JAMBO LA AJABU NA LA KUCHUKIZA LINAENDELEA TANZANIA!!(TAFAKARI-YEREMIA 5:20-31,YOSHUA 3:5).

maombiii

HASIRA ya Mungu aliye hai inawaka zaidi ya moto juu ya kanisa la Yesu Tanzania. Mungu anasema wateule wake tumekuwa WAJINGA TUSIO NA UFAHAMU!Tuna macho lakinihatuoni,tuna masikio lakini hatusikii!Na hivi ndiyo anavyoendelea kutuambia;

MMEKUWA NA MIOYO YA UASI NA UKAIDI.HAMTETEMEKI TENA MBELE ZA USO WANGU MIMI NILIYEWEKA MCHANGAKUWA MPAKA WA BAHARI KWA AMRI YA DAIMA ISIWEZE KUUPITA.HOFU YENU KWANGU IKO WAPI??MMEACHA KUNYENYEKEA CHINI YA MKONO WANGU ULIO HODARI,MIMI NIWAPAYE MVUA KWA WAKATI WAKE NA KUAMURU JUMA ZA MAVUNO. MAOVU NA DHAMBI ZENU NDIZO ZINAZOWAZUILIA MEMA MISIYAPATE.

MAANA KATIKA WATUMISHI WANGU WAPO AMBAO WAMEWEKA MITEGO ILI KUNASA KONDOO.MAKANISA YAO YAMEJAA HILA.KWAHIYO WAMEKUWA WAKUU,WAMEPATA MALI,WAMEWANDA SANA,WANG’AA,NAAM WAMEPITA KIASI KWA MATENDO MAOVU.HAWATETEI MADAI YA YATIMA,ILI WAPATE KUFANIKIWA WALA HAWAAMUI HAKI YA MUHITAJI.WATUMISHI WANAUMANA WAO KWA WAO NA KUSHINDANIA FEDHA BADALA YA UTAKATIFU.KWELI IMEACHA KUHUBIRIWA MAKANISANI.MADHABAHU ZANGU ZINAENDELEA KUNAJISIWA NA WAJUMBE WA SHETANI MNAOSHIRIKIANA NAO JE! NISIWAPATILIZE KWA MAMBO HAYA?NA NAFSI YANGU, JE! NISIJILIPIZIE KISASI JUU YA TANZANIA? MANABII WANATABIRI UONGO NA WATUMISHI WANGU WANATAWALA KWA MSAADA WAO NA WATEULE WANGU MMEPENDA MAMBO YAWE HIVI KWASABABU UWEZO WA KUSIMAMA KATIKA NAFASI ZENU MNAO.NANYI MTAFANYA NINI MWISHO WAKE?MAANA MNAENDELEA KUANGAMIA KWA

KUKOSA MAARIFA WAKATI MAARIFA YAPO NDANI YA NENO LANGU.MIMI NINAYEISHI MILELE NA MILELE AMBAYE NILIWEKA PUMZI YANGU NDANI YENU SIWEZI KUVUMILIA HUU UJINGA.NINAWEZA KUGHAIRI KUWAPA MAMBO MEMA NA MAKUBWA NILIYOWAANDALIA KWASABABU MMEKUWA VIPOFU NA VIZIWI ROHONI.LAITI MNGEONA KULE AMBAKO NAIPELEKA NCHI HII,NI KATIKA NURU YA AJABU NA YA KUTISHA NI MAHALI PAZURI MNO. KWASABABU YA KUKOSA UNYENYEKEVU MTAHARIBU MAONO YANGU NDANI YA TANZANIA.

JIFUNGENI NGUO ZA MAGUNIA, OMBOLEZENI NA KULIA KWA UCHUNGU KWA AJILI YA HAYA MNAYONITENDA ILI MUIGEUZE HASIRA YANGU NISIJE NIKAWAPATILIZA NA KUWAONDOLEA KABISA ROHO WANGU MNAYEMKATAA.ACHENI UJINGA WA KUONGOZWA NA NAFSI ZENU ZINAZOUFANYIA UPENDO WANGU BIASHARA.ACHENI KUIGA MAFUNDISHO YA MASHETANI,MPAKA LINI MTAENDELEA KUONGOZWA NA ROHO YA SHETANI ILIYOWAJAZA MAARIFA YALIYO KUFA.HUBIRINI INJILI YA UNYENYEKEVU WA YESU NA TOBA.MUDA UNAKWISHA HARAKA KULIKO MNAVYOWEZA KUTAKAFARI…..

 
–Dickson Kamugisha
Advertisements

10 thoughts on “JAMBO LA AJABU NA LA KUCHUKIZA LINAENDELEA TANZANIA!!(TAFAKARI-YEREMIA 5:20-31,YOSHUA 3:5).

