Kufanya kazi alizofanya na kubwa kuliko alizofanya!!

miracles

Amani ya Bwana iwe nayi enyi nyote,

Imeandikwa: YOHANA.14:8-12, “Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha.9 Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?10 Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake.11 Mnisadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! Hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe.12 Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba.”

Angalia kwa makini sehemu ya mstari wa 12 hii..”’……Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya,……”

 

Notice: Kuna kufanya alizofanya NA Kuna kufanya kubwa kuliko alizofanya

MASWALI:

Kazi kubwa kuliko izo alizofanya Yesu ni zipi hasa?

Nani ameshaga zifanya toka umeokoka na kuwajua Watumishi Duniani?

Kama hakuna, tatizo ni nini jamani? inaniuma why siwezi kupiga kazi kubwa sana zaidi ya za Master?

Lakini hata zile tu alizofanya Yeye, Je tunazifanya? kuna zinazotendeka kabla hata ya kufikiria zile za kubwa kuliko?

Kuna tumaini lolote la kufikia kuzitenda both izi za ”kawaida” na zile za ”kubwa kuliko-zile baabu kubwa”? when will it be?

Au tujitie moyo kua si lazima kila Mtu atende izo bali kama yupo aliyetenda na atakuja tokea mwingine akatenda, yatosha kumshukuru Bwana kwa pamoja then tuna sign off, we call it a day? tehe! Wapendwa bwanaaa!

Lakini mbona sifa ya kuweza tenda Makubwa zaidi ni simple sana namely KUMWAMINI Yeye na kwa maana iyo KILA Mtu AMEWEZA IYO, sasa why tuko wakavu na hamna lolote linatokea heavy weight? issue nini jamani seriously? dah! inaniuma sana siyo siri na kunivuruga, nyie wenzangu vipi, mko peace tu au?

Press on,

Edwin Seleli

Advertisements

15 thoughts on “Kufanya kazi alizofanya na kubwa kuliko alizofanya!!

 1. Ubarikiwe ndugu, Kamugisha.
  Mimi binafsi SIWEZI KUFANYA KAZI KUBWA KULIKO ZILE ALIZOFANYA YESU, KWA SABABU MIMI NILIKUWA MWENYE DHAMBI ALIYEOKOLEWA NA BWANA YESU KRISTO KWA NEEMA.
  Narudia kusema “Bwana Yesu anasema kuwa bila Yeye hatuwezi kufanya Neno lolote (Yohana Mtakatifu 15:5)”
  Nukuu yako inasema “Sikiliza kwa makini mtumishi Pandaeli Simon.Katika YOHANA 14:12,Yesu alisema
  na bado anaendelea kusema kuwa TUKIMWAMINI tutafanya kazi kubwa kuliko
  alizofanya yeye kwasababu yeye anaenda kwa Baba.”
  Sasa mbona sababu iko wazi kuwa tutafanya ‘nyingi’ kwa sababu BWANA YESU ananda kwa Baba?
  Unafahamu Bwana Yesu alifanya kazi kwa muda wa miaka mingapi?
  Pia, ndugu yangu anajikanganya mwenyewe kwa kauli yako ya kusema “Infact hakuna anayeweza kuwa zaidi ya Yesu ambaye ni Mungu mwenye nguvu,Baba
  wa milele na mshauri wa ajabu(ISAYA 9:6)”
  Je,ukifanya kazi kubwa kuliko BWANA YESU hujamzidi?
  Tunachotofautiana ni UFUNUO katika Neno la Mungu, hivyo usinilazimishe kukana Maandiko.
  Naomba unijibu maswali machache yafuatayo kuhusu ‘kazi kubwa kuliko alizofanya Bwana Yesu’
  1.BWANA YESU NI MWOKOZI,wewe unaweza kuokoa?
  2.BWANA YESU NI MPONYAJI,wewe unaweza kuponya?
  3..BWANA YESU NI MUUMBA MBINGU NA NCHI NA MUUMBAJI WA VIUMBE VYOTE ( YOHANA MTAKATIFU 1: 1-5,14) ,wewe unaweza?
  Kwa maswali hayo machache sana kati ya mengi ,nashawishika kusema “Hakuna hata mtu mmoja mahali popote awezaye kufanya kazi kubwa kuliko alizozifanya BWANA YESU”
  Usipende kukimbilia hukumu kwa sababu,HATUDAI HAKI BALI TUNAOMBA NEEMA YA BWANA YESU ITUSAIDIE.
  ******MAANDIKO HAYAJIPINGI BALI WATU NDIO WANAOPINGA MAANDIKO***
  Shalom.

