Ombea Taifa la Israel!

israelii

Shalom,

Ombea Israel,

1. Omba ulinzi na amani juu ya Israel hasa wakati huu kuna tension kubwa sana baada ya kupatikana miili ya watoto watatu waliotekwa na kikundi cha kigaidi cha kiislamu,  Waziri mkuu wa Israel amesema hao magaidi watalipa kwa kitendo hicho, na sasa Israel imeshaanza kurusha rocket kuelekea Gaza.

2. Omba kwa ajili ya familia ambazo zimepoteza hao watoto Mungu awafariji na pia awape roho ya msamaha na pia kwa taifa la Israel maana imekuwa ni majonzi makubwa huku, Mungu aipe hekima serikali ya Israel hasa wakati huu.

3. Ombea ulinzi juu ya Jerusalem hasa kwa wayahudi kila wakati wanapoenda temple mountain inatokea vurugu kutoka kwa waislam.

4. Pia kuna kikundi cha kigaidi kingine kimeibuka Iraq kilikuwa pamoja na al Qaeda na sasa wamejitenga na inasemekana kuwa ni radical kuliko al Qaeda kinaitwa ISIS itakuwa umeshakisikia kimeteka baadhi ya miji Iraq na sasa inasemekana kuwa lengo lao ni kuteka Jerusalem. Omba ulinzi juu ya Israel na kila lengo la adui lisifanikiwe juu ya Israel.

Unaweza kunukuu maandiko haya Zaburi 121, 122:6-7, Isaya 31:5, Isaya 62:1.

5. Ombea Mungu ainue waombaji wengi watakao simama na kuomba kwa ajili ya Israeli hasa kutoka Tanzania. Isaya 62:6-7.

Mungu awabariki,

I will bless those who bless you, and whoever curses you I will curse; and all peoples on earth will be blessed through you.” Genesis 12:3

Blessings,

–Grace

Advertisements

44 thoughts on “Ombea Taifa la Israel!

 1. Ni muda mrefu sijaingia kwenye blog hii, miaka 3 imepita ndio nimeingia kwa mara ya kwanza baada ya kipindi hicho, nimesoma niliyoyasoma katika mada hii, lakini sitachangia chochote, napita tu

 2. Sungura,
  Uliponiambia kuwa:
  “Unatoa analysisi amabazo si yakinifu kiuchambuzi, labda unazitoa kwa kudhani kwamba kila msomaji hapa anayatazama mambo sawa na wewe unavyoyatazama.”

  Kwa kiasi fulani ninalikubali jambo hilo, ni kweli yawezekana akawepo mkristo ambaye hajui lolote kuhusu hayo mambo, kwahiyo nimefurahi kukuona ukiliweka sawa jambo hilo na ninakutegemea kwamba wewe sasa katika somo hili ulilolipanua, utalikamilisha kwa kuja na “analysis yakinifu kiuchambuzi”; perfecto!

  Ninaamini una uelewa mkubwa ktk haya unayoyaongelea. Basi kwa kadiri ya maelezo yako kuhusu kanisa, kwamba ndio huo Mwili wa Kristo, nasi tukiwa ndivyo hivyo viungo vya Mwili huo; hebu niambie, Siyi ni kiungo kipi na Papa naye ni kiungo kipi ktk huo Mwili wa Kristo?

  Nakushukuru kwa kujitoa kwako kutupa uelewa wa mambo ya msingi!

  Gbu!

 3. Asante kaka sungura nazidi kuiva! roho huyo azidi kutulisha maziwa yasiyogoshiwa!!

  be blessed.

 4. Lwembe,

  Unatoa analysisi amabazo si yakinifu kiuchambuzi, labda unazitoa kwa kudhani kwamba kila msomaji hapa anayatazama mambo sawa na wewe unavyoyatazama.

  Kusema kwamba Israel Mungu anashugulika nao kama taifa, na wakristo anashughulika nao kama ‘individual’ halafu ukakomea hapo, ni uchambuzi wenye fikra nyepesi sana rafiki yangu.

  Kama ulikuwa umesahau, sasa nakukumbusha kuwa kanisa pia ni taifa linaloitwa mwili wa kristo. Kwa hiyo Mungu anapolitazama kanisa anaona mwili wa kristo, hamuoni Lwembe. Kama ambavyo makabila ya waebrania ynatengeneza Israel taifa, ndivyo ambavyo mkristo mmojammoja anatetengeneza taifa linaloitwa mwili wa kristo/kanisa.

  Kwa Isreal yanaitwa makabila, kwa kanisa tunaitwa viungo vya mwili wa kristo ambavyo kwa pamoja vinaitwa au vinafanya kanisa.
  Kama ambavyo bila hayo makabila kuja pamoja hakuna Israel kama taifa, ndivyo ambavyo hakuna kanisa/mwili wa kristo bila kuwepo wakristo/wafuasi wa Yesu.

  Hizi nadhalia mbili zina sura mbili tofauti. Israel kama taifa nadhali yake iko kimwili, na ya kanisa kama taifa ina sura ya kiroho.

  Tena kwa kujua kwako kuwa kuna wakati/kipindi cha kanisa na kipindi cha Israel, ambapo kipindi cha Israel kinakuja baada ya kipindi cha kanisa kumalizika, ulipaswa kwa urahisi kabisa kujua kuwa hivyo vipindi vilishaamuliwa. Havihitaji mwingilio au uhusika wa mwanadamu ili viwepo.

  Au huwa mnaiombea nini Israel, iwe na amaniau iwapige zaidi wapalestina? Mnadhani bila maombi yenu Israel inaweza kupigwa na maadui au waarabu, au kwa maombi yenu Israel itapata amani? Maombi hayo ni sawa na kumuomba Mungu Yesu arudi kunyakua kanisa.

  Kwa hiyo kuombea Israel mnakokomalia ndio maana nimewaambieni ni sawa na kujipendekeza kwa kitu ambacho hupati nacho faida yoyote, maana uombe usiombe yaliyoamriwa kutokea katika hicho kipindi yatatokea.

  Lakini pia hamtuoneshi mahali ambapo wakristo tumeagizwa kuiombea Israel ili tubarikiwe. Au neno kuitakia amani Israel ninyi mnaona linamaanisha kuiombea Israel. Na ni akina nani walikuwa wanaambiwa hayo maneno, na je ninyi mmo katika hilo kundi la waliokuwa wanaambiwa?

  Vinginevyo kazi sawa na yule anayemlaani aliyebarikiwa, na kumbariki aliyelaaniwa na Mungu.

  Ombeeni kanisa la kristo hilo ndo linahitaji maombi!

 5. HAKUNA BINADAMU MWENYE MAMLAKA YA KUMLAANI MWENZAKE, MAANA SOTE SI WAKAMILIFU NA UKIONA MTU ANALAANI, UJUE ANA KIBURI CHA UZIMA

  WAYAHUDI WA LEO WANAPASWA KUMPOKEA YESU. KAMA AKINA PAULO NA MAKUHANI WALIVYOFANYA. NDIO MAANA PETRO ALIWAOMBEA WAOKOLEWE.

  PAULO ALIKUWA MFARISAYO AKAACHANA NA UFARISAYO
  TUSIIPENDE MEZA YA MAFARISAYO/BALI TUIPENDE MEZA YA YESU
  ATUAMBIA;

  WARUMI 11:8
  “KAMA ILIVYOANDIKWA, MUNGU ALIWAPA ROHO YA USINGIZI, MACHO HATA WASIONE, NA MASIKIO HATA WASISIKIE, HATA SIKU HII YA LEO”

  MATENDO 11:9
  “NA DAUDI ASEMA, MEZA YAO NA IWE TANZI NA MTEGO, NA KITU CHA KUWAKWAZA, NA MALIPO KWAO.”

  MATENDO 26:4
  “KWA MAANA WAYAHUDI WOTE WANAJUA MAISHA YANGU TANGU UJANA, YALIYOKUWA TANGU MWANZO KATIKA TAIFA LANGU HUKO YERUSALEMU. WAKINIJUA SANA TANGU MWANZO, KAMA WAKIPENDA KUSHUHUDIA, YA KWAMBA NALIKUWA FARISAYO KWA KUIFUATA MADHEHEBU YA DINI YETU ILIYO SAHIHI KABISA.”

  MAFARISAYO WALIONA PAULO KAMA ALIACHA KITU SAHIHI/UFARISAYO NA KUMFUATA YESU WAKIDHANI AMEPOTOKA.

  ANATUAMBIA HIVI;

  WARUMI 11:1
  “BASI, NAULIZA, JE! MUNGU ALIWASUKUMIA MBALI WATU WAKE? HASHA! KWA KUWA MIMI NAMI NI MWISRAELI, MMOJA WA WAZAO WA IBRAHIMU, MTU WA KABILA LA BENJAMINI.”

  MUNGU HAKUWASUKUMIA MBALI WAISRAELI KATIKA AGANO JIPYA, ANAWAITA PIA, PAULO AMEACHA UFARISAYO NA KUIPOKEA NEEMA YA KRISTO/AKAWA MKRISTO. MAKUHANI WALIACHA UKUHANI KATIKA HEKALU LA MIKONO WAKAIPOKEA IMANI

  MATENDO 6:7
  “NENO LA MUNGU LIKAENEA; NA HESABU YA WANAFUNZI IKAZIDI SANA KATIKA YERUSALEMU; JAMII KUBWA YA MAKUHANI WAKAITII IMANI ILE.”

  BASI TUWE MABAKI TULIOCHAGULIWA KWA NEEMA YA MUNGU

  WARUMI 11:5
  “BASI NI VIVI HIVI WAKATI HUU WA SASA, YAKO MABAKI WALIOCHAGULIWA KWA NEEMA.”

 6. Sungura,

  Israeli wa kimwili na wa kiroho, usijidanganye kwamba wewe utawatambua! Hata wao wenyewe sidhani kama leo hii wanajitambua kwa makabila yao yale 12, sembuse hayo ya kiroho na kimwili! Bali Mungu anawajua wote, tena kwa makabila yao!!!

  Basi kwa kadiri ya Neno lilivyotufikia, tumelipokeo hilo kwa Imani, hatujawahi kumuona Kristo, wala mitume wake. Basi sisi kwa upande mmoja huwajibika kwa hilo Neno, tukilichukua kama lilivyo, na Mungu naye huwajibika kwa hilo hilo kwa upande wake. Kama alisema ukimbariki Israeli utabarikiwa, tena aliyasema hayo wakati Israeli akipita akipigana, ktk nchi ambazo si zake bali Mungu ndiye aliyemuahidi kumpa bila mashauriano na hao wenye nchi! Yaani maana yake ni kwamba Israeli wakikufikia, ktk hiyo sehemu unayodhani ni yako, wakakuambia kuanzia sasa utakuwa chini yetu, basi unatakiwa uwape kwa furaha! Hayo ndio mambo ya Mungu, hayana demokrasia!!!

  Baraka za Kanisa kwa Mataifa hazipimwi kama Israeli ambao wao huhesabiwa kama taifa, huku ni mtu mojammoja, jiweke moyo wako safi, unaweza kula bingo kwa kuwabariki tu!!

  Kuhusu kumuombea Kaini, jambo hilo haliwezi kulinganishwa na Israeli. Kaini alilaaniwa, Israeli alipofushwa kwa kusudi la mimi na wewe tupate wokovu, huo ambao Lenda hautaki kwa leo mpaka huko Hukumuni, ambako sijui ataupatia wapi, maana wote wenye kuukataa Wokovu, watasimama ktk Hukumu wapimwe ktk mzani wa Haki!

