Maoni juu ya Mpinga Kristo atakavyokuwa!!

mpingaakristo

WOKOVU WA BAADAYE WA ISRAEL.

KWELI KUU: Kukubalika kwa Kristo kama Masihi kutaleta matokeo ya kupandikizwa tena.

MSTARI WA KUKUMBUKA:
Na hao pia wasipokaa katika kutokuamini kwao watapandikizwa; kwa kuwa Mungu aweza kuwapandikiza tena (Rumi 11:23)

MAANDIKO YA SOMO: WARUMI 11:1- 36

UTANGULIZI:
Kitovu kikuu cha wokovu wetu ni kuamini kuwaYesu Kristo ni Bwana na kwamba Mungu alimfufua katika wafu. Rumi 10: 9-10, Mdo 4: 12,
Njia pekee ya kumfurahisha Mungu n ikukubali kwa njia ya imani kwamba Yesu pekee ndiye anaweza kutupumzisha na mizigo ya dhambi Math 11: 28-30. Hatuna uwezo wa kumridhisha Mungu kwa njia ya matendo ya sharia lakini tukawa tumemkataaYesu katika maisha yetu.
Matendo yanafaa kama u katika Bwana. Wayahudi walijitahidi kupata haki kwa kufanya matendo yaliyodaiwa na sharia lakini wamekataa kuufuata mpango wa Mungu wa wokovu kwa njia ya imani. Rumi 9:30-32.

Leo hii Wayahudi wengi wamemkataa Yesu Kristo katika maisha yao isipokuwa mabaki waliochaguliwa kwa neema Rumi 11:1-10. Kwa sababu ya kumkataa Yesu Wayahudi wengi wamejiweka wazi kwa Mpinga Kristo atakapokuja awatawale. Kwasababu ya uhusiano uliopo kati ya Mpinga Kristo na Wokovu wa baada ya Israel, tunalazimika pia katika somo hili kuangalia habari za Mpinga Kristo.

HABARI ZA MPINGA KRISTO:
Ufunuo 13:11-18
Mpinga Kristo (Anti – Christ) nimwonekano wa shetani katika hali halisi ya mwili. Katika vitabu vya unabii, kuna Mpinga Kristo, Nabii wa uongo, na Shetani mwenyewe. Huu ni utatu mwingine wa kishetani. Hatuelewi kama Mpinga Kristo ameshazaliwa bado, lakini tunajua kupitia maandiko ya kuwa yuko kazini hata sasa. 1Yoh 4:3

MAONI JUU YA MPINGA KRISTO ATAKAVYOKUWA:
1. Anaweza kuwa kiongozi wa dini: Atajifanya kuwa ni mtu wa dini mwenye uwezo wa hali ya juu sana hasa katika kuongea, kushawishi na kuvuta watu. Atasaidiwa na baadhi ya nchi kupata nguvu za kisiasa. Ufun 16:13. Baada ya kufanikiwa atadhihirisha wazi chuki yake juu ya Wakristo wa kweli na Kristo mwenyewe.
2. Ni kama Yesu: Anaweza kuwa ni Myahudi mwenye kadri ya miaka 30 atakapoanza kuwa mwenye nguvu. Atatangaza dini mpya nakufanya miujiza na ishara nyingi kama Yesu alivyofanya. Ufun 13:13, Math 24:24. Lakini yeye atapigania pia kupata nguvu ya kisiasa na ataipata.
3. Mhubiri mpya: Atakuwa anatabiri na mambo yanatokea. Atakuwa anawasiliana na  watu moja kwa moja. Yeye atatangaza kuwa kila mtu ni Mungu. Atakuwa ni mwanaume asiye na haja ya mwanamke.
4. Ni Philosophy: Ufu 16:14. Hata kuwa ni mtu bali ni wazo fulani, au siasa Fulani inayosisitiza uhuru wa kila mtu kufanya lolote linalompendeza. Siasa hii itazivumilia dini zote kuwa ziko sawa isipo kuwa Ukristo wa kweli.

Na; Mr Ndaki
15 / 06 / 2014

Advertisements

14 thoughts on “Maoni juu ya Mpinga Kristo atakavyokuwa!!

 1. Zote ni mbwembwe za wanadamu wa kizazi hiki wanaojiona wanaona,wanasikia na wanajua kumbe HAPANA !, kumkubali au kumpinga Kristo kuko ktk nafsi ya mtu , na wala siyo suala la kujua utatu wala dhehebu unalotoka ,maana hakuna nafsi itakayomuona Mungu bila Ubatizo na kujitahidi ANGALAU uwe na matendo kama ya Kristo, yaani UTAKATIFU .Nimetumia neno angalau kwani hakuna mwanadamu yeyote anayeweza kuwa Mtakatifu isipokuwa kwa neema.Rejea Mhb. 7:20 pia na kwa utakatifu rejea Ebr.12:14, Mhbr 12:1,13,14, Luk 13:28 Pet 1:16 Ufu 14:12,13 Ufu 2:9,10 n.k .zaidi tuombeana HEKIMA ya Mungu na siyo kubishana kwa mambo kama haya na kuwaona wengine wanakosea wanachoamini hakuna atakayehukumiwa kwa kuwa MSDA,MLUTERI au MKATORIKI n.k bali kila mtu kwa matendo yake,je? matendo yako yanamkiri Kristo? tuiangalie Dunia kwa ujumla wake yu wapi anayejiamini anatenda sawa atuombee Mungu aghairi ghazabu juu yetu?maana matukio ya duniani ya sasa yanahitaji aliyemkamilifu asimame atuombe HURUMA na HEKIMA ya Mungu na siyo kunyoosheana vidole na kukiri kwa midomo yetu kuwa wengine wanajifunza mafundisho ya shetani.

