Mtume Augustus Baraza apinga injili ya misukule!!

 • barazaa

  Misukule ni nini? Ni watu ambao hufa wakazikwa lakini sio kifo cha ukweli ni kifo cha kichawi ambapo wachawi wanafumba watu macho. Na mtu aliekufa huwa anapelekwa kulima mashamba. Wachawi wana uwezo wakuwateka watu kuwapeleka musukule ama kuwarudisha kwa nguvu za giza.

  Mimi sipingi kwamba watu wa Mungu hawawezi kurudisha mtu toka msukule.Lakini ninachopinga ni kwamba haiwezi kuwa ni kila siku nenda rudi ni kurudisha misukule

  Misukule ni disco na dansi ya wachwi. Na Mungu hawezi cheza mchezo huu na shetani kila siku kwani Yesu alishinda kifo mara moja wala haitaji kushindana na wachawi wa Misukule kila siku ili kuonyesha ana nguvu juu ya mauti.

  Alishinda mauti mara moja aliposema imekwisha UFUNUO 1-18 Mimi ni Alfa na Omega Mwanzo na Mwisho, nilikuwa nimekufa na sasa Tazama niko mzima hata milele ninazo funguo za Uzima na mauti

  Kumbuka Mungu hafanyi kazi kwa mwelekeo moja. Inapofika mhubiri kubuni Injili ya misukule inageuka na kuwa dini maana Roho wa Mungu ni kama upepo anafanya kazi kwa njia mbalimbali.

  Mtu wa Mungu anaweza kutumiwa kurudisha msukule mara kadhaa lakini hawezi kudai kwamba YEYE NISPECIALIST WAKURUDISHA WAFU WA MISUKULE EVERY DAY, EVERY CRUSADE HIYO NI MCHEZO WA KICHAWI mchezo huu unafanywa kwa wingi nchi ya HAITI ambapo wachawi huwapiga watu kufa kifo cha kimapepo hata siku 20 ambapo mtu anaonekana amekufa anazikwa halafu baada ya siku 10, 20,30,40 wachawi wanakuja kaburini mchana peupe na wanamfufua mfu.

  NAWABIENI KAMA MTUME WA YESU KRISTO.

  MUNGU HAYUMO KWENYE MCHEZO WA MISUKULE KILA SIKU NENDA RUDI HIYO NI DISCO NA NI NGOMA YA SHETANI. NI MCHEZO AMBAPO WACHAWI WANAJARIBU KUONYESHA WANA NGUVU JUU YA KIFO. SISI WAKRISTO TUNAJUA YESU AMESHINDA KIFO MARA MOJA NA WALA HATARUDIA KAMWE.

  Ishara nyingine za manabii wa Uongo hizi hapa:

  Wanauza mafuta, Vitambaa, Funguo, picha, udongo, kofuli, mishumaa, wanapenda pesa, wanaishi maisha a kifahari, wana kiburi tena wanadai wao ndio besy of the best

  Akijibu swali la ndugu Frank Daniel aliloandika kutoka Isaya 42:22 “lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa;wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka wala hapana asemaye, RUDISHA. kumbe kuna watu walioibiwa na kutekwa na hakuna awaokoae wala arudishaye

  Mtume Baraza akajibu “Mashimo na magereza ni mengi ndugu Frank andiko hili liko applicable kwa sehemu nyingi kama kwa mfano kuna gereza na mashimo mbalimbali kama ukahaba, ulevi, uchawi, wizi nakadhalika wala huwezi kulifanya misukule pekee.

  Zaburi 40 Daudi anasema Nalimgoja Bwana kwa subira akanitoa toka shimo la uharibifu. Daudi alikuwa shimoni wa msukule

  Isaya 58 Ukisoma inataja vifungu vya nira na kongwa mbali mbali kwahiyo andiko ulilotoa linazungumza juu ya nira aina nying halizungumzii msukule pekee.

