Tunatakiwa kutazama kwa macho ya rohoni! – Kamugisha

kanisa

Wapendwa katika BWANA YESU KRISTO.

Ni neema kubwa kutoa sadaka yangu katika blog ya INJILI HALISI.Binafsi sikujua kama kuna siku nitatoa hii sadaka kwa wale wote wenye DHAMIRA YA KUISHI NDANI YA UNYENYEKEVU HALISI yaani unyeyekevu wa YESU (Wafilipi 2:3-4).

Lakini Mungu aliye hai anayetangaza mwisho kabla ya mwanzo alijua ya kwamba UJUMBE WAKE  UTATUFANYA TUANZE KUISHI NDANI YA UHURU HALISI yaani uhuru wa Roho Mtakatifu(2Wakorintho 3:17).

 Kiini na chanzo cha kutamani na hatimaye kuingia ndani ya mioyo ya wanyenyekevu wote duniani ni mjadala wa mwaka 2012 kuhusu nukuu ya nabii TB JOSHUA ambayo alitabiri ajali ya ndege iliyotokea Kenya na kumuua marehemu George Saitoti.

Katika mjadala huo ambao ulionekana kuwa na mvutano mkubwa huku mioyo ya washiriki ikivua nguo na kubaki uchi kabisa, Roho Mtakatifu amenifunulia mengi makubwa na magumu ambayo sikuyajua (Yeremia 33:3).Kabla ya kueleza kile ambacho ROHO WA MUNGU

ALIYE ameniongoza kusema naomba katika hekima na unyenyekevu wote kutoa shukurani zangu kwa washiriki wote nikiwataja baadhi kwa majina kama ifutavyo: Pelesi,Mwangomo,Amina,Robert.Milinga,Stella,Gwamaka,Haggai,CK Lwembe,Nduta,John Paul, Edwin Seleli,Orbi,Ivan John, Eucalyptos, James, Mabinza LS, Primi Mosile,Daniel J,John Haule,Jerry na Sam. Mungu aliye hai awafiche ndani ya moyo wake.

Maisha ndani ya Kristo ni maisha yenye changamoto katika ulimwengu wa Roho na siyo ulimwengu wa mwili!!Kuna mstari mwembamba mno unaotenganisha kati ya maarifa ya Mungu na maarifa ya shetani. Ni mstari unaotenganisha na kutofautisha upendo ulio kufa na upendo unaoishi.

Ni mstari unaotenganisha na kutofautisha watumishi wa shetani na watumishi wa Mungu,Huo mstari ni NENO LA KRISTO NDANI YA ROHO MTAKATIFU

NA ROHO MTAKATIFU NDANI YA NENO LA KRISTO. Kwa mtazamo mpana wa unyenyekevu ni lazima tukubali kwamba sisi bado ni VIPOFU NA VIZIWI

WA MAISHA YA KIROHO(ISAYA 42:18-20).Tunahitaji kuendelea kunyenyekea sana ili TUWEZE KUTEMBEA NA MACHO SABA YA MUNGU(UFUNUO 5:6,ISAYA 11:2).

Tukiweza kuingia ndani ya Roho (macho) saba za Mungu KILA KITU KITAKUWA WAZI KABISA na yote yaliyokuwa yamefichika yatajifunua yenyewe na zaidi ya yote tutapata UTULIVU WA ROHO MTAKATIFU katika kufikiri, kunena na kutenda(1 Yohana 2:20.27,Luka 12;2).Mambo ya rohoni hujadiliwa rohoni japo yanafundishwa

katika ulimwengu wa mwili.WATUMISHI WOTE WA SHETANI WANAJULIKANA NA WATUMISHI WOTE WA MUNGU WANAJULIKANA NI KANUNI YA MUNGU KWAMBA MBWAMWITU NAO WASAIDIE KUTANGAZA INJILI YA YESU DUNIANI(WAFILIPI 1:15-18).MOTO WA YESU UNANIFANYA NITABASAMU!(LUKA 12:49-51)

Mnyenyekevu anayetafuta unyenyekevu ulio hai,

Dickson Kamugisha

Cape Town, SOUTH AFRICA.

