Kupata ujauzito kwa njia za kisayansi!

ujauzito

Kupata mimba kwa njia za kisayansi: je, ni dhambi?

Hana mchumba wala dalili za kuolewa bila shaka ktk mtizamo wa kibinadamu. Ameamua kuzaa kisayansi kwa kupandikizwa mbegu za toka benki ya mbegu za Kiume kama ilivyo tu benki ya Damu Mahospitalini. Je huyu dada atakuwa ametenda dhambi kwa kuzaa kwa njia hii ya kisayansi?

Dah! haya mambo ya kutopata Waume bwana tunayaongea na kujadili msiyachukulie simple kama tunapiga mastory, tuko ktk huduma kabisa na tumeona, kushughulika na mengi na hata kusoma mengi. Notice: Hii si story, huyo mdada anayeenda kupata mimba soon anafahamika na rafiki yangu Kanisani ambaye tuliyetafakari mada hii mahali fulani iliporushwa.

Kama Kiongozi wa Vijana, Wanafunzi, Mchungaji  na Mwalimu au hata Msoma Neno tu na Ufahamu wako huru, unasema nini juu ya hili?

Press on.

Edwin Seleli

Advertisements

22 thoughts on “Kupata ujauzito kwa njia za kisayansi!

 1. Mimi ningependa kujua kwa wale tunaofahamu zaidi kitendo hiki cha kandikizwa kisayansi kinafanyikaje na matokeo yake yanakuaje yaani matunda yake yanakuwaje.Maana uzazi wa asili unajulikana lazima kutakuwa na utofauti wa matokeo.Nikijua hapo nitachangia zaidi.

 2. Mungu atusaidie na kufungua fahamu zetu katika nyakati hizi za hatari.Roho Mtakatifu naomba unisaidie hapa ili nijue namna ya kutoka na kuingia katika suala
  hili la KUPATA UJAUZITO KWA NJIA ZA KISAYANSI.Kuna uumbaji unaokwenda kinyume na uumbaji wa Mungu aliye hai na uumbaji ulio ndani ya NENO LA KRISTO.
  Katika kila uumbaji uwe ni wa Mungu au unaokwenda kinyume na uumbaji wa Yesu ni
  lazima tutafute kujua sababu zinazoambatana na huo UUMBAJI.Kupata ujauzito kwa njia za kisayansi ni KUONGEZEKA KWA MAARIFA KATIKA NYAKATI HIZI ZA MWISHO KWASABABU YA IMANI ZA WATU JUU YA NENO LA MUNGU KUPOTOSHWA,KUIBIWA,KUHARIBIWA AU KUFILISIWA.Hizi ni nyakati ambazo imani
  za wakristo wengi zinatokana na kusikiliza MAFUNDISHO YA MASHETANI,ni imani zilizo kufa!IMANI ILIYO HAI ni ile inayotokana na kusikiliza na kutii NENO LA KRISTO(1 TIMOTHEO 4:1,WARUMI 10:17).

