Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu!

utatu

Naomba kufafanuliwa mambo haya yafuatayo:

Yesu ni nani, Mungu, Roho Mtakatifu

Na pia Kuna watumishi wengine wanawabariki watu ” Nawabarikini kwa Jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu”

Naomba kueleweshwa asanteni Mungu awabariki kwa kunifundisha

–Janeth Mmari

 

Mada Nyingine inayotaka kufanana hiyo (UTATU) uko hapa https://strictlygospel.wordpress.com/2012/02/09/utatu-mtakatifu/

Advertisements

101 thoughts on “Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu!

 1. Ndugu Lwembe,

  Nimeiona makala yako nikichelewa, samahani kabisaa. Naona hujaelewa unalolisema ama hujanielewa… Unasema kumkimbia mtu anaedai “miungu watatu”? Kwa nini unaogopa kusema kumtandika viboko vya kiroho? Sikiliza Lwembe wala usiwe mvivu kirahisi huku ukijificha ndani ya kile unachokiita lugha.

  1.Nimesisitiza sana nikikuuliza utofauti kati ya msimamo wako na wangu lakini hukupata jibu kwani hauko. Pia nikakuonyesha kama unaupendelea upinzani kuliko ukweli.
  Wewe kama mwalimu, sidhani kama unaweza kwamishwa na maneno kama “one” au “oneness”. Nafikiri hukukwama bali ni namna yako ya kuuchochea upinzani. Kwani wewe ukiwa na umaarufu sana ndani ya utafunaji wa lugha, pia ukiaminika na baadhi ya wasomaji huwezi poteza mda wako kwa maneno kama hayo.
  Sikiliza Lwembe, kama unakubali kama hiyo hesima unaistahili, tafakari kama huwezi andika kitabu juu ya hii neno moja “One”! Kwani kwa mfano Biblia inapotuambia”mme na mke wamekuwa mwili moja”, hiyo siyo “one” ambayo ulitafsiri!
  Nimekuambia pia kama Biblia haitajithahidi kutuelewa. Ni kazi yetu kuielewa. Sasa umependa sana lugha ya Biblia ndiyo isujudu mbele ya lugha yako!!!! Hiyo ni upungufu mwingi kiroho ambao sikutakie. Ndio maana katita Makala yangu ya 27/10/2014 at 12:45 PM nikatoa hiyo hiyo shairi ya 1 Yohana 5:8 katitka versions nyingi ili ijulikane kama Biblia inaongea tofauti ya wanaadamu. Pia nikakufahamisha kama Biblia tunayo ni tafsiri, wala hakuna lugha iliyo njema kuliko ingini. Lakini bado nakuona ukiamini wewe ni mtaalamu wa Kiswahili hapo ukikana tafsiri ya Biblia ya hiyo hiyo lugha, pia ukiitumia sana pasipo kuleta yako ambayo unaelewa.
  Mimi sikupenda niwe mvivu kama wewe, ndipo nikatafuta kindanindani ili mimi ndo nielewe kile Biblia inachosema. Ok, Hapo nikakuonyesha kama nilitafuta ndani ya dictionaries. Kweli kwa tafsiri iliyo rahisi, una haki. Lakini kila baadhi ya maneno yana tafsiri nyingi sana. Ile ikaniconnect kufahamu kwa nini oneness ilitumiwa pahali pa “one”, jambo ambalo ulipenda libaki katika mantiki ya juu juu. Nadhani nikikushawishi kunyenyekea mbele ya lugha ya Biblia sitakuwa nimekosea!

  2.Umekubali mwenyewe kama Baba, Mwana na RM ni udhihirisho wa Mungu Mmoja, nami naamini hivyo tu na nimeionyesha tangu mwanzo wa mjadala. Sasa sijue unakwamia wapi! Mbona ukisoma makala yako yote katika hii blog hutaona mahala ulipoandika kwa mfano “RM alitukufilia msalabani”. Udhihirisho siyo Mungu, pia Baba, Mwana na RM siyo majina ya Mungu.
  Ina maana mnaweka “=” mahala ambapo haistahili. Acha nikupe mfano wetu sisi watu: Fikiria mama msomi kiwango yeye ni mwalimu wa chuo kikuu pia amepewa kuwa waziri. Fahamu kama hawo walimu wanapenda sana fundisha. Huyu mama akiwa akifundisha ni MWALIMU, akiwa ndani ya siyasa ni WAZIRI na akiwa nyumbani ni MKE wa mme na MAMA wa watoto. Sasa kuandika “MWALIMU=WAZIRI=MKE” ni kosa licha ya kuwa ni vyeo vya mtu ule mmoja. Pia ukitaka akufundishe utakuja kwake ukimuita MWALIMU, lakini ukiwa mtoto wake utafika kwake ukimuita mama mzazi…. Ndio maana utasikia watu waliyoamini wakijazwa, wanasema kirahisi kama wamejazwa na RM. Kama wameokolewa kwenye ajali wanasema haraka kama Baba wa Mbinguni amewaokoa…

  Kwa mwisho kama jinsi nilivyokuuliza huko mbele, wewe unaona wapi nimekosea na wewe unasemaje? Kwani mpendwa, nafikiri kwa hii mjadala ulijilinda sana kuwafundisha watu ukipendelea kupingana tu.

  Bwana akubariki.

 2. Ndg Ziragora,

  Kwa kadiri ninavyoyasoma maelezo yako, naona bado tena yamejaa utatanishi, aidha labda ni kutokana na ujinga wa lugha, au tu kwamba jambo hili liko nje ya ufahamu wako. Unaniambia, “”Nilijithahidi kukuelewesha kama alietafsiri kwa kiswahili hakukosea na kama ukitafuta mantiki zote utakuta kama umoja ni mmoja”” hili si kwamba ni tatizo la uelewa tu, bali ni zaidi ya jambo hilo!!!

  Labda ktk kuliweka sawa suala la lugha, kama ukiona itakufaa, maneno “Umoja” na “Mmoja” si sawa kimantiki, kama vile ambavyo neno ‘One’ na ‘Oneness’ yasivyo sawa!
  ONE – (Mmoja or Moja): a single person or thing
  • Just one as opposed to any more or to none at all; single
  ONENESS noun [mass noun] – (Umoja) -unity, fellowship.
  • The fact or state of being unified or whole, though comprised of two or more parts: the oneness of all suffering people.
  • the fact or state of being one in number: holding to the oneness of God the Father as the only God.

  Kimsamiati maneno hayo yako hivyo lakini itategemea sana kulielewa kwako neno la msingi ambalo ni One au Moja!

  Pili unaposema kwamba Mungu ni Mmoja huku ukiyakataa maelezo ya dada Janeth kwamba “”Baba=Mwana=RM”” unasema kwamba hayo ni mapokezi ya chini sana; halafu hapo hapo unasema, “”Baba, Mwana, RM ni udhihirisho tofauti wa Mungu mmoja, … Ondoeni hiyo confusion. Kama Mungu anadhihirishwa kwa namna kubwa tatu tofauti siyo kusema kama amegawangika.””

  Ni kweli tunapaswa kuiondoa hiyo ‘confusion’ unayoileta; maana kama huo udhihirisho unaousema unauelewa sawa sawa basi sioni ni kwa vipi maelezo ya dada Janeth yawe ni “mapokezi ya chini sana”, zaidi nakuona wewe ndiye uliye ktk ufahamu wa chini sana kuhusu unaloliongea!

  Iwapo Mungu ni Mmoja, hakuna udhihirisho unaoweza kumbadili, maana Yeye yule, jana na leo na hata milele! Kama alijidhihirisha kama “Baba” hilo halimfanyi asiwe yule Mungu tunayemzungumzia kuwa ni Mmoja, bali ni huyo huyo akijifunua kama “Baba”; huko mbele tena akajifunua kama Mwana, ndani ya Yesu Kristo, Mungu yule yule; na ktk siku zetu, amejifunua kama RM ndani ya Kanisa lake, Mungu yule yule; HAKUNA wakati wowote ule alipojidhihirisha ktk hizo nafasi tatu zote kwa mara moja!!!!!!!

  Pia elewa kwamba roho wa udanganyifu si mjinga kama unavyofikiri, akikuambia kuwa Baba, Mwana na RM ni miungu watatu si utamkimbia!! Anakuambia kuwa hao si miungu watatu bali ni Mungu mmoja lakini si Mungu yuleyule, ndiko huko kukana kwako jambo la “Baba = Mwana = RM : kuwa ni Mungu huyo huyo Mmoja; “Ukiniona mimi umemuona Baba”!

  Kwa akili ya kawaida, wala huhitaji RM ili upambanue jambo jepesi na lililowazi kama hili, kwamba dada Janeth yuko sahihi kwa kuamini kwake kwamba Mungu ni Mmoja (ONE). Hivyo kuhusu huyo Mungu, ktk kuliweka wazi zaidi, basi kuwa kwake Baba ni sawa na kuwa kwake Mwana, na ni sawa na kuwa kwake RM; The Dynamics of the THREE Manifestations (the mechanics) is the VERY same GOD!!!

  Ukilikataa jambo hilo, maana yake unatuambia kwamba Baba SI Mwana wala SI RM; vivyo Mwana SI Baba wala SI RM, na RM SI Baba wala SI Mwana, bali (wote) ni Mungu Mmoja; GONE with the WIND!!!

  Gbu!

 3. Ndugu Lwembe,

  Nashukuru pia kwa hoja yako. Bila shaka ulitambua kama tangu huko mbele nilikuwa nikidai kama Mungu ni mmoja. Ulisikia utofauti kwa neno”umoja” lililo la kibiblia kwa version ya kiswahili. Hiyo ndo ilikutatiza sana licha ya kuwa ndo lile Neno la Mungu; kwani uliweka lile neno ndani ya AKILI zako ndipo ukatosha result kama nilitaka. sema kama kuna Mungu watatu wanaofanya umoja. Nilijithahidi kukuelewesha kama alietafsiri kwa kiswahili hakukosea na kama ukitafuta mantiki zote utakuta kama umoja ni mmoja. Lakini nafikiri hukutosheka. Kwa mfano rudilia ile makala yako ya 06/11/2014 na ile yangu ya 07/11/2014 uone jinsi nilikuwa nikikuhakikishia kama Mungu ni mmoja!!! Fahamu kwamba siyo Biblia ndo itatusikia bali ni wajibu wetu kuisikia.
  Lakini hata hivi Lwembe, hakikisha analolisema ni kweli. Unapofahamu kama Mungu ni mmoja na udhihirisho mbalimbali, kwa nini tena umrejee Dada Janeth ukisema Baba=Mwana=RM? Hayo ni mapokezi ya chini sana. Baba, Mwana, RM ni udhihirisho tofauti wa Mungu mmoja, ule Mungu wa Ibrahim, Isaka na Yakobo. Hivi kuna Mungu na udhihirisho wake. Ondoeni hiyo confusion. Kama Mungu anadhihirishwa kwa namna kubwa tatu tofauti siyo kusema kama amegawangika.

  Nashukuru tena kwa makala yako na kwa jinsi ulitambua kama hatuna utofauti ndani ya maelezo yetu.

  Mungu akubariki.

 4. @ Chemo,
  Ninakushukuru kwa kunielewa,
  & for the encouragement,

  May the Lord richly bless u!

  @ Ziragora,
  Ninakushukuru kwa mjadala, majadiliano yanatupa fursa nzuri ya kujifunza, hata tofauti zetu!

  Kama unavyoona tulianza tukiwa na versions tofauti za Mungu huyo Mmoja tunayemfahamu, lakini kwa kadiri tulivyoendelea na majadiliano na tafakari yake, naona tumefika mahali sote tunaona sawa, yaani binoculars zetu tumezi fine tune mpaka tunamuona sawasawa na alivyo na si zile versions ambazo alikuwa out of focus, au somewhat blurred, tunasema Mungu mmoja lakini tulikuwa tunawaona watatu!!!

  Hii Siri kuu inayofunuliwa ktk 1 Timotheo 3:16, umeirejea ktk uhalisi wake na ndivyo jambo hilo lilivyo, nalo ni Siri kama unavyolisoma, kwahiyo si kwamba watu wanakwepa, hapana, HAWALIELEWI tu kutokana na huko kuwa SIRI!!!

  Tazama kuna wakati dada Janeth ktk kuisoma michango alifika mahali Siri hiyo ikamfungukia, ndipo akasema, “”Baba=Mwana=RM””!!! Jibu lako kwa jambo hili likawa hivi:
  “” Unaposema Baba=Mwana=RM umekosea kabisa kwani ni mafikiri yako wala Biblia haikuambie vile. Ni vema zaidi kwako kusema kama hili jambo limekupita ufahamu kuliko kayasema yasiyo ndani ya Biblia.””!!!

  Lakini hapa mwisho naona umeungana naye nawe SIRI hiyo ilipokufungukia, ndipo unasema kutoka huo uelewa mpya kwamba:
  “” Mungu kwa namna zote ndo Baba, akidhihirishwa katika Mwili ndo Mwana, na Roho yake ndo RM. Hawapo watatu, ni mmoja tu anayetambulikana kwa kwa lugha ya kibiblia kama “Baba, Mwana na RM”””

  Yaani kwa kifupi, kama Janeth alivyolielewa jambo hili hapo mwanzo nawe pia umeufikia uelewa huo unapotuambia : Mungu kwa namna zote ndo Baba, akidhihirishwa katika Mwili ndo Mwana, na Roho yake ndo RM; au kwa urahisi, unapojiondoa ktk mwili uinukie huko Rohoni, ambako ndiko Mungu aliko na kufahamika na kuabudiwa, basi maneno hayo uliyoyasema kuhusu Mungu ndiyo haya: “Baba=Mwana=RM”!!!!

  Nikushukuru tena kwa jambo hili, Utukufu na Sifa ni kwa Bwana aigeuzaye mioyo yetu hata kumuelekea Yeye!

 5. FAHAMUNI: Mungu amekaa katika hali ya Roho, ili aabudiwe katika Roho na kweli ” WAABUDIO WA KWELI WATANIABUDU KATIKA ROHO NA KWELI” . Kristo amekuja katika mwili, ili awakomboe wanadamu ” SIFANYI MAPENZI YANGU, ISIPOKUA NAFANYA MAPENZI YA BABA YANGU ALIYENITUMA. Hivyo, ni vizuri kumjua Baba na mwanae wa kiroho…mwenye jina la wokovu kwa wote. nikweli kabisa kua, Mungu amejifunua katika mwili wa mwanae, lakini hivi unawezaje kumjua hapo billa ya kwanza kumjua na kumuamini mwanae!!!!….si mwishoe, tutamuita yesu ni mungu bila ya kumtambua mwana!!!!!!!!!!!!!

 6. sasa, biblia inapofundisha” msimuite mtu, Baba…kwa kua, Baba yenu ni yule aliye mbinguni, inamaanisha “MUNGU”. “msimuite mtu, Mwalimu…kwa kua, Mwalimu wenu ni kristo, inamaanisha, ni yule kristo mwana wa Mungu, aliyekuja katika mwili , ili kumfunua Baba yake, na kufundisha, yale yote aliyomuagiza. ndipo sasa, twapata zile maana muhimu, zisemazo hivi, (1) ” WAKUJUE EWE MUNGU WA KWELI NA WAPEKEE, NA YESU KRISTO ULIYEMTUMA”…..(2) ” KWA MAANA JINSI HII MUNGU ALIUPENDA ULIMWENGU, HATA AKAMTOA MWANAE WA PEKEE, ILI KILA AMUAMINIE, ASIPOTEE, BALI AWE NA UZIMA WA MILELE” …..(3) ” HAKUNA AMJUAE MWANA, ILA BABA, NA HAKUNA AMJUAE BABA, MPAKA MWANA APENDE KUMFUNULIA. NK NK. Sasa ndugu zangu, nikweli tunafanya juhudi kubwa ili tujue kila kitu, lakini mimi nafikiri kua haya mepesi tuliyofunuliwa, ndiyo yakwetu, alafu yale ya sirini kwakua ni ya muumba wtu, basi tumuombe Mungu atufunulie yeye mwenyewe. Bwana awabariki.

 7. Wapendwa,

  Hii siri ndo wengi wanapenda kwepa:”1 Timotheo 3:16 Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.”
  Mungu kwa namna zote ndo Baba, akidhihirishwa katika Mwili ndo Mwana, na Roho yake ndo RM. Hawapo watatu, ni mmoja tu anayetambulikana kwa kwa lugna ya kibiblia kama “Baba,Mwana na RM”
  Mbarikiwe.

 8. Ndugu Lwembe,

  Ikikupendeza kuwa wa nuru naomba uweke wazi ile version ya Mungu wako uliyoisema ili nikuelewe. Ndugu Mhina anpotuambia kuacha tu tofauti tudogo ndani ya hoja zetu iko sahihi kabisa. kwani hata mimi nashangaa ninpokuona ukinipinga bila sababu halisi inayotofautisha hoja zetu. Ili unipinge unajithahidi sana uutumie uongo ukihakikisha kama nimesema neno ambalo sijawai sema. Hiyo ndiyo uongo. Unaposoma hoja zangu utaona maswali kama “Lwembe unaweza onyesha mahala nilipoandika unayonidanganyia?” Ulipakosa mara nyingi. Baadae nikaamua katika hoja yangu ya 10/11/2014 kukupa kifupi cha hoja zangu ili usahihishe lililo wazi lakini ulikwepa licha ya kuwa ulifahamu kama ndipo utaeleweka. Wewe ulipendelea kutembea katika upinzani usiyo na lengo nzuri. Mungu hana version Lwembe! Au ni Mungu ama miungu. Jiweke basi sawasawa ujibu kwa ile hoja yangu ili tofauti ya hoja zetu iwe wazi kwani unapotukana Mungu wa Ziragora hakikisha siyo wako ili usiangamie kwa kukosa ufahamu. Na mpaka pale hujaonyesha tofauti iliyopo kwani unabahatisha tu ukipindisha hoja zangu ndipo uzipinge. Yaani unapinga hoja zako mwenyewe.

  Asante.

 9. Lwembe,

  Acha kupofusha wasomaji. Hakuna swali ya kipagani hapa. Ukipenda sema uko mpagani pia mpumbavu iweke hadharani.

 10. Du! Hongera CK Lwembe. Umefunua vema sana maandiko juu ya maada hii. Mungu atukuzwe! Maelezo yako yamenyooka sawasawa. They bear witness in my heart!

 11. ndugu zangu wote katika bwana, asanteni sana…dada janeth nakushukuru sana kwa kutuletea mada nzuri iliyotujenga vyema. Ndugu yangu ck lwembe na ziragora…asanteni kwa michango yenu yenye maana sana. Tofauti zenu ndogo ndogo, nawaombeni zisiwatoe katika upendo wa yesu, wote mpo sahihi tu, na Mungu anawapenda. Mimi niishie hapa, kwaherini.

 12. Mhina,

  Mbona umeniunganisha kwenye issue nisiyoijua?
  Mambo ya Mungu kuzaa na wanawake, Ziragora ndiye aliyeukuuliza maswali yake, mimi nilisema tu kuwa hayo maswali “yatawaweka sawa akili zenu”; si unaona yalivyo kuweka sawa mpaka umegundua kuwa ni maswali ya wapagani, “”” ‘U’siulize maswali kama watu wa Mataifa wasiemjua Mungu wa Biblia, hiyo ni aibu sana kwenu!!. Mungu anafanya, anazaa kwa uwezo, sio kwa msaada au mke yeyote wa kibinadamu””” !!!!

  Hayo mambo ndugu yangu mimi nimewakuta mnafundishana, kwahiyo hiyo hoja uliyoileta, Ziragora ndiye anayeijua; kama unalo ktk niliyoyaandika mimi, lete tuyatazame, maana Mungu anayemuongelea Ziragora si huyo ninayemuongelea mimi, hata wewe pia, nakuona nawe kama una Mungu wa staili yako, ila unamuonea haya kumtoa hadharani, mtoe bwana tumjifunze!!

  Gbu!

 13. Ndugu Mhina,

  Unazungmuza vizuri kabisa. Nashukuru sana kwa hoja lako. Unayoyasema ni kweli lakini unachanga namna ya kuitwa jina na nuru au umungu wa Yesu Kristo.

  Hujakosea, lakini fahamu kama alipotabiriwa iliyosemeka ni kwamba ataitwa Imanueli, Mungu pamoja nasi. Lakini alipoonekana kihalisi ndani ya mwili Biblia inasema alionekana kama Mwana pekee atokae kwa Mungu. Hivi kuna jinsi iko na jinsi alionekana kwa watu. Ndipo ukawa umekubali kama walimuita Mwana wa Daudi wala hakukataa na waliyomuita hivyo aliwatendea miujiza ili ifahamike kama alitoka kwa Baba.

  Asante.

 14. Lwembe,

  Nilifikiri unasemaga uongo kumbe wewe una definition nyingine ya uongo? Sasa ile ujanja ya kujifariji na mantiki ingine ndio itakuangamiza. Acha ile ujanja, leta hoja za mwalimu wa neno la Mungu, au kama hukulifahamu hili jambo ni wakati wako wa kujirekebisha.

  Sikiliza Lwembe kuna mda nitapastia uongo wako kwa kukufundisha tena kama hapo zamani tofauti ya uongo na kifra na pendekezo na msimamo….

  Kama kwangu najua Mungu anapita fahamu zote za binadamu na ni kibiblia kabisa, kwako unamuona rahisi sana, hapo siyo uongo kwangu na kwako. Pengine niseme kuna ukaidi wa kubeua Neno la Mungu kwa upande wako kwani wewe mwenyewe umabandika shairi nzuri kama hii ”1Kor 13:9-10 Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu; lakini ijapo ile iliyo kamili, iliyo kwa sehemu itabatilika.” inayothibitisha niliyosema ambayo unafika baadaye kuyaita uongo. Ukisema kumfahamu Mungu kindani ni shule rahisi sana utakuwa umehakikisha Mungu iko chini ya fikra za binadamu.
  Alimradi, pengine umechanganyikiwa katika hoja lako, wala hii siyo uongo ambayo ninaweza pastia hapa.
  In fact “uongo” ni kusema lisilo kweli ukiwa na uhakika kama ni uongo na ukiwa na kusudi fulani. Sasa hapa sione kusudi lako. Ila tu nikufundishe zaidi ili usiendelee ndani ya ujinga. Huwezi mfahamu Mungu kama hulitumie Neno lake. Na Neno lake linapatikana kiwango Mungu analoliachilia.

  Nakuona Lwembe, unapendaga uongo na Jela. Hutaimwa unachokitafuta, nataka ukiniulize mara pili ili uhakikishe wewe ni wa kuume au wa kushoto.

  Asante.

 15. Ziragora,

  Mtu muongo ni yule anayeliezea kwa umahiri mkubwa jambo asilolijua; huyo ndiye ana asili ya uongo inayojidhihirisha ktk hayo maelezo yake ya uongo kuhusu asilolijua!

  Wewe ulikiri kwamba si rahisi kumfahamu Mungu, nikakuelewa vizuri sana. Ila nikashangaa kukuona unatiririsha mafundisho mazuri ya kupendeza na yenye kueleweka kuhusu Mungu uliyesema si rahisi kumfahamu!!! Tazama ulichomwambia Sungura,
  “””Unapoongea, ninapata fursa ya kusema kama kumjifunza Mungu na kumuelewa kabisa kabisa haiwezikani kwani anapita ufahamu wa akili zote za wanaadamu. Tunamjua tu kwa kiwango anachokiachilia kulipitia Neno lake.”””
  Haya ndio maelezo ya kijanja yanayozalisha Uongo, ni wapi Maandiko yalipokuambia kwamba unaweza kumfahamu Mungu kupita Maandiko yanavyomfunua????

  Tafuta ktk maelezo yangu iwapo kuna mahali popote pale niliposema kwamba “si rahisi kumfahamu Mungu”, HAKUNA! Basi hata kwa akili ya kawaida tu, ni nani muongo kt ya mimi na wewe?

  Kumbe hujaacha bado yale mambo yako ya “Uongo na Jela zake”; acha hayo mambo ya kitoto, “telemsha maneno ya Mungu ueleweshe wasomaji!!!!

  Maelezo yako mengine kuhusu huyo “Mungu wako” asiyefahamika kwa akili za kawaida, nitakujibu kadiri itakavyohitajika!

  Gbu!

 16. Nawashukuruni ndugu lwembe na ziragola kwa Michango yenu imara…..lakini lazima muelewe kua, Mariamu kumzaa bwana yesu katika mwili wa kibinadamu, kamwe sio kigezo cha Muhimu cha kipekee cha kumfanya bwana yesu ndipo awe ni mwana wa Mungu. Biblia inasema kua “AMEDHIHIRISHWA KWA UWEZA WA ROHO (Mungu)….kua Mwana wa Mungu, sio kwa njia ya Mariamu, hapana!!, Mariamu alikua ni mjakazi au mtumwa wa Mungu, kwa hiyo, hakumsaidia Mungu chochote ili bwana yesu ndipo aitwe ni Mwana wa Mungu. Hapa mtapata jibu kua, ndio maana hata huko mbinguni, wapo wana wa Mungu teletele, Pasipo Mungu kua na Mariamu au kua na mke yeyote. Someni (Ayubu 2:1)…..Sasa niwaulize, mbona huko mbinguni, hamuulizi kama mlivyouliza kua, hao wana wa Mungu wa huko mbinguni, Mungu aliwazaa vipi? , alikua na mke gani?, Mama mariamu alikuwepo kule mwanzo ili kuzaa wana wa Mungu?!!….Kwa sababu mliuliza swali hilo kwa pamoja huku mkisifiana..haya na mimi nijibuni sasa. Msiulize maswali kama watu wa Mataifa wasiemjua Mungu wa Biblia, hiyo ni aibu sana kwenu!!. Mungu anafanya, anazaa kwa uwezo, sio kwa msaada au mke yeyote wa kibinadamu…Nuru ilipoangaza kwa yule bikira, kamwe haikumaanisha kua haikuwepo tangu Mwanzo, isipokua ilipitia tu, kwa mjakazi yule “NDIWE MWANANGU MIMI LEO NIMEKUZAA, UNIOMBE NAMI NITAKUPA MATAIFA KUA URITHI WAKO, NA MIISHO YA DUNIA KUA, MIKI YAKO….UTAWAPONDA KWA FIMBO YA CHUMA, NA KUWAVUNJA KAMA CHOMBO CHA MFINYANZI. Soma (Zaburi 2:7-9). Sasa ndugu zanguni, mkiniambia kua, jina la mwana wa Mungu lilianzia kwa Mariamu, wakati biblia inaonyesha kua, Mungu alitoa kile tayari alikwisha kuanacho, tazama pia, (Yoh 3:17) “MAANA MUNGU HAKUMTUMA MWANA ULIMWENGUNI ILI AUHUKUMU ULIMWENGU, BALI ULIMWENGU UOKOLEWE KATIKA YEYE!!…..Amwaminie yeye, hahukumiwi > asiyeamini amekwisha hukumiwa kwa sababu “HAKULIAMINI JINA LA MWANA PEKEE WA MUNGU !!!. Tumeona kua, Mwana wa Mungu, alikuwepo kiroho huko mbinguni, hata kabla ya kuzaliwa na Mariamu, wana wa Mungu wapo pia na wataendelea kuwepo katika ulimwengu wa kiroho.Sio jina la Mariamu wala mama zetu yanayotufanya tuiwe wana wa Mungu… Hayo mnayofikiri ninyi ni mambo ya kimwili tu, ambayo tutayaacha hapahapa duniani. Wewe kama biblia inakwambia kua, usipolikiri na kuliamini jina la Mwana wa Mungu, utakua tayari umekwisha hukumiwa, hivi huogopi kuliondoa na kutangaza eti “YESU NI MUNGU NA MUNGU NI YESU….NA MWANA WA MUNGU HAYUPO KWA KUA NI YULEYULE MUNGU?!!!!….mbona mwamuondoa mwana na jina lake, huku mkimtwika Mungu mambo yote kwa wakati mmoja?, mmeona wapi injili hiyo au wenzetu mwajua sana mambo yote ya Mungu!!. Mungu anakaa ndani yetu kwa sisi kulikiri jina la Mwanae bwana yesu aliyekuja katika mwili, huo ndio ule uzima wa milele jamani!!. Ndio maana wengine mnafundisha kua, aliyesulubiwa msalabani na wanadamu, pia ni Yuleyule Mungu ambae ni bwana yesu…hili mimi naliona ni tatizo kubwa sana. Ni lazima tumjue mwana wa Mungu na kumkiri kwa 100% kwa sababu, kupitia imani yetu kwake, ndipo yeye nae anatupa haki yake na kumjua baba yetu, haiwezekani kufundisha injili ya mkato mkato kua, Mungu ndie mwana na hapohapo ni Mungu, kwa hiyo, jina la Mwana wa Mungu halina maana, HAPANA!!,…Mungu kama Mungu ni roho ndani ya Mwana, na mwana kama mwana katika mwili ametumwa na baba ambaye kamwe hatuwemzi kumuona, ndio maana biblia inatuambia” BASI TUKIISHA KUHESABIWA HAKI ITOKAYO KATIKA IMANI, NA TUWE NA AMANI KWA MUNGU > KWA NJIA YA BWANA WETU YESU KRISTO!!!.Soma(warumi 5:1). Amen

 17. Shaloom Lwembe, Ziragora, na Mhina, Mbarikiwe tunaendelea kupata vitu vizuri sana huko kwa mada hii inayoendelea, kweli nashukuru sana

 18. Ndugu Lwembe,

  Mungu wangu akubariki !

  Nasema licha ya kuwa nimesoma kama huzipendi hizo baraka. Lakini maadam Mungu wa Biblia ndio Mungu wangu, unapokataa hizo baraka uwe umeapa kama hupendi baraka za Mungu wa Biblia. Kwani Mungu wa Biblia haishi kwa mtazamo wa Lwembe wala wa Ziragora, Anajitegemea Mwenyewe kabisa, ni Mungu Muumba mbigu na dunia na vyote vilivyomo pia Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo.
  Udhaifiu wa Lwembe wala wa Ziragora hupunguzi umungu wake, alimradi Mungu hahangaishwe na kwamba Lwembe ni dhaifu kwani ni jambo analolifahamu, lakini anachokichukia ni Lwembe kukataa kuyapokea maarifa.

  Sasa, unisamehe ukiona sikurahisishe kuitelemsha wino pasipo lengo. Katika kutokurahisisha mna faida yako ya kuthamatisha kurikodi uongo wako unaopatikana ndani ya ugeufu wa hoja za wachangiaji, zaidi zangu; pia contradictions unazoweka ndani ya hoja zako ili uonekane kuwa sahihi kwa ujanja; bila kusahau namna unavyopotosha mada yenyewe; na matusi.
  Ndo maana narudilia iliyo muhimu iwe nuru kwako ili nawe utie unayoamini; isiwe tu unajipendeza kwa kubandika comments kwa hoja za wengine.:

  1)MUNGU NI MMOJA,

  2)MUNGU ANAZIDHIHIRISHA KATIKA BABA, MWANA NA ROHO MTAKATIFU (unawaita sifa, na mwengine characteristics, na mwengine namna za kujionyesha kwa wanadamu, mwengine nafsi akiwa na namna yake ya kuelewa tafsiri ya nafsi, na mwengine utatu, na mwengine mihuri, …. haya yote ni maneno ya lugha ya binadamu siyo lugha ya Biblia. Kwa hivi sasa kusiwe kuhukumiana lakini tujithahidi tutumie lugha ya Biblia tu kuliko kuweka maneno mengine kwani maneno yale ni comments tu wakati Biblia imerudilia kwa maneno “Baba, Mwana, RM”).

  3)MUNGU ANA NAFSI MOJA NA SIYO 3. HIYO NAFSI YAKE NDIYE YEYE MUNGU MWENYEWE. PIA NAFSI YA MUNGU SIYO YA MTU.

  4)KUWA MTU NI MFANO WA MUNGU SIYO KUSEMA MTU NI MUNGU. PICHA SIYO MTU. SIJUE UTAPATA UFAHAMU NAMNA GANI !!! NILILETA CHANGAMOTO, TUONE KAMA TUNAWEZA FAHAMU JINSI MWILI, NAFSI NA ROHO NDANI YA MUTU VINAHUSIANA ILI NDIPO TUANZE UCHAMBUZI WA UHUSIANO WA BABA, MWANA NA RM. KABLA MTU HAJAFAHAMU KITU KIDOGO NI VIGUMU AFAHAMU KUKUBWA ZAIDI (ninapokusoma naona huna mashaka juu ya uwepo wa mwili, nafsi na roho ndani ya mtu na huo uhusiano upo pasipo hata kimoja kujitegemea)

  5)NAFSI YA MTU (MOJA TU ANAYO) INAPATIKANA NDANI YA DAMU. KAMA WEWE HUJUE SOMA SHAIRI HUKO MBELE. SIYO TU MTU HATA WANYAMA WANA NAFSI (AU UHAI WA MWILI)

  6)NDANI YA AGANO JIPYA JINA LA MUNGU NI YESU KRISTO NA SIYO KUSEMA NI MWANA.

  Hivi nimeweka in detail points 6 ambazo unaweza sahihisha kama unavyotaka ukiweka fikara zako wala siyo comments juu ya msimamo wangu. Pia sihitaji mafasiriyo mengi ndipo nielewe. Pia ni points ambazo zimekwisha thibitishwa kwa shairi za Biblia.

