Je ni ulimwengu wa Sasa?

mahusiano

“Habari za uzima wana SG wenzangu, mwenzenu nina linalonitatiza, nimeangalia ulimwengu wa sasa naona wakaka wengi wanaoa wadada wanaopenda mambo ya kidunia tena hawana hofu ya Mungu na kutuposa sisi ambao tumemtolea Mungu maisha yetu kwa kuomba kila jambo, natamani kujua ni wapi tunakosea hadi hawa wa kidunia wanakidhi haja zao na wenye kumpendeza Mungu kuachiwa maumivu, imenitokea mara tatu japo hao wanaofanya hivyo huangukia pabaya na kuniletea usumbufu tena. Huwa nasimama na kutorudi nyuma naishia kutishiwa na kulaaniwa nao, naomba kusikia mitazamo yenu nimejeruhiwa sana”

–TH

Advertisements

37 thoughts on “Je ni ulimwengu wa Sasa?

 1. T.H,

  Umejibu swali langu.
  Umesema hivi:
  1. siriaz, unahitaji kuwa kwenye ndoa(yaani inahitaji kuolewa)
  2. Pia umesema unahitaji kujua kikwazo cha wewe kutokuolewa.

  Sikia, swali la kwa nini hujaolewa, au nini kikwazo cha wewe lutoolewa, jibu ni kwa sababu hujapata mume wa kukuoa.

  Ok, unachotaka kabisa wewe ni kuolewa.

  Hapa ninahisi mambo mawili, aidha unahitaji companioship ya mume kama mwanamke kamili.

  Au unataka mtoto/ watoto na unahofu ya kupitwa na umri wa kawaida ya wanawake.

  T.H, kwani umejiandaa vyema kwa ajili ya ndoa na kulea familia, umejiandaa vema jinsi ya kuishi na mume?( optional kujibu)

  Sikia dada yangu, wala usijitaabishe nafsi yako, hakuna shetani anayeweza kukuzuia usiolewe. Achana na kujitaabisha kwa ajili ya kuolewa.

  Live yo life, mtumikie Mungu, fanya shuguli zako, tena mshukuru Mungu kwa kuwa hutegemei kuolewa ili kusaidiwa maisha.( bila shaka una maisha yako coz you have gone to school)

  Hakikisha wewe na Baba mko vizuri, hujamkorofisha. Fanya anayokutuma kufanya.

  U know what? He will give u the desires of yo heart without missing.
  Relax woman!

  Fanya jambo moja; yashinde mahubiri ya shetani masikioni mwako( unajua anachokunong’onezaga). Mojawapo ya minong’ono yake ni “utazeeka bila mtoto”.

  Shugulika na masuala ya Baba yako naye atashugulika na ya kwako.

  Halafu acha kijicho mpendwa, hahaaa!

  Swali la kwa nini wasiomcha wanaolewa hicho ni kijicho.

  Nikuulize kama Yesu alivyomuuliza Petro kwa habari ya Yohana ” kwani wewe inakuhusu nini na kuolewa kwao?”

  Wewe fanya kazi ya Babayo, achana na habari ya kuolewa kwao, haikuhusu!

  Where do u go church T.H?

  Bless u!

 2. UNA WITO WA NDOA!!! labda nikuulize t.h mtumishi alikufafanulia maana ya neno au sentensi hiyo? kama hakukufafanulia ulikaa ukatafakari na kumuuliza roho mtakatifu kwamba mtumishi alimaanisha nini? mimi nimeelewa hivi UNA WITO WA KUOMBEA NDOA MBALIMBALI MAANA WITO HAUWI KWA FAIDA YAKO BALI KWA AJILI YA WENGINE KWANZA KISHA NDIPO UNAKUJA WEWE KUFAIDIKA. narudia nilivyoelewa mimi si kwamba nimefunuliwa. ushauri wangu anza kuombea wengine walio ndani ya ndoa unaojua wanapitia magumu na changamoto mbalimbali halafu uone kama Yesu hajakupa haja ya moyo wako.

 3. Pole sana dada jitie nguvu katika kristo Yesu nna ushuhuda kuna dada mmoja alifikisha miaka 40 na alikuwa amekwisha kukata tamaa kabisa kuhusiana na habari za kuolewa lakini mungu alimfanyia muujiza usikate tamaa jitie nguvu katika kristo…kama hupo dar es salaam jitahidi tuwasiliane kama utapa nafasi via Petrus2012.pn@gmail.com…kuna vitu nimeguswa nikushirikishe.

  Yapo maswali mengi huwa najiuliza hivi ni kweli labda idadi ya waume ni chache duniani kushinda wake? swala hilo limekuwa zito kwa majira haya ya leo
  Lakini kwa kweli ecology ya interpersonal relation mara nyingi sana inachangiwa na wazazi wa kiafrika..sababu attention kubwa ya malezi wanapewa mabinti sana kuliko wa kiume..hivyo mwisho wa siku freedom ya vijana wakiume inawaingiza katika mazingira ya kutokuwa tayari kuoa sababu wengi wanaathirika na madawa ya kulevya, pombe, maisha ya uhuni, vifo kabla ya wakati, kushindwa kuanza maisha ya majukumu
  sababu naamini kwamba maandalizi ya kijana wa kiume mpaka kukomaa kiuchumi, kisaikolojia, kimwili na kiroho kuwa tayari kuoa na kutegemewa ni jambo refu sana na asilimia kubwa katika ulimwengu wa kileo vijana hawafikii..tofauti na mabinti sababu misingi na namna wazazi au walezi umakini na uangalifu wanaokuwa nao katika kuwalea

 4. Nduguyangu Sungura kwakua nimeexperience mahusiano yote mawili na sikuweza move on kua kwenye ndoa hadi sasa na siriazi nahitaji kuwapo kwenye ndoa nahtaji kujua nini kikwazo?
  NDICHO NINACHOHITAJI KAMA KUOMBA NIMEOMBA NA KUVUNJA LAANA ZIMEVUNJWA KUOMBA TOBA NIMEFANYA KAMA NI KUUSUBIRI WAKATI WA BWANA MBONA SINA AMANI KILA NIKIWAZA NDOA NAUMIA NA HOFU YA KUJA KUUMIZWA TENA.

  KWANINI PIA WASIO NA SIFA ZILIZOTAJWA KNY BIBLIA WANAINGIA KWENYE NDOA.
  UBARIKIWE.

 5. T.H,

  Happy new year!

  Kuendelea kwa mjadala huu bila kunaonesha jinsi ambavyo uko na serious concern kuliko ambavyo tubaweza kulibeba na kulichukulia zuala lako hapa kwenye mtandao.

  Kuna kitu nimekisoma kwenye post yako hapo juu kimenifanya kuona kuwa ni kweli moyo wako unaumia, japo naamini kristo anakusaidia.

  Ninaweza nikahisi ile guilt conscious ndani yako kuwa may be makosa fulani uliyofanya ndo yamepelekea wewe kupitia kwenye haya maumivu.

  Ukweli ni kwamba anaweza kuyatumia hayo makosa yako kukuadhibu ni shetani, Mungu hawezi kufanya hivyo.

  Adui anatumia hayo makosa kukuletea hatia moyoni mwako, kwa kujaribu kukuambia kuwa unapatwa na hayo kwa sababu ya makosa yale.

  Ukishasikia hiyo sauti moyoni mwako unajisikia kuhukumiwa, ukihukumiwa unakosa ujasiri mbele za Mungu, ukikosa ujasiri unahisi Mungu hayuko nawe.

  Bt believe me, He is just right there with u. U are never alone.

  Kupoteza bikira kunakutesa moyoni mwako, hasa unapokumbuka kuwa ulijikuta unaipoteza kwa kudhani kuitunza kulikufanya umpoteze mchumba wa kwanza, lakini ukakubali uipoteze ili usimpoteze mchumba wa pili, matokeo yake ukapoteza vyote( bikira na mchumba).