  UNABII kutika katika kitabu cha Danieli umetimia-DANIELI 12:4 “LAKINI WEWE
  DANIELI YAFUNGE MANENO HAYA………HATA WAKATI WA MWISHO; WENGI WATAENDA MBIO HUKO NA HUKO, NA MAARIFA YATAONGEZEKA”.Naomba tuanalie maneno WATAENDA MBIO HUKO NA HUKO na MAARIFA YATAONGEZEKA.Kinachotafutwa hapo ni kuyumbishwa kwa imani za wateule na hiyo hali ya maarifa kuongezeka.Huu ulikuwa ni unabii uliobeba MAONYO kuhusu
  yale yanayoendelea sasa.Si mpaka uwe na ufahamu wa rohoni kujua kwamba shetani
  anawatumia wanasayansi kujaribu kushindana na Mungu!Mungu yuko juu ya sayansi
  zote lakini sayansi hizo zinajaribu kushindana naye kwa kiburi cha kutisha mno!Tukirudi katika DANIELI 12:4 ,tukisoma kwa kutumia MACHO NA MASIKO YA NDANI
  tunaona wazi kwamba ni mambo ambayo Mungu mwenyewe aliyaruhusu ili iwe ni
  SHULE na MTIHANI wa IMANI NA MAARIFA KWA WATEULE.Ni mambo ambayo wakati Danieli anajulishwa yalikuwa yameshapitishwa katika ULIMWENGU WA ROHO!Lengo lingine
  tunaloweza kuliona katika mstari huu ni KUIBIWA KWA MAARIFA YA MUNGU ndani
  ya wateule kisha KULETEWA MAARIFA YA SHETANI ili waangamie.Mafunuo ya HOSEA 4:6 ni kwamba WATEULE WA MUNGU WANAANGAMIZWA KWA KUKOSA MAARIFA YA MUNGU NA KUKUMBATIA MAARIFA YA SHETANI!Kuna maarifa ya namna nyingi duniani lakini kweli inabaki pale pale kwamba kuna maarifa ya watu wa Mungu na kuna maarifa ya watu wa shetani.Tunatakiwa tusijichanganye.UCHUMI WA
  DUNIA hauhusiani na UCHUMI WA WATEULE WA MUNGU.Wateule wengi wanaangaika na uchumi wa dunia badala ya kushughulika na uchumi wa ufalme wa Yesu!Matokeo yake ni vilio na kusaga meno!(MATHAYO 6:26-34).Wateule wa Mungu hawatakiwi kutafuta FEDHA bali FEDHA zinatakiwa ziwatafute wao!!MAARIFA YA MUNGU yamefichwa ndani ya UNYENYEKEVU WA YESU unaoishi ndani ya mioyo ya wanyenyekevu walioko duniani.

  USHUHUDA WANGU BINAFSI.
  Namshukuru sana Yesu kwa kunikutanisha na watumishi wa shetani katika maisha
  yangu ya wokovu ili nijifunze SIRI ZA MBINU NA MAARIFA YA SHETANI.Nilikutana na
  mtumishi fulani ambaye ameoa na anamtumikia mungu wake kwa ujasiri wa kutisha
  na bidii iliyo dhahiri kwa watu wote.Huyu mtumishi alikuwa ananiuliza sana habari za
  jinsi ya kupata mtoto kwa njia za kisayansi kwasababu mke wake alikuwa na tatizo la kutoshika ujauzito kwa muda mrefu.Kwa kuwa mimi nilipata neema ya kufuta ujinga
  katika baadhi ya mambo ya kisayansi,huyu bwana akaamua kunibebea bango kwamba nifanye juu chini tutafute mahali ambapo wana utaalamu wa kuchanganya
  mbegu za kiume na za kike katika chupa ili kuumba mtoto wanaitwa TEST TUBE BABIES(WATOTO WA CHUPA).

  Mwanzoni sikujua lengo lake hasa na pia nilifikiri walikuwa na shida sana ya kupata
  mtoto,kumbe ilikuwa ni HARAKATI ZA KUTAKA KUIBA IMANI NA MAARIFA YA MUNGU ndani yangu na kunipandikizia imani na maarifa ya shetani.Yule mtumishi alikuwa akiponda sana suala la wateule ‘kupoteza muda mwingi katika kumuomba
  Mungu mtoto kwa muda mrefu badala ya kutumia maarifa ya maendeleo ya sayansi na tekinolojia’.Akawa anasisitiza kwamba huku ndiko kuangamia kwa kukosa maarifa!Jambo la kutisha nililokuja kulijua ni kwamba huyu mtumishi wa shetani kazi yake kubwa ni KUHARIBU KIZAZI CHA WANAWAKE walio katika ndoa za wateule na lengo ni kwamba akishafanya hivyo anarudi kuwachapa injili ya kutafuta maarifa ya shetani.
  Alikuwa anasema watu wanatakiwa waache ujinga kwasababu Mungu amewapa elimu
  na maarifa alafu hawataki kuyatumia badala yake wanazeekea katika kufunga na kuomba bila majibu!Kazi nyingine aliyokuwa anaifanya ni kuhakikisha vijana wanaomtumikia Mungu aliye hai WANAOA AU KUOLEWA NA MBWAMWITU!Kuna wateule ambao wamo ndani ya ndoa kama hizi na wamefungwa na sheria kwamba
  ni mpaka kifo kiwatenganishe!EZRA alipewa maono kwamba wateule wote ambao wamo ndani ya ndoa batili ni lazima waache wake au waume zao hata kama wameshazaa watoto.Na hili zoezi lilifanikiwa kwa asilimia mia moja(EZRA 10:1-19).Leo ukileta haya mafundisho ya siri ya ndoa za wateule unaweza ukapigwa mawe!

