“Wazazi wangu ni wachawi”

watoto

Bwana Yesu asifiwe.

Naomba kuuliza, amri ya 4 ya Mungu inazungumzia wazazi, wazazi wangu ni washirikina. na mimi nimeokoka na ninajua maombi ni vita ninaona mauti ipo ndani yetu kati yangu au mzazi wangu. kipi bora kukosa mzazi au kujitoa dhabihu?

–S

 

Advertisements

8 thoughts on ““Wazazi wangu ni wachawi”

 1. Usiogope, katika madraja yote ya kipepo, la wachawi ndilo daraja la chini kabisa yaani ndiyo jeshi la mgambo ambalo shetani analitanguliza kupiga kelele lakini halina chochote. Wewe kwa kuliogopa unalikweza bure. Wewe achana nalo endelea kujenga uhusiano wako mzuri na wazazi wako. Waheshimu kama amri inavyosema wasaidie na ukitaka kuwashinda wape kila wanachokihitaji. Usikubali kugombana nao kwa njia ya maandiko kwakuwa katika maandiko hamna uzima ndani yake ila katika neno la Mungu ndiko kwenye uzima. ndiyo maana mtume Paulo alisema neno huua na tena huhuisha. Usikubali likuuwe kwakuwa ukiua wazazi na wewe utauawa, je ukiuwa utakwenda mbingu ya wapi, je kuna mbingu ya wauaji? Halafu nani alikwambia ukimwomba Mungu auwe mtu anakubali? huko ni kudanganyana, Mungu anatoa uhai wa mtu kwa kutaka kwake mwenyewe wala hashinikizwi na mtu mwogope Mungu. Kusema utamwomba Mungu auwe mtu huko ni kumfanya Mungu kuwa yeye ni kitu simple si kweli. Mkumbuke yule jamaa aliyesimuliwa na Yesu aliyepewa talanta moja akasema ” Nilijua ya kuwewe ni mtu mgumu sana, wavuna usipopanda na wakusanya usipotawanya hivyo nikaogopa….” Je wewe humwogopi Mungu kumwamrisha auwe mtu? Kama huelewani na wazazi wako jirekebishe kwa vyovyote vile wewe ndiwe mwenye matatizo. Soma Mithali 16:7 ” Njia za mtu zikimpendeza Bwana hata adui zake huwapatanisha naye”. Jihadhari sana kama umeokoka sitegemei uwe na roho ya ukatili kutaka kuuwa wazazi wako. Wanaokushauri uuwe kaitka koo zao kuna wachawi vilevile. Sasa waulize wao wameuwa wangapi? au wanakushauri wewe uuwe wao wakae salama? utavunja amri ya ” USIUE”. !!! Kumbuka uchawi ni ibada kama yako wewe. Kwakuwa haikuhusu achana nayo waachie wenyewe. SASA JE SHETANI ANGEKULETEA JESHI LA MAKANALI UNGEFANYEJE? ACHANA NALO.

 2. Mimi nakushauri mambo 2 wakitaka watubu waokoke la hawataki neno Kutoka: 22:18 Litimilike kwao mara moja, kwa kuwa neno halikusema awe ni baba au mama au kaka au dada limesema MCHAWI ASIISHI, na ujue ndugu yangu nikueleze siri ya wachawi hawana huruma kabisa kabisa

 3. Wachangiaji wengi wameshaeleza
  waefeso 4:1-4 inatoa wajibu wa mtoto pia kutoka 22:18 inatoa hukumu kwa mchawi.
  we maliza kila kitu ktk ulimwengu wa roho.

 4. wewe endelea kuwaombea wazazi wako, wewe ni msaada mkubwa wa kiroho kwao

 5. Harris kamaliza issue yote hapo juu… waondoe ukiwaacha wakikupata wewe umeondoka ndugu yangu, u dont wanna go pre-maturely but live long to fulfill what God has pre-destined for you. but if you want go to heaven early thats ok let them live, since you are born again you will go to heaven.

  Omba dangerous prayers uwaue, ile habari ya wasemehe kwasababu hawajui walitendalo haipo hapa… hii mi-jitu inajua wanayoyatenda.. they are working for our advesary. wayahudi ndo walikuwa hawajui walitendalo kwa sababu mtu waliokuwa wanamuua hawakujua kuwa ndiye masiha.

