ZAKA Malipo ya Kabla!

fullgospelsadaka

 

Wapenda kwa jina la Yesu naomba msaada katika kuuliza, nimepewa bahasha kanisani nawatumia picha, Je, Zaka inatolewa kabla ya kupokea mapato au ukishapokea mapato? Mungu awabariki

–Paul

 

Advertisements

63 thoughts on “ZAKA Malipo ya Kabla!

 1. Duh, Christina,

  Ulikuwa unatoa unabii au ni nini hicho?

  Usitumie nguvu sana, mambo haya si kwa majeshi na silaha.

  Tatizo lako kubwa ni moja, unatumia vitisho zaidi kuliko kutumia muda mwingi kuchambua au kutuambia kwa nini Zaka ni lazima kutoa( si kwa moyo wa kupenda)

  Nimeona sehemu unesisitiza kutoa aina zote za sadaka, ikiwemo dhabihu.
  Lakini hebu niambie kuna dhabihu gani tena leo tunatakiwa kutoa wakati kuna dhabihu ya milele ambayo ni damu ya Yesu kristo? Au hujui maana ya dhabihu?

  Ok, labda ukisema zabihu ya sifa nitakuelewa. Lakini ukisema zaka na dhabihu inayosemwa kwenye Malaki, huko ni kutaka kubeba kongwa ambalo walioanza nalo liliwashinda.

  Ukisema kutoa zaka kwa hiari hapo hata hakuna wa kubisha, lakini unaposema ni lazima kama makuhani wanavyoambiwa na nabii Malaki, huko ni kupotea njia.

  Na kwa kweli sioni ni nini hasa kigumu katika kulielewa hili suala.

  Au mnamwonaje Mungu, yuko ‘illogical’ eh, kwamba anaweza kuwataka watu watoe zaka kama ilivyokuwa lazima ktk agano la kale, wakati sasa hivi sababu ya kutoa zaka kaiondoa mwenyewe?

  Kwamba yeye hukusanya mahali ambapo hakutapanya eh? Heheheee, mnacheza kweli ninyi.

  Na wengi wenu mnatoa hiyo zaka kwa hofu na uoga wa kutishwa, na hampata baraka yoyote ya utoaji maan huko si kutoa kwa moyo wa kupenda!

  Ni akina nani leo ambao urithi wao ni zaka, yaani wao ni kutumikia madhabahu tu?

  Hebu acheni bwana, wakati wa kudanganyana na kutishana kwa unabii ulishapita, huu ni wakati wa ukweli, maana maandiko yanatuelea!

  Agizo la mitume kwa kanisa la mataifa lilikuwa ni kutowasahau yatima na wajane.
  Siyo kuwapa wachungaji na maaskofu zaka tena kwa sheria na kujiandikisha majina!

  Kwa nini hamtaki maandiko yawaelee?!!!

  Eti Zaka kutoka kwenye gross salary, mna kesi ya kujibu!

 2. USHAURI UNAOWEZA KUTUSAIDIA SIYO WA CHRISTINA AU LWEMBE
  BALI NI WA YESU NDANI YA MOYO WA LWEMBE AU MTU MWINGINE
  YEYOTE.

  TUNAPASWA KUMSIKILIZA ROHO MTAKATIFU NDANI YA MTU NA SIYO
  KUMSIKILIZA MTU.HAPA NAONGEA NA WATEULE NA WANANIELEWA
  SIRUSHI NGUMI HEWANI BALI NAJUA NINAPOPIGA.

  WAPO WATU WENGI AMBAO WANASOMA COMMENT ZETU NA ILE
  KWAMBA HAWACHANGII CHOCHOTE HAINA MAANA KWAMBA SISI
  TUNAJUA AU TUNAWEZA KUWAELIMISHA KULIKO WAO WANAVYOWEZA KUTUELIMISHA.MIMI SIANGALII SURA YA MTU
  BALI NAANGALIA SURA YA YESU ILI YESU ANIPE MAARIFA
  YA NAMNA YA KUSHUGHULIKA NA WATU NA KUJIKAGUA MIMI
  MWENYEWE.

  WEWE NI NANI UNAYEWEZA KUMZUIA ROHO MTAKATIFU
  ASIWAELIMISHE WATEULE KUHUSU MBWAMWITU KWA JINSI
  APENDAVYO YEYE.KUHUSU SUALA LA ZAKA WATEULE WENGI
  ZAIDI WAMESHAELEWA UMUHIMU NA MAANA YA KUTOA ZAKA.
  HATA HIVYO YESU ANAWAHIMIZA WAPOTOSHAJI WAONGEZE BIDII
  ILI AZIDI KUWAACHA UCHI KABISA.WATEULE WENGI ZAIDI WANAENDELEA KUELEWA UHUSIANO ULIOPO KATI YA KUTOA ZAKA
  VIBAYA NA UWEPO WA MADHABAHU ZA MBWAMWITU.

  YESU ANACHOFANYA HAPA NI KUTEMBEZA MAKOFI YA HEKIMA
  NA MAARIFA.NI MAKOFI MAZITO NA UKISHAPIGWA LAZIMA
  UENDE CHINI NA KUINUKA INATEGEMEA SANA UNYENYEKEVU
  WAKO.KAMA UNADHANI NAKUTANIA KASOMA HABARI ZA ESAU
  NA KIZAZI CHAKE,TANGU WALIPOPIGWA MAKOFI YA HEKIMA NA MAARIFA KWA MKONO WA YAKOBO NA KIZAZI CHAKE HAWAJAWAHI
  KUINUKA TENA MPAKA LEO WANAGALAGALA CHINI NA WANAKUFA
  VIFO VYA AIBU.

  HITIMISHO LA YESU KRISTO
  MTU YEYOTE ALIYE WA KWANGU ASIPOTAKA KUJIFUNZA KWELI
  YA NENO LANGU ATAAMBULIA AIBU KUBWA.KIBURI HULETA ROHO
  YA UJUAJI AMBAO HUONDOA UNYENYEKEVU WANGU NDANI YA MTU NA KINACHOFUATA NI AIBU KUBWA.(MITHALI 11:2).

  NINAWAOMBA SANA MSIBISHANE NA MBWAMWITU BALI KWA
  HEKIMA PANDENI MBEGU NJEMA KWA WATU WEMA.KANISA LILILOJEGWA JUU YA MSINGI WA NENO LANGU(UNYENYEKEVU
  WANGU) KAMWE HALITASHINDWA NA MILANGO YA KUZIMU.KILA
  MTEULE ANAPASWA KUTUMIA FUNGUO ZA UFALME WA MBINGUNI
  NILIZOMPA.(MATHAYO 16:18-19).MSIFANYE MASHINDANO BALI ENENDENI KATIKA UNYENYEKEVU WANGU(WAFILIPI 2:3-4)

  TOENI SADAKA ZILIZO HAI.TOENI ZAKA NA DHABIHU KWA UAMINIFU NA USAFI.SIRI ZA UFALME WA MBINGUNI ZIMEFICHWA
  NDANI YA KUTOA NA KUPOKEA SADAKA ZA AINA ZOTE.KABLA YA
  KUTOA SADAKA NINAYOKUELEKEZA KUTOA KUMBUKA KWANZA
  KUTOA SADAKA INAYOITWA REHEMA.(LUKA 11:37-42,ZABURI 51:16-19).

  HUU NI WAKATI AMBAO WATEULE WANGU MNATAKIWA KUYAELEWA
  MAANDIKO(NENO LANGU) KUPITIA UWEZA WA ROHO WANGU
  MTAKATIFU ILI MSIENDELEE KUPOTEA(MATHAYO 22:29,1 YOHANA 2:20,27).

 3. Christina,

  Unatia huruma sana, maana wewe unachojua kukiongelea ni mbwamwitu tu.

  Mada ikiwa haihusiani ni ishu ya mbwamwitu utalazimisha kuipigisha mpindo mpaka ufike kwenye kuongea kitu pekee unachoweza kukiongelea(mbwamwitu).

  Hebu imagine kuandika comment ndeefu iliyojaa maelezo ya mbwamwitu katika mada ya zaka.

  Kitu pekee ulichoongea ktk mchango wako ni hiki hapa (nakunukuu):

  “Kutoa ZAKA ni lazima na zaka imeficha uchumi na ulinzi
  wa mkristo anayejitambua”

  Na hii ndio namna mliyofundishwa juu ya zaka, nanyi mwataka kuwafundisha wengine vivyo hivyo.

  Hamsemi ni mtume nani aliyeishi kwa zaka au kuwafundisha kanisa watoe zaka. Ila mnachokifanya ni kuwatisha watu na kile mnachokiita faida au hasara ya kutoa au kutokutoa hiyo zaka ya lazima.

  Ni aibu mtu mzima kutoa hoja ya nguvu kuwa kutoa zaka ni lazima na kuwa zaka ni mlinzi, bila kuithibatisha hicho unachokisema.

  Ni mtume yupi aliyewahi kuliambia kanisa hicho ulichosema?

  Mmeshindwa kabisa kuelewa tofauti ya Agano la kale na Jipya kimaudhui, mnajitwangia tu bila kujua kuwa mnatumikia laana.

  Kongwa ambalo Petro anasema liliwashinda wao na baba zao, wakakubaliana mitume wote kuwa hawawezi kuwatwisha kanisa mzigo huo.

  Ninyi naona mnaanzisha msingi mwingine tofauti na ule wa mitume.

  Mimi naona unachoongea ktk hii mada ya zaka ni non sense kwa kweli.

  Soma ushauri wa Lwembe hapo juu, kama utaweza kuyaelewa aliyosema yatakusaidia sana.

  Pole!

 4. Wakati mwingine rangi zetu zinaweza zikawa nzuri mno
  na za kupendeza machoni petu wenyewe LAKINI kumbe
  ni machukizo mbele za Mungu!!

  USHAURI NA MAAGIZO YA YESU KWETU
  AYUBU 22:21-22
  “Mjue sana Mungu, ili uwe na AMANI.Ndivyo mema yatakavyokujilia.
  Uyapokee tafadhali MAFUNZO yatokayo kinywani mwake na MANENO
  YAKE uyaweke kinywani mwako”

  Sikiliza mteule, tunatakiwa TULIJUE SANA NENO LA MUNGU(tumjue sana Mungu) kupitia MAFUNDISHO YA ROHO MTAKATIFU(mafunzo ya
  Mungu) ili TUPATE AMANI YA KRISTO na KULA MEMA YA NCHI.Hivi
  ndivyo Yesu anavyotuambia katika Ayubu 22:21-22.

  Tukitaka tusiwe na AMANI YA KRISTO na TUSILE MEMA YA NCHI
  basi tuongeze bidii ya KULIJUA SANA NENO LA SHETANI(Kumjua sana
  shetani) kupitia MAFUNDISHO YA MASHETANI ambayo huambatana
  na ROHO ZIDANGANYAZO(1 TIMOTHEO 4:1).Na hapa ndipo tutapokuwa
  TUMEJITENGA KABISA NA IMANI YA KRISTO!Neno la shetani linapokaa
  kwa wingi ndani ya mioyo yetu ndipo tunapokuwa na AMANI ILIYOKUFA ambayo inatutia upofu na uziwi wa kiroho(ISAYA 42:19-20).

  KINACHOENDELEA KWA SASA
  Mafundisho potofu kama haya ya kuwazuia wateule wasitoe ZAKA
  Hayataendea sana na upumbavu wa wanayoyasambaza UMESHAANZA
  KUWA WAZI KWA WATEULE WOTE.Mtume Paulo alimwambia Timotheo
  kwamba siku za mwisho kutakuwa na nyakati za hatari na kuna watu
  watajifunza siku zote ila HAWATAWEZA KABISA KUUFIKIA UJUZI WA
  KWELI!!(Soma 2 TIMOTHEO 3:1,7-9).Wakati mwingine tumepingana
  na KWELI kwa kujua au kutokujua.

 5. Dada Christina,

  Jambo la Zaka litakusumbua sana ilhali umemlazimisha Roho Mtakatifu akufuate ktk hisia zako za dini badala ya wewe kumfuata ktk jinsi anavyolijenga Kanisa lake Upya!

  Tafsiri ya Kanisa ni walioitwa watoke, na hawa ni hao walioitwa watoke kutoka ktk Sheria na Upagani. Agano la Kale ndilo Msingi wa Wokovu, lakini HALINA Wokovu!

  Neema ndiyo inayombadilisha mwaminio kufikia kuwa “mwana” wa Mungu na si mambo ya Sheria hiyo inayobeba Agizo la Zaka na Hukumu zake. Kwahiyo unapofanya jitihada ya kulirudisha Kanisa lililokombolewa kwa Damu ya Thamani ya Mungu, unapolirudisha ktk Laana za Sheria hiyo ni hila ya zaidi ya “mbwamwitu”!

  Unapowadanganya hao watoto wa Mungu, ukawaingiza ktk jitihada isiyo na kibali cha Mungu, sijui kama unaijua hasara yake vilivyo! Biblia imekuambia wazi kabisa kwamba HAKUNA aliyehesabiwa Haki kwa kulipa Zaka, woooote, walipaji na wapokeaji walikipungukia kipimo cha Sheria hiyo, na hiyo ndiyo maana KAMILI ya Sheria, LAZIMA uipungukie ili uhukumiwe!!!

  Leo hii nikikuuliza, ni wapi inapotendeka “Kazi ya Mungu” ktk ukamilifu wake, unaweza ukanionesha kweli? Wapi, TAG, au RC au kwa mchungaji Sungura, au EAGT, au wapi, kwa Sabato Masalia au kwa Sabato Matengenezo au …???” Msururu ni mrefu na kila mmoja anajipokelea tu Zaka akishiriki kifo chake mwenyewe kwa ujinga au tamaa iliyokithiri!

  Mnawaingiza kwa hila waumini ktk kutamka Nadhiri za mafungu ya kumi nk na kisha kuwashurutisha watoe hizo pesa la sivyo watalaaniwa, nao masikini inawabidi wazitunze ahadi zao hizo walizolazimishwa kuzitamka kwa Mungu! Kuna matoleo mengi sana ya Agano la Kale yamerudishwa makanisani ili kuwakamua waaminio bila huruma mithiri ya vampires!!

  Kanisa liko Rohoni sasa hivi, limeketi Utukufuni ktk Kristo, kama ni Zaka basi wanatoa kwa UFUNUO, hapo wanapoongozwa kufanya hivyo kulingana na Kazi ya Mungu ya kweli inapofanyika na si kwa kila “Mbwamwitu” wa Injili!!!

  Pia ni vizuri ukafahamu kwamba HAKUNA Roho Mtakatifu anayeyavuka Maandiko kwa sababu Yeye ndiye hayo Maandiko, ukiona unapata Mafunuo au maono yanayolivuka Neno la Mungu, kaa chini uitafakari njia yako upya, maana twafahamu kwamba hata Shetani hujigeuza awe mfano wa malaika wa Nuru! Hao hapo Wasabato, ni mfano mzuri wa jambo hilo, wao walimpokea Ibilisi aliyejigeuza awe mfano wa malaika wa Nuru, huyo aliyetoka na farasi mweupe ktk Ufunuo 6:2, wakampokea kama Kristo wakamsujudia, wakazikabidhi nafsi zao kwa huyo, HAWAJARUDISHIWA mpaka leo, ndio hao unaowaona wakiukana Wokovu kwa nguvu zao zote; jichunguze nawe pia maana naona unailazimisha Zaka ya Sheria kwa nguvu zako zote!

  Gbu!

 6. KAZI ZA WATUMISHI WA YESU WANAOJITAMBUA KIROHO
  Kuna kazi nyingi za kufanya katika kumtumikia Yesu tukiwa kama
  MAKUHANI na WAFALME kwa wakati mmoja.Jambo la kwanza
  ni kuhakikisha tunayakataa na kuyaweka wazi MAFUNDISHO POTOFU
  kama HILI FUNDISHO KWAMBA SI LAZIMA WATU WALIOOKOKA
  WATOE ZAKA.Kutoa ZAKA ni lazima na zaka imeficha uchumi na ulinzi
  wa mkristo anayejitambua.

  kazi nyingine ni kuhakikisha wateule wanapata ufahamu wa kutosha
  kuhusu uhalisia wa MBWAMWITU.Ni lazima kila mteule ajue mbwamwitu ni kina nani,wanatambulikaje,mbinu na hila zao ni zipi
  na pia mafundisho yao ni ya aina gani.HII NI MUHIMU ILI KUWAEPUKA NA KUJANASUA KAMA UMESHANASWA.Na ndiyo maana
  Yesu alisema TUJIADHARI NA MANABII WA UONGO.Maandiko
  yako wazi kabisa katika kitabu cha ufunuo kwamba manabii wa uongo
  wataendelea kuwepo isipokuwa WATAMTANGULIA SHETANI KWENDA
  KATIKA LILE ZIWA LA MOTO!Mwanzo 3:15 inaeleza wazi kwamba hapa
  duniani kuna vita kali sana kati ya wateule na manabii wa uongo
  ambao kimsingi wana majina mengi sana.Wanaitwa wana wa ibilisi,
  wana wa usiku,wajumbe wa shetani,wachawi na waganga n.k
  wa mkristo halisi.YUDA 1:3-4 inawaeleza wazi kabisa kwamba ni watu
  ambao WALISHAKATALIWA hawana fungu katika ufalme wa Nuru.

  Watu hawa ni zaidi ya wauaji kwahiyo ni lazima kuwajua vizuri na kazi
  yao kubwa ni kuhakikisha wanawatenga wateule na IMANI YA YESU
  Kwa kutumia roho zidanganyazo na MAFUNDISHO YA GIZA(Soma na
  utafakari 1 TIMOTHEO 4:1).Kazi ya wateule wanaojitambua ni kumuomba Yesu maarifa yatakayoachilia nguvu za kiroho za KUWARUDISHA WATEULE WALIOCHUKULIWA MATEKA KATIKA KAMBI
  ZA MBWAMWITU(Tafakari ISAYA 42:22).

