Si dhambi kuoa wake wawili – Magreth

biblia

Japo wengi watanishangaa lakini hakuna aliyepigwa na mawe kwa kuoa wake wawili katika biblia. Lakini ukificha na kufanya kimada walikupiga mawe hadi kufa. Biblia haisemi kuwa ni dhambi ukioa wake wawili, lakini kimada ni dhambi kwa kuwa unazini.

Mapokeo ya kanisa yanaambia watu ni dhambi kuoa wake wawili na sio kweli.

–Magreth

Advertisements

62 thoughts on “Si dhambi kuoa wake wawili – Magreth

 1. Mh! Tunakoelekea tutaambiwa hakuna dhambi kwa mwanamke kuolewa na wanaume wengi.

 2. Mabinza,

  Naomba unielewe. Nikitumia hisia zangu nitajipanga sawasawa kwa upande wako. Sasa kaka hiyo si tabia yangu. Ninazo hisia lakini najithahidi niyatii maandiko matakatifu. Nina mke mmoja na nimeonyesha umuhimu wa kuwa na mke mmoja, lakini nikisema kuoa wake wengi ni dhambi nitakua nimekufuru. Yaani siwezi daka nafasi ya Mungu ili ni decide pa nafasi yake.

  Kinachonishangaza zaidi kwako ni kuwa unapofanya demonstrations zako unajaribu kuweka pembeni agano la kale wakati unapolirudilia ukinukuu “HAPO MWANZO”. Umesahau kama agano la kale linaanza tangu Mwanzo hadi Malaki?
  Haya yote ukiyatafakari utakuta umekosa andiko kamili na sasa unabahatisha tu.

  Suala ya talaka limezungmuziwa katika Malaki sawa vile katika agano jipya .: “Malaki 2: 16 Maana mimi NAKUCHUKIA KUACHANA, asema Bwana, Mungu wa Israeli; naye aifunikizaye nguo yake kwa udhalimu namchukia, asema Bwana wa majeshi; basi jihadharini roho zenu, msije mkatenda kwa hiana.”
  Wakati Yesu anaposema kupana talaka ilitokana na mioyo migumu ya wanadamu hajasema tofauti na agano la kale. Kwani kuachana ni machukizo tangu agano la kale. Lakini inapofika kwa kuoa wake wengi ( wala siyo kuzini na nwake wengi), agano jipya na la kale haziseme kama ni machukizo.

  Inakuomba kabisa kwenda shuleni kwani kitu kidogo kama possessive adjective kinakutatiza. Kusema “mke wake” siyo kusema imekatazwa kuwa na wake wengi. Hii ina maana mtu asichukuwe mke wa mwengine. Akifanya vile atakuwa amezini.
  Sikiliza: mwalimu akiwaambia wanafunzi “kila mwanafunzi achukuwe kalamu yake”, hajamaanisha kama kuwa na kalamu zaidi ya moja ni kosa. Ina maana kusiwe mwanafunzi wa kusumbua wengine kwa kuikosa kalamu ao wa kuiba kalamu ya mwengine.

  Kuna jambo unalozusha kila mara ya kifungu hiki “kutompendeza Mungu ni tofauti ya kumchukiza”. Niliwaambia kama sitawarahisisha kugeuza mada ili mufiche udhaifu wenu. Ukiyasoma niliyoandika tangu mbele utapata polepole hakikisho ya hicho kifungo.

  Daudi, Suleimani, hawataigwa kwa machukizo waliyo yafanya kama uasherati, uzinzi, uuaji, … lakini wataigwa kwa lolote JEMA, na la KUMPENDEZA MUNGU, pia la UKAMILIFU walilolitenda.

  Mtihani ungali kaka: “hata kama hatutaiga yote ya Daudi, umehakikisha kipindi chote cha maisha ya Daudi, wakati alipokuwa akioa wake, ina maana alikuwa akizini?” Leta jibu, usikwepe.

  Ubarikiwe.

 3. Ziragora,
  Hata Mimi pia nakuona baadhi ya mambo upo sawa, unaposema kuwa, kuoa wake wengi, Agano la kale, haisemi waziwazi kuwa ni dhambi,na pia haitaji kama kunaadhabu katika kuoa wake wengi, lakini sijakukubalia unaposema kuwa yapo makosa ambayo siyo dhambi! Ukiusoma kwa utulivu ule mchango wangu uliopita, nimeeeleza kuwa, yapo mambo yaliyokubaliwa na Mungu mwenyezi kwa sababu za wakati ule, kwa nini? Hilo linabakia kuwa “anajua Baba” na yapo yaliyowekwa ama kufunuliwa kwa ajili yetu kwa wakati huu wa Agano jipya. Biblia inasema kila jambo na wakati wake kwa makusudi ya Mungu. Kwa hiyo, lazima tujue kuwa upo wakati ambapo mawe hukusanywa na upo wakati ambapo mawe hutawanywa, lakini yote hayo ni kwa makusudi ya Mungu!
  Katika kipindi hiki cha Agano jipya, mambo yote yanarejeshwa katika Sheria za Rohoni, kama ambavyo Biblia inavyosema, “Sheria za Bwana zitaandika kaika vibao vya mioyo” Kwa hiyo basi, tukimrejea Bwana Yesu alipokuwa akijibu swala la Taraka, lazima tujue kuwa pale alijibu mambo mawili katika jambo moja. Ni kawaida ya Kristo kujibu kama vile ‘double’ katika swali moja, alifanya hivyo pia alipokuwa akimjibu Yule Tajiri katika kitabu cha Lk. 18:22-24., yule Tajiri alipotaka kujua cha kufanya ili apate kuurithi uzima wa milele. Yesu alimjibu, 1. Kwa kumuuliza kama anazijua Amri, hiyo ilikuwa ni kwa habari ya uzima, maana maandiko yanasema, “shika Amri ukaishi”. Lakini ili mtu aupate uzima wa milele, lazima kwanza aupate ufalme wa Milele na ufalme unapatikana kwa kumfuata Yesu. Ndipo Yesu alipomjibu na hilo kuwa, 2. Lakini katika hilo la ufalme wa Milele (Lk.18:23-24) “Kauze ulicho nacho uwape masikini, kisha njoo unifuate” Mfano huohuo, katika kulijibu swala la Ndoa na Taraka, kwa pamoja alijibu kama ifuatavyo:-
  1. Katika kuwaacha wanawake kwa Taraka alisema, ‘Musa aliruhusu kuwepo na Taraka ni kwa kuwa Mioyo yao ilikuwa migumu’
  2. Katika swala la wake zaidi ya mmoja mimi nalitazama na kuliona kuwa aliliweka wazi tayari, nikipasoma aliposema, “hapo mwanzo haikuwa hivyo, Mungu aliumba Mme na Mke ili wawe mwili mmoja, na kwamba wakiisha kuunganisha hivyo na Mungu, mwanadamu asijekuwatenganisha” na nikajumlisha kuwa, kuoa wake wengi na kutoa taraka ili mtu aoe tena, ni UGUMU wa Moyo wa mhusika!
  Kwa mkutadha huo, Yesu Kristo alikuja ili kuturejesha katika mahusiano yetu na Baba yetu yale mahusiano mema ya kwanza, tusiwe wagumu wa mioyo, “TUWE NA MIOYO YA NYAMA” kama hapo mwanzo, katika makusudi na mapenzi yale yale ya kwanza kwa watoto wake, ambao ni sisi tuliojaliwa kufanyika wana wa Mungu, yaani tuliojaliwa KUYATENDA MAPENZI YAKE, na moja ya mapenzi yake ni kuoa, lakini kuoa huko ni kuoa mke mmoja kama ilivyokuwa imepangwa na yeye Mungu wetu HAPO MWANZO, wakati ambapo baba yetu na mama yetu walipokuwa wangali katika mahusiano mema na Muumba wetu Mungu.

  Na ukamilifu wa mambo yote hayo yaliyokuwa ya Torati yanadhihilishwa wazi wazi na Yesu Kristo kupitia injili na mashahidi wa Injili yenyewe, ndiyo Mitume kama Paulo kwa mataifa. Ambapo, Paulo mwenyewe anasema atakayeifuata Injili ambayo hakuihubiri yeye Paulo, ALAANIWE! Lakini, tukimfuatilia huyu Paulo, tunaona kasema kuwa “……kila mtu na awe na MKE wake……” Katu, hakusema, “…..kila mtu na awe na WAKE zake…..” kwa Sentesi hii, tunaona inazungumzia mke mmoja! Ndiyo maana nikasema kwa sasa, mtu akioa wake wengi atalaaniwa, sasa mtu kwa nini alaniwe kama hakutenda dhambi? Kutokutii maandiko ni dhambi, ndiyo maana najiridhisha kwa kusema kuwa, KWASASA WAKATI AMBAPO INJILI IMEIFUNUA KWELI YA MUNGU, NA INAFANYA KAZI YA KUTURUDISHA “HAPO MWANZO” HAIPO HAJA YA KUANGALIA NA KUSUMBUKIA HILO, So longer Sisi ni Makuhani pamoja na Kristo, na sina ufahamu wa kutosha iwapo katika Makuhani wawe wale wana wa Lawi na labda na wengineo (kama walikuwepo) sijui kwakweli ni yupi aliyekuwa na wake wengi na akaendelea kuwa Kuhani!.

  Kwa maana hiyo hiyo ya Torati na Agano jipya ni kasema, “(Mtu anaye dai kuwa ni ‘Mkristo’ wa Agano jipya) asimuige Daudi au Selemani mfalme (Maana wao walikuwa ‘wakristo’ wa Agano la Kale)” Kwakuwa tunaona tu kuwa, wao waliongeza wake tuuuu, lakini kujua ni nani aliwahamasisha katika hilo, hatujui (Maana Biblia haisemi oeni wake wengi). Heli kwa upande huu wetu, tunaoa Mke mmoja, tumehamasishwa na nani? Na Paulo, “kwa sababu ya Tamaa, oa Mke” Sababu yangu ya pili yakutojilinganisha na Wazee wetu hao, ni sababu inatubidi lazima tupate ni nani aliyewahamasisha na kwa sababu gani kufanya jambo hilo ambalo hata Mungu hakulipanga hivyo! Maana kwa Agano jipya sababu, “kama unatamaa, OA mke”, lakini kwenye Torati sababu, kama unanini uoe wake wengi? Kwakuwa sijaiona ile sababu iliyowaruhusisha waoe wake wengi siioni, basi, nami nanyamza, nafuata huku, ambako, sababu ya kuoa mke imeelezwa! Twendelee kujifunza.

  “Ufahamu ni chembe ya Uhai!”

 4. Wapendwa,

  Ktk mambo ya Mungu HAKUNA lililo gumu, bali sisi huupata ugumu kutokana na walimu wetu, wanazunguka katika bahari na nchi kavu ili kutufanya waongofu; na tukiisha kufanyika, hutukalisha chini kutujaza mambo yao yasiyohusiana na Ufalme wa Mungu waliotuitia, na mwishoni wanatufanya kuwa wana wa jehanum mara mbili zaidi kuliko wao wenyewe, Mt 23:15.

  Hata hili la kuoa wake zaidi ya mmoja, pia liko wazi. Lakini ndio kama tunavyoona, mafundisho ya dini yamezipindisha nia zetu mpaka tumekuwa watu wa mwilini, tumerudishwa kule tulikotolewa kwa kuyakosa Maarifa; ndio unaona tunazungumzia kutaliki wake kama ndio kuoa!

  Mungu ni mwenye Haki, ndio maana anatuonya kwamba Haki yetu isipoizidi ile ya Mafarisayo, HATUTAINGIA! Basi, Haki ya Mungu twafahamu kwamba inapatikana ktk Neno lake ambalo ndiyo hayo Maandiko na si ktk mafundisho ya dini na mafunuo yake!

  Suala la mfalme Daudi kuoa wake wengi limewatatiza wengi kiasi kwamba wapendwa wanajigonga kutoa jibu juu ya hukumu waliyoipitisha kwa mitazamo ya dini zao. Wanasema kuoa wake wengi ni Uzinzi, jambo ambalo si kweli, Uzinzi ni kulala na mke wa mtu, kama alivyofanya Daudi kwa Bath-sheba aliyekuwa mke wa Uria, lakini ndoa ile ilipokoma kwa Uria kufa, Mungu alimruhusu Daudi amuoe mwanamke huyo, basi kagueni iwapo hakuwa na mke, yaani alipomuoa huyo alikuwa anazidisha wake au alikuwa anafanya nini? Tena mtoto aliyezaliwa kutoka huyo mke aliyeongezwa, Mungu anasema akampenda!

  Mambo ya Nyakati 14:3 inayosema, “Tena Daudi akazidi kuoa wake huko Yerusalemu; akazidi Daudi kuzaa wana na binti” sioni ni kwa mlengo gani unaweza kujifikisha ktk kulihukumu hili linaloshudiwa na Roho Mtakatifu ktk usahihi kamili uliojengeka ktk Haki, hapo unapoambiwa “Daudi akazidi KUOA wake”; halafu wewe ukamhukumu kuwa alikuwa anafanya Uzinzi, hivi mnalielewa vizuri mnalolifanya kweli ndg zangu?

  Hata hii Kum17:17, jaribuni kuvua miwani ya dini muisome kwa kituo, “Wala asijizidishie wake, ili moyo wake usikengeuke”; inasema “asijizidishie wake”, nao wake huolewa, kama Mungu alionya kuhusu jambo hili la “kuzidisha wake”, hiyo haimfanyi kuwa Mzinzi anayezidisha hao wake, bali kama onyo linavyosema, wanaweza wakamzidi nguvu wakamkengeusha, naye atahukumiwa kwa kukengeuka na si kwa kuzidisha wake; kama ingekuweko Hukumu ya kuzidisha wake, basi tungaliiona ktk Sheria, lakini HAIPO, kilichopo ni maonyo yanayohusiana na tahadhari ya jambo hilo.

  Suleiman alikuwa na wake kibao, akilifanania kikamilifu hilo onyo kwa sehemu ya kwanza, ile ya kuzidisha wake; akilileta hilo onyo ktk uhalisi wa alivyoliona Mungu; wakamkengeusha! Ukipita taa nyekundu bila ajali shukuru Mungu, ukipigwa mzinga, jutia kutokuheshimu kwako maonyo na uugulie kimya kimya!

  Sasa tunayaongelea hayo kama yalivyokuwa huko ktk kipindi ambacho Mungu aliziweka Sheria ili kuifunua Dhambi. Dhambi imekuwa ikitawala kutoka siku ya Anguko hadi Sheria inapoifunua. Kwahiyo HUWEZI kuijua Dhambi pasipo Sheria, hata likiwa ni suala la kuoa wake wawili. Ukisema kwamba ni Dhambi utakuwa unapingana na Maandiko, hiyo Sheria ambayo haijalifanya jambo hilo kuwa Dhambi, labda ni kutokana na walimu wako hao wasio na ujuzi wa Sheria, wamekuondolea Ufunguo wa Maarifa!

  Basi, ndio kusema kwamba HAKUNA Wokovu bila Sheria! Maana kama unakiri Kuhesabiwa Haki, kwamba umempokea Kristo, iweje basi ukawa hata Dhambi huijui ni nini; ulimpokeaje Kristo wakati hata Sheria iliyoifunua dhambi yako hauijui, uliunga tela?! Au unazungumza tu kwa hisia za uoga bila kujua hata unachokiogopa ni nini kuhusu kuoa wake zaidi ya mmoja, kiasi kwamba mnaoa mke mmoja kwa Sheria ambayo hamuijui hata kuwa ni ya nani, ila kwa uoga mnatii tu, ingawa mnatamani kuoa kamke ka pili, sijui mnaogopa jehanam?!!!

  Unapompokea Kristo, kuna mambo huwa yanafanyika ndani yako, Mungu huibadilisha ile asili, hiyo uliyonayo inayotamani wanawake bila kipimo, yeye
  hukupa asili nyingine yenye kujitosheleza ktk ukamilifu wa kiUngu huo ulioupokea, 2Pet 1:3-4
  “Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe. Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya TAMAA.”

  Basi, Sulemani alipoiendekeza TAMAA ya wanawake, ikamletea hasara, kwani hao wake zake kila mmoja alikuja na roho za kwao, ndipo Sulemani alikuwa na kazi ya kuzitiisha hizo roho zaidi ya 1000, na Maandiko yanasema zilimshinda nguvu, zikamkengeusha. Na hiyo ndio hali ya wote walio na wake zaidi ya mmoja, sehemu kubwa ya maisha yao wanahangaikia kuwamiliki hao wake zao!

  Basi, mfano wa Suleimani na hao wake zake kulingana na lile onyo ktk Kum 17:17, hili latuthibitishia kwamba wanawake hawana tabu, hata ukitaka kuwaoa 2000, wao kwa asili haliwasumbui hilo, kwani kila anayeongezwa hujihesabia kuwa yeye ndiye anayependwa zaidi!

  Basi nalo Kanisa likiwa ni mfano wa mwanamke, ndipo kwa kadiri lilivyo ktk migawanyiko ya kidhebu, ktk hesabu twaweza kusema Kristo ana wake zaidi ya elfu kumi, roho elfu kumi za kidhehebu za kuzimiliki!!! Kama ni mkorogo, basi huu ni zaidi! Hawa ndio wale wanawake tunao wasoma ktk Isaya 4:1 “Na siku hiyo wanawake saba watamshika mtu mume mmoja wakisema, Tutakula chakula chetu, na kuvaa nguo zetu wenyewe, lakini tuitwe tu kwa jina lako; utuondolee aibu yetu.” Kristo si Sulemani, Sulemani yeye aliwakuta tu wanawake duniani wakamzingua, lakini Kristo ndiye aliye muumba mwanamke, anamjua vilivyo na kusudi lake, ndio hilo analoliweka wazi kwamba tangu Mwanzo Haikuwa hivyo! Yaani ktk Amani ya Bwana mke ni mmoja tu, na anatosha kwa mumewe huyo mmoja tu; huko ndiko anakorejeshwa huyo aliyempokea Kristo!

  Basi hilo rundo la wanawake elfu kumi wanaomlilia Kristo, kwamba wao watajihudumia, maana yake ni kwamba wametoka nje ya mzunguko, Kristo anataka mke mmoja tu! Kuna uongo tunaolishwa na walimu wetu eti sote tu “mwili wa Kristo” hizo roho elfu kumi tofauti, yaani mafundisho elfu kumi yanayopingana; basi huo mwili utakuwa ni mahututi, tena unahitaji kuombewa!