Advertisements

13 thoughts on “Tunatakiwa kutazama kwa macho ya rohoni! – Kamugisha

 1. Mtumishi CHEMO
  Mungu aliye hai azidi kukubariki sana!

  Nimesoma kwa muongozo wa ROHO MTAKATIFU mambo ambayo
  umemshauri Mtumishi Kamugisha.Ni kweli kwamba katika baadhi
  ya makala zake chache amejisahau kuweka AYA(Paragraph) ili kuwaraisishia wasomaji na hii ni muhimu sana kwa sababu anaandika
  mambo mazito TENA KWA KUTUMIA CHAKULA KIGUMU pale
  inapobidi .

  Binafsi sijaona utangulizi wowote ambao ametoa vitisho vinavyojenga
  hofu au kumfanya Mungu aonekane kuwa asiyekaribika na kuchukulina
  na madhaifu yetu.Nakubaliana naye kwamba wateule ni wanyenyekevu
  wanaotakiwa kutafuta kwa bidii kuishi ndani ya UNYENYEKEVU ULIO HAI.Kamugisha anaongozwa kuandika makala ambazo zinahitaji
  tafakari ya muongozo wa Roho Mtakatifu.Rudia kusoma makala zake
  zote hasa katika mada hii utakutana na unyenyekevu wa ajabu sana!

  Mungu azidi kumpa neema mtumishi kamugisha lakini pia amtie nguvu
  na kumpa ujasiri wa kufichua mambo ya Rohoni kwa HEKIMA YA
  ROHO MTAKATIFU.Makala ya TUNATAKIWA KUTAZAMA KWA MACHO
  YA ROHONI imebeba hekima ya ajabu sana ya jinsi mteule anavyoweza
  kufichua undani wa rohoni kuhusu mtumishi fulani kwa kuhepuka kujihesabia haki,kuhukumu au kuropoka kwa jinsi ya mwilini.Wenye hekima ya rohoni watakuwa WAMEELEWA SANA TENA KWA UNDANI
  kuhusu kile ambacho Kamugisha AMEONGOZWA KUFICHUA.

  Mtumishi SUNGURA anaonekana kuielewa hii makala kuliko tunavyoweza kufikiria!Ndiyo maana ameuliza SWALI LA MSINGI SANA.
  Mungu aliye hai awabariki sana wale WOTE AMBAO WAMEELEWA
  KILE AMBACHO ROHO MTAKATIFU ndani ya Kamugisha AMEAMUA
  KUKIWEKA WAZI SANA!!

  Chemo wewe ni mtumishi upendwaye sana kama alivyo Kamugisha
  na wengine wanaoweka jitihada katika KUYATAFUTA MAARIFA YA YESU
  aliyoyaficha ndani ya unyenyekevu wake.Sasa ndiyo nimeelewa kwanini
  Mtumishi Kamugisha aliwahi kuongozwa kusema kuwa hizi ni nyakati
  ambazo unabii uliotolewa katika LUKA 12:1-2 UNATIMIA NA ZAIDI
  YA KUTIMIA!!

 2. Ndugu Kamugisha unajumbe nzuri, lakini presentation zako zinaniacha nje kwa jinsi unavyoweka tangulizi zinazomwonyesha Mungu kama asiyekaribika. asiyechukuliana na madhaifu yetu; yaani, so untouchable.

  Hivi kama Yesu wakati wa huduma yake duniani angekuwa ana present kwa namna hii, angewapata wenye dhambi kweli? Bila shaka angeanzia kwa mafarisayo ambao walijionyesha kuwa watakatifu sana kwa kushika torati. Unavyofanya nakuchukulia kama vile una makusudi ya kujionyesha kwamba upo katika roho sana; usifanye hivyo ewe upendwaye sana.