  KAMA WEWE NI MTEULE NA UNAONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU
  UTAKUWA UMEMUELEWA ROHO WA KRISTO ANASEMA NINI HAPA.

  MWAKA 2015 NI MWAKA WA AJABU SANA…….HEBU TUSUBIRI
  TUONE KITAKACHOTOKEA MUDA SI MREFU SANA UJAO.

 7. Mrs. Christina,

  Paul mtume alimtaja Petro kwa jina akamkemea kuhusu unafiki aliokuwa anafanya wa kuchanganyika na wa mataifa wayahudi wasipokuwepo, na kujitenga na wa mataifa wauahudi wanapokuwepo.

  Kwa hiyo Paul alitenda dhambi kumtaja Petro na kumkemea hadharano?

 8. NAOMBA KURUDIA HILI KATIKA UZITO WAKE.
  Wakolosai 2:5 inazungumzia habari ya kuwatambua watu
  KWA JINSI YA ROHONI.Si hekima ya Mungu kumpoint fulani
  kwamba ni mbwamwitu na ndiyo maana ninapoongozwa na
  Roho Mtakatifu kuandika makala mbalimbali kuhusu mbwamwitu
  hasa tabia na mienendo yao sijawai kutaja jina la mtu au kikundi
  fulani cha watu.Kazi yangu ni kuachilia ufahamu na maarifa
  ili wateule wanaopitia ndani ya hii blog WAWEKWE HURU.

  Watu wanaopita kwenye hii blog ni wengi na vipengele vya kusoma
  vipo vingi pia.Wapo wapotoshaji waliodhamiria na wapo ambao
  kimsingi si wapotoshaji lakini wanaandika mapotofu na wanaamini
  wako sahihi.Wapo ambao kila siku wanaangalia na kupitia kinachoendelea lakini hawajawahi kuchangia hata siku moja.Suala kubwa hapa ni kujifunza kupitia upotoshaji na ile KWELI INAYOANDIKWA.Na ndipo tunapopata ukomavu zaidi.Na
  kwa wateule ambao bado ni wachanga ni muhimu sana
  Roho Mtakatifu anapotupa TAHADHARI MAPEMA kuhusu mbegu
  zinazopandwa na mbwamwitu.KILA MTU NI MTUMISHI KWA MUNGU
  WAKE BILA YA KUJALI KWAMBA ANAMTUMIKIA YESU AU SHETANI.

  Hata tukikasirika kwa ndani ni sawa na ni nzuri mno.Suala la
  kuwepo kwa mbwamwitu wanaochangia katika hii mijadala
  LIKO WAZI SANA NA HALIKWEPEKI.Ukitaka kumjua CHRISTINA ni
  nani kiuhalisia siyo lazima uangalie sana anachoandika maana
  anaweza akajificha kwenye maandiko na kujifanya anaongozwa
  na Roho Mtakatifu,ingawa kama unaongozwa na Roho Mtakatifu
  utaijua misingi ya yale anayoyaandika.LAKINI NJIA YA WAZI SANA
  AMBAYO HAINA UBISHI NI KUMCHUNGULIA CHRISTINA KWENYE
  ULIMWENGU WA ROHO.INGAWA HUJAWAHI KUONANA NAE
  UTAONYESHWA KILA KITU KUHUSU YEYE NA JINSI ANAVYOFANANA
  KIMWILI.ULIMWENGU WA ROHO HUFICHUA SIRI ZOTE ZA WANADAMU.LAKINI WANA WA MUNGU TULIO WENGI HATUJAJUA
  KUUTUMIA VIZURI.UNAWEZA USIWEMJUE AU KUMUONA MTU KWA JINSI YA MWILINI
  LAKINI UKAONYESHWA KWENYE ULIMWENGU WA ROHO UHALISIA
  WA MAISHA YAKE(Rudia kutafakari WAKOLOSAI 2:5).

  Hata hivyo hii si kanini rahisi sana ni mpaka uwe umeiva sana
  kiroho kama ilivyokuwa kwa mtume Paulo.Hata mimi kuna watu
  ambao wanapitia mafundisho kwenye hii blog WAMESHANIJUA
  KWA JINSI YA ROHONI.Kwahiyo kiuhalisia wameshanijua tena
  kwa undani ingawa mimi sijawahi kukutana nao!KAMA MBWAMWITU
  WANAUWEZO WA KUTUTAFUTA KWENYE ULIMWENGU WA ROHO
  ILI KUTUJUA BASI KWA WANA WA MUNGU NI ZAIDI.HAYA MAMBO
  YAKO WAZI SANA KWA WATEULE WANAOJITAMBUA KIROHO.MBWAMWITU WAMEWEKEWA MIPAKA YA JINSI YA KUTUTAMBUA SISI KATIKA ULIMWENGU WA ROHO LAKINI SISI
  TUNAWEZA KUUONA UHALISIA WAO , MBINU NA MIKAKATI YAO
  YOTE KWENYE ULIMWENGU WA ROHO NA HII NI KAZI YA ROHO
  MTAKATIFU(Soma na utafakari 1 WAKORINTHO 2:12-16).

  ULIMWENGU WA ROHO NI MALI YA WATEULE NA SI YA SHETANI
  NA WATUMISHI WAKE INGAWA WOTE TUPO KATIKA ULIMWENGU
  WA ROHO NA VITA YETU INAANZIA HUKO NA KUTHIBITIKA MWILINI.
  KAMA WEWE NI MBWAMWITU UWE NA UHAKIKA WATEULE WANAOJITAMBUA KIROHO WAMESHAKUJUA KWA JINSI YA ROHONI
  NA KUWATAJA WATU KWA MAJINA NI HEKIMA YA KIMWILI NA INA
  ADHABU YAKE KUTOKA KWA YESU.

  WATUMISHI CHEMO NA SUNGURA TUPO PAMOJA
  KATIKA KUUJENGA MWILI WA KRISTO.

 9. Chemo,

  Unapoteza muda wako kumuuliza swali mtu ambaye amejaa propaganda na unafiki wa kuyosha tu.

  Angekujibu kama ulivyouliza ningeshangaa sana.

  Acha tu aendelee kutuita mbwamwita, kuna siku ataelewa tu ukweli, na mapokeo yote yatakoma.

 10. Mtumishi chemo
  kwa kuwa tunaishi kwa ROHO ni lazima tuenende kwa ROHO.Hekima
  na kanuni za kiroho ndiyo zinatakiwa zitutawale.Ni kweli kwamba
  kuna mbwamwitu ambao wamejichanganya kwa siri katika mijadala ya
  wateule(YUDA 1:4) ili kupotosha NENO LA MUNGU na lengo hapa
  ni ili WATEULE WAISHI KWA KUFUATA UPOTOSHAJI WAO(MATENDO 20:29-30).

  Kwa muongozo wa Roho Mtakatifu tunashuhudia MAFUNDISHO MENGI
  SANA YA KISHETANI.kazi ya hekima na maarifa ya Roho Mtakatifu
  ni KUYAANIKA WAZI HAYO MAFUNDISHO YA MASHETANI BILA
  KUJALISHA KWAMBA YANAPANDWA NA WATUMISHI WA MUNGU
  WASIOJITAMBUA KIROHO AU WATUMISHI WA SHETANI.Kwahiyo
  si kila anayepotosha ni lazima awe mbwamwitu, wengine ni watumishi
  wa Mungu aliye hai lakini wamekaa katika kiti cha enzi cha shetani
  na ili Mungu aweze kuwatumia ni LAZIMA WATUBU(TAFAKARI UFUNUO
  2:12-16).Roho Mtakatifu hajawahi kunyoosha kidole kwamba fulani
  ni mbwamwitu japo ANAWAVUA NGUO NA KUFICHUA SIRI ZA
  UTENDAJI WAO WA KAZI.

  SWALI ULILOULIZA LINAJENGA UELEWA MPANA KWA WATU
  WA ROHONI NA LIMEBEBA SOMO ZITO.KAMA UNAFUATILIA KWA
  KARIBU POST AMBAZO ROHO WA MUNGU ANANIONGOZA
  KUANDIKA, WACHANGIAJI TUMEKUWA NA USHIRIKIANO MZURI
  SANA KATIKA KUYAWEKA MAMBO YOTE SAWA.

  ASANTE CHEMO UMENIONGEZEA UFAHAMU ZAIDI.

 11. Mrs CHRISTINA K

  Naomba kukuuliza swali, toka moyoni kabisa. Hivi hawa mbwamwitu wanaopotosha mafundisho ya utoazi wa zaka, wanaweza kuitwa watumishi? Mf. Mtumishi Sungura, na Mtumishi CK, kama ulivyoainisha mwisho wa “ONYO”.? Wanaweza kuwa wanamtumikia Mungu huyohuyo unayemwamini wewe, halafu wakawa “Mbwa………………Mwitu”? Naomba ujibu toka moyoni kabisa…

 12. Mrs. K,

  Kama kutoa zaka ni lazima, mimi nakushauri tu uendelee kutoa kwa hiyo lazima, hata ukipewa zawadi ya jojo kaitolee zaka.

  Unajua mtu uking’ang’ania giza la akili lazima utakula matunda yake.

  Maana inapofika wakati mtu analazimisha tu kusema kuwa Zaka ni lazima bila kusema kwa nini ni lazima ujue anatembea ktk utiifu wa mapokeo ya dini yake!

  Hakuna mmataifa hata mmoja aliyempokea kristo ambaye ana sifa za kutoa hiyo zaka ya lazima. Balo wote waliompokea kristo wana sifa ya kutoa zaka ile ya hiari kama baba yetu wa imani Ibrahim alivyofanya

  Yesu mwenyewe hakuwa na sifa za kutoa hiyo zaka ya lazima!

 13. ONYO KALI KWA WATEULE WOTE POPOTE WALIPO!!

  Hili siyo onyo kutoka kwangu bali kutoka kwa Yesu na linaanzia
  kwangu alafu ndiyo linaenda kwa wengine.Onyo hili HALIWAHUSU
  mbwamwitu(WAPOTOSHAJI).Hekima ya Mungu hairuhusu kumnyooshea
  mtu kidole bali kuiatamia KWELI YA MUNGU.

  Wateule popote mlipo, katika MITHALI 30:5-6 Yesu anatuonya
  kwa maneno yafuatayo “KILA NENO LA MUNGU LIMEHAKIKISHWA
  YEYE NI NGAO YAO WAMWAMINIO.USIONGEZE NENO KATIKA
  MANENO YAKE, ASIJE AKAKULAUMU UKAONEKANA MWONGO”

  Tukifika mahali tukavaa vazi la UONGO WA KUPOTOSHA NENO
  LA MUNGU tunawekwa katika fungu moja na mbwamwitu ambao
  wao kimsingi walishapotea tangu wakiwa tumboni mwa mama zao!
  na hatuwezi kuwashangaa kwa sababu WALISHAFUZU KAZI YA
  UPOTOSHAJI TANGU WAKIWA TUMBONI MWA MAMA ZAO na kwa
  JICHO LA ROHO MTAKATIFU BADO TUTASHUHUDIA UDANGANYIFU
  MWINGI ZAIDI YA HUU WA FUNGU LA KUMI.(Tafakari ZABURI 58:3).
  Si kila anayesema ameokoka na kufundisha neno la Mungu ni
  mteule wa Bwana.HUWEZI KUMTAMBUA MBWAMWITU mpaka uwe
  UNATEMBEA NA MACHO SABA YA ROHO MTAKATIFU katika ulimwengu wa roho na wa mwili.(WAKOLOSAI 2:5)

  TUNAELEKEA MAHALI PAZURI MNO KWA SABABU MAFUNDISHO
  YA UONGO SASA YAMESHAVULIWA NGUO NA KWA KUWEKWA WAZI
  SANA(Soma LUKA 12:1-2).

  WAPOTOSHAJI ONGEZENI BIDII KATIKA KUTUFUNGUA UFAHAMU.
  KUTOA ZAKA NI LAZIMA NA SIYO HIYARI!!KUNA MAMBO MENGI
  KUHUSU MAISHA YA WATEULE AMBAYO YAMEFICHWA NDANI
  YA ZAKA.NAKUBALIANA NA MTUMISHI SUNGURA KWAMBA NI LAZIMA
  TUJUE KANUNI ZITAKAZO TUFANYA TUTOE ZAKA ZILIZO HAI.(ZABURI
  51:16-19).Hapa Roho Mtakatifu anazungumzia ZAKA ZILIZO SAFI
  yaani sadaka za haki ambazo kimsingi LAZIMA ZIAMBATANE NA MOYO
  ULIOKUBALI KUPONDWA NA MUNGU.HUU NI MOYO ULIOKUBALI
  KUTAKASWA NA KUACHA DHAMBI.Kuna tofauti ya milele kati ya
  kuishi kwa kujitakasa(1 yohana 3:1-4) na kuishi kama mtumwa wa dhambi.

  Mtumishi Sungura amekazia vizuri sana kwamba tusipoishi maisha
  ya utakatifu na uaminifu ZAKA INAGEUKA LAANA BADALA YA BARAKA! Ni kweli wateule wengi tulikuwa HATUJUI KANUNI ZA NENO
  LA MUNGU ZINAZOHUSU WOKOVU LAKINI KWA NEEMA YA YESU
  WENGI SASA WAMESHAANZA KUZIELEWA NA WANATOA ZAKA
  ZAO VIZURI.

  MTUMISHI CK LWEMBE ENDELEA KUJIACHIA ILI ROHO
  MTAKATIFU ACHAMBUE NA KUTUTOFAUTISHIA KATI YA UONGO
  WENYE HILA NA KWELI YA MAANDIKO.

  ASANTENI NYOTE KWA MICHANGO YENU.NYAKATI HIZI ZA MWISHO
  SI TU KWAMBA NI ZA HATARI LAKINI PIA NI TAMU MNO KWA
  WATEULE WANAOJITAMBUA KIROHO NDANI YA NENO LA KRISTO.

 14. Tumaini,

  Watu hawataki kuelewa tuko nyakati gani za kiagano, wao wanaona tu kwamba kila kilichoandikwa kwenye biblia kunawahusu wao leo.

  Wakati kwenye viblia yako mambo yalishapita wakati wake, na hayatokea tena.

  Lakini ukiyasoma bado yanasomeka hivyohivyo yalivyosemeka tangu siku yameandikwa.

  Mfano: ni mpaka kesho kutwa biblia itasema ‘tazama bikira atachukua Mimba nae atamzaa mwana… Sasa usishangae akija mjinga akaanza kuhubiri kuwa kuna siku bikira atachukua mimba!

  Niliwahi kusema kuwa biblia siyo neno la Mungu, ila ni mkusanyiko wa vitabu vilivyoandikwa maneno ya Mungu.

  Kile kifendo cha Agano la kale na Agano jipya kuwa yameunganishwa kama yalivyo watu wengi hudhani kuwa kanuni zilizomo ndani yake zinafanya kazi tu ndani ya nyakati zote.

  Kuna miaka mingi sana kutoka kitabu cha Malaki kuja kitabu cha Mathayo au Luka.

  Bahati mbaya sana kwa kanisa la leo ni kwamba, watu wanamwelewa Mungu zaidi kwa sura ya agano la kale(la mwilini) kuliko wanavyomwelewa kwa sura ya agano jipya.

  Wanataka mpaka wahusishe kuamini kwao na kitu cha kuonekana. Utakuta maji ya upako, vitambaa vya upako, kupanda mbegu -fedha,n.k

  Watu wangeelewa maana ya agano jipya, huu ujinga ujinga tunaouona usingekuwepo.

  Utasikia; mshahara wako wa kwanza ni mzaliwa wako wa kwanza, au ni malimbuko yako, hivyo utoe kanisani.

  Malimbuko, mzaliwa wa kwanza yote hayo ni mambo ya mwilini ya agano la kale, lakini kwa kuwa watu wameamua kumjua Mungu kwa agano la kale, lugha hiyo ndo wanayoielewa zaidi.

  Hebu waambie kuwa leo hakuna cha malimbuko wala mzaliwa kwanza kwa kuwa kristo ndo alifanyika limbuko na mzaliwa kwanza wa wakati wote, uone kama watakuelewa haraka!

  Kanuni ya kubarikiwa ni kufanya kazi kwa bidii, ili upate kitu cha kutoa, ukishatoa kinachofuata si wewe kubarikiwa tena, bali ni kuzidishiwa!

  Lakini hawa watu ambao ni waroho wa pesa k siku wanatuambia kuwa ukitaka kubarikiwa basi toa!

  Na watu kwa ujinga wanatoa kweli, na baraka hawazioni!

  Give, it shall be given unto u!
  Not, give, u shall be blessed!

  To be given back is completely different from being blessed!

  Wasiofanikiwa, si kwa sababu hawatoi zaka. Hawafanikiwi kwa sababu ya kutoelewa kanuni za neno la Mungu kuhusu maisha haya!

 15. Mrs K,

  Utatuita majina yote unayojua, mara mbwa mwitu, mara mashetani, n.k, kwa maneno mengi au machache,lakini utakuja kuujua huu ukweli too late au hautaujua kabisa.

  Kututaka tuzidi kujadili Luk 11 kuhusu alichosema Yesu ni kutulazimisha kurudi kwenye diet ya maziwa wakati sisi si watoto wa kuishi kwa maziwa pekee, bali twala mifupa ndio kiwango chetu.

  Hakuna anayekwambia usitoe zaka, ispokuwa kaa ukijua zaka ni toleo la hiari kama matoleo mengine. Acheni hiyo dhambi ya kuwaita wezi watu ambao kristo kawakomboa kwa damu yake, ati kwa sababu tu hawakutoa zaka.

  Halafu nakuona bado pia unasumbuliwa sana na uelewa mdogo wa lugha, neno “Kutimiliza torati” tumelisema sana katika mijadala yetu hapa lakini nakuona bado huelewi maana yake, unalitumia tu kama wengi wanavyolitumia kimakosa.

