KARAMA ZA NGUVU: (IMANI)

nguvu

ANDIKO KUU: 1KOR 12: 4 – 11

Isingekuwa na maana yoyote kama mtu wa Mungu angepewa karama za ufunuo (Neno la Hekima, Neno la Maarifa na kupambanua roho) akaishia kujua tu kitu gani kinachoendelea katika Ulimwengu wa roho; vita gani inaandaliwa dhidi yake, au Nchi; udanganyifu gani au upotoshaji gani wa kweli za Mungu ambao umefanyika, au hata jambo gani Mungu amepanga kulifanya; akaishia kujua haya tu basi, isingekuwa na maana kwake.

– Kwa hiyo Karama ya Imani ni ule uwezo anaopewa mtu wa Mungu wa kutenda kwa hakika jambo ambalo huko nyuma alikuwa hawezi hata kuthubutu tu kulitenda. Anakuwa haogopi tena kutenda jambo
aliloagizwa kulitenda kwa sababu ya ile hakika aliyonayo rohoni kuwa hayuko peke yake, wala siyo yeye anayetenda kwa nguvu zake, akili zake au ujuzi wake, bali Mungu. Yoshua 5: 13 – 15.

– Yoshua wakati anazunguka ukuta wa Yeriko mara saba, asingeweza kufanya hivi kabla ya kupata karama ya Imani (kutenda bila woga wala maswali ya kuwa isipotokea itakuwaje? Mtu aliye na karama ya
imani hana maswali ya sijui itakuwaje! Yeye ana hakika ya kile akitendacho maana uwezo wa utendaji huo amepewa na Roho Mtakatifu ambaye hashindwi kamwe.

Ni vyema nikatofautisha kati ya Karama ya Imani na kumwamini Mungu.
(a) Kumwamini Mungu ni Pale tunaposikia injili (Neno la Mungu linapohubiriwa/linapofundishwa, tunalikubali mioyoni mwetu na kuchukua hatua za kuliishi (au kuishi kama Neno la Mungu linavyosema.
Ebr. 10: 38; Rum. 10: 17, efeso. 2: 8 – 9, Rumi 1: 17 n.k.

(b) Karama ya Imani inatolewa kwa mtu aliye amini aliyetubu dhambi zake tayari na amejazwa Roho Mtakatifu; anapokea uwezo maalum wa kuamini kisha kutenda bila woga jambo ambalo asingethubutu
kulitenda huko nyuma. Math. 14: 25 – 29.

– Petro alipokea uwezo maalum kutokana na Neno aliloambiwa na Yesu njoo akatembea juu ya maji kwa miguu kumwendea Yesu; jambo ambalo hajawahi kuthubutu kulitenda ingawa alikuwa amemwamini Bwana Yesu na kutembea naye kwa miaka miwili kabla ya tukio hili.

– Uwezo huu wa kutenda, iwe ni kwa Nuhu kujenga Safina miaka 100 au Petro kumshika kiwete mkono na kumwinua na kumwamuru atembee, n.k. siyo uwezo unaopatikana kwa kukariri mistari ya Biblia na ahadi zake, ni uwezo maaalum unaotolea kwa watu maalum na kwa wakati au makusudi maamlum Mdo. 3: 1- 10.

Mfano: Tulivyozaa watoto wetu wote; Mungu alinipa uwezo Maalum wa kukiri na kutenda juu ya jambo hili na badaye ndipo nilipokuja gundua kuwa Mungu alilitenda jambo hili kwa kusudi la kuwafundisha watoto wake waliofundishwa kuwa mtoto ni mtoto tu, bali wapange na kumwamini yeye; naye Mungu hatashindwa kuwapa haja ya mioyo yao.

Roho Mtakatifu ndiye anayegawa Karama hii ya Imani kwa wateule wa Mungu, uwezo ambao hautaogopa moto wala simba wenye njaa, karama ambayo ni ya muhimu sana kwa Kanisa letu la leo. Dan. 3: 15 – 30.
– Karama hii hufanya Mungu wetu atukuzwe sana kuogopwa na wapagani na kuwavuta watu wengi kuja upande wa Bwana wetu Yesu. Mdo: 5: 7 – 16

– Mteule anapewa uwezo na Roho Mtakatifu wa kumwamini Mungu kwa matendo yasiyo ya kawaida; na ya miujiza. Je tuko tayari?.

– Mwaka 1988 gari iliyozimika taa wakati naenda Dodoma, Roho Mtakatifu alinipa uwezo wa kutenda mambo ambayo sijawahi kutenda.

“Tunahitaji uwezo wako huu Roho Mtakatifu sasa kuliko wakati wowote katika Jina la Yesu Kristo.” Amina.

REV. L.M. MWIZARUBI 

Advertisements

9 thoughts on “KARAMA ZA NGUVU: (IMANI)

 1. Hello

  Praise Lord

  Jamani bila hii karama ya imani kuwa ndani mwetu tutalia sana mbele za Mungu jibu hatupati, tuiombe hasa maana bila imani hakuna kumpendeza mungu,

  Mtu unaweza ukawa kanisani baada ya kuhubiriwa neno unakuwa na imani kubwa kwamba hitaji lake linajibiwa sasa,

  Pale anapotoka kwenye mlango wa kanisa tu imani inashuka anaanza kuwaza mh! sijui kama itawezekana kwa hili maana nimeomba muda mrefu!! tayari shetani keshaingilia kati mawazo yale mazuri ya kupokea hitaji lake,

  Karama za rohoni ni za kuomba mwambie Mungu nahitaji karama hii hakika Mungu anajibu,
  Kuna siku nimeamua kuomba hii karama ya aina za lugha, Nilijifungia chumbani na kwenda MBELE ZA MUNGU!! nilizama hasa nikajiwekea mkono kichwani na kumwambia mungu nataka nijue aina nyingine ya kunena kwa lugha maana huwa nasikia watu wananena aina moja ya lugha, HAPO NDIPO nilipotambua lugha za mungu zipo nyingi

  Karama ya imani kuwa na uhakika muda wote kile kitu unachokitrajia kwamba utakipata, hata kama hujakiona!!
  ndipo hapo utampendeza Mungu.

  barikiwa

 2. kiukwel hli somo ni la kipekee kwa kwel na makanisa mengi yanabidi kufundishwa ili kuweza kufanya mambo makubwa hata yale tuliokuwa hatuyawezi

 3. Mh! kweli imani ni karama leo nimepata jibu kutoka kwako mtumishi wa Mungu. itanibidi hii karama niitafute kwa maombi maana kunajambo linanisumbua naomba, nafunga miaka inaenda ila hakuna jibu nahisi ni upungufu wa imani. kunawakati nakata tamaa natamani nifanye njia mbadala. Ubarikiwe mtumishi wa Mungu

 4. Asante sana kwa neno hili yahani lime nijenga Mbarikiwe mtumishi wa Mungu.

  Mt: Chris.

  Sent from my iPhone

  >

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s