Manabii wa Kweli ni wapi?

biblia

Bwana Yesu asifiwe Mtumishi, mimi nataka kujua Manabii wa kweli ni akina nani? pia kwenye Biblia unafahamu nabii ambaye ni wakweli na kazi alizofanya?

Gilbert Kijumbe

Advertisements

18 thoughts on “Manabii wa Kweli ni wapi?

 1. manabii wa kweli ni wale wanahubiri kuhusu ufalme wa Mungu ambao ni haki, amani, na furaha ndani ya Roho Mtakatifu

 2. Asanteni wapendwa swala hili ni muhimu sana, mimi ningependa tu kuchangia na kukumbusha kwamba yeyote aliyezaliwa mara pili ni nabii wa maisha yake kwanza, na pia kuna watu ambao Mungu Amewaweka Kutuongoza au kutuchunga, (wachungaji).hawa nao pia wana authority au mamlaka juu yetu kama waumini ndani ya kristo, ili watu wamwamini Mungu na pia wawe na adabu katika mwili wa kristo. Mungu atusaidie

 3. MANENO YA MANABII WA KWELI HAYAPINGANI

  1 WAKORINTHO 14:32
  “NA ROHO ZA MANABII HUWATII MANABII”

 4. Tukirejea katika mada, kuhusu jinsi ya kuwatambua manabii wa kweli, ukweli ni kwamba HAKUNA mtu anayeweza kwa uhakika akakuonesha kwamba huyu ndiye nabii wa kweli isipokuwa Mungu! Naye Mungu ni Neno lake yaani Bwana Yesu Kristo.

  Na kulingana na Biblia, nabii humuwakilisha Mungu, ndipo iwapo Mungu atamuinua nabii, basi neno la nabii huyo hujulikana kuwa ni Neno la Mungu. Nalo neno hilo hupokelewa na kusimamiwa na viongozi wa makusanyiko ktk uhalali wake.

  Lakini, juu ya hivyo, jambo hili la manabii Mungu hakuliacha lielee hewani bila ya utaratibu. Huko nyuma ktk AK kulikuwa na utaratibu wa kumtambua nabii; na leo hii ktk nyakati hizi za Agano Jipya Mungu ameweka utaratibu. Basi iwapo yeyote atasimama na kudai kuwa yeye ni nabii, utaratibu huu tuliopewa ndio utakaomdhihirisha kuhusu nafasi hiyo, maana pia tunawategemea manabii wa uongo!

  Katika kutamatisha utaratibu wa AK, hili hapa Neno linaloliweka wazi jambo hilo:
  “Kwa maana manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana.” (MT. 11:13). Hivyo twafahamu kwamba Yohana Mbatizaji ndiye aliyeufunga utaratibu huo akiwa ndiye nabii wa mwisho wa order hiyo.

  Sasa baada ya hapo inakuwaje? Hili hapa Neno la kutuongoza, likiviunga hivyo vipindi viwili katika utenganisho wa utaratibu. kanisa likipelekwa katika hatua ya juu zaidi ili kukabiliana na hao manabii wa uongo watakaojitokeza; “Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.” (EBR. 1:1, 2)

  Huu ndio Ukweli wa jambo hili la manabii ki Maandiko. Nabii anayekuja leo hii baada ya awamu ya kwanza kufungwa, ni Lazima ayaseme ya Yesu, yaani RM!

  Naye RM ndiye aliyeyachukua ya Yesu na kuwapa mitume, 2Pet 1:19 “Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing’aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.” Unaona! Neno la unabii walikwisha kupewa mitume ndio huu ushuhuda wa Yesu Kristo uliotufikia sisi, “… Kwa maana ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii.” Ufu 19:10

  Kwahiyo ni kwa kipimo hiki pekee ndio tunaweza kumtambua nabii wa kweli, ni lazima anene sawa na Injili waliyofundisha mitume, vinginevyo ni nabii wa Uongo! Ni katika urahisi huu ndio tunasema “nabii Eliya wa Siloamu” hawezi kuwa nabii wa kweli kutokana na yeye kunena tofauti na Yesu Kristo hapo anapojipachika nafasi ya u “Adamu wa Pili, Mungu wa majeshi” bila ya rejea yoyote ya Mwongozo (Biblia)!