  Kutimiliza ni Kiswahili cha zamani kabla ya lugha hiyo kufaniwa usanifishaji ( urasimishaji). Hilo neno ni la rahaja mojawapo kabla ya lugha kurasimishwe.

  Kwa Kiswahili sanifu ni Kutimiza.
  Kwa hiyo yesu alikuja kuitenda torati kiukamilifu kama ilivyotakiwa kutendwa.
  Wala kutimiza hapo haimaanishi kuwa torati ilikuwa imepungua kitu hivyo Yesu alikuja kukiongeza ili iwe timilifu.

  Ndio maana mwidhoni mwa maneno kuwa sikuja kuitangua torati…., kuna neno linasema ” mpaka yote yatimie”

  Maana yake ni kuwa mpaka yote ambayo yalikuwa yameandikwa katika torati na manabii yatimie ndipo torayi na manabii vitafika ukomo wake wa kutumika.

  Kama ulikuw hujui, ni kwamba, Yesu aliyatimi yote yaliyojuwa yameandikwa, ndio maana msalabani alisema imekwisha ( it is done). Na kuanzia hapo agano jipya likachukua hatamu.

  Mungu hakuw ameamuru watu watoe zaka bila sababu. Sababu ilikuwa ni utumishi wa madhabahuni pake/ patakatifu pake, kwamba lazima muda wote pawe na watu wa kupayumikia kwa sababu ya nature ya agano lenyewe( la mwilini).

  Ndio hao walawi ambao hawakutakiw kuwa na kazi nyingine, hivyo ili waishi akaamuru huo utaratibu wa wa zaka.

  Sasa leo patakatifu pa Mungu hapako hivyo, si pa kimwili, hapahitaji mtu kuwepo muda wote, hapahitaji kuhani w kuingia kila wakati kutoa sadaka.

  Ni pa kiroho ambapo paliingiwa nà kuhani mkuuwa ki mbingu Yesristo mara moja tu(once for all) na damu yake mwenyewe.

  Sasa mnapoendelea kung’ang’ana na utaratibu wa kwanza wa ukuhani wa kimwili mimi siku zote huwashangaa.

  Paul hakuwahi kuishi kwa zaka, Petro, Yakobo na mitume wote pia, wala hawakuwahi hata kulifundisha janisa la kwanza kutoa zaka kwa mfumo wa lazima, waluwafundisha watu ni kutoa kwa moyo wa kupenda.

  Sababu iliyomfanya Mungu kuagiza utoaji wa zaka ufanyike, leo haipo, na kwa kuwa Mungu si dhalimu,kwa nini zaka ya mfumo huo iendelee kuwepo?!!

  Acheni kuwaita wezi wale walionunuliwa kwa damu ya mauti ya kristo, maana mtakuwa na kesi ya kujibu mbele zake siku moja.

  Zaka yenyewe anayong’ang’aniwa leo ni pesa. Tangu lini zaka iliwa kuwa pesa toka mishahara ya watu?

  Petro hakuwahi kutoa zaka maishani mwake, Yakobo, Mathayo, Yohana, mpaka Yesu mwenyewe hawakuwahi kutoa zaka, ispokuwa Paul ndo mtume aliyewahi kutoa zaka maishani mwake.

  Mrs. K, kama hao wote hawakuwahi kutoa,wewe unatoa zaka kwa sheria ipi?

 16. Dada Christina,

  Jambo ambalo ninakuomba ulifanye, ni “Ujipe nafasi ya kulitafakari Neno la Mungu kwa FAIDA ya kuujua Moyo wa Mungu!”

  Zaka ni mojawapo ya Sadaka na Changizo zinazompasa Mkristo aliyezaliwa mara ya pili, huyo ambaye ni sehemu ya economy ya Mungu ktk kila hali.

  Sheria au Torati ndio mwalimu wa kwanza kwa Mkristo hapo anaporejeshwa huko ulikojengwa Msingi wa Wokovu. Sasa ieleweke kwamba hakuna mwenye akili timamu anayeweza kujisifia kuwa ana nyumba kwa kujenga msingi na kuishia hapo, japo ni msingi imara! Agano la Kale ni mwalimu anayetufunulia Msingi wa Wokovu tuuone na kuujua ktk uhalisi wake, tukiimarika ktk ufahamu.

  Nayo Zaka katika Maandiko inaonekana mara mbili, yaani iko ktk namna mbili. Namna ya kwanza ni ile inayohusiana na Imani, hii tunayoiona hapo Mwa 14:20 inayomhusisha Ibrahim, na Mwa 28:22 inayomhusu Yakobo. Namna ya pili ni hiyo inayohusika na Sheria, hiyo ambayo ndani yake HAINA Imani, lakini yenye mfano wa hiyo ya Imani hapo Mwa 14:20.

  Zaka inayoongelewa ktk makusanyiko yetu ni hii inayohusikana na Sheria, hiyo yenye kuwasimika Walawi ktk nafasi ya ukuhani ktk mfano wa Melkizedeki; na hii ndiyo Zaka inayosisitizwa ktk Malaki, na Kristo ktk Mt 23:23. Kanisa ktk wakati huo lilikuwa HALIPO, maana ya Kanisa ni “walioitwa watoke”; na ktk wakati huo, Sadaka inayolikamilisha Kanisa, ile Haki inayopatikana kwa Imani kupitia Sadaka hiyo ilikuwa bado haijatolewa; kwa maneno mengine hata Lazaro alipokufa licha ya kuwa ni kipenzi cha Kristo, HAKWENDA mbinguni!!!

  Pia ieleweka kwamba maelezo tunayoyaona ktk t 23:23 yanapaswa kubaki ktk context yaliyotolewa na si kuyavusha kwa hila kwa kisingizio kwamba ‘Kristo hakuikomesha zaka kwani ingekuwa ni hivyo basi angelisema wazi’; hili ni wazo duni linalotokana na kuyakosa mazungumzo hayo, na hali nzima ya Israeli ktk ujio wa Kristo! Israeli ktk mantiki ya Ufarisayo nk, wangali wanaendelea ktk Sheria mpaka leo hii kwa KUPOFUSHWA na Mungu mwenyewe; kwahiyo yeyote anayejiingiza ktk Upofu huo kwa kujitia “utomvu wa minyaa” machoni, huyo ni zaidi ya mjinga, maana anajaribu kumlazimisha Mungu alikiuke Neno lake!!!

  Sadaka ilipokwisha kutolewa ndipo Torati iliingia ktk UKOMO, si kwa sehemu, hapana, bali YOOOOTE ktk ukamilifu wake inakoma hapo unapompokea Kristo na KUJAZWA RM wa kweli. Kama haijakoma, basi jua ya kwamba kwa uhakika wewe hujajazwa RM, una roho wa dini tu ambaye anakuchanganyia mambo, kwa hila akikuondoa kutoka ktk NEEMA, na kukurudisha ktk kujitafutia wokovu kwa matendo kupitia mambo ya Torati, huku akikudhanisha kwamba eti unatoa kwa Imani; kumbe nawe unatoa kwa hila ili umshurutishe Mungu akufungulie hilo lango la baraka zikumwagikie kwa kutimiza kwako sehemu ya Sheria na hivyo kuwafanania wala Wafarisayo wanaoonywa ktk Mt 23:23!!!!

  Pia, wahubiri wengi saaaaana watapoteza nafasi zao ktk wokovu kwa ujinga wa kutoyaamini Maandiko. Wengi wamejipachika ktk nafasi ya Walawi ili wazile hela za Zaka kwa kisingizio hicho cha Ulawi! Hebu rudini ktk Maandiko mziangalie sifa za Walawi kwanza, na sharti la zaka, mnaweza mkapona kuliko hivyo mnavyojidhanisha! Mlawi ana nyumba anapangisha, mkewe ana duka kubwa la vipodozi nk nk; huko kama si kumtania Mungu ni nini!!!? Paulo ndiye mtume kwetu sisi kanisa, na anatuambia tumfuate yeye kama anavyomfuata Kristo; Je kuna mahali mlipomuona akijikusanyia Zaka? Au ni wapi mliposoma kwamba Kanisa limewekewa sharti la Zaka ktk mantiki mnayoirejea ya Malaki?

  Hahahahaha…., Injili si mchezo, unaweza kujikuta unaingia Hukumuni huku umebeba Biblia yako, na ukiimba “RM uniongoze”; kumbe alipokuongoza ulimpuuza ukazifuata hisia zako za dini bila kuukagua upako wake!

  Game imebadilika, imetoka ktk Sheria na kurudi ktk Asili yake, ile “IMANI”! Nayo Imani ni Ufunuo; “Kwa imani” Habili alimtolea Mungu sadaka iliyo bora! Kaini naye alimtolea Mungu sadaka, mazao yake ya shambani; wahubiri wengi wanawadanganya watu kwamba Kaini alimtolea Mungu mazao hafifu, jambo ambalo si kweli, alitoa kama mnavyotoa zaka leo hii kwa Nuru ya Malaki, hiyo isiyo na Imani, yaani mnatoa pasi Ufunuo, kama Kaini,- what a waste!!

  Kama umemfuata Paulo, ni lazima akufikishe kwa Kristo aliyemposea, naye Kristo akiisha kukupokea hukujaza Roho wake ikiwa ni ishara ya kukumiliki na hivyo kukuongoza ktk njia ikupasayo, akikuvusha ktk mitego yote waliyowekewa waigizaji wajikwae ili watumbukie huko shimoni, pamoja na zaka ya bila Maarifa!

  Unajua ni rahisi sana kusema ‘amelaaniwa asiyetoa fungu la kumi’; na wakati huo huo usijue ya kwamba kwa kuirejesha Sheria ndani ya kanisa lililotolewa kutoka hiyo, ni kufundisha Injili wasiyoifundisha mitume na hivyo wengi tunaishia kujiingiza ktk laana sisi wenyewe kwa ujinga na tamaa ya pesa na umaarufu!

  Jitahidini kuyafuata Maandiko na kuyaamini kwa kadiri yanavyojifunua, zikimbieni tafsiri za dini; wengi saaana watahukumiwa kwa wizi wa kula pesa za Zaka wasivyo stahili kulingana na “Vigezo na Masharti ya kula Zaka”!!!

  Gbu!

 17. UJUMBE WA MWISHO KUHUSU ZAKA NA SADAKA NYINGINE

  Changamoto ya wateule kutoutumia ULIMWENGU WA ROHO
  au kutoelewa kile wanachoonyeshwa katika ulimwengu wa roho
  itaenda inapungua sana.Wateule wataanza kuelewa sana yale
  wanayoonyeshwa katika ulimwengu halisi zaidi kuliko huu tunaoishi.

  UHAKIKA wa kila kitu ndani ya wokovu kipo katika ULIMWENGU
  WA ROHO.Ukitaka kujua uhalali wa kutoa ZAKA ingia kwenye
  ulimwengu wa roho kwa njia ya maombi.Mungu amekuwa akiwaonya
  wateule kwa njia ya ndoto au maono kuhusu utoaji mbaya wa ZAKA.
  Kama wewe ni mteule na una MACHO na MASIKIO ya rohoni
  utakuwa umeelewa kile ambacho Roho wa Yesu ananiongoza
  kukuambia.Kwa kulitambua hili ndiyo maana manabii wa uongo
  WAMEPOTOSHA MNO ELIMU KUHUSU NDOTO NA MAONO.Hata
  hivyo UDAGANYIFU WAO UMEENDELEA KUWA MAJIVU NA CHACHU
  YA WATEULE KUIJUA KWELI.

  Nikitaka kujua uhalali wa mafundisho yako na uhalisia wa maisha
  yako ya kiroho, NAKUTAFUTA KWENYE ULIMWENGU WA ROHO.
  Mtume Paulo alikuwa anaitumia sana hii kanuni ili kujua
  kinachoendelea katika kikundi fulani cha watu.Na huu ni uweza
  wa Roho Mtakatifu ambao umo ndani ya kila aliyezaliwa MARA
  YA PILI(soma WAKOLOSAI 2:5).

 18. NENO LA MUNGU LIKO WAZI SANA KWA WOTE AMBAO
  WANAPENDA LIWE WAZI KWAO.

  Mbwamwitu wanalifahamu neno la Kristo kwa undani sana
  na wanajitahidi kutumia udhaifu wa kanisa KULIPOTOSHA MNO.
  Watumishi wa Mungu ambao wamemezwa na mafundisho
  ya mashetani kwa sababu ya KUKATAA KUSHIRIKIA NA ROHO
  MTAKATIFU.Hizi ni nyakati za wateule kufunguliwa FAHAMU ZAO
  ILI WAYAELEWE MAANDIKO.

  Wateule wengi zaidi wataendelea KUKOMBOLEWA KATIKA KUIJUA
  KWELI na kuisimamia.Kama wewe ni mpotoshaji ongeza bidii ili na
  bidii ya mashujaa wa Yesu iongezeke zaidi na zaidi.Nyinyi ambao
  mnatufundisha tusitoe ZAKA hamtutakii mema na tuna mashaka na
  uhalisia wenu.Kwa kuwa mnapingana na maagizo ya Yesu bila shaka
  tunawatambua kwa matunda yenu.

  Asanteni kwa kufungua fahamu zetu kwa kuwa kadiri mnavyoendelea
  kutupotosha KWA WAZI AU KWA HILA ndivyo MAFUNDISHO YA ROHO
  MTAKATIFU YANAVYOZIDI KUWAACHA WAZI!!!
  mungu(m-herufi ndogo) wenu awabariki sana.

 19. Swala la zaka huwa nashindwa kuelewa kwa nini limekuwa kongwa kwa kanisa la leo,na sijajua ni kwa nini tumekuwa tukipigana mikwara na kuitana wezi,jambo hili lingefundishwa kwa uwazi na usahihi watu wangepona ktk hili,na wala watumishi hawakupaswa kuwatisha waumini ktk hili,walipaswa waliamini Neno la Kristo,na kuachana na hofu za kukosa fedha.Hofu zinapelekea washindwe kuliishia Neno.Sungura tutaacha lini kulipotosha kanisa?kwanini hatuwapi kanisa mlo sahihi?tumejikuta tuna utapia mlo wa Kiroho!Daaah!Mbombo ngafu.

 20. Wapendwa WATEULE

  YESU ANAENDELEA KUTABASAMU SANA!!

  Mafundisho potofu yamekuwa chachu ya kujulikana kwa KWELI
  ya neno la Kristo.Binafsi najisikia raha sana kwa jinsi ambavyo
  Roho Mtakatifu analiweka wazi sana suala hili la ZAKA.Hizi ni nyakati
  ambazo unabii wa Mtume Paulo unaendelea kutimia tena wazi
  wazi bila kificho.Paulo alimwambia Timotheo kwamba watu wanaofundisha MAPOTOVU hawataendelea sana(hawatafika mbali)
  kwa sababu UPUMBAVU WAO utakuwa kwa watu wote!Haijalishi kwamba sisi ni WATEULE au MBWAMWITU, tunapoendelea kufundisha
  mafundisho ya mashetani na kuacha mafundisho ya Roho Mtakatifu
  tunakuwa tunafanya upumbavu.Kwa mteule kutojitambua kiroho
  ni zaidi ya hasara.Kijitenga na mafundisho ya Roho Mtakatifu ni kujitenga na IMANI YA KRISTO yaani kujitenga na upendo wa Kristo.
  Hizi ni nyakati za hatari ambazo wateule wanalishwa sumu kali
  kwa sababu ya kutoyaelewa maandiko na matokeo yake wanawaza,
  kunena na kutenda kama mbwamwitu(TAFAKARI na usome kwa kurudia
  2 TIMOTHEO 3:1-9).

  Unataka tuamini kile ambacho Yesu anasema au tuamini kile ambacho
  WANA SG wanafundisha? Yesu anasema wafuasi wake ni lazima tutoe
  ZAKA tena inayoambatana na moyo wa adili na upendo(labda hatujaelewa anachosema katika LUKA 11:42) alafu wanaibuka waalimu
  wengine wanasema ZAKA ni suala la torati halipo kwenye agano jipya!!!
  kama wewe ni mteule utachagua mwenyewe ufuate mafundisho
  ya nani.Hata mashetani(manabii wa uongo) wamegawanyika kwa sababu maalum za kuwachanganya wateule.Kuna wanaosisitiza sana
  suala la kutoa ZAKA huku wakijua kwamba wanaotoa wanampa shetani( mungu wao). Na wapo wanaowazuia wateule wasitoe ZAKA kupitia mafundisho yaliyo kufa.

  Hebu turudie tena kwa mara ya mwisho kutafakari kwa undani
  kile ambacho Yesu alisisitiza kuhusu ZAKA tena kwa kutoa ONYO KALI
  katika LUKA 11:42 “…….OLE WENU Mafarisayo kwa kuwa mwatoa ZAKA za mnanaa na mchicha na huku mnaacha mambo ya ADILI na
  UPENDO wa Mungu, ILIWAPASA KUFANYA HAYA YA KWANZA, BILA
  YA KUYAACHA HAYO YA PILI ”

  Katika Maandiko Mafarisayo walikuwa ni watu ambao wanaamini
  kuwepo kwa uzima wa milele lakini changamoto waliyokuwa nayo
  ni kuwalisha watu mafundisho(chachu) ya madhehebu yao.Unaweza
  ukaamini kuhusu wokovu lakini ukaendelea kuongozwa na mafundisho
  ya wanadamu!Na huu ndiyo ulikuwa ugomvi kati ya Yesu na Mafarisayo(soma MATHAYO 15:1-9).Ndani ya luka 11:42 tunaona
  wazi kwamba Yesu hakatai suala la wao kukazana kutoa ZAKA bali
  anawasisitiza kuhusu suala la wao kutoa hiyo ZAKA kwa moyo
  wenye ADILI na UPENDO yaani watoe zaka zilizo hai, zisizo na unafiki.
  unaelewa nini maana ya maneno haya, ILIWAPASA KUFANYA HAYA YA
  KWANZA BILA YA KUYAACHA HAYO YA PILI.Yesu anasema msiache
  kutoa ZAKA lakini muwe na uhakika Mungu hapokei ZAKA za wanafiki
  waliojitenga na upendo wake na kuacha maadili ya ukristo.Yesu alikuwa
  anapanda mbegu ya moyo wenye adili na upendo ndani ya mioyo ya
  Mafarisayo ili waupate huo uzima wa milele waliokuwa wanauamini.
  Yawezekana hatujui kwamba kitabu cha Malaki ambacho kimesisitiza
  kuhusu kutoa ZAKA kwamba ni unabii wa agano jipya.Malaki anatabiri
  yale yatakayotekelezwa katika agano jipya!

