiyo iliyoileta Damu!

  Basi shurti uwe umefikiwa na hiyo Neema kwanza, ndipo utauelewa Wokovu ni nini, nje ya hapo ni Mahepe tu!!!

  Asante, Sungura,
  & Gbu all!

 152. Kwako Siyi & company,

  Sina mambo mengi sana ya kuwaambieni. Lakini ilikuwa ni vema mjibu hoja za Haule ktk mchangowake wa tar. 09/05/2014 at 3:40 PM.

  Naona mnajaribu kuhoja neno la Mungu kwa logic ya mataumizi ya lugha, ambayo pia hamuijui sawasawa. Yaani kwa akili zenu mnajaribu kulihoja neno ‘wokovu’ kwa tafsiri ya kufikirika.

  Mkiweza kujibu mistari iliyotolewa na Haule kwenye huo mchango wake, hasa inayoongelea past tense, mtakuwa mmejisaidia sana kuelewa nini hasa maana ya kuokoka.

  Tangu kwenye ile mada nyingine, Siyi nilijaribu sana kukuelezeni maana ya kuokoka kwa tafsiri ya biblia, na mpaka nikakwambia kuwa kama wewe unakiri kwamba Yesu kakuhamisha kutoka ufalme wa giza kwenda ufalme wa nuru, maana yake si kwamba ufalme wa giza = hatari na ufalme wa nuru = usalama!?

  Kwa nini sasa hamtaki kuelewa kuwa huko kuhamishwa ni kuokoka, yaani kule kutolewa ufalme wa giza (wa shetani) kwenda ufalme wa nuru (wa Yesu).

  Maana kwa kifupi wewe husema kuwa kuokoka ni kutoka hatarini kwenda kwenye usalama.

  Ngoja niwaulizeni swali hili kwa mfano wa biblia:

  Petro alimuomba Yesu atembee juu ya maji, Yesu akamkubalia. Lakini alipoanza kuzama alipiga kelele akimuomba Yesu amwokoe.

  Swali: Yesu alimwokoa au hakumwokoa?
  Swali: Na kama alimwokoa, walijikuta hawako baharini au waliendelea kuwa baharini lakini wako salama?

  Na kiswali kingine kwako Siyi:

  Ivi wokovu ni kwa ajili ya walioko duniani au walioko mbinguni?

  Inatosha kwa leo!

 153. Mjema,

  Inaendelea ……….

  Pia, kwa jinsi yoyote ile utakavyolichukulia neno “Wokovu” au “Kuokoka”, hutaweza kwenda nje ya tendo la “Kusalimika”. Dhihirisho la “Wokovu” linaanza baada ya Anguko, hapo Mungu alipowavisha ile ngozi ili kuificha aibu yao, akiruhusu angalau mawasiliano hafifu kupitia hiyo damu ya mnyama. Uhafifu huo unadhihirika ktk Ufunuo hapo Yohana alipoliona jambo hilo hata likamsababisha alie kwa uchungu wa kupotea viumbe wooote pamoja na yeye mwenyewe, Ufu 5:4 “Nami nikalia sana kwa kuwa hapakuonekana mtu astahiliye kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama.”

  Umeelewa Mjema? Wote tulichukuliwa mateka wa dhambi, Rum 3:23 “Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu” unaona, tumetenda dhambi kivipi? Rum 5:12 “Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi”!!!

  Sasa, iwapo mshahara wa dhambi ni Mauti, na sote tukiwa dhambini, ndiyo unamuona Yohana akilia kuhusu mshahara huo, maana kwa sehemu aliyategemea yale mawasiliano hafifu ya sadaka za wanyama walizozitoa kwamba yanamstahilisha “Wokovu” kutoka hilo Anguko, yaani kule Kuhesabiwa Haki kwa Sheria, lakini badala yake anaiona mauti mbele yake, ndio mshahara anaostahili kulipwa kulingana na hali yake kama inavyojidhihirisha, maana ukikosa ktk moja, umekosa ktk zote, nayo damu ya wanyama haikuiondoa Dhambi!

  Basi, Maandiko yanatufunza zaidi kuhusu mauti inayotukabili kupitia hiyo dhambi, yakilifunua jambo hilo kwamba mauti hiyo imekuwamo ulimwenguni kutoka siku ilipoingia kwa lile Anguko, na imetawala tangia hapo mpaka Musa, yaani ilipokuja Sheria na kuifunua!!! Je, Sheria ilipoifunua Mauti, iliishinda? Haikuweza, iliishia kuwatahadharisha tu, ikiwafungua macho yao kwamba yule waliyemzoea kuwa ni paka wa nyumbani ni chui mla watu usiku! Basi Sheria iliiondoa ladha ya nyama kwa chui huyo na hivyo aliishia kuwaua bila kuwala, hao waliodumu ktk Sheria! Sheria iliwapa TUMAINI la wokovu ambao ni sumu ya dhambi. Tumaini la wokovu huilegeza nguvu ya dhambi na mauti yake hata kuifisha. Tumaini la wokovu hukuingiza ktk wokovu kamili.

  Tumaini la Wokovu lilikuwa ndani ya Ahadi ya Masihi iliyomo ndani ya Sheria!!! Kwamba Sheria iliujua udhaifu wake ktk kuwafikisha wajoli wake kwenye kipeo cha Wokovu mkamilifu, ndipo kwayo ikawajengea hilo Tumaini lililowafanya wahimili vishindo vyote vya mauti, maana imefunuliwa kwao na nguvu zake, licha ya kuzidi kwake kuwashikilia kwa ule udhaifu wa Sheria, lakini kwa Tumaini waliishinda! Hebu waangalie Ayubu na Paulo jinsi Tumaini lilivyowaongoza:
  Ayu 19:25-6 “Lakini mimi najua ya kuwa Mteteaji wangu yu hai,
  Na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi. And though my skin worms destroy this body, yet in my flesh shall I see God”!!!
  1 Kor 15:55 “Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U wapi, Ewe mauti, uchungu wako?”

  Ayubu alichokiona huko nyuma, ndicho hiki hapa Paulo anachokishuhudia katika uhalisi wake na si katika kukitegemea huko mbele, anazungumzia Ushindi alionao na si atakaokuwa nao huko mbele ambako hakuna cha kushindania!!!

  Injili inapohubiriwa, ndiyo inayokuingiza katika Tumaini la Wokovu. Nayo Sheria ni sehemu ya Injili, ndiyo yenye kuifunua Dhambi na Mauti yake. Na kutoka kufunuliwa huko, ukioneshwa Mauti inayokukabili, hiyo ambayo ulikuwa ukiongozana nayo kama rafiki mpenzi huko kwenye Upagani au “dini mfu” (nikimnukuu Seleli), ikikushikilia kisawasawa hata usingeweza kuitoroka au kujitoa mikononi mwake, ndipo unapofikia kulitambua jambo hilo kwamba uko mkononi mwa Muuaji, ndipo tungeketi chini tukiwa wenye kuyakatia tamaa maisha na kuanza kulia kama Yohana au lile kundi pale Mdo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?”! Huchukua Mkono wenye Nguvu, lile Neno la Mungu, kumfanya Muuaji akuachilie, Neno linalovuja Damu; Nguvu za Ibilisi huvunjika kwa ile Damu, ndipo hukuachia huru! Umeuona Ukombozi?!!!!

  Msingi wa Wokovu ni Ukombozi. Kuna Ukombozi uliofanyika na kutuingiza ktk Wokovu! Tunakombolewa kwanza kutoka ktk makongwa ya dini na upagani, ndipo tunasajilwa Jeshini katika Wokovu kuipigania Imani! Basi tutokapo kwenda vitani, katika ukamilifu wa Neno tulibebalo mioyoni mwetu, hilo Tumaini la Wokovu wetu, sisi huushinda ulimwengu na dhambi na mauti yake, hapo lile toleo moja la Dhambi linapokuwa halisi kwetu, likiifunga Torati, hiyo ambayo ndiyo Nguvu ya Dhambi na kutuingiza katika Wokovu hata kuwa Jeshi lake; “… Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo.”!

  Basi ni kutokana na jambo hili la kwamba hao waliozaliwa mara ya pili kwa Roho, kwamba ndio wanaosajiliwa katika Jeshi la Mungu, yaani hao watoto wake aliowazaa kwa Roho, ndio tunafahamu kwamba Yuda Iskariote alikuwa ni “mgambo” wa dini tu, hakuwa mtoto wa Mungu kama unavyodhani, ndio maana aliikiri tu dhambi yake, wala hakuiungama!!!

  Mbarikiwe nyooote!!!

 154. Mjema,

  Shalom ndg yangu!

  Nimeyaona maswali yako yanayohusu “wokovu”, pia nimeyaona majibu ya kina aliyokupatia ndg Haule, ninaamini kwamba Msingi wa Wokovu umeanza kujengeka kwako. Juu ya msingi huo napenda nikuongezee changamoto ya kiufahamu kuhusiana na suala hilo la wokovu hapa duniani!

  Kwanza, nimekuona unatatizika na hali ya Mkristo kuwa vitani, ndipo unauliza utaokokaje ilhali uko vitani? Lakini, unaposikia kuna vita, basi jua kwa uhakika kwamba kuna majeshi yanayopigana, hii ndiyo maana kamili ya neno vita!

  Jeshi pia hutambulika kwa jina la kiongozi wake anayetoka nao kwenda vitani; majeshi ya Sadam au majeshi ya Mjema nk ndiyo hiyo kauli Mikaeli na jeshi lake!

  Nguvu ya Mungu iko ktk Neno lake. Ndipo unapozungumzia Jeshi la Mungu, unapaswa utambue kwamba hiyo Nguvu yake ni lazima iwe imewekwa ktk jeshi hilo, wawe ni malaika au binadamu, wote huwa ni Jeshi la Mungu hapo hiyo Nguvu inapokuwa ndani yao!

  Nalo jeshi hupigana ili kulinda falme au kukomboa. Kwahiyo unapoambiwa kwamba wewe ni askari, itakuwa ni jambo la kuchekesha iwapo hata hujui ni kwa jinsi gani umefikia kuitwa askari, na pia unapaswa ukijue na kikosi ulichosajiliwa! Maana kulingana na mambo ya mjini, askari ni wengi sana na ni wa aina tofauti. Unaweza ukawa ni “mgambo wa city” lakini umekizoelea cheo cha askari, nawe ukajijengea taswira kwamba wewe ni mwanajeshi! Unaona, kule kuitwa kwako kuwa wewe ni Mkristo, huyo ambaye ndiye askari wa kweli, ikakufanya uamini hivyo, kumbe masikini wewe ni mgambo tu wa dhehebu lako, hujafikia kuwa askari ktk maana ya kuwa na uwezo wa kupigana vita; hivyo vya rohoni anavyovizungumzia Paulo, Efe 6:12 “Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.”!

  Askari inaowazungumzia Biblia wanasajiliwa ktk wokovu! Vita ya kiroho si “lele mama”! Ni katika wokovu ndiko kuna kuzaliwa mara ya pili kwa Roho wa Mungu, Yn 3:6 ” Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.” Huyu aliyezaliwa kwa Roho, ndiye anayepewa silaha hizo za kiroho akiisha kusajiliwa katika hilo Super Jeshi la Mungu, hakuna mgambo wa dini humo!!!

  Wokovu uko ktk kulipokea Neno la Mungu, na huko ndiko kumpokea Kristo. Wengi tunazipokea taratibu za makanisa yetu na kujidanganya kuwa tumempokea Kristo! Kristo ndiye Mwokozi ndipo huyo ampokeaye, huupokea wokovu ambao ndio udhihirisho wa hiyo kazi aliyoifanya Kristo, Mwokozi!

  Basi jambo la kwanza tunalopewa ktk Jeshi hilo ni UZIMA wa Milele, basi ni nani awezaye kutuangamiza ilhali tunao Uzima huo? Hakuna Mkristo anayekufa vitani, huu ndio Msingi wa “Wokovu” tulionao, kinga dhidi ya kifo, kule kutengwa na Mungu!!!

  ………… itaendelea!

 155. Wapendwa katika Kristo Yesu,
  Kwanza kabisa naendelea kuwashukru ambao mmendelea kuchangia kwenye mada hii ya msingi sana katika imani yetu………akiwemo Mjoli Haule na wengine wanaofuatilia kwa ukaribu sana mada hii!

  Naomba nijitambulisehe kwanza kuwa jina langu mimi ni kaka Erasto na dada Catherine ni mke wangu jina linavyoonekana hapo lisiwachanganye wapenda nadhani itaedit!

  Kisha naomba tupitie andiko alilotoa
  Da Magreth 11/05/2014 at 9:46 AM kisha tuweze kuliweka sawa pale inapohitajika naona kama vile limeandikwa vizuri, Ingawa bado naona ni vizuri kukubaliana sote kisha tuweke msimamo mmoja kulingana na roho anavyonena ndani ya mioyo yetu!