  Mwili wa Kristo ni huu hapa, yule Mke wake mmoja, Efe 4:1-6:
  “Kwa hiyo nawasihi, mimi niliye mfungwa katika Bwana, mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa; kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendo; na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani. Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu. Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja. Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote.”

  Vunjeni kuta hizo, muwasikilize mitume walio msingi wa Kanisa, wao ndio wanajua Bwana Arusi anataka Mke wa namna gani; la sivyo bakini ktk mitala, mkijihesabia kuwa na Mume asiyewajua!!!

  Gbu!

 5. Mabinza,

  Ninachokiona kwako, kiwango fulani uko sahihi. Lakini tatizo unalo ni wazo la kuwa kuoa wake wengi inashurtishwa au kama ni tabia takatifu au kuna walimu wanaofundisha kama kuoa mke mmoja ni dhambi. Hapana kaka, sivyo. Neno kubwa ni kujiuliza kama kuoa wake wawili ni dhambi au la. Msomaji wa Biblia anajithahidi kuona mambo ambayo agano jipya linalotueleza kwani ni mapatano tunayo leo na Mungu. Kwa hiyo, Yesu hakusema kama kuoa wake wengi ni dhambi. Alichokisema kama dhambi ni kuachana. Paulo yeye anahisi kwamba ni heri kutooa. Akiendelea kuwavumila wadhaifu kiwango fulani anaruhusu askofu/shemasi kuoa mke mmoja, wengine hakuwakataza. Hivi mtu kusema kama kuoa wake wawili ni dhambi ni vigumu wakati hata agano jipya limenyamaza. Agano la kale linaponyamaza na agano jipya linafanya hivyo hivyo sione kama tutatafuta ukweli mwengine wapi!!!

  Sione hata kama agano jipya limetofautiana na agano la kale kwa hilo jambo kwani ukichunguza anachosema Malaki hutahakikisha kama kuachana na mke ni halali, vivyo hivyo Yesu anasema kama ilitokana na ugumu wa mwanadamu. Lakini ifikapo kuoa wake wawili, agano zote mbili ziko sawasawa.

  Kwa kifupi, mtu asijivunie kuwa yeye alioa mke mmoja kwani hajafikia heri Paulo anayotutakia. Kwa kuwa tunaupenda utakatifu ni heri kuwa bila mke wala utakatifu hutafutiwe katika kuwalaamu walio na wake wengi. Ina maana mimi nampongeza yule asiyeoa, yeye ni heri. Namuona sahihi yule anaeoa mke mmoja, na simlaumu yeye aliye na wake wawili kwani Biblia hainiruhusu. Yeyote atakayefanya vile afahamu kama anajipatia mamlaka inayotazama biblia kuwa haienee.

  Asante.

 6. Siyi,

  Nilikuambia kuwa mbingu si hadithi za vijiwe vya dini ndg yangu, lakini naona umezama sana ktk mapambio ya hivyo vijiwe kaka!! Tazama mapambio unayoniletea, “”Sina mtazamo wa dini wala dhehebu!!
Namwangalia Kristo tu kama kielelezo changu.”” Ungetafuta kujua kwanza Kristo ni nani, ingekusaidia sana kuliko hivi ninavyokuona ukijiridhisha na mapambio yasiyo na tija!

  Kristo ni NENO la Mungu, ndio hiyo Biblia yako bila kuongeza wala kupunguza chochote kile!

  Sasa, hayo mnayoyafanya humo kusanyikoni kwenu, mkiwakusanya wake za mtu huku mume wao mkimfungia huko nje ya ufalme aliwe na simba, mmeyatoa wapi? Ni roho yupi huyo aliyewaongoza ktk hayo, ndiye Roho wa Kristo huyo unayedai kwamba ndiye kielelzo chako? Kwa mawazo yako, au kwa hizo pambio, ndio unaamini mnao Utakatifu wa kumleta Kristo aje awachukue pamoja na hao mashoga na wasagaji na wake zake za watu mliowanyang’anya kutoka kwa waume zao halali??? Kama si ujinga wa dini nini hicho???

  Sodoma ilikuwa kama hivyo nayo, mji mzuri kabisa, lakini ulijaa uasi, nao waliuzoelea mpaka ikawa ni kawaida tu, wakajiaminisha kuwa wako salama, wakimngoja masihi!!!

  Dogo, Mungu hadhihakiwi, usijiunganishe tu na madude usiyoyajua, utapotea nayo hayo ambayo yenyewe ni ya kupotea kwa asili, na udhihirisho ndio huu tunakuonesha, usishupaze shingo!!

  Haya, 1Kor 7:24:
  “Ndugu zangu, kila mtu na akae mbele za Mungu katika hali iyo hiyo aliyoitwa nayo.”

  Jitahidi, Kristo awe kielelezo chako cha kweli!

 7. Mjema, Dickson,

  Mjema,

  -Mimi simtetee Yesu Kristo kwani najua anazo nguvu za kujitetea mwenyewe. Kama wewe unamtetea kiwango utengeneze sheria kwa nafasi yake, ok go ahead ukijua unapoenda. Lakini mimi namfwata nikifahamu kama kile anachosema ndicho kweli kuliko akili zote za binadamu. Sijakuelewa namna unataka chukua mamlaka ya Mungu ukidhani unamtetea. Wakati Yeye Mweyewe hajaweka sheria tayari umeiweka!!!
  Unasema siweki maandiko wakati unapigana nayo kila siku kwa hofu tu ukikwepa kila tunalokutolea!
  Ona jinsi unajibu kwa hofu ukiogopa hata kuweka msitari wote wa biblia ukihofia kushindwa na Neno. Nakupasha kama kamwe hutalishinda Neno la Mungu. Ni halali likushinde kwani ndilo likubwa, wala usijihangaishe kwa bure.
  Si hili ndo unaita jibu ukiliandika kwa hofu kiwango unaogopa kulimaliza? “Kumbukumbu 17: 17 Wala asijizidishie wake, ili moyo wake usikengeuke; wala asifanye fedha zake na dhahabu kuwa nyingi mno.”

  Nafasi yote ulipoandika ulirudilia hapa “Kumbukumbu 17: 17 Wala asijizidishie wake, ili moyo wake usikengeuke…” kiisha ukakwamia kwa neno “usikengeuke”. Kama Kiswahili kimekutatiza, someni katika ERV version: “Deut 17:17 Also the king must not have TOO MANY wives, because that will make him turn away from the Lord. And he must not make himself RICH with silver and gold”

  Mjema, unajibu kwa swali kama mtu anaejifunza kujadili. Unapopewa Neno la Mungu usidhani utalikwepa kwa kuleta lingine kwani Mungu hagawanyiki. Kila ninapojibu mtu ninafwatilia alilolisema. Huna maficho. Biblia yenyewe ilikuswali, kiisha ukatafuta jificha ndani ya hiyo Biblia, ukidhani utafaulu . Wewe mwenyewe ujiswali “kuzijidishia wake=to have too many wives”, umeiona neno KUOA ndani ya huu msitari unaoleta? Ni tofauti sana kuwa na wake na kuoa wake kwani kuna wake wasio wa ndoa ambao wanaitwa masuria au concubines.

  Tunapolizungmuzia jambo la kuoa wewe unatafutisha katika kuwa na wake. Plz isome biblia yako vizuri usiendelee hangaika kwa bure.

  Pia TOO many au wanaozidi ni wangapi? Na kwa nini umeficha hilo jambo la utajiri. Ni utajiri kiwango kipi unaoweza tatiza mfalme ?

  Ona Jinsi Neno la Mungu linasema :

  « 1 Wafame 11 :3 Akawa na wake mia saba binti za kifalme, na masuria mia tatu; nao wakeze wakamgeuza moyo ». Uneiona hiyo idadi? Hii ni sawa ulevi wa kupindukia, ni ulafi mno : Wake 700 !!!! Masuria 300 !!! Unaona unalolijibu Mjema, halifanani na mada inayosema « Si dhambi kuoa wake wawili »

  Kwa hivi nakujulisha kama unajipeleka nje ya mada ndio maana kiukweli huna swali. Kwa hiyo nilikujibu mapema kama SITAKURAHISISHA KUGEUZA MADA.

  -Unaposema tukuonyeshe namna agano jipya linaunga mkono ni kama mwenye kusema kwa nini agano jipya haina kelele ? Kuunga mkono na kutounga mkono ni mtindo wa wanaadamu lakini siyo tabia ya Biblia. Wewe unatakiwa ujiulize je ni wapi agano jipya linasema kama KUOA wake wengi (wasiopungua wawili) ni dhambi ? Kwani hata kama hutasoma lile agano jipya lote, ukiona nafasi linalosema kama KUOA wake wengi ni dhambi leta hilo shairi tukuelewe. Unapolikosa fahamu kama koze yako imeanguka. Lakini wewe, kwa hila, unapolikosa njo unauliza ni wapi linahalalishwa. Hii siyo tabia ya sheria yoyote. Sheria inaweka amri na ina define adhabu ya yeyote atakaevunja ile amri. Lakini sheria hailazimishwe kusema mambo yote yaliyo mema licha ya kuwa kuna yale yanayosemwa ili watu wanao ufahamu wapate msaada kwenye wangelikwamia.
  Kwa mfano, maksudi wenye ufahamu wasihangaishwe na wasio na ufahamu, Biblia imeweka katika agano jipya hii precision ya kwamba “1 Timotheo 3:2 Basi imempasa ASKOFUawe mtu asiyelaumika, MUME WA MKE MMOJA, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha;”.
  Kila mukristo angelilazimishwa kuoa mke mmoja, Biblia ingesema tu “Basi imempasa askofu awe mukristo”, full stop.

  -Kuupindisha ukweli , umepita kiwango kwani wewe ni sins creators, unaweka sheria ambazo Mungu hakuweka.

  -Magreth kutorudi siyo tatizo. Wengi wanaweka mijadala wala hawachangie tena. Jamani, unatafutisha kweli!!! Kushindwa siyo mwisho wa maisha, jitahidi uamue kuutafuta wokovu.

  Wengine kama wa akina Lwembe, unataka wakwambie nini wakiona unakwepa wanayokuambia? Wajibu kiukweli bila kutafuta kugeuza mada utawaona kwani wote wanapenda ukweli ambao nadai pia.

  -Swali linakungoja tu: Kipindi chote Daudi alipokuwa AKIOA wake unamaanisha alikuwa akizini na wake? Jibu bwana, usiendelee hangaika. Una hofu ya nii? Unaposema unahitaji maneno mengine ya Biblia ni mbinu za kuukimbia ukweli. Unaposhindwa moja utaweza mengi?

  Dikson,

  Wewe unataka litengeneza agano jipya lako la waongo? Umefunuliwa na nani kaka? Asiye na haki hujionyesha mwenyewe. Nani amekuambia kama haya ni mafundisho? Kaka, hii ni maonyo ili watu waisome biblia yao kindani kwani wengi wanaisoma kishabik tu hapo wakivutwa na Ibilisi kama jinsi wewe mwenyewe unavyojiona. Nakupa homework: “nenda kasome Makala yangu huko mbele ugunduwe wewe mwenyewe niliyoonyesha kibiblia na kushauria wasomaji. Ugunduwe kwa nini mimi mwenyewe nina mke mmoja, ndipo utafahamu kiini cha hii mada. Tabia ya ushabik, shetani anaipendaga sana kwani anaingilia pale kirahisi. Ukiwa shabik hupati mda wa kutafakari. Hivi, kaka, kaa taratibu, utafakari unayoyasoma kwenye Biblia yako. Katika hiyo jithihada pamoja na kuomba utaona shetani akikimbia hapo akiacha uanja wa nuru kwako. Ninachokukataza kabisa ni kujimwanga wewe wote ndani ya shetani ukijionyesha kuwa mwonaji wa siku za mwisho sawa jinsi ilivyotabiriwa katika ufunuo: “Ufunuo wa Yohana 19:20 Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa wangali hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti;”
  Sasa wewe na Daudi, utuambie ni nani anaye chapa cha mnyama. Dikson uwe mwerevu na uige wasomaji halisi wa Biblia. Usikurupuke tu.

  Kwa wote:

  Ni lazma tufahamu kama jinsi nilivyoandika huko mbele, kuwa bila muke ni vizuri zaidi, lakini kama huwezi vumilia hiyo hali, uoe. Ina maana hata kuoa mke mmoja ni kupungukiwa kiroho kwa kiwango fulani. Hicho kiwango kinastahili askofu na shemasi, wanao wake wengi wamepungukiwa nao kwa kiwango kingine, wao hawaruhusiwe kuwa askofu ama shemasi, inayomaanisha kama hawa wote wa aina tatu hakuna anaetenda dhambi . Watu wanaposema kuna kundi hizo mbili ni kweli: watakaoingia mbinguni na watakaoingia jehanamu. Lakini tunafahamu kwamba huko mbinguni kuna taji tofauti.

  “1 Wakorintho 7:8 Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, Ni heri wakae kama mimi nilivyo.”
  Paulo anaposema ni HERI, ina maana hii ndiyo inatakiwa. Ndo maana hata alieoa mke mmoja hana la kujivunia. Ukipenda uwe hata na kidogo ya kujivunia ni heri ubaki pasipo mke.

  Pia Paulo anasema : « 1 Wakorintho 11:1 Mnifuate mimi kama mimi ninavyomfuata Kristo. »
  “Waefeso 4:1 Kwa hiyo nawasihi, mimi niliye mfungwa
  katika Bwana, mwenende kama inavyoustahili wito wenu
  mlioitiwa;”
  Kulingana na kauli ya Paulo, waliyo wakristo wa kiroho kabisa kabisa kama yeye, ni kubaki pasipo mke, mengine yanatokana tu na udhaifu wa mwanadamu.

  Mwenyezi Mungu awabariki.

 8. Dickson,
  Walau umesema kitu rafiki!! Nimefuatilia vizuri (nilitarajia nikuone unanena kwa lugha) mtiririko wako ulioanza na sala. Hoja nzuri.
  Ubarikiwe na Bwana.
  siy

 9. Ndugu Zangu,

  Si kwamba kila walichokifanya wazee wetu, wale wa zamani kama vile akina Ibrhimu, Daudi, Selemani na wengineo kilikuwa chema tu mbele za Mungu, yapo makosa na hata maovu mengi tu waliyatenda, wao hawakuwa malaika wala si kwamba hawakuwa wanadamu, walikosea na kuharibu na kukiuka mapenzi na amri za Mungu, Biblia inasema hivyo! Hapa sina sababu ya kuorodhesha makosa na maovu yao na namna walivyoyatubia na kusamehewa, nahitaji tu kuzungumzia jambo lililopo mbele yetu, yaani kuoa wake wengi kama si dhambi ama ni dhambi.

  Tunajua kuwa Torati ilikuja kwa mkono wa Musa, ili kuwa kiongozi kwa wana wa Israeli. Na kabla ya Yesu kuja, Neno hili lilikuwa ni kwa ajili ya wayahudi kwanza na si kwa mataifa kwanza! Kama ambavyo Injili iliwapata mataifa kupitia Paulo, vivyo hivyo Torati iliwafikia wayahudi kupita Musa. Na kama ambavyo kuna maelekezo aliyoyatoa Paulo (na wala SI Bwana) ili yawe mwongozo kwa kipindi hiki cha Neema, vivyohivyo yapo Mambo ambayo Musa aliyaelekeza (wala SI Bwana) ili yawe mwongozo kwa kipindi hicho cha Sheria (Torati), mojawapo ya mambo hayo ni hili la kuoa na kuacha na kuoa tena kwa kanuni na misingi ya Talaka! “Musa aliwaruhusu katika talaka tokana na ugumu wa mioyo yao” Yesu alisema.

  Kwa tamko hilo la Bwana Yesu linathibitisha kwamba, jambo hilo la kuacha ama kuoa wanawake wengine halikuwa AGIZO LA BWANA MUNGU, bali lilikuwa AGIZO LA MUSA, kwa hiyo sheria hiyo HAKUITAMKA BWANA MUNGU, ILA ALIITAMKA MUSA, tokana na ugumu wa kushaurika kwa watu hao ambao aliokuwa akiwaongoza. Lakini Bwana alilitakasa jambo hilo kwa wakati huo ili lifae katika uongozi wa Musa kwa watu hao waliokuwa wagumu wa mioyo! Sababu ni moja tu kwamba, Bwana Mungu ni PENDO yeye hupenda watu kwa namna isiyotafasirika, yeye hachunguziki, huyaacha mambo yatumike kwa sababu zake na kwa wakati wake kwa makusudi yake kwani yeye ndiye Mungu. Biblia inasema, yapo mambo wakati Fulani yalionekana ama yalikuwa najisi, lakini Mungu huyatakasa na hivyo hakuna awezaye kuyaita najisi tena!

  Mtu asijaribu hata kidogo kujilinganisha na Daudi ama Selemani katika swala hili la ‘Tamaa’ katika Ndoa, kama Daudi aliongeza wanawake, mwache, yeye alilindwa na kibali cha Musa, lakini sisi katika swala la ‘Tamaa’ hiyo ya ndoa, tunamsikiliza Paulo kwamba, “…kila mtu na awe na MKE” hata kama mke huyo atakuwa ni mpagani, uwe naye tu, kama anakubali. Lakini hata hivyo ni mke ‘mmoja’ na siyo wake ‘wengi’! Kama nilivyotangulia kusema, ukisoma katika 1wakor 7:10 na kuendelea hadi mstari wa 17, utaona jinsi Paulo anavyoagiza, tena kwa makanisa yote kwamba, kama vipi mtu anaweza kuendelea tu kuishi na ‘mpagani’ kama wanakubaliana kuendelea kuwa mke na mme hata baada ya mmoja kuokoka, katika hilo Paulo anasema HILO SI AGIZO LA BWANA, ILA NI LA KWAKE PAULO! Na tena anasisitiza kuwa, iwe hivyo kwa makanisa yote! Sasa, Kwakuwa nawe ni mwana wa Ibrahimu kwa Imani, kwanini basi usimkataze Paulo katika hilo kuwa, Torati ya Bwana ilikataza?! Maana ukisoma katika Agano la kale utaona wazi wazi kuwa, Bwana aliwakataza waisraeli kuoa watu wa “mataifa” (wao walikuwa na Miungu yao – kwa hiyo ni wasiyo amini!) jambo hilo limefafanuliwa vizuri na kwa kirefu katika kitabu cha Wafalme, hasa juu ya kisa cha ndoa za Selemani Mfalme baada ya ‘kuongeza’ kuoa wanawake wa mataifa (wasiyoamini) kinyume na Bwana alivyoagiza katika Torati yake!. Kama huamini waweza kuachana na mkeo wa sasa ama ukamuongezea mke mwingine ili uhakikishe maana ya kwa nini Paulo alisema (wala si Bwana, ila ni mimi naagiza na iwe hivyo kwa makanisa yote) kutowaacha wanawake kwa kigezo kuwa ni mmataifa (yaani asiyeamini) iwapo mwenza huyo anakubali kuwa na wewe!