 1. mungu atusaidie, mtumishi wa mungu akiubiri kweli anachukiwa na kuitwa shetani, neon la mungu linasema mwanamke avae mavazi yampasayo mwanamke. lakini kwa kutokumuogopa mungu wanawake wanavaa suruali tena za kata k mavazi ya kubana wakati neno linasema mwanamke avae mavazi yanayostiri maungo yake!!!! wengine wanatembea na chupi tu eti amevaa. jinsia za aina moja wanaoana!!!! jamani tumuogope mungu!!!!

 2. Dickson Kamugisha,
  Baraikiwa kwa unabii huo, Ni uhalisia wa kanisa la leo, hakuna tena tofauti ya mtu aliyeokoka na ambaye hajaokoka wote ni sawa, Wachungaji wamekuwa wakihubiri fedha na mafanikio kuliko kuiihubiri kweli ya Kristo Yesu, watu wanatenda dhambi hadharani tena wanajiita wameokoka wala hawakemewi tena eti kwa sababu ana fedha anatoa michango kanisani lakini mtu asiye na kipato akitenda dhambi mara moja anatengwa na kufukuzwa kanisani lakini yule anayetoa michango utasikia” Ooooh ACHENI MAGUGU NA NGANO VIKUE PAMOJA” Jamani ni wapi kanisa la Yesu linakwenda ndugu zangu kweli tutubu na turejee ili Mungu aiponye TANZANIA yetu, si mnaona nchi nyingine vita kila kona???
  Yesu atusaidie jamani

 3. Mpendwa Amos Clement Kishaluli na wengine.
  Mungu aendelee kuwabariki kwa kuijua sauti yake.Kinachotakiwa sasa tuweke
  katika matendo kile tulichosikia.Na hatuwezi kuweka katika matendo kama hatuja
  elewa,kwasababu tunaweza tukajua kwamba ni sauti na ujumbe kutoka kwa Mungu
  lakini tusielewe hatua za kuchukua.Tunaposoma kwa kutafakari ujumbe huu kutoka
  ndani ya MOYO WA YESU uko wazi sana.Tunahitaji moyo wa unyenyekevu ili
  kupokea na kuelewa kile kilicho ndani ya NENO LA KRISTO(MATENDO 17:10-12).Huu
  ni ujumbe kutoka kwa Mungu aliye hai,sio mtazamo wala unabii unaotoka ndani ya nafsi ya mwanadamu.Ni onyo na unabii wa Yesu juu ya TANZANIA.Mimi nimetumika
  kama chombo tu kwa muongozo wa Roho Mtakatifu.1 PETRO 1:19-21 “…..MAANA
  UNABII HAIKULETWA POPOTE KWA MAPENZI YA MWANADAMU BALI WANADAMU WALINENA YALIYOTOKA KWA MUNGU WAKIONGOZWA NA ROHO
  MTAKATIFU” Lakini pia tukae vizuri na Roho Mtakatifu kwasababu KUNA UJUMBE
  NA UNABII UNAOLETWA KWA MAPENZI YA WANADAMU WAKINENA YANAYOTOKA KWA SHETANI KWA KUONGOZWA NA ROHO YA SHETANI(MATHAYO 24:24,25).Katika haya ujumbe kutoka kwa Mungu ni dhahiri na ujumbe
  kutoka kwa shetani ni dhahiri( 1 YOHANA 3:10).

  NA HAYA NDIYO AMBAYO YESU ANAMAANISHA KATIKA UJUMBE HUU UNAOTUTAKA TUINGIE KATIKA TOBA YA KUIMBEA NCHI YA TANZANIA.

  Ujembe huu si wa kila mtanzania bali ni kwa ajili ya wana wa Mungu wanaoishi
  Tanzania na nje ya Tanzania.Maana nchi ya Tanzania ni ya Mungu na ameiweka
  mikononi mwa watoto wake.Shetani na wajumbe wake wapo ili kuharibu maono
  na hatima nzuri mno ambayo Mungu aliiweka ndani ya Tanzania kabla ya kuanzishwa
  misingi ya dunia.Mungu alishautangaza mwisho wa Tanzania kabla hajaiumba!(YEREMIA 5:20.ISAYA 46:10).Mungu amekusudia kutupeleka mahali pazuri mno
  ambapo dunia nzima itaishangaa Tanzania lakini ni lazima turudi kwa Mungu kwa
  unyenyekevu katika umoja wetu ambao Yesu alituombea(YOHANA 17:9-26) ili
  nchi ISIANGAMIE MIKONONI MWA MANABII WA UONGO.Huu siyo wakati wa
  kuweka mbele ubinafsi na kuombea umoja wa madhehebu,tunatakiwa kuombea
  umoja wa mwili wa kristo(wateule) uliopo Tanzania na dunia nzima kwa ujumla.Yesu
  alikuja kuvunja madhehebu ambayo kimsingi yanaongozwa na mapokeo ya unafiki
  wa wanadamu na Roho ya shetani(MATHAYO 15:7-9,1 TIMOTHEO 4:1-5).Kanisa la
  kristo (mikusanyiko mbalimbali ya wana wa Mungu) linaongozwa na ROHO YA KRISTO(WARUMI 8:12-17).Mwenye masiko na asikie neno hili ambalo Yesu anaiambia TANZANIA.