  Fuata hii link hapa, kisha uchukue kigoda ukae, na kutafakari maneno haya.
  http://www.discoverrevelation.com/Salvation.htm#Doctrine%20of%20Losing%20Salvation

  Mungu awabariki!
  Erasto

 156. Da Catherine

  Naomba na mimi nichangie kidogo maswali au changamoto kama ulivyoandika
  Nakunukuu

  1.Changamoto niliyokuwa nimekutana nayo ni kuwa wokovu hauwezi potea haijalishi ya maisha ambayo utakufa nayo au Yesu atakukuta nayo.
  2.Mie niliamini kuwa mtu ukiacha wokovu ukatenda kinyume ungali unaujua ukweli wa neno wazi(ukafikia kuasi) utapoteza wokovu.
  3.Nahitaji ufafanuzi zaidi kwenye maeneo haya….kuwa ni kweli kuwa Mungu atakuadhibu tu ukiacha wokovu lakini huwezi poteza wokuvu? Au kuna mazingira yoyote ambayo mtu aweza poteza wokovu?
  ……32Tunapohukumiwa na Bwana,tunaadabishwa ili tusije tukahukumiwa pamoja na ulimwengu…….1Kor 11:27-32

  Nimeyaweka kwenye mtirirko maswali yako nitajibu kwa mtiririko huo,

  1.Ni kweli……. ukiacha wokovu(kuasi)utakuwa umepoteza wokovu,Ni lazima kuishindania imani tuliyopewa watakatifu mara moja tu.Yesu akija atesema sikukujua tangu awali
  imeandikwa
  Ebr10:26-27
  Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi; bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao.

  2.Ni kweli atapoteza wokovu,maandiko ni mengi yanasema hivyo hilio hapo juu Ebr10:26-27 ni moja wapo.

  3.Ndio kuna aina ya dhambi ya mauti na isiyo ya mauti,
  1Jon5:16 
  Mtu akimwona ndugu yake anatenda dhambi isiyo ya mauti, ataomba, na Mungu atampa uzima kwa ajili ya hao watendao dhambi isiyo ya mauti. Iko dhambi iliyo ya mauti. Sisemi ya kwamba ataomba kwa ajili ya hiyo.
  5:17 Kila lisilo la haki ni dhambi, na dhambi iko isiyo ya mauti.

  Tumeona kuna dhambi ya mauti na dhambi isiyo ya Mauti zote zinakupeleka ziwa la moto,Lakini dhambi isiyo ya mauti wewe mwenyewe au mtu mwengine anaweza akaomba toba kwa Mungu.Akasameha,Lakini utakuwa umepata adhabu, Lazima (kuadabishwa)kama yavyosema maandiko haya

  Ebr12:5-8
  Tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama kusema na wana, Mwanangu, usiyadharau marudia ya Bwana, Wala usizimie moyo ukikemewa naye;
  Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, Naye humpiga kila mwana amkubaliye.
  Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye?
  Basi kama mkiwa hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali.

  Kwa kutokumbanua kwa nafsi zetu ndipo sasa hayo yamefika kama ili andiko lenye changamoto kwako

  1Cor11:32
  Ila tuhukumiwapo, twarudiwa na Bwana, isije ikatupasa adhabu pamoja na dunia.
  Anatudabisha ili tuache hizo njia ambazo zitapelekea kutenda dhambi ya mauti

  Da Catherine Tutazame mfano mmoja wa dhambi isiyo ya mauti kwenye maandiko ya kibiblia

  Mfano wa Mariam
  Hes 12:1-2
  Kisha Miriamu na Haruni wakamnenea Musa kwa sababu ya mwanamke Mkushi aliyekuwa amemwoa; maana, alikuwa amemwoa mwanamke Mkushi.
  Wakasema, Je! Ni kweli Bwana amenena na Musa tu? Hakunena na sisi pia? Bwana akasikia maneno yao.

  Bwana anamudabisha Mariam

  Hes12:5-15
  Bwana akashuka katika nguzo ya wingu akasimama pale mlangoni pa Hema, akawaita Haruni na Miriamu, nao wakatoka nje wote wawili.
  Kisha akawaambia,Sikizeni basi maneno yangu;Akiwapo nabii kati yenu,Mimi,Bwana,nitajifunua kwake katika maono,Nitasema naye katika ndoto.
  Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa; Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote;
  Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; Na umbo la Bwana yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa?
  Hasira za Bwana zikawaka juu yao; naye akaenda zake.
  Kisha hilo wingu likaondoka kutoka pale juu ya hema; na tazama, Miriamu akawa mwenye ukoma, mweupe kama theluji; Haruni akamwangalia Miriamu, na tazama, yu mwenye ukoma.
  Kisha Haruni akamwambia Musa, Ee bwana wangu nakusihi sana usituwekee dhambi juu yetu, kwa kuwa tumefanya ya upumbavu, na kufanya dhambi.
  Nakusihi, asiwe kama mmoja aliyekufa, ambaye nyama ya mwili wake nusu imelika hapo atokapo tumbo la mama yake.
  Musa akamlilia Bwana, akasema, Mpoze, Ee Mungu, nakusihi sana.
  Bwana akamwambia Musa, Je! Kama baba yake angalimtemea mate usoni tu, hangaliona aibu muda wa siku saba? Na afungwe nje ya kambi muda wa siku saba, kisha baada ya hayo ataletwa ndani tena.
  Basi Miriamu alifungwa nje ya kambi muda wa siku saba; wala watu hawakusafiri hata Miriamu alipoletwa ndani tena.

  Unamuona Haruni hapo ehh anamsihi Bwana…Musa anasihi anaomba kwa kulia kabisa ….Jibu la Bwana….kama baba angelimtemea mate usoni……………linafuata anamudabisha mariam,
  Tunaiona hapo mfano wa ya dhambi isiyo ya mauti kumnena vibaya Musa,lakini wangekaa kimya ingekula kwake Mariam….ukoma mwisho mauti.
  Tuache kuwasema watumishi ni dhambi(hii haiwahusu mitume/manabii wa uongo,wachungaji wa mshahara,walimu wa uongo hao lazima tuwakemee waache kulitukanisha juna la Bwana).

  Kuna dhambi ya Mauti kwa hiyo hata ukiomba haisaidii(Ebr6:4-6)

  Tukumbuke tusisahau hata kidogo kuwa Watakatifu watauhukumu ulimwengu,Tutawahukumu malaika…sasa huwezi cheza na wokovu kama bibi au babu yako.Mungu ametukirimia mambo makuu.

  Tunaona kwa fundisho hilo mwana akiadabisha kwa dhambi isiyo ya mauti,

  Da Cathetine……Tuko na walimu wengi hapa …najua nimewatia shauku…..watakuja nasi tutafaidi gombo

  Barikiwa

  Mjoli Haule

 157. “NAAM, TUKIUJUA WAKATI, KWAMBA SAA YA KUAMKA KATIKA USINGIZI IMEKWISHA KUWADIA;

  KWA MAANA SASA WOKOVU WETU U KARIBU NASI KULIKO TULIPOANZA KUAMINI.” WARUMI 13:11

 158. Bro Mjema …..

  Swali 9:Kwani wewe Haule, Ulipesema Efe6-inatutaka tuvae silaha zote za Mungu tupate kuzipinga hila za mwovu unaelewaje? Ikiwa kuna kuvaha silaha, unafikiri ni ili kwenda kuzurura nazo tu mtaani eeh?

  Jibu: Kama unajua hatuzururi na hizo silaha sasa woga wako hupo wapi! Mjema !!Hata unahubiri injili ya hofu
  silaha zinatutaka tuwe….. Tuwe wakweli, Tusiambiane uongo,Tutende haki,Utayari,Tumwamini Mungu,kuokoka/kumpokea Kristo,Neno la Mungu,Maombi,
  Kama wana wa nuru tutembee nuruni ktk wema wote haki na kweli,Tuzae tunda la Roho/Haki/Nuru,Kujihakiki na Kuukomboa wakati. Tunafanya haya kwa kumaanisha sio kuimba mistari ya maandiko, Tunawezeshwa na ile nguvu itendayo kazi ndani yetu.tTunashinda zaidi ya kushinda kwake yeye atupendaye……Bila wokovu hizi silaha utaziweza,unaweza kuwa mpole lakini sio ule wa tunda la Roho.

  Swali 10:Mimi najua tunapoambiwa tuvae silaha ni ishara kuna Ole,Hatari, Vita ambavyo kama ulivyosema ni vya BWANA. Pia, fahamu kuwa kweli vita ni vya Bwana ila nasi tunasehemu katika kushinda au kushindwa.

  Jibu:
  (i)Nashukuru kama hili umelielewa ndio maana niliandika maandiko haya……
  “Tena napenda kuwakumbusha, ijapokuwa mmekwisha kujua haya yote, ya kwamba Bwana, akiisha KUWAOKOA watu katika nchi ya Misri, aliwaangamiza baadaye wale wasioamini.” Yuda1:5
  “Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua”.1Yohana 3 : 1-6.

  (ii)Sehemu yetu sisi ni kumpokea/kumwamini Mungu na Bwana wetu Yesu Kristo,vinginevyo kwa kutokuamini na kumuona/kumuogopa shetani ana nguvu kama Mungu yatakuwa yale ya wana Israel na ahadi ya nchi ya maziwa,ole ni tahadhari sio kitisho kiasi ufikiri huwezi kuokoka.Adamu alishindwa kwa kuwa aliacha kutii,kumbuka sisi tuna RM,Labda kama amezimishwa kwa udhalimu.
  Mimi sipendi ubabaishaji ktk wokovu, nachukia wale wanaotafuta mistari ya maandiko hili watetee dhambi zaona mara nyingi nawafananisha Yuda kwamba hawajaacha udhalimu.Na udhalima utawapeleka kwenye ziwa la moto,Mungu hafurahii udhalimu,Na wadhalimu wote hawajaikubali ile kweli ya wokovu,kwa hiyo haijawazukia ile nuru ya injili yake Kristo.

  “Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote” 1Jon1:9

  Swali 11:Kumbuka: Mwaz3:15- Mungu ameweka uadui kati yetu na shetani, wewe unafikiri penye uadui hakuna vita?

  Jibu
  (i)sijasema hakuna vita………. Sisi tuliompokea/okolewa tuko upande wa ushindi…….Bwana yuko upande wetu.
  (ii)Pia Yesu Kristo ameshinda Kalvari…..
  (iii)Tunaishinda nia ya mwili ambayo ni mauti, Na ndio uadui maana haitii sheria ya Mungu,Ashukuriwe Yesu Kristo aliyetuokoa …Roho ya Kristo ipo ndani yetu.

  Swali /Maelezo 12:Vita nilivyoeleza huku mbinguni sio vya kutumia M24 za kinabhoko haram la hasa kwani neno linasema vita vyetu sio juu ya nyama na damu, bali falme wa giza. Shetani alipingana na Mungu Mbinguni na hakataka yeye kuwa Mungu. Soma Isa14:12-18 na Ez:28:11-19. Mungu hakumuua shetani kwa kumkemea tu hadi leo. Bali ameachwa hadi siku aliyoiweka Mungu atakapokomesha dhami na mdhambi.

  Jibu:
  (i)Mjema Nakubaliana na wewe kwa sehemu, hv unadhani mimi ninadhani kuwa vita vya mbinguni ni kama boko haram!la hasha

  (ii)shetani kuachwa sio kwamba ana nguvu sawa na Mungu,hiyo miaka unayosema kwa Mungu ni kama siku tu kwake.katika ulimwengu wa roho unaweza ukaona/kuingia kwa sekunde kuyasimulia yale uliyoyaona ktk ulimwengu wa mwili ikakuchukua saa moja nzima.
  shetani aliasi ufalme wa mbinguni anajua kuwa ana muda mchache.watu wa maandiko wana usemi wao kuwa ana miaka mitatu na nusu sasa anahangaika kutafuta waumini wa kumuabudu.alijaribu kumlaghai hata Yesu aingie kwenye ufalme wake.

  (iii)kumbuka Uvumilivu wa Bwana kwetu ni wokovu.

  Swali/Maelezo 13:Hata, sisi leo tunapotenda dhambi, tunakuwa tunafanya vita na Mungu haina maana kuwa Mungu atuwezi bali rehema zake hudumu kuwa nyingi.

  Jibu:Unayosema ni kweli,Tunaokoka kwa rehema/neema ya Mungu yeye ametuhuruku na kutuita kwa majina yetu.kutuzaa mara ya pili kwa Roho,si damu au mapenzi ya mwili tunamepokea neema.

  Swali la Msingi: Tunawezaje kuokoka tungali vitani? Elezea hiyo hali?

