Kanisa la PAG Bukoba lavamiwa,wawili wakatwa mapanga,mmoja afa papo hapo!!

Katika hali isiyo ya kawaida,watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo wamevamia Kanisa la PAG tawi la Kagemu kata ya Kitendaguro manispaa ya Bukoba na kumua muumini mmoja kwa kumcharanga mapanga hadi kufa na mwenzake kujeruhiwa.hawakuiba chochote ikiwemo simu zao.

Hata hivyo tukio hilo linahusishwa na imani za kidini kwamba waliohusika na tukio hilo ni wapinzani ya dini yao.

Mwandishi wa mtandao wa harakatinews amefika katika eneo hilo na kushuhudia sehemu ya madhabahu ikiwa imetapakaa damu (tazama picha) na imeelezwa na mashuhuda kuwa damu husika ni wakati marehemu na mwenzake walipokuwa wakitaka kujinusuru kutoka kwa wakora hao.

Inaelezwa kuwa hadi wanatendewa kitendo husika walikuwemo peke yao majira ya saa 8 usiku baada ya wenzao kuondoka katika baada ya ibada usiku kumalizika saa 4 usiku hivyo wao waliamua kulala kanisani.

Mtoa habari aliyegoma kutaja jina amesema chanzo cha mgogoro huo na kifo cha muumini ambaye ni mwalimu katika shule ya sekondari KAGEMU ni baada ya marehemu kuoa mwanamke wa dini nyingine (inaifadhiwa) na kumbadilisha dini huyo mkewe na hapo waumini wa dini ya mkewe walianza vitimbwi kwa kanisa hilo na hadi mauaji hayo kumekuwa na vurugu za kila mara baina ya pande mbili.

Polisi bado wanachunguza na watatoa taarifa baadaye,mwili wa marehemu umeifadhiwa katika chumba cha maiti bukoba mjini,majeruhi amelazwa hospital ya mkoa.

Viongozi wa makanisa ya PAG watatoa tamko .

Credit: Harakati News

Advertisements

One thought on “Kanisa la PAG Bukoba lavamiwa,wawili wakatwa mapanga,mmoja afa papo hapo!!

  1. Hiyo ni habari ya kusikitisha sana.

    Wakati wote kitu CHEMA ndicho hushambuliwa. Kushambuliwa kwa Wakristo ni kielelezo kuwa ni IMANI BORA na sahihi kwa mwandamu katika kumtafuta Mungu, muumba wa Mbingu na nchi.

    Mungu na awape faraja wafiwa na kuwatia nguvu wapendwa katka eneo hilo katika kipindi hili cha kujaribiwa. Amina.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s