Mama mchungaji kuwa mshirika kanisa tofauti na baba mchungaji!

Picha kwa hisan ya Annah Brock

Nina swali wapendwa, mimi ni mke wa mchungaji kwa miaka miwili, nina maswali mengi, lakini leo nitauliza, Je ni vibaya mke wa mchungaji kuwa mshirika wa kanisa lingine ambalo mumewe halichungi?

Asanteni.

 

Advertisements

18 thoughts on “Mama mchungaji kuwa mshirika kanisa tofauti na baba mchungaji!

 1. Sungura,

  Katika yale uliyoniambia niyachunguze, nimefanya hivyo na nilichokiona ni hiki:
  Kuhusu
  1. Ivi ulishawahi kugundua kuwa hilo suala lilikuwa linahusu mwanaume aliyeoa na mwanamke aliyeolewa?
  Nilichokiona ktk suala hili la kufunika kichwa ni kwamba linawahusu wanawake wote, maana wote wanapaswa wamilikiwe, aidha na mumewe au na babaye kwa yule asiyeolewa. Na kwa wajane na walioachika, hawa humilikiwa na Kristo, na hivyo kubaki ktk fundisho la msingi kulingana na jinsia yao alimradi wanaendelea katika imani.

  Ukisoma HES. ‭30‬:‭3-9‬, unaweza kuliona jambo hili kuhusu wanawake kwa uwazi zaidi kiwajibu. Na ninaamini huu ndio msingi anaouongelea mtume Paulo, Torati, yule “mwalimu” anayetuleta kwa Kristo. Labda ngoja niyanukuu hayo Maandiko:
  “Tena mtu mke atakapomwekea BWANA nadhiri, na kufunga nafsi yake kwa kifungo, naye aketi katika nyumba ya babaye, katika ujana wake; babaye naye akasikia nadhiri yake, na kile kifungo chake alichofungia nafsi yake, na babaye akamnyamazia; ndipo nadhiri zake zote zitathibitika, na kila kifungo alichofungia nafsi yake kitathibitika. Lakini kama huyo babaye akimkataza siku hiyo aliyosikia; nadhiri zake ziwazo zote, wala vifungo vyake alivyoifungia nafsi yake havitathibitika; na BWANA atamsamehe, kwa kuwa babaye alimkataza. Tena kama amekwisha kuolewa na mume, wakati huo wa nadhiri zake, au wa neno hilo alilolitamka kwa midomo yake pasipo kufikiri, alilojifungia; na mumewe akasikia, naye akamnyamazia siku hiyo aliyosikia neno hilo; ndipo nadhiri zake zitathibitika, na vile vifungo ambavyo ameifunga nafsi yake vitathibitika. Lakini kama mumewe akimkataza siku hiyo aliyolisikia; ndipo ataitangua nadhiri yake iliyo juu yake na neno alilolitamka kwa midomo yake pasipo kufikiri, alilojifungia; na BWANA atamsamehe Lakini nadhiri ya mjane, au ya mwanamke aliyeachishwa mume, kila neno ambalo ameifunga nafsi yake kwalo, litathibitika juu yake.” (‭HES.‬ ‭30‬:‭3-9‬ SUV)

  2. Ulishawahi kugundua kuwa mwanamke alikuwa anatakiwa kufunika kichwa wakati anaposali na kuhutubu tu?
  Ni sawa, kulingana na mazingira yalivyokuwa ktk Agano la Kale, sala zilikuwa na nyakati na zilifanyika hekaluni; kwahiyo tunaweza kusema kusali na kuhutubu vilikuwa vikifanyika hekaluni, na kama vilifanyika majumbani, itakuwa ni hapo ilipolazimu. Lakini pia Maandiko hayohayo yanasema mwanamke asipofunika kichwa na anyolewe, na ikiwa ni aibu kwa mwanamke kunyolewa basi na afunike kichwa chake. Kutoka maelezo haya ninafika ktk uelewa kwamba mwanamke anapaswa awe amefunika kichwa chake wakati woooote ili asiwe ktk aibu, haswa ktk wakati wetu wa Agano Jipya huku ambapo amepewa ukuhani!

  3. Ulishawahi kugundua kuwa mwanamke alitakiwa au afunike kichwa au kama hataki kufunika awe na nywele ndefu?
  Hapa ndipo sehemu ya tatizo linapoanzia au kuzaliwa. Maelezo yako haya yanaongelea kitu kimoja lakini yamevifanya viwili!