  Jibu:Tuamini kwamba Yesu ni Mungu, Tumwabudu,tutende, tuishi, kuzungumza kama tunavyoamini.Tutimize wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka, Mungu ndiye atendaye kazi ndani yenu, tulitimize kusudi lake jema tufanye wajibu wetu na tumtendee Mungu haki,Tusiishi kwa kufuata mwili tuishi kwa kufuata roho,tuhubiri injili.

  Namshukuru Mungu kwa kunitia nguvu/uweza kuandika haya,ni muda mrefu nimeacha kuandika mikeka kama hii.

  Barikiwa Mjema

  Mjoli Haule

 159. Kwako Kaka Mjema,
  Swali1:Umesema Ufu 12-inayoelezea vita mbinguni ni Riwaya tu, Hebu tueleze iyo riwaya ina maana gani basi ili tuichukuaae maana yako.

  Jibu:Nilimaanisha Riwaya/Hadithi ni hili bandiko lako laTarehe 17/05/2014 at 9:18 AM
  Sehemu za riwaya yako,
  -Ufunuo 12:7-12-Inatwambia kulikuwa na vita mbinguni kati ya Mungu vs Shetani!

  Jibu:Shetani hawezi kupigana na Mungu yeye ni kiumbe tu…….angalia Yuda 1:9….kwanini hawakuzichapa? Huwezi kujenga hoja kwa kutumia mstari mmoja. Ndio nikakupa hile Ufu20.Joka nafungwa na Malaika mmoja tu.

  -Ufunuo12:4- inasema, theluthi (1/3) ya malaika watakatifu mbinguni hawakuokoka vitani”

  Jibu:wataokokaje wakati wamechaugua kuasi,yaani mtu kachagua kuasi halafu unataka aokoke kivipi!!!!!
  unatumia mistari hii ya biblia kujenga hoja/fundisho dhaifu.

  Swali 2:Ikiwa Michaeli sio Mungu, ni nani basi huyo? tupe jina la kiumbe huyo kumbuka aya inasema Michaeli na malaika zake wakapigana na……? Zingatia Malaika ni wa Mungu.

  Jibu:maana ya jina Mikaeli ni “NANI KAMA MUNGU”,pia ni malaika mkuu,.mkuu wa mbele(Jemedari),mkuu wa taifa la Israel,ni malaika wa MunguTafakari Dan10.,-12…utamuona na kazi zake au wewe unadhani Mungu alipotuma yule malaika wa kwanza aliposhindwa inamaaninisha Mungu alipigana na mfalme wa uajemi!!?Kwamba yule malaika wa kwanza sio Mungu!!! kwamba kushindwa kwa yule malaika kumpita mfalmea wa anga wa uajemi maana yake yake MUNGU ALISHINDWA!!!?kama utafsiri huko hivyo kazi ipo.Mungu amewapa Malaika uweza na nguvu vile yeye alivyowapa,ujiulize kwa kwanini asimkemee tu mfalme wa uajemi.

  3. Swali 3:Nini maana ya Kuokoka-najua ilishaelezwa maali Fulani lakini hebu na wewe tujulishe.

  Jibu:Kama unajua maana ya kuokoka na ilishaelezwa mahali fulani kwa nini! Unaniuliza? Soma quote yangu ya 09/05/2014 at 3:40 PM nilishajibu kuwa tulinunuliwa, sisi si mali yetu wenyewe “1Cor 6:19-29” Yeye aliungwa na Bwana ni roho moja naye “1Cor6:13,17

  Swali4:Inawezekanaje kuokoka ungalipo vitani?

  Jibu: Nimeshajibu 20/05/2014 at 6:22 PM Labda umeshindwa kuona,angalia jinsii ya kuvua na kuvaa… Efe 6:10-18 ,Rum13:12,14, Efe 4:21-32, Col3:10,12-17 maandiko yako mengi ila wewe huyatendei ,haki,hahuyaamini,unapenda sura na mistari yenye kukukatisha tamaa unadhani ndivyo sote tunayaona hivyo maandiko…MWAMINI YESU AWE BWANA NA MWOKOZI WAKO..mtazame Paul anavyosema
   Bwana ataniokoa na kila neno baya, na kunihifadhi hata nifike ufalme wake wa mbinguni. Utukufu una Yeye milele na milele. Amina.”2Tim4:18”
  Imani yetu ni ya matendo,sio ya maneno .

  Swali 5:Ni lini hasa mtu upata uzoefu wa vita vya kiroho, Je, ni pale tu anapompokea Yesu au Kabla ya Kumpokea Yesu.

  Jibu: Sijakuelewa “unaposema uzoefu wa vita vya kiroho” Kabla mtu hajampokea Kristo huyo mtu shetani ni baba yake ndivyo yavyosema maandiko.uzoefu anapata wapi! naye ni mfungwa.

  Swali6:Haule, hoja zako zinajichanganya, umeanza kwa kusema “Mungu apigani vita” bali yeye anakemea tu. Halafu umemalizia kwa kusema tena umeandika kwa herufi kubwa, VITA NI VYA BWANA. hebu tueleze lipi ni lipi hapa.

  Jibu:Hoja hazijajichanganya Mjema
  Wewe ni mwalimu!! hujui maana ya kukemea imamanisha nini kimaandiko!!?
  Nakuomba pitia maandiko haya ujifunze nini maana ya “kukemea na vita ni vya Bwana”……….Nitakupa mistari ya kuanzia…2Sam 22:7-51….. unashabiana na huu Zab18:1-18,Isa50:,54:9,Zab76:6………sina muda kuyaelezea,Bwana aponye akili zako upate kuelewa na maandiko

  Baada ya kusoma hayo maandiko ,Natumai umepata maana ya “kukemea” na “vita ni vya Bwana” ndivyo nilivyomaanisha mimi.sikuandika kutoka hewani ndiposa nilipokuambia usipite mpaka wa neno la Mungu unapotupiga injili.

  Swali 8:Naona ulianza na mhemuko wa Kipentekoste ukamalizia na Mhemuko wa Kineno. Tueleze msimamo wako kuhusu vita vilivyoelezwa katika Ufu12-ilimaanisha nini. zingatia kujichangaya kwako, Ooh, Mungu hajawahi kupigana vita…,,oooh-Vita nivya Bwana.

  Jibu:
  (i)Hayo ndiyo yakujazayo moyo ukikatwa na upanga wa roho unaona mtu ana mhemuko,UPENTEKOSTE umetoka wapi hapo kwenye maandiko yangu!!

  (ii)kwa hiyo sijajichanganya rejea jibu la swali la7 na maandiko yake kwa uchache nini maana ya vita ni Bwana na Bwana Mungu hajawahi kupigana na shetani, ni kimbe tu kimeumbwa yeye MOLA.

  (iii) ilimaanisha UASI
  (iv)Msimamo sio wangu kama ilivyoelezwa na Ufu 12, ….ni msimamo wa neno la Mungu kuwa tunashinda vita ya uasi kwa damu ya mwana kondoo na ushuhuda wetu……. kuishi ni Kristo kufa ni faida,hiyo vita unayoigopa wewe inaishia kwa joka kufungwa na malaika mmoja tu.Siwezi kusimama na mstari/sura moja nasoma maandiko yote huo ndio msimamo wa maandiko sio wangu

  (v)Msimamo wangu ni huu…
  Nami namshukuru Kristo Yesu Bwana wetu, aliyenitia nguvu kwa sababu aliniona kuwa mwaminifu, akaniweka katika utumishi wake;
  ingawa hapo kwanza nalikuwa mtukanaji, mwenye kuudhi watu, mwenye jeuri, lakini nalipata rehema kwa kuwa nalitenda hivyo kwa ujinga, na kwa kutokuwa na imani.
  Na neema ya Bwana wetu ilizidi sana, pamoja na imani na pendo lililo katika Kristo Yesu.
  Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa, ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni AWAOKOE wenye dhambi; ambao wa kwanza wao ni MIMI.
  Lakini kwa ajili hii nalipata rehema, ili katika mimi wa kwanza, Yesu Kristo audhihirishe uvumilivu wake wote; niwe kielelezo kwa wale watakaomwamini baadaye, wapate uzima wa milele.
  Sasa kwa Mfalme wa milele, asiyeweza kuona uharibifu, asiyeonekana, Mungu peke yake, na iwe heshima na utukufu milele na milele. Amina.1Tim 1:12-17

  …….Mjema nitakujia tena nimalizie yale uliyaleta kwangu.Biblia ina maandiko mengi nimejaribu kukupa hayo machache

  Mjoli Haule

 160. Nawashukru sana wapendwa kwa michango yenu,
  Kwa kweli nimezua na yaliyokuwa yamelala, mimi pia naamini kwa nguvu zote kuwa wokovu ni hapa hapa duniani (We have to start experiencing the beauty of the life to come(heaven) from now on…
  Changamoto niliyokuwa nimekutana nayo ni kuwa wokovu hauwezi potea haijalishi ya maisha ambayo utakufa nayo au Yesu atakukuta nayo.

  Mie niliamini kuwa mtu ukiacha wokovu ukatenda kinyume ungali unaujua ukweli wa neno wazi(ukafikia kuasi) utapoteza wokovu.

  Nahitaji ufafanuzi zaidi kwenye maeneo haya….kuwa ni kweli kuwa Mungu atakuadhibu tu ukiacha wokovu lakini huwezi poteza wokuvu? Au kuna mazingira yoyote ambayo mtu aweza poteza wokovu?
  ……32Tunapohukumiwa na Bwana,tunaadabishwa ili tusije tukahukumiwa pamoja na ulimwengu…….1Kor 11:27-32

  Mtoto wa Mungu hatendi dhambi(Hawezi dumu/endelea ktk dhambi)………….9Yeyote aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi,kwa sababu uzao wa Mungu wakaa ndani yake,wala hawezi tenda dhambi kwa sababu amezaliwa na Mungu. 1Yohana 2:28-29, 3:1-10

  Ahsanteni sana
  Erasto

 161. Haule,

  Asante kwa mcango wako utakaotaka tujue zaidi kuhusu wokovu.

  Kaka, umeeleza sana kupinga hoja nilizotoa. Ila kabla ya kukujibu kwa kina naomba utafakari na kujibu hoja zifuatazo;

  1.Umesema Ufu 12-inayoelezea vita mbinguni ni Riwaya tu, Hebu tueleze iyo riwaya ina maana gani basi ili tuichukuaae maana yako.

  2.Ikiwa Michaeli sio Mungu, ni nani basi huyo? tupe jina la kiumbe huyo kumbuka aya inasema Michaeli na malaika zake wakapigana na……? Zingatia Malaika ni wa Mungu.

  3. Nini maana ya Kuokoka-najua ilishaelezwa maali Fulani lakini hebu na wewe tujulishe.

  4.Inawezekanaje kuokoka ungalipo vitani?

  5. Ni lini hasa mtu upata uzoefu wa vita vya kiroho, Je, ni pale tu anapompokea Yesu au Kabla ya Kumpokea Yesu.

  Haule, hoja zako zinajichanganya, umeanza kwa kusema “Mungu apigani vita” bali yeye anakemea tu. Halafu umemalizia kwa kusema tena umeandika kwa herufi kubwa, VITA NI VYA BWANA. hebu tueleze lipi ni lipi hapa. Naona ulianza na mhemuko wa Kipentekoste ukamalizia na Mhemuko wa Kineno. Tueleze msimamo wako kuhusu vita vilivyoelezwa katika Ufu12-ilimaanisha nini. zingatia kujichangaya kwako, Ooh, Mungu hajawahi kupigana vita…,,oooh-Vita nivya Bwana.

  Kwani wewe Haule, Ulipesema Efe6-inatutaka tuvae silaha zote za Mungu tupate kuzipinga hila za mwovu unaelewaje? Ikiwa kuna kuvaha silaha, unafikiri ni ili kwenda kuzurura nazo tu mtaani eeh? Mimi najua tunapoambiwa tuvae silaha ni ishara kuna Ole,Hatari, Vita ambavyo kama ulivyosema nivya BWANA.

  Pia, fahamu kuwa kweli vita ni vya Bwana ila nasi tunasehemu katika kushinda au kushindwa.

  Kumbuka: Mwaz3:15- Mungu ameweka uadui kati yetu na shetani, wewe unafikiri penye uadui hakuna vita?

  Vita nilivyoeleza huku mbinguni sio vya kutumia M24 za kina bhoko haram la hasa kwani neno linasema vita vyetu sio juu ya nyama na damu, bali falme wa giza. Shetani alipingana na Mungu Mbinguni na hakataka yeye kuwa Mungu. Soma Isa14:12-18 na Ez:28:11-19. Mungu hakumuua shetani kwa kumkemea tu hadi leo. Bali ameachwa hadi siku aliyoiweka Mungu atakapokomesha dhami na mdhambi.

  Hata, sisi leo tunapotenda dhambi, tunakuwa tunafanya vita na Mungu haina maana kuwa Mungu atuwezi bali rehema zake hudumu kuwa nyingi.

