Kutoka Dodoma na Mchungaji Peter Msigwa…

msigwa

“Samwel Sitta HUNA uelewa wala mamalaka ya kulikosoa kanisa. Mmezoe kuweka Viongozi wa DINI mifukoni safari hii ndio mnaona Upinzani na uelewa wa kweli . Kwa Bahati mbaya hamkujiaanda hamjui namna ya kukabiliana ,na Upinzani wa kweli . Viongozi wa DINI wanayo haki ya kukemea , kufundisha kuonya ,kuelekeza na kuombea, Mungu hasemi tuitii mamalaka za kihuni ,kifisadi, WEZI , WAONGO, mbinu hizo zilitumiwa na wakoloni, MAKABURU , walitumia bibilia ili wabaki madarakani ili Hali wanakiuka haki za binadamu. Utumwa ili kuwa ni HALALI kisheria,
Yeyote aliyekataa kuuzwa alivunja Sheria, Ubaguzi wa rangi ilikuwa ni sheria . Ukiingia choo cha mzungu ungeshitakiwa,
Mandela alipobisha aliambiwa atii mamalaka, ,hapa KWEtu kuna sheria za kipuuzi na kuna Viongozi wapuuzi Kama wakina Sitta hawapaswi kuheshimiwa hata kidogo, Sitta kamwe huwezi kulisemea kanisa,WHAT WE SEE IN DODOMA IS IGNORANCE IN ACTION …. remember ignorance is very dangerous when is active”

–Mchungaji Peter Msigwa

Advertisements

12 thoughts on “Kutoka Dodoma na Mchungaji Peter Msigwa…

 1. Hahaa, Mabinza,

  Hayo ni maneno ya mtu anayeshindwa kulumbana kwa hoja.

  Naona unajaribu kunikimbia kisanii, nami nakutakia mkimbio mwema. Angalia tu usijigonge kwenye kisiki ktk kukimbia kwako,maana asiye jasiri hutimua mbio hata bila kufuatiwa na kitu nyuma!

  Vipi lakini, ulienda kwenye sherehe za makabidhiano ya katiba pendekezwa?

  You are simply a coward?

 2. Sungura,

  katika hili wala sitazami tena comments zako kwa makini, natazama za Mh. Ck Lwembe. weee huna mpya, ni katoto kanakochezea mchanga. Siasa na maana zake hujui, kwako ni fumbo kaka. Acha sisi tunaojua kama akina Lwembe Ck tupete!

  “Ufaham ni chmbe ya Uhai!”

 3. Mabinza,

  Wewe kwa muono wako unadhani sijui suala la uwepo wa Yesu kabla ya misingi ya dunia ninapoongelea umri wake fulani katika mwili?

  Kuba vitu vingine kulingana na miaka ambayo tunekuwa hapa SG, inabidi tufahamiane kwamba fulani anaweza akawa hajui hili, lakini hili na lile kulingana na ufahamu wake si rahisi akawa hajui.

  Katika hiyo hoja umepoteza muda wa bure kusema yote uliyosema.
  Kawaulize mafarisayo kama walikuwa wanajua Yesu katokea wapi na ni nani.
  Paul mwenyewe alikuwa hajui mpaka alipotokewa na yaliyomtokea.

  Leo angalao tunajua yote kwa sababu ya Roho mtakatifu. Kama ungekuwa mwaba wa farisayo lazima usingejua hayo mambo kwa hiyo ungeona Yesu ni kijana wa miaka 30.

  Lakini pia elewa alipovaa nwili hakuwahi kuishi maisha yake ya uungu.

  Ok, Msigwa hakuwa anawasemea maaskofu, alikuwa anasema yeye kama yeye kwa nafazi aliyonayo.

  Ndio maana nazidi kukutaka useme upuuzi au ukutokuwa na adabu wa Msigwa kwa Sitta. Nataka nijue kama alimtukana au alimtusi.