  Ingekuwa rahisi sana ku-present with boldness, the simple good news, whatever you have moja kwa moja tu, bila vile vikolombwezo vya kwenye utangulizi. Naona kama zina namna ya vitisho ambavyo havina uhusiano kabisa na Roho Mtakatifu; maana hakutupa roho ya hofu, bali Roho ya uwana.

  Jumbe fupi, zenye kulenga maada moja kwa moja zinawajenga wengi kuliko maneno mengi ya kujitia moyo na kujitambulisha binafsi.

  Pia toa nafafi ya aya ili kumpa msomaji vituo katika mtiririko wako.

  Kazi yako ni njema, na Mungu anakupendo mno kuliko unavyoweza kufikiri, uwe hodari tu na kazi yako njema.

  Barikiwa sana!

 3. hakika tusifikiri safar ya imani ni rahisi. tukumbuke kuwa ata Yesu mwenyewe kuna kupindi wanafunzi walimuacha ukiachilia wale 12 na alipowauliza wale 12 kama nao wanataka kumuacha Petro alijibu ” tuende wapi Bwana tukuache wewe, haya maneno ya uzima tutayapata wapi?” ndugu zangu tunamhitaji Roho mtakatifu atufundishe na kuamua mioyoni mwetu kwani wakati mgumu ndo wakati wa kuthibitisha imani ya mtu.

 4. EEH MUNGU NIREHEMU pale ambapo sikumpa Roho Mtakatifu kutawala ndani yangu.Naomba Roho wako atawale roho,moyo,mwili na nguvu zangu zote.

  Roho Mtakatifu naomba UFICHUE(LUKA 12:2).Roho Mtakatifu naomba ufundishe(1 YOHANA 2:27).Na UTUKUFU umrudiye yeye aishiye milele na milele-MSHAURI WA AJABU,MUNGU MWENYE NGUVU,BABA WA MILELE NA MFALME WA AMANI,BWANA WETU YESU KRISTO(ISAYA 9:6).

  ROHO MTAKATIFU NDANI YA NENO LA MUNGU NA NENO LA MUNGU NDANI YA ROHO MTAKATIFU maana yake ni kwamba hatuwezi kutenganisha kati ya Roho Mtakatifu na Neno la Kristo,NENO na ROHO hufanya kazi kwa kungojana ili washirikiane.NENO anapotangulia mahali inabidi amngoje ROHO na ROHO anapotangulia mnabidi amngoje NENO.Unaweza kuwa na NENO lakini kama huna upako wa Roho mtakatifu wa kulifunua hilo NENO hutalielewa.Unaweza kuwa na upako wa Roho Mtakatifu lakini huna NENO la kuunganisha na huo upako ili uvuke!USHIRIKIANO huu kati ya Roho Mtakatifu na NENO la Mungu unatufanya tupate ELIMU YA MAFUNUO YA NENO LA MUNGU badala ya ELIMU KAMA TAALUMA YA NENO LA MUNGU!Kinacholeta UKOMBOZI katika maisha ya wokovu ni mafunuo ya neno la Mungu ndani ya mioyo yetu na siyo taaluma ya neno la Mungu ambayo hubaki akilini tu.Roho Mtakatifu amebeba ROHO YA MAARIFA ambayo ndani yake kuna ROHO SABA ZA MOTO WA MUNGU(TAFAKARI-ISAYA 11:2,UFUNUO 5:6).Hizi ni roho ambazo zinaishi ndani ya wateule ambao wamekubali kuingia ndani ya UNYENYEKEVU WA YESU.Roho ya maarifa ya Yesu inaweza ikakufanya ulitambue jambo katika ulimwengu wa kimwili hata kabla hujaonyeshwa katika ulimwengu wa roho!Kwa mfano,inaweza kukuwezesha kumtambua mke au mume ambaye Mungu alikuandakia kwa kumuangalia tu mnapokutana!!Roho ya maarifa ya Yesu huwa unamuwezesha mtu kufanya mahesabu ya KUJULISHA NA KUTOA ili kutambua undani wa huduma fulani kama ni ya shetani au ni ya Mungu aliye hai.MACHO SABA YA MUNGU ndani ya mteule NI ZAIDI YA TISHIO KWA SHETANI NA WAJUMBE WAKE.