  Kazi nyingine ambayo huyu mbwamwitu anafanya kwa kushirikiana na mke wake ni
  KUNAJISI MADHABAHU ZA MAKANISA YA WATEULE WA MUNGU kila wanapompa
  nafasi ya kuhubiri katika ibada za jumapili na kwenye mikutano au semina!Hawa ni watu ambao wamelelewa katika vyuo vya mbwamwitu vilivyosambaa dunia nzima.Ni mbwamwitu hatari na zaidi ya hatari ambao wamevaa ngozi za kondoo kwa namna ambayo si rahisi kuwatambua mpaka ROHO MTAKATIFU amekufunulia.Ni watu ambao wamejipanga muda mrefu na kila wakati wanakuja na mbinu na maarifa mapya hata hivyo kwa kutumia ROHO SABA ZA MAARIFA YA MUNGU ni rahisi kuwatambua hasa katika kipengele cha unyenyekevu.Ni watu ambao wamejaribu sana kuigiza unyenyekevu wa Yesu bila mafanikio na katika hili eneo wameangukia ulimi na siyo pua!(WAKOLOSAI 2:18,MATENDO 20:28-35)……….

  NITAENDELEA KADIRI ROHO MTAKATIFU ANAVYONIONGOZA……..MOTO ULAO
  UNAONGEA NA WATEULE AMBAO WAKO TAYARI KUKUA NA KUTOKA KATIKA MAANGAMIZI.

 3. KWAKWELI NYENDO ZA MUNGU NI NGUMU. HASA HILI SUALA LA KUPATA MUME LIMEKUA GUMU MIMI MWENYEWE NI MFANO HALISI NIMEOMBA ZAID YA MIAKA 12. NAISHIA KUANGUKIA PUA NAKUTANISHWA NA MTU NIKIAMINI NI MWENZI TOKA KWA MUNGU BAADAE YANAYOTOKEA NABAKI KUJIULIZA ILIKUA SAUTI YA MUNGU KWELI AU? NA ANAYETOKA KWA MUNGU NTAMJUAJE?

 4. Stella,
  Nafikiri tuko ndani zaidi tukijadili kitu ambacho ni zaidi ya kupata mtoto, ambacho ni kupata ujauzito kwa njia za kisayansi.
  Wewe unasemaje juu ya ujauzito wa namna ile?

 5. Shalom

  Mungu wetu hashindwi kitu ni sisi wenyewe tunashindwa ,

  vilevile anatuwazia mawazo mazuri maana anayajua maisha yetu hata ya mbele, tumeambiwa tushukuru kwa kila jambo,hata ukikosa mtoto wewe shukuru tu, yeye anajua anakuandalia nini na

  kwa kwa sababu gani hujapata mtoto,

  barikiwa woote.

 6. Ndg Ziragora,
  Nakufuatilia kwa karibu!

  Labda nikuulize hivi; vipi kama mwanamke akipandikizwa kisayansi mbegu za mwanaume ambaye ni mume wake, ni sawa au si sawa?

  Sante!

 7. Ndugu Lwembe, Ndugu Milinga, Ndugu Sungura,

  Naamini hamjambo!