  In fact, ishu hasa siyo kupoteza bikira, bali ni kuvunja agano la uaminifu wako na Mungu(kutofanya mapenzi kabla ya ndoa) kwa ajili ya uliyempenda, lakini ukajikuta umepoteza vyote(uaminifu na aliyekuwa sababu ya kuupoteza huo uaminifu), hicho hasa ndo kinakuuguza moyo.

  Pengine nikuulize sasa kabla sijaendelea: What exactly do u want at the moment?

  Nitaendelea..

 6. Nashukuru kwa swali lako (CHRISTOWELLU)nduguyangu katika Kristu jIBU NI KWAMBA WAKATI NAOMBA ILI KUTAMBUA WITO WANGU NI UPI NIKAOTA NIMEVAA SHELA NA NILIPOULIZA MTUMISHI WA MUNGU AKANIAMBIA NINA WITO WA NDOA TENA ILITOKEA NIKIWA KAMBINI KUTAMBUA WITO MBALIMBALI ILIKUA 2001. TANGU HAPO NIKAANZA KUOMBEA NDOA NA KUPATA MWENZI WA MAISHA LAKINI NIMEAMBULIA MAUMIVU.

  NASHUKURU KWA USHAURI WAKO. NASUBIRI MICHANGO YA WALIONIULIZA MASWALI MR.MILINGA NA SERVANT. MBARIKIWE SAWA.

 7. dada TH hongera kwa kuota maana wengine huwa hawaoti kabisaaa, hongera pia kwa kutilia maanani ndoto unazoota wengine hawajali wameota nini.
  ndoto ni mawasiliano kati ya ulimwengu wa roho na wa mwili, ndoto huleta taarifa katika ulimwengu wa mwili toka ulimwengu wa roho, kama umeelewa msingi wa swali langu nataka uchunguze ndoto zako ili uweze kupata chanzo cha tatizo lako, je, umewahi kuota umevaa shela, umevalishwa Pete, unatolewa posta au mahari, upo kwenye sherehe mara nyingi au unakula hovyo kwenye ndoto? angalizo: kama haupo huru kujibu its OK your privacy matters too. ukishajua kama huwa unaota ndoto za namna hiyo fanya maombi ya kubatilisha uchumba, ndoa na mahari za kipepo ulizofungamanishwa bila kujua. ukiona unahitaji msaada wa maombi zaidi basi tafuta mtumishi anayeweza kukubebea mzigo huo kwa maombi ikiwezekana deliverance ifanyike KAMA UNAAMINI KWAMBA UNAHITAJI DELIVERANCE MAANA WENGINE HAWAAMINI KATIKA KUFANYIWA DELIVERANCE. kama huna ndoto za aina hiyo muombee roho mtakatifu akuombee kwa kuugua maana akiomba yeye anayejua kuomba jibu sahihi litakuja maana yeye huomba kwa usahihi.

 8. JIBU KWA NDUGUYANG CHRISTOWELLU Hua ninaota ndoto mbalimbali na nyngi hua zinakua kweli, nitoe mifano mitatu ya hivi karibuni.
  1,NILIOTESHWA JUU YA KUPEWA TAARIFA YA MTU NINAYEMFAHAMU KUFARIKI HAIKUPITASIKU 2 YULEYULE NILIYEMUOTA AKANIPA TAARIFA HYOHYO.

  2.NIKAOTA KUHUSU RAFIKI ZANGU WANNE KUINGIA KWENYE NDOA WAWILI KATI YAO WAMEINGIA TAYARI.

  3.NILIOMBA KUPELEKWA KWENYE SHEREHE YA RAFIKI YANGU NIKAOTA ILE GARI IMEPATA AJALI NIKAMUELEZA ALIYETAKA KUNIPELEKA KUA NIMEGHAIRI KWENDA KWAKUA NIMEOTESHWA AJALI MCHANA WA ILE SIKU AJALI YA HYO GARI IKATOKEA.

  NILIWAHI KULAUMIWA KUA NAENDA KWA WAGANGA NDO NAONYESHWA HAYO NINAYOOTA LAKINI UKWELI NI KWAMBA WAGANGA NAWAONAGA KWENYE MUVI ZA WANAIJERIA NA SIJAWAHI KWENDA HUKO. UBARIKIWE

 9. Jibu kwa kaka milinga.
  1.Kazi zilizokua mbele yangu kama usafi kupika na majukumu yaliyojitokeza nitakapokuwapo kama ni kwenye familia yake kwakua nilishatambulishwa.
  2.Umri wangu ni miaka 37.
  3.Alikua hapendi kuona nakosa amani na alijitolea kwa kila nilichohitaji kama bint. Pia alinishirikisha kila mahali na maamuzi yote.
  4.swali la nne nimejibu kutokana na ushauri niliokwishapewa kua wakaka wanapenda wachapakazi na sio Muda mwigi kuutumia kwa maombi tu. Nikatolea ufafanuzi swala la uvivu sina na pia inapofika majukumu ya familia sipendi kutumia elimu kama kigezo cha kuleta dharau
  NIMEELEZA SIFA ZA MTU ALIYEMCHUKUA HUYO KAKA HAZIMO SEHEMU YEYOTE KWENYE MAANDIKO KUA NI SIFA ZA MKE MWEMA. NDO MANA NAPATA UGUMU WA NINI KINAKWAMISHA KUMPATA MWENZI..

 10. Dada T.H

  Sisi wasomaji wako tungependa kujua mambo mengi sana kabla ya kujaribu kusema machache ambayo huenda yakakusaidia. Ingependeza kama pamoja na swali la ndugu Servant hapo juu, utusaidie na wengine kujua maswali yafuatayo:

  1. Je, wewe ulimfanyia kazi gani huyo mwanaume mpaka akajua kuwa una sifa zote za kuitwa mke hadi watu wote wakasifia?

  2. Kama hautojali, una umri gani tangu Uzaliwe? Natamani kujua umri wako ili kuona kama umefikia umri zaidi ya ule unaopendekezwa kuanzisha au kutoanzisha familia Kiafrika na Kimaandiko.

  3. Unaposema kwenye uhusiano wa pili “Kaka alinipenda mpaka nashindwa kueleza mfano wake…..” ulitumia vipimo gani vya kujua kuwa alikupenda kwa kiwango ambacho huna hata mfano wake?

  4. Unapokaa na kutafakari unaona ni kosa gani unafikiri lilisababisha kaka wote wawili wakuache wakati wewe ni Msomi mchapakazi na mcha Mungu?

  Asante na samahani kwa maswali mengi,

  Mr. Milinga

 11. Nashukuru kwa swali lako,Jibu la swali lako ni ndio isipokua nina experience ya relation zote za aina mbili ya kwanza niliachwa sabababu sikua tayari kushirikiana kimwili na niliyekua nae. Na wa pili nilishirikiana nae.Na ndo uhusiano wangu wa kwanza sikuwahi kuwa na uhusiano wa hivyo NA HUWEZIAMINI NI KITU KINACHONIUMA SANA KWAKUA NILISIMAMA SANA LAKINI NIKAANGUKA.

 12. swali langu moja tu dada t.h mpaka anakwambia unajua majukumu yako kama mke je? uliwahi kukutana nae kimwili?