  Tunapozungumza habari ya MACHO NA MASIKO YA ROHONI tunazungumzia UHALISIA wa mteule wa Mungu kuona na kusikia maelekezo ya Mungu KATIKA ULIMWENGU WA ROHO WA NURU na pia kuona na kusikia HILA ZA shetani KATIKA ULIMWENGU WA ROHO WA GIZA(TAFAKARI-2 WAKORINTHO 4:18) .Sisi ni watu ambao tunaishi katika ULIMWENGU WA ROHO WA NURU na ULIMWENGU WA KIMWILI kwa wakati mmoja!Tunaweza pia kuingia katika ULIMWENGU WA ROHO WA GIZA kwasababu ya dhambi(kutokutii maagizo ya Mungu).Hata hivyo anayetuwezesha kuona,kusikia na KUELEWA AU KUTAFSIRI tunapokuwa gizani au nuruni ni ROHO MTAKATIFU.MBWAMWITU(wajumbe wa shetani) wanapochukua umiliki wa macho na masikio yako ya rohoni kupitia sadaka yako ya FUNGU LA KUMI,ndipo unapoanza kuwaona wao KATIKA ULIMWENGU WA ROHO WA GIZA wakikupa maelekezo kuhusu maisha yako ya kila siku!!Na hii ni kukujengea IMANI kwa mungu wao ambaye ni IBILISI-SHETANI.SADAKA inaenda na moyo wako maana yake inabeba na roho yako(TAFAKARI-MATHAYO 6:21).Kwahiyo mtumishi utakayempa roho yako(sadaka) ndiye utakayemuona katika ULIMWENGU WA ROHO akikupa maelekezo kwa niaba ya mungu wake.Wajumbe wa shetani wanaposhidwa kuchukua umiliki wa macho na masikio yako ya rohoni wanachofanya ni KUYAZIBA,na hapo unakuwa KIPOFU NA KIZIWI ROHONI.Unakuwa ukumbuki ndoto unazoota au hata ukikumbuka WANAKAMTA UFAHAMU WAKO USIELEWE KABISA mambo unayoyaona kwahiyo unakuwa unayatasiri tofauti na yalivyo na ROHO MTAKATIFU hawezi kukusaidia kwasababu umejikita ndani ya himaya ya shetani(TAFAKARI- ISAYA 42:18-20).Makanisa ya shetani yanaitwa MADANGURO na kwa sasa yamechukua zaidi ya asilimia 85 ya makanisa yote duniani!!

  TUNATAKIWA TUJIANDAE KWA AJILI YA UJUMBE WA HASIRA YA MUNGU JUU YA TANZANIA.Ni ujumbe mzito na wa kutisha ambao utaingia ndani ya mioyo yetu hivi karibuni.SIYO UJUMBE KWA AJILI YA WANADAMU(MBWAMWITU) WANAOISHI TANZANIA AMBAO NI WATANZANIA BALI NI UJUMBE KWA AJILI YA WANA WA MUNGU AMBAO NI WATANZANIA NA WALE WALIOKO NJE YA TANZANIA LAKINI HATIMA YA MAISHA YAO IPO TANZANIA.

  Mambo haya ili kuyapokea yanahitaji unyenyekevu wa kudhamiria kutoka moyoni.Mungu aendelee kutuficha ndani ya moyo wake.

 5. @Sungura wengi hapa wamekuwa wakijadili kwa kutumia concept ambazo ni abstract kueleweka lakini esther mushi na mimi tumekuja na mifano ya kile kinachoendelea kutendeka kwa viongozi wa dini.

