HUKO BWANA AJAPO – (Yesu Kristo ni yeye yule jana, leo na hata MILELE…

wimbo

Bwana Yesu apewe sifa wanaSG, mada ya MTU ALIYEOKOKA ANAWEZA KUPOTEZA WOKOVU inaendelea hapa, Kaka yetu CK. Lwembe ameweza kuelezea kwa kirefu, naamini tutaendelea hapa. Mungu awabariki

“FUTURE TENSE” – HUKO BWANA AJAPO – (Yesu Kristo ni yeye yule jana, leo na hata MILELE…) – TUTAOKOLEWA

“Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.” MT. ‭24‬:‭13‬

Kifungu hiki cha Maandiko kina apply ktk sehemu mbili, ya kwanza ni ile kabla ya Kuja kwa Bwana kwa ajili ya kulitwaa Kanisa, na nyingine ni kwa wale ambao watapita ktk Dhiki Kuu.

Nitaanza na hiyo sehemu ya kwanza.
Pia nina amini kwamba nitakuwa nimelijibu swali aliloniuliza ndg Mjema kwamba: “”4. Ni kweli kuwa, Mungu aliandaa mpango wa Wokovu tangu kuumbwa misingi ya ulimwengu na yeye ni yule yule Jana, Leo na Milele, sasa wewe, Lwembe ulikuwepo tangu kuumbwa misingi ya ulimwengu ili uhusikane na iyo past?””

Vita yetu ni vita ya Imani, Tunaokolewa kwa Imani, tukimuamini Mungu ktk yote aliyotufunulia, haswa ktk KUCHAGULIWA kwetu kimbele ili kuudhihirisha ushindi aliotukirimia dhidi ya dhambi, ndio ule UTEULE! Efe 1:4 inalifunua jambo hili kwetu, nasi hulipokea ktk Nguvu yake, kwamba, ilimradi Mungu amelinena hivyo, basi limetufikia nasi kufanyika hilo Neno, “… Kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo. Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake”

Yaani Mjema, maana ya kifungu hiki ni kwamba, hao unaowasoma hapo, God has spoken them into existence! Sasa hatuwi hivyo Bwana ajapo, hapana, tuko hivyo toka kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, huko tulikochaguliwa kuwa hivyo, na sasa hivi tunalidhihirisha tu jambo hilo! Ayu 38:4 -7
“Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya nchi? Haya! Sema, kama ukiwa na ufahamu …. 7Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja, Na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha?”
Ulikuwa wapi Mjema ktk wakati huo, au haukuwepo huko ndio maana unatatizika na Utakatifu wa Mungu tuliopewa ili kushinda huku tukingali vitani??? 2Pet 1:3″Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa”!

Hebu fikiri, iwapo tutajiweka ktk kumsubiri ajapo ili atuokoe na Dhambi, basi kulikuwa na haja gani ya yeye kufa pale msalabani; wale kondoo wa kafara si wangetosha mpaka hapo ajapo na kutuondoa ktk dunia hii ya Dhambi, au kuna haja gani ya kutukomboa kisha asitudai kutoka kwa huyo anayetumiliki nasi tukiwa ni mali yake baada ya kutukomboa? Haileti maana hata kidogo!

Mungu alituchagua huko kabla ya misingi ya ulimwengu kuwekwa, akatutayarishia na hilo Neno ambalo kwalo sisi hukamilishwa kulilingania Kusudi lake. Nalo Neno hilo hutukamata tangu siku Nuru ya Injili ilipotupiga, ile mbegu iliyolala ndani yetu, ikachipua hata Tukahesabiwa Haki, kisha tukajengeka ktk Utakaso, Neno la Kristo likikaa kwa wingi ndani yetu, nalo Neno likiwa ndilo Roho na Uzima; basi tulipolinyenyekea na kuambatana nalo, jambo hilo likamfurahisha Mungu naye AKATUTIA Mhuri wake, hata siku ya ukombozi, Ule Ubatizo wa Roho Mt, Efe 4:30. Huku ndiko kukamilika kwa kule Kuzaliwa kwa maji na kwa Roho kunako waingiza hao ktk Ufame wa Mungu!!

Katika hawa HAKUNA anayeweza kupotea, hawa ni kondoo wake, Yn 10:27-28 “Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata. Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu.” Haleluyaaaaaaa, kuna PERFECT ASSURANCE inayoweza kulizidi jambo hili??? Nyie MLIOOKOKA, “pigeni kelele za furaha” mpaka majeshi ya kuzimu yazimie, kuta zianguke kama za Yeriko, na akiwapo Rahabu ktk miji yao na aipandishe Bendera ya Wokovu juu ili Malaika wa kuharibu aione Neema aliyokirimiwa!!!!

Mungu alipofanya Uamuzi wa Kutukomboa, Uamuzi huo ndio ulikuwa Wokovu wetu, kwahiyo haijalishi tulikuwa wafu kiasi gani, au wenye kuyakatia tamaa maisha kiasi gani, bali machoni pa Mungu tulirudishwa ktk Thamani ya Uungu wake tuliyokuwa nayo tangu hapo tulipokuwa Wazo lake, na majina yetu yakaandikwa ktk Kitabu cha Uzima cha Mwana Kondoo ktk ule UTEULE!

Hebu niambieni, Yerusalemu ilipozingirwa na Titus, yule jemadari wa Kirumi, mwana historia aliyeandika habari hizo, Yosephus, anasema WALIOOKOKA walikuwa ni wale cannibals tu; sasa hao ni wakristo waliolipokea lile Neno lililowaelekeza kukimbilia huko milimani watakapoona jeshi likiuzingira mji huo! Basi niwaulize, hao waliokoka lini, walipokimbia au walipolipokea hilo Neno la wokovu wao??? Wale ambao hawakulipokea Neno hilo, au waliolipuuzia hilo kwamba ni u FANATIC kujitoa ndani jiji lililozungushiwa ngome imara na kukimbilia huko maporini kwenye simba, WALIANGAMIA na wengine kuharibiwa maisha yao yote!

Ndipo kwa WATEULE, kwao mishale ya moto inakomea hapo, wanapotiwa Muhuri, kule “… kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka” kunaishia hapo, Shetani anawakimbia, maana anajua kuwafuata hao ni kazi bure Mungu hatamsikiliza zaidi ya kumkemea, hawa ndio huingizwa ktk Utumishi na kuhudumu ktk kanisa, ule ukuhani.

Siyi, Mjema & co,

Tunaendelea….

“Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.” MT. ‭24‬:‭13‬

Kundi la pili linalohusika na Andiko hili ni wale ambao mafundisho ya dini zao yaliwazuia kukifikia Kipeo cha Kujazwa RM, lakini hayakuwaingiza ktk KUFURU, hivyo majina yao kubakia ktk Kitabu cha Uzima, na kila mmoja wao kuwa na Kitabu cha Matendo, hawa wanapita ktk DHIKI KUU na kusimama Hukumuni, wakiwa wameukosa Ufufuo wa Kwanza, huo tunaousoma ktk Ufu 20:4, kwa kukosa Kujazwa RM, yule mwenye nguvu ya kutufufua, na hivyo watabakia makaburini mpaka ktk Ufufuo wa pili!

Ktk Dhiki hiyo kundi hili litashurutishwa liyakubali mafundisho yenye KUFURU, na hao ambao majina yao hayakuandikwa ktk Kitabu cha Uzima na wale ambao majina yao YALIFUTWA, wote hawa wakiwa na Chapa ya yule Mnyama, ndipo wengine watasilimishwa na KUPOTEA, na wengine watayakataa kwa gharama ya maisha yao, wakiling’ang’ania Neno lililofunuliwa kwao kuhusu hayo mafundisho ya Kufuru, wakiyavumilia mateso hata kifo, hawa ndio wanao okolewa huko Bwana ajapo kwa HUKUMU pamoja na hao walio watendea “kondoo” wema, labda waliwasaidia ktk shida zao au waliwatetea, kama Gamaliel, hao ndio WATAOKOLEWA huko MWISHO!!!

Na kuna wengine ambao wanaishi ktk tegemeo hilo kwa uongo wa dini, wakiwa ktk lile kundi lililojitenga na Imani ile waliyokabidhiwa watakatifu, iwaongoze ktk Kweli ya Mungu, lile Neno lake. Hawa ndio wale wenye mfano wa utauwa lakini wakilikana Neno lake kwa kulibadili na mafundisho ya mashetani!

Unapolikataa jambo ambalo Mungu amekufunulia, ni dalili mbaya; Yn 10:26 “Lakini ninyi hamsadiki, kwa sababu hammo miongoni mwa kondoo wangu.” Jichunguze tena moyo wako, uone umesimama wapi! Vita tuliyomo ni vita ya Hila, ukigeuzwa nia ukafikishwa ktk hali kama hiyo, sioni utaondokana vipi na jambo hili:
“Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu, wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri.” (‭Ebr‬ ‭6‬:‭4, 6‬)‬‬‬‬‬‬

Haya yanatokea ktk Hatua hii ya Utakaso, wengi wakikwamia hapo, nafsi nyingi sana zinaangamia ktk hatua hii kwa kuyakimbia Maarifa, majina yao yanafutwa ktk Kitabu cha Uzima! Na ukifutwa, mchezo unaishia hapo, safari ya kuuendea Mti wa Uzima inakomea hapo, unarudishwa Mautini na kusajiliwa kupigana na Imani, nawe kuwa kikwazo kwa hao wauendeao huo Mti wa Uzima!
Ndio lile jeshi kubwa la Kuzimu!!!

Ktk kumalizia, tutalitazama kwa kifupi lile Fundisho la kuwa TUTAOKOKA hapo tutapofika mbinguni, ili tulijue ni nini!

Gbu all!

–CK

Gbu!

Advertisements

81 thoughts on “HUKO BWANA AJAPO – (Yesu Kristo ni yeye yule jana, leo na hata MILELE…

 1. @ Sungura,
  Nashukuru kwa vile wewe katika hili, huna jibu kabisaaaa!! Unaonekana kupigapiga kelele tu. Oooh, mara wasabato walishashinda milimani miaka ya 80’s!! Hilo linakusaidia nini rafiki yangu?? Wewe jibu hoja, kwamba wale wanaomgonja Kristo kwa mara ya pili ni waadventista au siyo?? Jibu hilo tu. Usipate taabu sana kaka.

  @ Lwembe,
  Hebu niambie kama neno Adventist, halina maana ya Kurudi kwa Kristo mara ya pili kwa sasa tofauti na ilivyokuwa zamani, niambie sasa wakristo wa kijumapili, wanaomgonja Yesu kuja kuwanyakua/kuwachukua n.k., wao wanaitwaje kwa sasa kama siyo waadventista?
  Siyi

 2. Wow!

  Hata mimi nakumbuka japo nilikuwa mdogo, kwenye miaka ya themanini na kuja tisini hapo, wasabato waliwahi kukesha milimani kama mara mbili hivi wakimsubiri Yesu kurudi!

  Mimi nakosa uhakika kama Siyi anaujua kweli usabato au amedandia train bila hata kujua behewa alilopo.
  Maana inafika wakati namshangaa mno anapotetea au kupinga na kupindisha mambo ambayo yako wazi mno kwenye maandiko kana suala la kuokoka.

  Sijui kama wasabato wa miaka ya leo wameerevuka ña kutoka ktk ile misingi ya uongo wa Miller na Ellen. Lakini ni kwamba hakuwahi msabato kuniongelesha bila kumtaja Ellen G. White, au kukosa kunipa kijitabu chake.

  Ni huyu tu Siyi hapa anayejaribu kuikana hiyo misingi ya udanganyifu ambayo wasabato wamekuwa nayo siku zote. Anajaribu kuyavuta hayo mapokeo ya udanganyifu ili yakubaliane na kweli ya neno la Mungu lakini yanakataa.

  Anyway, Neema ya Mungu ni kubwa!

 3. Neno ‘Adventist’ ni neno la kawaida linalomaanisha “ujio” wa jambo au mtu fulani. Katika teolojia ya Kikristo, neno hilo humaanisha lile “Tegemeo la Tukio la Kuja kwa Pili kwa Kristo” kama ilivyoahidiwa ktk – Yn 14:1-3, “Msifadhaike mioyoni mwenu; … Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu…” na mahali pengine ktk Mt 24 na 25

  Lakini baada ya kujitokeza kwa kundi la Kiprotestanti ktk miaka ya 1830, lililoongozwa na mhubiri wa Kibaptist William Miller, ambalo lilijikita ktk kulichunguza jambo hilo la “Kuja kwa Pili kwa Kristo”, ktk mtazamo wa kisasa, ndipo neno hili, “Adventist” lilichukua maana mpya pale lilipohusishwa na kundi hilo lililojengeka ktk msimamo au imani ya “Kuja kwa Pili kwa Kristo”, nao wakatambulika kama wa “Adventists” ktk maana hiyo hata leo hii. Kwahiyo kucheza na neno hilo ukijaribu kulirudisha ktk maana yake ya kablaya 1830s kimatumizi, ili maana hiyo uisimamishe leo hii, ni hila ya kuwachanganya watu kama Baalamu alivyowashauri Moab jinsi ya kuwanajisi Israeli!

  Miller ktk kuyachunguza kwake kwa kina Maandiko ktk vitabu vya unabii vya Daniel na Ufunuo, ndipo akabaini na kutangaza kwamba Tukio hilo la Kuja kwa Pili kwa Kristo litatukia ktk mwaka 1843 au 1844. Ndipo ktk kujitayarisha na Tukio hilo la karne, kundi hilo likajitengenezea na mbawa ili waruke huko hewani wakamlaki Bwana!!! Unawaona hao wanao tumia akili? Ndio hawa hapa ktk Kol 2:18, wenye “…Kunyenyekea kwa mapenzi yake mwenyewe tu, na kuabudu malaika, akijitia katika maono yake na kujivuna bure, kwa akili zake za kimwili”; mnayaona hayo maono yao? Wamejitengenezea mbawa, wakiongozwa na ile sadistic spirit iliyokuwa juu ya malaika wao Miller waliomuabudu! Yaani walipopandishwa huko milimani, kuzimu yote iliangua vicheko kama ilivyokuwa kwa wale Sabato Masalia huko ktk mabonde ya Kinyerezi/Segerea walivyoishia kuumwa na nyoka na wengine kufa ktk jitihada yao ya kwenda kuhubiri Biblia huko ulaya bila nauli!!!

  Ktk miaka yote miwili halikutokea; na haswa pale utabiri wake uliokuwa na uhakika zaidi uliposhindwa kutimia tarehe 22 Oktoba, 1844, basi wengi wa wafuasi wake wakavunjwa moyo kwa “Aibu hiyo ya Karne”. Ndipo kundi dogo kutoka kundi hilo wakajitenga ili kufanya mapitio, wakiitafakari upya Imani ya Kikristo ili kuyavuka mapokeo kulingana na yalivyorithiwa ktk karne zote ili wajirudishe huko kwenye asili halisi ya mwenendo wa Kikristo na tabia zake.

  Ktk shauku hii, ndani ya miaka ipatayo kumi ya matengenezo ya Teolojia ya “imani” hiyo, baada ya unabii kushindwa, ktk miaka ya1850-60 ndio yakalizaa dhehebu la Adventist ambalo liliendelea na unabii huo ambao sasa ulirekebishwa kutoka Kuja kwa Pili kwa Bwana, na kufanywa kwamba ktk tarehe hiyo Kristo ndipo aliingia Patakatifu pa Patakatifu ili kuianza kazi ya Upatanishi!

  Naye nabii Ellen Gould White, alihudhuria mikutano mingi ya Miller na hivyo kuwa mfuasi wa kundi hilo. Baadaye alichukua nafasi ya “malaika” wa kusanyiko hilo pale alipotambuliwa rasmi kama nabii wa dhehebu hilo, hivyo wakayapokea maono na mafundisho yake kadiri ya uvuvio alioupata kutoka kwa roho anayeliongoza kusanyiko hilo.

  Wakatoliki walipowasikia Wasabato wakimuita papa kwamba ndiye Mpinga Kristo, na kuiona hesabu ya cheo chake ktk namba za Kirumi ikiifanya jumla yake kuwa namba ya Mpinga Kristo – 666; kwa vile huyo ni mtoto wao aliyekata kamba, basi wakawaonesha uhalisi wa mamlaka, kadiri ya utumishi kwamba nabii wao huyo ni sehemu yao, ndipo kulidhihirisha hilo, wakawapigia hesabu ya jina la ELLEN GOULD WHITE ikafanya jumla ya 666 pia, (ktk Kilatini U imekokotolewa kutoka V nayo W ni U2 au V2)!!!
  E = 0
  L = 50
  L = 50
  E = 0
  N = 0

  G = 0
  O = 0
  U = 5
  L = 50
  D = 500

  W = 10 (U2 au V2)
  H = 0
  I = 1
  T = 0
  E = 0
  JUMLA 666 !!!!

  Mambo ndio kama mnavyoyaona, “wote dugu moja”!!!

  Gbu!

 4. Siyi,

  Mwalimu mmoja akasema hivi; mtu a kianza form one mpaka akafanya mtihani wa form four halafu akapata zero au four, si kwamba ati kichwani mwake yuko kapa kabisa kama mtu ambaye hajamaliza form four.

  Ana akili kwa kiasi fulani na kuna kitu fulani anachokiweza, lakini bahati mbaya tu waliotunga mtihani hawakuleta maswali kutoka miongoni mwa mambo anayajua na kuyaweza. Wangempa maswali toka miongoni mwa topic anazozijua hakika naye angeambulia hata ki-division three.

  So, yawezekana hata wewe maana ya neno Adventista unalijua vizuri maana yake, lakini bahati mbaya sana kuwa hapa swali halikuwa kueleza maana ya neno Adventista, bali lilikuwa ni aghalabu kujadili suala la kuokoka wakati tungali hapa duniani.

  Kwa hiyo nakupa pole, maana marking scheme haikutambui kwa hicho kipya unachojaribu kukijadili.

  Bt thank u though!

 5. Sungura,
  Ha ha ha ha !! Leo umefanya kiume!! Kuachana kushindana na ukweli. Niliposema kuwa kuna waadventista wengi, wewe ulifikiri waadventista ni wasabato tu!! Ni jambo la kumshukuru Mungu sana kama leo umeelewa kuwa wakristo wooooote kwa madhehebu na majina yao, ilmradi tu wanamgonjea Yesu Kristo kurudi mara ya pili kulitwaa kanisa, hao wooooote ni WAADVENTISTA!! Oooh, what a joy!!!
  Kilichobaki, wanapaswa kuwa waadventista wa siku ya Saba- Sabato. Na hii ndiyo dini ya Mungu. Blessed
  Sungura
  Siyi

 6. Siyi,

  Ukizingatia ulichokisema kiko nje kabisa ya mada, nimeona ni vema nisipoteze muda kukisemea chochote!

  Cha muhimu tu ni kujua kuwa siku ya wokovu ni leo;

  Nakushukuru sana!

 7. Sungura,
  Kwa vile huelewi, utafikiri kuwa nimerukwa na akili!! Ukija kuelewa, utanielewa nilimaanisha nini!! Sikiliza Sungura. Sijui dini yako ni nini na mnaamini nini!! Mimi sijui!! Ninachojua ni kwamba, wakristo wengi (kwa idadi ya madhehebu yao), ni Waadventista!! Huuuh!! How comes!!? Twende polepole utanielewa tu!!
  Neno Adventist ni neno la Kilatini lenye maana ya kuja/kurudi -“ adventus—ad, to, venīre, to come”. Kwa maneno mengine, adventist maana yake kwa Kilatin -“adventus “a coming, approach, arrival,” or “the coming of the Savior,” from past participle stem of advenire “arrive, come to,” from ad- “to” (see ad-) + venire “to come”. Hivyo basi, “An Adventist is someone who believes in the soon return of Jesus Christ at the Second Coming. The connotation is often that he or she is also waiting for that event with anticipation, but the word itself only denotes the belief in it as a real future event”. Hizi zote ni nukuu za makamusi!! Leo ukiitwa mwadventista ndugu yangu Sungura, wewe kubali tu kwa sababu unaamini kuwa Yesu Kristo atarudi kukuchukua na kukukaribisha nyumbani kwa Baba yake kwa mujibu wa Yohana 14. Vinginevyo ukane kuwa huamini hivyo sasa hivi ili tusikuite hivyo maana najua kuna baadhi ya wakristo wasioamini hivyo, mf Mashahidi wa Yehova!! Tofauti na hapo wewe ni mwadventista na kuna wakristo wengi wanaoamini juu ya ujio wa Kristo kwa mara ya pili. Mf. kama sikosei, wakatholiki wanaamini kuwa Yesu atarudi, Walutheri wanaamini hivyo, Kanisa la Kristo wanaamini hivyo na aghalabu makanisa mengi ya kipentekoste yanaamini hivyo, japo yanayofautina kimafundisho jinsi ya kuja kwa Kristo kutakavyokuwa. Wengine wanaamini kuwa atakuja kwa siri (unyakuo), wengine wanaamini kuwa atakuja mbashala (live) n.k. Hoja iliyopo si kuja kwa namna gani, ila ni KUJA/KURUDI kwa KRISTO -adventism.
  Kwa madhehebu yooote ya kijumapili yanayoamini kuwa Yesu atarudi tena, hao ni Waadventista, japo hawajijui kama wanatambulika kwa jina hilo!! Wao hufikiri kuwa Mwadventista, ni kuwa msabato tu!! Tofauti kati yao na sisi wasabato ni kwamba, wao ni adventists kwa madhehebu yao na sisi ni adventists wa siku ya Saba (Sabato) –Seventh Day Adventists!! Hii ndiyo tofauti iliyopo kati yetu Wasabato na watu wa madhehebu mengine. Sisi tunatunza/tunaabudu siku ya Saba –Sabato, na ninyi wenzetu, mlishajichagulia siku ya kwenu ambayo haipo kwenye Biblia –jumapili –kosa kubwa kabisa!!
  Kama unafikiri kuwa niko out of my normal thinking ability, sidhani kama ni kweli ndugu yangu!! Huenda!! Ila mimi nafikiri, kuna mambo mengine naongea yako so much advanced, ndiyo maana wasomaji wangu wengi, hawanielewi!! Nadhani inabidi niwe nakaa chini kujityuni kujibu kwenye level ya uelewa kwa kila aniulizaye. Vinginevyo, nitaendelea kujibu watu nikidhani niko nao pamoja kumbe nimewaacha bila kujua!! Anyway, umesema jambo zuri ndugu yangu!! Ngoja nifanye hiyo ya kuvuta subira na kupumua kidogo kabla ya kujibu kwa kila atakayeniuliza tena!!
  Ubarikiwe sana.
  Siyi

 8. Ooh, my gudness,

  Siyi u are simply out of yo mind brother.

  Hii kazi bila shaka tumemaliza, kuanza kujadili mambo ya kusema Wa-adventists ndo wakristo wengi nafikiri ni dalili za akili iliyojazwa upotofu nayo ikapotoka kwelikweli.

  Ukitaka kujua wasabato mko wangapi hapa Tanzania, soma magazeti ya leo tar 17 March, ’15, kuhusu Mtikila kufungua kesi kupinga mahakama ya kadhi, utakuta takwimu ziko huko.
  Hamfiki hata milioni mbili kwa taarifa yako.

  Tafadhali nakushauri ukae upumzike, maana labda una fatigue, na kama huna fatigue basi sema tukuombee, maana utakuwa umevamiwa na nguvu za giza Siyi.

  Michango yako yote unayochangie tangu mwezi wa pili mwishoni inaonesha uko out of normality. Unaongea madudu mengi sana. Huna tena hata ule uwezo mdogo wa kujenga hoja.

  Umepatwa na nini rafiki yangu?

  Pole sana!!

 9. Sungura,
  Mbona unadanganya umma?? Ni lini ulipangua au kujibu hoja nilizokupeni kwenye andiko langu la mwezi mzima akama unavyoliita!! Huko nilikuonesha maana za maneno niliyoyatumia yakiwa kwenye LUGHA zake za ASILI kabisa!! Mbona kama ulikuwa na hoja, usingejibu au kupangua. Andiko langu niliweka wazi hadi rejea, kwa nini usingeenda huko ukajiridhisha kama niliyoyasema ni ya uongo??
  Mimi najua unaufahamu ukweli lakini hutaki kukiri tu hapa mbashala!! Na wenye akili zao, walishaelewa!! Wakristo walio wengi, ni “Adventists”, yaani wanaingoja mbingu mpya na nchi mpya!! Kama wewe una mafundisho ya tumefika ilhali bado tuko hapahapa duniani, nakupa pole!! Na kama kuna watu watakaokufuata kwa mafundisho hayo ya kifedhuli, nawapa pole pia!!
  Yesu hakuja na kufa ili tuendelee kuishi duniani wewe!! Sasa hivi tulishampokea Kristo, tunasafiri kiimani, na hatima ya safari yetu hii, ni siku ile Kristo atakapotukaribisha nyumbani kwa Baba yake!!
  “Na mwenye kuvulia (matatizo ya safari hii) mpaka mwisho, ndiye atakayeokoka”
  Neema ya Bwana ikufunike.
  Siyi
  Sabato njema

 10. Siyi,
  Unaelewa wazi kabisa kuwa wanaotufuatilia hapa wana akili timamu na wanamjua kristo vilevile, huhitaji kuwasemea.

  Unachokisema kuwa ulipangua hoja unakisema tu kwa sababu hakuna wa kukuzuia kusema.
  Nilikupa mistari mingi inayosema kuwa tumeokoka, ukakaa kimya kama mwezi mzima kisha ukaibuka na suala la kwamba huko kuokoka ambako biblia inakusema,eg; tumeokolewa kw neema, kanisa likaongezeka kutokana na waliokuwa wakiokolewa, n.k, ati kunaitwa halimanusura.

  Nikakutaka unioneshe hilo neno halimanusura liko wapi kwenye maandiko, hukufanya hivyo ila ukaleta maneno ya porojo.

  Mwishoni hapa nimekwambia kwa maandiko kuwa kuokoa kwa Yesu ni kule kuwatoa watu dhambini siyo duniani( universe), bado unakataa kwa makusudi tu.

  Nikakwamba tena kuwa Yesu aliomba akasema ..Baba sisemi uwatoe duniani, bali uwalinde dhidi ya yule mwovu.
  Lakini sasa hivi unaniambia kuwa nimesema ati tunaokoka na kukaa hapa duniani milele. Kwa hila unaongeza neno milele, ili angalao umpotoshe mtu asiyefuatilia vizuri.

  Sikia, tangu mwanzo nalikwambia kuwa siko hapa kukushawishi uokoke, lakini niko hapa kuhakikisha huwapotoshi wale ambao ni wachanga katika kristo na wale ambao wangependa kuupokea huu wokovu mkuu, kwa kuwadanganya kwako kuwa kuokoka ni kule kutolewa kwenye hii dunia.

  Na kazi hiyo nimeifanya, wala si mimi tu, wako wengi pia wameisema kweli kuhusu kuokoka, ikiwa ni pamoja na ndg. Lwembe.

  Kwa vile umeamua tutamatishie hapa, basi lisikie hili neno la kristo:

  Hivyo anasema, wakati uliokubalika nilikusikia, na katika saa ya wokovu nilikusaidia.
  Tazama, wakati uliokubalika ni SASA,
  Tazama, siku ya wokovu ni LEO.
  (2Cor 6:2)

  Naamini kwa neema ya Mungu utaelewa maana sahihi ya kuokoka,na utakubaliana na maandiko yanaposena kuwa tumeokolewa.

  Kwa neema ya Mungu utaelewa kuwa msingi wa kuokoka ni kule kutolewa dhambini, wala si kutolewa duniani( universe)

  Nakushukuru!

 11. Sungura,
  Kwa wale wanaotufuatilia kwenye mjadala, mimi naona wanazidi kutushangaa!! Ukiwa na akili timamu halafu ukawa unacheza na tahira, walimwengu watawaita matahira wote!! Mimi na wewe, kila mmoja alishmdharau mwenzake, kiasi cha kupuuza na kupindisha kila neno kwa nguvu tu kama unavyozidi kufanya hapa!!
  Sasa, mimi leo niseme hivi;
  Wewe endelea kuamini kuwa umeshaokoka!! Hakuna kutolewa duniani, na makao yako ni hapahapa duniani milele!! Amini tu wala usipate taabu!! Maana wokovu ni kwa kila mtu kufanya UAMUZI sahihi!!
  Yale niliyokufunulieni tangu mwanzo, ukazidi kubisha, nikachukua muda kukuonesha kwa vigezo vya Kimaandiko hadi vya lugha ASILIA, lakini bado shingo ikawa ngumu, unafikiri mimi nitaigeuza shingo yako hiyo??? Hasha!!
  Wewe songa mbele. Nafikiri mjadala huu, ufike mwisho. Maana nimekuona, huna lengo la kujifunza, ila unajaribu kuufunika UKWELI WOOOTE ambao nimeufunua tangu mwanzo. Na kwa vile umekosa hoja bainifu za kuupangua, ndio maana sasa hivi unapiga sebene tu!! Mimi sichezi!! Wewe endelea tu.
  Wenye macho, hawaambiwi tazama. Wenye akili za kusoma na kucheua vizuri, wataelewa tu!!
  Mimi naona kwa mada hii, ni vyema nikaishia hapa!! Neema ya Bwana ikufunike rafiki yangu tunapoendelea kwenye mijadala ya mada zingine!!
  Siyi

 12. Siyi,

  Hapa tunaongelea suala zima la kuokoka, lakini umetumia muda mwingi kusema hoja zingine tu.

  Nilipokuuliza suala kuvaa usoharibika kama Paul alisema huko ndo kuokoka, hujajibu umesema mambo mengine tu.

  Kisha nikakuuliza kuwa inaposema atawaokoa watu kutoka kwenye dhambi zao ilimaanisha atawapa nguvu ya kushinda dhambi, hujajibu swali umesema yasiyohusika, ati ni hatua ya kwanza…., hizo ni porojo na hila.

  Kisha nimakuuliza kama neno ‘ufalme’ humaanisha dunia ( universe)?
  Pia umejibu kitu kisichoulizwa kwenye swali. Swali liko specific kama neno ulimwengu humaanisha dunia hii, yaani universe.

  Tena ñikakuuliza, ni wapi biblia inasema wokovu kukamilika ni kufika mbinguni?
  Ukanipa mstari wa Ebr 11: 13. Lakini haijasema kuwa kukamilika kwa wokovu ni pale tutakapofika kwenye mbingu mpya na nchi mpya. Imesema habari za wacha Mungu walioishi kwa imani kabla ya kupokea ahadi ambazo Mungu alikuwa amewaahidia!

  Kwa ujumla umetoa majibu ya hila yenye naneno mengi bila kuwa na msjibu hslisi kwa nilichokuuliza.

  Ukweli utabaki wazi kuwa Yesu alikuja kutuokoa kutoka dhambini wala si kutuokoa kutoka kwenye hii dunia.

  Ndio maana biblia imejaa mistari ya tumeokolewa kama ambavyo nimeiainisha huko nyuma, lakini ati ukasema kuwa huko si kuokoka bali ni uhalimanusura.

  Na nikakwambia unipe mistari ambayo imelisema hilo neno halimanusura lakini hujafanya hivyo.

  Wokovu ni sasa!

 13. Sungura,
  Umeanza kwa kusema, “Unataka tutukanane au tuongee substance? Well, mimi ni kichaa in case u didnt know Siyi!”. Hili nano neno ndugu yangu!! Kimsingi mimi siko hapa kwa ajili ya kutukanana na mtu. Na hiyo siyo kazi yangu hapa mtandaoni. Niko kwa ajili ya kusema/kuhubiri injili ya Kristo tu!! Kile Biblia inachokisema, ndicho nitakachokinena siku zote. Wewe kama ni kichaa, nadhani kumbe napoteza muda kujibizana na mtu mwenye akili zilizoruka!! Huenda ndiyo maana unakuwa ni mgumu sana kuelewa!! Sasa, ikinibidi nitabadili modality ya kuhojiana nawe. Hata hivyo, nitajitahidi leo tena kukujibu maswali yako japo ni kichaa anayedai kureason vizuri, japo sina uhakika kama kuna kichaa anayereason sawasawa!!
  Swali la 1
  Biblia imesema wapi kuwa Yesu haokoi bali anakomboa, ambako unakuita ni hatua ya kwanza ya wokovu?