 13. Bwana Yesu asifiwe,natumai wote mu wazima. Nimerudi tena baada ya tafakari ya ushauri mlionipatia wapendwa katika bwana. NIMETAFAKARI PAST RELATION NI KWAMBA NILIPENDWA SANA NA KUKUBALIKA NAFAMILIA YA HUYO NILIYEFIKIRI AMETOKA KWA MUNGU MANA NILIKUTANA NAE BAADA YA MAOMBI NA KUFUNGA. SIKUZOTE ALIKUA AKISEMA ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUA NAMI KWANI NINAJUA MAJUKUMU YANGU KAMA MKE NA ALINITAMBULISHA KILA MAHALI KAZINI KWA FAMILIA NA MARAFIKI HATA RAFIKI ZAKE WAKAWA WANAMSIFU KUA AMEBAHATIKA KUMPATA MSOMI, MCHAMUNGU NA MCHAPAKAZI. NARUDI MTAA NINAOISHI HATA CHUO NILICHOSOMA.WANAJAMII WAMEKUA WAKISIFU WAZAZI WANGU KUA WAMENILEA VYEMA NA KWELI NI MKE MWEMA. NARUDI KATIKA UHUSIANO HUU WA MWISHO KABLA YA KUJA KUTAKA USHAURI HUYU KAKA ALINIPENDA NASHINDWA KUELEZA MFANO WAKE. LAKINI ILIKUJA KUTOKEA GHAFLA KUNICHUKIA AKAWA HATAKI KUONGEA KAMA KUNA TATIZO LILILOPELEKEA YEYE KUBADILIKA HAKUTAKA VIKAO VYA WAZAZI NA NDUGU.YANI AKAWA ANANIKWEPA KAMA NI KITU HATARI.NINACHOHITAJI KUJUA NI WAPI NINAKOSEA HADI NAISHIA KUUMIZWA TU.
  SAHIHISHO PAST RELATIONS NI 2 NILIANDIKA TATU KWENYE POST YA KWANZA.

 14. ni typing errors tu @mathew. but najua na ninaye mmaanisha hapo ni Yesu kristo alie hai

 15. Maelezo yako mazuri na ya kiroho nimeyapenda! Isipokuwa kumbukwa god is not the same with God. Mungu na mungu siyo sawa na hata yesu na Yesu! Mungu Akubariki.

 16. sija wahi changia humu and in actual fact leo ndio nime kutana na hii blog.

  mimi na weza kusema swala la ndoa shetani amelivalia njuga hasa kwa vijana wa Mungu. kwann na sema hivi
  1. imekua ngumu sanaa kwa watu wa Mungu kupata wenza mpaka kupelekea frustrations na hivo watu kuamua kuoa/kuolewa na yeyote yule atae jitokeza na most of the time ni wa mataifa.
  2. wanaume wamekua ni watafutaji katika mwili na sio wa rohoni same kwa wana wake.. hata tunao jiita wacha Mungu tumekua wakuangali vya mwilini na sio vya rohoni..

  mimi naweza jitolea mfano maana kwenye kusema yawezekana tukaponyana wengine hume.

  kwanza nilikua na kijana ambae haieleweki ni muslim au mkristo maana wazaziwe ni half of both. so nikajipa moyo nita mfanya aokoke na shetani aliteka fahamu zangu maana me nilikua naangali mwili nasio roho.. NIMEOKOKA ila naweza sema kipindi hiki ilikua vugu vugu maana kama ingekua moto nisinge kubaliana na swala hili.. hio ikaisha

  nanilikua naita GUNDU la kufatwa na muslim men all the time.. yaani kila niandako wanifwatao ni hao.. hayumkini roo mchafu alio kua ndani yangu ndie aliokua anavutia wa jinsi yake \utawajua kwa matunda yao” so ni wajibu wako kujiuliza kwann unafwata na aina flani ya wanaume.

  akaja kijana mwengine ambae alikua ni mlokole well wazazi wake ni watumishi kama alivyo sema mdau hapo juu haimaanishi akiwa kaokoka basi huyo ni wako.. hapana sababu yule kaka moyo wangu ulimkataa kabisaaaa na wazazi wangu walinigombeza kwann nakataa na kazania waislamu ila hata kwenye mabaya Mungu bado anatupigania.. yule kaka akapendwa na rafiki yangu wa karibu sanaa (bestfriend) and waka oana lakini am sad to say ndoa yao ili dumu mwaka na yule kaka akafariki. so unaona TH as time Mungu ana tuepusha na Mengi hata pale tunapokua wagumu kuelewa.

  nikapata mchumba ambae siwezi sema kaokoa just coz wazaziwe watumishi but neno analijua na ana hofu ya Mungu na kwa mara ya kwanza ndio kijana pekee na weza sema nime pata ambae ni mchaji Mungu kwa kiasi chake na nilimpenda kwa moyo wote… na kipindi hiki niliamua kuokoka mwili nafsi na roho.. mahisiano haya kwenda mbalisababu kijana alitaka sana vya mwili na mm nili kataa so haijalishi upendo wangu kwake maana warumi anasema ni nini kitakutenga naupendo wa kristo ni uchi LA HASHA na hapa am sorry to say ndiko vijana wengi tunashindiwa kua ukijiona umri umeenda has mabinti na shetani ndiko anaazakukuhubilia ujinga kichwa naww unaupokea.. nilipo mwacha yule kaka niliumia sanaa na bado naumia maana nilimpenda lakini siwezi kosa uzima wa milele kwa mambo ya duniani. nikaanza kuugua na kuumia kua nina gundu hivi nita pata mtukweli hivi vile hivi hivi.. ndoa sio shela na zawadi wapendwa ndoa ni ibada takatifu na pia nikujitoa pande zote mbili.. tuna shinda tukiombea wake/waume wema je umewahi kukaa chini ukaomba kwanza Mungu akufanye kua mke/mme mwema au hicho unacho hitajikwamwenzio na ww uwe nacho kwanza?

  mungu anaangali moyo na sio physical appearance kama yohana asinge pewa ishara ya dove aliposhuka na kumtulia begani kwakwe yy asingejua yule ni yesu anae mbatiza.. ishara tuna pewa lakini sababu tuko mwiilini tunakazana kuomba na kufunga ooh tuoneshe ila sababu sio utakae basi una mlalamikia mungu

  kuna say inasema nilisoma mahalikua “it’s not that you have strong sexual/marital desires, its that you have WEAK spiritual desires”

  yesu/neno likijaa ndani yetu haya mengine tutaona ni yakupita..
  and am not saying hatutakiwi kuwiwa na wenza hapana ila neno limejiweka wazi utafuteni kwanza uso wa Mungu na mengine tuta ongezewa..

  ni heri mwana mke single maana yy upendo wake kwa yesu ni anautoa wote hagawanyi kwa mume kwanza.. wen u love \god first truly and fully i promise u, u will love ur husband/wife with all ur heart hata bila ya ww kujua au kutaka utajikuta tu unampenda sababu yesu kajaa ndani yako na dnio maana ukipata mume/mke alio okoka hata kwenye mafarakano lakini Mungu atawarudisha mstalini sababi kakaa kati yeni na ndani yenu.

  ni gazeti refu kidogo but i hope litakusaidia

  be so full of christ that when a man/woman finds you anamkuta yesu kwanza nje ambae yeye ndie atamkaribisha ndani kukuta ww ulie umbwa kwa ajili yake.

  mbarikiwe wana wa Mungu

 17. bwana asifiwe watumishi wa Mungu kwa kweli nimevutiwa sana na hii maada kwani ndo changamoto kubwa inayotupata mabinti sayuni mbarikiwe sana mliotoa maoni kwani yametusaidia wengi jambo moja la msingi tunalopaswa kujua ni kwamba kuolewa au kuoa ni kwa neema na rehema za Mungu mbarikiwe

 18. Kama mengi unayetnda, timiza na hayo machache yaliyosalia. Halafu mgonje Bwana. Utazishangaa ahadi za Bwana. Dumu kumtafuta na kutimiza iliyo sehemu yako.
  Neema ya Bwana ikufunike ndugu yangu
  Siyi

 19. Dada T.H.,

  Yes, hatukudai mengi.
  Lakini endelea kumuacha Mungu ashughulikie tatizo lako. Hakuna lisilowezakana kwa Mungu. Usilione hata kuwa tatizo.

  Pia ukiwaza hii mada ina lengo ya kutafuta njama za kusaidia wadada ili nao wasikwame, tutaliongelea kitofauti sana, kwani hakuna cha kudharau: urembo, upole, ukristo, kupokea wageni, ujasiri, pesa, …

  Barikiwa.