  Kuna muhubiri alijizolea umaharufu lakini ameoa mke wa pili na kumwacha huyu: na anasema amefunuliwa na mungu. Binafsi namchukulia kama aliyeanguka kiroho. nimeshashuhudia mikutano mbalimbali ya TB Joshua kupitia Emanuel tv, ambapo wachungaji wanapeleka wagonjwa kule na wao wanakutwa wana mapepo tayari. Mungu anayeshauri umwache mkeo wa ujanani huyo ni shetani tu.Huyu mchungaji anahitaji maombi.

  Binafsi sijamkosoa TB Joshua ila nimetaka watu wajue kuwa na mungu hakukufanyi
  mtu kuepuka majaribu Mungu haruhusu jaribu lililokuzidi kimo.
  Twasoma kwenye bibilia Ayubu alijaribiwa ikafikia kipindi watu wa karibu wanamwambia kwanini usimkufuru mungu wako ukafe.

  TB joshua amesema kumjua true believers ni wakati wa hard times.Binafsi Sijajua ni kitu gani cha mimi kuonyesha shaka kwenye huduma ya TB Joshua.

  Askofu wa Anglican -UK Canterbury amekiri kuonyesha shaka yake kama mungu yupo ama la! Na pengine ni kwa haya yaliyotokea huko Nigeria.

  kuna mhubiri mmoja wa kisomali alisema maisha ya mkristo yana stage tatu. ya kwanza ni ile umeamua kumfuata yesu ambapo kila ufanyalo linapata kibali mbele za mungu. ukiomba unapokea kwakuwa huu mchanga, stage ya pili majaribu makubwa. Kwa kuwa umeshakomaa. unapaswa kuyashinda.

  sasa kama wewe unaishi una miaka 30 ya wokovu na hujawahi kupata majaribu ni wazi kuwa unatembea kweye wrong path. kikombe alichokinywa bwana yesu tutakinywa. siku zote yatupasa kuomba ili tusiingie kwenye majaribu.

  neno la mungu na likae kwa wingi ndani yenu.
  @Dickson kamugisha nashukuru kwa ujumbe wako. kwa bahati mbaya niliyoyaandika hapa niliandika kabla sijasoma ulichoandika.

 6. Ziragora

  Kule kusema kuwa tangu mwanzo Mungu aliumba mume mmoja mke mmoja,maana yake ni kwamba wakiwa wake wawili mume mmoja ni kinyume na alichosema Mungu.

  Ndio maana nikasema mada hii ni nyepesi sana kuliko tunavyotaka kuikuza.

  Zamani za akina Daudi na akina Yakobo na wengine ndio zile zamani za uovu ambazo Mungu alijifanya hazioni, yaani alizifumbia macho, siyo sasa hivi.

  Hiki ni kipindi cha uhalisia wa Mungu, kipindi cha agano lililo bora zaidi.

  Kuna nyakati za mwenye mke kuwa kama hana, si kweli kwamba kwa vile tu umeoa ati kila ukitaka kufanya tendo la ndoa ni lazima tu ufanye, kuna wakati unatakiwa kujiweza maana hauko katika nafasi ya kupata hilo hitaji.

  Eg, ukiwa safarini, mke kajifungua, anaumwa,n.k.

  Ndio hivyo!

 7. THANKS, ILA TUKUMBUKE UNABII UTAKAO KWA MUNGU SHARTI UTHIBITISHWE NA WATU 2 AU 3 KAMA PAULO ASEMAVYO, MAANA SHETANI HUTABIRI PIA NA YAKATOKEA. TUWE MAKINI WAPENDWA.