  Amini usiamini nakwambia kama mtume wa Kristo ni makosa kwa mhubiri yeyote kuhubiri misukule mkoa kwa mkoa mkutano kwa mkutano. Hiyo ni confusion na ni upotovu na nimafundisho yasiyo ambatana na Kristo.

  Ikiwa Gwajima anahuduma ya Misukule mbona asiende nchi ya Haiti huko kuna wachawi wanachukua watu misukule mchana sokoni hawajifichi. Huduma yake itapamba moto huko

  Mbona asiende huko kuna watu maelfu misukule hadharani mchana.

  Ikiwa yuko tayari nitamnunulia ticketi ya ndege nimlipie hoteli miezi sita twende naye huko nchini Haiti arudishe misukule, yaani watu wasiokoke lakini kila siku akiamka tunaenda naye sokoni Haiti kupambana na wachawi wanaoteka misukule na Gwajima anarudisha, ikifika jioni tunaenda kulala asubuhi ikifika tunakunywa chai tunaenda sokoni.

  Sijui kama mnaipata point yangu? Je hii ndio Injili Yesu ametutuma tuhubiri kila siku? Kuchalenge wachawi ama tuhubiri watu waokolewe?

  Naomba majibu labda nimechanganyikiwa!!

  –Mtume Augustus Baraza Matibila

Advertisements

20 thoughts on “Mtume Augustus Baraza apinga injili ya misukule!!

 1. imekupasa utambue kwamba kuna tofauti za kutenda kazi,bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote.Pia pana tofauti za huduma,na Bwana ni yeye yule.Mungu ameachilia kazi na huduma tofauti tofauti,na wote tunafanya kazi kwa ajili yake.
  wote tungekuwa engeneers nani angemtibu mwenzake? mtume Paulo anasema mwili si kiungo kimoja bali ni vingi.
  Obviously huwezi ukaihukumu huduma ya mtu na hali haukuwepo wakati anaweka agano na Mungu,unataka useme Gwajima hajawahi hubiri habari za watu kuokoka? No. hata manabii wamepishana kwenye huduma na karama.wewe unaweza ukaambiwa itamsukule ukakesha mpaka asubuhi asirudi,lakini na wewe unahuduma yako ambayo katika hyo wewe uko imara.na kama ulikuwa hujui hilo basi na ujue sasa na kama ulikuwa unajua yanini kumpinga mtu ambaye Kristo Yesu alikufa kwa ajili yake? acheni kuhukumu kazi ambazo Mungu anazifanya kupitia watu wake.huna hiyo karama basi mshukuru Mungu kwa ajili yake huyo aliye nayo.usikimbilie kuhukumu

 2. Chemo,

  Kuna tatizo gani la kibiblia ambalo unadhani lingekuwa sababu ya kuwashauri kondoo wasiende kanisani kwa Gwajima?

 3. Sungura,

  Je, unam-endorse Gwajima? Ninamaana, Je unashari kondoo waende kwa Gwajima?

 4. Mbarikiwe nyote mliochangia!

  Ni ukweli ulio dhahiri kwamba ndani ya Kanisa tunao watumishi wa Kweli na Mbwa mwitu waliojivika mavazi ya kondoo. Hawa mbwa mwitu wamekokota kundi kwa kuinajisi ile neema tuliyopewa na Kristo. Binafsi siamini kabisa ktk injili ya misukule – SIAMINI! Agizo la YESU kwetu liko wazi Math 28:19&20 “…Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; 20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi…” Hivi tunavyojaribu kuvitumia ati kujenga imani kwa watu ni mazingaombwe matupu. Hivi uwepo wa YESU au Nguvu unakoma pale miujiza/ishara zinapokoma? Kama tunamwamini YESU au Injili unayohubiriwa na mtu fulani kwa sababu ya ishara/miujiza ambayo anaitenda mtu huyo, basi hatuna tofauti na wale waliomfuata YESU kwa sababu walikula mikate.