  Kuhusu majuma sabini ndg yangu, nilikuwa namjibu Lenda, maana wao kulingana na manabii na walimu wao, waliviendea hivyo vitabu vya kinabii kuufungua huo nje ya wakati alioukusudia Mungu. Haya majuma sabini ni yale unayoyakuta ktk kitabu cha Daniel, hayo ndiyo yanaelezea Hali ya Israel kimwili na kiroho kwa ukamilifu. Yaani Israeli hawawezi kuwa chochote kile nje ya hayo majuma sabini! Ili Israeli hao taifa waondoke ktk Hesabu ya Mungu basi inabidi hayo majuma sabini yawe yamekamilika, na baada ya hayo majuma hakuna tena Injili, ndio maana walimu wa Lenda walibugi hesabu, maana ghafla Israeli imeibuka kama “mzuka wa Samweli”, na sasa wanalazimisha mambo kwa kujitia upofu wa Maandiko, wakiyatafsiri kwa kuyapapasa ili tu kulinda heshima yao!

  Lakini hesabu yake iko wazi, kama unataka kuikagua na hiyo uliyonayo si vibaya, nitaileta kwa kifupi tu compare notes, maana hiyo ndiyo inayomleta Kristo!

  Kuhusu kuwahubiri Wapalestina, mbona wako wakristo wengi tu, pia lazima ufahamu kwamba wakristo wa “kutengenezwa” huwa hawafiki popote, yaani usijikoki kuombea tu bila Maarifa, kama unataka kuombea taifa, we ombea Israeli, usipobarikiwa bishabna na Mungu mpaka akutimizie; lakini kuombea Mataifa, subiri Mungu akuoneshe wa kumuombea: “Mtu haji kwangu asipovutwa na na Baba”; usijivutie watu ovyo, wanawea kukuzidi nguvu wakakuvutia huko kwenye “njia pana”!!!!

  Otherwise acha ubishi wa akina Siyi, wenzako wamepelekwa maporini, shauri yako, hujamsoma Fred; “Njia iendayo……”

  Gbu!

 7. Fred,

  “NJIA IENDAYO KUZIMU NI PANA NA WAENDAO NI WENGI.”

  Sisi tunataka sana kupona, hebu tuletee basi maelezo ya maswali haya uliyoyauliza ili yatusaidie kuikwepa hiyo njia pana, maana kuzimu si mchezo! :
  1. Myahudi ni nani?

  2. Israel ni nani?

  3. Wanajiita wayahudi kumbe siyo bali ni wa sinagogi la shetani ni kina nani?

  4. Ni maana ya NJIA , KWELI NA UZIMA?

  5. JE NI KWA KIASI UNAJUA KUHUSU MIPANGO YA NEW WORLD ORDER? NI MADHARA YAKE KWA KANISA? JE WEWE UNAFANYA NINI JUU YA HAYO?

  6. NI NANI ALIANZISHA MTANDAO WA KIGAIDI?

  7. JE, UNAJUA MTAZAMO WA WANANCHI WA KAWAIDA WA ISRAEL, PALESTINA NA IRAN?

  8. JE NI KINA NANI WALIANZISHA ILLUMINATE? JE NI KWA KIASI WANAATHIRI MAISHA, MIENENDO, NA HATIMA YA MATAIFA YOTE DUNIANI?

  9. NINI KIFANYIKE KUPAMBANA NA UOVU UNAOENEA DUNIANI? NINI NAFASI YA MKRISTO KATIKA HAYA?

  10. JE NINI MAANA YA HUKUMU KUANZA KATIKA NYUMBA YA BWANA?

  Karibu sana kaka!

 8. Lenda,

  Inaweza kukuchukua eternity kuijua Injili ilipogawanyikia, na pia kuupata muktadha wa mawaidha unayoyasoma ktk Agano Jipya, haswa kuhusu Israeli! Mungu anapokuambia kwamba fulani nimempofusha, basi utakuwa ni mtu wa ajabu sana kumtegemea mtu huyo kuona! Vinginevyo ukimuona anaingia barabarani, unamsaidia kumpitisha njia isiyo na magari mengi! Hali inakuwa hivyo mpaka siku Mungu atakapomfungua kutoka kifungo hicho cha upofu, kama aliahidi, ambavyo ahadi ya kuondolewa upofu Israeli wanayo; Lakini sina uhakika kama Mataifa tunayo ahadi ya kuondolewa upofu tuliojitakia kwa kung’ang’ana na mafundisho yasiyoeleweka!!!

  Vifungu ulivyo vinukuu, ni mahubiri ya wokovu kwa watu wa Mataifa, mitume wakiwaonesha kukubaliwa kwao na Mungu katika Njia ya Kristo na si kwa Sheria, kama Israeli. Ndio unaona wanazungumzia tohara ya rohoni badala ya ile ya mwilini kama huko kwenye Torati, ambako wanaendelea na jambo hilo hata leo, wakijibidiisha katika Sheria, Amri na Hukumu zake, wakiendelea ktk utando!

  Mungu alipokishughulika na Israeli, hakushughulika na watu wa Mataifa! Ni makundi aliyoyagawa kulingana na Mpango wake wa Wokovu, ni muhimu kwako kuliona jambo hili kama lilivyo badala ya kutembea gizani. Ndio maana unawaona mitume wakitangaza KUWAGEUKIA Mataifa! Basi sisi tuliogeukiwa twapaswa tufahamu hivyo, maana kama lilivyo hili Neno la kugeukiwa kwetu, ndivyo lilivyo na Neno la kurejewa kwao hao walioachwa! Mungu ni Mwingi wa Rehema!!!!

  Haya ndio makundi mawili ya Mungu; Kanisa na Israeli, kila kundi lina wakati wake. Alianza na mwalimu akampa Sheria, hizo Amri na Hukumu zake. Akatuonesha kupitia huyo mwalimu jinsi ya mambo hayo yote, ktk kuyatii na faida zake, na uvunjifu na Hukumu zake; na mwisho alipowapofua, akawahukumu kwa waliyoyafanya ktk huo upofu, ikiwa ni jinsi ya mambo tunayoyaendea nasi kwa kujitia upofu wa makusudi; Basi kama kwa Israeli, lile neno walilolinena ktk huo upofu, hapo walipomng’ang’aniza Pilato amtoe wamsulubishe, wakapiga kelele, “Damu yake na iwe juu yetu na watoto wetu”, kweli ndivyo Mungu alivyowatimizia, mpaka hao milioni sita wa holocaust ni ktk ahadi yao waliyoiweka ktk huo upofu!!!!

  Ni kutokana na mambo kama haya, ambayo yatatufika nasi tusipokuwa wepesi wa kuyasikiliza na kuyaamini Maandiko kwa kadiri yanavyojifunua; itatufaidia sana iwapo tutayaacha yatufundishe na kutuondolea makengeza ya dini!

  Kama ambavyo sisi tuna Ahadi ya Kristo kulijia Kanisa, wao pia wanayo Ahadi ya Masihi, alipowajia Hawakumtambua, hivyo wangali wanamsubiri! Lakini Kanisa linafahamu kwamba wanayo Ahadi ya Kurejewa. Ndipo wakati wa Mataifa unapokwisha, Lk 21:24 “… na Yerusalemu utakanyagwa na Mataifa, hata majira ya Mataifa yatakapotimia”, watarejewa tena, na safari hii WATAMTAMBUA!!!

  Ni furaha iliyoje kwa Kanisa linalomngojea Masihi, maana linajua kuondoka kwake ndiko kurejewa kwao, hivyo hukesha LIKIWAOMBEA Israeli, Mungu awape uvumilivu, kwa pamoja “likiinua mikono yake juu” kama ilivyokuwa kwa Musa huko jangwani, kila Israeli inapoingia vitani na Wafilisti wa leo! Sisi tukiwa nuruni kuliko wao, je hatuna wajibu kwa Israeli???? Labda kanisa lililo gizani, maana Haki ya kanisa lililo gizani ni sawa na ile Haki ya Mafarisayo!!!!

  Gbu!

 9. Nicky,
  Narejea makala yako ya tar.16/07/2014, nilibanwa na mambo mengine nikawa siwezi kujibu.

  Kwanza nikupongeze kwa jinsi ulivyojitahidi kuisema historia na matukio ya Taifa la Israel. Umeeleza pia umuhimu (significance) wa Israel katika dunia hii. Ispokuwa nachelea kusema kwamba ni rahisi sana kunukuu andiko na kulipachika ukidhani kwamba uko sahihi katika kuuelezea utimilifu wake, just kwa sababu hilo andiko lipo limendikwa na litaendelea kuwa hivyo hivyo kama lilivyoandikwa.

  Msingi wa mada hii siyo umuhimu au nafsi ya Israel na matukio ya kinabii yanayolipata hilo taifa, ispokuwa msingi ni suala la kuliombea hilo taifa, hapo ndipo kuna mkanganyiko mkubwa na watu wengi wamedanganyika sana.

  Kwanza elewa kuwa sala zako haxziwezi kubadilisha unabii au utimilifu wa kile ambacho Mungu ametamka kuwa lazima kitimie, kiwe kizuri au kibaya. Maombi yasingeweza kwa mfano, kubadili unabii wa Israel kutawanyika katika mataifa mbalimbali, kama waliomba basi walipoteza muda.

  Kwanza jiulize; unatimiza agizo gani unapoombea Israel leo, wapi umeagizwa kuiombea Israel?

  Pili jiulize; Israel ni nani na kanisa ni nani na uhusiano wa Israel na kanisa ni upi?

  Tatu jiulize; Ni baraka gani kanisa limeahidiwa kuipata kwa kumwombea Israel wa mwilini?

  Nne jiulize; Israel wa mwilini yuko katika zamu ipi ya unabii wa Mungu leo, na wewe una nafasi gani katka hiyo zamu yake, na ni wapi Mungu kakuagiza umfanyie maombi Israel katika hii zamu yake?

  Tano jiulize; Ni wapi katika mitume/ katika agano jipya kanisa linapewa agizo la kuombea Israel kama linavyosisitiza leo?

  Ukiweza angalao kunijibu hayo maswali machache utakuwa umejenga msingi imara sana.

  Lakini cha ajabu, nauona unyonge mwingine wa kiufahamu katika ufahamu wa ndugu Lwembe, hata siwezi kuamini kama anamaanisha anaposema mambo ambayo kwa msomi yeyote wa maandiko mwenye ufahamu sahihi anaweza kuyaelewa kirahisi kabis.

  Lwembe anaongea habari ya majuma sabini bila hata uchambuzi wa kina kuwa hayo majuma sabini yalikuwa kitu kingine tofauti na muda wa siku saba unaotengeneza juma moja.
  Mtu anayewasilisha uchambuzi wa namna hii kimantika anakuwa amekosa uhalali wa kuaminiwa katika kile alichowasilisha

  Huku ndiko kule kutumia maandiko bila kujua wakati wa kutimia kwake alimradi tu mpaka kesho yenyewe yataendelea kusomeka hivyohivyo.

  Kwa mfano: Andiko linaposema ”nawe utazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu……” Liko hivyohivyo tangu lilipoandikwa na litaendela kusomeka hivyohivyo mpaka mwishowa dunia.
  Sasa asiyeelewa maana yake na utimilifu wake ni lini ataendelea kusubiria mwana kuzaliwa, bila kujua kuwa alishazaliwa na kinachoendelea sasa ni kingine kabisa kuhusu huyo mwana.

  Lwembe hebu tuchambulie basi pia kuwa ilipofika juma ya 69 majuma yalisimama kwa Israel, na utuambie ina uhusiano gani na kuiombea Israel?

  Na nimalizie kwa kusema kuwa, watu wengi hii mada mnairukia mkiwa mmejaa mitazamo ambayo siyo kitu tunayojadili hapa.
  Kwa mfano hapa hatujadili kama Israel ndio kalenda ya dunia au la, bali tunajadili kuhusu kuiombea Israel kama tunavyosisitizwa leo.

  Kama Israel ndio kalenda ya dunia, je ni kwa sababu hiyo tunatakiwa kuiombea, na je hivyo ndivyo tumeagizwa?