  Wakati wote Maandiko yanaposema mwanamke afunike kichwa chake ktk hivyo vifungu vya mwanzoni, ni kweli hayajatamka afunike kwa kitu gani, Makanisa mengi yaliyolivamia jambo hili, ktk haraka zao wakajitafsiria kifuniko hicho kuwa ndio hivyo vitambaa wanavyofunga wanawake ktk hizo ibada zao. Lakini hawa wameikosa KWELI ya jambo hili, kwani Neno la Mungu li kamili, basi, ktk ukamilifu wake haliwezi likakuachia sisi tumalizie jambo lake kwa akili zetu za kukisia kisia! Ndipo ktk vifungu vya kumalizia maelekezo hayo, Mungu anasema amempa mwanamke nywele ndefu ili ziwe hicho kifuniko!!!!

  4. Unajua kuwa agizo hilo pia linamtaka mwanaume asifuge nywele/asiwe na nywele ndefu?
  Hili ni sawa, tena si kufuga nywele tu bali hapaswi kusali akiwa amefunika kichwa chake kama maaskofu wanavyovaa zile kofia zao kwa order ya zamani wakiwa wameikosa hii mpya!

  Kuhusu makanisa yanayo practice maelekezo hayo, vipengele 1-3 tafakari yake nimeisemea ktk maelezo ya hapo juu.

  Kuhusu
  4. Je, wanawaruhusu wanawake kuwa na nywele ndefu kama mbadala wa kufunika vichwa?
  Hapa pia kuna tatizo la tafsiri. Kwa makundi yanayowafungisha wanawake vitambaa, kwa hawa haijalishi mwanamke ana nywele ndefu au amezikata, wote hufunga vitambaa siku za ibada, huko majumbani kwao, nahisi wakitaka kusali basi huenda wanafunga kwanza vitambaa halafu ndio wanaendelea na sala, labda ya mezani au ya usiku! Kulingana na niliowaona wa hayo makusanyiko, wakiwa ndio “waraka”, suala la nywele ndefu au kuzikata kwao sio issue kabisa, sijui kuhusu extremes nyingine ikoje, lakini nje ya Neno la Mungu unaweza kukumbana na chochote kile; si umewaona wengine wakilishwa majani kama ng’ombe!

  Halafu kuna kundi jingine, hawa ndio kali kuliko! Wenyewe kutoka vifungu hivyo wamelitafsiri Neno hilo kwamba mwanamke hapaswi kuwa na nywele ndefu, akiwa na hizo basi afunge kitambaa au anyolewe! Kwahiyo wanawake wengine kuliko kufunga vitambaa, wao huzinyoa na hivyo kuishia kusali wakiwa wamenyolewa!!!!!

  Mwisho kuna makundi ambayo hayajui chochote kuhusu Maelekezo hayo yanayohusu hali ya mwanamke asalipo, wao wanajiendea tu bila nanga, wa kunyoa na anyoe tu, akifunga kitambaa basi ujue ni fasheni, hata mwenye nywele ndefu leo, kesho anaweza kuja na kipara kinachong’aa!

  Pia kuhusu mawigi, hili ni jambo lisilo na rejea ya Maandiko kama huko kufunga vitambaa kwa masharti, au kunyolewa nywele, vyote ni ishara ya wazi ya kuyakosa Maandiko, ama kwa uhakika kugeuzwa kuwa dhihaka ya Maandiko bila wewe kulijua hilo licha ya kwamba unayo Biblia yako kwapani!

  Nayo makundi yote haya hudai kuongozwa na RM ktk hayo wanayoyafanya kinyume na Neno la Mungu!

  Unaonaje Sungura, tutapona kweli????

  Gbu!