  Nionapo mhubiri yeyote yule anatumia miujiza kama ndio base ya mafundisho yake, kwangu huyo ni wa kumpuuza kabisa. Maana hilo si neno la MUNGU. Ieleweke sipingi uwepo wa miujiza/ishara bali visiwe kigezo cha kusimamisha mafundisho. Cha msingi watu waeleshwe uzuri wa Kristo, na matokeo ya kutengwa mbali nae. Mtu atatengwa na Kristo kwa sababu ya kutenda dhambi au kuwa shirika na shetani kwa kuzifuata njia zake.

  Kama huyo mtume/sijui nabii ametanguliza misukule zaidi badala ya injili ya Kristo, liko tatizo. Sitashangaa hata akitumia “power” ili kuwateka maelfu ya watu. Na kwa sababu shetani amewatia upofu watu wengi, basi wengi watapotezwa kwa kupitia watu hawa. Ila OLE WAO WANAOWAPOTEZA WATU KWA MAFUNDISHO YAO YA UPOTEVU! Ghadhabu ya MUNGU iko juu yao milele, hata wakatubu!

 5. Bwana YESU ASIFIWE WAPENDWA,
  ndugu zangu mimi ninachojua kila mtumishi kaitwa kwa huduma fulani wengine kuhubiri maneno ya faraja, wengine namna ya kufanikiwa, wengine kufungua waliofungwa, kuponya na wengine ni kama Josephat Gwajima kushughulika na misukule ukijaribu kuona utakuta mtumishi wa MUNGU pamoja na kuhubiri mambo mengi utakuta ile huduma aliyotumwa ndiyo anayoifanya mara nyingi na kwa ufasaha kuliko huduma nyingine lakini kwa pamoja wanajenga mwili wa KRISTO. kitu ambacho huwa kinaleta maswali ni pale ambapo mfano mchungaji wangu hafanyi kitu fulani na mwingine anafanya ndipo tunaanza kuhoji mamlaka ya hilo jambo lakini pia bila kusikiliza mahubiri na misingi ya jambo hilo binafsi mimi simkubali mchungaji kwa miujiza anayoifanya kwani hata shetani anaweza kufanya bali biblia inasema mtawatambua kwa matunda yao matunda yepi? si kuponya watu wengi, kuwa na waumini wengi sana, kuwa na matawi ya dhehebu kila nchi bali ni matunda ya roho mt. Upendo, amani, utu wema……kiingereza wanasema the environment they produce. ninachoweza kumwambia mtumishi ni kuwa kufanya kitu mara nyingi si kuwa ni ibilisi kama ndicho kitu ambacho MUNGU kamtuma ndiyo kazi ambayo Mungu atamuuliza siku ya mwisho.

 6. Dickson,

  Nikushauri jambo ndugu yangu: jaribu kuwa wazi na mwenye kulenga kueleweka unapochangia.

  Itafika pahala watu tutaanza kupuuza comments zako japo wewe unakuwa umelenga jambo jema.

  Kila ukichangia mada unaongelea unyenyekevu, hauwi wazi sana na mada husika.

  Please, litazame hilo!

 7. TATIZO NI WIVU TU!WALA SI MISIKULE!UWEZI KUMZUIA ALIYETUMWA NI KAMA UNAMPIGIA MBUZI GITAA!UTACHEMSHA TU KA

  KIMYA FANYA MAMBO YAKO ACHENI KUMCHOKOZA MTU MSIYEMJUA.

 8. Roho Mtakatifu naomba UTULIVU WAKO katika kufikiri,kunena na kutenda.Naomba utumie kinywa changu jinsi upendavyo wewe kwasababu unaishi ndani ya moyo wangu.NAKUSHUKURU KWA HEKIMA YAKO YA MOTO ULAO(1 YOHANA 2:27,LUKA 12:49,1 WAKORINTHO 2:6-13).

