Kigauni cha Sarah Jakes chaibua mjadala!!

Suala la mavazi bado linasumbua wakristo? Je bado tunasumbuka na mwonekano wa nje kuliko tabia ya mtu?

Pichani ni binti wa mhubiri maarufu T.D Jakes, Sarah Jakes alipokuwa akiongea kuhusu ushuhuda wa maisha yake pia na kutangaza kitabu chake kipya, lakini hata hivyo wengi walijali sana alivyovyaa na kuibua mjadala kwenye mitandao ya kijamii.

–NewLight Christian Center

Advertisements

56 thoughts on “Kigauni cha Sarah Jakes chaibua mjadala!!

 1. CK Lwembe,
  Katika hili imebidi nimshukuru Mungu kwa ajili yako kabisa kabisa, mimi nimekuwa nikifuatilia / kusoma masomo/ mada nyingi humu ndani ya Strictly Ki – Ukweli Lwembe umekuwa ukinifundisha mambo mengi sana na Ndugu mmoja anayeitwa Seleli, katika hili la kigauni cha huyu mwimbaji kweli nimefurahishwa na hoja zako kiukweli kabisa Mungu anakutumia.

  Sungura na Stella jifunzeni kwa Lwembe acheni ubishi

 2. Lwembe,

  Moja ya mambo huwa sipendi ni kule kuongea tu bila kupima unayoongea unamwambia nani na yana ukweli gani.

  Nafikiri tumechangia vya kutosha katika hii mada, kilichobaki naona ni maneno tu na vijembe kama unavyofanya sasa.

  Niliyosema yanatosha,acha niseme tu vitu vichache nitoshe kuhusu hii mada.

  Sijakuelewa unaposema kuwa biblia imeandikwa kwa lugha moja tu ya Kiebrania, unaongea ukiwa unajua unachosema au umewaza tu kisha ukaamua kusema.

  Sijui hata kama unajua Yesu alikuwa anaongea lugha ngapi na ni zipi.
  Mamno mengine ni ya ki ithibati zaidi kuliko kiufunuo,hivyo hayahitaji hata kuvutana.

  Pia sijui Paul anaposema Wayunani wanataka hekima na Wayahudi ishara wewe hudhani ni wayunani wapi mpaka useme lugha yao si moja ya lugha za asili za maandiko.

  Unadhani hao wajane wa kiyunani waliolalamika kuwa wanabaguliwa wakati wa kanisa la kwanza walikuwa wanaongea lugha gani mpaka useme lugha yao si moja ya lugha za biblia.

  Wewe kama unadhani ninajenga tofali lisilo sawa katika msingi wa Injili, wala usipate shida mwenye kazi atakuja kukagua mwenyewe.

  Mambo mengine mengi umesema kwenye comment yako, lakini naona ni kama kupoteza muda kukujibu. Wewe Lwembe huwa ikifika kwenye mambo yanayohitaji ufaham mkubwa uwezo xako wa ku-argue huwa ni wa chini sana,na huwa nashangaa.
  Ok, nikiona kuna sababu ya kujibu kila kitu ulivhoanfika ntafanya hivyo

  Jambo la msingi ni jili kuwa, msiwafanye wanawake wawe watumwa wa mavazi kwa namna ambayo haijamaanishwa na maandiko.

 3. Sungura,
  Ninakimalizia kile kipande nilichobakiza kuhusu maelezo yako, kama kuna nililolisahau, utanikumbusha, ni furaha yangu kuyajibu yote ninayoulizwa kuhusu ninayoyaamini!

  Nilikuambia huko nyuma kwamba dunia huwezi ukaikwepa, maana hiyo ndiyo inayomuwakilisha Ibilisi, nasi sote tulikuwamo humo chini yake mpaka tulipotolewa, Rm 5:12
  “… kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi”; kwahiyo, yeyote anayedai utakatifu nje ya Andiko hili ni muongo kwa asili. Na muongo yeyote angali yuko dhambini licha ya “utakatifu wa dini” anaojipachika, maana dunia yote ilikuwa dhambini na asiyelijua hilo ni sawa na zezeta wa dini!

  Kwahiyo maelezo yangu kuhusu dunia, nilitaka tu nikuoneshe kwamba unajadili na mtu anayeyajua hayo ya dunia na si zezeta wa dini! Ndio maana nilikuambia huenda wewe umeshushwa kutoka mbinguni; hata huo mfano wako wa chuoni, ambao haujakutoka kichwani mpaka leo, ukiwa na ladha ile ile kama unavyourejea, nawe ukiwa haulitambui hilo kwamba ndiyo dunia yenyewe, ni ishara kwamba bado una hatua ya kupiga!!!

  Kwa bahati mbaya umeniona kama ninayekufundisha mambo yaliyoko huko duniani, kwamba “nitakutia najisi”, lakini si kweli, tunayarejea hayo katika kuifunua dhambi ili walio wachanga wayajue hayo, kama ambavyo Torati inaifunua dhambi ya Uzinzi, si kwamba eti ndio inashawishi watu wawe wazinzi, hapana; basi wigo wa wazinzi unapopanuliwa kutoka mwilini kwenda rohoni, ni vizuri kuliweka jambo hilo wazi zaidi ili watu wasipotee kwa kukosa Maarifa! Lakini, pia ni ujinga kulikataa jambo ambalo lipo na limekuzunguka!!!

  Niliyoyaeleza kuhusu mwili wa mwanamke, ninayaelewa hivyo kulingana na ufahamu wa Neno la Mungu na dunia; na mwanamke aliyeyasitiri maungo yake, maelezo yake yako hivyo hivyo. Kulikataa kwako jambo hili, ukiwa umeikataa mpaka tafsiri ya wasomi wa lugha, ndipo sioni tena nitakueleza nini ambacho utakielewa ili mradi hata elimu umeikataa, ukachagua ujinga ambao umekuacha hulijui hata vazi la kusitiri linakuwaje; wewe mwenyewe ni shahidi wa hili, kwamba ktk maelezo yako yoote, hakuna hata mahali ulipotuonesha hilo vazi la kusutiri likoje, sana sana nimekuona ukiyajumuisha mavazi ya vile vigozi vya kufunika vya wamang’ati kuwa navyo ni modest; ndio maana nilikuambia kuwa maelezo yako mengi, kama si yote, ni lile vazi la majani!!!

  Kuhusu huyo mtu ambaye kwake hata kwapa la mwanamke linamletea shida, mimi nilidhani kupitia huyo utaijua taswira inayompasa mwanamke wa Kikristo! Lakini badala yake nakuona unahangaika kuwashawishi wajifunue miili yao zaidi ili huyo jamaa atamani mpaka awe “numb”, halafu muongezeke ktk idadi ili siku ya kupiga kura mshinde kama mashoga wanavyoshinda makanisani, vimini viwe ruksa! Siku moja maharusi walifukuzwa St Peters kwa kuacha kwapa wazi wakataka wampige ngumi padri!!!

  Hata huyo wa bikini zilizotundikwa dukani, kwa kukosa “Maarifa” unadhani eti bikini ndiyo imemsisimua; hapana, hiyo bikini inamkumbusha tu yule dada “aliyeokoka”, yule uliyemfundisha kwamba bikini ni vazi la kusitiri huko beach, kwahiyo akaivaa huko Coco beach akajizururisha mbele ya jamaa kama hao, ndio unawaona wakiendelea ktk mifadhaiko na huyo dada, baada ya kuisoma hiyo barua yenu akina Sungura, huyo dada “aliyeokoka”!!

  Amri Mpya ktk Mt 5:28, haimkamati mkristo asiye na Maarifa pekee, bali dunia yote, ndio maana kuna umuhimu wa kujua jinsi ya kujitunza, 2Kor 3:2-3:
  “Ninyi ndinyi barua yetu, iliyoandikwa mioyoni mwetu, inajulikana na kusomwa na watu wote; mnadhihirishwa kwamba mmekuwa barua ya Kristo tuliyoikatibu, iliyoandikwa si kwa wino, bali kwa Roho wa Mungu aliye hai; si katika vibao vya mawe, ila katika vibao ambavyo ni mioyo ya nyama.”
  Barua iliyowazi inasomwa na kila mwenye kujua kusoma! mwanamke anayejiwakilisha katika namna isiyompasa mkristo, anasomwa na dunia kama alivyojiwakilisha, wenye kumtamani watamtamani haijalisha amedanganywa nini na akina Sungura, na atafika ktk Hukumu aujibie uzinzi alioufanya na wanaume wooooooooooooote aliowaamsha hisia kwa mapaja yaliyo wazi, na wa matiti, pamoja na wapenda bikini! Lakini kwa mabinti wa Mungu kwao ni tofauti, wana amani ya Kristo mioyoni mwao, inayowafunika wote wanaowatazama!

  Malaya, nilikuambia wanavaaga gubigubi kuzihadaa mamlaka, lakini kwa asili hawana cha kuficha, wanamficha nani wakati hawana uwezo wa kumkumbuka kila mteja wao! Huko Znz wavae kinguo kifupi, labda wasipite darajani, ni bakora tu!!!

  Kuhusu “jambo jipya” ulilolinukuu ktk Isaya, hilo ndg yangu umeliokoteza tu maana halina uhusiano wowote ule na jinsi unavyotaka kulitumia. Usome tena vizuri huo mlango, unahusu ukombozi wa Israeli ile ahadi ya matengenezo na urejesho na si haya mambo yako ya vimini, kwamba eti ndiyo mapya anayoyafanya Mungu, ndio maana nilikuambia tafsiri kama hizo ndiyo chanzo cha cults nyingi sana duniani. Hebu fikiria hili, kwamba kutoka Maandiko haya ktk 1Kor 11:5-6, “Bali kila mwanamke asalipo, au anapohutubu, bila kufunika kichwa, yuaaibisha kichwa chake; kwa maana ni sawasawa na yule aliyenyolewa. Maana mwanamke asipofunikwa na akatwe nywele. Au ikiwa ni aibu mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa, na afunikwe”, Wasabato wameondoka na tafsiri ya kuwanyoa nywele wanawake, sasa kuna tofauti gani na wewe uliyepata ufunuo kwamba hilo vazi la huyo binti ndio mambo hayo mapya yaliyonenwa na Isaya?!!!

  Kwa taarifa yako mimi sina shida yoyote na wanawake, nawapenda sana, ninaamini maisha bila ya hao yatasinyaa sana, hata Mungu alililona hilo, ndipo ninamshukuru kwa ajili yao tangu aliponipa ufahamu huu. Hii ndiyo sababu pekee inayonifanya niendelee kuandika kuyapinga haya mafundisho yako yaliyopotoka, na yenye kufisha. Naifahamu tabu wanayoipata wahubiri wa sampuli yako wenye kuchanganya Neno la Mungu na Tamaduni zao, hao watoto wa Kish wanaozishikilia mimbara nyingi, ni vigumu kwao kulielewa Neno la Mungu linachohitaji, kwahiyo wanaendelea ktk upotofu huku wakiamini kwamba wako sahihi, hii ndio balaa yenyewe, hawasahihishiki!!!

  Kuhusu Binti Jakes sijamshambulia, nilikuambia ni peer pressure inayowasumbua vijana, ambayo mapepo huitumia kuwadaka. Nikakuonesha na “Cult” inayowashikilia, inaitwa “Rebel Society”, na pia zile picha mbili, mojawapo amevaa modestly, lakini naona ufahamu wako umefungwa, una macho lakini huoni!!!

  Asante kwa leo,

  Gbu!

 4. Sungura,

  Hahahahahaha…… unachemka sana kaka!!!
  Tafsiri ya maneno niliyokuletea ni ya kikamusi, kwahiyo nakushangaa unapoikataa! Pia, elewa kwamba Kristo na mitume wake hawakuwa wanaongea Kiyunani, licha ya lugha hiyo kutumika ktk uandishi wa Biblia, lugha ya asili ya Biblia, kama Neno la Mungu, itabakia kuwa Kiebrania na si Kiyunani kama ulivyoaminishwa!

  Jambo jingine la msingi kuhusu lugha, jitahidi ujifikishe ktk kuyaamini unayoyakiri, usiwe mtu wa kukaririshwa mambo pasi ufahamu; Mungu amekupatia RM ili akuongoze, akutie ktk kweli yote, haijalishi ni lugha gani, kwahiyo unaponiambia eti nikatafute Biblia ya Kiyunani ndio nijue maana ya “uzuri”, basi huyo RM ana kazi gani, na pia kipawa cha lugha, kina kazi gani? Ni cha “kushandarize” tu?!!

  Unachemka saana ndg yangu; yaani kumbe huijui hata kasoro ya mke wa Potifa??!! Au uliuokota tu huo mfano pasi kujua kisa cha huo “uzuri” wa Yusufu kilikuwaje? Hiki hapa kisa cha “mtakatifu mke wa Potifa”!!! Mwa 39:11-20
  Mzinzi:
  “Ikawa, siku moja, akaingia nyumbani atende kazi yake, wala hapakuwa na mtu katika watu wa nyumbani humo ndani; huyo mwanamke akamshika nguo zake, akisema, Lala nami. Yusufu akaiacha nguo yake mkononi mwake, akakimbia, akatoka nje.”
  Tazama alivyo muongo:
  “… Ameingia kwangu, ili alale nami, nikalia kwa sauti kuu. Ikawa, aliposikia ya kuwa nimepaza sauti yangu na kulia, aliiacha nguo yake kwangu, akakimbia, akatoka nje.
  Haya huyu hapa muuaji:
  Basi akaiweka ile nguo kwake hata bwana wake aje nyumbani. Naye akamwambia kama maneno hayo, … Bwana wake akamtwaa Yusufu, akamtia gerezani, mahali walipofungwa wafungwa wa mfalme, naye akawamo humo gerezani.”
  Huyu mwanamke ni mzinzi, muongo, na ni muuaji na wala hajui kabisa kwamba kuna Mungu; vinginevyo basi kauli ya Yusufu ingemrudisha ktk hofu ya Mungu:
  “…wala hakunizuilia kitu cho chote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe. Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu?”
  Je, kutokuiona kwako kasoro yake si uthibitisho kwamba wewe nawe pia una kasoro?!! Au basi Yusufu aliyekataa kulala naye ndiye mwenye kasoro! Au Biblia yako ya Kiyunani inasemaje??? Mimi naona wewe ndiye mwenye kasoro kiasi kwamba hata hujui tunaongelea nini na katika kipimo gani?!!!

  Ngoja nikuokotee na mifano mingine labda itakusaidia kuujua Moyo wa Mungu katika jambo la “Kutamani Kulala …” Mtazame Ibrahim. Yeye ni nabii, na kwa huyu mambo ya ulimwengu wa roho hufunuliwa kwake, ndipo ilifunuliwa kwake jinsi mkewe atakavyotamaniwa huko Misri, soma hapa ujiondoe ktk vifungo vya tafsiri zisizo na tija, Mw 12:10-12 – ule unabii:
  “Basi kulikuwa njaa katika nchi ile; Abramu akashuka Misri, akae huko kwa muda maana njaa ilikuwa nzito katika nchi. Ikawa alipokuwa karibu kuingia Misri, akamwambia Sarai mkewe, Tazama, najua ya kuwa u mwanamke mzuri wa uso; basi itakuwa, Wamisri watakapokuona watasema, Huyu ni mkewe; kisha wataniua mimi na wewe watakuacha hai.”

  Tazama lilivyotimia jambo hilo, 14-15:
  “Basi ikawa Abramu alipofika Misri, Wamisri wakamwona huyo mwanamke ya kwamba yeye ni mzuri sana. Wakuu wa Farao wakamwona, nao wakamsifu kwa Farao; basi yule mwanamke akachukuliwa nyumbani mwa Farao.”

  Tena alipofika huko Gerari, mfalme wa huko naye akamtamani Sara, Mwa 20:2 “… Basi Abimeleki mfalme wa Gerari akapeleka watu akamtwaa Sara.”

  Huku ndiko kutamaniwa mwanamke Biblia inakokufundisha. Suala la mimi kuwa mwanamke ndio niijue tamaa yao, ni wazo finyu, aliyewaumba ndiye anayewajua zaidi, tumsikilize huyo! Lakini pia napenda kukuhakikishia kwamba sampuli ya mke wa Potifa, wako kibao huko duniani, na nadhani hao ndio wanaokuchanganya; madereva kibao wanatembea na wake za mabosi wao, shwari tu!!!!

  Kuhusu kauli ya Yesu, kwamba “Atakaye mtazama mwanamke kwa kumtamani…” iko hivyo ilivyo, ukipenda kujidanganya, yote ni sawa tu, lakini Neno likitoka limetoka ndg yangu, ukipambana nalo ni sawa na jogoo wangu aliyekuwa akipigana na kioo akidhani kuna jogoo mwingine, angefia hapo kama nisingemuondoa!!! Lakini nimelipenda hili uliloniuliza;
  “”Hujawahi kufikiria kwa nini hata kwenye kuoa biblia inasema mtu (mwanaume) atamwacha baba na mamaye ataambatana na mke wake, wakati unajua kabisa si mwanaume aliyekuwa anatoka kwao kwenda kwao na mke wake, bali mwanamke hutoka kwao na kwenda kwao na mumuewe?!!!””
  Hebu nifafanulie zaidi, napenda kujifunza hili jambo!

  Angalia Biblia yako ya Kiyunani inavyokupotosha nakunukuu:
  “”Kingine ulichopotosha hiki hapa Mwa 3:16c – Na tamaa yako itakuwa kwa mkeo, naye atakutawala!!”” Hili sijui umelitoa wapi!!

  Lakini kuhusu “…na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala” haya ni mambo mawili yaliyo ktk fungu moja, la kwanza linazaa la pili. Wanaume wote waliolibadili jambo hili, hao ma “gigolo”, wameishia kutawaliwa na wake zao!!! Debate inayoendelea ni nzuri, wakiiendea kwa Uaminfu wa Neno la Mungu, watakielewa hicho kilichonenwa hapo, otherwise ndio kama hivyo, tafsiri ya tamaa ya kumtawala mume ni wazo linalotokana na perversion ambayo ndio hao wanawake wanaowatawala waume zao, au wanaoihamisha tamaa yao kuipeleka kwa wanaume wengine, kwani spiritually wanakuwa wamejiondoa ktk kutawaliwa na waume zao kulikoagizwa!!!

  Jaribu kuyaamini Maandiko ktk urahisi wake!!!

  Nitayamalizia yaliyobakia……

 5. Lwembe,
  Najibu comment yako ya mwisho sasa!

  Kwanza kabisa nashukuru umekubali kuwa wewe umetolewa duniani, na dunia tunayoiongelea hapa ni ile ya mambo ya zinaa, na ngono, na ufuska!
  Umekuwa ikinipa shida sana na mtazamo wako kuhusu mwili wa mwanamke, maana umekuwa ukilazimishi hata vitu ambavyo wengine twaviona vya kawaida wewe unasema ni vitu nyeti!

  Hata hivyo, siwezi kukukubalia uwe mwalimu wangu Lwembe, maana utanijaza mtazamo hasi hata kwa viungo ambavyo kwa asili havihusiki na kuamsha hisia ya mwili, ispokuwa kwa mtu ambaye amevihuisha viwe hai katika hilo eneo ili vimpe mwanya mpana zaidi wa kumtamani mwanamke.

  Usijaribu kunifundisha uzoefu ambao umefundishwa na dunia huku ikidhani unanifundisha kweli ya Mungu. Unataka kunifundisha ‘your own weekness, ili kunitia unajisi nami nianze kuuona mwili wa mwanamke kama unavyouona.
  Badala ya kutaka kunifundisha mimi hayo, fanya zoezi mahususi la kuy-undo hayo toka kwenye kichwa chako ili uwe salama moyoni mwako.

  Nakataa kama nilivyowakatalia shuleni wale waliotaka kunilazimsha niyaone maneno ‘nyuma, na ‘ingiza’ kuwa yana maana nyingine zaidi ya hiyo ya kawaida.

  Watu mlijifunza sana kuhusu nafasi ya kila kiungo cha mwanamke katika kusisimua tamaa ya mwili, matokeo yake mmjikuta mnaona karibu 90% ya viungo vya mwili wa mwanamke vinahusika na sex, hapo lazima mpate shida kubwa, hasa katika kizazi hiki.

  Maziwa ya mwanamke ni kwa ajili ya kunyonyesha ntoto, lakini yamegeuzwa kuwa kiungo muhimu for sex, hips (nyonga) kwa mwanamke ni kwa ajili ya kusudi zima la kutengeneza njia ya mtoto kuzaliwa, zimefanywa kuwa kivutio cha sex, n.k

  Mbona wanawake kibao tu huwa wananyonyesha watoto wao maziwa nje, huwa mkiyaona huwa yanawasisimua pia?