 2. Swali hili ni zuri na linahusiana sana na mambo ya ufahamu wa kiungu na si wa kibinadamu. Wengi wametoa maoni yao, nami nimeona nitoe ya kwangu pengine yanaweza kumsidia mama mchungaji
  Tukisoma maandiko na tuyasome katika roho na si kama hadithi ndipo yatakuwa msaada kwetu. Kwanza, kabisa nianze kwa kusoma maandiko kutoka Waefeso 4:11. Mtume Paulo anachosema hapa ni kuwa baada ya Yesu kupaa alikuwa amekwisha kuwaachia watu huduma tano. Mtume Paulo akaziorodhesha kwa ukubwa wake akianzia na ya juu kabisa ya Utume nay a chini kabisa ya Ualimu. Ukubwa wake siyo umuhimu ila tunaweza kusema ni cheo cha huduma.
  Pili, Mwanadamu yeyote anapozaliwa anatoka na hizo huduma ila kama Mungu atakavyomjaalia ana-activate ama moja, mbili au hata zote kwa mtu mmoja. Ndiyo maana unaona kila mtumishi ana nguvu ya Mungu iliyotofauti na ya mwenzie kutegemeana na yeye anavyomchukulia Mungu. Yaani akimchukulia Mungu kwa wepesi na Mungu naye anakuja kwake kwa wepesi, kadhalika akimchukulia Mungu kwa uzito na Mungu naye atakuja kwake kwa uzito. Maana Mungu hamdhulumu mtu wala kumpendelea mtu ila anatoa kwa haki. Anasema katika Zaburi nimempa msaada aliye hodari. Kile alichokipokea kutoka kwa Mungu ndicho kinachomfanya mtumishi mmoja awe tofauti na mwingine kwa ufahamu, na namna anavyo kifikisha ujumbe kwa walengwa pamoja na mahitaji ya walengwa. Kile alichokipokea kinaweza kumfanya aamini mafundisho tofauti na ya mtumishi mwingine lakini wote wamepewa na Mungu. Lakini kumbuka hata shetani ni mtumishi wa Mungu. Tofauti ya kile watumishi wanachoamini ndiyo imeleta kuwepo kwa madhehebu. Wote wanamwamini Mungu/Yesu/Roho Mtakatifu lakini namna ya kufikisha ujumbe wa kile wanachoamini inatofautiana kati ya mtumishi na mtumishi.
  Mama mchungaji mumeo amepewa huduma yake ndiyo maana akawa mchungaji. Lakini je wewe kama mke wake una sehemu katika utumishi wa mumeo? Tuangalie yafuatayo:-
  (i) Amosi 3:1 Watu wawili (walioana) wakisema wanakwenda pamoja wakati huyu yuko
  dhehebu lingine, hao awaendi pamoja kila mtu ana nyumba yake. Kwa maneno mengine mke heshima yako unaipeleka kwa nani? Kwa mchungaji wako au kwa mumeo? Huwezi kuwatumikia mabwana wawili.
  (ii) Mtume Pauli akasema mume ni kichwa nyumba kama vile kristo alivyo kichwa cha kanisa. Ni lazima atapata taabu sana kuongoza nyumba iliyogawanyika ambayo kwa vyovyote vile ina ideologies mbili tofauti maana hawezi kuongoza dhehebu lingine kupitia kwa mkewe na kwa kweli hana haki ya kuliongoza maana sio lake. Soma Waefeso 5:22-24 Hivi unadhani ni rahisi kumtii mume kwa moyo au utamtii kwa mdomo lakini moyo wako ukawa kwenye dhehebu lako!!!?
  (iii) Kwenye Biblia unaona wanawake hawatajwi sana sababu wao wako kwa waume zao maana wao ni mwili mmoja na waume zao. Katika Isaya anasema “siku hiyo wanawake saba watamwendea mwanamme mmoja watasema na tuitwe kwa jina lako, lakini mavazi na chakula tutajitafutia wenyewe. Sasa huyo mke aliye katika dhehebu lingine atatajwa kwa nani? (it would seem unsensible but it remains to be a reality)
  (iv) Wakati mume wako anafundisha siku zote utalinganisha na mafundisho ya dhehebu lako na unaweza ukafika mahali pa kumkosoa mumeo. Na kwasababu mumeo pengine hajapewa huduma kama ya mchungaji unakosali sasa uwezekano wa kukosoa na kumdharau utakuwa ni mkubwa sana. Waweza kusema hutamdharau ila ufahamu ya kuwa shetani yuko kazini halali usingizi atakusababisha tu ukosee. Soma 1Petro 5:8 Je hatakumeza? Kumbuka shetani anatumia sana visababisho au mianya (Loopholes) kuwapata watu wa Mungu. Atasababisha tu ulete upinzani kwa mume wako kwa sababu ya tofauti ya imani katika Kristo Yesu. Haya ninayosema yalimkuta Mikali binti mfalme Sauli. “ 2Samweli 6:1-3, 14-16,20-23. Mikali akamdharau (moyoni) mpakwa mafuta wa Bwana akapata adhabu ya kutokuzaa maisha yake yote. Mungu hajabadilika ni yuleyule atamwadhibu tu mke atakayemdharau mumewe kwa sababu ya tofauti za kidhehebu.
  (v) Huwezi kuwa na hofu ya Mungu hata siku moja. 1Ptro 3:1-2 “wakiutazama mwenendo wenu na hofu” hofu kwa nani? Ya kumhofu Mungu usiyemuona? La! lazima iwe hofu ya Mungu (mumeo) unayemwona ambaye ndiye anaye muwakilisha Kristo. Hofu itatoka wapi wakati mnatofautiana kiimani? Haya uyapime mwenyewe
  (vi) Huwezi kumlinda mumeo! Soma Yeremia 31:22 Kumbuka mumeo kwa kupewa huduma anayo vita kubwa sana kwa sababu anabeba shida za waumini wote alio nao hivyo anahitaji mtu wa kumwombea ili kuweka ulinzi adui asije akammaliza. Huwezi kuweka ulinzi huko kwa mchungaji wako unakoabudu ukaweka na kwa mumeo hiyo nguvu unayo? Sababu hata mfumo wa maombi mtatofautioana na mumeo kwa kuwa utasema kwetu tukiomba lazima tufumbe macho pengine kwa mumeo si lazima, na hivyo ushirika wenu utabatilika tu.
  (vii) Utampa kazi ya ziada mumeo! Ipi? 1Petro 3:7 Itabidi mume akae kwa akili sana na mke wake (niwie radhi wanaume maana nimetoa siri). Soma Mika 7:5 “Wow” hata mke alalaye kifuani mwake asijue habari???!!! Yaani lile ambalo Mungu atasema naye kwa siri ni halali yake kukuficha kwakuwa utalipeleka kwa mchungaji wako. Unakumbuka habari ya Isaka na wanawe mapacha? Isaka alimpenda Esau sababu anamletea nyama ya porini akamfurahia sana. Rebeka akampenda Yakobo sababu alikuwa analima pamoja naye na kuchunga mifugo yao pale nyumbani. Siku moja Isaka alimnong’oneza mkewe akasema “mimi naona siku zangu za kuishi zimekwisha nataka nimbariki mwanangu Esau ili awe mrithi maana yeye ndiye mzaliwa wa kwanza” Rebeka alipopata yaliyo moyoni mwa mumewe na yeye akatamani kipenzi chake ndiye awe mrithi kama mzaliwa wa kwanza, hivyo akafanya maarifa arithi Yakobo mahali pa Esau na kweli akafaulu. Ni Kwa nini? alifunuliwa yaliyo ndani ya moyo wa Mungu (Isaka). Kwa mke wa mtumishi, ukitaka kujua ni nini Mungu anakuwazia jiambatanishe na huduma ya mumeo kwakuwa lolote Mungu atakalosema juu yako atakwambia. Hivi unadhani Mungu akisema “naua huyu mkeo na usimwambie” je? Atakuwambia? Soma habari za Ibrahim unadhani alimwambia Sara habari ya kwenda kumtoa sadaka Isaka? Ndiyo maana hata aliporudi kutoka Moria hakurudi kwa Sara ila alikwenda Bersheba mpaka aliposikia Sara amekufa. Mwanzo 22:15-19
  Nikali ninayo mengi lakini acha niishie hapa.