  Watu wa rohoni ambao wanaoishi katika ULIMWENGU WA ROHO WA NURU NA ULIMWENGU WA KIMWILI KWA WAKATI MMOJA,WAMEBARIKIWA NA MAARIFA YA MUNGU.Ni wanyenyekevu wanaoishi duniani(Isaya 11:4) wanaotawala na kumiliki kwa kutumia MACHO SABA YA MOTO WA MUNGU(Ufunuo 5:6).Ni watu ambao wanayaona mambo makubwa na magumu yanayofichwa(Yeremia 33:3) na mambo ambayo yalikuwa YAMESITIRIKA SANA yanasimama UCHI mbele zao(Luka 12:2,1WAKORINTHO 2:15-16).Kwahiyo ni watu ambao wanauangalia mfumo mzima wa maisha ya wokovu na hila zote zilizomo ndani yake kwa TABASAMU LA UNYENYEKEVU.Wanacheka KICHEKO CHA UNYENYEKEVU.Kila sekunde wanamshukuru Mungu aliye hai na kumrudishia utukufu kwasababu ya HEKIMA YA YESU INAYOISHI NDANI YAO.

  Nazungumza habari za wateule wenye uweza wa kupambanua kati ya MAFUNDISHO YA MASHETANI(1TIMOTHEO 4:1,WAFILIPI 1:17-18),MAFUNDISHO YA WANADAMU(MATHAYO 15:7-9,1WAKORITHO 2:12-13) NA MAFUNDISHO YA ROHO MTAKATIFU(1WAKORINTHO 2:6-16,1YOHANA 2:27).Kwahiyo kuna hekima ya mashetani,hekima ya wanadamu na hekima ya Roho Mtakatifu na ZOTE ZINASIMAMIA NENO LILILOANDIKWA NDANI YA BIBILIA!!HII NI INJILI YA UNYENYEKEVU ULIO HAI.

  Mungu aliye hai anazungumza wazi kabisa habari wa wateule wake WASIOWEZA KUPAMBANUA KATIKA MKONO WAO WA KULIA NA MKONO WAO WA KUSHOTO.MUNGU ANASEMA WANAHITAJI KUHURUMIWA(YONA 4:11).Hata hivyo kama NISIPOUKANA MOYO WA YONA HUKUMU YA MUNGU ITAKAA JUU YA KICHWA CHANGU.MIMI NAJICHUKIA KWASABABU YA KILE AMBACHO YONA ALIKUWA AMEDHAMIRIA MOYONI MWAKE.KWELI NI KWAMBA MUNGU AMECHOKA KUTAZAMA NAMNA WATU WANAVYOANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA(YONA 4:1-11).

  MUNGU ALIYE HAI AMESHATOA UNABII WA HATIMA YA WATUMISHI WA UONGO NA HUDUMA ZAO.TUSOME BIBILIA ZETU KWA MACHO YA UNYENYEKEVU.WAJUMBE WA SHETANI HAWATAAMINI KITAKACHOTOKEA KWASABABU MOTO WA MAARIFA YA YESU UNAITEKETEZA DUNIA KWA NAMNA YA KUTISHA MNO.ZIMEBAKI SEKUNDE CHACHE!!!MWENYE MASIKIO NA ASIKIE,MWENYE MACHO NA ATAZAME.

  UTUKUFU KWA YESU MILELE NA MILELE…..OLE WAKE ANAYEJARIBU KUJITWALIA HATA TONE LA UTUKUFU WA MUNGU ALIYE HAI.

 9. Esther Mushi,
  Umeongea vitu kama vitatu hivi nami napenda kuvisemea kitu;

  Kwanza umesema kuhusu watumishi kukemea dhambi
  Pili ukasema kuwa miujiza ni kwa ajili ya wasioamini
  Tatu umesema kuhusu kusikia kitu kimoja

  Ivi ni kweli kwamba watumishi wameitwa kwa ajili ya kukemea dhambi, au unaposema kukemea dhambi unamaanisha nini?
  Ukisema kazi yao ni kufundisha kweli ya Mungu nakubaliana nawe kwa asilimia zote. Dhambi haiondolewi kwa kukemewa bali kwa kujua /kufundishwa kweli ya Mungu. Dhambi ni utumwa kweli ndo inaweka mtu huru. Watumishi wanapaswa kuwafundisha watu kweli ya neno la Mungu, dhambi haitakuwa na nafasi.

