Useja wa mapadri sasa katika mjadala, wanawake nao ruksa kuwa maaskofu.

askofu

Wimbi la mabadiliko hayo limeyakumba makanisa hayo mawili baada ya viongozi wao wakuu kulazimika kufanya maamuzi mazito juu ya mapadri na maaskofu wanaoyatumikia , ambapo tayari wanawake wameruhusiwa kuwa wachungaji na maaskofu, huku suala la mapadri kutoruhusiwa kuoa likipata ruksa ya kujadiliwa.

Wimbi hili la mabadiliko limekuja wakati mmoja, ambapo kwa upande wake kanisa Anglikana tayari limeruhusu rasmi wanawake kuwa wachungaji na maaskofu , wakati kanisa katoliki nalo limeruhusu mjadala juu ya ama mapadri wake waendelee na utaratibu wa kutooa au waoe.

Vyombo vya habari vilielezea tukio hilo kama moja ya matukio makubwa katika karne ya 21 kwa kanisa Anglikana, lililoanza tangu miaka 20 iliyopita na hatimaye kukamilika hivi karibuni.

Shirika la habari la kimataifa la sky News limemkariri Askofu Welby akisema kuwa amefurahishwa sana na matokeo ya kura hizo na kwamba ni mwanzo mzuri wa shughuli kubwa ijayo.

Nayo Televisheni ya kimataifa ya CNN katika moja ya vipindi vyake vilivyoripotiwa juu ya tukio hili ilibainisha kwamba huenda kanisa Anglikana likawa na maaskofu wengi wanawake kuanzia mwishoni mwa mwaka huu.

Advertisements

12 thoughts on “Useja wa mapadri sasa katika mjadala, wanawake nao ruksa kuwa maaskofu.

 1. Wapendwa,

  Acha nimnukuu Mtumishi wa Mungu Paulo sawasawa na walionitangulia:

  “I Kor 7:8 Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, Ni HERI wakae kama mimi nilivyo.”
  “1 Tim 1:1-3:
  Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe; WAKIWAZUIA WATU WASIOE, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.”

  Ukilinganisha shairi hizi mbili ndipo utajilinda kuhukumu mwenzio. Hakuna andiko lililo kubwa kuliko lingine. Paulo anaposema ni heri kubaki kama yeye huku akiwa kiongongozi wa kanisa pia bila mke alipenda tujue kama kuwa na mke inaweza punguza nguvu za utumishi. Ndipo akasema ni heri kuwa kama yeye. Pia akaendelea akisema” I Kor 7:9 Lakini ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe; maana ni AFADHALI kuoa kuliko kuwaka tamaa”. Hivi hatuwezi sema kama tendo la kuoa kwa Mtumishi wa Mungu ni ujasiri wala utakatifu, la hasha, ni kukimbia tamaa.

  Nafikiri tusiwe haraka kukukumu kanisa la katoliki kwa hilo jambo lakini tuwahimize walioapa kuwa na ule ujasiri wa kutooa ili pamoja na hiyo wasiwake tamaa. Sivyo wataitwa wanafki.

  Ahsante wapendwa.

 2. Yuvenary,

  Hakuna dhambi ya kutokuoa, bali kuna dhambi ya kutamani au kuwaka tamaa! Kwahiyo kama ulidanganywa ukasaini kwamba hutaoa, ukapewa nafasi ya utumishi wa kitume wenye sharti la useja, huku Biblia yako unayo; mizaha kama hiyo utailipia huko mwisho kwa gharama ya nafsi yako!

 3. Kuna dhambi gani endapo MTU asipooa.Kwann Paulo hakuoa, to reference katika maandiko dhambi ni ipi kwa MTU asipoooa

 4. “BASI IMEMPASA ASKOFU AWE MTU ASIYELAUMIKA, MUME WA MKE MMOJA,..”
  1 TIMOTHEO 3:2

  NADHANI WAO SIO WAUME KAMA TIMOTHEO ANAVYOSEMA

 5. Sungura,

  Unapoingia kazini, jambo la kwanza huwa unapewa Masharti ya Kazi – Rules and Regulations, ukiyaafiki ndipo unapewa Mwongozo wa kazi. Hakuna taasisi isiyo na jambo hilo, labda iwe inaendeshwa kiholela!