  “NOTHING IMPOSIBLE TO GOD“

 8. Binafsi nasema ni jambo jema ambalo limezungumzwa na kwakweli pasipo unyenyekevu hakika tutashindwa kulijua na kutimiza kusudi la Mungu,hakika tunamhitaji Mungu atusaidie ili tuwe wanyenyekevu.ukiangalia tulio wengi hata Mungu anapotutumia mara moja tunashindwa kuwa wanyenyekevu na badala yake tunavamiwa na shetani na kugeuzwa ufahamu wetu na kujiona tayari tunaweza ndipo sa linapokuja swala la Mungu kuacha kukutumia na badala yake tunatumiwa na shetani!hivyo kushindwa kufanya mapenzi ya Mungu na badala yake tunafanya mapenzi ya shetani.Kwakweli pasipo kuwa wanyenyekevu na kukakaa kumsikiliza Mungu hakika tutafanya yaliyo mapenzi ya shetani tu.kingine usipolijua neno la Mungu hakika ni rahisi kusambaratishwa na shetani na kuendelea kuwa mtumwa wake.Pasipo kulijua neno hakika tutakuwa watumwa siku zote.

 9. Mungu akija katika nchi au eneo ninaloishi akaita watu kumi waliozaliwa mara ya pili
  yaani waliokoka,mimi nitatoka nikiwa wa kwanza tena kifua mbele nikiwa na ujasiri
  wote!Lakini akiita wanyenyekevu milioni kumi waliofuzu kuishi ndani ya unyenyekevu ulio hai kwa kweli sitathubutu kutoka.Bado nahitaji neema ya kujifunza unyenyekevu wa Yesu(Wafilipi 2:3-8) kwa jasho na machozi ya damu.Huu
  ni zaidi ya UKWELI bali ni KWELI.Maana kuna tofauti ya milele kati ya UKWELI(hekima ya wanadamu) na KWELI(hekima ya Mungu).

  Roho Mtakatifu naomba nisaidie hapa.Kamata kinywa changu na akili zangu huzitumie wewe jinsi upendavyo (1 Yohana 2:27).Ndugu zangu katika Bwana,Harris,E.Mushi,Sungura na CK Lwembe.Mungu atufiche(atubariki) ndani ya maarifa yake kadiri ya kiwango cha unyenyekevu(uchaji) kilicho ndani ya mioyo
  yetu(Mithali 1:7,Mithali 22:4).Mnanibariki sana na sadaka(michango) zenu.Na mimi
  nazipokea kwa unyenyekevu ili kumpa Roho Mtakatifu nafasi ya kunifunulia zaidi mambo makubwa na magumu ambayo siyajui(Yeremia 33:3)

  Kinachofanyika hapa ni mfumo wa kutoa na kupokea sadaka.Sadaka zetu ziko hai
  kwasababu tunaiacha uchi kabisa mioyo yetu yaani tunayaweka wazi yale yalijaza
  mioyo yetu.Kile kinachotoka ndani ya moyo wako ndicho kinacho kuwakilisha wewe kwa wakati huo.Pia ni utambulisho wako katika maisha yako ya kila siku.Ndiyo nguvu inayoendesha maisha yako.

  Ndugu yangu CK LWEMBE inabidi tuendelee kunyenyekea sana ili Roho Mtakatifu atufundishe maana halisi na namna ya kutembea kwa kutumia MACHO SABA YA MUNGU.NI MACHO SABA YA UNYENYEKEVU WA YESU au MACHO SABA YA MAARIFA YA MUNGU.Hizi ndiyo ROHO SABA ZINAZOWAFANYA WANYENYEKEVU
  WALIOKO DUNIANI WATAWALE NA KUMILIKI(Ufunuo 5:6,Isaya 11:2,4).Mungu aliye hai atutie nguvu.Nahitaji kuendelea kunyenyekea mno ili nipate mafunuo ya ndani kuhusu simulizi yako ya yule mbakaji alimaliza maisha yake ya hapa duniani
  kwa kusema “SHETANI NAOMBA UPOKEE ROHO YANGU”!

 10. Ndg Dickson Kamugisha,
  “Mnyenyekevu unayetafuta unyenyekevu ulio hai”

  Awali ya yote, napenda nikushukuru kwa tenzi nzuri sana yenye kuinua tafakari kwa “mioyo iliyo uchi” hata kuifikisha ktk kuvikwa “unyenyekevu ulio hai”, asante sana!