  Ndugu Lwembe, nimekupata vizuri sana, Mungu akubariki kwa elimu ya RM unayotolea Milinga; na wana SG sote tumeipokea.
  Nataka niongeze kidogo ili Ndugu Milinga na Ndugu Sungura waelimishwe zaidi. Tafadhali wandugu, si kwamba tunayo elimu kubwa kuliko yenu, lakini kuna mada moja moja mtu anaweza kosea kabisa kwani mind yake imemuongoza vibaya.

  Someni maandiko haya:

  “2 Wafalme 20:
  1 Siku hizo Hezekia akaugua, akawa katika hatari ya kufa. Isaya, nabii, mwana wa Amozi, akamjia akamwambia, Bwana asema hivi, Tengeza mambo ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona.
  2 Basi Hezekia akajigeuza, akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba Bwana akasema,
  3 Nakusihi, Bwana, ukumbuke sasa, jinsi nilivyokwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo mkamilifu, na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia sana sana.
  4 Ikawa, kabla Isaya hajatoka katika mji wa kati, neno la Bwana likamjia, kusema,
  5 Rudi, ukamwambie Hezekia, mkuu wa watu wangu, Bwana, Mungu wa Daudi baba yako asema hivi, Nimeyasikia maombi yako, na kuyaona machozi yako; tazama, NITAKUPONYA; siku ya tatu utapanda nyumbani kwa Bwana.
  6 Tena, nitazizidisha siku zako, kiasi cha miaka kumi na mitano, nami nitakuokoa wewe, na mji huu, na mkono wa mfalme wa Ashuru, nami nitaulinda mji huu kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Daudi, mtumishi wangu.
  7 Naye Isaya akasema, Twaeni MKATE WA TINI. Wakautwaa, wakauweka juu ya jipu, naye akapona.”

  Hapa nataka mfahamu kama Mungu alikuwa na uwezo wa kumponya Hezekia kwa Neno tu bila kutumia dawa yoyote. Lakini hapa kwa ule msitari wa 7 tunasoma kama dawa ya mti ilitumiwa. Hii inathibitisha kama mbele za Mungu, dawa hii ya kuponya ni halali.

  Pamoja na maendeleo, kama vile hatukuendelea vaa ngozi tu, kutumia kisu kwa ajili ya kumsaidia mtu apone ni vizuri. Chemchemi yake iko hapa tu ambapo Mungu anatumia dawa kutoka mti. .

  Ubarikiwe Lwembe kwa ufafanuzi ya kwamba kwenda kwenye hospital haipingane na kuwekewa mikono. Vyote vinatumika kwa lengo moja.

  Sungura,
  Tumekwisha kukuambia kama dada kupachikwa mimba na sayansa ni dhambi. Hii haichokeshe kwa mafasiriyo mengi. Uasharati siyo mimba, lakini mimba ni tunda la tendo. Kama hilo tendo ni halali, yaani mimba ya ndoa sawa. Lakini kama lile tunda ni mimba isiyo ya ndoa, ni ya uasherati. Wandugu, iwe uashetari na mtu au na sayansa, yote ni uasherati tu.
  Swali: Kama huyu dada ana mimba, mumewe ni nani? Na kama huyu mtoto amezaliwa babae ni nani? Na kama mume/baba iko alifanya ndoa na huyu dada siku ipi?

  Isiwe ni kwamba tuko wakati wa neema, dhambi zizidi ili neema iongezeke. Huyu dada akiwa amefanya vile akidanganywa na wengine anaweza tubu na kusamehewa. Mtoto akiokoka Yesu hatakataa kwani alifika kutafuta kilichopotea. Lakini dada huyu akieneda vile kwa kupinga neno la Mungu, atakuwa amemkataa Yesu, yaani kumfanya RM kuwa muongo, na hapo hatasamehewa.

  Mbarikiwe.

 8. Sikiliza Milinga,

  “LISILOWEZEKANA KWA MWANADAMU KWA MUNGU LINAWEZEKANA”, Andiko hili liko hivi katika maana kamili ya kuwa hivyo! Ukiliendea intellectually, litakuzungusha huko porini mpaka ufikie kujiuliza iwapo Mungu kweli yupo? Na ukilikabili kwa Imani, Mungu hushuka akusikilize na kukushauri, maana wewe ni mrithi wa Ahadi zake zote zilizomo katika Neno lake!!