 2. Mpendwa Pandaeli Simon

  Naomba nikurejeshe katika angalizo ulilotupa wakati unachangia mada ya MUNGU
  BABA,MWANA NA ROHO MTAKATIFU tarehe 22/10/2014 at 12:53 pm.
  Nanukuu;

  SHALOM
  AWALI , NITOE ANGALIZO LA KIMAANDIKO KWA WATU WANAOTAKA KUSEMA
  MAMBO AMBAYO HAYAPO KATIKA MAANDIKO (SOMA MITHALI 30:5-6,UFUNUO
  22:18-19,2 PETRO 1:20-21).
  BIBILIA INASEMA TUSIWE WAALIMU WENGI,MKIJUA YA KUWA TUTAPATA HUKUMU KUBWA ZAIDI(YAKOBO 3:1).KABLA YA KUONGEA HEBU PIMA
  UNACHOTAKA KUONGEA NA NENO KAMA VINALINGANA.

  …………………………………..Mwisho wa kukunukuu…………………………………………………………………….

  Sasa naomba turudi katika mada hii inayochanua vizuri zaidi kutoka YOHANA 14:12
  “AMIN, AMIN, NAWAAMBIENI,YEYE ANIAMINIYE MIMI,KAZI NIFANYAZO MIMI YEYE
  NAYE ATAZIFANYA, NAAM, NA KUBWA KULIKO HIZO ATAFANYA, KWA KUWA MIMI
  NAENDA KWA BABA”.

  Katika mchango wako wa tarehe 23/10/2014 at 7.07 pm ulisema “Hakuna hata mtu
  mmoja mahali popote awezaye kufanya kazi kubwa kuliko alizozifanya BWANA YESU”.

  Sasa ndugu yangu, Muheshimiwa Pandaeli Simon naomba twende taratibu,tumshike
  mkono Roho Mtakatifu kwasababu yeye ndiye mwalimu hapa.Mimi natumika kama
  chombo tu ambacho kinahitaji kukamilishwa pia(1 YOHANA 2:20,27).Roho Mtakatifu
  tunaomba UPAKO(MAFUTA) WA KULIELEWA NENO LA KRISTO.

  Ulichokisema wewe na kile kilichoandikwa katika YOHANA 14:12, HAVILINGANI.
  Kwa maana nyingine ni kwamba umeipinga kauli ya Yesu.Wewe umeongeza maneno
  ya kwako kwa kusema uongo!Mtazamo wako umekufa.Roho Mtakatifu ndiye
  anayetuwezesha kutofautisha kati ya mitazamo iliyo kufa na mitazamo iliyo hai.
  Lakini yote ni muhimu ili tujifunze tofauti kati ya TUI LA NAZI na MAZIWA!

  Tukirejea katika nukuu ya angalizo ulilolitoa,MITHALI 30:6 inasema “USIONGEZE NENO KATIKA MANENO YAKE, ASIJE AKAKULAUMU, UKAONEKANA U MWONGO”
  Hapa anayekulaumu kwasababu ya uongo wako ni Yesu siyo mimi.

  Sikiliza kwa makini mtumishi Pandaeli Simon.Katika YOHANA 14:12,Yesu alisema
  na bado anaendelea kusema kuwa TUKIMWAMINI tutafanya kazi kubwa kuliko
  alizofanya yeye kwasababu yeye anaenda kwa Baba.Yesu HAKUSEMA
  tukimwamini tutakuwa zaidi ya yeye kwa kufanya kazi kubwa kuliko alizofanya yeye!
  Infact hakuna anayeweza kuwa zaidi ya Yesu ambaye ni Mungu mwenye nguvu,Baba
  wa milele na mshauri wa ajabu(ISAYA 9:6).Unasikia kila ambacho Roho Mtakatifu
  anasema na sisi hapa.Roho Mtakatifu anasema pia na mimi na wengine.Hii ndiyo
  INJILI YA UNYENYEKEVU WA YESU.Ni lazima tuache biashara ya kula MAVI yetu
  wenyewe!Biashara ambayo Mtume Paulo aliikataa kwa nguvu zake zote.Katika
  WAFILIPI 3:8 Paulo anasema “……..Ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo
  yote nikiyahesabu kuwa kama MAVI ili nipate KRISTO”.Sasa Kristo ni Neno la Mungu(YOHANA 1:1,14).Kwahiyo tusipoachana na MAVI yaani ile roho ya ujuaji,kiburi,dharau,majivuno na jeuri(Kiburi cha uzima) na kukubali kutembea ndani
  ya unyenyekevu wa Mungu (WAFILIPI 2:3-4) hatuwezi kulielewa Neno la Mungu.Ni
  lazima tutalipotosha na kujihesabia haki.