  Pia nabii wa kweli hawezi akafungamana na Utatu Mtakatifu kwa sababu hilo si Neno la Kristo, Mungu hajawahi kujitambulisha kwamba yeye anazo nafsi tatu, hilo si neno la unabii kulingana na Bwana Yesu Kristo aliye Neno la Mungu!!!

  Hakuna mahali Mungu aliahidi kuleta Neno jipya, yeye ameahidi kulirejesha hilo Neno lililoliwa na hao wadudu waharibifu, kama huyo aliyebuni Utatu na kuupachika Uungu akiwaingiza watu katika ibada ya miungu!!!

  Litazameni Neno la Mungu linachosema, mkiamini hicho na kuyakataa yote yanayojiongeza au kujipunguza, maana hayo yanaletwa na roho ya Mpinga Kristo anayefanya kazi ndani ya wana wa kuasi, hao walikataliwa katika mambo ya imani!

  Mbarikiwe!

 5. Wapendwa,

  Kuhusu hili jambo la kuwatambua manabii wa kweli ni akina nani, mimi nadhani linahitaji zaidi tafakari iliyojikita katika Neno la Mungu, kuliko hisia zetu!

  Maelezo ya ndg Mwenda ni mazuri na yanaeleza uhalisi wa ufahamu tulionao wengi wetu, na uoga ama hofu inayotushikilia kuhusu jambo hilo. Hofu hii unaweza kuiona jinsi ilivyojificha chini ya maelezo mazuri ya ndg Mwenda hapo anapomkataza Kissa asimbeze “Nabii wa kweli aliyepewa AGIZO na Mungu mwenyewe, Nabii ELIYA ADAMU 2 MUNGU WA MAJESHI wa kanisa la THE POOL OF SILOAM”!!!!

  Kauli ya Kissa kuhusu nabii huyo akiyarejea aliyoyaandika Vai ni hii hapa:-
  “kweli vai unadiriki kusema mtandaoni Yesu alikuwa kizazi cha tatu kwahiyo sasa hivi hana kazi tena amesha pita, ni zamu ya munuo? hapana jamani tuwe macho wakristo ili jambo ni sirious kuna watu bado hawajaijua kweli na wakikutana na injili kama hii watapotea. wachungaji tufundisheni ili tuweze kutambua manabii wa ukweli”

  Mimi kwa mtazamo wangu, nikijaribu kuyarejesha maelezo ya Vai na Kissa katika Maandiko, ninampongeza Kissa kwa kusimama na Neno la Mungu na pia ninamuhurumia ndg Mwenda kwa ku compromise Neno la Mungu ili apate kuheshimiana kusiko na tija!!!

  Pia haya maelezo kwamba,
  “Nyakati hizi za agano jipya, vyeo ambavyo ni maalum kwa watu maalum ni vichache, labda ni uchungaji, kwa sababu mchungaji lazima awe na kundi analochunga, askofu kwa sababu atakuwa na makanisa anayoyasimamia, vyeo vingine vya kiroho karibu kila aliyeokolewa anakuwa navyo, mfano ni huo wa unabii, utume nk.”
  Sifahamu maelezo haya ameyatoa wapi katika Maandiko, licha ya uzuri wake, lakini ni kifo, kwa sababu ni kupitia maelezo matamu kama haya, wakristo wengi wanatekwa ufahamu wao na kubaki wanaelea juu juu na kusombwa na kila wimbi la ngonjera za dini, haswa hao manabii!!!!

  Lakini Mungu amekuwa very specific kuhusu vyeo vyake, sio vya holela, vina kazi maalumu, Efe 4:11-12 ” Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; 12 kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe”

  Mungu hajasema kila aliyeokoka ni mtume, au ni nabii, au ni muinjilisti, au ni mwalimu, hapana amesema “wengine”; Kanisa la Mungu lina utaratibu, kila mtu anapaswa akae ktk sehemu yake ya kazi aliyopangiwa na RM, hata ukiwa ni busati la mlangoni!!

  Gbu!

 6. Nimepitia comments za wachangiaji na nimefurahishwa nazo kwa kiasi chake japo mmoja yaani Vai amevuruga. Kwanza nabii ni mtu aliyetumwa na Mungu kuleta ujumbe wake duniani iwe ni kwa ulimwengu, Taifa au kikundi cha watu au kwa mtu kwa njia ya mafundisho au kutabiri. Ujumbe anaoutoa lazima uwe wa kweli pasipo kupotosha na uko sawa na neno la Mungu yaani Biblia. Akitoa utabiri ni lazima utimie kwa asilimia 100, na endapo haukutimia utabiri hata mmoja huyo atajulikana kama nabii wa uongo kwa kuwa amesema kitu ambacho Mungu hakumtuma. Soma kwa umakini Kumb-18:15-22.