  Hili suala la miujiza ni kwa ajili ya wasioamini wengi hulisema hivyo. Lakini huo ni ukweli au husema tu? Kwani Muujiza ni nini? Muujiza ni kitu kilitendwa kwa uweza wa kiungu (divive power). Hata kama ni kidogo sana alimradi kimefanika kiungu hicho ni muujiza, hata kama kimefanywa kwa namna ya kibinadamu lakini nguvu iliyotumika ni ya kiungu hiuo ni muujiza.
  Naamini hata wewe unahitaji muujiza katika maeneo mengi tu ya maisha yako

  Kitu ambacho ni kwa ajili ya wasioamini hicho kinaitwa ishara. Kwamba wanataka waone ishara ya kuwafanya wakubali kuwa Mungu yupo anafanya kazi ndipo wao wapate kuamini. Wanataka wakuone unashusha moto ndipo wajue kuwa Mungu wako ana nguvu, wanataka waone vitu mfano wa mazingaombwe, ubadili jiwe kuwa mkate, just kwa ajili ya wao kuona.
  Lakini masuala kama watu kuponywa, kutolewa mapepo, kufufuliwa, kurejeshwa kutoka misukule, n.k, hiyo ni miujiza ambayo ndiyo moja ya kazi ambazo tunapaswa kuzifanya pia, maana kwa kusudi hilo Yesu alidhihirishwa, yaani kuzivunja kazi za shetani.

  Kuhusu kusikia kitu kimoja, hebu tuacheni kusema tu mambo ambyo hata hatuyajui sana undani. Yesu alipowaagiza wanafunzi aliwaambia hubirini waambieni tubuni maana ufalme wa Mungu umekaribia, kwa hiyo hicho ndicho walihubiri kila siku. Hata Yohana mbatizaji alihubiri hichohicho kila siku.
  Neno la Mungu haliko kama diet ya wanalishe kuwa unatakiwa kila ukila kuwe na mboga za majani, kuwe na tunda, kuwe juice, usile sana wanga,n.k.

  Lakini hata hivyo jamani Gwajima hahubirigi habari za misukule kila siku, hebu fuatilieni kama mimi nilivyofuatilia, pamoja na kwamba si mshirika wake.

  Naamini angekuwa anahubiri hivyohivyo anavyohubiri lakini akawa na kikanisa kiogo, hakuna hata mmoja angesema chochote, lakini sasa kwa sababu kwa namna fulani kafanikiwa kuwa na kundi kubwa la watu maneno yatasemwa sana!

  Tuache!!!

 10. Jamani mungu atusaidie sana, kwa siku hizi za mwisho. tunatakiwa tusome maandiko na tuyaishi, maana bila kuwa na neno la mungu la kutosha ndani yetu, hatuwezi kuwa na uwezo wa kupambanua haya mambo. Biblia inasema siku za mwisho watatokea manabii wa uongo, bado hata sasa hatujahakikisha kama ndizo siku za mwisho, ingawa kwa mambo na matukio yanavyoonekana kulinganisha na neno la mungu, yaelekea kabisa hizo siku kwa kizazi hiki tumezikaribia.

  Mimi kwa maoni yangu, YESU kristo alisema “Njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo nami nitawapumzisha. Andiko hili ndilo walilopewa watumishi wa mungu, kwamba kila wanapokua katika kazi yao ya kuhubiri na kuokoa watu, msingi wa yote ni kuwaleta watu kwa YESU na sio vinginevyo. watakapookolewa watakua watoto wa mungu, na mungu peke yake ndio atakayeweka ulinzi juu ya maisha yao baada ya hapo.