  Biblia inasema, “kuna wakati mambo ya Mungu, watu tuliyaona kwa sehemu na sasa umefika wakati wa mambo hayo ya Mungu kuyaona kwa ukamilifu wote”! Kwa maoni yangu, mtu asijiridhishe kwa maelezo tu yaliyomo katika Agano la kale pekee bila kwanza kulinganisha na maelekezo ya jambo husika katika Agano jipya. Biblia inasema Agano hilo jipya ndiyo ukamilifu wa Torati. Bado naona na kuamini kuwa kuoa wake wengi si sahihi mbele za Mungu, na hasa kwakuwa mwanzilishi wa jambo hilo hakuwa mcha Mungu na kwakuwa Yesu mwenyewe alisema haukuwa mpango wa Mungu! Mungu aliumba Mme mmoja na Mke mmoja! Watu wanajilinganisha na akina Mzee Ibrahimu, akina Yakobo, akina Gidion, akina Daudi, akina Selemani nk, watu hao wote walikuwa wacha Mungu, lakini Biblia inasema upo wakati wana wa Mungu huyapenda mambo ya wana wa dunia hata kuoana nao! Lakini mara nyingi uzoefu umeonyesha wazi kuwa, ikitokea wana wa Mungu wakijichanganya katika mambo na wana wa dunia, jambo hilo hutokeza chukizo kuu kwa Mungu, na wana hao wa Mungu hulambishwa fimbo za kutosha tu, hadi wanapoifikilia toba!

  “Ufahamu ni chembe ya Uhai!”

 10. Mjema, Dickson,

  Mjema,

  Kufoka kama unavyofanya ni rahisi kwako tu. Lakini Neno la Mungu halifokiwe. Huna suala lolote. Suala linajijulisha lenyewe. Haka ndiko ka suala kako! “Kumbukumbu17: 17 Wala asijizidishie wake, ili moyo wake usikengeuke; wala asifanye fedha zake na dhahabu kuwa nyingi mno”. Mjema, hata hivi wewe ni muoga sana. Unashindwa hata kumaliza msitari wote ukihofia tu kuonekana dhaifu mbele ya Neno la Mungu? Hivi unadhani kuna siku utakapolishinda Neno la uhai? Kama hukuelewa kiswahili hiki ERV version inakuambia hivi: “Deut 17:17 Also the king must not have TOO MANY wives, because that will make him turn away from the lord. And he must not make himself rich with silver and gold.” Hivi umeona hili shauri linasemaje? “Usijizidishie wake=you must not have too many wives”. Pia si hiyo tu, na utajiri mno…. Hebu weka pale tu unapoleta wewe mwenyewe hesabu kamili. Ni wangapi mfalme anapashwa kuwa nao? Na ni mali kiwango kipi aliamriwa? Ndipo usiifanye suala jambo lisilo suala.
  Lakini umeulizwa kama Daudi, kipindi kile chote alikuwa akioa wake au alikuwa akizini? Mbona hujaleta jibu? Unaulizwa mara ya 6.
  Tunayoyasema hapa siyo mzaha, wewe zungmuza na Neno la Mungu, usipige chakacha tu..

  Dickson,

  Naona wewe umejiumbia agano jipya ingine! Unayo shahuku inayopita kiasi! Basi tukuache uendelee kuonyeshwa yanayopinga Neno la Mungu uokolewe kwa kuimba tu kama unaenenda na Kristo! Pole sana!!!

  Kwa wote, telemsheni Neno la Mungu jamani; hatuyataki maneno yenu wenyewe. Hakuna unabii unaokubalika ukipinga Biblia.

  Bwana Yesu awawezeshe.

 11. Ziragora,

  Narudia tena, usinishambulie mimi, Shambulia Hoja na Maswali niliyokupa kwny post zangu nilizotuma siku kadhaa zilizopita!

  Wewe ndiye uliyekurukupa! Hebu ona, mwanzisha mada mwenyewe,dada ,Magreth tangu mada ianze hajasema lolote,yupo kimya!! Hakuungi mkono ht wewe mdandiaji. Uenda siku akichangia,utajikuta upo mwenyewe huko mi$ri,maana elimu iliyotelewa hapa sio ya kitoto. Na hao kina Lwembe na Mr. Milinga na wenyewe wana beep beep tu. Rafiki kubali kushindwa na Neno la Mungu,Sio Mjema.

  Umesema,mimi nachangia mada km mtoto, asante, Ni kweli kabisa maana hata Yesu ametoa wito tuongoke na kuwa km watoto wadogo,maana walio mfano wa hao ufalme wa Mungu ni wao!

  Halafu kaka, sijui umeoteshwa au umetabirishwa,hv unashindwa hata kujiuliza, Mbona Agano Jipya hakuna aya hata moja inayounga mkono?!

  Kwa kweli haya ni mafundisho ya kishetani yaliyotabiriwa. Hafadhali umeweka wazi kuwe wewe upo miongoni mwa “wasioamini” kama ulivyosema,kuna Neno la Mungu, Usilounga mkono. ole wako.!

  Ziragora, Wito wangu, ukiacha kujibu hoja na maswali niliyokupa post za Nyuma,Nitaendelea kujua kwamba, Ukweli Umeshinda.Giza limefukuzwa na Nuru imetawala.! Halleluya, hata dada Magreth ameshajua hilo.!

  Karibu Mjoli.

 12. Hii ni sauti ya Mungu aliye hai.Huu ni ujumbe wa Yesu kwa watu wake katika nyakati hizi za hatari.Huu siyo mtazamo kutoka kwangu ni NENO LA KRISTO linaloishi milele.Hii ni hasira ya moto wa Yesu.Kuzimu haiwezi tena kuvumilia haya maarifa yaliyo hai.Mbwamwitu hawana tena namna ya kuendelea kujificha ndani ya kivuli cha neno la KRISTO.MOTO WA YESU UNAENDELEA KUTEKETEZA HILA NA MAFUNDISHO YOTE YA MASHETANI na Roho Mtakatifu anaufanya USO WANGU UTOE TABASAMU LA UNYENYEKEVU(LUKA 12:49).

  Ni lazima wanyenyekevu wanaoipaigania imani ya Yesu wajue kutofautisha kati ya MAFUNDISHO YA MASHETANI(WAKOLOSAI 2:18,1 TIMOTHEO 4:1) na MAFUNDISHO YA WANA WA MUNGU(WAFILIPI 2:3-4).Mafundisho ya wana wa Mungu yanaitwa MAFUNDISHO YA ROHO MTAKATIFU(1 YOHANA 2:20,27).MAFUNDISHO YA KUOA MKE ZAIDI YA MMOJA NDANI YA AGANO LILILO BORA ZAIDI(AGANO JIPYA) NI MAFUNDISHO YA MASHETANI(2 WAKORINTHO 3:6-16,MATHAYO 19:4-5,MARKO 10:6).Mashetani ni wajumbe wa shetani au watumishi wa shetani ambao wamo miongoni mwetu na wanatenda kazi kwa siri kama walivyo jiingiza kwa siri ili KUHARIBU KARAMU ZETU ZA UNYENYEKEVU(upendo)(YUDA 1:3-4,12-13).Lengo lao hapa ni kuvuruga uhalisia wa ndoa ambayo Mungu aliisimamisha ili KUMILIKI NA KUTAWALA DUNIANI.Mungu aliamua kuyaficha maarifa ya yake ndani ya ndoa za wateule wake.Shetani aliigundua hilo ndoa maana alihakikisha anaiacha UCHI ndoa ya ADAM na mkewe(MWANZO 3:1-12).Kuna tofauti ya ndoa za WENYE HAKI na WASIO HAKI.MWANA WA MUNGU USIJIFANANISHE WALA KUWAIGA WATU WASIO HAKI AMBAO HATA KABLA YA KUZALIWA WALISHAFUNDISHWA UONGO!(ZABURI 58:3).

  ANGALIZO LA UNYENEKEVU-Ni vema sana kutembelea BLOG ZA INJILI katika kujifunza NENO la Mungu na changamoto mbalimbali za wokovu.NI MUHIMU SANA ILI TUKUE KIROHO LAKINI NI LAZIMA TUWE NA MACHO SABA YA MUNGU TUNAPOTEMBELEA NDANI YA BLOG ZA MBWAMWITU AU TUNAPOSOMA MITAZAMO YA WAJUMBE WA SHETANI NDANI YA HIZI BLOG.KUNA BLOG ZA WANA WA MUNGU ALIYE HAI NA BLOG ZA MASHETANI.WENGINE SIYO MBWAMWITU ILA BADO HAWAJAIJUA KWELI.ZOTE LAZIMA ZIWEPO ILI TUKUE NA TUKOMAE(WAFILIPI 1:17-18) LAKINI NI LAZIMA TUTAFUTE KUWA NA HEKIMA YA ROHO MTAKATIFU.kipimo cha kutambua na kutofautisha kwa jinsi ya rohoni kati ya mbwamwitu na wana wa Mungu ni UNYENYEKEVU WA YESU.

  AMANI KWA WOTE AMBAO MUNGU AMEWARIDHIA.

 13. Ziragora,

  Rafiki, naona koments zako hapo juu ni lawama tu,hujajibu hoja wala maswali yetu kwny post zetu hapo juu,mara ooh, msikurupuke,ooh ninyi mnakwepa,ooh…sio dhambi,ooh..Daudi ame..’ tena umejibu maneno makavu yasiyo hata na aya ya andiko! hii ni ishara kuwa umeishiwa km sio kufilisika.pole sana.Halafu ujue hakuna anae tafuta umaarufu hapa,bali tunamtetea Yesu.

  pia,Hakuna anayepindisha au kukwepesha ukweli kwa upande wetu! Iyo inahusikana na wewe hasa!

  Umeng’ang’ania 1 Mambo ya Nyakati 14:3.hadi umepofuka.inaonekana upo moyoni mwako,una tamaa ya wanawake,km wafalme wa zamani,Daudi na suleiman.! Pole sana.

  Hakuna aliyekwepa 1 Mambo ya Nyakati 14:3. Nimekujibu vizuri tu,ukitaka biblia ijieleze soma rejea yake yaani Kumb17:17-“wala usijiongezee wake,wasije wakakukengeusha moyo wako.

  Kama,upo makini wakati wewe unangangnia 1 Mambo ya Nyakati 14:3, inayosema tu Daudi alifanya nini, wala hawakuagizwa na Mungu, Kumb17:17, nia agizo hasa toka kwa Mungu ambalo ni kinyume hasa na kitendao icho.

  Ziragora, moja ya sababu Mungu anayokataa kuoa wake weng ni kwa kuwa “watakukengeusha moyo” sasa wewe unafikiri kinachokengeusha moyo ni dhambi au sio dhambi.

  Unafikiri kati yetu sisi na nyie, ni nani anayepindisha ukweli!?

  . Ziragora, hamna sababu yeyote ya kimaandiko iliyomruhusu Daudi wala suleiman,kuoa wake wengi, wote walioa kwa tamaa zao na “UMWILI “tu ndio ulikuwa umewajaa!

  Hata,Mr. Milinga anaekuunga mkono kwny koments zake hapo juu,amedhihirisha kile ninyi mnaotaka ndoa za mitara. Amese ,ooh sijui,wanaume wana mbegu nyng vs wanawake,ooh mwanamka akijifungua ..sijui… Nini. “Umwili” mtupu. Pokeni. Mkasahau Wakristo wameitwa ili kujikana nafsi,kuifisha miili,kuiweza miili yetu!

  Naona mpo karibu kuanzisha dini\dhehebu jipya la kikristo-linaloruhusu ndoa za mitara! Ole wenu. Kwani hiki mnachofundisha Yesu wa Mitume hajawahi kukemea au kusemea haya mnayoita mapokeo! Ole wenu, wakati huu niwa mwisho badala ya kuwahamasisha watu waache dhambi mnawafundisha watu kufanya watu wakengeuke mioyo washindwe kumlaki kristo! Ole wenu!

  Ziragora, nimejibu hoja zako za msingi, Naomba nawe ujibu hoja na maswali yangu kwny post zangu hapo juu.Jibu tafadhali utafaidika sana na usieanye moyo wako mgumu. Sio ,Mjema,Siyi au Mabinza,anayetafuta kushinda,bali ukweli ndio utaoshinda!

  Sambamba na kujibu maswali yangu kwny post za nyuma,naomba ni jibu na hili.

  Karibu mjoli!

 14. Mjema,

  Pia wewe unajadili kama mtoto mdogo. Biblia kama kitabu cha sheria/neno la Mungu haijumuike na kuambia watu kinachoungwa mkono. Kinachoungwa mkono= Biblia yote – kisichoungwa mkono. Wakati wowote kuoa wake wengi haitajwe kama dhambi wala haionekane hata kwa sehemu kama uzinzi, ina maana yaiko miongoni mwa matendo yasiyoungwa mkono. Sasa inabaki ilko, yaani katika yale yanayobaki, ndio yale yanayoungwa mkono.

 15. Mjema,

  Unaposema”Wapendwa,msiifanye hii mada kuwa ngumu,mbona ipo rahisi”, unamaanisha hili jambo ni mchezo tu? Mbona hili jambo linakutosha jasho !!! Wewe sema kama makala hii ni rahisi kwa wale wanaoshikilia Neno la Mungu ipasavyo. Lakini kwako ni giza. Ndipo sasa unajifariji kama katika giza unayoishi mambo yote ni rahisi kama jinsi unakwepa kirahisi Neno la Mungu. Ukiweza tafakari Neno ulilopewa na kurudi kwenye nuru ndipo useme kama ni rahisi, sivyo urahisi unaousema ni kama mlevi anavyolewa kirahisi. Ao unapenda utuambie tukuhurumie tukuache uendelee zama ndani maanguko! Huruma kama hiyo hupati. Njoo uokolewe!

 16. Nitakachofanya ni hiki;
  Hakuna aya hata moja ndani ya Biblia inayosema kuwa, tunapaswa kuendelea kuishi maisha yaleyale hata baada ya injili kutufikia!! Kama wewe una hiyo aya, ilete nijifunze kwako!!
  Pili, Kama Daudi alizidikuoa na kuongezeka, unataka kusema kuwa Biblia ina visa vya mambo mema peke yake? Unafikiri, kama ni kweli, tungeijuaje dhambi?
  Sina mtazamo wa dini wala dhehebu!!
  Namwangalia Kristo tu kama kielelezo changu.
  Nakusubiri nione hizo aya!!
  Siyi

 17. Siyi, Mabinza, Mjema,

  Suala tunalolizungmuzia hapa silo suala la undugu, ujirani, urafiki, mitazamo, dini, wala demosntrations za akili za binaadamu kama jinsi munavyodhani. Hivi hamuoni ayibu kukurupukia tu maneno ambayo haina msinji wa Neno la Mungu?
  Mmepewa Neno lililo hai mara nyingi, ndugu Lwembe ameinukuu tena, lakini mnashindwa tu kulitafakari ila mnalikwepa tu. Ni upi huo ukweli wa kukwepa Neno la Mungu? Wakati wowote mnapokwepa Neno la uhai hamuoni kama munaangamia?
  Kimsingi mnapigana na Neno la Mungu, wala mimi siwezi lia kwani sina tatizo lolote. Hata hivi mnayo shahuka kwelli ya kishetani ya kutafuta watu wengine waangamie pamoja nanyi! Alie dhaifu pengine mtampata, lakini jueni ya kuwa ni vigumu kwneu kulipiganisha Neno la Mungu, ndio maana mnapojaribu andika mnaandika tu mkikwepa Neno hilo la Mungu. Kwa nini tangu makala yangu ya 17/09/2014 haadi leo mnashindana na Neno la Mungu hili“1 Mambo ya Nyakati 14:3 Tena Daudi akazidi kuoa wake huko Yerusalemu; akazidi Daudi kuzaa wana na binti.” bila kujibu hata herufi ndogo? Inawarudilia mara 5 ; hebu jitahidini muonyeshe kama Daudi, kipindi chote cha maisha yake alikuwa akizini na wake ili tuone umaarufu wenu!!! Msidhani hapa ni nafasi ya mizaha, ni mbele za Mungu. Kwa hiyo, kinachotumika ni Neno la Mungu tu. Litelemsheni wala msijifanye kuwa waandishi na wabishi wasio na lengo ya kibiblia.

  Mungu awatembelee.

 18. Siyi, Mabinza, Mjema,

  Suala tunalolizungmuzia hani siyo suala la undugu, ujirani, urafiki, mitazamo, dini, wala demosntrations za akili za binaadamu kama jinsi munavyodhani. Hivi hamuoni ayibu kukurupukia tu maneno ambayo haina msinji wa Neno la Mungu?
  Mmepewa Neno lililo hai mara nyingi, ndugu Lwembe ameinukuu tena, lakini mnashindwa tu kulitafakari ila mnalikwepa tu. Ni upi huo ukweli wa kukwepa Neno la Mungu? Wakati wowote mnapokwepa Neno la uhai hamuoni kama munaangamia?
  Kimsingi mnapigana na Neno la Mungu, wala mimi siwezi lia kwani sina tatizo lolote. Hata hivi mnayo shahuka kwelli ya kishetani ya kutafuta watu wengine waangamie pamoja nanyi! Alie dhaifu pengine mtampata, lakini jueni ya kuwa ni vigumu kwneu kulipiganisha Neno la Mungu, ndio maana mnapojaribu andika mnaandika tu mkikwepa Neno hilo la Mungu. Kwa nini tangu makala yangu ya 17/09/2014 haadi leo mnashindana na Neno la Mungu hili“1 Mambo ya Nyakati 14:3 Tena Daudi akazidi kuoa wake huko Yerusalemu; akazidi Daudi kuzaa wana na binti.” bila kujibu hata herufi ndogo? Inawarudilia mara 5 ; hebu jitahidini muonyeshe kama Daudi, kipindi chote cha maisha yake alikuwa akizini na wake ili tuone umaarufu wenu!!! Msidhani hapa ni nafasi ya mizaha, ni mbele za Mungu. Kwa hiyo, kinachotumika ni Neno la Mungu tu. Litelemsheni wala msijifanye kuwa waandishi na wabishi wasio na lengo ya kibiblia.