  Zaidi ya asilimia 85 ya mikusanyiko ya kuabudu nchini Tanzania ni Madhehebu
  ya mashetani na wana wa Mungu wengi sana wametekwa humo kwasababu
  mbalimbali ikiwemo kutafuta miujiza ya shetani badala ya kutafuta KWELI ya
  Mungu aliye hai.Zaidi ya asilimia 85 ya huduma za kiroho nchini Tanzania ni huduma
  za MANABII WA UONGO.Si ajabu kukuta kusanyiko lenye nembo ya TAG au EAGT
  kwamba ni huduma ya manabii wa uongo ambao wanatumia kivuli cha mwili wa kristo
  yaani kanisa la kristo!’Makanisa mengi ya kipentekoste’ ni kivuli tu cha majina yaliyo
  beba maono ya kanisa la kristo lakini uhalisia ni kwamba yanaongozwa na mashetani
  ambao wanaitwa mbwamwitu au manabii na mitume wa uongo.Hii ni mbali ni zile
  huduma zenye majina yaliyobeba maono mengine ambayo pia yanaendana na
  neno la Mungu!Wenye macho ya rohoni wanayaona haya.Lakini wengi TUMEKUWA
  WAJINGA TUSIO NA UFAHAMU.TUNA MACHO LAKINI HATUONI NA TUNA MASIKIO
  LAKINI HATUSIKII(YEREMIA 5:21).

  Sasa kumekuwa na ushrikiano kati ya madhehebu ya mashetani na makanisa ya Mungu!Watumishi wengi wa Mungu aliye hai wameolewa na fedha na kuikana ndoa
  kati yao na Yesu!Wameacha kufundisha KWELI ya Mungu na kuangalia tamaa zao.
  Hawatetemeki tena mbele za uso wa Mungu,hofu ya Mungu imetoweka na badala
  yake wameimgiwa na moyo wa kuasi na ukaidi na unyenyekevu wa kumtegemea Mungu anayetukirimia kila kitu kwa nyakati na majira yake umekatiliwa mbali.Kwahiyo maovu yao na yetu sisi tulio chini yao YAMETUZUILIA MEMA TUSIYAPATE(YEREMIA 5:22-25).

  Wachungaji waliokuwa wengi wamejiingiza katika hila za kufanya mashindano ya kutafuta fedha na mali.Wameweka uaminifu na utakatifu pembeni.Wanaumana wao
  kwa wao.Wamewanda sana,wang’aa,naam wamepita kiasi kwa matendo maovu.Hawashughuliki tena na mahitaji ya kiroho na kimwili ya kondoo zao.Yatima na wajane wanalia na kusaga meno.Wamejimilikisha madhabahu za Mungu na kuwafanya kondoo kuwa watumwa wao.Je tunadhani Mungu mwenye haki ataendelea kuvumili haya asujilipize kisasi juu ya taifa la namna hii??(YEREMIA 5:26-29).Unadhani Mungu atakuangalia wewe na familia yako au kusanyiko ulilopo kwasababu mnatubu kwa ajili yenu?Wote tumetenda dhambi na kutegemea tabiri za manabii wa uongo waliojaa kila kona na kujitangaza kwenye Tv na redio mbalimbali.Sisi ndiyo tumetaka mambo yawe hivi kwasababu uwezo wa kuyabadilisha tunao(YEREMIA 5:30-31).Tunatakiwa tuwaombee wenzetu ambao wamo katika mikusanyiko ya mashetani.Tunatakiwa tuwategemeze kwa maombi wachungaji ambao Mungu ametuweka chini yao.Tunatakiwa tuombee umoja wetu ili uwe hai tusimezwe na kuchangamana na mbwamwitu.Mbwamwitu wamenajisi madhabahu za Mungu wetu na umoja wetu kwa KUINGIZA ROHO YA UASI.MBWAMWITU WAMEJIPENYEZA NDANI YA MAKANISA YETU.

  NI LAZIMA KABLA YA YOTE TWENDE MBELE ZA MUNGU TUFANYA TOBA ILIYO HAI
  KWA AJILI YA TAIFA ZIMA ILI KUTULIZA HASIRA NA GHADHABU YA MUNGU.NI LAZIMA TUJITAKASE TUONDOE ROHO YA UASI NDANI YA KANISA LA KRISTO.