  Jibu
  Inaelekea huwa unasoma majibu yangu ukiwa na msongo wa mawazo rafiki yangu kama siyo ukichaa unaousema!! Mimi nilisema kuwa,kifo cha Kristo, kilikuwa mbadala wa wanyama wa kafara!! Watu wote wakahesabiwa haki kwa kumwamini tu bila kuingia gharama yoyote ya kutafuta mnyama/kitu cha ondoleo/kufutwa au kufunikwa kwa dhambi kama ilivyokuwa kwa watu wa zamani(OT). Watu wa OT, hawakukokoka!! Hali kadhalika watuwa NT, hawajaokoka bado, isipokuwa, wameshahesabiwa haki kwa njia ya imani pale tu wanapomwamini Mungu na kumfuata pasi na kuingia gharama yoyote kama ilivyokuwa kwa watu OT licha ya adhabu ya kifo iliyokuwa ikiwakabili. Tofauti iliyopo kati yetu na watu wa OT, ni kwamba, wao walichinja wanyama wa kafara ili kuondolewa/kusamehewa au kufunikwa kwa dhambi zao, wakati sisi leo (tukiwa wadhambi tunaostahili kufa), damu ya Kristo, inatuondolea/kufunika dhambi zetu bila gharama yoyote. Hii ndiyo maana ya Neema!!
  Wale watu wa OT, waliokufa wakiwa dhambi zao zimefunikwa/ondolewa, nao wanaingoja ile ahadi ya kuja kuondolewa duniani!! Nikakwambia kuwa, ukisoma sura ya waebrania 11, utakutana na mashujaa wa imani waliolala wakingali wakiingoja ile ahadi za kupewa nchi mpya. Biblia inasema, “Hawa wote wakafa katika imani, wasijazipokea zile ahadi, bali wakaziona tokea mbali na kuzishangilia, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya nchi”- Waebrania 11:13. Siyi anafundisha kama mitume walivyofundisha ya kwamba, ipo siku moja ambayo damu za wanyama (kwa watu wa OT) na ile ya Kristo (kwa watu wa NT), vitawapa watu fursa ya kuondolewa duniani!! Na hili ndilo fundisho la Kristo mwenyewe ya kwamba, pamoja na masaibu mengi tunayopitia hapa duniani(tukiwa wafuasi wake tayari), hatuna haja ya kufadhaika mioyoni!! Yeye anasema, “Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo” –yohana 14:1-3. Hii ndiyo mbingu na nchi mpya kama Biblia inavyosema kuanzia OT hadi NT, ya kwamba, “Maana, tazama, mimi naumba mbingu mpya na nchi mpya, na mambo ya kwanza hayatakumbukwa, wala hayataingia moyoni”- Isaya 65:1. “Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, nitakazofanya, zitakavyokaa mbele zangu, asema Bwana, ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa” Isaya 66:22. “Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake”- 2 Petro 3:13. “Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena” Ufunuo wa Yohana 21:1.

  Sasa jiulize, kwa nini Mungu aumbe mbingu mpya na nchi mpya kama ombi la Kristo kweli lilimaanisha kuwa tutaishi hapahapa duniani tu?? Au unafikiri Yesu alijichanganya kuomba kuwa “Baba siombi uwatoe duniani ila uwalinde na yule mwovu” na ile ahadi ya Yohana 14? Mbona kuna unabii mwingi wa nchi mpya na mbingu mpya hata kabla ya ujio wa Masihi?
  Nikushauri tena Sungura, acha kuduwaa!! Unadhani uko salama kumbe ndiyo unakaribia kupotea kabisa kijumla!! Uko mbali sana na wokovu!! Makao yetu, siyo duniani hapa!! Kwa nini?? Kwa maana Mbingu (za mwanzo) zitaondolewa kama ukurasa unavyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake – Ufunuo wa Yohana 6:14. Ina maana sayari dunia, itaondolewa!! Hakutakuwa na sayari dunia tena!! Kama ni mji mtakatifu kushuka kutoka mbinguni pamoja na watakatifu wote wakiwa ndani ya mji ule pamoja na Bwana wao(Kristo), utashuka ndiyo lakini, hautashuka duniani!! Maana dunia haitakuwepo tena!! Kwa hiyo, mchakato wa wokovu, ulishaanza tangu zamani baada ya anguko tu la Adamu na mkewe. Na litahitimishwa Kristo atakapokuja kuturejesha kwenye hali ile ya kwanza kabla ya dhambi –kuishi ya Bwana milele ndani ya nchi mpya na mbingu mpya ambayo haki yakaa ndani yake kama Petro anavyosema!! Kama kifo tu cha Kristo kingetosha kutuokoa, ina maanaYesu asingetoa ahadi tena ya kuja kutuokoa kutoka duniani –eneo atakaloliunguza kwa moto!!

  Swali la 2
  “Na tena ukasema wokovu kukamilika ni pale tutakapofika mbinguni sisi na wale waliolala zamani. Ivi hayo yote yameandikwa wapi Siyi? Kwani zamani Adamu alikuwa anaishi mbinguni?”
  Jibu
  a. Ivi hayo yote yameandikwa wapi Siyi?
  Jibu
  Nimehshakupa tayari aya ya waebrania 11:13 inayosema, “Hawa wote wakafa katika imani, wasijazipokea zile ahadi, bali wakaziona tokea mbali na kuzishangilia, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya nchi”. Aya zingine za Biblia ni;
  i. “Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika siku za mwisho watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe, na kusema, Iko wapi ahadi ile ya kuja kwake? Kwa maana, tangu hapo babu zetu walipolala, vitu vyote vinakaa hali iyo hiyo, tangu mwanzo wa kuumbwa. Maana hufumba macho yao wasione neno hili ya kuwa zilikuwako mbingu tangu zamani, na nchi pia, imefanyizwa kutoka katika maji, na ndani ya maji, kwa neno la Mungu; kwa hayo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji, ikaangamia. Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu” Petro 3:3-7.
  ii. “Lakini, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira, hamna haja niwaandikie. Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku. Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, WALA HAKIKA HAWATAOKOLEWA. Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi. Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi si wa usiku, wala wa giza. Basi tusilale usingizi kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi. Maana walalao usingizi hulala usiku, pia na walewao hulewa usiku. Lakini sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, hali tukijivika kifuani imani na upendo, na chapeo yetu iwe tumaini la wokovu. Kwa kuwa Mungu hakutuweka kwa hasira yake, bali tupate wokovu, kwa Bwana wetu Yesu Kristo; ambaye alikufa kwa ajili yetu, ili tuishi pamoja naye, kwamba twakesha au kwamba twalala” Thesalonike 5:1-9.
  iii. Matthayo 24:4-5; 11; 23-27, Mathayo 24:30-31, Mathayo 16:27, Mathayo 24:37-39, Luka 17:28-30, Luka 21:34-36, Mathayo 24:40-44, Mathayo 25:1-12, Luka 12:37-38, Yohana 14:1-3, Mathayo 25:13, Mathayo 24:36, Luke 12:40, Mathayo 25:31-46, Marko 8:38 n.k.
  b. Kwani zamani Adamu alikuwa anaishi mbinguni?”
  Jibu
  Kabla ya dhambi, Adamu aliishi duniani akiwa anatembelewa mara kwa mara na Mungu!! Baada ya dhambi, Mungu alikata matembezi yake kwa Adamu, ndiyo maana akaamua kutafuta njia nyingine ya kuwaweka karibu tena na viumbe wake wanadamu! Akaanzisha mfumo wa kuchinja kafara za wanyama (kama kivuli cha Kristo), ili baadaye wale wote watakaotii na kufuata maelekezo yake, siku moja waje waokolewe na kuhamishiwa kwenye mbingu mpya na nchi mpya ambayo Mungu ataishi na wanadamu tena. Biblia inasema, “…Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao”- Ufunuo wa Yohana 21:3 .

  Swali la 3
  “Pia umesema suala la kuvaa usioharibika kama lilivyosemwa na mtume Paul, je katika kusema kwake hivyo kuna sehemu amesema kuwa huko ndiko kuokoka, au wewe ndo unafikiri kuwa huko ndo kuokoka?”
  Jibu
  Naam, huo ndio utimilifu wa lile jambo lililoanzia bustanini Edeni pale Mungu alipowachinjia mnyama wa kafara Adamu na mkewe, na kuwakilishwa na kifo cha Kristo pale msalabani. Vyote hivyo (kafara za wanyama na kifo cha Masihi), vilikuwa ni vyanzo tu vya wokovu ambao Kristo atakuja kuukamilisha –wanadamu kuwatoa duniani!! Do you nderstand up to this juncture bro.??!!
  Swali la 4
  “Nilikwambia ” shame on u” koz unakataa kilichosemwa na biblia na kusema cha kwako. Nilikuuliza, je watu wnatolewa dhambini au hawatolewi? Ulijibu bila aibu kuwa hawatolewi ila wanapewa nguvu ya kuishinda dhambi. Ivi ni wapi biblia imesema hivyo Siyi?”
  Jibu
  Zipo nyingi tu ndani ya Biblia. Baadhi ya aya hizo ni hizi hapa;

  “Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda” – Warumi 8:37.

  “Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo” -1 Wakorintho 15:57

  “Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani” Efeso 6:11.

  “Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu” – Wafilipi 4:13.

  “Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu”- 1 Yohana 5:4

  “Basi huu uharibikao utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa kushinda” -1 Wakorintho 15:54

  “Tena nikaona kitu kama mfano wa bahari ya kioo iliyochangamana na moto, na wale wenye kushinda, watokao kwa yule mnyama, na sanamu yake, na kwa hesabu ya jina lake, walikuwa wamesimama kando-kando ya hiyo bahari ya kioo, wenye vinubi vya Mungu”- Ufunuo wa Yohana 15:2.

  “Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa” Ufunuo 21:11

  Swali la 5
  “Ivi inaposema kuwa atawaokoa watu kutoka kwenye dhambi zao (save them from their sins), humaanisha kuwa atawapa watu nguvu ya kushinda dhambi?”
  Jibu
  Hatua ya kwanza ni hiyo nguvu ya kuishinda dhambi. Na hatua ya mwisho ni kule kuchukuliwa/kutwaliwa mbinguni kwa wale walioishi maisha ya ushindi dhidi ya dhambi. Rejea jibu langu la msingi kwenye swali la 4.
  Swali la 6.
  “Ivi tena inaposema kuwa alituhamisha kutoka ktk ufalme wa giza na kutuingiza ktk ufalme wa nuru, humaanisha nini kwa neno “ufalme”, je humaanisha dunia hii (universe)?”
  Jibu
  Neno ufalme humaanisha “state of mind”. Mwanadamu yeyote ana state 2 za mind. Carnal mindi na spiritual mind. Kristo anapotupa nguvu ya kiungu, huwa tunaishinda ile carnal mind na spiritual mind hutawala ndipo huwa tunakuwa kwenye ufalme wa Mungu. Spiritual mind inapotawala, ndipo tunapoanza kuwa mateka wa Kristo, tayari kwa kutwaliwa siku ajapo. Hata kama tutalala, tutalala katika tumaini la ufufuo wa kwaza –ufufuo wa uzima wa milele.
  Mwisho (but not least), Kifo cha Kristo kiliwakilisha vifo vya wanyama wa OT. Vyote hivyo, vilikuwa na jukumu moja tu la kumpa mtu uwezo/nguvu ya kuishinda carnal mind na kutawaliwa na spiritual mind tayari kwa mavuno ya siku ya mwisho. Wale wote waliokwisha kumpokea, “…aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.” Yohana 1:12-13.

  Neema ya Bwana ikufunike
  Siyi

 14. Siyi,
  Naendelea…

  Umesema kuwa ukamilifu wa wokovu ni kule kurudishwa katka hali ya zamani ya kutokufa, kuugua, n.k, yaani kama alivyokuwa Adamu wa kwanza kabla ya dhambi ( ila hujanipa andiko).

  Na tena ukasema wokovu kukamilika ni pale tutakapofika mbinguni sisi na wale waliolala zamani.

  Ivi hayo yote yameandikwa wapi Siyi?

  Kwani zamani Adamu alikuwa anaishi mbinguni?

  Pia umesema suala la kuvaa usioharibika kama lilivyosemwa na mtume Paul, je katika kusema kwake hivyo kuna sehemu amesema kuwa huko ndiko kuokoka, au wewe ndo unafikiri kuwa huko ndo kuokoka?

  Nilikwambia ” shame on u” koz unakataa kilichosemwa na biblia na kusema cha kwako.

  Nilikuuliza, je watu wnatolewa dhambini au hawatolewi?
  Ulijibu bila aibu kuwa hawatolewi ila wanapewa nguvu ya kuishinda dhambi.
  Ivi ni wapi biblia imesema hivyo Siyi?

  Ivi inaposema kuwa atawaokoa watu kutoka kwenye dhambi zao (save them from their sins), humaanisha kuwa atawapa watu nguvu ya kushinda dhambi?

  Ivi tena inaposema kuwa alituhamisha kutoka ktk ufalme wa giza na kutuingiza ktk ufalme wa nuru, humaanisha nini kwa neno “ufalme”, je humaanisha dunia hii (universe)?

  Siyi, kwa habari ya kukombolewa hatukombolewi kutoka kwenye hii sayari dunia. Hii duniani haijawahi kuwa mali ya shetani, maana haikuumbwa kwa ajili ya shetani.

  Tunakombolewa kutoka kwenye dhambi/ ulimwengu wa giza maana huo ndo unaomhusu shetani

  Christ is the one who has saved us and called us with a holy calling(2Tim 1:9)

  Maana yake ni kwamba kristo ametutoa dhambini au kwenye ufalme wa giza na kutuita kwa mwito mtakatifu.

  Hakuna kitu kinaitwa halimanusura kwenye biblia, kama kipo Siyi nioneshe.

  Kristo ametuokoa ndivyo maandiko yanavyosema, na yanamaanisha hivyo kuwa katutoa dhambini.

  Yesu hakulipa gharama ili tutoke duniani, bali ili tutoke dhambini.

  Kuna tofauti kubwa kati ya duniani na dhambini!

  Period!

 15. Siyi,

  Unataka tutukanane au tuongee substance?

  Well, mimi ni kichaa in case u didnt know Siyi!

  Listen brother, swali langu la kwanza ni mtu asiyeweza kureason vizuri tu ndo anaweza kudhani ni jepesi. Hivi ndo vitu vidogovidogo vilivyo kwenye neno la Mungu ambavyo watu kama Siyi huwa wanadhani wanavifahamu, kumbe la!

  Haisemi biblia kuwa ataitwa jina lake Yesu maana ndiye atakayewaokoa watu wake kutoka katika dunia ( universe)

  Wokovu ni kutolewa dhambini au kwenye ulimwengu wa giza. Hiyo ndo kazi ya msingi ambayo Yesu alikuja kufanya.

  Hakuna andiko ambalo linakwambia kuwa msingi wa wokovu ni kutolewa duniani( universe).

  Ndo maana Yesu akamwambia Baba yake kuwa hauakuwa maombi yake tutolewe duniani, bali tulindwe na mwovu.

  Mara nyingi nimekwambia tofautisha kuokolewa kutoka dhambini na kunyakuliwa kutoka duniani (universe).

  Maana ya ukombozi ni kukirudisha kitu chako kilichochukuliwa kwa wewe kulipa gharama.

  Yesu aliturudisha kutoka ktk mikono ya shetani/ ulimwengu wa giza na kutuweka katika ulimwengu wa nuru.
  Huko ndiko kunaitwa kuokolewa kutoka dhambini ambako kunaambatanishwa na maana ya jina Yesu.

  Ni kweli sadaka za wanyama hazikuwaokoa na wala Biblia haijasema kuwa kazi ya damu ya mbuzi ilikuwa ni kusamehe au kuondoa dhambi, bali ilikuwa ni kufunika tu.

  Lakini Kristo mwenyewe alipokuja ndo alikuja kuokoa kwa maana ya kutoa kabisa dhambini na wala si kufunika tena.

  Siyi nijibu swali langu kuwa ni wapi imeandikwa wa kale waliingojea siku
  ya kutolewa duniani. Tena naona umeongeza kuwa siku hiyo ni ile ya kiama.

  Siyo kweli, ndio maana nimekwambia unioneshe hilo andiko. Siyi am sober, siwezi kukuuliza kitu cha kijinga.

  Biblia imesema wapi kuwa Yesu haokoi bali anakomboa, ambako unakuita ni hatua ya kwanza ya wokovu?
  Siyi hayo ni mafundisho ya jutengeza frm peoples ideas.

  Yesu katuokoa kutoka dhambini ndivyo biblia inavyosema. Katutoa dhamboni tayari kwa njia ya omani.
  Hakulipa gharama halafu akatuacha tuendelee kukaa mikononi mwa adui.

  Ndo maana nakushangaa unapokataa kile ambacho biblia inasema Yesu alikuja kufanya, uaani kuwaokoa watu toka dhambini, wewe unasema alikuja kuwaokoa watu toka duniani. Where do u get that scripture Siyi?

  Ntaendelea……

 16. Sungura,
  Unasema shame on me!! Ha ha ha ha ha pole sana!! Ukiwa huelewi, na huku hutaki kuelewa kwa sababu una mitazamo yako ya kifedhuli, misimamo ya kuamini kuwa ulishafika, kumbe ndo bado safari inaanza, itakuwa ni kazi sana kukuelewesha wewe!! Kwanza, una negative pre –conceived ideas towards me!! Hivyo, sidhani kama utajifunza lolote kwa mtazamo wako huo!! Nakuona hupangui hoja, ila unazidi kurudia aya zilezile nilizozijadili na kuzipangua kwa kipindi cha nyuma. Hata hivyo, wewe hujataka kupangua maelezo yangu niliyoyatumia kupangua aya zako hizo, badala yake, unang’ang’ana tu kuwa hivyo unavyoamini, ndiyo sahihi!! Kama si ukichaaa, ni nini basi??!!! Unafikiri wewe bado unasaidika?? Mimi naona utakufa tu kwenye dhambi pasi tumaini lolote!! Na ukichelewa kiasi hicho, utakuwa umepata hasara ya aina yake.Kujinyima ya ulimwengu halafu baadaye ukaja kupotea tena!!! Hasara iliyoje!! Pole sana.
  Maswali yako…
  1.
  Unakosema ni nyumbani unakwenda ni wapi na unakwenda kufanya nini?

  Jibu
  Kama huelewi nyumbani kwetu ni wapi na kwa nini Kristo aliahidi kuja kutuchukua kwenda kuishi naye, naona mimi sitakusaidia sana kuelewa katika hili!! Kaisome Biblia yako vizuri huenda itakupa sababu kwa nini Yesu alisema kuwa, nyumbani mwa Baba yake (wapi huko?) mna makao ambayo hata sisi tunapaswa kuishi humo!!

  2.
  Siku unayosema ya kutolewa duniani, na mabanoni ukasema kuokolewa ambayo wa zamani waliingoja imeandikwa wapi?
  Jibu
  Unaona unavyohoji!!! Maswali haya, hata mpagani anafahamu kuwa Biblia na hata Korani vimesema kuwa kuna kiyama!! Wewe unayejiita mkristo, huelewi kweli?? Au ni geresha tu!! Na mimi sikupi jawabu. Nenda kasome mwenyewe Biblia!! Maswali ya kipuuzi huwa sijibu!!

  3.
  Je kazi ya kuokoa kaifanya au hajaifanya?
  Jibu
  Yesu kakomboa watu (hatua ya kwanza ya wokovu). Atakuja kukamilisha hatua ya pili ya kuwaokoa watu (kuwatoa duniani)

  4.
  Watu wanatolewa dhambini au hawatolewi?

  Jibu
  Hawatolewi, isipokuwa wanapewa nguvu ya kuishinda dhambi. Bado wanaishi kwenye ulimwengu huohuo wa dhambi alimo ibilisi na malaika zake (muasisi wa dhambi). Vita baina ya wema na uovu, vitaisha Kristo atakaporudi. Ndiyo maana nasema, mchakato ya wokovu, bado haujakamilika, maana vita baina ya wema na uovu, bado vinaendelea!! Si kwa mkristo au mpagani tu, bali ni kwa wanadamu wote wako vitani!!
  5. Kama alikufa ili tutolewe duniani kwa nini bado tupo na wakati alishakuja akafa na akaondoka?
  Jibu
  Kifo chake, kilikuwa ni utimilifu wa vivuli vilivyokuwa vikifanyika hapo zamani (sadaka za wanyama za kutekezwa), ambavyo, navyo havikuwaokoa watu, isipokuwa viliwafanya wasamehewe dhambi tu kwa njia ya kumwaga damu za hao wanyama. Mwenye uwezo wa kuikomesha hiyo hali, alikuwa ni Kristo mwenyewe kwa njia ya kifo chake na kisha kurejesha uhusiano wa karibu kati ya Mungu na mwanadamu uliokuwepo kabla ya dhambi. Na hayo yote yasingefanyika isipokuwa kwa kifo cha Kristo na ukaribishwaji wa wanadamu (wa kuanzia agano la kale hadi jipya) wa kuishi na Mungu pamoja!!

  Watu wa zamani waliosamehewa kwa njia ya damu za wanyama hawakuokoka!! Saa ya kulala ilipofika, walipumzika tu wakiwa na tumaini la kuja kuokolewa baadaye!! Mashujaa wote wa imani walioorodheshwa katika warumi 11 na wengine ambao hawajatajwa, Biblia inasema, “Hawa wote wakafa katika imani, wasijazipokea zile ahadi, bali wakaziona tokea mbali na kuzishangilia, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya nchi”- Waebrania 11:13. Watu wa agano jipya, wanasamehewa dhambi kwa njia ya damu ya Kristo (kwa kuamini tu). wajapo lala sasa, saa inakuja ambayo wataamshwa wote (kuanzia wa agano la kale hadi jipya), ili wakaribishwe nyumbani wa Mungu, ambao ndio mpango wake wa kuishi pamoja na viumbe wake -wanadamu. Paulo anasema, “Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika, kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika. Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa. Basi huu uharibikao utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa kushinda” – 1 Korintho 15:51-54.

  Kukamilika kwa wokovu, itakuwa ni pale tutakapoirejea hali ya mwanzo kabla ya dhambi, -maisha ya kutokufa, kutougua n.k. Maisha ya kuishi pamoja na Mungu siku zote!! Hii ndiyo dhamira na lengo la Kristo tangu mwanzo.
  Neema ya Bwana ikufunike.
  Siyi

 17. Shame on Siyi,

  Katika hayo maelezo yako umeongea nini sasa cha mno ambacho hujawahi kusema, si umeongea ideology zilezile?

  Ngoja nikuulize haya:

  Unakosema ni nyumbani unakwenda ni wapi na unakwenda kufanya nini?

  Siku unayosema ya kutolewa duniani, na mabanoni ukasema kuokolewa ambayo wa zamani waliingoja imeandikwa wapi?

  Siyi acha kukwepa suala la msingi.

  Yesu aliitwa hivyo kwa kuwa alikuja kuwaokoa watu toka kwenye dhambi zao, alishakuja na akaondoka.
  Je kazi ya kuokoa kaifanya au hajaifanya?

  Watu wanatolewa dhambini au hawatolewi?
  Bila shaka wewe tu ndo unafurahia kukaa dhambini, maana wewe unamngoja aje akutoe duniani ndo umwokozi wa Yesu utimie kwako. Utasubiri sana, pole!

  Sikia, Yesu hakufa ili tutolewe duniani, alikufa ili tutolewa dhambini, na huo ndo wokovu. Kama alikufa ili tutolewe duniani kwa nini bado tupo na wakati alishakuja akafa na akaondoka?

  Nimekwambia aibu iwe kwako kwa sababu unakubali kutumika na cunning spirit ya shetani kupindisha kweli ya maandiko ili u-justify kile ambacho dini yako inasimamia.

  Ona kwa mfano maandiko haya:

  For we are the sweet aroma of Christ to God among those who are being saved, …..( present continous) 2Cor 2:15.

  Christ offered both supplications and requests …… to the one who was able to save him from death. ( from death not from the world) Heb 5: 7(past perfect)

  He is the one who has SAVED us and called us with a holy calling….2Tim 1: 9 ( past tense)

  Halafu Siyi anasema huwezi kuokolewa ukiwa duniani. Shame on u Siyi.

  Kupinga maandiko kama haya lazima mtu uwe na uendawazimu kichwani au unatumiwa na shetani.

  Period!

 18. Sungura,
  Ha ha ha ha !!
  Mwanzoni kabisa, wewe huyohuyo ulikataa mbashala kuwa, Yesu hakuja kututoa duniani ila kutuokoa tu!! Nikakuuliza, maana ya kuokoka, ni nini? Ukanieleza!! Nikakwambia kuwa, kifo cha Kristo msalabani, kilitimiza kile kilichokuwa kikifanyika agano la kale -kuchinja ng’ombe, mbuzi, kondoo, njiwa n.k. kwa ajili ya ondoleo la dhambi (japo kimsingi ulikuwa ni msamaha tu), ndiyo maana watu wa zamani, hawakuokoka ila walisamehewa dhambi tu!! Kile kilichofanyika zamani (OT), kiliwafanya watu wasamehewe dhambi na kuheseabika wenye haki (baada ya toba na kuishi kitauwa) kwa njia za damu za wanyama na njiwa!! Biblia inasema, pamoja na kusamehewa kwao dhambi, walilala katika tumaini wakiingoja ile siku ambayo hata enzi zile waliijifunza kuwa itakuja watolewe (waokolewe) duniani maana walikuwa ni wapitaji tu!!
  Halikadhalika hadi leo,tumaini lilelile tunalo akina Siyi na wengine ya kwamba, duniani, tunapita tu!! Tunaweza kulala umauti leo, lakini siku tunayoitarajia, siku (moja tu) ya kuokolewa, -kutolewa duniani, bado tunaingoja!! Sasa hivi, tunapata manusuru/maponyo tu huku tukikua katika imani tuliyokwisha ipokea ili siku hiyo ikifika, tukaribishwe nyumbani!! Ndiyo maana nimekuwa nakwambia kuwa huwezi kusema uko salama ilhali hujafika nyumbani wewe!!
  Ila nikupongeze kama na wewe sasa hivi umeshaanza kutambua kuwa kuna kuja kutolewa duniani siku moja. Lililobaki kwako, ni ile kutambua/kujua sasa maana sahihi ya kitendo cha siku hiyo in connection with what Jesus did/ is doing and w’ll continue doing for us!!
  Suala la kubweteshana eti, oooh tumeokoka, kula/ponda maisha tu, ilhali bado tuko barabarani kuelekea kwenye mji wetu wa milele, inabidi ulitazame upya!! Mmmh!! Huo ni ufedhuli mkubwa sana!! Udanganyifu wa aina yake!! Ni vyema ukautambua mapema kabla hujachelewa!! Mbinguni tutakuwa pamoja na watu wa zamani ambao hawakuokoka duniani!! Kuokoka ni siku ile kaka!! Acha kudanganyika sasa hivi na ufedhuli na wa ibilisi!!
  Neema ya Bwana ikufunike.
  Siyi

 19. Siyi,

  Umeongea ngonjera nyingi sana kwenye comment yako hapo juu wakati unajibu ya kwangu.

  Sitaki nikujibu hayo yote, ila nataka nikuoneshe kitu kidogo lakini kina maana kubwa sana, ili ujue kuwa nikikwambia kwamba kuna wakati unaongea upuuzi usikasirishwe.

  Kitu chenyewe kinahusu suala la Yesu alikuja kuwaokoa watu toka dhambini, siyo kuwatoa ulimwenguni.

  Ona nilichokisema ulinganishe na ulichosema kuwa nilisema, uone tunavyotofautiana kuyaona mambo.

  Mumu nilisema hivi;(najinukuu)

  “Biblia iko wazi kuwa Yesu alikuja kuwaokoa watu toka kwenye dhambi zao, kisha wanaendelea na maisha wakiwa duniani.”

  Kisha wewe ukasema nilisema hivi;( nakunukuu)

  “Kama Yesu alikuja kuwaokoa watu kutoka kwenye dhambi zao na kisha kuwaacha waishi duniani milele, unafikiri hatima ya hawa watu ni nini?”

  Zingatia neno “milele” kwenye ulichokisema wewe, utagundua kuwa mimi sikulisema, ila wewe ndo umeliongeza.

  Ningekuwa kwa kweli mpuuzi sana kama ningekuwa nimesema hivyo.

  Sasa sijui kwa nini unakasirika nikikwambia unaongea upuuzi!

  Ukweli unabaki palepale kuwa alikuja kutuokoa kutoka dhambini tukiwa duniani hivihivi. Alimaliza hiyo kazi akapaa, atakuja kuwanyakuwa hao waliookoka/ waliotolewa kwenye ulimwengu wa giza(yaani sisi)

  Ndo maana nakwambia kuwa mbona twabishana kwa jambo lililowazi sana?

  Sasa kwa nini kwa hali kama hii nisikuone mpuuzi?
  Unasema ambacho mie sijasema, halafu unalalama kuwa ati nakuita mpuuzi.

  Nafikiri imeona vizuri sas upuuzi wako!

 20. Lwembe,
  Umenena vyema kabisa. Hakuna mtu asiyeamini kuwa Kristo ni mwokozi. Hakuna mtu asiyekiri hivyo!! Kama unadhani watu au akina Siyi hawakiri hivyo, uko op!! Akina Siyi tunaukili sana wokovu. Na mchakato wa wokovu tulishauanza tangutulipoamini mwanaume!! Kama ni hatua ya makuzi kiimani, nina imani akina Siyi wana hatua fulani nzuri maana wanakufa kila siku katika ulimwengu wa mwili na kuzaliwa upya kila siku katika ulimwengu wa roho!! What a joy!!
  Yesu ni mwokozi. Alitukomboa msalabani kwa damu yake ya thamani!! Hatukulipa chochote, japo tulikuwa wadeni wakubwa!! What a wonderful NEEMA is that!!!?? Zaidi ya kulipa deni, na kutuhakikishia ulinzi dhidi ya mdai wetu mkuu -ibilisi, Kristo ametuahidi kufanya makao ya milele pamoja na sisi!! Makao ya milele ambayo hayatakuwa katika sayari hii tena ya dhambi!! Hiki ndicho alichokibakiza Kristo kwetu -kuitimiza ahadi yake aliyotuahidi tangu enzi za Ibrahimu baba yetu wa imani!! Siku si nyingi, Kristo atakuja kutimiza kile alichokiahidi tangu enzi zile na tutaokolewa pamoja (kutolewa duniani). Hili ndilo kusudi la Kristo tangu zamani. Huu ndio mpango wa Mungu tangu zamani -kuishi na viumbe wake wanadamu wakimfanyia ibada!! Kristo alituumba mara moja, akatukomboa mara moja, atakuja kutuokoa mara moja!! Na hilo ndilo tumaini na ahadi yake kuu kwetu atakayoitimiza siku nyingi!!
  Kijana, kaza mwendeo, Habari za usiku, asubuhi i karibu sana!! Kuna dalili zoooote za kupambazuka!! Changamka!!
  Siyi
  Ubarikiwe
  siyi

 21. Sungura,
  Unajua mtu asiyekufahamu anaweza kufikiri wewe ni mtu mwungwana vile, kumbe ni mtu wa ajabu sana. Hoja ikikugonga, huwa huna pa kukimbilia isipokuwa huishia kuiita upuzi tu na hivyo husema kuwa hutaki kujibu upuzi!! Very funny!! Kama unaongea na mtu anayesema upuzi, hivi kweli ungeendelea kupoteza muda wako mwingi wa siku zoooote hizo kujibizana na mtu anayeandika upuzi ambaye na yeye kimsingi ni mpuuzi??? Au na wewe ni wapuuzi walewale tu kwa vile unajibizana na mpuuzi?? Maana wafalme utawajua kwa vilemba!!
  Khah!! Yaani wewe, ni mtu wa ajabu sana rafiki yangu. Chenga zako za kutojibu hoja nzito, wajanja walishazielewa. Ni heri ungekuwa kama Lwembe, ambaye yeye hoja ikimgonga, huamua kukausha tu ili aendelee kujifunza mambo mengine zaidi!! Sasa wewe rafiki yangu Sungura… daah!! Pole sana. Mimi nitakuvumilia hadi mwisho wa safari yetu ya mijadala hapa mtandaoni.
  Kama Yesu alikuja kuwaokoa watu kutoka kwenye dhambi zao na kisha kuwaacha waishi duniani milele, unafikiri hatima ya hawa watu ni nini? Na Yesu ana kazi ya kuwalinda tu watu hawa ili wasishambuliwe/wasitekwe tena na Ibilisi siku zote??

