“Sema kitu juu yangu, nahitaji maombi yenu magonjwa yananisumbua”

maombii

Bwana Yesu asifiwe wapendwa… napenda kuomba maombi yenu kwani nimekua nikisumbuliwa na magonjwa ya mara kwa mara ambayo hata hayaeleweki… na wakati huu nasumbuliwa sana na sikio pamoja na kitezi kilichoota kichwani..nakosa amani kutokana na maumivu..naamini Mungu mwema na kwa maombi yenu ataniponya.. mbarikiwe

–Sarah Yona

Advertisements

8 thoughts on ““Sema kitu juu yangu, nahitaji maombi yenu magonjwa yananisumbua”

  1. NILIPOKEA MUUJIZA,KWANI INGAWA NILIFANYIWA OPERATION LAKINI SIKUTOLEWA KIZAZI(KAMA NILIVYOAMBIA KABLA NA KUTOKANA NA TATIZO KUANZIA KTK KIZAZI).TATIZO LA INI,CANCER PAMOJA NA MOYO VIMEPOTEA.GRORY BE TO GOD.DADA Sara KUMBUKA MUNGU SI MWANADAMU HATA ASEME UONGO,KWA HIYO HULIANGALIA NENO LAKE APATE KULITIMIZA(YEREMIA 1:12) NA NENO LAKE NI KTK(ISAYA 53:5,1PETRO 2:24)KUTOKANA NA HALI UNAYOPITIA.LAKINI PIA KUMBUKA KTK KUPITA UNAHITAJI ROHO MTAKATIFU AKUWEZESHE AKUTIE NGUVU NA FARAJA NA AMANI (YOHANA 14:16,26-27) .UBARIKIWE NA UPONE KTK JINA LA YESU ,NAMI NAKUWEKA KTK MAOMBI

  2. na wengine ili wapokee muujiza ni lazima wajazwe ROHO MTAKATIFU ili awape NGUVU,FARAJA ktk kustahimili mikiki ya tatizo yaani usitoke nje ya mstari kwa kutafuta msaada usio wa ki Mungu.(kwani nje ya msaada wa Mungu muujiza wako unakufa),pia ROHO MTAKATIFU ANAKUPA MWONGOZO,kwamba uliombee vipi tatizo ili litoke,ndipo mtu anakuwa huru.Kwa maana hiyo dada Sara pamoja na kutak kuombewa pia nawe fanya jambo ,KWAMBA KAMA HUJAOKOKA ,MKABIDHI LEO BWANA YESU MAISHA YAKO.2,IKIWA UMEOKOKA KUWA NA TABIA YA KUOMBA NA KUSOMA BIBLIA ILI HAYO MENENO YAKUSAIDIE KIPINDI HUWEZI KUOMBA mf.mimi kwakuishi na magonjwa muda mrefu na maumivu,nilikuwa nakiri Isaya 53:5 (kwa kupigwa kwake-Yesu mimi nimepona) hata kama ninatembea,lakin maumivu yakizidi ndivyo nilivyokuwa nakiri.naelewa KUNA KUKATA TAMAA NA KUKOSA AMANI KTK UGONJWA.kwa mimi ndipo nilipongundua kazi ya Roho mtakatifu hapa duniani.kwan nilikuwa namwita na mara nasikia faraja ya ajabu ndani ya moyo wangu,hivyo nikaendelea kusonga mbele.na HATIMAYE WAKATI WA MUNGU ULIPOFIK

  3. shalom dada Sara.miaka zaidi ya sita ya nyuma,nilianza kuumwa magonjwa mbalimbali yakiwemo ya tonsils,moyo,uvimbe tumboni na mbaya zaidi niliambiwa nina cancer na ini lina matatizo.magonjwa hayo yalizuka nikiwa nimeokoka.IMAGINE nilivyofadhaika kwa kuwa na maswali mengi kama kwanini ninaumwa? tena magonjwa ya ajabu kwa nini mungu haniponyi(hiyo ni baada ya kuomba sana na kuombewa sana lakin uponyaji haukutokea).dada sara ninapoandika hii sms,mimi ni MZIMA,SIFA NA UTUKUFU ZIMWENDEE YESU KRISTO AMBAYE NI BWANA NA MWOKOZI,kwa neema yake ya kunipa nafasi ya pili(second chance to live)ya kuishi.Hivyo dada sara UTAPONA TU AMINI.kumbuka Yesu ni yule yule wa jana(aliniponya mimi),leo(anakuponya wewe),na milele(ataendelea kuponya wengine.)KATIKA KUPOKEA UPONYAJI KUNA NGAZI TOFAUTI TOFAUTI namaanisha kuna wanaoombewa na MARA WANAPONA,lakini wengine wanalazimika kuomba na kufunga wenyewe ili tatizo liondoke.na wengine wanaenda zaidi kwa kukiri neno la Mungu linaloenda sambamba na kutatua tatizo,hadi tatizo linaisha

  4. Nasema kitu juu yako, MAUMIVU YA KILA NAMNA TOWEKA SASA HIVI, MWACHIE MTOTO WA MUNGU SARA ,POKEA UPONYAJI, SEMA AMEN.

  5. Mungu akabaliki kule kutaka maombi umeonyesha nia kuwa kwa Bwana yote yanawezekana mimi napenda kukuambia neno la Mungu linasema kila atakaye mtazama Yesu aliyeangakiwa pale Calvari atapokea uzima kwani pale msalabani alibeba kila kitu na kusema imekwisha wewe ni kuamini tu utapokea nami nasema kwa jina la Yesu uwe mzima ameni

  6. pole sana mungu atakuponya.ila pamoja nasisi kukuombea inatakiwa wewe uende kanisani ambalo liko karibu na wewe uombe watumishi wakakuombee na wakuongoze sala ya kuamishia maisha yako kwa Bwana yesu.utapokea mhujiza wako mara moja.na unapotaka kwenda usipange siku we nenda mdawowote maana adui wa mtu ni yule wa nyumbani kwake.

  7. Pole sana dada Sara. Hakuna kitu kisichowezekana kwa Mungu, Naye hujua haja za mioyo yetu. Lakini yote hayo ni kwa sala, maombi, na kushukuru.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s