  Mungu awatembelee.

 19. ziragora & Ck Lwembe,

  Poleni ndugu zangu, naona mpo karibu sana kuanzisha Ukristo Mpya ambao hata Yesu hajawaikuusapoti.!

  Hoja yenu ya msingi ni ktk 1Nyak14:3-“Tena Daudi akazidi kuoa wake huko Yerusalem…”

  Ndug zangu, wala msitumie hii aya 1 kujipa ruksa kuoa wake wengi, aya yenyewe inajieleza tu km ifuatavyo,

  MaJibu:

  1. tazama rejea za aya iyo, ambayo ni Kumb17:14-17- hasa aya ya 17 inasema “….Wala asijizidishie wake, ili moyo wake usikengeuke,…”.

  Haya sasa,mnachong’ang”ania ni nini hapo? Aya ipo wazi na ndo maana hatukuona muda wa kupeza kujadili hapo.

  Wapenda, yapo mambo mengi tu ambayo ” “Basi zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hazioni, bali sasa anawaagiza wa kila mahali watubu” Mdo17:30.

  Mfano:Baada ya Adam kuzaa watoto ME na KE- bila shaka kina Seth na Kaini walioa dada zao. Sasa jiulize, je Kwa Mungu kutowaadhibu basi iwe kigezo kwetu kuoa dada zetu?tafakari.

  2.Watu wote “zamani zile za Ujinga” waliooa wake 2+ waliishia Kwny Majanga kama sio Masikitiko, rejea,wazee hawa,Ibrahim, Daudi na Suleimani!

  Ushaidi:

  Suleimani ingawa alikuwa na wake 700 na masuria 300,kupitia uzoefu wake anatushauri hvi,

  1.katika kitabu cha Wimbo Ulio Bora, ni shairi la Mapenzi kwa Mke wake1 tu na sio Wakeze 1,000. soma ,Wim sura 1-8,uöne anamsifia mkeau wake! “…mahali fulani amesema, kati ya elfu 10 umewapita wote.”huyu mnayemtumia km rejea yenu kujitetea anawakana.Tafakarini rafiki!

  2.ushauri wa pili. kitabu cha Mhubiri. Anasema “Yote ni Ubatili”,ikiwemo kujitwalia wake wengi kwani iyo ni anasa na tamaa za mwili tu zinazo washawishi kujiolea wake wengi.

  Wapendwa,msiifanye hii mada kuwa ngumu,mbona ipo rahisi.

  Nanyi jibuni maswali yangu kwny michango yangu hapo juu.

  Swali:Ni wapi kwnye Agano Jipya dhana ya kuoa wake 2+ inaungwa mkono?

  Karibuni.

 20. Siyi,

  Suala la dunia ya dini kuchomwa moto si geni na wala halihitaji kujitoa akili kama unavyofanya!

  Iwapo kusanyiko lenu limewachukua wake za mtu, aliowaoa kihalali, likawaingiza ndani huku likimfungia nje huyo mume, je, si Uzinzi wa kiroho huo?

  Maandiko yamesema kila mtu na akae kama Injili ilivyomkuta, kama una wake mia, sawa, ila huwezi kuwa Shemasi nk; sasa ninyi mnawatengaje mtu na wake zake kama sio uhuni?!! Kuna wahuni watakaouona Ufalme wa Mungu???

  Halafu ndani ya kusanyiko hilo wamo mashoga na wasagaji kwa kisingizio kwamba “eti mnawarekebisha”; huku Maandiko yakitamka wazi kwamba wasiwepo watu wa jinsi hiyo kati yenu, nanyi mwajua fika kwamba Neno la Mungu ni Amri, je, hilo ni nini Kama si UASI?!!

  Dogo changamsha akili hiyo, mbingu si hadithi za vijiwe vya dini!!!

  Halafu mmekazana zambi, zambi; jibuni basi kuhusu Daudi, alikuwa anafanya zambi kila anapoongeza mke, kwamba alikuwa ANAZINI kama mnavyo ng’ang’ana, au ni vipi?? Nakunukulia tena Andiko mlilopewa:
  1 Mambo ya Nyakati 14:3 “Tena Daudi akazidi kuoa wake huko Yerusalemu; akazidi Daudi kuzaa wana na binti.”

  Haya, jirushe mwenyewe kwenye moto wa gesi kwa kung’ang’ania mafundisho yasiyoeleweka, au kimbia upesi kama fahamu zimekurudia!!!

  Nakutazama utakachofanya,

  Bwana na akupe ujasiri!

 21. Part IV,

  ..inaendelea…

  Kwa wale wanaosapoti kuoa wake wengi,

  Sababu za kuoa mke 1 vs wake 2+

  Baada ya kuwapitisha kwenye sehemu I-III hapo juu, napenda pande mbili zinazovutana kuoa mke1 vs wake 2+ kutoa sababu za kimaandiko kutetea hoja zao.

  Sababu za kimaandiko kusapoti monogame vs polygame hz hapa.

  1.Ndivyo ilivyokuwa Tangu mwanzo.Tamko la Mungu . Mwanz 2:24, Tamko la Yesu,Math19:5.Tamko la Paulo,kuwa “ila kwa sababu ya tamaa kila mme na awe na mke wake mwenyewe”.

  2.Mtu wa kwanza kuoa wake wengi ni mpagani Mwanz4:16-19.hvyo wana wa Mungu wamefanya tu kuiga. Mwaz6.

  3.”Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili, kwa maana atamchukia huyu na kumpenda huyu ama atashikamana na huyu na kumdharau huyu…” Mwanzo 6:24.

  4.Zingati: Kutokupigwa mawe kwa waliooa wake wengi sio sababu kwetu leo kujitwalia wake wengi.Hata Yesu alikemea hukumu iyo ili kuwa niya kibinadamu. Kwani “Zamani za Ujinga Mungu alijifanya hazioni…” Mfano:Mfalme Suleiman alikuwa na masuria 700 jambo ambalo si halali kuwa na mahawara hata leo ila hakupigwa mawe.!je hii ni sababu kuoa wengi.tafakari!

  Mwisho : Naomba mjibu maswali yafuatayo:

  1.Ni zipi sababu za kimaandiko kuoa wake wengi.?

  2.Waislam hudai idadi halisi ya wake wanao ruhusiwa kuoa ni 4 tu zaidi ya hapo ni dhambi-hii ni kwa mujibu wa quran na hadith yao!. Je,ninyi mnaotetea ndoa za wake 2+ kwa wakristo, Biblia inasema ni idadi gani ya wake iliyosahihi kuoa ili isiwe dhambi?

  3.Inawezekanaje, mwanamume 1 kutokuwa na upendeleo kwa wake wengi ili isiwe dhambi AU wake weng walioolewa kutokuwa na wivu kati yao ili isiwe dhambi?

  Karibuni.

 22. ZIRAGORA,
  Aaaaa, Ziragora, usilie Jirani yangu huonewi na mtu yeyote hapa, wewe ni jirani yangu kwa mjibu wa Neno la Mungu, wewe si ndugu yangu kwa sababu huna imani ninayoiamini mimi. Jukumu langu kama Jirani mwema kwako ni KUKUCHUKUA HADI NYUMBA YA WAGENI ILI NIKUFIKISHE , NA KUMUOMBA DAKTARI (YESU, AMBAYE TANGU MWANZO YEYE NDIYE NENO…..NA HUYO NENO NDIYE MUNGU) AKUGANGE MAJERAHA YAKO ULIYOPATISHWA NA MNYANG’ANYI (SHETANI), UTIBIWE KWA GHARAMA ZOZOTE, KWANI TAYARI ZIMEKWISHA KULIPWA,………LAKINI WEWE HUTAKI! BASI, BAKI NA MAJERAHA YAKO, UKIOZA UTAJIJUA, MAANA UNAPEWA DAWA YA VIDONDA WEWE UNATAKA YA MAFUA, KWA MAELEZO YAKO KUWA, “ DAWA NI DAWA HATA KAMA UNAMAJERAHA UNAWEZA TIBIWA KWA DAWA YA KUTIBU MAFUA”!

  Wewe fikilia tu kwa urahisi wa kawaida, inawezekanaje, mwanao ukamwambia kwamba, “Unachokifanya sikipendi, sipendezwi na matendo yako mwanangu!” ukaishia hapo, lakini baada maelekezo hayo kwa mwanao, ukamuona kwa macho yako na kumsikia mwanao huyo kwa masikio yako mwenyewe, akitenda na akiwaambia watu kuwa, “MIMI NAFANYA HAYA NIYAFANYAYO, SINA KOSA KWA BABA YANGU KWAKUWA ALINIAMBIA TU KWAMBA, MAMBO HAYA NINAYOYAFANYA HAYAMPENDEZI KABISA, LAKINI HAKUNITAMKIA WAZIWAZI KUWA NI MAKOSA KUYAFANYA!” wewe kwa ufahamu na akili yako, utajuaje, mwanao huyo anakuelewa mafundisho yako?! Swali la pili, Je, utawaelekeza na kuwataka wale Watoto wako wadogo waliobaki nyumbani mwako, waende wakafundishwe na mwanao huyo, kwa maelezo kuwa ni mwelewa na ni mtii kwako sana?

  Ki msingi shetani kazi yake ni kuwafanya watu wawe ‘Mbulura’ yaani wajinga wa Neno la Mungu!

  “Ufahamu ni chembe ya Uhai!”

 23. Ziragora,
  Mjema na Mabinza wamekueleza mambo makubwa sana. Sijui wapi huelewi!! Nadhani haya ndiyo mambo (ya kuoa wake wengi) tunayoyashikilia tukidhani tuko sahihi kumbe yanatuweka mbali na Mungu.

  Ibrahimu hakuamini kuwa Sodoma na Gomora, zingekosa hata wenye haki 50 tu!! Kulikuwa na wachaji Mungu wengi kama ilivyo leo!! Majibu ya Mungu kwa Ibrahimu, yalimthibitishia Ibrahimu kuwa, kuna makundi mawili tu duniani. Wenye haki na Wasio haki. Mawili tu!! Wenye haki, daima huwa ni wachache sana, sana!! Ukiangalia sensa ya miji ya Sodoma na Gomora, huwezi kuamini kwa haraka kuwa, haikuwa na wenye haki hata watano tu!! Hawakuwepo!! Watano tu!! Pamoja na kuwepo kwa waumini wengi (waliookoka kama wanavyojiita leo), Mungu aliwaweka kwenye kundi la wasio haki. Moto ulipokuja, uliwalamba wote!!
  Ndivyo ilivyo leo, watu wamefuata njia ileile ya uasi wa Sodoma na Gomora!! Wanakula kila kitu, wanaoa bila kuangalia jinsia tena kwa idadi watakayo, huku wakiitumia kauli ya Mungu visivyo. Wamejipa matumaini kwa kupaka chokaa isiyokorogwa vyema kwenye mioyo yao. Kila mtu amekuwa nabii akitoa ubatili ufishao. Kila mtu anatumia neno la Mungu kuhalalisha matakwa yake. Ibilisi yuko kazini kuhakikisha kuwa anakufa na wengi. “Na manabii wake wamewapakia chokaa isiyokorogwa vema, wakiona ubatili, na kuwatabiria maneno ya uongo, wakisema, Bwana MUNGU asema hivi; iwapo Bwana hakusema neno” -Ezekieli 22:28.

  Kiashiria kikuu cha kuangamizwa kwa dunia hii leo, ni pale watu watakapofikia hatua ya uasi mkuu kama vile enzi za Nuhu na miji ile ya Sodoma na Gomora!! Watu walipobadili tu matumizi ya asili, wakajitwalia wake waliowataka wao, wakaoana waume kwa waume na wake kwa wake, n.k., kikombe cha hasira ya Mungu kilijaa dhidi yao!! Ukiangalia tulipofikia leo, ni hakika kuwa kikombe cha ghadhabu ya Mungu hakiko mbali kujaa!! Take Heed!! Take Heed!!
  Ubarikiwe
  Siyi

 24. Mabinza,
  Hivi, kiroho//kimaandiko, umeleta msaada upi? Hivi ukiyatafakari unayoyasema pasipo kuhusisha Neno la Mungu ili ueleweki, ukitapika maneno maneno tu kutoka kinywani mwako ndipo umeonyesha ukweli na kudhani umethibithisha wewe si mgumu? Mbone mimi ndo naweka shairi hiyo ya mthihani niliyowapa wote wanaopinga Biblia?:
  “1 Mambo ya Nyakati 14:3 Tena Daudi akazidi kuoa wake huko Yerusalemu; akazidi Daudi kuzaa wana na binti.”

  Basi jamani, usijiweke hadharani kwa bure, ila uwe tu muungwana na utelemshe mambo dhidi ya msitari ule wa Biblia. Unawaza utaepuka hukumu ya Mungu kwa kutukana tu Ziragora ili usionekane unapinga Neno la Mungu? Ongea na Neno, lakini usinione jamani, mimi sikuandika Biblia. Ona jinsi munajisumbua kwa maneno isiyo na maana, mukisema: “kampuni ya Magreth, si mwepesi, … angalia ile § yako ya mwisho!!! Unashikwa na nini kaka? Tulia, hapa ni nyumbani mwa Bwana. Haleluya!!!

  Unapoongea hivo ukijibu kwa hoja inayotegemea Biblia hakikisha unaenenda na Neno la Mungu. Wala hakuna ufunuo wowote unaoweza kulipinga Neno la Mungu kama jinsi unavyodhani. Uwanja uko wazi ndugu yangu, ila huwo uwanja si ndani yangu, bali ndani ya Biblia. Wala hakuna atakaekucheka kama ukishindwa na Neno la Mungu kwani kamwe hutalishinda hilo Neno. Niliwaambia mapema kama neno dhambi halikurupukiwe kirahisi.

  Kwako Yona,
  Sijue unaongea na nani, lakini ninajiruhusu kusema kama nina mke mmoja tu. Lakini si hiyo ndiyo inaniokoa.Wako wengi wataangamia pamoja na kuwa na mke mmoja. Wokovu unatoka kwa Kristo. Ninakifahamu ninachotafuta ninapooa mke mmoja: ni maksudi niwe wa hesima mbele ya Mungu na kuutafuta upako. Ndio maana unashindwa jibu kwa hoja kwani hata kwa kuoa mke mmoja huna lengo, unawaza ni kawaida tu. Ila siwalaumu wale ambao walioa wake wengi. Ninachowatakia ni kama kile Paulo alichotakia watu wote akisema “ikiwezekana, ni vizuri kuwa kama yeye”. Nilitoa shairi za Biblia nyingi, rudia huko mbele na ukamate biblia yako vizuri, ukiwa uliisoma juu juu anza leo kuisoma kindani. Ukiisha kwamia ku shairi moja, nitakupa ingine ili ikusaidie nini tena? Yona, heshimu kwanza ulilopewa, kiisha lesson iendelee.

  Asante sana, na Mwenyezi Mungu awabariki.

 25. Ndg, yangu Mjema,
  Bwana wetu Yesu kristo asifiwe sana, sifa na utukufu ni juu yake yeye mwenye kuyafunua mafumbo yake. Biblia inasema, ‘Kila jambo lipo kwa wakati wake na kwa makusudi ya Mungu’ . Kwa mawazo yangu na kwakuoanisha na Neno hilo, naona kuwa Ndg. Ziragora si kwamba anakuja na udanganyifu kwa maana ya kuwaongopea watu, ila tu, jambo hili halijafunuliwa kwake. Lililofunuliwa kwako ndilo lako, maana Roho huyafumbua mafumbo ya Mungu, naye huyafumbua kwa wakati wake akiuangalia umri si kukua kwa mtu katika miaka la, bali, ni kule kuongezeka kwa kimo katika wokovu ki roho! Ndiyo maana Petro aliambiwa “Nimekuombea ili utakapoongoka uwaimarishe na ndugu zako”.

  Upo wakati yanayoonekana kwa kama kivuri yataonekana kwa uhalisi, kwa wale watakao ikubari ile kweli, maana kweli ndiyo inayomuweka mtu huru, kweli ni nini? Kweli ni NENO LA MUNGU. Ukikataa NENO la Mungu, unakuwa unaikataa kweli hivyo kamwe huwezi kuwa HURU, huwezi kamwe kuijua Kweli, na asiye na ile kweli, hataweza kusema ukweli, japo hataki kutokuwa mkweli yeye ataona hiyo aisemayo ndiyo kweli. Lakini watakaokuwa wamejaliwa kuipata ile kweli watasema “NIMUONGO MSIMSIKILIZE” akisikia hivyo, atakasilika, akikasilika lile DUDE (shetani) halitasogea mbali naye. Litamnong’oneza WEWE NDIYE MKWELI, hakuna andiko linalosema USIBWIE UGORO usikubaliane nao, wao ndiyo waongo!

  Mimi Binafsi sioni kama Ziragora ni muuongo kihivyo, ila ninavyomuona “SIMWEPESI” wa kuzirudisha nyavu katika maji mengi, yeye anaitazama ile kazi ya “BURE” aliyoifanya usiku kucha, na kuukaribisha uvivu na kujikataza mwenyewe katika kutafakari, na hivyo anasema moyoni mwake, mimi ni mvuvi wa siku nyingi, ni mzaliwa wa pwani, nayajua majira na na nyakati najua pia pepo zivumazo, nikikubali nitajichosha na kisha nitaaibika mbele ya wavuvi wa “NAMNA” yangu, kwa hiyo SIENDI! Kumbe anapaswa kusema tu bila maswali kuwa, kwa “NENO” lako nitakwenda Bwana!

  “Ufahamu ni chembe ya Uhai!”.

 26. WEWE UPO KTK NDOA YA WAKE WAWILI? TOA MAANDIKO KUSAPOTI HOJA YAKO HATUJENGI HOJA KAMA WANASIASA MAMA, KAMA HUNA MAANDIKO NYAMAZA.

  “NOTHING IMPOSIBLE TO GOD“

 27. Ndugu Mjema,

  Position unayo yaikulazimishe kujichanachana. Wewe unaleta unidirectional demonstration. Demonstration kama ile haiwezi kusaidia. Every demonstration must be bedirctional.
  Ona unayosema “Lakini pasipo imani haiwezekani KUMPENDEZA…”. Unaweza vilevile sema kama “Lakini pasipo kumpendeza Mungu imani haiwezikani…”?