 2. Mpinga Kristo ni dini ya Wakristo, lakini wanaoigeuza Injili kweli kuwa udharimu. Mtume Yohana alituambia kuwa wakati wake walikuwepo wapinga Kristo wengi, na akasema kuwa na wengine watatokea siku za mbele. Ili uweze kujua mpinga Kristo ni nani, lazima uangalie sifa zake kama Mtume Yohana alivyoziorodhesha.

  Sifa hizo ni; wapinga Kristo wanamkana Mwana na hatimaye hawana Baba pia. (1Yohana 2:22-23)

  Ni Wakristo lakini hawakiri ya kuwa Yesu ni Kristo. (1Yohana 4:3)

  Wanapinga kwamba Yesu Kristo Mwana Wa Mungu hakuja katika mwili (2Yohana 1:7)

  Wale wanaoshindwa kujifunza swala hili watajikuta wao wenyewe wako upande wa mpinga Kristo lakini wanaendelea kutazamia mpinga Kristo mwingine. Bofya kifuatacho kujua kama uko upande wa mpinga Kristo sasa.

  *. Je mpinga-Kristo ni nani?

 3. CHOMBO KINGINE KINACHOFANYA KAZI YA UPINGAJI NI KWA PAMBANO HILI LA MWISHO LA WEMA NA UBAYA NI;

  KNIGHTS OF MALTA

  1.WAKO CHINI YA SHIRIKA LA JESUIT

  2.MAKAO MAKUU NI ROME

  3.WANATAWALA MASHIRIKA YA KIJASUSI NA UKUSANYAJI TAARIFA KAMA KGB NA CIA KATIKA MPANGO MPYA WA DUNIA

  4.WANAYAONGOZA MASHIRIKA MAKUBWA YA BENKI, BIASHARA, SIASA, ELIMU,NYENZO ZA KIJESHI,UN

  5.KIONGOZI WAKE HUTUMIKIA MUDA WOTE WA MAISHA YAKE, BAADA YA UKUBALI KUTOKA KWA KIONGOZI WA KANISA LA RUMI

 4. THE KNIGHTS OF TEMPLARS
  BAADHI YA SIFA

  -WALIPIGANA VITA VYA MSALABA KWA KIVULI CHA DINI

  -WALICHORA RAMANI NA MPANGO MPYA WA KULIJENGA HEKALU LA SULEMANI, HUKO YERUSALEMU

  -WALIUA WAISRAELI NA WAARABU HUKO JERUSALEMU WATU 70,000/= NDANI YA SIKU TATU

  -WALITOKA NA KUNYANG’ANYA SHEMU ZA HISTORIA NA KUKABIDHI KWA KANISA LA RUMI

  -WALIKUWA HAWAOI

  -WALIKUWA NA IBADA YA USHOGA

  -SASA WANAONGOZWA CHINI YA FREEMASON BAADA YA KANISA LA RUMI KUHOFU JUU YA UTENDAJI WA MAMBO YAO WAZI WAZI..NA KUTIA HOFU WAUMINI JUU YA UHUSIANO WAO NA BIBLIA, KATIKA MIAKA YA 1000 NA KUENDELEA

  -WALIJENGA MAKANISA MAKUBWA YA KISASA TUNAYOYAONA LEO ULAYA KWA PESA NA DHAHABU WALIZOTEKA MASHARIKI YA KATI, ISRAELI NA UARABUNI

  -WALIIGA KUTOKA ISRAELI MBINU ZA UENDESHAJI WA FEDHA AMBAO KWETU NI MPYA..KUWEKA PESA SEHEMU MOJA NA KUCHULIA FEDHA MJI MWINGINE.
  NA KUANZISHA HUKO ULAYA.

  -NEMBO YAO NI MSALABA UNAOKUWA NA VICHWAMISHALE MINNE INAYOKUTANA KATIKATI, MAANA WALIKUWA WAPIGANAJI. HUTUMIWA NA MAKANISA YA LEO

  -NEMBO YAO YA KIDINI NI TAJI AMBAYO INA MSALABA KATIKATI ULIOINAMA, AMBAYO HUTUMIWA NA MAKANISA MENGI YA LEO

 5. VYAMA VYA MPINGA KRISTO VINAVYOUNGANISHA UPAGANI NA KUSHIKA NYEZO ZOTE ZA MAISHA YA BINADAMU,SIASA, UCHUMI,ELIMU NA KUANZISHA MAKANISA MENGI YANAYOCHANGANYA UPAGANI NA BIBLIA.