  Hilo ndo la msingi kujadili hapa. Lakini ukikwepa na kutaka tujadili suala la mtu kuwa kwenye siasa na kwenye madhabahu, hilo sioni kama kichwa chako kinaweza kikawa kinaling’amua vema. Naona kama uko shallow sana ktk kulifahamu hilo.

  Kama unatambua kuwa ukuhani ulikuwa kwa Lawi, akina Yuda waliachwa watumike katika mambo mengine ikiwemo siasa.
  Jiulize sasa imekuwaje leo ukuhani umehamishiwa kwa Yuda, na ukuhani (madhabahu)wenyewe umechanganywa na mambo ya kifalme(siasa)

  Mungu ameamua kuwapa wana wa Yuda ukuhani bila kuwaambia wasitumikie mambo ya kifame, yaani bila sharti la kutumikia ukugani pekee kama ilivyokuwa kwa Lawi.

  Ndio maana hili linaitwa agano jipya!!

  Halafu nakushangaeni kweli, katika suala la kutii mnasema mamlaka ya kisiasa imewekwa na Mungu, lakini ktika kutumika mnaiona ati ni mamlaka ya kidunia tu isiyokuwa na Mungu ndani yake.
  Huo ndio ninaouita ufaham mdogo sana wa kuyaona mambo.

  Ndio ninyi wajinga wanaozuia wacha Mungu/ wana wa Mungu kuingia kwenye siasa, lakini wakiingia watu waovu madarakani mnaanza kufunga na kuomba, kuwaombea ati wamjue Mungu na kumcha.

  Ivi Mungu ingetokea amesikia maombi yenu kuyakubali, akawapa neema wakampokea, ivi mlivyowajinfa si mgeanza tena kuwaambia hao viongozi watoke kwenye siasa maana huko ni kuitumikia duniani?

  Ndio maana Mungu huwa hasikii maombi yenu ya kijinga hayo. Jitieni maarifa ya kweli yake ili mpate kuyaona mambo katika taswira sahihi.

  Jifunzeni kwa Daniel yamkini unafiki na ijonga wenu ukawatoka.

  Sidhani kama Mabinza kwa hiyo blanketi-giza ulilovalisha ufahamu wako, unaweza kuchukua hata dakika tano kuwaombea wenye kumjua Mungu walio katika siasa kama akina Msigwa Mungu awape neema wafanye utumishi mwema huko.

  Iko tayari kumlaani Msigwa na kuwabariki walioko huko wanaolitukana kanisa.

  Jitie maarifa!

 4. “Mch.” Msigwa,

  Kimsingi, ingawa kuna kundi la watu wanaokusifia ktk hayo unayoyafanya, mimi napenda kukupongeza ktk mema yote, na ninakusikitikia ktk visasi vya kauli, kama hii lugha ninayoisoma hapa.

  Ninakuona ni mtu uliyejichanganya, na unaendelea kuwachanganya wajinga wanaokuona kwamba wewe eti ni mchungaji!! Siasa ndg yangu siyo lele mama, inaweza ikakufikisha mahali pa ujinga bila ufahamu, na ukaendelea kujipoteza ktk political maze, ukaishia kuwa kibaraka wa wanasiasa kama ninavyokuona, bila kujua umefikaje kuwa hivyo!

  Hebu liwazie jambo hili: Kwamba unasema, “”Mmezoe kuweka Viongozi wa DINI mifukoni””; halafu ktk hiyo picha hapo juu, “mchungaji” uko juu ya jukwaa la wanasiasa, ukiwasimanga viongozi wa Dini kwamba wamewekwa mifukoni; Lakini wewe by all standards ndiye uliyewekwa mifukoni mwa wanasiasa kama ulivyo hapo, nawe HUJUI; kwamba ktk huo “mkutano mkubwa wa Injili”ninaokuona hapo ukihubiri, ni watu wangapi wameokoka?!!!

  Ufisadi ni roho inayoifunika dunia yote, na hiyo ndiyo iliyokutoa kanisani na kukuingiza huko kuwatumikia wanasiasa kwa “heshima” ya kanisa, wakikutumia bila wewe kujua!!!