  UBARIKIWE SANA MAMA MCHUNGAJI

 3. Milinga,

  Umenena vizuri sana!
  Yote uliyoyaeleza ni kweli na yanafaa sana kuzirekebisha hali zilizoingia ktk upotofu, na kuirejesha Amani ya Bwana, isipokuwa jambo hili la mke wa mchungaji kumsaidia mumewe kuhubiri, hili ni tango mwitu; huyo mwanamke akipanda kuhubiri, mumewe itamlazimu achukue nafasi ya mkewe aongozwe naye, maana kwa hiyari yake amekataa kuwa kichwa cha mkewe!!!!

  Gbu brother!

 4. Kilimba,

  Jambo la kwamba makanisa uliyoyataja yako ktk imani moja ni jema na lenye kumpa Bwana utukufu, Yn 17:21-26:
  “Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma. Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja. Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja…”

  Labda nikuulize, kwa kauli yako hiyo ya kwamba TAG, EAGT, FPCT wako ktk imani moja, Je, ndio tuseme kwamba wanakidhi kiwango cha Maandiko hayo?

  Nimeyaona makanisa hayo, moja likiwa mtaa huu na jingine mtaa unaofuata, waumini wakilipita kanisa hili kwenda kuabudu ktk lile, Je, huo ndio umoja anaouzungumzia Kristo????

  Gbu!

 5. Lwembe,

  Kabla ya yote ningependa tujaribu kuona kwa upana kitu kilichosemwa hasa kuhusu wanawake kufunika vichwa vyao ktk 1 Cor 11: 3-16, halafu tulinganishe na kinachofanywa na makanisa ambayo wanawake wanafunika vichwa leo.