 20. TH ninakupongeza kwa kuwa muwazi na tena jasiri.
  Usikate tamaa, tena zingatia kuwa mambo ya Mungu wakati mwingine usiwaulize watu bali muulize Bwana Mungu mweneyewe. Akikaa kimya kukujibu nga’ngana kumuuliza na kumutafuta ndiyo imani. Wanadamu wengi tu wanafiki inawezekana ukapata majibu au hata ushauri ambao utakupoteza kabisa.
  Mwisho nikukumbushe wewe na wengine wotekusoma kwa makini Matayo 7:13-14. Njia ya kwenda Mbinguni ni nyembamba na imesonga na waionao ni wachache? Tafakari unataka kwenda wapi mbinguni au unataka ya dunia.
  Mengine hayanabudi kututokea kwa sababu ni sehemu ya kupimwa kwa imani zetu. Mungu Akubariki.

 21. Nduguzangu wawili hapo juu mmependa niweke jina langu nashukuru kwa ombi lenu lakini naomba mniite hivyo kifupi na mjue kwa ushauri wenu mmenijenga sana japokuwa mengi nayatimiliza na ndo mana nikapata ugumu wa kujua wapi hapakuenda sawa na kuwataka ushauri. NINA IMANI KWA MUONGOZO HUU WENGI WANAPATA KUONGOZWA VEMA.
  MBARIKIWE NA BWANA YESU,

 22. Kamugisha,

  Ni kwa namna gani suala la mahusiano ya +ke na +me yanayotengeneza ndoa ni la kiroho na si kimwili?

  Binti aliyeitwa ameposwa kwa utamaduni wa kiyahudi ni yule aliyekuwa ametolewa mahari tayari, na alikuwa akishatolewa mahari tayari anahesabika kuwa ni mke wa huyo aliyetoa mahari.

  Kwa mfano wazazi wa Rebeka walikuwa wametaka Rebela abaki kwao kwa muda baada ya mtumwa wa Ibrahim kutoa mahari. Kama mtumwa wa Ibrahim angekubali na kumwacha Rebeka kwa muda, tayari Rebeka angehesabika ni mke wa Isaka. Ndivyo ilivyokuwa kwa Mariam.

  Hakuitwa mke wa Yusuf ati kwa sababu ya ushahidi wa ulimwengu wa roho, bali ni kwa sababu mchakato unaokamilisha mtu kuitwa mke wa fulañi katika ulimwengu wa mwili ulikuwa umekamilika kwa mujibu wa utsmaduni wa kiyahudi.

  Wayahudi walikuwa hawaoi kwa kufunuliwa, walikuwa wanafuatilia vitu vya kimwili kabisa kama vile ukoo anakotoka mtu, wasifu wa huyo mtu katika jamii yake.

  Katika karibu mifano yote ya ndoa za mfano zilizo katika biblia, hakuna mtu aliyeoaga kwa ufunuo.

  Kuna Ibrahim, kuna Isaka, kuna Yakobo, kuna Obed kwa Ruthu, n.k.

  Lakini hata kama itatokea mtu amefunuliwa katika ulimwengu wa roho siyo guarantee ya kuepuka migogoro na changamoto za ndoa.

  Ndoa inahitaji kuishi kwa hekima na akili!

 23. Dada T.H

  Tafadhali ututilie jina lako hata kwa mwisho ya maandiko yako!

  Tunapenda tukuite kwa jina lako kama ni Tumaini kwa mfano, ok!

  Wakati swala kama hii linapewa watu wa Mungu, kinachotokea haswa ni kuyaona hayo majeraha na kuanza kuonyesha kila mlango wa hayo majeraha. Isikushangaze kama kuna mlango wewe usiyoona hauna maana. Pia hakuna mtu anaejifahamu kitabia. Kila awazapo anapima kuleta sababu.

  Kwa ujumla unayo majeraha kabisa kwani kila mara mchumba anapokutendea kwa hila unaumia, sivyo? Unapoumia, unasema unaomba lakini kigezo cha kuonyesha hukupona majeraha ni kwani ulileta tatizo lako ndani ya SG. Hii ina maana majeraha yapo kabisa. Lakini wewe u karibu kuyapona kwani huyaweki moyoni na kunyamaza.

  -Hatua ya kwanza, omba maombi ya toba wala siyo ya kumuuliza Mungu kwa nini uteswe.
  -Uombe maombi ya utakaso, yaani maombi ya kukuweka zaidi pamoja na Mungu..
  -Umuache Mungu ashughulikie tatizo lako. Kwani kupitia hawo wachumba wanaokuacha ukiwa mwaminifu na wanafwata wasichana wenye mwenendo mbaya, usidhani umepoteza. Wewe ni mshindi. Mungu anakuepusha mambo ambayo ungelijuta mno.
  Wewe tu shika zaidi Yesu Kristo, uone jinsi utaishi na mume mzuri kuliko jinsi unadhani.

  Ubarikiwe.

 24. NENO LA MAARIFA
  Misingi ikiharabika mwenye haki atafanya nini??Naomba turudi katika misingi
  ya kiroho nje ya hapo tunajidanganya.SUALA LA MAHUSIANO BAINA YA MWANAMKE NA MWANAUME YANAYOTENGENEZA UCHUMBA NA HATIMAE
  KUZAA NDOA NI LA KIROHO SIYO LA KIMWILI.NAOMBA NILIWEKE KWA MSISITIZO
  UTAKAO ELEWEKA ZAIDI.UFAHAMU,HEKIMA NA MAARIFA YA ROHONI NDIYO YANAYOTENGENEZA MAHUSIANO YALIYO HAI MWILINI.KUFANIKIWA AU KUTOFANIKIWA KATIKA MAHUSIANO MIONGONI MWA VIJANA YANATEGEMEA
  SANA JINSI WANAVYOLELEWA NA KUJILEA KIROHO.WENGI WANALIA NA KUSAGA
  MENO KWASABABU YA MISINGI MIBAYA YA KIROHO.WENGI WAMEJEGWA KATIKA
  MISINGI YA KIMWILI iliyo nje ya maisha ya utakatifu na uaminifu.

  BILA YA MUONGOZO WA ROHO MTAKATIFU MTU ANAYESHAURIWA AU KUFUNDISHWA KUHUSU NJIA SAHIHI ZA KUPATA MAHUSIANO YALIYO HAI,
  HAWEZI KUCHUJA SANA SANA ATACHANGANYIKIWA ZAIDI(1 YOHANA 2:20,27).
  Roho Mtakatifu ndiye anayetufundisha na kutuelekeza habari za mambo yote kuhusu mahusiano kwa njia ya NENO,MAONO,MAHUBIRI,UNABII,MAFUNDISHO
  NA NDOTO(ulimwengu wa roho).Roho Mtakatifu anaweza akakudhibitishia na kukuonyesha uhalisia wa mweza wako kupitia njia zote hizi.CHANGAMOTO YA WATEULE LEO NI KUTOBOLEWA AU KUVURUGWA KWA MACHO NA MASIKIO YA ROHONI(ISAYA 42:18-20).Wengi hawaelewi hata maana ya macho na masikio ya
  rohoni ambayo shetani pia huyatumia ili watu wasielewe yale ambayo Mungu amewakusudia.SOMO KUHUSU MACHO NA MASIKIO YA ROHONI LIMEPOTOSHWA
  SANA NA MADHEHEBU MENGI YA MASHETANI LAKINI PIA HALIFUNDISHWI KATIKA
  MAKANISA YA KRISTO NA MADHEHEBU YA KIKRISTO.KUNA WATU WALIOKOKA AMBAO WAKO NDANI YA MADHEHEBU NA WALIO NDANI YA MAKANISA YA KRISTO.MADHEHEBU YANAONGOZWA NA MAPOKEO YA WANADAMU AU ROHO YA SHETANI(MATHAYO 15:7-9,1 TIM 4:1-5) WAKATI MAKANISA YA KRISTO
  YANAONGOZWA NA ROHO WA KRISTO(WARUMI 8:14).Hata hivyo KOTE KUNA CHANGAMOTO ZAKE.