  Hao akina Sitta ni “manyota” wa siasa, yaani “makamanda”; hao ni men of valour, basi nyie ma amateur mnapojitutumua bila uzoefu ndio mnaishia kuunda vitu visivyo na maana kama UKAWA, ambao kwa maneno yako, ndio hii hali “”WHAT WE SEE IN DODOMA IS IGNORANCE IN ACTION”” mlipo uunda huo UKAWA huko Dodoma, it was ” IGNORANCE IN ACTION” per se; which “is very dangerous when is active”!!! Kwa ile ignorance mliyonayo, ndio inawaongoza kuwa incite watu waandamane ili kuficha your failures, caused by the very ignorance!!

  Tazama, CCM hawakutaka kabisa Katiba mpya, wao walitaka hiyo ya zamani iendelee, palipo na mapungufu iwekewe viraka. Upinzani ndio waliotaka Katiba Mpya, na wamekuwa mstari wa mbele kuidai hiyo. Kelele zilipozidi, wakawatazameni, ktk jicho la “Vita ya Katiba”, and they perceived that you are ignorant, amateurs ktk vita!

  Wakatengeneza Tume, wakaipa maelekezo, zile rejea, wakaituma kwenda kwa wananchi, ikarudi na maoni ya wananchi, IKATENGENEZA na muundo wa Serikali Tatu ambao haikutumwa. Wenye Tume wakaipitia ripoti kisha wakawakusanya wote na kuwarundika Dodoma muipitie rasimu hiyo na kuijadili. Na ninyi akina Msigwa mkakusanywa huko kwa ajili ya jambo hilo, out of ignorance, be it political or intellectual, mkaitikia mkusanyo huo!

  Sasa, mimi nilikutegemea mchungaji, kwa kipawa cha RM ulicho nacho, ungeuona mtego mliotegewa, ndipo mngegoma kwenda Dodoma mpaka muipitie hiyo rasimu pamoja na maelekezo waliyopewa, muitazame kama chama, halafu mtoe maoni yenu kama mnayo. Mmekurupuka kwenda huko kulipigania pando la Serikali Tatu lililochomekwa humo kimahili ili kuyavuruga majadiliano!

  Mmeletewa Muundo wa Serikali Tatu, kwanini hamkudai na Muundo wa Serikali ya Mkataba na wa Serikali moja na wa Serikali mbili ulioboreshwa? Kwanini Tatu na si Moja??? Walikuwa na muda wa kutengeneza Serikali Tatu tu, kwanini? Mtajadilije Katiba Mpya ya Muungano bila kuliweka sawa jambo la Muungano kwanza, ambavyo ndiyo ingewaongoza ktk hayo mengine? Mmepokea mlicholetewa kama watoto wadogo, mkaongozwa mkondo wa kufuata, ilipofika wakati wa kuwafyatua, mkafyatuliwa! Mmekimbia uwanja wa vita, mnakwenda kujificha kwa raia, kama wapiganaji wa kiPalestina!

  Halafu, niliwategemea kuwa mtakuwa revolutionary ktk mambo mengi, lakini naona mmekwama ktk mambo ya “wapigania uhuru” wakati wa amani! Mmekuwa wepesi kuitisha maandamano yasiyo na tija, kwa sehemu kubwa huishia kuwatia hasara hao wanaowasikiliza hapo wanapopambana na askari. Lakini mngeweza kuwakusanya watu hao hao, badala ya kutembea wakipiga makelele wanayoyasikiliza wao wenyewe, angalau mngeziongoza nguvu hizo ktk kusafisha mitaa, au kusaidia huduma za jamii, huku mmeyasimamisha mabango yenu, watu wangewakumbuka kwa hayo mema, kuliko hizo nguvu, wasted ktk makelele na kuwakimbia polisi!