  Lwembe kama ulivyosema habari za kumwombea Kaini vile ambavyo ingekuwa ni kazi bure, ndivyo hivyohivyo kuiombea Israel ni kazi bure, maana ilivyotamkwa na Mungu kuwa itakuwa juu ya Israel ndivyo itakavyokuwa, auombe ama usiombe.

  Ombeeni wapalestina wamjue kristo, maana wao wako katika fungu la mataifa kama mimi na wewe, wala tusipoteze muda kujipendekeza kwa Israel, maana hata wakristo ki mwili kwa mwisrael hawana tofauti na mpalestina!

  Maombi yenu kwa Israel ni sawa na kazi bure, hayatabadilisha chochote, zaidi sana mnafanya kazi ya kujipendekeza ambayo pia haiwaongezei kitu chochote kile!

 10. Napenda kuandika kwa msaada wa Bwana Yesu,
  ninashukuru kwa wote walwe waliochangia mada kama inavotakiwa, naunga mkono mada hii kwa 100%.
  Israel ndiyo dira/kalenda ya maisha ya kiimani hapa duniani, utake usitake. Na pia Mungu huwa si mbabaishaji, akiahidi ameahidi. Alishawaahidi waisrael kuwa ndio taifa lake na ahadi hiyo haiwezi kubadilika kamwe. Maadui watapigana na israel lakini kamwe hawatawashinda wana wa israel! Mungu mwenyewe alishasema ukiiombea/kuibariki israel nawe atakubariki lakini ukiwalaani wana wa israel/israel kama taifa nawe Mungu atakulaani, that’s all!
  Tunapaswa kuwaombea sana sana wana wa israel na taifa lao kwa ujumla katika mapambano dhidi ya maadui zao!
  Tubarikiwe katika jina la Yesu Kristo, ameen.

 11. Ndugu Lwembe,

  Hakika wewe ni mtu wa ajabu sana. Mimi sijamtishia mtu yeyote na kama umetishika basi ni ushahidi tosha wa ukweli wa nilichokueleza.

  Lakini pia umethibisha kwamba kumbe hujajiandaa kwa kazi uliyoandaliwa. Kinachokupa ujasiri wa kuendelea kuandika ni ulevi wa sifa ambazo umekuwa ukipewa na vipofu wa imani.

  Narudia tena wewe ni mpotoshaji na nabii wa uongo , narudia kukusihi acha mada hii maana kadiri unavyozidi kuandika unapotosha wengi.

  Hivi mtu mwenye uelewa wa kutosha anaweza kuthibitisha kwamba yeye si mvivu kwa kutembelea website niliyoweka? ACHA UTANI KAKA!

  UNASEMA MTU MZIMA HATISHIWI NYAU, HIVI UNATHIBISHAJE UTU UZIMA WAKO HAPA?

  MASWALI UNAYOULIZA HAYANIHUSU KWA KUWA HATA HUJUI NINACHOAMINI JUU YA MPANGO WA MUNGU KWA ISRAEL HALISI.

  UTAJITAFUTIA HUKUMU KWA MANENO MENGI YASIYO NA TIJA KANISA NA ULIMWENGU HUU. WEWE NI SEHEMU YA TATIZO NA UNAHITAJI MSAADA ILA KWA SABABU HUJITAMBUI MUNGU TU KWA NEEMA YAKE ATAJUA NAMNA YA KUKUSAIDIA.

  IKIWA UTAPATA AMANI KUSIKIA KUTOKA KWANGU ILI KUTOHUKUMU USICHOJUA BASI NIPIGIE SIMU 0762 183 361.

  NJIA IENDAYO KUZIMU NI PANA NA WAENDAO NI WENGI.

  MWENYE MASIKIO NA ASIKIE YALE AMBAYO ROHO AWAMBIA MAKANISA.

 12. TUJITAHIDI KUWA MABAKI YA ISRAELI TUTAOKOLEWA, NA HAWA WANAOITWA MABAKI NDIO HUITWA WAISRAELI,NA WOTE HAWA WATAOKOKA.

  WARUMI 9:27
  “ISAYA NAYE ATOA SAUTI YAKE JUU YA ISRAELI, KUSEMA, HESABU YA WANA WA ISRAELI, IJAPOKUWA NI KAMA MCHANGA WA BAHARI, NI MABAKI YAO TU WATAKAOOLEWA.”

  WOTE WANAOMTUMAINI YESU NDIO ISRAELI HAWA, NA HAWA WOTE WAISRAELI KWELI KWELI NDIO WATAKAOOKOKA WOTE

  “MAANA HAWAWI WOTE WAISRAELI WALIO WA UZAO WA ISRAELI” WARUMI 9:6

  “MAANA YEYE SI MYAHUDI ALIYE MYAHUDI KWA NJE, WALA TOHARA SIYO ILE YA NJE TU KATIKA MWILI.” WARUMI 2:28

  KWA NINI YESU ANAMWITA NATHANIELI MWISRAELI KWELI KWELI?

  YOHANA 1:47
  “BASI YESU AKAMWONA NATHANAELI ANAKUJA KWAKE, AKANENA HABARI ZAKE, TAZAMA, MWISRAELI KWELI KWELI.”

  ANASEMA;
  WARUMI 11:26
  HIVYO ISRAELI WOTE WATAOKOKA; KAMA ILIVYOANDIKWA, MWOKOZI ATAKUJA KUTOKA SAYUNI; ATAMTENGA YAKOBO NA MAASIA YAKE.

  WARUMI 11:27
  “NA HILI NDILO AGANO LANGU NAO NITAKAPOWAONDOLEA DHAMBI ZAO.”
  BASI TULIKUBALI AGANO JIPYA LA KAFARA YA YESU MSALABANI TUOKOLEWE
  “ANGALIA, SIKU ZINAKUJA, ASEMA BWANA, NAMI NITATIMIZIA NYUMBA YA ISRAELI NA NYUMBA YA YUDA AGANO JIPYA;”

 13. Fred,

  “Mtu mzima hatishiwi nyau!!”

  Unaniambia;
  “” Busara ya kawaida inaonyesha kwamba wewe hupendi kujifunza na ni mvivu wa kutafiti na mwepesi wa kutoa majibu bila kufikiri na kuchunguza.”

  Kama ningekuwa mvivu kama unavyosema, basi nisingekwenda kwenye hiyo site uliyoiwekea link! Nimekuambia wazi kwamba huko nimekuta speculations ambazo ni propaganda, hutaki kuelewa; unatutaka wote tuwe wajinga wa kupokea kila upuuzi!

  Acha kulalamika, sijui nimekataa kazi ya Bwana, hivi are you really serious? Kuamini huo uongo wa kidnapping ndio kazi ya Bwana?????

  Mnakuwa wepesi wa kuamini uongo kuliko Kweli ya Injili iliyowazi!!!! Maandiko yanakwambia Israeli watarudiwa na Mungu, na wewe mwenyewe unawaona hao hapo ktk nchi ambayo haikuwepo ktk ramani, leo hii unaiona hapo, sasa ni upofu gani unaowashikilia hata HAMUIONI kazi anayoifanya Mungu kwa Yakobo?

  Hata ukristo wenu ninautilia mashaka, unaonekana ni ukristo pori usio na dira!!!!

  Lete basi hayo masomo, tuone unachokisema ni nini, badala ya kuleta vitisho visivyo na tija, “Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba.” Rm 8:15

  Gbu!

 14. Lenda,

  Vifungu ulivyovinukuu viko hivyo hivyo, yote hayo ni kweli; mkristo, huyo wa Mataifa huyo ambaye alikuwa HANA Mungu, sasa amekirimiwa nafasi ya kumjua Mungu na kufanyika mwana wake.

  Ameyapokea yote hayo si kwa jitihada yake, bali kwa Neema. kwa kadiri ya Mpango wa Mungu. Ndipo ili Neema hiyo imfikie kulingana na Mpango huo, ilibidi Israeli APOFUSHWE macho yake ya kiroho kwanza! Yaani Mungu katika Hekima yake, aliwapofusha hao watu wake, ndipo akatufuata sisi tusio mjua na akajifunua kwetu, akatupa na Imani yake ili kukamilisha jambo hilo.

  Basi ukilijua hili kwamba wewe umemjua Mungu at the expense of Israel, hilo pekee lapaswa likujengee HOFU ya Mungu na si jeuri ya kuwaona hao waliopofushwa kwa ajili yako si kitu! Upendo haushii kusomwa tu ktk Biblia, Upendo ni halisi. Kama ungekuwa na hata chembe ya Upendo, basi wivu ungekukimbia. Tena basi Upendo huo ungekuongoza katika kutafuta HATIMA ya hao waliopofushwa kwa ajili yako!

  Pia kwa taarifa yako, ktk kukupa uelewa, Israeli walipomkataa Masihi wao, waliingia ktk awamu mpya ya kwenda bila Mungu; yaani Torati na Sheria zake vilikuwa vimefikia ukomo! Utakatifu uliotokana na Torati na Sheria, kiini chake, au ulikuwa una revolve around the Temple, humo kulimokuwamo Patakatifu pa Patakatifu. Ndipo kuukamilisha mwisho huo, lilianza Pazia kuraruka, na mwisho alipowajia Titus, alilivunja na kupora vito vyooote, na bishara ya Hekalu ikaishia hapo na wao kutawanyika dunia yote ya wakati huo! Ndio lile Neno la kutawanywa kwao likiwatimilia.

  Neno la wao kurejewa lipo kama nilivyokuonesha, na wao ndio hao hapo katika nchi yao! Israeli ni Taifa la vita, wanayo Ahadi ya Mungu ambayo ni lazima waitimize, hakuna anayeweza kuizuia.

  Basi mtu yeyote anayewategemea hao kuipokea Injili, atakuwa ni mchanga wa Maandiko, hayajui na wala hayaamini! Kwanza wanatushangaa sana sisi na ukristo wetu; wanasema tunaabudu tusichokijua, huyo Mungu wa Israeli tunayemwitia wanasema ni mungu wa kigeni ambaye wao hawawezi kuungana nasi kumuabudu maana sisi tuko ktk ibada ya kipagani, “Mtamkataje Mungu vipande vitatu halafu mseme eti ndiye Mungu wa Israeli?!!!

  Katika kurudi kwao, wangali hawajafanya IBADA, ni lazima wajenge upya Hekalu lao lilipobomolewa, huo msikiti ulio jengwa hapo juu wataubomoa kupisha ujenzi huo, halafu watafanya Ibada tena baada ya miaka 2000, tayari kwa lile juma la mwisho!!!

  Usijidanganye na siasa za dini zenye kupofua, Israeli ni kipenzi cha Mungu, mtumishi wake, amemrudisha ktk nchi ya Ahadi, na anampigania, huo ndio muujiza wa leo!!!

  Gbu!

 15. Ndugu Lwembe,

  Jambo la maana unaloweza kufanya kwa sasa ni kujitenga na mada hii maana wewe ni nabii wa uongo. Hujui lolote kuhusu dunia hii na hata hujui hatari iliyoko. Na naomba uache kumsingizia Roho Mtakatifu kuficha ujinga wako juu ya mambo ya msingi na halisi. JIPIME.

  Busara ya kawaida inaonyesha kwamba wewe hupendi kujifunza na ni mvivu wa kutafiti na mwepesi wa kutoa majibu bila kufikiri na kuchunguza.

  Kwa mtu yeyote utakaye mpotosha kwa kujifanya wajua UTALIPA GHARAMA aliye juu na muumba wa vyote anajua ni kwa kiasi gani.

  ACHA UBISHI NA MUULIZE MUNGU JUU YA VIPAUMBELE VYAKE KWA SASA DUNIANI NA ACHA KABISA MAZOEA KWA MAMBO YA MSINGI.

  HIVI UNAJUA KINACHOENDELEA KATIKA ULIMWENGU HUU? NA UNA FIKIRI MIMI NATEGEMEA MTANDAO KUJUA KWELI? MUNGU AKUSAMEHE SANA NA AKUKIRIMIE NA KUKUPA UFAHAMU NA UJUA WAJIBU WAKO.