  Kwa mwisho umeweka kitu kizuri:”1Kor 13:9-10 “Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu; lakini ijapo ile iliyo kamili, iliyo kwa sehemu itabatilika.”!!!”

  Kweli nakuomba, rafiki yangu, epuka sana uongo; nilipenda niirikodi nikaona imekuwa mno ndipo nikaamua kama si vema kwa leo niibandike hapa kwani ingenisukuma nibandike yote uliyoweka kwa uwingi ndani ya makala yako yaliyopita ndani ya hii mada. Pengine nitashurtishwa kubandika uongo wako wakati nitakapokuona kuwa mkaidi wa kupindukia. Pia siyo siri kwako, unafahamu kama niko adui ya uongo na nikiuchambua nitakuwa nimehakikisha wengine wote wamesikia hii mada na wewe muongo tu umebaki, kiisha kuibandika iwe mwisho wa mada.

  Asante.

 19. Ndg Mhina,

  Hoja uliyoileta ni nzuri sana, tena itasaidia kutufungua macho yetu ya kiroho ili tuenende ktk roho, na ibada zetu ziwe ktk roho, maana Mungu ni Roho, naye hufikiwa kwa imani ambayo haikai mwilini bali rohoni!

  Kuna mkanganyiko mkubwa sana kuhusu Uungu wa Yesu Kristo. Kuna wengi wanao amini kama kwamba Yesu Kristo alikuja ktk Mwili kutoka mbinguni, jambo ambalo si kweli! Na ktk wazo lao hilo, wao huishia kumwona kwamba ni Eternal Son of God, yaani Mwana wa Mungu wa milele, Eternal maana yake asiye na mwanzo wala mwisho! Ninaamini haya maswali ya Ziragora kwa hao wenye kulifundisha jambo hili hivyo, yatawaweka akili zao sawa: “”” Na kama unamuona kwa mtazamo wa Mwana wa Mungu tu, je Mungu alimzaa tangu mwanzo na mke gani? Pia Mungu ana mke? Je mamae ni Miriam? Huyu Miriam naye alikuwa tangu mwanzo?””” hahahaha….!

  Kinyume cha mambo hayo, Biblia inafundisha kwamba Yesu Kristo ni Alfa na Omega, yaani yeye ni Mwanzo na Mwisho! Basi ili awe ndiye Mwanzo na huo Mwisho, inakubidi umtazame ktk macho aliyokufungulia Ziragora, yule Neno!

  Na kuhusu huyo Yesu, alipozaliwa ndipo alipoanza, na Uana wa Mungu wake tunauona kutokana mimba yake kutungwa kwa RM, ambaye literally ndiye Baba yake; ndipo kila ulipomsikia akisema Baba, basi jua kwamba huyo ni RM!

  Ukiitambua jinsi ya Adamu wa kwanza, basi huyu Adamu wa pili utaujua uhalisia wake kirahisi sana, maana ujio wao duniani ni identical, both by the Word! Yaani uanzie rohoni upite mwilini na uishie rohoni, usikwamie mwilini! Huo Mwili wa Yesu Kristo ulifinyangwa tumboni mwa Mariamu kama ulivyofinyangwa mwili wa Adamu pale Mwa 2:7 na kupuliziwa ile pumzi ya uhai, ile “Spirit of man” ambayo ndiyo hii hapa, “… Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu” Lk 23:46; Mungu akiwa amekwisha kumuacha, Mt 27:46 ” Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?” Ule utimilifu wa Mungu uliokaa ndani yake, ndio huu umeondoka, yule Baba aliyekuwa ndani yake, yule tuliyemuona akiapa kwa Nafsi yake!

  Mhina, nenda pole pole na Maandiko, utayaona mengi saana; si unaona hapo, kumbe Baba ni RM!!!!!!

  Ubarikiwe brother!

 20. Ziragora,

  Tuendelee,
  1The 5:23 “Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi NAFSI zenu na ROHO zenu na MIILI yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama …”

  Tumeona kwamba mtu ana components tatu ambazo ni mwili + nafsi +roho. Hizo components 3 kila moja ina CHARACTERISTICS zake tofauti.
  Mwa 1:27 “Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba”, nasi twafahamu kwamba “Mungu ni Roho” Yn 4:24; hivyo ni dhahiri kwamba huyo aliyeumbwa kwa mfano na sura yake, atakuwa ni roho pia. Kwahiyo tunaposema “mtu”, ninaamini huyu ndiye halisi, ambaye ni roho.

  “Mwili” ni mavumbi; Mwa 2:5 “… wala hapana mtu wa kuilima ardhi…”
  Roho haiwezi kulima, hivyo, “7BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi…” Sasa ni LAZIMA tuelewe kwamba hapa Mungu haumbi mtu wa pili, bali amechukua kutoka alichokiumba tayari, ule udongo, ndio ” akamfanya mtu…” pia huyu anayekuwa formed hapa si wa ” mfano na sura” ya Mungu!

  Baada ya kuufinyanga huo udongo, ” akampulizia puani pumzi ya uhai…”Uhai wote watoka kwa Mungu, hata uhai wa hilo dongo pia! “Pumzi ya mwanadamu (the spirit of man) ni taa ya BWANA; Hupeleleza yote yaliyomo ndani yake.” (‭Mit ‭20‬:‭27‬)‬‬‬‬‬‬; hii ndio roho ya mwanadamu, Zek 12:1 “… Haya ndiyo asemayo BWANA, azitandaye mbingu, auwekaye msingi wa dunia, aiumbaye roho ya mwanadamu ndani yake [‘aiumbaye…’ – formeth the spirit of man…].

  Mpaka umbali huu, hili ‘dongo’ kwa kutiwa uhai, limekuwa activated na hivyo sasa linaweza kufikiwa na dunia kimwili kupitia hisi tano- ‘Kuona, Kusikia, Kuonja, Kugusa na Kunusa’; na kiroho kupitia hisi tano nyingine za kiroho ndizo: ‘Kuwaza, Dhamiri, Kupenda, Mantiki na Kumbukumbu.’ Basi ktk stage hii hili ‘dongo’ liko sawa na mnyama, lina intelligence, kumbukumbu nk kama tu Biblia inavyolifunua jambo hili kupitia Nyoka, Mwa 3:1 “Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu.” Nyoka alikuwa ‘subtle’! Subtle = crafty; cunning; making use of clever and indirect methods to achieve something. Alikuwa ana uwezo mpaka wa kuongea, kama unavyomuona akiongea na Hawa akiu
  manifest huo werevu alionao! Sasa ukumbuke kwamba huyu nyoka wa leo si yule aliyekuwako kule Edeni, huyu wa leo ni badiliko lililomtokea baada ya kulaaniwa, akiwa ameshushwa kutoka ktk order ya “beast” mpaka kuwa “reptile” yule mwenye kutambaa!

  Tukiendelea mbele na lile ‘dongo’ letu, likiisha kuwa activated, iwapo Mungu angeishia hapo, basi Maandiko yangejivuruga maana angekuwa hakumaliza uumbaji pale aliposema amemaliza kwani hiki alichokitengeneza kingekuwa ni kiumbe kipya! Lakini tunasoma, “… mtu akawa nafsi hai.” Basi tunapaswa tujiulize yule mtu wa mfano wa Mungu yu wapi? “Je! Si zaidi sana hao wakaao katika nyumba za udongo, ambazo misingi yao i katika mchanga, hao waliosetwa mbele ya nondo?” (‭Ayu ‭4‬:‭19‬) Huyu akaaye ktk nyumba ya udongo ni yule mtu wa Mwa 1:27 huyu ndiye hiyo Nafsi hai akiisha kuingia humo ktk hilo dongo kuliendesha!!! Na Nafsini mwake, ndimo imo ‘imani’ ambayo kwayo yeye huwasiliana na Mungu tangu huko Edeni aliko wekwa baada ya kuumbwa!

  Shetani huweza kuufikia mwili na roho yake ili kuishawishi nafsi iondoke ktk imani, huko ndiko kuvutana kwa mwili na roho yake ile spirit of man vikiishawishi nafsi iondoke ktk imani. Katika Anguko Shetani alifanikiwa kupandikiza “Mashaka” katika Nafsi na hivyo humo kukawa na “Imani” na “Mashaka”, huu ndio “Utu” wa ndani, au yule ‘Inner man’ ambaye ukimlisha Neno la Mungu lililo Kamilifu, huyo hukua ktk kimo, ile Imani, hata kumfanania Kristo na kulitiisha dongo na roho yake; na iwapo utamlisha mambo ya dini, hicho ndio chakula kipenzi cha “Mashaka”, ndipo huyo hukua ktk kimo akijiongeza ktk Kutokuamini, na mwishowe huchukua Chapa ya Mnyama, Imani ikiisha kufa na hivyo huyo mtu kubakia kuwa sawa na mnyama hapo Utu wake wa ndani unapofikia kufanana na ule wa Nje!

  Basi ktk kutamatisha hiyo dhana yako, upungufu wake wa kwanza ni pale ulipomchukulia huyu mtu tunayemuona ktk Mwa 2:7, yaani Lwembe, huyu ambaye ni mwili + roho + nafsi, kwamba huyu ndiye aliye “wa mfano na sura” ya Mungu jambo ambalo si kweli; ndipo hiyo hesabu yako ya Mungu = Baba + Mwana + RM inakuwa batili kwa kigezo hicho.

  Na pia neno Mungu ktk lugha ni Sifa, hivyo kulifanya kuwa ni Nafsi haileti maana, kwani inakuwa zaidi ni jambo la kufikirika kuliko uhalisi! Tazama, ulisema kwamba Baba ni characteristic, na Mwana ni characteristic na RM ni characteristic, nazo characteristics ndizo zinazo tuhakikishia uhalisi wa kitu, ile tangibility ktk msingi wa imani, ndipo kilicho halisi hakiwezi kuishia ktk kufikirika, maana Sifa ni za kufikirika!

  Ingawa wewe unakataa kwamba Mungu hana Nafsi, hilo likimaanisha kwamba Mungu ni wa Kufikirika tu, lakini Biblia inasema anayo Nafsi, na Nafsi hiyo ndiyo inayoichukua hiyo Sifa ya kuwa Mungu; Yer 22:5 “Lakini kama hamtaki kusikia maneno haya, mimi naapa kwa NAFSI YANGU, asema BWANA, ya kuwa nyumba hii itakuwa ukiwa.”!

  Ndipo kutoka ukweli huu wa Maandiko, yale maelezo yako unayosema, Baba yuko na Mwana yuko, na RM yuko, na kwamba wametajwa zaidi ya mara 200, ukikuthibitisha huko kuwapo kwao, na ukitusisitizia kwamba huyo Baba + na huyo Mwana + na huyo RM ndipo unakuwa na Mungu; pasipo Baba huna Mungu, na pasipo Mwana pia huna Mungu na vivyo pasipo RM huna Mungu pia! Haya ni mambo ya kipagani kabisa, yaani mizimu, yanayovuka ufahamu wa kawaida wa mtu yeyote yule mpaka awe initiated into such crafty religious stupid circles!! Subtleness ya dhana hii ni pale Attributes ( Sifa za kiasili) za Mungu zilipobadilishwa kuwa Characteristics ili kumtambulisha Baba, na nyingine kumtambulisha Mwana, na nyingine kumtambulisha RM, na kisha kukana kwamba hizo si Nafsi and yet they form GOD ktk ujumla wao!!!!

  1Yn 5:7 “For there are three that bear record in heaven, the Father, the Word, and the Holy Ghost: and these three are one” kifungu hiki kinasema hao watatu ni mmoja; maana yake hauwezi ukawa na Baba halafu usiwe na Mwana au RM, na vice versa; ndio kusema, ukiwa na Baba, basi una Mwana na unaye RM, na kama huna RM basi huna hata Baba wala Mwana!!!

  Mungu ni mmoja kweli Ziragora, naye ni Roho. U Baba ni Sifa yake, U Mwana pia ni Sifa yake, na U RM nao ni Sifa yake Mungu huyo huyo. Kama ukijikumbusha kuhusu sinema, waigizaji na wazalishaji, wao wanalijua jambo hili; Muigizaji mmoja anaweza kuigiza zaidi ya nafasi moja, kulibaini hilo mpaka uzijue characteristics zake, ndipo utamgundua kuwa hao watu watatu uliodhani ni tofauti ni mtu mmoja!!!!

  Basi, ndugu yangu Mungu akubariki sana, kwa kujitoa kwako ktk jambo hili jema, tukifundishana mambo mazuri yahusuyo Ufalme wa Mungu, naye Mungu kwa upendo wake akitukirimia kuyafikia hayo, ili kuyabatilisha yale yaliyolipungukia Neno lake; 1Kor 13:9-10 “Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu; lakini ijapo ile iliyo kamili, iliyo kwa sehemu itabatilika.”!!!

  Gbu!

 21. Ndg Ziragora,

  Hizo baraka ulizonitakia kutoka kwa “Mungu wako” siwezi kuzipokea kwa sasa mpaka nitakapomjua kama ndiye Mungu wa Biblia au la, maana dunia ina miungu wengi sana wanaojibanza kwenye Biblia kwa ujanja na watu wengi wanawasujudia miungu hao bila ufahamu!

  Seriously speaking, hebu tuache hii “hide & seek” game, and let us go for ‘the Deep Things of God’ for a learning of the Mysteries!

  Sasa, ili twende vizuri, labda nikufuate nyuma ktk unayoyafundisha huku tukiyalinganisha na kile Biblia inachokisema kuyahusu ili tusirudirudi nyuma bila sababu.

  Kwanza kuhusu “Mtu” na “Utu”, unasema, “”“Mtu” is different from “utu” as person is not personality. Mtu ana utu lakini utu huna mtu.””” Kimsingi kwa jibu hili utakuwa unakiri kwamba HAKUNA “utu” bila “mtu”; yaani hauwezi ukawa na Personality without a Person! Kwahiyo unapozungumzia “Utu” basi ni lazima uwe unamzungumzia “Mtu”; Tofauti na hivyo, ikiwa kama unavyoiweka, kwamba “Utu” ndio “Nafsi” (yaani damu!) basi hilo litamfanya mkristo kuwa na nafsi mbili, jambo ambalo si kweli, 2Kor 4:16 “Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa UTU wetu wa NJE unachakaa, lakini UTU wetu wa NDANI unafanywa upya siku kwa siku.” Ndio maana niliwahi kukuuliza, iwapo huko hospitalini nikiongezewa damu na watu wanne tofauti, je, nitakuwa na nafsi ngapi?!!!

  Kwahiyo, tukirudi katika ule mfano wako wa “”Lwembe= mwili + nafsi +roho””, ambao Andiko lake ndio lile la 1The 5:23; mfano huu uliutamatisha kwa kuuwianisha na Mungu = Baba + Mwana + RM. Na kwamba ukiondoa kimoja kati ya hivyo vitatu, hautakuwa na Lwembe tena; kama ambavyo ukijisahaulisha Baba, huna Mungu, ukijisahaulisha Mwana huna Mungu, na ukijisahaulisha RM huna Mungu! Halafu unasema, “”Mungu ni mmoja na ndani yake kuna manifestations au caractéristics tatu.””

  Labda tukijiondoa ktk msimamo wa ubishi, inaweza kusaidia kusahihisha makosa madogo madogo ya ufahamu ambayo mwishoni hukutoa ktk mtirirko sahihi, kama vile ambavyo ‘manifestations’ na ‘characteristics’ si maneno yenye maana moja kama ulivyoyatumia! Characteristics huwa HAZIBADILIKI ndizo zinazokitambulisha na kukitofautisha kitu kimoja kwa kingine. Kwa mfano, Characteristics za mbao si sawa na za chuma, ndio zile sifa bainishi, au distinctive. Manifestations, ndio kama ule mfano wa maji ambayo characterics zake ni H2O, lakini manifestations zake ziko tatu; Kimiminika (liquid), Mvuke (Vapour) na Mango ie Barafu [Solid (ice)], na ktk manifestations zote hizi tatu, characteristic zake hazijabadilika, zimebaki kuwa ni H2O wakati wote!

  Ndipo kuhusu Lwembe, ili kuwa sahihi, hatuwezi kusema kwamba ana characteristics tatu, maana characteristics tatu zinafanya akina Lwembe watatu!!! Bali huo mwili, na nafsi na roho, hivi vitu vitatu, ni components ambazo kila moja ina characteristic zake! Basi components hizo zikiunganishwa ndio tunampata Lwembe, ukiondoa moja wapo ni kweli huwezi kuwa na Lwembe. Hata hivyo, ifahamike kwamba components hizo tatu zinapounganishwa kumtengeneza Lwembe, zitazaliwa characteristics mpya za Lwembe ambazo zitakuwa ni tofauti na hizo za components individually!

  Kwahiyo unapomchukua Mungu ktk mantiki hii, utakuwa unatuambia kwamba Mungu ana components Tatu; Baba + Mwana + RM, na hizi kwa pamoja ndizo humfanya Mungu; huyo uliyesema ni Divinity; sijui kama unakielewa unachotufundisha!!

  Lakini kwa vile ufahamu wako umeujenga ktk jinsi alivyoumbwa mtu, hizo components, ngoja tumtazame kwanza huyo mtu ili tuone kama ni kweli kwamba anamuwakilisha Mungu kimaumbile kama ulivyoliweka.

  Gbu!

 22. Ndugu Mhina,

  Umesema sio lazma nikujibu lakini naona ni vema nikujibu kwa kukurushia asante kwa namna umekuwa sana online, umejitambulisha mwenye kupenda Neno la Mungu na jinsi umependa kwa upekee Yesu Kristo.

  Pia napenda nikwambie kama Mungu wetu akiwa Roho inatakiwa watu wote wamfahamu kiroho na hiyo ndio mafundisho mepesi haswa kwa waumini wapya ili wakiwakuta watu Wa imani ingine wasiwapotoshe kirahisi wakidai wakristo wanaabudu mwanadamu.

  Nisikusumbue, narudilia hapa licha ya kuwa nina mafundisho mengi. Wewe tukiwa ku hatua moja tunangoja swali kutoka wengine.

  God bless you.

 23. Nashukuru sana ndugu ziragora. Umenisaidia vyema kimawazo na kimtazamo….nikweli kabisa kua, nilihitaji msaada ambao tayari nilikua nimeutia mtazamo wangu, ili katika jibu nitakalopewa, niweze kusaidiwa vyema, na si ujanja…lakini wewe umeweza kunijibu vyema kama nilivyotaka. Kumbe nilikua sahihi kwa 100%. Jibu langu haswa nimeliona huko mwisho wa jibu lako, umenijibu hivi: YESU HAKUITWA TU MWANA WA MUNGU, ALIITWA MWANA WA WATU, MWANA WA DAUDI NA MWANAKONDOO > KWA MTAZAMO WA KIMWILI……LAKINI KIROHO YEYE NI MUNGU ALIEUMBA VITU VYOTE !!. Ndugu ziragora, jibu hilo ni sahihi sana kwangu, ndivyo hapo juu nilivyotaka nieleweke, isipokua sisi pamoja na ndugu zetu wengi tunaotakiwa tuwabubirie injili ni wa kimwili, kwanini sasa tusiwahubirie injili rahisi kwa kuwaambia kua, Yesu kristo ni mwana wa Mungu, halafu wakikomaa, ndipo tunawalisha hicho chakula kigumu kwao, kua yesu kiroho ni Mungu mwenyezi?. Ndugu yangu asante sana, sio lazima sana unijibu ila endelea na mjadala wako na wengine katika bwana, na Mungu akubariki.

 24. Ndugu Mhina,

  Shukran kwa makala yako.

  Lakini mna contrast kubwa: umeanza ukiomba msaada baadaye ukaweka namna ya msimamo wako ukichagua shairi zinazokusaidia kusimamisha fikara zako ukiruka kwa hiari yako shairi zilizopashwa kusaidia, pia ukaweka vizuri contradictions ndani ya hoja yako maksudi uaminishe wasomaji unayoweka rohoni mwako na kwa mwisho unangoja atakaekupinga. Huone kama unaleta ujanja?

  Ninaposoma comments zako nafikiri msaada kwako ungelipatikana ndani ya swali hili ” Je Yesu ni Mungu pia Mwana wa Mungu ule ule?”

  Unasema “Mungu alikua ndani ya Kristo mwanae akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake ili asituhesabie makosa”. Hiyo ni kweli usihofu, kazi yetu siyo ya upinzani. Lakini nimeona umesoma Injili kama ilivyoandikwa na Yohana; Je hukusoma pia hii shairi? Yoh 1:1-5. Na kama umeisoma, sasa huyu Neno si ndie Yesu Kristo na imeandikwa alikuwepo tangu mwanzo, yeye ndie alieumba vitu vyote akiwa Mungu kwa namna isiyotambulikana na ulimwengu? Na kama unamuona kwa mtazamo wa Mwana wa Mungu tu, je Mungu alimzaa tangu mwanzo na mke gani? Pia Mungu ana mke? Je mamae ni Miriam? Huyu Miriam naye alikuwa tangu mwanzo?

  Zingatia kama kabla Miriam hajamzaa kimwili Yesu alikuwepo naye ndiye alimuumba Miriam lakina hakuitwa Mwana tangu mwanzo. Hapo ulipoandika soma vizuri:”Alifanyika mwili ndipo akaonekana KAMA Mwana pekee atokae kwa Baba”.
  Inatakiwa umwone Yesu kwa mitazamo miwili ambayo yeye mwenyewe anakubali: Mungu kama jinsi uungu wake uko wazi tangu mwanzo na Mwana kama jinsi nuru yake ilivyojitambulisha kwa ulimwengu il huwo ulimwengu umutambue kama Imanueli, Mungu pamoja nasi.

  Pia fahamu Mungu alizidhihirisha katika agano la kale kwa namna tofauti: moto, hema takatifu, Sandugu la agano.

  Pia Yesu hakuitwa tu Mwana wa Mungu, aliitwa Mwana wa watu, Mwana wa Daudi na Mwana kondoo. Ile yote kwa mtazamo wa mwili. Lakini kiroho yeye ni Mungu alieumba vitu vyote.

  Ubarikiwe.

 25. Ndugu zangu katika Bwana, Mimi najifunza mengi mazuri kutoka kwenu, lakini naomba mwenye uwezo, basi anisaidie jambo lifuatalo: Hivi katika ile (Yoh1:14) inayosema” Naye neno alifanyika mwili > akakaa kwetu, nasi tukauona utukufu wake, “UTUKUFU KAMA WA MWANA PEKEE ATOKAYE KWA BABA AMEJAA NEEMA NA KWELI”. Huyo neno, aliyefanyika mwili, atokae kwa Baba, ni Yesu kristo mwana wa Mungu, na kamwe, Sio yule Mungu huyo Roho, kua ndiye aliyekuja katika mwili, Soma(1Yoh 4:2). Mungu hakuja katika Mwili wa kibinadamu, au niseme” HAKUJIDHIHIRISHA YEYE MWENYEWE KATIKA MWILI WAKE BALI ALIDHIHILISHWA KUPITIA MWILI WA MWANAE, Soma(1Timotheo 3:16). Hiyo maana yake ni kua, kamwe hatuwezi kumuona Mungu kwa macho ya kibinadamu, isipokua, ni kupitia mwili wa Mwanae pekee, ndipo tunaweza kujifunza mambo ya Mungu, sio kwa mwili bali ni kwa roho pekee, kwakua, Mungu haonekani wala hana mwili wa kibinadamu. Bwana Yesu, hakusema kua, “mimi ndiye Mungu kwa uhalisia wa Mwili na roho, isipokua, alisema” aliyeniona mimi basi amemuona Mungu, kwa maana ya jicho la kiroho, na kamwe sio jicho la kimwili, kwa kua, Mungu “HAONEKANI KWA MWILI WA KIBINADAMU. Istoshe, kama mtu ni kweli, yeye hawezi kumtenganisha, Baba na Mwanae, inampasa pia, atufafanulie maneno ya Bwana yesu, kama ninukuuvyo: ” SIFANYI LOLOTE KWA NAFSI YANGU, ILA NI BABA AKAAYE NDANI YANGU, HUZIFANYA KAZI ZAKE” ….BABA YANGU NDIYE BABA YENU NA MUNGU WANGU NDIYE MUNGU WENU” nk. Mungu hakujitoa yeye mwenyewe ili atuoko, ila alimtoa mwanae wa Pekee( Yesu kristo) ili “kila amuaminie mwanae huyo”> basi asipotee bali awe na uzima wa milele, ndio maana, kulikiri, kulipa nafasi na kuliamini jina la mwana wa Mungu, ni muhimu mno!, soma(Yohana 3:16). Sio kosa kiinjili, kutamka kua Yesu ni Mungu, lakini ni Muhimu kufahamu mambo haya vizuri, ili tuijue nafasi ya Mungu katika roho wa mwanae, na mwana wa Mungu aliyekuja katika mwili ili kutukomboa “MUNGU NDANI YA KRISTO ALIYE DHIHIRISHWA KUPITIA MWILI WA MWANAE….hakujidhihirisha yeye mwenyewe kwa kua, yeye hana mwili wa kibinadamu. Ni muhimu kufahamu kua, Pamoja ya kwamba, Mwana alimfunua Baba, bado Baba ni wa Pekee katika roho na mwana ni wa pekee aliyekuja katika mwili ili kumfunua Baba yake, ndiyo maana, Yohana, akasema” WAKUJUE EWE MUNGU WA PEKEE NA YESU KRISTO ULIYEMTUMA > kujua hivyo, ndio uzima wa milele ndugu zangu katika bwana…chukueni maini hayo nimewalisha!!!!, Soma(Yohana 17:3). Tazama katika andiko hilo, ukiendelea chini yake,Bwana yesu anaweka waziwazi kwa kumwambia Baba yake hivi”MIMI NIMEKUTUKUZA DUNIANI, HALI NIMEIMALIZA KAZI ILE ULIONIPA NIIFANYE”….Hali hiyo, ndiyo inayomaanisha ” BABA ATUKUZWE NDANI YA MWANA….Sio Baba aje hapaduniani yeye mwenyewe, halafu eti ajitukuze yeye mwenyewe katika mwili wake, kwani ninyi mnaamini kua, Mungu” ANAMWILI WA KIBINADAMU?!!.Hebu nisaidieni ndugu zangu. Mungu alikua ndani ya kristo mwanae > akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake ili asituhesabie makosa, sio alikuja yeye mwenyewe katika mwili wake, kwa kua, Baba yetu hana mwili wa kibinadamu, ndio maana pia, kwa kile kielelezo cha Baba yetu wa imani ya Mungu, yaani Ibrahimu nae, kamwe hakujitoa yeye mwenyewe, isipokua, alimtoa mwanae wa pekee. Sisi wanadamu, tunaweza kutoa na hata kujitoa katika mwili, kwa ajili ya kuwatumikia wengine, kama kile kielelezo cha Bwana yesu alivyojitoa yeye mwenyewe katika mwili, lakini, kwa kua, Mungu ni mkuu kupita wote, na wa pekee, basi inakua, yeye “HAJITOI KWA WENGINE ILA ANATOA KWA AJILI YA WENGINE KWA FAIDA YAKE NA UTAKATIFU WAKE YEYE MWENYEWE, PIA, AAPI KWA AJILI YA MWENGINE ILA ANAAPA KWA NAFSI YAKE YEYE MWENYEWE, KWA AJILI YA UTAKATIFU WAKE MWENYEWE. Yale yote ya mwili, yaliyofunuliwa ni kwa ajili ya Mungu wetu, kutaka sisi tumjue mwana, ili na mwana nae atufundishe na kutufunulia, yale yote yatokayo kwa Baba yake…ndio maana biblia inasema” HAKUNA KUMJUA BABA MPAKA KWANZA MWANA UMUAMINI NA KUMJUA ILI NAE AKUFUNULIE. Sasa, wewe kama unajua mambo yote kwa ufasaha, lakini unakosa kumjua mwana na nafasi yake ktk mwili, huku ukifundisha kua, Baba ni mwana na mwana ni Baba yuleyule, ila anabadilika kama kinyonga, kwakeli, hebu tujifunze zaidi kipande hiki cha ufahamu, nafikiri kitamsaidia kila mwanafunzi wa Yesu kristo, kwa kua, hili ni tatizo la wakristo wengi kushindwa kuelewa vizuri. Nilazima tuweze kutafakari mambo ya mwili na roho kwa hali zake tofauti. Hivi viwili, kamwe haviwezi kwenda kwa pamoja, tena biblia inasema kua, vilianza kupingana tangu mwanzo. Kwa hiyo, nia ya mwili ni mauti pekee > mauti ya mwana wa Mungu pale msalabani…lakini, nia ya roho ni uzima”MUNGU ALIKUA NDANI YA KRISTO, AKIUPATANISHA ULIMWENGU NA NAFSI YAKE”.Hivyo, ukifundisha kua, Mungu alionekana katika mwili kabisa, basi utapingana na Biblia inayosema kua”HAKUNA MTU ALIYEMWONA MUNGU WAKATI WOWOTE, MWANA PEKEE ALIYE KATIKA KIFUA CHA BABA, HUYU NDIYE ALIYEMFUNUA (Mungu).Soma(Yoh1:18). Biblia iwazi yatuambia kua”sio kwamba mtu amemuona Mungu, ila Mungu mwana pekee (sifa ya uungu wake, soma(2Pet.1:3-4)…ndiye aliyemfunua Baba(kwa mwili wake kama mwana wa Mungu, sio mwili wa Mungu, Mungu hana mwili. Nisaidieni watumishi, Pingeni sasa hoja yangu hii, nawasubiri.

 26. Ndugu Lwembe,

  Mungu wangu akubariki.

  Nadhani unamfahamu Mungu wa Biblia, kiisha unauliza version ya huo Mungu !!!
  Lwembe, try to be serious na maneno unayoyasema. Sikutakie kuwa out of the mind.

  Kuna wakati ninapoanza kusoma Makala yako tu hapo kwa mwanzo nashindwa kuamua kama unastahili jibiwa au la. Lakini kwa unyenyekevu na hekima ninavyo najithahidi nikujibu angalau kwa machache.
  Ninachokuomba upya ni kwamba usipime pindisha hoja ya mwenzio. Mwanadamu kama wewe anastahili heshima.

  OK , wapi nilisema kama kuwa Imanueli ndio kuwa ndani ya hema jangwani? Nilikuambia, Lwembe, kama huwo Mungu ambae ali decide kuwa pamoja na watu akilitumia hema, ni yule yule alie decide kuuvaa mwili ili akae na watu akiwafanana kimwili. Hivi umeshindwa daka neno kama lile?

  Hebu kwa nini ulete maswali wakati ulilazimishwa kwanza kuweka wazi wewe version (nakunukuu) ya Mungu wako iliyo tofauti na Mungu wa Biblia?
  Pia unapopindisha hoja ya mwenzio na unajiruhusu kumuita mjinga badala ya kungoja wewe ndiwe uitwe vile au wewe mwenyewe ujiite vile.

  Unapopindisha maneno ya mwenzio usilalamike ukiitwa muongo.

  Nini imekukataza kusema wewe unawaza ni Mungu upi huko jangwani na upi Imanueli, Mungu pamoja nasi? Uko huru, usijione gerezani ili ubahatishe la kusema ukiwa na hofu.

  Mimi nasema Mungu ni Yule Yule akiwa na namna zake za kujionyesha(nilipoongea juu ya characteristics) kiisha unafika na usahihisho ukisema “Mungu huyo wa jangwani ALIPOKUWA Imanuel amesema wazi kwamba HAKUJA KUHUKUMU bali KUOKOA…”.

  Swali ni hili, ukisema vile unamaanisha ni yule yule Mungu ambae anabaki Mungu, au ni Mungu wako mwingine anaebadilika kwa umri na kugeuka Imanueli, au ni miungu miwili? Eleza tufahamu unachotaka watu waelewe lakini usiingilie matusi.

  Ukiendelea unasema “AKIISHA kumaliza kazi hiyo, amerudi ktk hali yake, ndio maana leo hii tunapaswa tuwe makini ktk tunayoyasema au kufundisha kuhusu Mungu, maana ni siku ya RM, hujawaona majeruhi wa kwanza Anania na mkewe?!”
  Ni nani aliemaliza kazi hizo? Ni Mungu ao ni mtu mwingine ? Eleza, tutakusikiliza kwa hamu !!!

  Ninapoingia deep kabisa ndani ya hoja yako naona unazungmuzia Mungu ALIYEKUWA na watu ndani ya jangwa, baadaye AKAWA Imanueli, kwa Mwisho AKAMALIZA kazi, AKARUDI katika utukufu wake.

  Kila anaekusoma ameona ni Mungu mmoja aliyefanya kazi nyingi kwa styles tofauti.

  Sasa kama unataka ujifunze fahamu kwamba si kwa bure Biblia inarudilia mara nyingi hizo kazi kwa majina. Ina maana katika ulimwengu wa roho hizo kazi zinafananishwa kwa lugha nyingine rahisi na mihuri inayo kila moja manufaa yake. Ndio maana Biblia inasema kuna watatu wanaoshuhudia mbinguni.

  Manager anaweza akawa na mihuri mingi inayofalia wafanyakazi kwa vitu tofauti , kwa mfano mhuri wa administration, wa kiganga, wa maonyesho, ….