  Tengenezeni suala la Muungano kwanza, acheni cowardice! Mtu wa miaka 50 si mtoto mdogo. Muungano una miaka hamsini, walichokifanya Nyerere na Karume hakiwezi kudharauliwa leo hii nje ya utovu wa adabu! Hao walikuwa majasiri kuliko ninyi ambao mnaogopa hata kuujadili Muungano, mnachagua kujidanganya badala yake; sijui serikali mbili wengine tatu, wengine mkataba, na upuuzi mwingine, vyote vina chimbuko la woga; kaeni chini muitazama hali ya nchi ikoje na usalama wake; waangalieni wananchi na si tamaa zenu za vyeo na umaarufu at the expense ya hao mnaowaongoza kama ambavyo mchungaji kawaacha kondoo, yuko hukoo anazunguka na ngoma ya katiba, wamemvua kola nyeupe wamemvisha combat!!!

 5. Sungura,
  Ha ha ha ha haaa, hillu mayu!
  TAtizo langu siyo msigwa, tatizo langu ni tuhuma kwa Sitta, kama Sitaa. Bunge siyo Mzee Sitta, kumsakama ni utovu tu wa nidhamu. Kama Maasikofu walifanyiwa kitu mbaya na Mzee Sitta, kwa hiyo walimtuma Msigwa awasemee? Unanishangaza unavyo jaribu kupote kwa kumtaja Yesu eti alikuwa kijana Mdogo wa mika hiyo uliyoitaja, Yule alikuwepo tangu mwanzo, kabla ya kuwepo misingi ya Dunia yeye alikuwepo, Biblia inamtaja ni Mzee wa siku! Zaidi sana wote unaowaita mafarisayo ama Wafalme, wote walifanyika tokana na huyo, kwa hiyo kama Muumba alikuwa katika nafasi yake na kusema lolote, kama mwenye mamlaka kwa viumbe vyake! Kinachokusumbua, unautazama ule Mwili aliouzaa Mama Maria, ambao ulikua na kuongezeka; Masikini Sungura, unaropoka tu bila hata kujua hata kidogo kazi ya mwili ule, aliokuwa akitembea nao Kristo Yesu!!

  Sikatai kuwa Msigwa ni kiongozi wa kiroho na Kisiasa, watu wa ndini ndivyo walivyo, huwa wanadini na siasa kwa pamoja, kwa mawazo yako Mungu hakujua hilo, kwa hiyo kwa makosa akamchagua Lawi kuwa kuhani wa Israeli, na kwa mawzo yako hayohayo, hujiulizi kama Kuhani aweza kuwa ni Mfalme. Sungura, Roho ya unabii yaweza kumpata hata Mfalme, lakini hawezi kudumu kuwa Nabii wa Taifa na hapo hapo akaendelea kuwa Mfalme wa Taifa! Roho ndiye huteua viongozi, hawezi kupingana na hawezi kupendelea. Msigwa anapaswa kuchagua kimoja tu, kuwa katika mambo ya Kiroho ama abaki katika mambo ya Serikali za kidunia zenye kutoza kodi, ili ziendeleze mamlaka yake! Labda nisiende mbali sana, sasa Msigwa anachomsakamia Sitta, kinamanufaa gani kwa Taifa achilia mbali maasikofu? Kwa hiyo Msigwa ni yesu wa siasa kutokuwa na Adabu kwa wazee? Hapa najua tunajifurahisha tu, hakuna cha maana. Ila ili nicheke lazima siku zingine tuongelee upuuzi kama huu wa akina Msigwa na Sungura rafiki yake.

  “Ufahamu ni chembe ya Uhai!”

 6. Mabinza,

  Umeniuliza kama ninaweza nikamsikiliza Msigwa!
  Siyo tu naweza, huwa namsikiliza, na mtu yeyote mwenye akili pevu anaweza akamsikiliza.

  Ndiye aliyefichua biashara haram ya meno ya tembo na jinsi tembo wetu walivyokuwa wanauawa na mambo mengi yanayohusu maliasili yetu.