  Mwisho, mimi nikushauri, ujaribu kuujibu huo upuzi kwanza. Maana hata hivyo, bado unaendelea kujibizana na mpuuzi anayekupa mambo ya kipuuzi, hivyo, si vibaya kwa vile na wewe umeamua kuwa mpuuzi, ukajibu upuuzi wa mpuuzi Siyi!! Nataka upangue kwanza ule upuuzi ili nikupatie upper upuuzi mwingine. Uspokubaliana nao, nitakupa the uppest upuuzi(sijui kama kuna hicho Kiinglish) zaidi!!!
  Karibu sana.
  Neema ya Bwana ikufunike.
  Siyi

 22. Siyi,

  Vitu vingine ona aibu brother, ni vya kiwango cha chini sana kulinga na umri wako.

  Sikia, Theolojia siyo moja kama unavyojiaminisha. Bila shaka kuna mahali umesoma au mwanazuoni fulani kakuambia hivyo, nawe ukakubali kuwa ni hivyo bila wewe mwenyewe kufanya utafiti wako na bila kutumia common sense.

  Unachosema ulikifafanua ni kichekesho sana Siyi. Sikutaka nipoteze muda kubishania fafanuzi zako kuhusu mistari inayosema kuwa tumeokolewa.

  Kwa hakika fafanuzi zako ilikuwa ni mapokeo na theolojia ya uongo ya kisabato, ambayo kimsingi ni upuuzi mtupu kwa mtu anayejua kuyasoma maandiko na kuyaelewa.

  Ndio maana ilikuchukua karibu mwezi mzima kupata hayo majibu.

  Haiwezekani biblia ikasema wazi kuwa tumeokolewa kwa neema, kanisa likaongezeka kutokana na wale waliokuwa wakiokolewa, n.k, halafu msabato Siyi anataftiliza maana anazozijua mwenyewe akasema ati hapo haikumaanisha kuokoka kwa maana ya kuokoka.

  Ndio maana mara nyingi tu nimekwambia hujui maana ya kuokoka Siyi.

  Maana mantika ya maandiko imekukatalia kwa mujibu wa point tuliyonayo sasa hivi ya Yesu kuwa alikuja kuwatoa watu dhambini wala hakuja kuwatoa watu duniani.

  Biblia iko wazi kuwa Yesu alikuja kuwaokoa watu toka kwenye dhambi zao, kisha wanaendelea na maisha wakiwa duniani.

  What is so difficult to grasp there brother, or u just enjoy the endless argument?

  Mbona iko wazi!!!

 23. Sungura,
  Mistari yote uliyoileta kutetea hoja yako rafiki, niliifafanua yooote. Sasa unataka nianze kurudia tena?? Habari ya theolojia, nilikwambia kuwa, hakuna theolojia ya wasabato, wala waroma, wala walutheri. Hakuna. Kuna theolojia moja kutoka rumi basi ambayo ndiyo wanafundishwa wakristo wote. Sasa jiulize kama theoljia ni moja, kwa nini kuna madhehebu mengi tofauti?? Hapo ndipo tunazidiana akili!!
  HStani anacheza sana na akili zetu. Ukikubali kumeza mazimamazima, utaishia hewa!!
  Wewe kama una shida ya uelewa kuhusu wokovu, hebu uliza jambo ambalo hatuwahi kulijadili kabisaaa. Yale tuliyokwisha jadili, tujitahidi kuwa tunarejea kwenye michango yetu. Hii itatusaidia!!
  Ubarikiwe
  Siyi

 24. Siyi,

  Kuna mambo ambayo ni rahisi sana, lakini hugeuka kuwa magumu sana pale tunapojitoa ufahamu!

  Hivi kuna mtu anayeweza kuitwa “mwizi” akiwa hajaiba? Au kuna mlevi asiyetumia kilevi? Au mzinzi asiye zini? Haiwezekani kuitwa majina hayo iwapo hujawahi kutenda tendo hilo!

  Vivyo hatuwezi tukamwita Kristo kwamba ni “Mwokozi” wakati hajamuokoa yeyote yule, huo utakuwa ni UNAFIKI wa hali ya juu sana! Lakini kwa waliookolewa, kwao hao Kristo ni “Mwokozi” kulingana na kuookolewa kwao na huyo Kristo!!

  “Kweli” ina Nguvu sawa sawa na “Unafiki” ktk kumshikilia mteja wake; nguvu ya “Unafiki” ilimshikilia Yuda Iskariote hata akashindwa kujinasua, Mt 26:24 “… lakini ole wake mtu yule ambaye amsaliti Mwana wa Adamu! Ingekuwa heri kwake mtu yule kama asingalizaliwa. Yuda, yule mwenye kumsaliti, akajibu, akasema, Ni mimi, Rabi?…”

  Wengi wetu kwa makosa hudhania kwamba watu wanafiki hujitambua ktk unafiki wao; huyo hapo Yuda anauliza kama ni yeye atakayemsaliti, unaona! Licha ya mipango yote aliyoifanya ya kumsaliti, bali hajui kabisa anachokifanya kutokana na ufahamu wake kukamatwa completely na roho ya Ibilisi; yaani Ibilisi humuendesha anavyotaka: kama ni “utakatifu mbuzi”, angemuachilia ktk huo hata akaombea na wagonjwa wakapona. Si unajua ukitaka kumuombea mgonjwa ni lazima kwanza umuhubiri ili lile Neno limjengee imani ya kupona kulingana na Injili, ndipo umuombee na ainuke awe mzima; lakini mwisho wa siku Yuda aliiba sadaka!!

  “Basi Yesu akamwambia, Uyatendayo yatende upesi. …Basi huyo, akiisha kulipokea lile tonge, akatoka mara hiyo. Nako kulikuwa ni usiku.” Kama Yuda angekuwa na hata chembe ya RM, angeanguka chini akayatubia yote! Lakini alikuwa ni mtu wa dini tu mwenye nfano wa utauwa lakini ni nyumba ya Shetani kama alivyokuwa Kaini; ni watu wa kidini wasio na uelewa wowote kuhusu Mungu zaidi ya kujibidiisha ktk kuigiza wasiyoyajua!

  Msikiri mambo ambayo hamuyajui; Mungu anaheshimu sana ukiri wetu! Unapokiri kwamba umepata Wokovu, Mungu hukupatia huo kulingana na kukiri kwako; “KUKIRI” na si kumimic kama tunavyoongozana sala za toba, unakiri jambo lililokutokea, unatoa ushuhuda wa hilo kulingana na Injili ilivyokufanyia. Wengi wetu huyakariri maneno tunayoongozwa kuyanena halafu tukadhania kwamba ndiko kukiri kunakoongelewa ktk Biblia, nasi kwa jambo hilo huishia ktk intellectual faith ambayo haitusaidii kitu zaidi ya kutufanya washirika wazuri wa makusanyiko yetu!

  Kama kweli Kristo ndiye anayekutawala, inakuwaje tena ninakukuta ktk mstari wa maombi ilhali Yeye alikuambia kuwa “””Na ishara hizi zitafuatana nawe; kwa jina lake utatoa pepo; utasema kwa lugha mpya; utashika nyoka; hata ukinywa kitu cha kufisha, hakitakudhuru kabisa; utaweka mikono yako juu ya wagonjwa, nao watapata afya”””; hapo kwenye mstari wa maombi unafanya nini??? HUJAWAHI kumuamini Kristo, unadhani tu kwamba unamwamini, ulidanganywa ukakiri usilolijua, na mwisho wa siku ndio unakirishwa yenye kufisha kabisa!!!

  Tazama Mungu anavyoheshimu KUKIRI kwetu, chochote tunachokikiri, tuyaangalie yaliyojiri kuhusu “kukiri” ktk ufalme wa Suleiman, huyo aliyejaliwa Hekima, 1Fal 1:50-53:
  “Adonia naye akaogopa mbele ya Sulemani; akaondoka, akaenda, akazishika pembe za madhabahu. Akaambiwa Sulemani, kusema, Tazama, Adonia amwogopa mfalme Sulemani; kwani, tazama, AMEZISHIKA PEMBE ZA MADHABAHU, AKISEMA, MFALME SULEMANI NA ANIAPIE LEO KWAMBA HATANIUA MIMI MTUMWA WAKE KWA UPANGA. Akasema Sulemani, Akionekana kuwa mtu wa kweli, hata unywele mmoja wake hautaanguka chini; lakini uovu ukionekana ndani yake, atakufa. Basi mfalme Sulemani akatuma watu, wakamtelemsha toka madhabahuni. Naye akaja, akamwinamia mfalme Sulemani; naye Sulemani akamwambia, Enenda nyumbani kwako.”

  Adonia alizishika pembe za madhabahu akakiri Rehema kwa kosa alilolifanya, Mungu akampatia hiyo kulingana na kukiri kwake!

  1Fal 2:28-31
  “… Yoabu akakimbilia Hemani kwa BWANA, akazishika pembe za madhabahu. Akaambiwa mfalme Sulemani ya kwamba, Yoabu amekimbilia Hemani kwa BWANA, naye, tazama, yuko madhabahuni. Ndipo Sulemani akamtuma Benaya, mwana wa Yehoyada, akisema, Enenda, umpige. Basi Benaya akaja Hemani kwa BWANA, akamwambia, Mfalme asema hivi, Njoo utoke. Naye akajibu, La, sivyo; ILA NITAKUFA PAPA HAPA. Naye Benaya akamletea mfalme habari, akisema, Hivi ndivyo alivyonena Yoabu, na ndivyo alivyonijibu. Mfalme akamwambia, FANYA ALIVYONENA, UMPIGE, UKAMZIKE…”

  Yoabu naye alizishika pembe za madhabahu kama Adonia, lakini yeye akakiri kifo na Mungu akamzawadia kifo kama alivyokiri!!!

  Liaminini Neno linavyojifunua, mtapona. Likiwatangazia wokovu, upokeeni hata kama hamjui ni kivipi, timizeni yanayowapasa, yaliyosalia muachieni Mungu mwenyewe maana ni wajibu wake kuwatimizia na kuwafikisha ktk uelewa alioukusudia kwa kulingana na hilo Neno mliloliamini na kulikiri maana hilo ndilo Sheria na Amri, huko kukiri wokovu!

  Gbu!

 25. Aaaah, Siyi,

  Umekwams brother, na umekwama kweli kweli!

  Tuko tunaongelea kitu very specific, ambacho ni kama Yesu alikuja kuwaokoa watu na dhambi zao( kuwatoa dhambini), au alikuja kuwaokoa na ulimwengu( yaani kuwatoa duniani).

  Na nikaongeza na kitu kingine ambacho ni yale maombi ya Yesu kwa Babaye, kwamba hakuomba tutolewe duniani, bali tulindwe na yule mwovu.

  Yesu alishafanya kazi yake ya kuwaokoa watu na dhambi zao, akaondoka zake mbinguni.

  Kule kuwa amekuja na akaondoka na sisi tukaendelea kuwepo duniani kunatupa maana ya wazi kuwa kule kuitwa kwake mwokozi hakukua na maana ya kuwatoa watu duniani bali kuwatoa dhambini.

  Lakini pia nilishawahi kukwambia kuwa kile kitendo cha kanisa kunyakuliwa kwa lugha ya asili(Kiyunani) nacho kinaitwa ‘sozo’ (okoa, kuokolewa).

  Sasa wewe unapoanza kulaumh wanatheolojia sijui wamefanya nini, mara nini, ni kutapatapa.

  Sijaenda kumuuliza mwanatheolojia kujua haya nisemayo. Yako wako wazi kwenye biblia.

  Una tabia moja ya ajabu sana, kwamba ukiona mtu kaleta mstari wa biblia ulio wazi unaanza kusema kuwa huo mstari haumaanishi hivyo, blaa blaa blaa…

  Nimekupa mistari mingi mno yenye kusema tumeokolewa au tuliokolewa( nyakati timilifu), lakini umezisemea hivyovyo kuwa haimaanishi hivyo. Bila wwe kusema inamaanisha nini sasa.

  Hata huo mstari wa maombi ya Yesu umeuhoji hivyohivyo. Hebu sema wewe maana ya hayo maombi kama yalimaanisha tofauti na nilivyosema.

  Lakini hebu niambie, na wanatheolojia wa kisabato pia wanasema kuwa wokovu una phase tatu?

 26. Sungura,
  Siyo hoja ya kuogopa kukubali eti nitaonekana nimeshindwa. Hasha!! Ukweli ukisemwa, mimi huwa nakubaliana nao tu moja kwa moja. Kama ombi la Yesu unalitafsiri, hivyo, unafikiri hoja ya kuja kutukaribisha nyumbani mwa Babaye, bado ina nguvu kama wokovu ni kutulinda tu na yule muovu?
  Kama umejaribu kuuliza wanatheolojia, watakwambia hivyohivyo kuwa wokovu una phase tatu. Nalifahamu hilo. Na ninajua ni wapi wanatheolojia wameingizwa mkenge!! Makanisa yote yenye wachungaji waliosomea theolojia, wanafahamu hivyo, maana theolojia ni moja tu kwa wachungaji wote wa makanisa yote. Hakuna theolojia ya wasabato, TAG, Baptist n.k. Theolojia (syllabus) ni moja. Tofauti ni madhebu tu lakini mchungaji (mfundishaji wa key doctrines) wa madhehebu haya yote ni mmoja –Rumi.
  Hata mimi zamani nilifahamu hivyohivyo kuwa wokovu una phase 3. Baadaye nilikuja kukaa vizuri kujifunza zaidi. Nilipowauliza, wakaniingiza mkenge kwa kuniaminisha wakisema kuwa, katika lugha za asili za Biblia (Kiebrania, Kigiriki pamoja na Kiaramani), Biblia imefafanua vizuri kuwa wokvu una phase 3. Nikatia bidii kujifuna na huko nako, ndipo nilipogundua ufedhuli wao.
  Kama na wewe unaendelea kwenye tego la kuaminitheolojia, endelea tu rafiki. Lakini mimi nilishaamua kuachana na theolojia kabisa. Hakuna kitu kizuri chochote kinachoweza kutoka Rumi. Nimejaribu kuonesha kwa ufasaha hadi lugha za asili maana ya wokovu. Kama mtu hatakubaliana na maandiko, mimi sina ubavu wa kumlazimisha. Atakumbana na Mungu wake. Wokovu si mchezo. Yahitaji kujitoa kikamilifu na si kwa kukokotana kama inavyoafanyika leo ndani ya makanisa mengi ya Kikristo.
  Changamka!!
  SIyi

 27. Siyi,

  Of course unajua ninachotaka kusema coz kiko wazi mno.

  Kwa nini sasa tukisema kuwa tumeokoka( tumetolewa dhambini) hutaki kuelewa, unafanya mjadala ukae miezi na miezi kwa kitu kilicho wazi!

  Unayajua kabisa maombi ya Yesu kwa Babaye, kwamba tusitolewe duniani lakini tulindwe na yule mwovu.

  Tumefanya mjadala mrefu kwa jambo lililowazi kwa sababu tu dini yako imekufundisha kuamini hivyo, but maandiko yako wazi.

  Naona unaogopa kukubali ukweli ukidhani kuwa utaonekana umeshindwa!

 28. Sungura,
  Ha ha ha, pole sana rafiki yangu.
  Najua una kitu cha kusema. Ngoja nikufungulie njia useme. Kwa ufupi, Yesu alikuja kuwaokoa watu from their sins!! Sasa leta hoja kijana!!
  Ubarikiwe sana.
  Siyi

 29. Siyi,

  Tafadhali jibu hili swali;

  “Ivi Yesu alikuja kuwaokoa watu na dhambi zao(from their sins, au alikuja kuwaokoa watu na dunia( take them from the world?)”

  Hakuna mahali ulishawahi kulijibu!

 30. Sungura,
  Rejea makala zangu tatu nilizorusha kuhusu WOKOVU na kama hutanielewa hapo, njoo na swali hilo. Maana nimeelezea humo jibu la swali lako hilo. Jitahidi usome kaka.
  Neema ya Bwana ikufunike
  Siyi

 31. Siyi,
  Heri ya mwaka mpya!

  Nilichokusudia kusema ni kukutaka ujibu hilo swali tafadhali!

  Kama tumeshawahi kulijadili naomba tu uniwie radhi kukutaka ulijibu tena, lakini kwenye hii mada tumerudia vitu vingi tu. Hivyo si mbaya na hilo kulirudia.

  Thanks!

 32. Siyi,

  Hahahahaha…….!!!
  Umesema kweli, utapata shida sana kunielewesha hayo mambo yenu! Tazama, kuhusu hao kondoo waliokuwa wakichinjwa mara mbili kwa siku, unaniambia eti kulikuwa na foleni!!!

  “Mazoea yana tabu””; hii ndiyo tabu uliyonayo, kuunganisha vitu ambavyo HAVIPO! Ni wapi uliposoma kwamba kulikuwa na foleni ya kondoo wanaotolewa dhabihu? Kwanza foleni inahusu nini? Haya ndiyo yale mambo yenu ya “Sabato muhuri wa Mungu”, mara “sabato ishara/alama ya Mungu” na mengineyo mengi sana, sijui mnayatoa wapi!!!?

  Maandiko niliyoyarejea ktk Torati kuhusu sadaka hiyo ni haya hapa: Kut 29:38-39 “Basi sadaka utakazozitoa juu ya madhabahu ni hizi; wana-kondoo wa mwaka mmoja wawili siku baada ya siku daima. Mwana-kondoo mmoja utamchinja asubuhi; na mwana-kondoo wa pili utamchinja jioni.” Jambo la foleni hapa linatokea wapi!?

  Unanishangaa ninaposema kwamba dhambi ilikuwa ni sehemu ya maisha yao, naona utakuwa hujui lolote kuhusu mambo ya kafara; ukimuona mtu anatoa kafara maana yake ana dhambi na anatafuta kujipatanisha na Mungu! Na jambo la kwamba kondoo walichinjwa asubuhi na jioni, hili laonesha kwamba walihitaji utakaso kila siku, kama ambavyo hao unaosema wanaojiita waisraeli wa kiroho wanavyoendelea dhambini baada ya kuukataa Wokovu yaani kuikataa ile Sadaka, na hivyo wanaendelea na ibada zao za kujitungia!

  Tofauti na hilo, ni kwamba mkristo aliyejiambatanisha na Sadaka hiyo, hata kufikia kukamilishwa, huyo HATENDI tena Dhambi maana shina la dhambi limekwisha kung’olewa kutoka moyoni mwake na kurudishwa kwa muhusika Shetani! Mungu akiisha urarua ule Mwili pale msalabani, Damu ya Thamani ikamwagika kutukomboa, hiyo ambayo mfano wake ni ile damu ivisafishavyo vyombo vya hekalu, na sasa Damu halisi ndiyo inayoutunza wokovu wetu hata kumpokea RM atuongoze, si ktk kuyarudia rudia mambo ya kale, hapana, bali ktk mambo yaliyo bora zaidi, ule Upendo wa kiungu!

  Ebr 10:11-14 “Na kila kuhani husimama kila siku akifanya ibada, na kutoa dhabihu zile zile mara nyingi; ambazo haziwezi kabisa kuondoa dhambi.” Haya ndiyo mambo ya Sheria na Hukumu zake, kama Dhambi haikuondoka, basi unashangaa nini ninapokuambia kwamba Dhambi ilikuwa ni sehemu ya maisha yao? Dhambi ilikuwa ni “”Donda ndugu”” lililohitaji dressing kila siiiiku!

  Basi kwa kutolewa kwake Kristo, donda letu liliponeshwa nasi kuwa huru! “12Lakini huyu, alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele, aliketi mkono wa kuume wa Mungu; …. 14Maana kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa.” Kristo alipokwisha kuketi huko, Roho yake ilirudi Kanisani ndiyo Arabuni ya Wokovu wetu!

  Unasema “”Sisi leo hatuna hiyo foleni isipokuwa kila mtu anamwendea Kristo moja kwa moja kwa ajili ya ondoleo la dhambi zake”” Hahahaha! Unamfanya Kristo babu yako! Njia ya Ondoleo laDhambi ni moja tu ndugu yangu, kama ilivyotangazwa ktk Mdo 2:38, Mungu hashughuliki na mambo yetu ya kujitungia kama hayo ya kutubu kwa makasisi na uongo mwingineo kama huo wa sabato ishara ya Mungu! Usipotembea njia hiyo, ndio umeikataa Sadaka!

  Ondoleo la Dhambi linafanywa mara moja tu, Ebr 10:17-18 “Dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena kabisa. Basi, ondoleo la hayo likiwapo, hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi.” Umeelewa kaka, mambo ya nenda rudi hayapo!

  Kuhusu Watakatifu kwenda mbinguni, Maandiko ktk Yh 3:13 yako kama yalivyo, hayahitaji tafsiri zako bali uelewa tu. Hakuna aliyepaa kuingia huko alikoshuka Kristo, tena ambako saa hiyo anayoyazungumza hayo yuko huko! Hao akina Henoko waliwekwa ktk moja ya makao, kama anavyolibainisha jambo hilo kwamba nyumbani mwa Baba yake kuna makao mengi. Ni vigumu wewe kuyaelewa ninayokuonesha kwa sababu HAUAMINI ktk Wokovu hapa duniani, ingawa unatambua kwamba Kristo alisulubiwa hapa duniani, yaani Sadaka ilitolewa hapa duniani na si mbinguni; deni ya dhambi inadaiwa hapa duniani na si mbinguni! Basi kama watu wote kuanzia Adamu tuna deni, nayo damu ya mafahali na mbuzi haitoshi kulipa hilo deni, basi Haki ya Mungu i wapi iwapo aliwapokea mbinguni hao ambao hajawalipia deni yao!? Au unadhani kifo cha Kristo msalabani ni mchezo wa kuigiza?

  Ndg yangu bila hiyo Damu kumwagika, HAKUNA ambaye angepona, mtazame Yohana mwenye kuijua Haki ya Mungu: Ufu 5:3-4 “Wala hapakuwa na mtu mbinguni, wala juu ya nchi, wala chini ya nchi, aliyeweza kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama. Nami nikalia sana kwa kuwa hapakuonekana mtu astahiliye kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama.”

  Usitegemee kwenda mbinguni bila Maarifa, Mungu hakiuki Neno lake! Jitahidi uondokane na imani ya Kikatoliki inayoukataa Wokovu hapa duniani jambo ambalo kwao ni kweli hawana wokovu hapa duniani, huo ambao ungewapeleka mbinguni, na kwa kukiri kwao jambo hilo, ndio wamebakia hivyo!

  Wanaokua kiroho ni hao walio Ondolewa Dhambi zao na kisha kuzaliwa upya kwa Roho, hao walio ktk Agano Jipya, hilo livujalo Damu ya Kristo. Hakuna aliyejibakiza huko nyuma anayeweza kukua leo hii kwa Sheria; kukomaa, sawa, hilo lawezekana kwa sababu Jua la Haki limekwisha kuchomoza likivikomalisha vyote kwa ajili yake, kuitimiza ile Haki, ndio maana unaona leo hii kujirudi au kuyatubia mafundisho yaliyo nje ya Neno HAKUPO, tunaendelea tu, mbele kwa mbele mpaka kuvunwa, maana hata matita hufungwa ktk mavuno!!!

  Gbu!

 33. Naomba nichangie kwa uchache sana katika kiini cha maada.

  Maana ya kuokoka au kumpokea Yesu ni kuzaliwa mara ya pili, kuzaliwa na Mungu, kuuingia ufalme wa mbinguni. Kufanywa kiumbe kipya, kuungwa na Bwana (Mungu).

  Hayo yote yanatokea hapa duniani, kwa kuliamini jina la Bwana Yesu. Na matokeo yake ni uzima wa milele (yaani kumjua Mungu wa pekee na wa kweli, na Yesu Kristo aliyempeleka).

  Huku kumjua Mungu ni kuwa mmoja naye, kama vile alivyotabiri Adam, mwanaume atawacha baba na mamaye, atamfuata mwanamke na hao wawili watakuwa MWILI MMOJA.

  Kwahiyo kule kuokoka ni kuungwa na Bwana kuwa Roho moja naye(1Cor 6:17). Na zoezi hilo linafanyika tukiwa hapa duniani. Huyu aliyeokoka lazima ajue kilichotokea ndipo anaweza kuzaa matunda yake. Na matunda yenyewe ni uzima wa Mungu.

  MTU anaweza kuupoteza uhusiano huu endapo ataamua kwa ridhaa yake mwenyewe kufanya hivyo. Lakini, huu wokovu (as an object) nina maana kama ulivyo wenyewe haupotei. Ni wa milele, hauna majuto.
  Biblia inawema, SASA MNAO UZIMA WA MILELE. Huu uzima upo katika roho. Mtu anapookoka, anapokea roho ya Kristu ndani yake (Rumi 8:9).

  Sasa utambulisho wa huyu mwokovu utakuwa mpya, ya kale yamepita; si katika mwili bali katika roho. Na inampasa huyu mtu kubadilisha akili yake kwa kufanywa upya kupitia neno la Mungu (Rumi 12:1-2).

  Mtu aliyefanywa upya anakuwa na mtazamo wa Mungu. Anakuwanna God’s attitude. Anabadilika kabisa, anakuwa na asili y Mungu (2Peter 1:1-4)

  Anakuwa supernatural being. Kama alivyosema C.K Lwembe, hii ni siri kubwa inayohitaji kufunuliwa ndani ya moyo wa mtu, na ulimwengu ungefuniliwa basi wokovu ungeheshimiwa sana. Kila mwokovu anahimizwa kuuvaa utu huu mpya ulio katka roho, ambao katika kristo umefanywa katika Kristo umefanywa katika haki na utakatifu kweli.

  Naomba niishie hapa kwa sasa. Nawafurahia wachangiaji wote, pamoja na Siyi na Sungura na Lwembe.

 34. Sungura,
  Swali lako;
  “Ivi Yesu alikuja kuwaokoa watu na dhambi zao(from their sins, au alikuja kuwaokoa watu na dunia( take them from the world?)”
  mwitiko
  Nashukuru sana kwa swali lako. Kimsingi, swali hili tulishalijadili san asana. Kama ulikuwa na cha kusema tofauti na kile ambacho tumekizungumza sana kwa huko nyuma, ungekileta hapa tukakiona!! Nikushauri ueleze kile ulichokusudia kusema badala ya kuturudisha nyuma!!
  Asaante
  Siyi

 35. Lwembe,
  Kimsingi nitapata shida kweli kukuelewesha rafiki yangu. Sina uhakika kama kweli huelewi au ni ubishi tu wa hapa mtandaoni. Kama si hivyo, basi mafundisho yenu ya kanisa lenu ndiyo yenye shida rafiki. Tafadhari fungua akili yako ujifunze kana kwamba hukujua kitu chochote hapo kabla. Ndipo utaelewa. Unachanganya sana mambo. Kwa mfano, ona unavyosema, “Ukirudi ktk Torati utaona kwamba kondoo walikuwa wakichinjwa mara mbili kwa siku, asubuhi na jioni, kwa ajili hiyo, mwaka hata mwaka! Utolewaji wa dhabihu hizo ungekuambia kuwa Dhambi ilikuwa ni sehemu ya maisha yao”.
  Hata kama kondoo walichinjwa asubuhi na jioni, haina maana kwamba “Dhambi ilikuwa ni sehemu ya maisha yao”. Kumbuka ibada hizo zilikuwa zikifanyiwa sehemu moja kwa taifa zima la Israel. Hivi unafikiri kwa namna hiyo, foleni ingekosekana? Hebu tuseme sasa kweli huenda “Dhambi ilikuwa ni sehemu ya maisha yao”, je, leo wewe katika maisha ya Agano Jipya, ulishakoma kuomba/kutubu dhambi na makosa unayoyafanya kila uchao?? Je, ni sahihi na wewe tukwambie kuwa, “Dhambi ni sehemu ya maisha yako??”. Huenda ni kweli!! Mimi sijui!!
  Anyway, nilichotaka kusema hapa ni kwamba, maisha waliyoishi Waisrael, dhambi walizozitenda waisrael n.k., ndizo zinazotendwa leo na watu wanaojiita wasirael wa kiroho!! Tofauti iliyopo ni kwamba, wale walipanga foleni kwa ajili ya kwenda kutubu (kutoa kafara za waanyama). Sisi leo hatuna hiyo foleni isipokuwa kila mtu anamwendea Kristo moja kwa moja kwa ajili ya ondoleo la dhambi zake; japo natambua kuna makanisa wanapanga foleni kwenda kutubu dhambi na kuombewa kwa makasisi, nk. Hii nayo ni ajabu tu!!
  Aidha, sioni kingine cha maana cha kujibu ulichoandika rafiki yangu. Umekana kuwa akina Henoko, Eliya nk hawajaenda mbinguni!! Yesu aliyesema maneno ya Yohana 3:13, ndiye ambaye hakuwasahihisha wanafunzi wake walipomuuliza, “Petro akajibu akamwambia Yesu, Bwana, ni vizuri sisi kuwapo hapa; ukitaka, nitafanya hapa vibanda vitatu, kimoja chako wewe, na kimoja cha Musa, na kimoja cha Eliya”. Matt 17: 4. Kama Yesu alimaanisha kwa kauli yake hiyo ya Yohana 3:13, basi Yesu angewasahihisha wanafunzi wake. Au unafikiri alijipinga?? Maana ya aya hiyo ya Yohana 3:13, ilikuwa ni kauli ya Yesu ya kutaka kuwasadikisha watu ambao hawakumwamini kwa maneno yake. Akasema, “Wala hakuna mtu aliyepaa mbinguni, ila yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, yaani, Mwana wa Adamu”-SUV. “And no man hath ascended up to heaven, but he that came down from heaven, even the Son of man which is in heaven” –KJV. Hii ina maana gani?? Yesu alitaka waumini mambo ambayo yeye alikuwa shahidi kwayo, maana tofauti na YEYE, hakukuwa na mtu mwingine aliyekuwa amepaa mbinguni na kushuka duniani kiasi cha kusema mambo ya mbinguni akaaminika kwao. Huu ndio ulikuwa muktadha!! Ukilitumia fungu hili kuyakana maandiko mengine ambayo yako wazi kiasi hicho, unatia huruma kweli. Soma sura nzima ya Yohana 3 uelewe halafu ubishe kama mimi nakuongopea!! Anyway, sitaki kuendelea kujenga hoja na wewe maana naona roho nyingine kabisa inakutawala ndani yako, tena isiyo ya kawaida!! Ni zaidi ya Belizebuli!! Kwa hiyo ukiona unapambana na nguvu ya namna hiyo, inabidi uwe makini sana. Nami sina budi kufanya hivyo!!
  Kama wewe unaamini kuwa wokovu ni hapahapa duniani, pole. Endelea na imani hiyo!! Mimi naamini wokovu ni BAADAYE!! Nimewaonesha msingi wa hicho ninachokiaminni na maana yake kwa mujibu wa Biblia; lakini hamsadiki!! Badala ya kujibu nilichokisema, bado mnazunguka mbuyu tu, jambo ambalo tulishatoka huko zamani sana. Mwenye akili ataelewa!! Sasa hivi nilishampokea Kristo, nakua kiroho na hatimaye nitafikia ukomavu/ukamilifu tayari kwa kuvunwa-BAADAYE Kristo atakaporudi tena!!
  Siyi

  .