  Wakati wowote kunacho kitu kinachoanza na kingine ni kinyume chake, usijidanganye kama hiyo inaweza kusaidia kuthibitisha mambo yote yaliyo ndani ya akili zako.

  Mjema, unafikiri unasema neno ambalo ni jipya ao unarudilia niliyoyasema? Ungali ukipigana tu na dhambi, ndugu yangu!!!

  Fahamu hili jambo: Walio na koze ya kudai kama kuoa wake wengi siyo dhambi wao inawabidi kusoma biblia tangu Mwanzo haadi Ufunuo ndipo wahakikishe ukweli wao kwani “isiyo dhambi”= “matendo yote” – “dhambi jinsi biblia inaieleza”. Kwa maana matendo yote siyo dhambi, kuhakikisha kama tendo fulani siyo dhambi inaomba uhakikishe umesoma biblia yote na kuona kama hilo tendo halipo ndani ya orodha. Tunachokuomba ni kuonyesha cleary andiko unaloliamini, sivyo unacheza tu. Wewe unasema Lameki, kiisha unaenda kwa 1+1=1, kiisha tangu mwanzo… Jamani jitahidi, soma vizuri biblia yako pengine utapata la kuandika hapa.

  Wewe kuonyesha kama tendo fulani ni dhambi ni kuandika tu nafasi hii mmoja ambapo Biblia imeionyesha kama ni dhambi, pia kama ni dhambi ipi. Iwepo utaleta tu demosntrations zako hakikisha hujafika kiwango cha kuthibitisha koze yako.

  Huwo mthihani ungali nao na hii ni mara ya pili unaukwepa. Jitahidi ugeuze hii shairi “1 Mambo ya Nyakati 14:3 Tena Daudi akazidi kuoa wake huko Yerusalemu; akazidi Daudi kuzaa wana na binti.” ili uhakikishe Daudi hakuoa bali alizini.Full stop.

  Ukiisha halalisha koze yako ndipo ufike nikuelimishe zaidi katika ile unayotatizika nayo, yaani hiki kifungo “kutompendeza Mungu ni tofauti ya kumchukiza Mungu”. Wala usidhani sikuyatafakari maandiko kabla niandike, lakini sitakurahisisha kugeuza mada. Twende taratibu ndugu yangu.

  Ninaloamini ni Neno la Mungu jinsi lilivyo. Hebu mwalimu, lilete tulione. Au ukilikosa ujitoe mhanga kwa kusema pengine kama ulifunuliwa!!! Unaupenda upole upi tena kaka? Unamaanisha upole ni kuitika kila litokalo kichwani mwako?

  Mungu akubariki.

 28. Ziragora,

  Pole ndugu yangu, eti “kuna jambo lisilompendeza Mungu ambalo si dhambi!!” duh! Ajabu kweli, unataka kutufundisha nini hapa. Pole kwa kukataa ukweli wa 1yoh5:17- kuwa..kila lisilo haki ni dhambi.

  Umesema,haki inahusu zaidi sheria ya Mungu kwa kuwa dhambi ni uasi wa sheria ya Mungu! Binafsi,km alivyoeleza Mabinza,hapo juu,dhambi ni kukosa shabaha ktk kile Neno\Agizo la Mungu sio sheria pekee,wewe unaonaje hili!

  Hata ivyo ngoja nikupitishe njia uipendayo,umedai, “lipo jambo lisilompendeza Mungu ambalo si dhambi” ! Hebu tusome Neno:

  1.Biblia inasemaje, kuhusu jambo lisilompendeza Mungu?

  Waebrania11:6-“Lakini pasipo imani haiwezekani KUMPENDEZA…”!

  Kumbe jambo lisilo la Imani ndilo lifanyalo dhambi. Km wewe usivyoamini neno la Mungu , mke1,mume1.

  2.Warumi14:23b…”Na kila tendo lisilotoka ktk Imani,ni dhambi”.

  Umeona boss wangu, ukichukua aya hz mbili unapata hitimisho gani, ? Hebu nirudie tena, “..maana pasipo Imani haiwezekani KUMPENDEZA..,” NA “… kila tendo lisilotoka ktk Imani ni DHAMBI..”.

  Hii, ni sawa na kusema, Tukikosa Imani ktk kila tendo HATUTAMPENDEZA Mungu ,na Kutokumpendeza Mungu ni Dhambi!! umeona eehe!

  Usije na udanganyifu wako wa kupamba dhambi,eti lipo lisilompendeza Mungu ila sio dhambi!! Kwa mujibu wa aya mbili hapo juu,huo ni uongo mkubwa! Ni sawa na Mungu alisema ” utakufa hakika” ila shetani akasema “hautakufa hakika”.

  Usibishane na neno la Mungu,uwe mpole ndugu yangu.

  Hongera,kutafakari!

  Karibu!

 29. Mabinza,

  Ubarikiwe kusisitiza kuwa dhambi ni, kutoamini sio tu sheria bali Neno la Mungu. pia umesisitiza 1yoh5:17- kuwa kila lisilo haki ni dhambi. Ingawa nilimweleza A.Ziagora hivyo bado tu ameng’ang’ania misimamo yake ya kuwa eti “kuna jambo lisilompendeza Mungu ambalo si dhambi”. Ajabu kweli,kuipaka dhambi mafuta. Hata ivyo baada ya kukupongeza,ngoja nideal nae km ifuatavyo:

 30. Wapendwa,
  Isiwachanganye hata kidogo, Dhambi ni kutoamini Neno la Mungu, sasa hawezi kusema mtu kuwa yeye hatekelezi tu wajibu Fulani lakini anaamini Neno hilo la Mungu ila hatendi tu! Na vivyo hivyo mtu hawezi kusema kuwa yeye haamini Neno hilo la Mungu ila analitekeleza tu, watu hao wote wawili ni wenyedhambi, yaani hawajaokolewa! Biblia inasema, Jambo lolote lisilo la Imani ni dhambi na imani yoyote isiyo na matendo imekufa!

  KWAHIYO, DHAMBI NI KUTOAMINI, kutoamini nini? Kutoamini NENO LA MUNGU! Sasa, kama ndivyo, hebu sikia, Yesu akiwajibu mafarisayo, Marko 10:2-9 twasoma hivi,
  “……6Lakini tangu mwanzo wa uumbaji, ‘Mungu aliwaumba mume na mke………..”

  Iwapo Neno linasema “TANGU MWANZO WALIUMBWA MME NA MKE” ikiwa mtu hatalitenda Neno hilo na kujiolea wake wawili, watatu, wane ama hata elfu, kinyume na Neno hilo, Mtu huyo atakuwa haliamini Neno hilo la Mungu! Na ikiwa kutoamini Neno la Mungu ndiyo dhambi yenyewe,

  Je mtu huyo atakuwa hakufanya dhambi? Ikiwa atajitetea kwamba, yeye hafanyi dhambi ila anafanya tu, jambo ambalo Mungu hataki, na akasema “nafanya jambo ambalo Mungu hataki ila hakuna popote Mungu aliposema kuwa Jambo hilo ni dhambi, japo kuwa najua kuwa Mungu hataki jambo hilo litendwe!” Wapendwa huo si wendawazimu?!

  Kumbukeni kuwa Haki na Kweli ndiyo Neno la Mungu, jikumbusheni pia kuwa, 1Yoh5:17 inasema, “kila jambo lisilo haki ni dhambi” Kama hamuamini oeni tu wawili mtajua hapohapo!

  “Ufahamu ni chembe ya Uhai!”

 31. Milinga,
  Sikutarajia kuwa na wewe unaweza kutumia akili zako kuhojiana na Mungu!! Nimeshangaa sana. Umeuliza maswali kwa hoja dhaifu kabisa, kana kwamba aliyekuumba, hakujua kuwa wewe (mwanaume), una mbegu/nguvu nyingi za kiume na kwa mwanamke kinyume chake!!
  Maswali yako hayo ni hoja za kiibilisi alizotumia kuwahadaa akina Adamu na Hawa kutokula tunda!! Na wewe nakuona unataka Mungu afikiri kama unavyofikiri wewe. Atende kama unavyodhani wewe!! Na kwa ujumla, afuate hisia/matamanio na fikra zako zilizosheheni uovu!! mjema kajitahidi sana kukujibu. Nadhani utapata ufahamu japo unaonekana kuwa shingo ngumu pamoja na Ziragora wako!!
  Nawatazama tu!!!
  Siyi

 32. Ndugu Mjema,

  Usijaribu kumvika mwenzio joho lako. Ao unafikiri watu wote ni waongo? Nilisema kama kanisa langu haliwapokee waume waliyooa wake wengi hapo wake wao wanapokelewa. Ila twajua kama uzinzi unahusisha watu wawili. Nikasema kama hainisumbue wala hainikataze kuungalia msimamo wa Biblia. Nikawawekea mtihani huu: Jaribu kuigeuza hii shairi ifwatayo ionekane kama Daudi alizini na wake.
  “1 Mambo ya Nyakati 14:3 Tena Daudi akazidi kuoa wake huko Yerusalemu; akazidi Daudi kuzaa wana na binti.”
  Kama wewe unaweza, ok good, go ahead. Na kama huwezi tafakari zaidi.

  Unapokosewa hoja tulia kaka, jifunze.

  Lisilo haki haimaanishe lisilopendeza. Lisilo haki ina maana linalopinga sheria. Unapofika mahakamani, unaambiwa huna haki ni kwamba umevunja sheria.

  Ninaposema “mtu kumzika babae siyo dhambi” naamini huna la kukanusha pale. Ikiwa dhambi, ina maana na wewe ukimzika baba yako utakuwa umetenda dhambi.
  Jirebekisheni kaka, neno dhambi silo neno la kukurupukia kirahisI.

  Chukua mda uyatafakari tena niliyo post huko mbele, pengine kwa wakati wake utapona jambo la kumfanya Mungu kuwa muongo. Usijiangamize bure kwa kutofahamu.

  Kaka, kama ungali ukipigana na dhambi, hauko miongoni mwa wale wanaompendeza Mungu, wala Mungu hatakudai chochote cha kumpendeza iwapo hujatimiza mema yaani haki.

  Haki ndiyo inaanza, kunafwata kumpendeza Mungu; na baadaye ukamilifu.

  Asante.

 33. Part III

  Wapendwa,

  Nimerudi tena kuangusha nguzo ya tatu,katika mada ya dada magreth.

  Katika ufafanuzi wa Swali lake,amesema, hakuna aliyepigwa mawe kwa kuoa wake wengi bali waliopigwa mawe ni wale waliozini .wakimaanisha kuwa wale walioa wake wengi,kwa kutokupigwa mawe sio dhambi ya uzinzi. Au kwa maneno mengne, iyo hukumu ya kibinadamu-kupiga mawe ndio kiashiria cha kutueleza tendo fulani ni dhambi au sio dhambi!! mhm! ajabu ilioje.kupata hitimisho la watu wavivu kutafakari Neno kama kina Magreth na washirika wake.hebu tuone:

  1.Kama umesoma Part II, Hapo juu vizuri, tumegundua kuwa kuoa wake wengni ndio mapokeo toka kwa Mzee Mpagani Lameki Vs kuoa mke mmoja ni Agizo la Mungu pale Edeni, na Yesu alipokuja alisisitiza tena kwa kumnukuu Mungu.yaani kwa lugha ya leo, Ali-Copy na ku-Paste.!
  Kuoa wake wengi ndio mapokeo ya wazee ivyo usitegemee kuona mtu akipigwa mawe.

  2.Dhana ya kupiga Mawe wazinzi.

  Kisa cha Yesu na mwanamke aliyefumaniwa uzinzi.ktk. yohana 8:2-11 Kinaonyesha Yesu akikemea mapokeo ya kupiga mawe wazinzi. Yaani kutumia hukumu ya kibinadamu-kupiga mawe km ndio ishara ya kusema kufanya hv ni dhambi au la!

  Yesu aliwaambia, “…asiye na dhambi na awe wa kwanza kumpiga jiwe…”,.Yoh8:7

  Kisha akainama na kuandika chini na wakaanza kuondoka mmoja baada ya mwingne.! ikionyesha kuwa Yesu alikemea mapokeo ya kuamua kitendo hk ni dhambi na hk sio dhambi! Kwa kupigwa mawe. Hata wewe Magreth na wenzako usitumie kupga mawe km ndo ishara ya dhambi au la ivyo ni vigezo vya kibinadam ambavyo Yesu alivikemea.

  Hivyo rafiki, wale watesi wa yule mwanamke walionekana hawana dhambi,ndio maana hawakupigwa mawe!híi ni kibinadamu tu. Yapo mambo mengi hata leo tunafanya kwa siri ambayo km ni kupigwa mawe,hasingebaki ht mtu mmoja kupiga kifua kama ilivyokuwa kwenye kisa hiki.

  Yapo mambo mengi km ilivyo kuoa wake wengi ambayo Mungu alijifanya haziona ila leo anaagiza tutubu.kwa kuwa mawe-moto wa milele unakaribia.

  Badaa ya kuangusha hoja 3 zilizounda swali la Magreth,nitarudi tena na Part IV-Kujazia minofu na Part V-kuuliza maswali muhimu.

  Asante.

  … Inaendelea… Soma part IV….

 34. Mr.Milinga,

  Kabla ya Part III napenda nikujibu maswali yako yenye changamoto kweli.

  1.kuhusu muislam mwenye wake 4 au mmasai mwenye wake 10 na watoto 40. Je ,wakimpokea Yesu wataachana.

  jibu: NDIYO

  Kuachana kwa maana ya kushiriki tendo la ndoa hivyo,Itabidi, awaache wote, abaki na mke wa kwanza. ILA atawatunza wake wote na watoto kwa mahitaji yao yote. na nao wake walioachwa_kwa maana ya kushiriki tendo la ndoa watakuwa huru kuolewa na wanaume wengne.
  Maandiko nitakayotumia ni kama nilivyotoa coments zangu hapo juu,tar 199\14 saa 5:06.
  -Pia soma mwanzo habari Abraham dhidi ya Sara vs Hajiri. ilibidi hajiri aachane na Abraham. Mwanzo 21.

  2.ndoa ni utumwa au muunganiko wa hiari?.

  Jibu:Ndoa ni Muunganiko wa hiari kati ya mke1 na Mume1 sio utumwa. Soma mwanzo2 na mathayo15 hapo juu.

  3.maswali yako mengne yote. no.4-6. Kuhusu kibaiologia na nguvu za mapenzi!

  Majibu:

  1.kaka, katika kuoa hatuongozwi na hisia\mihemuko\tamaa.

  Biblia inasema. 1.tusienende kwa tamaa za mwili.Galatia 5.

  2.tujue jinsi ya kuiweza miili\tamaa zetu.

  3.tuitoe miili yetu kuwa dhabihu.Rom12:1-2

  4.tukiwa ndani ya Yesu sisi ni viumbe vipya,ya kale yamepita,tazama ni mapya.! 2kor5:17

  Hivyo, u mwili unaoueleza wewe hapa, sio sababu ya kuoa wake wengi! Kwani kama kuna mwanamume aliyewaikuwa fit kimwili katika historia ya wanadamu ni Adam,Ila Mungu alimpa Mke 1.

  Pia,unaposema kuwa ni wanaume ndio wenye nguvu za mapenzi kuliko wanaume, sio alwaz kweli. kuna wanawake pia wenye nguvu vilivyo! Hata midume 5 inaweza kushindwa kazi.Je na hao nao, waolewe na waume 2+

  Asante.

 35. Part ÍÍ ….inaendelea…. Wapendwa nimerudi
  tena, kueleza kile
  ninachokiamini kuhusu
  kuoa mke 1 au 2+ Magreth na kampuni
  yako, umeeleza kuhusu
  mapokeo.kwamba kuoa
  mke mmoja
  ni mapokeo ya
  kanisa.hebu tuone kati ya kuoa mke mmoja au
  wengi,ni
  yapi mapokeo? Mapokeo ni nini? Kwa mujibu wa Biblia
  mapokeo ni maagizo
  ambayo niya
  wanadamu ila watu
  uyachukulia kuwa niya
  Mungu. Soma.
  Math15:2,9-“…uyahalifu
  mapokeo ya
  wazee…”..Nao uniabudu
  bure,wakifundisha
  mafundisho yaliyo maagizo ya
  wanadamu”. Hebu tuone kati ya kuoa
  mke1 au wake2+, ni
  yapi mapokeo ya
  wanadamu: Mungu anaagiza
  hv,Mwanzo2:24-“kwa
  hiyo mwanamume
  atamwacha baba yake
  na mama yake naye
  ataambatana na MKEWE,nao watakuwa
  mwili mmoja” Zingatia neno Herufi
  kubwa MKEWE sio
  WAKEZE.Ndilo agzo la
  awali la Mungu. Yesu nae anasisitiza
  kauli iyo iyo ya Mungu
  kwa kumnukuu
  hv.Math19:5-“akasema,kwa
  sababu iyo,mtu
  atamwacha babaye na mamaye,ataambatana
  na MKEWE,na hao
  WAWILI Watakuwa
  mwili mmoja”.
  Unaona hapa tena Yesu
  anawasisitiza mafarisayo, MKEWE sio
  WAKEZE.Pia
  Yesu ktk aya hii
  anasisitiza kwa kusema,
  Na hao WAWILI-sio
  watatu,nne au zaidi.
  Paulo 1.Pia,kumbka mahali
  fulani paulo anasema,Ila
  kwa sababu ya tamaa
  Mume
  na awe na mke wake
  mwenyewe. 2.Paulo pia
  anafananisha
  mahusiano ya mume na
  mke sawa na Kristo na
  Kanisa.Sasa Je, Kristo
  ana makanisa/wake wengi.? never Sasa,ni waulize
  wapendwa kina
  Magreth haya ni
  mapokeo ya kanisa?
  ikiwa
  ndiyo Mbona Yesu anasisitiza yaendelee
  sio kama
  alivyokemea,kuhalifu
  mapokeo ya wazee
  kunawa mikono
  math15 au talaka aliposema lakini
  haikuwa ivyo ila ni
  ugumu tu wa mioyo
  yao! Summary:Hapa Mungu
  \Yesu, wanatufundisha:
  mume1+mke1=mwili1.
  Aya sio
  maagizo ya wanadamu
  bali Mungu hivyo SIO MAPOKEO YA KANISA. Magreth na Kampuni
  lako,tukigeuza upande
  wapili wa shilindi,kuoa
  mke
  zaidi ya mmoja ndo
  mapokeo tena ya wazee.hebu tuone: Kama tulivyoona,Yesu
  alikemea,mapokeo ya
  wazee.Math15:2. Tuliona ktk PartI,
  Lameki wa uzao wa
  Kaini-uzao uliochagua
  Kuacha
  uongozi wa Mungu.kwa
  maneno mengne Wapagani ndio wa
  kwanza kuoa wakewengi.Lameki alioa
  wake wawili
  Mwanzo4:19-kama
  anavyotuambia Magreth
  kwamba kuoa wake
  wawili sio dhambi. Summary2:Mzee
  Lameki
  anasema:Mume1+Wake2=mwili1. Sasa,Mage na wenzako,
  kati ya summary1 na 2
  hapo juu,ni yapi
  mapokeo?
  Zingatia maana ya
  mapokeo hapo juu! Nasubiri Majibu. …inaendelea…soma part
  III….