  Jambo alilosema Vai kuhusu Pool of Siloam hatuwezi kuliacha lipite hivi hivi kwani hili kanisa na nabii wake tunamfahamu vizuri na ya kwamba hii ni CULT. Hebu ona hii roho ya kujiinua ya huyu mtumishi eti yeye ni Eliya ajae, Adam wa pili, Bwana wa majeshi. Ikiwa mtu amechukua nafasi ya Mungu kuna shaka gani ya kujua hii ndio tabia aliyokuwa nayo Lusifer (ibilisi) hapo kabla hata akatupwa nje ya mbingu?. Kwa mtu makini anaye ijua biblia vizuri fuatilia au fanya utafiti mdogo tu kuhusu hii huduma utagundua ni imani potofu.

  Katika mafundisho ya hii huduma unaweza kubatizwa hata mara ishirini na zaidi, pia ukibatizwa lazima ubadili jina na kupewa lingine na hata la baba yako aliyekuzaa halitambuliki ila utaitwa mtoto wa eliya. Mfano mimi itabidi niandike Primi Eliya. Pia anadai kuwa ELIYA AMEMUUA SHETANI TANGU 2007, hivyo shetani hayupo tena dunia. Fundisho hili limewafanya kupotosha kwa kusema kuwa dhiki kuu imeshapita na sasa tupo kipindi cha utawala wa Yesu wa miaka 1000.

  JAMANI KWA HAYA MACHACHE KAMA UNAIJUA BIBLIA UTASUMBUKA KUJUA HII NI IMANI GANI?. EE MUNGU TUSAIDIE.

 7. BAADHI YA VIPIMO VYA MANABII
  1.SHERIA NA USHUHUDA
  ISAYA 8:20
  “NA WAENDE KWA SHERIA NA USHUHUDA; IKIWA HAWASEMI SAWASAWA NA NENO HILI, BILA SHAKA KWA HAO HAPANA ASUBUHI.”
  2. MTAWATAMBUA KWA MATUNDA YAO
  MATHAYO 7:20
  “NDIPOSA KWA MATUNDA YAO MTAWATAMBUA”
  3. KUTOKEA KWA JAMBO LA AMANI JUU YA NCHI ALILOTABIRI
  “NABII ATABIRIYE HABARI ZA AMANI, NENO LA NABII YULE LITAKAPOTOKEA, NDIPO NABII YULE ATAKAPOJULIKANA KUWA BWANA AMEMTUMA KWELI KWELI” YEREMIA 28:9

  KAZI ZA MANABII
  1. KUPELEKA UJUMBE ULIOTOKA MOJA KWA MOJA KWA MUNGU.
  2. KUFUNUA MIPANGO YA MUNGU KWA WANADAMU
  AMOSI3:7 YOHANA 14:3
  3. KUWATIA NGUVU VIONGOZI WA TAIFA LA MUNGU NA KUWAONGOZA
  ISAYA 36:2 ISAYA 37:6, 7 2 SAMUEL 7 1 NYAKATI 22:14
  4. KUWAONGOZA WATU KUWA WAAMINFU KWA MUNGU
  JOSHUA 24:20-23 MATHAYO 25:21
  5. KUKEMEA MAOVU
  MIKA 2:1-3 HOSEA 4:1,2 YOHANA 2:16 JEREMIAH 20:9
  6. KUSIMAMIA SHUGHULI ZA TAIFA LA MUNGU
  1 NYAKATI 28:11,12 EZARA 5:2 KUMBUKUMBU 4:6
  7. KUFUNDISHA 2 PETRO 1:21

  MAMBO YA UONGO WAFANYAYO MANABII WA LEO

  1 KUWATABILIA WATU MAMBO WATU WAYAPENDAYO REFER 2 PETRO 1:21
  2 KUSUBIRI TUKIO KISHA KUSEMA NILIWAHI KUTABIRI.
  3 UTABIRI WAO HUWA WA JUMLA JUMLA KAMA WAAGUZI WA NYOTA,
  4 KUDHANI KUWA TAIFA LAWEZA KUWA NCHI NA KUANZA KUCHANGANYA DINI NA SIASA WASIJUE ISRAELI YA SASA NI YA KIROHO (KANISA) NDIO TAIFA LA KUONGOZA.