  SINA CHA KUKUELEZA MAANA UMEIKATAA HUDUMA YA BWANA NA UNAFUATA MAZOEA UKIDHANI UTAKUWA SALAMA. USIJIDANGANYE.

 16. 1 PETRO 2:9
  “BALI NINYI NI MZAO MTEULE, UKUHANI WA KIFALME, TAIFA TAKATIFU, WATU WA MILKI YA MUNGU, MPATE KUZITANGAZA FADHILI ZAKE YEYE ALIYE WAITA MTOKE GIZANI MKAINGIE KATIKA NURU YA AJABU.

  NA LIFURAHI TAIFA LA ISRAELI KATIKA BWANA WALE AMBAO HAWAKUWA TAIFA BALI SASA WAMEKUWA TAIFA KWA DAMU YA ISRAELI WETU/MPIGANIAJI WETU(YESU) ILI TUBARIKIWE KWA JINA LAKE TUPATE KURITHI,ALIYEPIGANA NA ADUI SHETANI ALIYEUTAFUTA UHAI WETU, AKASHINDA NASI TUKARITHI JINA KAMA WANA WA YAKOBO WALIPORITHI JINA LA ISRAELI (YAKOBO) ALIYEPIGANA KWA AJILI YA MIBARAKA YA UZIMA WAKE NA MALI DHIDI YA ESAU ALIYEKUWA ADUI WA UHAI WAKE NA MALI ZAKE.

  1 PETRO 2:10
  “NINYI MLIOKUWA KWANZA SI TAIFA, BALI SASA NI TAIFA LA MUNGU; MLIOKUWA HAMKUPATA REHEMA, BALI SASA MMEPATA REHEMA.”

  MSIHANGAISHE MIOYO YENU KWA HEKALU LA ISRAELI YA KIMWILI, INGIENI SASA KATIKA HEKALU LISILOFANYIKA KWA MIKONO MPATE ONDOLEO LA DHAMBI.

  YESU MWENYEWE ALISEMA

  MATHAYO 23:38
  “ANGALIENI, NYUMBA YENU MMEACHIWA HALI YA UKIWA”

  PAZIA LILIPOPASUKA KILA MOJA ANAENDA MOJA KWA MOJA KUONGEA NA YESU SI KUPITIA MTU FULANI WALA HATUHITAJI KWENDA KUINAMIA MAWE YA KUTA KULE YERUSALEMU ILI TUOKOLEWE

  MATHAYO 27:51
  “NA TAZAMA, PAZIA LA HEKALU LIKAPASUKA VIPANDE VIWILI TOKA JUU HATA CHINI; NCHI IKATETEMEKA; MIAMBA IKAPASUKA;

  WAEBRANIA 9:24
  “KWA SABABU KRISTO HAKUINGIA KATIKA PATAKATIFU PALIPOFANYIKA KWA MIKONO, NDIO MFANO WA PATAKATIFU HALISI; BALI ALIINGIA MBINGUNI HASA, AONEKANE SASA USONI PA MUNGU KWA AJILI YETU.”

  MSIHANGAIKIE KUJENGWA HEKALU LA MIKONO HUKO YERUSALEMU

 17. @Dada Stella,

  Unapozungumzia Wokovu, jitahidi kubaki katika wigo wa Neno la Mungu badala ya kuendekeza hisia zako, hata zikiwa ni nzuri kiasi gani, fahamu kwamba Mungu haziangalii hizo!

  Hivi kwa mawazo yako, unadhani ungeweza kumuombea Kaini akaokoka? Angalia nawe usijeharibu ufahamu wako kama Fred! Wapalestina walinyang’anywa nchi yao na Mungu akampa Yakobo, sasa mnachojichoshea roho zenu ni nini kuhangaika na watu walioshughulikiwa na Mungu mwenyewe? Hivi ungekuwapo siku Mungu amewaambia waue mpaka watoto wadogo wa ki Amaleki, si ndio mngeandamana mpaka mshushiwe moto uwalambe!!

  Angalia maombi yako yawe ni hayo yenye kuongozwa na RM, usijitoe mbele eti wewe ndio umuongoze RM!!!

  WABARIKI Israeli nawe Ubarikiwe, jizungushe nawe uzungushwe!!!

  Gbu

 18. @ Fred,

  Niliifungua hiyo link uliyotuwekea, nilichokikuta huko ndicho kilinifanya niamini kwamba ufahamu wako ni mdogo! Habari niliyoikuta huko inatuambia kwamba Israeli ndio iliyowa kidnap raia wake watatu hao vijana, ikawaua na kisha kuwatupia lawama Wapalestina ili wapate kisingizio cha kuwasumbua!

  Haya, kwamba wewe unaamini kwamba hii ni kweli, basi kwa kiwango fulani utakuwa unashangaza, maana hao walioziandika habari hizo wanaonesha wazi kabisa kwamba wana speculate, wewe uhakika unautoa wapi kama sio ushabiki?

  Maswali uliyoyauliza nimeyaona, lakini naona yanakuhitaji wewe utoe somo kwanza halafu ndio utuulize maswali! Sisi ktk uungwana tumekuandikia yooote tunayoyafahamu, nawe jitahidi utuletee hilo somo; na kama una maswali ktk hayo niliyoyaandika, basi yalete, acha kulalamika bila kunionesha uongo wangu uko wapi na ukweli wako uko wapi, huo ndio uungwana wa majadiliano!!

  Gbu!

 19. @ Lenda,

  Inasikitisha jinsi ufahamu wa mtu unavyoweza kufungwa kwa Mapokeo mpaka asiyaelewe Maandiko!

  Mungu anashughulika na Israeli kama taifa na si individuals kama sisi wa Mataifa. Kwa hiyo anaposema Yakobo basi jua hilo ni taifa na si mtu mmoja!

  Pia ni lazima ujibidiishe ktk kweli unaposimamisha dai la kwamba wewe ni mkristo, ukifanya hivyo, hiyo kweli itakurudisha mpaka huko kwenu maporini mlikokuwa mnaabudu miti ya mibuyu na vitu vingine visivyoeleweka, ndipo uione na Injili ilivyokufikia, kwa mkono wa nani na ilikuwaje ikakufikia wewe, jambo linaloweza kukufanya ukawa mwingi wa shukurani!!

  Hebu jaribu kusoma Warumi 11, ujitazame katika kioo hicho, uone na jinsi Mungu alikujua kimbele akakuwekea na sababu za kukukatilia mbali kutoka hapo ulipopandikizwa maana kwa pride umefikia kujiona kwamba wewe u bora kuliko Myahudi; jambo linaloonesha kwamba hata Injili yenyewe hauijui!

  Kuambiwa kwako kuwa wewe ni muisraeli kulipaswa kukufanye utafute kujua ni kivipi, umewabadili hao au nawe umejumuishwa katika urithi wao?

  Kama mtu kapewa usingizi, ili wewe upite, basi utamlaumu vipi huyo aliyelazwa usingizi kwa ajili yako???

  ” 25 Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili. 26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake. Na hili ndilo agano langu nao, Nitakapowaondolea dhambi zao.”

  Je, hii siku ya kuondolewa dhambi zao imefika? Hayo unayoyasoma hapo yanatokea ktk Juma la 70 la Daniel wakiwa wamekwisha kukusanywa tena kama unavyowaona hapo nchini kwao leo hii!

  Gbu!

 20. Shalom

  Wokovu uliandaliwa kwa ajili ya Israel lakini wao wakauktaa!!!
  na mataifa tukaukubali , kwa hiyo hata sisi ni taifa teulee,
  mwingine anakwenda israel eti kutafuta upako!!!

  Luka 12:20-21
  mafarisayo walimuulza yesu ufalme wa mungu utakuja lini, ,walizoea imani yao ya kimwili, lakini mwanaume alikuwa rohoni, akawajibu tazama ufalme wa mungu hhaupatikani huko wa kule upo ndani yetu!!

  Vumilia yote ya dunia na adha za dunia hii kuusubiri huo mwisho wa kukombolewa na kwenda kwenye nchi anayotuadalia Bwana ,maana sisi ni watoto wake na warithi wake neema iliyoje???

  Ni nchi nyingi sana zina matatizo ni vyema tukawajumuisha wote na hiyo nchi ya Israel
  katika maombi yetu ,

  barikiwa

 21. MASAHIHISHO SWALI LA MWISHO: UNAKUWA NA UJASIRI KUTETEA USICHOKIJUA?

  LEMBWE MUNGU AKUSAMEHE MAANA HUJUI KUNACHOKIELEZEA.

  KWA UNAYOELEZA JUU YANGU NAKUSAMEHE PIA MAANA HUNIFAHAMU NA UMEKURUPUKA. ULICHOFANYA NI KAMA WANASIASA WETU NADHANI UNAFUATILIA MAMBO SIASA PIA. NA IKIWA UNATAKA UWE WA MSAADA KWA KANISA BASI TIMIZA WAJIBU WAKO KWA 1THESSALONIANS 5:21. ZINDUKA NDUGU YANGU! TUKO VITANI NA WEWE USIBAKI NYUMA. USIWE SEHEMU YA TATIZO BALI SULUHISHO. NAKUSIHI KWA SASA UTULIE USIJE WAPELEKA WENGI GIZANIA AU KUENDELEA KUFUNIKA WALIOKO GIZANI TAYARI. NA UACHE UONGO.

 22. NDUGU ZANGU NAOMBA KAMA MTU HUNA HAKIKA NA UNACHOTAKA KUANDIKA NI BUSARA KUTATHIMINI MBELE ZA MUNGU ILI KUHAKIKI IMANI YAKE ILIPO AU JUU YA JAMBO FULANI.

  WAKRISTO WANAPENDA KUELEZEA VITU BILA UCHUNGUZI ILA KWA MAZOEA AU KWA KUFUATA MAELEZO YA WAHUBIRI FULANI.

  MIMI NILITARAJIA MTU MAKINI ANGEONGOZWA NA MASWALI NILIYOULIZA KUJUA NINI HASA MUNGU ANAPENDA WATU WAKE WAKIELEWE.

  NDUGU CK LWEMBE NAOMBA KWA NEEMA YA MUNGU TAFUTA MAJIBU YA MASWALI NILIYOWEKA ACHA UBABAISHAJI.

  MUNGU NI MTAKATIFU NA HANA UPENDELEO KATIKA KILA NCHI AU TAIFA AU LUGHA MTU YEYOTE ANAYEMCHA NA KUTENDA HAKI ANAPOKELEWA KWAKE.

  NA KILA ROHO ITENDAYO DHAMBI ITAKUFA.

  TUKO VITANI, USIPOTEZE MUDA, TUACHE UBABAISHAJI.

  KAMA HUNA MAJIBU YA MASWALI YANGU NAOMBA KWA HESHIMA YOTE NYAMAZA BALI TULIA MBELE ZA MUNGU KUSAKA MAJIBU.

  HUDUMA INAYOHITAJI SASA KULIKO WAKATI WOWOTE NI

  HUDUMA YA UCHUNGUZI NA HUKUMU. WALA MTU ASIJIDANGANYE KWAMBA ATASALIMIKA KWA UJINGA WAKE.
  1 THESSALONIANS 5:21

  MTU YEYOTE ANAYEUITA WEMA KWAMBA NI UOVU NA UOVU NI MWEMA NI NABII WA UONGO.

  SWALI LA NYONGEZA KWA LWEMBE: NI NANI AMEANZISHA MACHAFUKO YANAYOENDELEA KATI YA PALESTINA NA ISRAEL KWA SIKU KADHAA SASA?
  ANGALIZO KAMA MAELEZO YAKO YANATOKANA NA MAINSTREAM MEDIA BASI MAJIBU YAKO NI YA UONGO NA BADO UNASEMA UNAONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU.