 36. Ziagora,

  Pole sana,naona mapokeo ya dini yanakubania? jiachie mtumishi.

  Hata,hivyo nakushangaa kusema “kuna mambo ambayo hayampendezi Mungu ila sio dhambi!” sijui umeitoa wapi.

  Biblia inasema, ” kila jambo lisilo haki ni dhambi”. 1Yoh5:17.

  Usitake kuhalalisha hitaji lako la kuwa polygame.biblia ndivyo inavyojieleza.usilete blah blah hapa.Kwani wewe hujui hilo lisilo haki ndio ilo ilo lisilompendeza Mungu.

  hata,mifano uliyotoa yote inakupinga.

  Kuhusu yule aliyetaka kuwazika wazazi ndo arudi kumfuata Yesu. Ni dhambi pia, kwani haikuwa haki kufanya hivyo. Yaani kwa maneno mengne,unapotaka kumtumikia Mungu,usiangalie udhuru\visingzio vinavyo kuzunguka.wewe unavikiri kufanya ivyo ni haki?

  Asante

 37. Ndugu Sungura,

  Hulazimishwe, wala hakuna anaelazimishwa kujibu. Kwako ni swali ndogo kulingana na makala yako ya 16/09/2014:”Lakini tangu mwanzo Mungu aliumba mme mmoja na mke mmoja (Mark 10:6)”
  Nilitaka utueleweshe kama ile unayonukuu inathibithisha kama Mungu alisema “kuoa wake wengi = dhambi ya uzinzi” ao kama ni mtazamo wako tu.

  Kuwa mada ni nyepesi zidhani kwani kuna maswali mengi ambayo yamekwepwa. Imejadiliwa na wengi kishabik bila kuhusisha Neno la Mungu. Tunapojiweka tayari kujadili, kiukweli tunahakikisha kama tumeweka pembeni doctrines za makanisa yetu ili tuone kimsingi Biblia inaongeaje.

  Kwa mfano, ndani ya kanisa ninayoshiriki, ninachoona ni kwamba aliyeoa wake wengi hapokelewi, lakini wake hawazuizwe. Hii ni msimamo na tabia za kanisa jinsi inavyoongozwa. Hii doctrine haiwezi nikataza kuisoma Biblia ili nielewe msimamo wa Mungu mwenyewe.

  Asante Ndugu yangu na Mungu akubariki.

 38. Ziragora,

  Sijaelewa kama umeniuliza swali ambalo napaswa kulijibu.

  Hii mada ni nyepesi tunataka kulitatisha tu bila sababu ya msingi.

 39. Ndugu Siyi,

  Kuna mambo ambayo haifae ikurupukiwe kirahisi. Ukitumia hisia zako ao akili zako, pengine unaweza tumia tamko kama hizi: hainipendezi/sifurahii/ni vibaya/ina vinyume vibaya/udhaifu, nk… Lakini ifikapo kusema hiki ao kile ni dhambi, hakikisha Mungu ameiweka kama dhambi. Hata kama wewe unaona kitu fulani ni kizuri, usikihalalishe kama Mungu alisema ni dhambi, halikadhalika, hata wewe ukikiona ni kibaya kwa macho yako usikiite dhambi kama Mungu hakusema.

  Asante ndugu Milinga kwa kuwakumbusha wanaochangia kama kinachosikilika ni hoja inayolingana na maandiko wala siyo hitaji/mitazamo yetu. Mungu mwenyewe ndiye ana define dhambi kuipitia sheria yake; ukikwepa ile utaanguka ndani ya uongo, ule uongo wa kifo wa kumfanya Mungu kuwa muongo.

  Ndugu Sungura, kweli usipozingatia fikara zako tu unaweza thibitisha kama ile unayosoma katika Mrk 10:6 inasema kama kuwa na wanawake wengi ni dhambi?

  Kwa mfano, unaposoma shairi ifwatayo, utaigeuzaje ili ionekane kama Daudi hapa alitenda dhambi ya uzinzi?

  “1 Mambo ya Nyakati 14:3 Tena Daudi akazidi kuoa wake huko Yerusalemu; akazidi Daudi kuzaa wana na binti.”

  Hapa Biblia inasema ALIOA WAKE lakini HAISEME ALIZINI na wake.

  Usifanye private hili jambo la dhambi. Hapa juu nimewaonyesha shairi zinazOthibitisha kama kumbe kuna mambo isiyompendeza Mungu pasipo kuwa dhambi.
  Kwa mwanaadamu kama wewe, ni halali uone mambo mengi inayokupendeza na mengine yasiyokupendeza, lakini usiende haraka kusema eti hii si dhambi ama hii ni dhambi kabla hujauliza biblia. Kuuliza bibila ni kuisoma kikwelikweli wala si kuwa shabik wa shairi fulani.

  Nataka nikupe kibiblia mfano mwengine wa mambo yasiyompendeza Mungu pasipo kuwa dhambi:
  “21 Mwingine katika wanafunzi wake akamwambia, Bwana, nipe ruhusa kwanza, niende nikamzike baba yangu.
  22 Lakini Yesu akamwambia, Nifuate; waache wafu wazike wafu wao.”

  Hapa tunamuona Yesu hapendezwi na kwamba mwanafunzi wake aende kumzika baba yake. Lakini kiukweli hakusema kama mtu kumzika baba yake ni dhambi.

  Kuna pengine mambo ambayo hujaelewa kibiblia licha ya kuwa yako wazi. Wakristo wote hawako ku step moja. Wamoja ni wakamilifu, wengine wanampendeza Mungu na wengine ni wema tu kama jinsi nilivyosema huko mbele.

  Tena Biblia inasema hivi:
  “2 Timotheo 2: 19 Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio wake. Na tena, Kila alitajaye jina la Bwana na auache uovu.
  20 Basi katika nyumba kubwa havimo vyombo vya dhahabu na fedha tu, bali na vya mti, na vya udongo; vingine vina heshima, vingine havina.”

  Hivi vyombo vilivyo ndani ya hii nyumba si wakristo? Wamoja wamefananishwa na vyombo vya mti, wengine vya udongo, wengine vya fedha, na wengine vya dhahabu.

  Pia angalia hili andiko:
  “1 Wakorintho 8:9 Lakini angalieni huu uwezo wenu usije ukawakwaza wale walio dhaifu.”
  Kuna wakristo walio dhaifu na wengine wanazo nguvu, lakini wote ni wakristo.

  Ndio maana nikawaonyesha hizo steps zote kulingana na ile sheria inayohusu tu Askofu/Shemasi. Pale Paulo anamaanisha kama tusiwaweke kuwa Askofu/Shemasi wale ambao ni dhaifu katika imani, yaani kile chombo cha mti, kisicho na heshima mbele za Bwana, ao yule mukristo ambae angali akipewa maziwa, ao yule mukristo ambae hakae ndani ya ukamilifu. Pia usifikiri kwamba Paulo ameamuru watu kuoa wake wengi. Hilo ni jambo lingine kwani akiamuru watu kuoa wake wengi ina maana mtu asiye na wake wengi ametenda dhambi.

  Nilichokisema ni kwamba, kuwa high ndani ya kuukomalia wokovu inalazimishwa kuwa na mke mmoja ao kutokuwa na mke.

  Tunawafahamu watu katika Biblia kama akina Yohana ambao hawakuruhusiwa hata kuwa na mke. Ile ni kiwango kubwa sana, ndiyo maana Yesu akamshuhudia kama katika wazaliwa wa wanawake yeye Yohana ni mkubwa kuliko wote. Paulo hali kadhalika, hakuoa na akasema, ungewezekana tuwe kama yeye. La kini yuko anaeshurtishwa kuwa na mke mmoja na wengine Mungu hakusema jambo lolote. Kinachoonekana kibiblia ni kwamba kuoa wake wengi siyo uzinzi. Na yeyote aliyesema ni uzinzi aliipinga biblia.

  Tatizo watu wengi wanalo ni kujidhania wao ni watakatifu, wamekwisha timiza sheria zote za Mungu, wanajiona kama wamekosa la kuheshimu tena, hapo wanaanza undaunda dhambi ambazo biblia haifahamu.

  Asante wapendwa na Mungu awabariki.

 40. Wapenzi

  Tunapojadili mada hii naomba pia tusisahau kunukuu maandiko huku tukizingatia changamoto zifuatazo:

  1. Akiokoka Muislam aliyekuwa ameoa wanawake 4 kihalali na kisheria kwa mujibu wa dini hiyo na kwa mujibu wa sheria za serikali yetu, Je, wewe kama Mchungaji wa kanisa alilojiunga utamwambia awafukuze wake zake wote abaki na mwanamke yupi na kwa nini?

  2. Kama akiokoka Mumasai aliyeoa wanawake 10 na mwenye watoto 40 aliowazaa kwa wanawake hao na ameendelea kuwalea vizuri hadi siku anaokoka; Je, utamwambia awafukuze wanawake wake wote? Hoja utakazompa za kimaandiko zitakuwa zipi?

  3. Je, ndoa ni utumwa au ni muungano wa hiari? Kama ni muungano wa hiari kati ya mwanaume na mwanamke maandiko yanasemaje kuhusu muunganiko huo wa hiari?

  4. Mwanaume anauwezo wa kibayolojia na kimaumbile kutoa mbegu zaidi ya milioni tatu kwa mkupuo mmoja tu. Lakini mwanamke akiwa na uwezo wa kutoa yai moja tu kwa mwezi!!!!! Je, hatuoni kuwa hoja ya kuwa na mke zaidi ya mmoja haina kipingamizi kimaandiko wala kisayansi?

  5. Wanaume wengi kibayolojia wana nguvu nyingi za kiume kiasi kwamba wana uwezo wa kuzaa na wanawake zaidi ya mmoja ndani ya wiki mmoja. Yaani wana uwezo wa kutungisha mimba zaidi ya mke mmoja kwa wiki moja. Lakini mwanamke hawezi kuzaa na mwanaume zaidi ya mmoja kwa mwaka mmoja au zaidi. Je, hoja hii haihalalishi wanaume kuoa mke zaidi ya mmoja?

  6. Wanaume wanapokuwa na mke mmoja tu hulazimika kujizuia kufanya tendo la ndoa kwa zaidi ya miezi 3 hadi 12 wakati mke anapokuwa amejifungua mtoto ili kutoa nafasi kwa mtoto kukua na mke kupata afya. Je, hoja hii haihalalishi mwanaume kuwa na zaidi ya mke mmoja ili kutolazimika kuwa na msongo wa hitaji la tendo la ndoa wakati mke awapo kwenye malezi ya mtoto?

  Kuna changamoto nyingi kwenye mada hii, ila kwa sasa nikomee hapa. Nawashukuru wote wanaotafakari maandiko kwa hoja na siyo kwa mazoea.

 41. Ziragora,
  Yaani hata sina cha kuandika sana kwenye mada hii zaidi ya kukutoeni woga/wasiwasi ambao nilidhani unao. Nashukuru kumbe hata wewe huogopi chochote isipokuwa Mungu tu. Mungu akubariki sana.
  Tukumbuke kuwa, ibilisi hutumia neno la Mungu (tunayemwogopa) ili kutimiza azma zake kwetu. Walevi hutumia neno la Mungu kuhalalisha ulevi, wezi nao kadhalika. Na hata wazinzi leo (tunaowajadili hapa), bado wanatumia neno la Mungu kulazimisha fikra na mawazo yao yahalalishe dhambi. Tena pengine, wanatafuta neno kabisa litamke, ‘usivute sigara, ndipo waache kuvuta sigara’, ‘kuoa wake wengi ni dhambi, ndipo waache n.k.’ Utambuzi wa kiungu juu ya miili yao (kama mahekalu ya Mungu), ulishapotea vichwani mwao. Wamelewa mvinyo wa Babeli. Tuombeane sana.
  Wale tusiopata muda mrefu wa kuzungumza na Mungu kwa njia ya kusoma neno lake na maombi mengi, tutapotea tu. Mungu atusaidie kuviinua vichwa vyetu juu, pindi unabii unapotimia maishani mwetu.
  Ubarikiwe Ziragora na wengine.
  Siyi

 42. Ndugu Siyi,

  Narudi kidogo kwako kwani pengine ulidhani niliogopa wakati niliposema mifano uliyoleta inaogopesha sana. Si kwamba niliogopa, lakini ni kwamba ulileta puzzle bila kuweka jibu. Unapojadili thamatisha hoja yako vizuri, yaani conclusion iambatane na changamoto.

  Asante.

 43. Ndugu Siyi,

  Ni vipi kaka?

  Uwe huru tu, usiogope. Sjue unahisi nini rafiki yangu!
  Tunaemuogopa ni Mungu na Neno lake. Ndio maana hatupendi kupunguza wala kuongeza chochote. Tunalisoma jinsi lilivyo. Kuna kitu kinachokurupukiwa haraka: “kusema kitu fulani ni dhambi” licha ya kukosa andiko linalothibithisha. Neno linaposema “kulewa mvinyo ni dhambi” bila kusema mvinyo ni dhambi, hutaniona nikilishurtisha kwani sina hayo mamlaka. Ufahamu wangu unarudilia tu kwa kile neno linathibithisha.

  Go ahead, labda utaeleweka zaidi.

  Ubarikiwe sana.

 44. Ziragora,
  Hakuna haja ya kuogopa rafiki. Laiti ungejua dunia nna asasi zote zilivyo chini ya mamlaka ya giza (asasi za mpinga Kristo), hata usingeogopa. Unamkumbuka Ibrahimu Lincoln na Kenedy (maraisi wa awali) wa Marekani? Unafahamu walivyokufa? Sababu zilizowaua unazifahamu? Aidha, unawakumbuka wafia dini wa karne 16 hususani huko Uingereza? Unamkumbuka mtu (mwanamke na Malikia katili) aliyewahi kuwepo duniani – Mariamu almaarufu “Blood Marry”?? Jaribu kuzipitia historia zao.
  Naufahamu mfumo wa Catholiki unavyouendesha ulimwengu katika mifumo yote ya serikali, dini zote, afya, elimu n.k. Sina chuki na wakatholiki. Nawapenda sana. Wengi wao, huwa hawaelewi mambo yanavyokwenda. Tatizo ni mfumo wao ulio chini ya Mpinga Kristo –Ibilisi mwenyewe na mawakala zake. Sishangai kuuona mfumo huohuo unapiga kampeni za ushoga, usenge, akina mama kutaka mamlaka ya wanaume n.k. Sishangai kuona wanaleta hoja ya wanaume kuhalalisha kuoa wake zaidi ya mmoja. Na hili vuguvugu litakuja kupitishwa tu na kuwa halali ndani ya imani za Kikristo, japo kwa sasa tunaonekana kupinga. Wanawake nao watataka haki iyohiyo.
  Kwa mantiki hiyo, ukitaka kuwa upande wa Mungu, sharti upingane na upande wa ibilisi. Na ukiwa kinyume na upande huo wa giza, sharti ukubali matokeo. Mimi nilishakubali matokeo ndiyo maana huwa nasema bila woga!! Ukisimama upande wa Mungu, hupaswi kuogopa rafiki yangu.
  “Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona. Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake? Kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake”-mtt 16:24-27

  Siyi

 45. Nami nichange kidogo tu !!!

  Kuchangia hii maada ni kuitika kuvunja mifupa kwani ni mada isiyo rahisi. Tukitazama michango yetu, sote tutakuta ni filosofia tu kwani hakuna kilicho very clear kwamba Biblia inasema kama “kuowa wake wengi” ni dhambi. Ndugu Siyi, ile mifano uliyoleta ya 08/09/2014 inaogopesha sana na maamzi siyo mepesi. Kwa ujumla wote waliochangia wako tu sahihi kulingana na wanachokisoma/wanachokifahamu.

  Hebu tuangalie maandiko:
  1) “Warumi 12:2 Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo MEMA, ya KUPENDEZA, na UKAMILIFU.”

  Hili andiko linatofautisha mapenzi ya Mungu. Yapo yaliyo MEMA, yapo yaliyo ya KUPENDEZA MUNGU, na mengine ya UKAMILIFU. Lakini haya yote ni mapenzi ya Mungu. Mtu aneweza weka comments zake jinsi apendavyo, lakini mimi naona kuna hatuwa dani ya kumfwata Mungu. Ndiyo maana lile neno lililorudiliwa mara nyingi “…. Askofu/Shemasi awe mume wa mke mmoja”, halikulenga wakristo wote angalau hawo maaskofu na mashemasi nao ni wakristo tu. Kinacholeta changamoto ni pale ambapo Biblia haikutaka kusema wazi kama “kuowa wake wengi ni dhambi”. Tunazoea kuyapokea maswala hayo, pia ni mengi kabisa. Swali ipo tu. Ikiwa kuowa wake wengi ni uzinzi na katika kipindi chote cha agano la kale, haswa tangu Musa, imewekwa adhabu ya uzinzi kuwa kifo, kwa nini watu wengi walioa wake wengi bila kuuwawa? Pia kwa nini tunajaribu sana kulitumia neno “kuowa” tukifahamu neno “kuzini” iko? Ni kitu gani kinachotuzuwiza kulitumia neno linalofaa?
  Ningilipenda tuambatanishe hili swali na haya mapenzi matatu ya Mungu. Kama Askofu/Shemasi ndiye mhusika tu kwa sheria hiyo ina maana hawa watu pengine wanatakiwa kuwa miongoni mwa wakristo wanaoyatimiza mapenzi ya Mungu yaliyo ya kupendeza na makamilifu, Wakristo wasiyo na upako mwingi wakiwa wale ambao wako huko chini katika mapenzi ya Mungu yaliyo mema tu.