  THE KNIGHTS OF TEMPLARS
  KNIGHTS OF MALTA
  ROSICRUCIANISM
  SKULL AND BONES
  THE BOHEMIAN
  KNIGHTS OF COLUMBUS
  OPUS DEI

  MTIRIRIKO WA PAMBANO LA SHETANI JUU YA WATU WA MUNGU NA VYOMBO VYAKEANAVYOTUMIA VILIVYO CHINI YA MPINGA KRISTO

  1.KABBALISM
  2.GNOSTICISM
  3.KNIGHTS OF TEMPLARS
  4.ROCICRUCIANS
  5.FREEMASONRY/ILLUMINATI
  6.WORLD COUNCIL OF CHURCHES
  7.NEW AGE MOVEMENT

  VIONGOZI WENGI WA KISIASA,UCHUMI,DINI HUUNGANISHWA NA VYOMBO HIVYO

  VYOMBO HIVI VYOTE VIKO CHINI YA MWANAMKE/KANISA LA UFUNUO 17:1-5

  NEW AGE MOVEMENT NA WCC NDIO IMELIINGIZA KANISA LA KWELI KATIKA PAMBANO LA MWISHO LA WEMA NA UOVU LIKIMUHUSISHA MWANAMKE/KANISA LA UFUNUO 17:1-5 NA YULE MWANAMKE/KANISA SAFI LA UFUNUO 12:1-6

 6. SIMON MCHAWI ALITUMIA KIVULI CHA DINI KUTEKA WATU NDICHO KINACHOFANYIKA SASA

  KNIGHTS OF TEMPLARS WALIOPIGANA VITA VYA MSALABA NA KUTEKA JERUSALEMU WALIJIFICHA KATIKA VAZI LA DINI

  WALICHORA RAMANI NA MPANGO WA KUJENGA HEKALU LA SULEMANI

  HAWAKUOA KUMBE WALIKUWA NA IBADA ZA USHOGA

  WALIPOGUNDULIKA WAKAINGIA KATIKA FREEMASON
  WANAFANYA KAZI KUPITIA KIZAZI KIPYA KWA KUFUNGUA MAKANISA KAMA VILE WALIVOKUWA WAKIJENGA /WAJENZI WAKUBWA WA MAKANISA MENGI HUKO ULAYA KATIKA ZAMA ZA GIZA.

  SASA ANAFANYA KAZI KUPITIA WCC.

  UKIMJUA ALIYERUHUSU NA KUANZISHA KNIGHT OF TEMPLARS NI RAHISI KUJUA MPINGA KRISTO

  WANAOJIUNGA NA CHAMA HICHO NA KUPATA PESA KUTOKA SHIRIKA HILO
  WAMEPOTEZA MISINGI YA BIBLIA NA KUFANYA MATAKWA YA ADUI KWA KIVULI CHA DINI KAMA SIMON MCHAWI KATIKA MATENDO YA MITUME.

 7. Naomba nami niwaelleze wasomaji wa habari hii maana ya mpinga kristo. Neno linasema kwamba, yule ASI ni roho ya mpinga kristo na ipo inatenda kazi hata sasa kwahiyo siyo kwamba mpinga Kristo atakuja baadae bali muelewe kwamba alishakuja tayari. Mpinga kristo huyo bila kuficha ni FREE- MASON na wengi wanafahamu japo sio kwa kina sana utendaji wake. Lakini tunamshukuru Mungu wa Eliya kupitia Nabii wake Eliya wa kizazi cha 4 ametufunulia siri zake, mitego yake, utendaji wake na pia amemwangamiza sawa na NENO lilivyofunuliwa katika 2THESALONIKE 2. Ili uweze kumshinda Adui ni lazima umjue kwanza vizuri. la sivyo huwezi kumshinda.

  ANDIKO linaua bali NENO linauhisha. NENO LILILOFUNULIWA ndilo lililotufunulia siri zote za mpinga Kristo / FREE- MASON. Hata dini na madhehebu yote yanayojulikana yameunganishwa na mtandao huo lakini waumini wao wengi sana hawajui wanafikiri wanamwabudu Mungu wa kweli. Neema ya Mungu wa kweli itusaidie sana katika kuyatambua haya.

 8. MPINGA KRISTO ANAFANYA KAZI HATA SASA

  “NIKAONA ROHO TATU ZA UCHAFU ZILIZOFANANA NA VYURA, ZIKITOKA KATIKA KINYWA CHA YULE JOKA, NA KATIKA CHA YULE MNYAMA, NA KATIKA KINYWA CHA YULE NABII WA UONGO.” UFUNUO 16:13

  TAZAMA ROHO CHAFU ZINATOKA KATIKA JOKA, MNYAMA, NABII WA UONGO
  JOKA ANAFANYA KAZI KUPITIA MNYAMA NA MANABII WA UONGO
  MNYAMA NI NINI KATIKA BIBLIA?

  DANIELI 7:17
  “WANYAMA HAO WAKUBWA WALIO WANNE NI WAFALME WANNE WATAKAOTOKEA DUNIANI.”