  Katika YOHANA 14:13 ndipo Yesu anatoa sababu ni kwanini Yeye mwenyewe ambaye yuko ndani yetu anatuwezesha tufanye kazi kubwa kuliko alizofanya yeye wakati alipokuwa hapa duniani akiwa amevaa mwili wa mwanadamu.Sikiliza vizuri
  anachosema “Nanyi mkiomba lo lote kwa JINA LANGU,hilo NITAFANYA, ili BABA
  ATUKUZWE NDANI YA MWANA”

  Kwahiyo ni Yesu yule yule ndani yetu, TUNAPOMWAMINI anatuwezesha KUFANYA
  KAZI KUBWA KULIKO ALIZOFANYA YEYE alipokuwa duniani ili BABA ATUKUZWE
  NDANI YA MWANA.Mungu anatuwezesha ili utukufu umrudie Yeye mwenyewe.
  Jambo la msingi hapa ni kumuuliza Roho Mtakatifu atujulishe hizo KAZI KUBWA
  ambazo Yesu akiwa na umbo la mwanadamu hakuzifanya alipokuwa hapa duniani
  na sasa ameamua kuzifanya kupitia wale wanaomwamini.Kwa jicho la mwilini hizo
  kazi zinafanywa na watumishi wenye imani lakini kwa jicho la rohoni ni Yesu ndani
  yao ndiye anayefanya.Na Yesu aliposema tutazifanya hakuwa anatupa sisi atukufu
  bali alitaka dunia ijue uweza walionao wana wa Mungu.Suala la kwamba mtu anawezeshwa kufanya na watu wote wanaona alafu huo utukufu anauchukua yeye
  badala ya kumrudishia Yesu,hiyo ni changamoto nyingine kubwa sana.

  Ni lazima tuwe makini sana tunaponena katika kuunga mkono mada au kuipinga
  kama ambavyo ulitupa angalizo ili TUSIJE TUKAPATA HUKUMU KUBWA ZAIDI.
  Lakini pia ni lazima tuwahurumie watu ambao wanafuatilia mafundisho tunayotoa
  kwasababu miongoni mwao wapo ambao HAWAWEZI KUPAMBANUA KATIKA
  MKONO WAO WA KULIA NA MKONO WAO WA KUSHOTO(YONA 4:11).

  Mungu akubariki sana Mtumishi.
  NATUMAINI UTAANZA KUFANYA KAZI KUBWA KULIKO ZILE ALIZOFANYA YESU.

 3. Shalom.
  Hakuna hata mtu mmoja mahali popote awezaye kufanya kazi kubwa kuliko alizozifanya BWANA YESU.
  Ni kweli Biblia inawaita Wakristo kuwa ni Miungu (wana mamlaka aliyokuwa nayo Bwana Yesu)
  Hayo aliyosema ndugu Lwembe hakika tunayafanya kwa msaada wa Bwana Yesu Kristo.Yesu Kristo ndiye aliyetupa mamlaka ya kutumia kutenda kazi hizo ( Mathayo Mtakatifu 10:1-14, Marko Mtakatifu 16:14-18),n.k…
  Hakuna atakayefanya kazi kubwa kuliko alizozifanya Bwana Yesu ( Mathayo Mtakatifu 10:24)
  Bwana Yesu anasema kuwa bila Yeye hatuwezi kufanya Neno lolote (Yohana Mtakatifu 15:5)
  Ndugu mpendwa muuliza swali umefanya vizuri kuwasaidia wengine kuondokana na dhana au mawazo yasiyo Neno La Mungu kuwa unaweza kufanya kazi kubwa kuliko alizozifanya Bwana Yesu.
  Tatizo la huo mstari ni maana na tafsiri inayopatikana.Kwa maneno mengine ni “kazi nyingi” na si kubwa kuliko alizozifanya Bwana Yesu kutokan na mistar ya BIBLIA niliyokwishataja hapo juu na mistari mingine mingi.Hii inatokana na sababu kuwa MUDA ALIOKAA BWANA YESU DUNIANI NI MFUPI KULIKO TULIONAO SISI.
  Barikiwa.