  1. Ivi ulishawahi kugundua kuwa hilo suala lilikuwa linahusu mwanaume aliyeoa na mwanamke aliyeolewa?
  2. Ulishawahi kugundua kuwa mwanamke alikuwa anatakiwa kufunika kichwa wakati anaposali na kuhutubu tu?
  3. Ulishawahi kugundua kuwa mwanamke alitakiwa au afunike kichwa au kama hataki kufunika awe na nywele ndefu?
  4. Unajua kuwa agizo hilo pia linamtaka mwanaume asifuge nywele/asiwe na nywele ndefu?

  Baada ya kuchunguza hayo, tuangalie kinachofanywa na makanisa ya leo yanayo-practice huo utamaduni:
  1. Je wanawaamuru wafunike vichwa walio kwenye ndoa tu?
  2. Wanawaamuru wafunike vichwa wakati wa maombi na wakati wanahutubu tu?
  3. Wanawaamuru pia wanaume au wao wenyewe wachungaji wasiwe na nywele ndefu?
  4. Je, wanawaruhusu wanawake kuwa na nywele ndefu kama mbadala wa kufunika vichwa?

  Kama wanawake wanatakiwa wafunike vichwa wanapokuwa wamekata nywele zao kama ishara ya kutawaliwa na waume zao, kwa nini wanawazuia kufunika vichwa kwa mawigi, maana huwafanya waonekane wana nywele ndefu? Maana biblia hapo haikusema wafunike vichwa kwa kutumia nini, ila imesema wafunike vichwa.

  Nimeuliza hayo maswali si kusudi la wewe kuyajibu, ila nataka tu usome hiyo passage uyaone hayo mambo kisha utoe mchango wako ili hatimae tufikie hitimisho jema

  Asante!

 6. Wapendwa,

  Ukiona mke na mume hawasali pamoja ujue kuna pepo mchafu yupo katikati. Kama siyo pepo ujue kuna imani potofu imeingia ndani ya kichwa cha mwanandoa mmoja.

  Haiingii akilini mke aende kusali kanisa liliko Mwenge (Mf. FGBF, BCIC, EFATHA, nk), huku mume naye aende peke yake kuchunga kanisa liliko Kigamoboni Tungi, Tuamoyo, Minazimikinda, au Mbagala Rangi tatu, nk halafu useme hawa wanandoa wako kitu kimoja. Haiwezekani.

  Hebu fikiria ilivyo ajabu wewe unawasha gari lako kuelekea Mwenge kutokea Magomeni na mumeo awashe gari lake kuelekea Kigamboni. Au Fikiria wewe unayeishi Mwanza, Mume anachunga kanisa kule Buhongwa mitaa ya Sahwa, Nyanembe, Bulale, Msituni, nk kisha wewe mkewe unakamata gari kuelekea kule Ilemela, Kona ya Bwiru, Kilimahewa pale Big bite, michungwani, nk hivi kweli wewe utajisikia raha rohoni kusali mbali na mumeo?

  Haiwezi ikaleta raha hata kidogo mumeo ni mchungaji wa kanisa lililoko maeneo ya Ujiji Kigoma halafu wewe ukaendelea kusali Mwandiga ukasema eti hapo wewe ni mke wake tena wa halali kabisa. Utajisikiaje raha ukiwa mbali na mumeo? Mumeo yuko Ujiji anafundisha waumini na wewe uko Mwandiga unasali kanisa lingine, jamani jamani jamani wapi na wapi tena? Maadili gani hayo yatakuwa? Daaaah ebbbooooo??!!!!! Ukristo gani mwataka kuleta hapa?

  Maandiko yansema ………Hebu ona ilivyo raha na vyema ndugu kukaa pamoja na kumwabudu Mungu pamoja? Sembuse Mume na mke? Khaaaaaaa?

  Hebu waza ilivyo raha ya hali ya juu, mume anahubiri mkewe akiwepo kanisani kumsapoti hata kubeba kabiblia ka mume wake amalizapo kuhubiri achilia mbali kumsaidia kuhubiri Neno au hata kwa maombi ya kufunga Ibada basi?

  Hebu tazama ilivyo vyema na ya kupendeza mume na mke ndani ya gari moja wamekaa kwenye siti moja wanarudi nyumbani, mara wanapita kunywa soda au juice pamoja wakiwa wametoka ibadani pamoja, ni raha iliyoje mbele za waumini?? Ni mfano mzuri sana sana mbele za watu wa dunia eti? Utatembeaje peke yako umemaliza ibada kama vile bado wewe ni bachela au msimbe bhaaaana?