  5 MANABII WA KWELI WALICHUKIWA NA UJUMBE WAO.MFANO ISAYA KUKATWA MSUMENO,ELIYA KUTAFUTWA,YEREMIA KUFUNGIWA KATIKA SHIMO LA MATOPE,KUMBUKA MANABII 400 KWA NABII MOJA ALIYEPASWA KUUWAWA N.K.
  6 MANABII WA LEO WANATABIRI ILI WAPENDWE NA WATU SIO ILI WAMPENDEZE MUNGU
  7 WAMEJAA UNABII WA KUAGUA NYOTA, MIKOSI, LAANA ZA FAMILIA, PESA, (astrology)

  “MIMI SIKUWATUMA MANABII HAO, LAKINI WALIKWENDA MBIO; SIKUSEMA NAO, LAKINI WALITABIRI”
  YEREMIA 23:21

 8. BAADHI YA VIPIMO VYA MANABII

  1.SHERIA NA USHUHUDA

  ISAYA 8:20
  “NA WAENDE KWA SHERIA NA USHUHUDA; IKIWA HAWASEMI SAWASAWA NA NENO HILI, BILA SHAKA KWA HAO HAPANA ASUBUHI.”

  2. MTAWATAMBUA KWA MATUNDA YAO
  MATHAYO 7:20
  “NDIPOSA KWA MATUNDA YAO MTAWATAMBUA”

  3. KUTOKEA KWA JAMBO LA AMANI JUU YA NCHI ALILOTABIRI
  “NABII ATABIRIYE HABARI ZA AMANI, NENO LA NABII YULE LITAKAPOTOKEA, NDIPO NABII YULE ATAKAPOJULIKANA KUWA BWANA AMEMTUMA KWELI KWELI” YEREMIA 28:9

  KAZI ZA MANABII
  1. KUPELEKA UJUMBE ULIOTOKA MOJA KWA MOJA KWA MUNGU.

  2. KUFUNUA MIPANGO YA MUNGU KWA WANADAMU
  AMOSI3:7 YOHANA 14:3

  3. KUWATIA NGUVU VIONGOZI WA TAIFA LA MUNGU NA KUWAONGOZA
  ISAYA 36:2 ISAYA 37:6, 7 2 SAMUEL 7 1 NYAKATI 22:14

  4. KUWAONGOZA WATU KUWA WAAMINFU KWA MUNGU
  JOSHUA 24:20-23 MATHAYO 25:21

  5. KUKEMEA MAOVU
  MIKA 2:1-3 HOSEA 4:1,2 YOHANA 2:16 JEREMIAH 20:9

  6. KUSIMAMIA SHUGHULI ZA TAIFA LA MUNGU
  1 NYAKATI 28:11,12 EZARA 5:2 KUMBUKUMBU 4:6

  7. KUFUNDISHA 2 PETRO 1:21

  MAMBO YA UONGO WAFANYAYO MANABII WA LEO

  1 KUWATABILIA WATU MAMBO WATU WAYAPENDAYO ILI KUWAFURAHISHA NA KUPATA SIFA REFER 2 PETRO 1:21

  2 KUSUBIRI TUKIO KISHA KUSEMA NILIWAHI KUTABIRI.

  3 UTABIRI WAO HUWA WA JUMLA JUMLA KAMA WAAGUZI WA NYOTA,

  4 KUDHANI KUWA TAIFA LAWEZA KUWA NCHI NA KUANZA KUCHANGANYA DINI NA SIASA WASIJUE ISRAELI YA SASA NI YA KIROHO (KANISA) NDIO TAIFA LA KUONGOZA BADALA WAFANYE KAZI KUYAPINGA YA ULIMWENGU YALIO KINYUME CHA MUNGU.