  Upendo wa Mungu(Yesu) ulikuja KUIKAMILISHA TORATI na siyo
  kuipinga.Hapa Roho Mtakatifu anapanda mbegu ya uhai wa mafundisho
  ya Mungu ndani ya wateule.Kama wewe ni mbwamwitu haya mafundisho hayakuhusu ingawa yanakuchoma na unatamani kama
  yasingefundishwa.HII NI MBEGU AMBAYO ITAENDELEA KUZIKOMBOA
  NAFSI NYINGI ZA WATEULE.Usijaribu kubishana na mtu ambaye
  anapingana na kile ambacho Yesu Kristo anasema bali UNATAKIWA
  UTUMIE HEKIMA YA ROHONI KUMUAIBISHA NABII NA MWALIMU
  WA UONGO.Hizi ndiyo nyakati alizotabiri nabii Malaki kwamba mafundisho ya mashetani YATAKUWA MAJIVU(MALAKI 4:2-6).MAFUNDISHO YA ROHO MTAKATIFU tuache kuishi ndani ya mafundisho ya shetani KWA KUFANYA TOBA YA KWELI.Kama mteule
  unatoa ZAKA vibaya au hutoi kabisa inabidi uombe REHEMA.Kumbuka
  kuwa makini kwa jinsi ya rohoni ili ujue ZAKA zako unazitoa
  kwenye madhabahu ya mungu yupi.UKITOA KWENYE MADHABAHU
  YA SHETANI UTAKUWA UMEMPA UMILIKI WA MACHO NA MASIKIO
  YAKO YA ROHONI!

  KWA WATEULE WANAOJITAMBUA KIROHO KUTOA SADAKA INAYOITWA ZAKA NI LAZIMA NA SIYO HIYARI.MWAKA 2015 MOTO
  WA MAFUNDISHO YA YESU UNAONGEZEKA ZAIDI NA HAUZUILIKI.

 21. Mrs K, inaendelea…

  Mwalimu wa kitabu cha Ebrania anasema kuwa ukuhani ukibadirika sharti na sheria ibadilike(Ebr 7:12)

  Ibrahim na Yakobo hawakutoa zaka kwa hiyo lazima ambayo mnaisema kuwa ati zaka ni lazima. Bali walitoa kwa hiari, tena Yakobo kwa nadhiri.

  Lazima mnayoisema iko kwenye torsti ya Musa kwa ajili ya wana wa Lawi( makuhani) ambapo hawakuwa na ardhi kwa agizo la Mungu ili muda wote watumikie madhabahu.

  Ndio hiyo Malaki 3 inayotumiwa kuwaumiza watu wa Mungu kwa mambo ambayo hayapo. Japokuwa waliokuwa wanaambiwa na Malaki ni makuhani ambao walikuwa wamakusanya zaka ya waisrael na kushindwa kuipeleka kwenye hazina.( soma sura ya pili ujue Malaki alikuwa anaongea na akina nani)

  Suala kuwa Yesu alifundisha kanisa watoe zaka kwa mujibu wa Luk 11 ni kutoelewa maandiko. Ndio maana huwa nawashangaa ati siku ya sabato ilikoma lakini sheria ya zaka ilibaki.

  Wewe mwenyewe umesema kabisa kuwa Yesu alikuwa anaongea na mafarisyo, hakuwa anaongea na kanisa. Alikuwa bado hajaitimiza torati. Kwa hiyo torati ndo ilikuwa imeshika hatamu.

  Wasome mitume uone kama kuna hata mmoja aliwahi kufundisha watu watoe zaka.

  Hatubarikiwi kwa sababu tumetoa zaka.
  Kulazimisha watu watoe zaka ni kufanyia uchuuzi injili. Hakuna aliyeamriwa aishi kwa zaka katika kanisa.

  Hebu ona, mpaka watu wanaandikwa majina na kupewa kadi maalum, hiyo kitu imetoka wapi?

  Zaka ni toleo la hiari wala si lazima!

 22. Mrs Christina,

  Acha tu nijibu comment yako kwa ajili ya faida ya wana SG.

  Kwanza nataka ujue kuwa hatuanzi leo kujifunza habari ya zaka. Kuna mada za zaka za kutosha tu hapa SG tulishachambua sana.

  Nataka ujue jambo hili kuwa Ibrahim hakubarikiwa na Mungu kwa sababu ya kutoa zaka. Wakati anafanya hicho kitendo alikuwa alishabarikiwa vya kutosha.

  Lakini zaidi ni kwamba hakuwa kutoa zaka toka kwenye mali zake, bali toka kwenye nyara, tena mara moja tu.

  Kingine, utoaji zaka kwa torati ya Musa ulikuja chini ya ukuhani wa Lawi.

  Ukuhani wa Yesu kristo katika agano jipya hautoki kwa Lawi bali kwa Yuda ambaye hakuwahi kuambiwa aishi kwa zaka.

 23. Mungu akubariki sana Mtumishi MOSHI

  Asante Mtumishi Sungura kwa kumsaidia Yesu.Injili inasonga
  mbele kwa sababu ya changamoto zilizopo katika KUTOLIELEWA
  NENO LA MUNGU.Suala la zaka limepotoshwa mno ili kuwafanya
  wateule wa Mungu walio wengi waendelee kuwa masikini kwa siri!

  Kutoa ZAKA au fungu la kumi ni lazima siyo hiari!Katika agano
  la kale tunawaona watumishi IBRAHIMU na YAKOBO wakiongozwa
  na Roho Mtakatifu kutoa ZAKA(TAFAKARI MWANZO 14:17-20, MWANZO 28:20-22).Na kwa sababu ya kumtolea Mungu sehemu
  ya kumi ya KILA ALICHOWAPA, hawa ndugu walibarikiwa mno!

  KATIKA AGANO JIPYA Yesu anafundisha somo la ajabu sana
  kuhusu watu kuendelea KUTOA ZAKA.Na kwa ujumla Mwalimu wetu
  Yesu anaeleza namna sahihi ya kutoa ZAKA ambayo itamgusa Mungu!
  Katika LUKA 11:42, Yesu ANAHIMIZA KUHUSU KUTOA ZAKA ZINAZOAMBATANA NA MIOYO ILIYO SAFI.Yesu anasema kutoa ZAKA
  ni lazima lakini kwanza tuhakikishe tunasafisha mioyo yetu.Yesu anatutaka tutoe ZAKA ZILIZO HAI.Mungu haguswi na ZAKA ambazo
  hazijaambatana na moyo wenye adili na upendo.Hebu tutafakari
  kile ambacho Yesu anawaambia MAFARISAYO katika hii luka 11 msatari wa 42 “……..Ole wenu Mafarisayo kwa kuwa mwatoa ZAKA
  za mnanaa na mchicha na kila mboga na HUKU MWAACHA MAMBO
  YA ADILI, NA UPENDO wa Mungu.ILIWAPASA KUFANYA HAYO YA KWANZA,BILA KUYAACHA HAYO YA PILI”

  Hapa Yesu anawaambia Mafarisayo(ambao walikuwa wanaamini kuhusu
  ufufuo wa wafu) kwamba WANAPOTOA ZAKA NI LAZIMA WAHAKIKISHE WAMEJITAKASA KWANZA ILI WASITOE ZAKA CHAFU!
  Wasijionyeshe ya kwamba wanatii kuhusu kutoa ZAKA huku wamejitenga na upendo wa Mungu! SADAKA yoyote ambayo haijaambatana au kubebwa na moyo safi, Mungu huwa HAIPOKEI.Na
  wengine tumekuwa tukitoa mafungu ya kumi yaliyo kamili LAKINI
  YA WIZI NA DHULUMA.Yesu anatuambia OLE WETU!

  Wajumbe wa shetani wanajua vizuri sana hatari ya kuwaruhusu
  wateule wampe Yesu fungu la kumi(ZAKA).Ndiyo maana zaidi ya asilimia 70 ya wateule katika jiji la DAR-ES-SALAAM,TANZANIA wametekwa ndani ya huduma za manabii wa uongo(mashetani) na
  wanachokifanya ni KUMPA SHETANI FUNGU LA KUMI yaani wameweka
  bidii katika kutoa ZAKA katika MADHABAHU ZA SHETANI!!!Huduma
  za mashetani zinaendelea kuanzishwa kila kukicha TENA KATIKATI
  YA MAKAZI YA WATU.Kama unadhani nakutania nenda MIKOCHENI ‘A’
  ujionee mwenyewe!HATA HIVYO kama hutembei na macho saba
  ya ROHO MTAKATIFU utaambulia patupu.Huwezi kuyatambua kwa
  jinsi ya ufahamu wa mwilini.Ukimpa shetani ZAKA maana yake umetoa
  vibaya.

  Unaweza ukawa unatoa ZAKA katika madhabahu ya Mungu aliye hai
  lakini unatoa vibaya kama wale Mafarisayo ambayo Yesu aliwakemea
  na kuwaelekeza katika luka 11:42.Pia unaweza ukawa unatoa ZAKA
  YAKO kwa usahihi kabisa ukiwa na kusudi jema lakini kumbe unampa
  shetani!WAPO PIA MBWAMWITU AMBAO WAMEKAZANA SANA
  KUWAZUIA WATU WASIELEWE ZAKA NI NINI ILI WASITOE.Mafundisho
  potofu yapo mengi mno hasa katika hizi blog za injili na kwenye
  mikusanyiko.Roho Mtakatifu asipotuatamia sawa na 1 YOHANA 2:20,27
  hakika tutaendelea kufilisiwa KIMWILI NA KIROHO.

  MALAKI 3:1-6 inaeleza kwa uchache lakini kwa undani sana namna
  tunavyoweza kutoa ZAKA na DHABIHU kwa usahihi na hasara
  tunazoweza kuzipata kama tukitoa zaka na dhabihu zilizo kufa au
  tukiacha kutoa.Roho Mtakatifu anaeleza mambo yafuatayo kama
  hasara za kutotoa zaka au kutoa vibaya;

  1: Mungu anaacha kuwa karibu na sisi ili kutoa maamuzi
  juu ya maisha yetu badala yake watu wabaya ndiyo watakao
  tuamulia na kutawala hatima zetu!

  2:Mungu anaacha kutupigania dhidi ya wachawi,wazinzi,waganga,
  mafisadi na wote waliojaa dhuluma na uongo.Tunakuwa hatuwezi kupigana
  na manabii wa uongo.Tutaendelea kuonewa majumbani na makazini
  na isitoshe vilio vya wale walio wajane na yatima havitakoma!

  3:Haki zetu zote zitazuiliwa na mashetani nasi tutajaa hofu badala
  ya ujasiri katika kuwaza, kunena na kutenda!

  kumbuka hii usije ukasahau, KULINGANA NA MATHAYO 6:21 tunapotoa
  vibaya ZAKA ZETU kwa kumpa shetani, TUNACHOFANYA NI KUMPA
  UMILIKI WA MACHO NA MASIKIO YA MIOYO YETU na kumruhusu
  roho wa shetani atawale maisha yetu ya kila siku!!!

  Huu ni mwaka wa WATEULE KUJITAMBUA KIROHO ILI MOTO WA
  ROHO MTAKATIFU UTEKETEZE KAZI ZOTE ZA IBILISI.

  Mteule TUJIUNGANISHE NA MAFUNDISHO YA ROHO MTAKATIFU
  ILI NAFSI ZETU ZIKOMBOLEWE.

 24. Moshi,

  Comment yangu ya kwanza hapo juu nilipotuma nilidhani imepotea, hivyo nikaandika tena nyingine.

  Ndio maana zina mfanano fulani.

 25. Moshi, salaam!

  Sababu ya msingi ya Mungu kuamuru walawi wapewe zaka kama mbadala wa utumishi wao madhabahuni ni nini?

  Je hiyo sababu bado ipo hata kwa watumishi wa madhabahuni wa leo?

  Je, hawa watumishi wa Mungu leo, wanahitaji zaka au wanahitaji pesa?

  Kuna mfano wa mtume yeyote katika agano jipya ambaye aliwahi kuishi kwa zaka au,kusema mahali popote kwa kanisa kuwa watu watoe zaka?

  Karibu!

 26. Moshi, salaam!

  Hebu niambie sababu ya msingi ya walawi kupewa zaka kama mbadala wa utumishi wao madhabahuni!

  Kisha niambie katika agano jipya makuhani ni akina nani, na ni wapi Yesu au mtume yeyote alisema waishi kwa zaka kama mbadala wa utumishi wao madhabahuni?

  Mwisho, Je Yesu alifundisha nini kuhusu utoaji kwa kanisa lake?

  Karibu!

 27. Shalom
  Naomba na mimi niongezee hii maswali/majibu,kwa nini zaka kwa nini zaka iliamriwa kutolewa ukisoma hesabu 18:21 na wana wa lawi,nimewapa zaka yote katika israel kuwa urithi wao,badala ya huo utumishi wautumikao,maana ni huo utumishi wa hema ya kukutania anaengeza katika malaki 3:10 leteni zaka kamili ghalani ili kiwemo chakula katika nyumba yangu…..
  Zaka ni kwaajili ya Makuhani/wachungaji/mitume n.k mtu anayekataa kutoa zaka wakati kuna mtumishi awe mchungaji/mtume n.k anayemtumikia afanyi sawa na zaka ni sehemu ya sheria ya Mungu na hata ujio wa agano jipya Yesu akulivunja raisi tu kwa kuwa hakukuwa na tatizo katka ili

 28. KUMBUKA KUTOA DHABIHU KAMA ZAMANI ZA MUSA.

  Kama unatoa ZAKA bila kutoa na DHABIHU wewe unamwibia Mungu. Ole wao wanaotoa ZAKA lakini hawatoi DHABIHU ingelikuwa heri hata ZAKA wasingetoa maana ukivunja sheria moja umevunja zote.

  LETENI ZAKA KAMILI ILI KIWEMO CHAKULA GHALANI.

  Ole wao wanaotoa ZAKA katika mfumo wa fedha maana maandiko hayajabariki kamwe kutoa ZAKA ikiwa katika Mfumo wa FEDHA. Maandiko yanatambua ZAKA kwa maana ya MAZAO na MIFUGO pekee. Wapi maandiko yanasema watu watoe ZAKA ikiwa kwenye mfumo wa FEDHA? Ole wetu?

  Ole wao wanaopeleka ZAKA kanisani kwa maana imeandikwa “LETENI ZAKA ILI KIWEMO CHAKULA GHALANI” . Hapa maandiko yanasema GHALANI siyo KANISANI. Hivi makanisa ndiyo MAGHALA yanayosemwa hapa Malaki 3:8-10?
  Kwa ni nini watu wanapeleka ZAKA makanisani badala ya MAGHALANI kama maandiko yanavyoelekeza?

  Hayo maswali yanahitaji TAFAKURI NENE.

 29. Amina Mtumishi Sungura,

  Asante kwa kunifundisha,kwa kweli ninaendelea kujifunza mambo mengi makubwa
  na magumu(Yeremia 33:3).Kwa muongozo wa ROHO MTAKATIFU nimeona unachosema.Neno ‘andiko’ katika 2 Wakorintho 3:6 linamaanisha SHERIA(torati) zinazowaongoza watu wenye mioyo migumu,ni sheria zenye adhabu ambazo sio lazima zisimamie Haki!(2 Wakorintho 3:9).Alafu neno ‘andiko’ katika 2 Tim 3:16
  linamaanisha NENO LA KRISTO ambalo linabebwa na huduma ya Roho Mtakatifu.Hatuwezi kutenganisha kati ya Neno la kristo na Roho Mtakatifu,siku zote
  NENO na ROHO wanasimama pamoja,wanakaa na kula pamoja,wanaishi na kulala pamoja.Mmoja anapotangulia mahali hawezi kufanya kazi mpaka mwezake amefika!
  KILA NENO AMBALO ROHO MTAKATIFU ANAISHI NDANI YAKE LAFAA KWA MAFUNDISHO YA MUONGOZO,KUONYA,KUKOSOA NA KUADABISHA(TAFAKARI-2 TIMOTHEO 3:16).

  Kwa habari ya TORATI kuna kitu kilikuwa kimepungua ndani yake ndipo Yesu(upendo) akajanacho ili kuikamilisha.Maana yake ni kwamba yaliyokuwa yamepungua ndani ya AGANO LA KALE,Yesu ameyakamilisha ndani ya AGANO JIPYA.Ni lazima tujifunze kusoma AGANO LA KALE KWA JICHO LA AGANO JIPYA.
  Agano la kale limo ndani ya agano jipya lakini agano jipya halijamezwa na agano la kale!Kwa mfano katika agano la kale Musa aliwaruhusu watu kuwaacha wake zao kwa kuwapa TALAKA,si kwa sababu ilikuwa ni sheria ya Mungu bali KWASABABU YA UGUMU WA MIOYO YAO na Mungu akaliacha hilo chukizo kama lilivyo kwasababu ndivyo watu walivyotaka kuendesha maisha yao!(TAFAKARI-Mathayo 19:3-8).Hii inaonyesha sehemu ndogo tu ya ujinga na upumbavu uliokuwa ndani ya torati.SHERIA ZA MUNGU katika agano jipya zinaongozwa na upendo wa Roho Mtakatifu(TAFAKARI-Warumi 5:5) na siyo mioyo ya watu.Ndani ya agano jipya lililo bora zaidi tunaongozwa na NENO LA KRISTO NDANI YA ROHO MTAKATIFU NA ROHO MTAKATIFU NDANI YA NENO LA KRISTO

  Nimetabasamu kwa unyenyekevu nilipoona umenichokoza kwa hekima(upendo) ili
  nichangie kwa undani kuhusu suala la ZAKA katika kipindi hiki cha agano jipya.Nimeta
  fakari kwa kina michango ya wengine na mitazamo yao kuhusu ZAKA.Nimejifunza mambo mazito na ya kutisha sana.Kuna wakati nilizimia alafu nikazinduka!kuna wakati nilianguka alafu nikanyanyuka!kuna wakati nilijilazimisha kuruka nikashindwa ikabidi nichuchumae tu!kuna wakati nilitamani kulia nikajikuta nacheka na kuna wakati nilianza kucheka kumbe nilikuwa nalia!Hatimaye Roho Mtakatifu akanikumbatia na kunituliza.Na hili ndilo aliloniambia ‘SUALA LA ZAKA NI TAABU KUBWA AMBAYO MUNGU AMEWAPA ILI MTAABIKE NDANI YAKE'(TAFAKARI-MUHUBIRI 1:13,MITHALI 25:2).

