Ushindi dhidi ya Upinzani – Mama Makange

DSC_0004

MAANDIKO: NEHEMIA 4: 1 – 23
MST. KUMB. ZAB. 37: 39;

NA WOKOVU WA WENYE HAKI UNA BWANA,YEYE NI NGOME YAO WAKATI WA TAABU.

KWELI KUU: Maombi, umoja, Ushirikiano na moyo kwa ajili ya kazi ya Mungu huleta ufanisi mkubwa sana. Kanisa lijihadhari sana juu ya vita vya ndani ya Kanisa.

KUSHINDA KUVIZIWA KWA MAOMBI NA ULINZI WA USIKU NA MCHANA

NEH. 4: 10 – 23.
– Kuviziwa ni ile hali ya kufuatiliwa kwa siri kwa lengo la kutia hatiani au kuangamiza, na kwamba hatua ya kwanza kabisa kuelekea kwenye kuvuka mitego iliyowekwa ni kuwa na tahadhari kwanza ya mwenendo wako mzima kwamba uko salama/sahihi katika mapito yako yote na mipango yote, hatua ya pili ni kukesha. 1Pet. 5:8; Muwe na kiasi na kukesha, kwa kuwa mshitaki wenu ibilisi kama simba angurumae, huzunguka , zunguka, akitafuta mtu ameze .

– Kukesha (be on the watch) – kuwa macho kwa malengo au matarajio mahsusi. Kukesha ni kungoja kwa uvumilivu kwa kusudi la kulinda/kuhakikisha usalama wa kitu cha thamani mtu alichonacho.

– Huwezi kuwa macho au kukesha kwa jambo ambalo hujaona uthamani wake, tunaona watu wakitumia gharama kubwa kuweka walinzi (wakeshaji) kwa ajili ya usalama wao na mali zao. Tunaona watu wa taaluma Fulani wakiwa kwenye ngazi za kufanya maamuzi makubwa yanayotegemewa wakiwekewa ulinzi (wakeshaji) ili kuwa hakikishia usalama wao

– Mungu mwenyewe ameweka wakeshaji wa kulinda vitu vyake vya thamani; Mwz 3: 22-24- Kwakuwa asili ya Mungu ni Mtakatifu, alipoona kwamba Mwanadamu aliyeumbwa kwa sura na mfano wake ameasi amri yake alimfukkuza na ili asitwae matunda ya mti wa uzima na kuyala na kuishi milele kama Mungu, aliweka ulinzi (wakeshaji) katika njia ya kuuendea mti wa uzima ili Uungu wake usinajisiwe.

– Kwa hiyo mtu anakuwa macho/anakesha pale tu napokuwa ametambua uthamani wa kile ambacho anakesha kwa ajili yake. Watu na Nehemia walikesha kwa sababu kwanza lengo lao lilikukwa ni kurudisha heshima ya Mungu kwa Taifa la Israeli na kwa mji ulioitwa kwa jina la Mungu wao, Neh. 2: 1 – 5, 17. Waliona thamani ya Mungu na ya mji wao.

– Ukisoma sura ya kwanza ya kitabu cha Nehemia na kuyaangalia kwa makini maombi yake, yalikuwa ni maombi ya kutaka rehema za Mungu baada ya kutambua kwamba hali ile dhaifu ya mji wa Yerusalemu ni kwa sababu ya uasi wao wa kutozishika sheria ambazo Mungu aliwapa Watumishi wake.

– Ndio maana akaomba fadhili za Mungu ili ampe kibali aujenge tena mji ili watu warejee kwa Mungu wao na Mungu aurejee mji wa Yerusalemu. Watu hawa walijitabisha sana kwa sababu walikuwa wanautambua uthamani wa Mungu maishani mwao, ndio maana kwa juhudi zote Nehemia alianza kwa kukesha peke yake akimtaka Mungu ampe nafasi ya kwenda kujenga tena Yerusalemu. Neh. 1: 4 – 6.