  Halafu Lwembe, kama kweli ulichokisema hapa ni cha kweli, basi au hujui unachokisema, ama hisia zako zimevuka katika kiwango cha kusisimuliwa na sehemu nyeti ya mwili wa mwanamke.
  Ona ulichosema; ” kwa kifupi kiwiliwili, ndicho kinachohusika na kuiamsha tamaa ya kulala na mwanamke; hiyo ndiyo sehemu inayopaswa isitiriwe.”

  Sasa kwa kuwa kiwiliwili ndo sehemu nyeti inaypoaswa kusitiriwa, mapaja siyo sehemu ya kiwiliwili. Sasa sijui kwa nini mnamshambulia biti Jakes hiyo nguo abayo imefunika kiwiliwili chote!

  Lwembe najua vizuri kuhusu mwili wa mwanamke (woman anatomy), kinachotakiwa kufanyika ni kujiweza ili uamue nwenyewe kuwaza nini wakati gani, kusisimuliwa na nini wakati gani.
  Maana bila kujiweza, kuna mtu mwingine atakuja kukufundisha jinsi ya kuutafsiri mwili wa mwanamke, na matokeo yake ni kujikuta unamfanya mwanamke kuwa mtumwa wa mavazi kwa sababu ya udhaifu wako!

  Tena wewe Lwembe, angalao mpka uone paja na robo ya titi likiwa wazi ndipo usisimke, kuna wengine nilikwambiieni wamejiachia kupelekeshwa kiasi cha kusisimka hata wakiona tu bikini imeanikwa au imening’inizwa dukani.

  Kwani wewe hujaona kuna mtu mmoja humu alisema kwake hata kwapa la mwanamke ni shidaaaa!! Ivi unafikiri mtu kama huyo anaishije sasa mjini, maana karibu 80% ya wanawake huvaa mavazi yenye kuacha makwapa nje!

  Sijui ni nani aliyemfundisha huo unyeti anaouona kwenye makwapa, duh jamani!!!!

  Leo wewe ndo umeniambia kuwa kuna cinema ya akina Habili, sijawahi hata kuiona,. Kwa hiyo siongei nikiwa na picha yoyote ya cinema. Wewe ndo unaongea ukiwa na picha ya ma- striptease, na ma-dadapoa, inakupa shida sana. Ya- undo hayo madude!

  Lwembe wewe umetembea dunia yote na kugundua kuwa hakuna nchi ambapo makahaba huvaa mavazi ya gubigubi?
  Hebu fanya tena study yako hiyo uone kama utakuja na findings hizo ulizozisema hapo juu kuwa hakuna nchi makahaba huvaa gubigubi!

  Unaweza ukaenda kufanya reasearch hata hapa Zanzibar tu, uone kama utakuta kahaba yeyote amevaa kinguo kifupi!

  Haya ngoja nami nikomee hapa leo!

  Unarikiwe.

 6. Lwembe rafiki yangu,

  Ukweli ni kwamba wewe umeishiwa utetezi wa kile unachokitetea, umepotoka katika vitu vingi sana kwenye hizi comments zako mbili za mwisho. Unataka kuibishia mpaka biblia ambayo imekuthibitishia kuwa mwanamke naye anaweza akamtamani mwanaume ( Mke wa Potifa na Yusuf), kwa kusema kuwa mke wa Potifa alikuwa na pepo tu, vipi na Daudi alipokuwa anamtamani mke Uria alikuwa na nini ?.
  Acha nikuoneshe upotofu wako:

  Ulipotoa mfano wa Daudi na Bath-sheba, bila shaka ulikuwa umeshau kuwa kuna mfano wa mwanamke ( mke wa Potifa). Kwa hiyo nilipkukumbusha huo mfano umepata shida sana ya jinsi ya kupiga kona ili uweze kusawazisha jambo hilo. Na bahati mbaya sana umekwama kabisa kulisawazisha ili kukubali ukweli kwamba mwanamke nae humtamani mwanaume.

  Umeamua kwenda kuokota tafsiri za maana ya uzuri wa mwanamke na mwanaume, ambazo kimsingi si za kibiblia kwa maana ya lugha ya asili ya biblia. Ulitakiwa uende kwa wayunani na waebrania wakuambie biblia iliposema Bathsheba alikuwa mzuri wa uso walikuwa wanaangalia vigezo gani, na iliposema Daudi, Yusuf, Sauli walikuwa wazuri walikuwa wanaangalia vigezo gani, ndipo baada ya hapo sasa uje na hitimisho!

  Cha ajabu umeamua kusema ati mke wa Potifa alikuwa ni mwanamke mwenye kasoro. Kasoro hiyo huwezi kuithibitisha Lwembe kwenye biblia.
  Kubali tu ukweli kwamba biblia imekufundisha kitu cha kisaikolojia ambacho ulikuwa hukijui, kwamba mwanamke naye anaweza kumtamani mwanaume.
  Wewe si mwanamke Lwembe, hisia za kike huna, hebu waulize wanawake wakwambie kama huwa hawawezi kumtamani mtu kwa kmumuona.
  Usikariri tu alichokwambi amwalimu wako wa Bilogy kuwa mwanamke hutamni kwa kugusana na mwanaume kwa kuona.

  Lakini pia nimekuona jinsi usivyoutambua msingi wa mwanaume kuwa ‘subject; zaidi na mwanamke kuwa ‘object; mara nyingi katika mfumo wa lugha ya biblia.
  Biblia ukikuta imesema ‘mtu’ mara nyingi kama si zote ni mwanaume.
  Muktadha wa wanawake kutokujumlishwa katika hesabu pale suala la kuhesabiwa lilipofanyika katika biblia (mfano kwenye muujiza wa vipande vya nkate na samaki kulisha watu elfu tano), ndio huohuo uliotumika kwa Yesu kusema kila mwanaume (subject)amtazamaye mwanamke (object) kwa kumtamani amekwisha zini naye….

  Yesu hakusema hayo maneno ati kwa sababu ambaye huwa anatamani ni mwanaume wala si mwanamke. Hujawahi kufikiria kwa nini hata kwenye kuoa biblia inasema mtu (mwanaume) atamwacha baba na mamaye ataambatana na mke wake, wakati unajua kabisa si mwanaume aliyekuwa anatoka kwao kwenda kwao na mke wake, bali mwanamke hutoka kwao na kwenda kwao na mumuewe?!!!

  Kingine ulichopotosha hiki hapa Mwa 3:16c – Na tamaa yako itakuwa kwa mkeo, naye atakutawala!!
  Lwembe wewe una command nzuri ya Kiingereza kuliko mimi( Mungu akubariki kwa hilo), lakini ulichokitafsiri hapa sijui kwa nini uligeuka ukawa kipofu mkubwa.
  Ona ulichosema: ” na tamaa yako itakuwa kwa mumeo”], yaani imekuwa contained hapo, hairandi randi ovyo!” ( Hapa umeweka ufafanuzi wa kibabaishaji rafiki yangu)

  Lwembe nakuruhusu usome tena na tena na utafute tafsiri za asili pia, utagundua kuwa tamaa inayosemwa hapo si ya mahaba kama unavyofikiri. Hapo kinachosemwa ni tamaa ya madaraka (position), ndio maana neno linafuata hapo ni kiutawala (naye atakutawala) -(Bado hapo kuna debate kubwa inaendelea kwa wasomi mbalimbali wa biblia)

  Lakini hata kama ingekuwa ni tamaa ya mwili (mahaba) bado imesema mwanamke ndo atamtamani mwanaume.

  Kwa hiyo concept yako ya alichokuwa anakisema Yesu katika Mt 5:28, kwamaba ati mwanaume ndo kaumbiwa kumtamani mwanamke, haiko sahihi!

  Angalia vizuri!!

 7. Sungura,

  Nikiliacha hilo la mke wa Potifa, ngoja tuyatazame haya mengine uliyoyaandika, maana picha ninayoipata kutoka hayo ni ya mtu aliyejichanganya ktk jambo na hivyo kuishia kuongea yasiyoeleweka!

  “”Halafu ni upuuzi bado kuendelea kufafanua jambo kwa kutumia neno ‘kusitiri’ ukimaanisha kuvaa mavazi marefu au yenye kufunika mwili wote, wakati hiyo siyo maana ya kusitiri kwa mantiki ya biblia.””

  Rudia tena kusoma michango yangu, hakuna mahali niliposema kwamba maana ya neno “kusitiri” ni “”kuvaa mavazi marefu au yenye kufunika mwili wote””! Wewe ndiye unayehangaika na hizo nguo ndeeefu!

  Ufahamu wangu kuhusu “kusitiri” nimeuweka wazi, ni ufahamu wa kawaida ya watu waliopevuka ktk Neno la Mungu, yaani hao waliotolewa huko duniani, huko kulikojaa hizo pilika! Ninakinukuu nilichokisema kuhusu “kusitiri” halafu kifananishe na hicho unachodhani kwamba nilikisema mimi:
  “”… maana rahisi ya kusitiri ni kuyazuia macho yasione zaidi ya hapo palipo wazi; unapolivuka goti kuja juu, kwa mwanamke, yaani mapaja hadi kifuani kwenye matiti, ni sehemu inayohusika na viungo nyeti vinavyotumika ktk jambo la kujamiiana, kwa kifupi kiwiliwili, ndicho kinachohusika na kuiamsha tamaa ya kulala na mwanamke; hiyo ndiyo sehemu inayopaswa isitiriwe.
  Mwanamke anapovaa nguo yenye kusitiri, maana yake ni kwamba, kwa makusudi, anaihamisha attention kutoka ktk mwili wake na kuipeleka kwenye hilo vazi; yeye mwanamke ndiye anayelifanya hilo kwa kusudi hilo! “”
  Kuna jambo la “” kuvaa mavazi marefu au yenye kufunika mwili wote”” hapo? Unaona unavyo chemka!!!

  Kwa kuuona kwako mwili wa mwanamke si wa kutamanisha kwa hizo sehemu, kama unavyokiri hapa, “” Wewe unapoona kuwa kuanzia gotini kwenda juu ni shida, elewa kuwa hiyo ni shida kwako, wengine hata hayo maeneo si lolote kwao.
Hiyo ni kasumba inayotokana na makuzi yenu, ndio maana mara nyingi nawaambia kuwa basi mnapokuwa mitaani mnakuwa na shida kubwa ninyi!”” Hili si jambo la kawaida!

  Mimi nimetolewa kutoka duniani, kwahiyo niache niwe mwalimu wako kuhusu mambo ya huko usiyoyajua! Ninapolizungumzia vazi fupi kama la huyo binti, pamoja na mavazi mengine yasiyo na “staha”, nayazungumzia hayo katika ufahamu wa dunia niloupitia, nikiujua mwanzo, huko chumbani yanakovaliwa, mpaka mwisho wake tena, chumbani yanapovuliwa, mzunguko kamili, nia na mafanikio yake!!!! Kwahiyo unaponiambia kuwa kwako wewe mwili wa mwanamke kuanzia magotini kuja huku juu mpaka kifuani, haukusisimui, “”wengine hata hayo maeneo si lolote kwao”, hali yako hii itakuwa inatokana na kukosa kwako ufahamu kuhusu mwili wa mwanamke, huenda ni kwa kule kushushwa kwako kutoka mbinguni huko ambako hakuna kuoa wala kuolewa, au ni Towashi, au una matatizo makubwa zaidi!!!

  Pia naona jambo la Utamaduni limekuvuruga sana kiasi kwamba unatulazimisha tuukubali kama sehemu ya maisha yetu. Nilipozungumzia wanawake kukuza makalio na matiti, nilizungumzia katika ujumla wao na si tamaduni zao; ndio maana unaponiambia kuhusu wachina na wajapani ninakuona ni mtu uliyeikosa mantiki ya tunachokizungumzia! Biblia haifundishi tamaduni za kidunia bali za kimbinguni, ndio huo Ukristo, yaani Upakwa Mafuta!

  Halafu unaniambia,
  “”Na labda sasa ningependa ufikirie upya, lengo la wanawake wakristo kuagizwa kuvaa nguo zinazokubalika lilikuwa ni nini, je ili wasitamaniwe? Kwa nini wanaume wakristo pia Paul hawaambii wajihadhari kutamani wanawake wa nje ambao wanavaa nguo zisizofaa walioko huko nje ya kanisa?””

  Mimi sioni jambo la kulifikiria upya kwa sababu nimelielewa vizuri Agizo la mt. Paulo, limetolewa kukidhi hiyo Amri Mpya ktk Mt 5:28, kuhusu Uzinzi. Wazo lako kwamba kwanini Paulo hawatahadharishi wanaume wakristo kuhusu kutamani wanawake wa nje ya kanisa wanaovaa kama huyo binti, ni irrelevant kutokana na kwamba onyo hilo ndilo hilo hapo ktk Mt 5:28; and God is not given to vain repetitions!

  Kuhusu “vazi la majani” kama nilivyokuambia, ni sawa na utamaduni, kwamba viko nje ya Neno la Mungu, kwahiyo havifai! kama hilo vazi lingekuwa ndani ya Neno la Mungu, kwanini aliwatengenea vazi jingine? It is that simple! Ila naona wewe ukipelekwa Umang’atini ukahudumu huko labda kwa miaka miwili, si ajabu ukaturudia mjini ukiwa umevaa vile vingozi vya “kuficha”!!!

  Na kuhusu urefu wa vazi la akina Adamu, usiwe mgumu wa kuelewa mambo; mtume Paulo hajawahi kuwa na Injili yake binafsi bali aliyopewa na Kristo kutuletea. Kwahiyo hilo Agizo la mavazi si lake binafsi bali ni la Yule aliyewavisha lile vazi la ngozi huko Mwanzo na sasa akiwavisha tena! Ukilijua vazi analolifundisha Paulo, basi umelijua na hilo walilovaa akina Adamu urefu wake; kama ni hicho kimini, ndio hivyo tena, picha za sinema ya akina Habili zitakuwa zingali kichwani mwako!!!!

  Pia kuchanganya muonekano ninakokuzungumzia, ni ule muonekano wa wazi. Hakuna sehemu duniani wanakojiuza wanawake halafu wawe wamevaa gubigubi! Ukimuona malaya amevaa gubigubi basi jua anaogopa polisi, lakini kwa hulka lazima atembee nusu uchi, na biashara inapokuwa ngumu, ikilazimu, huwaga wanachomoka uchi wa nyama usiku wa giza, taa za gari zikiwamulika, na hivyo kuwavuta wateja! Haya kaka ndio mambo ya huku duniani tunakoishi, wewe shukuru unaishi kwenye ma convent!!!

  kwaleo ngoja nikomee hapa, hayo maelezo yako mengine nitayarejea panapo wasaa!

 8. Sungura,

  Nimefurahi kwa mfano wako mzuri wa mke wa Potifa! Ni changamoto nzuri ya Injili inayoweza kukupa fursa ya kuyatafakari hayo ili kuuona Moyo wa Mungu ulikolalia hapo unapowaweka ktk mizani, Daudi kwa upande mmoja na mke wa Potifa kwa upande mwingine!

  Nikiichukua tafsiri ya ESV, ambayo nadhani ndiyo uliyoitumia, Maandiko yanasema Yusufu alikuwa mzuri wa sura (handsome), na mke wa Potifa alimtamani. Pia kuhusu Bath-sheba, huyo mwanamke aliyetamaniwa ni Daudi, Maandiko yanasema, “… naye huyo mwanamke alikuwa mzuri sana (very beautiful), wa kupendeza macho.” (‭2 SAM.‬ ‭11‬:‭2‬)

  Tukitaka kuipima tamaa iliyowafika Daudi na mke wa Potifa ktk kipimo cha huo “uzuri”, ukiwa ndicho kisababishi, basi itatulazimu kuirejea sifa hiyo ya “uzuri” ili tuione kama ni moja, yaani, Je, kiwango ni kimoja kulingana na maumbile?

  “Uzuri” wa mwanaume hukomea ktk kiwango cha “handsome”, lakini “Uzuri” wa mwanamke hukipita kiwango hicho!
  • Handsome:- (of a man) good-looking.
  (of a woman) striking and imposing rather than conventionally pretty.
  • Pretty:- (of a person, especially a woman or child) attractive in a delicate way without being truly beautiful
  • Beautiful:- [ mass noun ] a combination of qualities, such as shape, colour, or form, that pleases the aesthetic senses, especially the sight: I was struck by her beauty

  Basi, kwa kadiri tulivyolitazama jambo hili la “uzuri”, kipimo hiki ndicho kinachoidhihirisha tofauti ya maumbile, kwamba mwanamke ni mwenye kupendeza zaidi kuliko mwanaume, na hivyo kuvutia zaidi, kwa asili, na ndio maana mwanaume anaonywa kuhusu “kumtazama mwanamke kwa kumtamani”; hili pekee lilipaswa likuonesha kwamba, likiwa limekwisha kunenwa hivyo, basi limekwisha kuumbika hivyo, maana Kristo ndiye Neno liumbalo, ndipo ukimuona mwanamke anamtazama mwanaume kwa kumtamani, jua kwamba huyo amekumbwa na pepo kama la mke wa Potifa!

  Pia ukiitazama nature, ile asili, ndani yake yako mambo mengi sana ya kujifunza. Maandiko yanatuambia kwamba tamaa ya mwanamke imewekwa kwa mumewe, [Mwa 3:16 “… na tamaa yako itakuwa kwa mumeo”], yaani imekuwa contained hapo, hairandi randi ovyo! Ndio maana wanawake wanaweza kuolewa hata hamsini kwa mume mmoja na wakatulia hapo bila tatizo lolote, ilmradi wametongozwa na mwanaume huyo! Lakini, mwanamke aliyeolewa, akiihamisha tamaa yake kwenda kwa mwanaume mwingine mbali na mumewe, basi jua wazi kwamba mwanamke huyo ana kasoro, kama huyo mke wa Potifa! Kwahiyo kutoka tabia yenye mushkeli ya mwanamke huyu, hauwezi ukaifanya kuwa ndicho kipimo cha “uzuri” wa mwanaume kuwa sawa na wa mwanamke ktk jambo la kuiamsha tamaa!

  Ukiamuacha Yusufu, Maandiko yanasema Sauli pia alikuwa mzuri, “…. Sauli, kijana, tena mzuri; wala katika wana wa Israeli hakuwako mtu mzuri kuliko yeye; tangu mabega yake kwenda juu alikuwa mrefu kuliko watu wote.” (‭1 SAM.‬ ‭9‬:‭2‬) Kutoka “uzuri” huo wa Sauli, hatujaona tukio lolote linalo shabihiana na la mke wa Potifa. Basi “uzuri” wa mwanaume kwa asili hauiamshi tamaa ndani ya mwanamke ya kutaka kulala na huyo mwanaume; ni kinyume cha maumbile kwa mwanamke kumuinukia mwanaume! Kama hulijui hili la kwamba mwanamke ndiye ambaye hutamaniwa ili kulala naye, basi utakuwa ni mtu wa ajabu sana, au una tatizo kubwa sana!!

  Katika tamaduni nyingi sana wanaume ndio huoa wake wengi, na kumilki mahawara wengi ili kukidhi matamanio yao kwa hao wanawake. Lakini sijaona wanawake wanaoolewa na wanaume wengi; yaani mwanamke mmoja awe na waume halali hata wawili tu! Nalo jambo la kuoa au kuolewa likiwa ni kupenda kunakotokana na kupendeza, basi ndio kusema mwanaume ndiye ambaye hupendezwa na wanawake wengi hao na kuwa na tamaa juu yao na hivyo kuwaoa ili wawe karibu yake aendelee kuipata hiyo starehe ya kuwaona huo uzuri walionao!

  Hii ndio tafakari niliyoipata kutoka jambo hilo la Yusufu na mke wa Potifa, ktk reflection ya Andiko la Mt 5:28!!!

  Nakushukuru kwa changamoto,
  karibu sana, &
  Gbu!

 9. Lwembe,

  Ningependa uache kuniona kupitia ufahamu wako wa mambo, mimi siyo wewe. wewe siyo mwalimu wangu. Acha wewe uendelee kuona kama unavyoona na mimi kama ninavyoona, then mjadala uendelee.

  Hapa nakunukuu “Jaribu pia kuwa msikivu, kuvaa mavazi ya kimalaya hayakufanyi uwe malaya ingawa unasomeka hivyo na dunia iliyoyabuni hayo mavazi ya kimalaya; Au kuvaa ghubighubi hakukufanyi kuwa mtakatifu kama wewe mwenyewe unavyokiri! Umalaya ni wa rohoni au utumwa, haijalishi umevaa nguo gani! Kwani hao makasisi wanaolawiti wenzao, unadhani wanavaaga nguo gani barabarani, chupi au boxers? Wanavaa robes na misalaba mikubwa!! Au wachungaji wanaotembea na wake za watu, wanavaaga sketi? Wanavaa vizuri sana na zile kola nyeupe zenye mithiri ya utakatifu!! ”

  Lwembe kama hili unalifahamu vema, kwa nini mnalaumu huyo binti wa Jakes, kawakwaza nini? Na je hayo aliyovaa ni mavazi ya malaya, ni malaya wa wapi huyo? maana malaya huvaa kulingana na utamaduni wa jamii husika pia?