  Kuhusu kukopa sh 5000, kwa huyo mpendwa uliyemuendea kwa akili zako na akakupa, ukijidhania kuwa Mungu ndiye amekuongoza, wengi huishia kushindwa kulipa na kuiabisha Imani!!!! Na iwapo umefikia kuhitaji milioni hamsini, kisha ukamuendea mpendwa huyo huyo aliyekukopesha zile elfu tano ambazo ulifanikiwa kuzilipa kwa mbinde, hata yeye lazima machale yamcheze, ndio maana amekuelekeza uenda kwa huyo Baba yako uliyemkiri akufanyie huo mpango, lolote litakalo tokea mtajuana wenyewe; maana ana uhakika kwamba wewe, hata huyo Baba yako humjui sawa sawa maana ungalimjua basi ungalimuomba huko sirini kisha ndio akuelekeze umuendee huyo mpendwa akakupe hizo milioni, otherwise umemfuataje ilihali yeye hana hizo pesa?!!!

  Pia Milinga, ni vizuri ukafahamu hii “elimu” inatokana na nini, yaani huo upasuaji na tiba zote za kisayansi unazozijua leo hii na zitakazo vumbuliwa huko mbele; vyote hivi chimbuko lake ni ule Mti wa Ujuzi wa Mema na Mabaya; basi uongozi wa RM katika matunda ya Mti huo ni muhimu sana, ili kuyabaini yote yanayoli pervert Neno la Mungu. Hakuna mahali Mungu aliwaagiza wakajenge mahospitali, yeye alisema wawawekee mikono wagonjwa; lakini hilo halimaanishi kwamba hospitali ni mbaya au dhambi, hapana; na wala hospitali haliliondoi uwanjani hilo Neno la kuwawekea wagonjwa mikono hata kwa homa zenye tiba za kisayansi!!!

  Tena unapaswa ufahamu kwamba HAKUNA mtoto anayezaliwa duniani ambaye Mungu HAMJUI; hata huyo mwanaharamu! Mungu alimfungia nje ya kusanyiko lake kwa vizazi arobaini!!!! Yaani Mkristo uliyelipokea Neno la Mungu ukitoka ukazilisha wanaharamu, basi kama zao lako limezuiliwa ktk kusanyiko vizazi arobaini, je, wewe mwenyewe ndio utapokelewa??? Usijidanganye, wewe ni mfu anayetembea, nao wafu hawana ijara na wala hawajui neno lolote!!!!

  Macho ya Mungu ni Neno lake, na macho ya wanadamu ni tamaa zao; basi ili uwe salama nenda ukapewe “Eye salve” upate kuyaona yaliyojificha, hizo PERVATIONS!!

  Ubarikiwe!

 9. Yes, hii ni mada umeleta Edwin!

  Hapa ndipo rubber inapokutana na dust, maana ndio wakati pekee wa kujua kama hiyo rubber(kifutia) ni ya kweli au la.

  Hii ni ishu live inayotokea leo katika jamii yetu.

  Kwa taarifa yenu wa ndugu hii si mada ya kukurupuka, vinginevyo itakulazimu kutubu huko mbele kwa uliyosema kwa kukurupuka huku nyuma.

  Lazima mtu ufikiri kwa uzuri na kwa makini kabla hujatoa majibu. Unajua kuna vitu watu huvisema au hufikiri kuwa ni dhambi pasipo hata kujiuliza kwa kina kwa nini hivyo vitu wanadhani ni dhambi.

  Yes, kama ambavyo kuna dhambi kupitia tendo la ndoa, kuna dhambi pia kupitia chakula.

  Sasa basi lazima nyie ambao tayari mmeshaonesha misimamo katika mada hii mtuambie hilo suala la kupata mimba kwa njia za kisayansi ni dhambi au siyo dhambi kivipi!