  Swali la Msingi: Tunawezaje kuokoka tungali vitani? Elezea hiyo hali?

  Karibu.

 162. Mpendwa Mjema
  Napitia kwa uchache moja ya maandiko yako manyonge.

  Nanukuu
  “kulikuwa na vita mbinguni kati ya Mungu vs Shetani!”

  Bro ………

  Hakujawahi kuwa na vita Mungu vs shetani.

  shetani hawezi kupigana na Mungu haijawahi kutokea na haitatokea,Kamwe,
  shetani anakemewa tu na Bwana Mungu.hiyo vita unayosema ni riwaya ya kusisimua tu haina mantiki.sijui umeitoa wapi!!!?Usimlnganishe Mungu na shetani kiasi eti kuwe na vita kati yao.

  Maaandiko yameandikwa hivi.

  “Ufu12:7-8 Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.”

  Shetani alipigana na Michael na malaika zake sio Mungu

  Injili yako ni ya kupoteza,Umechagua fungu la woga kutuandikia na kumpa utukufu joka,Angalia hapa uweza/Nguvu na Mamlaka ya Mungu

  Ufu 20:1-3

  “Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake. Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu; akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache.”

  ukiendelea mistari ya mbele utaona anafunguliwa kwa muda mchache.

  Ile riwaya/hadithi ya kizee inayokutisha inaishia hapo,

  Tunamuona Malaika Mmoja tu !
  Anamtelemkia shetani na jeshi lake alikonalo toka Mbinguni peke yake anamfunga Dragon,

  Sasa hiyo hofu yako ipo wapi KWAMBA HUWEZI KUOKOKA KWENYE VITA hata kufikia kusema kabla ya hapo kulikuwa hakuna wokovu mbinguni mpaka shetani alivyotupwa chini,

  VITA NI VYA BWANA ………….hii hofu kiasi unatumia mistari ya biblia kujenga hiyo dhana ya mafundisho ya woga kana kwamba vita ni vyetu.

  Naomba utafakari maandiko ya 2Nyakati 20,Tazama Bwana Mungu wa Majeshi anavyotenda matendo makuu,vinginevyo haya maandiko Biblia ni upuuzi mtupu hayana maana yeyeto ni hadithi za kufikirika.

  Unapo tafsiri, Usipite mpaka wa neno la Mungu mpendwa “Hes24:13”

  Tuko na silaha za Mungu sio zetu….

  Unachotakiwa ni kuamini Mungu na kuzivaa kisha kusimama kwa ajili ya siku ya uovu, hii ni baadhi ya mistari ya waaminio….

  Efe 6:10-18 ,Rum13:12,14,Neno la Mungu, Jina la Yesu,

  Bro Mjema……Mwana wa Mungu alidhirihishwa ili kuziharibu kazi za shetani,usizitegemee injili za wasioamini zinapotosha maandiko,hazifundushi ile kweli iletayo utauwa.

  *2Pet1:4………..Yesu aliitoa Nafsi yake ili tuokolewe na uharibifu wa dunia hii”

  Tahadhari kwetu ni …………..

  “Tena napenda kuwakumbusha, ijapokuwa mmekwisha kujua haya yote, ya kwamba Bwana, akiisha KUWAOKOA watu katika nchi ya Misri, aliwaangamiza baadaye wale wasioamini.” Yuda1:5

  Tunaokoka vitani na kwa imani tunatangaza ushindi kama Kalebu na Joshua.

  Ndiyo imani inavyotutaka tuitimize.

  Haiwezekani na haitawezekaa kunywa roho ya mafundisho ya aina nyingine nyingine, Kuwa kuokoka ni baadaye,

  Hakika tutaangamia,Haya ni aina ya mafundisho ya watu waliongia kwa siri kuchunguza uhuru wetu ili watutie tena UTUMWANI.

  *Yoh3:18
  “Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.”

  ………“Mungu kwetu sisi ni Mungu wa kuokoa” Zab 68:20

  Maandiko yameandika wokovu ni sasa…..Amwaminiye yeye hahukumimi

  Hahukumiwi sasa na hata baadaye labda aache wokovu.

  Mjoli Haule

 163. Sungura,
  Kumbe upo rafiki!
  Namshukuru Mungu kukuona tena.
  Nasikitika kukuona umerudi bila ya jipya lolote!! Binafsi nilidhani una mistari ya kunithibitishia kuwa, Yesu alipokufa msalabani, alikufa kutukomboa/kutuokoa na kisha kuendelea kukaa hapa duniani!! Najua wewe na marafiki zako wenye uelewa kama wa kwako, hamtanielewa kwa sasa. Na mtaniona kama ni muongo, mzushi, laghai n.k. kadri mtakavyoweza kuniita. Lakini nina imani, na ninataka kuwatia moyo, mfuatilie maana ya kifo cha Kristo msalabani kama kweli kilimaanisha wokovu mara mbili (duniani na mbinguni).
  Dhana ya “Once Saved Always Saved” , itawatesa marafiki zangu japo baadhi yenu nimewaona mmeanza kuishtukia wenyewe. Sikutarajia miongoni mwenu kuona watu wanaoamini kuwa WAMEOKOKA wakiwa hapa duniani, halafu wanakiri kuwa wanaweza kupotea tena/kutenda dhambi tena!! Hivi kweli kwa maana yaa KUOKOA ya YESU aliyoitangaza msalabani, anaweza kumuokoa mtu (kwa maana ile) halafu bado akapotea? Kama ni ndiyo, bado tunakuita kuwa huko ni kuokoka? Hivi akina Paulo waliokatwa vichwa mchanamchana, nao waliokoka? Akina Yohana Mbatizaji, na mitume wengine waliokaangwa kwenye mafuta kama maandazi, nao waliokoka? Je, akina Bathromayo waliochunwa ngozi wakiwa hai, nao waliokoka? Huku ndiko kuokoka alikokumaanisha Yesu?? Na kama ni kuokoka, ni kuokoka kwa namna gani huku? Bado kweli kwa akili zetu timamu tunaweza kuendelea kukuita kuwa ni KUOKOKA??? Ipo siku Mungu atawafungua tu. Mungu wa Neema yote ni Mungu wa ajabu sana. Taratibu tutaelewana tu.
  Ipo siku mtaelewa kuwa, baada ya mtu kumpokea Kristo, kinachobakia huwa ni safari ya kuuelekea WOKOVU wa Kristo. Na hii ni safari ngumu sana. Inahitaji mtu kujikana nafsi yake na kubeba msalaba wake kila siku akimfuata Kristo kila aendako- Mtt 16:24-25. Kwa nguvu zake, hawezi isipokuwa kwa nguvu za kimbingu. Ni safari ya kutoa maisha yetu (kuacha miili yetu iangamizwe) kwa ajili ya hicho kinachoitwa WOKOVU wa Kristo baadaye. Kristo ni kielelezo chetu. Sharti nasi tuibebe misalaba yetu wenyewe (tafakari aya hii). Kama majemedari wafia dini waliovipiga vita vizuri vya imani, kazi wakaimaliza, na wakatangaza kuwa wanagojea ile medali ya thawabu baada ya kazi ngumu, sharti na sisi tupite njia ileile. Tofauti na hivyo, hakuna usalama wapendwa kwa maana ya WOKOVU. Ndiyo maana Biblia imeandika, ni heri wafao sasa ktk jina lake kama yule mwizi msalabani. Hao wanalo tumaini.
  Kaka Sungura, wokovu, ni zaidi ya hivyo unavyofikiria rafiki. Changamka !! Kama na wewe una ubavu kama ulivyoniambia mimi, nilitarajia kukuona angalau umeyajibu maswali ya ndg yetu Haule ambaye huenda bado anatafakari majibu.
  Siyi

 164. ANASEMA;
  “LAKINI SISI TULIO WA MCHANA , TUWE NA KIASI, HALI TUKIJIVIKA KIFUANI IMANI NA UPENDO, NA CHEPEO YETU IWE TUMAINI LA WOKOVU.” 1 THESALONIKE 5:8

  HIVI KWA NINI MKRISTO KAMA ASKARI ANAKABIDHIWA VITENDEA KAZI
  MARA ANAPOMPOKEA YESU?

  “TENA IPOKEENI CHEPEO YA WOKOVU, NA UPANGA WA ROHO AMBAO NI NENO LA MUNGU” WAEFESO 6:17

  “WALA MSIMHUZUNISHE YULE ROHO MTAKATIFU WA MUNGU; AMBAYE KWA KWA YEYE MLITIWA MUHURI HATA SIKU YA UKOMBOZI” WAEFESO 4:30

 165. Sungura na Rafiki zako,

  Hebu fikirini upya kuhusu “wokovu hapa duniani/katikati ya vita” kupitia mifano mitatu ifuatayo:

  1.Vita Mbinguni !!!?.

  Ufunuo 12:7-12-Inatwambia kulikuwa na vita mbinguni kati ya Mungu vs Shetani!

  -aya ya 12:9-10 inasema ” …yule joka/shetani akatupwa…pamoja na malaika zake…10.Nikasikia sauti mbinguni ikisema sasa kumekuwa WOKOVU,na nguvu….kwa kuwa ametupwa chini…”

  sungura, aya ya 10 inasema baada ya vita ivyo , WOKOVU ulikuwepo mbinguni pale tu alipotupwa hata chini/mbali na mbinguni shetani na malaika zake. Unaona hata mbinguni mahali salama kuliko pote,baada ya uasi wa shetani hapa kuwa salama!

  Pia, aya 12a inasema, “kwa iyo shangilieni mbingu nanyi mkaao humo..” Mbinguni walishangilia Wokovu mara tu adui alipoondolewa mbali nao, Na hvyo ni sahihi kusema Wameokoka. Kabla ya hapo,wakati shetani akingali kati yao haikuwa sahii kusema wameokoka,kwani walikuwa vitani!
  Zingatia: Kumbuka kuwa, katikati ya uwepo wa shetani/vita kuwa Mtakatifu sio kuokoka!Malaika ni watakatifu mno ila hata hivyo wawapo katikati ya vita sio sahihi kusema kuwa wameokoka. Ufunuo12:4- inasema, theluthi (1/3) ya malaika watakatifu mbinguni hawakuokoka vitani. iweje leo mudai kuna wokovu katkat ya vita vilivyo mbele yetu?! Ni kweli tumeitwa tuwe watakatifu lakini ni mpaka tuulinde utakatifu huo hata mwisho wa vita,ndipo tutakapookoka.

  2.Vita Duniani.

  Ufu12:12b-inasema”Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi,akijua ya kuwa ana wakati mchache tu”

  Baada ya Mbinguni kumaliza vita na adui na adui kutupwa hata nchi. Vita vimeamia duniani.Na hapo tunapewa Ole! tutadaije kuwa tumeokoka ktkt ya ole iyo!

  Kumkuka, Adam na Hawa walikuwa ni watakatifu na Weledi wa hali ya juu zaidi mno ya tulivyo leo.Ila hata ivyo walipewa Ole! Na walianguka pia licha ya utakatifu wao.

  daima adui km simba uzunguka zunguka akitafuta mtu ammeze. Usifikiri wanaotafutwa ni wadhambi, bali ni wale walio watakatifu na tusipoulinda utakatifu huo hadi mwisho, hataokoka hata mmoja wetu.

  Kwa iyo naweza kusema, Utakatifu ni sasa ila Wokovu ni hatimaye tutakapoulinda Utakatifu huo hata mwisho wa muda mfupi alionao adui.

  ….Inaendelea…..

