Kwanini Vifungo?

Shalom wapendwa! Napenda nichangie mada hii ambayo kwakweli inagusa maisha ya walokole wengi duniani. Napenda nitoe elimu japo kidogo juu ya swala hili la wokovu na vifungo ambatano. Ni kweli kabisa kuokoka si kipimo pekee kitakachokupa uhuru kwamba umeshinda mambo yote. Wokovu ni mchakato ambao unajumuisha mambo 3.
1. Roho
2.Nafsi na
3.Mwili.
Katika vitu hivyo vitatu ndivyo vinavyotoa tafsiri ya “mtu”. Mtu ni Roho inayoishi ndani ya nyumba nayo ni mwili. Asiri ya Roho ni mbinguni. Roho haiwezi kuishi na magonjwa ama laana kwakuwa asili yake ni mbinguni. Utaona katika maandiko matakatifu Mungu katika uumbaji anasema na tumfanye mtu kwa mfano wetu Mwanzo1:24″ Mungu akasema na tumfanye mtu kwa mfano wetu,kwa sura yetu;wakatawale samaki wa baharini,na ndege wa angani,na wanyama,na inchi yote pia,na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.”

Lakini mtu huyu mamlaka ya kutawala aliyapoteza baada ya kutenda dhambi,ndipo suala la laana lilifuata. Lakini baada ya uzao twaona laana,magonjwa na tabu mbalimbali zilianza kwakuwa nguvu ya utawala aliuchukua shetani. Twaona Ayubu namna alivyompenda Mungu na kumtumika kwa moyo wake wote,lakini Mungu alijivuna naye kwa CV nzuri aliyoijenga kwake ndipo Shetani akasemezana na Mungu juu ya Ayubu. Shetani alichojaribu kuweka hapa kwa Mungu ni namna pengine Ayubu japokuwa ameokoka huenda wewe Mungu anakupenda kwasababu umempa afya njema,ana watoto wengi,ana utajiri mwingi,mke mzuri na vitu vilivyo bora sana ndiyo maana anaona hajapungukiwa na kitu hana sababu ya kutokuabudu wewe Mungu. Shetani alimuomba Mungu amjaribu Ayubu kwa mambo ya Mwilini na katika nafsi yake je IKO SAWA SAWA japo Moyo wake unaonekana kumpenda sana MUNGU.

Kwakuwa Mungu hakuwa na wasiwasi kuhusu Ayubu,aliruhusu Ayubu ajaribiwe katika mambo 2 ambayo kimsingi ni yale ya mwilini na nafsi yake je ingesononeka na kuutiisha mwili? Mungu aliweka ulinzi juu ya Roho ya Ayubu. Na mapigo ya Ayubu yaliweza kumpata kwasababu ya ile dhambi ya asili ya Eden ambayo kwa uasi ule laana na mapigo ya kila aina yaliruhusiwa kukipatiliza kizazi hadi kizazi.

Kwakuwa ayubu alikuwa na utimilifu katika Roho,Nafsi na Mwili. Aliyashinda majaribu yote ikiwemo na lile la mkewe kumshawishi amwache Mungu. Ingekuwa leo tungesema ni mlokole kamili.

Nafsi ni daraja kati ya mwili na Roho,Nayo nafsi inafanya kazi ya kuchuja mambo ya Rohoni na mwilini na matendo ya kufikiri na kuamua. Roho yaweza kukombolewa lakini vifungo vikabaki katika Nafsi. Utasoma katika Biblia YESU alipotoa mfano wa Tajiri. Ilionekana Tajiri kuingia mbinguni ni vigumu sana kuliko ngamia kupenya katika tundu la sindano. Ushuhuda huu unatoa taarifa kwamba Tajiri yule Roho yake ilikuwa tayari imezikubali kazi za YESU na imekili na kumwamini YESU,lakini YESU aliiona nafsi ya tajiri huyu bado haijaokolewa;ilihitaji ukombozi. Na tunaona kwamba Bwana YESU alitoa muda kwa Tajiri huyu arudi atoe sehemu ya utajiri wake wote ndipo amfuate YESU. Yesu hapa alikuwa anampa Muda Tajiri ili nafsi yake na MAMBO YA MWILINI navyo vikombolewe lakini tajiri yule jambo hili hakulikubali,ndipo Yesu akahitimisha juu ya ugumu wa Tajiri kuiona mbingu. Twajifunza wokovu kamili una mambo makuu 3.

