Wakati mapepo yanatolewa, huwa yanasema kweli?

maombi

Dear wapendwa

Nawasalimu katika jina la Bwana. Mimi ni mkristo ambaye kusema kweli nilikuwa nimepotea kwa maana sikuwa na kweli ya Mungu ndani yangu. Baada ya kupata misukosuko mingi ya maisha nikaamua rasmi kumfuata Yesu.

Nilianza kwenda kanisani mimi na familia yangu  na kwenye maombi pia, tukiwa kwenye maombi msichana wa  kazi akapandisha mapepo na kuanza kusema mambo  mengi ambayo bibi yake, majirani zetu pamoja na ndugu zangu huwa wanaifanyia familia yangu ni vitu vingi sana. Baada ya maombi mchungaji akanisihi sana nisianze kugombana na watu waliotajwa  kuwa wanaifanyia mabaya familia yangu kitu ambacho hata mimi najua siruhusiwi kufanya kwa kuwa hata mimi ni mwenye dhambi mbele za Mungu.

Sasa swali langu wapendwa nataka kujua je mtu anapokuwa amepandisha haya mapepo wakati wa kuombewa yale mambo anayoyasema ni  ya kweli? kuna mda nilikuwa nasikia mpaka tone ya sauti za ndugu zangu kama ndio wanaongea wenyewe, imenichanganya sana sio kwa sababu nataka kulipiza hapana nataka kujua ukweli ili hata kama nawaombea niwe najua wamefanya kweli.

Pls nisaidie  kunijibu, mi bado mchanga  sana kiroho.

Its Daniel

Advertisements

7 thoughts on “Wakati mapepo yanatolewa, huwa yanasema kweli?

 1. maadam wewe umempa Yesu maisha yako na umejazwa na Roho Mtakatifu. Roho mtakatifu atakufundisha hatua hadi hatua Kuwa jambo hili lilotamkwa ni kweli au si kweli. mtegemee Roho Mtakatifu atakupa ufunuo wa kupambanua la kweli au la uongo maana mwenye uwezo wa kupambanua ni Roho Mtakatifu ndani yetu.huwezi kupata majibu kwa akili za kibinadamu Ila Roho Mtakatifu ni mzoefu atakushuhudia ktk kupambanua.

 2. roho huwa zinajua siri za binadamu.ex.mapepo yalijua kama Yesu ni mwana wa mungu sasa kwa kuwa baba yao ni muongo uwezekano upo wakuleta chuki kwa watu.

 3. Shalom Ndugu Daniel !.Naomba kuanza kwa kusema kuwa mapepo wote ni mawakala wa baba yao mkuu aitwae Ibilisi na shetani. Kuna ukweli kiasi kwamba baadhi ya mambo yanayosemwa na mapepo huwa yapo na mengine yamefanyika LAKINI si kila jambo ni la kweli kwani shetani ni baba wa UONGO.Ninakushauri uwe makini na jinsi hali hiyo inavyojitokeza,usipoteze muda kuyapa nafasi ya kusikilizwa ANGAMIZA KWA JINA LA YESU NA KUTORUHUSU MAZUNGUMZO NAYO.
  Ayoub

  FPCT-KISESA,Mwanza

 4. kaka Daniel, Hongera kwa kuokoka. Yesu ameingia ndani yako na sasa huishi mwenyewe maana Yasu yu ndani. Kwa sababu hiyo basi unaishi kwa Neno , na Neno lenye pumzi ya Mungu,( Neno le Mungu la wakati husika).
  Daniel ndio maana haijalishi pepo limesema kweli ama uongo hamna nafasi ya kuamini au kutendea kazi. Maana neno lake halimo ndani yako.
  pepo linapolipuka hupiga kelele wala si kwamba anataka maelewano ili ahurumiwe hapana bali ni mapambano ili kukupotezea /kupoteza mwelekeo wa mwombaji au anaeombewa, kwa muda huo au baadae.
  mfano- kuna pepo alikua anawatabiria akina paulo kuwa ni watumishi wa Mungu aliyejuu, hakuwa anaongopa, lakini paulo alimkemea. nirahisi sana kusema sio pepo bali nabii wa kweli, lakini Yesu aliyeko ndani yako atajua kilichoko.

  Bwana Yesu aliyeianzisha kazi ndani yako ni mwaminifu naye atafanya. BARIKIWA.

 5. mpendwa mapepo yanapokemewa kwa mamlaka ya jina Yesu huwa yanaogopa sana kwanza lazima ujue yalifanya vita na Yesu kule mbinguni yakashindwa vibaya soma ufunuo 12;7..12 hivyo lazima utambue yanafahamu uweza wa Yesu ila yakikemewa na mtu ambaye hana mamlaka ya jina la Yesu yanaweza kumdanganya ikiwa pamoja na kumdhulu kama vile wana wa sekawa kupata uhakikisho kuwa huwa yana sema kweli soma Marko 5:1..10 pamoja na hayo hata kama yamesema kweli hutakiwi kuyafanyia kazi yale mambo ambayo yamesemwa na mapepo kwani lazima utambue shetani ni baba wa uongo,pia watupaswi kuwachukia watu ambao bado wanatumikishwa na shetani wawe ndugu,jamaa,sisi tunapaswa kuwaombe wapate neema ya wokovu ambayo inakataa ubaya wa kila aina ubalikiwe

 6. Does Satan therefore lie? In John 8:44, Jesus says, “Ye are of your father the devil, and the lusts of your father ye will do. He was a murderer from the beginning, and abode not in the truth, because there is no truth in him. When he speaketh a lie, he speaketh of his own: for he is a liar, and the father of it.” There is no truth at all in Satan; he is a liar. Satan therefore deceives the entire world by lying. He is the grand master of subtlety and deceit. His lies are, for the most part, so subtle that human beings do not recognize them as lies; they accept them as truth. Thus they are deceived. Satan, however, does use the truth to deceive; for if a person were told something that is completely false, he often would be smart enough to recognize the lie. On the other hand, if some of what he is being told is the truth, he is less likely to detect the part that is false; he will accept the lie and be deceived.

 7. Shalom, Mapepo huwa yanasema kweli ,lakini ukweli huo kama hauko makini na neno la mungu huanzisha mafarakano!!

  Maana shetani yupo kugombanisha si kupatanisha, La msingi waombee wote wahusika ili neema ya mungu iwafikie

  barikiwa

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s