  sasa injili za siku hizi ni watu wabarikiwe, sasa watabarikiwa na nani kama hawajampa yesu maisha, watu hawajakiri kama yesu ni bwana na mwokozi wa maisha yao watapata Baraka toka kwa nani? ndio hapo sasa tunapata maswali mengi yasiyo na majibu. wahubiri hawakemei dhambi, wao na dhambi ni marafiki na bado wanaona haifai kanisa lake kukemea dhambi. Jamani huo ndio wajibu wenu watu wa mungu kemeeni dhambi. Mtawawekea mikono watu kila kukicha lakini mioyo yao iko mbali na mungu hamuwasaidii, ni bora ubakie na waumini wawili kuliko kujaza hekalu halafu wanaoijua kweli ya mungu ni wachache. Yesu alisema “itamfaidia nini mtu kuupata ulimwengu wote na baadaye aje aukose ufalme wa mungu” Tafuteni Ufalme wa Mungu kwanza na hayo mengine yooote mtazidishiwa” hayo mengine yote ndio hizo barka za magari, nyumba n.k

  Kufufua misukule sio jambo baya, ni moja kati ya ishara ambazo watu wa mungu wanapaswa wawe na huo uwezo pia. Mungu wetu hashindwi na jambo lolote. Tatizo ninaloliona kwa huduma nyingi kama hizi ni pale wale watumishi kujisahau, wanadhani hiyo nguvu ni yake na anaimiliki yeye!! yaani mungu amempa KIBALI sawa, lakini anakitumiaje? Kwa ninavyoelewa mimi hii miujiza biblia inasema ni kwa wale wasioamini, lakini sisi tuliokwisha amini tunapaswa tupate Injili ya kweli, sasa kama kila siku tutakua tunasikia kitu kimoja sidhani kama ni sawa. Vaeni mwili wa Kristo jamani maadamu mmeamua kuifanya kazi ya Mungu, basi ifanyeni kwa ukamilifu wake, watu wahubiriwe habari njema za Ufalme wa Mungu na si vinginevyo.
  Mungu atusaidie sote.

 11. Hii ndio shida ya nyinyi mitume wa dar,mnaamka Dar-es-Salaam na mnalala Dar-Salaam na bado mnajiita mitume.Mi siwezi kukuhukumu kwa sababu uwezo wako wa kufikiri ndio umeishia hapo.Hata Petro na Yohana walimwambia yule kiwete “Tulichonacho ndicho tukupacho” hivyo ingawa yule kiwete alihitaji fedha wao walikuwa wamepigika hawana fedha ila ashukuriwe Mungu walikuwa na upako.Nikushauri kama huna nguvu za Mungu za kurudisha watu waliokufa kichawi ni bora ukae kimya uendelee kuwaibia watu sadaka na mafungu ya kumi ingawa siku ya mwisho utatoa hesabu.Pia kila mtu ana eneo lake ambalo Mungu amemuitia hivyo kama wewe hujui wito wako na huku unaendelea kujiita mtume basi endelea tu kupiga blaah,blaah.Mimi si muumini wa Gwajima lakini nakuhakikishia Gwajima ameitwa na Mungu na hakuna wa kumzuia kutenda kusudi aliloitiwa.Nakutakia mizunguko mema na kuzurura katika jiji la dar huku ukikosa muda wa kuomba.Namna hiyo hutaweza hata kumuombea mgonjwa wa mafua.Na kadri unavyofilisika zaidi kiroho,ndivyo unavyozidi kushambulia zaidi huduma za wenzio walio serious na wito walio itiwa.Pole acha kujiita mtume,rudi kijijini kalime mchicha kuliko kubaki dar kuibia watu kwa wizi wa kiroho.

 12. UFUNUO 16:14

  “HIZO NDIZO ROHO ZA MASHETANI, ZIFANYAZO ISHARA,ZITOKAZO NA KUWAENDEA WAFALME WA ULIMWENGU WOTE KUWAKUSANYA KWA VITA YA SIKU ILE KUU YA MUNGU MWENYEZI.”