  UPENDO HAUPIMWI KWA USHABIKIA UOVU. UNAKUWAJE NA UJASIRI KUTETEA UCHOKIJUA?

 23. Nicky,
  … inaendelea:

  Laana kwa yeyote aliye ktk Ukristo, akiwa ameipata baada ya kuwa mkristo, huwa HAIONDOKI!!! Ni kutokana na jambo hili, ndio unayaona makundi hayo yakiwa vipofu wa Maandiko kuliko popo!!

  Kama kutawanywa kwao kulivyotabiriwa na kutimia, ndivyo na kukusanywa kwao kulivyotabiriwa pia. Mambo yote haya yanawatimilia ndani ya hayo majuma 70 waliyapangiwa. Ndio maana akina Lenda wanashindwa kujirudisha nyuma waitambue Israeli kama taifa la Mungu leo hii, kutokana na ukweli kwamba wakifanya hivyo watakuwa wameuvunja unabii wa Danieli, huo waliouvamia, watakuwa wamewaongezea muda, maana kulingana na hesabu zao, majuma hayo sabini yalikwisha malizika!!!

  Lakini ukweli ni kwamba Taifa la Israeli kwao muda ulisimama ktk juma la 69 hapo Injili ilipotugeukia sisi, Mdo 15:14 “Simeoni ametueleza jinsi Mungu hapo kwanza alivyowaangalia Mataifa ili achague watu katika hao kwa ajili ya jina lake”! Nayo majuma hayo 70 ni muda ambao Mungu amepanga kushughulika na Israeli na si majuma yasiyo na lengo!

  Basi juma la sabini ndilo hili ambalo fukuto lake tunaliona, Mungu akiunyoosha tena mkono wake kuwakusanya Israeli akiwarejesha katika nchi yao; Isaya 11:11-12:
  ”Na itakuwa katika siku hiyo, Bwana atapeleka mkono wake mara ya pili, ili ajipatie watu wake watakaosalia, kutoka Ashuru, na kutoka Misri, … atawakutanisha watu wa Israeli waliotupwa, atawakusanya watu wa Yuda waliotawanyika, kutoka ncha nne za dunia.”

  Basi Mungu atakapokuwa tayari kuwarudia Israeli, ktk namna ya Ibada, hapo wakati wa Mataifa unapofikia ukomo, Kanisa litaondolewa, yaani kunyakuliwa, ndipo, yeye atawarudia Israeli kikamilifu ili kulimalizia lile Juma la Sabini lililosalia katika jumla ya yale majuma aliyowapangia. Bali ni lazima Israeli wawe wamerudi katika nchi ya uenyeji wao kwanza, ndipo aweze kuwashughulikia.

  Huu ndio umuhimu wa Israeli kwa kanisa anaouongelea Nicky, HAUWEZI kuzungumzia wokovu bila kujua Israeli wanahusika vipi. Tazama hapa Mungu anavyowatazama hao Israeli: Kum 32:9
  “ Maana, sehemu ya BWANA ni watu wake, Yakobo ni kura ya urithi wake, alimkuta katika nchi ya ukame, na katika jangwa tupu litishalo; alimzunguka, akamtunza; akamhifadhi kama mboni ya jicho; mfano wa tai ataharikishae kiota chake; na kupapatika juu ya makinda yake, alikunjua mbawa zake, akawatwaa, akawachukua juu ya mbawa zake.”

  Sehemu ya mambo haya yamewatimilia Israeli ktk kurudi kwao, hao hapo nchini kwao, kwa hiyo, saa yoyote ile kuanzia sasa, lile Juma la Sabini laweza kuanza, maana hao wanaopaswa kuhudumiwa ndio hao hapo katika nchi yao wakilingojea hilo! Basi kwa jambo hilo kuwa katika kiwango hicho, lapaswa kuwa ishara kwetu ya kujitayarisha itupasavyo, na si wakati wa mchezo tena, dakika yoyote ile Kristo aweza kuja!!!

  Fred, hebu fikiria, kwamba Kristo anapokufikia, akakukuta na kiroba kizima cha baraka alizokuletea uwarushie Israeli, wewe kwa ubahiri umezifutika ndani, eti oh mimi siwachukii; sipati picha itakuwaje kwako!!!!

  Gbu!

 24. Nicky,

  Shalom!
  Ninakushukuru kwa maelezo mazuri, mepesi na ya kina kuhusu Israeli kuhusiana na Wokovu wetu. Ngoja nikunukuu, ““ TAIFA LA ISRAELI NDIYO KALENDA YA ULIMWENGU KWA UNABII NA MATUKIO YOTE YA SIKU ZA MWISHO WA DUNIA NA KURUDI KWA BWANA WETU YESU KRISTO WA NAZARETI”” huu ndio ukweli wa mambo, utake usitake!

  Kuna wakristo wanashangaza sana, Mungu amekwambia ukiwabariki Israeli, Atakubariki; ukiwalaani, atakulaani; basi unamkuta mtu anakwambia yeye hatawabariki na wala hatawalaani; halafu akibaki peke yake chumbani anamuomba Mungu ambariki!!! Au unamwambia mtu kuhusu Ahadi iliyowekwa kule kwenye kitabu cha Ufunuo, kwamba ukikisoma hicho au kuwasomea watu wakisikie utabarikiwa; lakini mtu anakwambia ah, kile kitabu wameniambia ni kigumu sana kukielewa, kwahiyo hakisogelei kabisaaaaa!!!!

  Kuhusu Fred, ni wa kuhurumiwa zaidi, kwa sababu maelezo yake yanaonesha dhahiri kwamba ni mtu mwenye ufahamu mdogo ambaye anapaswa aongozane na mtu mzima anapovinjari mitandaoni, vinginevyo ndio anaishia ktk upuuzi kama huu anaouandika, chezea mitandao, wewe!!

  Na kuhusu Sungura, sijajua kapatwa na nini, lakini huenda naye ktk jitihada yake ya kuwa tofauti, imempitilizisha kituo kenda kushukia nyumbani kwa kina Lenda, hao ambao ndio wamechanganyikiwa kabisa tangu zama hizo!!!

  Walimu na manabii wa akina Lenda, walijaribu kuufungua unabii uliomo ktk kitabu cha Daniel nje ya wakati alioupanga Mungu, wakaishia kuchukua laana badala yake! Unabii ktk kitabu hicho Mungu aliufunga: Dan 12:4 “Lakini wewe, Ee Danieli, yafunge maneno haya, ukakitie muhuri kitabu, hata wakati wa mwisho.” Mwisho wa wakati ndipo kitafunguliwa!!!

  Wao wakajaribu kukifungua kabla ya wakati, Israeli wanalijua jambo hilo, ndio maana marabi wao walikiwekea laana kwa yeyote atayejaribu kukifungua:
  “May the bones of the hands and the bones of the fingers decay and decompose, of him who turns the pages of the book of Daniel, to find out the time of Daniel 9:24-27, and may his memory rot from off the face of the earth forever!”
  An ancient Rabbinic curse in the Talmud.

  [“Na ioze na kuharibika mifupa ya mikono na mifupa ya vidole vya yeyote atakaye zifungua kurasa za kitabu cha Daniel, ili kutafuta kuujua wakati ktk Daniel 9:24-27, nayo kumbukumbu yake na iozee mbali na kufutika ktk uso wa dunia milele!”]

  Nayo laana hiyo ndiyo inayowaingiza katika aibu hii waliyomo; kwamba wao, miaka takribani 1800 baada ya kusambaratika kwa Israeli, hao manabii na walimu wa akina Lenda walipoinuka, kwa kukifungua kitabu hicho, wakauona wakati waliopangiwa Israeli, yale majuma 70, Dan 9:24 “ Muda wa majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako, na juu ya mji wako mtakatifu, …” kwamba ulikamilika hapo Injili ilipowageukia Mataifa.

  Ndipo ukichanganya na kule kusambaratika kwa taifa la Israeli mwaka 70 A.D, na Hekalu lao kuvunjwa na wao kutawanyishwa, na nchi yao kuporwa na kubadilishwa mpaka jina, kama Maandiko yalivyolitabiri jambo hilo: Law 26:33 “Nanyi nitawatapanya-tapanya katika mataifa, nami nitaufuta upanga nyuma yenu; na nchi yenu itakuwa ukiwa, na miji yenu maganjo”, wakaamini kwamba Israeli, kama taifa imekwisha, HAITAKUWEPO TENA!! Kwamba mshahara wa kumkataa kwao Masihi wao ndiko huko KUFUTWA kwa taifa hilo na Mungu. Basi katika mpangilio wao huu mpya, Israeli wakawa ndio wao au kanisa katika ujumla wa kiroho na kimwili!!!!!

  itaendelea…!

 25. TUWE KAMA WAYAHUDI WA KANISA LA KWANZA WALIOMPOKEA YESU,TUSIWE KAMA WAYAHUDI WALE WASIOIPOKEA IMANI YA UKRISTO

  MATENDO 13:45
  “BALI WAYAHUDI WALIPOWAONA MAKUTANO, WAKAJAA WIVU, WAKAYAKANUSHA MANENO YALIYONENWA NA PAULO, WAKIBISHA NA KUTUKANA.”

  MATENDO 14:4,5
  “LAKINI JAMII WA MJINI WAKAFARAKANA; HAWA WALIKUWA UPANDE WA WAYAHUDI, NA HAWA UPANDE WA MITUME. HATA PALITOKEA SHAMBULIO LA WATU WA MATAIFA NA WAYAHUDI PAMOJA NA WAKUBWA WA JUU YAO, KUWATENDA JEURI KWA KUWAPINGA KWA MAWE,”

  MATENDO 13:46
  “PAULO NA BARNABA WAKANENA KWA USHUJAA WAKASEMA, ILIKUWA LAZIMA NENO LA MUNGU LINENWE KWENU KWANZA; LAKINI KWA KUWA MNALISUKUMIA MBALI, NA KUJIONA NAFSI ZENU KUWA HAMKUSTAHILI UZIMA WA MILELE, ANGALIENI, TWAWAGEUKIA MATAIFA.”

  MATENDO 13:48
  “MATAIFA WALIPOSIKIA HAYO WAKAFURAHI, WAKALITUKUZA NENO LA BWANA, NAO WALIOKUWA WAMEKUSUDIWA UZIMA WA MILELE WAKAAMINI.”

  MATENDO 28:28
  “BASI IJULIKANE KWENU YA KWAMBA WOKOVU HUU WA MUNGU UMEPELEKWA KWA MATAIFA, NAO WATASIKIA!.
  INJILI IMEKUJA KWA MATAIFA TUITII TUACHE HABARI YA KUANGALIA USHABIKI, WA VITA YA KIMWILI YA ISRAELI NA PALESTINA, TAZAMENI VITA YA KIROHO

  MATENDO 13:45
  “BALI WAYAHUDI WALIPOWAONA MAKUTANO, WAKAJAA WIVU, WAKAYAKANUSHA MANENO YALIYONENWA NA PAULO, WAKIBISHA NA KUTUKANA.”

  WAISRAELI AMBAO HAWAKUMPOKEA YESU HUPINGA MAANDIKO. NA INJILI YA YESU, WAKRISTU WA LEO WAMEUZA UISRAELI WAO KWA MKATE KAMA ESAU ALIVYOFANYA

 26. Tuombee pia taifa la:congo,palestina,somalia,soudan,kenya,irack,nigeria,rca,syria,afganistan,

 27. Wapendwa katika Bwana Yesu Kristo,

  Sitarajii kweli kujulikana kwa mabishano na hakika kweli itasimama daima. Sishangai kuona maelezo ya kaka NICKY maana ni mtazamo wa wakristo wengi sana ambayo husoma Biblia kwa mazoea na kudhani wameelewa undani na kupata mafunuo ya kweli.