  MOTO ULAO UWE PAMOJA NASI SOTE.

 30. Edwin

  Badala ya kukutaja wewe kwenye comment yangu hapo juu, nimemtaja Kamugisha.

  Hiyo comment nilikuwa nakujibu wewe, siyo Kamugisha tafadhali.

  Kumradhi!!!

 31. Kamugisha,

  Nilichotaka ufuatilie ni kujua Neno ,andiko’ iliyotumika 2cor 3:6 , iko tofauti kabisa na neno ‘andiko’ lililotumika 2 Tim 3:16.

  Kwa hiyo hayo maandiko mawili yanaongelea vitu viwili tofauti kabisa. Moja ile ya wakorintho kwa Kiingereza ni ‘letter’ na ile ya Timothi ni ‘ scripture’.

  Sasa tafuta tofauti ya letter na scripture ndipo utagundua kinachoua siyo scripture ni letter!

  Pia mimi sidhani kama ni sahihi kutii kitu ambacho ni maagizo ya watu, lakini wao wanatuambia ni maagizo ya Mungu.

  Unakuta mtu yuko kwenye mimbari anamwita mwizi, kibaka au mnyang’anyi mtu ambaye kristo kamfia msalabani ati just kwa sababu hajatoa zaka.

  Zaka ya kisheria ilikuwa kwa ukoo wa Lawi, leo ukuhani uko kwa Yuda ambaye hajaamliwa aishi kwa zaka kama alivyokuwa Lawi.

  Barikiwa.

 32. Namshukuru sana Yesu kwa kuendelea kutumia KIDOLE (kalamu) chake kuandika
  ndani ya moyo wangu mambo MAKUBWA na MAGUMU ambayo sikuyajua lakini sasa nimeyajua kupitia sadaka(michango) zinazotolewa na watumishi ndani ya blog hii(TAFAKARI-LUKA 11:20,KUTOKA 8:19,YEREMIA 33:3).Naendelea kujifunza changamoto mbalimbali kuhusu ZAKA.Napokea sadaka za ajabu sana.Mungu aliyeweka ROHO YA UNABII ndani ya wateule wake wote awabariki sana(TAFAKARI-UFUNUO 19:10).

  Ni wazi kwamba kuhusu ZAKA bado SIJAJUA KWA JINSI INIPASAVYO KUJUA(TAFAKARI-1 WAKORINHTO 8:2).Kwahiyo natakiwa niendelee kunyenyekea sana
  ili Mungu anipe NEEMA ya ufahamu na maarifa kuhusu ZAKA.

  UNYENYEKEVU ULIO HAI NI TAABU KUBWA AMBAYO MUNGU AMEWAPA WATEULE WAKE ILI WATAABIKE NDANI YAKE!!(TAFAKARI-MUHUBIRI 1:13,WAFILIPI
  2:3-8).Ukitaka watu wakupige mawe kwa jinsi ya rohoni na mwilini,wahubirie INJILI YA UNYENYEKEVU WA YESU.

 33. Ndugu yangu Sungura,Nashukuru kwa changamoto.

  Mada tuliyonayo imo ndani ya makanisa ambayo ibada zake zinafahamika.Kwa makanisa mengi ya kipentecoste au makanisa ya kikristo ibada zake kuu ni jumapili.Pia zipo ibada za katikati ya wiki.Hata jumapili bado kuna watu kutokana na shughuli zao hawawezi kuhudhuria kila jumapili,utii wao wanauonesha kwa kutoa taarifa na inajullikana wazi lakini vilevile bado kuna watu wanashindwa kuhudhuria kwa kutokutii.
  Kwenye fungu la kumi japo tunafundishwa kutoa lakini si wote wanaotoa ni hiari kuchagua lakini kutii na kutoa ni jambo la muhimu.1korintho 9:17-“Maana nikiitenda kazi hii kwa hiari yangu nina thawabu,ila ikiwa si kwa hiari yangu,nimeaminiwa uwakili”

  kuhusiana na equation (Andiko+Roho=Neno la Mungu).Hili lipo kwenye 2Timetheo 3:16-Kila ANDIKO lenye PUMZI(ROHO) ya Mungu lafaa kwa MAFUNDISHO(NENO).

  Yohana 6:63-“ROHO ndiyo itiayo uzima,….maneno hayo niliyowaambia ni roho tena ni uzima”.

  2korintho 3:6-“..kwa maana ANDIKO huua bali roho huuisha.Nguvu ya neno inatokana na uhai waa neno ambao unatokana na uwepo wa Roho aliyevuvia hilo neno.Nilichosisitiza awali ndugu Sungura ni kuwa tumwachie Roho wa Mungu atuongoze na kikubwa hapa tuangalie mambo yanayotujenga kiufahamu(hapa nawashukuru wote kwa michango) na pia yatakayotujenga kiroho.

  Barikiwa na Mungu.

 34. Edwin,

  Vipi mchungaji wako wa kipentekoste angeweka utaratibu kwamba kila Jumamos lazima kwenda ibadani kanisani, hakuna kwenda kazini,

  Unaonaje, wewe ungetii hiyo?

  Hebu kasome tena kwa ipana ikiwezekana uangalie version kadhaa za biblia hilo andiko linalosema ‘andiko huua bali Roho huhuisha’
  halafu uje ufanye tena hiyo equation yako (Andiko + Roho = Neno la Mungu).

  Soma vizuri hilo andiko linaloua ni li nini, then uone kama kitu kinachoua ukikiweka pamoja na kitu kinachohuisha kama jibu lake litakuwa pumzi ya Mungu. Yaani ati kifo + uzima = pumzi ya Mungu!!!

  Mweh, hiyo formula imeniacha hoi sana!!

 35. BWANA YESU ASIFIWE,ZAKA maana yake ni fungu la kumi,na fungu lakumi ni ile asilimia kumi ya kile unachokipata kny mikono yako,na fungu la kumi ni lazima kwa sababu usipomtolea mungu fungu la kumi means unamwibia mungu na unayahatarisha maisha yako cz mali zako au fedha zako au kazi yako haitakuwa na ulinzi wa mungu,fungu la kumi unaweza kuwa unatoa kila wiki wiki au kila mwezi.yani inatakiwa uwe mwaminifu kwa mungu khs zaka ili mungu awe mwaminifu kwako.

 36. BWANA YESU ASIFIWE,ZAKA maana yake ni fungu la kumi,na fungu lakumi ni ile asilimia kumi ya kile unachokipata kny mikono yako,na fungu la kumi ni lazima kwa sababu usipomtolea mungu fungu la kumi means unamwibia mungu na unayahatarisha maisha yako cz mali zako au fedha zako au kazi yako haitakuwa na ulinzi wa mungu,fungu la kumi unaweza kuwa unatoa kila wiki wiki au kila mwezi.yani inatakiwa uwe mwaminifu kwa mungu khs zaka ili mungu awe mwaminifu kwako.

 37. Mbarikiwe kwa michango mizuri,Mr.Milinga amechambua vizuri sana,niliguswa hasa na pale aliposema wengine wanamtolea Mungu zaka kama nadhiri walizomwekea Mungu.Ushauri wangu kwa kuwa Mungu ametuweka chini ya Watumishi wa Mungu tofauti ili tupokee hapo,Madhaifu ya kila sehemu Mungu anayajua lakini alikuruhusu kuwa mahali hapo,basi heshimu taratibu zilizopo hata kama unafikiri unajua sana(1kor 8:2-Bado hujui ikupasavyo kujua)-Kama kanisa linasisitiza fungu la kumi toa kikamilifu,usije mkosa Mungu-Ni bora Ukamwomba Mungu ukawa kanisa lisilotoa zaka kuliko kuwa mhasi kanisani.Lakini Wakina Ndugu Milinga Ni kweli makanisa mapoabudu hayasisitizi zaka?kama hayasistizi ni sawa lakini kama yanasisitiza ni muhimu ndugu Milinga ukatoa zaka.Jinsi nilivyomuelewa Mr.Milinga hapingani na utoaji tena anasisitiza utoaji zaidi kwa moyo wa kupenda.Tunapochangia mada ni bora tujikubali kwamba hatuji asilimia 100%,Paulo anasema tukiwa mbinguni tutajua yote-hivyo pamoja na ufahamu huo mzuri wa maandiko tumwache roho mtakatifu atuongoze mioyo yetu(Andiko huua lakini roho huiisha-(Roho+Andiko=Neno la Mungu).Tukae chini ya baba zetu wanaotulea kwenye makanisa ili tuishi.Ebrania 13:7(Wakumbukeni wale waliokuwa wakiwaongoza,waliowaambia neno la Mungu;tena kwa kuuchunguza sana mwisho wa mwenendo wao,iigeni imani yao).watakaotoa hesabu za roho zetu ni baba zetu(wachungaji zetu),Ebrania 13:17(watiini wenye kuwaongoza,na kuwanyenyekea;maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu,kama watu watakaotoa hesabu,ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua;maana isingewafaa ninyi).

  Mbarikiwe sana

 38. Lwembe,

  Umenigusa sana ,na nimejisikia kutiwa moyo sana.

  Ubarikiwe sana.

  Millinga na Ziragora, Mungu awabariki sana pia.

 39. Wapendwa,

  Chagueni moja: Biblia iiongoze dini yenu au Dini yenu ndio iiongoze Biblia!

  Kwa waliochagua Dini zao ndio ziiongoze Biblia, ni dhahiri kwamba wamejitia ktk vifungo vya dini, kwahiyo hawana uwezo wa kuyatafakari Maandiko, labda tukutane na wanyapara wao!

  Lakini kwa wenye shauku ya kuijua kweli, michango iliyotolewa ni toshelevu sana kuweza kuuinua ufahamu hata kama ni milimita moja tu, utaliona jambo hili linavyojifunua, ukiwa umejiachilia kiufahamu ili kuzidaka nuggets za “Kweli” zinazodondoshwa na nduguzo!

  Lakini kuna wapendwa masikio yao ya rohoni naona yalikwisha tiwa nta, wameng’ang’ana na uongo wa dini waliodanganywa kuwa ndio kweli na hivyo ile Kweli kwao imekuwa ndio uongo!!!

  Unapotaka kuliendea jambo lolote lile, hata likiwa ni la Zaka, itakusaidia ikiwa utalitafuta chimbuko lake, ili kulijua undani wake, kuliko kuyarukia tu Maandiko na kujibebesha mizigo isiyotambulika na Mkaguzi, maana Baraka hazimwagwi kiholela kama mnavyodanganywa, Mungu ana utaratibu wake, huo ambao ameuweka ktk Maandiko!

  Wapendwa wamefundisha sana kuhusu utaratibu huo kwa kina; mimi nitagusa tu highlights zake.
  Kwanza jambo la Zaka tunaliona kwa Ibrahimu akimtolea Melkizedeki, na pili kwa Yakobo. Ibrahimu alitoa kutoka ktk nyara mara hiyo moja, na Yokobo alimtolea Mungu fungu hilo la kumi kutoka ktk mafanikio kama alivyomuahidi, kwamba “IWAPO” Mungu atamfanikisha, basi atamtolea Mungu Fungu hilo la Kumi; waote wawili hawa hawakutoa kwa Sheria, yaani Mungu HAKUWATAKA wamtolee, hilo fungu la Kumi kwa kuwaagiza, bali walimtolea Mungu kwa IMANI, ule Ufunuo, ndio ambao unaonesha kupendezwa kwa Mungu na jambo hilo!!!

  Pili, Fungu la Kumi lifanywa Sheria kulingana na mpangilio mpya wa taifa la Israeli, hapo walipopewa Sheria kuwaongoza kuelekea huko watakakopewa IMANI. Mungu alilisimamisha kabila la Walawi kulipokea Fungu hilo la Kumi kutoka kwa ndugu zao waliopewa urithi ktk nchi, wao wakipewa hiyo Zaka kuwa ndio urithi wao. Kwahiyo Mlawi hakujishughulisha na shughuli yoyote ile zaidi ya hayo mambo ya Mungu, alikuwa ndio msimamizi. Huu ndio Msingi wa Zaka uliojengwa ktk Sheria iliyousimika ukuhani kwa Walawi.

  Lakini twasoma kwamba ukuhani huo uliojengwa juu ya Sheria ulibadilika ktk ujio wa Kristo, Ebr 7:12 “Maana ukuhani ule ukibadilika, hapana budi sheria nayo ibadilike.” Basi badiliko la Sheria likoje? Rm 10:4 “Kwa maana Kristo ni mwisho wa sheria” kwa lugha nyepesi Sheria imefika ktk ukomo wake pamoja na hiyo ya Zaka maana ukuhani unaopaswa uipokee hiyo kwa Sheria umeingia ktk mabadiliko hapo Sheria inapokoma!!!!

  Basi yeyote yule anapojirudisha kuitimiza hiyo Malaki ionyayo juu ya zaka, hiyo iliyoamriwa Israeli, kama hiyo bahasha inavyojieleza, ni vizuri iwapo wahusika wote watakuwa ktk ufahamu kamili wa jambo wanaloliendea, “Laana na Baraka.”

  Kwanza ni kwamba kwa hiyari yao wenyewe wanakuwa wamejiondoa ktk Neema na kujirudisha ktk Sheria, kwani kwa tendo hili wanakiri kwamba Kristo si Mwisho wa Sheria, hivyo basi wanapaswa kuyatimiza yote yanayohusu Sheria, jambo ambalo HAWALIWEZI, kwahiyo wanapotea kwa ujinga!

  Pili ni kwamba kulingana na Shetia inayoliongoza suala Zaka, hiyo hupokelewa na Walawi hao ambao hiyo ndio urithi wao. Mlawi huwa hajishughulishi na chochote kile zaidi ya mambo ya hekalu. Basi hawa wanaoipokea Zaka leo hii wakiwa wana miradi na wengine wamewafungulia wake zao shughuli au wameajiriwa nk, kwahiyo wanaipokea zaka hiyo kinyume cha utaratibu, yaani wanamwibia Mungu zaka hiyo na hivyo nao pia wanajitumbukiza ktk Laana, licha ya unono wa hayo mafungu wanayoyapokea yakionekana kama baraka!

  Lakini kwa walio ktk wokovu, hawa wamerudishwa ktk IMANI, ndio maana tunakiri kuwa tu wana wa Ibrahimu, huyo baba wa Imani, basi Mungu akikupa Ufunuoa wa kutoa Fungu la Kumi, atakuonesha na Mlawi wa kumpa na si hizo Sheria za kwenye vibahasha, hayo ni mambo ya dini, yanayodhirisha kwamba wokovu wanaouimba ni wa mdomo tu, issue yenyewe hawaijui kabisa!!!!!!

  Sikilizeni nyie watu wa Zaka bila Maarifa, mimi nimepewa ukuhani,
  1Pet 2:5 “Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo”;
  Basi nitumieni hayo mafungu yenu ya kumi jamani, tumieni kwa Tigo Pesa namba: ooo ooo ooo; nawaambieni, shuhuda zenu zitafika mpaka polisi mtakako kwenda kufungua RB!!!

  Gbu all!

 40. ZAKA NI BAADA YA MAPATO KINYUME NA HAPO NI SADAKA YA HIARI HYO SIO ZAKA TENA

  “NOTHING IMPOSIBLE TO GOD“

 41. Milinga,Sungura, Mabinza, Ziragora niseme mmenibariki sana!Wapendwa hakuna kitu kizuri kama kuijua kweli,maana ukiijua kweli hakika utakuwa huru kweli kweli mbali na uchafu,usanii,vitisho.na kili kitu cha jinsi hiyo.watu wanatakiwa walijue neno ili wafunguliwe ufahamu wao.na watakapofunguliwa ndipo watakapofanya sawasawa na neno na si sawasawa na mawazo ya watu au mitazamo ya watu.

 42. Stephen,

  Asante kwa kunibariki.

  Lakini unaponambia kuwa umenibana nakushsngaa sana. Kuna hoja gani imenibana nayo kiasi cha kunifanya nikasirik?

  Wewe hujui unachokisems ils unajismea tu. Ndio maana nilikushauri usome mada ya zaka tuliyokwisha ijadili sana na akina Seleli. Ungefanya hivyo kuna hoja hata usingepoteza muda khziandika.

  Ni kweli pia kwamba Millinga kachambua vizuri sana, cha ajabu tu ni kwamba kwa nini hayajakuelea hayo aliyosema Milinga, maana yako wazi mno.

  Hslafu ni kweli Ibrahi alitoa zaka kwa hiari, tena alitoa mara moja tu,tena si kutoka kwenye mali alizokuwa nazo bali nya8ra. Sawsa ninyi leo kwa nini zaka mnatàka tutoe kwa lazima, kama hiyo si torati ni nini,wasiotoa waliitwa wezi kwenye torati na ninyi mwawaita hivyo, si utoaji kwa mujibu wa torati sasa huo?