 166. sungura, Sio kwamba tunajibu
  vile vile,style ile ile au
  sio kwamba mada
  haituusu. Hatuwezi
  kukaa kimya pale
  ukweli unapopindiswa. Tunajua mmezoea
  kusema “nimeokoka,
  nampenda Yesu” ayo ni
  mazoea tu
  ambayo kwenu nyie
  wapendwa usipoyatamka,
  unaonekana hufai. Kaka, hv kweli
  inaingiaje akilini mtu
  aseme “nimeokoka”
  wakati yupo
  hatarini/vitani. Hv utasemaje “kuna
  kuokoka hapa duniani”
  katikati ya ole/
  tahadhari
  zifuatazo alizozitoa
  Yesu,Yohana na Petro: 1.Ufu12:12- ” …ole wa
  nchi na bahari! kwa
  maana yule ibilisi
  ameshuka kwenu
  mwenye ghadhabu
  nyingi,akijua ya kuwa ana wakati
  mchache tu” 2.1petr5:8- “mwe na
  kiasi na kukesha kwa
  kuwa mshitaki wenu
  ibilisi km
  simba
  angurumaye,huzunguka zunguka akitafuta mtu
  ammeze”. 3.Yoh16:33-” ..ulimwenguni
  mnayo dhiki,lakini
  jipeni moyo mimi
  nimeushinda
  ulimwengu”. ukweli ni kuwa,
  tunapompokea na
  kumkiri Yesu, tunaanza
  kuukulia wokovu
  na tunakuwa
  wakamilifu kila sekunde ya maisha yetu!ambapo
  Yesu akija
  mara,unastahili
  kuokoka-kutengwa
  mbali na adui shetani.,
  Usichanganyikiwe na aya zisemazo, ..na
  Mungu akaliongeza
  kanisa kwa
  hao waliokuwa
  wakiokolewa…
  -okolewa hapo imetumika kuonyesha
  kumpokea au kumkiri
  Yesu. Ili uone
  ukweli wa hoja hii
  angalio swali lifuatalo
  na ujibu, Swali:1. kwa Mujibu wa
  aya mnayopenda
  kuitumia kuonyesha
  wokovu ni
  hapa duniani
  Mdo2:47-” ..Bwana akalizidisha kanisa kila
  siku kwa wale
  waliokuwa
  WAKIOKOLEWA” Hoja: Mdo5:1-11,
  inayoelezea kisa cha
  Anania na Safira,
  waliokuwa
  miongoni mwa hao
  walioliongeza kanisa kwa kuokolewa. Je,
  hawa nao
  walishindwa kuvumilia
  hata mwisho kwa
  kumdanganya Mungu,
  unawaweka kundi gani? Wameokoka
  au la? Swali2: Wakati fulani
  Yesu alisema “waitwao
  ni wengi ila wateule ni
  wachache” ,Je, unafikiri
  aya hii inausianaje na
  wokovu,hasa kusema ni hapa duniani. Swali3:hebu jaribu
  kulinganisha ufafanuzi
  wako wa wokovu
  katika
  nyakati ,past,present na
  future ulioutoa kwny mada ile ya wokovu
  halafu matendo na
  swali kuu ktk post hii,
  Je, mtu akiokoka aweza
  kuanguka tena? Ni sawa
  na muuliza swali angeuliza hivi, Hoja:Mtu akiokoka kwa maana ya past tense
  km ulivyosema, Je, ni
  lazima
  ataipata ile ya present
  na future tense automatic, au
  anaweza kukosa mojawapo
  kati ya izo? Na je,mtu
  akipungukiwa na moja
  wapo tumeweke kundi
  gani,
  ameokoka au hajaokoka? Zingatia
  historia ya Yuda au
  anania na safira
  hapo juu. -ukijibu swali hili kwa
  uaminifu utagundua
  mapungufu ya ufafanuzi
  wenu wa tense. Kumbuka:sio kwamba
  tupo nje ya mada, bali
  tunataka tusilishane
  matango
  pori.tuwe kwny mstari
  kwanza.

  Nakusubiri.Nitakujia na
  3 vivid examples.

 167. sungura,

  Sio kwamba tunajibu vile vile,style ile ile au sio kwamba mada haituusu. Hatuwezi kukaa kimya pale ukweli unapopindiswa.

  Tunajua mmezoea kusema “nimeokoka, nampenda Yesu” ayo ni mazoea tu ambayo kwenu nyie wapendwa usipoyatamka, unaonekana hufai.

  Kaka, hv kweli inaingiaje akilini mtu aseme “nimeokoka” wakati yupo hatarini/vitani.

  Hv utasemaje “kuna kuokoka hapa duniani” katikati ya ole/tahadhari zifuatazo alizozitoa Yesu,Yohana na Petro:

  1.Ufu12:12- ” …ole wa nchi na bahari! kwa maana yule ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi,akijua ya kuwa ana wakati mchache tu”

  2.1petr5:8- “mwe na kiasi na kukesha kwa kuwa mshitaki wenu ibilisi km simba angurumaye,huzunguka zunguka akitafuta mtu ammeze”.

  3.Yoh16:33-” ..ulimwenguni mnayo dhiki,lakini jipeni moyo mimi nimeushinda ulimwengu”.

  ukweli ni kuwa, tunapompokea na kumkiri Yesu, tunaanza kuukulia wokovu na tunakuwa wakamilifu kila sekunde ya maisha yetu!ambapo Yesu akija mara,unastahili kuokoka-kutengwa mbali na adui shetani., Usichanganyikiwe na aya zisemazo, ..na Mungu akaliongeza kanisa kwa hao waliokuwa wakiokolewa… -okolewa hapo imetumika kuonyesha kumpokea au kumkiri Yesu. Ili uone ukweli wa hoja hii angalio swali lifuatalo na ujibu,

  Swali:1. kwa Mujibu wa aya mnayopenda kuitumia kuonyesha wokovu ni hapa duniani Mdo2:47-” ..Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa WAKIOKOLEWA”

  Hoja: Mdo5:1-11, inayoelezea kisa cha Anania na Safira, waliokuwa miongoni mwa hao walioliongeza kanisa kwa kuokolewa. Je, hawa nao walishindwa kuvumilia hata mwisho kwa kumdanganya Mungu, unawaweka kundi gani? Wameokoka au la?

  Swali2: Wakati fulani Yesu alisema “waitwao ni wengi ila wateule ni wachache” ,Je, unafikiri aya hii inausianaje na wokovu,hasa kusema ni hapa duniani.

  Swali3:hebu jaribu kulinganisha ufafanuzi wako wa wokovu katika nyakati ,past,present na future ulioutoa kwny mada ile ya wokovu halafu matendo na swali kuu ktk post hii, Je, mtu akiokoka aweza kuanguka tena? Ni sawa na muuliza swali angeuliza hivi,

  Hoja:Mtu akiokoka kwa maana ya past tense km ulivyosema, Je, ni lazima ataipata ile ya present na future tense, au anaweza kukosa mojawapo kati ya izo? Na je,mtu akipungukiwa na moja wapo tumeweke kundi gani, ameokoka au hajaokoka? Zingatia historia ya Yuda au anania na safira hapo juu.

  -ukijibu swali hili kwa uaminifu utagundua mapungufu ya ufafanuzi wenu wa tense.

  Kumbuka:sio kwamba tupo nje ya mada, bali tunataka tusilishane matango pori.tuwe kwny mstari kwanza.

  Nakusubiri.Nitakujia na 3 vivid examples.

 168. Siyi na rafii zako,

  Nimeshangazwa sana kuona kuwa bado mnasema kitu kilekile kwa maneno yaleyale na kwa mtindo uleule.

  Siyi bado unaendelea kubisha kuwa hakuna kuokoka duniani, pamoja na kukuelimisha vya kutosha kuhusiana na nini maana ya kuokoka. Just kwa sababu ya ufinyu wa kuelewa application ya neno wokovu/kuokoka katika future tense, unaamua kuhitimisha kuwa hakuna kuokoka.

  Unapokutana na neno wokovu au kuokoka katika past tense unajikuta huna cha kusema.UImedanganywa sana na ukadanganyika.

  Umeshindwa kutofautisha tofauti kati ya neno KUOKOKA na neno KUNYAKULIWA.Kile kitendo cha watakatifu kunyakuliwa Yesu arudipo mawinguni wewe ndo unadhani huo ndo wokovu ambao Yesu aliufia msalabani.

  Huwezi kuupiga teke mchokoo, utaishia kuumia mwenyewe. Kuna hoja za Haule hapo juu huwezi kuzipinga wala kuzitolea majibu yamkini.

  Na kama wewe unajidanganya kuwa hakuna kuokoka duniani, tuambie kuokoka kuko wapi mbinguni au wapi? Na pia kama unaamini kuwa hakuna kuokoka duniani basi hukustahili hata kuchangia hii mada, maana kilichoulizwa kinahusu kuokoka hapa duniani.
  Na kwa sababu umeingilia mada ambayo imani yako haikupi nafasi ya kuichangia, ndio maana imejaribu kumlazimisha mleta mada abadili mada yake iwe kama wewe unaavyotaka.

  Siyi wewe ni muongo na umepotoka katika kuufahamu wokovu, acha kuwadanganya watu wa Mungu hapa.

  Kama una ubavu jibu hoja za Haule ukanushe kuwa hakuna wokovu!

 169. ASIYETII HATAOKOKA
  YESU ALIKWISHA FANYA SEHEMU YAKE, BADO SEHEMU YAKO AMBAYO NI UTII NDIO UTAOKOKA.

  “KWA AJILI YA HILO NASTAHIMILI MAMBO YOTE, KWA JILI YA WATEULE ILI WAO NAO WAUPATE WOKOVU ULE ULIO KATIKA KRISTO YESU, PAMOJA NA UTUKUFU WA MILELE” 2 TIMOTHEO 2:10

  “NA HIYO MNAOKOLEWA; IKIWA MNAYASHIKA SANA MANENO NILIYOWAHUBIRI ISIPOKUWA MLIAMINI BURE” 1 WAKORINTHO 15:2
  “JITUNZE NAFSI YAKO, NA MAFUNDISHO YAKO. DUMU KATIKA MAMBO HAYO; MAANA KWA KUFANYA HIVYO UTAJIOKOA NAFSI YAKO NA WALE WAKUSIKIAO PIA.” 1 TIMOTHEO 4:16

  “MAANA, KAMA TUKIFANYA DHAMBI KUSUDI BAADA YA KUUPOKEA UJUZI WA ILE KWELI, HAIBAKI TENA DHABIHU KWA AJILI YA DHAMBI; BALI KUNA KUITAZAMIA HUKUMU YENYE KUTISHA, NA UKALI WA MOTO ULIO TAYARI KUWALA WAO WAPINGAO.” WAEBRANIA 10: 26, 27

  “BASI, KESHENI NINYI KILA WAKATI, MKIOMBA, ILI MPATE KUOKOKA KATIKA HAYA YOTE YATAKAYOTOKEA, NA KUSIMAMA MBELE YA MWANA WA ADAMU.” LUKA 21:36

  “NA MWENYE HAKI AKIOKOKA KWA SHIDA, YULE ASIYEMCHA MUNGU NA MWENYE DHAMBI ATAONEKANA WAPI?” 1 PETRO 4:18

  “BASI, WAPENDWA WANGU, KAMA VILE MLIVYOTII SIKU ZOTE, SI WAKATI MIMI NILIPOKUWAPO TU, BALI SASA ZAIDI SANA MIMI NISIPOKUWAPO….,” WAFILIPI 2:12
  “ ..,UTIMIZENI WOKOVU WENU WENYEWE KWA KUOGOPA NA KUTETEMEKA” WAFILIPI 2:12

  USIPOZAA MATUNDA HUWEZI KUOKOKA, MATUNDA HUTOKANA NA KUTAKASWA NA NENO,UTAKATILIWA MBALI HAPO NDIPO UTAJUA KUMBE NILIKUWA NAUKULIA WOKOVU.

  “KAMA SIVYO, WEWE NAWE UTAKATILIWA MBALI.” WARUMI 11:22

 170. Stephen, kabla sijaomba ufafanuzi wa hoja yako hapo juu, naomba kunukuu maneno machache uliyoyafungia ktk mabano “(yaani ubatizo wa kibiblia wa maji mengi) hapo unakua umeokoka”.

  MASWALI:
  1.Je! hayo maji mengi yanaanzia lita ngapi kibiblia?
  2.kwakua wototo hawana sifa za kubatizwa, Je! wao hawataokoka/hawaokoki, ikiwa watafariki dunia kabla ya kuufikia utu uzima ili wabatizwe?
  3. ikiwa mtu amebatizwa leo na kuokoka, Je! akiiba kesho akapigwa na kuuwawa, atahesabika ktk kundi lipi?
  naomba ufafanuzi tafadhali.

 171. Ndugu na dada katika Kristo,

  Narudi tena ili nilete kwa upya mchango wangu baada ya kuwasoma wapendwa wengi ambao wamechangia vizuri kabisaa.
  Nadhani tatizo ni kuelewa imani na kumwekea Mungu mipaka.

  1. Imani :
  Kuwa na uhakika wa mambo yatarajiwayo, bayana ya mambo yasiyoonekana (EBR 11 :1)
  Watu wengi tuna zowezi la kutia imani katika future; lakini tupime soma tafsiri yote ya imani (EBR11 :2-40)
  -Utagundua imani inalenga vilevile past : « Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, …. »
  -Utagundua pia kama imani inalemga ufahamu wa jinsi wa kale walivyotembea pasipo kuwaona, Hence, hiki kitabu cha Waebrania kinazungmuzia imani katika mantiki ya kusadiki yaliyopita ambayo Mungu aliyafanya, pamoja na waliotutangulia, pia namna tutakavyoishi baada ya kutoka ndani ya mwili licha ya kuwa hatuvione.
  -Pia utaona kama si wote walioamini waliona kwa macho walichokiamini licha ya kuwa imani yao ilikuwa imara : « Ebr.11:13 Hawa wote wakafa katika imani, wasijazipokea zile ahadi, bali wakaziona tokea mbali na kuzishangilia, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya nchi. »
  -Utagundua pia kama imani inavizia kitu kisichoonekana wakati imani inaumbika.
  -Pia tukiendelea soma ile mistari tutafahamu mambo mengi juu ya imani.
  -Tukilirejea andiko « Kwa imani tunaokolewa », ina maana kunaumbika wazo ndani yetu kama tutaokolewa na kwa imani tunalifanya “present fact”, lakini bado kutimikika!!! Sasa tukiiambatanisha na hii Paulo aliyoandika :
  ”2 Timotheo 6 Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa KUFARIKI kwangu umefika. 7 Nimevipiga VITA vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, IMANI NIMEILINDA; 8 baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.”,
  Tutatambua kama utimilifu ni wakati mtu anafariki; hapo ndipo alichokiamini amekipata au la. Kwani unaweza kuwa ulikiamini baadaye ukawa mvivu kiwango ushindwe kukipata.