  Na hapa nakunukuu ”Biblia inachotufundisha ni kuepuka kuchanganya muonekano, ukivaa ovyo kama huyo binti popote pale walipo wanaume, wawe wameokoka au la, wote watakupigia hesabu, kama ni watakatifu watazigeuza shingo zao na kumsikitikia huyo anayejiwakilisha kimalaya maana wanajua kwamba hana Nanga! ”

  Aha, kumbe biblia inachotufundisha ni kuepuka kuchanganya muonekano, maana yake ni kati ya muonekano wa kahaba na mcha Mungu. Ukisema muonekano unaongelea utamaduni Lwembe. Hivyo biblia inapoongelea vazi la kukubalika haiongelei urefu wake, ufupi wake, kubana kwake au kupwaya kwake, bali inaongelei kujitofautisha kikutafsirika na jamii.

  Kwamba kama vazi la kikahaba wa sehemu fulani lingekuwa ni refu mpaka miguuni, basi tungewataka wanawake wakristo wa sehemu hiyo wavai vazi lisilo refu.

  Kumbe huu ukweli unaulewa halafu tunapotezeana tu muda hapa – acha huo unafiki Lwembe.

  Siyo kila kitambulisho cha kahaba ni vazi fupi, na juvaa mavazi yanakubalika si tu kwa ajili ya masuala ya kujitofautisha na makahaba, lakini hata kama kungekuw na wapunga pepo wanawake wenye kuva aina fulani ya mavazi (hata kama ni marefu na shela kichwani), Paul angewashauri wanawake wakristo kutovaa mavazi hayo ili kuweka tofauti.

  Halafu Lwembe hebu acha pia tabia ya kumhusisha mtu na cult just kwa vile amesema kitu ambacho ni tofauti na cha kwako usichokielewa.

  Niliposema kuwa Mungu hajakoma kufanya mambo mapya umenifananisha na cult, na ninakuelewa unachomaanisha. Lakini unatakiwa kwanza ujiulize ni nini kinachosemwa kilikamilika kwenye hiyo Mwanzo 2:1-.

  Lakini wewe nawe ufahamu wako ni mdogo tu kama mtu yeyote asiyejua sawasawa kuhusu Mungu lakini yeye anadhani kuwa anajua. Ni sawa tu anayedhani maana ya Yesu kuwa yeye yule jana,leo na milele ni kwamba amejilimit.

  Bsi isaya nae alikuwa cult kama mimi, maana naye anasema kuhusu Mungu kufanya jambo jipya (Isaya 43: 19)

  Lwembe unaongea sana kuhusu ‘striptease’ vipi huwa unahudhuria huko au hapo zamani ulikuwa huko na hivyo akili yako bado inawaza huko.
  Please usijaribu kufikiri kuwa wote tuko hivyo, huo ni udhaifu wako tu. Ni vema ukaushughulikia mwenyewe kuliko kumfanaya kila mwanaume awwze kama wewe. Jiweze mwenyewe!

  Wewe ndo umetekwa na dunia, all what u think is striptease, hayo ndo yamekujaa, unachoona kwa mwanamke kwanza ni uhusika wake na ngono. Na unadhani kila mwanaume anamwona mwanamke hivyo. Yawezekana hapo zamani ulikuwa huko hivyo ufahamu wko bado umejawa na hayo.

  Badilishwa nia yako kuhusu mwanamke na mwili wa mwanamke, mwone mwanamke kama kristo anavyomwona.

  Lwembe wewe una shida kuhusu wanawake, maana kila mjadala unaogusia mwili wa mwanamke huwa nakuona jinsi amabyo mwili wake unakupa shida. Inaonekana unashida juu ya makalio ya mwanamke, unashida juu ya mapaja ya mwanamke, unashida juu ya maziwa ya mwanamke, n.k

  Badilika!!

 10. Hahaa, Lwembe,

  Kuna mambo huwa unaongea ambayo ni ya kufikirika zaidi, na ni mazwazo tu ya mtu ambayo hata huwezi kuyathibitisha.

  Unaponimbia kuwa Daudi alimtamani mke wa Uria kama kithibitisho kuwa mwanaume anamtamani mwanamke, ni mawazo mepesi sana, vipi nami nikuambia kuwa mke wa Potifa alimtama Yusuf hapo utaleta longolongo gani tena ili uendelee kuisimamia hiyo falsafa?

  Halafu ni upuuza bado kuendelea kufafanua jambo kwa kutumia neno ‘kusitiri’ ukimaanisha kuvaa mavazi marefu au yenye kufunika mwili wote, wakati hiyo siyo maana ya kusitiri kwa mantiki ya biblia. Acheni kutafsiri mawazo yenu mkidhani mnatafsiri neno la Mungu.

  Jifunze kujiweza mwenuewe, siyo kuweka kongwa kwa wanawake kwa sababu ya udhaifu wako mwenyewe. Wewe unapoona kuwa kuanzia gotini kwenda juu ni shida, elewa kuwa hiyo ni shida kwako, wengine hata hayo maeneo si lolote kwao.
  Hiyo ni kasumba inayotokana na makuzi yenu, ndio maana mara nyingi nawaambia kuwa basi mnapokuwa mitaani mnakuwa na shida kubwa ninyi!

  Vazi linaweza kuvuta ‘lusting sprits katika jamii yenye kasumba hiyo. Jiukize na wewe ni jmii ipi ya watu ambayo wanawake wake wana hiyo tabia ya kukuza makalio. Ni wazungu wangapi au wachina wangapi ulishawahi kuwaona wamaekuza makalio?

  Ivi unafikiri kuwa mwanamke mwenye makalio makubwa ni kivutio kwa mchina au mjapani? Hiyo kasumba kwao haipo, ipo kwa waafrika ( ni utamaduni – kasumba)

  Na labda sasa ningependa ufikirie upya, lengo la wanawake wakristo kuagizwa kuvaa nguo zinazokubalika lilikuwa ni nini, je ili wasitamaniwe? Kwa nini wanaume wakristo pia Paul hawaambii wajihadhari kutamani wanawake wa nje ambao wanavaa nguo zisizofaa walioko huko nje ya kanisa?

  Halafu acha kuniambia kuwa upeo wangu haukufikia kujua kuwa hata pamba inyotengenezwa nguo ni vazi la majani, huko ningekufikisha tu!

  Ni udanganyifu mwingine wa kitafsiri kutuambia kuwa vazi la majani kwa Adam na Eva ni sawa na utamaduni ulio nje ya neno la Mungu. Lile lilikuwa vazi wala usitudanganye
  Naona unajribu kukwepa kujibu swali langu la urfu wa vazi la Adam na Eva ulikuwaje.

  Inawezekana kweli sijui vazi walilokuwa wamevaa kabla ya kula tunda , hebu mwenzangu nambie lilikuwa likoje hilo vazi?

  P.T.O

 11. Sungura

  Pia, kuhusu “vazi la majani”; ni vizuri ukatambua kuwa utamaduni wowote ule ulio nje ya Neno la Mungu ni “vazi la majani”. Kwa bahati mbaya, upeo wako kuhusu “vazi la majani”, naona haukufikia kujua kuwa hata pamba inayotengenezewa nguo ni zao la miti, kwahiyo kufikiri kwamba hilo vazi halidumu ni kuikosa maana ya fumbo la mavazi, ndio maana unaniuliza, “”Nguo ya ngozi waliyopewa akina Adamu ilikuwa ndefu kuanzia mabegani mpaka kwenye viwiko vya miguu?”” Lakini, kwanza ulipaswa utafute kujua kabla ya huko kuwa uchi kwao, walivishwa nini, ndipo ungeelewa na hiyo ngozi aliyowatengenezea ilikidhi kwa kiwango gani hilo vazi lililowatoka, ambavyo vazi lao la majani halikufaa; maana ili upate ngozi ni lazima achinjwe mnyama, na Biblia inatuambia “… Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia” (‭Ufu ‭13‬:‭8‬), panua wigo wa tafakari unapoisoma Biblia yako, maelezo yako mengi kama si yote, ni hayo majani!

  Jaribu pia kuwa msikivu, kuvaa mavazi ya kimalaya hayakufanyi uwe malaya ingawa unasomeka hivyo na dunia iliyoyabuni hayo mavazi ya kimalaya; Au kuvaa ghubighubi hakukufanyi kuwa mtakatifu kama wewe mwenyewe unavyokiri! Umalaya ni wa rohoni au utumwa, haijalishi umevaa nguo gani! Kwani hao makasisi wanaolawiti wenzao, unadhani wanavaaga nguo gani barabarani, chupi au boxers? Wanavaa robes na misalaba mikubwa!! Au wachungaji wanaotembea na wake za watu, wanavaaga sketi? Wanavaa vizuri sana na zile kola nyeupe zenye mithiri ya utakatifu!!

  Biblia inachotufundisha ni kuepuka kuchanganya muonekano, ukivaa ovyo kama huyo binti popote pale walipo wanaume, wawe wameokoka au la, wote watakupigia hesabu, kama ni watakatifu watazigeuza shingo zao na kumsikitikia huyo anayejiwakilisha kimalaya maana wanajua kwamba hana Nanga!

  Unasema, “Mungu hajaacha kufanya vitu vipya!” Hili si kweli, Mungu alikwisha maliza yote kama anavyotangaza ktk Neno lake ktk ile siku ya saba (Mw 2:1-2)!!! Hii kauli ya kwamba kauli yako ndio kiini cha Cults zote duniani, ni uongo wa Ibilisi! Huo ni Mpindo wa kilaghai wa Yn 5:17 inayozungumzia Mungu kuendelea kufanya kazi “… Baba yangu anatenda kazi hata sasa…”, ndipo Ibilisi ameitwist kauli hiyo kumfanya Mungu anaendelea kufanya vitu vipya, na hivyo kupingana na hiyo Mwanzo inayosema, “Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote…”; sasa hivyo vitu vipya anavifanyia wapi? Au ndo hayo yaliyoandikwa nyuma ya Biblia (Ufu 5:1 “Kisha nikaona katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi kitabu kilichoandikwa ndani na nyuma, kimetiwa muhuri saba”), mnayo hayo mambo tayari, ndio hayo mapya?

  Mungu hafanyi vitu vipya, bali anayatimiza yote aliyoyanena ktk Neno lake, anazikamilisha Ahadi zake, ndiko huko “kutenda kazi” anakokusema Kristo! Kama kupitia Isaya alisema, “Atazaliwa mtoto”, ndiye huyo Kristo, na Ahadi nyingine zote mpaka mpaka Hukumu na Moto!!!

  Kama nilivyokuambia, hakuna jambo lisilo na kusudi, hata kuvaa pia. Mungu akiisha kukupa mwongozo, hakulazimishi kuufuata huo. Katika uasi wako unaweza ukajiridhisha na chochote kile, unaweza ukajihalalishia vazi kama la huyo binti tunalolijadili hapa (hatumjadili binti, bali vazi), kwa ujinga ukasema ni la kitakatifu! Nasema kwa ujinga ili tu Mungu asilihesabie jambo hili kwamba hicho ndicho unachokikiri, kwani hata huyo binti katika siku ya Hukumu ni wazi kwamba atasimama dhidi yako, sijui kama utamuelewa kweli, nakuona utakavyomtolea macho!!!

  Nilikuambia kwamba huo utamaduni unaoupigania ni wa kishenzi, ni mapepo yanayowavagaa watoto yakiwaingiza ktk ule utamaduni unaoulilia wa “striptease”, lakini kwa kujifungia kwako ndani upeo wa ufahamu mdogo ulionao, ndio husikiagi lolote zaidi ya hilo unalolijua, cocooned in your own little world of understanding!!! Otherwise hebu zikague tena hizo picha mbili uione hiyo striptease wanayoifanya hapo!

  Picha ya chini ndiyo ya kwanza, ukimtazama huyo binti, utamuona amevaa modestly, two inches below the knee; a nice little kid of her age, befitting a saint!

  Picha ya juu, ambayo ndio inapaswa iwe ya pili, Lah! She is a rebel!!! Ameanza kuvua nguo, sijui hatua iliyofuata alikuwaje!!! Umeiona society aliyomo? Inaitwa “The Rebel Society” no wonder hali zao hizo, ni za uasi kama bango la jumuia yao linavyo sema. Kwa mavazi yao hayo yenye kuwapelekea kuwa uchi, hawaiasi dunia, bali Mungu, huyo aliyewavisha vazi jema la kuwasitiri miili na roho zao, lile Neno lake, ni jambo la kusikitisha unapowaona vijana wadogo kama hao wamenaswa ktk mitego ya Ibilisi kama hiyo!

  Je, wa kulaumiwa ni nani, ni hao watoto au wazazi wao au nani haswa? Anayepaswa kubeba lawama hiyo squarely ni wahubiri kama Sungura; wamelegea mikono na kuidhoofisha mimbara, wametekwa na dunia, na mazao ya injili wanayoihubiri ndio hayo makundi; ndio maana nilisema wa kuhurumiwa ni wewe na si hao mabinti, kwa maana Mungu ataidai damu yao kutoka mikononi mwa hao wachungaji!!!

  Karibu sana brother, tuendelee kujadili, wakati mwingine ili kumfikia nduguyo ktk kina anachotumbukia, hulazimu kamba ndefu, ndio hii mikeka!

  Gbu!

 12. Sungura,

  Naona turahisishe mambo!
  Kuhusu swali uliloniuliza jibu lake limo katika swali langu, tena ktk urahisi, maana unapozungumzia nguo, kimantiki huwa unazungumzia jambo la kuwa uchi; kama suala la kuwa uchi halipo basi na jambo la nguo haliwezi kuwapo pia!!!

  Sehemu gani za mwili ndizo zinahusika na huko “kuwa uchi” au “nyeti”, nilikuambia ni “siri iliyowazi.” Kimsingi,”unyeti” wa hizo sehemu unahusu jambo la kujamiiana kwa waliopevuka, ndio maana vijana wakifikia umri wa kubalehe au kuvunja ungo, hapo miili yao inapoingia ktk mabadiliko, hufunzwa jinsi ya kujitunza, pamoja na mavazi kulingana na tamaduni zao, hata hao wamang’ati, kama unavyowaona “wakificha” hizo sehemu nyeti; ni katika mantiki hii ndio nilikuambia kwamba mavazi yanahusiana na jambo la kujamiiiana!

  Jamii ya Kikristo pia inao utamaduni na mila zake, ndizo hizo anazozirejea mtume Paulo kuhusu mavazi akiwafundisha jinsi inavyowapasa kujivika mavazi ya kuisitiri miili yao, akiwaingiza ktk ufahamu kamili wa utakatifu wao; Paulo hazungumzii upuuzi wa beach au disco au mashindano ya mbio za wanawake, hao mnaowadanganya kwa hizo tuzo na vijihela at the expense ya kuiharibu miili yao mpaka ile hali ya uke kuwatoka, misuli imewakakamaa kuliko wabeba zege!

  Hebu itazame nature, ile asili, ujifunze jambo linaloweza kukusaidia ktk tafakari ya hili tunalolizungumzia. Katika viumbe vyote, ni binadamu pekee ndiye aliyeumbwa tofauti; viumbe vingine vyote, dume ndilo lenye kupendeza kuliko jike; lakini kwa binadamu mwanamke ndiye anayependeza! Hauwezi kulibadili hilo, ndio maana Kristo akaonya kuhusu mwanaume atakaye mtazama mwanamke kwa kumtamani, maana huyo ndiye aliyeumbwa kutamaniwa!
  “”Ikawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, akatembea juu ya dari ya jumba la mfalme; na alipokuwa juu ya dari aliona mwanamke anaoga; naye huyo MWANAMKE ALIKUWA MZURI SANA, WA KUPENDEZA MACHO.” (‭2 Sam‬ ‭11‬:‭2‬)
  Hiki ndicho Mungu anachokishuhudia!

  Kama nilivyokuonesha, kwamba mwili wa mwanamke umeumbwa kupendeza, basi kusudi hilo la kupendeza kwake hukamilika ktk kutamaniwa kwake, yaani huko kupendeza kwake kwa asili huiamsha tamaa kama unavyomuona Daudi, hapo alipomuona yule mwanamke akioga! Je, unadhani iwapo angemuona akiwa amevaa nguo kama hiyo unayoisema, yenye kumfunika kuanzia mabega hadi viwiko vya miguu na isiyomchora mwili wake; tamaa yake ingewaka kama ilivyomuwakia alipomuona akiwa uchi? Kiwango cha tamaa kisingefikia hapo kilipofika, kingekuwa chini, na chenye kumilikika!!!

  Hii ndiyo sababu Mungu anawaelekeza mabinti zake kujivika nguo zenye kuisitiri miili yao ili kuwaepusha kuwa kivutio kwa wanaume. Pia elewa kwamba maana rahisi ya kusitiri ni kuyazuia macho yasione zaidi ya hapo palipo wazi; unapolivuka goti kuja juu, kwa mwanamke, yaani mapaja hadi kifuani kwenye matiti, ni sehemu inayohusika na viungo nyeti vinavyotumika ktk jambo la kujamiiana, kwa kifupi kiwiliwili, ndicho kinachohusika na kuiamsha tamaa ya kulala na mwanamke; hiyo ndiyo sehemu inayopaswa isitiriwe.

  Mwanamke anapovaa nguo yenye kusitiri, maana yake ni kwamba, kwa makusudi, anaihamisha attention kutoka ktk mwili wake na kuipeleka kwenye hilo vazi; yeye mwanamke ndiye anayelifanya hilo kwa kusudi hilo!

  Kuvaa kuna “kusudi”. Hivi kwa akili yako, unadhani ni kwa ajili gani wanawake wanatumia madawa ili kukuza matiti na matako yao?!! Unapoyakuza nje ya asili, hayo hugeuka kuwa vazi pia, kulingana na kusudi ambalo ktk hili ni sawa tu na kuziacha wazi sehemu zinazobidi zisitiriwe ili kuwavuta wanaume! Unaona, vazi linaweza kuzivuta “lusting spirits” zikakuvamia na kuyaharibu maisha yako au ukazizuia huko mbali nawe, ukabaki salama!!

  nitaendelea…

 13. Lwembe,

  Hebu jibu kwanza wewe swali langu la muda kitambo: Nguo ya ngozi waliyopewa akina Adamu ilikuwa ndefu kuanzia mabegani mpaka kwenye viwiko vya miguu?

  Halafu hicho unachonitaka mimi nikijibu,wewe na wenzio mnaomlalamikia huyo binti hapo juu ndo mnatakiwa kukijibu, ni nini kilichowakera kwake mpaka mkamwona amevaa mavazi yasiyofaa. Ukikisema hicho utakuwa umejipatia jibu la swali uliloniuliza.

  Unataka rejea gani ya maandiko yanayohusiana na suala la kuwa uchi, kwani jibu la Adamu kwa Mungu, baada ya Mungu kumwita na Adam kujibu kuwa u chi halitoshi kukuonesha kuwa naongelea suala ambalo liko kwenye maandiko? Wewe vipi!!

  Au wewe sehemu ulizosema kuwa akina Adam walizijua kuwa ni nyeti ulikuwa unamaanisha sehemu gani, viganja vya mikono?

  Hata hivyo, jaribu kuelewa kitu hiki kwamba badala ya kutaka kujua kilichosemwa kinasapotiwa na andiko gani, angalia kama kimepingana na andiko lolote ndipo uhitimishe kwa hicho si cha Mungu. Mungu hajaacha kufanya vitu vipya!

  Tuendelee kujadili!

 14. Dah! Sungura,

  Usinilazimishe nifikiri kama wewe! Kwani mawazo yako umeyafungia ndani ya upeo ulionao kuhusu hayo unayoyajua, kwahiyo dunia yako inakomea hapo!

  Unalalamika kuwa nimekupeleka kwenye Torati, sasa, bila Torati, umefikaje kwa Kristo? Umepitia dirishani kama wakristo wengi ninavyowaona?

  Tazama matokeo yake, umekuja na maelezo marefu yaliyojikita juu ya “kuwa uchi” yasiyo na rejea ya Maandiko, na hata ufafanuzi basi, kulingana na elimu yako unayoifundisha, kwamba sehemu fulani ya mwili ndiyo inayohusika na huko kuwa uchi, maana mimi kwa kweli sijui haswa, kuwa uchi, ni kivipi unakuwa uchi!!!

  Au basi utuoneshe katika Maandiko hapo tunapofunzwa kuwa tukiiacha wazi sehemu hiyo ndiyo tunakuwa uchi; ndio maana nilikuuliza, Je, yawezekana kwamba akina Adamu walipojitambua kuwa wako uchi, walifunika viganja vyao vya mikono, au vidole vya miguu yao au nywele, au wakajiziba macho, kwamba ndiko huko kuwa uchi?