  Katika agano jipya magonjwa tumeponywa si kwa kutoa zaka, bali kwa kupigwa kwa Yesu!

  Ndiyo, Yesu aliwaambia hayo maneno mafarisayo, sasa sisi siyo mafarisayo wala masadukayo.

  Ubarikiwe!

 43. Sungura Mungu akubariki kwani biblia inasema wabarikini wanaowaudhi
  mimi ninacho ludia hapa sitaki kutuletea maneno ya kichwani biblia inasema leteni hoja zenye nguvu lete misitali ya biblia mimi nimpongeze ndugu Milinga ni mtu anaye jua kujenga hoja usikasilike unapobanwa na hoja
  kila mkija mnasema wakati wa sheria unaonekana husomi hata kile ninacho sema naludia kwa faida yako na wale wasipenda kupotezwa na kundi ambalo liko upande wako
  1.zaka ilitolewa kabra ya kipindi cha sheria baba yetu wa imani kwa hiari soma mwanzo 14:18..20 watu tuliookolewa tu uzao wa ibrahimu kwa njinsi tulivyo wazao wa ahadi(wagalatia 3:28,29) tunapaswa kuenenda kwa imani kama ibrahimu(warumi 4:12,16)
  hapa tunaona baba yetu wa imani anatoa kwa imani hata kipindi mnacho ng`ang`ania cha sheria kilikuwa bado hakijanza biblia inasema pasipo imani haaiwezekani kumpendeza mungu soma waebrania 10:38
  ujue kazi ya zaka ni kulinda maana Neno linasema atamkemea aibaye Yakobo alilielewa hili ndio maana anasema Mungu akimlinda yeye kwa kila atakalo anapata atakuwa anatoa zaka soma mwanzo 28:20..22 unaona alitoa kabra ya kipindi cha sheria na Yakobo alijua amemkimbia ndugu yake Esau alijua kimbilio ni mungu leo watu wanaibiwa mapato yao kwa magonjwa,misiba nk toa zaka kwa imani uone Mungu atakaavyo kulinda mimi ni shaidi baada yaa kuokoka nimemuona Mungu akinilinda kipekee natoa kwa imani na kwa hiari zaka 1/10
  sasa nyie mnaopinga mnasema yesu wala mitume hawajaongelea ebu nipe ufanunuzi mambo ambayo yalileta utata kwenye agano la kale Yesu aliyasemea kwa mfano sura la ndoa biblia inasema mafalisayo walimwendea wakajalibu wakimwambia je ?ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu (mathayo 19:3…12
  hebu tuone Yesu anapotoa ufafanuzi juu ya zaka ambayo watu ambao hamtaki kuokoka manapiga vita mimi nasema pingeni potosheni mtapata ujila wenu ukisoma katika mathayo 23:23 ole wenu waandishi na mafalisayo,wanafiki,kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari,na jira,,lakini mmeacha mambo makuu ya sheria yaani adili,na rehema na imani,hayo imewapasa kufanya,wala yale mengine msiyaache
  hii ina maana aliwaona wanalipa au kutoa zaka akawambia imewapasa kuendelea kutoa kama ingekuwa haitakiwi angewambia kama alivyo wambia kwenye maswala ya talaka
  mimi nazidi kusema kutoa zaka ni mpango wa Mung toka mwanzo acheni kuwapoteza watu wa mungu kwa kusingizia na kutafuta sababu zitawapoteza
  TOA ZAKA KWA IMANI NA MUNGU ATAKUBALIKI

 44. MR. Milinga,
  Umesema sawasawa Bro, watu tumetingwa sana!

  Sungura,
  ulivyowaambia watu kupitia Oscar ni sawa haswaaa, urafiki wa mtu na mchungaji wake usiwe sheria! Fungukeni wandugu.

  “Ufahamu ni chembe ya uhai!”

 45. Oscar,

  Si dhambi kumpa mchungaji wako sehemu ya mshahara wako,hata kama utaamua kumpa nusu yote kwa hiari yako.

  Usiifanye tu iwe sheria ya lazima kwa wengine .

  Ubarikiwe.

 46. Stephen,

  Nimecheka kwelikweli!!

  Lakini kwa kuwa umeamua kuja kwenye jukwaa hili, lazima akili yako itatolewa ujinga wa mapokeo uligabdanana ndani yako.

  Umeongea nini sasa kwenye comment yako, au unadhani unaongea na watu waliochanganywa na ulokole wakabakiza kazi moja tu ya kumvunjavunja leo shetani,kumkatakata, na kumtupa kuzimu,lakini sijui nani huwa amemuunganisha tena na kuwafanya wamvunjevunje tena?

  Huna tofauti na wachungaji ninawaonaga wanatokwa povu wakiwaambia watu kuwa wamelaaniwa alhali wanaowaambia hivyo ndio wanaowafuata siku za machangizo.

  Hebu sa uhalali wa ulazima wa zaka kwa mkristo leo,nA uyuambie huo uhalali uliagizwa na mtume nani,maana mitume wa Yesu wote hawajawahi kufundisha mtu atoe zaka.

  Lakini ili kujua kwamba akili yako ni ndogo sana ni vile ulivyosema kuwa ngoja useme maana ya laana halafu ulichokiita maana ya laana kimsingi ni sababu za mtu kulaaniwa. Inaonekana hata maana ya laana huijui.

  Jifunze namna ya kuongea unapokuwa unapngea na watu wenye akili.

 47. Wapenzi katika Bwana

  Kama wewe unataka kuwa milionea aliyeupata umilionea kwa kutoa sadaka kwa Bwana fuata kanuni ya Yesu Kristo katika Kutoa kwako. Achana na Kanuni za Agano la Kale ambazo kiukweli zimebaki ndani ya Biblia ili kuwa ukumbusho wa jinsi wenzetu walivyoishi katika Imani na Uchaji.

  Kanuni ambayo Yesu aliitoa naona wengi wa wahubiri wadogo kwa wakubwa hawaisisitizi. Na hii mimi ndiyo ninayoiona kuwa ya pekee sana katika kipindi hiki cha Agano Jipya kuliko nyingine utakazonisomea kwenye maandiko.

  Hebu isome hapa kanuni hiyo inasema hivi:

  “Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa. Kipimo cha kujaa na kushindiliwa na kusukwasukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho, ndicho mtakachopimiwa…….” Luka 6:38

  Kama unatamani kuwa milionea mwakani wewe anza kuwapa watu vitu. Wape watu vitu kama vile unga, nguo, mahindi, pesa, viatu, chakula, gari, nyumba, kiwanja, maharage, viazi, nk

  Unaweza kufanya hivyo iwe kwa wapendwa na wasiowapendwa. Unaweza kuwapa watu vitu bila kusubiri kupewa asante wala kupigiwa makofi.

  Wapeni watu vitu bila kubagua kumpa aliyekupatia. Iwe mchungaji, askofu, mjane, yatima, mkimbizi, fukara, maskini, kiwete, ombaomba, wenye uhitaji kama vile waliokumbwa na mafuriko, waliokumbwa na njaa au magonjwa ya milipuko, nk.

  Toa vitu vizuri vyenye uzuri na ubora. Wape watu vitu hata kama huwajui. Wasaidie watu bila kujali ni wa kanisani kwako.

  Wape watu vitu bila kujali wanaenda kuvitumia wapi au kwa njia ipi? Fanya hivyo kama vile unampa BWANA MUNGU WAKO na siyo wanadamu. Wape watu vitu na wewe utaona Mungu atakavyokubarikia na kufungua madirisha ya mbinguni kwako na utajiri utakavyokufuata kupitia kwa watu usiowajua.

  Toa vitu au pesa kwa kiwango chochote unachopima wewe mwenyewe. Nadhani umeona kwamba Yesu ametutaka tupime sisi wenyewe. Kipimo kile upimacho……. utaona kwamba Yesu alifuta kabisa utaratibu wa ZAKA. Zaka lazima upime 10%.

  Yesu alifuta utoaji wa ZAKA kwa kutupatia KANUNI mpya ya sisi wenyewe kupima kulingana na jinsi tunavyotaka kubarikiwa. Kama unataka kubarikiwa kwa 10% wewe endelea kutoa 10% ya mapato yako.

  Badala ya kupima kwamba unataka ubarikiwe mara 100% ambapo unaweza kuamua kutoa mshahara wako mzima eti sasa unafungwa na fundisho lisilokuwa ka Yesu la kutoa fungu la kumi halafu unakomaaa kutoa fungu la kumi kwa wachungaji au kanisani……!!!!!???? Nani kakuambia ukitoa Fungu la kumi unatakiwa uwape wachungaji? Walimu, Mashemasi, Waimbaji, Wainjilisti, Manabii, na Mitume nao mbona hawapewi sasa? Je, wao siyo watumishi?

  YESU AMETUPATIA KANUNI MPYA: WAPENI WATU VITU KWA KIPIMO MTAKACHOPIMA NINYI WENYEWE…………ILI NANYI MPEWE KWA KIPIMO KILE KILE MTAKACHOTUMIA.

  Mimi hadi sasa nashangaa watu wanaongangania kutoa 10%. Hivi hawasomi maandiko yahusuyo UTOAJI katika Agano Jipya?

  Ukiwapa Watu vitu au pesa nao wataleta pesa na vitu kwako hata bila kuwajua kwa kipimo cha kujaa na kushindiliwa kama wewe ulivyokuwa unatoa. Hii ndiyo siri ya kubarikiwa hadi kuwa milionea unayeweza kukopesha watu na bila wewe kuteteleka.

  “FANYA WEMA UENDE ZAKO USINGOJEE KUPEWA SHUKRANI”. Huu ni msemo wa kiswahili ambao unafanana na kanuni mpya ya kutoa ili ubarikiwe.

  Narudia, “……KAMA UNATOA SADAKA KWA LENGO LA KUPATA BARAKA YA FEDHA NA VITU…….” BASI TOA VITU AU PESA KWA KIPIMO UNACHOJIPIMIA WEWE MWENYEWE. MAHALI POPOTE, WAKATI WOWOTE, SAAA YOYOTE, KWA MTU YEYOTE NAWE UTABARIKIWA KWA MAMILIONI YA PESA NA VITU.

 48. bwana sungura na ziragora kumbe nikiamua kwa hiari kwamba kila mapato ninayo pata asilimia kumi nampatia mchungaji wangu si dhambi.

 49. Nataka niongeze neno kidogo.

  Nikikwisha gundua ile, rafiki yangu mmoja naye alikuwa ndani ya kanisa ingine akiwa mwaminifu sana kwa utoaji wa zaka. Alifanya hesabu kama yangu kabisa. Aliendelea pigwa na kupoteza hela pahali pa kubarikiwa. Alifika kuniomba shauri. Nikamuelezea mapito yangu lakini hakunifwata haraka. Ndipo akapigwa zaidi licha ya kuwa alikuwa na kazi nzuri sana. Alifikia kuniambia kama alianza kutoa kwa hiari, sasa anaona mafanikio.

  Alie na sikio amesikia!

  Mbarikiwe.

 50. Ndugu Milinga,

  Bwana akubariki kabisa. Umechambua mambo.

  Kipindi kimoja, mimi binafsi niliwai kuwa mwaminifu sana(100% mwaminifu) ndani ya utoaji wa zaka. Nikaishia kuona kama nimepigwa pahali pa kubarikiwa; nilipokonywa hata ile niliyokuwa nayo. Ndipo nikakaa, nikatafakari jambo hili “kwa nini ninapata kinyume na maandiko?”. Msishangae , hii ni haki kabisa. Kwa kipindi kile nikajikuta nimekwisha julikana kanisani kuwa tajiri licha ya kuwa nilikuwa bila utajiri kabisa. Waumini wenzangu walianza fika kuniomba mikopo ambayo sina. Nilifanya uchambuzi nikajikuta nimeheshimu sana hili toleo tena kwa imani. Kiisha kutafakari nikauliza Biblia. Ndipo nikaona mambo mawili.

  1) Kwa kuwa wachungaji wamependa pesa sana wanafundisha hiyo zaka ya zamani vibaya kwani wanasema ni 1/10 ya pato yote. Ndio maana kumbe mimi nilikuwa special kwani kwa waumini wengine ukitoa 1/10 wanafikiri ulitoa 1/1000 kwani hivi ndivyo wanafanya kwa kudanganya wachungaji. Hii ilisababisha waumini wengi, kupitia hiyo siri ambayo mashemasi wanashindwa weka, kuniwazia mimi nina pesa nyingi. Walikuwa wakikafanya hesabu hivi: Net Pay =Zaka x 1000 .
  Hapa wachungaji watufwate vizuri kwani wanapofika ku ile history ya Anania na Safira wanahubiri kama walikufa kwani hawakutoa. Ile ni uongo. Ukweli ni kwamba walikufa kwa sababu walidanganya Roho wa Mungu katika utoaji wao. Ni pale ndipo baadhi ya wachungaji wanapeleka waumini. Hence, mwisho wa ile utoaji wa zaka itakuwa kifo.
  Ndipo nikajiswali “je wa Israeli wao waliwezaje?” Biblia ikanipa majibu mengi na moja wapo hili : “Kumbukumbu la Torati 14:22 Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika MAONGEO yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwako baada ya mwaka.”
  Nikaona kama Maongeo, kwa lugha ingine ni faida ao baki. Ina maana, familia ilikula, ilivaa, kama ni harusi ziligharamiwa, nk…. mwisho ni kufanya account na kuona ni nini inayobaki kama hakiba, na hiyo ndiyo ilishurtishwa mtoke zaka. Tukizungmuzia salary, huwezi ikamata kama maongeo. Ile ni mbegu tu.
  Ina maana leo wachungaji, katika kuambatana na lililo na faida kwao licha ya kuwa halifae katika agano jipya, wanaomba isiyowezekana na wanaweka waumini waoga ao wasiyofahamu katika hali ya kudanganya Roho wa Mungu.

  2) Katika agano Jipya, zaka haina nafasi. Hivi nikajikuta nina imani katika lile lisilofaa. Ndipo nikaacha.

  Kwa leo ninaweza toa hata inayopita 1/10 lakini kwa hiari wakati nasikia royo yangu inanisukuma kutoa, yaani kwa hiari. Hiyo ni sadaka ya hiari ambayo ndiyo ilibaki yenyewe katika agano jipya. Naona ndipo mapigo ya kupoteza pesa imepunguka sana. Nilitoka ndani ya ujinga ule.

  Concllusion:
  -Wachungaji wawape waumini neno la kweli,wasiogope, watabarikiwa kuliko wale wanaodanganya wakristo.
  -Wakristo tuwe macho, tusome biblia sana.

  Mungu awabariki.

 51. Bwana Yesu asifiwe wapendwa
  kwanza nikupongeza ndugu yangu Edwini kwa mchango wako na pia nataka nimshangae ndugu yangu Sungura mimi simuelewi na huwa sielewi anafanya makusudi mimi sipati picha ?

  ebu nije kwenye mada wengine wanawapotosha wapendwa ebu niwambie mnaosoma mahali hapa ebu muwe makini mtu asiwe mchangiaji kwa kutumia akili alete hoja za nguvu na ushahidi wa maandiko sio kuleta maneno ya kichwani
  Ebu fuatana nami sasa kutoa zaka ni mpango wa Mungu toka mwanzo mpaka sasa tunatakiwa kutoa zaka kwa uaminifu
  1.nianze na maana ya laana laana inampata mtu anapokosa utii iwe kwa wazazi au Mungu sisi ni watoto wa Mungu yohana 1;12
  lakini itakuwa usipotaka kusikiliza asuti ya Bwana Mungu ako usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake nikuagizazo hivi leo,ndipo zitakapokujia laana hizi zote (16)utalaniwa mjini,utalaniwa mashambani. soma kumbu kumbu la tolati 28:15……58
  mnapinga kutoa zaka sielewi mnamwamini Yesu kama bwana na mwokozi wa maisha yenu au bado mnapinga hata wokovu angalieni msije mkawa na roho za akina kora watu wa kupinga kila kitu.

  kwani Yesu anakusudia mtu anapokuwa amemwamini Yesu ankuwa mtu wa kutii si wa kupinga maneno ya Mungu au kuchagua mambo mepesi na kuyaacha mambo magumu hizo ni hila za shetani unajua sisi ni raia wa mbinguni kama unavyo ona serikali mbalimbali hapa duniani kuna kodi kwa ajili ya kuendeshea nchi viongozi wa hapa wameiga serikali ya mbinguni hii zaka wakati mwingine iliitwa kodi ya Bwana ebu soma maandiko haya hapa chini.

  sisi ni raia wa mbinguni waefeso 2:19
  hii ilikuwa inaitwa kodi ya Bwana 2nyakati 24:9..11,hesabu31:37…39
  jambo lingine ebu nieleze kazi ya zaka ni nini ?
  1.kuwa na chakula nyumbani mwa bwana (malaki 3:10) chakula ni kazi ya Mungu soma yohana 4:34) zaka inafanya kazi ya Mungu ifanyike Yesu kazi yake kuja hapa duniani alikuja kutafuta na kuokoa watu wenye dhambi pia Mungu anasema hapendi kuona hata mtu mmoja anapotea bali wote anataka waookolewe sasa leo maelfu ya watu wanaendelea kupotea kwa madawa ya kulevya ,pombe ,uzinzi, wizi,rushwa. nk kisa watu hawataki kumtolea Mungu zaka
  soma warumi 10:13.. .15 kwa kuwa kila atakayeliitia jina la Bwana ataokoka,(15) tena wahubilije,wasipopelekwa
  mwisho nije kwenye mgawanyo wa hii zaka mungu amekusudia kuwawezesha watumishi wa Mungu kuitumia kwa kueneza injili,kupeleka semina,mikutano ikiwa pamoja na wageni,masikini,na wajane wa kweli pamoja na matumizi kwa watumishi wa Mungu
  sasa sungura kama kanisani kwenu haya hayafanyaki usifikili ndio makanisa yote,watumishi wote wanafanya hivyo pole acha kuwakosesha wana,watu wa Mungu ninawasihii wote mtoe zaka kamili ziko baraka tele nikirudi kwa mara nyingine nitatoa baraka zinazotokana na utoaji wa zakakamili.