  KATIKA MNYAMA WA NNE NDIPO MPINGA KRISTO ALIPOANZA KUFANYA KAZI
  MAANA PEMBE NDOGO YA MPINGA KRISTO NDIPO ILIPOTOKEA

  1. MPINGA KRISTO ANATOKA KATIKA YULE MNYAMA

  DANIELI 7:8
  “NIKAZIANGALIA SANA PEMBE ZAKE, NA TAZAMA, PEMBE NYINGINE ILIKUWA NDOGO, AMBAYO MBELE YAKE PEMBE TATU KATIKA ZILE ZA KWANZA ZIKANG’OLEWA KABISA;”

  2. MPINGA KRISTO ANATOKA KATIKA ZILE PEMBE KUMI

  DANIELI 7:8
  “NIKAZIANGALIA SANA PEMBE ZAKE, NA TAZAMA, PEMBE NYINGINE ILIKUWA NDOGO, AMBAYO MBELE YAKE PEMBE TATU KATIKA ZILE ZA KWANZA ZIKANG’OLEWA KABISA;”

  3. ANAKUWA KWA NGUVU BAADA YA ZILE PEMBE KUMI

  DANIELI 7:20
  “NA HABARI ZA ZILE PEMBE KUMI ZILIZOKUWA KICHWANI MWAKE, NA ILE PEMBE NYINGINE ILIYOZUNGUKA, AMBAYO MBELE YAKE ZILIANGUKA PEMBE TATU;YAANI, PEMBE ILE YENYE MACHO, NA KANWA LILILONENA MAKUU, AMBAYO KUONEKANA KWAKE KULIKUWA HODARI KULIKO WENZAKE.”

  6. PEMBE HII/UTAWALA UNA MACHO NA MDOMO KAMA WA BINADAMU/HAUNA MASIKIO

  DANIELI 7: 20
  “….YAANI, PEMBE ILE YENYE MACHO, NA KANWA LILILONENA MAKUU, AMBAYO KUONEKANA KWAKE KULIKUWA HODARI KULIKO WENZAKE.”

  7. ANAFANYA VITA NA WATAKATIFU WATAKATIFU WA MUNGU

  DANIELI 7:21

  “NIKATAZAMA, N A PEMBE IYO HIYO ILIFANYA VITA NA WATAKATIFU, IKAWASHINDA;”

  8. ANA TOFAUTI NA ZILE PEMBE NYINGINE/FALME NYINGINE

  DANIELI 7:19
  “KISHA NALITAKA KUJUA MAANA YA YULE MNYAMA WA NNE, ALIYEKUWA MBALI NA WENZIWE WOTE, MWENYE KUTISHA SANA, AMBAYE MENO YAKE YALIKUWA YA CHUMA, NA MAKUCHA YAKE YA SHABA; ALIYEKULA, NA KUVUNJA VIPANDE VIPANDE, NA KUYAKANYAGA MABAKI KWA MIGUU YAKE;”
  9. ITAONGEA KINYUME CHAKE ALIYE JUU

  DANIELI 7:8
  “..NA TAZAMA KATIKA PEMBE HIYO MLIKUWA NA MACHO KAMA MACHO YA MWANADAMU NA KINYWA KILICHOKUWA KIKINENA MANENO MAKUU.”

  DANIELI 7: 20
  “….YAANI, PEMBE ILE YENYE MACHO, NA KANWA LILILONENA MAKUU, AMBAYO KUONEKANA KWAKE KULIKUWA HODARI KULIKO WENZAKE.”

  10. ANABADILI AMRI ZA MUNGU NA NYAKATI
  “..NAYE ATAAZIMU KUBADILI MAJIRA NA SHERIA; DANIEL 7:25

  11. ANATAWALA SIKU ZA KIUNABII 1260 KATIKA AWAMU
  UFUNUO 7:25
  “..NAO WATATIWA MIKONONI MIKONONI MWAKE KWA WAKATI, NA NYAKATI MBILI, NA NUSU WAKATI.”

 9. ANTICHRIST LINA MAANA YA KUSIMAMA KATIKA NAFASI YA KRISTO

  LUGHA YA KIGENI “ANTICHRIST”= “IN THE PLACE OF CHRIST” KATIKA NAFASI YA KRISTO

  UKIACHA SIFA ZA KITABU CHA DANIELI NA UFUNUO, VITABU VINGINE VINASEMA HIVI JUU YA MPINGA KRISTO;

  1 YOHANA 2:18
  “WATOTO, NI WAKATI WA MWISHO NA KAMA VILE MLIVYOSIKIA KWAMBA MPINGA KRISTO YUAJA, HATA SASA WAPINGA KRISTO WENGI WAMEKWISHA KUWAPO.”