  Kwa kuwa tunatakiwa kuheshimu kila mamlaka kwa maana hiyo, iheshimu pia mamlaka ya shetani maana nayo ni mamlaka.

  Msemaji wa kanisa siyo maaskofu, wao ni wasemaji wa umoja wao wa maaskofu. Msemaji wa kanisa ni mtu yeyote aliyesehemu ya kanisa na ambaye position yake inamruhusu kusema, kama alicyodanta Msigwa.

  Alikuwa anamjibu mwanasiasa mwenzake aliyejaribu kulisema kanisa kutoka katika kona ya siasa.

  Linapokuja suala la mamlaka heshima haiangaliwi kwa umri, hata ukiwa mzee kiasi gani ukienda isivyokupasa unakemewa tu hata na mtoto mdogo .

  Tena ninavyokuoana, shida yako na Msigwa shaiko ktk alichokisema, bali iko kwenye yeye ni nani.
  Bado ujinga umekaa kwa kichwa chako, akili yako ikijaribu kukwambia kuwa mchungaji hawezi kywa mwanasiasa. Yaleyale ya usichanganye siasa na dini.
  Hicho kizaji jinga kimeisha, kama bado kuna watu wa namna hiyo wanajitokeza, basi ndio masalia wa hicho kizazi ambao wanamalizikia malizikia.

  Imani(belief) ni maisha ya kila siku, na siasa nayo ni maisha ya kila siku ambayo lazima uyaishi, utake usitake lazima unayaishi.

  Sijui kama unajua alichokisema mzee Sitta baada ya jitihada za kuwashawishi maaskofu waunge mkono rasimu ya katiba pendekezwa iliyochomolewa vifungu vingi vya maoni ya wananchi kukwama.

  Inawezekana wewe umeibukia tu kwenye kitu alichosema Msigwa kwa Sitta. Na kwa vile watu kama wewe mnapenda kulipuka bila kukusany taarifa za kutosha, uliamua kufungya kinywa kuongea pumba.

  Namna hiyo, mimi nikikuona kama hivi lazima nikupe vipande vyako hata kama utalalamoka kuwA natumia naneno mskali, labda itasaidia kupunguza akiba ya ujinga iliyohifadhiwa kichwani mwako.

  After all, maneno yangu hayajakatibia kabisa ukali wa maneno ya Yesu, kwa hiyo nitajitahidi kuyaongeza ukali ili angalao yakaribie.

  Nilikutaka usema upuuzi ulio katika maneno ya Msigwa ni upi, usimshambulie Msigwa kwa position yake. Wewe kuelewa uhalali wa position yake ni mpaka ukubali kuondoa
  fungus of ignorance katika fikra za kwako.

  Huelewi Mabinza hata maana ya hekima. Hekima si kukosoa kwa busara na upole. Ni wapi Yesu aliwahi kukosoa kwa upole?

  Ungejisikiaje kama mzee wako angejuwa farisayo, halafu anakuja kijana wa miaka 31 anamwambia ‘ ninyi ni wa baba yenu ibilisi’? Au angemwita kaburi lililopakwa chokaa kwa nje, lakini ndani ni mifupa mitupu. Si ungeenda polisi ukilalama kuwa mzee wangu ametukanwa!!

  Kama babayo angekuwa mfalme halafu kijana wa miaka 30 anamwita mbweha, si ungefungua kesi?

  Tunataka watu jasiri kama Msigwa, wenye kutumia nafasi zao kusema ukweli, na kumkemea yeyote anayeleta unafiki katika mstakabali wa taifa letu!

  May Msigwa be blessed!!!