 4. Mjema,

  Kumbe nina viporo vya kujibu, basi ngoja nijaribu ili twende sawa!!!

  Kuhusu jambo la Yesu kuwa Mwokozi, kulingana na maswali uliyoyauliza, inadhihirisha jinsi ya kutatizika kwako ktk jambo hilo. Kwa sehemu naweza kusema, hili linatokana labda na msingi uliojengewa, yale mafundisho ya awali uliyoyapitia.

  Hata hivyo, ni maswali mazuri yanayohitaji majibu, karibu tuyatafakari kwa pamoja majibu ya maswali yako kulingana na kile INJILI inachokifunua kuhusu jambo hilo.!

  Kwanza, ni vizuri tujiridhishe kuhusu maana ya hilo neno “Mwokozi” ili tafakari yetu iwe na mwelekeo ulio sahihi.
  Mwokozi = Saviour
  Saviour = a person who saves someone or something from danger or difficulty (mtu anaye mwokoa mwingine au kitu fulani kutoka katika hatari au ugumu)

  Basi kutoka maana ya neno hili, Mwokozi au Saviour, likiwa linasimama kama jina, ndipo tendo linalomfanya huyo apewe jina hilo linaitwa KUOKOA, ndiko kule kumuondoa au kumtoa mtu YEYOTE ASIYEJIWEZA, katika ugumu au hatari inayomkabili.

  Na kwa huyo anayeokolewa katika hiyo hatari inayomkabili, huyu huingia katika fungu la hao waliookolewa, ambao hutambulika kama WALIO OKOKA, kulingana na rejea ya hatari iliyokuwa ikiwakabili. Pia ni hawa ambao humwita yule aliyewaokoa kwa jina hilo la MWOKOZI. Na kama watakuwepo wengine wasiohusika na tendo hilo lililofanyiwa hao watu, basi wao wanapomwita huyo kwa jina hilo, ni lazima wawataje na hao waliookolewa naye, ili kuikamilisha maana ya jambo hilo, km “huyu ndiye mwokozi wa Mjema”

  Na katika ujumla wa tendo hilo la kuokoa, yaani Mwokozi na hao waliookoka, ndio huitwa WOKOVU. Yaani hakuna Mwokozi bila waliookoka, na wala hakuna waliookoka bila Mwokozi!

  Kimsingi Mungu ndiye Mwokozi, bali ili ufike katika uelewa kamili, unapaswa kwanza utoke ktk kongwa la dini linaloushikilia ufahamu wako, ndipo uweze kumpambanua Kristo hata upate kujua amekuwaje Mwokozi ilhali Mungu ndiye Mwokozi!

  Pia unapaswa uliangalie jambo jingine hili la “Mkombozi”; ni lini Mungu au Kristo, alikuwa Mkombozi na lini alikuwa Mwokozi, ktk maana ya Kukomboa na Kuokoa; je, ni tendo moja?

  Nakushukuru Mjema tunapoendelea na tafakari ya maswali yako, pia na ndg wengine.

  Gbu!

 5. Mada nzuri: Mimi naungana na Ombeni na wote waliotangulia. Tunaomba vibaya, na tunaomba tukitaka kuona dhahiri kwa macho na papo kwa papo. Msingi wa mambo makubwa ambayo Yesu aliahidi tutafanya kwa ufahamu wangu naungana na Lwembe, kwamba tunatakiwa tuwalete watu wengi kwa Mungu, wamjue na kumtumikia. Tumesoma katika Biblia kwamba Yesu aliifanya kazi hii kwa miaka mitatu tu, lakini sisi je? au watumishi je? wako waliopata wokovu kwa zaidi ya miaka 40 wanaishi ndani ya wokovu, je ni jambo la kujiuliza kama kwa miaka mitatu Yesu aliweza kupata wafuasi labda 300,000, je mtu aliye ndani ya wokovu kwa miaka 40 alipaswa alete kwa Yesu watu wangapi? mimi nadhani kazi kwetu bado ni kubwa sana ya kuutengeneza ufalme wa mungu katika maisha ya watu, wengi wa watumishi waliopo ni watumishi ambao tamaa yao kubwa ni kuona watu wanapata vitu vinavyoonekana kwa macho kama passport, kazi, safari, gari, vitu ambavyo kiroho havimsaidii sana japo atakua na amani ya mwili, lakini amani ya rohoni bado hajampa nafasi ya kuipata.