  Mungu wa mbinguni awabaliki ni mimi mtumwa wa Kristo… Stephen Ngullo

 52. ……………………………..MWANIIBIA ZAKA NA DHABIHU…………….maana yake nini?

  Je, KUTOA ZAKA peke yake bila kutoa na DHABIHU ni sawa? Mbona Mal 3:8-10 inatamka vyote vitolewe pamoja? Je, mtu asipotoa DHABIHU anakuwa amemwibia Mungu? Mbona sioni watu makanisani wakitoa DHABIHU kama ilivyo kwenye ZAKA?…….

  Mpendwa, Zaka na Dhabihu vimetajwa kwa pamoja kwamba vinaendana. Hutakiwi kutoa zaka kama hutoi dhabihu kwa Mungu. Kama umeamua kufuata sheria moja unapaswa kuzifuata zote ili usihesabiwe dhambi. Ukifuata sheria moja ukavunja nyingine bado wahesabiwa laana na umevunja sheria.

  Siku moja nilimuuliza mtumishi mmoja wa Mungu, hivi ni kwa nini watumishi wengi kama siyo wote huwa wanahubiri kwamba kutokutoa zaka ni wizi kwa Mungu lakini swala la kutoa dhabihu halipewi uzito unaolingana na swala la zaka? Mtumishi huyo hakuweza kunipa jibu hadi leo.

  Maandiko ya Malaki 3:7-10 yanatumika sana kuhamasisha wakristo kutoa sadaka aina ya zaka.

  Wapo wahubiri wengi sana wametafsiri andiko hilo kwa namna nyingi kila mmoja akifafanua anavyoweza. Watu wengi sana makanisani wamelielewa andiko hilo kuwa mkristo asiyetoa zaka ni “mwizi” ni “jambazi” ni “kibaka” na majina mengi sana yamekuwa yakitumika kuwataja wasiotoa zaka.

  Kuna wakati makanisa mengine huweka hata sheria za kuwabana waumini wasiotaka kutekeleza kwa vitendo andiko hilo.

  Wapo wachungaji wengine wamefikia hatua za kuwatenga waumini wao wasiotaka kutekeleza andiko hilo la kutoa zaka. Wapo wachungaji wengine ambao hukataa hata kuwapa waumini wao huduma za kiroho kama vile huduma za ibada ya ndoa, ibada ya mazishi au jambo lolote kama tu waumini hao wataonekana kuwa hawatoi zaka.

  Yapo madhehebu mengine ambayo yameweka swala la kutoa zaka kuwa la kikatiba zaidi kwenye KATIBA ZA makanisa au madhehebu yao.

  Kwa hiyo kutoa zaka limewekwa kuwa swala la sheria kanisani kwa mujibu wa katiba za kanisa kabisa na kwamba muumini asiyetimiza matakwa ya katiba ya kanisa na kutotimiza agizo la katiba ya kanisa atachukuliwa hatua za kinidhamu kwani itakuwa utovu wa utii kwa mamlaka za madhehebu hayo.

  Ukichunguza makanisa mengine hapa Tanzania yameweka utaratibu wa kuwa na vitabu maalum kama vile kitabu kikubwa (Counter Books) ili Kuweka kumbukumbu za waumini wanaotoa zaka.

  Makanisa hayo yanafanya hivyo kwa ajili ya kurahisisha kuwabaini waumini wasiotaka kutoa zaka kanisani na kuweza kuwabana.

  Makanisa mengine wanaweka utaratibu wa bahasha maalum za watoa zaka. Bahasha hizo huwekwa mahali pa wazi au hutunzwa mahali maalum na mashemasi au wazee wa kanisa au wahudumu wa kanisa ili kila muumini apewe pindi anapotaka kutoa zaka siku za ibada.

  Kila muumini anayetoa zaka kupitia bahasha hizo huandikwa jina au namba yake juu ya bahasha na huandika kiasi alichotoa. Kwa kufanya hivyo baadhi ya makanisa huwa na utaratibu wa kutoa stakabadhi au risiti kwa kila anayetoa zaka yake. Yaani kanisa linakuwa na kitabu cha kukata risiti za kukiri kupokea zaka iliyotolewa.

  Makanisa mengine yameweka utamaduni wa kuwataka waumini wote wanaofanya kazi za kuajiriwa serikalini au mashirika na makampuni wawasilishe hati zao za mishahara (salary Slips). Makanisa hayo hufanya hivyo ili uongozi wa kanisa ujue wazi na dhahiri kiasi halisi cha mishahara yao kabla ya makato yoyote ya kisheria kama vile kodi, marejesho ya mikopo, makato ya hifadhi ya jamii na bima ya afya.

  Yaani wanatakiwa kuleta hati zinazoonesha hali halisi ya mshahara ghafi(basic/gross salary). Kwa Kuwasilisha hati za mishara (salary slips) kiongozi wa kanisa atajua wazi kila muumini anapaswa kulipa zaka kiasi gani kwa mwezi.

  Kwa mfano:
  Kama wewe Mshahara wako ni Tshs 1,200,000.00 kwa mwezi unatakiwa kila mwezi utoe Tshs 1,200,000 x 10/100 = Tshs 120,000 kila mwezi. Hii haijalishi kwamba wewe unakatwa makato ya Pensheni, Bima ya Afya, Chama cha Wafanyakazi, SACCOS, Marejesho ya mkopo uliochukua Benki ya NMB au CRBD, nk. kama umewahi kukopa kutoka benki. Malipo halisi baada ya kutoa makato yote(Net pay Salary) ni Tshs 750,000. Na ukitoa ZAKA Tshs 120,000 ambayo huwa haionekani kwenye Salary Slip yako utapaswa ubakiwe na Tshs 630,000 kwa mwezi.

  Kwa hiyo tunawezaa kufupisha kuwa Salary Slip yako inapaswa kuonekana hivi:

  Basic Salary …………………………………………………………….Tshs 1,200,000.00
  Toa Income Tax (PAYE= 30%)……………………………………………Tshs 360,000.00
  Toa Bima ya Afya (3%)……………………………………………………..Tshs 36,000.00
  Toa LAPF, NSSF, PPF, PSPF, (10%)……………………………………Tshs 120,000.00
  Toa CWT, TUGHE, TUICO, nk (3%)……………………………………..Tshs 36,000.00
  Toa Mkopo wa Benk CRDB, NMB, nk (kama upo)…………………..Tshs 150,000.00
  Toa ZAKA (10%)……………………………………………………………….Tshs 120,000.00
  Jumla ya makato (Total deductions)…………………………………Tshs 822,000.00

  Net Pay in Hand/at Bank……………………………………………………Tshs 378,000.00

  Kwa maelezo hayo mfanyakazi wa serikali au mashirika ya umma na ya binafsi mwenye mshahara wa Tshs 1,200,000 kwa mwezi anapaswa aambulie Tshs 378,000 kwa mwezi.

  Kama akimaliza marejesho ya mkopo aliochukua benki au SACCOS alipokuwa anakatwa Tshs 150,000 kila mwezi ndiyo kusema kwa mwezi atapata Tshs 538,000.00 kwa mwezi

  Kama halipi zaka kila mwezi atapata Tshs 538,000.00 + 120,000 = 658,000.00.

  Unaweza kujifunza jinsi ilivyo KONGWA kubwa sana kila mwezi kulipa kutoka kwenye mshahara wako bila kusema kuna siku malipo hayo yatakoma. It is all along your life in Christ.

  Je, hapo utasema kwamba umebarikiwa kwa kulipwa Tshs 1,200,000 kama mshahara lakini baada ya makato ikiwemo ZAKA unabakiwa na Tshs 378,000?

  Je, ulishawahi kuona mtumishi wa serikali mwaminifu kwa serikali na kanisa ambaye amepanda chati hadi kuwa milionea kwa sababu amekuwa mwaminifu kwenye kutoa ZAKA? Mimi sijamwona!!!!! Wafanyakazi wengi serikalini ni masikini na watu waliokata tamaa. Wengi hawana furaha kabisa hata inapofika mwisho wa mwezi kwa sababu anajua kuwa waliomkopa wanamsubiri ikiwemo kanisa linamsubiri apeleke ZAKA.

  Kumbuka kuwa, Muumini asiyepeleka hati yake ya mshahara anatengwa kanisani. Muumini atakayeleta zaka isiyolingana na ukweli ulioko kwenye hati yake ya mshahara (yaani BASIC SALARY) atafukuzwa kanisani kwa sababu amewasilisha zaka isiyokuwa kamili yaani isiyokuwa 10% kutoka kwenye Tshs 1,200,000. Kumbuka kuwa kuna waumini wengine wanataka walipe ZAKA kwa kutumia kiasi kinachobakia kwenye mshahara baada ya makato yote. Hii kwa mujibu wa makanisa kama yale yanayotoa BAHASHA ni makosa. Hiyo ndiyo wanayoita ZAKA = MALIPO YA KABLA.

  Yaani ni malipo unayolipa kabla ya kukatwa vitu vingine vyote vya kisheria kwa mujibu wa sheria za nchi na mkataba wako wa ajira.

  Makanisa hayo yanasema kwa kufanya hivyo wanafukuza laana makanisani inayoweza kuletwa na watu wasiotoa zaka kamili.

  Tukijaribu kulichambua andiko maarufu kuhusu zaka tutagundua kwamba pamoja na kwamba andiko lasema,”….mwaniibia ZAKA na DHABIHU…..” wahubiri wengi na walimu wa andiko hilo wameendelea kuhamasisha utoaji wa zaka peke yake tofauti na maelekezo ya andiko lenyewe. Na hapo ndipo utagundua kwamba panahitaji uelewa mkubwa na uchambuzi usiogemea mapokeo yoyote ya kanisa.

  Hakuna anayehubiri kuhusu DHABIHU. Wengi wameendelea kuweka utaratibu wa utoaji ZAKA peke yake kana kwamba andiko hilo linawataka waumini watoe zaka peke yake na kana kwamba ndiyo pekee watu wanamwibia Mungu.

  Kumbe hata kutokutoa dhabihu ni wizi? Hebu tafakari kwanza. Ni wahubiri wangapi wanakazia waumini kutoa dhabihu kama yasemavyo maandiko?

  Wahubiri karibu wote hawasemi kuhusu Wizi wa “Dhabihu”. Hakuna wahubiri wanaohimiza waumini wao kutoa “dhabihu”. Utoaji wa dhabihu hausemwi na wala haisisitizwi kamwe.

  Ni kana kwamba “dhabihu” haina tatizo na wala haitakiwi kutolewa kwa Mungu kwa mujibu wa andiko hilo hilo.

  Hivi, mpendwa wanguu, kama wewe ni mkristo umewahi kutoa “dhabihu?”

  Hakuna kanisa linalosisitiza utoaji wa dhabihu kabisa. Kila mmoja amekazana na zaka. Swali kubwa la kujiuliza ni “Je, zaka tu ndiyo inayoibwa?”

  Jiulize swali hili kisha ujitafutie majibu:

  KWANINI WATU HUPENDA KUITEGEMEA TORATI ILIYOKUJA KWA MKONO WA MUSA KULIKO NEEMA NA KWELI ZILIZOKUJA KWA MKONO WA YESU KRISTO?

  Endelea kujifunza NENO zaidi ili uwe huru kweli kweli.

 53. HISTORIA FUPI YA KWA NINI WAPENDWA WAKRISTO WANADHANI UTOAJI WA ZAKA BADO NI SHERIA HALALI KWA VIZAZI VYOTE MPAKA LEO HII

  Pamoja na kwamba wapendwa katika Kristo tunakubaliana kwamba TORATI ilishaisha matumizi yake baada ya Agano Jipya kuanza kwenye swala la utoaji ZAKA bado hatujaelewana. Pamoja na kwamba kwenye ZAKA hatuelewani ila kwenye maswala mengine inaonekana kuwa tunaelewana ikiwemo KUTOTOA KAFARA YA WANYAMA au tuseme DHABIHU kama ilivyoamuriwa pia.

  Hebu tazama, bado Wapendwa wengi kama siyo wote hukubaliana kwamba kuna Baadhi ya sheria zilizokwishapitwa na wakati hasa baada ya Yesu kufa msalabani.

  Baadhi ya sheria ambazo hukubaliana kwamba hazitumiki katika Agano Jipya ni:

  1. Kutoa sadaka za kafara ya wanyama,

  2. Sheria ya tohara kwa wanaume,

  3. Sheria za kutunza sabato yaani kusali Jumamosi kwa lazima,

  4. Sheria za kutokula baadhi ya Vyakula vitokanavyo na wanyama kama vile kambale, nguruwe, sungura, nk,

  5. Sheria za kushika miandamo ya mwezi na siku kuu.

  6. Sheria ya kutoa talaka na kuoa mke mwingine ambapo wakati wa agano la kale ilikuwa ruksa kutoa talaka lakini Agano Jipya wakristo wote wanakubaliana kwamba talaka imekatazwa na Yesu Kristo na kwa kweli hakuna Mchungaji wa Kikristo anayeruhusu talaka.

  7. Sheria nyingine ya Agano la kale iliyopitwa na wakati ni ile ya kuwazuia makuhani wasiruhusiwe kumiliki ardhi ambapo wanaoitwa makuhani wa sasa (wachungaji) ingawa siyo sahihi, wote wanaruhusiwa kumiliki ardhi.

  Hivyo basi, Wakristo wengi wanakubaliana kwamba sheria hizo na nyingine nyingi zilikoma mara baada ya kifo cha Yesu.

  Wapendwa Wengi wanakubaliana kwamba Utoaji wa sadaka za wanyama uliendelea hadi Yesu Kristo aliposulubiwa msalabani basi.

  Wapendwa wote wanakubali kwamba damu ya Yesu iliyomwagika msalabani ilifuta utaratibu wa kuchinja wanyama kwa ajili ya ondoleo la dhambi za watu.

  Wapendwa pia wote wanakubaliana kwamba damu ya Yesu ilisitisha taratibu zote za sheria ya Musa zilizotaka watu watoe kafara ya wanyama kwanza ndipo wasamehewe dhambi zao.

  Wakristo karibu wote wanakubaliana kwamba sheria hizo zilikoma kutumika kwa sababu ya kifo cha Yesu msalabani.

  Hakuna Askofu wala Nabii anayebisha kwamba taratibu na sheria za Torati ya Musa zilikoma mara tu baada ya kanisa la Pentekoste kuzaliwa siku ile ya Pentekoste.

  Wakristo wapendwa karibu wote duniani wanakubali kwamba siku ile ya pentekoste ndiyo siku ambayo miiko mingi ya agano la kale ilikoma kutumika hekaluni na ibadani.

  Wapendwa karibia wote wanakubali kuwa kuanzia siku ile ambayo zaidi ya watu 3,000 waliamua kuokoka na kumfuata Kristo Yesu baada ya mahubiri ya Petro Mtume na wenzake ndipo kanisa la kwanza lilipozaliwa.

  Siku ile Roho Matakatifu aliposhuka kwa mara ya kwanza kanisa likaanza kuchipuka kwa kasi ya juu. Wakristo wengi wanakubali kwamba kanuni za uendeshaji ibada na utoaji wa sadaka ulikuwa mwisho.

  Kwa mujibu wa maandiko hata historia inaeleweka kwamba, baada ya kifo cha Yesu msalabani, Kanisa jipya la Agano Jipya lilianza likiongozwa na Mtume Petro Jijini Yerusalem na liliendeshwa na kusimamiwa kwa utaratibu mpya kabisa ambao haukuegemea utamaduni wa jinsi Musa alivyokuwa akiendesha ibada wakati wa Agano la kale.

  Wote tunasoma maandiko kwamba utaratibu wa sadaka za hiari kama vile michango, watu kuuza mali zao, kujitolea kwa muda wao, nk ndivyo vilivyotumika kulifanya kanisa lienee dunia nzima.

  Historia ya kanisa la kwanza haioneshi kuwa gharama za kuhudumia wachungaji na mitume zilitokana na kanisa kutoa Zaka.

  Zaka hazionekani kamwe zikitajwa na mitume kuwa zilikuwa miongoni mwa matoleo yaliyoliwezesha kanisa la kwanza kukua na kusambaa mpaka Afrika, Ulaya na Asia yote.

  Wapendwa wote tutakubaliana kwamba Kanisa la kwanza halikuendeshwa tena na makuhani wa kabila la Lawi walioambiwa chakula chao ni zaka tu.
  Kanisa la kwanza lilisitisha utamaduni na utaratibu wa Musa wa kutoa kafara za wanyama ili wasamehewe maovu yao.

  Tukumbuke kwamba nyakati za Musa Kafara ilikuwa ndiyo njia pekee iliyotumika kuwasaidia watu waliokuja kutubu maovu yao waweze kusamehewa lakini enzi za kanisa la kwanza huduma hii iliondolewa hapakuwepo na utaratibu wa kutoa sadaka fulani ili mtu atendewe jambo fulani na Mungu ikiwemo wale waliokuwa wanataka Baraka kifedha .

  Utaratibu wa kuendesha ibada za kanisa kwa mtindo wa Agano la Kale ikiwemo kutoa zaka na dhabihu (kafara) iliyokuwa ni chakula cha wakimbizi, wajane, yatima na kabila la Lawi lililoteuliwa kuwa kabila la kikuhani ulikomea hapo hapo. Kanisa la kwanza halikupenda wala kutaka kuendeleza tamaduni za Agano la kale kama kanisa la leo tunavyotaka iwe.