  Ukinipatia jibu la maelezo haya, itaturahisishia kujadiliana ktk namna ya kupanuana ufahamu kuhusu kile Mungu anachotutaka kuhusu mavazi, maana ninaamini mavazi yanasehemu ktk kuukamilisha wokovu wetu.

  Mambo mengine uliyoyaandika, nimeyaacha hivyo hivyo, maana naona yanaelea na mawimbi ya dunia, ngoja nilione jibu lako kwanza, huenda yakapotea yenyewe by their irrelevancy!

  Asante!

 15. Lwembe,
  Point yangu kwamba mavazi ni kwa ajili yetu si kwa ajili ya Mungu ilikuwa rahisi, ila nashangaa umeipeleka kwenye torati na sheria.
  Iko hivi, wewe unapokuwa umevaa haina maana umemficha Mungu kuona uchi wako, bali unawaficha wanadamu kukuona uchi wako. Maana kumbuka ukiwa bafuni unaoga Mungu yupo, ukiwa chumbani umelala na pajama tu Mungu yupo anakuona,na ukiwa kwenye suti macho ya Mungu yanakuona mwili wako zaidi ya exray inavyoona. Sasa utamfichaje sasa?
  Na hata masuala ya mavazi yaliyo kwenye sheria kama mambo ya mwanamke kuvaa vazi lakiume na mwanaume la kike kuwa ni chukizo mbele za Bwana, halina maana kwamba huwa tunavaa mavazi ili yatufiche uchi mbele za Mungu. Lina muktadha mwingine tu wa kimamlaka na madaraka kti ya mwanaume na mwanamke.
  Vazi la majani lilificha nini na lile la ngozi lilificha nini ambacho la majani halikuficha? Majibu ya hili swali yatatusaidia kujua kama mantiki ya vazi la ngozi ilikuwa kuficha ambacho la majani lisingeweza kuficha au kama mantiki ya vazi la ngozi ilikuwa ni ubora kinyume na la majani ambalo kufikia kesho yake wangetakiwa kushona mavazi mengine.
  Lwembe unaongea mambo kama mtoto mdogo asiye na ufahamu komavu, unasoma katikati ya mistari lakini huoni kilichobebwa humo. Huoni kwamba hilo vazi la ngozi aliwatengenezea baada ya kuwa ameshakutana nao,keshamhoji Adam, keshamhoji Eva, keshamhoji na nyoka, kwa nini hakuwashonea kwanza hilo vazi kabla hajakutana nao ili lifiche kwanza hicho ambacho vazi la majani unadhani halikuwa limeficha?
  Hebu fikiria brother, ivi huwezi kuingia katika uwepo wa Mungu ukiwa amevaa chupi au boksa? Kama utakuwa unafikiria sawasawa lazima utaniuliza swali ‘chupi au boksa nikiwa wapi’?
  Kuna nini unachokificha na vazi lako mbele za Mungu ambacho unafikiri itakuwa ni aibu Mungu kukiona katika huo mwili wako? Ukipata jibu la hili litakusaidia kurudi kujiuliza nini hasa kiliwafanya Adam na Eva wakimbie uwepo wa Mungu, maana bado walikutana nae kabla hajawapa mavazi ya ngozi.

  Na kitu kingine nafikiri nilishawahi kukiuliza tena, kwamba vazi alilowatengenezea Mungu lilikuwa linafunika kuanzia mabegani mpaka chini ya magoti au?
  Kwa kifupi sijaona uchambuzi wowote uliofanya kuonyesha kuwa vazi linahusiana na ngono.
  Zaidi sana umekiri tu kwamba dunia ndo iliyowafundisheni kuyahusisha mavazi na ngono

  Kwa hiyo Lwembe pale kwapa la mwanamke, kifua cha mwanamke, mapaja ya mwanamke, vinapowapeleka kwenye kutamani unakiri kwamba mmepokea fundisho la dunia, ambalo limewafanya mvione hivyo viuongo kuwa ni zana za kuwapeleka kwenye tama ya ngono? Maana kumbe dunia ndio iliyofundisha watu maeneo ya mwanamke ambayo ni nyeti kwa ajili ya kutamani.

  Kwa kuwa sisi ni chumvi maana yake si kwamba dunia ndio inayotakiwa kutufundisha nini kibaya na nini kizuri, maana si dunia iliyopokea fundisho la kristo, bali ni sisi. Sasa dunia inajuaje kuwa hili ni sawa na lile si sawa mpaka itufundishe sisi? Siyo kutokana na kile biblia imesema ni sawa au si sawa, bali ni kutokana na kile jamii husika inajua kuwa ni kizuri au kibaya, ambapo na sisi ni sehemu ya hiyo jamii. Kuna vingine jamii imesema si sawa lakini ni sawa na vingine ni swa lakini si sawa.
  Wakati niko boarding school kulitokea mtindo wa kubadili asili ya neno kwa matumizi yasiyo ya asili. Mfano: ilifka wakati mtu akitamka neono ‘nyuma’ inakuwa ni shida kubwa, au mtu akisema neno ‘niingizie’ inakuwa taabu, hivyo watu wengi wakawa wanakwepa kuyatumia.
  Mimi nilikakataa, nikawaambia nitayatumia kama ilivyo maana yake ya asili, atakayejikwaa shauri yake, maana mimi siko tayari dunia yenye kubadili jambo jema liwe baya, na baya liwe jema inifundishe matumizi mema ya vitu kuwa matuimizi inayotaka yenyewe.

  Lwembe hakuna sehemu nime-compromise neno la Mungu, ninyi ndo mnataka kuwafanya wanawake kuwa watumwa wa mavazi kwa sababu ya udhaifu wenu.
  Tuliongelea mifano mizuri ya nchi za kiarabu ambako mwanamke huvaa ghubighubi, lakini ufusika uko kiwango cha juu bado. Inategemea tu na nin umei-train akili yako.

  Ni hayo tu!

 16. Sungura,

  Mtazamo wako kuhusu kile dunia inachowafundisha watu, ni sahihi kabisa! Na hilo limewezekana na linaendelea kutokana na Anguko, ambalo limeigubika dunia nzima, jaribu kukisia idadi ya wakristo ktk ulinganishi na dini nyingine pamoja na upagani, tuko wachache sana. Kwahiyo influence ya hilo kundi kubwa, usiidharau, ina nguvu, na ndiyo hiyo dunia!!!

  Na ukitafuta kuidharau dunia, ktk namna ya mafundisho yake, ukajifanya eti hayakuhusu na huku umejivika hayo hayo, hii ni hatari zaidi kuliko ya aliyeyafuata mafundisho hayo akiyajua ni nini! Dunia inapokufundisha kumtamani mwanamke, inakuelekeza kwanza kipi cha kukitamani, halafu ndio inakushusha ktk mpangilio maalumu wa vibwagizo vya hicho central, yaani sehemu mbali mbali za maungo ya mwili wa mwanamke kama ulivyosema, na kukufikisha ktk kilele cha matamanio hayo!

  Kristo alisema, “Siombi uwaondoe duniani”. Basi ni lazima tufahamu pia kwamba kubakizwa kwetu hapa kuna sababu, twapaswa kuwa chumvi kwa dunia. Nayo chumvi ni mwokozi, bali mpaka igusane na hicho chenye kuokolewa, ndiko huko sisi kuwa waraka! Sasa waraka ni maisha yetu, ndipo haijalishi una maneno matamu kiasi gani, ni muhubiri maarufu sana au chochote kile, watu watakuangalia jinsi unavyoishi, na mavazi ni sehemu ya maisha, yanaongea kuhusu familia yako!

  kuhusu Mt 5:28, naweza kuikubali tafakari yako kwamba, kuanzia hapo ilipotolewa hiyo amri mpya, uzinzi unaweza kumhusisha mtu mmoja tu, huyo mwanaume aliyemtazama kwa kumtamani mwanamke aliyejivika vazi linalousitiri mwili wake, modest apparel! Lakini iwapo mwanamke, kwa kuvaa kwake mavazi yasiyousitiri mwili wake, huo ambao dunia imetufundisha jinsi ya kuutamani, sioni ni kwa jinsi gani atasalimika kuhesabiwa uzinzi pamoja na hao wanaume aliowaamshia hiyo tamaa! Tena jambo hili la kuwatamani wanawake si kwamba eti linaishia kwa wapagani tu. ingekuwa ni hivyo basi Paulo asingesemea kuhusu “kuwaka tamaa”. Kwahiyo ni vizuri tukalifahamu hili kwamba kuna wakristo wachanga ambao wasipofundishwa kuzigeuza shingo zao wanapokutana na wanawake wa jinsi hii yenye kujiwakilisha ktk namna ya kujifunua utupu wao, haswa humo makanisani kuliko jaa hivi vitimbi, ni rahisi sana kwao kuangukia katika mtego huo.

  Ndipo kwa mkristo mbumbumbu wa jambo hilo, huishia kuvalishwa kama hao mabinti na kuwa kivutio kwa dunia iliyomshawishi kujivika hivyo, na Maandiko kuhusu huyo mwenye kujivika jinsi hiyo na kuwaangusha watoto wa Mungu, yanasema hivi: “…bali atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, yamfaa afungiwe shingoni jiwe kubwa la kusagia, na kutoswa katika kilindi cha bahari.” (MT. 18:6 SUV) Umeona, hayasemi kuhusu watu wa dunia, hapana, hao ni wazinzi maisha yao yote, shetani hawezi kutenda dhambi kwani yeye mwenyewe ni dhambi!

  Pia mtazamo wako kwamba sisi tunawageuza wanawake kuwa ni vyombo vya ngono, hili si sahihi. Hujalitazama tu ktk kina chake, kinyume chake ni sahihi! Rudi kule Edeni halafu uitafakari hali ilikuwaje. Hivi, ni Adamu ndiye aliyempa mkewe tunda walilokatazwa? Hiyo hapo “blank mind”, umeiona? Adamu anayo maagizo ya kutokula tunda hilo, lakini anajiingiza ktk “sintofahamu” anakula kinyume cha Agizo kwa ushawishi wa mkewe! Ndani ya Adamu hakuna uongo ndio maana analisema jambo hilo sawa sawa na lilivyomtokea, hajamtaja nyoka wala shetani bali mwanamke! Basi kanisa likiwa ndilo mwanamke, chunguza unacholetewa ule!

  Sulemani alikuwa na wake 1000, kwa mawazo yako unafikiri walikuwa wanamsaidia kupika??? Mwisho wa mchezo waliondoka na Hekima yoooooote akabaki mtupu!

  Umeniuliza ninamuonaje huyo binti, mimi naona its all peer pressure kulingana na umri wake, na kuhusu Jakes, siwezi kumsemea, lakini iwapo atakuwa ameridhishwa na uvaaji huo, akauona ni wa kawaida kulingana na utamaduni wao, then it shows he’s sucked in, his preaching notwithstanding!

  Wewe mwenyewe Sungura, ume compromise Neno la Mungu ili tu uwafurahishe wanawake ktk hayo mavazi yao ya aibu, chezea mwanamke wewe!

  Gbu!!

 17. Sungura,

  Twende pole pole brother! Kutokujua jambo si dhambi na pia huwezi ukawa unayajua yote, na ktk kujifunza kunahitaji usikivu; basi hebu tuliangalie hili jambo ktk usikivu, haswa wa kile Maandiko yanachokifunua.

  Kuhusu mavazi unaniambia,
  “”Nataka unionyesha ni kwa jinsi gani tunavaa si kwa ajili yetu, bali kwa ajili ya Mungu.””
  Halafu ukaongeza,
  “”Lakini pia niambie ni kwa jinsi gani mavazi kwa ujumla wake yanahusiana na ngono””

  Kwa vile mambo haya mawili yanauwiana, kwa kadiri nilivyojaribu kuyarudisha ktk Maandiko, naweza kusema kwa uhakika kwamba, kuvaa kwetu ni kwa aina mbili, moja ikiwa ni kwa ajili yetu na nyingine kwa ajili ya Mungu! Labda tulitazame kwa pamoja ili tuone ni kwa namna gani.

  Aina ya kwanza, ambayo nawe unahusika nayo, ndio hii ambayo sisi huvaa kwa ajili ya kujipendezesha nafsi zetu, ndio kama hizo nguo walizovaa hao mabinti ktk picha, na nyingine ambazo huwa zinawaacha wazi kiasi, kwapa na sehemu ya matiti (daring you for more!), kwa ajili ya kuwapendezesha akina Sungura, na wakati mwingine hizo hupasuliwa ili wanapotembea, basi sehemu ya paja ionekane kwa kificho kidogo kwa ajili ya wachunguliaji, ambavyo ni nzuri na inachangamsha jamii hiyo kulingana na mila na ustaarabu waliomo; a Programmed Striptease!

  Suala la kuvaa nguo kwa mwanadamu, linaonekana kwa mara ya kwanza huko Mwanzo, na linahusisha jambo la kuwa “uchi”. Nalo jambo la kuwa uchi linawahusu watu waliofikia kuwa na Ujuzi wa Mema na Mabaya, na hivyo kuzijua na sehemu za maungo yao ktk namna tofauti na vile walivyozijua wakiwa ktk ufahamu wa kitoto, kwani ufahamu wao ulipopevuka wakazijua na sehemu hizo kuwa ni “nyeti” na hivyo kuzihifadhi, kulingana na umuhimu wake, ambao ni siri iliyo wazi, ndiko huko kuwa “nyeti”; Mwa‬ ‭3‬:‭7
  “Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wa uchi, wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo.”‬‬‬‬

  Katika kulitazama chimbuko la “kuvaa kwa ajili yetu”, Andiko hili ndilo linaloshabihiana na maelezo yako. Kama tunavyowaona Adamu na mkewe wakijivisha nguo kwa ajili yao kulingana na mapenzi yao, ni sawa kabisa na wazo lako. Yaani kama unavyoziona tamaduni mbalimbali za dunia ktk jinsi wanavyojivika, wote hujisikia raha ktk hayo mavazi yao mazuri na mitindo yake yenye kukaribia kuzifunua hizo nyeti, kimtindo, kwa kusudi, pamoja na wamang’ati nk. Dunia na fasheni zake, ingali ikizitengeneza hizo nguo za miti, ktk hicho kiwango cha akina Adamu.

  Lakini, Mungu alipowafikia, mambo yaligeuka. Yale mavazi yao mazuri hayakuweza kustahimili Uwepo wa Mungu, hayakuwahifadhi, ktk maana ya kuficha wala kuwasitiri kulingana na hali yao mpya hapo ilipowalazimu kukutana na Mungu! Iwapo yale mavazi yao yangetosha, basi kulikuwa na haja gani ya kukiri kuwa wako uchi ilhali wamevaa hizo nguo zao nzuri walizojitengenezea?
  “Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha.”

  Hii inaonesha kwamba mavazi waliyojitengenezea hayakukidhi kiwango kinachokubalika na Mungu na hivyo upungufu wake ukawa wazi kwao kutokana na huo Uwepo wa Mungu uliowazingira. Na hii ndiyo sababu pekee inayonifanya niamini kwamba Uwepo wa Mungu ukikukaribia, basi ni lazima ufahamu wako utafunguka kuhusu hali yako ktk hizo nguo za miti na utakuwa tayari kulipokea Neno la Mungu ili likusitiri aibu yako, hiyo ambayo huko nyuma ulijiona ni mwenye kusifika.
  “BWANA Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika.”

  Hili ndilo vazi lenye kusitiri mwili. Hili ndilo modest apparel! Basi jambo hili ndilo nilitegemea litakuonesha kwamba Mungu aliwavika hilo vazi kwa ajili yake, ili aweze kuwapokea tena ingawa ni ktk kiwango cha chini, bali kwa vazi hilo wangeweza kumsogelea; ndiko huko kujali kwake tunachovaa. Tazama hapa tena anachosema kuhusu mavazi:
  “Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako.” (‭KUM. ‭22‬:‭5‬)‬‬‬

  Kwahiyo kuna namna utakayovaa ambayo itakusababishia uwe chukizo mbele ya Mungu. Sasa si kwamba eti ukivaa kanisani ndio unakuwa chukizo, hapana, unakuwa chukizo wakati wote wa maisha yako as long as unavaa hivyo, na dhamira yako kujengeka ktk mavazi hayo, ingawa kanisani kwenu hilo si tatizo!

  Halafu, hebu jaribu kuchunguza sehemu nyeti ktk maungo ya binadamu, hizo Adamu anazozisemea kwamba yu uchi, unafikiri ni zipi; ni viganja vya mikono, au miguu, au ni nywele; kwamba yawezekana kwamba hizo nguo zilikuwa ni kofia au soksi? Pia chunguza, umuhimu unaopelekea kuzificha, yaani uliolazimu watengeneze nguo, unatokana na nini?

  Ukilitazama hili with an open mind utaiona maana halisi ya mavazi katika uhusiano wake na ngono, pia linaweza kukupanua uelewa kuhusu utamaduni ukajua jambo la ngono lina command kiasi gani ktk huo unaouita utamaduni kama si central!!!!

 18. Yes Lwembe,

  Nataka mpendwa mwenye kutamani apone kwanza kabla ya mpendwa mwenye kuvaa hivyo kwa sababu kuu moja; Huyu mpendwa kama atatamani kwa kumwona mdada kavaa nguo hizo kanisani, basi huko nje ambako ndo anakuweko muda mwingi anatamani sana, maana huko mavazi hayana control.

  Nawe nimbie kwa nini mimi ndo nahitaji msaada a kiroho kwanza kuliko mtamaniji na mvaaji?

  Lwembe maelezo yako uliyoyatoa kutokana na Mt 5:28, si ya kweli rafiki.
  Kwenye kumtazama mwanamke kwa kumtamani, si lazima huko kuzini moyoni kutamhusu na mwanamke aliyetamaniwa. Labda kama tu hao wawili wote walikuwa na kusudio la kuzini. Vinginevyo linamhusu mwanaume tu aliyetazama kwa kutamani.
  Kwa mara ya kwanza labda unatakiwa leo ujue kuwa kwa hiyo unayoiita amri mpya, Yesu alionesha kuwa kuzini kunaweza kukafanywa na mtu mmoja pia ndani ya moyo wake!

  Kwanza hapo haijasema kumtazama kwa kumtamani mwanmke aliyevaa mavazi ya aina fulani, haihusiki na mavazi. Si kila mwanaume mwenye kutamani humtamani mwanamke kwa sababu amevaa nguo tunazodhani zinahamasisha ngono. Bali wengine hutamani tu rangi, au kimo cha mwanamke, au macho , au midomo, au tabasamu.

  Naona untafsiri mambo kulingana na wewe ulivyo au uonavyo ukidhani kila mtu yuko hivyo, siyo!
  Lwembe unanitengenezea ‘assumptions” zako mwenyewe kisha unaanza kunijadili katiki hizo, unafanya jambo la hatari sana! Unapojaribu kuniambia kuwa nam -proach Mungu kwa ‘blank mind’ unalazimisha kuniweka kwenye kutokujua kwako!

  Elewa huu ukweli kwamba hatuishi kwa utamaduni wa kiyahudi, hatuvai kama walivyovaa wayahudi, wala hatuli kama walivyokula wayahudi, wala hatuongei kama wayahudi au kiebrania.
  Neno la Mungu linafit katika tamaduni zote zilizopo duniani. Likiongelea mavazi ya kustahi halimaanishe mavazi ya kiyahudi wala ya kigalatia wala kirumi, bali litamaanisha ya kihvyo kwa hao niliowataja, bali kwetu litahusu mavazi ya kustahi ya kitanzania! Paul mwenyewe hakuwa anavaa suruali ambayo leo tunavaa.

  Ndio maana anakwambia; kwa waebrania alikuwa kama mwebrania, kwa wakorintho kama wakorintho, n.k. Lakini elewa katika huko kuwa kwake bado alikuwa katika mipaka ya kanuni za Mungu. ( Sijui kama umenielewa)

  Kama inafika mahali tunafanana na bwana Siyi katika yale ya kweli tunayokuwa tumesema bado ni baraka, maana pamoja na tofauti zetu na Siyi, bado Mungu anatupenda sote.

  Sasa usikomee tu kusema kuwa mimi nimefanana na Siyi, sema pia kwa nini Paul aliwaagiza wanawake wa kikorintho wafuge nywele au wafunike vichwa?

  Wewe kwa fikra yako unadhani kabisa kwamba sielewi kuwa kimira cha wayahudi ni torati?

  Ehe, kwa kuwa kimira cha wayahudi ni torati unataka kusemaje Lwembe?

 19. Lwembe,

  Ni maona mara kadhaa unaniambia neno ‘hujui’, yaani mimi sijui kitu fulani. Cha kwanza umesema sijui tofauti ya mavazi yapi yanahifadhi na yapi yanasitiri.

  Pili ukasema sina ufahamu juu ya suala la kusema tunavaa kwa ajili yetu.

  Kwa sababu unadhani kuwa sijui na hapa tunajifunza ungeonesha jinsi gani sijui kwa wewe kusema vile unavyodhani unajua kuwa ndio ukweli wa hayo mambo ungekuwa umefanya la maana sana.