  Tunataka facts zilizochambuliwa siyo tu kuleta hitimisho!

  Milinga ninakufuatilia kwa umakiniiii!!

  Haya twendeni!

 10. Wapendwa,

  Maandiko yanasema, “LISILOWEZEKANA KWA MWANADAMU KWA MUNGU LINAWEZEKANA”

  Sidhani kama kuna mkristo asiyejua andiko hilo hata kama hajui liko kitabu gani. Hata hivyo nadhani falsafa iliyoyomo kwenye andiko hilo wengi hawaijui.

  Ni hivi, Mambo yoooooooooote ambayo mwanadamu hawezi na ameshindwa kuyatatua hayo ndiyo tumtwike Mungu atusaidie. kama una jambo ambalo wewe mwenyewe na wataalam na mabingwa wote mmeshindwa hayo ndiyo apelekewe Mungu. Haiwezekani wewe ukawa unamtwika Mungu fadhaa zako ambazo kwa mwanadamu inawezekana kutatuliwa.

  Mathalani, kama una shida ya Tshs 5000 tu kwa ajili ya jambo linalolingana na pesa hiyo huna haja ya kuanza kufunga na kuomba Mungu akupe shilingi elf tano, unamwendea mpendwa akuazime shs 5,000 na unafanya jambo lako kisha unamrejeshea pesa yake. Lakini kama unahitaji Tshs 50,000,000 (milioni hamsini) ukamwendea mpendwa huyo huyo ni wazi atakwambia kwamba hana uwezo wa pesa hiyo. Na bila shaka atakwambia jambo la kufanya kwamba ni kuomba Mungu afungue milango ya baraka upate pesa hiyo ujenge nyumba yako unayotaka.

  Mfano wa pili: Zamani mwanadamu alikuwa hawezi KUZAA MTOTO kwa njia ya kufanya upasuaji (operation). Sasa hivi mtoto akishindikana kutoka kwa njia ya asili yaani mwanamke kusukuma mtoto mpaka atoke, madaktari wenye kuweza jambo hilo la operation ni wengi siku hizi. Hapo ni kukamata visu nakuanza kufanya upasuaji na mtoto anakuja kilaiiiiiiiini tu. Hapo ujue wapendwa wameshaooooomba mpaka wameshindwa kuvumilia. Mzazi naye ameshamwita Mungu naye amekuwa kama yuko kimya ingawa yupo na anwatazama.

  Swali: Je, kujifungua mtoto kwa njia isiyokuwa ya kawaida (OPERATION) kama Mungu alivyokusudia ni dhambi? Kama unasema siyo dhambi inakuwaje kupata mtoto kwa njia ya kupandikiza iwe dhambi?

  Kama kupandikiza mimba ni uasherati au ni sawa na kufanya uzinzi, je uzinzi ni kupata mtoto au uzinzi ni kitendo?

  Je, kama mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa ni mwanaharamu mbele za Mungu akiokoka anaendelea kuwa mwanaharamu mbele za Mungu?

  Au Mtoto wa nje ya ndoa anakuwa mwanaharamu kwa wanadamu kwa kuwa Mungu nijuavyo mimi hatazami kama wanadamu tunavyotazama mambo?

 11. WAPENDWA KUPANDIKIZA MIMBA KUNAONYESHA NI JINSI GANI AMBAVYO TUNAKUWA TUMESHINDWA KABISA KUMWAMINI MUNGU KWA ALICHOKISEMA, NA NENO LINASEMA PASIPO IMANI HATUWEZI KUMPENDEZA MUNGU. TUKIMCHUKIZA MUNGU NI DHAMBI AU SIO DHAMBI NADHANI JIBU TUNALO.
  PILI NI KUKOSA TUNDA LA ROHO (UVUMILIVU), NA KUAMUA KUENDESHA MAISHA KWA STYLE YETU, TUKIJARIBU KUYAHALISHA KUWA MUNGU ALITUPA AKILI, THAT IS WRONG.
  NENO LINASEMA WALE WANAOONGOZWA NA ROHO HAO NDIO WANA WA MUNGU. ROHO MTAKATIFU ALIWAHI MWONGOZA MTU KWENYE KUPANDIKIZA MIMBA, SIDHANI.
  KWA VIGEZO HAPO JUU MIMI NINAAMINI KUWA HILI NI DHAMBI YA KUTOMWAMINI MUNGU KWA KILE ALICHOSEMA. TUKIENDELEA NA UTARATIBU HUU TUTAFIKA MAHALI TUTAHALILISHA HATA MAMBO YA SAMUNGE.