  Wakati tunakua miaka ya 80, tulikua tukienda kanisani ilikua watu wakiamua kuokoka wanapita mbele then wanaanza kushuhudia yale madhambi yao na wanalia kwa uchungu kwa maana ya kujutia, hapo akiongozwa sala ya toba ana uhakika kweli ya kuwa ameokoka, na ilikuwa mara kwa mara mtu akiwa na jambo labda alilipitia na linahitaji kushuhudia, basi ilikuwa anapata nafasi ya kutoa ushuhuda na wote wanamshukuru mungu kwa ushindi. Nafasi hiyo sasa hakuna, kiu kubwa iko kwenye vitu (tangible) wokovu wa kweli hakuna na Mungu atusaidie sana, tupaze sauti, kauli mbiu ya yesu ni “Njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na kulemewa na mizigo, name nitawapumzisha” Tuwalete watu kwa Yesu wapate kupumzika. Huo tu ndio muujiza mkubwa na mengine yote tutazidishiwa.

  Amani iwe nanyi nyote.

 6. Kwa kweli kaka inasumbua na hiyo ni kwasababu watu wanataka kuendana na mambo ya dunia ndio maana Paulo mtumishi wa Mungu anasema kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu, hivyo wengi hupotea na kutafuta yaliyo yao na sio ya Mungu na ndio maana biblia inatuambia mnaomba hampati kwasababu mnaomba kutimiza tamaa zenu wenyewe hivyo tutazame yatupasayo kutenda na tuyatende na Mungu atusaidie wanadamu

 7. Lwembe,

  Habari? Umechangia vizuri. ila kuna jambo umelisema binafsi nahitaji kueleweshwa zaidi.

  umesema kwa kuwa Yesu ni mwokozi, yeye hakuitaji kuokolewa!?

  Binafsi najua ni kweli Yesu ni mwokozi wetu. Ila naye aliitajikuokolewa na Baba hadi pale alipopata ushindi msalabani. Kama unakumbuka kwenye mada fulani niliwahi kukuuliza,km sio wewe ni mchangiaji mwngne kuwa, Yesu yeye aliokoka lini!?

  Hebu nieleweshe kaka, mimi mtazamo wangu umejengeka ktk aya zifuatazo,

  1.Maisha ya Yesu yalikabiliwa na majaribu km sisi, ivyo aliitaji kushinda,sio kwa nguvu zake,bali za BABA. ndio maana kila wakati alitawaliwa na maombi.mfano. Math4.

  2.kuomba maana yake ni kuhitaji msaada kwa mtu mwngn mwenye uwezo wakuokoa.

  _Rafiki ndio maana ktk Sala ya Bwana Yesu aliwafundisha kuwa tuombe, “Baba yetu uliye mbinguni…….. USITUTIE MAJARIBUNI, BALI UTUOKOE NA YULE MWOVU”……

  -Unaona kumbe wanaotaka kuokolewa na Yule mwovu ni wale wanaojaribiwa.Yesu alijaribiwa,hvyo aliitaji kuokolewa.na ndio maana aliwafundsha kuomba km yeye.

  3.Kumbuka wakati alipokuwa akiteswa alimwambia Baba, “Ikiwezekana kikombe hk kiniepuke” hii ni kiashiria kuwa aliitaji kuokolewa.

  Zipo sababu nyngn ila kwa leo tuanzie hapo.

  -Najua wengi mtanishangaa, ila uo ni mtazamo wangu naomba kueleweshwa.

  YESU PIA ALIITAJI KUOKOLEWA NA BABA, KM SISI TUNAVYO MTEGEMEA YEYE.

  Twende kazi.