  Katoliki kama taasisi ya kidini, kupitia Masharti hayo, huwazuia KUOA au KUOLEWA wote wanaotaka nafasi ya utumishi ktk “Huduma ya Kitume” ya taasisi hiyo, hawa ndio tunaowaongelea ktk mada hii na si waumini wote wa kanisa hilo. Pia kuwa mtumishi ktk kanisa hakukufanyi usiwe “mtu” mbele ya Mungu, ndio maana Maandiko hayajasema “kuwazuia mapadre wasioe”; hata hivyo, upadre wenyewe wameupata baada ya kulikubali zuio hilo wakiwa ni watu!!

  Pia licha ya kwamba waliyaridhia Masharti ya hiyo “kazi ya kitume”, bado inaonesha kwamba wengi waliingia humo kukidhi dhiki ya maisha waliyokuwa nayo au kwa ushawishi, jambo linalojionesha kupitia utandawazi uliopo ktk huko kushindwa kwao. Mambo mengi yanafumuka hadharani yanayohusu udhalilishaji wa kijinsia, na inaonesha kwamba yamekuwepo karne nyingi ndani ya jumuia hizo, wengi wanashindwa kuzitimiza nadhiri zao walizojidhania wameitiwa, ndiyo hayo manung’uniko ya akina askofu Milingo!!!

  Kuhusu 1Tim 1:1-3, hili ni Andiko la unabii, kwahiyo unaponiambia kuwa si lazima wawe Katoliki, sina la kukujibu, kwani hali nzima inategemea kiwango chako ktk kuyaamini Maandiko kutimia kwake. Watu wengi huyategemea mambo kama hayo kutimia huko nje, wanapoambiwa watu watajitenga na Imani, wao hudhania ni hao Waisilamu au hizo dini nyinginezo; wakiambiwa kuhusu hali kuwa kama ya siku za Nuhu, au Sodoma ktk siku ile ya kufunuliwa kwake Mwana wa Adamu, wao huyatazamia mambo hayo huko nje, na hapo ndipo hulikosa jambo zima, maana hayo yapaswa kutokea kanisani; kanisa, hilo lililokabidhiwa hiyo Imani mara moja, ndilo linalojitenga na hiyo Imani na kuyafuata mafundisho ya mashetani; na pia ni kanisa ndilo litakalokuwa ktk hali ya Sodoma kama unavyoliona leo hii!!

  Kwahiyo unapoliona kanisa limezama ktk ushoga, na mafundisho mengine yaliyo kinyume cha Neno la Mungu, kama una macho huambiwi tazama!!!!

  Ninakutegemea uje na “analysis yakinifu kiuchambuzi” ktk msingi wa Maandiko, utuoneshe uhalali wa masharti hayo yanayowazuia mapadre na masister, wasioe au kuolewa, ili kuhalalisha huko kuwa na “dhambi” kwa anayeyavunja kama ulivyoainisha kiwepesi wepesi, huku ukijua fika kwamba “dhambi” inaweza kukusababishia kwenda Jehanum, labda kwa vile ni Wakatoliki, basi watatupwa huko Toharani wakaulipie ulawiti wao!

  Gbu!

 6. Mnaposema kuwa mapadre walizuiwa kuoa nawashangaa sana, tena nawaona mnaongea kishabiki tu wengi wenu.

  Hakuna padre aliyewahi kuzuiliwa kuoa au mtawa (sisters) kuzuiliwa kuolewa. Hawakuijua hiyo condition au sharti baada ya kuwa wameingia kwnye hizo huduma bali mtu anaingia akiwa anajua.

  Kwa hiyo aliyetamani hiyo kazi ilimpasa apige hesabu kwanza kama ataliweza hilo sharti, ndipo aingie. Kanisa katoliki halimwingizi mtu kwenye huo utumishi ndipo baadae linampa hayo masharti, bali anaamua kuingia huku akiwa anjua.

  Na wala hilo sharti siyo dhambi kibiblia kuliweka kwa ajili ya mambo ya kitumishi, na yule anayejiona atauweza huo wito aingie.

  Alichokisema Lwembe kutoka 1 Tim 1:1-3, si lazima kihusiane na suala la mapadre. Kanisa katoliki halijazuia watu kuoa au kuolewa, bali limeweka sharti la kutooa/kuolewa kwa watu wanaotumikia nyadhifa fulani katika kanisa. Sharti liko maalum kwa watumishi wa wadhifa fulani na wala si zuio la jumla kwa wakatoliki wote.

  Mapadre kutooa au kuoa yote ni mema tu wala hakuna dhambi yoyote, cha msingi ni mtu anayetaka kuingia kwenye hiyo kazi ahesabu gharama, maana akiingia na kulivunja hilo sharti wakati aliingia huku akijua lipo kwake huyo ndo dhambi!