ii watu wote wanampenda Mungu,lakini Mungu anapenda watu wote waokolewe. lakini sii watu wote amewapa fulsa ya kuwahudumia. Wenye haki hapa ni waliookoka tu. Twasoma katika maandiko matakatifu:

Yohana 1:12-13” Bali wote waliompokea ,aliwapa uwezo kufanyika watoto wa Mungu,ndio wale waliaminio jina lake;waliozaliwa si kwa damu,wala si kwa mapenzi ya mwili,wala si kwa mapenzi ya mtu,bali kwa Mungu”.

Mungu ameweka ulinzi tu! kwa watu ambao wameokoka wameziacha njia mbovu, kwa maana wamefanyika kuwa wana wa Mungu; na wana beba tabia za Mungu na ndio wenye haki zote, na upendeleo wa kuomba kitu chochote watakacho kwa JINA LA YESU KRISTO, na BWANA akafanya. Kwa maana BWANA Mungu si mwanadamu aseme uongo.

Zaburi 33:7
” Malaika wa BWANA hufanya kituo, akiwazungukia wamchao nakuwaokoa”.

Zuburi125:2-3
”Kama milima inavyouzunguka Yerusalem, Ndivyo BWANA anavyowazunguka watu wake, Tangu sasa na hata milele. Kwa maana fimbo ya udharimu haitakaa juu ya fungu la wenye haki; Wenye haki wasije wakainyosha mikono yao kwenye upotovu”.

 Mungu hasikii maombi ya mtu mwenye dhambi kwa maana imeandikwa:

Isaya 59:2
”Lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu,na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone,hata hataki kusikia”.

Yohana 8:44
” Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuwaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli,kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwasababu yeye ni mwongo na baba wa huo”.

Katika maandiko haya;tunajifunza kwamba KUOKOKA kumekupa tofauti kati yako wewe uliyeokoka na mtu ambaye hajaokoka,lakini kuhusu suala la usawa hapa ni kwenye maombi. WOTE waliokoka na wasio Okoka wanamwomba Mungu. Lakini Mungu anajibu tu maombi ya watu waliookoka. Jambo hili linatupa picha yakwamba Majaribu kwa mtu aliyeokoka yamewekwa katika makundi 3,yapo ya Rohoni,kwenye NAFSI na Mwili. Kwamaana Andiko lile ambalo Mungu anasema Ombeni Lolote nanyi mtapewa. Andiko hili wameandikiwa walokole tu na sii watu wenye Dhambi ,kwamaana maombi ya mwenye dhambi ni sawa na mAKELE AU KUPAYUKAPAYUKA machoni pa Mungu. Mungu anajua kabisa pamoja na wewe mlokole unasema kwamba umeokoka!!! Bado kuna vifungo utakuwa navyo. Kinachookolewa hapa kwanza ni ROHO…then Nafsi na mwili navyo vyafuata. Na ndio maana unaweza kuona Mtu Roho yake imeokolewa lakini yapo matendo ya mwilini na nafsi vikawa bado havijapata muujiza bado viko katika madhabahu za Ibilisi. But it is a process.

Mungu angeruhusu wokovu mtu akiokoka tu basi kila kitu kinakwisha pale pale,jambo hili watu wengi duniani na matatizo waliyonayo wangemkimbilia Mungu. Ipo sababu kwubwa kwanini Unaokoka na bado ukaona bado unafungwa. Na suala hapa ni kwamba WOKOVU ni Process ya vitu 3,vyote vyapaswa kuokolewa. Kwa jambo hili,Roho itakombolewa kwa mambo ya Rohoni(Neno la Mungu),nao Mwili utakombolewa kwa matendo ya Mwilini yakitiishwa kwa kuyakana. Vitu hivi 2,kati ya Roho na mwili vikikombolewa ndipo nafsi kwakuwa ni chujio la mambo ya Rohoni na Mwilini ndipo inapata afya na ukombozi na utamwona mtu huyu anakuwa ni kiumbe kamili” MLOKOLE KAMILI”.

