Tamaa ya kimwili inanisumbua sana!!

Kneeling

Mimi nimeokoka muda mrefu.. na nimeoa na nina watoto 3. wote wakiume. wa kwanza ana miaka 12 sasa, tatizo linalonisumbua ni kupenda wasichana, roho yakutamani inanisumbua sana, nina mke mzuri, lakini bado tamaa inanitesa yaan mimi kila mwaka ni mtu wakuanguka tu, nikijitaidi kukaa mbele za Mungu vizuri mpaka mimi mwenyewe nahisi kabisa upako wa Mungu ndani, ghafla nimeshasahau natenda dhambi ya uzinzi.

Mke wangu hajui niko nae sasa miaka 12 ya ndoa. Lakini kila mwaka naanguka, ila nikiwa hivyo natembea na msichana mmoja tu, sio wengi mpaka sasa nasikia hata aibu kumshirikisha mtu maana mimi ni mtu tu wakuanguka kila mwaka naomba mnisaidie jamani ninajiona labda mimi sijaitiwa ufalme wa Mungu, kwanini nashindwa kusimama na sasa nimekuwa mtu mzima nina miaka 41, lakin bado sijampendeza Mungu kwa utumishi ninaoufanya wa kupiga mziki kanisani napiga mziki kwenye kanisa la kiroho, jina langu ….

–J

Advertisements

15 thoughts on “Tamaa ya kimwili inanisumbua sana!!

 1. Ashukuliwe Mungu wetu, mwenye utukufu, ufalme na nguvu na hekima na mwenye manabii wa kweli, mwenye kufundisha na kuelewesha na kuchukuliana nasi kwa upole na uvumilivu usio na mwisho. Nakupenda Mungu kwa kuwa ulinipenda tangu mwanzo. Watu tumepitia maudhi na matata mengi tulipapasa na kujitahidi kwa akili kumcha maovu na mabaya yetu, Mungu nasi hatukuweza! Hadi ulipofika wakati wako Mungu wetu, kutuokoa kupitia UJUMBE KATIKA KILE “KITABU KIDOGO” CHA AJABU! Endelea kuwepo nasi Mungu wetu mwema, kwani usipokuwepo Bwana, “NI LAZIMA LAZARO ATAKUFA!” Nasi tutalazimishwa kufanya mambo mengi, sheria na kanuni nyingi na kubebeshwa mzigo mizito zaidi hata kuliko dhambi ambazo tunadhani bado tunazo!

  Nakushukuru Mungu wangu kwa kunigundulisha, ile hazina kuu ndani ya ule ujumbe katika kile kitabu kidogo! Lakini kama ulivyosema mwenyewe kuwa, akilaye “kitamtia utamu kinywani na kisha kitamtia uchungu katika tumbo lake” kwa nini? Ili akitoe na wengine wakile! Sasa Bwana wangapi wamekila? Hakika ni wachache Bwana, lakini natiwa moyo na Neno lako kuwa heri ya lile “Kundi dogo” maana walio wako si wachache! Nashukuru kuwa, HATUKOSA NENO LAKO, MAANA TUNGESIKIA MENGI, MARA ETI KWASABABU YA “ZABIBU MBICHI ALIZOKULA BABA AU MAMA, BABU AU BIBI NDIZO ZILIZO SABABISHA ETI KIWI YA MENO YETU!” Endelee kushukuliwa kwasababu ulikuja kuondoa hisia na kuuweka uhalisia wa mambo, kama ambavyo yalikusudiwa yawe. Najifurahisha nikikumbuka maneno ya Mtumishi wako mmoja, nimpendaye sana, ambaye alisema, “SI KWAMBA MUNGU HUFANYA YASIYOWEZEKANA YAWEZEKANE TU, BALI, HUYAFANYA PIA KUWA HALISI!”