  Ni hayo tu!

 7. Harris,

  Musa na Petro walikuwa na wake:
  Kut 21-22 ”Musa akawa radhi kukaa kwake mtu yule, naye akampa Musa binti yake, Sipora. Huyo akamzalia mwana, akamwita jina lake Gershomu, maana alisema, Nimekuwa mgeni katika nchi ya ugeni.”

  Mk 1:30 “Naye mkwewe Simoni, mamaye mkewe, alikuwa kitandani, hawezi homa…”

  Lakini suala la Wakatoliki na fundisho lao la kuwazuia mapadre kuoa , hilo liko wazi kama utayaamini Maandiko, 1 Tim 1:1-3:
  “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe; WAKIWAZUIA WATU WASIOE, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.”

  Umeelewa ndg yangu? Na wengine walio ktk mafundisho ya mashetani ni Wasabato, hao wenye kuwaamuru wafuasi wao wajiepushe na vyakula!!!

  Hakuna sehemu ktk Maandiko yanapotuambia hao wenye mafundisho ya mashetani watayatubia, ndio maana unawaona wakiwa ktk majadiliano kuhusu jambo hilo haswa wanapolitazama ktk gharama kwa kanisa, iwapo padre mmoja wa kiswahili ataoa halafu awe na watoto kumi, wote hawa watunzwe na kusomeshwa na kanisa, inakuwaje kwa mapadre 1000??

  Gbu!

 8. pole, vai, INAONYESHA HUJUI HATA KILE UNACHIKOSEMA NA BIBILIA HUJAISOMA VIZURI .LABDA NDIO MAANA UNAPATA HISIA KALI HIVYO.NATUMAINI UNAFAHAMU KWAMBA PAULO HAKUOA, LAKINI KABLA HUJAWAJAJI MAPADRE WAKATOLIKI KWANZA WAPENDE KISHA UJUE KWANINI HAWAOI? WANAWAKE WENGI WANA HISIA KALI, LAKINI NINGEKUSHAURI UKAFAHAMU SABABU. ZINGATIA KWAMBA KILA ANAYEKUPA SABABU USIZIFANYE NDIO MWISHO ENDELEA KUCHUNGUZA. NADHANI USINGEKUJA NA MAJIBU KAMA HAYA. KWANI NI MAJIBU AMBAYO HATA PADRE MWENYEWE ATAKUSHANGAA NA KUJUA UELEWI UNACHOSEMA. MUNGU AKUBARIKI SANA.

 9. Kwakweli tunamshukuru MUNGU WA ELIYA KWA KUENDELEA KUUFUNUA UWONGO WA DINI NA KUUWEKA WAZI. HUO NI MWANZO TU YAPO MAMBO MENGI YALIYOKUWA YANAFANYWA NA DINI NA MADHEHEBU AMBAYO HAYAKUWA MPANGO WA MUNGU BALI NI MIPANGO YA WATU TU. MTAENDELE KUYASIKIA TU. KULIKUWA NA SIRI KUBWA YA KUWAZUIA MAPDRI, MASISTER, MAASKOFU N.K KUTOOA/ KUTOOLEWA. NINA HAKIKA HAKUNA SEHEMU YOYOTE KWENYE KITABU CHA NENO (BIBLIA) AMBAPO MUNGU ALIKATAZA WATUMISHI WAKE WASIOE! SHIKA NENO! HAKIKAZI 12!

 10. @M.J. Siyi halikuwa tatizo bali jambo jema limegeuka Tatizo. Kwani kiliwazuia nini manabii kama Musa, Eliyah, Paulo, petro wasioe?.
  Ile ni sadaka walikuwa wanatoa-huwezi toa sadaka ile kama wewe sio mzima. Hivyo alihitajika Padre mzima kimwili aweze kuitoa kwa ajili ya kumtumikia Mungu. But utandawazi na maendeleo yameathiri kila kitu.

 11. Heggerian principle;
  “They created the problems, and are the ones to find solutions” Heretics!!!! Mungu atusaidie

 12. Nadhani mwisho Wa binadamu kuwa civilized ulikuwa haujafika peak.walioufanya ukawa stagnant kwa kuzuia mabadiliko wanaanza kuonja joto ya jiwe.maendeleo ni matokeo ya mabadiliko chanya.waache mapadre Wa dot com waoe. Na wanawake wapewe nafasi.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s