  Usiwaze ukiwa na document inayo mhuri mmoja utaitumia kwa kazi isiyo yake.

  Ndio maana ukifahamu kama RM ndiye msaidizi, Mwalimu, ndie anayegawa uwezo wa kunena kwa lugha, … muite kwa jina lake. Ukifahamu kama Baba ndiye anapana mke mwema muite kwa jina lake. Ukifahama kama Mwana anaponya kwani kwa kupigwa kwake tumepona, muite kwa jina lake.

  Mungu atakufurahia ukilitumia Neno lake jinsi ipasavyo. Lakini ukisema Baba hayupo, Mwana hayupo na RM hayupo licha ya kuwa Neno la Mungu linakushurtisha kutambua huo ukweli, au ukiwaita miungu(yaani Mungu 3), hakikisha humfurahishe Mungu kwani hutimize maandiko.

  Kwa mwisho unasema « Najua haya yatakupa shida kutokana na kushikilia kwako dhana Ngumu isiyoeleweka, kama tu ya Utatu, licha ya kuzikimbia kwako “Nafsi”, naona ndio umezidi kujichanganya. Ngoja tuitazame vizuri hiyo version yako ya “Mungu” huenda tukalipata jibu, hapo tutakapo “telemsha maneno ya Mungu”! »

  Sina tatizo lolote. Anaejithahidi adanganye kama wewe ndiye analo tatizo. Wapi nimekimbilia “Nafsi” wakati nasema kwa sauti kubwa kama tamko kama “nafsi tatu” siyo lugha ya biblia na nikasema wazi kama naikataa? Hebu niambie kama na wewe unaikataa kama mimi! Ikiwa hivyo you’re welcome na huna hoja ingine..

  God bless you!

 27. Ndugu John,

  Ninaanza nukikuombea baraka nyingi kwa Mwenyezi Mungu.
  Kwa swali langu hukuleta jibu. Sikushutumu kwa lolote kwani mimi mwenyewe nimeweka comments kiwango niliongea kuhusu IQ. Haimaanishe kama nilisema kwa uhakika, lakini nilikuwa nikitafuta jibu kutoka kwako. Kwani nilipenda nifahamu umri wako, experince unayo ndani ya mijadala na ndani ya uchambuzi wa Neno la Mungu. Pia hukulazimishwa leta jibu. Jibu lako lazma lithamathishe au lisahihishe niliyoyasema kuhusu IQ. Lakini hukulazimishwa, ndio maana nimeona umekuwa na hekima kwa hiyo ni wajibu wangu kukupongeza.
  Unasema unapenda ujifunze. Naomba usikuwe umesema kama mzaha kwani nina uhakika watu wengi wamejifunza kutoka kwangu, nami naendelea kujifunza kutoka kila makala ya wengine.

  Kuna rulers nzuri za kujiweka sawasawa ndani ya mijadala :
  -do not think mjadala is rahisi.
  -tegemea sana Biblia hata kama hutaandika shairi kwani fahamu watu watakuuliza tu.
  -kabla hujaandika pendelea sana development za ideas kuliko kutelemsha wino. Wanaotelemsha wino wanalemea hii blog kwa bure. Wala usiwe na mashaka, kuna wachangiaji wengi waliobadili style yao kwani wamepokea mafunzo. Na wengine kama waislamu katika ule mjadala wa “ukristo//uislamu” wamenyamazishwa kwa kushindwa ndani ya imani yao mbovu. Wale wote nawashukuru kwani ni heri kuupokea ukweli kuliko kujiangamiza mwenyewe.
  -Kwa hiyo ukitaka jadili kirahisi na mtu, mlete polepole hadi anapojiweka kwenye focus moja kwani wengi wanajifanya wajanja kwa kuweka chungu moja nyama na samaki ili kwa wino yao nyingi waonekane wameshindana.
  -Usishikilie mjadala kama uwanja wa mapambano, ni uwanja wa ukweli tu. Kwani mapambano hayajali ukweli bali yanajali ushabik.
  -Ukiitaka telemsha wino hakikisha mna ideas nyingi kuliko mchoro.
  – Ukitaka simamisha neno nzito uwe umefikiri kila kona ya swali. Ukiona utakwama kwa swali fulani usiandike au uwe tayari kuomba masamaha kwani kila mwanaadamu ni dhaifu.
  -Usikurupukie shairi fulani pasipo uhakika wa mantiki yake na uhusiano na shairi nyingine katika hiyo Biblia.
  -Usidhani Biblia ni lugha yako. Ni lugha ya RM licha ya kuwa imetafsiriwa kwa lugha zetu.
  -ukisoma shairi tafakari juu ya muandishi, kwani mwenye maarifa ya mithali si kama muinjilisti, si kama nabii wa agano la kale, si kama mtume, si kama mfalme.
  -Nakuruhusu na wewe endelea……

  Halafu kuhusu maneno “roho”, “nafsi”na « moyo », nayikurudishia uijifunze polepole, ukipata swali moja kwa moja uniulize siyo kwani niko na maarifa inayozidi lakini kwani nimezoea kuingilia mambo kindani. Ni maneno yanayotumiwa sawasawa kwa versions na shairi fulani lakini yakitofautishwa nafasi ingine. Mfalme anaweza kuwa ameandika moyo kumbe analenga nafsi. Nabii anaweza andika nafsi wakati analenga roho, nk… Ni kazi yetu kupambanua significations kufwatana na mantiki iliyo ndani ya shairi pasipo kusahau kuomba RM atufundishe zaidi. Ninachokutakia ni kudaka kwanza the basic meaning kwani upazifikia mantiki zote unaweza jidanganya kama roho, nafsi na moyo ni neno moja. Nikupe mfano fulani ma neno kama matrix kiisha uitafute ndani ya dictionary ya Maths, Biology, Computer, Printing, ….
  Ukiona ni tofauti, fahamu kama watumishi wa Mungu wana RM mmoja lakini upako tofauti na ufahamu tofauti. Ni kazi yetu kusoma vizuri wala siyo kazi yao kurudia kusema eti mimi nilisema kwa mithali lakini kwa lugha kawaida siyo moyo bali ni nafsi.

  Kuhusu mada hii mim nawashangaa wote wanaosema ni rahisi wakifahamu kama Makuhani, Manabii, Mitume, Wafalme, …. Wameshindwa kuweka wazi ujuzi wa kumuelewa Mungu kwa jinsi iliyo ya akili za binadamu. Ninawaalika kusoma makala yangu licha ya kuwa yanaweza kuwa hayaeleweki kirahisi, lakini ukweli uko humohumo. Dada Janeth naye asilete swali akishabikia jibu analodhania. Atulie asome ili apate elimu ya Neno la Mungu.

  Asante Ndugu yangu, niko na wewe, pale tu pembeni yako. Nawe uwasalimu ambao sikuweza salimia.

  God bless you.

 28. Pendael,
  Majibu yako haya hapa:

  Ukristo ni ufuasi wa Kristo au uanafunzi wa Kristo.

  Udhehebu ni mfumo wenye msimamo wa kufuata liturujia ya kundi fulani la imani, ambao aghalab ni tofauti na kundi jingine la imani.

  Sasa karibu tuendelee!

 29. Ndg Ziragora,

  Asante kwa majibu, umenisogeza ktk hatua! Kama nilivyokuambia, nina shauku ya kuijua version yako ya huyo Mungu, ni nani? Maana ktk kila hali, jambo tunalolitazama hapa ni la muhimu saaana, kwani linahusu Ibada; basi kumjua unayemuabudu ni zaidi ya kuabudu!!

  Kabla hatujaendelea napenda tuyarejee machache ili tuwekane sawa. Kuna mambo madogo madogo ambayo tulipaswa tuwe tumejifunza huko Sunday school utotoni kwetu, ambayo si haki kuanza kuyajadili leo hii mithiri ya watu tuliotokea ktk upagani! Sote tunafahamu kwamba Mungu hakuwahi kujifunua huko jangwani kama Imanueli, kwahiyo unapojitoa ufahamu na kulazimisha kwamba kwa kusema kwake, “Nao na wanifanyie patakatifu; ili nipate kukaa kati yao” Kut 25:8, basi kwa kukaa kwake kati yao alikuwa ndiye Imanueli, huku ni kumfanya Mungu kuwa Muongo, jambo ambalo ni hatari licha ya kufanywa ktk ujinga!

  Nasema ni ujinga kwa sababu licha ya kwamba Mungu ni mmoja, lakini amekuwa akijifunua ktk namna tofauti kulingana na jambo analolifanya, nasi tunapaswa tumfahamu na kumrejea hivyo. “Kukaa kati yao” na kuwa “Pamoja nasi” ni mambo mawili tofauti; la kwanza ilikuwa ni Uwepo wake ndani ya ile Hema, kwa sababu Yeye alibaki ktk hali yake ya Roho; lakini alipokuwa Imanueli ni pale alipofanyika mwili: Yn 1:14 “Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake…” Hakuna aliyewahi ku shake hands with God in the desert, kama ilivyokuwa of the same God when He was Emmanuel!!!

  Nilikuambia huko jangwani Mungu alikuwa ni Baba, Kut 4:22 ” Nawe umwambie Farao, BWANA asema hivi, Israeli ni mwanangu mimi, mzaliwa wa kwanza wangu”; nako kumkufuru kulikupelekea kuuawa, ndivyo ilivyokuwa.

  Mungu huyo huyo alipokuwa ni Imanueli; ni lazima kwanza ufahamu alikuwa anafanya nini, ndipo utajua ni kwanini aliwasamehe waliomkufuru, kama hulijui hilo ndio utaishia kubisha na kubaki ukishikilia mambo yasiyo na faida yoyote kiUngu! Alipokuwa Imanuel amesema wazi kwamba HAKUJA KUHUKUMU bali KUOKOA; ndio sababu alimwambia yule mwanamke mzinzi kwamba nami SIKUHUKUMU; Yeye HAJAWAHI kumuua mtu yeyote yule, Yeye alikuwa ni Mwana-Kondoo!!!!

  Akiisha kumaliza kazi hiyo, amerudi ktk hali yake, ndio maana leo hii tunapaswa tuwe makini ktk tunayoyasema au kufundisha kuhusu Mungu, maana ni siku ya RM, hujawaona majeruhi wa kwanza Anania na mkewe?!

  Najua haya yatakupa shida kutokana na kushikilia kwako dhana Ngumu isiyoeleweka, kama tu ya Utatu, licha ya kuzikimbia kwako “Nafsi”, naona ndio umezidi kujichanganya. Ngoja tuitazame vizuri hiyo version yako ya “Mungu” huenda tukalipata jibu, hapo tutakapo “telemsha maneno ya Mungu”!

  Gbu, my brother in Christ!

 30. Mkuu Alphonse Ziragora…..

  Naona umeongeza ID ya pili…Hongera!

  Pole kwa yote…..Mimi kushindwa kuandika unavyotaka au kukupendeza wewe,
  ndio uhalisia.

  Awali niliomba ridhaa kuwa niko nje ya mada,
  kwa kujibu swali la 3 la Millinga kuna aina ngapi za moyo..

  Sikutumia andiko la Mhubiri…..kuelezea moyo wa upumbavu na hekima..

  Nimelitazama hilo andiko….kumbe mioyo ipo inayokaa upande wa kuume
  na mkono wa kushoto..

  1Fal 3.12d
  “nimekupa moyo wa hekima na wa akili”

  Ni kweli akili zangu zimewekwa na si nimeweka ktk moyo….

  Moyo ndipo kwenye uhai…………….. nafsi/roho zinaketi hapo..

  Nakubaliana nawe 100% uelewa wa maandiko tumetofautina…

  Ni tayari kujifunza toka kwako………. nifundishe…IQ zangu labda zitapanda.

  Amani ya Bwana Yesu iwe nawe

  Wasalimie pande za huko

  Mjoli Haule

 31. John,

  Naomba ujibu kwa swali hili: “una AKILI za kitoto” au “unakabiliwa na ujinga”?

  Kuna swali ambazo ni za kupima IQ. Sasa IQ yako ni chini sana. Nakushangaa kwa kujitoa mhanga ili ujadili kabla hujakuwa.

  Kwanza unaanza ukiomba huruma. Ni ya nini? Nimekudai tu ulete jibu kama mtu aliesikia zaidi. Hukulazimishwa kusema Kabila zilizo ndani ya kanisa lako.

  Hivi utoto wako unakuambia. watanzania wote wana lugha moja ya kizalikio kabla hujawataja hawo wandungu wote Wa taïfa mbalimbali?
  Au uko mtoto kiwango hujaona mtaalam Wa lugha isiyo ya kwake?
  Niko ili niwafunze ee ninyi watoto! Mtu mzima hawezi omba msamaha ili ndipo aanze kosa lake.

  Kabla hujajibu soma vizuri hoja. Unapojibu swali la kwanza hakikisha hujibu la pili ndani ya lile la kwanza.

  Ukijibu juu ya moyo usishambulie nafsi kama nayo ni swali ingine. Ndio maana unaandika mingi iliyo empty.

  Unapoulizwa kitu kiko wapi huulizwe kikoje? Jaribu kuwa mtu mzima!

  Akili zako unaziweka moyoni ndiyo maana zinatumika nyuma ya wakati. Pia unasikia uombe masamaha na bado hujakosa ndipo ujiruhusu kukosa kwani moyo wako(feeling) ndiyo inakuongoza. Biblia ina lugha ambayo si ya kukurupukiwa kirahisi. Uwe ukichukuwa mda upime tia AKILI zako ndani ya ubongo ndipo nafsi yako ipate afya.

  Akili na hekima ni tofauti sana. Mtu anaweza akawa na hekima akiwa na akili kidogo. Pia mtu anaweza kuwa na akili nyingi pasipo hekima.

  Hii fact ya kuviweka nafasi moja ndio inapunguza IQ yako.

  Unasema mtu ana mioyo miwili mmoja Wa upumbavu ulio upande wa kuume na wa hekima ulio upande wa kushoto. Sasa huyu mtu anayo mioyo miwili tutamuita mpumbavu au mwenye hekima?

  Huone kama unapoweka AKILI zako ndani ya moyo inakufanya kuwa mpumbavu?

  John, naona hujaelewa lugha ya Biblia na sasa unaanza isingizia kwa kuisoma vibaya. Suleiman alitofautisha watu wawili: alie na hekima akaona AKILI zake hazipo ndani ya moyo Wa nyama na alie kama wewe anaziweka moyoni ill ziongozwe na hisia.

  Mungu akujalie neema.

 32. Ziragora
  Unisamehe kama umekwazika,kwa kweli sikuwa nazungumzia kuhusu lugha,Nilifurahiswa na majibu yako yalikuwa sahihi kwa sehemu lakini ayakumsaidia mtu aliyetaka kuelewa kwa majibu ya maswali yale kiroho aliyouliza Ndg Millinga.

  Nikupashe habari kidogo mahali ninapoabudu mimi kuna watu wa mataifa mbalimbali ktk hiyo kanisa (nyumba sala)wanaofanya kazi hapa DSM.

  kumekuweo wacongo,wanyarwanda,rundi,malawi,zimbambwe,msumbiji,kenya,uganda nk na wote wanaweza kuongea kiswahili kwa lafudhi ya lugha za mama zao kati ya hao wengine ni wazee wa kanisa hata mmoja alifikia kuwa mchungaji ila kwa sasa shirika lake limemuamisha yupo cape town.kwa hiyo siko na shida na lugha yako.niko na hawa ndugu ktk Bwana kwa muda mrefu.

  Kwa mfano angalia ulivyojibu swali la 3

  Millinga
  3. Moyo ni nini na unakaa wapi mwilini? Na Kuna mioyo aina ngapi?

  Jibu lako Ziragora:
  Ndani ya mwili. Ndiyo inasambaza damu mwilini.

  Hili ni moja la jibu lililonifutahisha…ndiposa nilipokumbuka zile methali za swahili kwa wahindi.

  Kwa kuwa ulikuwa unanigoja sawa na wito wako kwa nafasi hii ngoja nijibu hili swali la tatu la ndugu Millinga.Wapendwa mtanisamehe kwa kuwa nje ya mada husika.

  Binadamu ana mioyo kwa uchache miwili
  1. moyo huu wa nyama ambao Ziragora amaongelea ,unaoendesha mzunguko wa damu ktk mwili kama ogani.

  2.Moyo ni mahali ambapo maamuzi yote ya binadamu utoka,maamuzi haya yanazalisha kuona,kusikia,kuhisi,kunusa,kuonja ,wema uovu ,kuamini ni pahala pa utu nk
  Moyo huu tofauti na ule wa nyama huu una masikio,macho, mdomo,mawazo,hisia,chuki,upendo,unainama ,unaburudika,unadanganyika,unadanganya,huzunika,unaambatana ,shauku,unazimia,uchungu,ugumu,unyenyekevu,mzito,hiyari ,unakufa ,unakengeuka ,yeyuka,unalia ,unatetema,potoka ,ushujaa ,hofu,woga,haja ,unaumia nk
  Ni pahala pa Nafsi/roho ndio uhai ulipo pakifa hapa na mtu huyu atakuwa amekufa kiroho au kimwil

  majaribu yanakuja kwanza moyoni

  Mdomo wa moyo ndio unaongea sana kuliko mdomo huu tunalia chakula,masiko ya moyo yanasika masauti/maneno mengi kuliko masikio ya mwili

  unaweza ukafurahi ktk uso bali ktk moyo umechukia,
  mtu mwenye furaha ya kweli ni yule aliyefurahi ktk moyo(kama furaha walio nayo waliompata Yesu Kristo)

  Akili /hekima zinakaa moyoni na sio ktk ubongo

  Moyo unavaa….unaweza ukavika moyo wako vazi laana,umaskini,ukahaba,hofu,ujasiri,huzuni,furaha,hasira,chuki,husuda,amani nk

  unaweza sema unampenda mtu/kitu lakini moyo wako haupo huko ,upo kwingine

  Mungu pekee ndiye anauwezo wa kuwabilisha watu mioyo

  Hata Bwana akiongea nasi tunasikia kwenye masikio haya ya moyoni na sio masiko ya mwili ,

  Maneno yanakaa moyoni

  Hata wapumbavu wanasema moyoni hakuana Mungu

  Linda moyo wako
  Heri wenye moyo safi
  moyo ni mdanganyifu
  mpende Mungu wako kwa moyo wako wote
  moyo wako ulipo ndipo hazina yako ilipo
  maandalio ya moyo ni ya mwadamu
  Mna hila nyingi moyoni pa mtu
  ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto

  Labda unataka kujua hii mioyo miwili inakaa wapi kwa mtu(binadamu)

  Mhu 10:2…………sulemani anaonyesha mioyo yote mieili aliyonayo binadamu inapokaa…

  ” Moyo wake mwenye hekima upo upande wa kuume; Bali moyo wake mpumbavu upo mkono wa kushoto”.

  Huu ndio mioyo halisi ya mtu

  Bro ZIragora tupo pamoya

  Mjoli Haule

 33. Ndugu Lwembe,

  Nashukuru kwa makala yako.

  1) Unauliza swali ambalo halilingane na personality yako. “Mtu” is different from “utu” as person is not personality. Mtu ana utu lakini utu huna mtu.

  2) Nilipotia mwili Lwembe, nilikuwa naitofautisha na mwili wa mtu mwengine.

  3) Niliposema tuyaongelee maneno ya Biblia sikusema hatutaweka maneno yetu au kama tutafanya copy-paste maneno ya Biblia tu. Nafikiri ulisoma niliposema maneno yetu iwekwe katika comments. Nikitaka nikufahamishe maneno ni lazma niweke lugha yangu lakini isiwe ndiyo kiini cha mada.
  Unayoniuliza iko ndani ya Biblia kwa lugha ya Biblia na katika shairi nyingi, ndio maana sikupenda niandike kitabu at once.Kwa mfano “Unapoona maandiko kama ‘Mungu akasema”, hapo ni Mwana’ “. Mwana ndilo Neno. Huwezisema kama hutumie neno. Ukisoma Injili ya Yohana 1 utapata uhakikisho kwamba Yesu(Mwana) ni Neno.
  Nimerudilia tu hii moja kuthibitisha kama niliyoyasema, licha ya kuwa nilifanya summary ya shairi nyingi, ni maneno ya Biblia wala si yangu au mtu fulani ambae simfahamu. Huwezi linganisha kwa mfano hili jambo na anaesema “utatu” pasipo kufahamu ule utatu, wapi ameupata, nani alieleta hilo tamko, pia kuugeuza uwe mada halisi.

  4)Nashukuru kwani naona unapima kwenda deep, Mungu aendelee kukuwezesha. Umegundua bila shaka kama neno “karakteristiks” ni yangu wala siyo ya Biblia. Kwa lugha ingine ni namna Mungu anavyojionyesha kwetu. Kiroho hizo namna, Biblia inazipatia nafasi sana ndani ya ulimwengu wa Neno la Mungu kwani zimeandikwa sana ndani ya Biblia. Plz, sishurtishwe kurudilia definitions zako kwani dictionaries zote hazilingane.

  Nimekujibu kaka, kama una swali njoo ujifunze zaidi ili uelewe ninachokisema. Pia telemsha maneno ya Mungu kuelewesha wasomaji.

  God bless you!

 34. Ndg Ziragora,

  Kwanza nikushukuru kwa maelezo yako mapya, very interesting!

  Unasema, “Nafsi” siyo “mtu” bali “utu”; ungenipa na tofauti ya “mtu” na “utu” ingesaidia sana, labda nikusubiri ktk hili

  Pia unasema, Lwembe= mwili Lwembe + nafsi Lwembe+roho Lwembe; na kutoka mfano huu ndio unatamatisha kwamba, Baba+Mwana+RM= Mungu, na kwamba Mungu ni Mmoja!

  Hili suala la Lwembe, yaani mtu, (au ni Binadamu?) kuwa ni : mwili + nafsi +roho ninaamini Maandiko yake ni haya: 1The 5:23 “Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi NAFSI zenu na ROHO zenu na MIILI yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama …”

  Sasa hapa kuna jambo jingine linalojitokeza, hili la 1The 5:23 ambalo tukisema tulichunguze zaidi, ili liwe msingi wa kutuelimisha kuhusu Mungu, tutatoka nje ya mada na itakuwa si rahisi kurudi tena na kuukamilisha ufahamu wetu.

  Kwahiyo, ninalichukua jambo hili la Lwembe= mwili Lwembe + nafsi Lwembe+roho Lwembe; ambavyo ule mfano wako ungeuiana vizuri kama na kwa upande wa Mungu nako ungesema: Baba Mungu+Mwana Mungu+RM Mungu= Mungu; Tofauti na hilo basi kwa upande wa Lwembe inapaswa iwe:
  Lwembe= mwili wa Lwembe + nafsi ya Lwembe +roho ya Lwembe au ktk urahisi ni: Lwembe= mwili + nafsi +roho kama Biblia inavyolionesha!
  Ktk haya, nichagulie ni kipi kinacho reflect tafakari yako!

  Halafu umeniambia, “”Pia nilieleza kama tukiendelea kuongelea maneno kama isivyoandikwa ndani ya Biblia ni utani mno””, hata mimi hili limenifurahisha sana maana linarahisisha majadiliano hata kufikia tamati yenye Baraka! Basi nakuomba unioneshe sehemu ulipoyasoma haya:
  “””-Unaposoma «Mungu akasema, Mtetezi, …», fahamu kama Neno limetumika, hapo ni caracteristic inayoitwa Mwana.
  -Unaposoma « Mungu akijitokeza, akafinyaga udongo, … », fahamu kwamba nguvu zimetumiwa, na hapo ni caracteristic inayoitwa Baba.
  -Unaposoma Mungu kama Msaidizi, Mwalimu, …. Pamoja na kusema kama Mungu ni Roho, Kama kuna Roho saba, Utakatifu,….., hapo ni caracteristic inayoitwa RM.”””

  Pia haya maelezo yako umeniambia ndio CHARACTERISTICS za Mungu,
  “””Ndivyo Mungu anazitumia caracteristics zake. Nataka nikukumbushe kama siyo nafsi tatu au watu watatu kama ulivyojaribu kupindisha maandiko.”””
  Ngoja nikuwekee hapa tafsiri ya hilo neno ili ulinganishe na hayo maelezo yako kama ndicho ulichomaanisha:
  CHARACTERISTIC: a feature or quality belonging typically to a person, place, or thing and serving to identify them: Distinctive, distinguishing, particular, special, individual, specific, singular, unique, exclusive –
  Kiswahili ni : SIFA BAINIFU

  Hebu niweke sawa kwanza ktk mambo haya, ili usiniache nyuma!

  Gbu!

 35. Simon,

  Umeona kama yale mambo uliyofichwa yamefichuliwa wengine? Good!!! Kaa chini sasa ujifunze. Hivi huwezi jiuliza kwa nini huelewi Neno la Mungu lakini unaelewa tu maneno ya wanadamu? Hiyo udhaifu ndiyo tunataka isionekane tena. Chukua mda ujifunze, wala usishangae ukiwaona wanafunzi ndo wengi. Ni kawaida kabisa wakufunzi wawe wachache. Usiporomokee tu njia pana kwani umepaona watu wengi. Wanahitaji wanyonye ndipo wakuwe. Karibu tena kwa mazungumzo ndipo upewe maarifa. Mungu anakupenda sana.

  God bless you my friend.

 36. Simon

  Usiogope shule. Unapopungukiwa ujuzi Wa Neno la Mungu kaa kimya ujifunze. Usidhani ufahamu hutoki kwa Mungu kwani kuukosa ndiyo kuangamia. Pia usidhani shule la RM ni mchezo. Ondoa ndani ya ubongo wako kama Mungu anajifunzwa kirahisi. Chukua hâta miaka tatu kama wa kina Petro ukijithahidi kulielewa Neno. Wala usishangae kuona kama kuko wanafunzi wengi ambao hawajaelewa. Hiyo ni kawaida ya kuwa wakufunzi ndiwo wawe wachache. Pia usijali na utulie ndipo utapata maarifa. Utaanza jishangaa mwenyewe.

  Asante

 37. Wapendwa,

  Hoja ya Ndugu Lwembe na hii mada ya Dada Janeth inanisisimua niwaambie wote yafwatayo:

  -Mimi sihitaji nieleweki kirahisi katika hii mada,
  -Kwani nikieleweka nitakuwa nimejipanga sawasawa au la kwa upande wa utatu na nafsi tatu.
  -Ni maneno ambayo hayapo ndani ya lugha ya Biblia,
  -Hivi ukijipanga huku au kule unajipanga tu bila kufahammu kwa nini wewe ni pale ulipo,
  -Utaupigania utatu wakati hujue alietamka lile neno alihisi nini,
  -Utaupinga wakati vile vile huna ufahamu juu na hiyo neno,
  -Utajimenyamenya ili uthibitishe kuna nafsi tatu wakati hujue hata kama nafsi ni nini na kuwa tatu ni nini.
  -Ndio maana mwenye mada akaileta licha ya kuwa ni msomaji wa Biblia,
  -Alikwamia kwa zile tamko za wanaadamu ambazo zinaonekana kuwa rahisi kusikia lakini kumbe zinaongea mambo ambayo si ya kibiblia.
  -Ukibaki ndani ya Lugha ya Biblia ndipo utapata jibu halisi,
  -kwani utakuwa umeondoa vocabularies za kibinadamu ili nuru ionekane.
  -Kwa hiyo, anaesema utatu ni sahihi na anaesema siyo sahihi hawajatofautiana kabla hawajaweka wazi kama ile utatu ni nini na alieisema wa kwanza alikuwa anahisi nini.
  -Inategemea ulisikiaje hiyo utatu na nafsi.
  -Iwepo umesikia vibaya utakamata uamzi ambao hufae kwako na kwa wengine, ndiyo inayoitwa “kuangamia kwa kukosa ufahamu”
  -Ndo maana mimi naenenda tu na maneno jinsi Biblia inayasema, licha ya kuwa nafahamu kuyasikiya siyo rahisi.
  -Nisikilike kirahisi au la ya muhimi ni kuheshimu Scriptures.
  -Kwa mwisho, kiukweli Mungu ni mmoja, pia utatu ni lugha ya wanaadamu. Ningelipenda washabik wa utatu na wasio shabik wa utatu watuambie “utatu” ni nini na waliifunzwa wapi. Pia watuambia walipata elimu ya nafsi tatu ndani ya Mungu wapi.

  Asante.

 38. Ndugu Lwembe,

  Nimekupata vizuri sana. Wewe unawaza swala tunalolizungmuzia ni rahisi mno na ni kila mtu ambae anaweza lifahamu.
  Unapoanza unasema « nafsi » ni « mtu ». Ukiisema tu kirahisi hivi pengine utaeleweka na baadhi ya watu wengi wanaodhani swala linaloitwa « utatu » kwa lugha ya binaadamu ni jambo rahisi. Lakini fahamu kama « nafsi » siyo « mtu » bali « utu ». Pia nilieleza kama tukiendelea kuongelea maneno kama isivyoandikwa ndani ya Biblia ni utani mno. Ndio maana nikasema mapema kama maneno « utatu » na «nafsi tatu » siyo lugha ya Biblia. Lwembe, nilikuonyesha sawasawa kama Lwembe= mwili Lwembe + nafsi Lwembe+roho Lwembe. Pengine ungeliniuliza, mbona wewe una sehemu tatu, zinashirikianaje ? Na kusudi zishirikiane zinalazimishwa kuwa nafsi ?
  Nazikataa tamko zozote ambazo sizo za kibiblia kwani pale ndipo wengi wanakwamia. Zitumiwe kama comments wala si kama hoja. Hata Dada Janeth aliyeweka mada hakujaribu kuandika nafsi tatu wala utatu. Lwembe, utamfanya Mungu ana nafsi, pia hizo nafsi uziite watu, hebu niambie kabisa utakuwa uko na Mungu gani?
  Kuwa Mungu ni divinity ndo maana humuelewi ukitumia lugha kawaida kama jinsi unavyodani. Itumie lugha ya Biblia ndipo utamfahamu. Akiwa divinity ndipo inaeleweka kama yeye ni Baba+Mwana+Roho. Kwa Lugha nyingine ni “Baba U Mwana U Roho”.Sijue unaelewa ninachosema? Biblia haiwezi tuonyesha uwepo wa Baba kwa idadi isiyopungua 200 kama hayupo. Hali kadhalika Mwana na RM. Jithahidi kusikia inayozungumziwa ndani ya Biblia kuliko kutafuta chini juu kukwepa ao kugeuza maandiko.

  Biblia inapozungumza kama Mungu ni mmoja, basi!!!! Na kama inazungumza kama katika huwo Mungu mmoja mna Baba, Mwana, na RM, huwezi sahihisha. Jithahidi tu usikie.

  Unaniomba nikufunze kwa upya kama Baba, Mwana na RM wanauhusiano gani ? Kwanza usiwaite nafsi. Pia usidhani ni watu kama Lwembe, Ziragora, …. Ni caracteritics za Mungu. Lwembe nilikuambia hivi :
  -Unaposoma « Mungu akasema , Mtetezi, …», fahamu kama Neno limetumika, hapo ni caracteristic inayoitwa Mwana.
  -Unaposoma « Mungu akijitokeza, akafinyaga udongo, … », fahamu kwamba nguvu zimetumiwa, na hapo ni caracteristic inayoitwa Baba.
  -Unaposoma Mungu kama Msaidizi, Mwalimu, …. Pamoja na kusema kama Mungu ni Roho, Kama kuna Roho saba, Utakatifu,….., hapo ni caracteristic inayoitwa RM.
  Ndivyo Mungu anazitumia caracteristics zake. Nataka nikukumbushe kama siyo nafsi tatu au watu watatu kama ulivyojaribu kupindisha maandiko.
  Na iwepo utazingatia urahisi wa hili swala utaona tu kama unakwama. Go deep my friend!!!

  Lwembe, ile literature pale uliposema kumkufuru, Imanuel, RM unajichanganya sana. Mungu akiwa mmoja hagawanyike. Yule yule aliyesema “mnifanyie hema nikae pamoja nanyi” huko ndani ya jangwa ni yule yule Imanuel(Mungu pamoja nasi), pia ni Yule yule ambae huna ruhusa ya kumkufuru, yaani RM.

  Sikiliza Lwembe, Yesu katika mwili aliitwa sana mwana wa Daudi, pia mwana wa watu. Aliposhutumia kwa hiyo namna ya mwana wa mtu, waliyokwama walikuwa wakilenga mtu maana mwana wa Daudi, ndio maana haikuwa makufuru. Lakini akaleta angalisho inayolenga kile kilicho ndani yake yaani RM kama yeye ukimkufuru huna msamaha. Lwembe endelea strictly deep again!

  Kusema “Umoja “ ni shairi ya Biblia inayosema wala siyo Ziragora. Sasa kuisema sikulenga utatu kama jinsi unavyojidanganya, kwani umoja siyo utatu. Nilipokuwa nikimjibu mpendwa Simon, nilisema wazi kama ni tafsiri, na kwa sababu mimi siyo mtu juu juu nilienda deep kabisa, nikaonyesha kama alietafsiri kigiriki katika Kiswahili hakukosea kwani “mmoja”=”oneness”=”moja”. Hence, unapofika ambapo husikie vizuri, tulia ukaulize versions za Biblia katika lugha nyingine, dictionaries, …. Ili ukuwe. Usipendelea kubaki bila ufahamu kaka!