  Tukiongelea hata jambo lisilo la wokovu, tafakari ukiomba Mungu gari kwa imani; hiyo imani itakuambia kama tayari gari unayo; lakini wakati utakapoomba mara moja tu Mungu akitaka uendelee omba hiyo imani itakuwa imelindwa vibaya na gari hutapata.

  Mimi sisemi kama wokovu ni wakati Yesu atakaporudi(hiyo ni wakati wa kupewa zawabu) lakini wokovu inaota katika imani, inakomaa mpaka utimilifu kwa siku ya kufa. Kwani nyuma ya kifo hakupo tena kulinda au kutolinda imani; hakuna kusimama wala kuanguka, hakuna kufanya kosa wala kuitubu.

  2. Mungu hatiliwe mipaka:

  Si wote wanapitia steps ambazo wandugu wamoja walitiya : “kuamini, kubatizwa katika maji mengi, kukomaa katika imani, kuokoka”. Mfano wa mwivi msalabani watosha ili tufahamu kama Mungu hana mipaka kwa kuokoa mwanaadamu. Huyu mwivi alibatizwa wapi katika maji mengi, alifanya siku ngapi za kukomalia imani?
  Mtu, kwa mfano, anaeamini akiwa mzee anavipiga vita mda kidogo tu lakini akiwa kijana pengine anaweza vipiga mda mrefu. Kila jambo lina mafaa yake: kwa mfano kupiga vita mda mrefu inazaa taji ambayo yule ambaye hakupiga vita hawezi ipata.

  Hizo steps ni moja wapo wa kuokoka lakini si hivyo kwa wote.

  KWA HIVI MTU ANAOKOKA KABISA KABISA ANAPOSHINDA, ANAPOPATA FINAL USHINDI DHIDI YA ULIMWENGU NA MWILI, MAANA YAKE ANAPOFIKA SAA YA KUFA AKIWA AMEPIGA VITA VIZURI KAMA PAULO ALIVYONENA. HII MAPAMBANO INAWEZA IKAWA MAFUPI AU MAREFU. MUNGU MWENYEWE NDIYE ANAFAHAMU MDA.

  HENCE, HIVI NI KWA MWISHO, MTU ANAPOOKOKA, HAWEZI TENA POTEZA HUO WOKOVU. YUDA ALIAMINI LAKINI HAKUOKOKA. ANGELIOKOKA BILA SHAKA ANGELIUSHINDA ULIMWENGU. LAKINI ULIMWENGU ULIMSHINDA AKAAMUA MWENYEWE KUJITUNDIKA.

  Mbarikiwe wapendwa!

 172. catherine,

  Jibu1.-Biblia inasema tuenende kwa Roho kamwe hatutatimiza matendo ya mwili. Pia inasema wenye matendo hayo aliyoyataja paulo kwa hao ndugu yaani wivu na magombano kamwe hawataiona mbingu. soma Gal6.

  Jibu2- ndio biblia inayo mfano wa mtoto wa Mungu aliyetenda dhambi bali kurudi kutubu.

  Yuda: mwanafunzi wa Yesu baada ya kumsaliti Yesu, aliungama tu, ila hakufanya toba. kifo cha Yuda kinaonyesha hakutubu hivyo bila shaka hataokoka Yesu ajapo.

 173. Mimi naamini kabisa kua, mtu aliyeokoka ni kweli anaweza kupoteza wokovu wake tena. Kuokoka ni kuokolewa kutoka kwenye nguvu za giza(dhambi) ambapo kupitia Yesu kristo, tunapata msamaha wa ondoleo la dhambi. Kwa hiyo, Kuokoka ni “kufanywa mpya” > kubadilika na kumuendea Mungu katika njia zake kama anavyotaka kwenye neno lake, Yaani sasa unakua ni mtoto wa Mungu. Lakini pale tunapomkosea Mungu kwa sababu ya udhaifu wetu wa kibinadamu, basi itatubidi tuache mara moja njia zetu mbaya na kutubu kwa jina la Yesu, kwa lengo la kuendelea kuukulia wokovu ili tubakie kua watoto wa Mungu. Sasa, kwa maelezo hayo hapo juu unafikiri ni kwanini isiwezekane mtu kuupoteza wokovu wake, kama atayarudia maisha yake ya dhambi na kukataa kutubu kwa njia ya kristo Yesu?, hapo huoni kua wokovu sio tiketi kwamba umeishika siku zote bali wokovu ni kusamehewa dhambi na kuishi kwa kufuata neno la Mungu ili shetani asikuangushe tena?. Istoshe mimi sikubaliani pia na yule mchangiaji wa kwanza aliesema kua eti hapa duniani hatuokoki, ila tutaokoka siku ya mwisho bwana yesu atakapokuja !!!!, Sio kweli kabisa. Sisi watoto wa Mungu tunasema kua tayari tumekwishaokoka kwa kua tayari tumeukiri wokovu wetu kwa vinywa vyetu kama biblia inavyofundisha na kutaka tuamini hivyo. Sisi tumeshamuamini bwana yesu na kwa hiyo, Tayari kwa njia ya kristo Mungu wetu anatuhesabia haki kwenye maisha yetu kama watoto wake sasa hivi na hata mwisho wa dunia kristo atakaporudi, hatuwezi tena kuishi maisha ya unyonge kama watu wanaosubiri kutayarika, Soma(warumi 10:10-11). Sisi ni tofauti kabisa na watu wa dini nyingine, ndiyo maana watu wa dini nyingine wanafundishwa kuiogopa ile siku ya mwisho, wakati sisi tunaisubiri kwa hamu kubwa ili tumuone bwana akija kututwaa. Swala la siku ya mwisho haswa linahusu kutwaliwa”Kunyakuliwa” , hivyo, usitegemee kabisa kuja kutwaliwa na wakati kwa sasa hujiamini na unasema eti mpaka siku hiyo ndiyo utaokolewa. Wokovu wetu hauwi nje kwa macho ya kibinadamu bali unazaliwa ndani ya mioyo yetu tayari. Neema ya kristo inayosamehe, pia inabadilisha, kwa hiyo, kama wewe hujabadilishwa basi Pia hujasamehewa, ndio maana neno la Mungu linasema” JIJARIBUNI WENYEWE KWAMBA MMEKUA KATIKA IMANI, JITHIBITISHENI WENYEWE, AU HAMJUI WENYEWE KWAMBA YESU KRISTO YU NDANI YENU?,Soma(2Wakorintho13:5-6). Sisi hatumsubiri kristo ili eti ndio tuokolewe, LA HASHA…Kwa kua tayari kristo tunae mioyoni mwetu ila tunachosubiri ni ile parapanda ya mwisho ya kuja kunyakuliwa kutoka katika ulimwengu huu wa dhambi na uonevu. Bwana yesu tayari alikwisha tuokoa toka kwenye dhambi, magonjwa, umasikini, huzuni, taabu, nk….ndiyo maana biblia kumhusu shetani na nguvu zake kwetu inasema”AMEKWISHASEGWA CHINI YA MIGUU YENU”. Sasa kwa hali hiyo tunataka tuokolewe vipi tena zaidi ya kuchukua jukumu letu la kupandisha viwango vyetu vya imani lili tuanze kufaidi matokeo kungali bado kweupe ?!!, Sisi inatupasa tue na mamlaka ya kufaidi hapahapa duniani hata kabla ya ile faidi kuu katika uzima wa milele kwa kua tayari tunalo jina kuu lipitalo majina yote. MBARIKIWE.

 174. Mungu akubaliki muuliza mada nami naomba nichangie kama ifutavyo baada ya kuona wapendwa wanachanganya sana na hiyo inatokana na mapokeo ya madhehebu ebu tuangalie neno la Mungu linavyo sema
  1.kuokoka kunakuja baada ya kukamilisha mambo yafuatayo moja sharti uwe umehubiliwa habali njema za Yesu ambazo zinakataza ubaya wa kila aina.pili uwe umeziamini au kuamini neno ulilo hubiliwa.tatu unatakiwa kubatizwa ubatizo wa kufa na Yesu(yaani ubatizo wa kiblblia wa maji mengi) hapo unakuwa umeokoka. soma ushaidi (marko 16:-15..16/warumi 6:1….6) jambo linalowachanganya wengi ni hiliambalo limenukuliwa katika (mathayo 10:22) hapa Yesu alikuwa anaeleza kipindi cha dhiki kubwa ambacho kitaanza baada ya kanisa la Mungu kunyakuliwa na hao waozungumuzwa hapo ni waisrael ndio yesu anasema kama siku zisingefupizwa aingeokoka hata mmoja unajua katika kipindi cha dhiki kubwa watakaookolelewa ni waisrael peke yake yaani katika makabira kumi na mbili ya wana wa israel kila kabila watu kumi na mbili elfu na hili ni somo lingine nalo ni lefu naomba nikaze hapa wokovu ni sasa soma (2wakolinto 6:-2/zaburi 16:3) na wengine wameingiza kutakaswa au utakso hii ni kwa wale waliookolewa wapoendelea kujifunza neno neno ndilo linalowatakasa soma (yohana 17:17)kwa kuelewa soma hiyo sura yote mwisho niseme mtu aliyeokoka anaweza kuanguka tena yuda isikaliote aliokolewa lakini alianguka ndio maana biblia inaasema mwenye haki anaanguka mara saba na anasimama hii ina maana unapookoka unakuwa mwenye haki unapojua umekosa unapaswa kuomba rehema na kuendelea kutenda haki
  balikiwa wote kwa michango

 175. Bro Siyi,
  Sikubaliani na Mafundisho yako kwa sehemu,

  1.UTAOKOKA NI FUTURE TENSE/wokovu sio sasa
  (Tutumie hiyo Biblia ya kiswahili).

  Angalia hii mistari na haya maneno ALITUOKOA/TULIOKOLEWA/ALITUOKOA
  *2Tim1:9 -12 Ambaye ALITUOKOA akatuita kwa mwito mtakatifu, ……………………wala sitahayari; kwa maana namjua yeye niliyemwamini, na kusadiki ya kwamba aweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake hata siku ile.(He has saved us and called us to a holy life)
  *Rumi8:24 Kwa maana TULIOKOLEWA kwa taraja; lakini kitu kilichotarajiwa kikionekana, hakuna taraja tena. Kwa maana ni nani anayekitarajia kile akionacho?
  *Tito3:4-5 Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, ALITUOKOA; si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu;

  Unaona Bro Fundisho lako halina mashiko kwamba kuokoka ni baadaye.kufutana na mistari hii.

  2.KWAMBA KUNA TOFAUTI YA KUMPOKEA KRISTO NA KUOKOKA
  Umeandika….
  ”Erasto, inabidi utofautishe kuokoka na kumpokea Kristo. Duniani hapa, hatuokoki.
  Angalia maandiko haya……
  Yoh1:12 -13Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.
  Rum10:9  Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.

  Unaona Bro….
  Ukimuamini/Mkiri Kristo maana yake ndio KUMPOKEA/KUOKOKA kwa hiyo hakuna tofauti ya kumpokea na kuokoka.

  Tupitie maandiko haya………….
  Efeso 2.1-10 Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu;
  ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi;
   ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine.
  Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda;
  hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema.
  Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu;
  ili katika zamani zinazokuja audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu sisi katika Kristo Yesu.
  Kwa maana MMEOKOLEWA kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;
  wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.
  Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.

  Bro Siyi Tulikuwa wafu,
  Mungu kwa mapenzi yake ametuuisha tumeokolewa kwa neema,tukiitwa/tukijiita TUMEOKOKA ndivyo tulivyo maandiko yanasema hivyo,Yaani kubali/ukatae /ukasirike/ucheke.

  1 Yohana 3 : 1-6
  Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye.
  Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo.
  Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu.
  Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi.
  Nanyi mnajua ya kuwa yeye alidhihirishwa, ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo ndani yake.
  Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua.

  Bro Siyi neno linabaki hivyo hakuna tafsiri hapo.