  Kwa hiyo, kama wewe unasema umebarikiwa kwa sababu ya kutimiza sheria ya kutoa ZAKA inabidi wapendwa waone ishara hii aliyoitoa BWANA Mungu kwa wapendwa wote wanaosema wamebarikiwa kifedha; …………………. BWANA Mungu wenu atawabariki kama alivyoahidi, nanyi mtawakopesha mataifa mengi lakini hamtakopa kwa ye yote….….” (Kumb. 15:4-6).

  Ukitaka kujipima kuwa umebarikiwa iwe ni kwa sababu umetii sheria ya zaka au umetoa kwa hiari sadaka yoyote ni kule kuwa na uwezo wa kukopesha watu wengine hata wasiokuwa wa imani yako yaani mataifa. Hadi pale Afrika itakapoanza kukopesha mataifa ndipo tutasema imebarikiwa.

  Na wewe pia hadi tutakapoona unaweza kuikopesha hata serikali au mashirika ya umma au watu wengine bila ya wewe kutetereka kifedha ndipo tutasema umebarikiwa.

  Kwa sasa kuna kasumba ya watu kudhani wamebarikiwa kwa sababu wana gari moja au mbili au nyumba moja au mbili nakudhania wamebarikiwa. Siyo kweli. Kama huwezi kukopesha watu hadi wasiokuwa walokole bado hujabarikiwa kwa mujibu wa andiko hilo Mungu alilowaapia Waisrael.

  Endelea kujifunza nawe utakuwa huru kweli kweli.

 54. Dah, Milinga.

  Umekamua shule tamu saaana mpendwa, bravo!

  Huwa nawauliza watu, kwamba mtu ambaye Yesu kamwokoa kwa kumfia msalabani ati aje amlaani kwa sababu hajatoa fungu la kumi, lakini amewakumbuka yatima, wajane, wahitaji na wenye mahitaji mbalimbali ambao hao wanakusanya hicho kiitwacho zaka ati ili kiwemo chakula ghalani mwa Bwana hata huwa hawawakumbuki watu hao.

  Milinga ulishaon makanisa mangapi ambayo siku za ibada watu wenye mahitaji (ombaomba) hukusanyika katika malango ya mahekalu yao kusubiri kupewa misaada?

  Kma hujaona ni kwa sababu huwa hawapewi. Sasa mimi najiuliza ghalani mwa Bwana ni mfukoni kwa mchungaji?
  Zaka leo imekuwa mali ya mchungaji na mke wake,kana kwamba wao pekee ndio watenda kazi nyumbani mwa Bwana. Waimbai hawapewi wanaambiwa wajitolee( sijui Mungu aliwahi kutumikiwa na nani kwa kujitolea), mashemasi hawapati, wajane hawapati, yatima hawapati, n.k!

  Zaidi sana hao wajane na yatima na maskini wengine wengine ndio wanaokamuliwa ili kumtunza mchungaji.
  Nawaambieni ole wenu wachungaji wa namna hiyo, mna kesi ya kujibu siku mwenye kanisa akirudi.

  Asilimia kubwa ya watoa zaka wanaitoa kwa vitisho na hofu, kwa mantiki hiyo wanaitoa kwa manung’uniko ya kutosha tu. Ndio maana sehemu kubwa ya kanisa haina financial breakthru.
  Ndiposa mimi husema zaka imeongeza laana ya umasikini kwa sababu watu wameng’ang’ania sheria ambayo hawawezi kuitimiza kwa ukamilifu.

  Yesu alisema, Give and it shall be give to you, a good measure, pressed down, shaken together and running over….(Luk 6:38)
  (Inayosemwa hapa siyo zaka). Lakini hii ndio financial breathru kupitia kutoa, siyo hiyo ya madirisha ya mbinguni, mbinguni hakuna pesa, pesa ziko kwa watu hapahapa duniani.

  Na mimi Milinga nilishaamua kumuiga Paul na mitume wengine!!!
  ………

  Lusubisyo, gloss income ni kitu gani hicho?

 55. Unatoa asilimia kumi ya income yako I mean gloss income name unatoa baada ya kupata kipato

 56. LAANA LAANA LAANA LAANA LAANA AMELAANIWA ASIYETOA ZAKA.

  Maandiko yametaja mara nyingi neno LAANA. Lakini ukichungulia sana utaona kwamba Laana iliendana na sheria. Ndiyo maana nyakati za Agano la Kale kitu kikishakuwa sheria ilikuwa ni lazima mtu akitii na asipotii alilaaniwa.

  Ukifuatilia Mtume Paulo utaona kwamba anakanusha kabisa kwamba katika Kristo hakuna laana tena. Utaona kwamba ukimwamini Kristo swala la kulaaniwa tena halipo kwa namna yoyote kwa sababu hatubarikiwi kwa sababu ya kuzitii sheria za Kale.

  Kwa mfano tazama hapa Mtume Paulo anasemaje katika Galatia 3:10-14
  10Kwa maana wote wanaotumainia matendo ya sheria, wako chini ya laana, kwa kuwa imeandikwa, “Amelaani mtu yule asiyeshika na kutii mambo yote yaliyoandikwa katika kitabu cha sheria.’’ 11Basi ni dhahiri kwamba hakuna mtu ye yote anayehesabiwa haki mbele za Mungu kwa sheria, kwa maana, “Mwenye haki ataishi kwa imani”. 12Lakini sheria haitegemei imani, kinyume chake, “Ye yote atendaye matendo ya sheria ataishi kwa sheria.” 13Kristo alitukomboa kutoka katika laana ya sheria kwa kufanyika laana kwa ajili yetu, kwa maana imeandikwa, “Amelaaniwa yeye aangikwaye juu ya mti.” 14Alitukomboa ili kwamba baraka aliyopewa Abrahamu ipate kuwafikia watu Mataifa kwa njia ya Kristo Yesu, ili kwa imani tupate kupokea ile ahadi ya Roho.

  Kwa hiyo kama wewe unataka kuendelea kuishi chini ya sheria inabidi ushike torati yote. Zaka ni miongoni mwa sheria za torati wakati wa Musa. Kushika sheria ya kutoa zaka huku ukiacha kushika torati yote ikiwemo kusali siku ya SABATO na kutokula KITIMOTO ujue unavunja TORATI na hivyo unaendelea kuishi chini ya laana. Hii ni kwa mujibu wa maandiko niliyoyanukuu kwa Paulo Mtume.

  Kristo alitukomboa katika laana ya TORATI pale alipofanywa laana kwa ajili yetu. Huwezi ukahesabiwa haki yaani kubarikiwa kwa sababu umeshika sheria ya zaka. Mungu hukubariki kwa Imani. Siyo kwa matendo ya sheria. Wote wanaotoa zaka kwa mujibu wa sheria hawawezi kukwepa laana itokanayo na kutafuta mibaraka ya Mungu kwa njia ya MATENDO badala ya njia ya IMANI.

  Wapendwa, pamoja na maandiko hayo ya Malaki 3:8-10 kusema kwamba amelaaniwa asiyetoa zaka tuelewe kwamba ilikuwa nyakati za Agano la Kale. Lakini kwa Agano Jipya HAKUNA KULAANIWA TENA KWA KUTOSHIKA SHERIA HIYO.

  Aidha, hakuna watakatifu wa kale kabla ya Musa waliotoa ZAKA kama sheria. Abraham na wengine wote walitoa kwa IMANI. Kitu unachokitoa kwa IMANI hakiwi tena sheria au amri ambayo usipoitii unalaaniwa au kuuawa.

  Pia kabla ya Musa waliotoa zaka wote walitoa mara moja tu kwa Imani kwa lengo la kutafuta uhusiano na Mungu kwa nyakati na sababu maalum. Wapo waliofanya hivyo kama kutimiza viapo au NADHIRI zao walizomwekea Mungu.

  Ukichunguza sana utagundua kwamba katika Agano Jipya tunakosea sana hasa tunapotaka watu wa Mungu watoe zaka kila mwezi au kila jumapili. Tunakosea sana kwa sababu nyakati za Agano la kale hakuna watu waliokuwa wakitoa ZAKA iliyokuwa katika mfumo wa pesa. HAKUNA. HAKUNA HAKUNA KABISA.

  Kutoa zaka kila mwezi tena kwa lazima na kwa shinikizo la uongozi wa kanisa siyo AGIZO LA AGANO JIPYA. Wanaodhani hivyo wanajirudisha kwenye AGANO LA KALE. Naam wataendelea kuishi chini ya laana itokanayo na kutaka kuishi chini ya sheria za Agano la Kale.

  Kwa kuwa Mtume Paulo, Petro, Yohana, Yakobo, nk hawakuwahi kuzungumza kuhusu utoaji wa ZAKA, yaani neno zaka halikutamkwa vinywani mwao pamoja na kufundisha saaaaana kuhusu utoaji , hata mimi nimeamua kuwa kama akina Paulo. Nimeamua kujitoa kwenye laana. Natafuta baraka za Mungu siyo kupitia ZAKA bali kupitia sadaka nyingine zilizotajwa na Mitume wa Yesu.

  Nimeamua kujitoa kabisaaaa. Namuiga Mt. Paulo na wenzake. Sitatoa wala kuwahamasisha watumishi wa Mungu kufuata kamtolea Mungu zaka kama kigezo cha kubarikiwa, bali nitaendelea kuwaeleza wenzangu kwamba TUNABARIKIWA KWA IMANI NA SIYO KWA MATENDO YA SHERIA.

 57. Stephen,

  Naona wewe ni mgeni kabisa katika hii shule. Kama ulikuwa hujui tulishaiongea sana na akina Edwin Seleli. Ni vema ukafuatilia hiyo mada maana utakuta mambo mengi sana.

  Lakini kwa uchache acha nikwambie.
  Ibrahim alitoa zaka mara ngapi, na kwa nini alitoa kwenye nyara siyo kwenye mali aliyokuwa nayo?

  Ni nani ambaye aliitegemeza huduma ya Yesu kwa kutoa zaka?
  Yesu isingewezekana apewe zaka,kama wewe unaielewa torati unatakiwa kujua kuwa mmbele ya wayahudi Yesu hakuwa na sifa ya kuchukua zaka.
  Yesu alitegemezwa na sadaka za watu waliokuwa wanamwamini na kumfuata. Siyo zaka.

  Wewe kama hutoi zaka kwa mujibu wa torati hauo mambo ya kujaza fomu na kadi ni ya nini wakati amri ya Yesu inasema sadaka haipadwi kupigiwa panda?

  Yesu wala mitume hawakuwahi kuliagiza kanisa litoe zaka, Yesu aliwaambia mafarisayo waendelee kutoa zaka, hakuliambia kanisa. Hakuna mahali katika agano jipya tumeagizwa kutoa zaka.

  Kazi ya Mungu haihitaji zaka ili isonge mbele,bali inahitaji fedha. Siyo lazima kutoa zaka ili kazi iende bali kinachotakiwa ni fedha ili kazi iende.

  Mwisho, niambie mtu mmoja ambaye aliwahi kutoa fedha kama zaka kwenye maandiko.

 58. Kama unayeuliuza swali umeokoka vizuri,ni vizuri ukawa na mahusiano mazuri na kanisa lako,muone kiongozi akueleweshe vizuri.Malipo ya kabla ina maana gani?(Labda ina maanisha malipo kabla ya matumizi?-naomba ufuatilie).

  Mimi kwa uzoefu wangu nilioupata mpaka sasa-watu wengi wasiomtolea Mungu zaka ndiyo waliowalalamishi,na wanaomtolea Mungu kwa uaminifu huwa hawalalamiki,Jifunze Kumtolea Mungu zaka kwa uaminifu.Kupitia zaka nimeona Mungu akinibariki,nimeponywa Magonjwa,Mungu amewainua ndugu zangu.Nimejifunza kuitii kwanza kabla ya maswali(1kor 8:2-Mtu akidhani anajua neno hajui bado kama impasavyo kujua).Mtu anaweza kukushinda kwa maswali ya zaka lakini hawezi kukushinda kwa ushuhuda wa yale Mungu atakayokutendea pale unapokuwa mwaminifu,Mjaribu Mungu katika hili(ameturuhusu tumjaribu-Malaki 3).

 59. kwako sungura na wengine mnaopenda kujifunza
  biblia ni neno la Mungu ambalo limehakikishwa likaonekana liko sahihi sasa ndugu yangu sungura ukiacha kuamini nakupa pole ebu sasa nije kwenye mada
  wengi kwa kutoelewa wadhani fungu la kumi au zaka ilianza kutolewa kipindi cha sheria yaani wakati wa musa ndio maana ndugu yangu sungura unasema ni kuhama na kongwa
  nipende kusema zaka au fungu la kumi limeanza kutolewa hata kabra ya kipindi cha sheria na mtu wa kwanza kutoa zaka ni baba yetu wa imani iibrahimu soma mwanzo 14:20 hapo biblia inasema ibrahimu baada ya kutoka vitani kumukomboa ndugu yake ruthu alitoa zaka au fungu la kumi kwa kuhani Melkizedeki tunapotoa zaka au fungu la kumi tunaonyesha heshima,utii wa neno la Mungu,pamoja na shukrani hapo unaona haikuwa kipindi cha sheria kwani hata musa alikuwa hajazaliwa
  mtu wa pili kutoa zaka alikuwa yakobo anasema mwanzo 28:22 yakobo anasema kama Mungu akimulinda na kumludisha kwa amani kwa kila pato atakuwa anatoa zaka au fungu la kumi
  leo tunashudia watoto wa Mungu wanaishi maisha ya shida maisha ya kupungukiwa kwa sababu ya kutembea kwenye laana
  ebu soma kitabu hiki kumbukumbu la tolati 28:1…10 itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana,Mungu wako,kwa bidii,kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo Bwana Mungu wako,atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani.na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana Mungu wako utabalikiwa mjini utabalikiwa na mashambani
  kipindi cha sheria kilikuwa kipandi cha tatu lakini bado tunaona umuhimu wa zaka bado unasisitizwa watu watoe soma hesabu 18:21 hapa tunaona Mungu asema zaka au fungu la kumi amewapa wana wa lawi hili ni kabira la kikuhani leo makuha ni wachungaji wanaotufundisha kweli ya Mungu lazima kutoa zaka kwa uaminifu tukitaka baraka za Mungu zisipungue maishani mwetu
  nije kwenye mada ambayo sungura kwamba zamani hazikutolewa fedha hapa kinachoongelewa sio fedha hapo ni kila pato sasa inategea ni pato fedha,kilimo,au ufugaji ebu soma hapa Mungu anavyosema mabo ya walawi 27:30 hapa Mungu anasema zaka ya nchi (yaani mazo ya mkulima)kama ni mbegu ya nchi,au kama ni matunda
  nne pia kipndi cha wafalume walipotawala vyema walisisitiza watu watoe zaka au fungu la kumi soma 2nyakati 24:9
  biblia inaposema leteni zaka nyumani mwa Bwana ili kiwepo chakula kazi ya Mungu haiwezi kufanikiwa kama hakuna fedha hata huduma ya yesu ilifanikiwa kwa sababu walikuwepo watoaji waliokuwa wakimuhudumia Yesu kwa mali zao soma luka 8:-3
  kwa leo nishie hapo kwa mchango wangu ni mimi mtumwa wa Bwana Yesu stephen ngullo

 60. Huu nao ni utapeli wa aina yake. Maana hapo kinacholengwa ni mshahara wa mtu.
  Nani kaagiza zama itolewe kila mwezi, achia mbali ukweli kwamba zaka ni kongwa ambalo limelazimishwa kuhama nalo toka agano la kale? Na wala zaka haijawahi kuwa pesa.

  Utashangaa mishahara ikianza kutolewa kwa wiki na form zitabadilishwa zisiwe za kila mwezi tena ila za kila wiki.

  Paul, Yesu mwenyewe hakuwahi kutoa zaka.
  Kama unatoa toa tu kama toleo la hiari ambalo umeamua kutoa,lakini si kwa kitisho kuwa usipotoa ati unamwibia Mungu,hiyo haipo ila no janja to za watu.

  Ubarikiwe.

 61. watu wengi sio waaminifu na wanashindwa kutoa zaka kwa kutafuta sababu mbalimbali za kupata visingizio ndugu yangu uliyeleta mada je? wewe ni mshilika wa hilo kanisa au umechukua fomu hiyo mahali kwani mimi kwa ufahamu wangu na jinsi nilivyo fanya uchunguzi moja ya makanisa yanayofundisha kweli ya Neno la Mungu kwa usahihi na hilo ni miongoni ambapo utata wako huo ungeishia huko sasa naomba nitoe majibu kwako na faida kwa wengine
  1.zaka inatolewa baada ya kupata mapato ya aina yoyote ile maadamu yawe ya halali soma mwanzo 28:22
  2.zaka ni sadaka inayotolewa ambayo ni moja ya kumi ya mapato ambayo Mungu anakuwa amekuwezesha kupata kwa mfano:-
  mfanyakazi mshahara wake anautolea moja ya kumikama mshahala ni tsh 1000,000/= fungu la kumi inakuwa tsh 100,000/=kwa mfugaji unafuga ng`mbe moja wanapozaliana na kufika kumi ng`ombe moja inakuwa zaka ya Bwana kadharika na kwa wakulima ukilima umepata gunia kumi moja inakuwa zaka ya Bwana soma mambo ya walawi 27:30 na baada ya mapato hutakiwi kuchelewesha au kutumia kama ukitumia uanapaswa kuikomboa kwa kulipa moja ya tano kuna maandiko mengi yanayoeleza umuhimu wa kutoa zaka soma pia malaki 3:7…12 ziko baraka nyingi za kutoa zaka ukisoma vizuri hapo na mambo ya Mungu yanaenda kwa imani pasipo imani haiwezakani kumpendeza Mungu pia Yesu alisema hatutakiwi kuacha kutoa zaka soma mathayo 23:23 akiwa na maana tuwe waadilifu na kupenda rehema na sio kuacha mengine wako wengine wanasema zaka ilikuwa kipindi cha agano la kale tu huo ni uongo wa shetani toa zaka uone baraka za Bwana juu ya maisha yako na familia yako. Mungu wa mbinguni awabaliki wote

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s