  Lwembe, usipime leta ujanja ndani ya mada. ELOHIM ni Mungu na siyo Kiswahili, ni kiebrania. Nimekuonyesha jinsi waebrania walionyesha tayari katika lugha yao Mungu in plural. Unachotakiwa kama unataka zidisha ubishi ni kukiingilia kiebrania wala siyo Kiswahili. Kwani nikiingia katika uchambuzi wa wale Ibrahim aliowaona itakuwa ni ingine mada. Ona jinsi unavyojisumbua sana ukilinganisha viumbe vya Mungu na Mungu mwenyewe. Malaika, waitwe Bwana au la wanabaki tu viumbe vya Mungu.

  Miti miwili ni kibiblia kabisa, ya « kujua mema na mabaya » na ya « uzima ». Tatizo lako nililitatua zamani nikisema kinachoaminika ni kwamba yote haikutakiwa moja baada ya ingine. Kama moja ilikatazwa na ingine ikazuizwa siyo tatizo. Ya muhimu ni kuutazama huo ukweli kama ndani ya shamba moja kulikuwa mti wa kujua mema na mabaya na mwingine wa umilele. Na kama unakubali sijue unajihangaisha tena kwa nini. Lakini mna siri ambayo ilionekana ulifahamu.

  Usijionyeshe dhaifu kiwango hicho ili ulazimishwe kuomba msaada kwa Dickon. Hatupo katika mapambano. Unachotakiwa ni kuonyesha msimamo wako na kuuambatanisha na Neno la Mungu. Unaposhindwa, hakikisha koze yako haipo.

  God bless you !

 39. Ndugu Simon,

  Unayokana ndiyo unathibitisha. Angalia jinsi unajadili ukisema “TANGU LINI MKRISTO AKAWA “THEOLOGIAN”?”. Unaungaunga sana maneno na unajifanya kama hukusikia hoja kama tu politicians wengi wanayoyafanya.Kwa nini unaunganisha mkristo na theologian? Unapoambiwa wewe siyo mukristo wala theologian ina maana huko mukristo na huko theologian. Kuiambatainsha ni njama za kukwepa tu.
  Mengine uliyoandika ni hisia zako wala huko katika mada. RM hupatikana ndani ya Neno la Mungu wala si katika maneno ya mtu binafsi. Kigezo ni kimoja tu, kusema sawa Neno la Bwana linavyoagiza kusema. Huwezi kuwa na RM kiisha ukwepe ukweli wa Neno la Mungu kama jinsi unavyofanya.

  Mungu akuwezeshe.

 40. Bwana Sungura;
  Kabla sijakujibu baadhi ya maswali yako,naomba uniambie tofauti kati ya UKRISTO na UDHEHEBU.
  Ahsante.

 41. Dada Janeth,

  Kuhusu maswali uliyoyauliza, sehemu ya kwanza ya swali lako, majibu yake kwa sehemu kubwa yamekuja ktk Fumbo Kuu la Utatu Mtakatifu, ambavyo bado ninaamini kwamba hata hayo majibu yenyewe yangali ni Fumbo!

  Nasema ni Fumbo kutokana na kauli za wachangiaji wenyewe, kwamba wanatangaza kwamba hili ni fumbo gumu kueleweka kwa akili za kibinadamu, halafu mbele kidogo wanalielezea vizuri sana, kiasi hata aliye mjinga anawaelewa, lakini mwisho tena watakuambia kuwa hilo ni gumu sana kueleweka kwa akili za kawaida! Ndipo hilo linaashiria kwamba walianza kibinadamu halafu yule roho anayelisimamia Fundisho hilo akachukuwa mamlaka, ndiyo haya maelezo mazuri aliyoyaleta, ambayo ukirudi ktk ubinadamu huwezi kuyaelewa tena mithili ya mtu aliyepandisha mapepo!!

  Kilichofunuliwa hakiwezi kuendelea kuwa Siri, ukiona huyo anayekwambia kimefunuliwa, halafu anakirejesha ktk Usiri tena, basi jua kwamba kuna hitilafu!

  Basi, nami napenda nijaribu kuijibu hiyo sehemu ya kwanza ya swali lako, kama ulivyoliuliza, huenda na Fumbo Kuu la Utatu likafumbuka pia kwa kadiri tutakavyo yatazama yanayojiri kuhusu hizo Nafsi Tatu.

  YESU NI NANI:
  1. Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu aliye hai.
  Mt 26:63 ” Kuhani Mkuu akamwambia, Nakuapisha kwa Mungu aliye hai, utuambie kama wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu.”

  Bali tunapoendelea napenda kwanza ujiweke ktk ufahamu kwamba neno “Mungu” ni sifa, ndipo sifa haiwezi kuwa baba wa huyo Mwana, hivyo tukitaka kujua mwenye sifa hiyo ni nani basi Yn 4:24 inatuonesha, “Mungu ni Roho” – (God is a Spirit). Ndipo jambo hili likiwa liko hivyo, linakuwa linakubaliana na Maandiko ya kuzaliwa kwake, Mt 1:18 “… Mariamu mama yake … alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu.” Huu ndio Uana wa Mungu wa Yesu.

  2. Yesu Kristo ni Nabii.
  Yule Mungu, alipojimimina ndani ya Yesu, yule Mwana wa Mungu, ndipo akawa Nabii, Kol 1:19 “Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae.” Ndio maana unaweza kusikia akiitwa Nabii wa Galilaya au Mwana wa Adamu.

  3. Yesu Kristo ni Neno la Mungu.
  Yeye ni Neno la Mungu lililodhihirika katika mwili. Yh 1:1 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.” Kifungu cha 14, ”Naye Neno akafanyika mwili…”

  4. Yesu Kristo ni Mungu.
  Tukiongozana na mtume Yohana hadi kule Mwanzo, tunaona katika Mwz 1:1 “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.” Sasa jambo hili linapooanishwa na Yoh 1:1, ndipo tunajua kwa uhakika kwamba huyo Mungu ni huyo Neno ambaye ndiye Kristo aliyedhihirika ktk mwili, 1Tim 3:16 “… Mungu alidhihirishwa katika mwili …”

  MUNGU BABA NI NANI:
  “Mungu ni Roho” Yn 4:24 huyo Roho, alipojidhihirisha ktk mwili kwa Neno lake ndipo aliitwa “Bwana Yesu Kristo” Mdo 2:36 “Basi nyumba yote ya Israeli na wajue yakini ya kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo mliyemsulibisha kuwa Bwana na Kristo”; Israeli wanaijua vizuri maana ya neno hili kama tulivyomuona Kuhani Mkuu ktk Mt 26:63! Pia ikumbukwe kwamba neno na mnenaji havitenganiki, Yn 6:63 “… maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.”

  ROHO MTAKATIFU NI NANI:
  Roho Mtakatifu ni Mungu, huyo Roho, anapojimimina kwa kipimo ndani yetu, vile vyombo vya “utukufu” alivyovihesabia haki na kuvitakasa, ili kutuongoza katika njia yake. Mt 28:20 “… na tazama mimi (Yesu) nitakuwa pamoja nanyi siku zote hata mwisho wa dahari” ahadi hiyo ikiwatimilia mitume katika siku ile ya Pentekoste, akiwa ni Mungu yule yule (Roho).

  “Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele”; Yeye hujibadili umbile lake kulingana na hitaji la huduma anayoitimiza. Mtume Paulo alikutana naye akiwa NURU iliyo angaza toka mbinguni. Mdo 9:3; Yeye alikuwa ule Mwamba wa Roho waliounywea jangwani (1kor 10:4); Yeye hujibadili, hata akina Petro walipokuwa wakivua samaki baharini, na pia wale wanafunzi wake, walioongozana naye wakiongea naye njia nzima kwenda kijiji cha Emausi hawakumjua kuwa ni Yeye!

  JE, NI NANI HUYU YESU, AITWAYE BWANA NA KRISTO?
  Yeye ni Mungu, yule ROHO, yule NENO, alipojimimina ndani ya ule mwili, lile Pazia, alikuwa ni Emanueli, Maandiko akiyatimiza kama alivyowafunulia watumishi wake manabii kuhusu mambo hayo (Isaya 9:6). Yeye ni: Mimi Niko Ambaye Niko; Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, Aliyeko na Aliyekuwako na Atakayekuja, Mwenyezi; yeye Ibrahimu asijakuwapo, mimi NIKO. Huyo ndiye Mungu mwenye NAFSI MOJA tu, Yer 22:5 “Lakini kama hamtaki kusikia maneno haya, mimi naapa kwa nafsi yangu, asema BWANA, ya kuwa nyumba hii itakuwa ukiwa.”

  Hiyo ndiyo SIRI KUU ya utauwa, Mungu alidhihirishwa katika mwili. Maana katika yeye unakaa utimilifu WOTE wa MUNGU, kwa jinsi ya kimwili. 2Kol 2:9
  “YESU KRISTO NDIYE SIRI YA MUNGU ILIYOFUNULIWA!”

  Kama kipofu Bartimayo aliijua Siri hii ilipofunuliwa kwake, kipofu Lwembe hana namna ya kulikwepa jambo hili lililowazi kama tunavyoliona, labda awe mwenyewe amechagua kuendelea na ibada ya miungu, ambayo ni sawa na yule ndama wa dhahabu waliyejitengenezea Israeli huko jangwani, nalo Kanisa leo likilirudia jambo hilo!

  Gbu!

 42. Pendael Simon,

  Umeiponda Theology, lakini maelezo yako yanaonesha wewe ni mwanatheolojia.

  Pengine huwa mnaiponda theology bila kujua sana yenyewe ni nini hasa.

  Unajuaje kuwa biblia iliandikwa katika lugha ya Kiebrania na Kigiriki kama husomi historia ya biblia( ndio thelojia yenyewe)

  Ivi unamjua King James wa hilo toleo la biblia ya King James unalolipenda, alikuwa ni mchungaji au nabii wa wapi mpaka atoe toleo la biblia?

  Ni lini Roho mtakatifu kwa kupitia nabii au mtume nani aliamuru biblia iwe na vitabu 66, na kwa nini vingine viliondolewa?

  Kwa mfano, una uhakika mwandishi wa kitabu cha Luka mtakatifu alikywa anaongozwa na Roho kuandika hicho kitabu?

  Mbona hamwambii watu wasijifunze kusoma na kuandika maana watafundishwa tu Roho mt.wakitaka kusoma biblia?

  Kwa nini Timoth anakaa na kujifunza chini ya miguu ya Paul, si angefundishwa tu Roho mt.?

  Hebu tuongee kuhusu Theologia ya kweli, ni nini?

  Kosa la mafarisayo na masadukayo na waandishi lilikuwa ni lipi hasa, kule kuzikariri sheria vichwani mwao, au ni kule kutozitenda hizo sheria walizokariri?

  Je ni vibaya kukaa na kuamua kudadisi kwa kufikiri nini maana ya fungu fulani la maandiko?

  Je ni vibaya kujifunza Mungu ni nani?

  Ni nini hasa ambacho ni kibaya katika kusoma Theolojia ya kweli?

  How do u know kama alichotengeneza Yesu pale Kana ya Galilaya kilikuwa ni kileo au la?

  Au wewe unadhani/unajua Theolojia ni nini?

  Simon hebu tusemezane kidogo!!

 43. Bwana Ziragora,
  Wewe umenipachika cheo cha MAWAZO YAKO cha kuuongea kama “politician”, hayo ni maneno ya kuishiwa na kufilisika kiroho.
  TANGU LINI MKRISTO AKAWA “THEOLOGIAN”?
  Mimi nashawishika kuamini kuwa wewe ni msomi unayetumia ubongo wako vizuri wala usimzingizie ROHO MTAKATIFU hata lugha yako si ya Kikristo si kwangu tu bali pia kwa wachangiaji wengine.
  Kwa kutumia akili lazima ushinde na inawezekana hata darasani uliwashinda wengi na pengine WALIMU wako walipata kazi ya ziada.Hakika wewe ni mwanafalsafa mzuri.
  Hujaangalia tafsiri ya maneno hayo katika muktadha husika bali umetumia akili na si ROHO MTAKATIFU.
  NAMSHUKURU MUNGU MUULIZA SWALI (Dada Janeth) AMEKIRI KWA KUTUMIA MAANDIKO HAYO HAYO UNAYOYAKANA WEWE KUWA AMEPATA UFAHAMU.
  SIJUI KAMA ANDIKO HILI LITAKUSADIA KWA SABABU UMEKUWA UNAYAKOSOA.
  LUKA 10:21 ‘ Saa ile ile alishangilia kwa Roho Mtakatifu,akasema,Nakushukuru,Baba,Bwana wa mbingu na nchi ,kwa kuwa mambo haya umewaficha wenye hekima na akili; umewafunulia watoto wachanga; Naam,Baba,kwa kuwa ndivyo ili kupendeza.”- YOU CAN’T HELP!
  MAELEZO YAKO MAREFU HAYAWEZI KUNISAIDIA KWA SABABU SI YA ROHO MTAKATIFU BALI NI KITHEOLOJIA.
  SINA MPANGO WA KUENDELEA KUJIBIZANA NA WEWE ILA UNAWEZA KUENDELEA NA HOJA ZAKO NA UTAFITI WAKO WA WA KISAYANSI.
  Ahsante.

 44. Ndg Ziragora,

  Kimsingi mafundisho yako yamenifurahisha sana. wakati wote nimekuwa nikijaribu kujua unasema nini ktk michango yako, ingawa ni vigumu sana lakini nadhani nimefanikiwa kwa sehemu!

  Wachangiaji wengine haikuwa shida kuwaelewa wanachokisema, kama akina Fralugg au Dickson nk ambao wanaamini kwamba Mungu ana Nafsi Tatu, na hao wengine kama Milinga, Pendael, Mhina nk ambao wanaamini kwamba Mungu ana Nafsi Moja; na pia michango yao inaeleweka kirahisi kwa kule kuikubali kwao lugha ktk matumizi ya kawaida kulifafanua jambo lolote lile.

  Kwa kadiri nilivyoisoma michango yako, nakuona ni mtu anayejaribu kubahatisha kuhusu uwepo wa Mungu; ndipo ninakushauri uchukue muda kidogo ujifunze maana ya maneno yanayotumika ktk lugha ili unapojadili jambo, basi wazo lako lipate nafasi ya kumfikia mtu mwingine ktk ufahamu!

  Kwa mfano, msingi wa mjadala huu ni suala la “NAFSI”; wote waliochangia, kasoro wewe, wanajua maana ya “Nafsi” kuwa ni “Individual”, yaani “mtu” au “Personality”; na pia kwamba, watu wawili au zaidi, HAWAWEZI kuwa Nafsi Moja. Tena unaposema “”Kibiblia ni kwamba Baba, Mwana na RM ni umoja. Biblia inaposema Baba ina maana Baba yupo, inaposema Mwana, ina maana naye yupo, inaposema RM inamaanisha yupo”” kutoka maelezo haya ulitakiwa utuambie kuwepo kwao ni kwa jinsi ipi, Je, hao wote ni NAFSI MOJA, au ni NAFSI TATU zilizo katika UMOJA; au kuhusu hiyo kauli yako kwamba Baba, Mwana na RM ni umoja, nao umoja maana yake ni ushirikiano, Je, huyo Baba na huyo Mwana na huyo RM ambao wote wapo, wanashirikianaje iwapo wao si Nafsi?
  Unaona! Ni maluwe luwe matupu!!!

  Tazama conclusion yako: “”Baba+Mwana+RM= Mungu, bila kujali uhusiano wa hizo caracteristics moja kwa ingine” Hiyo hesabu yako haileti maana labda uwe ni mtu unayeyatumia tu maeno bila kuijua maana yake! Neno “Mungu” ni sifa na si personality au Nafsi, (GOD: object worshipped as divine). Huko jangwani walipopewa Sheria, Mungu alijifunua kama BABA, hakukuwa na jambo la Mwana wala RM, na kumkufuru kuliwaletea adhabu ya kifo! Alipokuja Kristo Mungu alijifunua kama Imanueli, Mungu pamoja nasi, yule BABA, akijipatanisha nasi; kumkufuru huyo, ulisamahewa! Leo hii, Mungu amejifunua kwetu kama RM, BABA yule yule, Mungu ndani yetu; kumkufuru huyu, HAKUNA msamaha! Kwahiyo unaposema, “” Baba+Mwana+RM= Mungu”” inaonesha ni kwa kiasi gani hujui unachokisema, utakuwa liunakimbia tu neno la “Utatu” lakini mafikiri yako yote yamejengeka ktk “Utatu” huo huo, ndio maana you are at peace hao wakiwa ni UMOJA kuliko wakiwa ni MMOJA; kwa sababu deep in your soul, unawaona WATATU, which is paganism!!!

  Hebu jaribu kurefresh receptors zako ili zidake mambo ya Mungu hata umjue vizuri zaidi kuliko hayo mafundisho yalizozitia kutu spiritual receptors zako mpaka zimekuwa twisted kudaka mambo ya dini yasiyoeleweka! Mtazame Ibrahim hapa ktk Mwa 18:1-3, spiritual receptors zake ziko superfine, hababaiki kabisa:
  “BWANA akamtokea Ibrahimu karibu na mialoni ya Mamre, alipokuwa ameketi mlangoni pa hema yake mchana wakati wa hari. Akainua macho yake akaona, na tazama, watu watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga mbio kuwalaki kutoka mlangoni pa hema, akainama mpaka nchi, akasema, Bwana wangu, kama nimeona fadhili machoni pako nakuomba usinipite sasa mimi mtumwa wako.”
  Unaonaje hapo Ziragora, bila shaka hao walikuwa, Baba + Mwana + RM= Mungu!! Kwahiyo walipoondoka wale wawili, ibrahimu akawa tena hayuko na “Mungu”, wale wawili akiwa amejisahaulisha walipoondoka! maluwe luwe matupu! Ibrahimu anamjua Mungu ni Mmoja tu na si hadithi zisizoeleweka za +++=Elohim, haya hao wawili wameondoka huyo aliyebaki hapo na Ibrahim ni nani?

  Haya muangalie Lutu hapa, Mwa 19:1-2,
  “Basi, wale malaika wawili wakaja Sodoma jioni; na Lutu alikuwa amekaa mlangoni pa Sodoma. Lutu akawaona akaondoka akaenda kuwalaki, akainama kifudifudi. Akasema, Bwana zangu, karibuni nawasihi mwingie nyumbani mwa mtumwa wenu”
  Ibrahimu aliwaona watu watatu, ” akasema, Bwana wangu” na Lutu aliwaona wawili, “akasema, Bwana zangu” Refresh your receptors!!!

  Kwa kukusaidia, hiyo tafsiri ya UTATU MTAKATIFU niliyoileta hapo juu si yangu mimi bali ya wana Teologia. Nimeiweka hapo ili iwasaidie kukijua mnachokiamini, kuwa ndiye Mungu baada ya kuona wengi wetu HATUIJUI tafsiri hiyo, tunaimba tu “UTATU”!!!

  Pia, hii dhana yako ya “nafsi” ni mafikiri yako zaidi kuliko kile Biblia inasema. Unasema, “”Hivi hatuone kama kibiblia mtu ana mwili, nafsi, na roho akiwa ni mtu mmoja bila sehemu moja kujitegemea?” Hakuna Biblia inayosema hivyo, wewe umejichanganya tu, umeikosa maana ya “mwili” ndio unajaribu kujenga hoja ya kitu cha tatu ambacho hakipo! “Nadhani umeona kama nafsi ni damu. Mtu ana nafsi na wanyama wanayo.” Haya si kweli ni hadithi za vijiwe vya dini! Je, ukiongezewa damu hospitali, ya watu wanne tofauti, unaishia kuwa na nafsi ngapi? Hata hao wanyama, Mungu alisema hao ni Hayawani wao hawana nafsi! Chunguza zaidi, Nafsi zinawajibika kwa Mungu, na vile vile neno Nafsi” na “Roho” ktk Biblia vimetumika interchangeably, kwahiyo uwe makini kidogo ktk unayoyafundisha, usije ukazipoteza “nafsi” za watoto wa Mungu kwa kukosa Maarifa!

  Kuhusu Elohim, hebu jitazame wewe mwenyewe, ulipokuwa na umri wa miaka 13, kuna yeyote aliyekuita “baba”? Hakuna! Lakini ukweli ni kwamba ulikuwa ni “baba”, watoto wote ulionao leo hii, hata wakiwa ni 20, wote walikuwa kiunoni mwako, wewe ukiwa ndiye baba yao! Basi akiwepo mwenye kuweza kuijua siri hiyo, akawajua na wanao hao, huyo angekuita baba fulani tangu ukiwa na siku moja duniani, jambo ambalo lingedhihirika huko mbele watakapozaliwa hao watoto, ndipo dunia ingelijua hilo. Basi nawe usiwe kama dunia, siri ya Mungu ikiisha kufunuliwa kwako!

  Biblia inapokuambia “Hapo mwanzo alikuwako Neno” tafuta kujua ni kwanini inasema hapo mwanzo alikuwako Neno na si Mungu; Mungu ni sifa anayopewa baada ya kuumba na hao aliowaumba!

  Kuhusu ile miti, mafikiri yako ndio yanakuongoza, halafu wewe unaamini kwamba ndilo Neno la Mungu! Hakuna mahali ambapo Mungu aliwakataza kula tunda la Mti wa Uzima, Mwa 2:16-17 “BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, 17walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.” haya liko wapi hapa Neno la kuwakataza kula matunda ya Mti wa Uzima? Walipokosa ndipo WALIZUIWA wasiufikie ule Mti wasije wakayala matunda yake wakaishi milele! Na nikakuambia kuwa mti waliokula sio huo hapo ktk kifungu cha 17!!! Ila ile Siri uliyoigundua bado hujatupatia nasi tuishiriki, usiwe mchoyo wa mafunuo!

  Ziragora ndg yangu, nimeandika mingi, lakini hebu yapitie hayo kisha twende mbele zaidi, ingawa Dickson amesepa kidogo!

  The Lord bless u!

 45. Ndugu Dikson,

  Naomba ukubali nikupongeze kwa michango yako yote. Ila hakuna la kudhani kama utaeleweka kirahisi kwani hata watu wengi hawakumuelewa Yesu mwenyewe. Hapa tunachokifanya ni kumuiga yeye Yesu. Sasa kama watu wengi walishindwa kumkubali Yesu, unafikili watakubali Dikson kirahisi?

  Pamoja na kuomba Mungu ili aangazie wachangiaji, mimi nakushukuru pia nakuomba kuendelea, wala usichoke kwani njia ni ndefu.

  Ubarikiwe.

 46. Ndugu Simon,

  Unaongea kama politician wala si kama mukristo wala theologian.
  Unayoyazungumza hayaeleweki. Pengine una mada ingine ndio maana hueleweki. Yaani mada imekuwa ni “ipi version ya Biblia nzuri kati ya Biblia ya kiswahili na kingereza”? Jamani, mbona hakuna lugha inayotafsiri ingine sawasawa %100? OK, sasa usisingizie Biblia, unisingizie mimi , utazame comments zangu ndizo usahihishe kabisa. Kwani ninapoandika shairi, palipo “umoja” siruhusiwe kuandika “mmoja” licha ya kuwa nimezingatia moyoni mwangu kama ni “mmoja”. NInapokuta neno kama hili mimi sijiulize mengi ila kuangalia ndani ya lugha nyinginge: Kiswahili, kingereza, kifaransa, kiebrania, kigriki, … Baadae siwezi badili shairi kwani siruhusiwe pia nitakuta katika zile versions zote kuna utofauti kidogo tu. Kwangu sione kama unasumbuliwa na nini. Au uhakikishe wewe una akili za kitoto, tutakuchukulia.
  Hivi pengine unataka ufahamu , acha hio shairi niyiweke katika tafsiri za Biblia kwa lugha amabazo tunazozizungmuza hapa inchini , yaani kingereza na Kiswahili:

  -Swahili Union Version(SUV):1 Yohana 5:8 kwa maana wako watatu washuhudiayo mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni UMOJA.

  -Biblia Habari Njema(BHN): 1 Yohana 5:7-8 Basi wako mashahidi watatu,Roho, maji na Damu, na ushaidi wa hawa watatu WAAFIKIANA.

  -Complete Jewish Bible(CJB):1John 5:7-8: There are three witnesses- the Spirit, the water and the blood- and these three are IN AGREEMENT.

  -English Standard VersionESV): 1John 5:7-8: For there are three that testify: the Spirit, the water and the blood; and these three AGREE.

  -New International Version(NIV): 1John 5:7-8: For there are three that testify; the Spirit, the water and the blood; and these three are IN AGREEMENT.

  -King James Version(KJV): 1 John 5:7: And there are three that bear record in the heaven, the Father, the Word, and the Holly Ghost; and these three are one.

  -Amplified Bible(AMP): 1 John 5:7: So there are three witnesses in the heaven, the Father, the Word, and the Holly Spirit; and these three are One.

  -Easy To Read Version (ERV): 1 John 5: 7-8 So there are three witnesses that tell us about Jesus: the Spirit, the water and the blood. These three witnessess AGREE.

  -Expanded Bible(EXB):1. John 5: 7-8 So [or For] there are three witnesses [ who testify/bear witness]: the Spirit, the water, and the blood; and these three witnesses AGREE[ are one].

  Notice: kama kwenye AMP, na KJV, sikuweka “one” kwa herufi kubwa ni kwani nilitaka wasomaji waone jinsi ile “one” imeandikiwa kitofauti. KJV inaandika “one” halafu AMP inaandika “One”.

  Simon, ni ipi sahihi? Na zingine umezitupa wapi? Zisisomwe? Na kama kwa mfano mtu hafahamu kingereza asisome Biblia?

  Nilichoona kwako, kuliko kuingilia mada unakwamia ndani ya upinzani. Kinachonishangaza unaupeleka hata kwenye versions za biblia. Katika zile kidogo nilizobandika pale ni zipi ambazo zinasema %100 sawasawa?

  Ninarudilia tena kifupi cha makala yangu ambacho ndicho nataka usahihishe ili uepuke sahihisha Biblia ukidai tu kwamba ni ya Kiswahili:

  “1) Mungu ni mmoja na ndani yake kuna manifestations au caractéristics tatu: Baba, Mwana na RM ambazo hata ukijiunga na majini huezi ziondosha; zinaandikwa waziwazi kwa idadi kubwa sana ndani ya kila version ya Biblia.
  2) Katika agano jipya jina la Mungu muumba mbingu na dunia ni Yesu Kristo, pia hilo jina halimaanishe Mwana.”

  Ukitazama vizuri utakuta katika shairi niliyobandika ni version moja inayoweka wazi kama jina la Mungu ni Yesu, yaani ile ya ERV. Haijamaanisha kama versions zingine zimekanusha huo ukweli. Simon, jifunze kuisoma biblia kama Neno la Mungu ndipo utaelewa.

  Unasema “umoja” = “unity”. Hii ni lugha yako. Inafaa uitazame kwa mtazamo wa RM yaani kwa mtazamo wa Biblia. Ukiingia ndani ya kamusi unakuta “union”, “oneness”. Pia ukitafuta tafsiri za “oneness” kwa lugha ya kiswahili utakuta “moja”. Hence usipime sahihisha biblia kwani lugha nayo siyo rahisi. Ninayokupasha ni kwamba “umoja”=”oneness”=”moja”(according to dictionaries EN-SW & SW-EN). Kabla ujiruhusu kusahihisha maandiko hakikisha umeufanya utafiti mkubwa in bidirectional logic; sivyo utakurupuka tu na kukufuru pasipo kufahamu.

  God bless you.

 47. Shalom.
  Napenda kuwatia moyo wenye nia ya kutaka kujifunza ili kufikilia utimilifu kuwa wasiogepe vitisho vyovyote vinavyotolewa na WANATHEOLOJIA Bali wajisikie vizuri kuuliza maswali yanayojenga.
  Kama nilivyosema mwanzoni Theolojia haikuanzishwa na Bwana Yesu bali ni mpango wa mwanadamu wa kuwatawala binadamu wenzake.Ndio maana hakuna Mtume hata MMOJA alikwenda kusoma theolojia baada ya Kuitwa na Bwana Yesu.
  Mafarisayo,Masadukayo na Waandishi leo ni Wanatheolojia . Kazi kubwa waliyonayo hawa wanatheolojia ni KUWATISHA watu na KULIFANYA NENO LA MUNGU LISEME KILE WANACHOTAKA WAO.Soma MARKO 7:1-15.
  Theolojia ni MAPOKEO YA WANADAMU TU (MARKO 7:8…”Ninyi mwaicha amri ya Mungu,na kuyashika mapokeo ya wanadamu.”
  Bwana Yesu hakuwahi kuogopa kitisho chochote hata Herode alipomtishia ( LUKA 13 :31-32)
  Mitume wenyewe walifuata nyayo za Bwana Yesu za kutomuogopa mtu yeyote,wao walimuogopa Mungu tu ( MATENDO 4:1-22, 5:17-33)
  Siku zote hata ukitafuta Andiko la Kutendea uovu utapata na utapewa kulingana na haja ya Moyo wako. Na hii ni Kibiblia kabisa kwa sababu ‘Waisraeli waliambiwa wawape wake zao talaka kutokana na ugumu wa mioyo yao’
  Ukitafuta Andiko la kukuhalalishia mungu mwenye nafsi tatu utalipata tena, utayapata Maandiko mengi na utaona uko sahihi kabisa hutahitaji kumsikiliza yeyote.
  Kumbuka mpendwa;
  1.Kama Mungu amekunyima ufunuo wa Neno lake hata ujitahidi vipi hutafanikiwa kamwe (MARKO 4;10-12, LUKA 10 :21-24)
  2.Neno la Mungu halifasiriwi apendavyo mtu ( 2PETRO 1:20)
  3.Kuna injili ya namna nyingine inayohubiriwa hapa Duniani (WAGALATIA 1:6-7)
  4.Uwe mwangalifu (WAGALATIA 1:8-9)
  KUANDIKWA NA KUTAFSIRIWA KWA BIBLIA.
  -Bila shaka Wakristo wa kweli wanajua kuwa BIBLIA iliandikwa na watu Walioongozwa na ROHO MTAKATIFU, kwa maneno mengine Mwandishi wa BIBLIA ni ROHO MTAKATIFU.
  -Waliotafsiri BIBLIA wapo katika makundi mawili;
  (A) Kundi la kwanza ni la wale waliotafsiri BIBLIA wakioongozwa na ROHO MTAKATIFU
  (B) Kundi la Pili ni la wale waliotafsiri BIBLIA wakiongozwa na roho wa Ibilisi
  Ndio maana wamebadili maana ya asili ya maneno ili kukidhi haja za mioyo yao kama vile Mafundisho ya nafsi tatu za mungu.
  Najua kusema hivi kwa mwanatheolojia ni ‘kukufuru’ kukuu sana
  Ubarikwe ndugu Lwembe kwa kuwasaidia Wasomi kuwa Biblia Ya Kwanza ni ya Kiebrania na wala si ya Kiyunani.
  Lugha ya Kiswahili imechukua tafsiri ya BIBLIA kutoka Lugha ya Kiingereza
  Wakristo wa kweli daima watapinga mafundisho ya Baraza la Nikea (Mafundiso ya mashetani)
  WAKRISTO WA KWELI hawakosoi BIBLIA bali pia HAWATAKUBALI KUPOTOSHWA KWA NENO LA MUNGU kwa kuingizwa kwa tafsiri za Mafundisho ya mashetani (1TIMOTHEO 4:1-6).
  MUNGU alitupa mamlaka ya kujaribu roho zote ili tusilishwe au kunyweshwa sumu ( Kitu ambacho si Neno la Mungu),soma 1YOHANA 4:1-3
  Kwa kuwa niIilionekana kana kwamba napendelea BIBLIA YA “HOLY BIBLE-KING JAMES VERSION” kurekebisha tafsiri ya Biblia ya Kiswahili.
  Nitatumia tafsiri zingine ili mwongo aonekane.
  Kuna tofauti kubwa kati ya neno “unity”-umoja na “one” mmoja kama ilivyotumika katika Biblia ya Kiingereza (one) na Biblia ya Kiswahili ikatafsiri ‘umoja’
  Bila shaka neno ‘umoja’ na neno ‘mmoja’ ni maneno mawli tofati kabisa kimaana.
  THE HOLY BIBLE-NEW INTERNATIONAL VERSION ( JOHN 17:22 ” I have given them the glory that you gave me,that they may be one as we are one”
  Je,neno ‘umoja’ linapatikana katika mstari huu?
  Kama shida ni lugha ya Kiingereza hilo ni tatizo la mtu binafsi.
  Hata sentensi hii kwa Kiswahilili si sahihi 1Yohana 5:8 ‘….na watatu hawa ni umoja’.
  1 YOHANA 5:8 inasomeka hivi Kwa Kiingereza ;
  THE NEW TESTAMENT…WITH PSALM AND PROVERBS (THE GIDEONS INTERNATIONAL) … 1JOHN 5:7 “For there are three who bear witness in heaven:the Father, the Word, and the Holy Spirit; and these three are one” Je,neno ‘umoja’ linapatikana katika mstari huu?
  Tafakari tena mwisho wa huu mstari……”and these three are one”
  Roho wa mungu mwenye nafsi tatu akikukolea hutaamini Ufunuo Halisi wa ROHO MTAKATIFU mpaka BWANA YESU akuondolee hiyo roho.
  KARIBIA KILA KILA DHEHEBU LEO LINA BIBLIA YAKE TOFAUTI NA LINGINE.
  WENGINE WANA TAFSIRI TOFAUTI TOFAUTI YA BIBLIA YENYE VITABU 66 NA WENGINE WANA BIBLIA YENYE VITABU 77 !!!
  SWALI;KWANINI KILA DHEHEBU LINATAFSIRI BIBLIA KIVYAKE?
  ****INATEGEMEA NI JICHO GANI UNALOTUMIA KUSOMA BIBLIA****
  Amina.