  Ubarikiwe

  Mjoli Haule

 176. Ahsanteni sana Joyce, M.J. Siyi na lenda kwa michango yenu;

  Naomba tuchunguze pia Paulo aliandika akisema; Ndugu zangu, mimi sikuweza kusema nanyi kama watu wa kiroho,bali watu wa mwilini, kama watoto wachanga katika Kristo.2Naliwanywesha maziwa, wala si chakula kigumu, kwa kuwa hamkuwa tayari kwa hicho chakula kigumu.Naam hata sasa hamkiwezi.3Kwa maana ninyi bado ni watu wa mwilini.Kwa kuwa bado kuna wivu na magombano miongoni mwenu, je, ninyi si watu wa mwilini, nanyi mnakwenda kwa jinsi ya kibinadamu?………….. 1Kor 3:1-4

  1.Swali langu hapa; hawa wapendwa kama Yesu angerudi wakati Paulo anawakuta wangepata wokuvu/wangeokoka, maana tunaona walikuwa wameamini lakini bado walikuwa wanamatendo ya kimwili kwa sababu ya uchanga wao.

  15 Kama kazi ya mtu itateketea,atapata hasara,ila yeye mwenyewe ataokolewa, lakini kama mtu aliyenusurika kwenye moto 1Kor 3:12-15

  2.Ninachohitaji hapa ni kupata ufafanuzi wa kifungu hicho….

  3.Hivi wapendwa, kibiblia tunaweza pata mfano wowote wa mtoto wa Mungu ambaye aliwahi tenda dhambi asirudi kutubu?

  Mbarikiwe sana watumishi!

  Erasto

 177. LUGHA YA KIGENI IMETUMIA MANENO HAYA;
  1. JUSTIFICATION/KUHESABIWA HAKI
  HII NI KAZI YA MUNGU MWENYEWE KAMA HAKIMU.

  “NI NANI ATAKAYEWASHITAKI WATEULE WA MUNGU? MUNGU NDIYE MWENYE KUWAHESABIA HAKI.” WARUMI 8:33
  KUMBUKA MWIZI MSALABANI ALIMWAMINI YESU AKAHESABIWA HAKI PALE PALE LAKINI ANGEENDELEA KUISHI DUNIANI ANGETAKIWA KUONYESHA KUWA AMEAMINI KWA KUTAKASA MAFU KWA KUONYESHA HAIBI TENA. HAPO ANGEONYESHA AMEZALIWA UPYA KWELI KWELI. NI KOSA KUBWA KUSUBIRI UMEKARIBIA KUFA NDO UTENGENEZE MAMBO YAKO. NAFASI YA HUYU MWIZI SI YAKO.

  2. SANCTIFICATION/KUTAKASWA
  HII KAZI YA MUNGU KAMA TABIBU AU DAKITARI KUTUTIBU NA MAMBO YA UFU/KUFISHA ROHO.
  “ILI MPATE KUJUA YA KUWA MIMI NDIMI BWANA NIWATAKASAE” KUTOKA 31:13
  YESU NI BWANA NA NDIYE NENO, NA NENO NDIYE/NDILO LITUTAKASALO
  “UWATAKASE KWA ILE KWELI; NENO LAKO NDIYO KWELI” YOHANA 17:17
  “NA BAADHI YENU MLIKUWA WATU WA NAMNA HII; LAKINI MLIOSHWA,LAKINI MLITAKASWA,LAKINI MLIHESABIWA HAKI KATIKA JINA LA BWANA YESU KRISTO,NA KATIKA ROHO WA MUNGU WETU.” 1 WAKORINTHO 6:11
  “MUNGU WA AMANI MWENYEWE AWATAKASE KABISA;..” 1 WATHESALONIKE 5:23

  3. REGENERATION/KUKUA/KUZALIWA UPYA
  HUU NI MWITIKIO UNAOONEKANA/MABADILIKO/ANAOONESHA MTU ALIHESABIWA HAKI NA KUTAKASWA BAADA YA KAZI YA MUNGU YA KUTUHESABIA HAKI NA KUTUTAKASA,
  “MTU ASIPOZALIWA MARA YA PILI,HAWEZI KUUONA UFALME WA MUNGU” YOHANA 3:3
  “KAMA WATOTO WACHANGA WALIOZALIWA SASA YATAMANINI MAZIWA YA AKILI YASIYOGHOSHIWA,ILI KWA HAYO MPATE KUKUKULIWA WOKOVU.” 1 PETRO 2:2

  AINA ZA KUOKOA ZILIZONGUMZIWA NDANI YA BIBLIA
  MOJA: KUOKOA KUTUTOA MATEKA KUTOKA KWA SHETANI KATIKA VITA YA MUNGU NA IBILISI.

  “NAYE ALITUOKOA KATIKA NGUVU ZA GIZA, AKATUHAMISHA NA KUTUINGIZA KATIKA UFALME WA MWANA WA PENDO” WAKOLOSAI 1:13
  “LAKINI WEMA WAKE MWOKOZI WETU MUNGU, NA UPENDO WAKE KWA WANADAMU, ULIPOFUNULIWA, ALITUOKOA.” TITO 3:4

  MBILI: KUOKOLEWA KILA SIKU KAMA HATUA YA KUTAKASWA NA JAMBO TULILOKUWA HATUJALIFUATA KATIKA NENO LAKE.
  “MKIOKOLEWA NA UHARIBIFU ULIOMO DUNIANI KWA SABABU YA TAMAA” 2 PETRO 1:4

  TATU: KUOKOLEWA /KUTUTOA MAKABURINI/KUTUPA MIILI MIPYA NA DUNIA MPYA ILIYOTENGWA NA UOVU/MWISHO WA PAMBANO LA WEMA NA UOVU.
  “NANYI MTAKUWA MKICHUKIWA NA WATU NA WATU WOTE KWA AJILI YA JINA LANGU; LAKINI MWENYE KUVUMILIA HATA MWISHO, NDIYE ATAKAYEOKOKA”
  MATHAYO 10:22
  “BALI TWAAMINI KWAMBA TUTAOKOKA KWA NEEMA YA BWANA YESU VILEVILE KAMA WAO”
  MATENDO 15:11

  KUMBUKA KAZI YA YESU NA MSALABANI NI KUTUOKOA NA DHAMBI LAKINI YUKO PATAKATIFU MBINGUNI AKIFANYA UPATANISHO. SISI TUNAPEWA OLE MAANA TUKO UWANJA WA VITA.

  MUNGU ANATUPA HAKI KWA IMANI.
  “SASA KUMEKUWA WOKOVU,” UFUNUO 12:10 NI TANGAZO LA HAKI KWA KUIAMINI DAMU.
  MAANA SHETANI HASIMAMI TENA MBELE YA MUNGU KUTUSHITAKI KAMA AYUBU.
  “NAO WAKAMSHINDA KWA DAMU YA MWANAKONDOO NA KWA NENO LA USHUHUDA WAO; AMBAO HAWAKUPENDA MAISHA YAO HATA KUFA” UFUNUO 12 :11

  KWA HIYO HAKI,UTAKASO NA KUKUA NI VITU VITATU AMBAVYO KILA MKRISTO ANAYEISHI DUNIANI LAZIMA AWE NAVYO ILI AOKOKE.
  LAKINI KAMA NINGEKUFA PALE MSALABANI KAMA YULE MWIZI NINGEKUWA NIMEPITA NIMEANDIKWA MBINGUNI KWA KUAMINI TU. MWIZI HAKUHITAJI BIBLIA KWA KUWA ALIMALIZA SAFARI PALE.
  HIVYO , ALIHESABIWA HAKI. ILA ANGEENDELEA KUISHI DUNIANI. ANGETAKIWA AFUATE NENO.

  PETRO INGAWA NI MKRISTO ALIPITIA MAMBO MATATU YA LAZIMA KWA MKRISTO ANAYEMPOKEA YESU NA KUENDELEA KUISHI DUNIANI;
  1. KUHESABIWA HAKI/JUSTIFICATION
  2. UTAKASO/SANCTIFICATION
  3. REGENERATION KUKUA KATIKA KRISTO.

  BAADA YA KUSEMA UONGO/KUSEMA HAMJUI YESU, ASINGETUBU ANGEPOTEA
  “BALI TWAAMINI KWAMBA TUTAOKOKA KWA NEEMA YA BWANA YESU VILEVILE KAMA WAO”
  MATENDO 15:11

  UKIMPOKEA YESU TEMBEA KATIKA KUITII KWELI/UTAPATA SANCTIFICATION UTAKASO WA MAMBO MAFU NA KUTENGENEZWA KAMA PETRO ILI UFANANE NA TABIA YA MBINGUNI. NA BIBLIA/NENO NDIYO HUTUTENGENEZA TABIA. USIPOSOMA BIBLIA NA KUTII UTARUDIA MATAPISHI. BILA KUWA NA TABIA YA MBINGUNI HUWEZI KUOKOLEWA SIKU YA MWISHO/WALA KUMWONA MUNGU. MAANA YEYE NI MOTO ULAO NA HUUNGUZA KILA UCHAFU DHAMBI. HUONDOA KILA UCHAFU KWA NENO.
  YOHANA 17:17

  “AMBAYE ALIJITOA NAFSI YAKE KWA AJILI YA DHAMBI ZETU, ILIATUOKOE NA DUNIA HII MBOVU,ILIYOPO SASA, KAMA ALIVYOPENDA MUNGU,BABA YETU.” WAGALATIA 1:4

  JE WAWEZWAFUTWA BAADA YA KUMKUBALI BWANA?

  “BWANA AKAMWAMBIA MUSA, MTU YEYOTE ALIYENITENDA DHAMBI NDIYE NITAKAYEMFUTA KATIKA KITABU CHANGU” KUTOKA 32:33

  UNAPOMPOKEA YESU UNAANDIKWA KATIKA KITABU CHA UZIMA. LAKINI SI KWAMBA UMEMALIZA KAZI UNAWEZAFUTWA UKICHAGUA DHAMBI TENA. KAZI YAKO NI KUPALILIA JINA LIBAKI KITABUNI (KUUKULIA WOKOVU/REGENERATION.) KWA KUTII KILA NENO.

  “NA KUWAFUNDISHA KUYASHIKA YOTE NILIYOWAAMURU NINYI” MATHAYO 28:20

 178. Joyce
  Shaloom,
  Naomba ulinganishe na kulinganua kati ya kuokoka hapa duniani vs uzima wa milele mbinguni!
  Nakungoja

 179. Ubarikiwe sana Erasto
  Nimekupata ndg yangu. Nami naanza kudonoa lile la kwanza uliloulizia kwanza la warumi 11:17-24. Umeulizia kwa habari ya mstari wa 22 Tazama, basi, wema na ukali wa Mungu; kwa wale walioanguka, ukali, bali kwako wewe wema wa Mungu, ukikaa katika wema huo; kama sivyo, wewe nawe utakatiliwa mbali.
  Maana yake,
  Kama mtu (wewe) uliyempokea Kristo utaendelea katika utakatifu (utiifu wa neno la Mungu), rehema za Mungu zitaandamana nawe naam, agh. uzima wa milele. LAkini kama utakaidi(utaanguka), hasira ya Mungu itawaka juu yako. Tii uishi, asi ufe!!
  Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.Warumi 10:9-10
  Maana yake;
  Unapompokea/mwamini Kristo, hata kama utakufa leo au kesho, siku atakapokuja Kristo, atakuokoa siku ya mwisho. Wokovu ni siku ya mwisho kaka na siyo sasa. Ndiyo maana kuna future tense hapo “UTAOKOKA” baadaye!!. Ndiyo maana mtu anaweza kumpokea/kumwamini Yesu leo, kesho akaasi tena. Hatuwezi kusema kuwa aliokoka halafu akapotea tena!! Hata waswahili wa kawaida watatushangaa!!! Sasa hivi, tunaunza tu mchakato wa wokovu kwa kumwamini na kutembea katika Kristo. Hatima/kukamilishwa kwa wokovu huu, ni mpaka Yesu aatakaporudi kuwakomboa waatakatifu wake, ukiwemo wewe na mimi kama tutaishi kwa kulitii neno la Mungu huku tukisulubishwa kila siku katika miili hii ya nyama.
  Kaka, M.J. Siyi
  Unaweza eleza zaidi kuwa mtu aliyempokea Kristo anapashwa awe hatua ipi kati ya
  1.kumpokea Yesu 2.Kutakaswa(process) 3. Kutukuzwa ili aweze pata wokuvu siku ya mwisho?Sijakupata vizuri hapo
  Mwitiko wangu
  Kwa kawaida ndg Erasto, hatua ya mtu kuupata wokovu siku ya mwisho ni ile hatua ya kutukuzwa- Glorification. Hii ni hatua ya mwisho mtu anaupata wokovu. Lakini ikumbukwe kuwa, kuna mazingira ambayo mtu anaweza kupata wokovu hata kabla ya kufikia hatua ya 2 au 3. Kwa mfano, mgonjwa anayetaka kufa, ukimwamini Kristo saa ya mwisho ya kukata roho na akatubu dhambi zake zote, Yesu atamtukuza mtu huyo siku ya mwisho. Kuna wengine hufariki baada tu ya kumwamini Yesu aidha kwa ajali, au kuuawa kwa makusudi, hawa Kristo atawatukuza pamoja naye siku atakaporudi. Mfano mwingine mzuri ni wa yule mwizi msalabani.
  Lakini tofauti na mazingira hayo au yanayofanana na hayo, mtu sharti aanze na kummwamini Kristo kwanza, halafu amjifunze (akue katika imani, akiacha uovu mmoja baada ya mwingine) na hatimaye ajapokufa au kama atakutwa yu hai Kristo atakaporudi, atatukuzwa katika ufalme wa Mungu.
  Nina imani nimeeleweka . Kama kuna shida nyingine zaidi, karibu tena rafiki.
  Ubarikiwe sana.
  Siyi

 180. imeandikwa mtu akiwa ndani ya Kristo amekua kiumbe kipya ya kale yamepita sasa yanekua mapya.na imeandkwa aamibiye na kubatizwa ataokoka.hvo tunaokoka duniani na mbinguni uzima wa milele.

