Mshirika wa Kanisa!

kanisaa

Bwana Yesu Asifiwe kumekuwa na tabia ya watu kuhudhuria makanisa mengi kwa wakati mmoja au kutembelea makanisa mbali mbali. Mimi nina swali Je unaweza kuwa mshirika wa kanisa zaidi ya moja? Au nini maana ya kuwa mshirika wa kanisa la mahali pamoja?

–Emmanuel

Advertisements

3 thoughts on “Mshirika wa Kanisa!

 1. kwako dada annatella na kwa niaba ya wengine kwanza tuache tabia ya kuwa wakristo wa jina sifa za mkristo ni yule aliyezaliwa mala ya pili yaani aliyemkiri Yesu kuwa ni Bwana na mwokozi wa maisha yake kwa lugha laisi awe ameokoka sio kwa kusema leo watu wote wana sema Bwana asifiwe mzinzi,mlevi,fisadi,mwenda kwa waganga wa kienyeji,nk mtu wa namna hiyo ni mkristo wa jina kwani neno linasema kila alitajaye jina la Bwana na auache uovu sasa mkristo wa kweli kama unasali mahali ambapo hafundishi kweli yaani mahali wanapopinga wokovu,wanaposema kunywa kidogo usilewe unalusiwa kuhama na kutafuta mahali wanapofundisha kweli ya mungu biblia katika mithali inasema kama mbayuwayu inapotafuta chakula na laana isiyo na sababu haimpigi mtu wengine wanaogopa kuhama makanisa yao kwa kufikili watapata laana hivyo wanavyo kuwa na shida za kiloho wanaanza kutafuta msaada mahali pengine unakuta makanisa mengine watu wana shida hakuna maombezi halafu washilika wanaambiwa nendeni kwa amani huwezi kwenda kwa amani wakati una shida ukisoma katika injili ya marko Yesu anasema ishara hizi zitafutana na waminio kuwa wataweka mikono juu ya wagonjwa nao watapokea afya sasa leo kuna wachungaji hawaamini uponyaji kwa maombi sijui wanasoma biblia gani jamani kama upo dhehebu,kanisa ambalo halifundishi kweli hama tafuta mahali wanapofundisha kweli ya MUNGU MUBALIKIWE WOTE MNAOSOMA MTANDAO HUU ACHANI KUZAMIA MITANDAO YA KIDUNIA AMENI

 2. Asante mtoa mada ni kweli kabisa mtu hawezi kuwa na makanisa mengi kwa wakati mmoja. inatubidi wakristo tusimame mahali Yesu alipotuweka. hili suala linawapa shida sana wachungaji hasa pale tatizo la msiba linapotokea unakuta wachungaji wawili wanagongana kwenye ibada ya mazishi jambo ambolo sio zuri kabisa. lakini kwa upande mwingine wakristo huwa wanatafuta sehemu ambayo akienda hatarudi kama alivyoingia mtu anahitaji uponyaji wa roho na mwili pia lakini makanisa mengine hakuna badiliko lolote hata mchungaji mwenyewe unakuta haeleweki kama ameokoka au hajaokoka anaumwaumwa hovyo sasa hiyo ndo sababu inayotufanya tutangetange jamani.

 3. mimi kwa mtazamo wangu nasema haiwezekani mtu kuwa mshirika wa zaidi ya kanisa,dhehebu,au mchungaji,mmoja kwa vigezo hivi hapa.
  1.ukisoma katika wagalatia biblia inasema mwanafunzi amshilikishe mkufunzi wake haisemi awashilikishe wakufunzi wake(wagalatia 6:-6) leo washilika wengi waameshindwa kusaidiwa,kuelekezwa,kuchungwa.kutokana na tabia hii na shida hii ipo sana mijini utakuta mtu leo yupo hapa kesho yupo pale mtu hajulikani kazi ya wachungaji ni kuchunga kwa maana hii ndio maana Yesu anasema mchungaji akipotelewa na kondoo moja kati ya mia sharti aache wale tisini na tisa aitafute ile moja sasa wewe unayeabudu zaidi ya sehemu moja hata ukipotea kwa mda mlefu hawatajua kwani hujulikani kama ni wa pale au la na mtu unapomwamini Yesu unafanyika mwanafunzi wa Yesu.na mwanafunzi lazima uwe na shule moja,na ujulikane kwa mkufunzi.
  2.shida shingine ni kwa wachungaji kuwa ni wachungaji wa mishahara hawana shida na kondoo. wanashida na pesa mtu anaweza kuhamia kwenye kanisa,dhehebu lako hakuna kumuuliza umetokea wapi kutaka kujua historia ya mhamiaji na ikitokea huyo mtu akawa na pesa hata kama ana shida,matatizo,sio nuru ya ulimwengu,ni mtenda dhambi akatokea hata mshirika,kiongozi,wa ngazi ya chini akataka kujua historia yake anaweza hata kuzuiliwa leo kanisa la bwana limechafuliwa sana kwa wachungaji kushindwa kusimama kwenye nafasi zao inavyopaswa leo makanisani kuna wezi,mafisadi,wazinzi,wachawi,nk na kanisa kupoteza mwelekeo hata watu wasio mjua Yesu kuwahubili inakuwa kazi maana watu walio ndani hajawa nuru ya ulimwengu
  Mungu akubaliki sana mtoa mada ndugu zangu wakristo ebu tuishi kama kristo anavyotaka tuwe kwa mujibu wa neno la Mungu tuwavute wengine wote walio nje kwa mwenendo wetu
  balikiwa na Bwana ameni

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s