 48. Shalom.
  Wapendwa mnaopenda kutafuta Ukweli msiogope kujifunza kwa sababu bado mlango wa Mbinguni uko wazi.Ipo siku Neema itafungwa (Isaya 55:6-7)
  Msiogope vitisho vya Wanatheolojia pindi mkitaka kuuliza maswali kwa sababu wao ndio Mafarisayo,Masadukayo na Waandishi wa leo. Kazi Kubwa Ya Wanatheolojia ni kulifanya NENO LA MUNGU liseme kama wao wanavyofikiri.Ndio maana ukitaka kujua Bwana Yesu si mwanzilishi wa Theolojia,hakuna hata mtume mmoja wa Bwana Yesu aliyekwenda kusomea theolojia baada ya Kuitwa na Kristo.
  Wakristo wa Kweli hawaogopi vitisho vyovyote vya kwenye Biblia na nje ya Biblia ,hata BWANA YESU alitishwa na wengi akiwemo Herode na hata hakuogopa chochote.Majibu ya Bwana Yesu kwa Herode ni “…………,Nendeni, mkamwambie yule mbweha….(Luka Mtakatifu13:31-32)
  Mitume nao walitishwa na hawakumwogopa mtu yeyote bali waliihubiri Kweli ya Neno la Mungu kama BWANA YESU alivyowaagiza ( Matendo 4:1-22, 5:17-33)
  Zipo Nyaraka nyingi zinazodhaniwa ni za Injili lakini ni za uongo ( Wagalatia 1: 6-7)
  Kwa hiyo Biblia inawatambua hasa Wale wanaoigeuza Injili ya KRISTO.
  Bila shaka kila Mkristo anajua kuwa Biblia iliandikwa na Watu walioongozwa na Roho Mtakatifu.
  Ubarikiwe ndugu Lwembe, uliweza kuwakosoa wanatheolojia kwa kuwaambia Biblia ya asili si Kiyunani.Biblia ya Asili ni ya Kiebrania.
  Biblia ILIANDIKWA KWA UONGOZI WA ROHO MTAKATIFU lakini Biblia IKATAFSIRIWA NA WATU WENGINE WAKIONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU NA WENGINE WAKIONGOZWA NA THEOLOJIA.
  KUNA TAFSIRI NYINGI ZILIZOINGIZWA KATIKA BIBLIA AMBAZO SI ZA KWELI NA MTU WA KIAKILI ANAFIKIRI UNAKOSOA BIBLIA!!!
  Neno la MUNGU halifasiriwi apendavyo mtu fulani (2 Petro 1:20-21)
  Nilishutumiwa kuwa napendelea Biblia ya ” HOLY BIBLE-KING JAMES VERSION” naomba nitumie Biblia nyingine ya ” THE HOLY BIBLE-NEW INTERNATIONAL VERSION” kuonesha tofauti kati ya neno ‘UMOJA’ kwa Kiingereza “:unity” na neno ‘ MMOJA’ kwa Kiingereza “one”.
  Hata lugha ya Kiswahili haikubali sentensi “….na watatu hawa ni umoja,”
  THE HOLY BIBLE-NEW INTERNATONAL VERSION ( JOHN 17:22 ” I have given them the glory that you gave me,that they may be one as we are one:”
  Neno ” UMOJA” liko wapi kwenye hiyo sentensi?Tatizo ni lugha ya Kiingereza?
  Mstari mwingine uliooneshwa na mchangiaji kuunga mkono wazo la Kithiolojia na Mafundisho ya awali ya Baraza la Nikea ya Kwamba Mungu ana nafsi tatu ni “1Yohana 5:8″
  NEW TESTAMENT( THE GIDIONS INTERNATIONAL) hii Nukuu ipo 1 JOHN 5:7 “For there are three who bear witness in heaven :the Father,the Word,and the Holy Spirit;and these three are one”
  Ndugu zangu Neno ” UMOJA” liko wapi kwenye hiyo sentensi?
  INATEGEMEA NA JICHO UNALOTUMIA KUSOMA BIBLIA.
  AMEN.

 49. Mpendwa ZIRAGOZA
  Siri ya UTATU MTAKATIFU haiwezi kuelezwa kwa mitazamo yetu bali inaelezwa
  kwa uhalisi wa Roho Mtakatifu ambaye ndiye mwalimu wa kanisa.Sisi bila ya upako
  wa Roho Mtakatifu tutakuwa tunajidanganya.Mafunuo na mafumbo ya Mungu kama hili la UTATU MTAKATIFU yaani hekima ya Yesu kijufunua kama BABA, MWANA NA ROHO MTAKATIFU ni kazi ya Roho Mtakatifu kutufunulia(1 WAKORINTHO 2:9-10).

  Kwa sasa kumetokea mapamabano makali sana kati ya Mbwamwitu ambao kimsingi
  wamefundishwa namna ya kupotosha NENO LA MUNGU, na wateule wa Yesu ambao
  hawana hekima ya Roho Mtakatifu katika kuchanganua mambo na kuwatambua
  nyoka wenye sumu kali.

  NAPENDA KUCHUKUA FURSA HII MUHIMU SANA KUWAAGA WANA SG WOTE
  WAKIWEMO KINA CK LWEMBE,MR.MILINGA,DADA JANETH,MABINZA LS,EDWINI
  SELELI,OBRI,KINYAU HAGGAI,JOHN PAUL,DADA TH,PRIMI MOSILE,SUNGURA,JOHN
  HAULE NA WENGINEO WOTE.

  ROHO MTAKATIFU ATAENDEKEA KUFANYA UKAGUZI.LAKINI MIMI MWENYEWE
  SITACHANGIA MADA YOYOTE TENA.NAPENDA KUENDELEA KUJIFUNZA ZAIDI.ASANTENI KWA USHIRIKIANO NA UPENDO WENU.

  Nina kazi nzito na kubwa ya kufanya katika ulimwengu wa roho na wa mwili.
  Bila shaka Mungu akiendelea kutupa uzima TUTAKUTANA USO KWA USO.

  TUKUMBUKE YESU AFANYI BIASHARA YA REJA REJA BALI ANAFANYA
  BIASHARA YA JUMLA(MATHAYO 10:26-28).

  MUNGU ALIYE HAI NI MOTO ULAO NA ANAIPELEKA TANZANIA MAHALI PAZURI SANA.

 50. Ndugu Simon,

  Unayoifanya nimeizoea kwani si wewe tu bali wengi wanapenda jivua joho lao na kulivika wengine. Badala ya kujihukumu umekimbilia kirahisi kunihukumu ukiongeza kwa ile usahihisho uliyonipa kupitia kusahihisha biblia ya SUV ambayo ni kiswahili kinachoaminika Tanzania. Siwezi kukuzuiza kuonyesha hisia zako lakini unaposema neno hakikisha limetoka moyoni mwako. Basi ikiwa Biblia haitupe kibali cha kubishana, jambo ambalo nalikubali %100, tuseme basi hiyo biblia unayobishana nayo imekuruhusu? Ninazo versions nyingi sana za kingereza, ningelipendelea ubishi kama wewe, ningeenenda katika mtindo kama wako. Kama Biblia ya kiswahili inasema “umoja” na wewe umeikataa kwani ni kiswahili tu na kama KJV inasema “one”, where is the problem ili uifanye kuwa hoja? Unapoona ile fahamu kama ile neno “umoja” ndani ya SUV ndio “One” ndani ya KJV lakini usiwe kama umeumwa na nyuki. Si unafahamu sikuandika biblia? Naisoma kama wewe jamani. Unyenyekevu imekutorokaje ukiwa mukristo? Huwezi heshimu hata maandiko matakatifu? Na kama umedhani nimeisoma bibilia ya kiswahili ili nihalalishe utatu, unaweza zisoma hoja zangu ili uonyesheshe kihalisi nafasi nilipoihalalisha? Niko ndani ya nuru, na ni lazima niikupe: “Tunaongea lugha moja kwa hii mada, yaani kwamba Mungu ni mmoja”. Kinachotutofautisha pengine ni kwamba sipendi niondoshe ndani ya Bible maneno “Baba; Mwana, RM”. Swali ni kufahamu ni nani ambae ni sahihi mimi na wewe? Hayo maneno yaondolewe au la?

  Ndugu, unasema ninajibu bila maandiko wakati ninayokupa ya kiswahili unasema siyo. Do you think I’m obliged to give you only english Scriptures? Kwa nini huwezi ona kama hii “umoja” inayosemwa ndani ya SUV ndiyo ile “one” in KJV?

  Mimi siwezi kataa sahihishwa lakini biblia usiisahihishe bwana. Wewe unajiona bingwa kuliko Biblia? Sikiliza, hukusema hata kama nimesoma vibaya, lakini ulishambulia Biblia niliyosoma kupitia jina langu ndio maana ukaonyesha kwa nguvu version ingine. Case kama hiyo ina namna ya kuzungmuziwa, Kufokea Biblia haifai. Hebu angalia kwenye SG Biblia inayotumiwa haswa ni version ipi.

  Unauliza kama KJV, imetafsiriwa kutoka Biblia gani?
  Hili ni swali ambalo yalifae kwa jibu. Pia mimi sikuikataa, naifahamu na ninaitumia sana. Kabla uniulize hukujiuliza kama SUV ilitafsiriwa kutoka Biblia gani. Hence kwako siyo hoja ya “Baba, Mwana, RM” bali ni hoja ya tafsiri za Biblia. Ni heri nikuache upigane na Biblia. Ninachokijua kwanza ni kwamba KJV ni kingereza na SUV ni Kiswahili, pili SUV ni version inayoaminika hata kama katika kila version mnaweza kuwa upungufu fulani amboa hutokana haswa na wasomaji.

  Ubarikiwe mpendwa.

 51. Wakaka na wadada,

  Nasikitishwa sana na wachangiaji wanaotupilia mbali maneno Biblia inayotupasha. Maneno Baba, Mwana, Roho yanarudiliwa ndani ya agano jipya kwa idadi isiyopungu 200. Sasa kwa nini tuseme hawapo? Tutakuwa tukiisoma Biblia gani? Kuokolewa siyo kufahamu jinsi Mungu iko 100% kwani anapita fahamu zote, lakini kukana Neno lake ni laana.
  Niliwaambia mapema kama utatu, nafsi siyo maneno ya lugha ya Biblia. Ikiwezekana wenye kuitumia waiache wakifahamu kama Mungu ni mmoja. Kuwa mmoja na uwepo wa Baba, Mwana, Roho MT havipingane. Pale ndipo pengine wengi wanakwamia. Ndio maana nikajaribu kuleta ile changamoto ya uumbaji wa mtu kwa mfano wa Mungu iliyosikilika kwa wamoja kama ina lengo ya kuthibitisha utatu. La hasha, unaposoma hoja, tulia uisikie. Nilikuwa wazi mno nikasema ukiisha sikia jinsi sehemu zako kubwa tatu ziko ndani yako ukiwa mmoja, ndipo unawezajaribu kusikia jinsi Baba,Mwana na RM wako ndani na Mungu mmoja.
  Tujaribu kusikiliza kama watu wanaolipenda neno la Mungu:
  -Si mwili wa mtu inafanya kazi nyingi kwa utumizi wa nguvu?
  -Si mwili wa mtu haiwezi chochote bila damu kuzuunguka ndani ya huo mwili?
  -Si sote twajua kama damu ikipungua sana, mtu anapoteza hata ufahamu na kufa?
  -Si sote twajua kama bila damu hai mwili ni maiti?
  -Si sote twajua kama damu yenyewe siyo mtu?
  -Si sote twajua kama mtu pasipo roho hayupo mtu bali mnyama tu kwani hana uwezo wa kuishi milele baada ya kuupoteza mwili?

  Hivi hatuone kama kibiblia mtu ana mwili, nafsi, na roho akiwa ni mtu mmoja bila sehemu moja kujitegemea?

  Mungu naye ni mmoja na anadhihirishwa na Baba, Mwana, RM. Kinachosumbua watu ni kusikia vibaya na kuweka maneno mengine wakisema “Mungu Baba, Mungu Mwana, Mungu RM”. Wanaosema vile wafahamu kama wanaongea mambo ya miungu.

  Tukisoma mashairi yafwatayo, bila shaka tutatambua kama Mungu ni mmoja ambaye ana Baba, Mwana na RM. Kuelewa Baba, Mwana, RM wanauhusiano gani ni jambo ambalo silo rahisi, lakini kutambua jinsi mtu iko inasaidia sana kuepukana na maneno kama nafsi tatu, utatu,… maneno inayoweza sababisha watu kudhani kama ni miungu!!! Mungu wetu ni mmoja katika uwingi wake wa kiteolojia. Tatizo lingine ni kudhani kama teolojia ni kama kila sayansa. Ina lugha yake inayopashwa kuheshimiwa na wote. Ndio maana hata mtu kisayansa hana sehemu tatu tu, anazo nyingi. lakini kiteologia anazo tatu. Tukifahamu kama Mungu ni mmoja hatutajiswali kama Baba, Mwana na RM wanakaaje mbinguni. Ni kama kuuliza kama Mtu anapokaa kwenye kiti, mwili unakaa wapi, na roho wapi na nafsi wapi.

  Ndo haya mashairi ambayo nadhani si mapya kwa baadhi ya wachangiaji:

  “1 Yohana 5:8 Kwa maana wako watatu washuhudiao mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja.

  Ufunuo wa Yohana 22:17 Na Roho na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure.

  Yohana 14:11 Mnisadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! Hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe.”

  Wapendwa , siwaombe kunisadiki mimi, lakini sadikini Biblia inayotupasha uwepo wa Baba, Mwana na RM ndani ya Mungu mmoja, pia epukeni chochote kinachopinga, kinachosahihisha wala ninachoongeza neno la Mungu.

  Mbarikiwe.

 52. Dada Janeth,
  Ubarikiwe na Bwana Yesu.
  Kumcha Bwana ni Chanzo cha Maarifa (Mithali 1:7 )
  YEHOVA WA AGANO LA KALE=YESU KRISTO WA AGANO JIPYA.

 53. Bwana Ziragora,
  Usipende kujibu ili mradi ujioneshe unajua kujibu bila kuzingatia unayoyajibu yapo Kwenye Maandiko au la.
  Hiyo tafsiri ya Kiingereza umeielewa au umeamua kubisha tu?
  Majibu yako yanaonesha kuwa wewe ni muumuni wa nafsi tatu,ndio maana unaipenda hiyo tafsiri ya Kiswahili.
  Biblia haitupi kibali cha kubishana.( 1 Timotheo 2:23-26)
  Kama hutaki kusahihishwa natilia shaka Ukristo wako kwa maana hata Bwana Yesu hutataka akusahihishe.
  BWANA YESU ALISEMA SISI NI WANAFUNZI WAKE (Mathayo Mtakatifu 28;19-20, Yohana Mtakatifu 8:31)
  Je, Biblia Ya “KING JAMES VERSION” imetafsiriwa kutoka kwenye Biblia gani?

 54. Tusiogope kujadiliana…..Hakuna uthibitisho wa asilimia mia moja ya kusema kwamba, Mungu ni mmoja lakini ana nafsi tatu, umeziona wapi hizo nafsi tatu au ni wapi katika biblia palipoandikwa waziwazi kua, Mungu wetu anazo nafsi tatu?…Biblia inafundisha waziwazi Mungu ni Mmoja wa pekee na Bwana yesu ni mwanae wa pekee aliyemtuma. Soma(Yohana 17:3). Wewe ukiamini kwamba, sifa zote za utendaji wa Mungu, hutendwa na nafsi yenye haiba nyingine, basi itakuwa ni vigumu sana kwako, kusema kua, unamuamini Mungu mmoja mwenye nguvu zote na uweza wote. Kwanini?, ni kwa sababu, ile hali ya kusema kua, unamuamini Mungu mmoja, ni lazima pia, huyo Mungu awe na nafsi moja na haiba yake mwenyewe. Sitaki kupingana na misingi yetu, tuliopewa Makanisani mwetu, kanisa halijafanya kosa kutujengea sisi misingi ya awali ya ufahamu, lakini inatupasa tulitafakari neno la Mungu zaidi bila ya kuliogopa, na kama kuna tatizo, basi ni kheri tukasaidiana na kujengana vizuri zaidi, kuliko kulaumiana na kuhukumiana wenyewe kwa wenyewe. Ukweli ni kwamba, Neno la Mungu ni “HAI” , uweza wa Mungu ni “HAI” ,Vipawa vya Mungu ni “HAI” ,na uungu wake ni “UHAI KWETU”. Sasa, tatizo kubwa linalowapa tabu watu wengi ni kumuwekea mipaka Mungu katika utendaji wake wa kutumia vipawa vyake hivyo. Biblia iwazi kuhusu sisi, jinsi tulivyoumbwa pale Eden, na Mungu, inasema”AKAMPULIZIA PUANI PUMZI YA UHAI MTU > AKAWA “NAFSI HAI”. Soma(Mwanzo 2:7). Pumzi ya Mungu au uweza wake ni Uhai kwetu. Sisi hatuhitaji tena nafsi hai nyingine wala Mungu mwenyewe, ahitaji tena nafsi yake nyingine ili aweze kutenda kazi ndani yetu. Kazi zote za Mungu juu ya wanadamu wake, zinahitaji nguvu yake na vipawa vyake pekee vya uungu wake, ili kutimiza makusudi yake yote, halafu inakua, ni ile nia ya nafsi zetu wenyewe zikipokea vipawa vya Mungu ndiyo yenyewe kwa asili yake ya rohoni hutufundisha, hutuletea habari kutoka kwa Mungu, hutuonya, nk. Soma(2 Timotheo 1:6)(warumi 12:6-8). Hebu sisi wenyewe tujiulize kua, kama roho mtakatifu ni nafsi hai nyingine ya Mungu, hii nafsi iliwezaje tena kugawanyika mbele ya mamilioni ya watumishi wa Mungu ili iweze kuwafundisha, kuwaletea habari nk, wakati nafsi yenyewe ni mmoja?….utanijibu kua, haigawanyiki, isipokua inafanya yote hayo kwa uweza wake na kua popote kwa wakati mmoja. Nami nitakuuliza tena, kama hivyo ndivyo, Sasa baba yetu wa mbinguni atashindwa vipi kufanya hayo yote kwa uweza wake mwingi, mpaka eti agawanyike tena katika nafsi tatu za utendaji?!!. Utanijibu kua, ni kwa sababu huyu roho mtakatifu ameongelewa kama nafsi hai, akiitwa huyo, huyo…nitakufundisha kua, hiyo ni heshima tu, ya vipawa vyote vya Mungu kuongelewa kwa uhai kwa kua vyote vitokavyo kwa baba vinaheshima ya uhai wake, na ndio maana hata ile roho, maji na damu katika (1Yohana5:9), waliitwa,hawa, tena wanaumoja wa kushuhudia mambo ya duniani…sasa, hata hayo maji na damu navyo vina nafsi hai ya kushudia mambo ya duniani au ni heshima tu, ya uweza wa kiungu wa kuitwa hawa, hawa?!!. Ukweli ni kwamba, roho mtakatifu ni kweli ameongelewa maranyingi katika biblia kama nafsi nyingine hai yenye utashi wake, lakini kamwe haikua na maana kua ni nafsi nyingine ya Mungu, na ndiyo maana mwanafunzi mmoja wa yesu, aitwae Yohana, aliona ni kheri amfananishe roho mtakatifu na “MAFUTA YA KUJIPAKA” ili watu waweze kuutafakari zaidi uweza wa Mungu na vipawa vyake vya ajabu mno.Yeye roho mtakatifu hakumuongelea kama ni nafsi hai, bali ni kama mafuta yetu ya kujipaka yatufundishayo mambo yote kutoka kwa Mungu.Twasoma katika(1Yohana2:27) anatuambia hivi” NANYI, MAFUTA YALE MLIYOYAPATA KWAKE YANAKAA NDANI YENU, WALA HAMNA HAJA YA MTU KUWAFUNDISHA, LAKINI KAMA MAFUTA YAKE YANAVYOWAFUNDISHA HABARI ZA MAMBO YOTE, TENA NI KWELI WALA SI UONGO, NA KAMA YALIVYOWAFUNDISHA, KAENI NDANI YAKE !!!!. Sasa, hapo pia, inatupasa kupatafakari kwamba, hivi mafuta ya kujipaka nayo yana nafsi hai ya kukaa ndani yetu na kutufundisha mambo ya Mungu?…kama hayana nafsi hai, wala hayawezi kukaa ndani yetu na kutufundisha, sasa ni kwanini yamemuwakilisha huyo roho mtakatifu? Je, hatujagundua bado, kua huyo roho mtakatifu sie kiumbe hai au nafsi ya Mungu, isipokua ni vipawa na uweza mkuu wa baba yetu aliembinguni?, hebu pia, kama haitoshi, soma(1Yohana 2:20). Tazama pia, yule malaika alie mletea mariamu habari njema, alimwambia” Roho mtakatifu atakujilia juu yako “NA NGUVU ZAKE ALIYE JUU, ZITAKUFUNIKA KAMA KIVULI !!!, Soma(luka 1:35), kumbe, roho mtakatifu ni uweza wa Mungu unaotuletea nguvu zake na vipawa vyake vya uungu kutoka juu!!. Hata kwa ushahidi wa sisi wenyewe, tunapohisi roho mtakatifu wa Mungu, kamwe hatuhisi kua na nafsi nyingi ya Mungu inayotufundisha ila tunahisi nguvu nyingi ndani yetu na uweza wa aliye juu. mbarikiwe

 55. Ndugu Simon,

  Hivi umeandika ukiwa serious au kishabik tu?
  Unasema unanisahihisha kwa neno “umoja” baadaye unalaumu kiswahili ambacho Biblia inatumia ukipendelea kingereza KJV. Hivi ni mimi umesahihisha au umesahihisha Biblia yenyewe? Pia una uhakika uko sahihi kuliko hiyo Biblia?

  Nafasi ingine umejitoa muhanga kusema unanipinga wakati unaposema kama YESU NI MUNGU. Ulikua out of thé mind ili usitambue kama unarudilia kwa udhaifu mkubwa ambayo nilisema kama JINA LA MUNGU KATIKA AGANO JIPYA NI YESU KRISTO? Uwe ukiomba Kabila ujajadili, pia uwe mtulivu na mwenye kuyapenda maandiko matakatifu bila kuyafanya yako.

  Mungu akuwezeshe.

 56. Ndugu John,

  Kinachotakiwa siyo kutabasamu wala kukenua meno hadi kilomiita mia saba sabîni na saba lakini ni kuleta majibu. Hushurtishwe kuleta ya Muhindi kama mimi. Lakini yalete ya kitanzania jamani, nakungoya, usiogope kaka yangu !!!

  Barikiwa.

 57. Mpendwa CK LWEMBE

  Naomba nianze kwa kunukuu maelezo yako ya TAREHE 14/10/2014 at 8:46 kama ifutavyo;

  Dada Janeth,
  Unasema
  “Wandugu zangu katika kristo!!Je nikifupisha tu kwa kusema kuwa Baba ni Mungu
  ambaye ndiye huyo Yesu na Mwana ni huyo huyo Yesu na Roho Mtakatifu ni Roho wa Mungu ambaye Mungu ndiye huyo huyo Yesu, je nitakuwa nimekosea ???
  HAUJAKOSEA, 1Yn 5:8 “Kwa maana wako watatu washuhudiao mbinguni, Baba, Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni MMOJA”

  Heri wewe Janeth, kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba aliye
  mbinguni !!!!
  Hayo ndiyo mafumbo ya Mungu anayafunua ili “Wakapate utajiri wote wa kufahamu kwa hakika,wapate kujua kabisa siri ya Mungu, yaani Kristo” kol 2:2

  —————————Mwisho wa kunukuu—————————————————-

  Hii ni nukuu ambayo inamaliza kabisa biashara ya SIRI YA UTATU MTAKATIFU ndani
  ya NAFSI ya CK LWEMBE!Unasema Kamugisha una maanisha nini?Sikiliza kwa makini
  Muheshimiwa Lwembe,Mungu anasema tukimtafuta kwa bidii tutamuona,kama ambavyo Janeth amemuona Mungu kwa kufunuliwa na Baba wa mbinguni,ndivyo
  na wewe pia ulivyoweza kumuona!YESU AFANYI BIASHARA YA REJA REJA,YESU
  ANAFANYA BIASHARA YA JUMLA(MATHAYO 10:28).Shetani anaweza kutuua nusu nusu lakini Yesu akiamua kukuangamiza nakwambia hata mifupa haitaonekana na ndiyo maana akiamua kukufufua anakufufua JUMLA.Shetani hawezi kutuua kiroho
  milele na kwa kuwa Yesu(Baba aliye mbinguni) amekufufua katika HILI LA UTATU
  MTAKATIFU,nakuomba sana tena kwa kukupigia magoti USIJARIBU KUYARUDIA
  MATAPISHI YAKO KWA KUFUATA MAFUNDISHO YALIYO KUFA.Neno ambalo linatudhihirishia kuwa Yesu alishuka kutoka katika kiti chake enzi kuja kukufufua
  ni pale ulipomuambia Dada Janeth kwa kutumia nguvu zako zote kwamba HAUJAKOSEA alafu ukakazia kwa kutumia 1 YOHANA 5:8.

  Sasa naomba twende taratibu ndugu yangu Lwembe.Kwanza kabisa naomba nikupongeze kwa kuwa na moyo wa kupenda kujifunza na kuchambua mambo
  kwa kina.Mara kadhaa MBINGUNI wamekuwa wakifanya sherehe kwasababu ya
  hekima na ujasiri wako katika kusimamia baadhi ya mafundisho ya Neno la Mungu!
  Japokuwa wakati mwingine katika baadhii ya mitazamo yako umekuwa ukijiamini
  kupita kiasi jambo ambalo ni dalili ya kukosa unyenyekevu wa Yesu(WAFILIPI 2:3-4).
  Kila mtu kuna sehemu kwa namna moja au nyingine huwa anakosa unyenyekevu
  na dawa ni kuomba Rehema na kumsii Mungu atuonyeshe mahali tulipopungua.
  kuna wakati huwa unamfanya Yesu akunje sura kwa maumivu unayomsababishia
  na kuna wakati unamfanya atabasamu sana tu si kidogo,kama ulivyo itikisa kambi
  ya shetani KWA KUELEZA KWELI KUHUSU HILA ZA KIROHO ZILIZOJIFICHA KWA
  WATU AMBAO WANAABUDU MCHEZO WA MPIRA WA MIGUU!Roho Mtakatifu
  anafuatilia kwa karibu sana mafundisho na mitazamo yetu ndani ya hii blog kuliko
  tunavyoweza kutafakari.

  Katika makala ya Roho Mtakatifu inayoitwa NI LAZIMA TUTAZAME KWA MACHO YA
  ROHONI,niliona umegusia suala la UTATU MTAKATIFU kama kigezo cha kutomkubali nabii fulani.Ulisema kwa kuwa hili fundisho haliko katika Bibilia ni wazi
  kwamba huyo ni nabii wa uongo.Naomba nikueleze jinsi ya kumtambua nabii wa uongo na Roho Mtakatifu anisaidie.Wakati mwingine si rahisi kumtambua nabii wa uongo kwa kufuatilia Neno analofundisha kwasababu wengi wananukuu yaliyo ndani
  ya Bibilia kwa asilimia mia moja!Pia ni vigumu kumtambua nabii wa uongo kwa matendo anayoonyesha na ishara na miujiza anayofanya(Mathayo 24:24,25).Unaweza kumtambua nabii wa uongo KWA MATUNDA YA MAFUNDISHO
  YAKE INGAWA ANATUMIA MISTARI HIYO HIYO YA KWENYE BIBILIA.Mafundisho yao
  wanayapindisha kwa hila sana kwa kutimia HEKIMA NA MAARIFA YA SHETANI.Kama
  huna ROHO SABA ZA MAARIFA YA ROHO MTAKATIFU(Isaya 11:2) lazima utaingia kwenye
  ‘kumi na nane’ zao.Neno la Mungu ni lile lile ambalo Roho wa Kristo anaweza kulifunua kwa namna mbali mbali na Roho wa shetani analifunua kwa namna mbali
  mbali.Ukienda faragha na Roho Mtakatifu utaona wazi bila chenga kwamba mafundisho ya imani yanayofundishwa na manabii wa uongo yanakwenda kinyume
  kabisa na mafundisho ya ROHO MTAKATIFU.Na imani za wengi ndipo zilpokamatiwa
  hapo.Njia nyingine ambayo ni rahisi zaidi ya kuwatambua manabii wa uongo ni KUWACHUNGULIA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO(ulimwengu wa ndoto) kama una MACHO YA ROHONI.Na ndiyo maana unapoingia tu kwenye makusanyiko yao
  jambo la kwanza watakalofanya ni kuyapofua macho yako ya rohoni.Unaota lakini ukumbuki ulichokiota.Ukikumbuka huelewi tafsiri ya ulichokiota.Na ili kukuchanganya watakuambia usiangaike na ndoto zinazotoka kwa shetani(Isaya 42:18-20).Kwahiyo ili
  usije ukastuka wanakukamata kwenye fungu la kumi.Hii ni sadaka ambayo inawapa umiliki wa moyo na roho yako.Unaanza kuwaona wao kwenye ndoto wakikupa maelekezo mbali mbali.Kama ulikuwa na mchumba kutoka kwa Bwana ambaye umepanga kumuoa,wanakutokea katika ndoto wanakwambia siyo mchumba halali.
  Wanakuonyesha mwanamke mwingine ambaye anatoka katika kambi yao ili ukimuoa
  aharibu maono na hatima ya maisha yako ambayo Mungu alikupangia.Wateule wengi katika hayo makusanyika ambayo kimsingi wanafuata miujiza wameishia kuoa au kuolewa na mbwamwitu.Na wengi wanazuiwa wasioe wala kuolewa bila ya wao
  kujua kwasababu ya kusikiliza ROHO ZIDANGANYAZO NA MAFUNDISHO YA
  MASHETANI(1 TIMOTHEO 4:1-3).

  Kupitia macho ya rohoni kuna wateule ambao wameona mambo ya kutisha na kusikitisha kwenye hizi huduma za manabii wa uongo.Kuna wengine baada ya kugundulika walionywa kwamba wakisema watakufa.Wengine baada ya kuona walichukua hatua ya kuhama kimya kimya.Wengine baada ya kuonyeshwa uhalisia
  wakaenda kufanya kama matangazo ya biashara na ndiyo maana siri za manabii wengi
  wa uongo ziko wazi sana kuliko vazi la kahaba mzoefu!Ukimuona mtu anabishana na
  kutetea huduma fulani ya nabii wa uongo inawezekana ni kipofu rohoni au ni agent
  mwenzao.Kwa wateule walio waaminifu Mungu huwaonyesha uhalisia wa huduma
  nyingi za manabii wa uongo ambazo hawajawahi hata kuzitembelea na hata zile ambazo ziko nje ya nchi zao!WATU WANAOTEMBEA NA MACHO SABA YA MUNGU
  WANAJUA SIRI ZOTE ZA MANABII WA UONGO NA HUWEZI KUWAKUTA WANAPOTEZA MUDA KUWATAJA AU KUSHINDANA NAO KWA JINSI YA MWILINI.ISIPOKUWA HUWA WANATUMIA MAARIFA YA YESU IKIWEMO MAOMBI
  KUWASIDIA WATEULE WALICHUKULIWA MATEKA NDANI YA HUDUMA ZA MANABII
  WA UONGO(Isaya 42:22).Unaweza kumchomoa mteule kwenye HAYO MADANGURO KWA NJIA YA MAOMBI na njia nyingine kadiri unavyoongozwa na Roho Mtakatifu.Ukitumia akili yako kudeal na hao misukule utakwama.

  Kwako MR.MILINGA
  Ukitaka kujua hicho kiti cha enzi kikoje na Mungu anakaaje au Mwana amekaaje
  mkono wa kuume, na pi ukitaka kujua uhaisia wa nafsi,mwili na Moyo.Neno linakaaje
  ndani ya moyo.Na nafsi inakaa sehemu gani ndani ya mwili pamoja na maswali mengine mengi uliyo nayo kuhusu mambo haya ITABIDI UMUOMBE YESU AKUPELEKA MBINGU YA TATU KATIKA MAKAO YAKE ILI AKUONYESHE NA KUKUFUNDISHA UHALISIA WA MAMBO HAYA YOTE.Unasema Kamugisha una maana gani ? Sikiliza Muheshumiwa Milinga naomba ukasome habari za Mtume
  Paulo(2 WAKORINTHO 12:1-4) jinsi alivyopelekwa KATIKA ZIRA YA MAFUNZO
  MBINGUNI alafu akarudishwa duniani ili aje KUFUNDISHA KWELI YOTE!!NYARAKA ZA PAULO ZINAELEZEA MAMBO ALIYOFUNDISWA NA YESU ALIPOTEMBELEA
  MBINGUNI(katika mbingu ya tatu).Mtume Paulo ametumia Hekima na Maarifa ya kutisha mno kueleza kila kitu alichokiona na kufundishwa kule mbinguni.