 181. Ahsanteni sana kwa wale ambao mmechangia mpaka sasa; Mungu azidi kuwabariki!

  Naomba ufafanuzi wa mafungu haya wapendwa…..naamini nitaelewa kirahisi zaidi nikiwa nataja mistari ambayo hunitatiza!

  ………22 Tazama, basi, wema na ukali wa Mungu, kwa wale walioanguka, ukali,bali kwako wewe wema wa Mungu, ukikaa katika wema huo;kama sivyo, wewe nawe utakatiliwa mbali.(………..22 Notice how God is kind and severe .He is severe toward those who disobeyed, but kind to you if you continue to trust in His kindness.But if you stop trusting,you also will be cut off.) Warumi 11:17-24

  Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.Warumi 10:9-10

  Kaka, M.J. Siyi
  Unaweza eleza zaidi kuwa mtu aliyempokea Kristo anapashwa awe hatua ipi kati ya
  1.kumpokea Yesu 2.Kutakaswa(process) 3. Kutukuzwa ili aweze pata wokuvu siku ya mwisho?Sijakupata vizuri hapo

  Barikiweni sana!
  Erasto

 182. DHANA YA YESU YA ALIYEOKOKA NI JAPO MTU KUWA AMEMWAMINI
  APIGANE MPAKA MWISHO. NDIYO ATAOKOKA/ATAITWA AMEOKOKA.

  “NANYI MTAKUWA MKICHUKIWA NA WATU NA WATU WOTE KWA AJILI YA JINA LANGU; LAKINI MWENYE KUVUMILIA HATA MWISHO,NDIYE ATAKAYEOKOKA”
  MATHAYO 10:22

  “NA KAMA SIKU HIZO ZISINGALIFUPIZWA,ASINGEOKOKA MTU YEYOTE;;LAKINI KWA AJILI YA WATEULE ZITAFUPIZWA SIKU HIZO.
  MATHAYO 24:22

  ONA HAPA MUHUSIKA MWENYEWE (YESU) ANAVYOSEMA;INGAWA KUNA WATEULE AMEHITAJI MUDA UFUPISHWE ILI WAOKOLEWE.

  HATUSEMI NIMEOKOKA KATIKATI YA VITA.
  SOMA UFUNUO, KWA NINI YESU JAPO YA KUTOA SIFA KEMKEM KWA YALE MAKANISA. BADO ANAYATAKA YASHINDE.
  MAKANISA HAYO YALIKUWA KATIKA KUUKULIA WOKOVU
  1 PETRO 2:2,3,9

  SIKIA PETRO TAYARI AMEMPOKEA YESU LAKINI ANASEMA HIVI;

  “BALI TWAAMINI KWAMBA TUTAOKOKA KWA NEEMA YA BWANA YESU VILEVILE KAMA WAO”
  MATENDO 15:11

  MTU ALIYEMPOKEA/ALIYEONGOKA YESU ANAWEZA KUANGUKA?
  “WALA ASIWE MTU ALIYEONGOKA KARIBU,ASIJE AKAJIVUNA AKAANGUKA KATIKA HUKUMU YA IBILISI”
  TIMOTHEO 3:6

  MUULIZA SWALI TAZAMA PIA WOKOVU IMETUMIKAJE?

  “ATATOKEA MARA YA PILI, PASIPO DHAMBI,KWA HAO WAMTAZAMIAO KWA WOKOVU.”

  “..KWA KUWA MUNGU AMEWACHAGUA TANGU MWANZO MPATE WOKOVU,KATIKA KUTAKASWA NA ROHO NA KUIAMINI KWELI,”
  1 WATHESALONIKE 2:13

  “KWA MAANA WALE WALIOKWISHA KUYAKIMBIA MACHAFU YA DUNIA KWA KUMJUA BWANA NA MWOKOZI YESU KRISTO, KAMA WAKINASWA TENA NA KUSHINDWA,HALI YAO YA MWISHO IMEKUWA MBAYA KULIKO ILE YA KWANZA”
  2 PETRO 2:

  NI JAMBO LA KUTISHA KUANGUKA MIKONONI MWA MUNGU

  “NI JAMBO LA KUTISHA KUANGUKA KATIKA MIKONO YA MUNGU ALIYE HAI”
  WAEBRANIA 10:31

  MWISHO:KUMBUKA KUTOFAUTISHA KUOKOKA NA KUONGOKA

  MAFUNGU HAPO JUU YAMETOA MAJIBU MATHAYO 10:22,TIMOTHEO 3:6

 183. Bwana Yesu asifiwe !

  Jambo hili linaonekana kuwa rahisi kujibu, lakini kujibu ipasavyo ni vigumu.

  Tusome pamoja maandiko haya matatu :

  « Waebrania 6 : 1 Kwa sababu hiyo, tukiacha kuyanena mafundisho ya kwanza ya Kristo, tukaze mwendo ili tuufikilie utimilifu; tusiweke msingi tena wa kuzitubia kazi zisizo na uhai, na wa kuwa na imani kwa Mungu,
  2 na wa mafundisho ya mabatizo, na kuwekea mikono, na kufufuliwa wafu, na hukumu ya milele.
  3 Na hayo tutafanya Mungu akitujalia.
  4 Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu,
  5 NA KULIONJA NENO ZURI LA MUNGU, NA NGUVU ZA ZAMANI ZIJAZO,
  6 WAKAANGUKA BAADA YA HAYO, HAIWEZEKANI KUWAFANYA UPYA TENA HATA WAKATUBU; KWA KUWA WAMSULIBISHA MWANA WA MUNGU MARA YA PILI KWA NAFSI ZAO, NA KUMFEDHEHI KWA DHAHIRI.
  7 Maana nchi inayoinywa mvua inayoinyeshea mara kwa mara, na kuzaa mboga zenye manufaa kwa hao ambao kwa ajili yao yalimwa, hushiriki baraka zitokazo kwa Mungu;
  8 bali ikitoa miiba na magugu hukataliwa na kuwa karibu na laana; ambayo mwisho wake ni kuteketezwa.
  9 Lakini, wapenzi, ijapokuwa twanena hayo, katika habari zenu tumesadiki mambo yaliyo mazuri zaidi, na yaliyo na wokovu.
  10 Maana Mungu si dhalimu hata aisahau kazi yenu, na pendo lile mlilolidhihirisha kwa jina lake, kwa kuwa mmewahudumia watakatifu, na hata hivi sasa mngali mkiwahudumia. »

  Pia :

  « 2 Timotheo 4 : 6 Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika.
  7 NIMEVIPIGA VITA VILIVYO VIZURI, MWENDO NIMEUMALIZA, IMANI NIMEILINDA;
  8 baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake. »

  Pia :

  « Yohana 10 : 24 Basi Wayahudi walimzunguka, wakamwambia, Hata lini utatuhangaisha nafsi zetu? Kama wewe ndiwe Kristo, utuambie waziwazi.
  25 Yesu akawajibu, Naliwaambia, lakini ninyi hamsadiki. Kazi hizi ninazozifanya kwa jina la Baba yangu ndizo zinazonishuhudia.
  26 Lakini ninyi hamsadiki, kwa sababu hammo miongoni mwa kondoo wangu.
  27 Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata.
  28 NAMI NAWAPA UZIMA WA MILELE; WALA HAWATAPOTEA KAMWE; WALA HAKUNA MTU ATAKAYEWAPOKONYA KATIKA MKONO WANGU.
  29 Baba yangu aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote; wala hakuna mtu awezaye kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu.
  30 Mimi na Baba tu umoja. »

  Tukiyatafakari, tutaona mara na mara tunaambatanisha mambo yasiyo na mantiki sawa : « kuamini » na « kuokoka »
  -Anaeamini ni yule anaeonja. Akiacha na kurudi nyuma anapoteza vyote.
  -Anaeokoka ni yule anaeamini na kuitika kuambatana na Kristo, kupiga vita mpaka mwisho.

  Kuamini ni neema tu, lakini kuokoka ni kuitika pia mapambano.

  Hivi tukitofautisha haya mambo mawili, tutaona kama ALIEOKOKA HAWEZI ANGUKA TENA kwa sababu amekuwa ndani ya mikono ya Kristo,Kristo ni ndani yake naye ndani ya Kristo, ameitika kuteswa kwa ajili ya Kristo ; lakini alieamini tu anaweza rudi nyuma na kuanguka. Biblia inasema kama alieonja akirudi nyuma na kuanguka hawezi fanywa upya. Hii ina maana kwamba wote walioamini, imewapasa vilevile kuokoka, kufanywa wana wa Mungu.
  Kwani imeandikwa kama hata mashetani wanaamini na kutetemeka (Yakobo 2:19).
  Hence, “alieokoka hawezi poteza huo wokovu.”

  Najua hii mada ni nzuri na wengi wataleta michango.

  Bwana Yesu Kristo awabariki.

 184. MAzengo,
  Binafsi nasikitika na kuhuzunika jinsi unavyochanganya mambo rafiki yangu. Lakini umefanya vyema kuyaleta mbele za watu ili upate msaada. Mimi napenda kukuhakikishia kuwa, Mungu wetu si mwanadamu abahatishe mambo yake. Mungu hawezi kukuokoa halafu akakuachia upotee tena! Neva bro!!
  Kwa sasa mtu haokoki, isipokuwa anampokea Kristo tu. Unapompokea Yesu, unahesabiwa haki kwa imani hiyo. Ya kwanza(maovu yako) yanafutwa. Unakuwa mpya. Wokovu huanzia hapo sasa. Zoezi linalofuata, ni kuukulia wokovu(sanctification). Hapa ndipo unapaswa kufa kila siku katika ulimwengu wa dhambi. Kwa maneno machache, katika hatua hii ya pili, unapaswa kukua kiimani. Kumbuka mpaka hatua hii bado hujaokoka.
  Hatua ya mwisho ni kukamilishwa katika imani (glorification), na ukifikia hatua hii, dunia na walimwengu wengine wote, watakuona kama siyo mtu wa kawaida. Wengine watakuita umeehuka, wenye macho ya rohoni, watauona uongofu wako n.k. Unapofikia hatua hii, ndipo utakuwa na sifa ya kuitwa mwana wa Mungu asiyetenda dhambi. Hata kama utakufa, au utaendelea kuishi mpaka Yesu arudi ukiwa katika hali utakatifu huo, Yesu atakuja kukuokoa sasa.
  Yesu haokoi mara mbili au mara tatu nk. Anaokoa mara moja tu. Na hiyo mara moja, bado haijafika. Wapo waliokufa, wanasubiri kuokolewa na Kristo. Walio hai pia, wanasubiri kuokolewa na Kristo. Yesu atakapokuja, wote waliokufa na watakaokutwa hai (watakatifu), wataokolewa wote na kupelekwa sehemu isiyo na shida tena. Watapewa miili mipya isiyojua dhambi. Hii ndiyo maana ya kuokoka kaka Erasto.

  Hivyo, kichwa cha mada yako kilipaswa kusomeka hivi; JE, MTU ALIYEMPOKEA KRISTO, AWEZA KUPOTEA TENA? Na jibu lake lingekuwa rahisi kabisa kuwa ni NDIYO. Erasto, inabidi utofautishe kuokoka na kumpokea Kristo. Duniani hapa, hatuokoki. Tukiokoka, tutatolewa kabisa duniani hapa na miili hii yenye asili ya dhambi, hatutakuwa nayo. Na ili tufikie hatua ya kuokolewa na Yesu atakaporudi, kwa sasa hatuna budi kumpokea/kumwamini Kristo na kisha kutembea katika utakatifu siku hadi hadi(kuukulia wokovu), ili tufikie glorification.
  Ubarikiwe sana

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s