Ombea tumbo la uzao wako!!

uzao

Mlio kwenye Familia yaani Mwili mmoja,na Mnaoelekea huko.

Jifunze kuomba kwa ajili ya maisha yako na Familia ya hapo baadae,hili somo linazidi kunikaa kila siku nikikaa kwenye utulivu linanijia, Mke hakikisha unaliombea tumbo lako mara nyingi kadiri unapopata nafasi,hili upate uzao mwema,Mume pia hakikisha unaliombea tumbo la mkeo ili upate uzao Mteule,ndani ya tumbo kuna vitu vya KiMungu na vingine siyo vyake….Ndo maana Mungu anasema,

Yeremia 1:5 “Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa;
Maana ya Kutakaswa ni kutengwa na vitu ambavyo ni kinyume na mapenzi ya Mungu.

Luka 1:15 Atakuwa mkuu mbele ya Bwana. Hatakunywa divai wala kileo, atajazwa Roho Mtakatifu tangu tumboni mwa mama yake.

Angalia hapa ni raha ilioje Yohana Mbatizaji alijazwa Roho Mtakatifu tangu tumboni,watu wengi hawaelewi Maisha ya Mtoto yanaanza tangu tumboni,usijipe likizo ni vema ukaomba mbele za Mungu.

Nabii Isaya nayeye ananipa siri hapa anaposema, Isaya 49

1 Nisikilizeni, enyi visiwa; tegeni masikio yenu, enyi kabila za watu mlio mbali sana; Bwana ameniita tangu tumboni; toka tumbo la mama yangu amenitaja jina langu. 

Mwanzo 25:22-23 Watoto wakashindana tumboni mwake. Naye akasema, Ikiwa ni hivi, kuishi kwanifaa nini? Akaenda kumwuliza BWANA. BWANA akamwambia, Mataifa mawili yapo tumboni mwako, Na kabila mbili za watu zitafarakana tangu tumboni mwako. Kabila moja litakuwa hodari kuliko la pili, Na mkubwa atamtumikia mdogo…

Maisha yanaanza tangu tumboni….jifunze kuomba….usisahau

–Conrad

Advertisements

3 thoughts on “Ombea tumbo la uzao wako!!

  1. Shalomu wapendwa!

    Naomba mtoa hoja (Bwana Conrad) unifafanulie unaposema kuwa katika tumbo la mwanamke kuna vitu vya Kimungu na visivyo vya Kimungu una maana gani? Nilitegemea katika maandiko uliyoyatoa ungetuonyesha pia yanayotaja vitu vya Kimungu na visivyo!

    Ubarikiwe na Bwana!

  2. Uzao ni matarajio au ni mambo ya mbeleni au ni matokeo ya baadaye, je katika uzao wako UNAKUSUDIA KUTOA PRODUCT ya nani MUNGU au shetani, na wote hawa wanawania/wanapigania njia hiyo yako kupitisha kilicho chake. Kuombea ni muhimu sana na matokeo yake utayaona baadae. ANZA KUOMBEA SASA. Ubarikiwe mtoa mada.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s