 7. KIONGOZI BORA NI YUPI?

  Mchungaji Msigwa ni kiongozi wa kiroho na siyo kiongozi wa kidunia.Kutokana
  na Neno la Mungu,kiongozi bora ni yule anayeongozwa na Roho Mtakatifu(Warumi 8:14).Kwa mantiki ya sentensi hii kila mteule anayeongozwa na Roho Mtakatifu(mwana wa Mungu) ni kiongozi kwa jinsi ya rohoni na anatakiwa kuusimamia huo uongozi kwa jinsi ya mwilini mahali ambapo Mungu amemuweka.Unasema Kamugisha unamaanisha nini,naomba tumsikilize Roho Mtakatifu ambaye ndiye mwalimu hapa.Aliyekuwa Mfalme wa Babeli enzi hizo alikuwa ni Danieli na wenzake na siyo Nebukadreza!!Danieli na wenzake ndiyo walikuwa viongozi halisi waliowekwa juu ya Babeli ili kusimamisha kusudi la Mungu wakati aliyekuwa anaitwa Mfalme Nebukadreza alikuwa ni kiongozi wa kidunia aliyekuwa anaiongoza Babeli kwa kutumia wachawi pamoja na jeuri ya hekima yake mwenyewe,jambo ambalo lilimtokea puani(Danieli 4:1-37).Danieli na wenzake walikikomesha kiburi cha kiongozi kivuli wa Babeli kwa kumgeuza kuwa mwendawazimu kwa muda wa nyakati saba!Na mwisho wa adhabu akaongozwa sala ya toba na kumtukuza Mungu wa kina Danieli.Mambo haya yalifanyika kwa NJIA YA MAOMBI,wala si kwa msukumo wa mambo ya mwilini.

  Kilichomfanya Danieli kuwa kiongozi bora na halisi ni UNYENYEKEVU NA HEKIMA YA ROHO MTAKATIFU iliyo kuwa ndani yake(Danieli 2:30,Danieli 6:3).Kiongozi bora ni yule ambaye unyenyekevu wa Yesu unaishi ndani yake na yeye ndani ya unyenyekevu wa Yesu(Wafilipi 2:3-4).Ni mtu ambaye anaongoza kwa kutumia Maarifa,hekima na busara ya Roho Mtakatifu(1 Yohana 2:27).Mtume Paulo ambaye alikuwa na huduma zote tano ndani yake alimpa mwanae Timotheo ushauri wa kiroho kwamba AFANYE BIDII KATIKA KUSOMA,KUONYA NA KUFUNDISHA(1 Tim 4:13) na pia AWAKEMEE WANAODUMU KATIKA KUTENDA DHAMBI TENA MBELE YA WATU WOTE ILI WENGINE WAOGOPE (1 Tim 5:20).Haya yalikuwa ni maagizo ambayo kiongozi kijana Timotheo alipewa kwa ajili ya waamini au wateule.

  Mungu anapokupa maagizo au ujumbe kwa ajili ya mtu au watu ndani yake pia kuna
  kuwa na hekima au utiisho wake.Ni lazima tuliangalie hili jambo kwa jinsi ya rohoni kwasababu sisi ni watu wa rohoni.Kuna changamoto nzito kuwa kiongozi wa kiroho ndani ya siasa za duniani!Ni kweli kwamba si kila onyo la Mungu lazima lipokelewe vizuri lakini kwa kuwa limebeba mamlaka huwa linadhibitika.Mungu anaweza kumuomya mtu yeyote na kwa njia yoyote kupitia watumishi wake.Na kama mtumishi ameamua kuonya kwa msukumo wa siasa na siyo wa rohoni pia jambo hili hudhibitika kwa watu wa rohoni.Watu wakawaida wanaweza wasijue wakabaki tu kushabikia au kuponda.Takwimu za kiroho zinaonyesha watumishi ambao wameingia katika siasa
  wengi wanatamani kumalizia MWILINI LICHA YA KWAMBA WALIANZIA ROHONI(Wagalatia 3:3).Na hii ni kwasababu hawajitegemezi kiroho na pia hawana watu wa kuwategemeza kiroho katika maombi.Wamezungukwa na wapambe kama wale walio mshauri Mfalme Sauli apeleke sadaka ya vitu ambayo Mungu alimwambia haviharibu visionekane kabisa(1 SAMWELI 15:2,3,10,14-26).Mfalme Sauli alifukuzwa kazi ya utumishi kwasababu ya kosa la kuwasikiliza wapambe.SWALI LA MSINGI NI KWAMBA ,NI ROHO IPI ILIYO MUONGOZA MCHUNGAJI MSIGWA KUSEMA ALIYOYASEMA??