 36. Siyi,
  Wewe una kichwa kigumu na roho yenye kuamini kisicho kweli sijawahi kuona.

  Mpaka kesho kutwa nitakwambia ukweli kwamba suala zima la wokovu wewe lilishakuchenga, na ulishadanganyuka.

  Hujui maana ya kuokoja Siyi.

  Acha nikuulize teba hili swali moja tu.

  Ivi Yesu alikuja kuwaokoa watu na dhambi zao(from their sins, au alikuja kuwaokoa watu na dunia( take them from the world?)

  Nijibu tu hilo swali kwa kifupi kwa maandiko.

  Asante.

 37. ……inaendelea:

  Siyi,

  Kwa jinsi ya uelewa wako ulivyopotoka, basi ili uwe sahihi kwamba hao Watakatifu walikwenda mbinguni, italazimu hao wawe aidha waliishi kabla ya Adamu, au waliingia mbinguni na Dhambi zao, jambo ambalo halipo! Iwapo hao wanatokana na Adamu, basi Maandiko yanatuambia hivi: Rum 5:12 “…kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi.” Ndio kusema pia hao Watakatifu walikuwa na dhambi, na tumesoma hapo juu kwamba damu ya mafahali na mbuzi haikuiondoa dhambi, nasi twafahamu kwamba Mungu ni Mtakatifu hivyo hawezi kukipokea kichafu chochote kile, basi waliingiaje huko mbinguni ktk hali yao hiyo? Au ndio unatuambia kwamba Mungu alikuwa ana shirika na vichafu?!

  Kwa taarifa yako Mungu hajawahi kumpokea yeyote yule kwa malipo ya damu ya mbuzi au mafahari! Hakuna mnyama anayefanana na binadamu wala Mungu! Kwahiyo weka kando hadithi za Kipare za kuuza ng’ombe ili uendeshe kesi ya kuibiwa kuku!!! Binadamu ndiye aliye wa mfano wa Mungu, basi malipo ya Ukombozi yasingeweza kufanywa kwa damu ya mbuzi isipokuwa kwa Damu ya Mungu huyo tunayemfananania, na ndio maana alifanyika Mwili ili kuilipa gharama hiyo nasi kurejeshwa mikononi mwake tena!

  Hata hao Watakatifu wako waliingia baada Damu kumwagika, ndipo jeshi lote la Watakatifu alipoondoka nalo Mwenyewe na kuliingiza huko mbinguni, akiisha kuukamilisha wokovu wao kwa Damu yake, hiyo iletayo ONDOLEO LA DHAMBI: Mt 26:28 “Kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi (For this is my blood of the new testament, which is shed for many for the remission of sins).” Umeliona Agano Jipya Siyi! Ni Agano la Damu ya Mungu, ndiyo inayoiondoa Dhambi kutoka humo ilimojichimbia mioyoni mwetu tangu Anguko, na sasa ikiondolewa na kutupwa huko nje ili RM aje akae humo atuongoze, huo ndio Wokovu tunakuitia ndg yetu; Dhambi haikai duniani bali ndani ya watu, hadithi za kuokolewa kwa kutolewa ktk dunia ya Dhambi sijui kupelekwa mbinguni ni za kitoto na ndio kukosa Maarifa kwenyewe!!!

  Kabla ya Damu ya Kristo kumwagika HAKUNA mtu aliyeingia huko mbinguni: Yn3:13 “Wala hakuna mtu aliyepaa mbinguni, ila yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, yaani, Mwana wa Adamu.”!!!!

  Siyi, kuna jambo moja ambalo nimekuona siku nyingi kuwa hujalielewa: UHALISI wa Wokovu. Hakuna dini inayoweza kukupa wokovu isipokuwa Kristo mwenyewe! Wokovu ni kujazwa RM na si kuishi ktk mategemeo ya uongo. RM ni Uzima Kristo ndani ya mwaminio, hiyo ndiyo Nguvu inayoweza kukufufua KABLA ya siku ya Hukumu, maana Kristo alikwisha kuhukumiwa hivyo hawezi kusimama ktk Hukumu tena akiwa ndani yako, vinginevyo Haki ya Mungu itakuwa imevurugika!!! Ndipo kutegemea kwako Kuokolewa ktk siku ya Hukumu, ni ukiri tosha unaotutangazia kwamba HUNA Uzima wa milele ndani yako, Yaani RM, na hivyo unategemea kupewa huo huko Hukumuni ktk ule Ufufuo wa pili, pamoja na hao waliopita ktk Dhiki Kuu na hao walio waliowatendea wema Kanisa lake.

  Kwahiyo tunapozungumzia Wokovu, kimsingi tunazungumzia Kujazwa RM, ndiko huko KUKAMILISHWA; hakuna hatua inayolizidi jambo hilo kwa Mkristo! Kama kushika Sabato kungekuwa ndio kipeo cha wokovu, basi jambo la kwamba Haki yetu inapaswa iizidi ile ya Mafarisayo lingekosa maana! Haki iko ktk nini, iko ktk Imani. Nayo Imani huja kwa kusikia ambako huja kwa Neno la Kristo!

  Nalo Neno hilo la Kristo ndilo linalotufundisha umuhimu wa KUONDOLEWA Dhambi zetu ili RM apate nafasi ya kuja kuishi ndani yetu. Kuziungama dhambi zako leo hii hakukupatii Ondoleo la Dhambi bali msamaha tu. Ndipo jambo hilo lingekurudisha ktk kuliishi Agano la Kale bila kujua licha ya ukiri wako wa ukristo huo usio na Imani maana hukulisikiliza Neno . Maandiko yanatangaza wazi ktk Mdo 2:38, kwamba ili upate ONDOLEO la Dhambi, unapaswa uyatubie maovu uliyoyaamini kwamba ndiyo Kweli, hayo mafundisho uliyoyashikilia yasiyotokana na Neno la Mungu, kama hiyo imani mliyotokanayo Katoliki kwamba hakuna Wokovu duniani, kisha Ubatizwe kwa Jina la Bwana Yesu Kristo (Maji ya kukuzamisha na sio vibakuli) ndipo Dhambi iliyopiga kambi moyoni mwako, hiyo inayokuaminisha uongo kirahisi baada ya kukupofusha, ITAONDOLEWA na kutupwa huko ktk kilindi cha usahaulifu, nawe kupokelewa mikononi mwa Mungu, ukiwa umezaliwa upya kwa Roho wake, na hivyo kuwa kiumbe kipya; HAPA HAPA DUNIANI, nawe utamdhihirisha Kristo mbele ya ulimwengu wote!!!!

  HUO NDIO WOKOVU HALISI!

  Gbu!

 38. Siyi,

  Maelezo yako ndiyo yaliyonionesha kwamba umejichanganya, na hata haya mapya nayo yanalidhihirisha jambo hilo!

  Msamaha wa dhambi unahusika na zile kafara za wanyama, ambavyo Torati ilivihuisha pamoja na Dhambi yake, ili msamaha ujulikane. Ukirudi ktk Torati utaona kwamba kondoo walikuwa wakichinjwa mara mbili kwa siku, asubuhi na jioni, kwa ajili hiyo, mwaka hata mwaka! Utolewaji wa dhabihu hizo ungekuambia kuwa Dhambi ilikuwa ni sehemu ya maisha yao.

  Katika ile “porojo”, umelikosa jambo la msingi sana, aidha ni kutokana na uelewa mdogo, au uoga wa kukabiliana na Kweli. Kuhusu Msamaha wa Dhambi, ulipaswa ujiulize, zile kafara walizokuwa wakizitoa zilikuwa na faida gani kiungu? Jibu ungelilipata ktk vifungu hivi vya porojo niliyokuletea, Ebr 10:1,5 “Basi torati, kwa kuwa ni kivuli cha mema yatakayokuwa, wala si sura yenyewe ya mambo hayo, kwa dhabihu zile zile wanazozitoa kila mwaka daima, haiwezi wakati wo wote kuwakamilisha wakaribiao … Maana haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi KUONDOA dhambi.”

  Kutoka Maandiko hayo ulipaswa ujiulize zaidi, hiyo Dhambi haikuondolewa kutoka wapi, duniani au wapi? Lakini inaonesha kuwa hayo yamekupita mbali sana, ndio sababu huyajui hata haya ya msingi, ndipo inakuwa ni vigumu saaana kwako kujua hata Wokovu ni nini! Maelezo yako haya yanalionesha jambo hilo kwa uwazi zaidi:
  “”Masuala ya maponyo, manusuru au mabadiliko ya tabia ayapatayo mtu, hayo siyo Salvation!! Acha kudanganyika kijana!! Hizo ni alama za barabarani tu kukuonesha kuwa, unaelekea njia sahihi kukwepa hukumu ya kifo ya mwisho itakayohusisha SALVATION na UANGAMIVU!!””

  Basi hayo maponyo, manusuru na hilo badiliko la tabia tunayapata kutoka wapi, kwa Sheria hiyo isiyo na Imani? Hata kama ni mabango, unapoyaona hayo yanakuwa ni arabuni ya kufika kwako! Je, Sheria inayo nguvu ya kumbadilisha mtu? Injili, hiyo iletayo Wokovu, ndiyo pekee yenye nguvu hiyo, ambayo wewe huijui, ndio maana unazungumzia “”jitihada za kukwepa kuja KUANGAMIA TENA siku ya hukumu”” jambo ambalo linahusiana na Sheria, ila kwa kukosa Maarifa, umeunganishwa tena na kurudishwa huko ulikotolewa! Na Iwapo Hukumu ya mwisho itahusisha “Salvation na Uangamivu”, basi hao ambao Kristo anasema hawatapita ktk Hukumu hiyo, Yn 5:24 ” Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani.” Hawa unawaweka ktk fungu gani?? Au hujui kwamba hawa ndio watakaouhukumu ulimwengu???

  Kuhusu Watakatifu wa Agano la Kale kwenda mbinguni, nakuona unanipa pole, kwamba siiamini Biblia! Sikushangai sana ktk hili kwani nina uhakika kwamba hiyo pole unayonipa ni ya dhati kabisa kutoka moyoni mwako! Lakini anayestahili pole hiyo ni wewe! Niliwahi kukuambia huko nyuma kwamba iamini Injili ili upewe RM kwanza , ndipo urudi ktk Agano la Kale akufunulie Maandiko upate kuyaelewa yanasema na kufundisha nini! Agano la Kale lilikamilishwa ktk Jipya!

  Damu ya mafahali na mbuzi HAIKUONDOA dhambi, nasi twafahamu kwamba hiyo damu ilitolewa ktk Sheria, yaani damu na Sheria kwa pamoja vilikuwa ni kivuli cha mema yatakayokuwa, wala si sura yenyewe ya mambo hayo. Basi hayo Mema yakiisha kukufikia, una haja gani tena ya kivuli hicho ambacho wala si sura ya hayo Mema, kama si ishara ya kuchanganyikiwa ni nini??? Unakataa kilicho HALISI ukiking’ang’ania kivuli ambacho HAKISHIKIKI, ndio maana HAKUNA aliyehesabiwa Haki kwa kivuli, maana si halisi!!

  Nitaendelea……..

 39. Lwembe,
  Nashukuru kwa mwitiko wako. Lakini nasikitika kuona kuwa umeandika POROJO nyiiiiingi rafiki yangu!! Kwa nini? Nilitarajia ungeiacha Biblia ikazungumza yenyewe!! Lakini badala yake, porojo zimekuwa nyingi sana na wala hujajibu hoja yoyote niliyoiweka kuhusu wokovu!! Nimejitahidi kusoma ili nipate chochote, lakini sikuona la maana na mimi ngoja nidokeze tu baadhi ya kauli zako ulizoibuka nazo pengine kwa kutaka kupotosha nilichokisema au kutokuwa na uelewa tu wa hicho ulichokuwa unakizungumza!!
  Kwanza, umesema kuwa, “Msamaha wa Dhambi na Ondoleo la dhambi ni mambo mawili tofauti!” Waweza kueleza tofauti yake???
  Pili, umesema, “Kwa kadiri nilivyoyasoma maelezo yako, naona umejichanganya saaana! Maana ya neno SALVATION haijawahi kubadilika! masuala ya kuwa saved kutoka ktk hatari fulani fulani au kuponywa, na hayo mengine unayoyaita temporal ni EARNEST ya Wokovu wetu, yaani ARABUNI, hayo ndiyo yanayotuhakikishia kwamba Wokovu wetu ni Halisi na hivyo kutuondelea hofu ya KUANGAMIA ktk Hukumu ijayo!”
  Mwitiko
  Elewa kwanza kuwa, mimi sikujichanganya hata kidogo. Hata hivyo ungeonesha ni wapi nilichanganya?? Na sahihi ilitakkiwa iweje?? Masuala ya maponyo, manusuru au mabadiliko ya tabia ayapatayo mtu, hayo siyo Salvation!! Acha kudanganyika kijana!! Hizo ni alama za barabarani tu kukuonesha kuwa, unaelekea njia sahihi kukwepa hukumu ya kifo ya mwisho itakayohusisha SALVATION na UANGAMIVU!! Na ndiyo maana Siyi, Mjema na wengine, tumekuwa tukipiga kelele iweni makini na alama za barabarani. Kuna alama zingine feki!! Unafikiri uko njia sahihi kumbe unazidi kupotea!! Kama mapomyo, manusuru nk yangekuwa ni WOKOVU, kusingekuwa na haja ya wewe kuwa na jitihada za kukwepa kuja KUANGAMIA TENA siku ya hukumu!! Acha kubweteka kijana!!

  Tatu, umesema kuwa, “Watakatifu wote walioishi ktk nyakati za Agano la Kale, HAKUNA aliyekwenda Mbinguni licha ya Haki waliyohesabiwa kwa Imani, yaani hao kabla ya Torati au Sheria, na hao waliokuwa ktk Sheria HAKUNA pia aliyehesabiwa haki kwa Sheria; makundi yote haya ili kuufikia UKAMILIFU wao walimsubiri Kristo!”

  Mwitiko
  Pole sana kama mpaka leo wewe huiamini Biblia. Biblia inasema kuwa, baadhi ya watakatifu wa Agano la Kale, wapo walioenda mbinguni. Mf. Henoko na Eliya. Wasingehesabiwa haki bila ya kuwa na imani kwa Mungu wao na kuzishika sheria zake. Hata Baba yetu wa imani Ibrahimu, alihesabiwa haki kwa imani na matendo ya sheria. Biblia inasema, “Kwa sababu Ibrahimu alisikia sauti yangu(aliniamini), akayahifadhi maagizo yangu, na amri zangu, na hukumu zangu, na sheria zangu (akatii sheria zangu)”- Mwanzo 26:5. Imani na matendo huwezi kuvitenganisha. Hivi ndivyo vilivyowafanya watu wa Agano la Kale, wahesabiwe haki. Paulo anasema, “Kwa maana ikiwa Ibrahimu alihesabiwa haki kwa ajili ya matendo yake, analo la kujisifia; lakini si mbele za Mungu. Maana maandiko yasemaje? Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa haki” – Warumi 4:2,3. Ndiyo maana tunasema, hata katika Agano Jipya, tunapomwamini Mungu, tunahesabiwa haki kikamilifu, endapo tutamwamini Mungu na kuishi sawasawa na maagizo yake. Biblia inasema, “Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa” – Yakobo 2:26.
  Nne, umesema kuwa, “Adamu alimkosea Mungu alipokuwa ktk mwili na si ktk roho, kwahiyo kutegemea Wokovu mbinguni ni kukosa Maarifa!”
  Mwitiko
  Mbinguni hatuokoki rafiki yangu. Maana huko hakuna hatari tena!! Tutaokoka kutoka duniani kwenda mbinguni. Duniani ni pa hatari na mbinguni ni pa usalama. Hivyo, kuokoka itakuwa ni hatua ya kutoka sehemu hatari kwenda sehemu salama!! Ukisema mbinguni tutaokoa, ni kweli utakuwa huna maarifa rafiki yangu!! Kwa sasa, tuko safarini tu kuelekea mbinguni. Tuko sehemu ya hatari kuelekea sehemu salama. Destination ya safari hii, ni Kristo atakaporudi kutuchukua kutuingiza kwenye makao yake aliyotuandalia.

  Hivyo tutakuwa tumeokoka/tutaokoka –yaani tutakuwa salama pale tu tutakapofika mbinguni. Hiyo ndiyo concept sahihi ya wokovu.

  Siyi

 40. …..ninaendelea:

  Siyi,

  Kwa bahati mbaya wengi wetu hatuilewi maana kamili ya Sheria au Torati. Hatujajipeleka uweponi mwa Mungu kikamilifu ili kujua alikuwa anafanya nini kwa kuileta Sheria au Mwongozo wa maisha mapya kwa hao Wateule wake waliokulia utumwani, wasiomjua Yeye zaidi ya kuzisikia hadithi zake tu, maana wanayemjua kikamilifu ni Farao na miungu yake!

  Torati ilikuwa ni mwalimu, ikiifunua Dhambi na Hukumu yake; na hao wateule wake walikuwa ndio chuo chetu ili Neema ijulikane kwetu sisi tunapoyarejea hayo yaliyojiri huko Torati ilipowaongoza! Sijui kama unaelewa Siyi, huko ambako hawakuwa na Mungu, huko Misri, ukizini unatozwa ng’ombe au mbuzi; huku kwenye Torati unapigwa mawe mpaka unakufa! Umeliona badiliko hilo? Je, waliacha uzinzi?? Si unamkumbuka yule “Magdalene” wenu? Dhambi inayo nguvu kubwa sana ya kutawala!

  Kama HAKUNA aliyehesabiwa Haki kwa Torati, yaani Dhambi iliyofunuliwa kwao, Torati haikuifisha bali ili ihuisha na hivyo Adhabu ya dhambi mwilini ikawa ndio shule yenyewe! Watu walizihofu adhabu na si Mungu, nayo imani ni kumwamini Mungu, ndio maana Hakuna aliyehesabiwa haki kwa kuitii sheria! Bali kadiri walivyodumu ktk Sheria, hilo liliwapeleka ktk kumjifunza Mungu ktk kuijua Haki yake. Na ndani ya hiyo sheria kulikuwa na Ahadi ya ushindi ambao Mungu angewapatia kupitia Yeye, huyo Masihi, ili WAITAWALE dhambi na si kuziondoa Hukumu za dhambi!

  Dhambi inapofunuliwa na nguvu yake kudhihirika, ndipo hitaji la Wokovu huzaliwa ndani ya mioyo ya watu hao walio ktk Utumwa wa Dhambi, kama ilivyokuwa kule Misri mateso yalivyozidi mioyo yao iliingia ktk masononeko hata yakamfikia Mungu. Wokovu ni kwa walio ktk UTUMWA, hao wenye kujitambua kuwa wako utumwani!

  Kuna makundi mengi yasiyojitambua hali zao, na hivyo wao wameridhika na hali zao hizo kiasi kwamba hawajui hata wokovu ni nini, wanategemea wokovu wao huko mwisho wa safari! Ndipo wanaendelea kuitumikia Dhambi maisha yao yote, wakiwa wamejirudisha ktk Agano la Kale lakini kwa ubahili hawatoi dhabihu za wanyama na badala yake wamejityuni kwa maombi na sala zisizo na tija kama ibada ya Kaini. Wanafikiri eti Mungu atawasikiliza hayo maombi na sala zao, kumbe Mungu anataka Damu tu, tena ya Mwanae hiyo iliyo safi, ambayo ndiyo WOKOVU! Nao Wokovu usio na Damu ni Uongo wa Ibilisi. Dhambi ilifanyika duniani ktk mwili, Adamu alimkosea Mungu alipokuwa ktk mwili na si ktk roho, kwahiyo kutegemea Wokovu mbinguni ni kukosa Maarifa! Kristo hakusulubiwa mbinguni ili kuilipa Deni yangu ya Dhambi bali aliilipa hapa duniani nami natolewa katika mikono ya Dhambi inayonishikilia hapa duniani, ndio maana ndugu zangu wa huko nyuma waliitamani siku yangu ya Leo ambayo Mungu ameniweka niitawale Dhambi kwa Wokovu wake na si wokovu wangu!

  Rum 3:24-25 ” …Yesu Kristo; ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake, ili aonyeshe haki yake, kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa Mungu dhambi zote zilizotangulia kufanywa” Remission of sins ni katika Kristo hapa duniani na si huko mbinguni! Roho ya utumwa inapokutawala, ni vigumu sana kwako kuujua Uhuru, tunaweza kusema kwamba unapatwa na “Uhuruphobia”; ndio sababu kila unapojaribu kujitoa humo, mwisho wa siku unajikuta uko pale pale ulipoanzia, “Wokovu mbinguni”!! Jamani, mbinguni wanakwenda waliuoitawala dhambi na si vidampa wa dhambi walioshindwa na kuwa wahubiri wa ushindi wa dhambi!

  Ukamilifu wetu ni kulipokea Neno lote na si vipande vipande. Roho Mtakatifu ndiye Ukamilifu wetu, kwahiyo sharti uwe umejazwa RM ndipo utamuona Mungu, vinginevyo ni hadithi tu za vijiweni! Iwapo RM ametangaza kuokolewa kwetu hapa duniani, basi ni kwa roho yupi unatangaza kwamba Wokovu ni huko mbinguni? Basi ile Imani yetu ilishinda nini? 1Yn 5: Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, HIYO IMANI YETU.”Siyi, Prince wa ulimwengu ni nani? Huyo ndiye tunayemshinda kwa IMANI YETU!!!

  Siyi, ngoja nijirudishe ktk Maandiko upya ili tuiangalie hiyo “imani” uliyonayo, tulijue chimbuko lake, maana haya uliyoyasema ni tip tu iceberg!

  Gbu!

 41. Siyi,

  Napenda nikupe “Bigup” kwa jinsi ulivyocheza na maneno ya kizungu na kigiriki na kiebrania na mwisho kiswahili, ni sarakasi ya hali juu kiasi kwamba hata nikikuuliza sasa hivi hapo ulipo umesimamia miguu au kichwa, au umelala chini, najua utakuwa hujui hata uko ktk hali gani!!

  Kwa kadiri nilivyoyasoma maelezo yako, naona umejichanganya saaana! Maana ya neno SALVATION haijawahi kubadilika! masuala ya kuwa saved kutoka ktk hatari fulani fulani au kuponywa, na hayo mengine unayoyaita temporal ni EARNEST ya Wokovu wetu, yaani ARABUNI, hayo ndiyo yanayotuhakikishia kwamba Wokovu wetu ni Halisi na hivyo kutuondelea hofu ya KUANGAMIA ktk Hukumu ijayo!

  Kristo hakufa msalabani ili tuponywe magonjwa, bali kwa kupigwa kwake ndio sisi tulipona! Alikufa msalabani ili tupate ONDOLEO la Dhambi, sijui kama unaijua maana halisi ya ONDOLEO la Dhambi! Msamaha wa Dhambi na Ondoleo la dhambi ni mambo mawili tofauti!

  Kwa kujirudisha kwako huko nyuma ktk Agano la Kale na kujaribu kuutafuta Wokovu huko ambako ziko Ahadi zake tu, umekuwa ni sawa na mtu aliyejifunga Ufahamu kwa ujinga! Watakatifu wote walioishi ktk nyakati za Agano la Kale, HAKUNA aliyekwenda Mbinguni licha ya Haki waliyohesabiwa kwa Imani, yaani hao kabla ya Torati au Sheria, na hao waliokuwa ktk Sheria HAKUNA pia aliyehesabiwa haki kwa Sheria; makundi yote haya ili kuufikia UKAMILIFU wao walimsubiri Kristo! Ebr 10:1,5 “Basi torati, kwa kuwa ni kivuli cha mema yatakayokuwa, wala si sura yenyewe ya mambo hayo, kwa dhabihu zile zile wanazozitoa kila mwaka daima, haiwezi wakati wo wote kuwakamilisha wakaribiao … Maana haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi.”

  Mungu ni Mtakatifu, kwahiyo pasipo kukamilika HAKUNA anayeweza kumsogelea, yaani HAIWEZEKANI sisi kurudi ktk mazingira ya Edeni ambako Mungu alishuka na kuwatembelea akina Adamu, huku tukiwa nje ya Programu yake, na hilo ndilo hitaji la Wokovu, ndio maana wote waliutazamia wokovu wao huko mbele, kulingana na Ahadi waliyopewa. Yaani mtu mwenye uwezo wa kuipokea Ahadi ni yule tu aliye na ufahamu kamili wa hali yake ktk mapungufu aliyonayo, ndipo Ahadi ya kuondelewa mapungufu hayo huwa na maana kwake, na si kila mbumbumbu anaye mimic ahadi asiyoijua hata maana yake!

  Nyoka hana Ahadi yoyote na wala hajui chochote kuhusu Wokovu, lakini Adamu na mkewe wanalijua jambo hilo hata maana ya huyo kondoo aliyechinjwa na wao kupewa ngozi yake ili liwe vazi lao jipya lenye ishara ya “utakatifu”, ule msamaha wa dhambi na si Ondoleo!

  Unapoichukua hali ya Agano la Kale kuhusu wokovu, inakupasa kwanza ujifunze ni HATARI ipi iliyowakabili hata kuhitaji wokovu! Kwa maana hakuna mpagani anayetegemea wokovu, wanajiendea tu kadiri ya akili zao zinavyowatuma, kama ni miungu basi wanayo kemkem. Israeli walipokuwa huko Misri walikuwa ktk kundi ambalo HALINA Mungu, Efe 2:12 “… Mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu duniani.” Na wengi wetu tungali tunaendelea bila Mungu kwa kulikataa Neno lake na kushikilia miungu ya dini zetu!!

  Nitaendelea….!

 42. Sungura,
  You are very cunning brother!! Very cunning!! Ila kwa mtu anayekufuatilia vizuri, atakuona jinsi unavyorukaruka na hoja!! Tangu mwanzo Siyi nilikwambia kuwa, sikatai wokovu!! Ninachokikemea ni tafsiri mbovu ya wokovu!! Na hilo nililifahamu siku nyingi ndiyo maana nilikwambieni na Mjema akaja akakwambieni maelezo ya namna ileile!! Ila kwa vile hutaki kuonekana umekuwa defeated kwa hoja, wenye macho ya rohoni wataelewa na watapona!! Yaelekea una sikio la kufa!! Yale yote uliyotaka niyathibitishe, sasa yoooote nimeyaweka wazi… Bado unaanza tena, zilifika Sima na Magu… Mungu akusaidie.
  Mtu anapompokea kikamilifu Kristo aliye wokovu, ni kweli Kristo hukaa kwake (ndani yake), kwa njia ya nguvu itokayo juu. Na siyo Yesu mwenyewe hushuka physically na kuja kukaa ndani ya mtu! Hasha!! Isipokuwa, hushuka kwa njia ya nguvu ya kiungu na kukaa ndani ya mtu. Na hayo yanapotokea, sisi tunasema Kristo yu ndani ya Siyi, Sungura, n.k. Pamoja na Kristo kuwa ndani ya Siyi, Sungura n.k., bado watu hawa hatuwezi kusema wameokoka, maana bado vita/mashambulizi ya ibilisi dhidi yao, yako palepale. Kama ni maradhi yatawapata pamoja na nguvu ya kiungu kuwemo ndani yao. Na hatima ya maisha yao hapa duniani, bado asili ya dhambi –mauti ya kimwili, itawafunika hadi siku ya ufufuo. Hapo ndipo ile dhana ya wokovu, itakapotimilika –kutwaliwa mahali pa salama, sehemu ambayo watu hawataugua tena, hawatalia tena, wala kufa tena.

  Wale wote wanaompokea Kristo, assurance yao ya kuwa na wokovu, siyo leo rafiki yangu. Kimsingi tunaweza kuwa waumini wazuri sana lakini hatuwezi kujihakikishia kuwa tuna uzima wa milele. Mungu pekee ndiye anayejua!! Kamwe, hatuwezi kujihesabia haki eti kwa sababu tu tunamwamini Yesu. Tukifanya hivyo, tutapotoka sana!! Tunaweza kufa tukiwa na tumaini la kuja kuokolewa, lakini hatuwezi kufa tukiwa na uhakika wa kuja kuokolewa!! Duniani hakuna kuokoka from eternal condemnation halafu ukaendelea kula ugali na mchicha!! Wokovu ni matarajio ya mambo makubwa mno ambayo jicho na sikio la kibinadamu halijawahi kuona na kusikia; naam hata rojorojo ambazo ulimi haujawahi kuonja!! Yohana wa ufunuo alipofunuliwa, alishindwa kuyaelezea kwa lugha ya kibinadamu!!

  Kuwa makini na soteriology!! Usiudhalilishe wokovu tafadhali!! Akina Siyi, Mjema na wengine, tuko makini sana, naam hata kupoteza vyote kwa ajili ya wokovu –mambo makubwa ajabu wanayoyatarajia mashujaa wote wa imani wa tangu Agano la Kale hadi Jipya!! Sungura, be smart kijana!! Acha kubahatisha!!

  Wokovu unaozungumziwa na Biblia, ni ule utakaowaotoa watu kwenye ulimwengu huu uliojaa uasi wa kila namna na kupelekwa sehemu penye haki milele. Hii ndiyo ilikuwa injili ya Yesu na mitume wake. Maana Kristo aliahidi. “Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake”-2 Petro 3:13.
  Duniani hakuna haki, ndiyo maana hatuokolewi hapa!!
  Mwenye sikio na asikie!! Na asomaye na afahamu!!
  Siyi

 43. Siyi,

  Hiki ndo umemaliza miezi na majuma anakitafuta eh!
  Pole sana, umefanya kazi ya kuchosha sana ndugu. Najua imekubidi upekue huko na huku ili upate madesa, lakini ndio hivyo yamekupoteza zaidi.

  Umeandika kazi ndeefu ya kuchosha ambayo haina chochote cha mno zaidi ya kukufanya upotee zaidi rafiki yangu.

  Nataka tu nikuoneshe kitu kidogo ambacho pamoja na kukodoa kwako macho yakatazama lakini hayaoni:

  Umenukuu hivi; ..For he shall save his people from their sins. ( note neno SINS)

  Chini yake kwenye maelezo yako ukasema Yesu atasosei wateule wake kutoka kwenye ulimwengu huu dhambi kwenda kwenye makao ya milele(nime-paraphrase).

  Tena ukasema kuwa kulazimisha kuwa kuna kuokoka duniani ni kubadili jina la Yesu ambaye biblia inasema atawaokoa watu na dhambi zao.

  Sasa Siyi usichokiona ni hiki: i.imesema atawaokoa watu wake kutoka kwenye dhambi zao( dhambi zao).

  Lakini wewe kwa sababu ya preconceived ideology ya kwamba hakuna kuokoka duniani, hiyo sentensi ” from their sins” unaona iko sawa na sentensi ” from the world” ikimaanisha huu ulinwengu au dunia halisi.

  Siyi u have eyes but u don’t see brother. Yesu anaokoa watu kwa kuwatoa kwenye dhambi, wala si kwa kuwatoa kwenye ulimwengu.

  Haijasema kuwa he shall save his people from the world, ila imesema from their sins. Wewe kipofu ndo unayeona imesema he shall save his people from the world.