Na ukamilifu huu wa vitu 3 ndiyo unavyompa mtu nguvu kubwa sana ya Mungu kushinda mambo yote ya Rohoni ,mwilini na katika Nafsi. Mambo haya 3 yakikamilika kwako ndipo andiko lile la Mungu kupendezwa na watakatifu waliopo duniani linatimia kwako,Pamoja na lile andiko WENYE NGUVU NDIO WATAKAOTEKA NGUVU ZA MUNGU. Bila kuwa na ukamilifu katika ROHO,NAFSI NA MWILI hakika hutoiona mbingu wala kuziteka nguvu za Mungu kwamaana utawezaje kuziteka nguvu hizi ingali u mateka wa vitu vya Mwilini umesongwa na Magonjwa,laaana na balaa zinakukabili?Ukiwa navyo hivyo vitakupa nafasi ya kusononeka,kukata tamaa,huzuni,majeraha,uchungu n.k. Utakatifu yaani ulokole kamili uko katika mambo haya 3 tu. Na Mungu hajatuacha Nyuma ametupa kanuni za kuufikia utakatifu huu ni kwa njia kuu kama 4 nazo yatupasa sasa tuzitafute kwa jasho letu wenyewe,lakini Mungu ameachilia REHEMA YA WOKOVU BUREEE:
1. Kuacha dhambi: ( Tii amri kuu 10 zote za Mungu)
2.Soma sana NENO la Mungu 😦 KUIMARISHA AFYA YA ROHO,Maarifa ya mambo ya Rohoni)
3.Kufunga 😦 Kuutiisha mwili usiingie katika majaribu) ISAYA:58:6
4. Maombi 😦 Kufungua kamba za umauti,Magonjwa,umasikini,vifungo vya Rohoni,Nira na Uhuru wa Nafsi)

Nitarudi tena wapendwa hopeful MMEPATA kitu hapa,na natarajia kupata Mada nyingine tena ama muendelezo wa michango yenu. BWANA awabariki na kuwalinda katika jina la YESU!!!!

OSCAR A.CHARLES

Advertisements

7 thoughts on “Kwanini Vifungo?

 1. Jamani hii mambo kwa mimi inanichanganya sana.
  Ni mara nyingi kila nianapoamua kumfuata Yesu shida majaribu maumivu mabalaa…yaani sijui ndo malaana yote yanaamka kwa wakati mmoja.
  sasa sijui ndo nafsi na mwili bado viko kwa ibilisi au inakuwaje.

 2. Mi naamini kuwa ukiokoka majaribu yapo na changamoto tena zaidi ya zile ulizokua nazo hapo mwanzo sasa mi huwa nachanganyikiwa haswa kwa swala la mafundisho ya laana kujumlisha maswala ya muunganiko na ukoo wako sasa ni laana laaana laana tupu kila jaribu imekua laana kila changamoto imekua laana za ukoo mababu nk
  mi mafundisho ya dizaini hii yananichanganya kias kwamba naanza kuona kama vile Yesu alifanya kazi bure,