  NENO LA KRISTO HALITIKISWI KAMWE NA MUNGU WANGU NI MOTO ULAO(WAEBRANIA 12:28-29).NEEMA YA BWANA IPO JUU YA WATEULE WAKE.

 8. Sungura,
  Ama kweli ukipenda chongo utaliita kengeza! Na wapenda ubishi utawaona tu, Sasa wewe bwana mkubwa Sungura, kama unafikira nzima, unaweza kusimama pahara ukamsikiliza Msigwa? Kwa lipi? Siasa ama Kanisa? Mimi nakushangaa sana, unasema naongea pumba, inawezekana kweli zikawa pumba kwako, maana huelewi somo; umekalia ushabiki. Waroma wa kale walimuua mwanasayansi mmoja (Sitaki kumtaja) kwa madai kuwa anakufuru Kanisa na Mungu, aliposema, Dunia ni duara na wala si kama meza, vilevile dunia ndiyo inayozunguka wala si jua. Baada ya miaka kupita ikathibitika kuwa kweli Dunia ni Duwara na kwamba ina zunguka kulizunguka jua! Waroma wa kanisa, wakamurudishia eti ‘HESHIMA’ Marehemu kwa kuiita moja wapo ya Kanuni za Sayansi ya Anga jina lake! Kama waroma wasomi, walimuona mwenzao ‘Pumba’ nitashangaa nini wewe kusema mimi ni mtu wa pumba, wakati najua sipo upande wako kwa hili la Msigwa?

  Usidhani simpendi Msigwa ama nakichukia chama chake, kinachonifanya ni muone mpuuzi, ni kutokueleweka kwake! Yeye ni nani? Hebu nielezee mwenzangu wewe unayeongea nafaka zilizokobolewa. Msigwa ndiye msemaji wa Maasikofu au ndo msemaji wa Kanisa? Hao Ma Baba Afikofu, unataka kusema ni maadui wa Mzee Sitta? Maana kama Msigwa hana kitu cha Kipuuzi moyoni mwake, angeainisha ubaya wa lile Bunge la katiba,na Rasmu yenyewe, na wala siyo Sitta kama Sitta! Wenzako tunawaheshimu wazee, kutokuwa na adabu si ndiyo demokrasia, mchungaji hana hekima hata kidogo, apunguze ukali wa maneno! Inawapasa mjue (wewe na wachungaji wa namna ya Msigwa) kwamba, haipo Mamlaka inayojiweka yenyewe, ukiipuuza unampuuza aliyeifanya iwepo, ambaye ndiye Mungu. Unapaswa kutoa maoni na ukosoaji kwa Busara, adabu na upole. Vilevile jueni pia kuwa, mchngaji siyo kusimama na kuhubiri tuuuu, mwanzo mwisho, bila maswali kwa wasikilizaji, kisha unaombea tu sadaka, halafu unakaa! Wachungaji wa namna hiyo ndiyo hawa waliopo kuwili, siasa na kanisani, ni lazima wabolonge!

  “Ufahamu ni chembe ya uhai!”

 9. Timothy na Mabinza,

  Kosa la Msigwa ni nini katika yale aliyosema hapo?

  Mnakielewa anachomwambia mzee Sitta, mlisikia Sitta alichowaambia maaskofu na wachungaji walipokemea maoni ya wananchi kuondolewa kwenye rasimu ya katiba?

  Naona kama mmetumia akili ndogo sana kuandika mlichoandika kuliko ilivyowapasa.