  5 MANABII WA KWELI WALICHUKIWA NA UJUMBE WAO.MFANO ISAYA KUKATWA MSUMENO,ELIYA KUTAFUTWA,YEREMIA KUFUNGIWA KATIKA SHIMO LA MATOPE,KUMBUKA MANABII 400 KWA NABII MOJA ALIYEPASWA KUUWAWA N.K.
  6 MANABII WA LEO WANATABIRI ILI WAPENDWE NA WATU SIO ILI WAMPENDEZE MUNGU

  7 WAMEJAA UNABII WA KUAGUA NYOTA, MIKOSI,UMIZIMU (UFU) LAANA ZA FAMILIA, PESA, (astrology)

  “MIMI SIKUWATUMA MANABII HAO, LAKINI WALIKWENDA MBIO; SIKUSEMA NAO, LAKINI WALITABIRI”
  YEREMIA 23:21

 9. ELLY KOMBE unamaana Yesu naye alikuwa nabii kama akina Elia, Yesaya na akina Hosea, au unamaanisha nini. Hivi baada ya ujio wa roho mtakatifu kama tukiwa wakweli na maisha yetu masafi mbele za Mungu na roho mtakatifu yuko ndani mwetu ambaye Yesu aliahidi atatutia katika kweli yote na kutujuza yajayo, hawa manabii watafuta pesa. Yesu hakuwa hata na mahali pa kulaza kichwa chake, niambie hao mnaowaita manabii wa leo wako je. Kazi yao kubwa ni kujilimbikizia mali lukuki. Waumini wamechoka manabii wanaishi maisha ya kifuru. Mpende jirani yako kama nafsi yako haliwahusu. Nipeni mfano wa aliyesafi kwenye hili.

  TZ kila siku nabii mpya anainuka, na ilikuwazuga watu anatafuta mstari wa kusimamia ilikutoleta utofauti na wenzake ilinaye apate wavivu wanaotaka kulishwa kama makinda ya ndege, hata ukiyapa jiwe yanabugia.

  1. MTAWATAMBUA KWA MATUNDA YAO SIO MANENO, SIO UPONYAJI NA MIUJIZA MAANA HATA SHETANI ANAWEZA FANYA. MIZANI NI MAISHA YA YESU WANAMFANANIA AU MADHABAHUNI NI WAMUNGU LAKINI URAIANI NI WATU KAMA WATU WENGINE. NI NANI MWENYE MAISHA YA AINA HII AMBAYE TUKITEMBELEA MAJIRANI ZAKE WATASIFIA MAISHA YAKE KUWA YAMEKUWA UKOMBOZI KWAO. WENGI NI WATAKATIFU MBELE YA MAKUSANYIKO YAO TU LAKINI HAWAFAI HATA KIDOGO WAKATILI WAKITUMIA PESA ZA SADAKA WANAZOJIKUSANYIA MAKANISANI KUKANDAMIZA WENGINE NA WENGINE WANATEMBEA MPAKA NA WAUMINI WA MAKANISANI YAO.
  2. NABII WA KWELI ATALITUMIA NENO LA MUNGU KWA USAHIHI NA SIO KULIPINDISHA KWA AJILI YA KUTAKA UMAARUFU AU KUWAVUTA WATU WENGI WAJE KWAKO.

 10. SIKU ZOTE NABII UKWELI WAKE NI WITO WAKE.MUNGU KAMWITA KUSEMA AU KUFANYA NINI KAMA ASEMAVYO VAI
  LAKINI NABII AKISEMA NENO LISIPOTIMIZWA NI USHAHIDI WA KUTOSHA MUNGU HAJAMTUMA POPOTE

 11. Asante kaka bernad nilikuwa sina lengo la kumbeza. Naendelea kujifunza Barikiwa

 12. Bernard Bruno Mwenda UMENENA VYEMA MPENDWA NA HUO NDIO UKWELI MAANA KILA ALIEYOKOKA AMETUMWA NA KWA KUWA ANAROHO WA MUNGU ANAFANYA HUDUMA YA KINABII PIA, AMA LABDA AWE AMEKUFA KIROHO.

  VAI HUO NI OPOTOSHAJI KUMFANANISHA YESU NA AKINA MUNUO, ELIYA, ELISHA.
  1. YESU HAKUJA KWA ZAMU ZA KUPOKEZANA KAMA MNAVYOTAKA KUTUDANGANYA. YEYE NI MUNGU, SOMA YOHANA 1:1-5. KUNA NABII ALIYEKUJA KUOKOA. YESU ALIKUJA KUOKOA.
  2.HIKI SIO KIZAZI CHA NNE JAMANI HAMNA HATA HAYA KUDANGANYA WATU. VAI UTAHUKUMIWA KWA UONGO UNAOUSAMBAZA MATHAYO 1:17 TANGU IBRAHIM MPAKA YESU ANAKUJA NI VIZAZI 42 KWA HESABU RAHISI KASOME BIBLIA UONE.
  3. ELIA WA KWELI HAKUPIGIWA UPATU KAMA MNAVYOFANYA LEO HII, YESU MWENYEWE HAKUPIGIWA UPATU KAMA MNAVYOFANYA, MAISHA, MANENO NA MATENDO YAKE LIKUWA MATANGAZO YA KUTOSHA.