  Enyi wanawake watiini waume zenu. Maandiko ndiyo yanayosema. Siyo mimi. Kumtii mumeo ni pamoja na kumtii hadi kuelekea njia moja kwenda kusali pamoja na ikiwezekana kurudi njia moja bila kuachana, yaani bega kwa bega, mguu kwa mguu hadi chumbani na kubadilisha nguo za kanisani pamoja chumbani ikiwezekana wewe mke unakuwa mstari wa mbele kumvua suti baba Mchungaji kama siyo kumvua nguo zote na kumpa haki yake. Umeona eeeeeeh?

  Achana na tabia mbaya sana za watu wasioelewa wanakokwenda. Mke na mume wasiosali pamoja hasa wale waliookoka wanafanya makosa makubwa sana katika ulimwengu wa roho. Kama wote mwamcha Mungu, hakuna budi kusali pamoja kwenye tawi moja, mtaa mmoja, ikiwezekana kukaa pamoja kanisani, tena wao wanasema kukaa beneti beneti. Mmoja kulia mwingine kushoto. Hii ndiyo ndoa ya kichungaji, tena ndiyo ndoa ya kilokole naaaaam ndiyo ukweli wa Maandiko.

  Kama hutaki kusali kanisa moja au tawi moja na baba Mchungaji mumeo basi ujue umeachana naye kiroho ingawa kimwili usiku mko pamoja.

  Stay alert, Coz Jesus gonna come again!!!!

 7. ck lwembe pamoja na wengine naomba niwajibu kwa niaba ya sungura.kwanza nianze na maana ya imani maana yake biblia katika waebrania inasema ni kuwa na uhakika na mambo yatalajiwayo,kama Yesu ameenda kutuandalia makao mbinguni. kwa makanisa kama TAG,EAGT FPCT nk yote yanaamini katika mambo haya yafuatayo
  1.Bwana mmoja(Yesu mwokozi wa maisha yao) wakati makanisa mengine wanasema huwezi kuokoka ukiwa duniani wanasema kunywa kidodo usilewe,jisaidie na mungu atakusaidia ebu soma juu ya agizo la Mungu juu ya pombe anasemaje(HABAKUKI 2:15) kama mhudumu anayempa kileo vipi kwa anayekunywa kidogo ?
  2.imani mmoja(ya kumwamini Yesu kwamba alikuja kumtafuta mwanadamu aliyepotea ktk dhambi na kumwokoa na sasa ameenda kutuandalia makao
  3.ubatizo mmoja(wa maji mengi wa kufa na Yesu sio wa kuwabatiza watoto wadogo ambao hawana sifa za ubatizo ebu oneni sifa za wanaostahili kubatizwa kwanza wanatakiwa wawe wanaamini neno la Mungu,soma maliko 16:16
  4Mungu mmoja
  sasa hayo mambo mengine uliyo sema kujifunika vitambaa,kutovaa wigi,kwanza niwapongeze fullgospol kwa kulitendea neno la Mungu na wale ambao wanavaa kwa vile ni wanafunzi wa Yesu ipo siku watalitendea neno la Mungu hiyo haiwatofautishi katika imani
  sasa nije katika makanisa mengine uliyo yataja hapo juu.yako nje ya imani kama ilivyofafanuliwa katika( waebrania11:1) ebu nikutajie mfano mmoja biblia inasema baada ya kufa hukumu (waebrania 9:27) sasa mtu anakufa muhimbili,bmc,kcmc nk marehemu anakaa siku kadhaa katika chumba cha kuhifadhia maiti halafu anakuja kiongozi wa dini anaombea marehemu,watu wanatoa na sadaka eti sala za kiongozi zibadili hukumu ya Mungu.nyie ndungu zangu ambao muko upande wa huko acheni kuwa vipofu geukeni acha kudanganywa someni neno la Mungu mtu alikuwa mlevi,mzinzi,kahaba,fisadi,mchawi,nk eti afe aombewe alale mahali pema peponi biblia inasema apandacho mtu ndicho atakivuna (wagalatia 6:7)
  kwa leo niishie hapo mungu awabaliki wote

 8. CK Lwembe;hilo limeniingia kabisa chunga tumusikie mpendwa Sungura anasema nini.

 9. Sungura,

  Nitafurahi ukiliweka wazi zaidi jambo hili unalotuambia, kwamba:
  “”Eg; kusali mmoja Full gospel na mwingine TAG, hizo si imani mbili tofauti, ni makanisa tofauti tu.”

  Kwanza, ninachofahamu ni kwamba Imani ni kamilifu. Nayo mifumo ya ibada na mafundisho yake, ndivyo vinavyoidhihirisha Imani Kamilifu inayotangazwa na kundi lolote lile la kidini (hapa sizungumzii usahihi wa hayo).