 12. Ndugu Milinga,

  Acha nijaribu kuongea nawe:
  Hii unayoita maswali, ni kweli ulitafakari ukayaona yanastahili?
  -Kulea mtoto asiye wako si dhambi, bali Mungu anamuona kama mwanaharamu. Ni dhambi ya yule mama ambae alitenda uzinzi. Hali kadhalika, huyu mdada anayepachikwa mimba kisayansa amefanya uwasharati wa kisayansa. Ile yote ni nje ya ndoa.
  -Hapa hakuna jambo la kulinganisha na chakula. Kwani kula na kuzini au kutenda uasherati huwezi vilinganisha. Chakula kiwe natural au syntentic kinabaki chakula tu.
  -Kuongezwa damu siyo kutengeneza mtu mwengine. Anaeongezwa damu, DNA yake haibadiliki. Kuongezwa damu siyo uasherati wala uzinzi wala kuzaa mtoto. Mtoto anafanyika wakati mbegu ya kizazi ya mwanaume inaambatana na ya mwanamke. Sasa katika damu hamna mbegu ya kizazi.

  -Dhambi zote zinajulikana ndugu yangu. Ni Mungu anae define dhambi. Uasharati na uzinzi wa aina yoyote ni dhambi. Dawa na chakula siyo dhambi kwani hakuna nafasi ambapo unaweza ionyesha ndani ya biblia kama dhambi

  Endelea…..

 13. mimi nafikiri kwa yule ambaye hana uwezo wa kupata mtoto kwa njia halali anaweza akapandikiziwa mbegu za mume wake. lakini lakini ambaye uwezo wa kuzaa anao lakini ameamua tu mi naona ilo nichukizo mbele ya Mungu

 14. Utafiti unaonesha kwamba idadi kubwa ya wanawake wanawabambikiziaa wanaume watoto. Yaani kuna watoto wengi wanachukua ubini wa baba ambaye siye aliyepachika mimba kwa mama.

  Ukweli ni kwamba unaweza ukawa unalea watoto wa baba mwingine hapo ulipo wewe ukawa unadhani unalea watoto wako kumbe mwenzio alichepuka akazaa na huyo uliye naye.

  Kama hujapima DNA ukajua kuwa watoto unaolea ni wa damu yako ni vyema ukajinyamazia tu labda kama watoto wako wanafana na wewe angalau kwa sehemu hapo unaweza kujipa matumaini kwamba watoto hao ulio nao ni wako.

  Kuzaa watoto ambao siyo wa mbegu ya kuingizwa kwa tendo la ndoa baali kwa sindano kama utasema ni dhambi, ni sawa na kusema wote wanaokula kuku wa kisasa walioatamiwa mayai yao kwa mashine na kupandikizwa kwa mashine nao wanakula kuku haraaaaaaam?

  Kama utasema kuzaa mtoto aliyepandikizwa kwa kutumia sindano maalum ni dhambi, je kumuongezea damu mtu ni dhambi? Maana unapandikiza damu yako kwa mtu mwingine? Je, hiyo damu uliyonayo ni haraaaam?

  Nina maswali meengi ya kuhoji watu wote wanaowahi kusema kuwa swala hilo ni dhambi, ila kwa leo naomba watu wajihoji maswali hayo kisha twendelee na majadiliano.

 15. Huyu dada amefanya machukizo mbele za Mungu. Kama anashiriki ndani ya kanisa, amewakwaza wakristo wote vile vile. Yaani atamzaa mwana haraaaaamu wa kupindukia.