  Pia wengi wanadhani kama Mungu aliwafurahia wale wote wa agano la kale waliyooa wake wengi. Hii ni udanganyifu. Tufahamu kama siyo kuja kwa Yesu tu kuliofunua kama Mungu hafurahie kuowa wake wengi.

  Andiko hili lathibitisha ninayosema:

  ” Malaki 2:13 Tena mnatenda haya nayo; mnaifunikiza madhabahu ya Bwana kwa machozi, kwa kulia na kwa kuugua, hata asiiangalie tena hiyo dhabihu, wala kuitakabali mikononi mwenu na kuiridhia.
  14 Lakini ninyi mwasema, Ni kwa sababu gani? Ni kwa sababu Bwana amekuwa shahidi kati ya WEWE na MKE wa UJANA wako, uliyemtenda mambo ya hiana, angawa yeye ni mwenzako, na mke wa agano lako.
  15 Hakuna mtu mmoja aliyetenda hivi, ambaye alikuwa na UFAHAMU KIDOGO. Au je! Kuna mtu mmoja atafutaye mzao mwenye kumcha Mungu? Kwa hiyo jihadharini roho zenu; mtu awaye yote asimtende MKE WA UJANA wake mambo ya hiana.”

  Yes, Mungu hajasema kama hii ni dhambi, lakini kwa andiko hili anaonyesha kupitia kinywa cha Nabii Malaki kama hapendezwi na yeyote aneyemtendea hila mke wa ujana. Anamuweka katika watu wasiyo na ufahamu. Ndio Maana inapofika katika agano jipya hawa watu wasiyo na ufahamu hawaruhusiwe kuongoza wengine. Malaki ametumwa pia kusema kama kuna mtu mmoja tu alliyewai kuwa na wake wengi akiwa na ufahamu, naye ni Ibrahim kwani alipokwenda kwa Hajiri haikutokana na matakwa ya mwili lakini alikuwa akitafuta kile Mwenyezi Mungu alichoahidi.

  Nitamathishe nikisema kama ukitaka umpendeze Mungu/uwe rafiki kamilifu wa Yesu Kristo/chochote unachokiomba kwa jina lake ukipewe, usijaribu kuwa na wake wengi. Unapojaribu hiyo hakikisha wewe unaweza kuwa mkristo ambaye hawezi ongoza wengine, mtu bila ufahamu mbele za Mwenyezi Mungu. Lakini twajua kwamba lengo la mukristo ni kusonga mbele, wala siyo kubaki nafasi moja; ndio maana hata pasipo kuwa dhambi, kuowa wake wengi haimpendezi Mungu wala si kamilifu. Kwa hiyo tunashawishi wakristo wote wawe na nia njema ya maendeleo katika ukristo, yaani kujithahidi kuwa na mke mmoja. Hawo wanawake wa mume mmoja wanakubaliwa katika makanisa mengi kwani katika Biblia wao hawatajwe kwa lolote. Ndiyo maana tusilinganishe kuoa wanawake wengi na uzinzi, kwani kila pa’li inaonekana kwa tabia ya Biblia kama ni mume anae uamzi mingi ndani ya ndoa. Kwa tabia ya kibiblia, mume akiowa wake wengi anaejumuika ni mume ambae alimchokoza mke wake wa ujana, lakini hao wanawake kibiblia hawana hatiya. Si sote tunafahamu kama kuna mambo fulani ambayo yanaweza husu mume bila kuhusu mke, ao kuhusu mke bila kuhusu mume?

  Wapendwa, Mungu awabariki.

 46. Mjema,
  Mungu akubariki sana kwa mchango mzuri ulioshiba. Nazidi kuangalia kama kuna sehemu imesalia ya kuchangia ili na mimi niongezee mchango wangu.

  Lwembe,
  Kwa hiyo unataka kusema kuwa, na hawa wanaofanya dhambi sasa hivi, ni uzao wa Kaini tu au una maana gani? Kwa vile Yakobo, Daudi,Suleimani walioa hadi wajakazi/mahawara, unataka na sisi tuoe wajakazi/mahawara?

 47. Hebu twendeni polepole, hivi,
  Yakobo alikuwa na wake na mahawara (concubines) wangapi?
  Daudi naye alikuwa na wake na mahawara wangapi?
  Na Sulemani alikuwa na wake wangapi?
  Je, HAWA WOTE NI WA UKOO WA KAINI, au ni wa UZAO WA NYOKA???

 48. shalom wapendwa,

  PART I

  Mbarikiwe kwa kuwa km waberoya kuyachunguza maandiko.

  Dada, Magreth,höngera kwa ujasiri kusema kiliujaza moyo wako. Hata ivyo hakuna ukweli ktk madai yako kuwa “kuoa wake wawili sio dhambi”!!. Bali mimi naamini mtazamo wa Biblia ni Kuoa zaidi ya mke mmoja ni dhambi, tena dhambi ya uzinzi inayotokana na tamaa iliyokomaa.

  Nawapongeza wachangiaji walotangulia,na ninawapa pole wenye mtazamo km wako.

  Ushahidi wa maandiko unaojibu hoja yako zenu ni km ifuatavyo:

  1.Mtu wa kwanza kwenye Biblia kuoa mke zaidi ya mmoja ni mtoto wa mtoto, wa mtoto wa aliyemuasi Mungu/Mpagani Kaini anaeitwa Lameki na sio Adam. soma Mwanzo 4:16-19 “Kaini akatoka mbele za uso wa BWANA akakaa nchi ya Nodi…. 17.kaini akamjua mkewe ….akamzaa Henoko,akamzaa… Methushaeli..akamzaa Lameki…19.Lameki AKAJITWALIA WAKE WAWILI….Ada na … Sila.”

  Dada Mage,unaona kuoa mke zaidi ya mmoja ni matokeo ya “kutoka mbele za uso wa BWANA”. wapagani wa kwanza kitukuu wa Kaini ndiye aliyeanza uasi huo,na hivyo kufanya ivyo ni kuiga wapagani-watu wanaokataa uongozi wa Mungu.

  Pia, zingatia kitenzi kilichotumika hapo “Lameki ..AKAJITWALIA…” Neno AKAJITWALIA wake ndilo lililopelekea ghadhabu ya Mungu kuleta gharika. soma mwanzo 6:1-3. ” ikawa wanadamu walipoanza kuzidi….na wana wa kike wakazaliwa kwao..2. Wana wa Mungu wakawaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri, WAKAJITWALIA WAKE wowote waliowachagua.3.Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu….”

  Nadhani umeona neno “WAKAJITWALIA WAKE” limetumikaje.! Sasa Ikiwa hii ndio sababu moja wapo ya kujitwalia wake iliyomudhi Mungu,unafikiri ni dhambi au la?

  Mchangiaji mmoja amedai, Adam ndiye wa kwanza kuoa wake zaidi ya mmoja kwa kigezo kuwa wanefili ambao Biblia inasema “nao wanefili walikuwepo duniani siku zile”Mwanz6:4,kuwa ni kiashiria cha Adam kuoa mke zaidi ya Hawa!! ajabu kweli!dhana hii na sawa na kusema, Adamu alimwoa binti yake!! Umeitoa wapi iyo kaka.

  Hata hivyo ukisoma vizuri, Wanefili ni Watoto wa Anaki.Hesabu 13:33. waanaki bila shaka wametokana na uzao wa Kaini,kwani hao walikuwa kinyume na taifa la Mungu,Israel.

  Tusibahatishe Wapendwa Biblia inatoa taarifa kuwa, Hawa na Hawa tu ndiye aliyempatia Adam uzao. Na watoto wake ni watatu ambao ni Habili, kaini na Sethi!Mwanzo4:25-“Adamu akamjua MKE wake tena,akamzaa….Sethi…maana alisema, MUNGU AMENIWEKEA UZAO MWINGNE MAHALI PA HABILI…”

  Maneno yenye herufi kubwa ni ushaidi kuwa Adam hakuwa na mke wa pili!

  3.pia kumbumka Ibrahimu na Sara.

  Mwanzo16:1-6.Inaeleza kisa cha Sara na Ibrahimu.ambapo kutokana na utasa Sara alimshawisì ibraimu ampatie uzao kupitia mjakazo wao Hajiri! Kama ingekuwa ni mapenzi ya Mungu wala abraham asinge ngoja aambiwe na mkewe bali angejitwalia tu. na biblia inasema. “Abrahamu akaisikiliza sauti ya Sarai”. mwan16:2b.Sio “sauti ya Mungu”. Ikumbukwe kuwa: Hata uasi wa mwanadamu pale edeni ni matokeo ya “Adam kuisikiliza sauti ya Mkewe”.!! Ajabu iliyoje jinsi ninyi wanawake mnavyotukosesha! Nawewe Mage kupitia hapa SG unataka utukoseshe,na hadi sasa umeshajipatia kama wawili.Ila mimi nasema , Hadanganywi mtu Hapa!!

  Lesson1 Summary:Umeona Magreth na supotas wako, Kuoa zaidi ya mke mmoja ni desturi ya Kikaini/Kipagani na ni matokeo ya:

  1.”..kutoka mbele ya macho ya BWANA” yaani kukataa uongozi wa BWANA na

  2.”kuisikiliza sauti za wanadamu”. Km Adam na Abraham walivyowasikiliza wake zao wakaingia dhambini

  Plz,nawe usifuate mkondo huo huo kutudanganya.

  Baada ya mifanö iyo miwili toka Agano la kale,nakupa nafasi upumue,kisha nakujia mara na mifano toja agano jipya!

  MBARIKIWE Nyote in Jesus Name.

  ……..Inaendelea…….

 49. Neno la Mungu ni Neno la wakati, linatosha kwa wakati uliopita, kwa wakati uliopo na kwa wakati ujao. Yapo mambo yaliyoachwa yawe hivyo yalivyokuwa kwa wakati wake. Biblia inasema kuwa, Roho huyafumbua mafumbo ya Mungu, na pia Neno linaendelea kusema kuwa Mambo ya Roho hujulikana kwa waliozaliwa katika Roho na yale ya Mwili hujulikana na waliozaliwa katika Mwili! Kwa maana hiyo haishangazi mtu akisema Yesu hakukataza wanaumme kuwa na Wake zaidi ya mmoja!

  Biblia inamtaja Yesu kuwa ndiye Mungu, na kama yeye ndiye Mungu, na tayari kesha sema kuwa “Musa aliwaruhusu kuwaacha “WAKE ZENU” kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu. Lakini tangu mwanzo haikuwa hivyo.” Utasemaje kuwa Biblia haikatazi ndoa za wake wengi? Mimi naona watu wengi hawaelewi vipindi vya Neno kwa wakati wake, kipindi cha sheria na kipindi cha Neema. Nasema hivyo kwa sababu, Yesu moja ya kazi kuu ya kumleta hapa Duniani ni kuja kuitimiliza Torati. Ikiwa Torati kupitia Musa ilikubali uwepo wa Taraka na wake wengi, Yesu kaja ambaye ndiye Bwana wa hiyo Torati na ndiye aliye kuja kuitimiliza na kusema kuwa, “Talaka haikuwa mpango wa Mungu, ilisababiswa na ugumu wa mioyo ya watu” na ndiye huyo huyo aliyesema kuwa, mpango ulikuwa, “Mke mmoja na Mme mmoja” sasa hapo kuna ubishi gani?

  Kitu kingine ninachokiona hapa kama ni kutoelewa, na hivyo kusababisha mkanganyiko wa pili ni kuwa, Watu wengine wanadhani kuwa Talaka hufuta mtu asitambulike kuwa alishawahi kuoa kabisa katika maisha yake, au kufanya iwe mwanamke huyo hajapata kuolewa kabisa ati kisa anatalaka! Kutokuelewa alichokisema Yesu juu ndoa na taraka ndiyo sababu kuu ya mkanganyiko huu, ni kama mchangiaji mmoja amesema hapa kuwa –nanukuu,

  “Yesu alichosema ni kwamba Musa aliwaruhusu kuwaacha wake zao kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao. “…..Yesu akawajibu, “Musa aliwaruhusu kuwaacha “WAKE ZENU” kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu. Lakini tangu mwanzo haikuwa hivyo. Mimi nawaambia, ye yote amwachaye mkewe isipokuwa kwa sababu ya uasherati naye akaoa mke mwingine, anazini.” Naye amwoaye yule mwanamke aliyeachwa pia anazini.” ……Yesu alichokuwa anafundisha ni kwamba hatutakiwi kuwapa talaka wake zetu. Uwe na mke mmoja au zaidi ya mmoja hutakiwi kutoa talaka ili upate ruhusa ya kuoa mwingine. Ukioa mwingine UNAZINI. Na atakayeoa mke aliyeachwa naye ANAZINI……TALAKA ni MWIKO katika Ukristo.” Mwisho wa kunukuu.

  Ukimtazama mchangiaji huyu, utaona kuwa watu, wanajua kuwa Talaka hufuta historia ya ndoa, ukioa na ukatoa talaka unakuwa hukuwahi kuoa! Kinachosemwa na Yesu hapa ni kuwa, ukimwacha mke iwe kwa hiyo talaka iliyokubaliwa na Musa, na kuoa tena, kwanza utakuwa umefikisha wake wawili kwa maana ya ule usemi wake kwamba “hapo mwanzo haikuwa hivyo, Mungu aliumba mme mmoja na mmke mmoja,….nao watakuwa mwili mmoja” Lakini pia, ni vilevile ukitoa talaka kwa mke naye akaonekana kuwa ameachika, mtu atakaye muoa huyo aliyeachwa, mmoaji atakuwa amezini sawa na mke aliyeachwa naye atakuwa amezini! Kwanini? Kwanza Yesu katika hilo anasema “aliyekiungansha Mungu mwanadamu asikitenganishe” pili, Talaka haifuti historia ya kuwa mtalaka kwa kumaanisha kuwa mtalikiwa hakuwa na ndoa maishani mwake, na kama Aliisha wahi kuolewa ama kuoa, basi alichokiunganisha Mungu mwanadamu asikitenganishe; kwa maana hiyo mtalaka Yule huwa bado mke ama mme wa mtalikiwa!

  Sasa, kwakuwa Yesu ndiye Mungu, na ndiye aliyekuja kuitimiliza Torati, na diye aliyesema kuwa, mpango wa Mungu hapo mwanzo ilikuwa Mme mmoja kwa Mke mmoja, na kwamba SABABU YA UGUMU WA MIOYO YENU, Musa akawaruhusu mtoe Talaka, basi, hapa ni wazi kuwa hatakiwi, kuongeza mke kwa kupitia talaka. Inafaa pia kutambua kuwa, aliokuwa akiongea nao Yesu ni waliokuja “KUMJARIBU” na ukumbuke mjaribuji ni shetani, yeye ndiye aliyemjaribu jangwani, na hapa tunaona tena kaja akita kumjaribu ndivyo Biblia inavyosema! Lakini ukirudi katika kitabu cha Yohana utaona kuwa, hao Mafalisayo, ndiyo aliokuwa akiwaita wana wa Nyoka! Kwa maana hiyo wana wa nyoka ndiyo hasa waliokuwa wakiitetea hiyo sheria ya kuwa na wake zaidi ya mmoja, kwa kisinzio cha Talaka, eti iwe kwamba, kwakuwa mme kampa mke Talaka, basi hana mke na hivyo atakapokuwa ameoa ahesabike ana mke mmoja! Lakini Yesu aliiweka sawa hiyo kuwa, ukitoa talaka mke huyo aliyepewa talaka ukimuoa umezini, kwanini? Kwakuwa yungali mke wa mtu, kwa maana ya kuwa Mungu alichokiunganisha, na Yule aliyetoa talaka naye akioa amezini kwa maana hiyohiyo kuwa yeye yungali mme wa mtu na pia mke huyo mpya ni wapili, kinyume na mpango wa Mungu kuwa, mme mmoja kwa mke mmoja. Vilevile yeye (mme) ndiye huwaacha wazazi wake na kutafuta mmke ili asababishe kuwa mwili mmoja! Unaona kitu hicho?!

  Nahitimisha kwa kusema kuwa ukitoa taraka na kuoa mke mpya, hata kama aliyeolewa nawe kwa mara hii ni ka-Binti kigoli, binti huyo atakuwa anazini na mme wa mtu nawewe uliyeoa unakuwa umeongeza ki-mke cha pili na kwa hiyo nawe una MOYO MGUMU wa Kifalisayo na kuikataa sheria ya Mungu isemayo “Mme mmoja kwa mke mmoja”! Tangu mwanzo tumekwishaona kuwa waoaji wenyekutaka wake wawili wawli na wenyekutetea hilo wanaanzia kwa Lameki mwana atokanaye na Kaini mwasi, na ndiyo walioliomba hilo kwa Musa. Yesu anasema wanaume kama hao ni wenye Mioyo migumu, na ni haohao waliokuja kumjaribu Yesu, nao wanatokana na mjaribuji wa mwanzo ambaye ni shetani. Na mafalisayo waliokuwa wakijiita wana wa Ibrahim, Yesu aliwaita wanawa nyoka! Sasa tujiulize, watu wanaposimamia mambo na sheria zilizoachwa kwa ajili ya wana wa nyoka, je, wao ni akina nani?! Samahani lakini kama kuna jambo ama neno kali nimetumia.

  “Ufahamu ni chembe ya uhai!”

 50. Lamso,
  Umesema jambo jema sana. Hata mimi sidhani kama ni jambo jema kumbeza dada yetu Magreth. Ninavyomfahamu Magreth, ni miongoni mwa akina dada mahiri wa maandiko hapa SG. Aidha, kama mwanamke ni jambo gumu sana kwake yeye kushabikia ndoa za wake zaidi ya mmoja!! Hata wanawake wa Kiislamu ukiwahoji, huwa hawapendi kabisa pamoja na kwamba dini yao inaruhusu jambo hilo. Kwa mawazo yangu, nina imani kabisa dada Magreth, kaileta hoja hii kwa ajili ya ama yeye au watu wengine kujifunza. Na itapendeza sana tukabaki na hiyo dhamira ya kujifunza hasa kwa vile amepata wa kumuunga mkono kwenye hoja yake hii.
  Hebu tushambulieni mada badala ya kushambulia watu.
  Bwana awabariki sana.
  Siyi

 51. Wapendwa, michango kama ya akina kaka Milinga inajustfy hoja hii kuwepo na si vema kumbeza dada Magreth ukizingatia watu wengi wanajifunza kupitia hapa. Ni hoja nzuri kuijadiri nami nitarudi hivi punde kwa ajili ya kuchangia!

