Mpende adui yako!

mlk

‘‘Mmesikia kwamba ilinenwa, ‘Mpende jirani yako na umchukie adui yako.’ Lakini mimi ninawaambia, Wapendeni adui zenu na waombeeni wanaowatesa ninyi, ili mpate kuwa watoto wa Baba yenu aliye mbinguni. Kwa maana Yeye huwaangazia jua lake watu waovu na watu wema, naye huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki. Kama mkiwapenda wale wanaowapenda tu, mtapata thawabu gani? Je, hata watoza ushuru hawafanyi hivyo?

Mathayo 5:43-46

Advertisements

2 thoughts on “Mpende adui yako!

  1. Asante kwa ujumbe mzuri. Kwangu mimi umekuja wakati muafaka. Japo siwezi kusemea nafsi za wengine lakini nafikiri ni mtihani mkubwa sana kwa wengi kuwapenda na kuwaombea adui zao kwa maana ya kumaanisha kweli kutoka moyoni bila kuwa na kinyongo chochote.

    Lakini kwa upande wangu huwa napata shida pia katika hili. Mfano unakuta labda mtu anasumbuliwa na nguvu za giza au uchawi na anajua kabisa kwamba anayenitumia nguvu hizi za giza ni fulani. sasa hapa inapokuja kwenye kuomba binafsi huwa napata shida maana nimeshakutana na maombi mengi yanayosema mfano, ” maombi ya kusambaratisha wachawi, maombi ya hatari, sala za mapambano n.k na mengine mengi tu ambayo ukisoma ndani unaweza kukutana na vipengele kama “wachawi wote nawatumia moto wa Roho Mtakatifu au wachawi wote nawasambaratisha wasiinuke milele mpaka siku ya hukumu na vitu kama hivyo. Binafsi huwa najiuliza hivi ni sahihi kuomba maombi kama haya wakati neno la Mungu linatuambia tuwapende maadui zetu, tuwabariki na wala tusiwalaani.

    Tukirudi kwenye Biblia pia kuna zaburi kama ya 35 ambayo ukiisoma unaona kabisa kuna mistari ambayo inawalenga adui kama binadamu na si kama roho chafu. Binafsi niliwahi hata kuambiwa na mtumishi mmoja wa Mungu nisali zaburi hii mara kwa mara, (Nilikuwa na tatizo ambalo nilimshirikisha). Pia kuna maombi kama “I am returning back to the sender all the evil spirits n.k. Binafsi huwa napata shida na natumani kwenye mada hii nitapata mwanga zaidi.

    Mbarikiwe

    Kokusima

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s