  Unapozungumzia sisi kuwa ” VIPOFU NA VIZIWI WA MAISHA YA KIROHO, ambao hutujui kwamba tuko hivyo, na unatuasa tuikubali hali hiyo; hili ni jema na ni changamoto ya kutufanya tuinuke tutafute uponyaji wa hali yetu hii ya kusikitisha, kwani ktk kipimo chochote kile, hakuna mtu anayetia huruma zaidi ya huyo ambaye ni kipofu na kiziwi halafu hajui kwamba yuko hivyo; yeye hujiona ni mwenye macho na masikio safi, kumbe ni masikini na yuko gizani na hajui kwa Upofu, na wala haonyeki kwa ukiziwi alionao, hii ni balaa kubwa!

  Lakini, kwa kadiri ya majadiliano uliyoyarejea, ninaamini kwamba ulifanya haraka kuinuka kabla ya “ono” hilo ulilooneshwa kukamilika na hivyo umeondoka na sehemu tu ya jambo hilo na mwishoni umetumia akili zako kuliunga kufikia hiki kiwango ulichotuletea!

  Nakushauri, kwa “unyenyekevu ulio hai”, rudi tena magotini, mshukuru Mungu kwa kukupa wasaa ili ulikague upya Neno lake, upatafute mahali popote ambapo Mungu alimuinua nabii, na kisha nabii huyo kuja na Neno linalopingana na nduguze waliomtangulia; kwa uhakika hutapaona!

  Basi, kuja na jambo lolote ambalo si Neno la Mungu ndiko kuwa “uchi”; ndio maana nilisema na ninaendelea kulisema hilo hivyo, kwamba ninaweza kumuelewa mchungaji au mwinjilisti au mwalimu anayetokana na dhehebu akiniambia kuwa Mungu ni UTATU MTAKATIFU maana najua kwamba wanatumia rejea za mafundisho yao kutoka kwa wakufunzi wao waliolichunguza Neno la Mungu ili kulioanisha na hiyo dhana waliyoibuni na hivyo kuujenga huo msingi ambao hao wanasimamia.

  Lakini nabii ni mtu anayetoka Usoni pa Mungu, yeye huja na Neno la Mungu ktk ukamilifu wake, ambalo ktk hilo huo Utatu Mtakatifu HAUMO ktk Maandiko, si kwa mitume wala manabii, hao ambao ndio Msingi wa Kanisa; basi kulipokea jambo ambalo si la Mungu huko ndiko kuwa “uchi”! Ufu 3:17 “… nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu na uchi.” Ndipo nilipoona kwamba huduma hiyo inakiri Utatu ambao haumo ktk Biblia, kutoka jambo hilo nikamjua kuwa huyo si nabii wa kutoka Uweponi mwa Mungu bali ni nabii tu wa kipawa, hicho ambacho ni kama vipawa vinginevyo visivyo na majuto, kama cha Balaamu!

  Hivyo nina uhakika kwamba ukirudi ktk “ono” lako hilo, utaona kwamba mimi siko kati ya hao ambao “mioyo yao imevua nguo na kubaki uchi kabisa”; mimi niko kando kidogo nimejifunika Injili iliyohubiriwa na mitume, jaribu kucheck vizuri, utakuwa umenifananisha tu na akina Seleli na Mabinza kama sikosei; watupie basi kivazi wasitirike!!!!

  Karibu utupe hayo mambo matamu ya Macho Saba ya Mungu, wengi tungependa kujua kuhusu hayo Macho, ni nini na unafikiaje kutembea ktk hayo.

  Gbu!

 11. Kwa hiyo hapa mnaongelea nini sasa, na lengo likiwa ni nini?

  Je ni kumpinga TB Joshua kwamba ni nabii wa uongo au mnasema kitu gani?