  MARKO 13:21
  MPINGA KRISTO ATAANDA UJIO WA MASIHI ASIYE SAHIHI
  “NA WAKATI HUO MTU AKIWAAMBIA, TAZAMA KRISTO YUPO HAPA, AU YUKO KULE,MSISADIKI”

  MPINGA KRISTO NI YULE AKETIYE KATIKA HEKALU NA KUJIFANYA MUNGU.
  2 WATHESALONIKE 2:3
  “AKAFUNULIWA YULE MTU WA KUASI, MWANA WA UAHARIBIFU;4 YULE MPINGAMIZI, AJIINUAYE NAFSI YAKE KANA KWAMBA YEYE NDIYE MUNGU AMA KUABUDIWA; HATA YEYE MWENYEWE KUKETI KATIKA HEKALU LA MUNGU,AKIJIONYESHA NAFSI YAKE KANA KWAMBA YEYE NDIYE MUNGU.”
  MPINGA KRISTO KAMA ROHO ISIYOKIRI KUWA YESU HATOKANI NA MUNGU

  1 YOHANA 4:3
  “NA KILA ROHO ISIYOMKIRI YESU HAITOKANI NA MUNGU. NA HII NDIYO ROHO YA MPINGA KRISTO AMBAYO MMESIKIA KWAMBA YAJA; NA SASA IMEKWISHA KUWAKO DUNIANI.”

  MPINGA KRISTO NI YULE ANAYEKANA KUWA YESU AJA KATIKA MWILI.
  2 YOHANA1:7
  “KWA MAANA WADANGANYIFU WENGI WAMETOKEA DUNIANI, WASIOKIRI YA KUWA YESU KRISTU YUAJA KATIKA MWILI. HUYO NDIO YULE MDANGANYIFU NA MPINGA KRISTO.”

  MPINGA KRISTO ANAFANYA KAZI HATA SASA
  “NIKAONA ROHO TATU ZA UCHAFU ZILIZOFANANA NA VYURA, ZIKITOKA KATIKA KINYWA CHA YULE JOKA, NA KATIKA CHA YULE MNYAMA, NA KATIKA KINYWA CHA YULE NABII WA UONGO.” UFUNUO 16:13

  TAZAMA ROHO CHAFU ZINATOKA KATIKA JOKA, MNYAMA, NABII WA UONGO
  JOKA ANAFANYA KAZI KUPITIA MNYAMA NA MANABII WA UONGO
  MNYAMA NI NINI KATIKA BIBLIA?

  DANIELI 7:17
  “WANYAMA HAO WAKUBWA WALIO WANNE NI WAFALME WANNE WATAKAOTOKEA DUNIANI.”

  KATIKA MNYAMA WA NNE NDIPO MPINGA KRISTO ALIPOANZA KUFANYA KAZI
  MAANA PEMBE NDOGO YA MPINGA KRISTO NDIPO ILIPOTOKEA

 10. Mpinga Kristo katika ujumla wake ni Shetani!

  Anatumia mbinu gani, tafakari ya jambo hili ni ngumu kidogo, hata Maandiko yanaudhihirisha ugumu wake hapo yanapotamka wazi “yamkini”; kwamba uongo utakuwa ni wa hali ya juu saaana, yaani unaweza kuwa unatumika ktk kambi ya Mpinga Kristo na ukawa HUJUI!!!! Tazama hapa jinsi ya hali inavyokuwa:
  “”kwa maana wataondoka Makristo wa uongo, na manabii wa uongo, watatoa ishara na maajabu, wapate kuwadanganya, kama yamkini, hata hao wateule.”” (‭MK.‬ ‭13‬:‭22‬)

  Bali Neno la Mungu ndilo pekee liwezalo kumshinda Shetani, mahali popote, wakati wowote na ktk hali yoyote!

  Shetani alipomfuata Kristo, Kristo hakutumia kipawa chochote kile kumshinda Shetani. Kristo aliuteremsha Ufalme wa Mungu hadi chini sana kiasi kwamba mkristo yeyote dhaifu anaweza kuutumia kumshinda Ibilisi!

  Ktk kila jaribu alilompelekea Kristo, Kristo alilirejea Neno la Mungu, hilo ndilo pekee linalomvunja nguvu Ibilisi maana lina majibu yoote ya majaribu yake! Hata akija na “Imeandikwa…” Bado liko jibu lake, “Imeandikwa pia…”!! Ndio maana tuna aswa Neno la Mungu lijae kwa wingi ndani yetu na si mafundisho ya dini, huwezi kumshinda Shetani kwa hayo!!!!

  Pia tunapoambiwa jambo la Mpinga Kristo, tunapaswa kujua kwamba si jambo la “lele mama”, Mpinga Kristo ni “Mpango Mzima” wa kutupeleka Kuzimu!!! Hakuna elimu ya dini inayoweza kumfunua huyo zaidi ya Neno la Mungu. Roho ya Mpinga Kristo inatokea huko Mwanzo, alipo Kristo naye lazima awepo!!

  Huko Edeni tunafahamu kwamba Kristo alikuwa ni ule Mti wa Uzima, na Shetani alikuwa ni ule Mti wa Ujuzi wa Mema na Mabaya!

  Katika Anguko Shetani alipata nafasi ya kujidhihirisha ktk mwili. Watazame wale watoto wawili. Kaini na Habili, wote walikuwa wakimcha Mungu; lakini mmoja alikuwa ni wa Ibilisi!!