  Hiyo ingenisaidia nami kujua kama kweli sijui kutokana na kile ambacho wewe ungekuwa umekisema. Lakini kukomea kwako kusema tiu kuwa mimi sijui, haisaidii chochote.

  Japo suala la kuhifadhi na kusitiri si la kupotezea muda ni dogo sana. Nataka unionyesha ni kwa jinsi gani tunavaa si kwa ajili yetu, bali kwa ajili ya Mungu.

  Lakini pia niambie ni kwa jinsi gani mavazi kwa ujumla wake yanahusiana na ngono

  Umesema wanaficha” katika kiwango cha ufahamu walionao; na mimi nakukubalia kabisa. Ndio maana nami nasema nanyi mnatafsiri mavazi kuwa ni mabaya kulingana na maarifa mliyonayo juu ya dhambi, ndio maana mmefika sehemu mkaona mwili wa mwanamke kazi yake ni ngono,kiasi kwamba viungo vingi ktk mwili wake mnaviona vinawavuta kwenye ngono. Hilo ni tatizo sio dogo!

  Ukisema ”HAKUNA kusanyiko la Mungu unaloweza kuwa unaingia na hayo mavazi ya kuhifadhi, kama hayo ya Wamang’ati, labda RM asiwepo,..” Siyo kweli, bali kusanyiko likiwa la watu wenye kuvaa kama wamang’ati au likiwa la wamang’ati wenyewe utaingia na utasali na RM atakuwa pamoja na wewe!

  Vinginevyo Lwembe umeulazimsha ufahamu wako usiolewa kabisa muktadha wa kwa nini tunavyaa nguo, tena tunavaa nguo fulani mahali fulani!

  Dunia kujua kwamba umbile la mwanamke linatamanisha wanaume kingono si kigezo cha kuwafanya wanawake wawe watumwa wa mavazi. Kwanza hatuongozwi na nini dunia inasema ama inajua, bali tunaongozwa na kweli ya Mungu, whether inakubaliana na kile dunia injua na kuamini au haikubaliani hicho ndo twapaswa kukifuata.

  Dunia ndo imefanya mwanamke aonekane kuwa ni chombo cha starehe, dunia ndo inalazimisha kutufundisha mwanamke mzuri ni yupi, ndo inalazimisha kutufundisha umbo zuri la mwanamke ni lipi, ndo inatufundisha kiungo kipi kwa mwanamke ndo kinavutia zaidi kingono, n.k.

  Na watu wengi wameamini hayo na ndo yametengeneza mtazamo wao juu ya mwanamke, hii ni pamoja na wanawake wenyewe nao wamejitazama hivyo, ndo maana pia wengi wanatumia mali na muda wao mwingi waonekane kama dunia inavyotaka kuwaona. Huo nao ni uongo wa shetani.

  Nawe Lwembe nakuona umo katika hilo kundi la wanaofundishwa na dunia jinsi ya kumtazama mwanamke.
  Wewe unapoona kuwa manamke anaevaa nguo fupi maana yake anakufanyia marketing for ngono, wengine wenye mtazamo sahihi juu ya mwanamke wanaona kitu kingine kabisa.

  Hebu niambie unaona nini unapomwangalia Sarah Jakes kwenye hilo vazi?
  Vipi unadhani mzee Jakes nae anaona hivyo hivyo kama wewe uonavyo?

  Amini nakwambia, mavazi ni utamaduni zaidi ndio unaotawala!

 20. Sungura,

  Mwisho katika maelezo yako kuhusu kutamani unasema,
  “” Mimi mtu akisema kwamba mtu akivaa nguo kama ya huyo binti wa Jakes eti inamsababisha atamani, naona huyo anahitaji msaada wa kiroho kwanza kabla ya mvaaji…””

  Unataka kumtibu huyo anayetamani umpunguzie huko kutamani, ili huyo binti aendelee kuvaa hivyo vigauni! Mimi nakuona wewe ndiye unayehitaji msaada wa kiroho kuliko hao wawili! Pia hata jambo la kuwavalisha hao wanawake magunia halina mantiki ktk haya tunayoyazungumzia, Biblia inasema “modest apparel” na sidhani kama magunia yanakidhi jambo hilo!

  Msingi tunaouongelea hapa kuhusu hayo mavazi, pamoja na hayo maelezo ya Paulo, vimejengeka katika Amri hii mpya, Mt 5:28 “… lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.” Basi kutoka Amri hii ndio nilikuambia uje na intelligence yote aliyokupatia Mungu siku ulipoukubali wokovu, kuzini kunachukua watu wawili waliokubaliana ktk jambo hilo. Basi mwanamke mkristo anayejiwakilisha katika namna yenye kuamsha hisia za kingono, iwe ni kwa wapagani au wakristo, anakuwa ni legitimate partner katika huo uzinzi wa kiroho utakaoendelea na wanaume wote pamoja na Wamang’ati watakao simama kumtazama na kutamani kulala naye! Yaani mwanamke mwenye ujuzi wa mambo hayo, huwa anakuwa annointed kuwavuta wanaume, ndio maana hata Mmang’ati wako atakumbwa na mfadhaiko moyoni mwake akiisha kumuona tu mwanamke wa jinsi hii!

  Ni hatari kwa mkristo kuvaa nguo za jinsi hii, na ni hasara kubwa saaana, maana uzinzi kwa mkristo, hauna msamaha!

  Pia nimekuona ukijidhanisha kwa bidii, kwamba Wayahudi walikuwa na mila za kikabila cha kienyeji chao, na hivyo unajitahidi sana kuyachukua mafundisho ya mtume Paul na kuyaingiza ktk ukabila na mila usizo na ufahamu nazo, ili tu kuyafanya yaliwahusu watu fulani na si Kanisa. Hili ni zao la “a Blank Mind” approach! Don’t approach God with a blank mind, you will end up presuming Him; sum up all the Intelligence that God has given you when you approach Him, He loves that!!!

  Unajua wakati mwingine huwa mnafanana sana na Siyi; fikiria jambo hili kwamba wewe unaamini kwamba Paul alikuwa ana address jambo la kimila kwenye Biblia kuhusu nywele na mambo mengine, in your presuming; kama ambavyo Siyi naye anaamini kwamba Amri ya kuitunza Sabato ilikuwepo toka kwa Adamu; Hii ndio “a Blank Mind” approach inayowakamata mnapozisoma Biblia zenu, naye Ibilisi anaipenda sana hii maana humpa fursa ya kuwapa sensations mpaka muuamini ujinga ulio wazi kabisa!

  Israeli waliotolewa Misri ni kundi lililozaliwa huko Utumwani, kwa hiyo kudhani kwamba walikuwa na mila na jinsi tofauti ya kuendesha maisha yao kimila ni kukosa ufahamu au kuwa umeharibiwa. Tabia na mienendo yao ilikuwa ni ya kimisri pamoja na ibada, hicho ndicho kimila walichokijua! Kati ya hao waliotoka Misri ni wawili tu walioingia Kaanani, Joshua na Kalebu, wengine wote walifia jangwani huko kusiko na Ufufuo (ule wa Kwanza), na walioingia Kaanani ni hao waliozaliwa jangwani katika Utamaduni mpya wa Torati; ndipo unapaswa uelewe kwamba kimila cha Wayahudi ni Torati kaka!!!!

  Gbu!

 21. Sungura,

  Kuhifadhi, na Kusitiri! Unapata shida kulielewa hili kwa sababu ni kweli hujui mavazi yepi yanahifadhi nini, kama vile usivyojua yapi yanasitiri nini!!! Ni muhimu kuyajua haya kwanza, ndipo utayaelewa na Maandiko.

  Kuhusu maneno, Apparel na Modest, naona kimaudhui tafsiri zote ziko sawa tu. Na kuhusu hili neno, “impropriety”, hili ndilo Msingi wa haya tunayoyazungumza hapa, ni kutoka ktk standard ya Ukristo kama taifa au kabila! Tumechukua hizo kamusi kama shahidi kutoka duniani (intelligent people), ili kuipima hiyo TABIA ya huyo binti ILIYOJIDHIHIRISHA katika hilo vazi, ili kuona kama inaendana na ukiri wake wa wokovu, haswa katika reflection ya baba yake?

  Ni rahisi kujichanganya katika tafsiri na mitazamo ya kikabila ukiisha ikosa maana ya jambo hili kimaudhui ya kikristo, ndio maana umejifikisha ktk hatua ya kuamini kwamba Mungu hajali tunachovaa!!

  Lakini Mungu anajali sana tunachovaa! Kule Edeni aliwavua yale mavazi waliyojivika, akawatengenezea vazi jipya na kuwavika, sasa ukisema kwamba eti tunavaa kwa ajili yetu, basi ni kwamba huna tu ufahamu ktk hilo!!!

  Hata ukirudi kwa hao Wamang’ati, licha ya kutofikiwa kwao na Injili, bado wanao ufahamu kiasi fulani hata wanajua kuwa sehemu hizi ni nyeti ktk miili yao na hivyo inawalazimu wazifiche; basi, nikikuuliza, kati ya jicho la binadamu na hizo sehemu nyeti wanazozificha, ni kipi ambacho ni rahisi kudhurika? Mimi nadhani jicho liko more vulnerable kuliko hizo nyeti wanazozificha, labda unioneshe tofauti!!!!

  Mavazi kaka yanahusiana na NGONO ktk ujumla wake, ndio maana hata wamang’ati “wanaficha” katika kiwango cha ufahamu walionao; Pia HAKUNA kusanyiko la Mungu unaloweza kuwa unaingia na hayo mavazi ya kuhifadhi, kama hayo ya Wamang’ati, labda RM asiwepo, vinginevyo akikufikia utatafuta nguo UJISITIRI UTU wako! UTU wetu unajumuisha na hizo nyeti ambazo tunazihifadhi kwa “nguo za ndani”!

  Kama dunia inajua kwamba umbile la mwanamke linatamanisha wanaume kingono, na ndio wanakwambia nguo zake ziusitiri mwili wake ili asiwe kishawishi, sasa wewe sijui unaishi dunia gani, maana wanawake wenyewe wanayajua mambo haya, labda awe mtoto mdogo, lakini mwanamke mwenye kumjua mwanaume, huwa wanajua nguo zina maana gani, wewe tu na utoto udogo wako ndio hujui!!!

  Kuvaa nguo zisizo sitiri mwili, kimsingi unawaambia wateja watarajiwa kwamba “Ninapatikana!”, huu ndio ujumbe anaotuletea thru body language; ndio hiyo sehemu ya mapaja unayoiona ambayo yapaswa iwe imesitiriwa! Lakini pia unapaswa uelewe kwamba hapa hatumzungumzii mwanamke wa duniani, hao wana uhuru wa upofu walionao; hao wanazo nguo za jioni see thru, bikini za beach, za disco na za night club na mwishowe huvaa chochote kinachoweza kuwashawishi wanaume kwa haraka ili awe appreciated katika level hiyo kingono!

  ……….

 22. Lwembe nimekuja sasa.

  Hii comment yako ya mwisho nafikiri ulikosa la kusema!!

  Nguo za ndani zinahifadhi nini unachosema zinahifadhi?

  Ok, ulileta maana za kikamusi za maneno fulani ingawa hukusema ni Dictionary ipi uliyotumia.

  Mimi natumia ‘OXFORD ADVANCED LEARNER’S DICTIONARY’ Inasema hivi:

  Apparel:
  2. (old fashioned or formal) clothes particularly those worn on a formal occasion

  Modest:
  3.(of people, especially women or their clothes) shy about showing much of the body; not intended to attract attention especially in a sexual way.

  Katika tafsiri yako ya neno ‘modest’ kuna neno ‘impropriety’ umelitumia. Neno hilo linaonesha kuwa lazima kuwe na kiwango (standard) ndipo mtu awe judged kama yuko ‘propriate’ au ‘impropriate’.

  Sasa, hiyo standard haijaandikwa kwenye biblia, ispokuwa ni ya kijamii.
  Kwa mfano; wamang’ati katika mazingira ya kwao,aborigines wa Australia katika mazingira ya kwao, nguo za kufika magotini siyo standard yao, nguo zao ni za kuficha maeneo nyeti tu, na haiwasumbui.

  Elewa jambo moja kuwa hatuvai nguo kwa ajili ya Mungu, ispokuwa ni kwa ajili yetu wenyewe.

  Kuhitimisha kwamba nguo ya staha ni ile inayovuka magoti ni kufanya hukumu iliyopinda, maana vazi liko la namna mbalimbali kwa ajili ya kuvaliwa mahali mbalimbali, na ndio maana kulikuwa na vazi la makuhani lililokuwa tofauti na mavazi mengine.

  Kosa ktk mavazi ni ‘conditional’, lazima lizingatie mtu amevaa nini wapi, siyo tu mtu amevaa nini. Lakini zaidi sana nia ya mvaaji kuvaa nguo fulani mahali fulani ni ipi pia!

  Mimi mtu akisema kwamba mtu akivaa nguo kama ya huyo binti wa Jakes eti inamsababisha atamani, naona huyo anahitaji msaada wa kiroho kwanza kabla ya mvaaji. Maana si lazima ukiona sehemu fulani ya mwili wa mwanamke uko wazi kinachofuata ni kutamani, hiyo ni kasumba tu.

  Hakuna vazi ambalo mwanamke anaweza akavaa likatosha kumzuia mwanaume mwenye tamaa kutamani, hata kama wanawake watavaa magunia tamaa ya mwenye tamaa itapenya tu hata kwenye hayo magunia.

  Wanasaikolojia wanasema kuna kundi kubwa tu la wanaume wanatamani hata kwa kuona tu nguo za ndani za wanawake zimetundikwa kwenye boutique.

  Kinachofanya wanaume wengi kutamani ni kuwa na loose mind, na kuona kuwa mwanamke yupo tu kwa ajili ya ngono, ndio hao wanaojikwaa hata na makwapa tu ya wanawake, na wengine wanajikwaa tu kuona makalio makubwa ya mwanamke hata kama amevaa nguo ndefu ya kufika viwikoni.

  Lakini uliongelea pia suala la wanawake kutokata nywele ukilifananisha na hili suala la mavazi kuwa ni agizo kwa wanawake wakristo. Sishangai, ndio maana wengine wakaamuru wanawake wawe wanafunga vilemba.

  Ila sijui kama unaijua vizuri historia nyuma ya hilo agizo, sijui kama unaelewa sawasawa nini kilikuwa kinaendelea mpaka Paul akatoa hilo agizo

  Jambo la msingi ni kwamba wanawake hata wanaume pia wanatakiwa kuvaa nguo zinazokubalika katika eneo husika na jamii iliyopo.

  Wanaume wakristo hasa waache kasumba ya kuona kuwa maungo ya mwanamke ni kwa ajili kuvuta hisia za ngono tu, mtazamo huo wawaachie wapagani.

 23. Sungura,
  Nimefurahi kwamba angalau umeanza kulielewa somo! Umebakiza hatua chache tu, ngoja nikusaidie kidogo ili usije ukatoka nje huku umechomekea shati kwenye hizo” nguo za ndani”!!

  Nakunukuu:
  “””Kama vazi ‘modest’ ni linalofika angalao magotini, basi nguo za ndani si mavazi yenye kusitiri maana hayafiki magotini.”””

  Ni kweli nguo za ndani hazisitiri bali zinahifadhi!!!

  Karibu sana!

 24. Lwembe,

  Una akili nyingi ambayo haina akili ndani yake, lakini wewe hujaiona una akili nyiiingi. Unapoanza kuandikia makala mtu naweza kudhani kuna hoja nzito sana ndani yake lakini huwa ni wingi wa maneno tu bila nguvu ya hoja.

  Kama vazi ‘modest’ ni linalofika angalao magotini, basi nguo za ndani si mavazi yenye kusitiri maana hayafiki magotini.

  Ndio nyie wenye kujikwaa hata na mabega na makwapa ya wanawake kuwa wazi, mmejawa na tamaa hivyo mwataka kuwafanya wanawake wawe watumwa wa mavazi kwa sababu ya tamaa zenu.

  Hiyo ni salaam tu, nitakuja Lwembe!

 25. Nicky,

  Unamaanisha nini unaposema ‘nyumba ya Mungu’ kiasi cha kujenga hoja ya nguo za kuvaa nyumbani mwa Mungu?

  Je unaposema nguo ya kuvaa kanisani unamaanisha lile jengo ambalo huwa tunakutana kwa ajili ya ibada au unamaanisha kusanyiko la watoto wa Mungu?

  Bilashaka unajua kuwa wewe na mkeo na watoto wako mnapofanya ibada ya pamja usiku hilo tayari ni kusanyiko/kanisa.

  Sasa jiulize wewe huwa unavaa nini wakati huo na mke wako huwa anavaa nini, halafu utagundua kuwa kuvaa kwenu huwa hamvai kwa sababu mko kanisani wakati huo bali huwa mnava kulingana na utamaduni mliojijengea wenyewe, na huo utamaduni hutikana na utamaduni wa jamii iliyowazunguka au mliyolelewa kwayo.

  Yawezekana kabisa mke wako huvaa pensi na kisinglend na wewe huvaa bukta na kisinglend halikadhalika.

  Kwa hiyo jibu langu kwa swali lako kwamba ni nguo gani inafaa kuvaliwa kanisani, jibu ni kwamba hakuna nguo maalum.
  Swali kwamba nguo aliyovaa huyo binti wa Jakes (yaani nguo fupi), inafaa kuvaliwa kanisani au la, jibu lake ni kwamba inaweza ikafaa au isifae.

  Majibu yangu yako hivyo kwa sababu nguo ipi inafaa na ipi haifai inategemeana na setting ya utamaduni wa jamii inamovaliwa, ambapo kanisa katika sehemu hiyo pia ni sehemu ya jamii hiyo.
  Ndiomaana ukienda kwa kanisa la wamaasai utakuta wengi wamevaa mashuka, kwa sababu huo ndio utamaduni wao, na Mungu hana tatizo na hilo.

  Ndiposa nikasema kama anakosa lisiwe kwa sababu ya kuvaa nguo fupi, ila liwe kwa sababu amevaa nguo isiyokubalika kuvaliwa hapo alipoivaa.
  Saa sijui ninyi mnamhukumu kwa sababu amevaa nguo fupi au kwa sababu amevaa nguo ambayo hakupaswa kuivaa mahali hapo.

  Kimsingi biblia haijatuchagulia nini cha kuvaa bali imetuagiza namna ya kuvaa. Kwa sababu ukishajua namna ya kuvaa ndipo linakuja suala la nini cha kuvaa uwe katika namna unayotakiwa kuwa.

  Mwanamke aliyenyuma ya Sarah Jakes amevaa suruali ya kubana,sijajua kwa nini mwenyewe hammuongelei!

  Lakini pia nakuona wewe kama mtu mwenye shida, kwa sababu unaonekana kukwazwa hata na mabega na makwapa ya mwanamke kuwa wazi, wakati wengine tunaona hivyo vitu ni vya kawaida.

  Nafikiri unapaswa kubadilika katika jinsi unavyomwona mwanamke Nicky, she is not an object for sex. Ilikuwa kawaida sana kumwona mwanamke ametoa ziwa nje linachezewa na mtoto, lakini sasa hivi hilo nalo mnalifanya ni jambo nyeti kiasi cha kumfanya mtu aingiwe tamaa.

  Tusijiongezee uwanja wa kututendesha dhambi, bali tujitahidi kuupunguza huo uwanja kwa kuweka sawa nia zetu. Hatuwezi kutawaliwa na fasheni za dunia kiasi kwamba tulazimike kujitofautisha nao kimuonekano kwa nguvu.

  Si lazima ukimwona mwenye nguo fupi umtamani, acha wasiomjua Mungu watamani kwa kumuona mwenye nguo fupi.

  Ukitamani ni kwa sababu umeamua kutamani!