 52. Nadhani kuna kitu Margaret unataka kuhalalisha lakini huwezi kufanikiwa. Soma Mt 19 ili ujue kuwa kuoa mke wa pili ni dhambi

  Sent from my Huawei Mobile

 53. KUOA WAKE WAWILI??

  Ukweli ni kwamba maandiko hayajasema idadi ya mwenza wa maisha. Hata hivyo mada hii ni tata sana. Huwezi ukaifundisha kwa kanisa la leo ukaeleweka hata ungekuja na maandiko lukuki. Maandiko siyo hoja. Hoja ni mapokeo ya kanisa la Agano Jipya.

  Pamoja na kwamba hapo kale enzi za manabii kuanzia akina Nuhu na wengine wengi, wanaume walikuwa wanaoa zaidi ya mke mmoja. Pamoja na ukweli huo mapokeo ya kanisa la Agano Jipya yameendelea kuwa mke mmoja kwa mume mmoja.

  Kanisa la leo limekuwa na maelezo yanayotumika kukataza mume kuoa zaidi ya mke mmoja. Kwanza wanasema Kama Mungu angekuwa amepanga iwe hivyo Adam asingepewa mke mmoja Eva. Hata hivyo hoja hiyo inakosa ukweli kwa sababu kulikuwepo watoto waliozaliwa nje ya Eva walioitwa Wanefili au majitu. Nadhani hakuna aliyewahi kujiuliza hao wana wa manefili walizaliwa na nani kama siyo Adam? (Mwanzo 6:4)

  Hoja nyingine inayotumiwa kukataza kanisa lisijiingize kuwa na ndoa za mitaala ni pale Yesu aliposema, Mwanaume atamwacha baba na mama yake naye ataambatana na mkewe nao watakuwa mwili mmoja (Mt. 19:1-20). Hapa walimu wa maandiko wanasema kwamba mume na mke wanapooana wanakuwa mwili mmoja. Wengine husema kabisa kwamba 1 + 1 = 1. Yaani mume jumlisha mke unapata mwili mmoja. Hapa sasa inahitaji watu wenye kuelewa maandiko ili waeleze maana halisi ya andiko hilo kama limezuia mume kuoa zaidi ya mke mmoja?

  Hivi ukiwa umeoa mke mmoja unakuwa mwili mmoja naye kiukweli au ni kisaikolojia tu ndo munakuwa mwili mmoja? Mbona bado tunaendelea kuwa watu wawili tena wenye mitizamo na hisia tofauti? Mbona mume anaweza kusafiri mbali na mke na hawawi pamoja kila saaa kimwili bali wako pamoja kifikra au kimawazo tu?

  Kwa hiyo kusema kwamba mke zaidi ya mmoja inakubalika kimaandiko huenda ikawa ngumu sana kueleweka. Ukichunguza maandiko hautapata andiko linalosema kuwa kuoa mke zaidi ya mmoja ni dhambi. Bali utapata maandiko yanayokataza kutoa talaka.

  Yesu aliwakataza wafuasi wake Kutoa Talaka. Hii ilikuwa siku ile walipomuuliza kama ilikuwa sawa kumfukuza mke kwa kila sababu. Yesu akawajibu kuwa siyo. Mungu hakukusudia iwe hivyo tangu zamani. Mungu alikusudia watu waishi pamoja hadi kifo kiwatenganishe. Kwa hiyo YESU alikataza kutoa TALAKA siyo kuoa mke wa pili au wa tatu, nk. Watu wanapaswa wasichanganye kukataza kutoa talaka na kukataza kuoa mke zaidi ya mmoja. “……Baadhi ya Mafarisayo wakamjia ili kumjaribu wakamwuliza, “Ni halali mtu kumwacha mke wake kwa sababu yo yote?’’ (Mathayo 19:3).

  Utaona kwamba wao walitaka wawe wanatoa talaka kwa wake zao kwa kila sababu hata zile zisizokuwa na msingi. Ukisoma utaona Yesu aliwajibu kwamba Musa aliwaruhusu watoe talaka kwa shingo upande kwa sababu tangu mwanzo haikuwa hivyo. Tazama Yesu alivyowajibu;

  Yesu Akawajibu, “Je, hamkusoma kwamba hapo mwanzo Mungu aliwaumba mtu mume na mtu mke. Naye akasema, ‘Kwa sababu hii mtu atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja?’ Hivyo si wawili tena, bali ni mwili mmoja. Kwa hiyo kile alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.’’ Wakamwuliza, “Kwa nini basi Musa aliagiza mtu kumpa mkewe hati ya talaka na kumwacha?’’ (Mathayo 19:4-7)

  Ukifuatlia kuanzia mstari wa 8 utaona jinsi Yesu alivyowajibu swali hilo. Kwamba Yesu hajakataza mwanaume kuwa na mke zaidi ya mmoja. Yesu alichosema ni kwamba Musa aliwaruhusu kuwaacha wake zao kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao. Hebu soma hapa tena “…..Yesu akawajibu, “Musa aliwaruhusu kuwaacha “WAKE ZENU” kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu. Lakini tangu mwanzo haikuwa hivyo. Mimi nawaambia, ye yote amwachaye mkewe isipokuwa kwa sababu ya uasherati naye akaoa mke mwingine, anazini.” Naye amwoaye yule mwanamke aliyeachwa pia anazini.”

  Ukisoma vizuri utaona kuwa Yesu alisema “WAKE ZENU”. Neno hilo laweza kumaanisha wake wengi kwa mtu mmoja au wake zao kwa maana ya wingi wa wanaume waliokuwepo.

  Yesu alichokuwa anafundisha ni kwamba hatutakiwi kuwapa talaka wake zetu. Uwe na mke mmoja au zaidi ya mmoja hutakiwi kutoa talaka ili upate ruhusa ya kuoa mwingine. Ukioa mwingine UNAZINI. Na atakayeoa mke aliyeachwa naye ANAZINI.

  Kwa hiyo kuoa mke aliyeachwa isipokuwa kwa sababu za KIFO peke yake UNAZINI. Kama wewe umeokoka ukiwa na wake wengi unapaswa kuendelea kuishi nao. Hupaswi kuwapa talaka kisa eti umeokoka. TALAKA ni MWIKO katika Ukristo.

  Kwa hiyo, naweza kuhitimisha kwa kusema maoni yangu kuwa Kuwa na wake wengi siyo DHAMBI. Kama umeoa wake zaidi ya mmoja na wako kihalali kabisa kwa mujibu wa taratibu za mila na desturi au sheria za nchi na kisha ukaokoka ukiwa na wake zaidi ya mmoja, hupaswi kuwaacha wake zako. Kwa mfano kama wewe ulikuwa mmasai au mgogo au mjaluo au mwislam ukawa umeoa wake wengi kwa mujibu wa imani yako au kabila lako na sasa umeingia kwenye imani ya Ukristo, UKWELI NI KWAMBA WAKE ZAKO UNAPASWA KUENDELEA KUISHI NAO KAMA WAKE ZAKO HALALI. Itakuwa dhambi kuwapa TALAKA kisa eti sasa umeokoka.

  Mwenye sikio amesikia na mwenye macho amesoma na asomaye na afahamu.

 54. Mpendwa Magreth, na wengine wote.
  Ikiwa wapo wengi watakushangaa Magreth, mimi si mmoja wa hao. Sikushangai na sitashangaa mtu yeyote katika hili. Wanaume wengi hujihusisha sana na wake wengi kwa namna mbalimbali zile wanazojua na kudhani kuwa ni harali na zile zinazojulikana kuwa si harali, na katika mambo haya ya kimahusiano pia kuna uzinzi na uasherati, japo kwa kiwango chote asilimia mia watu wamezoea na pengine kuharalisha “UMALAYA” kwa maelezo ya u-‘Boyfriend na Girlfriend’ hata wanaojiita wameokoka wamo katika mkumbo huu kwa sana wameukumbatia na kuuita ustaarabu! Sikio la kufa halisikii dawa Magreth, ukiwa na gonjwa hili la kutosikia Injili ya kweli ya Yesu Kristo, utamaliza Pharmacy matokeo ni ziro hiyo ndiyo maana ya mimi kusema sina sababu ya kushangaa!

  Unajua, Biblia inasema “Mwana hafanyi jambo ambalo hakumuona Baba yake akilifanya” kwa hiyo, swala la wake zaidi ya Mmoja linafanywa na watoto wa NYOKA! Maana yeye aliwalithisha wanae hilo, ukisoma katika Mw. 4:19, tunaona kuwa, Lameki wa ukoo wa Kaini, ambaye alitoka mbele za uso wa Bwana (Mw.4:16), ndiye mwanzilishi wa Ndoa ya mke zaidi ya mmoja, lakini kutokana na uongo wa shetani watu wengi wanaliona jambo hilo kuwa zuri na lina faa kama suruhisho la utata wa ndoa, lakini madhala ya jambo hilo limeelezwa katika kisa cha Mtawala Selemani (katika Wafalme 11:1 na kuendelea.).

  Labda niingie kwenye Maada yenyewe kwa kusema hivi, yapo maandiko mengi tu yanayozungumza kuwa NDOA NI YA MME MMOJA na MKE MMOJA! Sikiliza: Neno la Mungu ndiyo Mungu mwenyewe na huwezi kulitofautisha Neno lake na yeye mwenyewe. Tukisoma katika Neno hilo tunaona kuwa , katika Mw. 2:21- inasema, 21Hivyo BWANA Mungu akamfanya Adamu kulala usingizi mzito, naye alipokuwa amelala akachukua moja ya mbavu zake akapafunika mahali pale kwa nyama. 22Kisha BWANA Mungu akamfanya mwanamke kutoka kwenye ule ubavu aliouchukua kutoka kwa huyo mwanaume, akamleta huyo mwanamke kwa huyo mwanaume. . 23Huyo mwanaume akasema, “Huyu sasa ni mfupa wa mifupa yangu na nyama ya nyama yangu, ataitwa ‘mwanamke,’ kwa kuwa alitolewa katika mwanaume kwa sababu hii mwanamme atamwacha Baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe nao watakuwa mwili mmoja.

  Hivyo ndivyo Mwanzo ilivyokuwa, na hata Yesu mwenyewe alipokuja hapa Duniani alikutana na swala hili tunalolizungumza leo hapa, lakini naye akawakumbusha watu jinsi mpango huo ulivyokuwa umepangwa uwe, hivyo akawarudisha ilivyokuwa hapo mwanzo! Sikiliza; Biblia katika Marko 10:2-9 twasoma hivi, “2Baadhi ya Mafarisayo wakaja ili kumjaribu kwa kumwuliza, “Je, ni halali mtu kumwacha mke wake?” 3Yesu akawajibu, “Je, Mose aliwaamuru kumwacha.”
  5Yesu akawaambia, “Mose aliwaandikia sheria hiyo kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu. 6Lakini tangu mwanzo wa uumbaji, ‘Mungu aliwaumba mume na mke. 7Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe na hao wawili, watakuwa mwili mmoja.’ 8Kwa hiyo hawatakuwa wawili tena bali mwili mmoja. 9Basi, alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe” unaona? Mke mmoja Mme mmoj ndiyo Mwili Mmoja. Je, wake wawili Mme mmoja ndiyo mwili wa namna gani na unatoka katika andiko gani la Mungu?

  Haya ukienda mbele hata viongozi ama wafundishaji na wenye kusimamia Kanisa katika 1Timotheo3:1-2 inaagizwa hivi, “Hili ni neno kweli, kwamba mtu akitamani kazi ya askofu, atamani kazi nzuri. 2Basi, imempasa askofu awe mtu asiye na lawama, mume wa mke mmoja,…….” Magreth, kuna mengi tu naweza kusema juu ya hili, ila acha tu niishie hapa kwa leo, ikibidi naweza kurudi tena, ila Neno likikaa kwa wingi shetani hawezi kukudanganya kama anavyokudanganya kuwa neon la Mungu linaunga mkono ndoa za mke zaidi ya mmoja!

  “Ufahamu ni chembe ya uhai!”

 55. Mmmh,
  Ha ha ha ha, Magreth!!
  Ni wewe ninayekufahamu kabisa kwa hapa SG au Magreth mwingine? Duuu, anayway niamini kuwa ni wewe na niamini kuwa umeleta mada hii kwa lengo la kujifunza na kuwafunza wengine. Nimefurahi na kucheka sana nilipoona umeleta mada yenye changamoto kubwa hasa kwa kipindi hiki. Tena ni changamoto kwa makanisa yote ya Kikristo. Bwana akubariki sana Magreth.
  Aidha, nimpongeze ndg Ngullo kwa mchango wake mzuri. Kimsingi, mchango wake ni too Biblical. Bwana ambariki sana.
  Hoja ya kuwa na wake zaidi ya mmoja, siku hizi imetanza watu wengi sana. Kwenye kanisa ninalosali mimi, wanawake walioolewa na mume mmoja, wanaruhusiwa kuwa waumini wa kanisa waliobatizwa na pengine hata kupewa majukumu kama vile ya ushemasi na kadhalika (kwa sababu leo kuna mashemasi wanawake). Mwanaume aliyewaoa wanawake hawa wengi, yeye haruhusiswi kubatizwa na kuwa muumini kama wake zake. Mwanaume akitaka kuwa mmumini, yeye inabidi aachane na wake wengine wote na kubaki na mmoja tu (yule mkubwa). Sasa hoja inakuja, kwa nini wanawake wengi (zaidi ya mmoja) waruhusiwe kubatizwa na kuwa waumini wa kanisa na huku mume wao akataliwe??? Mbona dhambi, inakuwa kwa mwanaume tu? Wanawake wanapoolewa na mume mmoja, wao hawazini? Na mpaka sasa kuna majadiliano juu ya jambo hili na watu wengine wanatoa mifano hai kabisa ya kuhalalisha muumini kuwa na wake zaidi ya mmoja. Mf. Mzee wa kimasai mwenye wake wengi waliozeeka ambao wanaishi kwenye boma moja, mzee huyu anapotaka kuwa muumini, kwa kanuni za Kikristo, inabidi aachane na wake zake wengine wote (ambao ni wazee-vikongwe) na kubaki na kikongwe wa kwanza tu. Je, hawa vikongwe wasiojiweza, wataenda wapi? Watatunzwa na nani? Mawazo kama haya, yanaweza kupigiwa kura mwisho wa siku, halafu ikakubalika mwanaume kuwa na wake zaidi ya mmoja. Na ikipitishwa hivyo, wanawake nao watadai kuwa na mume zaidi ya mmoja otherwise utakuwa ni unyanyasaji na ukandamizaji dhidi ya wanawake n.k., jambo ambalo ni kinyume na sera na maazimio ya Umoja wa Mataifa juu ya haki za Binadamu. Na hii ndiyo kazi ya mpinga Kristo. Michombezo ya ibilisi, huja kwa namna ya kiujanjaujanja na kificho Fulani. Na agh. watu hujikuta walishaingia ndani wanaelea. Hatari iliyoje!! Mungu atusaidie tuwe na macho ya kuona haya!!
  Kwa mujibu wa Biblia, ndoa ni ya mume mmoja na mke mmoja tu basi. Ngullo amesema vizuri. Hata kipindi cha mitume, Mf. Paulo alitaka viongozi wa dini wawe ni wale waliongoka (waongofu), wale wanaoifuata Biblia kwa kiasi kikubwa. Ndiyo maana alisema, kiongozi sharti awe ni mume wa mke mmoja, mtu asiyependelea ulevi n.k. Hoja ya Paulo haikuwa kurusu wanaume wasiokuwa viongozi waoe zaidi ya mke mmoja. Hasha!! Bali ulikuwa ni msisitizo wa baadhi ya vigezo vya mtu yeyote ambaye angechaguliwa kuliongoza kanisa. Wale watakounga mkono sera ya lusifa ya wanaume kuwa na wanawake wengi au kinyume chake, watambue kuwa, watakuwa wameuasi mpango wa Mungu wa tangu uumbaji. Na hilo ni jambo hatari sana!!
  Bwana atusaidie sana
  Siyi

 56. Biblia inasema kila mtu awe na mke wake mwenyewe pia mke wake mwenyewe 1kor7:2. Na sio waume au wake

 57. WAEFESO 5:31
  “KWA SABABU HIYO MTU ATAMWACHA BABA YAKE NA MAMA YAKE, ATAAMBATANA NA MKEWE NA HAO WAWILI WATAKUWA MWILI MMOJA.”

  1 TIMOTHEO 3:2
  “BASI IMEMPASA ASKOFU AWE MTU ASIYELAUMIKA, MUME WA MKE MMOJA,…”

  1 TIMOTHEO 3:12
  “MASHEMASI NA WAWE WAUME WA MKE MMOJA,…”

 58. mpendwa kwanza nikupongeze kwa mada uliyoleta nami nimepata kutoa elimu na kwa wengine
  kwanza niaanze na kueleza maana ya neno dhambi DHAMBI maana yake ni uasi juu ya maagizo,sheria za Mungu,na Neno la Mungu kwa ujumla wake sasa nije kwa maada yako kuoa mke zaidi ya mmoja ni dhambi ukitaka kujua ni dhambi nikurudishe kwenye historia ya uumbaji na adhabu Mungu ambazo ameshazitoa
  1.kwanza mpango wa Mungu alimuumbia Adamu mke mmoja kama ungekuwa ni mpango wake angemuumbia wake wengi ili awahihi kujaza dunia kwani Mungu si kigeugeu wa kubadilika badilika leo hivi kesho vile kama dini nyingine zinavyosema dini zao zinaluhusu kuoa wake zaidi ya mmoja huyo ni mungu gani sio aliye umba mbingu na nchi
  2.wakati wa gharika Mungu aliwaghalikisha watenda dhambi wote wakati wa kipindi hicho walikuwepo watu kama akina lameki.kama kuoa mke zaidi ya moja sio dhambi kwanini hao hawakupona?
  3. wakati wa agano la kale watu walikuwa wana oa na kuacha hata kwa kutoa talaka lakini nikwambie huo haukuwa mpango wa Mungu hata baathi ya viongozi kwa kipindi hicho waliingia kwenye dhambi hizo ndio maana Yesu anasema zamani za ujinga alijifanya haoni lakini sasa anaona kupitia mwana wake Yesu soma (matendo ya mitume 17:30)
  4. sasa tuone Yesu anavyo sema soma mathayo 19:1…12

  Mungu awabariki nitaendelea kutoa ufafanuzi

  nini mimi mtumwa wa Bwana Yesu stephen ngullo

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s