  Wewe ni PENDO ndilo leo unajulikana kuwa ndilo jina lako, kale ulijulikana wewe NIKO AMBAYE NIKO nk. Lakini leo tumekujua kuwa wewe ni PENDO, na kwa jinsi ya jina lako hilo uliupenda ulimwenu. Na ulimwengu ni nani kumbe? Ni PAMOJA NA WALE WALIKUWA KATIKA UZINZI NA UASHERATI, AMBAO TAYARI UMEKWISHA KUWAOKOA INGAWA KWA MACHO YA KIMWILI BADO WANAONEKANA NA KUITWA HAWAJAOKOLEWA, AMA WAO WENYEWE KWA KUTOKUAMINI KWAO WANAJIONA BADO HAWAJAOKOLEWA NAWE! Lakini, wewe ni PENDO, kama lilivyo jina lako hilo, huchunguziki kabisa! Ulinishangaza hapo mwanzo, lakini sasa sishangai tena, baada ya kujua kuwa wewe ni PENDO sishangai kuwa ni kwanini Yule Sauli wa kale ulimwambia, juu ya kosa lake kwako kwa upole na upendo wa ajabu kwa sauti iliyojaa upendo mkuu eti tu kwamba, “….MBONA UNANIUDHI?…”! Hukutaka hata ajitetee, ukamuokoa!

  Ulipomuokoa Sauli, hakuwa “PAULO MTUME” siku hiyohiyo katika macho ya watu, ingawa tayari wewe kiroho ulisha mgeuza kuwa PAULO MTUME, lakini watu waliendelea kwa mda wakimujua kuwa ni “SAULI MUUAJI” wa watumishi wako Bwana! Hata ulipomkabidhi kwa “Wachungaji” wa wakati huo ili atiwe moyo na aonyeshwe cha kufanya, bado alitiliwa mashaka na kuogopwa na kuitwa SAULI MUUAJI!

  Sasa Bwana, nakuomba niendelee kumwambia rafiki na ndugu yetu “J” ambaye watu wanamuona anadhambi huenda tokana na marafiki anaofatana nao, labda ameoa majini, labda Babu na Bibi yake au Baba na Mama yake walikuwa wazinzi na waasherati, labda ni kutokana na kanisani kwake au labda ni kutokana na SINEMA anazopenda kuangalia, ameambiwa pia atoe maelezo kwa uwazi juu ya Historia au Bakigraundi yake binafisi, eti hiyo ndiyo itakuwa nafuu yake na kwamba hiyo ndiyo itakayo kuwa njia safi ya kumponya na tatizo, na hivyo kumufanya AONEKANE kaokoka kikweli! Hivi Bwana, ulimuuliza historia yake Sauli kabla ya Kumuokoa? Na je, Bwana ulimuuliza swali juu ya historia yake Yule Mwanamke mzinzi aliyekuwa ameletwa kwako ili utoa hukumu ya yeye apigwe mawe kwa mjibu wa Torati?

  Nikisoma habari za watu hao, hukukataa kuwa si wenyedhambi, uliwakubali tu na ukatoa maelekezo kwa kila mmoja yaliyompasa kutendewa na kwa mhusika kutenda. Tokana hilo, napata ujasiri kumwambia ndugu yangu “J” kuwa, ajikubali na kuamini tu kuwa ni kwelikweli alishaokolewa, angojee tu kwa Imani wakati wa Bwana, ambao utamkamilisha na kumtambulisha kilichokusudiwa kwake; kama alivyoandaliwa “SAULI MUAJI” na kuwa leo anajulikana kuwa “PAULO MTUME” mpelekaji Injili Duniani! Asijali hata kama ni kweli wazazi wake, mke wake, marafiki zake,kanisa lake na au sinema zake zisiwe kigezo cha kushuka kwa imani yake, kwa sababu wewe unalichunguza Neno lako upate kulitimiza. Ulisema TUJE KWAKO KAMA TULIVYO NA MIZIGO YETU YOTE NAWE UTATUPUMZISHA, pia ulisema SASA ALAYE ZABIBU MBICHI ZITAMTIA GANZI MENO YAKE MWENYEWE! Kwa Neno hilo ambalo unaliheshimu hata kuliko jina lako, kama mtu huyo ni mbegu yako, sinashaka mimi Bwana! Kwa jina la Yesu Kristo Bwana wetu Amina! Kwani,

  “Ufahamu ni chembe ya Uhai!”