– Mtu anayekesha mara zote pamoja na kuona uharibifu lakini pia anaziona fursa ambazo ziko kwa ajili ya kuleta usalama kwake na kwa kundi la Mungu. Unajua Mungu peke yake 2 ndiye ambaye ametoa fursa sawa kwa wote lakini inategemea kiwango cha macho ya mtu kuweza kuziona fursa hizo ili kuzitumia vyema na kuleta matokeo chanya.

– Kwa kuziona fursa hizo mtu huyu atapanga mikakati ya makusudi ya kumletea ushindi katika yale ambayo anakabiliana nayo. Neh. 4: 16 – 23, Nehemia hakuridhika tu na ile hali ya kuona kwamba adui amekata tamaa na kuwaachia lakini alijihakikishia ulinzi endelevu.Kwa kuweka zamu pamoja na kumfanya kila mtu aone umuhimu wa kufanya majukumu yake huku akijihakikishia usalama wake na wa ndugu zake.

– Kwa nini kujihakikishia ulinzi endelevu? Maandiko yanasema kwa sababu mshitaki wetu anazunguka zunguka akitafuta mtu ili amwangamize au amtie hatiani. Ayub. 1: 6 – 7.

– Swali la Mungu kwa shetani ni kwamba unatoka wapi? Jibu la shetani anasema natoka katika kuzunguka zunguka. Shetani anauzungukia mwenendo wako mzima na mipango yako yote na haishii hapo anakufuatilia hata jinsi unavyojihudhurisha mbele za Mungu.

– Kwa hiyo kukesha kunakoendelea au ulinzi endelevu ni wa muhimu sana kwa kusudi la mtu kujihakikishia uhalali wa kupokea ahadi zake kwa Mungu. Biblia inasema kwamba Mungu hakuliacha neno la Samwel kuanguka chini lakini aliliruhusu neno liyaumbe maisha yake ndio maana akawa mwamuzi na nabii ambaye alitumika bila kumkosa Mungu kuanzia mwanzo wa huduma yake hata mwisho. (As Samuel grew up the Lord was with him and
made everything that Samuel said come true).

– Kwa kuwa Samwel alikesha alipokaa ndani ya nyumba ya kuhani ambaye watoto wake walikuwa waasi aliweza kupata uhalali wa kupokea ahadi ya kusema neno na lile neno kuthibitika.

– Usidhani kwamba watoto wa Eli hawakumshawishi Samwel kutenda kinyume na Bwana, kwani kwanza wao pale palikuwa ni nyumbani kwao na pia walikuwa watoto wakubwa ambao ilimpasa Samwel kuwasikiliza. Lakini kwa kuwa Samwel alikuwa na kawaida ya kulala katika hekalu la Bwana tena karibu na Sanduku la agano hakuvutwa wala kushawishwa moyo wake kuzifuata njia mbaya za wana wa Eli. 1Samw. 3: 2 – 4.

– Unajua ukiwa umemwekea Bwana shauku yeye anauteka kabisa moyo wako na wewe unakufa ganzi kwa mambo ya dunia lakini unakuwa sensitive kwa mambo ya Mungu. 1Pet. 4: 2 – 4.Maandiko yanasema mambo ambayo wao huona kuwa ni ajabu ya ninyi kutokwenda mbio pamoja nao katika ufisadi ule ule usio na kiasi, wakiwatukana. Hatujikazi kutokutenda dhambi bali tumeikinai dhambi na mazalia yake.

– Kwa hiyo kukesha kwako kutakuwa ndio nanga itakayofanya usitikiswe wala kung’olewa katika maazimio na maagano yako na Bwana.

ANGALIZO:
Hatua hii  ya vita ina gharama kubwa kwani haihitaji mtu kuziweka silaha zake chini hata  kama hajasikia tetesi za vita bali ni kukaa macho kwa kusudi la kukabiliana na chochote ambacho kinaweza kutokea wakati wowote. Kumbuka kwamba mshitaki wetu anazunguka zunguka hivyo sio kwamba amelenga kwenda mahali Fulani bali popote atakapoamua kwamba ndio mtego wake anapouweka anauweka, hivyo ili nishinde ni lazima nikeshe.