  Naona wote kuanzia mleta mada na wachangiaji mnaongea kimafumbo tu, si mseme wazi nanyi tuuone unabii wenu tujue kama ni wa kweli aul la.

  Harris, nikijaribu kukuelewa naona kama unashangilia kiana kunguka kwa jengo la TB Joshua. Japo siona kama unachokisimamia kiko sahihi.

  Anyway, ngoja niendelee kufuatilia ili kuona ni nini kinachosemwa hasa hapa!

 12. Mungu atusaidie sana, kuisoma Biblia na kuielewa bila kutegemea msaada wa mtu bali Roho Mtakatifu, ambaye ndiye rafiki yetu wa karibu atusaidiaye.

  Siku hizi ni za mwisho, wengi watahangaika huku na huko kutafuta amani, lakini amani ya kweli iko kwa Yesu peke yake hakuna replacement. watumishi wa mungu wako na wa shetani pia hawajalala usingizi, tena mikakati yao ni progressive ni ya uhakika, sisi wakristo tuamke maana siku ziko karibu sana. Kuna wengine tayari Yesu wao ameshafika na wameshaaminishwa kuwa ndiye Masihi, lakini alishaona na akaachana na mke na ameoa tena, bado watu wameaminishwa ndiye, sasa unaweza kuona jinsi gani wakristo tulivyo wavivu wa kusoma biblia na kuelewa. Tunapenda kusomewa na kutafsiriwa na wengine kitu ambacho kinatugharimu sana, maana wako waliolijua hilo, ndio hao wanaotuyumbisha kila kukicha, pamoja na matatizo yetu kimbilio letu ni kwenda kupokea miujiza lakini roho zetu hazina neno ili kuweza kutunza hata huo muujiza. Mimi always ninatamani sana kama watu wangetafakari na kuomba mungu sana atupe roho wa kweli, ili kuweza kujua nani ni agent wa mungu aliye hai na nani ni agent wa Ibilisi.

  Mtumishi Dickson asante kw aujumbe

  Esther

 13. Binafsi sina macho ya rohoni: Siwezi kutazama kwa mfumo huo.Mi huwa natumia past, present experience kuelezea fyucha. pia mfumo wa cause and effects. Mungu mwenyewe kupitia maandiko anasema mawazo yetu sio mawazo yake.
  Nabii TB Joshua mwanzoni mwa mwaka huu miongoni mwa yale aliyotabiri alisema ni Mwaka wa kuvuka Daraja (2014 is the Year Crossing the Bridge) na akasema wengi wataanguka. Kwa maana hawataweza kustahimili katika Imani zao. Jambo hili lilinijengea wasi wasi nikahisi pengine ni end of days kwani sikuelewa litatokana na kitu gani.Hasa nikizingatia kwamba niliamini Huduma yake inakuwa siku zinavyozidi manake hata hapa Tanzania kuna waliokuwa wakishawishika kujengamawazsiliano. kuweka stika kwenye magari yao na kununua maji ya Baraka.
  Ila mpaka sasa naweza kuhisi labda ule utabiri wake wa watu kuanguka kiimani utakuwa unaanzia hapa kwenye jengo lililoanguka kisha unamalizikia kwenye utabiri wa ndege ya malaysia iliyopotea. Ambapo Si uchawi wala sijui kitu gani kimeweza kuelezea ilipo mpaka sasa.
  . Nakubali kuwa hatuwezi kujua yale yanayotendeka kwenye Ulimwengu wa kiroho labda mpaka tuwe na macho ya kiroho. Ila wengi tunashida sana kiasi hatuna muda wa kutazama hilo tunachotaka ni deliverance. Kwahiyo ni wazi kuwa kuanguka kwa jengo la TB Joshua na utabiri wake kuhusu ndege utakuwa umeanza kufananishwa na wa Babu wa Loliondo. Wengi wataachana na boti yake. Wataacha kuvuka Daraja..

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s