  Watu wanaokolewa kutoka kwenye DHAMBI wakiwa hapa duniani.

  Siyi, umeokoteza maneno mengii kama vile umanusura, uponyo n.k, just ili kutaka kudanganya watu kuwa hakuna kuokoka duniani. Unamtumikia adui bila kujua.

  Kama umekiri kuwa Yesu ni wokovu, kumbuka kwamba wanaomwamini anakaa ndani yao, kwa hiyo wanakaa na wokovu ndani yao. Hawawezi kukaa na wokovu halafu wakawa hawajaokoka.

  Mtu aliyempokea Yesu amevuka eternal judgement, maana hakuna hukumu ya adhabu kwa walio ktk Yesu.
  Ndio maana mtu akishampokea Yesu anakuwa amepata uzima wa milele ndani yake.

  Kumbuka nilikwambia ufikirie vizuri kuhusu neno uzima wa milele, kuwa ni nini hasa.

  Neno Sozo na Soteria hata hayana shida yoyote. Moja ni kitenzi na jingine ni nomino.

  Ndio maana niliwahi kukwambia kuwa upana wa matumizi ya hayo maneno na maana ya kuokoka kwa ujumla.

  We are saved from our sins, we still live in the world!

 44. Tuendelee kuumalizia mkia…

  Je, Siku ya Hukumu nako kutakuwa na Sozo??

  Katika Biblia ya Agano Jipya, maana ya jina la Yesu ilitolewa sanjari na kazi ya jina hilo. “Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu –(“Iesous”), maana, yeye ndiye atakayewaokoa (Sōsei) watu wake na dhambi zao –(SUV). And she shall bring forth a son, and thou shalt call his name JESUS (-“Iesous”): for he shall save (Sōsei) his people from their sins (KJV)” – Mathayo 1:21. Yesu atasosei FROM na siyo IN their sins!! Ukisema mtu anaokoka akiwa duniani, unataka kuilazimisha Biblia kubadili maana ya jina la Yesu – for he shall save his people from their sins. The name means “Salvation of Jehovah” or “Jehovah is the Savior” of people from their sins!! The Savior of all men (refers to Jesus Christ alone). Yesu atasosei kwa maana ya kuwatoa wateule wake kwenye ulimwengu huu wa dhambi na kuwaweka sehemu pa salama milele zote. Duniani hapa siyo salama!! Usalama wa dunia hii, utapatikana baada ya shetani na malaika zake kuangamizwa. Hivyo, siku ya mwisho, hakutakuwa na “sozo”, bali kutakuwa na “Sosei”!! http://biblehub.com/greek/so_sei_4982.htm. Na hizi ni baadhi ya aya za Biblia zinazoonesha kuwa siku ya mwisho Yesu hatasozo watu, bali atasosei watu.

  Matthew 1:21 And she shall bring forth a son, and thou shalt call his name JESUS: for he shall save (Sōsei) his people from their sins.
  Matthew 10:22 And ye shall be hated of all men for my name’s sake: but he that endureth to the end shall be saved (Sōsei).
  Matthew 18:11 For the Son of man is come to save (Sōsei) that which was lost.
  Matthew 19:25 When his disciples heard it, they were exceedingly amazed, saying, Who then can be saved (Sōsei)?
  Matthew 24:13 But he that shall endure unto the end, the same shall be saved (Sōsei).
  Acts 2:21 And it shall come to pass, that whosoever shall call on the name of the Lord shall be saved (Sōsei).
  Hebrews 7:25 Wherefore he is able also to save (Sōsei) them to the uttermost that come unto God by him, seeing he ever liveth to make intercession for them.
  James 4:12 There is one lawgiver, who is able to save (Sōsei) and to destroy: who art thou that judgest another?
  James 5:20 Let him know, that he which converteth the sinner from the error of his way shall save (Sōsei) a soul from death, and shall hide a multitude of sins.
  I Peter 4:18 And if the righteous scarcely be saved (Sōsei), where shall the ungodly and the sinner appear?
  Revelation 21:24 And the nations of them which are saved (Sōsei) shall walk in the light of it: and the kings of the earth do bring their glory and honour into it.

  Ukisoma kwa tafakuri kubwa, utagundua kuwa, sosei, itafanywa na Kristo kama hatima ya kile alichokianzisha bustanini baada ya anguko la mwanadamu dhambini. Tangu Agano la Kale, Kristo amekuwa akishawb tu na kuwapatia watu nacham ambayo wengi wao katika Agano la Kale, walilala wakiwa na tumainni la kuja kusoseiwa na Kristo siku ya mwisho. Hata katika Agano Jipya, Yesu na mitume wamekuwa wakisozo watu mbalimbali na kuwapatia fursa za wao kufanya maandalizi ya kuja kusoseiwa siku ya mwisho na Kristo. Hivyo basi, kusosei, kutajumuisha watu wa Agano la Kale na Agano Jipya. Na hili halitakuwa jambo lingine, bali litakuwa ni lile la kuwahamisha watakatifu wake kutoka mahali pa dhambi (alipo ibilisi na malaika zake) na kuwapelekea sehemu pa salama pasipo na dhambi kama ahadi yake aliyoitoa akisema; “Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo” – Yohana 14:1-3.

  Wapendwa, Yesu alikufa mara moja, ataokoa mara moja tu-baadaye. Wale wanaosema kuwa kuna kuokoka duniani from eternal condemnation, kimsingi wanaikana ahadi ya kuja kwa Kristo kutukaribisha kwake. What a Sadyyy!! Mungu atusaidie tunapojifunza jambo hili kwa utulivu na hekima itokayo juu.
  Bwana awabariki sana.

  Siyi

 45. Mpendwa Sungura na wengine,
  Nawasalimu tena ktk Kristo. Ile ahadi niliyoahidi muda mrefu, naomba kuitimiza saa hizi pekee za utulivu.
  Karibuni tuendelee na mada yetu….

  Kama tulivyoona kwenye Agano la Kale maana ya neno WOKOVU kuwa lilitumika kumrejelea Mungu mwenyewe – (Yeshua/Yehoshua/Jehoshua/Joshua) lenye maana ya YAHWE anayeokoa (or “Yahweh is salvation”); kimsingi tulikuwa tukimwangalia Yesu Kristo aliyekuwepo na aliyeviumba vyote kama tulivyokwisha kuona huko nyuma. Jina hili “Jesus Christ” ni jina mahususi -“Jesus the Christ.” Jina Yesu -“Jesus” (Iēsoús) alipewa liwe ni jina la kibinadamu lenye kubeba na kusadifu dhana ya kazi yake ya ukombozi – YAHWE anayeokoa (or “Yahweh is salvation”), -GENDER: Masculine in nature. Katika andiko hili, tutaangalia jina hili katika lugha ya Biblia ya Agano Jipya.

  Neno Wokovu katika Agano Jipya

  Kama tulivyokwisha kuona maana ya jina la Yesu wakati tunatoa faiwa yake katika pachiko la kwanza kabisa; katika vitabu vya Injili; kwa kiasi kikubwa, neno Salvation, lilitumika kumrejelea Yesu mwenyewe au kurejelea kile ambacho Yesu angekifanya mwisho wa siku hapa duniani. Kwa mfano, katika kumrejelea Yesu mwenyewe, Kristo alipoingia kwa Zakayo, neno Wokovu lilitumika kumrejelea Kristo mwenyewe. “Yesu akamwambia (Zakayo), Leo wokovu (mimi mwenyewe Kristo) umefika nyumbani humu, kwa sababu huyu naye ni mwana wa Ibrahim”- Luka 19:9. Katika Kitabu cha Matendo ya Mitume, neno WOKOVU pia lilitumiwa na mitume kwa kiasi kikubwa kumaanisha Kristo mwenyewe. Na inaonekana kuwa, jina Yesu chanzo chake si Kigiriki bali lilihawilishwa kutoka lugha ya Kiebrania (Yeshua/Yesua/Joshua n.k.), Kigiriki hadi Waswahili tukawa na jina Yesu. http://www.yahuyahweh.org/eaoy/pdf/where_did_the_name_jesus_come_from.pdf

  Katika nyaraka nyingi za Paulo, neno WOKOVU limetumika kama lilivyotumika katika Agano la Kale. Limetumikaje?? Lilitumika kwa faiwa ya;
  1. Zawadi itokanayo na faida chache azipatazo mtu baada ya kuupokea WOKOVU pindi akiwa duniani – manusuru dhidi ya magonjwa, ulevi, uraibu n.k. aupatao mtu baada ya kumpokea Kristo. Kwa maneno mengine, badiliko la maisha yake baada ya kuwa muumini. Hatima ya manusuru (imani) hayo (japo si ya lazima) ni kuja kuupokea wokovu (eternal life). “Katika kuupokea mwisho wa imani yenu, yaani, wokovu wa roho zenu”, -1 Petro 1:9. Dhana hii ya wokovu haina maana ya ile ya kuokoa kutoka kwenye eternal condemnation, bali ni nusuru tu la muda, kama ilivyokuwa kwa watu wa Agano la Kale ambao walikufa katika tumaini, wakiwa hawajaipokea ile ahadi ya uzima wa milele (-hawajaondolewa kwenye eternal condemnation). Dhana hii ya wokovu (manusuru ya maradhi au tabia), kwa Kigiriki husomeka kama “soteria, meaning “to cure, to provide recovery, to rescue, to effect one’s welfare.”- http://www.buzzardhut.net/Salvation.pdf. Hii ni dhana ambayo, mtu hupata athari zake chanya akiwa hapahapa dunini na aghalabu baada ya kumpokea Kristo.
  2. Zawadi aipatayo mtu kama hatima ya imani yake ndani ya Kristo. Biblia inasema kuwa, Yesu ndiye wokovu kama tulivyokwisha kuona katika Agano la Kale, ya kwamba Wokovu ni Bwana Mwenyewe na daima hutokana na YEYE mwenyewe – “… Wokovu hutoka kwa Bwana” –Yona 2:9, na kuwafikia wote. Kristo alitolewa na Baba yake kama zawadi kwetu –mbadala wetu kwa mauti yetu ya milele baada ya kuasi. Alikuja kama neno- injili iokoayo ikianzia kwa Wayahudi hadi wamataifa. Paulo anasema, “Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia” – Rumi 1:16. Na hii injili ipo kwa wale watakaomwamini huyo aliye WOKOVU – “Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki (kama atatii sheria zake), na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu (kama atatudumu katika utii huo)’ –Rumi 10:10. Hivyo basi, hii ndiyo injili (Kristo mwenyewe) ile maana ya WOKOVU ambayo ndiyo itakayowatoa watu kutoka kwenye eternal condemnation yenye kitenzi yesha (kiebrania) ambacho hufanywa na Mungu peke yake. Kitenzi Yesha, si sawa na sozo kwa Kigiriki, japo vina uhusiano fulani. Wala nomino ya Kiebrania Yeshua/Yesua/Joshua n.k., si sawa na nomino Soteria/soter kwa Kigiriki. Ngoja nifafanue kidogo hapa;
  a. Soteria-kama nilivyoitolea maana yake hapo juu kuwa ni Noun, Feminine in nature lenye maana ya “to cure, to provide recovery, to rescue, to effect one’s welfare.”; hii haina maana ya Yeshua/Joshua, ambayo ni noun na masculine in naturel!! Neno hili Soteria, si neno lenye misingi ya Kibiblia, bali ni neno la kiteolojia tu. Ndiyo maana ukitaka kulithibitisha kwa mujibu wa maandiko kwa misingi ya Line upon line, precept upon precept, here a little and there a little, huwezi kupata usahihi wa hicho kinachozungumziwa na badala yake wanateolojia, utawakuta wanalilazimisha kulifanya liwe na tenses tatu, jambo ambalo hata yale manusuru au maponyo, nayo huwekwa kwenye foleni ya wokovu ambao ni assurance of eternal life.
  b. Na hata ukiangalia jina la Kiebrania Yesua/Yeshua/Joshua kwa Kigiriki ni “Iesous”. Inaaminika kuwa, kisawe hiki, ndicho kilichozaa neno Jesus kutoka katika lugha ya Kiingereza au kihispaniola na waswahili tukawa na neno -Yesu. Hata injili iliyomhusu “Iesous” kwa Kigiriki ilijulikana kama “euaggelion”, kitenzi chake Euaggelizó -chenye maana ya kutangaza habari njema ya ufalme wa Mungu. Baadaye katika Agano Jipya, tunaiona “euaggelion”, hiyo ikibadilika na kuwa ‘mwili’, “Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli” – Yohana 1:14. Huyu ‘mwili’, ndiye Paulo amekuwa akimsisitiza watu wampokee maana yeye ndiye wokovu wenyewe; “na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.” – Wafilipi 2:11. Na huyu (Kristo) ndiye atakayekuja katika mwili kuwaokoa watu wakiwa katika miili yao iliyobadilishwa kufumba na kufumbua -1 korinto 15:50-55. Mtu yeyote asiyeamini hivi, huyo ni wakala wa mpinga Kristo. “Kwa maana wadanganyifu wengi wametokea duniani, wasiokiri ya kuwa Yesu Kristo yuaja katika mwili. Huyo ndiye yule mdanganyifu na mpinga Kristo”- 2 Yohana 1:7.

  Je, mbona Kuna aya zinzoonesha kuwa kuna kuokoka hata kabla ya ujio wa Kristo??
  Kuna aya chache ndani ya Biblia zinazotumiwa vibaya na watu ili kuhalalisha fundisho la kuokoka ilhali wakiwa duniani. Na aya hizi zimetafsiriwa na wanateolojia kuhalalisha dhana yao ya Soteria katika njeo tatu –past, present na future. Kimsingi ukisoma vizuri Biblia, utaona wazi kuwa, dhana ya tenses tatu haipo na kilichopo ni msamaha wa dhambi kwa wadhambi pindi wanapompokea Kristo, badiliko la tabia zao, maponyo ya maradhi n.k. Haya yote Mungu anaweza kuyatenda kwa yeyote na wala haitamaanisha kuwa, mtendewa ameokoka ilhali mauti ya kimwili na mashambulizi mengine ya ibilisi, vinamgonja!! Katika Biblia, kuna aya zinazoonesha manusuru/maponyo ya kimwili. Neno Soteria kwa maana ya mzizi wake kitenzi –sozo, limetumika sana. Mf.,
  a. Miongoni mwa aya zinazoonesha maponyo ya kimwili (physical deliverance) ni pamoja na hizi zifuatazo;
  Matthew 8:25 And his disciples came to him, and awoke him, saying, Lord, save (sozo) us: we perish.
  Matthew 14:30 But when he saw the wind boisterous, he was afraid; and beginning to sink, he cried, saying, Lord, save (sozo) me.
  Matthew 27:42 He saved (sozo) others; himself he cannot save. If he be the King of Israel, let him now come down from the cross, and we will believe him.
  Matthew 27:49 The rest said, Let be, let us see whether Elias will come to save (sozo) him.
  Mark 15:30 save (sozo) thyself, and come down from the cross.
  Luke 23:39 And one of the malefactors which were hanged railed on him, saying, If thou be Christ, save (sozo) thyself and us.
  John 12:27 Now is my soul troubled; and what shall I say? Father, save (sozo) me from this hour: but for this cause came I unto this hour.
  Acts 27:31 Paul said to the centurion and to the soldiers, Except these abide in the ship, ye cannot be saved (sozo).
  James 5:15 And the prayer of faith shall save (sozo) the sick, and the Lord shall raise him up; and if he have committed sins, they shall be forgiven him.

  Kimsi huu siyo wokovu –eternal life!! Haya ni maponyo tu. Ni neema tu azipatazo mtu (na mara nyingine anaweza asizipate) pindi anapompokea au kumwamini Kristo kuwa anaweza kumtendea jambo Fulani katika maisha yake. Kwa misingi ya Maandiko, huu siyo wokovu kama wanateolojia wanavyosema.

  b. Miongoni mwa aya zinazoonesha msamaha wa dhambi na mabadiliko ya tabia (physical and spiritual changes) ni pamoja na hizi zifuatazo;
  1 Corinthians 1:18 For the preaching of the cross is to them that perish foolishness; but unto us which ARE BEING SAVED (SŌZOMENOIS) it is the power of God.
  Ephesians 2:5 Even when we were dead in sins, hath quickened us together with Christ, (by grace YE ARE BEING SAVED-SŌZESTHE;)
  Ephesians 2:8 For by grace are ye SAVED (SESŌSMENOI) through faith; and that not of yourselves: it is the gift of God:
  1 Timothy 2:4 Who will have all men TO BE SAVED (SŌTHĒNAI), and to come unto the knowledge of the truth.
  2 Timothy 1:9 Who hath SAVED (SŌSANTOS) us, and called us with an holy calling, not according to our works, but according to his own purpose and grace, which was given us in Christ Jesus before the world began,
  Titus 3:5 Not by works of righteousness which we have done, but according to his mercy HE SAVED (ESŌSEN) us, by the washing of regeneration, and renewing of the Holy Ghost;
  Romans 10:10 For with the heart man believeth unto righteousness; and with the mouth confession is made unto SALVATION (SŌTĒRIAN).
  2 Corinthians 6:2 For he saith, I have heard thee in a time accepted, and in the day OF SALVATION (SŌTĒRIAS) have I succoured thee: behold, now is the accepted time; behold, now is the day OF SALVATION (SŌTĒRIAS).
  Ephesians 1:13 In whom ye also trusted, after that ye heard the word of truth, the gospel of your SALVATION(SŌTĒRIAS): in whom also after that ye believed, ye were sealed with that holy Spirit of promise,
  Ephesians 6:17 And take the helmet of SALVATION (SŌTĒRIOU), and the sword of the Spirit, which is the word of God:
  2 Timothy 3:15 And that from a child thou hast known the holy scriptures, which are able to make thee wise unto SALVATION (SŌTĒRIAN) through faith which is in Christ Jesus.
  Hebrews 6:9 But, beloved, we are persuaded better things of you, and things that accompany SALVATION(SŌTĒRIAS), though we thus speak.
  Nitoe angalizo kidogo hapa. Aya zote tulizoziona hapo juu, mzizi kitenzi chake ni sozo, pamoja na kwamba, kuna tofauti za njeo, viwakilishi vya watenda n.k. zinazoonesha maumbo tofauti ya vitenzi hivyo, ambavyo katika baadhi ya Indo-European languages, kama vile Kilatini, Kihispaniola, Kiarabu n.k., infixation process (mchakato wa kuambika viambishi ndani ya mzizi wa neno) huwa ipo. Sitaki kwenda kwenye isimu zaidi. Msomaji mwenyewe afuatilie.
  Biblia iko wazi sana. Kama tulivyoangalia dhana ya maponyo/manusuru katika kipengele cha a. hapo juu, kuwa neno okoa/wokovu limetumika, dhana hiyo inafanana na hii nyingine hapo juu (b. yenye mzizi –sozo vilevile), yenye maana ya msamaha (unaofanywa na Mungu tu). Kwa upande mwingine, mtu anapoisoma Biblia (hasa aya hizo hapo b. juu), atagundua kuwa, watu wanapomwamini Kristo, huhesabiwa haki kwa njia ya imani. Kwa maneno mengine, mambo ya zamani hufutwa na kuonekana wapya mbele za Kristo –yaani watu wasio na mawaaa!! Kadri maisha yanavyosonga kwa watu hao, mashambulizi ya ibilisi dhidi yao huzidi kila uchao kadri wanavyomsogelea Kristo, na pengine wengine hujikuta katika ulimwengu wa dhambi japo unaweza usiwe sawa na ule uasi wa hapo mwanzo kabla hawajaamini!! Pamoja na kwamba walihesabiwa haki kwa imani, na sasa wanaonekana kuvunja tena sheria za Mungu, naam hata kwa fikra tu, kimsingi wanahitaji toba. Kwa nini wahitaji toba kama walishahesabiwa haki kwa imani? Mbona wako salama hao? Jibu ni hapana!! Kiroho wanaweza kuwa salama kweli kwa kiasi fulani, lakini kimwili na kiroho pia, hawako salama. Ndiyo maana wanahitaji kufa kila siku katika ulimwengu wa dhambi (carnal mind) kama Paulo anavyosema, “Naam, ndugu, kwa huku kujisifu kwangu niliko nako juu yenu katika Kristo Yesu Bwana wetu, ninakufa kila siku”, -1 Wakorintho 15:31. Mtu aliyeokoka (kwa maana ya jina la Yesu), hawezi kuwa anakufa kila siku. Kwa mujibu wa Biblia, mtu aliyehesabiwa haki (dikaioo –justified), -yaani mtu mwenye haki, ni yule anayemwamini Mungu/Kristo na kuishi sawasawa na sheria zake. Huwezi kuwa mwenye haki mbele za Mungu, kama wewe bado ni mvunja sheria za Mungu ikiwemo na Sabato. Tangu Agano la Kale hadi Jipya, Biblia inaonesha kuwa, wenye haki ni wale ambao wamekuwa wakimwamini Mungu na kutii/kufuata sheria zake. “Kwa sababu Ibrahimu alisikia sauti yangu (alimwamini Mungu), akayahifadhi maagizo yangu, na amri zangu, na hukumu zangu, na sheria zangu (kisha akaenenda sawasawa na sauti hiyo)”., Mwanzo 26:5. Biblia inatuambia kuwa, pamoja na jitihada hizo za Ibrahimu, hakuna hata aya moja inayosema kuwa Ibrahimu aliokoka!! Badala yake, Biblia inatuambia kuwa, Ibrahimu pamoja na uzao wake (mashujaa wa imani), walilala umauti wakiwa hawajaipokea ile ahadi ya kuokolewa from eternal condemnation!! “Hawa wote wakafa katika imani, wasijazipokea zile ahadi, bali wakaziona tokea mbali na kuzishangilia, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya nchi”, -Ebrania 11:13. Kama sisi ni uzao wa Ibrahimu (Israel wa Kiroho), hatuwezi kujigamba kusema kuwa tumemtangulia kuokoka hata baba yetu wa imani –Ibrahimu ambaye yeye bado anaingoja hiyo ahadi kaburini!! Kimsingi, tunafanya vichekesho sana!! Na kupitia teolojia, shetani amekamata sana uelewa wetu katika jambo hili!! Tumeaminishwa kuwa, wanateolojia ndio watu pekee wenye Roho Mtakatifu wa kuwafunulia neno!! Tumesahau kuwa Mungu hana upendeleo. Mungu atusaidie tunapojaribu kuliangalia kwa marefu na mapana yake kwa mujibu wa Biblia na Biblia pekee.

  Itaendelea kipande kidogo kilichosalia…

 46. Siyi rafiki yangu,

  Hayo yote umeyatafutiliza kwa ajili tu ya kukana kuwa hakuna wokovu duniani? It’s very sad.

  Sijui hata ujasiri unautoa wapi wa kuleta hoja ndeefu hiyo lakini haina nguvu ya kuthibitisha kuwa hakuna kuokoka duniani.

  Unajaribu kurudi nyuma sana ambako kimsingi tulishapavuka na tukaendelea mbele sana katika kuchangia hii mada.

  Kitu cha msingi kabisa ambacho ulipaswa kufanya ni kuikanusha ile mistari yote niliyokupa inayosema tumeokolewa au tuliokolewa/ alituokoa/ ametuokoa.

  Kama utaweza kusema ilimaanisha nini hiyo mistari tofauti na kile ambacho sisi akina Sungura tunaelewa ilimaanisha.

  Halafu fikiria vizuri unapoongelea uzima wa milele, maana nakuona unaelekea njia isiyo!

  Take care!

 47. Sungura, na wengine,
  Shalom
  Mnisamehe kwa kuchelewa kuleta mwendelezo wa kile nilichokisema kuwa, ni historia ya matumizi ya neno WOKOVU. Nilibanana wapendwa. Majukumu yalinizidi sana. Ila kwa sasa, napumua kidogo. ndio maana nimeleta. Badp pachiko moja linakuja kukamilisha series nzima. Karibuni tuendelee.

  Kama tulivyokwisha kuona hapo mwanzo katika Agano la Kale ya kwamba Kristo ndiye Mungu muumbaji, -wokovu na mwokozi wet; ni vyema sasa tukaangalia kama zama hizo za Agano la Kale watu waliokolewa –walipata wokovu kwa maana ya jina la Kristo au walipata kitu kingine tu.
  Wokovu katika Agano la Kale
  Napenda nianzie kwenye tukio la anguko la mwanadamu bustanini badala ya kuanzia huko nyuma zaidi ili niikwepe theolojia. Adamu alipoanguka dhambini, sote tunaelewa yaliyotokea. Jambo la msingi katika mada yetu, ni kile kitendo alichokifanya Mungu cha kuutangazia ulimwengu kuwa, pamoja na ibilisi kuughiribu, bado kuna ushindi kwa watu wake (kanisa lake) dhidi ya ibilisi na uzao wake kwa njia ya Mwana wa Mungu (uzao wa mwanamke –Yesu Kristo). Mungu anasema, “nami nitaweka uadui kati yako(wewe ibilisi) na huyo mwanamke (kanisa langu-watu wangu-Ebrania 2:14), na kati ya uzao wako (wafuasi wa ibilisi) na uzao wake(wafuasi wa Kristo); huo utakuponda kichwa (utakushinda siku zote/utakugharikisha), na wewe utamponda kisigino (utawafanya wachechemee tu lakini hutawafanya lolote zaidi)”-mwanzo 3:15. Utekelezaji wa tangazo hili, ulienda sambasamba na Mungu kumchinjia Adamu mnyama (kumwaga damu kwa ajili ya nusuru la kifo cha papo hapo) na kisha kuwavika vazi lingine la mnyama huyo –ngozi yake, -mwanzo 3:21. Na kwa sababu ya upendo wa Mungu kwa wadhambi hao, Mungu anatoa kielelezo cha kile ambacho mwanaye angekuja kukifanya kwa ajili ya ondoleo la dhambi za watu hao –Yohana 11:25-26 na Ufunuo 1:18; 21:4. Na kwa vile wokovu ulifanywa kuwa ni wa masharti baada ya anguko, ndipo kila mdhambi hata baada ya uzao wa Adamu alipaswa kufanya masharti hayo –kutoa kafara za wanyama kwa ajili ya ondoleo la dhambi. Aliyekiuka utaratibu huo wa ibada kama akina Kaini, dhambi ilikaa naam iliwaotea milangoni mwao.

  Baada ya Adamu, Mungu ameonekana kuwa akiwanusuru watu ambao wamekuwa wakifikwa na mabaya kwa sababu ya dhambi (uvunjaji wa sheria zake) na hasa wale ambao wamekuwa wakitambua makosa yao, na kutubu kwa ajili ya kuja kuokolewa milele baadaye. Hakuna nusuru lililotolewa na Mungu kwa waasi. Nipende kusema kuwa, nusuru (temporal delivarence) siyo uzima wa milele (eternal life). Mungu amekuwa akiwawanusuru wote ambao wamekuwa wakiishi kwa kutii na kuheshimu maagizo yake, ili baadaye, aje awaokoe, naam hata wale waliokufa “katika imani, wasijazipokea zile ahadi, bali wakaziona tokea mbali na kuzishangilia, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya nchi”- Waebrania 11:13. Hata wale walioonekana kuziasi sheria zake kabla, Mungu aliwanusuru pale walipoamua kurejea, kutubu, kurudi au kugeuka mioyo yaani -‘Shuwb’ kama hatua ya muhimu ya kuokoa nafsi (miili iliyo hai) zisife kwa dhambi na hatimaye zikose uzima wa milele baadaye. Matokeo hayo ya ‘Shuwb’ yaliwafanya watu kupata liwazo, farijiko, pumziko, ahueni, uhuru yaani –‘Nacham – naw-kham’ au tamîm. Lengo la Mungu kuwapatia ‘Nacham’ hii lilikuwa ni kuwafanya waishi maisha matakatifu yenye tumaini la kuja kuokolewa baadaye ili wapate uzima wa milele hata kama hapa katikati wangelala usingizi wa mauti. Katika Agano la Kale, matumizi ya neno wokovu, yalimaanisha ‘Nacham’ lenye maana ya manusuru ya muda ya uhai wa mtu, manusuru ya maradhi, majanga, maadui n.k. Manusuru hayo yalienda sambasamba na utoaji wa kafara za wanyama kwa wadhambi ambayo kimsingi yalikuwa ni ya muda tu maana hayakuondoa dhambi. Yote haya, yalilenga wokovu wa milele ambao Masihi angekuja kuwaokoa watu wake na hukumu ya milele (eternal condemnation). Mifano ya aya ndani ya Biblia zilizotumika kumaanisha manusuru…

  “Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa Bwana atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele” Kutoka 14:13;
  1 Sam. 11:11-13, “Ikawa, kesho yake, Sauli akawapanga watu katika vikosi vitatu; nao wakaingia katikati ya marago kwenye zamu ya asubuhi, wakawapiga Waamoni hata wakati wa jua kali; kisha ikawa wale waliosalia wakatawanyika, hata wasiachwe wawili wao pamoja. Ndipo watu walipomwambia Samweli, Ni nani yule aliyesema, Je! Huyo Sauli atatutawala? Walete watu hao, ili tuwaue. Lakini Sauli akasema, Hakuna mtu atakayeuawa leo, maana leo Bwana amefanya wokovu katika Israeli. Lakini Sauli akasema, Hakuna mtu atakayeuawa leo, maana leo Bwana amefanya wokovu katika Israeli”. nk.

  Je, ndani ya Agano la Kale, Neno WOKOVU kwa maana ya Yesha/Yeshua lilitumika pia??

  Jibu ni NDIYO! Neno WOKOVU lilitumika kumrejelea Mungu mwenyewe. Likiwa limetajwa mara 140 katika Agano la Kale. Na pale neno Wokovu –Yeshua, yaani mwokozi lilipotumika, lilitumika kumrejelea Mungu mwenyewe, ambaye ndiye wokovu. Mf. Limetumika kumtaja Kristo- Yeshua/Joshua

  “Wokovu wako nimeungoja, Ee Bwana”- Mwanzo 49:18,
  Zaburi 18:46 Bwana ndiye aliye hai; Na ahimidiwe mwamba wangu; Na atukuzwe Mungu wa wokovu wangu
  Zaburi 25:5 Uniongoze katika kweli yako, Na kunifundisha. Maana Wewe ndiwe Mungu wa wokovu wangu, Nakungoja Wewe mchana kutwa.
  Zaburi 27:1 Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani? Bwana ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani?
  Isaya 12:2 Tazama, Mungu ndiye wokovu wangu; Nitatumaini wala sitaogopa; Maana Bwana YEHOVA ni nguvu zangu na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu.
  Isaya 62:11 Tazama, Bwana ametangaza habari mpaka mwisho wa dunia, Mwambieni binti Sayuni, Tazama, wokovu wako unakuja; Tazama, thawabu yake i pamoja naye, Na malipo yake yako mbele zake nk

  Hivyo, neno WOKOVU (Salvation) kwa maana ya Kristo –“Yeshua/Yesha/Joshua au YAHWE”, katika Agano la Kale, lilitumika kumrejelea Mungu mwenyewe aghalabu kiunabii kwa ajili ya utimilifu wake wa Masihi katika Agano Jipya. Pale lilipotumika kama kitenzi kumwelezea Mungu atakayeokoa watu kutoka kwenye hukumu ya milele, neno ‘yasha’ lenye maana ya save/deliver lilitumika. Kwa hiyo, tuna “yasha” kama kitenzi, kinachozaa “Yeshua/Joshua” kama nomino; ambayo huwezi kuyakuta kokote kwingineko isipokuwa pale Mungu mwenyewe alipotajwa kuhusika kwenye wokovu wa kuwatoa watu kwenye hukumu ya milele

  Itaendelea….
  Siyi

 48. Siyi,

  Karibu sana ndg!

  Naomba tu uendelee ili nikupate kwa utimilifu wote.

  Karibu!