 26. kwako mpendwa noel matulwa na wapenda neno la Mungu
  kwanza nianze kusema neno la Mungu limehakikishwa mara saba hivyo Neno ni pumzi ya MUNGU ndio maana katika kitabu cha ufunuo limefungwa kwa kusema.na mtu ye yote akiondoa lolote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki,Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima,na katika ule mji mtakatifu,ambao habali zake zimeandikwa katika kitabu hiki (ufunuo 22:-19) sasa nije kwenye mada uliyoomba tuchangie kuna watu wanadhani Mungu ni kigeugeu kilingana na utandawazi.Mungu anasema mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanaume,wala mwanaume asivae mavazi ya mwanamke;kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa bwana,Mungu wako(kumbukumbu la tolati 22:-5) kwa kusema hivi ina maana kuna mavazi ya kike na kiume mimi nasema vazi la suruali ni vazi halali kwa wanaume. wanawake wote wakristo wanao wavaa suruali ni machukizo kwa Mungu najua kuna wabishi watajitokeza kupinga na kutetea kwa vile wanapenda dunia biblia inasema dunia inapita pamoja tamaa zake bali Neno la Mungu litaendelea kusimama daima sasa nitoe mfano moja wa wanaume watakatifu walio kuwa tayali kufa kwa kuipigania,kuilinda imani yao nao walikuwa wanavaa suluari soma habali za akina Daniel,meshaki,abednego (daniel 3:-21) nawasubili wabishi nitaendelea kutoa mifano na niwaase akina dada,wanawake mnaovaa suruali mjue kwa kufanya hivyo mnafanya machukizo achani kufuata dunia Mungu anakatataza soma ( balikiwa walumi 12:-2) balikiwa nyote

 27. WARUMI 16:17-18
  “NDUGU ZANGU, NAWASIHI, WAANGALIENI WALE WAFANYAO FITINA NA MAMBO YA KUKWAZA KINYUME CHA MAFUNDISHO MLIYOJIFUNZA; MKAJIEPUSHE NAO. KWA SABABU HIVYO HAWAMTUMIKII BWANA WETU KRISTO, BALI MATUMBO YAO WENYEWE; NA KWA MANENO LAINI NA YA KUJIPENDEKEZA WAIDANGANYA MIOYO YA WATU WANYOFU.” WARUMI 16:17-18

  MSIDANGANYIKE MAVAZI YA KIKAHABA YAPO.

  MITHALI 7:10
  “NA TAZAMA, MWANAMKE AKAMKUTA, ANA MAVAZI YA KIKAHABA, MWEREVU WA MOYO;”

  Leave a Reply

 28. WARUMI 16:17-18
  “NDUGU ZANGU, NAWASIHI, WAANGALIENI WALE WAFANYAO FITINA NA MAMBO YA KUKWAZA KINYUME CHA MAFUNDISHO MLIYOJIFUNZA; MKAJIEPUSHE NAO. KWA SABABU HIVYO HAWAMTUMIKII bWANA WETU kRISTO, BALI MATUMBO YAO WENYEWE; NA KWA MANENO LAINI NA YA KUJIPENDEKEZA WAIDANGANYA MIOYO YA WATU WANYOFU.” WARUMI 16:17-18

  MSIDANGANYIKE MAVAZI YA KIKAHABA YAPO.

  MITHALI 7:10
  “NA TAZAMA, MWANAMKE AKAMKUTA, ANA MAVAZI YA KIKAHABA, MWEREVU WA MOYO;”

 29. c.k.lwembe.
  Mungu akubaliki kwa kuwapa ufafanuzi wapotoshaji wa neno la Mungu

 30. Sungura, Tumaini

  …..inaendelea

  Na kutokana na kupindwa tabia, ndiyo kumewasababisha msiweze hata kuyaona yaliyo wazi kama ambavyo unaikataa maana halisi ya hili onyo ktk 1Tim 2:9, ukilipindisha kwa hila kukidhi Mapokeo ya Kiteologia uliyokaririshwa, eti:
  “”Kama wewe ni msomi mzuri wa biblia nafikiri unajua kuwa kwenye lugha za asili hiyo 1Tim 2:9 haijasema mavazi yanayoficha uchi, bali mavazi suitable, appropriate, modest, n.k.
(KJV -9 In like manner also, that women adorn themselves in modest apparel, with shamefacedness and sobriety; not with broided hair, or gold, or pearls, or costly array;)
 Neno ”Apparel” linamaanisha vazi maalum linalovaliwa kwenye tukio fulani (yaani vazi la mahali pake””

  Yaani kama kuwa “msomi mzuri wa Biblia” ndio unafikishwa ktk kiwango cha “Ujinga wa Maandiko” kiasi hiki, ni bora ubakie ktk upagani, maana Hukumu yako itapoa kidogo kuliko huyo “msomi mzuri wa Biblia” anayelipindisha Neno la Mungu!
  Na kwa kuyapokea maelezo ya Uongo wa ki dini kama haya, ndio kwa mpindo wake umefikishwa mpaka huko beach ambako wanawake na wanaume walio katika huo mpindo, huchanganyika pamoja wakiwa nusu uchi, wakijidhania wana “enjoy” maisha, hapo wanapokodoleana macho ya husda, kama wale wanao shiriki “strip tease” katika jina la ‘ustaarabu’, au kihalisia “Mwaga radhi”; ni roho za uasherati na uzinzi ndizo zinazowahangaisha!

  Biblia haiwezi kufundisha huo upuuzi wa mavazi katika namna ya eti kuyagawa hili ovaroli lisivaliwe kanisani! Jamani, ovaroli safi lililovaliwa vizuri likiusitiri mwili lina shida gani? Acheni akili za Kisabato za kumvalia Mungu suti na tai! Ndio maana mna kuja na tafsiri za ajabu ajabu kwa mambo yaliyo wazi kabisa kwa visingizio vya “lugha za asili”!!! Eti: “”””Agizo halisemi wanawake wavae nguo zinazozuia wanaume kutamani.”””” Hahahahaha…. “…. Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani? ……. Hakika hamtakufa..”!!! AGIZO LINAWATAKA MSIVAE MAVAZI YATAKAYO WASABABISHA WANAUME WAWATAMANI, mkikaidi mtaishia katika Hukumu ya WAZINZI na WAASHERATI kulingana na Maandiko, sio Theologia kama aliyopewa Hawa!!!!!

  Kwa faida yenu ya kuunyoosha huo mpindo mliopindishwa, hii hapa tafsiri ya kikamusi ihusuyo hayo maneno mnayoyapindisha:
  APPAREL: 1. noun [mass noun]: CLOTHING. 2. verb (apparels, appareling, appareled) [ with obj. ] : CLOTHE (someone)

  Tafsiri rahisi ni hii hapa:
  1. jina (jina la jumla) – MAVAZI. 2. tendo – VISHA, VALISHWA, VAA (mtu fulani)

  MODEST:
  • (of a woman) dressing or behaving so as to avoid impropriety or indecency, especially to avoid attracting sexual attention.
  • (of clothing) not revealing or emphasizing a person’s figure. modest dress means that hemlines must be below the knee.
  • (kuhusiana na mwanamke) mwenye kujivika au kujiheshimu ili kuepuka aibu kulingana na kiwango kinachokubalika katika jamii kitabia, haswa kuepuka kuwa kivutio kingono.
  • (kuhusu mavazi) yasiyo uweka wazi au kuyaonesha maumbile ya mwili (tight); yaani yenye kusitiri. Vazi lenye kusitiri ina maana kwamba pindo zake lazima ziwe chini ya goti.

  Basi ukichanganya haya maneno mawili “Modest Apparel” ndio unapata Kiswahili sanifu cha “Mavazi ya Kusitiri mwili” na si hizo hadithi zako zisizoeleweka za mavazi ya beach; mkristo hajichanganyi na dunia, hayarudii matapishi, humo alimotolewa; amepelekwa huko juu yaliko mambo bora na mazuri zaidi ya huko kujianika beach kama kauzu!

  Vazi kama la huyo binti mdogo ni matokeo ya aidha mafundisho ya hovyo kama haya ya akina Sungura mimbarani, yakiwatoa uweponi mwa Mungu kwa kuwanyoa nywele zao kama Wasabato, na kuwavisha vigauni visivyoustahili ukiri wao wa wokovu, kwa upande mmoja, au ni ule ukaidi unaotokana na ujana katika ule ushawishi anaoutumia Ibilisi kuwaharibu vijana wetu, ambao kwa kadiri wanavyoukulia wokovu wa kweli, chini ya walimu wa kweli, Neno litawachonga waufananie Ufalme kama yalivyochongwa mawe ya kujengea Hekalu!

  Ingawa Hukumu ya Mungu inaazia kanisani, bado ni vizuri mkaelewa kwamba Mungu hakaagi kanisani! Wengi tunanafikiri kwamba si Haki kuvaa vigauni kama hivyo Kanisani, kanakwamba Mungu anakaaga kanisani; bali Mungu amejaa dunia yote, yupo kila mahali na anaabudiwa ktk kila sekunde ya maisha ya mkristo, kwahiyo twapaswa kuwa tulio tayari kila wakati, kufanya ibada popote tulipo, ndiko huko kuwa waraka!

  Ni kweli Sungura, “” Tukielewa inachomaanisha Biblia itatusaidia sana.””!!!!

  Mbarikiwe!

 31. Sungura, Tumaini,

  Nimefurahi sana kuwaona!

  Lakini nimesikitishwa sana pia, na hali yenu ya kiroho; kwa kadri ya maoni yenu na kukiri kwenu kuhusu wokovu, sikuwategemea kabisa mje na mafundisho kama haya mnayoyaleta. Inaonesha kwamba hata wokovu wenyewe hamuujui sawa sawa kuwa ni nini; kumbe huwa mnayarejea tu mafundisho mliyokaririshwa kama akina Siyi, without an understanding! Na mnaishia ku argue out of ignorance kama ninavyowaona hapa leo!!!

  Najua mtaendelea kubisha, lakini take it from me, it is just out of ignorance, otherwise hicho kimini alichokivaa huyo binti, si “modest apparel” by any standard or language, au “formal” kwa tukio lolote lile linalohusiana na maisha ya mkristo, unless muwe kama hivi ninavyowaona kwamba hamjui hata mkristo yukoje, kitabia, yaani characteristics! Mnadhani kuimba kwamba ” umeokoka” ndiko kunakufanya kuwa mkristo, ua kusali rozali, au kusali Jumamosi na upuuzi mwingine wa Mapokeo; unakuwa Mkristo hapo unapozaliwa kwa Roho wa Mungu, ndipo na mambo ya Rohoni utayaelewa!!!!

  Wasukuma hufanya mambo yao Kisukuma; Wangoni nao hufanya mambo yao Kingoni, vivyo mataifa yote ya dunia, kwa sababu wanaongozwa na hizo roho zao za kikabila au kitaifa. Nasi wakristo, tunaye Roho wa kitaifa. Huyo ni Roho Mtakatifu atokaye kwa Mungu mbinguni, nasi hutenda kama yeye. Huyo hukufanya nawe kufanya kama wanavyofanya huko juu mbinguni, kwa sababu mkristo ni wa ulimwengu mwingine!

  Tunaishi usukumani; sawa, bali ni sehemu ya mwili tu. Lakini roho ambaye anatuongoza, tabia zetu, ni wa kutoka juu. Tunaishi kutoka juu kwa sababu tumezaliwa kutoka juu. Wakristo wote ni wa kutoka juu. Yesu alisema, “Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu. Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi wangu wangenipigania, nisije nikatiwa mikononi mwa Wayahudi. Lakini ufalme wangu sio wa hapa.” Yn 18:36. Ufalme wake ni wa juu!!!

  Na hivyo ndivyo ilivyo kwa kila mtu aliyezaliwa ktk Ufalme wa Mungu, Yeye ni wa kutoka juu. Nazo tabia ziwahusuzo hao ndizo hizo unazoziona ktk Maandiko, ambayo Roho huwafafanulia wote anaowaongoza. Kama aliwaonya Wakorinto waliozaliwa katika Ufalme wake kuhusu wanawake kutokukata nywele zao, basi jua wazi kwamba Ufalme haujawahi kubadilika, ukiwa nawe umezaliwa humo utayaelewa maonyo hayo na yataibadilisha tabia yako ili uulinganie Ufalme huo; Lk 12:32 “Msiogope, enyi kundi dogo; kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule ufalme.” KJV inaliweka vizuri zaidi jambo hili, “… for it is your Father’s good pleasure to give you the kingdom.”!!! Mwangalie huyu aliye limbuko la Ufalme huo anachokisema hapa kama unaweza kuliona jambo hilo; Yn 3:13 ” And no man hath ascended up to heaven, but he that came down from heaven, EVEN THE SON OF MAN WHICH IS IN HEAVEN” (msisitizo ni wangu) Hayo anayaongea hapa duniani lakini anakwambia YUKO MBINGUNI!!!!

  Na kama umezaliwa ktk ufalme wa dini, basi roho wa Mapokeo pia atakuongoza, akiutengua uwezo wako wa kulipokea Neno la Mungu, akiipindisha tabia yako kuyalingania Mapokeo ya kiteologia kama haya unayotuletea, ukiamini kabisa kwamba mavazi modest ni pamoja na “bikini”!!!

  Itaendelea…..

 32. JE BIBLIA INATAMBUA KUWA KUNA MAVAZI YA KIKAHABA? NDIYO

  MITHALI 7:10
  “NA TAZAMA, MWANAMKE AKAMKUTA, ANA MAVAZI YA KIKAHABA, MWEREVU WA MOYO;”

  MOJA: BIBLIA TANGU AWALI HATA SASA INATAMBUA MAVAZI YA AINA FULANI NI YA MIUNGU FULANI

  ASILI YA ULIMBWENDE NI LUCIFER
  MBILI: SIKU ZOTE MUNGU ALIPOWAITA ISRAELI KUJITENGA NA MATAIFA ALIWATAKA WAACHE ULIMBWENDE WA NJE NA KUSHUGHULIKIA ULIMBENDE WA NDANI (ROHO)

  MWANZO 35:2
  “YAKOBO AKAWAAMBIA WATU WA NYUMBANI MWAKE, NA WOTE WALIOKUWA PAMOJA NAE, ONDOENI MIUNGU MIGENI ILIYOKO KWENU, MJISAFISHE MKABADILI NGUO ZENU.”

  MWANZO 35:4
  “NAO WAKAMPA YAKOBO MIUNGU MIGENI YOTE ILIYOKUWA MIKONONI MWAO, NA PETE ZILIZOKUWA MASIKIONI MWAO, NAYE YAKOBO AKAZIFICHA CHINI YA MWALONI ULIOKO SHEKEMU.”

  WAAMUZI 8:24
  “KISHA GIDEONI AKAWAAMBIA, MIMI NINA HAJA YANGU NIITAKAYO KWENU, NI YA KILA MTU KUNIPA HIZO PETE ZA MASIKIO YA MATEKA YAKE.(KWA MAANA WALIKUWA NA PETE ZA MASIKIO ZA DHAHABU, KWA SABABU WALIKUWA NI WAISHMAELI.) WAAMUZI 8:24

  YEREMIA 4:30
  “NA WEWE, UTAKAPOTEKWA, UTAFANYAJE? UJAPOJIVIKA MAVAZI MEKUNDU, UJAPOJIPAMBA MAPAMBO YA DHAHABU, UJAPOJITIA WANJA MACHONI, UNAJIFANYA KUWA MZURI BURE TU; WAPENZI WAKO WANAKUDHARAU; WANAKUTAFUTA ROHO YAKO.”

  EZEKIELI 23:40
  “TENA MMEWATUMA WATU KUWAITA WATOKAO MBALI; AMBAO MJUMBE ALITUMWA KWAO, NA TAZAMA, WAKAJA; NAWE ULIJIOSHA KWA AJILI YAO, ULITIA RANGI MACHO YAKO, NA KUJIPAMBA VYOMBO VYA UZURI.”

  EZEKIELI 23:42
  “NA SAUTI ZA WINGI WA WATU WENYE HALI YA RAHA ZILIKUWA PAMOJA NAE; NA PAMOJA NA WATU WASIO NA ADABU, WALILETWA WALEVI TOKA JANGWANI; WAKATIA VIKUKU MIKONONI, NA TAJI NZURI JUU YA VICHWA VYAO.”

  HOSEA 2:13
  “NAMI NITAWAAMWADHIBU KWA SABABU YA SIKU YA ZA MABAALI, ALIOWAFUKIZIA UVUMBA; HAPO ALIPOJIPAMBA KWA PETE MASIKIONI MWAKE, NA KWA VITO ASEMA BWANA.”

  KADILI MTU ANAVYOSHUGHULIKIA ULIMWENDE WA NJE, ULIMBWENDE WAKIROHO HUSAHAULIKA.

  KUTOKA 33:5,6
  “BWANA AKAMWAMBIA MUSA, WAAMBIE WANA WA ISRAELI, NINYI NI WATU WENYE SHINGO NGUMU; KAMA MIMI NIKIINGIA KATI YENU DAKIKA MOJA, NITAWAANGAMIZA; BASI SASA VUENI VYOMBO VYENU VYA UZURI ILI NIPATE KUJUA NITAKALOWATENDA. BASI WANA WA ISRAELI WAKAVUA VYOMBO VYAO VYA UZURI, TANGU MLIMA WA HOREBU NA MBELE.” KUTOKA 33:5, 6
  MUNGU HAPENDI ULIMBWENDE WA NJE AMBAO HUMFANYA MTU ANASAHAU KUSHUGHULIKIA ULIMBENDE WA NDANI, NA KUJIONA WA MAANA KWA KUJIANGALIA KWA NJE.

  ISAYA 3:18-23
  “SIKU HIYO BWANA ATAWAONDOLEA UZURI WA NJUGA ZAO, NA KAYA ZAO; NA PETE ZAO ZA MASIKIO, MA VIKUKU, NA TAJI ZAO; NA DUSUMALI, NA MAFURUNGU, NA VITAMBI NA VIBWETA VYA MARASHI, NA MATALASIMU; NA PETE, NA AZAMA, NA MAVAZI YA SIKUKUU, NA DEBWANI; NA SHALI, NA VIFUKO, NA VIOO VIDOGO, NA KITANI NZURI, NA VILEMBA, NA UTAJI.” ISAYA 3:18-23

  HAPO ANAZUNGUMZIA VIOO VIDOGO AMBAVYO HATA WATU WA SIKU HIZI PIA HUJIANGALIA KATIKA SURA ZAO HATA,TUMIGUU NDANI YA VIMINI VYAO KUMBE NI WAFU KIROHO.WAKIJIPA MOYO KUWA WANAFAA MBELE YA MACHO YA WANADAMU, WAKIIMBA MAPAMBIO, NA KUCHEZA KWA MADAHA MADHABAHUNI,WAKITIKISA NYWELE ZAO KULIA NA KUSHOTO, KUMBE NI WACHAFU.

  ROHO YA YEZEBELI ALIYEABUDU MIUNGU YA BABELI NA KUMFUATA LUCIFER ALIYEKUWA NA KIBURI KWA MAPAMBO YA MADINI ALIYOUMBWA NAYO, NDIKO HUTIA ROHO NGUMU NA KIBURI CHA KUJIONA TU WA MAANA TUKISAHAU UREMBO WA NDANI (HEKIMA YA MUNGU)

  EZEKIELI 28:16,17
  “…..EWE KERUBI UFUNIKAYE, UTOKE KATIKA HAYO MAWE YA MOTO. MOYO WAKO ULIINUKA KWA SABABU YA YA UZURI WAKO; UMEIHARIBU HEKIMA YAKO KWA SABABU YA MWANGAZA WAKO;”

  EZEKIELI 28:13
  ULIKUWA NDANI YA ADENI, BUSTANI YA MUNGU; KILA JIWE LA THAMANI LILIKUWA KIFUNIKO CHAKO,AKIKI, NA YAKUTI SAMAWI, NA ZUMARIDI, NA BAHARAMANI, NA DHAHABU; KAZI YA MATARI YAKO NA FILIMBI ZAKO ILIKUWA NDANI YAKO; KATIKA SIKU YA KUUMBWA KWAKO ZILITENGENEWA TAYARI.”

  BAKI YA SHETANI KUWA MWANAMUZIKI, ALIFUNIKWA NA MAWE HAYO HAPO JUU, UREMBO UKAMTIA KIBURI. AKASAHAU KUTENGENEZA MOYO WAKE KWA SIFA YA MUNGU AKAJIINUA.
  UCHAFU WA BAAL WA BABELI NA WA YEZEBELI YA ULIMBWENDE NDIO ILIYOINGIA KATIKA MAKANISA YA LEO. KWA MAANA WATU WAMEKATAA HEKIMA (NENO) WAKAPOKEA YANAYOWAFURAHISHA MIOYO.

  “..YEZEBELI AKAPATA HABARI; AKATIA UWANJA MACHONI MWAKE, AKAPAMBA KICHWA CHAKE, AKACHUNGULIA DIRISHANI.” 2 WAFALME 9:30

  WANAWAKE WAWILI WA UFUNUO (AMBAO HUWAKILISHA MAKANISA MAWILI LA UPAGANI NA LILE LA MUNGU) WANATUPA MTAZAMO WA MWANAMKE AMBAYE ANAWAKILISHA UKAHABA ALIVAAJE NA ANAYEWAKILISHA KANISA VEMA ALIVAAJE.

  UFUNUO 17:4
  “NA MWANAMKE YULE ALIKUWA AMEVIKWA NGUO YA RANGI YA ZAMBARAU, NA NYEKUNDU, AMEPAMBWA KWA DHAHABU, NA KITO CHA THAMANI, NA LULU, NAYE ALIKUWA NA KIKOMBE CHA DHAHABU MKONONI MWAKE, KILICHOJAWA NA MACHUKIZO, NA MACHAFU YA UASHERATI WAKE.”