 8. Da! Mungu akubariki sana ndugu yangu lwembe. nimefurahi sana kwa kunisaidia. ubarikiwe sana

 9. Haya, dada annastellah,
  !meandikwa “ombeni mtapewa”, wengi wamefundishwa kuomba mali kabla ya kuomba Mapenzi ya Mungu ktk maisha yao, wanaishiaga kuzungukia kila mjengo! Nayo Mapenzi ya Mungu ndilo hilo Neno lake ambalo wewe umeliomba!! Basi ktk kufaidiana, pokea hii tafsiri uliyoiomba kutoka mchango wa ndg Edwin Richard, inaweza isiwe sawa sawa kabisa, bali ninaamini kwa kiasi itakidhi haja yako, yaliyopunguka Bwana atakutafsiria, maana yeye ndiye Mwamba wa lugha!

  “””Kazi kubwa? Watu wengine wanaposoma “kazi kubwa zaidi mtazifanya”, wanaikosa ile maana ya kwamba Mungu anaihamishia Nguvu yake ya kiroho kwao, na kwamba sisi hatunao uwezo wa kuokoa, kuponya au kukomboa. Badala yake, sisi ni vyombo katika mikono yake Mwenyezi ambaye ndiye mtendaji wa hiyo miujiza.

  Ni kazi zipi zipi zilizofanywa na Yesu Kristo ambazo zinaweza kupitwa na wafuasi wake? Kwa uhakika haziwezi kuwa huko kuokoa, uponyaji. kukomboa, na kuwaweka huru walio utumwani. Mambo haya yatafanyikaje ktk kiwango kikubwa kuliko alichokifanya Bwana Yesu?

  Hivyo basi kwa kuwa Bwana Yesu aliwafufua wafu, akatoa pepo, akaituliza tufani, ni jambo gani moja ambalo Yesu hakuweza kulifanya ambalo sisi tunaweza kulifanya? Yeye haweza kusimama mbele ya halaiki na kusema, “NILIKUWA NILIYEPOTEA NA SASA NIMEPATIKANA, NILIKUWA KIPOFU BALI SASA NAONA”

  NI JAMBO AMBALO ASINGEWEZA KUFANYA- Muujiza ulio mkuu na wa msingi ktk Ufalme wa Mungu, ni muujiza wa wokovu. Unaweza kuiambia dunia, “DHAMBI ZANGU ZI CHINI YA DAMU, NIMEKOMBOLEWA. BWANA YESU ASINGEWEZA KUSHUHUDIA HABARI YA WOKOVU WAKE YEYE BINAFSI, KWA SABABU YEYE HAKUOKOLEWA- YEYE NDIYE MWOKOZI. LAKINI WEWE UNAWEZA KUSHUHUDIA KUHUSU WOKOVU WAKO. UNAWEZA KUSIMAMA NA KUSEMA, “NILIKUWA MALI YA SHETANI, BALI SASA MIMI NI MALI YA MUNGU BABA NA MWANAYE YESU KRISTO”

  Bwana Yesu hakupotea- Yeye alikuwa ndiye njia. Hakuwa kipofu- Alikuwa Nuru.
  Hakufungwa- Aliwaweka huru waliotekwa.

  (Chanzo: ‘Karibu Roho Mtakatifu’ na Benny Hinny)”””

  Asante & Gbu!

 10. Edwin,

  Swali nzuri. Kiukweli hata mimi siko poa, na wengi wetu wako hivyo. Kilio chetu kiwe kama cha wanafunzi “Bwana tuongezee Imani” au “Nisaidie kutokuamini kwangu”.Yesu aliwaambia na anatwambia hata leo tukiwa na Imani km punje ya haradali.tutafanya hayo. Wanafunzi pia hawakuweza kuzifanya kazi hizo za Kristo na walipomlilia aliwapa uwezo.

  Kabla sijajibu maswali yako ya msingi naomba tutambue mambo yafuatayo

  1.Pamoja na kuwa ameahidi kuwa tutatenda kama yeye na hata zaidi yake. Ieleweke kuwa huko kutenda kama yeye au zaidi yake. ni matokeo ya yeye kuwa ndani yetu. Yaani ni yeye Anayetenda akiwa ndani yetu kwa njia ya RM,zaidi ya hata alivyotenda akiwa nasi ktk mwili. Kwa iyo ht ikitokea tumetenda tujue ni Yeye yeye anaetenda sio sisi. MTU AWAYE YOTE ASIJE AKAJISIFU!

  2.Ahadi hii ilikuwepo tangu agano la kale kabla ya kuja kwa Yesu. soma Yeremia33:3 -inasema “niite nami nitakuitikia,nitakuonyesha mambo MAKUBWA NA MAGUMU usiyoyajua!!”. Edwin, can you sense over tis, it looks more or less de same.

