Unamwabudu Mungu kwa ajili ya nani?

Mama mchungaji Victoria Osteen ameibua mjadala kwa Wakristo wengi baada ya kuongea maneno yafuatayo hivi karibuni “Unapoabudu (na kumtii) Mungu, hatufanyi hivyo kwa ajili ya Mungu, tunafanya hivyo kwa ajili yetu, kwasababu hicho ndicho kinachomfurahisha Mungu”

Kutokana na mtazamo huu, Kwa maoni yako, Unamwabudu Mungu kwa ajili ya nani? Je ni kwa furaha yako? Unapoenda kanisani unaenda kwa ajili ya nani?

Sikiliza video hii kwa makini alivyosema:

 

Advertisements

12 thoughts on “Unamwabudu Mungu kwa ajili ya nani?

 1. Yona,

  Nani kasema anamwabudu Mungu kwa ajili ya kujifurahisha?

  Tuonyeshe ni kwa jinsi gani hilo fundisho ni la uongo kuliko kuanza tu kusema hizi ni siku za mwisho.

  Siku za mwisho zilishaanza hata kabla ya wewe kuzaliwa, kama ulikuwa hujui.

  Hakuna cha fundisho la uongo hapo, ni ufinyu wa kuelewa kwako tu!!

 2. Lwembe,

  Hujui maana ya faida? Au unataka mimi niseme maana ya faida ili iweje?

  Sema wewe maana ya faida kisha usema unatala kusema, nitakuelewa.

  Amen

 3. MIMI NAZANI SHIDA NI UELEWA WA MAFUNDISHO, MM NAABUDU KWAAJILI YA MUNGU NA SIO KUJIFURAHISHA. HZ NI SIKU ZA MWISHO TUJIHADHARI NA WAALIMU WA UONGO.

  “NOTHING IMPOSIBLE TO GOD“

 4. Sungura,
  Uki define “faida” itasaidia kuendelea kujadili, hata nadhani kwa hilo twaweza kufikia kuelewa pia “utukufu” ni nini!

  Asante.

 5. Lwembe,

  Unayemwambia hayo ni nani?

  Mungu alituumba ili tumwabudu kwa sababu alikuwa anahitaji kuabudiwa?

  Yes, tunamwabudu Mungu ktk roho na kweli, suala ni unaponwabudu ktk roho na kweli ni kwa ajili ya faida ya nani kama si ya kwako mwenyewe?

  Wewe unaongelea mambo ya choyo na kusema mpeni Mungu kilicho cha kana kwamba kuna mtu hataki kumpa Mungu ibada.

  Na suala la bikira Maria limefikaje hapa Lwembe?

  Tunapomwabudu faida ni ya kwetu, wa kwake ni utukufu.

  Sioni nini kigumu hapo.

 6. Hivi watoto wako uwapendao sana wasipokuheshimu, ni kweli kwamba HAUPUNGUKIWI???

  Ukijiona hivyo basi nenda kwa wataalamu ukaongee nao, utakuwa una tatizo!

  Wivu maana yake ni hitaji, na Mungu alipohitaji kuabudiwa ndipo akatuumba, alipohitaji kututunza ndipo akaruhusu shida, alipohitaji kutuponya ndipo akaruhusu magonjwa!!

  Acheni ujeuri, vya Mungu mpeni; hiyo ibada inayo ambatana na utii wa Neno lake kulingana na wakati na si mambo ya kujitungia madude yasiyoeleweka, ukiulizwa ni wapi mitume walifundisha “tumuombe Mama Bikira Maria bikira wa milele atuombee” au ni wapi mitume walifundisha kuwa Yesu ni Mungu Mwana; mnabaki mnang’aa ng’aa macho tu kwa Choyo cha Kumnyima Mungu Ibada iliyo Safi na mwisho tunajidanganya kuwa eti Mungu hapungukiwi; sasa kama ni hivyo, kwanini anasema anawatafuta hao watakao mpa ibada safi hiyo iliyo ktk roho na kweli? Amechoka na madude ya mwilini yasiyo na maarifa, sijui sabato, wengine wanajipandisha mori kwa kutiririsha “Asante Yesu” x 666 nk; Yote hii ni choyo kilichofichika ktk hila!

  Nawatakieni Ibada njema itakayo mtukuza Mungu, maana Yeye anapendezwa na hiyo !

 7. Victoria alisema kitu kizuri sana. Tunapoabudu Mungu, lengo si kumfurahisha Mungu maksudi tuwe karibu naye, naye atukaribie.

  Yesu akasema “Luka 19:40 Akajibu, akasema, Nawaambia ninyi, wakinyamaza hawa, mawe yatapiga kelele.”

  Hence, Sisi kuabudu ni vizuri, lakini Mungu hapungukiwe wakati hatumuabudu. Tunapomuabudu tunatafuta kitu kwake. Yawezekana ni upako, msaada kwa safari ya kwenda mbinguni, nk… Yote ni kwa faida Yetu.

  Kuna watumishi wanaosubutu kumwambia Mungu eti “Mungu, kama hunipe kitu fulani sitakutumikia tena”. Heh, jamani, unapawaza unamtumikia, ni wewe unajitumikia kwanza. Na ukiacha kumtumikia ni wewe unapoteza.

 8. Alichosema Victoria kiko sahihi bila chenga. Ila ni shule ya kiwango cha juu kidogo.

  Ni sawa na kuulizwa huwa unafunga kwa ajili ya nani?
  Usipofikiri vizuri unaweza kudhani kufunga kwetu no kwa ajili ya Mungu,lakini ukweli ni kwa ajili yetu wenyewe kutiisha mwili ili kuwa katika kusikia vema toka kwa Mungu.

  Mungu yeye yuko vilevile ufunge usifunge.
  So huwa tunamwabudu Mungu kwa ajili yetu wenyewe.

 9. Mimi naona watu hawakumuelewa Victoria ila yupo sahihi. Maana unapomuabudu Mungu au kushika sheria zake na kuzifanya FAIDA NI YAKO WEWE. UKIMWABUDU MUNGU NI KWA USALAMA WAKO, FAIDA INAKURUDIA WEWE MWENYEWE. UKIMWABUDU MUNGU UTAPATA FURAHA/RAHA NAFSINI MWAKO NA MAISHANI MWAKO. USIPOMWABUDU MUNGU , Yeye hana hasara maana anaweza kuinua hata mawe yamsifu! Tatizo la watu wanapenda kujudge bila kufikiria kiundani!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s