 3. Mimi najua Yesu Kristo alisema kama tukiokoka na tukadumu kwake alisema njia hiyo ni nyembamba (Matayo 7:13) na akasema kama tutamfuata basi imetupasa kuingia mbinguni kwa njia ya dhiki nyingi(Matendo 14:22). Hizo ziki zaweza kuwa magonjwa, umasikini , kuchukiwa na waipendao dunia na mambo yoyote Shetani anayoweza kuyatupa katika maisha yetu. Ila Mungu ni mwaminifu aliyetuahidi hataruhusu dhiki au majaribu kuvuka kiwango cha imani yetu. Ndugu yangu kama uliwahi kuokoka na ukauonja uzuri wa kumjua Yesu, usikate tamaa hata kama unapatwa na mabalaa yanayofululiza kama yaliyomtokea Ayubu hata kama yamekaa muda mrefu maishani mwako! Jipe moyo, siku moja utamuona Mungu na kufutwa machozi yako. Hivi mnajua Yusufu alisingiziwa kuzini na mke wa Potifa na alifungwa miaka 13? Hivi walokole wa leo wakifungwa miaka 13 si wengi wao watakata tamaa na kuona wapo kwenye vifungo vya laana na kuanza kuvunja laana? MUNGU ANATAKA TUMPENDE KWA MIOYO YETU YOTE HATA KAMA KWA NJE TUNAONEKANA WATU WA HOVYO NA MAFUKARA!(Soma 1Korintho 4:9-13). HEMBU ANGALIA MAISHA YA PAULO, HIVI walokole wengi leo wangepitishwa kama Paulo si wangesema wana laana za mababu ndio maana dhiki na taabu zinawafuata?
  ONYO: JAMANI TUSIPENDE KUWATEGEMEA SANA WATU WENGINE WATUFUNDISHE NENO LA MUNGU . TENGA MUDA KILA SIKU UWE UNASOMA NENO MWENYEWE. SOMA INJILI ZA YESU. SOMA NYARAKA ZA PAULO. SOMA ZABURI. SOMA VITABU VYOTE VYA BIBLIA. KISHA JIFUNZE KUMTAFUTA MUNGU MWENYEWE KWA MAOMBI KILA SIKU. Ukitegemea ati kila kitu kinachofundishwa makanisani au kwenye internet au TV kwamba ni sahihi nakuambia siku moja ukakwenda na maji maana walimu na mitume na manabii wa uongo ni wengi leo hii na wataendelea kuwa wengi siku zijazo kadri Kuja kwa YESU KUNAVYOKARIBIA.

  TUKIISHA OKOKA HAKUNA CHA KUTUTENGA NA KRISTO: Warumi 8:35-39
  35 Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?
  36 Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa.
  37 Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.
  38 Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo,
  39 wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.

 4. Mtumishi wa Mungu Oscar, kwanza nakushukuru kwa kunifundisha jambo kweli nimepataa kitu, ila nina swali kama ulivyosema kuwa, ”Bila kuwa na ukamilifu katika ROHO,NAFSI NA MWILI hakika hutoiona mbingu wala kuziteka nguvu za Mungu kwa maana utawezaje kuziteka nguvu hizi ingali u mateka wa vitu vya Mwilini umesongwa na Magonjwa,laaana na balaa zinakukabili?”

  Kwanza hebu niweke sawa kwa neno hilo ya kuwa ufalme wa Mungu unatekwa na wenye nguvu, sasa ina maana kama Ukimkiri Yesu kwa kinywa na kuamini kuwa alikufa na kufufuka utaokoka, je hii inakuwaje hapo? na je watu wote wanakufa kwa magonjwa mbinguni hawaendi??

  Asante naomba msaada

 5. ndugu Oscar A. Charles nashukuru sana kwa somo lako japo nimi pia kuna jambo ambalo natakakujifunza hapa ”……Mtu Roho yake imeokolewa lakini yapo matendo ya mwilini na nafsi vikawa bado havijapata muujiza bado viko katika madhabahu za Ibilisi.” ninavyofaha mimi na kwamba roho ya mwanadamu inapookolewa inapewa uwezo na mamlaka ya kuutisha mwili. hivyo pale mtu anapookoka anpewa ulinzi na Roho wa Mungu na kumfundisha namna anavyopaswa kuenenda jambo kubwa hapa ni utii. haiwezekani Roho ya mwanadamu iwe imeokolewa wakati huo nafsi na mwili wako uko madhabahuni mwa ibilisi sababu hata miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu, Roho ya Mungu inakaa ndani yetu na Zetu zinakaa ndani ya Roho wa Mungu hivyo kunakuwa na ulinzi kamili hadi kwenye nafsi na mwili pia. Roho zetu zingali na mawasiliano na Mungu hata na miili yetu inakuwa hai labda Mungu aweameruhusu vinginevyo juu ya miili yetu.
  Asante na Mungu Akubariki sana.
  Julius

 6. amina Mungu akubariki sana kwa ujumbe muzuri sana. Bwana akutie nguvu katika kipindi chamitihani hiki

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s