  Haya, hawa hapa tena, Kristo na Yuda Iskariote. Mungu ndani ya Kristo na Shetani ndani ya Yuda, “Yesu akawajibu, Je! Mimi sikuwachagua ninyi Thenashara, na mmoja wenu ni shetani?” (‭YN.‬ ‭6‬:‭70‬) Unaona, wote waumini wa kusanyiko moja, mmoja mwinjilisti mwingine mweka hazina!!!

  Kristo alipoondoka katika mwili, aliposulubiwa, na Yuda naye aliondoka, akajinyonga! Kristo aliporudi kanisani ktk RM ili kuliongoza kanisa lake, Yuda naye alirudi ktk roho ya Mpinga Kristo kulipotoa kanisa; Yohana analiweka wazi jambo hilo, “… Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani. (‭1 YOH.‬ ‭4‬:‭3‬)

  Sasa hiyo roho si kwamba eti ikija itakuwa inakaba watu mitaani, hapana, inakuja ikihubiri injili tamu isiyo na wokovu, ambayo inapendeza masikioni, tena ina ishara zote za kimbinguni;
  “Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.” (‭2 KOR.‬ ‭11‬:‭14‬)

  Ni elimu gani inayoweza kukuchomoa ktk makucha ya huyo aliyejigeuza kuwa mfano wa malaika wa nuru? Si rahisi, kama hulisikilizi Neno la Mungu kwa umakini wote, ndg yangu, basi “Umekwenda na maji”!!

  Mtazame hapa alivyojigeuza kuwa mfano wa malaika wa nuru ndiyo utakijua wanachokuonya mitume:
  “Nikaona, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda ana uta, akapewa taji, naye akatoka, ali akishinda tena apate kushinda.” (‭UFU.‬ ‭6‬:‭2‬)

  Huyo hapo Mpinga Kristo akienda sambamba na RM! Neno likisema jambo ni lazima litimie, ktk huko kushinda, wengi wa kanisa wamempokea huyu kama RM, kupona ndio ile yamkini; kinachofuata baada ya hapo hakina maelezo!!!!

  Gbu!

 11. Mungu akubaliki sana mtumishi wa Mungu kwa kuleta somo hili nami naomba niongeze maelezo kidogo kwa habali ya mpInga kristo.watu wengi sana hawajui hizi habali hasa wale wanao sema hakuna kuokoka au wanaopinga wokovu biblia inasema ile sili kwa sasa inatenda kazi lakini kanisa ndilo linalozuia soma(2WATHESALONIKE 2:-7)yule mpinga kristo kwa sasa anafanya matayalisho mbalimbali ya kutawala ikiwa ni pamoja na kushika njia zote za uchumi kwani katika utawala wake kutakuwa hakuna kununua wala kuuza bila kuchapwa namba ya mpinga kristo katika vipaji vya nyuso ambayo ni (666)ufunuo 13:-18 sasa mimi nawasihi ndugu zangu wote ambao bado mnasitasita kumpa Yesu maisha yenu kamaa bwana na mwokozi wa maisha yenu,.na wengine mnadanganywa na viongozi wenu wa dini walimu wa uongo wanaopinga wokovu.wanaowombea wafu wakidhani maombi yao yanaweza kubalidilisha hukumu ya Mungu.baada ya unyakuo kanisa likinyakuliwa watakao baki wataingia kwwenye utawala wa mpinga kristo kipindi cha miaka saba ndugu zangu kipindi hicho kitakuwa ni kipindi cha dhiki kubwa ambayo hajawahi kutokea tangu kuumbwa kwa ulimwengu soma (mathayo 24:-21) wakati wa kipindi cha dhiki kubwa watu wa mataifa tofauti na wana wa israeli hakuna atakayeokolewa.sisi watu wa mataifa nafasi yetu ni wakati huu kabra ya kanisa kunyakuliwa wapendwa ebu tumpe Yesu maisha yetu tupate neema ya kuishi maisha matakatifu ambayo yako mbali na dhambi.
  Mungu awabaliki nitaendelea kutoa ufanunuzi wa habali hizi

 12. KINA CHA MTAZAMO WA WANAMATENGENEZO

  SIFA ZA MPINGA KRISTO KATIKA DANIELI 7

  1. NI PEMBE NDOGO
  KWANINI MPINGA KRISTO AWE ILE PEMBE NDOGO?
  2. ANATOKA KATIKA YULE MNYAMA
  3. ANATOKA KATIKA ZILE PEMBE KUMI
  4. INAKUWA KWA NGUVU BAADA YA ZILE PEMBE KUMI
  5. PEMBE HII/UTAWALA UNA MACHO NA MDOMO KAMA WA BINADAMU/HAUNA MASIKIO
  6. INAWAUWA WATAKATIFU WA MUNGU
  7. INA TOFAUTI NA ZILE PEMBE NYINGINE
  8. ITAONGEA KINYUME CHAKE ALIYE JUU
  9. ITABADILI AMRI ZA MUNGU NA NYAKATI
  10. ITATAWALA SIKU ZA KIUNABII 1260