 49. Sungura,
  Nakusalimu katika Kristo. Samahani nilitingwa na majukumu tu ndiyo maana nikachelewa kuleta hoja niliyoahidi. Naomba leo tuanze na sehemu ya utangulizi wa hoja yangu…..
  Utangulizi

  Awali ya yote, inabidi tutambue kuwa Yesu ndiye aliyeumba mbingu na vyote vilivyomo. Biblia inasema, “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika” –Yoh. 1:1-3. Maandiko yanatuthibitishia kuwa, Kristo amekuwapo tangu uumbaji. “Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake”, – Wakolosai 1:16. Kwa maneno mengine, “Kwa neno (Neno wa Yohana 1) la Bwana mbingu zilifanyika, Na jeshi lake lote kwa pumzi ya kinywa chake”, – Zaburi 33:6. Kwa hiyo Yesu ndiye aliyesema na vyote vikawa.

  Maana ya Jina la Yesu

  Jina Yesu, linatokana na tafsiri ya Kiingereza –Jesus ambayo nayo ilichomolewa kwenye lugha chanzi –Kiebrania ikisomeka kama Yeshua au “Yoshiah” likiwa na maana “Ataokoa”. Biblia inasema, “And she shall bring forth a son, and thou shalt call his name Jesus [YESHUA (SALVATION)]: for he shall save [or salvage] his people from their sins” (Matthew 1:21). Ni Mungu ambaye ni Sacred, – Qadosh au Kedushsha –(Resp. 5), (Mtakatifu aliye Bwana wa Sabato) —“One is our God; One, our Father; One, our King; One, our Saviour; One…”, Online jewish encyclopedia. Zama za Agano la Kale, alikuwa Mungu aliyejitambulisha kama mwokozi – (redeemer > go’el, kutoka kwenye kitenzi ga’al -“to redeem”. Maana ya jina hili, – Yeshua ” -“Ataokoa”, lililenga destination ya kitendo SAVE. Kuwatoa watu wake aliowaumba kwenye dunia aliyoiharibu ibilisi baada ya uasi wake. Pamoja na Mungu (Yesu), kufanya manusuru ya muda kadhaa kwa ajili ya toba katika Agano la Kale ukianzia na tukio la Mungu kuwachinjia kondoo bustanini kwa ajili ya toba, hayo yote yalikuwa ni ISHARA ya kile alichokifanya msalabani na ambacho atakihitimisha siku si nyingi zijazo!

  Sasa, jina la Yesu kama mwokozi, kiebrania linasomeka kama “yasha” likitamkwa kama “(yaw-shah’)” likiwa na maana ya okoa –save/deliver. Wokovu unasomekaje kwa Kiebrania? Jina/Neno wokovu, ni nomino dhahania yenye maana ya Mungu Mwenyewe rejea Kedushsha/Qadosh hapo juu. Biblia inasema, “…Bwana ndiye jabali langu, na ngome yangu, na mwokozi wangu, naam, wangu; Mungu wa mwamba wangu, nitamwamini yeye; Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, mnara wangu, na makimbilio yangu; Mwokozi wangu, waniokoa na jeuri”, -2 Samweli 22:2,3. Mungu mwenyewe ndiye wokovu – Yesha au Elishua (masculine in nature). Yeye ndiye WOKOVU/UZIMA wa milele –Ayasha au Ayashah. Wakati wa Musa, alijulikana kama Yehoshua, -Bwana (YHWH) ni WOKOVU. http://biblehub.net/searchstrongs.php?q=salvation.
  Neno Sodzo, mimi sijaliona.

  Katika Agano la Kale, Kristo amejitambulisha sana kwa jina hilo la Mwokozi. “Maana mimi ni Bwana, Mungu wako; Mtakatifu wa Israeli, mwokozi wako, nimetoa Misri kuwa ukombozi wako; nimetoa Kushi na Seba kwa ajili yako, …Mimi, naam, mimi, ni Bwana, zaidi yangu mimi hapana mwokozi.” –Isaya 43:3, 11. “Hubirini, toeni habari; naam, na wafanye mashauri pamoja; ni nani aliyeonyesha haya tangu zamani za kale? Ni nani aliyeyahubiri hapo zamani? Si mimi, Bwana? Wala hapana Mungu zaidi ya mimi; Mungu mwenye haki, mwokozi; hapana mwingine zaidi ya mimi” –Isaya 45:21

  Tutaendelea… ukiwa na swali leta haraka!!
  siyi

 50. Haya Siyi,
  Hebu “nena kwa lugha” kidogo hapa Sungura ajue kwamba ile “roho ya unabii” iliyokuwa kwa White sasa imehamia kwako!!!

 51. Hahahaaa,

  Come back quickly Siyi.

  Am hungrily waiting!

  Si nilikwambia hiyo mistari inakusumbua, na bado kuna nondo za kutosha tu nimezituliza chini, unapochelewa kujibu unanichelewesha kuziachia.

  Njoo tafadhali!

 52. Sungura,
  Nimeahidi kuanika chote ulichoudanganya umma wa SG. Wewe subiri tu. NAkuja!!

 53. Siyi,

  Acha utoto!

  Kama umetafuta kwenye google hujapata basi, cha msingi/muhimu siyo kujadili maneno Sozo na Soteria. Cha muhimu ni mistari ya biblia inayosema tumeokolewa, na iko hapo ninekupa.

  Na nashangaa unaponiambia kuwa hiyo mistari ndo nashikia mpini, ulitaka nishikie mpini nini, google au kitu gani?

  Na iko mistari mingi tu. Kwa hiyo wewe kama hukubali kinachosemwa ktk hiyo mistari, kipinge hapa hadharani.

  Au la, kama huna cha kupinga, basi kubali hapa hadharani pia, kuwa wokovu ni sasa kama biblia inavyosema.

  Najua hiyo mistari inakusumbua Siyi!

 54. SUngura,
  KWenye google kuna website nyingi. Cites nyingi!! Hebu nielekeze niende website/cite ipi palipo na source za Sodzo na Soteria? Nielekeze tu. ZIle ya za Biblia ndo na wewe unataka kushikia mpini au? Kufikia nakuuliza hivyo, mimi si tahira kaka. Nimeenda kote huko. Nimeishia kizungumkuti tu! Nimekuomba ulete rejea. Acha mchezo kaka. I’m really serious on this!!
  Nahitaji rejea basi, ili tuanzie hapo.
  Nakungoja sana
  Siyi

 55. Siyi,
  No thank u!

  Nimejadili mistari inayoongelea kuokoka na wokovu, hasa inayoonesha kuwa tayari wokovu upo!

  Wewe unataka tujadili neno Sozo na Soteria, hii si sawa. Hapa mjadala si Kigiriki wala Kiebrania, kama unataka hizo lugha tafuta kuna biblia za hizo lugha.

  Unataka nikupe source gani wakati nimekwambia u-google nawe utayapata hayo maneno ya Kiyunani na mistari ambayo iko kwenye biblia ambayo biblia za hiyo lugha zimetumia hayo maneno?

  Do your homework bwana, acha kuleta visingizio visivyo na nashiko.

  Umeniambia kuwa hata mistari niliyonukuu kwenye biblia ina ukakasi. Hapo ndo napataka haswaa, nionyeshe huo ukakasi tafadhali!

  Ni hayo tu kwa leo!

 56. Sungura,
  Kaka sina siasa wala zengwe kwenye jambo hili! Ninachosema, ni wewe tu kunithibitishia kile ulichosema kuhusu Sodzo na Soteria katika Kiebrania na Kigiriki kwa kunipatia rejea. Hata kwenye aya za Biblia ulizonipa, kuna ukakasi mkubwa tu. Huenda mimi sijafanikiwa kuipata aya inayotaja maneno Sodzo na Soteria, hivyo nitaomba msaada wako. Maana tunafundishana!!
  Leo sitaki kuwa na maneno mengi. Lakini nakuomba unipatie chanzo au aya husika inayotaja Sodzo au Soteria kwa Kiebrania na Kigiriki ili kuanzia hapo, tuijadili mada. Nina mambo mengi ya kusema, lakini kwanza, naomba hilo tu kwa sasa!! Mwambie hata Lwembe akusaidie kupata hizo rejea maana na yeye aliyarejea (yale maneno) kwenye michango yake.
  Wasalaam
  Siyi

 57. Sungura,
  Kaka sina siasa wala zengwe kwenye jambo hili! Ninachosema, ni wewe tu kunithibitishia kile ulichosema kuhusu Sodzo na Soteria katika Kiebrania na Kigiriki kwa kunipatia rejea. Hata kwenye aya za Biblia ulizonipa, kuna ukakasi mkubwa tu. Huenda mimi sijafanikiwa kuipata aya inayotaja maneno Sodzo na Soteria, hivyo nitaomba msaada wako. Maana tunafundishana!!
  Leo sitaki kuwa na maneno mengi. Lakini nakuomba unipatie chanzo au aya husika inayotaja Sodzo au Soteria kwa Kiebrania na Kigiriki ili kuanzia hapo, tuijadili mada. Nina mambo mengi ya kusema, lakini kwanza, naomba hilo tu kwa sasa!! Mwambie hata Lwembe akusaidie kupata hizo rejea maana na yeye aliyarejea (yale maneno) kwenye michango yake.
  Wasalaam
  Siyi

 58. Siyi,
  Ngoja niiweke sawa zaidi hii;

  Kuwaza kwamba huwezi kuwa umeokoka ukiwa duniani just kwa sababu shetani ungali duniani na kesho anaweza akakurejesha gizani/ dhambini/ mautini ni kujaribu kuuhoji uwezo wa Mungu wa kutulinda dhidi ya shetani. Ambapo kulindwa dhidi ya mwovu ni part ya Wokovu( Soteria)

 59. Siyi,

  Nimeamua kuwa very specific sasa hivi kwenye hii mada ili tufikie hitimisho yakinifu na lililo wazi.

  Lakini wewe bado unaleta politics ambazo zina utando mwingi wa kuendelea kujadili mambo kwa ujumlajumla.

  Sikia brother, mimi kukupa rejea maalum za google au kitabu nilikosoma maneno Sozo na Soteria hakuna uzito kuzidi rejea ya maandiko ambayo nimeyaweka kwenye comment yangu.

  Tafadhali usijaribu kukwepa wajibu kirahisi namna hiyo. Wewe yaangalie hayo maandiko niliyonukuu kisha nenda mwenyewe kwenye lugha za asili unazozijua au kiingereza uone wamesemaje.

  Tofauti na falsafa na misemo ya Kiswahili, kisemantiki kuokoka ni kumtukana mamba kabla ya kuvuka mto, maana kuvuka huo mto kuko chini ya uwezo wa utashi wako.(if u know wat am saying)

  Na nilinukuu tu maandiko ambayo hata kwa version za Kiingereza yanasomeka ‘save’kwa maana ya kutolewa katika ulimwengu wa giza kwenda wa nuru.

  Unacholazimisha kuwa wokovu ni wa milele, kwamba tunaponywa milele, tunakombolewa milele, tunasamehewa milele, tunanusuriwa milele, n.k huwezi ukakipatia rejea ya maandiko, kwa sababu kiko katika dhana ya kufikirika zaidi.

  Suala la mtu kudumu katika kuchagua kwake uzima au kifo liko katika uwezo wa utashi wake, wala haliko ktk uwezo wa Mungu. Hilo limewekwa chini ya utashi wa mtu, yaani kule kuendelea kukaa nuruni au kuamua kurudi gizani liko chini ya mwanadamu husika wala si Mungu.

  Kuwaza kwamba huwezi kuwa umeokoka
  Just kwa sababu kesho unaweza ukaamua kutenda dhambi, ama kurejea gizani ni kujaribu kumwona Mungu kuwa hana uwezo wa kutosha wa kukulinda ( ambapo kulindwa dhidi ya mwovu ni part ya Soteria) hadi unapofika kwenye wakati wa kuingia kwenye umilele.

  Siyi, dont bit around the bush plz, chukua hayo maandiko niliyonukuu kwenye comment yangu iliyopita, fanya rejea zako zote unazozijua halafu uone kama yatakuletea tafsiri inayosema kuwa hatuokoki tukiwa duniani.

  Nalijua neno Kuokoka na Wokovu kwa upana wake, ikiwa ni pamoja na hivyo visawe vyake ulivyovisema.

  Kunyakuliwa ni moja tu ya hivyo visawe, na wala siyo maana kuu ya Kuokoka au Wokovu.

  Nipe majibu brother.

 60. Sungura,
  Wewe ni ndugu yangu, rafiki yangu na mtu unayependwa sana na mimi. Hata kama nitakukosea, sitaachelea kukuomba radhi. Halikadhalika ukinikosea, sitachelea kukusamehe hata kabla ya kuniomba msamaha!! Unachokisema, kwa akili ya kawaida, inaonekana mimi sikujitaabisha kujua maana za maneno haya –Sodzo na Soteria. Nilijitaabisha sana rafiki yangu. Kwenye google unakoniambia niende, nilishaenda, na kukutana na mambo tofauti, ndio maana nikaomba unieleze rejea uliyotumia wewe ili inisaidie na mimi pia. Vinginevyo, baada ya kuona dhana tofauti za maneno hayo na ulivyotufundisha wewe hapa kwenye blog, nilishawishika kujua ulipoyatoa!! Hilo tu basi!! Na nitaendelea kuomba ufanye hivyo, maana hata kwenye google, kuna wavuti/tovuti nyingi sana. Ni wavuti/tovuti ipi? Sema tu usiogope kaka!!
  Aidha, si lazima kukitumia kitu ni mpaka ulishamuona aliyekitengeneza!! Hata mimi sikukuuliza habari za Calvin John. Nilichokwambia ni kuhusu doctrine zake ambazo kwa kiasi kikubwa, zinayasumbua sana makanisa ya kikristo hadi leo. Na siyo kanisani kwenu tu. Ni makanisa mengi. Na walio wengi wetu, hatujui kama tunatumia falsafa za John Calvin! Tunaamini kuwa ni mafundisho ya Mungu kumbe sivyo!! Nilipokwambia, nilitarajia badala ya kujibu kwa ghadhabu kubwa, ungelifanyia kazi ili kujiridhisha katika hilo. Au ungeniuliza kuthibitisha nilichokisema!! LAkini badala yake, umekuja na maneno ya dhihaka, wala sijakua nk…Pole ndugu yangu!!
  Shida ninayoiona kwenu, ni multiple matumizi ya neno ‘okoa’ kama vile neno ‘pamba’ lilivyo na maana nyingi. Ni kweli kuwa neno la ‘okoa’ lina maana zinazohusiana. Pengine tungesema kuwa lina visawe murua vyenye ukuruba!! Okoa, lina visawe kama vile ponya, afua, nusuru, salimisha, linda nk. Kazi iliyopo, ni kukwambia tofauti ya kimaana kwenye visawe hivi na ukaelewa, maana una pre-conceived ya cult doctrines!! Hatima ya jukumu la Kristo, ilikuwa ni kutuokoa milele, kutuponya milele, kutulinda milele, kutusalimisha milele, kutunusuru milele, kutuafua milele nk. Kama tutalichukua neno OKOA na kulitumia kwa maana ya kusalimishwa milele, tutakuwa kwenye ile maana halisi ya jukumu la Kristo. Kwa sasa, hatuokolewi, maana ukisema tunaokolewa sasa, kama mwanafunzi wa Yesu, utapata shida kutofautisha kitendo cha kuokoa atakachokifanya Kristo na kile anachokifanya daktari au muuguzi –kunusuru maisha ya mgonjwa!! Na katika lugha ya Kiswahili, Biblia imetumia maneno hayo interchangeably!! Ndiyo maana nakuuliza ulete rejea ya Sodzo na Soteria ili zituongoze kwenye lugha awali za Biblia kusudi tupate maana lengwa ya kila neno lililotumika kwa mujibu wa faiwa husika. Maeneo mengine ndani ya Biblia za Kiingereza, maneno Save, rescue, etc , yametumika interchangeably!
  Mimi nazidi kukusitiza ulete rejea sawia za maneno SOdzo na Soteria ili zituongoze kwenye hitimisho la mada hii. Nakungoja.
  Siyi

 61. Lwembe,
  Nimekuwa nawe kwa muda sasa. Nimejifunza mengi kwako. Kimsingi una mambo mazuri (mafundisho), yenye uzima ndani yake na mengine ni cults tupu! Cults tupu kaka!! Huwezi amini, kuwa kuna mamb uko chaka, hata huwa nashangaa kwa nini pamoja na ujanja wote huo ulio nao, umetekwa na teosofia!!?? Kwa nini??
  Shida yako iko hapo tu. Hutaki kuyachunguza mafundisho yenu kwa kujiridhisha upya wewe mwenyewe ukiaachilia dogma zenu!! Yako mengi ambayo uko chaka. Mf. Hili la ‘TUMEOKOKA”, Mungu ni Yesu, Yesu ni Roho Mtakatifu na Roho Mtakatifu ni Mungu (yaani wote hawa ni Mungu mmoja), Anguko la Adamu na Hawa bustanini, mfumo wa ibada ya Mungu nk. Yako mengi. Na hapa siko kwa ajili ya kuyajadili. Tulishayajadili mengi huko nyuma.
  Ninachotaka kusema ni kuwa, Mungu bado anatupenda sana mimi, wewe, Sungura, Milinga. Seleli, Ziragora, Janeth, Magreth, Mariam, Mhina, Pendeli, Yusha,Mjema, Kamugisha na wengine wengi hapa kwenye blog. Siwezi kuamliza kuayataja majina yao. Wengi sana. Mungu anatupenda sana marafiki zangu. Na kwa sababu anatupenda, nasi hatuna budi kumpenda pia –kuzishika amri zake.
  Aidha, kama imeonekana kutofautiana kwenye fundisho hili la tumeokoka, tunaokoka na tutaokoka, kisiwe kigezo cha kuitana majina lukuki weee yasomaana. Sisi sote tu mali ya Mungu. Na Mungu atatuokoa si kwa sababu tulihojiana sana hapa kwenye blogi, bali ni kwa sababu tuliujua ukweli na tukaishi sawasawa na ukweli huo. Tutaokolewa kwa kuzishika amri za Mungu. Sina maana kwamba naleta uligalism hapa. Hasha!! Ninachosema ni kwamba, hatuwezi kuwa wenye haki(watakatifu), isipokuwa tumeishi sawasawa na Neno la Mungu (imani + matendo ya Neno/sheria). Hii ndiyo imani hai itakayotuokoa!
  Tukiendelea kudanganyana kuwa tumeokoka ilhali tuko kwenye uasi mkuu wa kimafundisho, ibaada, tukimtaja na shetani kwenye ibada zetu kwa jina la kificho, n.k., tusitarajie kuuona ufalme wa Mungu. Tusiutarajie kabisa!! Maana badala ya kuwa na imani ya Mungu, tumehamia kwenye imani za mashetani. Tusipoutafuta ufalme wa Mungu kwa nguvu, tutapotea tu. Na hili ndilo lingekuwa kusudio letu sote kwamba, tufanye nini ili tuurithi uzima wa milele?? Jawabu la Kristo lingeendelea kubaki lilelile “Wazijua amri, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo, Usidanganye, Waheshimu baba yako na mama yako”??? – Marko 10:19. Ni vyema kwanza tungejitathimini kulijibu swali hili mioyoni mwetu kama kweli tumeyashika hayo yote; ndipo tungekuwa na ujasiri wa kujibu na hoja ya pili ya kumpenda Mungu zaidi ya mali zetu, wadhifa wetu, nk. Maana imeandikwa, “…kila mmoja wenu asiyeacha vyote alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wangu” – Luka 14:33. Swali kwako kaka Lwembe, Una nini ulicho nacho mkononi mwako??

  Unaweza kuwa na majibu mengi. Lakini mimi nakwambia, usipokubali kuacha cults zenu, watu wa kwenu (pengine waumini wenzako), kazi nzuri uliyo nayo, mali uliyojilimbikizia, cheo kizuri ulicho nacho kanisani kwako nk, huwezi kuwa mfuasi wa Kristo. Wokovu ni wa mtu mwenyewe. Huna budi kuamua mwenyewe!! Ukiamua kufanya hivyo, hutaitwa mkristo tu na wala hutaitwa tu kwa jina la kanisa lenu, bali utaikwa kwa jina la mwanafunzi halisi wa Kristo –mtarajiwa wa ufalme wa Mungu. Nilipoligundua hili, sikuona sababu ya kuitwa msabato, mkatholiki, mlutheri nk. bali kuwa mimi na Mungu wangu.

  Mungu anasema “…mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka” – Mathayo 24:13. Na kulitambua hilo basi, hatuna kumtafute Bwana, maadamu anapatikana, kumuita, maadamu yu karibu, Isaya 55:6.
  Bwana akubarini sana.
  Siyi

 62. Mistari ya maandiko niliyomalizia ni 1Cor 1:18 … Neno la msalaba kwa wanaopotea……!

 63. Siyi,

  Napiga konde moyo ili nisikujibu sawasawa na ulivyonijibu, maana haitatusaidia chochote. Hakuna kitu ulichonipatia nacho, wala hakuna kitu nilichokwepa.

  Unaweza hata ukagoogle ili upate maana ya hayo maneno ya Kigiriki Sozo na Soteria, na utapata source nyingi tu kuyahusuna rejea zake kwenye maandiko.

  Halafu usipende sana kumlazimishia mtu kitu kama afanyavyo juha vile. Nilishakwambia sijawahi kusoma andishi hata moja la Calvin unayemsema. Lakini naona kila ukikosaga la kusema unalazimisha hilo. Grow up brother.

  Let ‘s go to the point now:

  Luka 23:35 soma utakuta haya maneno; aliokoa wengine sasa na ajiokoe mwenyewe ‘. Hapo Yesu walikuwa wanamwambia ajiokoe ina uhusiano gani na kufika mbinguni, au walikuwa wanamwambia aende mbinguni, na hao ambao wanasema Yesu aliwaokoa ni wapi hao? Na kumbuka hapo kuna past tense na present tense – Siyi nataka ujibu. Soma na 23:37 utakuta present tense ya Save.

  John 12: 27. Soma utakuta maneno haya’ Father save me from this hr’ maneno hayo yana maana gani Siyi?

  John 12:47; For I came not to judge the world but to save the world.
  Siyo Yesu atakaporudi ndo atakuja kuokoa ulimwengu, hiyo ambayo alishakuja ndo ilikuwa safari ya kuja kuokoa ulimwengu.

  1Cor 15:2; And u are being saved if u hold firmly to the message I preached to u, unless u belived in vain.

  Suala la kuokoka na kupoteza wokovu liko ndani ya hii mistari. Ba liko ktk hii sentesi “if u hold firmly” hiyo tungo ni conditional. Which means if u dont hold firmly unapoteza huko kuokolewa ulikookolewa.

  2Cor 2:15 …among those who are being saved…
  Siyi hiyo sentensi ni present tense, siyo future.

  1Tim 1:15 ….. Christ Jesus CAME into the World to save sinners….
  Haijasema Christ Jesu will come into the world to save sinners.
  Hata Paul alikuwa miongoni mwa waliokoka.

  Hiyo mistari kwa leo inatosha, maana nataka tuwe tunaongea tu kidogo ili kupunguza wingi wa maneno yasiyo ya muhimu sana.

  Siyi nataka ufike mahali ukubali kuwa inawezekana kabisa hujui maana ya neno Kuokoka na Wokovu. Kwamba unachofikiri kuwa ndio wokovu ni kitu kingine tu.

  Neno la msalaba kwa wanaopotea ni upuuzi, lakini kwetu sisi TUNAOOKOLEWA ni nguvu ya Mungu.

  Watch out!

  N

 64. Siyi,

  Duh! Kumbe hujui hata tunaokolewa na nini! Nakuona unavyojiongelesha mpaka umejifikisha kuamini kwamba Hukumu ni sawa na kupewa “pipi”!!!

  Hukumu kaka si mchezo, walimu wenu watakuwa wameipoza sana mpaka mnaiona ni jambo la “kuzawadiwa uzima wa milele na wengine kuzawadiwa umauti”!!! Hao wenyewe wanaopewa Uzima wa Milele huko mwisho wameponea kwenye “tundu la sindano”!!

  Dogo, kila siku nakusihi uchangamshe akili hiyo, lakini nakuona unajisikia umefiiika! Iwapo Mungu mwenyewe anashughulika na jinsi ya kuwaepusha wanae na Hukumu yake hiyo, halafu wewe ndio kwanza unalala tu unajionea shwaaari na sabato yako, eti “”ataniokoa na dunia yenye zambi atanipeleka nikaishi huko mbinguni, kweli uko sawa sawa dogo? Mal 4:5 “Angalieni, nitawapelekea Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya BWANA, iliyo kuu na kuogofya”!!!

  Waangalie hawa wenzako wanaoijua Hukumu:
  “Enyi nyoka, wana wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehanum?” (‭MT.‬ ‭23‬:‭33‬)
  Hahahaha….! Wanadhania Yohana anaandikisha majina upya!!!
  Ufu 20:11 “Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana.” Nyie ndo wale sehemu ambazo malaika wanabana mbawa zao zisipige kelele, nyie mnapita na kokoko zenu na miruzi mingi!!!

  Hao hapo wenzako wanahangaika na jinsi ya kuimbia hiyo Hukumu, wanajua kuwa majina yao hayajaandikwa ktk Kitabu cha Uzima, ule Uzao wa Nyoka, ndio hao hapo wanajaribu usajili!!!

  Angalau hao wanaijua shughuli huko mbele, shida iko kwetu tunaofutwa majina kutokana na huko kuongeza au kupunguza kutoka Neno la Mungu kwa uongozi wa dini; upofu tunaokuwa nao huwa ni mkubwa sana, kiasi kwamba hata ile mianya inayojichomoza mbele yetu ya kuikimbia Hukumu huwa hatuioni kabisa ktk siku zetu za kuendea huko kufutwa kwetu majina. Huenda tungeweza KUOKOKA kama tungelisimama kidogo kuyasikiliza tunayoambiwa! 2The 2:10-12 “Kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate KUOKOLEWA. Kwa hiyo Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo; ili wahukumiwe …”

  Basi ukisha kufutwa jina, mambo ya Mungu huwa hayaeleweki tena kwako, unabaki kuwa ni kasha tupu. Israeli walipomkosea Mungu kwa ile ibada ya ndama, walifutwa majina yao, ndio sababu walishindwa kuingia ktk nchi ya ahadi pale Kadesh Bania, imani ikiisha kuondolewa unabaki mtupu, ndio kama hivi, huna unalolielewa zaidi ya dini!!

  Ebr 10:31 “Ni jambo la kutisha kuanguka katika mikono ya Mungu aliye hai”; uwe makini dogo, otherwise PREPARE TO MEET GOD!!!

  Gbu!

 65. Sungura,
  Rafiki yangu, mimi nakufahamu kwa kiasi Fulani. Ukiguswa penyewe, ni kawaida yako kulalamika, kuonekana kama mwanadini saaana wakati huwa hukumbuki mtindo na namna unavyojibu wenzako. Sijui kama huwa unaliona hilo!! Nyani huwa haoni kundule!! Na hata huwa hutaki kujifunza kwa wengine. Na mimi sikuachii uendelee kupotosha rafiki yangu.
  Tangu mwanzo, nilikwambieni kuwa, Biblia imetumia neno okoa katika mukitadha wa kutoa hatarini kwa muda (kuponya). Mimi na Mjema tumetumia muda mwingi sana kukuelimisheni maana hiyo ya neno kwa mujibu lilivyotumika Agano la Kale na Jipya.
  Concept ya “Once Saved Always Saved” nilikwambia ni doctrine ya John Calvin. Very canning doctrine!! Na niliwaambia maana yake. Na huwa mnaitumia ndivyo visivyo!! Maana yeye (Calvin) alisema kuwa, Mungu anawajua walio wake. Kama umeandikiwa kufa, utakufa tu. Na kama umeandikiwa kuokoka, utaokoka tu bila kujali imani yako kwa Kristo ikoje! Ninyi mnajichanganya nayo bila ya kuielewa kiundani. Ninyi mnasema wokovu unaweza kupotezeka!! Calvin hakubaliani na dhana yenu hiyo. Mnadandia concept inayosema tofauti na hivyo mnavyoamini!! Kimsingi ninyi na yeye, nyote mko chaka ile mbaya!! Poleni sana.
  Kuhusu Sodzo na Soteria, tatizo ni nini? Mimi sikusema unipe maana ya maneno hayo, nilichotaka kujua, ni source ya hayo maneno. Uliyapata wapi? Lete chanzo chake. Acha kupiga chenga!! Maana najua kwa nini unapiga chenga. Umedanganya watu weee!! Sodzo, Soteria, Sodzo Soteria, ukitoa maana ulizoziona wewe zinaunga mkono hoja yako. Ulitudanganyaje!! Aaa, kweli wewe Sungura!! Ni Sungura kwelikweli!!
  Itabidi tukupatie zilizowiva tu, mbichi kwako ni shida!! Narudia kukuomba tena, kama uko sincere, nakuomba ukanushe definitions za Sodzo na Soteria ulizotupa au unipatie chanzo chake!! Sihitaji maneno mengi.
  Kama kweli unataka turudi kwenye mada husika. Leta chanzo cha Sodzo/soteria. Maana hizi ndizo msingi wa mada yenyewe. Hatuwezi kuzungumzia kitu bila kujua usuli wake.
  Acha kulalamika kaka. Leta hoja!!
  Siyi

 66. Siyi,

  Niwapongeze moderators wa SG.kwa uvumilivu wao wa kuziruhusu comment zako fulani hapa, hasa ulizomjibu Lwembe na zingine chache ukanijibu mim.

  Zina maneno ambayo kwa kweli ni ya kufuru kwa kiasi cha kutosha tu.

  Mimi niwe honest, nimekuvumilia sana ktk huu mjadala. Maana kwa std za kwangu za mijadala wewe hata hujui kujadili ila ni msumbufu tu.

  Pili, sikuwa nimegundua kuwa mjadala kupoteza wokovu umehamishiwa huku. Na mimi hii heading sikuwa nimeshawishika sana kuifuatilia, mpaka nilipoona watu wengi mnaijadili sana ndo nikagundua.

  Siyi mimi ningeomba tubadili sasa namna ya kujadili hii mada, sasa tuandike kwa kifupi na strait to the point, ambayo ni wokovu.

  Wewe unaandika maneno mengi sana ambayo hayako kwenye mada, na matokeo yake unaacha kujadili msingi wa mada na kujaza maneno yako tu.

  Back to the point ;
  Nitajibu swali lako la kwanza na la tatu, la pili sihitaji kujibu.

  1. Kunyakuliwa/ unyakuo (rapture) ni kile kitendo cha Yesu kuja kuchukua kanisa kwa ajili ya harusi ua mwanakondoo.
  – Kuokolewa, kwa kofupi ni kutolewa katika ulimwengu wa giza wa shetani na kuingizwa katika ulimwengu wa nuru wa Yesu Kristo.

  2. Neno Sodzo nililitumie mimi kwenye ile mada kwanza kabisa ya wokovu( once saved always saved)
  Neno Soteria wewe ndo ulilitumia kwa mara ya kwanza kwenye hiyohiyo mada, lakini kwa sababu nilikuwa nalifaham, niliendelea na mimi kulitumia interchangeably na neno Sodzo.

  Sasa unaponitaka nikuoneshe nilipoyatoa hayo maneno nakuona ni jinsi gani huwa hukumbuki ulikotoka.

  Tafuta ulikolitoa neno Soteria na neno Sodzo utalipata hukohuko.

  Siyi, unapoamua kuropoka kuwa mafundisho yetu ni kuzimu, sikushangai ila nakusikitikia sana.

  Hebu jaribu kufikiri kama wewe ungekuwa miongoni mwa mafarisayo waliojiona wanajua na wako sahihi mno, lakini kumbe walikuwa wamefichwa siri kubwa na kushindwa kuelewa kuwa huyo wanaemwambia anatoa pepo kwa belizebuli kumbe ndiye kristo mwenyewe wanaesema yuaja!