  Mungu anatuambia katika Yoshua 3:5 “JITAKASENI MAANA NATAKA KUTENDA MAMBO YA AJABU KATI YENU”

 4. Ni kweli kabisa kanisa la leo halitaki mafundisho ya utakatifu limekuwa likifuatisha namna ya dunia wakati neno la Mungu limetukataza katika Warumi 12:2.Ukitaka uchukiwe katika kanisa fundisha viwango vya utakatifu kama neno la Mungu lilivyo unaweza ukashushwa madhabahuni, ni mafundisho ambayo hayapendwi lakini fundisha kuhusu mafanikio kama vile kupata magari, kujenga majumba n.k utapendwa sana. Kinachotakiwa kila mtu sasa ajisimamie mwenyewe kwani siku ya hukumu hakuna kujitetea kuwa kanisa letu au mchungaji wetu hakutufundisha kuwa kitu fulani kuwa ni dhambi kwani kila mtu atahukumiwa sawa sawa na injili ya Kristo. Mbarikiwe.

 5. BWANA MUNGU atusaidie tatizo kubwa leo limelikumba kanisa la mungu ni kutafuta miujiza kuliko kumtafuta mungu…..kutaka baraka za mungu kuliko kuacha na kuchukia uovu…..ivyo kwa sababu hiyo uovu hauondoki kwetu sababu hamna anayetubu (Kuna mafundisho mapya nimeyasikia kwa masikio yangu mwenyewe yaani utakiwi kutubu tena tangia siku ile ya kwanza ulioendeshwa sala ya toba na kumpokea kristo yesu kama BWANA na mwokozi wa maisha yako)…tunaenda wapi mungu atusaidie tusijefikia kama mataifa baadhi ya magharibi majengo ya kanisa kugeuzwa kumbi za starehe……..

 6. Ahsante sana Mtumishi wa Mungu kwa neno ambalo umelitoa kupitia uwezo wa Roho Mtakatifu. Ni kweli kabisa kanisa la sasa tumejisahau kwa kiasi cha kutia aibu mbele na machoni pa Mungu. Leo hii hata vitu ambavyo haviko kwenye maandiko [Biblia], baadhi ya watumishi wa Mungu wanavihalalisha tena kwa macho makavu mbele za waumini kwa lengo la kutetea uovu wao. Ooh ni wakati wa kanisa la Mungu kwenda mbele Mungu kunyenyekea, kutubu na kuziacha njia zetu mbaya na kumrudia Muumba wetu. 2Mambo ya nyakati 7:14

 7. Amen! “With practice, we make theories applicable!” Tatizo siku hizi tumechukulia Neno la Mungu kama siasa, wote mhubiri na muumini ni watenda maovu! Hatutafika popote tusipoweka mahubiri katika vitendo, zaidi ya kumghadhabosha Mungu tu.
  Kama unaona Mungu hajakuita umtumikie, acha kuuishi unafiki. Nakuhakikishia hutoambulia chochote zaidi ya kupoteza wakati wako! Akubarikini Mwenyezi Mungu wale nyote mnaoamini na kumtumikia katika Roho na kweli!

 8. Mathayo 24:12 Na kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa
  Hizi ni nyakati za mwisho.Yote yaliyotabiriwa yatatokea. Pia elewa kabla Yesu Kristo kurudi kutatokea the great falling away( wengi waliokuwa wakidai kuwa ni watu wa Mungu/ waliookoka watakengeuka na kuiacha Imani.
  2Wathessalonike 2:1-3
  1 Basi, ndugu, tunakusihini, kwa habari ya kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, na kukusanyika kwetu mbele zake,
  2 kwamba msifadhaishwe upesi hata kuiacha nia yenu, wala msisitushwe, kwa roho, wala kwa neno, wala kwa waraka unaodhaniwa kuwa ni wetu, kana kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwapo.
  3 Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu;
  KAMA UMEOKOKA BASI USIWAANGALIE WATU. WEWE ANGALIA YESU NA NENO LAKE. TII NENO NA UWE MTENDAJI WA NENO ILI UPONYE ROHO YAKO NA KUWAPA MFANO MWEMA WALE WANAOKUZUNGUKA.
  HIVI UNAJUA WAKATI WA NUHU DUNIA NZIMA ILIANGAMIA WAKAPONA WATU 8 TU? JAMANI KILA MTU AJITAHIDI KUTAFAKARI NENO MWENYEWE NA KULITENDEA KAZI. UOVU NI MWINGI KATIKA DUNIA YA LEO , SASA PONYA ROHO YAKO KWA KUDHAMIRIA KUMTII MUNGU KWA KULIFUATA NENO LAKE WALA SI KIPI WATU WENGI WANAPENDA AU SUPPORT.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s