Mwanamke kunyongwa kwa kuasi dini (Uislam) Sudan!!

Daktari Mariam Yahya Ibrahim Ishag, ambaye babake ni muisilamu alishitakiwa kwa kosa la kuasi dini pamoja na kufanya zinaa kwa kuolewa na mwanamume mkristo, kitu ambacho dini ya kiisilamu imeharamisha kwa wanawake.Mariam mwenye umri wa miaka 28 pia ni mjamzito na ataadhabiwa kwa kuchapwa mijeledi miamoja kwa kosa la zinaa.

Maafisa wakuu wanasema kuwa licha ya Mariam kulelewa kwa njia ya kikristo yeye bado ni muisilamu kwa sababu hiyo ndiyo dini ya babake.

Alipewa siku tatu baada ya kuhukumiwa aweze kurejea katika dini ya kiisilamu lakini akakataa na ndio maana adhabu ikasalia.

Kwa kawaida wanawake waisilamu hawaruhusiwi kuolewa na wanaume wakristo ingawa wanaume waisilamu wanaruhusiwa kuwaoa wanawake wakristo.

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Amnesty International linasema kuwa Bi Ishag alilelewa kama Mkristo muorthodoxi kwa sababu babake hakuwepo naye maishani mwake.

‘Kesi ya kwanza’

Kesi ya Ibrahim ni ya kwanza ya aina yake kusikika nchini Sudan , kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.

Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu, wamelaani uamuzi huo wa mahakama na kuitaka serikali ya Sudan kuheshimu haki na uhuru wa watu kuabudu.

Maafisa wa balozi za mataifa ya magharibi pia wamekemea vikali kesi hiyo na kuelezea asiwasi wao kuihusu.

Maafisa hao wamewataka maafisa wa sheria nchini humo kuangalia kesi hiyo upya na kuhakikisha kuwa Mariam anatendewa haki.

Waziri wa mawasiliano amesema kuwa sio Sudan peke yake ambako sheria za kiisilamu zinafuatwa na ambako sio sawa kwa mtu kubadili dini yake, hali hiyo pia ipo nchini Saudi Arabia na katika nchi zingine zinazofuata sheria za kiisilamu.

Serikali ya Rais Omar al-Bashir inakabiliwa na changamoto nyingi za kiuchumi na kisiasa hasa baada ya kujitenga na Sudan Kusini ambako mafuta yake yalikuwa yanatoka mwaka 2011.

–BBC Swahili

Advertisements

5 thoughts on “Mwanamke kunyongwa kwa kuasi dini (Uislam) Sudan!!

 1. Jamani kuwauwa wakristo na wayahudi kwa sababu ya imani yao ni andiko, msishangae kwani kila neno la mungu lazima litimie ingawa ni kwa maumivu makubwa sana. Yesu alisema furahini iwapo watu watawachukia na kuwatesa kwa ajilinya jina langu kwa maana ndivyo waliowafanyia manabii waliowatangulia, Pia Yesu anasema itafika muda ambapo watu watawauwa wakidhani wanamfanyia mungu ibada. la kujiuliza ni je ungekutwa na hayo ungesimamia imani yako hata pumzi yako ya mwisho? kumbuka yesu anasema ukinikana mbele ya watu nami nitakukana mbele ya baba yangu wa mbinguni na ukinikiri mbele za watu nami nita kukiri mbele ya baba yangu ya mbinguni, huyo dada aliyehukumiwa na kuuwawa na waislamu kama atauwawa tayari ameshamuona kristo uso kwa uso.

 2. Swala si wanawake kuonewa ndipo tuombe kwa ajiri hiyo. Cha msingi Biblia inasemaje juu ya mateso ya watoto wa Mungu!

  Hicho ndicho kitakacho fanya uamzi. Hisia na mitazamo ya Kibinadamu ni yakini hakiwezi kumfanya mwanamke ama mwanamme atoke katika mateso ya kishetani!