  Kwa ustaarabu kabisa nakushauri kama ni lazima kwa wewe kukufuru, basi tukufuru sisi akina Sungura, lakini kwa habari ya mafundisho tunayoyasema yenyewe yapinge tu kwa hoja na neno la Mungu maabna hiyo ndio maana ya mjadala. Lakini mafundisho tunayoyasema na kuyanukulia maandiko , hayo usiyakufuru.

  Siyi, tumekuthibitishieni kwa maandiko matakatifu yakisema tumeokolewa, tuliokolewa, tunaokolewa na tutaokolewa. Wewe unayaita hayo ni mafundisho ya kuzimu. Ni biblia inayosema yumeokolewa kwa neema, ni boblia inayosema utimilifu wa wakati ulipofika alituokoa, wewe unasema tumefundisha mafundisho ya kuzimu.

  Tumekuonesheni biblia inasema “sasa kumekuwa wokovu….

  Na neno lingine hili hapa: Tazama saa ya wokovu ni sasa( 2cor 6:2c)

  Tumekuonesheni Yesu anapowafundisha wanafunzi wake jinsi ya kusali: utuokoe na yule muovu..

  Wewe kila ukiibuka inaongea tu maneno yako; ya Mungu habahatishi, Mungu haokoi na kuangamiza, oh wokovu wenu ninyi ni kupotezeka, n.k

  Tuthibitishie basi kimaandiko kuwa Mungu haokoi na kuangamiza.

  Ulikataa Israel hawakuwa wameokoka kule kutoka Misri ispokuwa Kaleb na Joshua, tukakuthibitishia kwa maandiko, kuwa biblia onasema walikuwa wameokoka walipoasi Mungu akawaangamiza.

  Siyi kinachokufanya kuwa hivyo ni kitu kidogo sana; kwa kifupi ni kwamba hujui maana ya kuokoka. Unacholazimisha kuwa ndo maana ya kuokoka ni dhana ya kiakili tu ya kufikirika kuwa kuokoka ni kutolewa duniani. Na sijui unaipata wapi.

  Ndio maana unajikuta unapingana na mistari mingi sana iliyo ktk past tense na past participle na present tense.
  Ila ukikuta mstari uko kwenyd future unasimamia hapo ili kujustify fikra yako kuwa wokovu ni wakati ujao pekee.

  Lakini hata iliyo kwenye future tense tukiamua kuifuatilia msingi wake si lazima kuwa inaongelea future kwa maana kutolewa duniani.

  Yesu hakufa msalabani ili tutolewe duniani, kwani tunamkimbia nani ambaye anaweza kudhuru! Hayupo.

  Nimeandika makala ndefu hii, ili zinazokuja zote tujikite kwenye nini maana ya neno Kuokoka!
  Siye ukijua nini maana ya kuokoka according to scriptures, hii hata haitaendelea.

  Let’s go back to square one
  Kuokoka maana yake nini Siyi?

 67. Lwembe,
  Shaloom kaka!! Pole kwa kuningoja kwa muda mrefu. Nimekuwa busy kiasi Fulani. Yote ni kheri na tunamshukuru Mungu.
  Aidha, nikwambie kuwa WOKOVVU siyo siri/fumbo!! Siyo siri hata kidogo. Uko bayana mno. Ila wafundishao upotovu, ndio husema hivyo ili kutukokota. Yale yalifichwa kwetu hayo ni ya Mungu mwenyewe. “Mambo ya siri ni ya Bwana, Mungu wetu; lakini mambo yaliyofunuliwa ni yetu sisi na watoto wetu milele, ili tuyafanye maneno yote ya sheria hii” Torati 29:29. Mungu hajatuficha jambo lolote linalohusu wokovu wetu. Kwa maana “Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lo lote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake”-Amosi 3:7. Kwa hiyo kaka Lwembe, wokovu siyo siri. Na ninaomba hilo ulielewe hivyo maana liko bayana mno. Wasikuuzie mbuzi kwenye gunia kijana!!
  Aidha, sidhani kama nilisema kauli hii, ““”Tutaokolewa na dhambi kwa wakati ujao””. Sikumbuki kwa kweli. Kama wewe una ushahidi naomba unioneshe. Hata hivyo, iko kimakosa. Hatuokolewi na dhambi. Mbinguni hakiendi chochote kilicho kinyonge. Tutaokolewa kutoka kwenye dunia na taabu zake ikiwemo na dhambi. Hata wewe sidhani kama ni sahihi kusema kuwa, “TUNAOKOLEWA na HUKUMU”. Vishazi hivi (cha kwangu na cha kwako) vinaweza kuwa na maana tata. Ili visieleweke vinginevyo kwa wengine, nadhani ni vyema tungesema kuwa, “Tutaokolewa kutoka dhambini kwa wakati ujao” na “tunaokolewa kutoka kwenye hukumu (ya kifo)”. Ieleweke kwamba, neno HUKUMU, halina maana hasi peke yake. Hata hao watakaopewa uzima wa milele, hiyo nayo ni hukumu kwao –hukumu ya uzima wa milele-uhuru. Na wale watakaozawadiwa umauti, hiyo nayo ni hukumu.
  Ni kweli Yesu alishabeba dhambi zetu sisi tuliomwamini. Lakini ieleweke kwamba, kila siku huwa tunazidi kumbebesha!! Tunapoomba atusamehe kwa lolote tulilomkosea!! Zigo hilo la dhambi tunalomkabidhi Yesu, hatima yake atakuja kumkabidhi Ibilisi mwenyewe ili ahangaike nalo. Na kwa sababu mpango wa Mungu ni kuangamiza uovu, Ibilisi ataangamzwa kwa sababu ya mizigo mingi ya dhambi ya wamataifa na waisrael aliowasababisha watende dhambi. Rejea historia ya tukio la siku kuu ya upatanisho –walawi 16. Kwa hiyo Yesu hana pa kuzipeleka dhambi isipokuwa kwa ibilisi. Ndiyo maana ibilisi usiku na mchana yuko kazini akijitahisi kumdanganya Siyi, Lwembe, Mjema, Seleli,Sungura nk ili wampunguzie mizigo yao ya dhambi endapo hawataokolewa siku ya mwisho. Hii ndiyo sababu inayomfanya Ibilisi awe busy kuudanganya ulimwengu saa zote!!
  Wokovu usiodumu… ha ha ha haa!! Wewe kijana!! Acha kufunika kombe mwanaharamu apite!! Wewe kula tu hata vumbi likikutimukia, ndipo utaelewa kumbe haukuwa sahihi!! Wokovu usiodumu katika Agano jipya, haupo!! Katika Agano la Kale, kuna nasaba/elements za wokovu unaousema. Mf. Kipindi cha gharika, sodoma, gomora, zoari, jangwani nk, walioponywa na majanga hayo ya maji na moto, uzima/uhai wao haukudumu milele. Baadaye walikufa wengine kwa matumaini na wengine bila matumaini. Hata hivyo, nachelea kuuita wokovu maana hauna sifa za wokovu!! Ni uponywaji tu ndiyo dhana sahihi!!
  Wokovu tunaojifunza Agano Jipya, siyo uponywaji Lwembe. Ni kuwa na hali ya kudumu milele kama Mungu. Jambo hili si mchezo. Huwezi kulilinganisha na jambo lolote!! Huu ndio wokovu usiopotezeka. Yaani mtu hawezi kwenda mbinguni, halafu akaja akapotea tena!! Haiwezekani!! Mungu habahatishi mambo yake!! Uponywaji (ninyi mnauita wokovu usiodumu), wa agano la kale, huku kwenye Agano jipya, nao upo. Watu huponywa maradhi wanapomwamini Yesu nk. lakini huo siyo wokovu. Maana huo, huwezi kuufananisha na kitu cha kudumu!! Wokovu ni ETERNAL!! Ndio huo unaohubiriwa na Siyi, Mjema na CO. yao.
  Aidha, ikumbukwe kuwa, “…kuna watu waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo” –Yuda 4. Hawa ni jamii ya akina Yuda Iskariote. Wapo wengi. Si kila mtu anayekiri kwa mdomo wake kuwa anamwamini Yesu, hupokelewa na YEYE, bali ni Yule anayemwamini kwa moyo wa dhati. Hao wengine (majesuits) waliojiingiza kwa siri, hawa huwa hawana shida ya kwenda mbinguni. Hatuwezi kusema wameponywa. Hawako kwa hilo!! Ndiyo maana nasema, wanaomwamini Kristo kwa maana ya kuja kuokolewa, daima wataokolewa siku ya mwisho ajapokufa leo. “Kwa kuwa mapenzi yake Baba yangu ni haya, ya kwamba kila amtazamaye Mwana na kumwamini yeye, awe na uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho” – Yohana 6:40. Wapendwa siyo sahihi kutumia mifano ya akina Yuda Iskariote nk kuhalalisha dhana ya kupoteza wokovu. Dhana hiyo haipo!! Wokovu wa Kristo ni wa kudumu. Ndiyo huo unaotupatia fursa ya kuula mti wa uzima. Mti wa uzima hauliwi na watu wanaweza kuja kufa tena baadaye!! Unasikia!!??
  Hoja yenu ya Mungu kufuta majina mimi siifahamu. Sidhani kama ni hoja ya kibiblia!! Huenda ni fundisho lenu tu. Nitaomba kujifunza kwenu. Nielewavyo mimi, Mungu huwa hafuti majina ya wateule wake. Akikuandika, amekuandika. Na hadi anakuandika, ina maana umefikia hali ya utakatifu sana. Si mchezo!! Mungu huwa hafanyi vitu vya kubahatisha kwamba mara aandike mara afute!! Hafanyi maigizo hayo wapendwa!! Acheni kudanganyika!!

  Siyi

 68. Sungura,
  Ha ha ha ha ha!!! To be paid is not to be saved!! Wuuuu!!!
  Kaka nilijibu mapachiko kama mawili matatu hivi (tar. 15 hadi 17). Bado hayajaruhusiwa. Nayaona yanasubiri moderations!!. Kabla sijajibu maswali yako uliyoniuliza, naomba unitofautishie kati ya;
  1. Kunyakuliwa na kuokolewa.
  2. Wale watakaonyakuliwa na wale watakaolipwa sawasawa na kazi zao, tofauti yao ni nini? Kila kundi litakuwa sehemu gani?
  3. Swali la Sodzo na Soteria, linahitaji rejea tu. Kwa maneno mengine, ulisoma wapi ili na mimi Siyi nikajiridhishe hapo?
  NB: Kama nilionekana kukutusi sana, wewe nisamehe tu rafiki yangu. Sikuwa na lengo la kutukana mtu. Naamini niliandika with a little irritations!! Huu nao ni udhaifu ambao sharti niushinde. Ndiyo safari yenyewe ya kiimani kaka. Nakungoja ujibu maswali yangu kwanza, ili nilete mwitiko kwa maswali yako fasta.
  Ubarikiwe sana.
  Nakungoja
  Siyi

 69. inaendelea…..

  Ufufuo wa pili unafanyika huko Mwisho, baada ya miaka elfu na Shetani kufunguliwa, yaani Uongo na Maasi vikirudi kwa kasi duniani, Ufu 20:7-10! Ndipo baada ya hayo, Ufu 20:11-12 “Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana. Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.

  Hii ndio Hukumu aliyoiona Daniel, maana inawahusu na watu wake, 7:9 “Nikatazama hata VITI VYA ENZI VIKAWEKWA, na mmoja aliye mzee wa siku ameketi; mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi; KITI CHAKE cha enzi kilikuwa miali ya moto…” Aliviona hivyo viti vya enzi vikishushwa lakini vikiwa ni vitupu! Hao wazee ishirini na wanne walikuwa bado hawajakombolewa! Kwahiyo unapoyasoma hayo huko kwa akina Daniel, usiyakurupukie; ndio maana niliwahi kukutahadharisha huko nyuma kwamba ni vizuri ukalitii Agano Jipya ktk Ukamilifu wake ili upewa RM, kisha huyo ndiye akuongoze huko ktk AK, ndio utayaelewa vizuri ya huko!

  Yohana naye anaizungumzia Hukumu hiyo hiyo aliyoiona Daniel ktk huo Ufufuo wa Pili. Ila yeye anaiona stage iliyokamilika baada ya Kanisa kunyakuliwa, anawaona mpaka akina Petro, wale mitume 12 na wazee wa makabila 12 ya Israeli wamekalia viti vya Hukumu- wazee 24! Si unakumbuka Petro alimuuliza Kristo, watapata nini; ndio hao hapo!!!

  Tazama alichokiona Daniel, 12:1-2 “… na wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile. Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele”; ndio hiki hapa ktk Mt 25:31-46:
  “Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake; na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi”
  Siyi, hapa anasema, ” KAMA VILE mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi”, hasemi kwamba hapo anawabagua kondoo na mbuzi; maana twafahamu kwamba “kondoo”, ni wale tuliowasoma ktk Yn 10:27-28, ambao anao tayari!

  Huku ndiko vile vitabu vya matendo vinafunguliwa pamoja na cha majina, huku ndiko hao ambao wanaopita hukumuni watabaguliwa kulingana na matendo yao, hao ambao majina yao yamo katika Kitabu cha Uzima, ila mavazi yao yameingia madoa. kati ya hao wengine watatupwa ktk ziwa la moto, na wengine ndio hawa hapa wanaokolewa huku mwisho, huku ndiko wanapewa Uzima wa Milele tena, yaani Siyi unaweza ukaokolewa huko kwa kumtetea kwako Sungura tu!:
  “33atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto. Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu; kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha; nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia. Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha? Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika? Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia? Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.”
  Hawa ndio wale walioamka, wakapata uzima wa milele!

  Na hao waliofufuliwa kupata aibu na kudharauliwa milele ndio hawa hapa:
  “41Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake; kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe; nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama. Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie? Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi. Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele.”

  Siyi, Mjema na Co, kagueni vizuri majina yenu kama bado yamo, Maandiko yanawapeni Elimu, tusiwe mazezeta wa maisha ya kiroho, tukaicha Elimu;
  Elimu kuhusu jana inaniongoza leo ili niifikie ile kesho niliyooneshwa na jana ktk njia ya leo! Tunaishi leo, na kwa kuishi leo tunaikomboa kesho, huo ndio Wokovu au huko Kuokoka, ktk urahisi wake!

  Bwana na awatie Nguvu yake, Muokoke na Hukumu yake!!

 70. Siyi, Mjema & co,

  UFUFUO:
  Maelezo uliyoyatoa kuhusu Ufufuo, licha ya kwamba umetoa nukuu za Maandiko, bado hayajakaa sawa, yamelipotoa jambo zima la Ufufuo, kiasi kwamba hali yenu itakuwa ni mbaya sana! Ni mbaya kwa sababu kukosa kwako kujua utafufukia wapi, ni dalili ya kutokuwa na ile Nguvu iliyomfufua Kristo ndani yako!

  Lakini, najua shida hii mliyonayo inatokana na lile fundisho la Majuma Sabini ya Daniel, lile Juma la Sabini hamkuliweka sawa, na hivyo Injili kuwaparaganyikia!

  Bali Kweli ya Ufufuo iko kama Injili inavyoutangaza. Hapa ieleweke kwamba tunazungumzia Ufufuo wa Wafu walalao makaburini, na si kufufuliwa kwa mtu mmoja hapa na pale ktk Huduma ya kuhubiriwa Injili, km Lazaro, au yule kijana aliyeanguka kutoka ghorofani au mazingaombwe ya “kufufuliwa kwa misukule” nk.

  Ufufuo, ni kweli uko mara mbili, wa kwanza ukiwa ni wa Watakatifu, wale Wateule, na wa pili ni wa watu wote, huko mwisho.

  Ufufuo wa kwanza ndio huo tunaousoma ktk baadhi ya hivyo vifungu nawe ulivyovinukuu,
  1Kor 15:52-53 “… wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu…”
  1The 4:16 “… na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.”
  Vifungu hivi vyote vinazungumzia Ufufuo wa Kwanza, wa hao waliotukuzwa, hao waliobatizwa kwa RM, lile kundi ambalo halipiti ktk Hukumu. Hawa ndio wale waliosemwa kwamba Watahukumu, 1Kor ‭6‬:‭2-3 “Au hamjui ya kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu? … Hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika, …?” Ufufuo wa hawa‬‬‬‬‬‬ ndio unaotimia ktk Ufu 20:4, unaojumuisha na Kunyakuliwa kwa Kanisa, hao watakaokutwa hai watabadilishwa na kundi hilo kuondolewa hapa duniani, kuelekea Karamuni, nao Wokovu kwa Mataifa ukiwa umefikia ukomo ingawa watu wataendelea kudhani kwamba wanaokolewa!

  Ufu 20:4-6 “Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu. Hao wafu waliosalia hawakuwa hai, hata itimie ile miaka elfu. Huo ndio ufufuo wa kwanza.”

  Hivyo viti vya enzi unavyoviona hapo ni vya hao Watakatifu wanaopewa kuhukumu, ndio lile neno alilolinena Paul ktk 1Kor 6:2; kati yao ndio hao ambao “roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake.” Wengi tunamtazamia huyo mnyama huko siku za mbele, lakini huyo amekuwepo wakati wote. Mnyama huyo ndiye aliyewalisha simba wenye njaa Watakatifu, huko ktk viwanja vya starehe vya Rumi, ndio hao waliokatwa vichwa, wengine kuchomwa moto na ukatili mwingine wa kutisha waliofanyiwa hao Watakatifu waliogoma kumsujudia, nadhani inakadiriwa watakatifu wapatao milioni 68, kama sikosei; Papa Yohane II aliwaomba Walutheri msamaha kwa mauaji hayo!

  Katika Ufufuo huu HAKUNA vitabu vinavyofunguliwa!

  Pia ieleweke kwamba, Ufufuo huu wa Kwanza ukiisha itamatisha Injili kwa Mataifa, Mungu anamgeukia mtumishi wake Israeli yule aliyempofua kwa ajili yetu sisi. Israeli anarejeshwa ktk nafasi yake ya utumishi. Wanapogeukiwa ndipo wanapopatikana wale 144,000! Nalo kanisa lililoachwa linaingizwa ktk kisago cha Dhiki Kuu, wengine nilikuambia watamsujudia huyo Mnyama, dhiki itawakwepa, lakini majina yao yatafutwa, na wengine watayavumilia hayo mateso mpaka kifo.

  Mwisho wa hiyo Dhiki Kuu, ndipo hao wanaohusika na Ufufuo huo wa Kwanza watatawala miaka hiyo elfu, Shetani akiwa amefungiwa kuzimu, na wafu wengine wote pamoja na hao waliokufa ktk hiyo Dhiki Kuu, watabakia makaburini; “Hao wafu waliosalia hawakuwa hai, hata itimie ile miaka elfu.”!

  Daniel hakuoneshwa Ufufuo huu kwa sababu hauwahusu Israeli, hao watu wake, huu unalihusu Kanisa, hao Mataifa!

  inaendelea…..

 71. ……….Inaendelea

  Basi tukiyaacha makundi hayo yenye shida, hebu tuligeukie lile kundi jingine, hilo ambalo Kristo anasema, Yn 10:27-28 “Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata. Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu.” Kondoo hawa ndio walioupokea ule “Wokovu wa Kudumu”, waliupokea hapa duniani ktk miili yao, kulidhihirisha hilo Neno la Mungu ktk Yn 10:27-28. Twafahamu kwamba neno ni wazo lililodhihirika, kwamba unapolisema jambo ndipo mtu mwingine aweza kujua unawaza nini.

  Naye Mungu kwa hilo Neno, ndio twafahamu kwamba hao anaowazungumzia hivyo hapo, walikuwa ni wazo lake huko kabla ya kuwekwa misingi ya dunia, na sasa wazo hilo likidhihirishwa kwa Neno hilo liumbalo, na ndio kusema hao watakuwa wameumbwa ktk jinsi hiyo, kulilingania Neno hilo; ndio hao ambao hawakuyachafua Mavazi yao, hawa ambao “… kama yamkini, hata walio wateule” (Mt 24:24), hawa wanatokana na Mungu, naye Mungu akaae ndani yao ni mkuu kuliko huyo roho wa upotevu mtenda miujiza na ishara kubwa na maajabu ambaye amewasomba wote ambao hawakutiwa Muhuri, ule Ubatizo wa RM!

  Nilikuambia kwamba hawa ndio hao ktk Efe 1:4 jaribu kurudia kusoma tena inaweza kukufungua macho maana hayo ndio ile “Eye salve”! Lakini waweza kulitazama jambo hilo tena hapa, ukajipiga msasa kidogo maana hiyo ndiyo Injili yenyewe, Rum 8:28-30 “Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza.” Hawa wamezaliwa ili kulidhihirisha Neno hili ktk Utii wenye shina la Upendo na si Sheria! Hawa ndio hivyo vyombo vya Utukufu!!!

  Unaona Siyi, utakatifu wa hao au kuwa kwao “wasio na hatia” si mambo ya huko mbinguni, hapana, haya ni madhihirisho ya hapa duniani. Nayo mambo hayo yawezekana hapa duniani kwa kule kuisikia sauti ya Kristo na kumfuata hapa duniani na si huko mbinguni, ndipo kwa hawa, ule Mwisho wao huuishi huku Mwanzo; hawa ndio wale Wanawali Watano wenye Mafuta ambayo wameyapata hapa duniani waziwashe taa zao ili kulifukuza hili Giza nene la mafundisho ya dini, “… ili audhihirishe wingi wa utukufu wake katika vile vyombo vya rehema, alivyovitengeneza tangu zamani vipate utukufu; ndio sisi aliotuita …”! Rm 9:23

  Kwa kifupi hawa ndio wanaoufanya ule Mwili wa Kristo, yule Bibi Arusi wake, yule ambaye Paulo alimposea Kristo, ndipo lile Andiko la Mwa 2:24 linatimia katika Ukamilifu wake hapo Kristo anapomuacha Babaye na kumfuata Bibi Arusi wake na kufunga naye Ndoa, ndio huo Mwili wa Kristo, hao waliovuka kutoka Mautini na kuingia Uzimani wakingali hapa duniani!!!

  Kundi hili HALIPITI Hukumuni; Yn 5:24 ” Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani.”!!!

  Nitamalizia kwa kuyaangalia tena makundi haya yote, tamati ya kila kundi, kulingana na Ufufuo, tuyaone yanakoishia!

  Gbu!

 72. Siyi, Mjema & co,

  WOKOVU UNAODUMU:

  “Lakini unayo majina machache katika Sardi, watu wasioyatia mavazi yao uchafu. Nao watakwenda pamoja nami hali wamevaa mavazi meupe, kwa kuwa wamestahili.” (Ufu 3:4)

  Injili tuliyoipokea, ndilo Vazi Jipya tulilopewa, lile Jeupe, ile Haki ya Mungu tuliyohesabiwa kupitia Kristo! Wote ambao majina yao yameandikwa ktk Kitabu cha Uzima walipewa vazi hilo, ndio unaona anasema, “watu wasioyatia mavazi yao uchafu”, wako ambao waliyachafua hayo mavazi waliyopewa. ndio hao wenye kufutwa majina yao na wengine kupita ktk Hukumu.

  Basi kama ilivyoandikwa ktk Rm 10:10 “Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu”; Wengi wetu, hulikariri au hu ‘mimic’ jambo hili tukadhania ndiko kukiri na hivyo tukaishia ktk intellectual faith au ile imani ya kiakili, ambayo Mungu haitambui; ni hasara iliyoje!

  Bali kukiri kunakozungumziwa hapo kunatokana na kuiamini Injili kwanza, huko KUOKOKA. Ndipo kwa kukiri kwetu KUOKOLEWA, hilo huzalisha Nguvu ya kuuishi Wokovu, ile Haki ya Kristo ikijishuhudia ktk maisha yetu; kama tu ambavyo kwa imani tunaamini kuponywa magonjwa yetu, na kwa kukiri kuponywa huko sisi hupokea uponyo ktk miili yetu. Yule kipofu Bartimayo, alipomwita Kristo kwa sauti kubwa, alikuwa akiikiri imani ya uponyo aliyokuwa nayo moyoni mwake, naye Mungu hututimizia hayo tunayoyakiri kutoka ktk kilindi cha imani mioyoni mwetu!

  Kinyume cha hayo ndiyo hili tunalooneshwa hapa ktk 1Yn 4:3 “Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani.” Sasa, wengi wetu hudhania kwa kuwa kwetu wakristo, basi huwa tumemkiri Kristo, bali hayo ni mambo ya dini na uongo wake! Kumkiri Kristo ni Kukiri Kuupokea Wokovu tulioitiwa. Jina “Yesu”, maana yake ni “Mwokozi”, basi huwezi ukamkiri “Mwokozi” wewe ambaye hujaokoka, utakuwa ni muongo! Na iwapo utamkiri “Mkombozi”, katika siku ya Wokovu, hilo laonesha kwamba aliyekukomboa hajakudai bado kutoka kwa huyo anayekushikilia hata ufike ktk hatua ya kumkiri huyo “Mkombozi” wako kuwa sasa ni “Mwokozi” wako akiisha kukutoa huko ulikokuwa umeshikiliwa! Kulikataa jambo la Kuokoka ni fundisho la Balaamu!

  Nayo Injili huutangaza Wokovu, huo wenye kutupa Nguvu za kuishinda Dhambi inayotuongoza kuelekea Hukumuni. Ndipo, yeyote asiye kiri KUOKOKA, maana yake ameuziwa “injili kanyanga”, nayo roho inayo muongoza ndiyo hiyo isiyotokana na Mungu, bali Mpinga Kristo, na hivyo wao kujidhihirisha kwamba ndio hivyo vyombo vya Ghadhabu ya Mungu vilivyofanywa tayari kwa uharibifu, (Rm 9:22)!

  Itaendelea……..

 73. Siyi, Mjema & co,

  Hakuna lililo jipya kwa Mungu. Kama ni Wokovu, yeye ndiye Muasisi, anaujua mwanzo kama anavyoujua mwisho. Ndipo hauwezi kulijua jambo la Wokovu kwa uhakika, bila kulijua kwanza jambo la Kuandikwa kwa Majina ktk Kitabu cha Uzima, huko ndiko ulikoanzia Wokovu; kutokulijua kwenu jambo hili ndio sababu ya ninyi kutatizika sana na jambo la KUOKOKA hapa duniani; hebu msikilize mtume Paulo, “… kwa maana waliishindania Injili pamoja nami, na Klementi naye, na wale wengine waliotenda kazi pamoja nami, AMBAO MAJINA YAO YAMO KATIKA KITABU CHA UZIMA” (FLP.‬ ‭4‬:‭3‬); mliniambia mnaye nabii, ni nabii gani huyo asiyelijua jambo la msingi kama hili, akawaacha mnatembea gizani mkibahatisha Njia, hata ile Njia ya Kweli mkaishia kuiita ya Kuzimu, na ile ya Kuzimu ndio mkaifuata mkiaminishwa kwamba ndio Njia ya kweli?!

  Majina ndiyo yanayotujulisha jambo la Wokovu! Tumewaona hao ambao majina yao hayakuandikwa ktk Kitabu cha Uzima walivyomsujudia Shetani. Tukaona ambavyo hawana namna ya Kuokoka kwani hatma yao ilikwisha kufungwa tangu huko ilipokiwekwa misingi ya dunia.

  Pia tulifika mahali sote tukauona “Wokovu wa Kudumu” na huo “Unaopotezeka”, jambo ambalo linaligawa kundi la hao ambao majina yao yameandikwa ktk Kitabu cha Uzima ktk hayo makundi mawili.

  Kuhusu hilo kundi la pili, hao wenye “Wokovu Usiodumu”, hao wazembe, wavivu na wasio waangalifu; hawa ambao hawakuuthamini Wokovu waliopewa, wakaukanyaga kama nguruwe waliotupiwa lulu, kama alivyofanya Esau au mke wa Lutu, hao WALIUPOTEZA Wokovu wao na hivyo majina yao YAKAFUTWA kutoka ktk Kitabu cha Uzima.

  Mifano ya hawa pia nilikupatia, nikakutajia Yuda, Anania na mkewe Saphira; hata Israeli nao kule jangwani walipoasi, unaweza kuona Mungu akiahidi kuwafuta majina yao, Kut 32:33! Nikakuambia kwa siku ya leo wengi wa hao walioandikwa majina yao ktk Kitabu cha Uzima wanafutwa kwa ibada za KUFURU wanazoingizwa na hizi Cults za Kikristo; nikakupa na mfano wa kanisa la Siloamu ambalo nabii wao anajulikana kama “Adam wa Pili Mungu wa Majeshi”, na kusanyiko lote linaitikia Amina! Nikakuambia kwamba Mungu anasema atamfuta jina yeyote atakaye punguza au kuongeza ktk hayo yaliyoandikwa ktk Biblia, ndipo Cults, ili kulipa Uhai andiko hilo, ziko ambazo zinayabadili Maandiko, nao mfano wake nikakuonesha hao walioisogeza koma ktk kifungu cha Lk 23:43, “Yesu akamwambia, Amin, NAKUAMBIA, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi.” wakakitoa ktk maana hii iliyokusudiwa na kukileta ktk maana ya mafundisho yao kikawa hivi: “Yesu akamwambia, Amin, NAKUAMBIA LEO HIVI, utakuwa pamoja nami peponi”; halafu watu wanaitikia Amina! Thats how SLY them Cults are, ni nyoka! Na hivi ndivyo wengi wetu tunafutwa majina yetu kwa kukosa Maarifa, ndiko kule kuangamizwa!

  Nikakuambia kwamba ktk kundi hili pia kuna ambao watapotezwa kwa kufuata Miujiza, na Uongo mwingineo wa Dini, Mt 24:24 “Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza …” Hawa wataendekeza misisimko na kuliacha Neno la Mungu linalojidhihirisha machoni pao, na hivyo watakosa Kupigwa Muhuri unaoukamilisha Utakatifu wao kulingana na kazi ya zile Huduma Tano zilizo wekwa kanisani kwa ajili hiyo (Efe 4:11), hivyo WATAUKOSA UBATIZO wa RM, tunaousoma ktk Efe 4:30, wakiendelea kupokea roho za dini zinazowaaminisha kwa UPUMBAVU kwamba ndiye RM; hawa ndio wale wa mfano wa Mabikira Wapumbavu, hawakuingizwa ktk kufuru, ni waaminifu kabisa, bali hawakulipokea Neno lote; nikakuambia hawa wanaukosa ule ufufuo wa Kwanza na hivyo watapita ktk Dhiki Kuu na watasimama Hukumuni huko mwisho; wenye KUVUMILIA mateso na dhihaka na vibano vya hiyo Dhiki Kuu, wakiikataa ibada ya sanamu, hawa ndio WATAOKOLEWA huko mwisho, Ufu. 3:5 “Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala SITALIFUTA kamwe jina lake katika kitabu cha uzima”; basi, kuna ambao watashindwa na hivyo kuishia kumsujudia Mnyama, hawa WATAFUTWA majina yao na kuungana na hao WASIOANDIKWA!

  Sasa, ni vizuri ieleweke kwamba, waliofutwa majina yao hawana nafasi ya kutubu, kwahiyo wanapotelea ktk ziwa la moto. Kundi jingine la hawa ambao hawakupigwa Muhuri, kwa kukosea kwao, lakini hawakumkufuru RM, hawa ndio watasimama Hukumuni na vitabu vyao vya matendo kufunguliwa nao kuhukumiwa kulingana na yaliyomo humo, hawa ndio wanaobaguliwa kama mchungaji awabaguavyo kondoo na mbuzi!

  Tutalitazama zaidi jambo hili tutakapo liangalia jambo la UFUFUO, ili tukione kile Maandiko yanachokisema, tupate na fursa ya kuchagua cha kukiamini!

