Yasiyowezekana kwa wanadamu, Kwa Mungu yanawezekana!

wezekana

MAANDIKO: MATH 19:16 -26, MARK. 10: 17-17 NA LUKA 18: 18-27

1. UTANGULIZI:
Maisha ya wateule karibu wote katika Biblia yalikuwa na mfululizo wa vitu vilivyokuwa vinawajia/vinawatokea/vinawapata kila siku au kila wakati, na wakati mwingine vitu hivyo vilikuwa vinarudiarudia vikiwa na lengo la kuwafanya wavunjike moyo na kujikuta wamefanya maamuzi mabaya mbele za Mungu.

– Katika kipindi cha namna hii wateule walikuwa waangalifu sana na hasa wale waliomjua Mungu wao na nguvu zake; lakini wengine katika kipindi kama hiki na hasa ambao walikosa uangalifu, waliona wokovu ni mgumu na kwamba kudumu katika Utakatifu ni jambo lisilowezekana kabisa. ( life can be a perpetual barrage of things coming at us, and they can leave an impression that every thing is impossible or very difficult but Jesus specializes in the impossible things. He is able to do more than we can think or ask; yaani maisha ya wokovu ni mfululizo wa mambo yanayotujia kila siku bila kukoma na tena kwa kurudiarudia na kuacha picha kwetu kwamba mambo ya wokovu ni magumu na yasiyowezekana; lakini Yesu Kristo naye AMEBOBEA katika kufanya mambo magumu na yasiyowezekana kwa wanadamu, na anaweza kufanya hata zaidi ya tunavyofikiri au tunavyoomba. Efeso 3:20-21

– Hii ndiyo picha iliyowapata wanafunzi wa Yesu hadi wakasema kama mambo ya ndoa yako hivi basi haifai mtu kuoa!! Math:19: 3- 10, lakini leo wateule wengi waliojazwa Roho Mtakatifu swala la kuoa wake zaidi mmoja linaonekana kuwa ni ushamba na siyo ustaarabu- Haleluya.

– Yaani Mungu ndiye aliye na ubavu wa kubadilisha yale mambo yasiyowezekana kwa mwanadamu, na anataka afanye zaidi hata ya vile tunavyofikiri ili kukomesha kiburi cha binadamu.

2. Katika maisha ya kawaida mwanadamu yeyote anataka awe na usalama wa maisha kwanza anajua akiwa na nyumba nzuri na mali za kutosha maisha yatakwenda; sasa Yesu anamwambia huyu mtu auze vyote, abaki hana kitu hana usalama wa chakula chake halafu ndiyo amfuate!! Huu ulikuwa ni mtihani mgumu sana; lakini ukweli unabaki kuwa ukweli kwamba MTEULE yeyote ambaye hatakuwa tayari kujihatarisha maisha yake huyo hatafaa kamwe kuwa kiongozi. Waliokuwa tayari kujihatarisha ndiyo waliotenda mambo makuu sana baadaye.

– Mwandishi mmoja anasema ( it is better to be a lion for only one day than to be a sheep all your life” simba yeye ni wa kujitosa haogopi litakalompata ni mpambanaji porini ili aweze kuishi!! Lakini Kondoo yeye majani yameota yenyewe, anakula bila jasho; bila kujishughulisha!! Maisha ya jinsi hii kiroho hayafai popote pale utakapomwona mteule amefanikiwa katika maisha na kihuduma, nakuambia hakika kuwa 2

lazima huko nyuma alichukua hatua za kkujihatarisha maisha (NO ONE REACHES THE TOP WITHOUT DARING”) hakuna mtu yeyote aliyefika juu kama hakuwa jisiri au mtu mwenye kuthubutu na tena wataalamu wa mafanikio ya kiroho na kimwili wana msemo usemao “ success favours the bold” yaani mafanikio huwapenda/huwafuata watu majasiri, wanaojitoa. Hiki ndicho Yesu Kristo alichochukua muda mrefu sana kuwafundisha Wanafunzi wake na kweli mafanikio ya Injili hadi leo ni kwa sababu walimwelewa na wakawa tayari kujitosa katika hatari zote maadamu walijua kuwa Yesu Kristo amebobea katika kufanya yale yasiyowezekana kwa wanadamu. Kama Malkia Esta asingekuwa tayari kujitosa, Wayahudi wasingeokoka. Ester 4: 16 -17, 5: 1-3, 8: 15-17.

Na Ruth asingejitosa/asingejihatarisha – asingeolewa na Boazi na wala shamba lisingekuwa lake!!. Ruth 3: 1 – 18. Elisha lijihatarisha mno!! 1Wafal. 19: 19 – 21

– Watu Wakuu walijihatarisha kwanza, walithubutu, walijitosa, waliacha vyote wakamwangalia Yesu aliyebobea katika kutenda yasiyowezekana kwa wanadamu. Haleluya!!

3. Katika maisha yangu nimejifunza kuwa wateule wengi tunasema kuwa tunaishi kwa imani na tunampenda Yesu wakati hakuna jambo lolote linalohatarisha usalama wetu!! Lakini ukweli wa mambo ni huu” kwa kadri utakavyompenda Yesu na kutembea naye kwa ukamilifu ndiyo utakavyopambana na hatari nyingi na kubwa; na kama katika maisha haya ya wokovu mteule unajikuta katika maisha yako huna kovu (alama) huna hatari zozote au kuaibishwa na wala huna watu wanaokuvunja moyo, wanaokuudhi au kukufanya usikitike!!