 6. Pole sana rafiki yetu katika Kristo!.soma 1kor 10:12-13. Hilo ni jaribu tu,kikubwa usipanik ila muombe Mungu akupe busara za kuweza kuwabadilisha maana wewe umekuwa NURU kwao hivyo usichukue hayo maamuzi magumu ila uwe na subira katka Kristo Yesu Bwana Wetu. Pia jaribu kuwashirikisha viongozi wako wa kanisa!. Pole sana na Mungu akusaidie kwa hilo. Amen

 7. MOJA: KUHUSU AMRI YA NNE

  NDUGU AMRI YA TANO NDIO YA KUHUSU WAZAZI/YA NNE NI YA SABATO/ANGALIA MPANGILIO HUU HALAFU. soma KUTOKA 20:2-17

  1.USIWE NA MIUNGU MINGINE ILA MIMI.

  2. USIJIFANYIE SANAMU YA KUCHONGA,WALA MFANO WA KITU CHOCHOTE KILICHO JUU MBINGUNI, WALA KILICHO CHINI DUNIANI,WALA KILICHO MAJINI CHINI YA DUNIA. USIVISUJUDIE WALA KUVITUMIKIA; KWA KUWA MIMI, BWANA, MUNGU WAKO, NI MUNGU MWENYE WIVU; NAWAPATILIZA WANA WA MAOVU YA BABA ZAO, HATA KIZAZI CHA TATU NA CHA NNE CHA WANICHUKIAO, NAMI NAWAREHEMU MAELFU ELFU WANIPENDAO, NA KUZISHIKA AMRI ZANGU.

  3.USILITAJE BURE JINA LA BWANA, MUNGU WAKO, MAANA BWANA HATAMHESABIA KUWA HANA HATIA MTU ALITAJAE JINA LAKE BURE.

  4. IKUMBUKE SIKU YA SABATO UITAKASE. SIKU SITA FANYA KAZI, UTENDE MAMBO YAKO YOTE; LAKINI SIKU YA SABA NI SABATO YA BWANA, MUNGU WAKO, SIKU HIYO USIFANYE KAZI YOYOTE,WEWE, WALA MWANA WAKO, WALA BINTI YAKO, WALA MTUMWA WAKO, WALA MJAKAZI WAKO, WALA MNYAMA WAKO WA KUFUGA, WALA MGENI ALIYE NDANI YA MALANGO YAKO. MAANA, KWA SIKU SITA BWANA ALIFANYA MBINGU, NA NCHI, NA BAHARI, NA VYOTE VILIVYOMO, AKASTAREHE SIKU YA SABA; KWA HIYO BWANA AKAIBARIKIA SIKU YA SABATO AKAITAKASA.

  5.WAHESHIMU BABA YAKO NA MAM.A YAKO; SIKU ZAKO ZIPATE KUWA NYINGI KATIKA NCHI UPEWAYO NA BWANA, MUNGU WAKO.

  6.USIUE.

  7.USIZINI.

  8.USIIBE.

  9.USIMSHUHUDIE JIRANI YAKO UONGO.

  10.USITAMANI NYUMBA YA JIRANI YAKO, USIMTAMANI MKE WA JIRANI YAKO; WALA MTUMWA WAKE,WALA MJAKAZI WAKE, WALA NG’OMBE WAKE, WALA PUNDA WAKE, WALA CHOCHOTE ALICHONACHO JIRANI YAKO.

  PILI: KUHUSU WEWE NA WAZAZI

  WAEFESO 6:1-4

  “ENYI WATOTO, WATIINI, WAZAZI WENU KATIKA BWANA.MAANA HII NDIYO HAKI. WAHESHIMU BABA YAKO NA MAMA YAKO; AMRI HII NDIYO AMRI YA KWANZA YENYE AHADI, UPATE HERI, UKAE SIKU NYINGI KATIKA DUNIA. NANYI, AKINA BABA, MSIWACHOKOZE WATOTO WENU; BALI WALEENI KATIKA ADABU NA MAONYO YA BWANA.”

  HILO FUNGU LINATUAMBIA TUWATII WAZAZI KATIKA BWANA, KAMA JAMBO NI KINYUME NA MAPENZI YA MUNGU HATUPASWI KUWATII KATIKA JAMBO HILO.

  MCHAGUE YESU, SIO KILE WAZAZI WAKO WANACHOKITUMIKIA

  YOSHUA 24:15
  “NANYI KAMA MKIONA NI VIBAYA KUMTUMIKIA BWANA, CHAGUENI HIVI LEO MTAKAYEMTUMIKIA; KWAMBA NI MIUNGU ILE AMBAYO BABA ZENU WALIITUMIKIA NG’AMBO YA MTO, AU KWAMBA NI MIUNGU YA WAAMORI AMBAO MNAKAA KATIKA NCHI YAO; LAKINI MIMI NA NYUMBA YANGU TUTAMTUMIKIA BWANA.”

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s