  Gbu!

 74. Ha ha ha ha… Siyi,
  Wokovu ni MYSTERY ndugu yangu, no wonder unauona ni ufedhuli!!!!

  Twende pole pole brother, hauko mbali sana na Kweli ya Wokovu, lakini ukiendelea ktk makosa inaweza ikakugharimu nafsi yako, maana naona unazihubiri nguvu za Shetani kwa uhodari mkubwa sana, kiasi kwamba hata hatma yako inaonesha iko ktk kukoswa na huyo Shetani, jambo ambalo si rahisi!!! Basi, uwe hodari ktk Imani, naye Shetani atakukimbia, Yak 4:7.

  Pia, hakuna mahali niliposema kwamba, “”Tutaokolewa na dhambi kwa wakati ujao””; hili ni fundisho lenu ambalo sasa hivi naona limekuchanganya kidogo! Mimi nimekuambia kuwa TUNAOKOLEWA na HUKUMU ijayo na si dhambi, dhambi zetu alikwisha kuzichukua Kristo, ndizo zilimfanya asulubiwe! Yaani nilipokuwa huko mautini, nilikuwa ni mtumwa wa Dhambi na wala sikujua kwamba hayo yote niliyokuwa nikiyafanya yalikuwa Dhambi. Sheria ilipokuja ndiyo iliyoifunua Dhambi; ndipo Neema ya Kristo iliponifikia, ikaiondoa Kiu ya Dhambi iliyokuwa imepandikizwa moyoni mwangu, na Kiu ya Haki Yake ikaibadili; ndivyo Dhambi ilivyoondolewa kwa huo Wokovu!

  Kuhusu Wokovu unasema,
  “” Kimsingi wokovu anaouzungumzia Kristo ktk Yoh 10:27-28 si sawasawa na ule anaoujadili hapa Lwembe, Haule, Sungura & Co. Maana wa kwao unaweza kupotezeka!! Sasa kama unaweza kupotezeka, kwa nini mnukuu aya zenye kuonesha wokovu wa kudumu wanaouhubiri akina Siyi na Mjema?? Mmetuelewa hadi sasa au bado mnaimba liturujia tu??””

  Niseme ile kweli, umenifurahisha saana kwa kauli yako hii, yaani hii ndiyo iliyonifanya nikuambie kuwa hauko mbali sana na Kweli ya Wokovu!

  Kwamba Yoh 10:27-28 inazungumzia “Wokovu wa Kudumu”, ni sawa kabisa kama ulivyoliona na kulitambua hivyo. Labda tukianzia hapa, tunaweza tukafika mahali tukaliona sawa jambo hili la Wokovu!

  Kwanza, kwa kusema kwako kwamba huo ni “Wokovu wa Kudumu”, maana yake unatambua kwamba kuna “Wokovu Usiodumu”, ndipo huo wa Kudumu ukiwa umejipatia sifa hiyo kutoka huo Usiodumu! Kwahiyo kwa msamiati huu mpya, basi ule “Wokovu unaopotezeka” sasa tutauita “Wokovu Usiodumu”. Hivyo basi, jambo hili la Wokovu linakuwa limegawanyika ktk hayo makundi mawili, moja ndilo hilo lililoupokea “Wokovu wa Kudumu”, nako kudumu kwa jambo twafahamu kunategemea UTUNZAJI, na kundi jingine ndilo hilo la “Wokovu Usiodumu”, nako kutokudumu kukiwa ni ishara ya kutokuwa waangalifu, labda ni kwa uvivu au uzembe au kwa hulka, maana Wokovu ni mmoja kwa wote kama kulivyo KUKOMBOLEWA kwetu!

  Tulipoanza kuzungumzia jambo hili la Wokovu, tulisema mtu anaweza kuupoteza wokovu alionao humo njiani, kutokana na ukweli kwamba Wokovu ni MCHAKATO, ndiposa tunatambua kwamba huyo aliyeupoteza atakuwa alishindwa kuutunza na mwishowe akanyang’anywa, maana Wokovu ni Mtakatifu, hivyo Shetani hawezi kuuiba. Pia kati yetu hakuna aliyesema kwamba ukiisha kuupokea Wokovu shughuli inaishia hapo, tulikwambia kwamba ktk wokovu ndipo tunaposajiliwa ktk Super Jeshi la Kristo kuipigania Imani! Nayo Injili ndiyo iliyotukaribisha kuupokea Wokovu, Mk 16:16 “Aaminiye na kubatizwa ataokoka”; nao walioipokea Injili ktk siku zake za Kwanza za Kuhubiriwa kwake hadharani, Injili hiyo hiyo ndiyo inayolithibitisha jambo hilo waliloahidiwa kwamba walitimiziwa, Mdo 2:47 “… Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa WAKIOKOLEWA.” Sasa haya si mambo ya UONGO, hii ndio KWELI ya Injili unayopaswa kwanza UIAMINI, kisha uichunguze kama Mberoya ktk tafakari yake ili ulibaini jambo zima, ndipo likuinue ktk ufahamu!

  Ktk jambo la kuupoteza Wokovu, tukaileta mifano ya hao walioupoteza, tukawarejea Israeli huko jangwani, halafu tukawatazama pia akina Yuda Iskariote na Anania na mkewe Saphira. Lakini hatukuishia hapo, tukatafuta kujua ni kwa vipi hawa tena WALIUPOTEZA Wokovu??? Ndipo ktk kulitafakari jambo hilo, Maandiko yakaturudisha huko nyuma ulikofanyika uumbaji. Huko ndiko kwanza tukayaona makundi mawili ya watu, kutokana na jambo la kuwepo kwa Kitabu cha Uzima cha Mwana – Kondoo, ambacho kiliandikwa orodha ya majina ya watu fulani, na waliobakia, majina yao hayakuandikwa, ndiyo hayo makundi mawili tuliyoanza nayo.

  Sasa, tukiwa tunafahamu kwamba watu wote walioipokea Injili, wakabatizwa, kimsingi WALIOKOLEWA hapo walipoipokea Injili, na jambo hili tukasema ndiko Kuhesabiwa Haki kwa Imani. Tulipoliangalia zaidi, tukalibaini kwamba Kuhesabiwa Haki ni Kurejeshewa Haki ya Kuuendea Mti wa Uzima tuliokuwa TUMEZUILIWA baada ya Kuanguka na Kufukuzwa Bustanini, na makerubi kuwekwa kuulinda ili tusiufikie; ndipo kutoka jambo hili tukajua ya kwamba hao walioipokea Injili na kupewa fursa ya kuuendea huo Mti wa Uzima, basi ni dhahiri kwamba hawa ndio walioandikwa majina yao ktk kile Kitabu cha Uzima!

  Tukirudi tena ktk Maandiko yaliyo tuonesha jambo la majina kuandikwa na wengine kuachwa, Ufu 13:8 “Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo”, kutoka Maandiko haya tunaliona kundi hilo ambalo majina yao hayakuandikwa likichukua Chapa ya Mnyama moja kwa moja, yaani Wokovu hauwahusu kabisa; hawa tunawabaini kwamba ndio hao walioukataa Wokovu, wakauona kwamba ni UFEDHULI, na hivyo walikwisha kuhukumiwa tangu hapo walipoukataa, Yn 3:18 “Asiyeamini amekwisha kuhukumiwa”, ndio kusema hawa wanasubiri adhabu tu, na wakihubiriwa Injili, basi huwa kwa ajili ya ushuhuda tu, kama zile roho zilizokuwa kifungoni zilivyohubiriwa na Kristo, kwa ushuhuda na si kwa ajili ya kuokolewa. Hukumu yao ilikwisha kukatwa pamoja na ya mkuu wao, Yn 16:11 “Kwa habari ya hukumu, kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa.”!!!

  Basi Kundi hili ambalo majina yao hayamo ktk Kitabu cha Uzima, nalo likiwa limekwisha kuhukumiwa, licha ya tamati ya hali yao hiyo, bado inaonesha kwamba kati yao ni watu wazuri tu wa dini, yaani mioyoni mwao wanayo shauku ya kumuabudu Mungu, lakini ni wepesi wa kuupokea Uongo kuliko Kweli, na hivyo wakadanganywa kuhusu Mungu, wakamsujudia Ibilisi ktk jina la dini zao zinazotafsirika kwa hao mitume wao na manabii na mizimu iliyojiwakilisha ktk nafasi za upatanishi na Mungu. Hawa Maandiko yanasema, walitupwa ktk ziwa la moto moja kwa moja, HAWAKUSIMAMA HUKUMUNI, maana walikwisha kuhukumiwa!

  Nitaendelea, tulitazame Kundi lililobaki hao ambao Majina yao YAMEANDIKWA ktk Kitabu cha Uzima…..!

  Gbu!

 75. Ziragora na Sungura,
  Inaweza kuwachukua muda mrefu kuelewa somo hili , lakini ukweli wake hautabadilika. Hakuna cha usabato wala umasalia. Kinachozingatiwa hapa ni utii wa neno wa neno la Mungu. Tusipokubali kukifuata kile Kristo alichokifanya pale msalabani, tusitarajie chochote kwa baadaye!! Tukipumbazika kuwa tumeokoka tukaduwaa eti na kutofanya lolote kwa ajili ya wokovu wetu, hatima yetu ni uangamivu milele. . Hatuna budi kuiacha dunia na mambo yake yote kwa ajili ya kile alichokifanya Kristo ili hatimaye tupate uzima wa milele. Enzi za Kristo akiwa duniani, Petro alihoji swali kama hilo,
  ” …Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata; tutapata nini basi?”
  Petro hakuuliza kuwa tumeshapata nini kwa kuacha familia zetu, kazi zetu nk. Aliuliza, kwa future tense, TUTAPATA nini basi???
  Jibu la Kristo nalo lilikuwa yakinifu kweli; “Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli”. mtt 19:27-28.
  Yesu aliwaambia, wataketi kwenye ufalme wake baadaye. Siyo sasa!! Sasa hivi, (tuliotambua ukombozi wa Kristo)tunajitahidi tu kuiacha ndunia na mambo yake kwa njia ya nguvu za RM. Hatima ya kuviacha vyote hivi, ni uzima wa milele. Lini? BAADAYE!!
  Mbarikiwe.
  Siyi

 76. Sungura,
  Kumbuka huu ni mwendelezo wa hoja yetu ya kuleeee…

  Nilikwambia umekwama rafiki. Nimekuona umemwuliza Mjema kuwa mtu anaweza kupoteza ukombozi?? Sijui atakujibuje!! Lakini ngoja tumsubiri. Mimi navyoona hizi athari za mafundisho yenu ya kizushi ndani ya makanisa yenu. Alichokifa Kristo msalabani, alikifanya kwa dunia nzima. Na wala hakitakuja kubadilika hata siku moja. Nipende nisipende Kristo alishafanya. Kilichobaki ni mimi tu kukikubali kile alichokifanya pale msalabani basi.
  Matokeo au malipo ya kukikubali na kukifuata kile alichokifanya Kristo, ndio huo wokovu. Kwa kukusaidia zaidi, fuatilia hilo fundisho lenu la NIMEOKOKA< NIMEOKOKA, limeingia lini ndani ya ukristo. Jaribu kulifuatilia. Huenda utapata msaada kwa hilo.
  Nakungoja ujibu maswali yangu.
  Siyi

 77. Tumaini,
  Nzuri rafiki. Habari za kupotea pia??
  Nimefurahi kukuona!!
  Huna haja ya kupata taabu. Mimi na Mjema, tunafundisha fundisho la Biblia na siyo la wasabato. Ukifika kwa wasabato, unaweza usilikute. Ndiyo maana nakwambieni kuwa, hatuna haja ya kuweka mbele udini kwenye mambo ya msingi kama haya. Shida iliyoko kwa walio wengi wetu, ni pre-conceived ideas!! Perceptions!! Nani anasema nini!! Hata kama jambo lina ukweli kabisa, watu huwa hawauangalii huo ukweli, badala yake huangalia nani kasema!! Kama ni msabato, ooh, utawasikia watu wakisema, mtu wa dini kasema!! Kwa mtindo huo hatutafika wapendwa!!
  Tangu mwanzo niliwaambia ni vyema tukaweka pembeni kabisa udini na umadhehebu hapa. Acheni Biblia izungumze yenyewe!! Akina Siyi na Mjema, wanafundisha wokovu ambao mtu akiupata, hawezi kuupoteza kamwe!! Maana Yesu anasema, wale atakaopewa na Baba yake, hatampoteza hata mmoja. Nafikiri ulisoma pachiko la Mjema. Kama bado kalisome kwenye shina la mada hii – Je, mtu aliyeokoka anweza kuupoteza?? Nenda kasome!!!

  Mjema na Siyi tangu mwanzo tuliwaambia kuwa, wokovu hauwezi kupatikana halafu ukapotea!! Msipokubali kuacha vikaragosi vya miungu na mfundisho yenu ya dini, mtaendelea kubakia wakavu hata mvua inyesheje!! Hata Sungura, naye aligamba eti anajua wokovu hadi kiebrania na kigiriki chake. Nimemwomba rejea tu za hizo faiwa (maana), hajatokeza hadi leo!! Kimsingi wapendwa, imani zenu mmjenga kwenye mchanga. Hamuwezi kuzitetea kibiblia. Na hilo halina ubishi kwenu!!

  Leo hadi kesho tutaendelea kupiga mbiu ya kwamba, wokovu ni baadaye, japo safari yake tulishaianza kwa waliomkiri Kristo tayari!! Ukisema umeshaokoka ilihali bado uko duniani na majaribu kila saa yanakuandama, tutakuona sawa na mgonjwa mahututi anayehitaji uangalizi mkubwa wa daktari!! Ndiyo maana tuko hapa na tunaendelea kuwapeni dawa. Mkiitema, mtakufa tu maana hakuna namna ya kuwasiaidia!!
  Ubarikiwe sana
  Siyi

 78. Ndugu yangu Siyi habari za masiku.mimi binafsi huwa siwaelewi na fundisho lenu kuhusu wokovu,na huwa napatwa na shida,iweje Roho iliyo ndani yangu na Roho aliye ndani yako kama ni mmoja,iweje atupe mafundisho tofauti?je ni mimi ndiyo mwenye roho wa dini au wewe?napata shida.Lakini nimefuatilia somo la Lwembe na maelezo yako ndipo napogundua kama unazungumza lugha kama ya Lwembe lakini kwa mtazamo wa dini yako na mapokeo uliyopoke.daaah!napata tabu ndugu.

 79. MAARIFA YA YESU
  Kuna mistari mingi ndani ya Bibilia kama tukiisoma kwa utashi na uelewa wa kibinadamu tunaweza kudhani INAPINGANA LAKINI KWELI NI KWAMBA NENO
  LA MUNGU HALIJIPINGI KAMWE.AGANO JIPYA HALIPINGANI NA AGANO LA KALE.Changamoto nzito tuliyonayo sasa ni kuwa na uhakika kama tunatafsiri
  neno la Kristo tunaongozwa na Roho mtakatifu,nafsi zetu au roho zingine.Wengi
  tunajaribu kulichunguza neno la Mungu na kulifanyia utafiti kwa kuongozwa na akili
  zetu wenyewe au mafundisho yaliyo kufa.Huu unaweza ukawa ni ujinga lakini wakati
  mwingine ni zaidi ya upumbavu!Mara nyingi tunaongozwa na roho ya ujuaji,kiburi,jeuri,dharau na majivuno.Kujiamini nje ya muongozo wa Roho Mtakatifu
  ni sawa na MAITI INAYOTEMBEA!

  Tukitaka kulielewa neno la Mungu NI LAZIMA TUMPE ROHO MTAKATIFU NAFASI
  YAKE ANAYOSTAHILI NA HATUWEZI KUFANYA HIVYO KAMA NGUVU YA MUNGU
  ITUWEZESHE KUNYENYEKEA.WAFILIPI 4:13 inasema tunayaweza mambo yote katika YESU atutiaye nguvu na hii ni pamoja na kulielewa neno la Mungu.1 YOHANA 2;20.27 inazungumzia habari za UPAKO(nguvu) wa Roho Mtakatifu ulio ndani ya watu waliookoka ambao HUWAFUNDISHA HABARI ZA MAMBO YOTE.Kuna upako wa
  kusoma na kulielewa neno la Mungu.Ni upako ambao tunatakiwa tukae ndani yake ili
  utufundishe habari zote za neno la Mungu.Mstari wa 27 unasema”……HAMNA HAJA
  YA MTU KUWAFUNDISHA…………NA KAMA YALIVYOWAFUNDISHA KAENI NDANI YAKE”.Upako wa Roho Mtakatifu umeelezewa kama mafuta ambayo wateule wanapakwa na Yesu.Ndani ya wokovu kuna upako wa Roho Mtakatifu unaotuwezesha kufanya mambo mbalimbali.Kuna upako wa kuongea kwa hekima na
  maarifa ya rohoni,kuna upako wa kuendesha gari,kuna upako wa kupika chakula,kuna upako wa kuhubiri n.k inategemea unataka upako wa namna gani.

  UPAKO ni uweza wa Mungu ulio ndani ya Roho Mtakatifu kwa ajili ya wateule ili kuwawezesha kuwa jinsi Mungu anavyotaka wawe na kufanya yale ambayo Mungu
  anataka wafanye.Tukiwa ndani ya upako wa Roho Mtakatifu tunafundishwa habari za
  mambo yote yanayohusu neno la Mungu.Hapo tafsiri batili za neno la kristo haziwezi
  kupata nafasi.Tukiwa nje ya upako wa Roho Mtakatifu tunakutana na tafsiri nyingi tu
  za neno la Mungu ambazo zinavuruga sana maisha yetu ya kiroho na kutufanya tusikue.KAZI YA UPAKO WA ROHO MTAKATIFU NI KUTUWEZESHA KUPATA MAFUNUO YALIYOMO NDANI YA NENO LA MUNGU NA HAYO MAFUNUO NDIYO
  YANAYOLETA UKOMBOZI KATIKA KILA ENEO LA MAISHA YETU.Biblia iliandikwa kwa ajili ya wanyenyekevu walio hai wanaoishi duniani(ISAYA 11:4).Kilichomfanya Yesu afanikiwe katika huduma yake hapa duniani ni unyenyekevu na wateule wanapaswa
  kupita njia hiyo hiyo(WAFILIPI 2:2-8).

  TUZAME NDANI YA UPAKO WA ROHO MTAKATIFU(1 YOHANA 2:20,27)

  Je mtu aliyeokoka anaweza kupoteza wokovu wake?Unawakumbuka wapendwa wenzetu ndugu ANANIA na SAFIRA ambao walipoteza wokovu wao kwa kumdanganya Mungu katika utoaji wa sadaka?(MATENDO 5:1-11).Anania na Safira walikuwa ni mume na mke ambao WAMEOKOKA.Roho Mtakatifu aliwapa maelekezo ya kuuza kiwanja ili fedha itakayopatikana wakaitoe yote kanisani kama
  SADAKA YA KIWANJA.Walipouza kiwanja wakakubaliana kwa siri kupeleka fedha pungufu.Wakati Mtume Petro anaipokea sadaka yao,Roho Mtakatifu alimjulisha
  kwamba Anania na Safira wamemuibia Mungu alipowauliza wakakana lakini Petro
  aliwaambia wazi kuwa hawamdanganyi mwanadamu bali wamemdanganya Mungu.
  Wote wawili walikufa gafla mbele ya madhabahu ya kanisa kwasababu ya kutotii maagizo ya Mungu,hakukuwa na mazishi bali walizikwa kwa dharula kama mizoga.Maandiko yanasema waumini wote kanisani wakaingiwa na HOFU NYINGI.
  Lilikuwa ni fundisho la kutisha kwa wote ambao walikuwa wamedhamiria kutoa sadaka
  zao vibaya.Anania na Safira walipoteza wokovu na kupokelewa na shetani kuzimu!Hawakupata nafasi ya kutubu lakini pia walifundishwa kanisani kuhusu umuhimu wa kutii maagizo ya Mungu.

  Kama unadhani natania kuhusu kupoteza wokovu kwa hawa wapedwa wawili,kasome
  kwa kutafakari EZEKIELI 33:1-13.Mstari wa 13 unasema”NIMWAMBIAPO MWENYE HAKI,YA KWAMBA HAKIKA ATAISHI,KAMA AKIITUMIA HAKI YAKE AKATENDA UOVU,BASI KATIKA MATENDO YAKE YA HAKI HATA MOJA WAPO HALITAKUMBUKWA BALI KATIKA UOVU WAKE ALIOUTENDA ATAKUFA KATIKA UOVU HUO”.Ni wazi kwamba damu ya Anania na Safira ILIKUWA JUU YA VICHWA
  VYAO WENYEWE WALA SI JUU YA KICHWA CHA MCHUNGAJI PETRO.ANANIA NA SAFIRA WALIUTUMAINIA WOKOVU WAO WAKIDHANI WANAWEZA KUMUIBIA MUNGU BILA KUTUBU ALAFU WAENDELEE KUBAKI NA WOKOVU!NA MUNGU AKAAMUA KUWAUA KIFO CHA GAFLA ILI IWE FUNDISHO KWA KANISA ZIMA.

  Hata leo tunapotenda dhambi kwa siri alafu tukakataa kutubu tukizani Mungu hajatuona TUNAKUFA KIROHO NA KUPOTEZA WOKOVU.Ikitokea tumekufa kifo cha
  kimwili tunaenda moja kwa moja kuzimu.Wako watu ambao WALISHAPOTEZA WOKOVU na bado wanashiriki ibada ndani ya mikusanyiko ya watu waliookoka.NDIYO
  MAANA KILA SIKU TUNAPOENDA MBELE ZA BWANA KWA UNYENYEKEVU,ROHO
  MTAKATIFU UTUKUMBUSHA KUFANYA TOBA YA DHATI YA DHAMBI AMBAZO TUMEFANYA KWA KUWAZA,KUNENA NA KUTENDA TENA KWA KUZITAJA.HATUTAKIWI KUJIHESABIA HAKI KATIKA JAMBO LOLOTE.UKIKAA NDANI YA UNYENYEKEVU WA YESU,ROHO MTAKATIFU ATAFICHUA MAOVU YAKO YOTE NA KUWEKA KIU YA TOBA NDANI YAKO.

  YOHANA 10:27-28 inaeleza habari ya KONDOO WANAOSIKILIZA NA KUTII MAAGIZO YA MUNGU YA KWAMBA KAMWE HAWATAPOTEA WALA HAKUNA ATAKAYE WAPOKONYA MIKONONI MWA YESU.KWAHIYO UHAKIKA WA KUTOPOTEZA WOKOVU UPO KWA WATEULE WALIOKUBALI KUSIKILIZA NA KUTII MAAGIZO YOTE YA YESU NA KUJINYENYEKESHA KATIKA TOBA PALE WANAPOKENGEUKA,NJE YA HAPA ADHABU INAYOELEZWA NDANI YA EZEKIELI 33:1-13 LAZIMA IFUATE MKONDO WAKE.Ndiyo maana Yesu anatueleza wazi kwamba katika mchakato wa WOKOVU MWENYE KUVUMILIA HATA MWIISHO HAWEZI KUPOTEZA WOKOVU(MATHAYO 24:13).

  Anania na Safira WALISHINDWA KUVUMILIA TAMAA YA FEDHA ILIWAPONZA WAKAAMUA KUMUIBIA MUNGU SADAKA.MBAYA ZAIDI WALIPOULIZWA KUHUSU
  DHAMBI WALIYOFANYA WALIKANA.MATOKEO YAKE WAKAPOTEZA WOKOVU KWA AIBU NA FEDHEA KUBWA NA TUKIO HILO LIKAREKODIWA VIZURI MNO
  NDANI YA BIBILIA.

  Hii ni sadaka yangu kwa Bwana kwa ajili ya wateule wote wanaotembelea BLOG YA INJILI HALISI NA THABITI.Mungu atuwezeshe kuwa na ROHO YA UTII NA KUTOJIHESABIA HAKI.UNYENYEKEVU WA YESU NI ZAIDI YA USHINDI.

  ROHO MTAKATIFU ATAENDELEA KUZAMA NDANI ZAIDI…………..

 80. Lwembe,
  Sidhani kama ni sahihi kusema kuwa, tutaokolewa na dhambi kwa wakati ujao. Hili dhana yenu ya kumwamini Yesu kuwa ndiko kuokolewa kwa wakati ujao, ndiyo inayowasumbua. Mbinguni hakitaenda kilicho kinyonge kaka. Wale watakaoenda huko, ni ile ngano safi. Haijalisi watakuwa wangapi kwa idadi, but ni lazima wawe pure!! Kifo cha Kristo msalabani(kukombolewa), ndicho kinachotufanya tujiandae kwa ajili ya wokovu. Usipotoshe Lwembe taafadhali!!
  Unashangaza sana Lwembe, unawaambia waliokoka kupiga kelele za shangwe kwa wokovu unaoweza kupotezeka??? Kimsingi wokovu anaouzungumzia Kristo ktk Yoh 10:27-28 si sawasawa na ule anaoujadili hapa Lwembe, Haule, Sungura & Co. Maana wa kwao unaweza kupotezeka!! Sasa kama unaweza kupotezeka, kwa nini mnukuu aya zenye kuonesha wokovu wa kudumu wanaouhubiri akina Siyi na Mjema?? Mmetuelewa hadi sasa au bado mnaimba liturujia tu??
  Aidha, kwa taarifa yako Lwembe, shetani anahangaika sana na wale wanaitwa kwa jina la Kristo. Hana shida wala hajisumbui kwa walio upande wake. Acha kudanganya watu Lwembe. Bibllia inasema, “Lakini mwisho wa mambo yote umekaribia; basi, iweni na akili, mkeshe katika sala” – 1Petro 4:7. Unafikiri ni kwa nini wakeshe?? Wanaambiwa kukesha kwa sababu ni saa mbaya!! “Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze. Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kuwa mateso yale yale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani”-1 petro 5:8-9. Ukiwa upande wa Kristo, ndiyo hasa kuuwasha moto wa mashambuzi ya ibilisi dhidfi yako. Ukituambia kuwa eti sisi hatutaguswa(hatutashambuliwa/kujaribiwa, kuteswa n.k.) na ibilisi kisa tuko upande wa Mungu, unatudanganya kabisa. Mungu amekuwa akiruhusu haya yawapate hata watakatifu wake wa zamani. Na ataruhusu hata sisi yatupate japo ana uweza wa kuyazuia. Mojawapo ya sababu zinazomfanya ayaruhusu yatupate, ni kuimarisha imani zetu. Wale wote watakaoonekana kuhimili majaribu yote ya ibilisi, naam hata umauti ukawafika kwa ajili ya Kristo, hao ndiyo wanaovumilia hadi mwisho. Na ndio watakaookoka. Ukisema kuwa wale walio upande wa Mungu kuwa hawataguswa na ibilisi, ina maana kwamba, watakuwa na maisha ya raha mustarehe hapa duniani. Hawatakuwa na uvumilivu maana hawana cha kuvumilia. Hivyo hawatakuwa na sifa ya kwenda mbinguni, maana wanaoenda mbinguni, wana sifa ya kuvumilia maudhi ya ibilisi. Nao huyashinda kwa nguvu za Mwanakondoo, yakaja mengine wakayashinda, yakaja na mengine wakayashinda n.k. yaani hadi imani zao, zitakapokuwa thabiti. Ukiwa duniani, kwa Yesu hakuna tambarare kijana. Acha ufedhuli!!

  Lwembe, shetani si kiumbe wa kula ugali na maharage ukamwendea!! Ni kiumbe wa ajabu sana. Huwezi kudanganya watu kuwa sisi tuliomwamini Yesu, shetani hatusogelei kutushambulia!! Huo ni uongo kabisaa!! Kama aliweza kutangaza vita kati yake na Mungu, akatangaza vita kati yake na Mwana wa Mungu japo vita vyote hivi alishindwa. Lakini hakurizika!! Akatangaza tena vita vya tatu kati yake na uzao wa mwanamke (kanisa) – Kristo(ufun. 12), jamaa huyo sio wa lelemama. Ndiyo, maana Yesu alisema, sisi hatuwezi lolote dhidi ya ibilisi isipokuwa kwa njia ya imani katika YEYE aliyemshinda kwa vita hivyo vyote. Vita vya tatu alivyotangaza, bado havijaisha. Yesu alishalipa deni wanalodaiwa hawa viumbe walioasi –wanadamu. Yesu alishawapa silaha na nguvu za kupambana dhidi ya ibilisi. Mwisho wa mapambano haya, bado. Kristo atakuja kulihitimisha pambano. Na sisi kwa ujasiri mkubwa, chini ya kivuli cha jemedari mkuu -Kristo, hatuna wasiwasi wowote dhidi ya ibilisi. Tujapokufa (kwa kitambo) kama alivyokufa YEYE, tutafuka milele kama alivyofufuka YEYE.
  Lwembe, Halafu sijui unsoma Biblia gani rafiki. Wote wanaokufuatilia kama hawako makini, watapotea kabisa. Biblia inasema kuna fufuo mbili tu. Ufufuo wa uzima na ufufuo wa kudharauliwa milele –“Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele” – Danieli 12:2.

  Ufufuo wa uzima wa milele ni ule ambao watu watafufuliwa wasife tena (Rumi 6:9, I Korintho 15:23, Kolos. 1:15, 18) Hawatakufa tena kwa sababu, ni sharti pawe na mabadiliko ya kimwili wakati wa kufufuka – “kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika. Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa” 1 Korintho 15:52-53. Huu ndio ufufuo aliofufuka Kristo. Na watakatifu wote watafufuka kwa ufufuo huu.
  Katika Kitabu cha Ufunuo wa Yohana, ufufuo huu wa uzima, unaitwa ni ufufo wa kwanza. “Huo ndio ufufuo wa kwanza. Heri, na mtakatifu, ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu” – Ufunuo 20:6. Huu ndio ufufuo wa kwanza kwa watakatifu watakaokolewa.
  Ule ufufuo wa kudharauliwa milele ni ule ufufuo wa mwisho ambao watu watafufuka halafu watakuja kufa tena milele. Ufufuo wa namna hii unaweza kufananishwa na ule uliofanyika ktk Agano la Kale na Jipya. Watu walifufuliwa, lakini walikuja kufa tena. (rejea 2 falm 4:32-37, 13:20-21, Mathayo 9:18-26, Marko 5:21-24, 35-43, Luka 8:40-42, 49-56, Luka7:11-17, Yoh 11:1-44 na mathayo 27:52-53). Kimsingi ni ufufuo wa mauti ya kwanza. Wale waliofufuliwa kwenye ufufuo huu wakajifungamanisha na Kristo, kuna uwezekano wa wao kuchomoka kwenye mauti ile ya pili –ufufuo wa pili.

  Yohana wa ufunuo anauita ufufuo wa pili kuwa ni mauti ya pili, kwa sababu haitakuwa na tumaini lingine tena la kuja kufufuliwa. Mtu yeyote atakayefufuliwa kwenye ufufuo wa pili, huyo yuko moja kwa moja kwenye mauti ya pili. Hana ujanja tena. Ni mateka wa ibilisi hata kama angefanyeje!! Maana atakuwa amefufuliwa pamoja na kundi la “waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili” – Ufunuo 21:8.
  Ufufuo wa pili ni Ufufuo wa maangamizi. Mimi katika kuisoma Biblia, sijawahi kuona ufufuo wa tatu wala ufufuo wa wale watakaoipitia dhiki kuu!! Huo ni uongo na ni mafundisho ya kuzimu ya akina Lwembe. Iweni makini nayo!!

  Aidha, changamoto nyingine, Lwembe inabidi afafanue, Mungu anapofuta majina ya watu, anafuta kutoka wapi? Aliyaandika lini? Kuna vitabu vingapi mbinguni? Asitake kutuletea mafundisho yake ya kuzimu hapa!!

  Ukiwa m-beroya, hautadanganyika!!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s