  Mawazo kwamba wanawake ndo wanaonyanyaswa zaidi, hilo ni wazo la kimtazamo, napia ni la kimaumbile. Kwa sababu. Biblia haisemi kuwa mateso kwa watakatifu wa Mungu yatategemea jinsia, bali inasema tu kwamba, “Mateso ya wenye haki ni mengi, lakini Bwana huwaponya nayo tote”

  Biblia inasema, mbinguni hakitaingia kinyonge, je, Mwanamke akombolewe kwa MKONO wa nani katika unyonge huo anaodhani anao? Mbinguni hakuna cha mwanamke ama mwanamme! Wanawake kujibagua kijinsia katika mateso kunatoka wapi? Au wanawake mnadhani kuwa ni haki ya wanaume kuteswa nashetani? BADILIKENI!

  “Ufahamu ni chembe ya Uhai!”

 3. Nimesikitishwa sana na uamuzi huu wa mahakama ya Sudan. Naomba tumwombee huyu mama na familia yake Mungu afanye kitu. Haya yamekua yakitokea hata nchi zingine zinazoongozwa na sharia. Mungu baba, muumba wa mbingu na nchi tunakuomba rehema na neema uingilie kati hili jambo ili huyu mama aachiliwe haraka iwezekanavyo. Kwako yote yanawezekana Bwana Yesu!!! Wapendwa wenye mzigo please lets pray for this innocent woman!!!

 4. mwanamke ni kiumbe wa kuonewa sana hapa duniani. hayo ni madogo sana kwa vile yamekuwa wazi. yale ambayo hatuyaoni juu ya ulimwengu wa mateso ya mwanamke ni mengi sana na ya kutisha usiombe kuyaona na kuyasikia. kwani boko haram wako kwenye community tunazoishi nyumba kwa nyumba, hata kanisani wapo. wanawake wapo kwenye nyimbo kanisani, wanahubiriwa, wakati wa Yesu akiwa hapa duniani, waliambiwa watapigwa mawe hadi wafe, lakini cha ajabu na cha kushangaza ,je ? kwa nini hawakumleta mwanaume aliyezini na mke huyo? huoni jambo hili limeanza zamani sana hata makanisani? tusiwashangae akina Juma. ukombozi wa mwanamke unahitajika sana kwani ameonewa vya kutosha sana katika huu ulimwengu. hakuna mwanamke anaruhusiwa kuwa na waume wawili, lakini mume akiwa na wake wawili community haishangai. mtoto wa kike mwanafunzi akibeba mimba na mwanafunzi wa kiume , huyo mwanadada anafukuzwa lakini wa kiume anaendelea na masomo. kwenye mila na desturi ndiko kumejaa boko haramu ya hali ya juu. nimeolewa kule Musoma, nikatembelea wakwe, nilichoona , nimestaajabu sana. eti mke hali kuku anatakiwa apike na kumpa mumewe chungu chote asionje hata chumvi? je? huu ni uungwana jamani? na mengi sana siwezi kuyataja. ukienda kanisani mahubiri yanaweza kuwa siku hiyo kuwasema wanawake mienendo na tabia zao, hutakaa usikie mabaya ya kiume. Jesus never condem any one.
  tunahitaji ukombozi wa haraka sana wa mwanamke. umri wa mama yangu wengi hawakwenda shule kisa ni mila na tamaduni zilimwandaa mwanadada kuolewa tu na sio shule. hili linafahamika katika community na society zetu. kwa hiyo namaliza kwa kusema hapo mitaani kwako angaza macho utawaona boko haramu wa kisirisiri ni wengi sana . kaa na kusogoa na wanawake hasa wazee watakuambia mambo utashangaa?????????????????????????????????????????????????????????????? na roho yako.
  samahani kama nimemuudhi mtu yoyote.

 5. SHETANI NI MFANO WA SIMBA AUNGURUMAAYE, LAKINI SI SIMBA HALISI, SIMBA HALISI NI WA YUDA! SHETANI MARA ZOTE NI WA KUSHINDWA, WANA WA MUNGU TWENDENI MBELE!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s