 16. KWANZA KABISA NINAOMBA TUJUE KUWA KUNA AKILI MBILI TU NDANI YA UUMBAJI. 1. AKILI YA MUNGU WA KWELI NA 2. AKILI YA MAREHEMU SHETANI. HAKUNA AKILI NEUTRAL. HIVYO CHOCHOTE UNACHOKIFANYA KAMA KIPO NJE YA MSINGI WA NENO LA MUNGU UJUE HICHO SIO CHA MUNGU NA CHOCHOTE UNACHOKIFANYA KAMA KIPO KWENYE MSINGI WA NENO LA MUNGU BASI HICHO NI CHA MUNGU. HILO JAMBO LA KUPATA MIMBA KWA NJIA YA KISAYANSI LIKO NJE YA MSINGI WA NENO LA MUNGU KWA HIYO NI LA SHETANI NA NI UOVU MBELE ZA MUNGU. PIA MJUE KUWA AKILI YA SAYANSI SIYO AKILI YA MUNGU KWAKUWA AKILI YA SAYANSI NDIYO INAYOTUMIKA KUZALISHA MAMBO MABAYA MENGI SANA DUNIANI MFANO MAGONJWA MBALIMBALI TUNAYOYASIKIA YAMETENGENEZWA TU NA AKILI YA SAYANSI. MUNGU ATUSAMEHE KWA KUFANYA MAMBO KINYUME NA UFALME WAKE.

 17. Neno la Mungu linasema wakat mwingine maarifa ya mwanadam ni machukizo mbele zake, ikiwa anahitaji mtoto anachotakiwa ni kumwomba Mungu ampe mtoto kwa Mumewe au kama ni mwanaume kwa mkewe, kama hana anahitaji kuanza msingi( ndoa) then atafute mtoto kwa Bwana, bank sperm naeza sema madhara yake ni makubwa manake hujui imetoka kwa mwanaume wa aina gan, mwenye tabia zipi na pia sio natural way iliyowekwa na Mungu, manake unaenda kinyume na asili ya Mungu.

 18. nadhani hilo si jambo jema kabisa,kwani Mungu alikusudia tendo halisi la ndoa liwe kwa ajili ya mwongezeko wa wanadamu duniani na si kupandikizwa kwa mbegu za kiume…amekiuka mpango maalum wa Mungu!!!

 19. Iko hivi, iwapo mama hawezi kumtambua baba wa mwanae, yaani katika case hii baba wa mtoto huyo atakayezaliwa atakuwa ni Sperm Bank; ndipo mtoto huyo labda ataitwa “Lwembe”, basi jina lake kamili litakalo onekana katika cheti chake cha kuzaliwa litakuwa “Lwembe Sperm Bank”; kwa lugha rahisi “Mwanaharamu” au “a Bastard”!!!

  Na mama yake? Mrs ‘Magdalene’ Sperm Bank!!!

  Msubirini Bwana; Sara alikuwa na umri wa miaka 90 alipopata mtoto, hakuna lisilowezekana kwa Mungu!

 20. Shalom watumishi wa Mungu,huo UTATA hata mimi unanisumbua,binafsi nilishawahi kuuliza hilo swali kwa Pastor wangu akanijibu kuwa ni dhambi ingawa hakuambatanisha na NENO ktk JIBU LAKE.so nami ni mmoja kati ya wanaohitaji kujua KWELI ktk hilo KIMAANDIKO kwan KUJUA KWELI, KWELI ITATUWEKA HURU,na hasa kwa sababu kwenda motoni kwa sababu ya mtoto tu HAPANA KWAKWELI .MBARIKIWE

 21. IKIWA KUPANDA GARI AU NDEGE ILIYO ZAO LA SAYANSI NI DHAMBI BASI TUNAWEZA KUHOJI PIA IWAPO MUNGU ALITUPA AKILI YA KAZI GANI NA KWA NJIA HIYO SIYO DHAMBI KABISA KWA UPANDE WANGU

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s