  UFUNUO 12:1
  “NA ISHARA KUU ILIONEKANA MBINGUNI; MWANAMKE ALIYEVIKWA JUA, NA MWEZI ULIKUWA CHINI YA MIGUU YAKE, NA JUU YA KICHWA CHAKE TAJI YA NYOTA KUMI NA MBILI.”

  NDUGU, YESU, JUA LA HAKI, NA KANISA LIMEJENGWA JUU YA MSINGI WA MITUME NA MANABII

  NURU YA KIVULI ILIYOSONDA KUWA KUNA MWANGA (AGANO LA KALE) NA /NENO/KRISTO NURU HALISI, ILIYOFUNULIWA (AGANO JIPYA) NDIO HUTIA NURU KANISA

  “NA MJI ULE HAUHITAJI JUA WALA MWEZI KUUANGAZA, KWA MAANA UTUKUFU WAMUNGU HUUTIA NURU, NA TAA YAKE NI MWANAKONDOO.” UFUNUO 21:23

  BASI SIFA ZA MAVAZI YA KWELI YA MTU WA MUNGU NI KUJIVIKA HAKI YA KRISTO.

  JE WAJUMBE WA MUNGU HUSITIRI MIILI YAO? NDIYO

  UFUNUO 1:13
  “NA KATIKATI YA VILE VINARA NIKAONA MTU MFANO WA MWANADAMU, AMEVAA VAZI LILILOFIKA MIGUUNI, NA KUFUNGWA MASHIPI WA DHAHABU MATITINI.” UFUNUO 1:13

  MITHALI 7:10
  “NA TAZAMA, MWANAMKE AKAMKUTA, ANA MAVAZI YA KIKAHABA, MWEREVU WA MOYO;”

 33. amani ya bwana iwe nanyi

  Kaka nicky mchango wako umenifanya nitambue zaidi shetani anavyoteka wana wa mungu kwa mbinu , analegeza kanuni za mungu ili mradi tu awapate walio wake
  Haya mambo ya kuruhusu kutokuvaa vazi la kujisitri ndio maana hayo mavazi yanaingia kwenye nyumba ya mungu,

  Ufunuo 22:11-19) ibilisi anazidi kutenda kazi yake tena kwa kasi, mchafu anazidi kujichafua na msafi azidi kujitakasa,

  mpendwa kuongozwa na roho mt ni jambo la muhimu sana, haijalishi ni sehemu gani ya vazi linatakiwa kuvaliwa,
  roho huongoza maana kila kilicho cha mungu huwa na amani moyoni,

  Lakini unavaa nguo unahisi kama umekosea vua hiyo nguo haraka na uvae nyingine ambayo utakuwa haikuhumu ndani mwako,

  barkiwa

 34. Wapendwa Sungura na Tumaini, Ni kweli kila vazi lina sehemu yake kama mnavyosema hauwezi kulala na suti au kuvaa ovaroli kanisani ni ukweli kabisa. Na ni kweli kabisa umalaya haupimwi kwa mavazi.Lakini ni ukweli kuwa 90% ya wanawake wanaouza miili yao (Machangudoa) wanavaa nguo fupi na zinazoangaza ili kutangaza biashara yao. Labda ni hoji kuhusu vazi na mahali pake. Je nguo fupi zinazoonyesha mapaja ni mahali pake kanisani?? Nguo zinazoonyesha (transparent) ambazo tunaona dada zetu wanavaa kanisani siku hizi je kanisani ndio mahali pake?? Je nguo zinazo onyesha mabega na matiti wazi ni mahali pake kanisani. Kwa mfano hicho kivazi alichovaa mtoto wa Jakes hapo juu kina tofauti gani na mwanamke anyetoka kwenda disko?? Maana kila nguo ina mahali pake je nguo inayoonyesha mapaja kiasi hicho inastahili kuvaliwa kanisani?? Kama ofisi za serilkali na baadhi ya makampuni dunia nzima wameweka sheria ya mavazi ya kiofisi ndio maana tunaona bungeni mtu akivaa jeans anatolea, ukivaa nguo fupi unafukuzwa. Hizo nguo wanazovaa wanawake makanisani siku hizi hata ofisini hawawezi kuzivaa. Sasa je Kanisa si zaidi ya ofisi ya kiserikali au kampuni?? Kama watu wanaheshimu mavazi kwenye ofisi za serikali sasa je nyumba ya Mungu si inatakiwa iheshimiwe zaidi?? Mwanzoni kabla sijatembelea na kuishi ughaibuni nilikuwa najua wanaume wa kizungu au wanaume wanaoishi ulaya na marekani hawana mfadhaiko na wanawake wanovaa nguo fupi au nguo zisizo faa, lakini baada ya kukaa nao nikangundua sio kweli, kuna kesi nyingi tu za wanaume kupatwa mfadhaiko na kudhalilisha wanawake kwasababu ya mavazi. Hata kama mtasema huu ni udhaifu wa mwanaume mwenyewe, je huyo mwanamke anayesababisha mwanume amtamani utamweka kwenye kundi gani? Je Bibilia inasemaje kuhusu kumsabibisha mtu mwingine atende dhambi? (Luka 17:1). Shetani anatafuta kila aina ya njia kufanya wanadamu watende dhambi? Mavazi ni moja ya silaha ya maangamizi ya shetani? Shetani shaivi anajikita kwenye slogani ya Haki za wanadamu, kwamba kila mtu ana haki ya kufanya chochote mradi havunji sheria za nchi, wanaharakati na wanasheria wanatumia hilo rungu vizuri sana. Wachungaji wengi nchi zilizoendelea wanaogopa kuhubiri kweli kwasababu ya kuogopa kushtakiwa na wanaharakati Huwezi kuongelea ushoga, huwezi kuongela mavazi, huawezi kuongelea taraka, hauwezi kuongelea utoaji mimba, uvutaji bangi unahalalishwa, mtoto akifikisha miaka 15 hurusiwi kuhoji hata akileta mwanaume au mwanamke ndani, watoto wanawashitaki wazazi wao kwa kuwawekea sheria za maadali. Shetani anajua wakati wake ni mchache (Uf 12:12) anautumia muda huu mchache kudanganya maelfu ya wanadamu.

  Wapendwa Tuhubiri injili watu waokoke, waijue kweli.

 35. Stephen,

  Sijajua kama wewe ni mgeni kwenye hili jukwaa au ndo hivyo hutaki kufikiri nje ya box.
  Kwanza hakuna lugha chafu iliyotumika, labda imekuwa chafu kwako wwe kama wewe ni mchafu, maana mtu huwa haoni kama vitu jinsi vilivyo ila kama yeye alivyo. Hapa kuna moderator, ambaye anamjua Mungu na anajua lugha chafu ni ipi na safi ni ipi, hivyo hawezi kuruhusu lugha chafu ziwe mbele ya umma.

  Pili unavyoongea na kujenga mantiki zako nikitaka nikuchambue ndo utaona nimekutukana kabisaaa.

  Lakini ngoja nikupe tu dondoo kidogo labda utasaidika:

  Umenipa mfano wa swali kama naweza kwenda ukweni na kaptura, hii imenionesha kuwa unafikiri kutoka katika kona ya wasukuma, wanyakyusa, wajita,wasambaa, n.k, kwa kudhani utamaduni wa hayo makabila kuhusu mkwe na mkamwana ulivyo, ndivyo wa dunia yote ulivyo.

  Hebu elewa kuwa hapa tunamwongelea Mungu wa makabila yote duniani, ambaye haufungwi na utamaduni wa kabila lenu. Kuna makabila mengine mama mkwe ni mama tu kama mama mzazi. Mungu siyo msukuma na wala hafungwi na utamaduni wa wasukuma. Na utamaduni upo kwa ajili yetu siyo kwa ajili ya Mungu.

  Jambo jingine la ajabu kabisa unaniuliza ati kama ninaweza kukaa uchi mbele ya wanangu. Unaendeleza haya maswali ya kitoto kwa sababu hutaki kujibu maswali niliyokuuliza, likiwemo swala ”nini maana ya uchi”?

  Inaonekana kwenu kwapa uchi, mapaja ni uchi, kifua nacho ni uchi. Na kwa kuwa kwako hivyo vyote ni uchi unataka kila mtu na kila kabila nao waone kuwa hivyo vitu ni uchi – Pole sana.

  Lakini pia umesema ati watu wanakuja nyumbani mwa Bwana na nguo zisizo na heshima. Hebu nikuulize swali: hizo nguo hazina heshima kwa Mungu au kwa watu?

  Ni rahisi kusema kuwa mimi nina macho lakini sioni kwa sababu hilo ni andiko liko hivyo tangu lilipoandikwa mpaka leo, jifikirie tena kama wewe unaona kweli hapo ulipo, utagundua kuwa umechelewa sana Stephen.

  Ni kweli kustiri kwa Kiswahili maana yake ni kufunika, kuficha, kuziba, lakini bahati mbaya sana maandiko ya asili yamesema kuwa mavazi yanayoitwa ya kustiri kwenye Kiswahili,kwenye hizo lugha ni mavazi yenye kukubalika kuvaliwa mahali yalipovaliwa. (Soma tu hata King James Version utajifunza)

  Na kama tunapaswa kuvaa mavazi yenye kustirii kwa maana hiyo ambayo umeishadadia, basi ni wazi kuwa chupi si vazi la kusitri, kaptura si vazi la kusitiri, fulana (sing-lend ), si vazi la kusitiri, sidiria si vyazi la kusitiri, n.k

  Stephen jiongeze kiufahamu, Mungu ni wa ulimwengu wote, si wa kabila lenu tu nchi yenu.

  Upewe kuelewa!

 36. Naona wapendwa wanamlaumu Sungura badala ya kujaribu kuangali kwa jicho la ndani kile anachokiongea!mfano Tanga watu wanavaa ninja na still wanauza mwili!vazi linalositiri mwili ni lile linalovaliwa sehemu husika mfano vaa ovaroli thn ingia kanisani!au wakati wa kulala piga suti na tai!je hamuoni Sungura anayozungumza yanamashiko?

 37. sungura kwanza nakuomba tulumbane kwa hoja acha kutumia lugha chafu,unaonekana ni mwelewa lakini hutaki kuelewa dada stera amesema vema nyie ndio mnatimiza unabii kwamba kusikia mtasikia wala hamtaelewa,kutazama mtatazama wala hataona maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito na kwa masikio yao hawasikii vema na macho yao wameyafumba wasije wakaona kwa macho yao na wakasikia kwa masikio yao,wakaelelewa kwa mioyo yao ,wakaongoka nikawaponya(mathayo 13:1415) mimi sikushangai kwa ubishi wako huenda unafanya hivyo kutaka maada iendelee kujadiliwa,au ndio huelewi majibu unayo mimi nakuongeza kama ifuatavyo
  1.maana ya kustili ni kufunika,kuficha,kuziba,nije swala la mavazi mimi siongelei watu walio nje mimi naongelea watu walio ndani ya kristo kama huyo mtoto wa mhubili alipaswa kuwa kielelezo sasa usituletee mifano ya michezo,bechi.nk huko tutakuja baadaye sasa unasitili nini katika mwili wa binadamu kuna sehemu zinatakiwa kusitiliwa kama kifua,tumbo,mgongo,makalio nitumie lugha hiyo,makwapa,mapaja,nk ndio maana nikakuuliza swali wewe unaweza kukaa uchi mbele ya wanao,watu unaoweheshimu au niseme unaweza kwenda na kaputura kwa wakwe.sasa leo watu wanakujaje na nguo ambazo hazina hesima nyumbani mwa Mungu ,au kwenye matamasha,makongamano ya ki Mungu sisi tunaojiita wakristo kwa ujumla wake tunapaswa kuwa balua,vielelezo kila mahali tusomeke tabia za kikristo nimpongeze sana mpendwa Nicky,stera,kwa michango yao mubalikiwe

 38. Nicky,

  Usilaumu watumishi wa Mungu kwamba wameshindwa kukemea dhambi kana kwamba wewe ni mtumishi wa shetani. Kama kuna dhambi unaona hawazikemei nafikiri ni pamoja na hiyo ya kwako ya kulaumu badala ya wewe kusimama na kufanya ambacho unaona hakifanywi.

  Halafu ni wapi Sungura amesisitiza injili ya kwenda na wakati?

  Nafikiri mnakosa kuelewa ni nini hasa tunalumbana hapa, matokeo yake mnabaki kusema tu lolote.
  Kama wewe ni msomi mzuri wa biblia nafikiri unajua kuwa kwenye lugha za asili hiyo 1Tim 2:9 haijasema mavazi yanayoficha uchi, bali mavazi suitable, appropriate, modest, n.k.
  (KJV -9 In like manner also, that women adorn themselves in modest apparel, with shamefacedness and sobriety; not with broided hair, or gold, or pearls, or costly array;)
  Neno ”Apparel” linamaanisha vazi maalum linalovaliwa kwenye tukio fulani (yaani vazi la mahali pake)

  Wala biblia haijasema vazi la kusitiri ni vazi refu, wala haijasema lisilositiri ni vazi fupi, au la kubana. Jifunzeni kusoma between the lines ndipo mtoe huku, ili hukumu zenu ziwe za haki.

  Nimetoa mfano huku nyuma kuwa bokta michezoni pamoja na ufupi wwake ndio mahali pake, vichupi vya kuogelea ufukweni ndo mahali pake,na hiyo ndo maana ya vazi linalositiri.

  Kwa kuwa machanguduo hutumia nguo fupi kuvutia wateja wao, unatakaje sasa, wanawake duniani kote wavae nguo ndefu ili wasifananishwe na machangudo?

  Nimekwambieni fuatilieni ufuska unaofanyika kwenye nchi za wavaa hijabu ndo mtajua tamaa inafanyaje kazi. Huko hata machangu huvaa hijabu na bado wanaume wanawafuata.

  Tuambieni basi, na mashoga nao huvutiwa na mavazi ya namna gani ili tujiepushe na hayo mavazi!

  Jaribu kumshauri mtumishi mwanamke siku moja avae ninja hijabu kisha asimame madhabahuni kuongea neno la Mungu, halafu uone watu wangapi watamwelewa kwa urahisi na kupokea ujumbe wake.

  Agizo halisemi wanawake wavae nguo zinazozuia wanaume kutamani. Nakuambieni kama wakati huo wa Paul machangudoa walikuwa wanavaa nguo ndefuuu zenye kuficha mpaka miguu, basi inawezekana wakristo waliambiwa wasizivae kama walivyoambiwa wakorintho wasinyoe nywele.

  Ttukielewa inachomaanisha biblia itatusaidia sana.

 39. Mpendwa Stephen, Mungu akubariki sana kwa ufafanuzi mzuri. Ukweli upo wazi watumishi wa wengi wa Mungu wa nyakati hizi wameshindwa kusimama katika zamu zao na kukemea maovu (Habakuki 2:1). Matokeo yake dhambi zimeshika hatamu kiasi kwamba zinaonekana kama kitu cha kawaida. Watumishi wengi wanaogopa kuhubiri kweli ya Mungu kuhusu dhambi hii siyo kwenye mavazi peke yake jaribu kuangalia uasherati kwa vijana na uzinzi. Huku wenzetu wana utamaduni wa vijana kuwa na marafiki wapenzi (Boyfriend and Girlfriend) kwa miaka mingi ya nyuma waliweza kumudu na kuwafundisha vijana wao hakuna kufanya mapenzi mpaka ndoa (No sex until marriage) lakini huu utamaduni umeshawashinda siku hizi vijana wanafanya uasherati (fornication) kwa kasi katika umri mdogo matokeo yake mimba katika umri mdogo, utoaji wa mimba umeshika kasi mpaka umehararishwa na serikali zao. Hii ni kwasababu ya injili za kwenda na wakati ambazo Mpendwa Sungura anasisitiza lazima twende na wakati. Ndoa za jinsia moja nako ni kwenda na wakati kwahiyo tuanze kukubalina na wanaharakati wa ndoa za jinsia moja kuwa ndoa siyo lazima iwe ya mwanaume na mwanamke, ila iwe ya kwa watu waliopenda si umesikia Presbyterian Church wameshamua kubadilisha maana ya ndoa na kuweka definition yao kuwa ndoa ni kwa watu wawili waliopendana. Nirudi kwenye mada kuu ya mavazi, maandiko yapo wazi wanawake wajipambe kwa mavazi ya kujistiri (1Tim 2:9), sasa mwanamke anapovaa nguo ambayo hata kukaa inamsumbua, kutembea inamsumbua, kupanda gari inamsumbua hivi utasema hiyo nguo inamsitiri. Mpendwa Sungura napenda tu kukutaarifu ukweli ni kwamba Mwanamke yupo tayari hata kutembea uchi mradi aambiwe umependeza (wanawake ni viumbe wanaopenda kusifiwa hasa sifa zinapotoka kwa wanaume bila kujali hao wanaume wanamtamani). Mwanamke akiambiwa hujapendeza harudii kuiva hiyo nguo tena na hata moto anaichoma. Maandiko yapo wazi wanawake wanachukuliwa mateka kiurahisi sana (2Tim 3:6) na Shetani analijua hilo toka mwanzo (Mwz 3:1-7). Hivi Mpendwa Sungura kama mavazi mafupi hayaleti tamaa kwa wanume kwanini machangudoa wanayatumia kuvutia biashara zao??? We unafikiri kwanini Machangudoa wanaacha mapaja na maziwa nje??? JIbu ni rahisi Kwasababu wateja wao ambao ni wanaume ndio wnatamani vitu hivyo vitu. Mwanamke akivaa nguo fupi iwe Kanisani au mtaani wanaume watawakwa na tamaa tu. Ni wanaume wachache sana wanaomtamani mwanamke kwa mkumuangalia sura yake, Lakini wanaume wengi sana huwakwa na tamaa wanapoona mapaja, tumbo au kifua cha mwanamke.Hebu jaribu hata kuangalia matangazo ya biashara wanayotaka kuvutia wanaume wanatumia picha za mwamke aliyeuchi au aliyevaa vibaya kwasabau wanajua wanume wataangalia tu. Moja ya silaha ambayo shetani anaitumia na amefanikiwa ni swala la Mavazi yasiotiri mwili kwa wanawake, hii mpaka wachungaji wandondoka kwenye tamaa ya mwili na kujikuta wanafanya uzinzi.
  Tuhubiri Injili Iliyokweli bila kuogopa

 40. Stephen,
  Acha uongo na umbayuwayu, nani kasema mavazi yasiyositiri miile si kitu?
  Jifunze kusoma maandiko na usome vizuri katikati ya misitari ili ufahamu wako uelewe kilichoandikwa na maana yake.
  Usisome tu kwa macho halafu ukatoa tafsiri ambayo umeisikia kwa mchunga au mhubiri wako ukadhani ndicho kilichobebwa na maandiko uliyosoma.

  Unasema unashuhudia leo watu wakivaa mavazi yasiyostahili, ni mavazi gani hayo yasiyostahili, hayastahili wapi? Wewe hapo najua umevaa boxer au bukta au chupi huko ndani, je hilo ni vazi linalostahili au halistahili?

  Jaribu kuipa akili akili yako(sijakosea) ili ujue kuongea kitu kwa umaalum wake. Naona unaongea tu mambo kwa ujumla jumla.
  Hakuna vazi lisilostahili wala lisilofaa kwa asili. Kustahili na kutokustahili huja katika matumizi

  Jaribu wewe kuchukua hiyo boxer yako unayosema inafaa halafu ivae huu ya suruali, halafu nenda barabarani hapo ndo utajua ni kwa jinsi gani inafaa.

  Nimekwambia kuwa maana ya vazi linalositiri ni vazi linalovaliwa mahali pake na kwa wakati wake, na wala siyo vazi linaloficha uchi. Kwani kama ni vazi linaloficha uchi, je chupi haifichi uchi? Mbona mnaendekeza hoja za kimaamuma wakati mna akili za kufikiri na kuona ukweli mkitaka?

  Ukivaa suruali yako na tisheti kisha ukaenda Ikulu pale Magogoni ukawaonyesha barua yenye crown kuwajulisha kuwa umealikwa na Rais, watakutimua tu, wala hautaingia. Wakiulizwa watasema umevaa nguo ambazo hazistahili, ndo utabaki unashangaa!

  Mimi huwa sipendi mtua ambaye haongei sense lakini ila anaongea ongea tu.

  Stephene kuna vitu nilikuuliza nataka unijibu ili twende sawa:

  1. Huyo dada hapo juu yuko uchi? Nini maana ya kuwa uchi?

  2. Wewe uliyaona mavazi ya Adam na Eva kuwa yale ya Eva yalikuwa marefu mpaka miguuni au yalikuwaje?

  Tafadhali jiongeze katika kufikiri na kujua nini hasa fungu fulani la maandiko linamaanisha, vinginevyo huna tofauti na mafarisayo waliomtuhumu Yesu kuwa alisema atalivunja hekalu na kulijenga kwa siku tatu, wasijue alichokuwa anaongea.