 2. AMKA NA UCHUKUE HATUA EWE SHUJAA!!

  Wewe ni shujaa kwasababu umekubali kwenda mbele za Mungu ukiwa uchi ili
  akuvalishe nguo na pia una kiu ya maji yanayoitwa MAARIFA YA NURU ambayo
  yanatolewa na Yesu peke yake.Unaishi ndani ya maangamizi kwa muda mrefu
  kwasababu ya kukosa hayo maarifa(Hosea 4:6).ROHO MTAKATIFU naomba unisaidie hapa,naomba hekima na maarifa yako(1 yohana 2;27).Maarifa haya ni
  UKOMBOZI KWA NAFSI NYINGI ZILIZO KUFA.

  Hongera kwa ujasiri ambao kama ukiutendea haki utakutoa ndani ya kaburi(utumwani).Wewe umekufa kiroho kwasababu nafsi yako ILISHAIBIWA (Isaya 42:18-22).HII NI CHANGAMOTO KWA KILA MTU ALIYE NDANI YA WOKOVU NA WALE AMBAO WAMEKUSUDIWA WOKOVU INGAWA BADO HAWAJAOKOKA.NI CHANGAMOTO YA KIMAUTI KWA WOTE WALIO NDANI YA NDOA(UZINZI) NA AMBAO HAWAJAINGIA NDANI YA NDOA(UASHERATI).Hii ni changamoto ya kiroho yaani kiini na chanzo chake ni katika ULIMWENGU WA ROHO(utawala wa majini mahaba) wala siyo changamoto ya kimwili.Kama ni mwanaume unaweza ukafungishwa ndoa na jini mahaba la kike(spiritual wife) na kama ni wanamke unafungishwa na la kiume(spiritual husband).Tatizo hili linatakiwa kutatuliwa kwa SAIKOLOJIA YA KIROHO na wala siyo SAIKOLOJIA YA KIMWILI.Elimu ya ufalme
  wa mbinguni ndiyo mwalimu,muongozo na uhai wa elimu zote zinazofundishwa
  hapa duniani(1Wakorintho 1:19-25).Tatizo hili limevunja ndoa nyingi za wapendwa
  na kuzuia vijana na mabinti wasioe wala kuolewa.Pia limesababisha vifo vingi kwa
  ugonjwa wa ukimwi.Hii ni kwasababu wapendwa wengi wanatawaliwa na ROHO ZA NGONO ambazo zimedanganya wengi ndani ya makanisa ya mbwamwitu(wajumbe wa shetani) kwa kuongea ndani ya miili ya watu.Wateule huwekewa hizi roho katikati ya ibada hasa wakati wa maombi bila ya wao kujua.Roho hizi ambazo huachiliwa kutoka kwenye madhabahu ni ROHO ZA TAMAA YA KUFANYA NGONO,ROHO ZA VIRUSI VYA UKIMWI,ROHO ZA KUJICHUA n.k.Mungu akinipa
  kibali nitalizungumzia hili suala kwa undani zaidi kwa kadiri ninavyotiririka.Kikubwa amacho huwa kinatafutwa hapa ni maono(huduma),uchumi na ndoa kama tayari ameshaoa au kuolewa.

  Maoni au michango yote ni mizuri kwa kadiri nilivyoipitia.Hata hivyo baadhi ya vipengele ndani ya mchango wa Kiongozi mpakwa mafuta wa Bwana,ndugu MABINZA LS yameugusa moyo wa Mungu aliye hai kwa namna ya kipekee sana
  na hatimaye UMRI WANGU WA KUISHI UMEONGEZEKA GAFLA!Yesu akambuke mpaka kizazi chako cha mwisho hapa duniani.Nimeshaanza kuvigusia hivyo vipengele kwa
  lugha ya kiroho zaidi na Yesu anitie nguvu.

