Toba ya kweli ni Ipi Haswa?

toba

Amani ya Bwana iwe daima nanyi enyi nyote,

Hapa SG kuna Neema/Karama/Vipaji/ Akili/ Huduma/Uzoefu/ Ufunuo na NENO KWELI KWELI toka kwa Bwana ndani ya Washirika wa Kanisa hili, nina hakika umekua unajifunza mengi na hata nawe kufundisha mengi na hata leo pia utadaka matamu sana na pia hata kufurahi na kuchekeshwa unapo fellowship sana hapa, raha kweli humu Watu tulio nao.

Maswali ya kuchangia/Muongozo

…..Je, mtu anaweza kutubu dhambi zake kimya kimya au ni lazima aje hadharani kuzisema na kukiri kwa majuto? ?

…….Je, toba ipi yenye nguvu, ile ya kutaja na dhambi ulizofanya aidha ukiwa mwenyewe chumbani au hadharani unatubu au hata kusema tu ” umekuja  kwa kua unataka kutengeneza na MUNGU” anaona NIA yako, yatosha?

……. Je  Ni lazima uende kwa Kiongozi wa kanisa ili kutubu dhambi? Au maliza mwenyewe kivyako-vyako kama Mwana wa Mungu sawa tu na Kiongozi yoyote maana wote tu Wana, hakuna aliye Mwana zaidi au kupendwa kiuspesheli?

….. Au ni ile ambayo ukishatubu, iwe kivyako chumbani au umeenda kwa Kiongozi wa Imani/Dini, uwe umetaja au la, bali muhimu ni utakavyoiishi baada ya Toba?

……Kama ni ivyo, basi inakuaje Toba kweli kweli unafanya kisha siku nyingine lazima kufanya/jitakasa tena na kila leo kujitakasa/kutubu kadri tuinapo SIKU ILEE yaja upesi maaan imeandikwa..”’Mtakatifu ana azidi kua Mtakatifu-simply means-kujitakasa…..

Karibuni mlete shule na kwa kweli hii mada ni sawa kweli kwamba yataka mawazo na michango huru kwa kadri ujuavyo uwe huru tu kushare, haina shaka lakini pia kwa jinsi ilivyo, hasa nondo  za Neno na Ufafanuzi wake itasaidia sana kujua Ki-Biblia TOBA YA KWELI ni ipi haswa.

Press on,

Edwin Seleli

Advertisements

3 thoughts on “Toba ya kweli ni Ipi Haswa?

 1. Huwezi KUTUBU kama hujui kosa, na TOBA ni ile hali ya ki-elimu ya kutambua kuwa umekosea, sasa TOBA ni ile hali ya kujutia kwamba umekosea. Kutoka kwa Torati kuja kwa Kristo Yesu, toba ilibadilishwa kutoka ktk damu (Pesa ya kununulia msamaha) na kuwa ktk Neema. Sahihi ni kwamba, ukiwa ndani ya Yesu, HAKUNA DHAMBI, humu ni ndani ya Miliki ya Bwana mmoja (Ufalme wa Mungu), ambae amewakomboa wale wote ambao wanamkubali, hii sasa huitwa NEEMA, yaani kabla hujakosa ushasamehewa, hivyo HUNA SABABU YA KUTENDA KOSA kwani KOSA linakuwa halina nguvu juu yako. Warumi 6:22-

  Kidogo, ni ngumu kuielezea hata mtu kuielewa, lakini ntajaribu kutoa mfano ambao Bwana mwenyewe ametaka tujifunze leo kuhusu MSAMAHA. Luka 15:10-24 Ktk mfano huu, Bwana ametuletea kosa ambalo si la kawaida (Kijana aliamua kumuua babake kwaajili ya mali zake ili tu aingie kwenye urithi, yaani aweze kujiamulia yeye mwenyewe juu ya mali ya babaake ambae ilimbidi ‘afe’ kwanza ili yeye aweze fanya ufuska wake kwa raha zake !) kwa ukubwa wa hili KOSA, MSAMAHA sio kitu rahisi kupatikana.

  NENO linasema, Luka 10:17-19, ‘Alipo zingatia moyoni mwake’ akasema…….. ……. :18: Nitaondoka na kwenda kwa baba yangu (aliekuwa babayangu) na kumfahamisha kuwa …… …… :19:….. …. :20: Akaondoka …. alipokuwa angali ……
  Ukiutafakari mfano huu ktk Roho, utaona jinsi huyu baba alimvyo mchukia huyu mtoto kwa ule uovu wake na kutokuwa na fadhila kwake kwa jinsi alivyompenda na kumhudumia ktk maisha yake yote na hatimae yule kijana akautamani uhai wake ‘ili apate kuwa huru’ na utaona kwa miaka mingi alivyo kaa kwa ‘raha’ bila ya yule ‘nunda’ wakistarehe pamoja na yule kijana ‘mtiifu na kipenzi chake’.

  Lakini ghafla, hali ya baba ilianza kubadilika, alianza kummiss yule ‘nunda wake’, yule alie mlaani na kufarijika kwa kuondoka kwake ktk ‘familia’ yake, yule alietamani bora akafie mbalini, akawa hana raha juu yake akijijutia akihisi kwamba ni ‘yeye ndie aliemfanya kijana wake apotee’!! Je!? ninini kiliweza kuubadili moyo wa huyu mzee!? Jibu liko ktk sura ya 17 hadi 19 ! Msamaha (wakweli) hakuna yeyote anaeweza kuukataa, msamaha ni tabia (character) ya Mungu, kila tunapokuwa na Roho ya Msamaha tunafanana na Jehovah Yahweh.

  Toba ya kweli ni kumjua Mungu wetu na makusudi yake kwetu hivyo SHERIA yake itakuwa ni maisha yetu na Damu yake itakuwa ni ya thamani ktk maisha yetu.

  Asalaam aleikum.
  Jackson Mulele.

 2. Mungu akubariki mpendwa Edwin Seleli kwa somo hili,ninaamini nitajifunza mengi kupitia walimu tunao hapa.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s