  Hapa hatupo kwa ajili ya kuongeaongea tu mambo ya kishabiki na kuyajumlisha mambo yote katika fungu moja, tunachambua na kupembua ili kujua ipi mbichi na ipi ni kavu.

  Nakungoja!

 41. Bwana Yesu asifiwe wapendwa wasomaji
  kwako sungura na wengine mnaotetea mambo ya mavazi kuona mavazi yasiyositili miili si kitu ingekuwa sio kitu biblia isingesema wanawake wavae mavazi ya kujisitili miili tena imeongeza na adabu soma 1timotheo 2:9 unajua Mungu ni wa leo,jana,na milele hivyo alijua zitakuja siku ambazo watu watajichafua na kutokujali na kufikili Mungu anaangalia ndani tu kumbe anaangalia na nje kama muumbaji leo tunashudia watu wanavaa mavazi yasiyositili miili mavazi yasio na adabu kama kuvaa vimini,suruali,vinguo vya kubana na yote haya wanafanya kwa kutokujua neno la Mungu maana biblia inasema mwapotea kwa kutokujua neno la Mungu wapendwa unajua mambo yaliyofunuliwa, yaliyo wazi,ni ya kwetu yaliyofichwa ni ya Mungu sisi tunapoona watu wanakosea kama kuvaa mavazi yasiyo na adabu lazima tuyakemee.leo hata viongozi wa makanisa wameshindwa kusimama kwenye zamu zao kwa kushindwa kukemea mambo haya ndio maana mtu kama sungura anajalibu kutetea ebu nikujibu hata mfano ulioutoa wa luka7:36….50 unajua Yesu alikalibishwa nyumbani kwa falisayo yule falisayo alichokuwa ameona aliona mtazamo wa nje akajua yule mwanamke ni mwenye dhambi akaanza kuwaza vibaya hata juu ya huduma ya Yesu lakini Yesu yeye kama mwokozi aliyetumwa na Mungu kumtafuta mwanadamu aliyepotea na kupungukiwa na utukufu wa mungu aliona moyo wa toba ndani ya yule mama na yule mama maisha yake ya mbele yalibadika akawa nuru ya ulimwengu.leo niishie hapo. sungura usihangaike na makosa ya uchapaji angalia ujumbe unauelewa pia dada yangu stera simama juu ya neno la Mungu acha watu wanaotetea madhehebu maana Mungu hakuleta madhehebu bali alileta wokovu kupitia Yesu na kama wote wangempokea yesu kama bwana na mwokozi wa maisha yao tusingekuwa tunapata shida ya kubishana kwani wangekuwa na hofu ya Mungu maana mungu anasema atamuangalia mtu anayesikia,anasoma neno la Mungu ana hofu na kukutemeka soma isaya 66 :1,,,2 mubalikiwe nyote Amina

 42. Shalom,

  Wana macho lakini hawaoni na wana masikio lakini hawasikii!!!
  mtasikia jambo jipya na masikio yenu yatawasha !
  barikiwa

 43. Nicky,

  Fikiri vizuri sana juu ya unachokiandika, usilete Injili ya kufikirika huku ukitafsiri mambo sawasawa na udhaifu wako.

  Wewe ndo umemtamani huyo dada wala usingizie ati wanaume wangapi wamemtamani.

  Na tamaa ina macho beyond nguo. Nenda kwa wavaa hijabu ukaone ukahaba unaofanyika pamoja na hizo ninja hijabu.

  Wewe hiyo Mat 5:27-28, inaiona sawasawa na kilichojaza moyo wako. Yenyewe hata haijasema kila amtazamayee mwanamke aliyevaa nguo fupi au ndefu kwa kumtamani …..
  Wewe unasubiri uone mapaja ndo utamani, wenzako wakiona macho tu tayari tamaa imeshawaka. Acha hiyo injili ya zamani isiyo na ukweli ndani yake.

  Kwani wewe unatofauti gani na nguo wanazovaa wasanii wa kiume wasiomjua Mungu?

  Na kama unataka tofauti iwe katika mantiki hiyo , kwa hiyo wakianza kuvaa nguo ndefu mpaka miguuni basi wa kwetu waache kuvaa ndefu ili tuone tofauti siyo?

  Nguo fupi zinakuwa kero kwa sababu ya dhambi iliyo ndani yako siyo kwa sababu ya nguo kuwa fupi. Ikiwa hayo masaa machache ya kukaa kanisani zinakuwa kero, vipi hayo masaa ya kumwaga unapokuwa mtaani ambako ndiko zinavaliwa tena kwa malengo, si unatenda dhambi sana wewe.

  Jifunze kuuweza mwili vinginevyo utaumia sana maana kanisani tunakaa masaa machache sana, na mtaani zinakovaliwa ndo masaa mengi.

  Shetani hajapofusha macho wanawake, bali amepofusha macho wanaume waliojawa na tamaa, wenye kumwangalia mwanamke kama chombo cha starehe. Shetani anafanya kazi yake anayotakiwa kufanya, wala simlaumu.

  Kumbumbka hakuna dhambi inaitwa ”dhambi ya kuvaa nguo fupi”
  Acheni kutukuza tamaa kuliko kutukuza uweza wa Mungu, kuna dhambi zingine tunazitengeneza wenyewe wala katika akili ya Mungu hazijawahi kuwa dhambi.

  Mwenye tamaa hata mkiwavika wanawake magunia, atatamani tu.

  Tuweni kama Lutu aliyeweza kuishi katikati ya Sodoma na Gomora, na bado akawa imara.
  Kuna mambo aya muhimu zaidi ya kufanya kuliko kupoteza muda kuchunguza masuala ya nguo fupi na ndefu, za kubana na za kuachia.

  It’s all nonsense!

 44. Stephen,

  Kwanza mimi naitwa Sungura wala si Sungula, halafu inaitwakabila wala si kabira.

  Haya, sasa naomba unioneshe nilichopotosha ni nini, ili tuone kama wewe unaongea kitu unachokijua au ulichokifanyia study, au unaongea tu kwa kukariri utamaduni wa dhebu lenu au kabila lenu.

  Wewe kwa kutazama kwako, huyo dada yuko uchi? au hata maana ya uchi haujui mpendwa?

  Ulishawahi kujiuliza yule aliyemfuta Yesu kwa nywwele zake walimtambuaje kwamba ni kahaba, kama si kutokana na mavazi yake? Kwa hiyo ulivyosema kuwa mavazi hututambulisha uko sawa.

  Sasa niambie Yesu alikuwa anaona nini kwa huyo kahaba mpaka akamruhusu amfanyie hayao aliyofanya, amabacho wengine walikuwa hawakioni mpaka wakamhukumu?

  Vipi weweuliyaona mavazi ya Adam na Eva kuwa yale ya Eva yalikuwa marefu mpaka miguuni au yalikuwaje?

  Mavazi si kwa ajili ya Mungu, bali kwa ajili ya watu, Mungu chake ni nia iliyo ndani ya mvaaji. Mwanamke atavaa nguo ndefu bmbele yako si kwa sababu ya Mungu bali kwa sababu yako ili usitende dhambi wewe uliye dhaifu.

  Kwa hiyo wewe ukienda kwenye mashindano ya Olmpiki halafu ukawaona akina dada walivyovaa kisha ukatamani, utahitaji kufanyiwa maombi haraka sana. Maana ulipaswa kujua kuwa huko nguo ndefu huwa hazivaliwi kabisa, ila huvaliwa vichupi tu. Na ndio utamaduni wa huko unaokubalika.

  Kwa hiyo tatizo siyo aina ya nguo, ila ni wapi hiyo nguo imevaliwa. Na hiyo ndio maana ya kuvaa mavazi yenye kustiri.

  Ndo nikasema kosa la huyo dada yawezekana alivaa vazi ambalo halikubaliki kuvaliwa hapo alipokuwa na hiyo jamii

  Standard yetu siyo dunia inachosema ni kizuri au kibaya, ni kile biblia imesema ni kizuri au kibaya.
  Ni nani au biblia ipi iliyokwambia kuwa hilo alilovaa ni vazi la kikahaba, au unadhani kuwa dunia nzima makahaba huvaa nguo fupi ili kujulikana kuwa ni makahaba?

  Stephen, nusu ya uchi ni ipi?

  Halafu hebu sema, ivi unadhani Yesu angekuwepo kimwili kwenye hilo tamasha angemhukumu huyo dada kuwa ametenda dhambi kuvaa hivyo?

  Karibu.

 45. Dada Stella,
  Twende taratibu, tukiliacha Neno lituongoze safari inakuwa nyepesi. Basi Neno likiwa ndilo hivyo vito vya thamani, tujihadhari na yule mwovu ambaye kazi yake ni kuvibadili hivyo vito na makorokoro yasiyo na thamani kama hili:
  “”Ni kweli Mungu alipowatengenezea mavazi ya magome ya miti Adamu na Hawa ni AlIWASITIRI aibu yao maana walijitambua kuwa wako uchi baada ya ile dhambi””

  Ingawa inaonekana kama ni Kweli, lakini jambo hili uliloliandika SI KWELI ni korokoro lisilo na thamani yoyote mbele za Mungu, na badala yake linaweza kukuingiza katika matatizo ya “Kuongeza au Kupunguza” kwenye Neno la Mungu na hivyo kukustahilisha kubaki huko Nje! Yaani ukifika Mlangoni ili kupimwa Uzito, utakuwa ni mzito kuliko kawaida ya Neno la Mungu! Labda Neno la Mungu kama lilivyo ktk biblia, ukiliishi hilo, likiwa limejaa kwa wingi wake ndani yako unakuwa na uzito wa Kilo za Kiroho 70; lakini ukiongeza chochote kile ambacho si Neno wewe ukakifanya ni Neno, loh, kilo zinaruka pengine kupita mia mbili, kama za Wakatoliki au Wasabato, au ukipunguza kutoka hilo Neno unakuwa mwepesi kiasi kwamba hata kutulia juu ya mzani upimwe haiwezekani, ndio hao wengi wa wapentekoste, leo yuko kwa nabii huyu kesho huyooo kwa mtume yule, anapeperushwa kama kishada!

  Lakini ukidumu ktk Neno Kamilifu, maisha yanakuwa rahisi na yenye shukurani kama unavyomuona Petro alipoulizwa baada ya wapentekoste kurudi Roma, alipoulizwa ninyi hamuondoki? Alimwambia wao hawaondoki, hawawezi kuliacha Neno, basi nawe dada yangu usikubali kupokea usichokikagua, kama hilo ulilolikiri kuhusu akina Adamu, kula hiki hapa kilicho halisi kiujaze moyo wako:
  “BWANA Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika.” (‭MWA.‬ ‭3‬:‭21‬ SUV)

  Ubarikiwe!

 46. halleluyah,

  Natumaini wote wa zima KWA UWEZO NA NGUVU za BWA NA wetu YESU KRISTO;

  kAKA Stephan nashukuru kwa ufafanuzi zaidi juu ya mavazi ya kujisitiri ,
  Ni kweli Mungu alipowatengenezea mavazi ya magome ya miti Adamu na Hawa ni AlIWASITIRI aibu yao maana walijitambua kuwa wako uchi baada ya ile dhambi,
  Sasa Basi tukiingia ktk roho kuwa uchi ni kuwa na dhambi, kama vazi lime kusitiri huwezi kuwa uchi,

  biblia ufunuo 3:5….(soma ) Yesu atatuvika mavazi meupe ya kitani nzuri ambayo ni UTAKATIFU, Usichafue vazi lako kwa kushindwa kukusitiri mwili wako, vilevle usiache roho yako ikaangamia kwa dhambi kwa kutokuwa mtakatifu,

  barikiwa

 47. kukaa uchi au kuvaa mavazi yanayoonyesha mapingili ya uchi wako ni makosa kibiblia, hiyo ni ishara ya laana…ndiyo maana hata Baba yetu Adamu alipomkosea Mungu alijihisi yuko uchi.

 48. sitiri sana maumbile yako ewe binti unaejiita ni mtoto wa Mungu. Huo mwili wako unaouita ni hekalu la Bwana unausojoa na kuuanika vibaya mbele za watu hauwakilishi vema tabia ya kiungu ya kujisitiri na kujiletea adabu na heshima mbele za watu.

 49. Sungura, kwakweli nasikitika kwa maelezo yako, sijui unamwamii Mungu gani? Ni huyu Yehova Mungu asiyebadilika au unaye mungu mwingine anayebadilika kutokana na nyakati?? Hivi waislamu wanawake wanavaa hijabu na manguo yao hayo tena meusi Dunia nzima kwa hiyo woote ni single culture ya waarabu??? Hivi kwanini watu mnapenda kutetea dhambi. Hivi kweli ni haki kwa mwanamke kusimama madhabauni na nguo ipo juu ya magoti?? Hivi siku hizi dhambi ya kutamani imefutwa?? Au siku hizi watu wameacha kutamani au wanaume siku hizi wamebadilika (evolution) wamepata gene mpya zinazozuia kutamani? Mat 5:27-28 “Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; 28 lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake”. Kwa kumuangalia huyo Sarah Jakes kwa hilo vazi lake ni wanaume wangapi wameshamtani ni wangapi wanaendelea kumtamani wanapoona picha yake. Hivi huko Mbinguni kutakuwa na uchafu wa nguo wanazolazimisha wanawake kuzivaa makanisani siku hizi? Hivi nguo kama hiyo aliyovaa Sarah Jakes inatofauti gani na vinguo wanavyova wasanii wanapokuwa majukwaani au mwanamke anayekwenda disco? Kwa kweli nguo fupi ni kero makanisani hasa huku kwenye nchi zilizoendelea, wachungaji wengi kwenye huku nchi zilizoendela wanogopa kukemea dhambi ndiyo maana uasherati ni mwingi kupita kiwango kiasi kwamba uzinzi hauonekani kama ni dhambi tena, ndio maana hata ushoga unaingia makanisani. Shetani amewapofusha macho wanawake wanaenda na fashion hata kamaa ikimaanisha kutembea uchi wapo tayari.

 50. sungula acha kuwapoteza watu au wana wa Mungu kwani biblia inaposema tuvae mavazi yanayo sitili mwili maana ya biblia ni hii kuvaa mavazi yenye heshima na adabu bila kujali ni nchi gani,au kabira gani je!ni nchi ,au kabira gani ambalo mzazi,au mtoto,anaweza kukaa na watoto akiwa uchi au wewe unaweza kukaa uchi mbele ya wanao? sasa wewe mtu yuko uchi mbele ya watu wewe unatetea wewe vipi?Baada ya anguko wazazi wetu wa kwanza waliona aibu leo watu hawana aibu Mungu aliwashonea mavazi ya ngozi kwa kusitili miili ya akina adamu na hawa unafikili Mungu angetaka kuwavika mavazi ya trans parent ambayo dada zetu leo wanavaa mbele ya jamii bila aibu ngugu zangu wasomaji mimi nataka kuwaeleza kuwa mavazi yana sehemu kubwa kumtambulisha mtu kuwa yeye ni nani mfano kwa mavazi tunajua kuwa huyu ni police,mwanajeshi,mgambo,pia kwa mavazi tunajua huyu ni changu doa,malaya,kahaba,nk sasa yesu anasema iweni nuru ya dunia,mwanga,chumvi unafikili kwa mavazi haya ya kikahaba nuru yetu itawaangazia watu wasioamini na bado biblia inasema kimujacho mtu ndicho kimutokacho watu wanao vaa mavazi wakiwa nusu uchi wanapenda dunia,tamaa,anasa watu wa namna hiyo ni adui wa Mungu
  balikiwa nyote

 51. Lenda,

  Mistari uliyosema kuhusu suruali ni kwenye lugha zingine hakuna neono ‘suruali’, ispokuwa linapatikana tu kwenye Kiswahili. Hapakuwa na snaa ya vazi la suruali wakati hayo maagizo yanatolewa, waliotafsiri Kiswahili walitafsiri hilo vazi linalosemwa kulingana na utamaduni waliokuwa nao wakati wanatafsiri.

  Kuongelea suala la mwanaume asivae mavazi yampasayo mwanaume ni kupoteza muda katika zama hizi. Kanisa halijengwi na watu wanaotoka kwenye ”single culture” kwa jinsi ya mwili. But maelekezo mengi ya agano la kale yalikuwa ya ”single culture’ (waebrania)

  Ninachoweza kusema kuwa ni kosa kwa huyo dada ni kule kutokumbuka kuchukuliana na watu ambao ni dhaifu wa imani, watu wachanga, wasioweza kula mifupa, ispokuwa maziwa. Ninachosema hapa ni kwamba inawezekana hilo vazi halikubaliki au siyo utamaduni wa jamii aliyosimama mbele yake na hilo vazi katika tukio la namna ile.
  Kwa walio wanyoofu mioyoni mwao hilo vazi hata haliwezi kuwakosesha mioyoni mwao.

  Mavazi yanayositiri si mavazi yanayoficha mwili, bali ni mavazi yanayokubalika kuvaliwa mahali yalipovaliwa.
  Swimming costume ni vazi linalokubalika beach au kwenye kuogelea, lakini suti siyo vazi linalokubalika kwenye kuogelea. Suti inakubalika kwenye harusi, lakini fulana na bukta au kaptula zinakubalika uwanja wa michezo.
  Huko ndiko neno ‘mavazi yenye kusitiri’ linakomaanisha.

  Mungu kawaita watu wa jamii, lugha, kabila, na tamaduni mbalimbali wawe kanisa.
  Hajawaagiza wavae kama kabila au wawe na utamaduni wa kabila fulani.
  Mchina atavaa kama mchina, mmasi kama mmsai, mjapani kama mjapani, myahudi kama myahudi, mhindi kama mdindi, n.k

 52. Asante mtumishi kwa maelezo yako,
  mimi nasisitiza cha msingi hapa nikuangalia je nimevaa vazi la kunisitiri mwili wangu? na je nimejipamba kwa nje na ndani?
  kujipamba kwa ndani ni kuweka ndani ya moyo wako yale mungu anayotaka na ya kumpedeza, maana sisi ni mabibi arusi na yeye bwana arusi akukute umejipamba na upendo,huduma yako kama ni
  mch,muinjilisti,nabii,mwalimu,mtume ziwe hai zichochewe ili zifanye kusudi la mungu,kusamehe,karama zote yaanimapambo ya mungu yako mengi ,kama unajipamba nje lakini mwako halafu moyo wako umejaa chuki,huchochei karama za mungu , kila takata iko ndani mwako ambazo si pambo la mungu, mpendwa utaachwa siku ya bwana arusi kuja kutuposa, !!!!

  barikiwa.

 53. MWONEKANO AU TABIA NDIYO BORA

  BIBLIA MWONEKANO WA MAVAZI NA TABIA

  “VIVYO HIVYO WANAWAKE NA WAJIPAMBE KWA MAVAZI YA KUJISITIRI, PAMOJA NA ADABU NZURI, NA MOYO WA KIASI; SI KWA KUSUKA NYWELE,WALA KWA DHAHABU NA LULU, WALA KWA NGUO ZA THAMANI;
  1 TIMOTHEO 2:9

  FUNGU HILO LINAHITAJI VYOTE TABIA NZURI NA MAVAZI YAFAAYAO KADILI LILIVYOELEZA.

  “WAKIUTAZAMAMWENENDO WENU SAFI, NA WAHOFU.” 1 PETRO 3:2

  “KUJIPAMBA KWENU KWENU,KUSIWE KUJIPAMBA KWA NJE,YAANI,KUSUKA NYWELE; NA KUJITIA DHAHABU, NA KUVALIA MAVAZI;BALI KUWE UTU WA MOYONI USIOONEKANA, KATIKA MAPAMBO YASIYOHARIBIKA;YAANI ROHO YA UPOLE NA UTULIVU,ILIYO YA THAMANI KUU MBELE ZA MUNGU.” 1 PETRO 3:3-4

  MAFUNGU HAYA PIA YANASEMA YANAHITAJI UVAAJI BORA NA TABIA NZURI

  “MWANAMKE ASIVAE MAVAZI YAMPASAYO MWANAMUME, WALA WMANAMUME ASIVAE MAVAZI YA MWANAMKE; KWA MAANA KILA AFANYAYE MAMBO HAYO NI MACHUKIZO KWA BWANA,MUNGU WAKO.” KUMB.22:5

  SURUALI
  BIBLIA INAZUNGUMZA JUU YA WANAUME KUVAA SURUALI. SIJAONA WANAWAKE.
  KUTOKA 28:42

  “NAWE WAFANYIE SURUALI ZA NGUO YA KITANI”
  KUTOKA 39:28

  “….NA HIZO SURUALI NGUO YA KITANI NZURI ILIYOSOKOTWA”
  EZEKIEL 44:18
  WATAKUWA NA VILEMBA VYA KITANI JUU YA VICHWA VYAO NAO WATAKUWA NA SURUALI ZA KITANI VIUNONI MWAO;”

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s