  Namshukuru Mungu sasa naingia ndani ya mada yenyewe.Kwanza kabisa anabidi
  niingie ndani ya viatu vya shujaa wetu aliyeibiwa.Suala la majini au mapepo ya ngono linahitaji Maarifa ya rohoni katika kujua kiini na chanzo cha tatizo la kuanguka katika uzinzi.Hapa ni lazima tufuatilie kwa undani historia ya ukoo wa muhusika,historia yake binafsi pamoja na kujua ndugu na marafiki zake wa kiroho na kimwili.Ni lazima atueleze mambo anayopendelea sana kufanya au kuangalia.
  Ni lazima tujue undani wa mahusiano ndani ya ndoa yake na wakati ambao tatizo lilianza.Ni lazima atuambie ndoto anazoota kama anazikumbuka.Ni lazima tujue kwa undani uhalisia wa kiroho wa kanisa analosali.NI lazima pia tuangalie uhalali wa ndoa yake.Katika mchakato mzima ni lazima itafutwe hekima na mamlaka ili na mke wake ajue kinachoendelea kama alikuwa hajui.Kama mke au mume anamilikiwa na majini mahaba huyo si mke wako au mume wako mpaka utakapomkomboa au atakapokombolewa.Mapepo yanakuwa na uhalali wa maisha yake kwa asilimia mia!Kwa ujumla anakuwa ni mtu ambaye hana maamuzi yake binafsi kwasababu nafsi yake inatumiwa na mapepo ya ngono.NI neema tu ndiyo
  inamlinda katika aibu nyingi zlizokusudiwa katika ulimwengu wa roho kwasababu yeye kama yeye hawezi kujizuia ingawa hapendi kumkosea Mungu(Warumi 7:15,19).Mapepo ya ngono yanakuwa yameshaiba AKILI YAKE-azinie na mwanamke au mwanaume hana akili kabisa.Afanya jambo ambalo litaiangamiza
  nafsi yake.Huu mstari una maana nzito mno katika ulimwengu wa roho kuliko tunavyoweza kuuelewa!

  Kiini siku zote ni mizizi kutoka kwa mababu na wazazi,ni maovu tuliyorithi ambayo Mungu huyapitisha kutoka kizazi hadi kizazi cha waovu au watu ambao waliingia hayo maagano na akuna mtu aliyeingia gharama ya kuyavunja(Kutoka 20:3,5,Maombolezo 5:7).Mungu huwa anarehemu kama ukimuomba kwa dhati ya moyo yaani ukiwa umekusudia kuvunja maagano(ndoa) na hizo roho.Hata hivyo yanahitaji maarifa sahihi na mshauri sahihi katika mchakato mzima wa mtu kuingia
  katika MAOMBI YA REHEMA(Maombolezo 3:22,31-33,Kutoka 20:6).Kimsingi hapa
  shetani huwa na uhalali wa kusimamia madai(sheria) ya maovu aliiyorithi muhusika na dhambi za zinaa au uasherati anazoendelea kufanya.Kwa hiyo kama muhusika akupata maarifa ya kuvunja hayo maagano na kukataa kwa kukiri kwa kinywa chake lazima hizo roho ziendelee kumtumikisha kwa mateso ili AUJENGE UFALME WA SHETANI YEYE NA KIZAZI CHAKE(Ufunuo 12:10).