  SIFA ZA MPINGA KRISTO KATIKA UFUNUO 13
  1. ANATOKEA KATIKA BAHARI
  2. ANA MANENO YA MAKUFURU VICHWANI MWAKE
  3. ANAPATA JERAHA LA MAUTI HALAFU LINAPONA
  4. ANAFANYA VITA NA WATU WA MUNGU
  5. ITATAWALA KWA NGUVU SIKU ZA KIUNABII KINABII 1260

  SIFA ZA MPINGA KRISTO KUPITIA MWANAMKE KAHABA/ KANISA LENYE MAFUNDISHO POTOFU
  1. ANAKAA KATIKA MAJI MENGI
  2. WAKUU WA MATAIFA WAMEFANYA UZINZI NA HUYO MWANAMKE/KANISA
  3. ANAWANYWESHA MATAIFA MVINYO/MAFUNDISHO POTOFU
  4. ANAKAA JUU YA MNYAMA MWNYE VICHWA SABA
  5. ANAVAA NGUO ZA RANGI YA ZAMBARAU NA NYEKUNDU
  6. KAJIPAMBA KWA DHAHABU NA VITO VYA THAMANI
  7. NI MAMA WA MAKAHABA
  8. AMELEWA DAMU YA WATAKATIFU
  9. NI UTAWALA UNAOTAWALA JUU YA UFALME WA DUNIA

 13. AINA YA MITAZAMO JUU YA MPINGA KRISTO INAYOITIKISA DUNIA

  1.PRETARISM
  2.HISTORICISM/REFORMATION
  3.FUTURISM

  NINI KIPO KIPO JUU YA MITAZAMO HII
  MOJA: PRETARISM/MPINGA KRISTO AMEPITA HUTAJA KUWA ALIKUWA NERO

  MTAZAMO HUU ULIANZISHWA NA MTU WA SHIRIKA LA JESUIT ANAYEITWA ALCASAR AKISEMA MPINGA KRISTO ALIKUWA NERO.

  MBILI: HISTORICISM NI YA WANAMATENGENEZO. HUSEMA UPAPA NI UPINGA KRISTO

  MTAZAMO HUU NI WA WATU WALE WALIOPINGA UKARISARIA WA UFALME WA RUMI ULIOVAA VAZI LA UKRISTO NA KUINGIZA MAMBO YA KIPAGANI KATIKA UKRISTO,KUZUIA WATU KUSOMA BIBLIA MPAKA MIAKA YA 1500.KUBADILISHA AMRI KUMI,SANAMU,NA KUFANYA HUDUMA MBADALA YA UPATANISHO WA DHAMBI KUPITIA MAKASISI, NA KUUA WAKRISTO WALIO NA MISIMAMO YA BIBLIA TAKRIBANI MILLIONI 50,000,000.HUTUMIA VITABU VYA DANIELI NA UFUNUO KATIKA KUELEZEA. NI LINI MPINGA KRISTO ANATOKE NA NINI ANAFANYA.

  TATU: FUTURISM
  MTAZAMO HUU ULIANZISHWA NA KIONGOZI WA SHIRIKA LA JESUIT ANAYEITWA RIBERA MWAKA A.D 1580

  NI MTAZAMO ULIOCHUKULIWA NA MAKANISA MENGI YA SASA
  MTIZAMO HUU HAUONYESHI/HUPINGA KUWA MUNGU ANAKUJA KUKAA KATIKA MIILI YETU KUPITIA ROHO MTAKATIFU,HIVYO HUTAMBUA UJENZI WA HEKALU HUKO YERUSALEMU KATIKA UPYA WAKE AMBAMO MPINGA KRISTO ATAKAA NDIO HEKALU AMBALO MUNGU NA MPINGA KRISTO WAWEZA KAA. MBINU AMBAYO IMETUMIKA KUHADAA MAKANISA.

  HUPINGANA NA MAFUNGU HAYA YA BIBLIA;

  1 WAKORINTHO 3:16:
  “HAMJUI YA KUWA NINYI MMEKUWA HEKALU LA MUNGU, NA YA KUWA ROHO WA MUNGU ANAKAA NDANI YENU?”

  1 WAKORINTHO 3:17
  “KAMA MTU AKILIHARIBU HEKALU LA MUNGU, MUNGU ATAMHARIBU MTU HUYO.KWA MAANA HEKALU LA MUNGU NI TAKATIFU, AMBALO NDILO NINYI.”

  1 WAKORINTHO 6:19
  “AU HAMJUI YA KUWA MWILI WENU NI HEKALU LA ROHO MTAKATIFU ALIYE NDANI YENU, MLIYEPEWA NA MUNGU” WALA NINYI SI MALI YENU WENYEWE;”

  MATHAYO 23:38
  “ANGALIENI, NYUMBA YENU MMEACHIWA HALI YA UKIWA”
  JIULIZE UHALISIA WA KIROHO WA MPINGA KRISTO KUKAA NDANI YA HEKALU NA KUJIFANYA NDIYE MUNGU NI UPI.

  KAMA BIBLIA SASA INATAMBUA MWILI KAMA HEKALU.
  NINI HASA SIFA YA MPINGA KRISTO KUTOTAMBUA KUWA MUNGU HAJI KATIKA MWILI.