  Kwa mfano, Full Gospel wanawake hufunga vitambaa vichwa vyao ktk ibada, tena hawavai wigi ktk maisha yao, na haya ktk ujumla wake ndiyo yanayoionesha imani ktk jinsi walivyolipokea hilo Neno kutoka kwa Mungu, na kulitii.

  Lakini TAG, sidhani kama wanalijua hilo Neno linalowafungisha wenzao hivyo vitambaa na kuwakataza wasivae wigi; basi kama kipimo cha kupokelewa kwetu na Mungu ni hiyo Imani Kamilifu, Je, kama Full Gospel wako sahihi ktk hilo ambalo TAG wamepungukiwa, watakuwa sawa ktk kipimo hicho? Logic inatuambia TAG watapungukiwa kuufikia huo Ukamilifu wa Imani na hivyo watatupwa huko nje kuliko na ‘vilio na kusaga meno’! Na iwapo Full Gospel wamejitungia tu mambo yao na kuyafanya ni sehemu ya Neno la Mungu litakasalo, loh, nao yatawakuta hayohayo huko nje!

  Ndipo ikiwa mke atasali huko TAG na mume Full Gospel, ni dhahiri kwamba ndoa hiyo haipo, labda makundi yote mawili yawe makosani kwa hiyo huko mwisho wataendelea pamoja ktk hicho kilio walichokianza hapa duniani kwa huo utengano wanaouishi, haswa hapo wanapojiwakilisha mbele ya Mungu, wakiwa ni mwili mmoja ulio ktk utengano!

  Imani moja, ningekuelewa iwapo ungetuambia kuwa mume anachunga Parokia ya Mabwepande, ingawa anaishi Msasani; kwahiyo mke anasali St Peter’s. Haya makanisa mawili, yote ni Katoliki na hivyo ni imani moja, wote wanaamini ktk kuombewa na wafu!

  Labda nikusikilize zaidi, huenda kuna namna ambayo mnaweza mkawa katika mafundisho tofauti lakini mkawa na “imani moja”, dunia ina maajabu mengi!

  Asante, ndg yangu,
  Gbu!

 10. Wapendwa!
  Tukumbuke swali halijasema imani mbili tofauti, bali limesema kanisa jingine. Kanisa jingine si lazima kuwa ni imani mbili tofauti.

  Eg; kusali mmoja Full gospel na mwingine TAG, hizo si imani mbili tofauti, ni makanisa tofauti tu.

  Ila kusali mmoja sabato na mwingine FPCT au EAGT, au RC, hizo ni imani mbili tofauti.

  Nimekuona Stephen!

  Tuendelee!!

 11. kwako sungura na wengine
  mpendwa sungura nimepata kitu kwenye maelezo yako leo kwani ni kweli leo dunia inaingia makanisani leo utakuta mama wachungaji wengi wako kwenye mabalaza ya uongozi hata kama hawana uwezo wa kuongoza tena makanisa mengine wamefika mbali hata kama mchungaji anafaliki mama wachungaji wanachukua nafasi hata kama hawana wito mimi siwaonei wivu mama wachungaji shida yangu ni pale wanapokosa huduma ndani yao kama wana huduma hiyo haina shida nije kwenye mada ya huyu mama mchungaji anayesali imani tofauti na mchungaji mme wake
  1,kama imani anayosimamia mch ni ya kweli halafu mama mchungaji unataka kwenda sehemu nyingine mimi kwa mtazamo wangu mimi naona ni kosa
  2,pili kama mchungaji kapata wito baada ya Ndoa na Ndoa ilikuwa imefungwa kwenye imani nyingine,halafu mch kapata wito labda mch anaenda kuwa mch kwenye imani potofu na mama mch anaona wanapotea hapo yuko sawa kusali mahali anapoona ni sahihi kwani Yesu anasema mbinguni hakuna kuolewa wa kuoa mambo ya kuolewa na kuoa ni ya hapa duniani ndio maana yesu anazidi kusema wawili watakuwa kitandani mmoja atatwaliwa na mwingine ataachwa hivyo sio vizuri kumlazimisha mama mch kama anasababu ya msingi kusali tofauti na mchungaji kama hana sababu ya msingi aende kufanya kazi ya mungu na mwezi wake mchungaji kwani yeye ndiye mlinzi wa mchungaji
  mama mchungaji tupe sababu ya msingi wewe kusali tofauti na mwenzi wako
  ubalikiwe

 12. Hello,

  Ivi wazo la mama na baba mchungaji tunalipata wapi kwenye biblia? Biblia mimi naona ina wazo la mume na mke!