  Chanzo ni uzinzi ambao anasukumwa kuufanya na majini mahaba.Anapolala na mwanamke au mwanaume anakuwa analala na jini mahaba ambalo liko ndani ya yule mwanamke au mwanaume ambalo lilifunga nae ndoa katika ulimwengu wa roho.Kwahiyo hilo jini mahaba lina kuwa lina mkutanisha na wanaume au wanawake mbalimbali linalowamilliki kisheria.Wateule wengi hawajui kwamba unapofanya ngono na mwanamke au mwanaume ndiyo chanzo cha kuingiwa na majini mahaba.Vyanzo vingine vya kuingiwa na majini mahaba ni kuzini au kufanya uasherati kwa kutamani kwa macho,kuangalia vitabu au mikanda ya ngono,kufanya ngono za kuongea kwenye simu.Mara nyingi wanaotumika kusambaza majini mahaba kupitia ngono ni maanjenti wa kiume na wa kike ndani ya makanisa,majumbani,makazini na kwenye semina,mikutano na matamasha ya nyimbo za injili.Wasichana wanaofanya kazi za ndani pia baadhi yao ni maajenti wa shetani.Ajenti yoyote wa shetani huwa ana akaunti maalum ya kulipwa mshahara.

  NITAENDELEA KWA UNDANI ZAIDI……………

 3. Mpendwa J,
  Mimi nimekuelewa sana tu kwamba tamaa unazozisema za mwili ni kule kuwaka tamaa kingono, mwenyewe unasema zimepita kiasi na hasa inapotokea kutakataka visichana! Msaada unao uomba ni ushauri ili ujue namna utakavyoachana na tatizo hilo, ambalo limekusumbua kwa muda mrefu sasa.

  Kwanza napenda nikutoe wasiwasi kwamba, wewe si wakwanza na kwamba hautakuwa wa mwisho kuvaliwa na haja kama hiyo! Tabia za kushindwa shindwa mambo ni za kibinadamu, ambazo kwakweli zililetwa na shetani baada ya kuwaangusha wazazi wetu pale Bustanini. Lakini habari ya kufurahisha ni kwamba alikuja Mungu mwenyewe ambaye ndiye YESU KRISTO kuulejesha ule utu wetu wa ushindi ambao kwa asili tulioumbiwa kwanza, na hivyo kuutupilia mbali ule itwao “UBINADAMU” wenye kushindwa! Kuingia katika tatizo lolote ni lazima kwanza ufike pahala uelewe kwamba, Binadamu yeyote kama Binadamu hana ujanja wala nguvu au maalifa ama akili ama elimu ama uwezo ama madaraka nk ya kuweza kujiondoa ama kujikinza katika tatizo lolote lile. Watu wengi na hasa wanao ukubali wokovu, hulitazama kwa macho mia swala la uzinzi, matendo ya kingono na pombe kama dhambi kubwa sana, na pia hufikili kwamba mtu akiokoka siku hiyohiyo watu watamuona kaacha vyote vya zamani na kuwa mfano wa malaika! Waumini kama hao hutazamia nguvu “zinazoonekana” kwa macho zitokeze mara moja mtu anapoukili wokovu, ndiyo maana utawaona na kuwasikia wapo kuombewa sala za toba na kutaka matendo ya kimiujiza kila kukicha na kuhama hama majengo yao ya Ibaada, utawasikia mara wapo kwa Kakobe, mara kwa Mwingira mara kwa Mzee wa upako, mara wapo mlima wa Moto, mara wapo ufufuo na uzima, mara wapo katika mito ya Baraka na kadhalika na kadhalika – wakijilisha upepo, wakiendelea kupanda Upepo ili wavune Kimbunga!