  VAI KUSHUPAZA SHINGO NI KUPALILIA JEHANAMU TU.

 13. Shalom wapendwa katika Kristo Yesu. Nimeyasoma maelezo ya kissa chris na vai kuhusu yupi ni nabii wa kweli, maelezo yao yameweza kutuonesha jinsi ilivyo au inavyoweza kuwa vigumu kwa mtu mmoja mmoja kufahamu au kutufahamisha, yupi ni nabii wakweli na wote tukaamini.

  Kabla nami sijaanza maelezo yangu juu ya yupi ni nabii wa kweli, ningependa kwanza kumwambia ndg kissa kris asimbeze vai kwa maelezo yake yeye kuamini hayo anayoyaamini. Ndiyo maana tunajadili tupate kushirikishana, hivi nabii wa kweli ni yupi?

  Baada ya ya hayo, mimi nami ninapenda nichangie mada hiii kadiri ninavyofahamu, zaidi sana ikiwezekana nitatumia na maadiko ya biblia kidogo maana ndiyo msingi wetu wa ukristo.

  Katika maisha ya wokovu wangu nimeona mtazamo wa wengi wanaamini kuwa nabii ni yule anayesema au anayetabiri mambo yajayo. Huyo wanamwita nabii. Au wengine wanasema nabii ni yule anayeweza kumwelezea au kumtabiria mtu mambo yajayo ambayo yataweza kumtokea yawe mabaya au mazuri, huyo naye wanamwita nabii. Kwa namna nyingine hata mchawi kwa msimamo huu anaweza kuwa manabii. Kwa sehemu inakuwa ni kama ukweli wa maana ya nabii.

  Lakini utokana na maandiko, ninavyofahamu mimi sasa ni kwamba, nabii ni yule anayeyanena maneno ya Mungu. Nabii ni yule anayesema sawasawa na neno la Mungu linavyosema. “Yohana 3:34 Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu kwa sababu hamtoi roho kwa kipimo” Kila atakalolinena nabii lazima liwe sawasawa na Neno laMungu. Mtu wa Mungu anapohubiri na kusema “mwamini Yesu ili sije hukumiwa na ukaenda Jehanamu ya Moto, okoka” Mtu wa namna hii anakuwa amesema unabii kwa sababu ni kweli ndivyo maandiko yanavyosema, kwamba mtu asipomwamini Yesu atahukumiwa na kutupwa katika ziwa la moto, Yohana 3:17-18.

  Kifupi, inavyofahamu mimi ni kwamba neno nabii siyo zito saana kama tunavyolikuza, kwamba labda linawahusu watu maalum, hapana, kila aliyeokolewa mimi naweza kusema kuwa anaweza kunena neno la unabii, na mtu asipoliamini neno hilo kwa hakika atakwenda Jehanamu ya moto kabisa kama neno la Mungu la unabii linavyosema.

  Nyakati hizi za agano jipya, vyeo ambavyo ni maalum kwa watu maalum ni vichache,labda ni uchungaji, kwa sababu mchungaji lazima awe na kundi analochunga, askofu kwa sababu atakuwa na makanisa anayoyasimamia, vyeo vingine vya kiroho karibu kila aliyeokolewa anakuwa navyo, mfano ni huo wa unabii, utume nk. Ukiwa nabii utanena maneno ya Mungu, ukiwa mtume utanena pia maneno ya Mungu, na kimsingi kila aliyeokolewa ni mtume kwa sabau tumeokolewa ili tumtumikie Mungu. Na katika kumtumikia Mungu ni pamoja na kuwaleta watu kwa Krito Yesu katika kuwaelezea unabii kwamba wasipolisikia neno tunalowaeleza hakika mwisho wao ni mbaya, na ndivyo ilivyo. Mtu asipozaliwa mara ya pili hawezi kuurithi ufalme wa Mungu, Yohana 3:3 huo ni unabii na mtu akipinga asiufuate hakika hataona huo ufalme. Yesu Kristo ni njia kweli na uzima, mtu hatafika kwa Baba ila kwa njia ya yeye [Yesu] Yohana 14:6, huo pia ni unabii, mtu asipoufuata hakika siku ya mwisho hatamwona Mungu. Na kama watu walivyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu, waebrania 9:27 pia huu ni unabii mtu asipojitengenezea hapa hapa duniani, akiondoka hapa duniani ni katika hukumu.