– Kukesha /(kungoja)/ kuwa macho kuna faida nyingi kiroho ambazo hazionekani kwa dhahiri katika mwili, ndio maana kunahusisha kuwa na subiri na uvumilivu. Mark. 6: 30 – 44.Unaweza ukaona kwamba andiko hili linahusiana vipi na kukesha na kushinda kuviziwa. Tunaona kwanza Wanafunzi walikuwa wametoka kufanya kazi ya kuchosha hata Bwana. mwenyewe akataka wapate mahali faragha angalau wapumzike kidogo na kula chakula.

– Lakini walipoondoka tu watu wakaenda kwa miguu wakatangulia kufika kule ambako Yesu alitaka angalau Wanafunzi wake wapumzike. Jambo hili lilifanya ratiba ya Yesu ibadilike na kuendelea kuwafundisha makutano hata muda mwingi ukapita. Hapa wanafunzi bado
walikuwa hawajala wala kupumzika.

– Kwa kuwa kukesha ni gharama Yesu akatangulia kuliona hitaji la Makutano la kupewa chakula. Kumbuka kwamba wanafunzi walikuwa bado hawajala, lakini Bwana akatoa kipaumbele kwa makutano. Tunaona kwamba Wanafunzi hawa hawa ndio ambao walioambiwa wawahudumie watu, hata wakala mpaka wasaza.

– Hatua iliyofuatia ndio inayoonyesha faida ya kungoja/kuingia gharama ya kukesha pale walipokusanya vipande vya mikate na samaki vilivyobaki walipata zaidi ya vile ambavyo walitarajia/ yaani zaidi ya vile ambavyo waliwapa watu.

– Pale mtu anayekesha anapoona kana kwamba anateketea hapo ndipo anaiinuliwa na Bwana na sio faida katika ulimwengu huu tu bali heshima kubwa katika ulimwengu ule ujao, Dan. 12:3

– Faida nyingine kubwa ya mtu huyu anayekesha ni kuwa na uhakika wa usalama wake katika Ulimwengu huu na uhakika wa kule aendako. Math. 25: 10. Mtu anayekesha hana matendo ya kubahatisha bali anakuwa na hatua za uhakika katika yale yote anayoyatenda na anayotarajia kuyatenda.

– Kwa hiyo kwa ujumla wa somo hili la ushindi dhidi ya upinzani, mteule atashinda na zaidi ya kushinda kama yeye mwenyewe ameamua kwamba ni lazima ashinde.

 Yaani ushindi wangu hauko mikononi mwa Mungu au mikononi mwa mtu bali umo katika uwezo wangu mwenyewe kwamba ninaamua kuyapangaje maisha yangu kuelekea kwenye kushinda au kwenye kushindwa. 2Pet. 1: 3 -11.

– Mungu ametupa kujua uwezo tulionao dhidi ya mpinzani wetu, ametufunza mbinu za kutumia ili kumshinda adui, ameziweka wazi mbinu za adui anazotumia mbele yetu, kwa hiyo ni wajibu wetu kama tutaamua/tutaridhia kuyafuata maelekezo yake ili tushinde au tutegemee akili zetu ili tushindwe.

– Ushindi wetu umehakikishwa kama tumejihakikishia kumfuata Bwana kwa nia ya kumkubali

Note: Hakuna muijiza wa kushinda kama sitamtafuta Bwana na kukaa katika sheria yake na pia kutumia akili kama ipasavyo; na kuepuka uvivu wa kiutendaji na uvivu wa kifikra. Ni lazima wakati wote niwe macho ili nione na kutambua kwamba katika kila changamoto ninayokutana nayo Bwana ameniwekea fursa ya kutoka hatua moja ya chini kwenda kwenye hatua ya juu zaidi.  Ni lazima pia uelewe/nielewe kwamba fursa ni kitu cha thamani sana ambacho huweza kumfikisha mtu kwenye hatima yake lakini ambacho hakionekani na mtu ambaye hatajitaabisha kutaka macho yake yatiwe nuru. Mith. 17: 8. Amen.

Na
Mama Makange
2/6/2013

Advertisements

2 thoughts on “Ushindi dhidi ya Upinzani – Mama Makange

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s