  Kilichomfanya Paulo apelekwe Mbinguni ni kwasababu aligundua SIRI YA UDHALIMU
  WA MUNGU inayoitwa UNYENYEKEVU WA YESU.Nabii,Mwinjilisti,Mchungaji na Mwalimu Paulo aligundua kwamba UDHAIFU NA UPUMBAVU WA MUNGU unaitwa
  UNYENYEKEVU WA YESU(1 WAKORINTHO 1:25,WAFILIPI 2:3-8,2 WAKORINTHO 12:11-13).Mungu anazungumza na sisi maneno magumu sana hapa.Roho Mtakatifu
  naomba utusaidie kuyaelewa.

  UTATU MTAKATIFU ni hekima ya utendaji kazi wa Mungu aliye hai.Kazi ya Roho Mtakatifu ni kuhakikisha MTU-ROHO,MTU-MWILI NA MTU-NAFSI ambao wanamkamilisha mtu anayeitwa MWANADAMU,wanakuwa na ushirikiano mtakatifu
  ILI MWANADAMU AFANYE IBADA TAKATIFU NA YA UAMINIFU KWA MUNGU ALIYE HAI.MTU-MWILI NDIYE AMBAYE AMEKUWA AKIHARIBU HUU USHIRIKIANO KWAHIYO NI LAZIMA KUMDHIBITI KWA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU.MTU-MWILI
  ANAPOWATAWALA MTU-ROHO NA MTU-NAFSI NDIPO MWANADAMU ANAPOKUWA AMEKUFA KIROHO NA KULAZIMIKA KUFANYA YALE AMBAYO HAPENDI KUYAFANYA.ANAKUWA NI MTUMWA WA DHAMBI(WARUMI 7:17-19).Mungu alikusudia utatu mtakatifu ndani ya mwili wa mwanadamu chini ya uongozi wa ROHO MTAKATIFU.Kinachotafutwa na shetani na wajumbe wake ni MTU-NAFSI ambaye ndiyo KIUNGANISHI cha MTU-ROHO na MTU-MWILI ambao huwa wanapingana(WARUMI 8:6-11).

 58. Milinga,

  Ukiwa na tatizo juu ya moyo, jaribu ujifunze lile neno. Pengine unaweza likuta mahala limeandikwa kama feeling. Ukiweka Neno la Mungu in your feeling, well. Lakini the main signification of “moyo” is “heart” as part of the body.

  Thanks.

 59. Mr Milinga,

  Safi kabisa,

  Kinachokuchanganya ni kipi haswa?

  -Moyo= heart (chukua kamusi yako). Hujue heart ilipo na inafanya nini? Kuna wakati kiswahili chetu kinatumia moyo pahali pa roho. Unapokuta nafasi kama ile tulia utafakari na ujaribu kuweka the correct word.
  -Nafsi ni ndani ya damu, ndiyo uhai wa mwili. Shairi nilitoa, soma vizuri.

  -Roho iko ndani na nje kwani mwili unapokufa unaoza lakini roho inabaki. Biblia inasema wazi kama roho inapigana na mwili.Tukisema roho ni ndani ya mwili tu ina maana mwili ukiharibika au ukikufa na roho itakuwa hivyo. Pili, roho inaishi pasipo mwili, lakini mtu aliye hai akijazwa inafanyika ndani ya mwili. Nafikiri umesikia kivipi roho iko ndani na nje ya mwili. Kuna mambo mengi lakini tunaenda taratibu tu.

  Kusema mwanadamu ana nafsi tatu ni lugha yako tu kwani unasema tena hiyo nafsi ni mwili + NAFSI + roho. Kiukweli nafsi iwe tena na nafsi?????? Mwanadamu, kibiblia, ana sehemu kubwa tatu.

  Asante ndugu yangu, usichanganyikiwe, maswali yako ni mepesi sana.

 60. SHALOM.
  AWALI,NITOE ANGALIZO LA KIMAANDIKO KWA WATU WANAOTAKA KUSEMA MAMBO AMBAYO HAYAPO KATIKA MAANDIKO (SOMA MITHALI 30:5-6, UFUNUO 22;18-19, 2PETRO 1:20-21)
  BIBLIA INASEMA TUSIWE WALIMU WENGI ,MKIJUA YA KUWA TUTAPATA HUKUMU KUBWA ZAIDI (YAKOBO 3: 1) .KABLA YA UONGEA HEBU PIMA UNACHOTAKA KUONGEA NA NENO KAMA VINALINGANA.
  MUNGU NI WA KUABUDIWA,HIVYO MUNGU AMEDHIHIRIKA KAMA BABA,MWANA NA ROHO MTAKATIFU.YESU NI BABA,MWANA NA ROHO MTAKATIFU KULINGANA NA BIBLIA.
  NIMSAHIHISHE NDUGU YANGU Alphonse ziragora KUWA YESU NA BABA SI UMOJA BALI NI MMOJA.HIYO TAFSIRI YA UMOJA IPO KWENYE KISWAHILI SI KIINGEREZA (HOLY BIBLE -KING JAMES VERSION…….ST.JOHN 17:22 “And the glory which thou gavest me, I have given them; that they may be one, even as we are one”.
  MCHORO ULIONESHA HAPO JUU NI YA BARAZA LA NIKEA AMBAO NDIO WAASISI WA FUNDISHO HILI AMBALO HALIPO KATIKA BIBLIA BALI NI THEOLOGIA AMBAYO NI MAFUNDISHO YA AKILI YA MWANADAMU.
  BARAZA LA NIKEA,BAADA YA MUNGU KUWAONESHA WATUMISHI WAKE KUWA NDIO BARAZA AMBALO IBILISI AMELITUMIA KUUA NENO LA MUNGU WAMEBADILI JINA ILI KUWADANGANYA WASIO WATUEULE NA WAMEJIITA BARAZA LA MAKANISA ULIMWENGUNI LAKINI SERA NI ZILEZILE ZA BARAZA LA NIKEA .
  MADHEHEBU YOTE YANAAMINI MCHORO HUO KUWA MUNGU WAKO WATATU,HAKIKA HILI NI FUNDISHO LA KIPAGANI. KUNA TOFAUTI KUBWA SANA KATI YA DHEHEBU NA KANISA.KANISA NI MWILI WA KRISTO NA MADHEHEBU NI MWILI WA SHETANI. MADHEHEBU YOTE YAKO KWENYE BARAZA LA MAKANISA ULIMWENGUNI AIDHA KWA SIRI AMA KWA WAZI. HAYA NI BAADHI TU YA MAANDIKO YANAYOONESHA YESU KUWA NI NANI.
  YESU NI MUNGU (SOMA ISAYA 9:6, YOHANA MTAKATITIFU 1:1-3,…14 , TITO 2:13, MATHAYO 1:23)
  YESU NI MUNGU ALIYEDHIHIRISHWA KATIKA MWILI (1TIMOTEO 3;16)
  YESU NI BABA ( ISAYA 9:6, YOHANA MTAKATIFU 14:7-8, 17:1-26)
  YESU NI ROHO MTAKATIFU ( 2 WAKORINTHO 3:17, WAFILIPI 2:10-11 YOHANA MTAKATIFU 14:16-20, 17:1-26).HIVYO;
  BABA, MWANA NA ROHO MTAKATIFU =BWANA YESU KRISTO
  NDUGU LWEMBE KALISEMA VIZURI ( WAKOLOSAI 3 :17)
  NI KILA MFANYALO KWA NENO AU KWA TENDO, KWA MFANO:
  -MAOMBI (NENO) NI KWA JINA LA BWANA YESU
  -UBATIZO (TENDO) NI JINA LA BWANA YESU KRISTO ( MATENDO 2 :37-39)
  BWANA YESU KRISTO ANAWAITA KONDOO ZAKE KWA AJILI YA KWENDA NYUMBANI.

 61. Mkuu Ziragoza…….umenifanya nitabasamu …kwa kweli nimekenua meno yangu bila kupenda kwa majibu yako……….umenikumbusha wakati nasoma elimu ya msingi kwa zile mithali za kiswahili walizoulizwa jamaa zetu wa kihindi……mtaka cha uvunguni …wao wanajibu ……..nyanyua tanda

  Ubarikiwe

 62. Asante sana Bwana Ziragora kwa majibu yako.

  Ukweli ni kwamba maswali hayo nimeyauliza baada ya kuona kuwa yanafanana na mada ya UTATU wa Mungu.

  Kuna mtazamo kwamba mwanadamu naye ana Nafsi tatu yaani MWILI + NAFSI + ROHO.

  Sasa mimi huwa inanisumbua sana kuelewa. Hata majibu ya Ziragora nayo yamenichanganya zaidi.

  Mpendwa Ziragora amezidi kunichanganya anaposema kwamba:

  1. Roho iko Ndani na nje ya mwili
  2. Nafsi inakaa Ndani ya mwili.
  3. Moyo unakaa Ndani ya mwili. Ndiyo inasambaza damu mwilini.

  Hivi hapo kuna ukweli wa kiasi gani? Inakuwaje roho ya mtu ikae ndani na nje ya mwili wake?

  Pili, inakuwaje Nafsi ikae ndani ya mwili. Kwanza inakaa wapi?

  Kama Moyo ndio unaosambaza damu mwilini inakuwaje sasa, tuseme kwamba Neno Mungu linakaa ndani ya moyo. Kwa nini tunaambiwa sasa tuliweke Neno la Mungu moyoni? Neno la Mungu hukaa moyo gani sasa? Wengine utasikia wakisema kwmba “Linda sana moyo wako kuliko vyote ulindavyo…” Je Moyo unaosemwa ni upi?

  Kama roho inakaa ndani na nje ya Mtu, je tesemapo Mungu aiweke roho ya marehemu pema peponi. Je mtu akifa roho yake ndiyo hutoka mwilini,.

 63. Daka tu lakini siyo condition ya kuendelea kwa mada. Haya ni maswala mengine.

  Naomba kabla mada hii haijaisha kujadiliwa, naomba pia tujadili haya:

  1. Roho ni nini na iko upande gani wa mwili?
  Ndani na nje ya mwili
  2. Nafsi ni nini na inakaa wapi mwilini ?
  Ndani ya mwili.
  3. Moyo ni nini na unakaa wapi mwilini? Na Kuna mioyo aina ngapi?
  Ndani ya mwili. Ndiyo inasambaza damu mwilini.
  4. Mwili ni nini na uko wapi?
  Mwili ni ile inayoonekana zaidi kwa mtu au mnyama.
  5. Akili ni nini na ziko wapi mwilini?
  Akili ni uwezo wa kufikiri, kupanga, … na inakuwa ndani ya ubongo
  6. Dhamira ni nini na inakaa wapi mwilini?
  Dhamira inakaa ndani ya Roho

  Baada ya kujadili hayo hebu jadili pamoja na haya:

  1. Baba (Mungu) anakaa wapi mbinguni? kama utasema ni kwenye Kiti cha enzi, Hicho kiti kiko vipi? Kina ukubwa gani?

  Ndiyo, ni kiti cha enzi. Upana na ukukubwa unajulikana na Mungu Mwenyewe. Ukifanya utafiti kidogo utakuta ni pale pahali patakatifu pa patakatifu pa hema takatifu ya Mbingu. Ukipenda ujuwe kina upana gani ukaulize Biblia na Musa jinsi Mungu alimuambia aijenge hema takatifu kwa mfano wa ile ya Mbinguni.

  2. Mungu Mwana naye anakaa wapi? Kama utasema ni mkono wa kuume wa Mungu Baba, je Mbinguni kuna viti viwili kimoja cha Mungu baba na kingine cha Mungu Mwana?

  Kinachosemeka ni kile kinachoandikwa ndani ya Biblia, yaani mkono wa kuume kwa Mungu. Hailazimishwe viti vingi ili Yesu awe upande wa mkono wa kulia. Pia Mungu hafungiwe mbinguni. Ni pahali pote anapotaka. Yupo pia duniani.

  3. Roho Mtakatifu naye anakaa wapi? Kama utasema anakaa mbinguni anakaa kwenye kiti kipi? Maandiko yanasemaje?

  Anapokaa Baba na Mwana.

  4. Mbinguni ni wapi? Kama utasema ni juu au mawinguni mbali kabisa, je ni kule kwenye nje ya mfumo wa Jua hili (Out of Solar Galaxy) au ni kwenye sayari za mbali?

  Mmoja tu ndiye aliyetoka Mbinguni na kurudi kule, yaani Yesu Kristo. Hakuna mtu anayeweza pafahamu. Ni kwa Imani tunajua tu kama mbingu iko wala si kwa akili zetu.

  Naomba niishie hapo nisiwachoshe kwa leo.

  Pengine uendeleshe ukiuliza kama imani nayo inaishi wapi?

  Thanks my brother.

 64. Ndugu yangu Lwembe,

  Asante kwa kunijibu kiisha mda mrefu kabisa. Nimeona kumbe ulikuwa ukizichunguza hoja zangu, tangu mwanzo wa mada hii; good job my friend!!!

  Lakini unapochanga hoja zote hakikisha umefanya hoja yako kuwa ndefu na ya kujivuruga yenyewe. Lakini nikifahamu kama hii mada siyo mzaha nitajitahidi kwa majibu ili ijulikane kama Ziragora hana contradictions katika yale yote aliyoyasema.
  Kinachokutatiza nimekisema mapema, kumjifunza Mungu na kumjua kabisa kabisa siyo rahisi kwani anapita fahamu zote za wanadamu; ndio maana hata katika yaliyo wazi wewe unaona tatizo. Nitakueleza tu pasipo shairi tena na wakati wowote utahitaji uipate utapewa.

  a) Nilitangulia kusema kama utatu ni lugha ya wanadamu wala siyo lugha ya kibiblia. Unaposoma hoja ya mwenzio tulia, usiisome katika negative idea. Kibiblia ni kwamba Baba, Mwana na RM ni umoja. Biblia inaposema Baba ina maana Baba yupo, inaposema Mwana, ina maana naye yupo, inaposema RM inamaanisha yupo, kwani Biblia yaitudanganye. Sasa kwa hiyo nafikiri ni heri uulize Biblia yako vizuri lakini usikwamie pale kwani niliyosema si mimi bali ni Biblia yenyewe. Distinctives or not (tamko yako mwenyewe), nayo inasomeka kibiblia. Ni hiyo ndo nimekupa shairi zinazoonyesha kama ni Mungu 1 wala siyo miungu 3. Niliyokupa inaonyesha kama ni Mungu mmoja na jina lake katika agano jipya ni Yesu Kristo. Niliendelea kukuonyesha kama ukijisahaulisha Baba, huna Mungu, ukijisahaulisha Mwana huna Mungu, na ukijisahaulisha RM huna Mungu. Rudilia tena hoja zangu utakuta hizo ideas. Mpaka pale haiyamaanisha kama Baba=Mwana=RM, Kinachoweza sikilika ni kwamba Baba+Mwana+RM= Mungu, bila kujali uhusiano wa hizo caracteristics moja kwa ingine.

  b) Distincts na kujitegemea ni tamko zako, ni hila za kugeuza hoja za mwenzio; hainipendezi kabisa kwani umeninukuu ukipindisha hoja zangu kwa jinsi nisingelikuwazia; Mungu akusamehe.
  Mwili usiyo na damu wala uliyo na damu isiyona uhai unaitwa maiti. Damu isiyo ndani ya mwili haiwezi ishi. Na roho inabaki roho tu hata bila mwili na damu(nafsi) . Hivi Mwili Lwembe+Damu Lwembe+Roho Lwembe= Lwembe jinsi unamfahamu, unamsikia, …. Ninaposema Damu Lwembe ni hiyo damu ya Lwembe yenye uhai. Kama ukipinga, wende wakuondoe damu yote kabisa kiisha ufike tena jadili tukuone ukiwa Lwembe. Hence, Hata kwako ni vile tu, una caracteristics tatu, wala huishi hapa duniani ukikosa moja. But distinct, ya kujitegemea, unaitengeneza wewe mwenyewe!!!

  c) Lwembe, usilete ubishi kwa bure, fahamu kama kamwe Biblia haitajipinga yenyewe. Tafuta namna ipasavyo ili uelewe somo. Shairi ya biblia haibomolewi na ingine ya hiyo Biblia. Mungu akisikia damu iliyomwagwa ikilia siyo ishara. Kwake hata miti inaimba na mawe yanaweza msifu, mtoto tumboni mwa mama yake anapewa upako wa RM, …. Mungu alihitaji Abeli aishi, sasa unaona akiisha pigwa na kupoteza damu, akafa. Hiyo damu hai ndiyo inampa mtu au mnyama uhai hapa duniani. sasa unafikiri Mungu alipendezwa na kumwagwa kwa hiyo damu? Na kama hakufurahi ina maana amesikia kilio cha nafsi(damu).

  d) Kwa neno ELOHIM, nenda shuleni bwana, hujue unachokisema. ELOHIM ni kusema MUNGU katika kiebrania wala siyo jina na siyo hadithi. Hata leo Biblia zinazonukuu maneno makubwa makubwa ya biblia kwa lugha ya kiebrania zinasema tu ELOHIM pahali pa Mungu.
  Notice: sikusema NAFSI za miungu, hiyo ni kauli yako. Lwembe try to be serious!!!

  Wakati Yesu alikaribia kufa akasema ELOH, ELOH, …. , nafahamu unajua ina maana gani! Katika kiebrania unapotia IM unafanya uwingi (ELOHIM).

  Homework to Lwembe: Kwa nini Yesu hakusema ELOHIM kama hilo ndilo jina la Mungu?

  e) Unauliza “Pia Mwa 3:22 haina tofauti na Mwa 1:26, labda nikuulize tena huyu anayeongea ktk vifungu hivyo ni nani, Baba au Mwana au ni RM? ”

  Jamani umeisoma ukakosa jibu? Mimi nilipoisoma niliona wazi kama ni Mungu mwenyewe. Ukitaka uliza kama ni Baba, Mwana au RM, ungeliuliza namna ingine. Ni caracteristic haswa ya Mungu iliyojumuika?
  Tulia nikufundishe: Kila nafasi unaposoma “Mungu akasema”, fahamu kwamba ni Neno lake limehusika, Unapoona Biblia inasema akafinyaga udongo, hapa huoni tamko yoyote, unaona tu action; hapo ni caractéristic inayoitwa Baba. Kibiblia RM yeye ni mfanyakazi katika ule umungu, anazo kazi nyingi sana, iwemo kumfanya mwenyewe Mungu pamoja na Baba na Mwana, kwani ndiye anaye umilele na utakatifu. Ndiyo maana anaitwa Roho Mtakatifu. Kutoelewa kwako ndiko kunakufanya kujaribu kudanganya kwani hili somo halijifunzwi kwa filosofia au kwa akili za kibinadamu. Ni kwa akili za kibiblia.

  f) Yesu ni Neno la Mungu. Neno likitutoka, na yule RM hayupo. Sasa hawakuwa wawili kwani RM aliwafundisha mitume Neno, yaani ufahamu halisi wa Yesu. Alipokuwa akiwafundisha, aliwakilisha caracteristic ya Mwana na ya Baba. Ina maana palipo Mwana, Baba yupo, na RM yupo, vivyo hivyo. Kama vile palipo Lwembe hai, utakuta pana mwili, damu(nafsi) na roho.

  g)Pia unasema “Halafu hebu nifafanulie zaidi kuhusu hili jambo: “” Kwa mfano, unaposoma katika Mwanzo 2:16-17 na Mwanzo 3:22 utagundua siri ingine ya Mungu. 1) Miti 2 tu ilikatazwa wala siyo miti 3.”
  Hili pia sidhani kama uko sahihi, maana huo mti ktk Mwa2:22 HAWAKUKATAZWA bali WALIZUIWA wasile. Pia kwa taarifa yako, hawakula ule mti unaousoma ktk Mwa 2:17 bali mti wa Mwa 3:3!!”

  Ufafanuzi uko tu palepale unaposoma ukitosha Mwanzo 2:22 uliyoandika bila kutaka. Kukatazwa na kuzuizwa yote ni maneno yetu namely na siyo tatizo. Tunafahamu tu kama ile miti miwili haikutakiwa itumiwe moja baada ya ingine. Lakini MNA SIRI na ninaamini umeigundua kwani swali lako halikuelekea hiyo siri.

  h) Unapoleta swali jaribu kuwa concise ili watu wote wafaidike.

  Ubarikiwe sana.

 65. Naomba kabla mada hii haijaisha kujadiliwa, naomba pia tujadili haya:

  1. Roho ni nini na iko upande gani wa mwili?

  2. Nafsi ni nini na inakaa wapi mwilini ?

  3. Moyo ni nini na unakaa wapi mwilini? Na Kuna mioyo aina ngapi?

  4. Mwili ni nini na uko wapi?

  5. Akili ni nini na ziko wapi mwilini?

  6. Dhamira ni nini na inakaa wapi mwilini?

  Baada ya kujadili hayo hebu jadili pamoja na haya:

  1. Baba Mungu anakaa wapi mbinguni? kama utasema ni kwenye Kiti cha enzi, Hicho kiti kiko vipi? Kina ukubwa gani?

  2. Mungu Mwana naye anakaa wapi? Kama utasema ni mkono wa kuume wa Mungu Baba, je Mbinguni kuna viti viwili kimoja cha Mungu baba na kingine cha Mungu Mwana?

  3. Roho Mtakatifu naye anakaa wapi? Kama utasema anakaa mbinguni anakaa kwenye kiti kipi? Maandiko yanasemaje?

  4. Mbinguni ni wapi? Kama utasema ni juu au mawinguni mbali kabisa, je ni kule kwenye nje ya mfumo wa Jua hili (Out of Solar Galaxy) au ni kwenye sayari za mbali?

  Naomba niishie hapo nisiwachoshe kwa leo.

 66. Dada Janeth,

  Samahani kabisa, labda kwa mfano niliyokupa hukuelewa kwani wakati nilipousoma tena sikuelewa sana ka sababu vidole vimeandika isiyo kweli pale nilipotaka andika “katiba”, nilijikuta nimeandika “katibu”. Sorry !

 67. Kumradhi,
  Ktk kunukuu vifungu nimekosea kidogo hicho kifungu cha mwisho kilipaswa kisomeke hivi:

  “”Hili pia sidhani kama uko sahihi, maana huo mti ktk Mwa 3:22 HAWAKUKATAZWA bali WALIZUIWA wasile. Pia kwa taarifa yako, hawakula ule mti unaousoma ktk Mwa 2:17 bali mti wa Mwa 3:3!!””

 68. Ndg Ziragora,

  Ninakushukuru kwa kunipatia majibu ya maswali yangu, asante sana. Ninajua kwamba umeyajibu kwa uaminifu, hilo ni jema sana na Bwana akubariki!

  Nikirudi katika ujumla wa michango yako, pamoja na huo ulionijibu, kwa kweli nimeshindwa kwa uhakika kuelewa ni nini haswa unachokisema, unaonekana kuzikataa Nafsi Tatu za Mungu kwa upande mmoja, halafu maelezo yako yanajizungusha, tena unafika sehemu unazikubali, halafu unaendelea mbele zaidi unasema hizo Nafsi kivuli chake ni jinsi ya binadamu alivyo; yaani umenifanya niwe na maswali mengi zaidi kuhusu hayo maelezo, usinichoke tafadhali!

  Unasema,
  1. Ninachokifahamu ni kwamba Baba na Mwana ni mmoja na Roho Mtakatifu ni hiyo Roho ya Mungu. It means that the picture shown is not correct.
  -Yohana 10:30 Mimi na Baba tu umoja

  2. Kilicho ndani ya Biblia ni kwamba Baba yupo, Mwana yupo naye ni Neno, na Roho yupo anayetugawia karama, mwalimu, ….

  Unavyoyaona hayo maelezoko, yana uwiana kweli? Unaposema “Baba yupo, na Mwana yupo, na Roho Mtakatifu yupo”; kimsingi unazungumzia uwepo wa THREE DISTINCTIVE PERSONALITIES na ndio sababu umelikataa lile alilolisema Janeth kwamba: Baba=Mwana=RM; ukamwambia umekosea kabisa kwani ni mafikiri yako wala Biblia haikuambie vile. Hapo mwanzo ulisema Baba na Mwana ni mmoja, lakini hapa umewatofautisha tena, na kama si hivyo alivyosema Janeth, basi hao ni nini!!!

  Pia katika kuufafanua huo Utatu wa Mungu kwamba kivuli ni jinsi ya binadamu ukasema:
  “Nikitaja Sungura, nimetaja mtu mmoja. Hii haina tofauti na kusema mwili-nafsi-roho Sungura.”
  Basi nikiyakariri uliyoyasema kuhusu yaliyo ndani ya Biblia kuhusu Mungu kwamba Baba yupo, Mwana yupo na RM yupo; Je, kuhusu Sungura ndio kusema, mwili upo, nafsi ipo, na roho ipo, vyote vikiwa distinct na vyenye kujitegemea, yaani unaweza ukawasiliana na mwili, au nafsi au roho separately na vyote ni Sungura!!!

  Pia umesema kwamba nafsi ni damu, ukanukuu Law 17:14 inayozungumzia uhai wa mnyama, hiyo damu yake ni moja na uhai wake; sijajua umelitoa wapi hili jambo la kwamba damu ndiyo nafsi, Mwa 4:10 “Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi”! Labda nikuulize pia, Adamu aliyeumbwa hapo Mwa 1:26, nini tofauti yake na huyu aliyefinyangwa Mwa 2:7?

  Kuhusu Mungu kuwa Elohim, hilo ni jina lake kabla HAJAUMBA, na kabla ya kuumba hakuwa Mungu, alikuwa ni “The Self Existent” na vyote alivyoviumba vilikuwa bado viko ndani yake, hence kujitambulisha ktk wingi wa hizo attributes zake na si NAFSI za miungu! Alipoumba, ndipo akawa Mungu kwa hao aliowaumba!

  Pia Mwa 3:22 haina tofauti na Mwa 1:26, labda nikuulize tena huyu anayeongea ktk vifungu hivyo ni nani, Baba au Mwana au ni RM?

  Na Ktk Mt 28:20 anasema, “… na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari. Je, hapo Kristo anaposema YEYE atakuwa pamoja nao, ndio tuseme Roho Mtakatifu naye alipowashukia wakawa wote wawili na Mwana ndani ya mitume, au ni vipi?

  Halafu hebu nifafanulie zaidi kuhusu hili jambo: “” Kwa mfano, unaposoma katika Mwanzo 2:16-17 na Mwanzo 3:22 utagundua siri ingine ya Mungu. 1) Miti 2 tu ilikatazwa wala siyo miti 3.”
  Hili pia sidhani kama uko sahihi, maana huo mti ktk Mwa2:22 HAWAKUKATAZWA bali WALIZUIWA wasile. Pia kwa taarifa yako, hawakula ule mti unaousoma ktk Mwa 2:17 bali mti wa Mwa 3:3!!

  Kwa leo niishie hapa nikiusubiri ufafanuuzi wa hayo machache.

  Gbu!

 69. Dada Janeth,

  Unasema,
  “”Wandugu zangu katika Kristo!! Je nikifupisha tu kwa kusema kuwa Baba ni Mungu ambaye ndiye huyo huyo Yesu na Mwana ni huyo huyo Yesu na Roho Mtakatifu ni Roho wa Mungu ambaye Mungu ndiye huyo huyo Yesu je nitakuwa nimekosea??????””
  HAUJAKOSEA, 1Yn 5:8 “Kwa maana wako watatu washuhudiao mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni MMOJA”

  Heri wewe Janeth; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yako aliye mbinguni!!!!

  Hayo ndiyo mafumbo ya Mungu anayafunua ili “wakapate utajiri wote wa kufahamu kwa hakika, wapate kujua kabisa siri ya Mungu, yaani, Kristo” Kol 2:2

  Tazama, Wayahudi walikuwa na Torati na manabii. Kulingana na mafundisho kutoka ktk rejea hizo, wao waliishi ktk tegemeo la ujio wa Masihi, ambaye kiuhusiano walijua kwamba huyo ni Mungu ktk mwili. Na walijua kuwa ajapo, mambo yatabadilika, sadaka zitakoma nk. Nayo mafundisho yao yaliwaelekeza jinsi ya kumtambua Masihi ajapo; viwete watapona, vipofu wataona na atazijua zile siri za mioyo yao nk; ndio kusema ktk umbali wote walioishi, tangu kuumbwa kwa uhai, hakuna kiwete wala kipofu aliyewahi kuponywa, wala hakuna aliyewahi kuwasoma siri za mioyoni mwao isipokuwa atakapofika Masihi.

  Ishara zote hizo zilifanywa, Kuhani mkuu, huyo anayeyasimamia mambo hayo, pamoja na jopo lake la Walawi wenzake, hawakujua kabisa kwamba Masihi amewafikia, licha ya kuziona Ishara zote; wao wakamwita Belizebub! Lakini mwanamke wa mtaani, yule Msamaria, alipokutana naye hapo kisimani, kwa ishara moja tu, aliruka akaibwaga ndoo yake ya maji, akatimua mbio mjini na kuwatangazia kwamba upesi waende wakamuone Masihi, amewafikia yule waliyemngojea vizazi vyao vyote leo yuko hapa, Mungu ametufikia!!!!

  Ndivyo yalivyo mambo ya Mungu; “… Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga.”

  Ninaamini kwa jambo hili, Biblia yako imekuwa wazi zaidi, bila shaka sasa ni Mpya, basi na tuendelee kujifunza, hata tuufikie ukamilifu ktk Kristo!

  Gbu!

 70. Dada Janeth,

  Baadhi ya wanadamu tunabaki na majina yetu pengine tangu utoto hadi uzee. Lakini Mungu sivyo. Mungu siyo Jina. Tulipewa Jina na hilo jina ndilo Yesu Kristo. Hilo jina lina mamlaka mbinguni, duniani, na chini ya dunia, kwa jina hilo kila goti lipigwe na kila ulimi ukiri ya kuwa Yesu ni Bwana(Wafilipi 10: 9-11).
  Jina hilo, siyo kusema Mwana, kwani utazunguuka hutapata lingine la baba au la RM katika agano jipya hata katika Biblia yote.
  Ni jina tulilopewa kama jinsi zamani walipewa jina kama Jehovah, na mengine.
  Lakini jina hilo halitufundishe uhusiano kati ya Baba-Mwana-RM.

  Pili, Unaposema Baba=Mwana=RM umekosea kabisa kwani ni mafikiri yako wala Biblia haikuambie vile. Ni vema zaidi kwako kusema kama hili jambo limekupita ufahamu kuliko kayasema yasiyo ndani ya Biblia.

  Kilicho ndani ya Biblia ni kwamba Baba yupo, Mwana yupo naye ni Neno, na Roho yupo anayetugawia karama, mwalimu, ….

  Nataka niongee kama kawaida ya wanaadamu kwani tupo tu katika dunia. NInaleta mfano wa kampuni. Kinachofanya kampuni ni “Director”, “katibu inayoongoza kampuni”, na “mkusanyiko wa wafanyakazi wanao ujuzi mbalimbali”. Hebu jiulizeni, kimoja kati ya vile nimetaja kikikosekana, kampuni iko? Kwa kuangalia utawaza kama Director ndie wa maana, lakini bila katibu, kampuni yaipo. Pengine tuseme kama katibu ni ya maana, lakini bila wafanyakazi kampuni haitumike

  Kwa mfano huu, pasipo kusahau mifano ya kibiblia tuliyoileta, ni rahisi kwa kiasi kufahamu kinachoendelea katika uhusiano kati ya Baba-Mwana-RM. Baba yupo na anatenda vyote kwa Neno. Mwana ndiye Neno na ndiyo hiyo katiba inayoongoza vyote, iliyoamuru kwamba mitume watapokea RM, na RM anatenda kazi nyingi na hata mojawapo ni kumpa Mwana nguvu.

  Tumesikia biblia inatueleza kuna Roho saba, pengine zaidi. Hii inamaanisha idadi ya wafanyakazi, tukijua kama mkusanyiko ya wafanyakazi inaitwa mfanyakazi.

  Dada Janeth, barikiwa sana. Nafurahi sana kwani hatuwapati wadada wengi wanochangia mada. Uko shujaa.

 71. Ndugu Sungura,

  Nadhani tayari umefurahi kwani ulipokuwa ukiniandikia kumbe nilikuwa nikimjibu Ndugu Lwembe kwa heshima kabisa.

  Tunapoongea, ninapata fursa ya kusema kama kumjifunza Mungu na kumuelewa kabisa kabisa haiwezikani kwani anapita ufahamu wa akili zote za wanaadamu. Tunamjua tu kwa kiwango anachokiachilia kulipitia Neno lake.