  Sikusudii kumjibu kaka Nicky maana hawezi kunielewa hata chembe maana amekwisha funga masikio na moyo wake kwa kile anachoamini ni kweli. Neema ya Mungu tu inaweza kumletea ukombozi na kuijua na kuiona kweli yote.

  Amehukumu asichokijua na amewaita wasioamini anachoamini kuwa wana mapepo. Mungu atathibitisha punde nani hasa mwenye mapepo.

  Kaka Nicky kunukuu maandiko hakuthibishi chochote kwamba waijua kweli hata chembe. Maana hata shetani anamjua Mungu na anatetemeka, je wewe umefikia kiwango hicho.

  Ndugu zangu hatari iliyoko mbele yetu ni kubwa sana na kama tutawaachia watu wa aina ya kaka Nicky waeneze sumu yao basi ni majanga makubwa sana kwa kanisa.

  Naomba ieleweke wazi kwamba mimi simchukii MYAHUDI YEYOTE WALA ISRAEL BALI WALE WANAOJIITA WAYAHUDI KUMBE SIYO BALI NI WA SINAGOGI LA SHETANI.

  Maswali kwa NICKY AND COMPANY:

  1. Myahudi ni nani?
  2.Israel ni nani?
  3. Wanajiita wayahudi kumbe siyo bali ni wa sinagogi la shetani ni kina nani?
  4.Ni maana ya NJIA , KWELI NA UZIMA?
  5. JE NI KWA KIASI UNAJUA KUHUSU MIPANGO YA NEW WORLD ORDER? NI MADHARA YAKE KWA KANISA? JE WEWE UNAFANYA NINI JUU YA HAYO?
  6. NI NANI ALIANZISHA MTANDAO WA KIGAIDI?
  7. JE, UNAJUA MTAZAMO WA WANANCHI WA KAWAIDA WA ISRAEL, PALESTINA NA IRAN?
  8. JE NI KINA NANI WALIANZISHA ILLUMINATE? JE NI KWA KIASI WANAATHIRI MAISHA , MIENENDO, NA HATIMA YA MATAIFA YOTE DUNIANI?
  9. NINI KIFANYIKE KUPAMBANA NA UOVU UNAOENEA DUNIANI? NINI NAFASI YA MKRISTO KATIKA HAYA?
  10. JE NINI MAANA YA HUKUMU KUANZA KATIKA NYUMBA YA BWANA ?

  NK: IKIWA KUNA HATARI HALAFU WEWE UKASEMA KUNA AMANI NA SALAMA WEWE NI NABII WA UONGO.

  WAKRISTO NA WATU WOTE DUNIANI MBINGU ZINATUTAKA KUCHUKUA HATUA. MAPENZI YATIMIZWE DUNIANI KAMA MBINGUNI.

  KWA UPENDO NA UPENDO

 28. Nick mpk
  May the lord bless you for the powerful analysis about israel.
  Stay Blessed.

 29. Bwana Yesu Asifiwe,
  Napenda kuchukua fursa hii kukupongeza uliyeleta post hii kwa kutukumbusha kuliombea taifa la Israeli. Pili napenda kutoa masikitiko yangu kwa wapendwa Fred, Sungura na lenda kwa jinsi walivyolipokea jambo hili kwa mtazamo hasi na kunukuu vifungu ambavyo kwa hakika kama siyo msomaji wa bibilia unaweza ukapotezwa. Ndugu Fred amekwenda mbali zaidi kiasi cha kuita wanaisraeli kama ndiyo wafadhili wa ugaidi duniani kwa kutumia vigezo vya vitabu na nukuu za mitandaoni bila kufuatilia watu waliondika hivyo vitabu na hiyo mitandao wanachuki kiasi gani na waisraeli. Kabla sijakwenda mbali Zaidi kufafanua kwanini taifa la Israeli linachukiwa, na kwanini tunapaswa kuliombea taifa la Israeli napenda kuwaambia wakristo na wasio wakristo “ TAIFA LA ISRAELI NDIYO KALENDA YA ULIMWENGU KWA UNABII NA MATUKIO YOTE YA SIKU ZA MWISHO WA DUNIA NA KURUDI KWA BWANA WETU YESU KRISTO WA NAZARETI” (Mat 24:32, Danieli 9:24-27). Kwa mkristo wa kweli uliyeokoka na unayeongozwa na Roho Mtakatifu hauwezi kulipuuzia jambo la kuliombea taifa la Israeli. Roho ya chuki dhiki ya Israeli ni roho ya shetani (pepo), shetani analichukia taifa la Israeli (wayahudi) anatamani wasiwepo kabisa katika uso wa dunia. Waisraeli (Wayahudi)ndiyo jamii ya watu ambao wameuwawa kwa wingi kuliko watu wa jamii nyingine yoyote hapa duniani kwa mfano vita ya pili ya dunia peke yake iliangamiza wayahudi karibia milioni sita. Kwa miaka zaidi ya elfu mbili wayahudi wamekuwa wahanga wa kuuliwa usiku na mchana tena maauaji ya kimbari (Anza kuanzia kipindi cha Babeli (Nebukadineza) Warumi , Hitler, na sasa waarabu bado waisraeli (Wayahudi) wanaendelea kuuliwa.
  Sasa Fred unaposema waisraeli ndiyo chanzo cha ugaidi kwa mtazamo gani? Tangu wamepata Uhuru 1948 waisraeli wanapigana vita na maadui zao pande zote. Na ninakuhakikishia bila mkono wa Mungu taifa la Israeli lisingekuwepo sasa. Kwanini shetani analichukia sana taifa la Israeli (Wayahudi), jibu ni rahisi Nchi ya Israeli (Ardhi) ni mali ya Mungu (Walawi 25:23), ambayo Mungu alimpa Ibrahimu na uzao wake (Mwanzo 15:18) kwahiyo shetani anatafuta kila njia ya kuinyang’anya. Waisraeli (wayahudi) ndilo taifa ambalo Mungu alilichangua kupitisha ukombozi wa wanadamu. Taifa la Israeli ndio uthibitisho (evidence) wa mambo mengi kwamba Mungu yupo kama umeshatembelea Israeli au kama ukibahatika kwenda Israeli utalitambua hilo bila ubishi. Kila kitu cha Mungu kinapita kwanza kwa waisraeli. Mji wa Jerusalemu ni picha (symbolic picture) ya Jerusalemu ya mbinguni.
  Jerusalemu ni mji ambao Mungu mwenyewe anaulinda, aliucha ukanyagwe namataifa lakini mwaka 1967 aliuchukua na hatutarudi kamwe kwa mataifa hata hao wamarekani na umoja wa mataifa wanaotaka kuugawa hawataweza. Mji wa Jerusalemu kwa nyakati hizi za mwisho ni jiwe la kujikwaa (Zekaria 12:2-3) “Angalia, mimi nitafanya Yerusalemu kuwa kikombe cha kuyumba-yumba kwa watu wa kabila zote, wazungukao pande zote; tena kitakuwa juu ya Yuda pia wakati wa kuhusuriwa Yerusalemu. 3 Tena itakuwa siku hiyo, nitafanya Yerusalemu kuwa jiwe la kuwalemea watu wa kabila zote; wote watakaojitwika jiwe hilo watapata jeraha nyingi; na mataifa yote ya dunia watakusanyika pamoja juu yake.” Ukisoma mstari wa sita utaona kuwa wakuu wa Jerusalemu watakuwa kigae cha moto “ Zekaria 12:6 Siku hiyo nitawafanya wakuu wa Yuda kuwa kama kigae chenye moto katika kuni, na kama kinga cha moto katika miganda; nao watateketeza watu wa kila kabila, wawazungukao pande zote, upande wa mkono wa kuume na upande wa mkono wa kushoto; na baada ya haya Yerusalemu utakaa mahali pake, naam, hapo Yerusalemu.” Mpendwa Sungura na lenda mnaposema taifa la Israeli lilikuwa agano la kale mnashindwa kuunganisha agano la kale na agano jipya na kupima kizazi chetu tupo wapi kinabii kwa sasa. Kama mnasema Israeli ni taifa la agano la kale na Mungu hashughliki tena na waisraeli mnapotea, mpendwa lenda unganisha vizuri agano jipya na agano lakale utapata picha kamili ya taifa la Israeli.Mungu ana agano la MILELE na uzao wa Ibrahimu (Kiroho na kimwili) (Mwanzo 17:7, Zaburi 105:10,Waebrania 8:1-13 hii uisome kwa umakini na kwamsaada wa roho mtakatifu upate kuielewa). Mungu mpaka sasa anashughulika na taifa la Israeli, ngoja nikupe unabii wa Israeli ambao Mungu anutimiza au ameutimiza hivi karbuni.
  1. Kulikusanya taifa la Israeli (Ezekieli 37:21, Eze 37:11-12, Isaya 11:12) “Amosi 9:14-15 Nami nitawarejeza tena watu wangu Israeli waliohamishwa, nao wataijenga miji iliyoachwa maganjo, na kukaa ndani yake; nao watapanda mizabibu katika mashamba, na kunywa divai yake; nao watafanyiza bustani, na kula matunda yake. 15 Nami nitawapanda katika nchi yao, wala hawatang’olewa tena watoke katika nchi yao niliyowapa, asema Bwana, Mungu wako.” Hii ilitimia 1948 taifa la Israeli lilipoanzishwa tena. Kwa taarifa yako Israeli (Wayahudi) ni taifa pekee ambalo lilitawanyka na kuishi uamishoni kwa Zaidi ya miaka 2000 na wakaendelea kushika na kutunza utamaduni wao (culture) na kushika sharia za Mungu wao kwenye hayo mataifa walikotwanyikia kwa miaka yote na wakakusanyika tena katikaArdhi yao na kuendelea kushika utamaduni wao na Sharia za Mungu kama walivyokuwa mababu zao. Kama siyo mkono wa Mungu kutimza unabii taifa la Israeli lisengekusanyika. Mataifa mengi yanayotawanyika huwa yanapoteza identity au culture yao na kufuata utamaduni wa mataifa wanakotawanyikia. Chukua tu hata mfano wa watanzania wanahamia na kuishi Ulaya watoto wao wanozaliwa ulaya wanapoteza kabisa utamaduni wa Tanzania n kuiga tamaduni za nchi hizo.
  2. Mpaka mwisho Yesu atapigana vita upande wa Israeli (Zekaria 12:1-14, Zekari 14:1-10) na baada ya kushinda ndipo watakoanza kuuliza kuhusu makovu yake ya mikononi Zekaria 13:6 “Na mtu atamwambia, Je! Jeraha hizi ulizo nazo kati ya mikono yako ni nini? Naye atajibu, Ni jeraha nilizotiwa katika nyumba ya rafiki zangu.” Kama mnafikiri vita hivi vitakuwa vya kiroho peke yake mnapotea mnahitaji Roho mtakatifu awafunulie ili mpate kuujua ukweli.
  Hivi ndugu Fred unaposema waisraeli ndiyo watakaleta vita vya tatu vya dunia, inamaana haujasoma maandiko kwenye bibilia inasema kuhusu vita kuu siku za mwisho? (Ezekieli 38:1-23, Zaburi 83:1-18) utaona shetani anajiandaa kulifutataif la Israeli “Zaburi 83: 4 Wamesema, Njoni, tuwakatilie mbali wasiwe taifa, Na jina la Israeli halitakumbukwa tena. “
  Kwanini wakristo tunapaswa kuliombea taifa la Israeli, mtoa mada ameshalieleza vizuri na kunukuu vifungu vya bibilia (Zaburi 122:6, Isaya 31:5, Isaya 62:1), Wakristo tunapaswa kutambua nyakati na majira ya kurudi mwokozi wetu kwa kuliangalia taifa la Isrieli. Kama hauwezi kuliombea taifa la Israeli utawezaje kutambua majira na nyakati za kurudi Yesu na za mwisho wa dunia?
  Tuiombee Amani Jerusalemu, Tuiombee Amani Israei.

