Matangazo tiba asili marufuku!!

Baraza la Tiba za Asili na Tiba Mbadala Tanzania limesitisha vibali vya kurusha matangazo ya tiba za asili na mbadala kwenye vyombo vyote vya habari kwa kile kilichoelezwa kuwa yanapotosha jamii.

Taarifa iliyotolewa na kwa vyombo vya habari , imeeleza kuwa katika siku za karibuni kumekuwapo na matangazo mbalimbali ya tiba hizo ambayo baadhi yake hayaisaidii jamii.

Kutokana na taarifa hiyo ya baraza, vyombo vya habari havipaswi kupokea kibali chochote cha kutangaza matangazo ya tiba hizo hivi sasa, kwa kuwa ni batili.

Pia taarifa hiyo inaeleza kuwa, chombo chochote kitakachorusha tangazo au kipindi kitatozwa faini na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

naye mtaalam wa tiba asili, tabibu Rahabu Rubago ameiambia BBC kuwa hatua hiyo ya Baraza imetolewa bila wao kupatiwa taarifa hiyo mapema na kueleza kuwa watapata hasara kwa kuwa baadhi yao wametengeneza vipindi tayari kwa ajili ya kuvirusha kwenye vyombo vya habari.

–BBC

Advertisements

3 thoughts on “Matangazo tiba asili marufuku!!

  1. Nashukuru kwa walioliona hili japo kwa kuchelewa lakini muhimu. Matangazo haya yanaipotosha mno jamii.

  2. Wengi wao wanatafuta pesa tu. Lakini dawa nyingi hazina msaada wowote kwa mgonjwa.

  3. Mimi, nilidhani wangepiga marufuku waganga wa kienyeji tu!! Hawa ndio wanaoleta shida kubwa. Lakini watu wa tiba asili, hao hhawana shida yoyote. Labda kama kweli kua watu waliojiingiza huko (wanaodanganya watu). Lakini kwa ujumla tiba asili ndiyo tiba hswaaa inayozuia hata hayo maradhi mengine!!
    Kwa mawazo yangu, mimi naona kama tumeingia tena kwenye kulazimishwa kutumia dawa za kemikali tu ambazo kimsingi, zina madhara makubwa kwa afya zetu.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s