  MFANO WA MARIAMU NA YUSUFU(MATHAYO 1:18-24)
  Yusufu alitaka kuvunja UCHUMBA baada ya kugundua kwamba Mariamu anaujauzito
  ambao sio wake na kwahiyo amefanya uasherati!Mimi sijui kama Mariamu alikuwa na UHAKIKA kwamba Yusufu ni mwanaume ambaye alichaguliwa na Bwana kuwa mume wake.Lakini pia sijui kama Yusufu alikuwa na UHAKIKA kwamba Mariamu alikuwa ndiye mke aliyechaguliwa na Bwana,ninachjua ni kuwa walikuwa WACHUMBA
  yaani Yusufu alikuwa amemposa Mariamu(Mstari wa 18).

  Yusufu na Marimu waliishi katika mahusiano ya uaminifu ili wafunge ndoa takatifu.Mariamu alikuwa bikira na Yusufu alikuwa mtu wa haki.Pamoja na kwamba walikuwa na wachumba lakini katika ulimwengu wa roho
  yusufu alikuwa tayari ni mume halali na mariamu ni mke halali kwasababu walikuunganishwa na Mungu(Mstari wa 19,20,23).Kwahiyo mchumba aliyotoka kwa
  Bwana tayari ni mke au mume.Yusufu wakati anataka kumkimbia Mariamu kwa siri bila ya kujua kuwa mimba ile aliipata kwa uweza wa Roho Mtakatifu,ndipo malaika
  akamjulisha KATIKA ULIMWENGU WA ROHO,kwanza Mariamu ni mkeo(hakutumia neno mchumba pamoja na kwamba walikuwa hawajaoana bado) na amebeba mimba hiyo kwa kusudi la Mungu(mstari wa 20 -23).kupitia taarifa hii kutoka katika ulimwengu wa roho ndipo tunapata UHAKIKA KWAMBA Yusufu alikuwa mume halali wa Mariamu na Mariamu mke halali wa Yusufu.Na Yusufu akafuta maagizo yote kama alivyopewa katika ulimwengu wa roho(mstari wa 24).Nina uhakika hata Mariamu atakuwa alijulishwa na kufarijiwa kuhusu hofu ya Yusufu katika ulimwengu katika ulimwengu wa roho.

  SOMO TUNALOJIFUNZA HAPA
  Katika mahusiano kuelekea katika uchumba na hatimae ndoa ni lazima kuishi maisha
  ya uaminifu na utakatifu sawa sawa na misingi hai ya kiroho uliyolelewa.Yusufu na Mariamu walilelewa katika misingi ya TORATI(LUKA 2:22-24).Na kama kuna maovu yatatokea ni lazima kufanya toba ya kweli ingawa mara nyingi dhambi ya uasherati kabla ya ndoa inaweza kuharibu kila kitu.UHAKIKA KUHUSU MWENZA WAKO MARA NYINGI UTAPEWA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO.Yusufu na Mariamu walikuwa na
  MACHO NA MASIKIO YA ROHONI.Kama Yusufu kupitia ulimwengu wa roho aliweza
  kujulishwa kuhusu ujauzito wa mchumba wake ni dhahiri pia alishajulishwa pia kuhusu uhalali wa uchumba wao.Roho Mtakatifu ndiye anayeweza kutofautisha na kutujulisha kuhusu taarifa zinazotoka kwa shetani na zile zinazotoka kwa Mungu.Ukiwa unasali ndani ya madhehebu ya shetani utapata na kuona vitu kutoka katika ulimwengu wa roho wa giza.Utakuwa unawaona hao hao watumishi wa shetani
  na maagenti wenzao.Pia watakuonyesha mwanaume au mwanamke asiye sahihi katika ndoto.
  Ni lazima

 25. NAMSHUKURU ROHO MTAKATIFU ALIYEWAONGOZA NDUGUZANGU KTK KUNISAIDIA KUNIONGOZA KWENYE HILI JARIBU.NASHUKURU KWAKUA NIMEFARIJIKA NA MICHANGO YENU. NAOMBA KUJIBU MASWALI YALIYOULIZWA NA WACHANGIAJI KUNA SWALI KUA NILIPOSEMA ASIYEMJUA MUNGU NILIMAANISHA NINI. JIBU MIMI NIMEMTOLEA MFANO HUYU ALIYEMCHUKUA NILIYEKUA NAYE NI MSHIRIKINA, MCHAFU YANI ANA MAHUSIANO ZAIDI YA MTU MMOJA, ANATUMIKA KINYUME NA ASILI YA MWANAMKE INAVYOMPASA, MLEVI KUPINDUKIA HAYO NI MACHACHE KATI YA NINALIYOYAONA KUA NI MAPUNGUFU KWA MACHO YANGU. SWALI KUHUSU MAMA YANGU KUNA KIPINDI WALIHITILAFIANA NA BABA LAKINI WALISULUHISHWA NA IKAWA AMANI HADI UMAUTI ULIPOMFIKA BABAYANGU.NAE ALIKUA AKIWAASA KINA KAKA KUA MSIJE KUKWAZA WAKE ZENU KAMA NILIVYOMKWAZA MAMA YENU. KUHUSU KUJITUMA HUA NAJISHUGHULISHA NAFIKIRI KUPITA UMRI NILIONAO NA HATA KUA NA MAENDELEO YALITOZIDI UWEZO WANGU. SWALI KUHUSU NIMEWAPATA KWA NJIA GANI HAO WALIONITENDA NA NDILO LILILONIUMIZA SANA KICHWA. HUA NASALI NAFUNGA NA KUOMBA NA HATA BAADA YA KUONYENSHWA MTU HUA NAOMBA TENA KUJUA KATOKA KWA MUNGU MFANO NILIPOKUTANA NA HUYU WA PILI NILIINGIA KUOMBA KUA AONYESHE NIA YAKE HAIKUPITA WIKI MBILI AKANIULIZA TARATIBU ZA KUJA KWETU NIKAMUELEZA IKAWA NI AMANI FAMILIA YAKE ILINIFURAHIA YETU PIA. ALIPOBADILI MAWAZO ALISHAURIWA SANA NA FAMILIA ALIKUA ANAWAJIBU VIBAYA NDUGUZAKE.MIMI TANGU KIPINDI HICHO NIMEKUA NIKIMWOMBA MUNGU ANIJULISHE KUSUDI YA HAYA KUTOKEA NA SIJAPATA JIBU HADI LEO NDO MANA NIKAOMBA MSAADA WENU NDUGUZANGU. MBARIKIWE

 26. Pole dada TH,
  Lakini mimi naomba kukuuliza kitu kimoja; Hao wanaokuacha na kukutosa, umewapata kwa njia ipi? maana kawaida unapoingia kwenye mahusiano mpaka uchumba na hatimaye ndoa, lazima unafanya maombi, toba na mafungo ili Mwenyezi Mungu akuoneshe kama ni mume mwema au la! Sasa wewe inakuwaje?
  Nachokuomba, Mwabudu Mungu katika Roho na kweli.”Mungu wetu alivyo wa ajabu,hata siku moja habariki Upumbavu” Acha kuigiza aina ya maisha ambayo si ya kwako, kama umeamua kuokoka na uokoke kweli na wala hakuna jambo la kipumbavu litakufadhaisha! Ukiigiza utakatifu ndipo mambo kama hayo yanakukumba na kuumiza moyo wako.

 27. Ndugu Sungura,

  Inaomba tu uvumilivu kwani anaechokoza na hicho kinyuki wote ni sawasawa.

  Amen.