  Juweni kwamba, WOKOVU ni Mchakato, hivyo ukishaokoka unapaswa kujiachilia mikononi mwa Mungu mwenyewe, usijilazimishe KUACHA ama kujisumbua ama kujihudhunisha na jambo ama tendo lolote ulilokuwa ukilitenda ama kulifanya ama kuwa nalo kabla ya kuukili wokovu, ukifanya bidii yako kuacha matendo yako ya kale, utakuwa hujajua maana ya wokovu na humjui wala kuzijua nguvu za MWOKOZI huyo unayedai kakuokoa, na kibaya zaidi utakuwa unajisumbua bure maana HAUTAACHA KAMWE, kitakachokuwepo ni kwamba utaacha kwa muda kisha unarudia tena nawe utaombewa tena sala ya toba, mchezo huo utaendelea nao hadi utakapokufa! Wokovu ni NEEMA hivyo kujaribu kujiachisha mwenyewe kitendo ama matendo yoyote mabaya uliyokuwa ukiyafanya kabla ya kuokoka ni KUTEKELEZA SHERIA, na Sheria si NEEMA! Neema ni nguvu isiyotegemea kanuni za kimaumbile, mfano kujizuia kukutana ama kujichanganya na wanawake, kutopita karibu na Baa au Klabu nk, ili itende kazi. Neema hutenda kazi kivyake kabisa huku ikiwa kinyume na kanuni zote za kimaumbile, pale maumbile yanaposema haiwezekani yenyewe ndipo inapoonyesha kuwa inawezekana! Na ili Neema ikupate na itende kazi ni mtu kuwa na IMANI isiyotikisika, maana Neema ni MUUJIZA hai!

  Labda nimalizie kwa kutoa USHAURI kwa mhusika kama yupo “siliazi” kuondokana na hali kinzani aliyonayo, ni kwamba, AWE NA IMANI NA NENO LA MUNGU, AJIACHILIE NA AKOME KUJISUMBUA ILI KUACHANA NA HALI ILE KWA BIDII ZAKE YEYE MWENYEWE! ASITAKE KUJUA NI LINI ATAONDOKANA NA HALI ILE, WALA ASIJISUMBUE NA KUTAKATAKA KUOMBEWAOMBEWA MARA KWA MARA ILI KUONDOKANA NA JAMBO HILO, KWANI MUNGU HUOMBWA MARA MOJA TU NA KULE KUTAMANI KWA NIA YA DHATI YA MTU, HILO NDILO HUWA OMBI TOSHA MAANA MUUNGU HUANGALIA KILICHOMO MOYONI MWA MTU YAANI NIA YA MOYO NDIYO MUNGU HUHANGAIKIA HIYO!

  Mwisho elewa kwamba, Wokovu ni Mchakato (Process) kwa hiyo kinachomtakasa Mtu baada ya kuokoka ni NENO la Mungu. Kama unajijua kweli kuwa umekwisha okolewa, basi usafi na ondoleo la dhambi lilisha fanyika siku nyingi huko nyuma kabla, kinachoendelea ni kutakaswa kwako na Neno! Kwa Mungu hakuna majuto utajikuta umetua mzigo huo bila hata kujitambua na ikawa ni historia tu kwamba zamani nilikuwa hivi ama vile, achana na mawazo kuwa eti ukiokoka ndiyo huwezi mwenyewe kama wewe kuonekana katika mambo na matendo yako ya kale kwa mara moja, inaweza hata kukuchukua muda mwingi tu kabla ya kuongoka!.

  “Ufahamu ni chembe ya uhai!”

 4. Hapo ni afanye maungamo kwanza yatakayohusisha mtumishi wa mungu wa ukweli na mke wake……hiyo ndio itakapokuwa foundation itakayoanza kun’goa mizizi ya dhambi.

 5. Naomba wapendwa tuweze kutofautisha kati ya TAMAA YA MWILI na UZINZI.

  Tuelewe kwamba TAMAA YA MWILI siyo UZINZI na UZINZI siyo lazima iwe tamaa ya Mwili.

  Tunapaswa kuelewa kwamba MWILI una tamaa zake ambazo ni za lazima kabisa. Kwa mfano, mwili hutamani KUVAA NGUO, KULA CHAKULA KIZURI, KUPUMZIKA, KUFURAHI, KUMILIKI NYUMBA NZURI, KUMILIKI GARI ZURI, nk. Hayo yote ni TAMAA ZA MWILI. Tamaa hizo mwanadamu akiwa nazo siyo dhambi. Lakini kuna mtazamo potofu kwamba ukitaja tu TAMAA ZA MWILI wapendwa wengi huelekeza fikra zao kwenye UZINZI.