  Kwa mfano, unaposoma katika Mwanzo 2:16-17 na Mwanzo 3:22 utagundua siri ingine ya Mungu. 1) Miti 2 tu ilikatazwa wala siyo miti 3. 2) Adamu na Hawa walipokula tunda la mti moja, Mungu akasema wazi kama “binaadamu amekuwa kama mmoja wetu…” akaendelea akasema “Lazima kumzuia kula lile tunda la mti wa uhai kwani akilila ataishi milele”. Katika hii tafsiri ya Mungu, mti mmoja ulidhihirisha umungu kiwango fulani ambacho hakiambatane na kuishi milele. Mti ingine ilidhihirisha umilele wa Mungu. Hapa tunaona caracteristics mbili za Mungu:”Ufahamu halisi wa mema na mabaya” na “umilele”. Ifikapo katika ulimwengu wa roho kwa kiwango Mungu anachokitaka kwa wakati wake, utaona Yesu akisema Yeye na Baba ni mmoja, ina maana wako na caractéristic moja. Kinachotofautiana ni namna ya kujitambulisha tu; Roho wanayo pia inayowafanya jinsi walivyo ndiyo umilele, kwani hakuna roho inayokufa.
  Pia Yesu anaposema NITAWATUMIA Msaidizi, tufahammu kama yule ndiye anawapa umilele wote walioliamini jina la Yesu.

  Kifupi changu ni hiki: utatu sawa jinsi watu wanaoutumia siyo kitu cha kugusika. Ni sawa caractéristics kubwa kubwa zipatikanazo ndani ya Mungu mmoja. Kusema nafsi tatu, utatu, … ni tabia ya maneno yetu wanaadamu, lakini siyo lugha ya biblia
  Asante, naamini umeelewa.

 72. Lwembe, Kamugisha, Mungu awabariki sana sana !!

  Ninanukuu kutoka kwa Kamugisha!!
  Samahani si kwamba ninaiacha mada ila kuna mambo mengine nimeyasoma humu kwenye mada nikaona niingie na mimi moja kwa moja kabla sijapitwa na msomo ya UBATIZO.

  “”Sasa ninaomba kwa kadiri ninavyoongozwa na Roho Mtakatifu nieleze kidogo
  kuhusu suala la watumishi kuwabariki watu kwa jina la BABA, na MWANA,
  na ROHO MTAKATIFU.MATHAYO 28:19 inasema ” BASI, ENENDENI, MKAWAFANYE MATAIFA YOTE KUWA WANAFUNZI,MKIWABATIZA KWA JINA LA BABA, NA MWANA, NA ROHO MTAKATIFU”. Mwisho wa kunukuu.
  Kweli neno limetuamuru kuwabatiza kwa Jina la Baba hilo jina ni lipi?? baba hana jina?? hapo naomba mnifafanuliwa kidogo.

  Hebu tusome Mdo 19:2 – 5, akawauliza, je! mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakajibu, La, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusika. Akawauliza mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema, Kwa ubatizo wa Yohana. Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani Yesu. Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu,
  Lwembe !! Ni kweli ulivyosema kwa habari ya sala ya toba sijaona kabisa kwenye Biblia. Watu wametoa wapi hayo mambo ya kusema tuwaongoze sala ya toba??? Au ndo mapokeo ya watu binafsi???

  Ina maana ukishamwamini Yesu tiyari umeshapata ondoleo la dhambi: Kama anavyosema katika Mdo 10:47 – 48: AKATUAGIZA TUWAHUBIRI WATU NA KUSHUHUDIA YA KUWA HUYU NDIYE ALIYEAMRIWA NA MUNGU AWE MHUKUMU WA WALIO HAI NA WAFU. HUYO MANABII WOTE HUMSHUHUDIA YA KWAMBA KWA JINA LAKE (YESU) KILA AMWAMINIYE ATAPATA ONDOLEO LA DHAMBI.

  {AMEKIRIMIWA JINA LIPITALO MAJINA YOTE – YAANI JINA LENYEWE NI YESU}

  Mdo 2: 37: Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.

  Mdo 10:47: Ni nani awezaye kuzuia maji, hawa wasibatizwe, watu waliopokwa Roho Mtakatifu vile vile kama sisi? Akaamuru wabatizwe kwa Jina lake Yesu Kristo.

  Wandugu zangu katika Kristo!! Je nikifupisha tu kwa kusema kuwa Baba ni Mungu ambaye ndiye huyo huyo Yesu na Mwana ni huyo huyo Yesu na Roho Mtakatifu ni Roho wa Mungu ambaye Mungu ndiye huyo huyo Yesu je nitakuwa nimekosea??????

  Mungu awabariki sana
  Asanteni kwa mufundisho tuendelee kufundishana
  Nawashukuru sana Ziragora, Lwembe, Kamugisha,Mhina John, Sungura, Yona, Fralugg, Millinga na Mdalingwa. TUENDELEE MBELE

 73. dah..hapana. Naombeni na mimi niweke hapa kumbukumbu ya mchango wangu, halafu niwaache ili muendelee.,..,.Mimi ninaamini kua, Baba ndiye Mungu muumba wa mbingu na vitu vyote hapa duniani. Nayo roho mtakatifu ni uweza wa uungu wa Baba au kipawa chake, katika kufanya mapenzi yake, mahali popote, kwa mtu yeyote, kwa hiyo, roho mtakatifu wa Mungu ni Mungu mwenyewe ndani ya utendaji wake. Kwa mfano, wakati wa uumbaji wa Dunia, Soma(Mwanzo 1:2-3). Pia kwa mfano, katika usaidizi wa kiroho kwa watakatifu wake, Soma(yohana 14:26). nk. Naye, Yesu kristo ni Mwana wa Mungu aliyekuja duniani katika mwili, ili kumfunua Baba na kufanya mapenzi yake, akimdhihirisha Baba kwa tabia yake ya uungu na vipawa vyake ili tuweze kumuanini. Soma(2 Petro 1:3-4) (Yohana 1:18). Bwana yesu, aliwaambia wayahudi hivi” ……KWA KUA, BABA AMPENDA MWANA, NAYE HUMUONYESHA YOTE AYATENDAYO MWENYEWE, HATA NA KAZI KUBWA ZAIDI KULIKO HIZO ATAMUONYESHA, ILI NINYI MPATE KUSTAAJABU, MAANA KAMA BABA ANAFUFUA WAFU NA KUWAHUISHA, VIVYO HIVYO NA MWANA AWAHUISHA WALE AWATAKAO, Soma(Yohana 5:19-22). Kwahiyo basi, kwa kua Mungu wetu ni mmoja, nayo roho mtakatifu ni uweza wake au kipawa chake cha utendaji, na pia, kwa kuwa mwanae ni neno lake katika tafsiri ya mbinguni, basi tunaona ya kua, ni sahihi kabisa kwa tafsiri za mbinguni kuonekana hivi” BABA + NENO LAKE + ROHO WAKE = MUNGU MMOJA !!, Soma(1Yohana 5:8). Lakini katika tafsiri ya hapa duniani, kwa kua, neno alifanyika mwili, akawa ni mwana wa Mungu, basi ushuhuda wetu pekee aliotuandalia Baba yetu wa mbinguni ili tuushuhudie kwa watu wote ni huu kwa tafsiri ya hapa duniani ” ROHO + MAJI + DAMU = MMOJA KWA HABARI MOJA YA UFALME WA MUNGU YA KUA, YESU NDIYE MWANA WA MUNGU !!. Soma(1Yohana 5:9). Huu ndiyo ushuhuda mkuu kwetu na uzima wa milele ya kua, Mungu alimtuma mwanae kuja kutengeneza kanisa lake. Soma(Yohana 17:3). Kivipi?….ushuhuda huu ni kwamba, huyo roho ndie kweli na kweli hiyo ni neno la Mungu alilotuachia bwana yesu. Nayo, maji + damu ni kwa ajili ya ubatizo wa imani na utakaso, ndiyo maana biblia inasema hivi kuhusu kifo cha bwana yesu pale msalabani” LAKINI ASKARI MMOJAWAPO ALIMCHOMA UBAVU KWA MKUKI, NA MARA ” IKATOKA DAMU + MAJI !!!. Soma(Yohana 19:34). Kwa hiyo,jina la Mwana wa Mungu ndilo ni Muhimu kwa imani yetu, kwa sababu, ndilo jina ambalo Baba yetu wa mbinguni alimshuhudia mwanae kwa kazi hizo tulizoziona, na tena tukiomba kitu chochote kwa Baba yetu wa mbinguni kupitia jina hilo la mwanae, basi na yeye atayasikia na kuyakubali maombi yetu kwa sababu alikwisha kumuweka huyo mwanae ili awe mpatanishi wetu kati yake na sisi kwa ajili ya utakatifu wake.Soma(yohana 14:13-14). Hapo haiwi tena ni mambo ya utatu kama wengine walivyoaminishwa, ila inakua ni kitu tofauti kabisa kama ifuatavyo: “kuomba kwa jina la Baba, ni kutambua uwepo wa Mungu mmoja Yehova muumba mbingu na vitu vyote, mkuu wa chanzo cha nguvu zote. “kwa jina la mwana, ni kuomba kwa kupitia jina la Mwana wa Mungu akiwa ndiye mpatanishi na muombezi wetu mbele za Baba yetu wa Mbinguni ili ayakubali maombi yetu kwa thamani ya jina la mwanae aliyemshuhudia kwetu. “kwa jina la roho mtakatifu, ni kuutambua uweza wa Mungu na vipawa vyake kua, atatusaidia katika roho zetu, tuombe sawa sawa na mapenzi yake. Endeleeni na mijadala yenu wana wa Mungu ili tuchanganye mawazo na kujifunza zaidi kwa kua, sisi sote bado ni wachanga kiimani ila tunachangia mawazo kama viungo, tukiujenga mwili mmoja wa kristo ambao ni kanisa lake. MBARIKIWE SANA.

 74. Asante Lwembe kwa tafakuri yako,
  hapo ilipoandikwa kitabu cha enzi ndiyo ilivyopaswa isomeke,kitabu cha uzima sikukopi toka biblia moja kwa moja samahani kwa usumbumbufu uliowafika.

 75. Ndugu Lwembe,

  Nakufurahia sana kwa makala yako yaliyo wazi kabisa katika lile unaloniuliza.
  Nami nitajaribu kwenda taratibu kwa kukujibu.

  1) Tafsiri ya utatu jinsi inaonekana katika Biblia niliyoisoma niliileta katika makala yangu ya 03/10/2014. Wala sikuona umuhimu wa kuandika mengi. Nililolileta baadaye ni neno ambalo halishughulikiwe licha ya kuwa ndilo naona liko kivuli cha ule utatu unaosemwa na watu kwani hii siyo lugha ya biblia. Hata hivyo, inatumiwa tu kwani tunayoyatamka yote hatusemi neno kwa neno yaliyomo ndani ya biblia lakini kila mara mwanadamu anatafuta neno analodhani litasikiwa kirahisi.

  2) Huwo msitari(Mwanzo 2:7) unaoleta si sawa kabisa pia unajulikana na baadhi ya wasomaji wa Biblia. Kinachojificha humo ndani ni kwamba haionyeshe vizuri nini nafsi na kwa sababu gani imekuwa hai. Inasema tu nafsi hai. Je myama ana vile vile nafsi iliyo hai?

  Lakini nimeona ni vizuri pia nikutolee hii msitari uijumlishe na hiyo nafsi hai uliyoisoma ili twende pamoja:
  “Walawi 17 :14 14 Kwa maana kuliko huo uhai wa mnyama, hiyo damu yake ni moja na uhai wake; kwa hiyo naliwaambia wana wa Israeli, Msile damu ya mnyama wa aina yo yote; kwa kuwa uhai wa wanyama wote ni katika hiyo damu yake; atakayeila awaye yote atakatiliwa mbali. »

  Nadhani umeona kama nafsi ni damu. Mtu ana nafsi na wanyama wanayo. Hivi tukirudilia kwenye nafsi na mwili, mtu si tofauti ya mnyama. Ina maana kwa mtu na mnyama, nafsi inayokufa ni damu isiyosambazwa na engine (moyo) ndani ya mwili.

  Kinachofanya tofauti ya mtu na mnyama ni hiyo roho ambayo wanyama hawana. Hence, mtu kuwa nafsi, ok iko kama mnyama, lakini kwa kivuli ya ufalme wa mbingu, mtu akatiliwa uhai, ndipo akawa nafsi iliyo hai.

  3) Unaposema hivi “2: Unapozungumzia UTATU, umeinukuu Mwa 1:26 inayosema, “Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu…” kisha kutoka maelezo hayo umetamatisha kwamba hayo yalikuwa ni mazungumzo kati ya Nafsi Tatu za Mungu. “, nadhani hukusoma vizuri niliyoandika. “Tumfanye mtu kwa mfano wetu” haimaanishe utatu bali inamaanisha tu kufahamu Mungu pasipo kufahamu mwanadamu haiwezikani. Kwani kinachoshughulikiwa sana ni kutafuta kumfahamu mtu scientifically bila kuwaziya kumfahamu kibiblia. Hivi kile unachokisema hakifanane na nilichokisema.

  4) Mfano siyo kitu, na picha ya mtu siyo mtu lakini kuna uhusiano fulani. Kwangu, kinachojulikana ni kwamba nina mwili, nafsi na roho. Nikikosa kimoja siko tena Ziragora unaezungmuza naye.

  5) Niongeze tu kwa majadiliano haya kama tunatumia kiswahili lakini siyo lugha kamili ya Biblia. Biblia inatumia lugha za binaadamu mbili tu: kiebrania na kigriki. Sasa ukipenda ufanye utafiti ndani ya lugha ya kiebwania, utakuta huyu Mungu alieumba mbingu na dunia na alietuumba kwa mfano wake maana yake ni ELOHIM na hili jina ni la uwingi. Katika hilo jina tu bila tafsiri ingine, nafsi zinaonekana na ufafanuzi kama ni tatu inafunuliwa zaidi katika agano jipya.
  Pia angalia “Mwanzo 3: 22 Bwana Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama MMOJA wetu, kwa kujua mema na mabaya; na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala, akaishi MILELE;”. Lwembe najua unafahamu kuyatafakari maandiko, go ahead.

  Asante ndugu yangu, niko tayari kabisa kuendelea kukuongelesha iwepo kuna umuhimu.

  God bless you!

 76. Ziragora,

  Tabia ya Mungu kuwa na vikao au kauli za wingi zimedhihirishwa katika matukio kadahaa.

  Kuna wakati kikao kilifanyika Mungu akitaka mtu wa kumtuma kwenda kumdanganya Mfalme Ahab.
  Kama hiyo hadithi isingeendelea tukajua kilichotokea, hapo napo bila shaka mngesema Mungu Baba alikuwa anawauliza Mwana na Roho mt.

  Kuna kikao kilifanyika Mungu akitafuta wa kuja kumfia mwanadamu.

  Lakini wakati Adam anafukuzwa kwenye bustani ya matunda(orchard) Mungu alisema Adam amekuwa kama mmoja wetu. Sasa jiulize kama hapo inamaanisha kuwa Adam alikuwa kama Mungu Baba, au kama Mwana, au alikuwa kama Roho mt.

  Tena kumbuka kwa habari za mnala wa Babel, Bwana alisema ” na tushuke chini tukawachafulie lugha yao….
  Hapo napo unaonaje, alishuka Baba, Mwana, Roho au simply ilikuwa Mungu na delegation ya mbinguni?

  Ndo maana nikasema tusirahisishe sana kwamba hiyo “na tufanye mtu…” kwamba inamaanisha Baba, Mwana, na Roho.
  Tunawahi sana kuamini hivyo kwa sababu tangu tulipoanza kumjifunza Mungu tumeaminishwa hivyo.

  Labda nikutake nawe unidhihirishie kuwa inamaanisha Baba, Mwana, na Roho na si vinginevyo ambavyo wengine tunadhani.

  Kumbuka Yesu ni neno la Mungu lililovaa mwili. Ndio hilo neno ambalo Mungu aliposema “na kuwe nuru” liliondoka likaifanya hiyo nuru.

  Kinachoitwa utatu, just ni udhihirisho wa Mungu alivyoamua kujifunua kwa wanadam.
  Kumbuka kuna roho saba za Mungu sijui na zenyewe ni nafsi au siyo nafsi, maana sijasikia tunasema usaba wa Mungu.

  Tutaumiza akili sana kujaribu kuchunguza uweza wa Mungu.

  Kuna swali umeulizwa na Lwembe pale mwishoni mwa comment yake kwako, ukilijibu itapendeza sana.

  Bless u

 77. Ndg Ziragora,

  Ukitufafanulia zaidi somo hili litatujenga kiimani. Pia ninaamini kwamba umeiona tafsiri ya kiteolojia ya UTATU MTAKATIFU, kama ina kidhi hiyo uliyonayo ni vema la sivyo basi nawe tuwekee tafsiri ya Utatu unayoijua ili tuioanishe na maelezo yako tupate kujifunza zaidi.

  Hata hivyo ktk umbali tuliofika ninapenda kukuuliza maswali machache:
  1: Unasema,
  “Mtu ni mmoja lakini ana mwili, nafsi na roho. Nafsi inapokufa mwili huwezibaki hai, lakini roho inabaki tu. Ndio maana kwa mtu nafsi na mwili ni kitu kimoja na roho inaishi ndani.”

  Biblia inasema hivi:
  Mwa 2:7 “BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.”
  Je, unachosema wewe ndicho inachofundisha Biblia?

  2: Unapozungumzia UTATU, umeinukuu Mwa 1:26 inayosema, “Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu…” kisha kutoka maelezo hayo umetamatisha kwamba hayo yalikuwa ni mazungumzo kati ya Nafsi Tatu za Mungu.

  Basi wewe ukiwa ndiye huyo binadamu uliyeumbwa kwa mfano wa Mungu, unaweza ukatuthibitishia kwamba nawe unazo nafsi tatu zilizo dhahiri ambazo ni tofauti lakini ni Ziragora Umoja?

  Gbu!

 78. Ndg Haule,

  Asante kwa tafakari, Neno la Mungu linapotafakariwa huongeza ufahamu na hivyo kutuimarisha!

  Katika haya uliyoyaeleza, nami nilipoyapitia ktk kuyatafakari, kuna machache ambayo ningeomba tuyatazame zaidi.

  1: Sala ya Toba
  Kimsingi, mimi sidhani kama sala hii ina tatizo, haswa kulingana na maudhui ya inapofanyika, baada ya kipimo cha imani kusimamishwa ili waliohubiriwa Injili wajipime, ndiko kule kuitwa kwao mbele kwa wale wanaopenda kumpokea Kristo, basi muhubiri akiendelea nao katika sala yenye kuiinua zaidi imani ndani yao, kadiri ya uongozi wa Roho mwenye kuyajua mahitaji ya mioyo ya hao, hilo huwa ni jema sana.

  Shida inakuja ktk kuikariri sala hiyo kama liturgia, ndipo na mambo yasiyo husiana na Neno la Mungu hujitokeza kama huko kumuomba Mungu AFUTE jina lako ktk Kitabu cha Hukumu, jambo ambalo wale wanaoujia Ufalme hupandikizwa mioyoni mwao wakiaamini kwamba majina yao YAMEFUTWA ktk kitabu hicho ambacho HAKIPO! Ndipo tunajiuliza huyu mhubiri anaongozwa na Neno la Mungu kweli, kwamba Roho ndiye aliyemshuhudia jambo hilo ambalo haliko ktk Maandiko??

  Kisha unamuona huyo mpendwa aliyempokea Yesu akimshukuru kwa KULIANDIKA jina lake ktk Kitabu cha Uzima siku hiyo, baada ya kulifuta ktk “Kitabu cha Hukumu”; jambo ambalo halina ushaidi wa Maandiko kwamba kuna majina yanayoandikwa ktk Kitabu hicho leo hii, je, kazi yote nzuri aliyoifanya haiingii ktk hitilafu kwa kuuingiza Uongo huo?? Au ndizo hizo “Extra Biblical Revelations” anazoziita ndg Orbi!!!?

  Kuhusu Musa, tunaona alimuomba Mungu awasamehe na kama hawezi basi AMFUTE yeye jina lake ktk Kitabu cha Uzima na si cha Hukumu ambacho Mungu hajawahi kuwa nacho.

  Jibu alilopewa Musa liko wazi pia, kwamba Mungu alikataa kumfuta na akamwambia anawafuta waliomtenda dhambi, ndio hao kundi zima waliofia jangwani kusiko na ufufuo!

  Kuhusu hivyo vitabu na kitabu kingine kilichofunguliwa, Biblia ya SUV inasomeka tofauti kidogo, hicho unachokiita “kitabu cha enzi” huku kinasomeka “kitabu cha uzima”, Ufu 20:12 “Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima…” nayo Zab 69:28 inazungumzia hao kufutwa ktk kitabu hiki, maana ndio kitabu pekee chenye majina, nayo yaliandikwa humo kabla ya misingi ya dunia kuwekwa, hayaandikwi leo unapotubu! Hivyo vitabu vingine vilivyofunguliwa ni vya matendo ya hao waliomo ktk Kitabu cha Uzima, hao ambao hawakuwemo ktk Unyakuo wa hao wasio pitia Hukumu, basi wao watasimama ktk hukumu wakiisha kupita ktk Dhiki Kuu kama tunavyowaona hapo.

  Pia kuna kundi jingine ambalo halikuandikwa majina yao, hilo linaungana na wale ambao majina yao yalifutwa ktk Kitabu cha Uzima, aidha kwa kuongeza au kupunguza ktk Neno la Mungu, au waliomsulubisha mara ya pili Kristo, au waliojitenga na imani wakajiunganisha ktk mafundisho ya mashetani na waliojiingiza ktk ibada za miungu km Freemason nk; hatma yao ndio hii hapa:
  “15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.”!!!!

  Asante sana ndg yangu na Mungu akubariki!

 79. Sungura,

  Mungu alipokuwa akiumba mtu hakushirikisha hilo jeshi unalosisema kwa uumbaji. Sungura, unataka sema kama malaika pengine nao waliumba mtu?

  Pia hukuelewa nilichokisema. Nilichokisema ni kwamba mtu ameumbwa kwa mfano wa Mungu. Sijue kama unakanusha!!!! Pengine wewe hukuumbwa kwa mfano wa Mungu….

  Iwepo mtu ni mfano wa Mungu, utajinyola kichwa kwa kutafuta jinsi Baba-Mwana -Roho MT wanashirikiana kabla hujafahamu jinsi mwili wako na nafsi yako na roho yako wanashirikiana kukufanya wewe Sungura uwe jinsi ulivyo.

  Nikitaja Sungura, nimetaja mtu mmoja. Hii haina tofauti na kusema mwili-nafsi-roho Sungura.

  Asante.

 80. Jaribuni na kurejea mada ile utatu tuliyokwishaijadili, kama moderator alivyoshauri mwanzoni kabisa.

  Ziragora, hiyo tungo “na tufanye mtu kwa mfano wetu” si lazima inalenga utatu. Mbinguni kuna jeshi kubwa tu ambalo wakati mtu anafanywa lilikuwa tayari lipo!

 81. Wapendwa SG
  Naelimika/pata ufahamu kwa michango yenu….inanipa kutafakari zaidi neno la uzima mbarikiwe sana..

  Mimi nilikuwa nataka tuone ni wapi hawa/huyu mtunga sala ya toba alikopata wazo la kutunga hiyo sala ya Toba ambayo Kaka Lwembe ameizungumzia kwa sehemu katika mchango wake, Pia kuna wakati hata Bro Sungura alipata kuniuliza wakati fulani kuhusu hii sala ya toba,Basi nilipa wasaa wa kupitia maandiko ambayo yanaweza kukidhi haja ama lah, Lakini nimeona mantiki ya mtunga sala ya toba.

  Baada ya Israel kuharibu nafsi zao yeye Musa alikwenda fanya upatanishi na Mungu kwa niaba ya Yakobo waliotenda dhambi akiwemo mke wake Sipora na mwanae Gershoni ili Bwana asamehe kosa lao wapate ondoleo la dhambi.

  Nilitafakari mistari hii ifutayo

  Kut 32.30 Hata asubuhi yake Musa akawaambia watu, Mmetenda dhambi kuu; na sasa nitakwenda juu kwa Bwana, labda nitafanya upatanisho kwa ajili ya dhambi yenu.

  32.31 Musa akarejea kwa Bwana akasema, Aa! Watu hawa wametenda dhambi kuu wamejifanyia miungu ya dhahabu.

  32.32 Walakini sasa, ikiwa utawasamehe dhambi yao — na kama sivyo, unifute, nakusihi, katika kitabu chako ulichoandika.

  32.33 Bwana akamwambia Musa, Mtu ye yote aliyenitenda dhambi ndiye nitakayemfuta katika kitabu changu.

  Ufunuo 20:12 “Nikawaona wafu wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi na vitabu vikafunguliwa na kitabu kingine kikafunguliwa ambacho ni cha enzi na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu sawa sawa na matendo yao.”

  Kwa maandiko haya tunaona kuwa kila mtu atapokea ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili kadiri alivyotenda kwamba ni mema au mabaya.Zab 69.28  Na wafutwe katika chuo cha uhai, Wala pamoja na wenye haki wasiandikwe.

  Nikamuona huyo/hao mtunga sala ya toba alikuwa rohoni aliposema/alipoandika “Futa jina ktk kitabu cha hukumu andika ktk kitabu cha uzima”

  Ni Maandiko yanayoruhusu Mtu wa Mungu kuwaombea ndugu wenye dhambi na wadhambi kufutiwa dhambi zao kama alivyofanya Mtu wa Mungu Musa baada ya mahojiana hayo au kusemezana na Bwana.Ni vema kwao wanaombewa kujiweka wakfu(kujiona huu mdhambi na kutubu moyoni mwako)kwa Bwana ili waongozwe kufikia huo utakaso.

  Samahani dhamiri yangu sio kuwaondoa ktk mada lah,Naomba tuendelee na mada husika,Nimeona si vibaya likatutafakarisha na hili nalo ambalo Ndg Lwembe aligusa kidogo.

  Karibu

  Barikiwa

 82. Bwana Yesu asifiwe,

  Mungu awabariki wote kwa kuchangia hii mada.
  Hili suala limefunuliwa tangu Mwanzo, wakati wa uumbaji, Mungu aliposema “Mwanzo 1:26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu…”
  Ndio maana haiombe kufoka sana ili tusikiwe kwani ukiweza kujifahamu wewe mwenyewe utaufahamu ule uhusiano Baba-Mwana-RM. Kipindi kile aliejulikana kirahisi ni Mungu, lakini Yesu akatufunulia mwenyewe kama kuma katika ule Mungu kuna Baba, Mwana na RM.
  Sasa hili silo jambo la kutulazimisha kuita wengine ni wa shetani kwani hata Biblia haikufafanua kwa limoja hilo fumbo.

  Mtu ni mmoja lakini ana mwili, nafsi na roho. Nafsi inapokufa mwili huwezibaki hai, lakini roho inabaki tu. Ndio maana kwa mtu nafsi na mwili ni kitu kimoja na roho inaishi ndani.
  OK, Mungu alisema “tumfanye mtu kwa mfano wetu” lakini hakusema tumfanye mtu awe Mungu jinsi tulivyo. Ina maana kujifahamu siyo kufahamu Mungu lakini anaejifahamu amepata maarifa inayoweza msaidia kwa kumfahamu Mungu.

  Ndio maana kushikana mashati kwa hili jambo ndo upotofu. Mwalimu anaposema Mungu ni mmoja ni kweli kwani ni kama mtu ni mmoja, pia hajamaanisha kama anazikana nafsi hizo tatu. Hence, inategemea focus. Mwengine kwa fundisho hilo hilo anasisitiza juu ya nafsi hizo tatu bila kukana kama ni Mungu mmoja.

  Nina swali kabla tuendelee: Ni nini inayotofautisha mwili, nafsi na roho ya mtu? Na hivi vitatu vinatumikaje ndani ya mtu mmoja?

  Asante.

 83. ONYO KALI KUTOKA KWA MUNGU ALIYE HAI!
  Nilikuwa sijui kwamba Mungu anaweza kutabasamu kwa hasira!ONYO hili linaanza
  na mimi maana siku zote kama ROHO MTAKATIFU akikuongoza kusema au kufundisha jambo ujue anaanza na wewe alafu wengine ndio wanafuatia.Naomba
  tumsikilize Yesu kwa makini”Ni zaidi ya hasara kutaka kujifunza NENO la Mungu kwa mazoea.Mnapoweka mada mezani kwa ajili ya kujifunza inabidi kumtanguliza Roho
  Mtakatifu na siyo kuangalia ni nani anachangia.Bila ya kuingia ndani ya unyenyekevu
  wangu, Roho Mtakatifu hawezi kuwapa ushirikiano wa kulielewa neno la Mungu.Jitunzeni nafsi zenu na mazoea katika kuwaangalia na kuwategemea wanadamu ili LAANA YANGU ISIWAKALIE.Enyi watu wangu mpeni Roho Mtakatifu
  nafasi inayomshahili maana yeye ndiye anaye liongoza kanisa langu”(TAFAKARI-YEREMIA 17:5,1 YOHANA 2:20,27).

  TUZAME NDANI YA UNYENYEKEVU ULIO HAI.
  Naomba kwa unyenyekevu wote yaani katika hekima,maarifa na ujasiri wote niseme
  kwamba Mungu anirehemu.Ninajitahidi kuchangi hii mada ya UTATU MTAKATIFU kadiri ninavyoongozwa na Roho Mtakatifu.ROHO WA BWANA ananifundisha mambo
  mapya kutoka kwenye michango ya watu wengine.Napata utajiri wa ajabu ndani ya
  mitazamo ya neno la Mungu.NI LAZIMA WAKATI WOTE TUWEKE BIDII KATIKA KUSEMA KILE AMBACHO ROHO MTAKATIFU ANASEMA.NA HATA TUNAPOTOA
  MAWAZO YETU BINAFSI,MUNGU HUYADHIBITISHA NA KUYAPINGA ILI YASIFANYIKE SUMU NDANI YA NAFSI ZETU NA ZA WENGINE.Siku zote tunapojadili
  neno la Mungu huwa kuna makusudi maalum ndani yake,ni mpaka tumeyajua hayo
  makusudi ndipo tunaweza kuuona upande wa pili ambao Mungu amekusudia kutupeleka.Na hili linahitaji UNYENYEKEVU WA YESU yaani unyenyekevu usio na
  unafiki.Hebu tusikilize ushauri wa Roho Mtakatifu ndani ya mtume Paulo,ni ushauri
  kwa wateule wa Mungu waliotayari kukua katika kujifunza MAFUNUO YA NENO LA
  MUNGU-WAFILIPI 2:3-4″ MSITENDE NENO LOLOTE KWA KUSHINDANA WALA KWA
  MAJIVUNO, BALI KWA UNYENYEKEVU, KILA MTU NA AMHESABU MWENZIWE KUWA BORA KULIKO NAFSI YAKE.KILA MTU ASIANGALIE MAMBO YAKE MWENYEWE BALI KILA MTU AANGALIE MAMBO YA WENGINE “.Tusipozingatia ushauri huu ni wazi kwamba hatuwezi kuwa na unyenyekevu wa kutaka kujua yaliyomo ndani ya SIRI SABA ZA UPENDO WA MUNGU ikiwemo hii SIRI YA UTATU MTAKATIFU.

  Sasa ninaomba kwa kadiri ninavyoongozwa na Roho Mtakatifu nieleze kidogo
  kuhusu suala la watumishi kuwabariki watu kwa jina la BABA, na MWANA,
  na ROHO MTAKATIFU.MATHAYO 28:19 inasema ” BASI, ENENDENI, MKAWAFANYE MATAIFA YOTE KUWA WANAFUNZI,MKIWABATIZA KWA JINA LA BABA, NA MWANA, NA ROHO MTAKATIFU”.Neno hapa linasema MKIWABATIZA halisemi
  MKIWABARIKI! Kwahiyo inabidi tujue tofauti kati ya kuwabatiza na kuwabariki.Na pia
  inabidi tuangalie kwa muongozo wa Roho Mtakatifu ndani ya neno la Mungu kama tunaweza kuwabariki watu
  kwa jina la BABA,na MWANA,na ROHO MTAKATIFU.Jambo lingine la msingi ni kwamba UTATU MTAKATIFU unatumiika katika kuwabatiza watu wa mataifa ili wawe
  WANAFUNZI WA YESU kama wengine wengine waliompokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yao.Pia ndani ya maagizo haya ya Yesu tunaweza kuona wazi kabisa kwamba mtu anapobatizwa anakua ameianza safari kujifunza mafunuo kuhusu
  SIRI YA UTATU MTAKATIFU.

  Tunatakiwa tujue ni kwanini tunabatizwa kwa jina la BABA, na MWANA, na ROHO MTAKATIFU.Kwanii tuzibatizwe kwa jina la BABA TU au MWANA TU au ROHO MTAKATIFU TU?Bila shaka wanafunzi walipopewa haya maagizo na Yesu walitakuwa
  waulize undani wa maagizo hayo kama ambavyo waliwahi kumuuliza Yesu kuhusu mamlaka au amri kutoa pepo wachafu na magonjwa yote na udhaifu wa kila namna(MATHAYO 10:1) pale walipojaribu kutumia mamlaka hayo na yakashindwa kufanya kazi .Tunaona jinsi walivyomuendea Yesu kwa faragha na kumuuliza”…..mbona sisi hatukuweza kumtoa” MATHAYO 17:19.Tunaona Yesu anawajibu katika MATHAYO 17:20,21″ ……..kwasababu ya upungufu wa IMANI YENU………lakini namna hii haitoki ila
  kwa KUSALI NA KUFUNGA”.Kwa sasa Yesu anawakilishwa na Roho Mtakatifu kwa hiyo tunapoona hatujapata mafunuo au kuelewa neno la Mungu inabidi TUMUENDEE ROHO MTAKATIFU KWA FARAGHA NA KUMUULIZA MBONA HATUELEWI.Nimevutiwa na jambo alilolisema Dada Janeth(06/10/2014 at 9:31 Am)
  kwamba “………….nimeendelea kusoma majibu ya wengine nayo yamenichanganya,NGOJA NIMWACHE ROHO MTAKATIFU AENDELEE KUNIFUNDISHA ZAIDI” mwisho wa nukuu.

