Pardoned!

The Good News is that the pardon for your sins has already been given. But you need to accept it by faith.

–Mike Walters

Advertisements

One thought on “Pardoned!

 1. Wapendwa,

  Jambo hili ni kweli kabisa, kwamba ” Msamaha wa Dhambi” umetufikia!

  Lakini, Msamaha, hata ukiwa ni wa Dhambi, hauwi Msamaha mpaka hapo unapopokelewa na huyo aliyesamehewa!

  Kwa asiyeupokea Msamaha, hata ukilifungua lango la gereza, ukaliacha wazi, na akawaona wafungwa wengine wakitoka huku wakiushangilia “wokovu” wao walioupokea kwa Neema, si kwa kumaliza kazi za gerezani au kifungo; bado yeye atasimama pembeni akiwapisha wapite, akilifananisha jambo hilo la KUTOKA kwao na mchezo wa kuigiza, na hivyo kuishia kuwacheka saaaaana, maana haamini kwamba mdhambi anaweza kusamehewa; naye atabakia humo gerezani akitumika, na kuingojea kwa hamu siku yake ya kumaliza kifungo, hapo “Kristo atakaporudi”, ili atoke humo akiwa huru kweli kweli na si huu mchezo wa kuigiza, lakini siku anayoingoja ni ya KISASI, masikini naye HAJUI!!!

  Hilo ndilo linalosikitisha, kwamba wengi wetu hatuijui “Nguvu ya Sheria”. Sheria ni sawa na malaika aliyetumwa kazi fulani, Kut 23:20-21 “Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengezea. Jitunzeni mbele yake, mwisikize sauti yake; wala msimtie kasirani; maana, HATAWASAMEHE MAKOSA YENU …” Unaona, hakuna malaika anayeweza kumhesabia Haki yeyote yule, ndiyo hiyo Sheria!

  Ndipo, hata huo Msamaha wa Dhambi, pia unaongozwa na Sheria, na si jambo la kiholela! Kut 21:
  “2Ukimnunua mtumwa wa Kiebrania, atakutumikia muda wa miaka sita; mwaka wa saba atatoka kwako huru bure…. 5Lakini huyo mtumwa akisema waziwazi, Mimi nampenda bwana wangu, na mke wangu na watoto wangu; sitaki mimi kutoka niwe huru; 6ndipo hapo huyo bwana wake atamleta mbele ya Mungu na kumleta mlangoni, au penye mwimo wa mlango; na bwana wake atalitoboa sikio lake kwa uma; ndipo atamtumikia sikuzote.” Hii ndiyo Sheria ya Utumwa, hata ukiwa ni mtumwa wa Dhambi, itawahusu hivyo, bwana na mtumwa wake!

  Nayo Habari Njema anayoitangaza Isaya kwamba siku ya Jubilei yetu yaja, ambayo itatufungua kutoka vifungo vya Dhambi, huko kutengwa kwetu na Mungu, hii ni Habari yenye kutia moyo sana na kulitia Uhai Tumaini lililokufa, ndani yao walio ktk vifungo vya dhambi, licha ya mateso wanayo endelea kuyapata ktk kutumikishwa nje ya maumbile aliyowaumbia Mungu siku ile alipovitazama vyote na kuviona ni vyema! Isaya 61:
  1Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu BWANA amenitia mafuta NIWAHUBIRI WANYENYEKEVU HABARI NJEMA; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao. 2Kutangaza mwaka wa BWANA uliokubaliwa …”

  Mwaka huu uliokubaliwa ndio ule mwaka wa saba ambao unapaswa utoke BURE, ukiisikia tu tarumbeta, ile Injili ya Wokovu (Lk 4:16-22), unatoka zako mbio kwa furaha uwe huru ktk Kristo, hakuna dini inayoweza kukuzuia usitoke ktk Mwaka huo. Nayo dini, unapokataa kutoka, ndiyo inayokupeleka mpaka Mlangoni kwa Kristo ikiwa ni shahidi wa kukataa kwako kuipokea Injili ya Wokovu, ikikunawa lawama kama Pilato alivyomnawa Kristo, kwamba damu yako iko juu yako mwenyewe maana Injili uliisikia!!!

  “19Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa. 20Akakifunga chuo, akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho. 21Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu. 22Wakamshuhudia wote, wakiyastaajabia maneno ya neema yaliyotoka kinywani mwake …”
  Wengi waliisikia Injili na wakaistaajabia Neema waliyokuwa wakitangaziwa, lakini ni wanyenyekevu pekee ndio walioipokea Habari Njema hiyo, hapo ilpowafikia.

  Basi, “Mwaka wa Bwana uliokubaliwa” ndicho hiki kipindi cha Neema, huo Msamaha kwa wote, haijalishi ulikuwa na kosa gani, Dhambi nzito kiasi gani, au ulikufuru kiasi gani ktk upofu uliokuwa nao huko kwenye dini; Ujio wa Neema ni wema wa Mungu unaotufunika sote; 2 Kor 6:2
  “Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia; tazama, wakati uliokubalika ndio sasa; tazama, siku ya wokovu ndiyo sasa.”
  Ndipo, twapaswa tufahamu kwamba kama tumeambiwa “wakati”, huo mwaka, bkwamba hiki si kipindi cha milele, bali ni kipindi ambacho Habari hiyo Njema inahubiriwa, na ndani ya kipindi hicho ndimo ilimo “Siku ya Wokovu wako”. Yaani hiyo Siku utakayoipokea hiyo Injili iliyohubiriwa na mitume, ndiyo “Siku ya Wokovu wako”. Nao Wokovu hupokelewa kupitia Injili hiyo na kudhihirishwa katika Ubatizo uletao Ondoleo la Dhambi (huo wa kwa Jina la Bwana Yesu Kristo, Mdo 2:38), nawe kuwa sawa na chombo kilicho safishwa na kuwekwa tayari kwa kazi!

  Vyombo hivyo vilivyosafiwa, wale “wanyenyekekevu” walioipokea hiyo Injili, ndio hawa hapa tukioneshwa hali zao: Kol 2:13-14
  “Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu, aliwafanya hai pamoja naye, akiisha kutusamehe makosa yote; akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani.”

  Basi ule “Mwaka uliokubaliwa” kwa kadiri unavyoendelea, Injili ikihubiriwa, wengi wakiendelea kuupokea Msamaha huo, wakiingia katika Siku yao ya Wokovu, kama ambavyo wengi wanaudhihaki Msamaha huo, yaani wakikataa kutoka humo ktk magereza ya dini walimofungiwa kwa kanuni na dogma, wakisema “”Tunazipenda, tunabaki humu””, ndipo, hao, kiroho wanaletwa mpaka Mlangoni, nao Mlango ukiwa ndiye Kristo aliyewaita watoke, hapo wanatobolewa masikio yao ya kiroho na HAWATAWEZA kamwe kuisikia Injili tena, watabakia humo wamagerezani wakitumika maisha yao yote, mpaka Mwaka huo utakapofungwa, yaani ile Jubilei, ili kuiruhusu ile “Siku ya Kisasi cha Mungu wetu”, ile iliyo Kuu na ya Kuogofya, kuwafikia humo magerezani; ndio hao wanaousubiri Ujio wa Pili wa Kristo, huo wa Hukumu!!!!

  “Jamani, mbona walisema tutanyakuliwa kwanza kabla ya huu mooooootoooooo!!!!!

  Gbu!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s