  Tamaa za mwili inapaswa kutafsiriwa vizuri isiwekwe kwenye kapu la UZINZI bali ijulikane kwamba mambo yote mema ayatamaniyo mwanadam kwa maendeleo yake hapa duniani nayo pia ni tamaa za mwili.

  “UKWELI KUHUSU UZINZI” NI UPI? MBINU ZA KUACHA UZINZI.

  Ukweli ni kwamba “UZINZI” ni matokeo ya fikra HASI zilizojaa kichwani mwa mtu kuhusu tendo hilo. Kisaikolojia unapomwona mwanamke au mwanaume unajenga taswira kichwani kuhusu maungo yake ya uzazi na kuanza kujiuliza pakoje ndani? Fikra hizo zinapokuwa zimejaa kichwani mwako kila mwanamke au mwanaume utakayemwona utatamani kushiriki nye tendo la ngono.

  Tatizo kubwa ni saikolojia yako ilivyojengeka kuhusu faida au hasara za ngono kiroho au kimwili. Kisaikolojia ukiamua kutamka kwa kinywa chako kwamba sasa naachana na ngono nje ya ndoa inawezekana.

  Unachojaza kichwani mwako ndicho utakachofanya kila siku. Hii ndiyo kanuni ya saikolojia ya watu. Hata ukitubu vipi, ukaombewa sana, ukatafuta ushauri saaana, ukafunga na kuomba kama kisaikolojia hujaamua kuachana na utamaduni uliojengeka kichwani mwako, hautaachana na UZINZI.

  Amka na ubadilike, achana na kuwaza UZURI AU UTAMU WA NGONO nje ya mkeo/mumeo. Hata ukimwona mtu amependeza sura sana kimaumbile au kimavazi unatakiwa kisaikolojia ujue kwamba hakuna lolote utakalolipata linalozidi lile unalolipata kwa mwanandoa wako.

  MBINU NYINGINE ni hii hapa: Chukua simu yako ya Mkononi, Pili fungua phone book yako hasa pale unaposave majina ya watu wote. Hatua ya pili anza kufuta (deleate) majina yote ambayo ni ya wanawake au wanaume uliowahi kutembea nao kingono. Futa majina yote. Hata kama kuna namba ulishaikariri kwamba ni namba ya fulani akikupigia simu usiipokee wala kujibu sms yake. Kaa kimywa usiwajibu sms wale wote waliowahi kutembea na wewe. Usipokee simu yake please? DELEATE FUTA KAABISA NAMBA ZOTE ZA WAHUNI KWENYE SIMU YAKO. Usipofuta namba zao utaendelea kufanya UZINZI.

  Mbinu nyingine ni kuhakikisha kwamba watu wote unawafanya kuwa dada zako au kama wewe ni mwanamke uwafanye wanaume wote kuwa kaka zako. Hili ni swala la kisaikolojia zaidi. Ukimfanya mwanamke kuwa dada yako huwezi kufanya naye uzinzi. Hali kadahalika mwanamke ukimtazama mwanamume kama kaka yako hautakubali kulala naye kingono.

 6. Bwana Yesu Asifiwe! unaheri hujaficha dhambi yako mbele ya Mungu na wanadamu. Maana afichae dhambi zake hatafanikiwa bali aziungamae na kuziacha atapata rehema Mithali 28:13 soma tena 2 wak 7:10

  Kiongozi peleka udhaifu wako msalabani mwambie Yesu akusaidie atakupa msaada wa nguvu wa kuushinda uovu huo.