 28. Dada yangu ni kupongeze sana kwa namna ulivyoendelea kusimama na kumtumainia Mungu.Dada nikwambie mambo haya ktk hali ya kawaida hayana kanuni,eti useme,uongee hivi,au uvae hivi,utembe vile,huo ni uongo wa watu.naomba ni kwambie just endelea kusimama na Mungu na endelea kuwa mwaminifu mbele za Mungu,siku zote Mungu ni mwaminifu na atakupatia yule wa kwako.usiumie eti kuona watu wanaoa au kuolewa kinamna yeyote vile,tambua ndoa nyingi ni majanga,kwa maana watu wanaenda kama mbuzi,wanadhani waonavyo ni sahihi,lakini wanapoingia wanakuta wamebugi.wewe mwenyewe ni shahidi wale waliodhani walipatia hurudi tena kwako kwa majuto.Dada endelea kumtegemea Mungu,maana amtumainiaye Mungu siku zote hawezi kuaibika.shida ni pale vijana wanaposhindwa kutambua wakati wa Mungu si sawa na wakati wa mtu autakao.kukosa subira kumgojea Bwana kumefanya wengi wakose kile Mungu alichokusudia juu yao.kusema kuzamazama ndiyo kigezo cha kutoolewa huo ni uzushi.maana hatukupewa roho wa utumwa ..soma warumi 8:14-25.Mgoje Bwana Dada.

 29. ni kweli kaka sungura wengi wadada wanaomjua mungu wanamsemo wao YESU ANAKIDHI YOTE au ANATOSHA (samahani umenitoka huo msemo)….alafu basi hata kujiweka msafi akavutia basi hamna….hata heleni kuvaa tu wanagoma nimesikia ivo kwa masikio yangu mdada mmoja akishuhudia hilo na akisema ivyo…….wanajiweka wanakuwa kama wabibi hata mavazi yao(sina maana wajifananishe na dunia)…..ni kweli BEAUTIFUL IS VAIN kama mithali inavyosema…..nasema ivo jambo ilo linanigusa sana sikupata eneo hata la kucomment tu…..ninyi wadada mnaomjua mungu badilikeni inatupa shida sana sisi vijana wakaka ….na wengi vijana wenzetu kuingia katika mtego ambao wengi wa kiume walijutia maamuzi yao na hawana namna ya kutoka tena hata maana wengi hawakumsikiliza roho wa mungu na mafundisho a mungu yaletayo maarifa na hekima kuhusiana na habari za mahusiano ambayo yanayompa mungu utukufu (Hosea 4:6b) wamejikuta wakipoteza furaha na kuambulia majuto na hata kuishia kuanguka kiroho (Your best career decision is who you marry) na tunamuhitaji mungu sana eneo hili atusaidie…….Kweli wadada maomjua mungu BADILIKENI!!! kwa hili…vijana wenzangu (single) mkipata muda angalieni mafundisho ya mtumishi huyu wa mungu Youtube…Choosing a wife/Beauty is Vain-Tim Conway….Barikiwa sana

 30. Unajua mtu anayefurahia kukuchokoza, hata kama utakuwa umeongea kitu kizuri tu chenye utulivu ndani yake, lazima akichokonoe ili tu uamke akuchokoze vizuri.

  Kuna mtu hapa kwa makusudi anajaribu kurushia mzinga madongo ili angalao kitoke kinyuki kimoja kianze kumfukuza, ndo raha yake hiyo!

  Jamani, ukioa Delila nao unaweza kuwa mpango wa Mungu vilevile, kwa ajili ya kusudi maalum la Mungu.
  Si lazima kuwa ilikuwa bahati mbaya Samson kunasa kwa mrembo Delila!

  Umaridadi na urembo nao ni muhim katika ulimwengu wa uwenzi, siyo maombi tu!

 31. Dada,

  Shukrani kwako kwa msaada unaouomba, shukrani pia kwa wote wanaokutolea mashauri. Sitarudilia ya wenzangu kwani yote ni mazuri kabisa. Nataka nikushaurie kama aliekukomalia kimwili na kiroho.

  Biblia inasema hivi:
  “2 Petro 1: 5 Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa,
  6 na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu saburi, na katika saburi yenu utauwa,
  7 na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo.
  8 Maana mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele, yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda, kwa kumjua Bwana wetu Yesu Kristo.
  9 Maana yeye asiyekuwa na hayo ni kipofu, hawezi kuona vitu vilivyo mbali, amesahau kule kutakaswa dhambi zake za zamani.
  10 Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe.”

  Dada, bila shaka unaona ninapoelekeza. Nataka “imani” isitembee katika upofu.
  Kaka anapotaka kuoa anachunguza kwanza mama mzazi wako anaishije na baba mzazi. Tatizo wamama walokole wengi wanalo ni kujifanya walokole kuliko Yesu mwanyewe aliyewaokowa. Mama mzuri anatosha chembechembe yake katika Mithali 31. Ingine inaendelea katika kumwamini Yesu Kristo.
  Tatizo iliyopo ni kwamba wanawake walokole wengi hawajali na nyumba zao, wageni, kuwatii waume wao, …. Wanakuwa kama wamerogwa na wachungaji wao au wasimamizi wa makwaya, au wasimamizi wa maombi. Hawo wamama wanapoteza wema, utiifu ndani ya jamaa wakidhani wameolewa na Yesu, wala wengine ni watu bure tu. Kuna wanawake walokole wanaoweka dishes za dhahabu kuwawekea chakula wachungaji wao lakini eti hawawezi zitumia kwa waume wao !!!

  Dada, pamoja na kuvumilia, jihoji vile vile kama namna yako ya kuokoka siyo ile ya ujinga, ya kuaminishwa wala siyo ya kuamini kabisa.

  -Upole wako umejulikana na watu wote?
  -Je na upendo wako?
  -Na wema wako je?
  -Unawapokea watu sawasawa?
  -Unafahamu kupanga sawasawa mda wako?
  -Unafahamu unachokitafuta?
  -Hulaumiwe kwa mambo ya uasherati? (Kwani wadada wengi wanajionyesha kuwa walokole wa kupita kiasi hapo wakizini). Kuna wasioamini ambao wanaogopa uasherati, na hawa ndiwo wanapendwa sana kwa kuolewa)
  -Wewe husemi kama umeisha olewa na Yesu, full stop?
  -Mama mzazi wako ni je? Anamheshimu mumewe kwa kutetemeka?

  Hii ni dondoo ndogo tu , lakini jithahidini kuenenda kama dada anaestahili kuolewa hata kama mama ameishakorofisha mambo. pamoja na kuomba Mungu, utajibiliwa.

  Asante.