  Kutokana na maelezo hayo ya awali naweza kujibu ya maswali yako kama ifuatavyo:

  Swali: Je tumeweza kutenda kama yeye?

  Jibu: Binafsi bado. Ila naamini wapo wenye uzoefu huo hata ktk kizazi chetu kama ilivyokuwa kwa kanisa la mitume,ambao ingawa mwanzoni walishindwa ila waliweza kufanya aliyotenda Yesu. ila makubwa kuliko ya Yesu, sina ushaidi wa maandiko.

  Swali: Je, tumeweza kutenda zaidi ya Yesu?

  Jibu: Kwa kweli bado,kwa uelewa wangu, hata wanafunzi wa Yesu hawajampiku Kristo.Bado .waliojitahidi sana wapo droo.

  -binafsi nashauri kuwa kabla ya kutafuta kufanya zaidi ya Yesu,ni bora tutafute kwanza kufanya yale aliyofanya yeye kwanza ndo tutafute kufanya zaidi.

  Swali:kwa nini hatuwezi kutenda km yeye na zaidi yake?

  Jibu:sababu nijuazo mimi ni,

  1.Imani haba itokanayo na kutofanyia kazi karama tulizonazo. Wapendwa nilazima tuwe na mzigo na Roho za watu na kuingia shambani mwa Bwana ndo tutaweza kukua ktk huduma hadi tumfikie yeye aliye kichwa na hata kumpita.

  2.kukosa muda wa kutosha pamoja Mungu kupata uwezo wa kutenda hayo kwa njia ya Maombi na kusoma.

  3.kukosa RM maishani-Mdo1:8-nanyi mtapokea Nguvu akiwajilia huyo RM,nany mtakuwa mashaidi wangu…tutaweza kutenda iwapo tunae RM.

  …inaendelea…

 11. Mpendwa changanya kidogo na kakiswahili ili na mimi nielewe. kama unaweza lakini. Barikiwa

 12. Greater works?”when some people read greater works will you do”,they have mistaken the notation that God is transferring his spiritual power to them,but we do not have the ability to save,heal or deliver.instead we are instruments in the hands of the almighty and He performs the miracles.
  what” works” were done by Jesus Christ that would be superseded by His followers?certainly it can’t be savings,healing,delivering,and setting captive free.How could these things be done to a greater extent than the Lord Jesus did?
  So since the Lord Jesus raised the dead,cast out demons,and caused the storm to cease,what is one thing Jesus could not do that we can?He could not stand before a crowd and say”ONCE I WAS LOST AND NOW AIM FOUND.ONCE A BLIND AND NOW I CAN SEE”

  SOMETHING HE CAN’T DO-The most pivotal miracle in God’s Kingdom is the miracle of salvation.You can tell the world,”MY SINS ARE UNDER THE BLOOD.I HAVE BEEN DELIVERED.THE LORD JESUS COULD NOT TESTIFY OF HIS OWN SALVATION FOR HE DID NOT GET SAVED-HE IS THE SAVIOR. BUT YOU CAN TESTIFY ABOUT YOUR SALVATION.YOU CAN STAND AND SAY”ONCE I BELONGED TO SATAN BUT NOW I BELONG TO GOD THE FATHER AND HIS SON JESUS CHRIST.

  The Lord Jesus was not lost-He was the way.He was not blind-He was the Light.
  He was not bound-He set the captives free.

  (Source:Welcome Holy Spirit by Benny Hinny)

 13. tunajichanganya sana wokovu wetu umekuwa uvuguvugu inafikia hadi kutoa pepo wakristo tuliookoka tunashindwa Jina la Yesu tunalitamka kama jina la kawaida tu. Unakuta mtumishi wa Muungu au mlokole ni muongo, msingiziaji, mkorofi na kila aina ya uchafu anao unafikiri anaweza kuponya hata mafua kweli? wakristo sasa tunaona dhambi ni ulevi, uzinzi, uchawi na yale yanayoonekana kwa macho tu lakini kiburi, uchoyo, nk tumeyazoea. mimi naamini tukikaa kwenye mstari tutafanya zaidi ya Yesu kama alivyo sema mwenyewe. neno limesimama jamani halitabadilika. mbarikiwe

 14. Swali nzuri sana,nina amini nitafaidika kupitia waalimu wa kundi hili kama ndugu Lwembe na wengine.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s