  Mungu awabariki

 30. OMBI LA PETRO LILIKUWA KUWAOMBEA ISRAELI WAOKOLEWE, SI VINGINEVYO

  WARUMI 10:1-
  “NDUGU ZANGU, NITAKAYO SANA MOYONI MWANGU. NA DUA YANGU NIMWOMBAYO MUNGU, NI KWA AJILI YAO ILI WAOKOLEWE. KWA MAANA NAWASHUHUDIA KWAMBA WANA JUHUDI KWA AJILI YA MUNGU, LAKINI SI KATIKA MAARIFA”

  SHIDA YA ISRAELI ILIKUWA NI HII HAPA CHINI, AMBAYO HATA WAKRISTO WENGINE TUMETUMBUKIA HAPO;

  WARUMI 9:30-32
  “TUSEME NINI, BASI? YA KWAMBA WATU WA MATAIFA, WASIOIFUATA HAKI, WALIPATA HAKI; LAKINI NI ILE HAKI ILIYO YA IMANI; BALI ISRAELI WAKIIFUATA SHERIIA YA HAKI HAWAKUIFUATILIA ILE SHERIA. KWA SABABU GANI/ KWA SABABU HAWAKUIFUATA KWA NJIA YA IMANI, BALI KANA KWAMBA KWA NJIA YA MATENDO. WAKAJIKWAA JUU YA JIWE LILE LIKWAZALO,”

  KANISA LA MITUME WENGI WA MAKUHANI WALIACHA HABARI YA KUFUKIZA UVUMBA NA KUTOA KAFARA YA WANYAMA NA KUIPOKEA IMANI YA UKRISTO

  MATENDO 6:7
  “NENO LA MUNGU LIKAENEA; NA HESABU YA WANAFUNZI IKAZIDI SANA KATIKA YERUSALEMU; JAMII KUBWA YA MAKUHANI WAKATITII ILE IMANI.”

  MFANO WA PETER KUWAOMBEA WAOKOLEWE UNGEFAA ZAIDI KULIKO KUWAOMBEA ISRAELI WAINGIE KATIKA MAJANGA, YA KUFIKIRI KISASI NA VITA

  MUNGU NI PENDO, HABARI ZA KISASI NI ZA WATU WASIOIKUBALI KAFARA YA YESU.

  1 YOHANA 4:8
  “YEYE ASIYEPENDA HAKUMJUA MUNGU, KWA MAANA MUNGU NI PENDO.”

  WARUMI 9:24
  “NDIO SISI ALIOTUITA, SI WATU WA WAYAHUDI TU, ILA NA WATU WA MATAIFA PIA.”

  WAKRISTU TUACHE UBAGUZI,MUNGU SI MBAGUZI

 31. Father in the name of Jesus… protect your people from their enemies oh God, let your Mighty hand be upon them and let them emerge victorious in this on going conflict and the conflicts to come, i pray that you give knowledge and wisdom to military leaders and prime minister Benjamin Netanyahu so that they would make best decision for your Glory in Jesus Mighty name i pray, Ameeeen.

 32. ISRAEL MNAYOSHABIKIA NDIYO ILIANZISHA NA INA FADHILI UGAIDI DUNIANI, NDIYO WANAANZISHA NA KUFADHILI VITA DUNIANI NA SASA WANAANDA VITA YA TATU YA DUNIA(WWWIII). MIKONO YAO IMEJAA DAMU. TUACHE UPOFU HUU NA TUONGOZWE NA AMANI YA KIKRISTO NA KUUPINGA UNYAMA HUU DHIDI YA WASIO NA HATIA. WANADHOOFISHA SERIKALI ZOTE DUNIANI ILI KUUNDA SERIKALI MMOJA DUNIANI.
  KWA HIYO MTU ANAYEOMBEA ISRAEL YA MWILINI ANAOMBEA MATESO NA DHIKI DHIDI YAKE MWENYEWE NA JAMII YOTE DUNIANI. WAMEPANGA KUUA WATU BILIONI 6.5

  INASIKITISHA KUSIKIA MTU ANAYEITWA MKRISTO ANAOMBEA MASHETANI ILI WAFANIKIWE ILI HALI BIBLIA INASEMA MPINGENI SHETANI NAYE ATAWAKIMBIA. NDUGU ZANGU TUMESALIWA NA MUDA MFUPI SANA WAKUJITETEA MAANA HAYA MASHETANI YAMEFIKA MBALI SANA KWENYE MIKAKATI YAO.

  HAYA MASHETANI YAMESHATEKA MAKANISA MENGI TU NA SERIKALI KARIBU ZOTE DUNIANI.

  UNGANA NA JUHUDI ZOTE KUPINGA MASHETANI HAWA
  http://www.klagemauer.tv/

  FUNGUA MACHO YAKO ROHONI.

  MWENYE MASIKIO NA ASIKIE YALE ROHO MTAKATIFU ANAYAMBIA MAKANISA

 33. KUNDI LA WAISRAELI WASIOMFUATA MUNGU WAMEANZA ZAMANI KUABUDU NYOTA TUJILINDE DHIDI YA HIZI NYOTA ZA IBADA AMBAZO ZIMEPEWA MAJINA MAZURI KAMA DAVID KUONDOA HOFU WATU HUKU, ZIKIWA NA IBADA NYINGINE.

  “NAAM,MTAMCHUKUA SIKUTHI,MFALME WENU, NA KIUNI, SANAMU ZENU, NYOTA YA MUNGU WENU,MLOJIFANYIZIA WENYEWE.” AMOSI 5:26

 34. “MAANA HAWAWI WOTE WAISRAELI WALIO WA UZAO WA ISRAELI” WARUMI 9:6

  JE MUNGU NI MBAGUZI WA RANGI, AU KABILA?

  “NINYI NI WA BABA YENU, IBILISI, NA TAMAA ZA BABA YENU, NDIZO MPENDAZO KUZITENDA” YOHANA 8:44

  “FAHAMUNI YA BASI, YA KUWA WALE WALIO WA IMANI, HAO NDIO WANA WA IBRAHIMU.” WAGALATIA 3:7

  “MAANA SISI TU TOHARA,TUMWABUDUO MUNGU KWA ROHO…,” WAFILIPI 3:3

  “MAANA YEYE SI MYAHUDI ALIYE ALIYE MYAHUDI KWA NJE, WALA TOHARA SIYO ILE YA NJE TU KATIKA MWILI.” WARUMI 2:28

  JINA ISRAELI NA UZAO WAKE

  JINA ISRAELI LINAWAKILISHA USHINDI WA KIROHO, WA KUPIGANA KATIKA MAOMBI KUIPATA NEEMA YA MUNGU.

  “AKAMWAMBIA, JINA LAKO HUTAITWA TENA YAKOBO,ILA ISRAELI, MAANA UMESHINDANA NA MUNGU, NA WATU, NAWE UMESHINDA.” MWANZO 32:28

  MARA YA KWANZA JINA ANAPEWA MPIGANAJI MMOJA, BAADAE WOTE KAMA ANAPOSEMA KUTOKA 4:22,23
  “NAWE UMWAMBIE FARAO, BWANA ASEMA HIVI, ISRAELI MWANANGU MIMI, MZALIWA WA KWANZA WANGU.” KUTOKA 4:22

  ISRAELI WA MPIGANAJI WA KIROHO(SASA) NA KIMWILI (KALE)

  MOJA:

  MWANZO 45:5 JOSEPH ANAOTA NDOTO HALAFU ANAPELEKWA MISRI KWA AJILI YA KUILINDA FAMILIA NA NJAA, VIVYO KATIKA AGANO JIPYA JOSEPH ANAOTA NDOTO ANAKIMBILIA MISRI KUILINDA FAMILIAMATHAYO 2:13.

  MBILI:
  WAKATI ISRAELI WANATOKA MISRI KUTOKA 4:22,23 ANATUMIA JINA “ MWANANGU”
  YESU ANAPOTOKA MISRI MUNGU ANASEMA KUTOKA MISRI NALIMWITA MWANANGU. MATHAYO 2:15

  TATU:
  WAKATI ISRAELI WANATOKA MISRI “WOTE WAKABATIZWA WAE NA MUSA KATIKA WINGU NA KATIKA BAHARI.” 1 WAKORINTHO 10:2, MUNGU NAYE ANATAMKA “MWANANGU MPENDWA” MATHAYO 3:15-17

  NNE:

  ISRAELI WALIPOTOKA BAHARINI WALIONGOZWA NA NGUZO YA MOTO NA ROHO WA MUNGU MIAKA AROBAINI. NA YESU BAADA YA KUTOKA YORDANI AKAONGOZWA NA ROHO WA MUNGU SIKU AROBAINI
  MATHAYO 4:1,2

  TANO:

  MWISHO WA MIAKA AROBAINI MUSA ANAANDIKA KUMBUKUMBU LA TORATI, NA YESU BAADA YA KUKAA JANGWANI YESU ANAJARIBIWA NA SHETANI NA ANAJIBU MAPIGO KWA MAFUNGU YA KUTOKA HILOHILO KUMBUKUMBU LA TORATI.

  SITA:
  ZABURI 80:8 MUNGU ANAITA ISRAELI MZABIBU ALIOUTOA MISRI. YESU ANAJIITA “MIMI NDIMI MZABIBU WA KWELI” YOHANA 15:1

  TAIFA JIPYA LA ISRAELI LIKOJE?

  MUNGU ALIITA ISRAELI YA WAKATI ULE ANASEMA;
  “NANYI MTAKUWA UFALME WA MAKUHANI, NA TAIFA TAKATIFU.” KUTOKA 19:6

  KATIKA AGANO JIPYA PETRO ANALIITA JINA HILO HILO KANISA

  “BALI NINYI NI MZAO MTEULE,UKUHANI WA KIFALME, TAIFA TAKATIFU, WATU WA MILKI YA MUNGU” 1PETRO 2:9

  “NA KAMA NINYI NI WA KRISTO, BASI, MMEKUWA UZAO WA IBRAHIMU, NA WARITHI SAWASAWA NA AHADI.” WAGALATIA 3:29
  KWA HIYO ISRAELI NI WALE WALIOZALIWA KATIKA KRISTO.

  MTAZAMO WA HAKI KWA IMANI WA HEKALU LA SASA HAPA CHINI ANASEMA;

  “ANGALIENI, NYUMBA YENU MMEACHIWA HALI YA ULIKWA” MATHAYO 23:38

  “YESU AKAENDA ZAKE, AKATOKA HEKALUNI; WANAFUNZI WAKE WAKAMWENDEA ILI KUMWONYESHA MAJENGO YA HEKALU. NAYE AKAJIBU AKAWAAMBIA, HAMYAONI HAYA YOTE? AMIN, NAWAAMBIENI, HALITASALIA HAPA JIWE JUU YA JIWE AMBALO HALITABOMOSHWA.” MATHAYO 24:1,2

  “SISI TULIMSIKIA AKISEMA, MIMI NITALIVUNJA HEKALU HILI LILILOFANYIKA KWA MIKONO, NA KATIKA SIKU TATU NITAJENGA JINGINE LISILOFANYIKA KWA MIKONO .” MARKO 14:58

  “PAZIA LA HEKALU LIKAPASUKA VIPANDE VIWILI TOKA JUU HATA CHINI.” MARKO 15:1

  LAKINI HATA YESU AKIWA MSALABANI ALIPEWA KEJELI NA WATESI WAKE,KUMBE ALIMAANISHA HEKALU LISILOFANYWA KWA MIKONO.