 32. Dada, TH,
  Pole mjoli wa Bwana kwa yaliyokukuta. Mimi napenda kukwambia kuwa, unapaswa kumshukuru Mungu kwa hayo yote yaliyotokea. Maana huenda ungeolewa na mmojawapo wa hao akina kaka, ungeimba wimbo usio na chorus maisha yote!!
  Nikijuacho ni hiki kwa mabinti wanaochelewa kuolewa/kuachwa/wanaotendwa.
  1. Kujirahisi rahisi tu kwa kila kitu. Acha kabisa. Kama nilivyokusoma kuwa u mwaminifu, zidi kuwa mwaminifu sana. Hata kama ungekuwa na jicho moja, sikio moja, mguu mmoja, kalio moja plus kibyongo nk, kama ukidumu kuwa mwaminifu ukingoja Bwana, nakuhakikishia utapata mume bora. Mgoje Bwana, wala usitahayarike kabisa.
  2. Mche Mungu kwa nguvu zote. Kuwa mtu wa maombi sana na kusoma Biblia. Penda kuchangia logic/sensitive ideas kwenye mijadala. Changia lakini kwa heshima na adabu kubwa bila kujali una aina gani ya wanaume. Ili uwe mchangiaji, sharti uwe mtu wa kujisomea. Punguza muda wa fcbk na whatsapp then uwekeze kwenye magombo. Uwe mzungumzaji mwenye kiasi. Ukiwa mkimya tu sana, utakosa waume!!
  3. Jiweke nadhifu mwili wako wote(Kuanzia mavazi, kinywa nk). Sungura amesema jambo la maana kwenye usafi japo kasema kimasihara sana. Sina maana kwamba uvae vya gharama sana, uvae mawigi na kusuka nywele. Baki binti Sayuni tu. Baki natural. Unapendeza sana wewe!! Mawigi, misuko na manywele yenu hayo ya kukari kwa walio wengi huwa yananuka ila huwa hamuelewi maana ninyi harufu hizo mmeziozea. Mungu hajawaumba na hayo, acheni. Kwa kuzaliwa mwanamke tu wewe ni ua tayari. Vaa mavazi mazuri na yenye heshima yawapasayo wanawake wachaji Mungu. Hata kama ungevaa magunia, bado wanaume tungekufuata tu. So huna haja ya kumrekebisha Mungu kimwonekano zaidi ya kuwa msafi tu. Wanaume tuna tabia ya kibeberubeberu!! Huwa tunapenda kunusa harufu za wasichana. Ukinuka kikwapa tu au kinywa, wanaume watakukimbia.
  4. Weka mazingira ya kwenu, nyumba unayolala nk katika mazingira ya usafi. Kama kuna wazee wachafuwachafu, watoto wasiooga kwa siku mbili na kuendelea, wafulie nguo zao, wapatie maji ya kuoga, ilmradi wawe nadhifu. Fanya hivyo siku zote.
  5. Chapa kazi sana. Usipende kulala mapema wala kuchelewa kuamka. Biblia imewaponda sana wanawake wa namna hiyo. Fanya kazi kama punda ikiwezekana mama yako hadi awe anakwambia “mwanangu pumzika basi” unachapa kazi tu.
  6. Usiwe mtu wa kuropokaropoka. Msengenyaji wa watu. Mtu wa kuzungumzia mambo ya wengine. Acha!! Acha kuwa na muda wa porojo!! Wacha Mungu huwa hawana mida ya porojo. Be organized dada.
  7. Hata ukionewa kwa isivyo bahati au kwa makusudi, acha kung’aka. Ukishindwa kusema kwa upole, nyamaza au ondoka eneo hilo, na usichukue muda mrefu bila ya kusamehe! Samehe tu hata kabla mkosaji hajakuomba msamaha!! Wanaume tuna njia nyingi sana za kutafuta wanawake wenye sifa. Mojawapo ni kukuchokoza kwa makusudi na baadaye kukusikilizia, utasemaje!! Angalia sana.
  8. Epuka vya bure. Vitakutokea puani. Hakuna cha bure chini ya jua, utavilipa tu. Epuka sana. Kama ni kwenye daladala, mara nyingine na wewe walipie wanaume nauli. Walipie chakula. Wawekee vocha!! Usipende kuwa mzigo kwa kijana. Huwezi kufanya haya, bila ya kuwa mchakalikaji. Chakalika na kazi.
  9. Uwe mtu wa kuiga mazuri kutoka kwa wengine. Kuwa mbunifu kwa kila jambo. Acha tamaa. Uswe mtu wa kulalamikalalamika.
  10. Jitahidi kujali pia mwonekano wa marafiki plus mchumba kama yupo kimavazi. Washauri nini wavae na wavaeeje. Onesha kuwajali pia.
  11. Penda watu wote hata wale wanaokusema vibaya sana. Usiwaombee mabaya. Penda wenye shida. Kaa, zunguma na wenye shida. Onesha upendo kwa watu wote, lakini usiwaamini sana, maana wa kumwamini ni mmoja tu – Kristo.
  12. Penda kupata ushauri kutoka kwa wazee wa kike wenye hekima. Utapata mengi zaidi ya chini ya kapeti kwenye suala la mahusiano, hivyo utajua namna ya kujipanga kukabiliana na hali ya namna hiyo endapo itatokea kwako.
  Nikipata muda, nitakuja tena, yapo mengi ya kukwambia. Lakini zaidi ya yote, funga, omba, changamka, tabasamu, mshangilie Bwana ktk yote, maana hiyo ndiyo njia ya waaminifu!!
  Bwana akuangazie nuru ya uso wake. Bwanakupatie mume mwema endapo utakuwa mwema pia.
  Wasalaam
  Siyi

 33. Hongera sana Dada TH kwa kulipasua jipu la uchungu linalosumbua ndani ya moyo
  wako!Tunachotakiwa kukusaidia sasa siyo kusafisha na kuondoa usaa wote ndani ya hilo jipu bali ni kuondoa kiini chote au mtoto wa jipu ili kusudi jipu lisije likaanza upya
  tena alafu work done ya kulipasua jipu ikawa ZERO!Kazi ya kuhakikisha unajisafisha na kuondoa usaa wote ni ya kwako.Nakupa pole kwasababu nayajua vizuri maumivu
  ya jipu la uchungu.Roho Mtakatifu naomba unisaidie hapa ili UPAKO WA KUFICHUA
  UTAWALE NA KUMILIKI(LUKA 12:2,YEREMIA 33:3).

  Naomba tumsikilize Roho Mtakatifu kwa makini sana.CHANGAMOTO tuliyonayo
  ndani ya kanisa kwa sasa ni kina dada kutamani wanaume WA UKWELI na kina kaka
  kutamani wanawake WA UKWELI.Ni wachungaji wachache sana ambao wanaingia gharama ya kuhakikisha wanawake wanafunga ndoa na wanaume WA KWELI na wanaume wanafunga ndoa na wanawake WA KWELI.Kuna tofauti ya milele kati ya
  mwanaume wa KWELI(uliyepangiwa na Bwana) na mwanaume wa UKWELI(ambaye hujapangiwa na Bwana).KWELI inatokana na Mungu na UKWELI unatokana na mambo ya mwilini(YOHANA 17:17)Hasira ya Mungu ilipowaka mpaka akaamua KUUA VIUMBE HAI WOTE kwa gharika ya maji kipindi kile cha NUHU(MWANZO 6:1-6),sababu hasa
  ni CHUKIZO LA WANA WA MUNGU KUFUNGA NDOA NA MBWAMWITU(wanadamu).Sikiliza! mwanaume anaweza akawa ni mwana wa Mungu mwezako lakini
  siyo yule ambaye Mungu alikuchagulia toka kuanzishwa kwa misingi ya dunia kwahiyo
  akaingia katika kundi la mwanaume wa UKWELI AMBAYE SIYO MBWAMWITU.Mwanaume ambaye ni mbwamwitu yuko connected na mungu mwingine na anapokuja kwako kazi yake ni kuharibu MAONO NA HATIMA YA MAISHA YAKO NDANI YA WOKOVU.Zipo ndoa za wana wa Mungu ambazo siyo sahihi na ndoa kati ya mbwamwitu na wana wa Mungu ambazo zimeelezewa kwa uwazi sana katika kitabu cha EZRA 9:1-15 na EZRA 10:1-19.Ndoa kati ya wana wa Mungu(mbegu takatifu) na mbwamwitu ni LAZIMA ZIVUNJWE.Ukiwa na macho na masikio ya rohoni ni rahisi kutambua uhalisia wa mahusiano uliyonayo na kuchukua tahadhari mapema kabla ya kuingia kwenye MAUMIVU.Hii inahitaji kuishi maisha ya uaminifu na uatakatifu-MAISHA YA TOBA ISIYO NA UNAFIKI.LAKINI PIA INATEGEMEA NA MISINGI NA UHALISIA WA KANISA UNALO KULA CHAKULA CHA KIROHO.WACHUNGAJI WALIOOLEWA NA FEDHA BADALA YA KUOLEWA NA YESU
  HAWANA MUDA WA KUSIMAMIA HALI ZA KIROHO ZA WAUMINI.KATIKA SUALA LA MAHUSIANO NA NDOA VIJANA WENGI WANALIA NA KUSAGA MENO.WATEULE WENGI SASA WANATANGATANGA KWENYE MAKANISA KUTAFUTA WACHUMBA
  MATOKEO YAKE WANAANGUKIA MIKONONI MWA MBWAMWITU(EZEKIELI 34:1-8).HUU NI WAKATI WA BWANA KUWAACHISHA KAZI WACHUNGAJI KAMA HAWA MAANA WANAFANYA KAZI YA MBWAMWITU IWE RAHISI(EZEKIELI 34:9-10).MITAZAMO,FASHION NA USHAURI WA KIDUNIA NDIYO UNATAWALA MIND-SET
  ZA VIJANA MAKANISANI!!!