  Pia katika WAKOLOSAI 3:17 tunakutana na changamoto nyingine ambayo inabidi tumuulize Roho Mtakatifu kwa faragha ili atueleze maana halisi ya “NA KILA MFANYALO,KWA NENO AU KWA TENDO, FANYENI KWA JINA LA BWANA YESU,MKIMSHUKURU MUNGU BABA KWA YEYE”.Hapa tunaonyeshwa uhusiana uliopo kati ya jina la YESU na Jina la BABA.Ni uhusiano uliopo kati ya jina la MWANA, na jina la BABA.Maandiko yanasema kila tunapofanya kwa neno au kwa tendo tutumi jina la MWANA huku tukimshukuru BABA kwa ajili ya MWANA.Kwahiyo tunafanya kwa jina la MWANA lakini tunatakiwa tushukuru kwa jina la BABA.Huu ni uhusiano wenye hekima ya kutisha sana.Tukiendelea kuingia ndani ya huu mstari tunaweza kuona kwamba MWANA anamuheshimu BABA na BABA anamuheshimu MWANA!Kama unadhani natania hebu tusome kwa pamoja YOHANA 17:1 “……BABA, SASA SAA IMEKWISHA KUFIKA. MTUKUZE MWANA WAKO ILI NAYE AKUTUKUZE WEWE”.Na mstari 5 Yesu anaendelea kusema ” NA SASA, BABA UNITUKUZE MIMI PAMOJA NAWE, KWA UTUKUFU ULE NILIYOKUWA NAO PAMOJA NAWE KABLA YA ULIMWENGU KUWAKO”.Huyu BABA ni nani ambaye anamtukuza MWANA na MWANA ni nani ambaye anamtukuza BABA? Na wana mahusiano gani na ROHO MTAKATIFU?Je ni nafsi tatu tofauti zinazowakilisha ROHO TATU tofauti au ni ROHO MOJA? HAPA NDIPO SIRI YA UTATU MTAKATIFU INAPOANZA KUNOGA.HAWA WOTE NI MUNGU KWAHIYO INA MAANA KUNA MUNGU WATATU MBINGUNI??AU HUU UTATU(UMOJA) WAO UNA MAANA GANI
  KWETU? NA TUNATAKIWA TUITUMIEJE?(YOHANA 17:21-23).

  Mr.MILINGA ameibua changamoto nzito mno kuliko uzito wa dunia pale aliposema
  kwamba TUKIENDA MBINGUNI HATUTAKUTA VITI VITATU VYA MUNGU WATATU BALI TUTAKUTA KITI KIMOJA TU CHA MUNGU ALIYE HAI!Hii ni changamoto ambayo pengine inaweza kuwafanya malaika,wazee ishirini na nne na wenye uhai wanne waendelee kuinama kwa speed zaidi mbele ya KITI CHA ENZI CHA MUNGU ALIYE HAI huku wakisema”………ASTAHILI MWANA-KONDOO ALIYECHINJWA , KUUPOKEA UWEZA NA UTAJIRI NA HEKIMA NA NGUVU NA HESHIMA NA UTUKUFU NA BARAKA.NA KILA KIUMBE KILICHOKO MBINGUNI NA JUU YA NCHI
  NA CHINI YA NCHI YA JUU YA BAHARI ,NA VITU VYOTE VILIVYOMO NDANI YAKE,
  NAVILISIKIA,VIKISEMA,BARAKA NA HESHIMA NA UTUKUFU NA UWEZA UNA YEYE AKETIYE JUU YA KITI CHA ENZI NA YEYE MWANA-KONDOO,HATA MILELE NA MILELE”-UFUNUO 5:11-13

  Dada Janeth naomba tumshike mkono Roho Mtakatifu alafu twende nae FARAGHA
  ILI ATUELEZE KWA UNDANI ZAIDI SIRI HII YA UTATU MTAKATIFU(1 YOHANA 2:20,27).CK LWEMBE,tuko pamoja ndugu yangu!

  MUNGU ALIYE HAI AWABARIKI NYOTE.SOMO LITAENDELEA.

 84. Dada Janeth,

  Katika sehemu ya kwanza ya maswali yako, majibu uliyoletewa nayaona yamegawanyika ktk namna tatu. Moja ni hilo jibu la ndg Ziragora ambalo naona kama ameishia kwamba Mungu ana Nafsi Mbili yaani Baba na Mwana wakiwa ni Nafsi Moja na RM akiwa ni Nafsi ya Pili; au RM si Nafsi, sijui ni nini, na hivyo Mungu kubakia kuwa ana Nafsi Moja tu – Baba na Mwana.

  Namna ya pili ni hiyo ya Millinga, ambayo inaliweka wazi jambo hili kwamba Mungu ana Nafsi Moja iliyojidhihirisha ktk jinsi Tatu za utendaji wa Baba, wa Mwana na wa Roho Mt.

  Na namna ya tatu ndiyo hiyo inayoonekana ktk michango ya ndg Dickson na Fralugg ambayo inamfunua Mungu akiwa ni mwenye Nafsi Tatu dhahiri zilizo tofauti.

  Huenda namna zikaongezeka, lakini, ninapoiendea ile sehemu ya pili ya swali lako, napenda kusema kwamba, maelezo ya ndg Milinga ndio msingi nitakaolijibia swali hili linalohusu watumishi kuwabariki watu ktk namna hii ya: “”Nawabarikini kwa Jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu””

  Baraka za jinsi hii zinatokana na hilo “Fumbo Kuu la Utatu.” Mtumishi huamini kwamba amekubariki kwa Nafsi zote Tatu za Mungu, yaani ni sawa na manabii watatu kukuwekea mikono ili kukubariki, ninaamini kwamba ikiwa ni hivyo, moyo wako utatulia sana wewe unayebarikiwa; hata mtumishi huyo pia, hulifanya jambo hilo ktk imani hiyo!

  Sasa, hilo ni kwa upande mmoja, upande wa pili huwa ni kuutimiza ukiri wa imani hiyo ya Utatu, kwamba ktk mlolongo mzima wa ibada, hiyo ambayo Yesu ametajwa sana, na wokovu kuhubiriwa sana, ndipo mambo hayo yangehitimishwa ktk jinsi hiyo ya kuwabariki watu katika jina la Baba na Mwana na Roho Mt, na hivyo kuziondoa baraka zote za rohoni zilizoambatana na mahubiri hayo, haswa ktk siku ya leo ambayo jambo hili limewekwa wazi kwa mtu yeyote mwenye shauku ya kumjua Mungu kwa faida ya kumuabudu na kuwa na Fellowship naye.

  Kimsingi, ukimuona mhubiri leo hii anahudumu ktk jinsi hiyo, ni ushahidi wa wazi kwamba hahusiki na Ufalme wa Mungu, ni watu wanaotimiza ajira zao tu, hawana uhusiano wowote na Mwenye Kazi!

  Ni watu wazuri tu, lakini ndio hivyo, walikosa nafasi za masomo ya juu waka opt kwenda Bible School, na wengine walijigundua kuwa wana vipawa, hivyo visivyo na majuto, wakaanzisha huduma zao, nayo mapepo ya dini yanayajua mambo hayo, ndipo huwanyemelea na kuwaongoza nje ya Neno la Mungu!

  Hebu mfikirie huyu mtumishi aliye wahubiri kundi la watu labda 2000, kati ya hao, 1000 wakajisikia ni wenye dhambi wanaostahili Jehanamu, ndipo wakajiwakilisha hapo mbele ili waongozwe ile “sala ya toba”; halafu ungemsikia mtumishi huyo akiwaongoza wamfuatishe hivi:
  “Baba Mungu, nimetambua kwamba mimi ni mwenye dhambi, na kuamini kwamba, Bwana Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zangu msalabani, na akafufuliwa kwa ajili ya kuhesabiwa haki kwangu, Tangu sasa ninakupokea Yesu na kukukubali kama Bwana na Mwokozi wa maisha yangu binafsi. Nakuomba Bwana Yesu Kristo, UNIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU NA ULIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA CHA MWANA-KONDOO, Asante Bwana Yesu kwa kuniokoa!”

  Ni sala nzuri sana, tena inasisimua hata ukajisikia utakatifu; lakini ukimuuliza huyo mtumishi ni wapi Mungu aliposema kwamba wenye dhambi wastahilio Hukumu yake anawaandikaga majina kwenye Kitabu cha Hukumu? Au, hicho Kitabu chenyewe cha Hukumu, ki wapi ktk Maandiko? Hata hicho cha Uzima cha Mwana-Kondoo, ni wapi Mungu alituambia kuwa leo hii anaandika humo majina ya watu wanaotubu? Ni uongo wa dini tu kama huo wa kuwabariki watu kwa “Jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu”, wakiliruka Neno la Mungu lililowazi kabisa, Kol 3:17 “Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu”; ni kipi kilicho kigumu kueleweka hapa kama si msukumo wa roho zilizo nje ya mapenzi ya Mungu zinazojidhihirisha ktk ukaidi?!!!

  Kama alivyosema ndg Dickson, MBWAMWITU waliovaa gozi ya kondoo ni wengi saana, labda tutalitazama jambo hilo vizuri ktk Nuru ya Maandiko, ili kulibaini, tupate na kuzijua hasara za kiroho zinazoweza kuwafika wakristo waliosombwa na mafundisho hayo, maana hakuna mafundisho ya mashetani yanayoweza kumuingiza yeyote yule ktk Ufalme wa Mungu.

  Gbu!

 85. Dada Janeth,

  Nikiyatazama maswali yako, naona yamegawanyika ktk sehemu mbili, moja ndiyo hiyo unayotaka UFAFANULIWE “Yesu ni nani, Mungu na Roho Mtakatifu.”

  Naona wapendwa wanalishughulikia hili kwa ukamilifu kabisa kulingana na jinsi walivyokuelewa, ambavyo inaonekana maswali yako wameyaunganisha na huo mchoro wa UTATU MTAKATIFU hapo juu ambao unasema umekutatanisha!

  Ili mradi umemtaja Yesu, Mungu na Roho Mtakatifu, katika mtiririko mmoja, basi akili za kawaida za wakristo wengi, huishia ktk huo Utatu, na majibu huwa kama unavyoyaona!!! Bali ninaamini kwamba ulitaka ufafanuliwe: 1. Yesu ni nani; 2. Mungu ni nani na 3. Roho Mtakatifu ni nani, kama nimekuelewa vizuri.

  Lakini kwa vile hayo uliyoyauliza yana uhusiano na UTATU MTAKATIFU, na wapendwa wameanza kukutiririshia majibu, ambayo kimsingi yanaweza kukupa jibu la swali lako, hata ikiwa ni kwa sehemu, ktk kulirahisisha jambo hilo, ninakuwekea maelezo ya huo mchoro ili ikusaidie kuwaelewa wapendwa ktk michango yao!

  “”Mchoro unaouona hapo juu unawakilisha Fundisho la UTATU MTAKATIFU ambao unamfunua Mungu ktk zile Nafsi zake Tatu: 1. Baba 2. Mwana 3. Roho Mtakatifu; hili ndilo lile Fundisho Kuu la Nafsi Tatu lakini ni Mungu Mmoja.

  Fundisho hili, wanasema ndilo asili na kiini cha Agano Jipya, linapinga tu kama Agano la Kale wazo la kwamba kuna zaidi ya Mungu mmoja, hata hivyo Agano Jipya kwa udhahiri ule ule linafundisha ya kwamba Baba ni Mungu na Mwana ni Mungu na Roho Mtakatifu ni Mungu, yaani zile Nafsi Tatu.

  Nafsi hizi tatu, si jinsi tatu za Nafsi Moja (mtu mmoja), bali ni Nafsi Tatu dhahiri (yaani watu watatu), zikiwapo hapo katika ushirikiano wa dhati baina yao, na katika uhusiano wa kibinafsi mmoja kwa mwingine. Yaani, Baba si Mwana wala si Roho Mtakatifu; naye Mwana si Baba wala si Roho Mtakatifu; pia Roho Mtakatifu si Baba wala si Mwana; ingawa Baba ni Mungu, na Mwana ni Mungu, na Roho Mtakatifu ni Mungu. Wote Watatu wakisimama kwa kweli katika Umoja wao. Mungu kulingana na Biblia si jinsi ya mtu mmoja tu (one personality), lakini yeye ni Nafsi Tatu, yaani jinsi ya watu watatu (three personalities) katika Mungu mmoja hilo ndilo lile Fumbo Kuu la Utatu.””

  Ninategemea huo mchoro wa “Fumbo Kuu la Utatu”, sasa utakuwa umeuelewa vizuri!

  Punde nitaiendea ile sehemu ya pili ya swali lako ihusuyo mtumishi kuwabariki watu: ”kwa Jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu” ili tuitazame sote tupate kujua uhakika wake kulingana na Neno la Mungu.

  Gbu!

 86. Mr. Milinga,
  Barikiwa kaka nimekuelewa sana nakushukuru na Mungu akubariki,
  Nimeelewa japo nimeendelea kusoma majibu ya wengine nayo yananichanganya, ngoja nimwache Roho Mtakatifu aendelee kunifundisha zaidi

  Barikiwa

 87. unachosema Yona Kayuni ni zaidi ya UKWELI!Jambo ulilolisema ni KWELI,maana
  kuna tofauti ya milele kati ya UKWELI(Maarifa ya wanadamu) na KWELI(maarifa ya Mungu).Kuna tofauti ya milele kati ya UKWELI(elimu ya duniani) na KWELI(elimu ya Neno la Mungu)-YOHANA 17:15-17

  Hebu tusikilize kilio na maombolezo ya uchungu aliokuwa nao Mtume Paulo alipokuwa anatoa unabii wa kile ambacho kingetokea baada ya yeye kumaliza huduma yake na kwenda mbinguni kupumzika,MATENDO 20:28-36″JITUNZENI NAFSI ZENU……..NAJUA MIMI YA KUWA BAADA YA KUONDOKA KWANGU MBWAMWITU WAKALI WATAINGIA KWENU,WASIRIHURUMIE KUNDI, TENA KATIKA NINYI WENYEWE WATAINUKA WATU WAKISEMA MAPOTOVU, WAWAVUTE HAO WANAFUNZI WAWAANDAMIE WAO.KWAHIYO KESHENI MKIKUMBUKA YA KWAMBA MIAKA MITATU USIKU NA MCHANA, SIKUACHA KUWAONYA KILA MTU KWA MACHOZI……….NI HERI KUTOA KULIKO KUPOKEA…………WAKALIA SANA WOTE
  WAKAMUANGUKIA PAULO SHINGONI……….”

  Huu ni unabii wa kutisha sana ambao ulishatimia na unaendelea kutimia kwetu.Mbwamwitu wamevamia ndani ya kanisa la Yesu Tanzania ili kuhakikisha wateule hawafunuliwi SIRI SABA ZA UPENDO WA MUNGU.SIRI YA UTATU MTAKATIFU yaani Mungu Baba,Mungu mwana na Mungu Roho Mtakatifu ambao ni uhalisia wa MUNGU ALIYE HAI,imebaki kuwa fumbo tata kwa wakristo wengi.Na sasa nchi nzima yametapakaa MAFUNDISHO YA MASHETANI.Watumishi wengi wa Mungu aliyehai wanawaongoza watu kwa kutegemea nabii za manabii wa uongo.JAMBO HILI LA AJABU NA LA KUCHUKIZA LINAENDELEA TANZANIA!Mungu anasema wateule wametaka mambo yawe hivi yalivyo kwasababu uwezo wa kuishi maisha salama tunao.Tunalo neno la Mungu ambalo ndani yake kuna MAARIFA YA YESU yanayotuepusha na MAANGAMIZI YA MBWAMWITU(TAFAKARI-YEREMIA 5:30-31,HOSEA 4:6)

  SIRI YA UTATU MTAKATIFU inafunua Hekima ya kutisha mno ya UTENDAJI KAZI WA MUNGU.Tunaposoma kitabu cha YOHANA tunauona huo utendaji kazi na namna ambayo Mungu anajifunua kama BABA,MWANA na ROHO MTAKATIFU.Mungu huyo huyo mmoja anasimama kwa hekima ya ajabu katika nafasi tatu tofauti!ISAYA 9:6 inamtambulisha Yesu kama MUNGU MWENYE NGUVU ambaye ni BABA WA MILELE!Ni mstari ambao watu wa dini fulani wameuondoa ndani ya “BIBILIA YAO”.Sasa hivi kuna makundi ya mbwamwitu ambayo yanatumia BIBILIA ZA SHETANI!Ni bibilia ambazo zimegeuzwa kwa manufaa ya shetani na wafuasi wake ili kuwapotosha wateule.Niliwahi kutembelea kanisa fulani la mbwamwitu nikamuona mtumishi fulani anawapa waumini bibilia yake alafu wanarushwa na kuangukia mbali zaidi ya mita 5!!!Ndani ya ile bibilia kulikuwa na nguvu fulani za giza ambazo kwa mtu mwenye nguvu za Mungu haziwezi kumrusha,kwahiyo yule mtumishi alikuwa anachagua watu wa kuwashikisha ile bibilia.Niliona pia kwa macho ya rohoni kabla ya mahubiri zinarushwa roho za mapepo ya kufunga fahamu za watu ili wasitafakari neno jinsi lilivyoandikwa katika bibilia zao.Ni roho ambazo zinarushwa kutokea madhabahuni………….

  NITAENDELEA KWA UNDANI ZAIDI…

 88. shaloom wapendwa,nawasalimu kwa jina la Bwana Yesu!

  Jibu:Mungu ni mkubwa kuliko sisi na tusitarajie kumuelewa katika kila jambo.Utatu ni jambo gumu kulieleza kwa kina.Hakuna mwanadamu anayeweza kulielewa kwa undani zaidi.Biblia inafundisha ya kuwa Baba ni Mungu,ya kuwa Yesu ni Mungu na pia Roho Mtakatifu ni Mungu.Biblia inafundisha pia kuna Mungu mmoja tu.Ijapokuwa tunaweza kufahamu uhusiano tofauti tofauti wa sehemu za utatu huu ni vigumu kuuelewa kwa akili ya kibinadamu.Hii haimaanishi kuwa si kweli au si maagizo ya biblia.

  Utatu ni Mungu mmoja katika nafsi tatu.Aya za biblia zifuatazo zitatumika kufafanua neno hili.
  1) Kuna Mungu mmoja:kumbukumbu la torati 6:4;wakorintho wa kwanza 8:4;wagalatia 3:20;Timotheo wa kwanza2:5.

  2) Utatu una nafsi tatu,mwanzo1:1; 1:26; 3:22; 11:7 Isaya 6:8; 48:16; 61:1; Matayo 3:16-17; 28:29 wakorintho wa pili 13;14. Katika mwanzo1:1 neno la wingi “elohim”linatumika, katika mwanzo 1:26; 3:22; 11:7 na Isaya 6:8,neno la wingi “sisi” limetumika kumaanisha zaidi ya mmoja halina pingamizi.
  Katika isaya 48:16 na 61:1, Mwana azungumza huku akihusisha Baba na Roho Mtakatifu. fananisha isaya 61:1 na luka 4:14-19 kuona Mwana akizungumza.Mathayo3 :16-17 inaelezea ubatizo wa Yesu. Anayeonekana hapa ni Mungu Roho Mtakatifu akimshukia Mungu Mwana huku Mungu Baba akitangaza furaha yake katika Mwana.Mathayo 28:19,wakorintho wa pili 13:14 ni mifano ya nafsi tatu katika Mungu mmoja.

  3) Nafsi hizi tatu zinzatambulika katika maandiko.Katika agano la kale “Bwana” linatofautishwa na “bwana”(mwanzo 19:24; hosea 1:4). “Bwana” ana “mwana” (zaburi 2:7, 12; methali 30:2-2) Roho anatofautishwa na “BWANA”(hesabu 27:18) na pia kutoka “Mungu”(zaburi 51:10-12). Mungu mwana atofautishwa na Mungu baba (zaburi 45:6-7,waebrania 1:8-9). Katika agano jipya Yohana 14:16-17 ndipo Yesu anazungumza na Baba juu ya kuleta msaidizi, Roho Mtakatifu. Hii ina mana kuwa Yesu hakujichukulia yeye mwenyewe kuwa Baba wala Roho Mtakatifu. Katika kila mahali ndani ya agano jipya Yesu alipozungumza na Mungu Baba alikuwa akizungumza na nafsi mojawapo ya utatu-Baba.

  4) Kila nafsi katika utatu huu ni Mumgu: Baba ni Mungu:Yohana 6:27; warumi 1:7; petro wa kwanza 1:2 Mwana ni Mungu Yohana 1:1,14, warumi 9:5; wakolosai 2:9; waebrania 1:8; Yohana wa kwanza 5:20. Roho Mtakatifu ni Mungu matendo ya mitume 5:3-4; wakorintho wa kwanza 3:16; (anayedumu ndani ni Roho Mtakatifu warumi 8-9; Yohana14:16-17; matendo ya mitume 2:1-4)

  5) Katika mpangilio ndani ya utatu huu, maandiko yanaonyesha kuwa Roho Mtakatifu humtumikia Baba na Mwana na Mwana humtumikia Baba.Huu ni uhusiana wa ushirika wao na wala haupunguzi uungu wa nafsi yoyote ile. Kuhusu Mwana tazama luka 22:42; Yohana 5:36; Yohana 20:21; Yohana wa kwanza 4:14. Kuhusu Roho Mtakatifu tazama Yohana 14:16; 14:26; 15:26; 16:7 na hasa Yohana 16:13-14.

  6) Majukumu ya kila nafsi katika utatu: Baba ndiye aliyesababisha kuwako kwa 1) ulimwengu (wakorimtho wa kwanza 8:6; ufunuo wa Yohana 4:11, 2)ufunuo wa kimungu (ufunuo wa Yohana 1:1) 3)wokovu (Yohana 3:16-17); matendo ya kibinadamu ya Yesu (Yohana 5:17; 14:10). Baba anaonekana kwanza katika haya yote.

  Mwana ni wakala ambaye Baba humtumia kufanya haya 1)kuumba na kustawisha ulimwengu (wakorintho wa kwanza 8:6; Yohana1:3; kolosai 1:16-17) 2) ufunuo wa kimungu (Yohana1:1; mathayo 11:27; Yohana 16:12-15; ufunuo wa Yohana 1:1; 3) wokovu (wakorintho wa pili 5:19; mathayo 1:21; Yohana 4:42).Baba alifanya mambo haya yote kupitia Mwana anayetenda kazi kama mwakilishi wake.

  Roho mtakatifu ndiye anayetumiwa na Baba kutenda mambo haya 1)uumbaji na ustawishaji wa ulimwengu mwanzo 1:26; Ayubu 26:13; zaburi 104:30 2)ufunuo wa kimungu (Yohana 16:12-15; waefeso 3:5; petro wa pili 1:21 3) wokovu Yohana3:6; Tito 3:5; petro wa kwanza 1:2 na 4) matendo ya Yesu 10;38). Haya yote Baba ayatenda kupitia Roho Mtakatifu.

  Baba, Mwana na Roho Mtakatifu si vipande vya Mungu bali kila nafsi ni Mungu . Mungu asiyeonekana kwa macho hawezi kuelezwa kwa usahihi na mwenye kuona kwa macho ya kibinadamu akaeleweka. Lakini katika hali zote tazama Mungu kama nafsi tatu zisizogawanyika kuwa miungu mitatu bali Mungu mmoja tu.”jinsi zilivyo kuu utajiri wa hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki,wala njia zake hazitafutikani! Maana ni nani aliyeijua nia ya Bwana”
  warumi 11:33-34

  Bwana Yesu awabariki nyote!

 89. SIRI ZA MUNGU ZINAFYNULIWA KWA WALE WALIO KUBALI KUNYENYEKEA.

  ANGALIZO ;Unyenyekevu ulio hai ni unyenyekevu wa Yesu(Wafilipi 2:3-8).Kuna unyenyekevu ulio kufa(Wakolosai 2:18) ambao unalenga kuwazuia watu wasipate Maarifa(baraka) ya Mungu.Maandiko yako wazi sana kwamba hakuna anayeweza KUTUFUNULIA SIRI ZA MUNGU NA KUTUFUNDISHA NENO LA MUNGU zaidi ya Roho Mtakatifu(TAFAKARI-1 WAKORINTHO 2:1O,11,1 YOHANA 2:20,27).Roho Mtakatifu anafuatilia kila nukta,hatua,mitazamo na Mafundisho tunayotoa ndani ya hizi BLOG za injili kuliko tunavyoweza kutakafari!Na hasira ya Mungu aliye hai ipo juu ya kila NAFSI ambayo inajaribu kulipotosha Neno la Mungu huku ikiwa inajua na imedhamiria kufanya hivyo kwasababu maalum.Kuna maajenti wa shetani ambao wamejikita ndani ya hizi blog ili kufanya utafiti wa uelewa wa Neno la Mungu miongoni mwa wateule na lengo hapa ni kupanda mapando ya mafundisho ya mashetani ndani ya watu wa Mungu(TAFAKARI-1 TIMOTHEO 4:1).Mteule uwe macho,huu ni wakati ambao KILA PANDO LINALOPANDWA NA WAJUMBE WA SHETANI LINANG’OLEWA(TAFAKARI-MATHAYO 15:13).Roho Mtakatifu anatutoa ujinga ili tuukomboe wakati na kuyajua mapenzi ya Mungu katika nyakati hizi ambazo Neno la Mungu(upendo) linafanyiwa biashara haramu(WAEFESO 5:15-17).

  UTATU MTAKATIFU ni halisi kuliko uhalisia wenyewe na ni utajiri kwa ajili ya wateule walio wanyenyekevu.UTATU MTAKATIFU NI SIRI inayofunuliwa na Roho Mtakatifu peke yake.Hili ni FUMBO LA HEKIMA YA MUNGU inayotisha na zaidi ya kutisha(TAFAKARI-1 TIMOTHEO 3:16,YOHANA 1:1-14).Tukiwa na roho ya KUJITIA UJUAJI
  ambayo ni roho ya uasi iliyojaa kiburi kamwe hatutaweza kufunuliwa siri hii(WATHESALONIKE 1:3-4,MITHALI 11:2).SI KILA MKRISTO YUKO UPANDE WA KRISTO!SI KILA MKRISTO ANAMJUA KRISTO!SI KILA MTU ANAWEZA KUPOKEA NEEMA YA WOKOVU,WENGINE NI MBWAMWITU WALIOJIINGIZA KWA SIRI NDANI YA WOKOVU,NI WATU AMBAO WALIFUNDISHWA UONGO TANGU WAKIWA TUMBONI MWA MAMA ZAO!(TAFAKARI-YUDA 1:3-4,12-13,17-23).Duniani kuna watu wa aina mbili tu,watu wa Mungu na watu wa shetani yaani wenye haki na wasio haki!Walio na rehema na wasio na rehema,watu wabaya na watu wazuri(MITHALI 16:4,MITHALI 14:9,MITHALI 24:16).

  NDANI YA AGANO JIPYA,Roho Mtakatifu ametufunulia SIRI SABA ZA MUNGU na ndani ya siri hizi kumefichwa utajiri na makusudi makuu ya Mungu juu ya wateule wake.Siri hizo ni;
  SIRI YA UTATU MTAKATIFU(1 TIMOTHEO 3:16,YOHANA 1:1-14)
  SIRI YAKE KRISTO(WAEFESO 3:4)
  SIRI YA MAPENZI YA MUNGU(WAEFESO 1:9-14)
  SIRI YA INJILI ILETAYO WOKOVU(WAEFESO 6:19,WARUMI 1:16-17)
  SIRI YA NDOA ZA WATEULE NA NDOA KATI YA KRISTO NA KANISA(WAEFESO 5:32)
  SIRI YA MUNGU YAANI KRISTO(WAKOLOSAI 2:1-3)
  SIRI YA KRISTO NDANI YETU TUMAINI LA UTUKUFU(WAKOLOSAI 1:26-29)
  Hakuna mtu anayeweza kufahamu yaliyomo ndani ya siri hizi bila kufunuliwa na
  Roho Mtakatifu.Hizi ndizo siri ambazo mbwamwitu wanafanya juu chini kwa kuwalazimisha wateule kutoa
  makafara ya damu na ngono katika makanisa ya shetani ili wasizijue.Mbwamwitu wamesambazwa katika kila sekta
  katika maisha ya kila siku ili KUHARIBU AU KUIBA UNYENYEKEVU WA WATEULE.Mtume Paulo alishatuonya kwa machozi juu ya harakati za wajumbe wa shetani(MATENDO 20:29-38).

  INJILI YA UNYENYEKEVU WA YESU NI MOTO ULAO NA DUNIA NZIMA IMESHAFUNIKWA NA HUU MOTO WA MACHO SABA YA MAARIFA YA MUNGU(LUKA 12:49,UFUNUO 5:6,HABAKUKI 2:14).MANABII WA UONGO NA WALIO CHINI YAO WANAENDELEA KUTEKETEA KILA KUKICHA TENA KWA AIBU NA FEDHEA(ISAYA 30:1-3).WENYE MACHO YA ROHONI WANAYASHUHUDIA HAYA(LUKA 12:2).

 90. Mpendwa Janeth Mdogo wangu!

  Utatu unaosemwa hapa ni mafundisho ambayo kanisa limeyapokea toka zama za karne ya tatu. Lakini kusema ukweli mafundisho hayo yanatakiwa kutazamwa upya na kupata usahihi unaotakiwa.

  Ukweli unabakia kwamba HAKUNA KITU KINAITWA UTATU KWA MAANA YA NAFSI TATU. Mungu ni mmoja tu. Mungu hana nafsi tatu kama inavyodhaniwa na wengi

  Kwa kweli ni watu wanapotosha tu kwamba Mungu ni ROHO MT. + MWANA + BABA. Hiyo haina ukweli wa kimantiki bali ni ukweli wa kufikirika tu.

  Ukweli ulivyo ni kwamba huko ni kujichanganya tu. Maandiko yanasema MUNGU NI ROHO. Je, kama Mungu ni ROHO ni nini maana ya ROHO? Kama ni MWANA nini maana ya MWANA? Kama ni BABA ni nini maana ya BABA?

  Ukichunguza yote hayo ROHO MWANA na BABA yana maana moja tu. Hayo ni majina ya au maneno yenye maana ile ile kama unavyoweza kusema; MTU, BINADAMU, MWANADAMU. Yote yana maana ya kitu komoja tu na yana maana moja kabisa. Ni maneno tu.

  Ukisema kwamba ROHO MT. siyo BABA na MWANA siyo BABA wala siyo ROHO ni kujaribu kuwachanganya watu tu.

  Ukweli ni kwamba Mungu ni mmoja ila amewahi kujifunua kwa wanadamu katika njia au namna tatu yaani enzi za ADAM hadi NUHU Mungu alijifunua kwa wanadamu kama BABA.

  Baada ya NUHU enzi za Mussa Mungu kajifunua kwa mwanadam kama MWANA ambapo alikwenda nao wanadamu hadi kwenye kifo cha Msalabani.

  Na baada ya Kifo cha Yesu Msalabani Mungu amejifunua kwetu kama ROHO MTAKATIFU.

  Kwa hiyo ukijaribu kufupisha somo hili utaona kwamba kusema ukweli ROHO MT = BABA = MWANA. Yaani yote yana maana iliyo sawa sawa.

  Kuna watumishi wapendwa wanadhani kwamba ukienda mbinguni utakuta kuna viti vitatu ambavyo vimekaa kwaajili ya MUNGU MWANA, MUNGU ROHO MT na MUNGU MWANA. Halafu wanaamini kuwa kila mmoja amekalia kiti chake yaani BABA amekaa kulia na MWANA ameketi kulia na ROHO MT amekaa sijui kushoto au juu sijui.

  Huku ni kujipotosha tu, ukweli unabakia kuwa Mungu Roho Mtakatifu ni sawa na Mungu Mwana na ni sawa na Mungu Baba. Yote yana maana moja tu ila ni njia za kumtaja Mungu tu.

 91. Ziragora,
  Asante sana ndugu yangu kwa kunifafanulia nimeelewa ila huo mchoro hapo juu umenitatanisha

  Barikiwa sana

 92. Janeth,

  Ninachokifahamu ni kwamba Baba na Mwana ni mmjoja na Rohon Mtakatifu ni hiyo Roho ya Mungu. It means that the picture shown is not correct.
  -Yohana 10:30 Mimi na Baba tu umoja
  -Yohana 14:11 Mnisadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! Hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe.
  -Mathayo 1:23 Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.
  -Yohana 16:7 Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu.

  Ubarikiwe.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s