  Huku ni kulazimisha masuala ya kifamilia kuwa masuala ya kiofisi (utumishi). Kwa mtu anayejua mambo ya usimamizi (Management) anaelewa vizuri ambavyo kunatakiwa kuwe mipaka kati ya masuala ya kibiashara/kiofisi na masuala ya nyumbani/ kifamilia..

  Mimi sisomi hata mtume mmoja akimvutavuta mke wake kwenye huduma(ofisi), hilini suala limeachiliwa sana leo. Lakini hata watumishi wengi wa mwanzo kama akina mzee Moses Kulola hawakuwa na hiyo tabia ya kupelekapeleka mbele wake zao, labda kama mke nae ana huduma/ wito ndani yake.

  Tukirudi sasa kwenye swali, lazima tujiulize ni kitu gani kinapelekea mke kusali sehemu tofauti na mume wake, hasa huyo mume akiwa ni mchungaji.

  Huwa kuna sababu ambazo ni lazima tu suala la kusali sehemu mbili tofauti litokee, na kwa mimi sababu ya kwa nini kusali sehemu mbili tofauti ndiyo ya muhimu zaidi kuangalia/kuzingatia.

  Tukumbuke mchungaji na mkewe kusali sehemu moja siyo fundisho (is not a doctrine).
  Kulazimisha mke wa mchungaji awe mchungaji msaidizi, au awe sehemu ya kabineti ya uongozi wa kanisa siyo wazo la biblia, ni ingizo geni tu la kiustarabu wa kimtazmo wa dunia ambalo limelazimishwa.

  Namfahamu mchungaji mmoja (Dustan Maboya) ambaye anachunga kanisa Arusha na mke wake anachunga kanisa Dar.

  Lakini pia wazo zima la kuambatana kati ya mume na mke siyo kufuatana mgongoni kama kumbikumbi , bali ni kule kukubaliana kuanzisha familia na kuishi kama mume na mke.

  However, kama hakuna sababu yoyote ya muhimu tena ya makubaliano, ni muhimu mke/mume kuwepo sehemu ambapo mwenzi wake anafanya huduma.

 13. haleluya!,
  Pole sana mama mchungaji, hayo ni madhaifu makubwa sana mnayo/unayoonyesha kwani familia kuwa na Imani mbili tofauti ni tatizo, Ephesians 5:31 Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja. lakini pia Genesis 2:24 Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.

  Matthew 19:5 akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?

  Mark 10:8 na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja.
  kulingana na hayo maandiko unataka kuniambia kuwa ninyi mmekuwa mwili mmoja?.
  Je, huamini dini ya mumeo?. Ninyi si nuru tena bali ni giza maana mataifa watajifunza nini kutoka kwenu zaidi ya kutawanyika nao?. Mama mchungaji inatakiwa muwe na imani moja haiwezekani kichwa kiwe kule na kiwili wili kiwe pengine;huo si mwili mmoja tena.
  wenu katika shamba la Bwana;
  L. M. Mollel
  Chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine(SUA);
  Morogoro Tanzania, East-Africa.

 14. “What is the duty / role of a pastor’s wife?”

  Answer: The Bible does not address the involvement of the pastor’s wife in any ministry. In other words, it depends upon the denomination, the individual church within a denomination, the church board, and the pastor and his wife to determine how active the pastor’s wife should be. The main area of responsibility for any wife is to support and be submissive to her husband (Ephesians 5:22-24). However, if the Lord calls a man into the ministry, He calls the whole man, and that includes the man’s wife and his family.

  The Apostle Paul in 1 Timothy 3 gives us the qualifications of a “bishop” or what we call a pastor, and in verse 4 we see the following: “one who rules his own house well, having his children in submission with all reverence.” “Rules well” is an idiom for being a biblical husband with a submissive wife and children that love and respect him. The pastor who is the head of his home will be more successful as a leader in the church, and of course this means that his wife is his helper in the ministry of the home as well as the church. The ministry is a partnership in all areas of life and not just in the home life.

  The wife does not do the work of the pastor, but the pastor and his wife are a team who are yoked together to do God’s work. Too few recognize the reality of this and want to put the pastor’s wife in a box and relegate her to keeping the home fires burning and prayer support for her husband. That certainly is her responsibility, but quite often the pastor’s wife has gifts that can and should be used in the ministry. On the other hand, there are women whose husbands are pastors and they see it as “his” ministry and do not enter in to the work in any way. There should be a good balance between these two ideas with the goal of bringing glory to God in all things. An active, outgoing pastor’s wife is a valuable asset to any church in today’s climate of apathy to the things of God.

  http://www.gotquestions.org/pastors-wife-duty-role.html

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s