 13. Mtumishi wa Mungu,

  Mimi nafikiri kweli kwa sehemu fulani umechanganyikiwa.
  Kwanza haya mambo ulitakiwa umfuati Mch. Gwajima mwenyewe ukamwambie badala ya kuyasema kwenye vyombo vya habari. Maana kwa kuanya hivi unatangaza uadui juu yake

  Pili wewe mwenyewe umekiri kuwa misukule ipo, lakini ukasema tatizo lako ni pale Gwajima anapohubiri habari za misukele kila siku wakati neno la Mungu ni kama upepo kwamba lazima uvume pande zote.
  Ile tu wewe kukubali kuwa misukule ipo ni ushahidi tosha kuwa leo mtu anaweza akaongea habari za misukule na kesho na kesho kutwa, kwa sababu neno la Mungu halitulazimishi kuwa leo ukiongea habari hii kesho lazima uongee habari nyingine.

  Mbona mimi huona mikutano mingi tu ikifanyika kila siku huwa kuna kuombea wagonjwa? Labda kama ulimaanisha kuwa kila siku wanaombewa watu walewale hilo ni suala jingine.

  Lakini pia si kweli kwamba Gwajima huwa kila siku anafundisha habari za misukule. Kwa mafano mimi nina dvd yake moja ya kama mwezi mmoja umepita haiongelei habari ya misukule, bali inaongelea suala la ‘Ukoo Tata’

  Ila pia jinsi ulivyosema kuwa kama anataka kushughulika na mambo ya misukule aende Haiti, kwamba utamnunulia tiketi na kumlipia hotel miezi sita, mimi naona kama unamdhihaki vile. Na sioni sababu ya kumwambia maneno kama yale wakati ninyi nyote ni watumishi wa Mungu. Haya ni maneno ya kejeli ambayo yanasababishi watumishi wa Mungu muingie kwenye malumbano yasiyo na tija.

  Ukisema kuwa injili anayohubiri Gwajima si injili ya watu kuokolewa mimi sikuelewi, mbona kwenye mikutano yake watu wengi tu wamekuwa wakiokoka, mbona ana kundi kubwa la watu waliookoka?

  Na jambo la mwisho, mimi ningeshauri wewe usimwongelee Gwajima wala kushughulika nae, bali wewe shughulika na kazi amabyo Mungu amekuitia, maana kama wito wako wewe ni wa Mungu na wa Gwajima una uwalakini, basi kazi zenyewe zitadhihirisha hilo!

  Ubarikiwe!

 14. Mtume Augustus,

  Hujachanganyikiwa bali umejichanganya!

  Gwajima ni mtumishi wa Mungu pia, mavuno ni mengi; kuna wanaoipeleka Ngano gharani, na pia wako wanaoyafunga magugu matita matita tayari kwa moto; basi huduma ya misukule ingekudhihirishia jambo hilo, hapo unapoliona kundi kubwa la “misukule fresh” ikishikiliwa kisasa kwa injili za kugombana na wachawi!

  Wewe jaribu kuja na stori za kutisha, jinsi ulivyopelekwa kuzimu halafu ukatoroka, ila uifanye ndefu kidogo labda wiki nne hivi, yaani kila Jumapili; ikifika Jumapili ya nne, jinsi watu walivyoitana waje kuisikia, kutakuwa hakuna hata nafasi ya kusimama huko nje wanavyopigana vibega kuingia ndani!!

  Halafu katikati ya stori hiyo tumbukiza Injili, waambie wasipoacha Uzinzi, ufisadi, kuiba fungu la kumi, usengenyaji, umbea nk, Moto kwao ni hakika kama jua linavyochomoza; waambie wote, kwa matendo yao, wamemsulubisha Yesu Kristo pamoja na wale Wayahudi, watubu dhambi zao, wote wabatizwe kwa Jina la Bwana Yesu Kristo ili wapate Ondoleo la Dhambi zao … mpaka ukimaliza utakuwa umebaki na waimba kwaya tu huko mbele!!!!

  Gbu!

 15. Yawezekana huyo Gwajina ni messeger of devil;sababu injili ya Yesu inazama kwenye TOBA.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s