  MTAZAMO HUU HUELEZA UNYAKUO WA KIMYA KIMYA NDIO UTAKAOTOKEA
  MTAZAMO HUU NI WA KIMWILI HUCHUKULIA PIA VITA YA AMAGEDDONI NI YA KIMWILI NA KUANDAA MAZINGIRA HUKO ISRAELI ILI WATU WATAZAME MATUKIO YA KIMWILI KATI YA ISRAELI NA MAJIRANI ZAKE.

  MTAZAMO NAMBA MOJA NA NAMBA TATU ILIKUWA NA LENGO LA KUWAONDOA WATU KUUSHUKU UPAPA KAMA UNAENDA KINYUME NA MUNGU NA BIBLIA.
  NDIO MAANA MTAZAMO NAMBA TATU UMEANZA (1580) WAKATI WA MARTIN LUTHER UKIPINGA MAWAZO YA LUTHER NA WANAMATENGENEZO.
  ITAHITIMISHWA KWA KUKUTANISHA TENA WALUTHERI NA KANISA LA RUMI MWAKA 2017 KUBADILI MTAZAMO WALUTHER NA MAANDISHI YAKE.

  MITAZAMO NAMBA MOJA NA NAMBA TATU ILITOLEWA NA JESUIT/SHIRIKA LA KANISA LA RUMI.

  MTAZAMO WA WANAMATENGENEZO NDIO ULIOWAFANYA WAUWAWE
  KATIKA UKWELI NI KWAMBA PAMBANO LINALOENDELEA SASA LITAMALIZIKA KWA UHALISIA WA MAUAJI YA KIMWILI KWA WALE AMBAO WATAENDELEA KUSHIKILIA BIBLIA KAMA MSIMAMO WA IMANI. NA WATAAMBIWA KUWA MISIMAMO YAO INAVURUGA AMANI NA UMOJA.

  NI LINI KUNYAMAZISHWA KWA MTAZAMO WA WANAMATANGENEZO?

  KATIKA MKUTANO WA MTAGUSO WA II WA VATICAN VIONGOZI WA MAKANISA WALITIA SAINI MKATABA NA KANISA LA RUMI KUTOTHUBUTU KUITA UPAPA NI UPINGA KRISTO KAMA WANAMATENGENEZO WALIOPIGANA MPAKA LEO BIBLIA INASOMWA NA KILA MTU KUPITIA MARTINI LUTHER ALIANZA KUANDIKA BIBLIA KWA KIJERUMANI BAADA YA KUIKUTA BIBLIA KATIKA MAKTABA.

  JAPO WAFARANSA WALICHOMA BIBLIA KWA MIAKA MITATU ZITOWEKE MUNGU HAKUKUBALI NENO LAKE KUWA INJILI ITAHUBIRIWA ULIMWENGUNI KOTE LIENDE BURE.

  MPINGA KRISTU AKAJA NA MBINU YA KUANZISHA MAKANISA YATAKAYOTETEA MAWAZO YAKE. BADALA YA KUONYESHA WAZI ANAPINGA BIBLIA.ILA AIFAFANUE KWA FASILI KADILI YA MATAKWA YAKE. NA KUONDOA YALE MAMBO YANAYOLETA TOFAUTI KATI YA MADHEHEBU.

  NINI NANI HUFASIRI BIBLIA? NA UNABII
  2 PETRO 1:20
  “MKIJUA NENO HILI KWANZA, YA KWAMBA HAKUNA UNABII KATIKA MAANDIKO UPATAO KUFASIRIWA KAMA APENDAVYO MTU FULANI TU, MAANA UNABIII HAUKULETWA POPOTE KWA MAPENZI YA WANADAMU; BALI WANADAMU WALIYANENA YALIYOTOKA KWA MUNGU, WAKIONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU.”

  NINI HASA MPINGA KRISTO HAPENDI: JIBU: KUTUMIA MSTARI KWA MSTARI BIBLIA IKIJIFASIRI YENYEWE KULETA MAJIBU YA NINI MUNGU ANASEMA. NDIO MAANA VITABU VYAUNABII PAMOJA NA DANIELI NA UFUNUO VINAPINGWA SANA MAANA HUUNGANISHA MSTARI NA MSTARI KUFUMBUA SIRI ZA MPINGA KRISTO.

  YESU ALIJUA SIRI YA VITABU HIVI AKASEMA
  UFUNUO 1:3
  “HERI ASOMAYE NA WAO WAYASIKIAO MANENO YA UNABII HUU, NA KUYASHIKA YALIOANDIKWA HUMO; KWA MAANA WAKATI U KARIBU.”

  ISAYA ANATUMBIA 28:9-10 ANATUMBIA MAARIFA YA NENO TUNAYASOMA KWA KUUNGANISHA MASTARI MMOJA WA BIBLIA NA MWINGINE,HOJA MOJA HAPA NYINGINE PALE NDIO TUTAPATA AMAARIFA

  LEO KUFASIRI BIBLIA KILA MMOJA ATAKAVYO NDIKO ANAKOTAKA SHETANI ILI APATE UHURU WA KUINGIZA MAFUNDISHO YASIYOSEMWA NA BIBLIA.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s