( Never scared never embarrassed, never disappointed) basi hii inamaanisha wazi kuwa hujachukua kwa usahihi wote viwango vya wokovu) wewe ni mteule unayekubaliana na dunia huipi shida haioni tofauti!! Na usitegemee kuona matendo makuu ya Bwana Yesu. Yoh 9:1-38 Mdo 4: 36- 37, 5:17-33, 40-42, na Mwanzo 22:1-18

– Dunia ndugu zangu ni kama kitabu kikubwa ambapo mtu yeyote asiyekuwa tayari kujihatarisha husoma ukurasa mmoja tu akadhani amesoma kitabu chote na amekijua!!

Sasa leo nawaambia wateule wa Sayuni na mwingine yoyote atakayesoma au kusikia ujumbe huu ya kwamba “Hakuna njia nyingine yoyote ya mkato itakayotufanya tukue na kumjua Mungu na nguvu zake kama hatutakuwa tayari kuthubutu/kujihatarisha maisha na usalama wetu kwa ajili yya Jina lake ( There is simply no way we can grow without taking chance/ risks). Luka 9:23-27

– Tusikunje nyuso nasi leo na kuamua kama ndugu huyu alivyoamua na historia yake ikapotea!! Mark 10:22; Bila Yesu hatuna usalama wowote hata kama tungekuwa na kila kitu. Amina.

–Askofu Dr. Leonard Mwizarubi

Advertisements

2 thoughts on “Yasiyowezekana kwa wanadamu, Kwa Mungu yanawezekana!

 1. amina mwana wa Mungu hayo yote uliosema ni kweli, Mungu azidi kukupa nguvu kwa ajili ya watu wake kwa namna tofautitofauti

 2. Askofu Dr. Leonard Mwizarubi,

  Nukuu zote za Maandiko kama ulivyo zinukuu, ni kweli vinasomeka hivyo na vinamaanisha kama vilivyoandikwa. Lakini, ninachokielewa ni kwamba, Mungu ni Neno, na Neno ndiye Mungu, na pasipo hilo Neno hakuna chochote ambacho kinaweza kufanyika!

  Kama ukweli ni huo, basi yatupasa kujua ni kwa kiwango gani tupo katika Neno lenyewe kila tunaposema ama kutenda jambo lolote. Biblia inasema, “Neno ndiyo kweli yenyewe na kweli hiyo ndiyo inayomuweka Mtu huru, na si huru tu, bali ni HURU KWELI KWELI” Kwa mkutadha huo huo, sisi sote tunatakiwa kufika hapo.

  Biblia kama Neno la Mungu hajipingi na kamwe haitajipinga, litakuwa kiongozi cha maisha yetu sote sisi tuaminio. Kwa hiyo, sioni sababu tena ya kujidhiki na kufanya bidii kwa nguvu na juhudi nyingi zinazoongonzwa na Akili zangu, ili KUUPATA WOKOVU AMA USHINDI wa jambo la Rohoni ama la mwilini! Nasema hivyo kwasababu, maandiko yananieleza hivyo.

  Nikiisoma kwa makini ile Yohana 15:5 inasema “Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lolote” nikipaangalia hapo najiona sina cha kufanya, zaidi ya kumwambia yeye afanye kwa niaba yangu (kama kuna kitu ambacho hajafanya!) kama itampendeza! Nikisema nijihangaishe na kujitaabisha kwa bidii nyingi, hakutanifanya kufikia katika ufanisi wowote kwa hicho ninachokihitaji, na si kwamba sitaufikia ufanisi tu, yaani na hata hicho ninacho kihitaji sitakipata! (“……….bila mimi ninyi hamuwezi kufanya neno lolote”!)

  Sisi ni watoto wa Mungu na ni watoto katika Nyumba ya Baba yetu, wote tunapaswa kuwa ndani, kumwangalia yeye baba yetu, kumtegemea na kumwamini yeye Baba yetu pekee kwa kuwa tu kama tu wachanga sana tu, mbele ya mambo yote yaliyotuzunguka hapa Duniani, hatujui chochote, tunachoweza kujua ni “KUCHEZA” kama afanyavyo mtoto, yaani kujifurahisha tu katika Bwana, na kujua tu kwamba tumo katika Raha ya Sabato. Hivyo Yeye kama Baba alilijua hilo tangu mapema mwanzoni kabisa, kabla ya kuwekwa kwa misingi ya Dunia, alijua pia uwepo wetu, alijua mahitaji yetu makuu yatakavykuwa na namna yatakavyotatuliwa ili tufikie kuishi kama itakavyotakiwa kuwa!

  Ujasiri wa kusema haya yote naupata ninapoangalia ile Isaya 53:4-5, naona kuwa, sina cha kufanya, maana anasema, “Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu;……….Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu. Na kwakupigwa kwake sisi tumepona” Nasema kuwa sina cha kufanya, hasa ninapoiona hiyo sentesi ya mwisho kuwa, “NA KWAKUPIGWA KWAKE SISI TUMEPONA” si kwa kupigwa kwake sisi TUTAPONA, hasha, TUMEPONA!

  Na hata pia, alipokuwa akikaribia kukata roho, pale Msalabani alisema, “YOTE YAMEKWISHA…..”! Sasa kama yalikwisha yote, kwa maana ya yote, kimebaki tena nini cha kunipa Presha? Sioni kama ipo haja ya kupeana Stress kwa sasa, maana tunapo pa kuiweka mizigo yetu yote!

  “Ufahamu ni chembe ya Uhai!”

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s