  NGOJA NA MIMI nipasue jipu.MISINGI IKIHARIBIKA MWENYE HAKI ATAFANYA NINI?
  Tatizo ni kuharibika kwa misingi ya unyenyekevu ndani ya makanisa ya wateule.Wateule hawafundishwi jinsi ya kutembea ndani ya ULIMWENGU WA ROHO
  na wachungaji hawaingii gharama ya kuwafundisha vijana kuhusu MAARIFA YA KUELEKEA KATIKA SIRI YA NDOA.Neema ya Mungu inatupigania lakini bado yapo
  mahusiano mengi ambayo ni ya KIMWILI.Vijana wanaangalia zaidi mapenzi yao badala ya mapenzi ya Mungu na wachungaji hawaingii ndani ya ulimwengu wa roho
  kuangalia uhalali wa mahusiano ya vijana.Mtu anaendelea kuumizwa mpaka anazeekea kanisani!Mahusiano ya kishabiki yanayoangalia mambo ya kimwili yametawala zaidi.HII NI TISA(WAGALATIA 3:3).

  KUMI ni kwamba JARIBU ZITO TULILONALO KWA SASA NI UWINGI WA MAKANISA YA MBWAMWITU(MATENDO 20:28-31).Zaidi ya asilimia 85 ya makanisa yote duniani ni makanisa ya mbwamwitu!!Ndani ya haya makanisa ndoa nyingi za wateule zimevunjwa na vijana wengi wamezuiwa wasioe wala kuolewa.MAFUNDISHO YA MASHETANI NA ROHO zidanganyazo zinatumika sana kuvuruga misimamo ya kiroho ya wateule.Ndani ya haya makanisa wateule wameishia kuteseka kwa uvumilivu ulio kufa au kuoa na kuolewa na mbwamwitu(1 TIMOTHEO 4:1-3).Lakini pia kuna mbwamwitu wengi tu ambao wamejiingiza kwa siri ndani ya makanisa ya wateule(YUDA 1:3-4,12-13,17-230 ili KUBATILISHA MAHUSIANO SAHIHI YA VIJANA na kuharibu unyenyekevu wa wateule,kazi yao kubwa ni KUNAJISI MADHABAHU NA MAFUNDISHO YOTE YANAYOTOLEWA KANISANI.Wanakuja kusambaza roho za uzinzi,uasherati,majivuno,kiburi,majivuno,mafarakano,roho za kuharibu maombi,sifa na kuabudu n.k.KWA UJUMLA WANATAFUTA SANA KUTOBOA MACHO NA MASIKIO YA ROHONI(ISAYA 42:18-20).Wateule wengi ni vipofu na viziwi katika ulimwengu wa roho.MBWAMWITU VIJANA WALIO WENGI WAMEJIKITA KATIKA HUDUMA ZA UNJILISTI NA UIMBAJI.Na wote hawa wamefuzu katika vyuo vya manabii wa uongo
  mara nyingi HUTUMIA NDOTO ZA UONGO KUDANGANYA MABINTI NA WANAUME
  AMBAO NI WANA WA MUNGU(YEREMIA 23:32).WENGINE TUNACHANGIA NAO MADA NDANI YA HIZI BLOG ZA INJILI wakikazana sana kupanda mbegu za uongo.MMWAMWITU HAWANA SHIDA YA KUOA WALA KUOLEWA KAZI YAO NI KUHARIBU MAONO NA HATIMA ZA WATEULE.NI LAZIMA UJUE KWA JICHO LA ROHONI UHALISIA WA KANISA UNALOSALI NA WAPENDWA WALIOKUZUNGUKA.

  ROHO MTAKATIFU ataendelea kufichua kwa undani zaidi…………………

  MOTO WA YESU HAUZUILIKI KWA SASA UNATAFUNA MIFUPA YA MBWAMWITU
  (LUKA 12:49).UKILISHINDA JARIBU LA MBWAMWITU UTATOKA KWENYE TANURU
  LA MOTO KAMA DHAHABU SAFI NA HALISI(AYUBU 23:10).

 34. This is interesting eh!
  Mpendwa,(japo sijui kwa nini umeficha jina na kutumia initials) hawa unaowaita wa kidunia wakoje hao, hawajaokoka au ni wasafi sana, au wakoje yaani?

  Ivi ninyi akina dada mnajua wanaume(hususani wenye mfano wangu) hatufurahii kuoa mtu wa kirohoroho, yeye muda wote ni halelluya, muda wote ni toka shetani, muda wote ni kunena kwa lugha.

  Badala yake tunapenda kuwa na mtu ambaye ana make sense, ni msafi na anajua kupangilia mambo, mchapa kazi, anajua jinsi ya kujiweka, mwenye kufungua kinywa kwa hekima, ajuaye jinsi ya kuwa romantic.

  Mkono wa kuume wa hayo niliyotaja kuwe na kumcha Bwana sasa! Lol, yeyote anayejua maana ya mke mwema hawezi kumwacha aende zake binti wa namna hiyo.

  Ukisoma sifa za mke mwema kwenye Mithali 31:10-31, utagundua namna ya mambo kama hayo niliyotaja, ndio sifa za mke mwenye kumcha Mungu.

  Mtu(mwanaume) mwenye kufuata tu mwanamke mwenye kitu ambacho biblia imekiita upendeleo(mstari wa 30) lakini neno halisi lingekuwa Kuvutia/ attractivess/ charm , hudanganya na urembo ni kitu kisichodumu, bila kujali hiyo sifa niliyoiweka mkono wa kuume wa huyu binti, yaani kumcha Bwana, vasi huyo huishia kujuta kama hao uliosema hujata baadae.

  Nifupishe hivi: ninyi mabinti wengi mnaomcha Bwana, mara nyingi mnatoswa kwa sababu mnazingatia tu kumcha Bwana na kuyapuuza hayo mambo mengine.

  Hao wanaume wanaowatosa nao huzingatia tu hayo mengine na kusahau sifa ya kumcha Bwana.

  Kwa hiyo wewe dada hakikisha unayo yote, na yamebalance uone kama kuna mtu atakutosa.

  We dont marry a beautiful one, we marry a woman of noble character!!

 35. dada TH,

  Pole sana kujeruhiwa. Hata ivyo usijali, Mungu ni Mwema atakupatia mume mwema.dumu ktk imani.

  Wala hayo yanayo kupata hauko peke yako, wala sio ya ulimwengu wa sasa, yalikuwepo tangu kale, enzi na Nuhu, soma Mwanzo 6 utaona uzoefu km huo.

  Pia hata samsoni, ktk waamuzi, alifanya vivyo hivyo!

  Sio kwamba enyi binti za Yerusalem mna mapungufu au kasoro. Sio,hata kidogo. Ishu ni kuwa wakaka wengi hawajaongoka kikweli kweli, wameenendelea kuufuata mwili na tamaa zake. Wanaendenenda kwa kuona sio kwa imani, na hivyo mjaribu anapowajia kwa kuwapitishia vimodel, huwa wepesi kuangukia majaribuni!

  La msingi, endelea kujitunza na kudumu ktk imani.,huku ukijua kuwa mume mwema kumpata ni gharama.

  Ubarikiwe.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s