  “EWE MWENYE KULIVUNJA HEKALU NA KULIJENGA SIKU TATU, JIOKOE NAFSI YAKO; UKIWA NDIWE MWANA WA MUNGU, SHUKA MSALABANI.”MATHAYO 27:40

  “HAMJUI YA KUWA NINYI MMEKUWA HEKALU LA MUNGU, NA YA KUWA ROHO WA MUNGU ANAKAA NDANI YENU?” 1 WAKORINTHO 3:16:

  “KAMA MTU AKILIHARIBU HEKALU LA MUNGU, MUNGU ATAMHARIBU MTU HUYO.KWA MAANA HEKALU LA MUNGU NI TAKATIFU, AMBALO NDILO NINYI.” 1 WAKORINTHO 3:17

  “AU HAMJUI YA KUWA MWILI WENU NI HEKALU LA ROHO MTAKATIFU ALIYE NDANI YENU, MLIYEPEWA NA MUNGU” WALA NINYI SI MALI YENU WENYEWE;” 1 WAKORINTHO 6:19

  “PETRO AKAFUMBUA KINYWA CHAKE, AKASEMA, HAKIKA NATAMBUA YA KUWA MUNGU MUNGU HANA UPENDELEO. BALI KATIKA KILA TAIFA MTU AMCHAYE NA KUTENDA HAKI HUKUBALIWA NA YEYE” MATENDO 10,34
  “HAPANA MYAHUDI WALA MYUNANI. HAPANA MTUMWA WALA HURU. HAPANA MTU MUME WALA MTU MKE. MAANA NINYI NYOTE MMEKUWA MMOJA KATIKA KRISTO YESU.” WAGALATIA 3:28

  KWA NINI INJILI ILIPELEKWA KWA MATAIFA NA WOTE WALIPOKEA IMANI KUITWA ISRAELI?

  “HAO THENASHARA YESU ALIWATUMA AKAWAAGIZA, AKISEMA, KATIKA NJIA YA MATAIFA MSIENDE,WALA KATIKA MJI WOWOTE WA SAMARIA MSIINGIE. AFADHALI SHIKENI NJIA KUWAENDEA KONDOO WALIOPOTEA WA NYUMBA YA ISRAELI.” MATHAYO 10:5,6

  “PAULO NA BARNABA WAKANENA KWA USHUJAAA WAKASEMA, ILIKUWA LAZIMA NENO LA MUNGU LINENWE KWENU KWANZA LAKINI; LAKINI KWA KUWA MNALISUKUMIA MBALI, NA KUJIONA NAFSI ZENU KUWA HAMKUSTAHILI UZIMA WA MILELE, ANGALIENI TWAWAGEUKIA MATAIFA.” MATENDO 13:46

  JE WAPO WAYAHUDI WA ASILI WALIO WAKRISTO?

  ANASEMA;
  “IKAWA HUKO IKONIO WAKAINGIA PAMOJA KATIKA SINAGOGI LA WAYAHUDI; NA KWA VILE WALIVYONENA KUNDI KUBWA LA WAYAHUDI NA LA WAYUNANI WAKAAMINI.” MATENDO 14:1

  JE WAYAHUDI WANAOWALIPIZA KISASI LEO NA KUUA MAJIRANI, NA BAADHI YA MAKANISA KUTUNDIKA BENDERA KANISANI NDIO WAKRISTO WA IMANI TULIORITHI.
  “WALAKINI WAYAHUDI WASIOAMINI WAKAWATAHARIKISHA WATU WA MATAIFA NA KUWATIA NIA MBAYA JUU YA NDUGU.” MATENDO 14:2

  KWA NINI YESU ALITUMIA KISA CHA LAZARO NA TAJIRI?

  TAMUD INAYOTUMIWA NA WAYAHUDI WASIOTUMIA BIBLIA YENYE INJILI YA YESU HUITA WATU WA MATAIFA MBWA TANGU WA KATI WA YESU HATA SASA.
  TAMUD HTUPILIA MBALI MAFUNDIHO YA YESU YA KUTOLIPIZA KISASI, NDIO MAANA LEO UISRAELI MMOJA AKIUWAWA WAO HULIPIZA MARADUFU

  “AKAJIBU AKASEMA, SI VEMA KUKITWAA CHAKULA CHA WATOTO NA KUWATUPIA MBWA.” MATHAYO 15:21-26
  HAPA YESU ALITOA HAYA MANENO AKIFUATISHA WAYAHUDI WALIVYOWAITA MATAIFA

  “AKAMWAMBIA, WASIPOWASIKIA MUSA NA MANABII, HAWATASHAWISHIWA HATA MTU AKIFUFUKA KATIKA WAFU” LUKA 16:31

  YESU ALITOA UNABII JUU YA KUFUFUKA LAZARO KUTOKA WAFU AMBAYE HATA HIVYO BADO HAWAKUAMINI WAKATAKA WAMUUE KAMA WALIVYOWAFANYA MANABII NA LAZARO MWENYEWE ALITOKEA KABURINI SI KIFUANI PA IBRAHIMU HIVYO YESU ALITUMIA MFANO HUU WA FUMBO LA LAZARO NA TAJIRI.

  KUMBUKA LAZARO KATIKA KISA CHA YESU ALIONEKANA KULA MAKOMBO NA MBWA (WATU WA MATAIFA)

  MAKUHANI WALITIMIZA UNABII WA YEU KATIKA KISA CHA LAZARO KWA KUTOKUAMINI HATA WALIOFUFUKA

  “AKAMWAMBIA, WASIPOWASIKIA MUSA NA MANABII, HAWATASHAWISHIWA HATA MTU AKIFUFUKA KATIKA WAFU” LUKA 16:31

  “NA WAKUU WA MAKUHANI WAKAFANYA SHAURI LA KUMWUA LAZARO NAYE;” YOHANA 12:10

  MUNGU ALITAKA ISRAELI WAWE NURU YA MATAIFA KWA KULISHA MATAIFA CHAKULA /NENO (LAZARO NA TAJIRI)

  “NAAM, ASEMA, HIVI, NI NENO DOGO SANA WEWE KUWA MTUMISHI, WANGU ILI KUZIINULIA KABILA ZA YAKOBO, NA KUWAREJEZA WATU WA ISRAELI WALIOHIFADHIWA; ZAIDI YA HAYO NITAKUTOA UWE NURU YA MATAIFA, UPATE KUWA WOKOVU WANGU HATA MIISHO YA DUNIA.” ISAYA 49:6

  WAISRAELI WALIONGEZA SHERIA 613 NA YESU ALIPOKUJA AKAWAFUNDISHA NAMNA YA KUSHIKA TORATI IVYOPASWA SI KUWAONGEZEA WATU SHERIA. BADO WAKIKATAA IMANI

  “PAULO NA BARNABA WAKANENA KWA USHUJAAA WAKASEMA, ILIKUWA LAZIMA NENO LA MUNGU LINENWE KWENU KWANZA LAKINI; LAKINI KWA KUWA MNALISUKUMIA MBALI, NA KUJIONA NAFSI ZENU KUWA HAMKUSTAHILI UZIMA WA MILELE, ANGALIENI TWAWAGEUKIA MATAIFA.” MATENDO 13:46

  TUNAASWA NINI WATU WA MATAIFA WA LEO?

  “VEMA. YALIKATWA KWA KUTOKUAMINI KWAO, NA WEWE WASIMAMA KWA IMANI YAKO.USIJIVUNE BALI UOGOPE.” WARUMI 11:20
  1.
  PALESTINA NA ISRAELI NI VITA YA KIMWILI, LENGO LA SASA NI KUWACHANGANYA WAKRISTO KUWASHABIKIA WAISRAELI KWA BENDERA KATIKA MAKANISA, NA KUWAPOTEZA KISYCKOLOJIA KATIKA VITA YA AMAGEDONI. ILI WASHABIKIE VITA YA KIMWILI ITAKAPOKUWA INAPIGANWA KATI YA ISRAELI WA KIMWILI NA KUSAHAU VITA HALISI YA AMAGEDONI.

  2.JIULIZE KANISA LINALOWAUNGANISHA WAYAHUDI NA WAISALAMU SASA, WAKATI KANISA LINGINE KUBWA LIKIUNGANISHA WAKRSTO WOTE NA KUWAELEKEZA KWA WAYAHUDI KWA IBADA,SADAKA NA MAOMBI WA KIMWILI WAMEKUWA NA AGENDA GANI?

  3.KUMBUKA ALIYETIMIZA UNABII KARNE YA 70 A.D KUBOMOA HEKALU, NDIYE ALIYEWAFANYA WAISLAMU WAPATE FURSA YA KUJENGA HEKALU JUU YA HEKALU LA ISARELI AMBALO YESU ALITABIRI LISINGEBAKIA JIWE.

  “HAMJUI YA KUWA NINYI MMEKUWA HEKALU LA MUNGU, NA YA KUWA ROHO WA MUNGU ANAKAA NDANI YENU?” 1 WAKORINTHO 3:16:

  KAMA ILIVYOKUWA KWA KAINI NA ABELI PAMBANO LA AMAGEDONI. MTU AMBAYE ANAMTOLEA DHABIHU (MIILI YESU) MUNGU KWA USAHIHI NDIO ATACHUKIWA NA KILA MTU NA KUONEKANA KAMA NDIYE MUASI.HIVYO SHETANI KULAZIMIKA KUTUMIA MANABII WA UONGO HATA KWA NGUVU ZA SHETANI KUSHUSHA MOTO (NA ROHO ZA AJABU) HATA WATU WATAAMINI CHA UONGO NA KUCHUKIA CHA KWELI.

  “WALAKINI WAYAHUDI WASIOAMINI WAKAWATAHARIKISHA WATU WA MATAIFA NA KUWATIA NIA MBAYA JUU YA NDUGU.” MATENDO 14:2

  “MAANA HAWAWI WOTE WAISRAELI WALIO WA UZAO WA ISRAELI” WARUMI 9:6

 35. SHALOM WAPENDWA
  SUALA LA ISRAEL WENGI WANALISHABIKIA BILA KUJUA UNDANI WAKE. BIBLIA HAITUAGIZI KULIOMBEA TAIFA PHYSICAL LA ISRAEL. KIUHALISIA TAIFA PHYSICAL LA ISRAEL LINAONGOZWA NA MASHETANI WABAYA SANA NA NDIYO WANAOSABABISHA SHIDA NYINGI SANA DUNIANI NA WANA MIPANGO HATARI YA KUTESA NA KUUA WANADAMU DUNIANI. KWA HIYO UNAWEZA KUWA UNAMWOMBEA SHETANI AFANIKISHE MIPANGO YAKE KWA KUPITIA TAIFA LA ISRAEL PHYSICAL. KWA UNDANI GOOGLE
  NA USOME THE PROTOCOLS OF THE LEARNED ELDERS OF ZION.
  UKISOMA NA KUELEWA UTAGUNDUA KWAMBA HATA MAHUBIRI YETU YA SASA SIYO TUNAYOTAKIWA KUHUBIRIWA MAANA TUKO VITANI NA HATARINI. NA TUMELALA HAKUNA ANAYECHUKUA HATUA, TUMEISHIA KUOMBA TU BILA KUCHUKUA HATUA NA SHETANI ANAFANYA SHEREHE.

  SOMA TENA KITABU THE UNSEEN HANDS.

  MAKANISA MENGI YAMEPEWA HELA KUHUBIRI UONGO NA KUHAKIKISHA WAKRISTO HAWAIJUA KWELI YOTE.

  WATU WAENDE SHULE LAKINI KAMWE WASIELIMIKE HATA KAMA MAMILIONI WANAPATA PhD, wanabaki watumwa tu.

  MUNGU ATUPE MACHO YA ROHONI

 36. Ivi kuomba ndio maana yake kubariki,au tumekariri tu?
  Kama ni kuomba,hata wapalestina wanamwitaji Yesu,tuwaombeeni.

  Let’s pray for the church not for Israel if u guys know how to translate scriptures.
  Time for Israel will come, whether we pray or not.

 37. Amen!Nimuhimu tuendeleze maombi tukumbuke hata wenzetu wawanaelekea kutembelea IZRAEL wiki ijayo mbarikiwe(F.Marandu———————

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s