 7. Kumbuka kuwa ukimkosea mtu hutafuti suluhu kwa kumkemea au kumpiga au kuvunja huo ni ukatili ambao Mungu hataki kwakuwa Mungu ndiye anayekulipiza kwa dhambi ya baba zako (Kutoka 20: 1-6) na shetani (roho za uzinzi zimeruhusiwa na Mungu). Usishughulike na aliyetumwa (shetani) ila ila shughulika na aliyetuma (Yesu).

 8. Hakuna dhambi mpya duniani. Wewe unalipizwa na Mungu kwa dhambi walizofanya baba zako ambazo hawakutubia. Ndiyo maana ni lazima utakuwa kila wakati unaota unaona au kufukuzwa na mbwa. Hiyo roho haijali mtu kaokoka ila mtu aliyepatana na Yesu. Hivyo ni vema kuomba rehema mpaka Yesu akujibu kuwa amekurehemu. Kama hutajibiwa (yeye siku zote hujibu ila hatujui majibu yakoje) ujue bado hujasamehewa. Pole ndugu yangu jipe moyo mkuu utashinda kwa njia hiyo tu ya kunyenyekea.

 9. Bwana yesu asifiwe,pole sana ndugu yangu ila cha kufanya inabidi ushughulike na hiyo roho ya uzinzi,unaweza ukawa umeokoka ila kama hujavunja roho ambazo walikuwa nazo mababu zako itakuwa kazi bure cz hizo roho zitakuwa bado zinakufatilia.inabidi uchukue atua yakuchunguza kwenye ukoo qwenu nani alkuwa na tabia hiyo,ukishajua anza kuomba rehema kwa mungu juu ya hiyo roho ya uzinzi kwenye kizazi chenu,ukishamalzax hivyo anza cmaombi ya kuvunja hiyo roho.mungu wetu ni mungu wa rehema akika atakurehemu na atakupa nguvu ya kushinda hiyto roho ya uzinzi.

 10. Shalomu,

  mimi naomba kumshauri ndugu J. kuwa inabidi afanye toba ya kweli kwa wote aliowakosea kwa uzinzi. Aliowakosea ni Mungu pamoja na mke wake ambaye ni muathirika mkubwa wa kitendo anachokifanya.

 11. Hiyo ni matokeo ya pando ambalo limekwishamea na kuota mizizi, ndio unatubu na kujaribu kusimama lakini bado unaanguka, shughulika na hilo pando na mizizi ambayo imekwisha komaa, ukitaka mti usiendelea kukua usijaribu kukata matawi wala shina, ila aharibu mizizi, fukua na kuharibu mizizi, ingia mbele za Mungu kwa toba na mwambie akusaidie kuharibu mizizi ambayo imeota na kumea ndani sana ambayo wewe huwezi kuifikia kwa nguvu zako, hiyo mizizi imejikita ndani hasa

 12. Kuna Jambo moja kubwa la kujua kwamba siku zote mwili hupingana na Roho kwa kuwa mwili ni wa kubaki na Roho ndiyo inayopokea uzima,sasa basi Wagalatia 5:16-26 Usitafute kutimiza tamaa za mwili bali Umruhusu Roho Mtakatifu atawale maisha yako kwani Roho yako ikiwa na nguvu mwili hautakuwa na nguvu na hivyo utaweza kuzishinda tamaa za mwili.
  Waefeso 6:13-18 Inatupa eneo la silaha za kiroho, simama thabiti na utayari wa Injili ya amani ya Bwana wetu Yesu Kristo
  Waefeso 6:10-12 Hatimaye mzidi kuwa HODARI katika Bwana na katika Uweza wa nguvu zake…
  Pia toka enzi za Yohana Mbatizaji hata sasa Ufalme wa Mungu unatekwa na wenye nguvu….kinachopungua kwako ni nguvu za kiroho ambazo ndizo zina uweza wa kuzishinda tamaa za mwili na yule mwovu……Embu jipange upya tathmini kujitoa kwako kwa Bwana , weka mbele uhodari katika mambo ya rohoni ..UTASHINDA !

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s