  Shalom.

 14. Ndugu Vai,

  Please, ondoa mambo ya madhehebu. Hata kwa mtindo huu siumizwe na kwamba unalo. Sasa hilo jambo unaloingiza kisirisiri ya “kanisa la THE POOL OF SILOAM” limefikaje ndani ya mada hii? Tunapotafuta Nabii wa kweli, yaonekana kunajitokeza nabii tofauti. Angalisho!!!!!

 15. vai ww unataka kuleta mada nyingine hapa.Mungu atusaidie tuifutilie mbali mada mpya ya vai ya munuo mungu wake wa majeshi. kweli vai unadiriki kusema mtandaoni Yesu alikuwa kizazi cha tatu kwahiyo sasahivi hana kazi tena amesha pita nizamu ya munuo? hapana jamani tuwe macho wakristo ili jambo ni sirious kuna watu bado hawajaijua kweli na wakikutana na injili kama hii watapotea. wachungaji tufundisheni ili tuweze kutambua manabii wa ukweli

 16. Gilbert, Hongera kwa swali zuri ili tuweze kupata ufahamu wa kiungu.
  Nabii ni kiti cha Mungu . Nabii amembeba MUNGU wa kweli/ NENO LA KWELI. Nabii wa kweli aliyetumwa na Mungu ni lazima awe na AGIZO alilopewa na Mungu mwenyewe na lazzima apewe maelekezo na Mungu juu ya lile aliloagizwa kulifanya. Nabii ambaye atashindwa kulisema agizo alilopewa na Mungu huyo siyo nabii wa kweli bali amejiita mwenyewe au ameitwa na watu na wanadamu. Nabii ambaye hana agizo atatambulikana kwa matendo yake na pia hawezi kuwatoa watu utumwani kwakuwa hana maelekezo ya Mungu ya namna ya kuwatoa utumwani. Mfano wa Manabii wa kweli waliokuwa wamepewa AGIZO na Mungu ni MUSA kizazi cha 1, Eliya kizazi cha 2, Yesu kizazi cha 3 na kizazi hiki cha 4 Nabii wa kweli aliyepewa AGIZO na Mungu mwenyewe ni Nabii ELIYA ADAMU 2 MUNGU WA MAJESHI wa kanisa la THE POOL OF SILOAM. AGIZO alilopewa ni KULIJENGA KANISA LITAKALOMWABUDU MUNGU KATIKA ROHO NA KWELI NA KUVUNJA MISINGI MIBOVU YOTE NDANI YA WATU NA MAENEO WANAYOISHI. KARIBU UENDELEE KUJIFUNZA KUMJUA NABII WA KWELI NI YUPI KWAKUWA NABII ndiye aliyembeba Mungu na pasipo kumpata nabii mwenye AGIZO la Mungu mwenyewe /Nabii wa kweli huwezi kutoka utumwani.

 17. Gilbert,

  Hili swali lako ni la maana sana. Na kulijibu inaomba kutulia sana. Yaani najua halitapata jibu at once.

  Nabii wa kweli ni yule aneenena maneno Mungu anaemtuma. Hawezisema Mungu amenena anapotumia akili zake mwenyewe, dhamiri zake, ndoto zake za kawaida au habari alizozipata kwa mtu mwengine. Pia anamcha Mungu na anatambulikana kwa matendo.

  Utendaji wa miujiza, kutafuna lugha vizuri, kufoka, kunena kwa lugha, nk sivyo vigezo vya kumtambua,

  Lakini Nabii wa kweli anaweza kumkosea Mungu.

  Wanabii wa kweli katika Biblia ni wengi:

  Elia, Elisha, Yeremia, Zakaria, Mika, Habakuki, ……..Yoana Mbatizaji. Kazi walizozifanya ni nyingi sana. Unaposoma Biblia utaona hizo kazi.

  Ubarikiwe sana ndugu yangu.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s