  Hebu fikiria Timothy unaposema wangebaki bungeni, inaonesha wewe au huelewi kilichokuwa kinaendelea huko bungeni au unaelewa lakini unakubaliana na ufisadi unaoendelea ktk taifa hili, maana bila shaka wewe nawe unanufaika na huo ufisadi.

  Mabinza nawe sijui utaacha lini kuongea pumba kwa nambo ambayo yabahitaji akili pana, wewe bila kuoima huwa unavagaa tu.

  Msigwa abampi fa Sitta kwa maneno yake dhidi ya viongozi wa dini waliopinga kilichofanywa na bunge maalum, lakini wewe unaongelea mambo ya itikadi kuwa si uadui kutofautiana.

  Wewe umeona Msigwa ameongelea mambo ya itikadi hapo?

  Ati unamwambia Msigwa aache kumhusisha Mungu mkuu katika mambo ya kipuuzi.
  Ni jambo gani la kipuuzi alilosema hapo, au akili yako wewe ndo puuzi hivyo inaona kila kitu ni upuuzi?

  Nani alikuwa na haki ya kumwambia Sitta huo ukweli kama Siyo Msigwa?

  Haihitaji akili nyingi ki hivyo kuelewa kuwa kilichofanyika bungeni kilikuwa na wingi wa hila na ujanjaujanja wenye lengo la kuendelea kuumiza watu.

  Msigwa angekuwa na tamaa angebaki bungeni kuendelea kupokea laki tatu ya wafuka jasho wa Tanzania, lakini alitoka na kuachilia mbali huo wingi wa fedha. Halafu leo mtu bila kufikiri sawasawa unamwita mwenye tamaa, lazima utakuwa hutaki kutumia akili yako jinsi ipasavyo.

  Ishu hapa si itikadi ya Msigwa against itikadi ya Sitta, kisiasa. Ila ni matamshi ya Sitta dhidi ya viongozi wa dini, na matamshi ya Msigwa dhidi ya Sitta.

  Jiongezeni ufahamu ili muone mambo kwa mapana yake waungwana!!

 10. MSIGWA,
  Unatetea kanisa la nani, linaamini nini na linatumia Kitabu gani? Kwani Mzee Sitta, ndiye Amelishikia akili Bunge? Wewe unadhani waliomo humo Bungeni hawawakilishi wanachi, akiwemo nani ndiyo atawakilisha wananchi? Ninyi mlichagua kutoka nje, waliokuwa wamewatuma humo mliwauliza wakawaambia tokeni nje? Kama hamkupata rlidhaa hiyo kwa waliowatuma, mnamtetea nani, kwa hayo mnayoyasema? Kumbukeni kuwa utofauti wa maoni na itikadi siyo uadui, unachojaribu kukipanda kwa kofia ya uchungaji kujumlisha unasiasa, matokeo yoyote yawe hasi ama chanya utavuna! Maana Neno linasema apandacho mtu ndicho atakachovuna, jiulize unapanda nini Msigwa? Usimhusishe Mungu Mkuu kwenye upuuzi, na tamaa. Mhusishe katika kuitafuta haki ya kweli!

  “Ufahamu ni chembe ya Uhai!”

 11. Mch. Msingwa, achaguwe, moja tu kuliko kulalamika, hekima ni muhimu, angejuwa hayo asingetoka Bungeni, Tanzania tuna nyumba moja tu ya kutunga sheria na sio kwenye majukwaa ya siasa. Yeye kama mchungaji aliktakiwa kusimama katika na fasi yake kuwashauri wenzake, ila na yeye amekubali kuketi katika mabaraza ya watu wenye mizaa na maisha ya watu. Anacho fanya ni kupoteza mda tu, Tuhubiri injili watu waokoke, kuliko kupandikiza watu chuki zisizo na msingi wowote. Pole sana, hata suala la kukemea lina utaratibu wake, sio kukurupuka tu na kutoa matamko ambayo yanapotosha uma. KAMA KANISA TU KAZI YA KUFANYA, HERI WAPANISHI MAANA HAO WATAMUONA BWANA.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s