Msaada wa kutafsiriwa ndoto zifuatazo!!

ndotoYakwanza; niliota napewa dawa ya tumbo ya kienyeji nisiyoifaham na watu ninaoishi nao(mkena mume) si ndugu zangu

Yapili; niliota napikia ndan ya nyumba ambayo siishi,katika upishi tulikuwa na mke wa mwenye Nyumba.mwanamke huyo alikuwa uchi na mwenye uume uliosimama alikuwa kavaa kanga moja mara anaifungua mara anajifunga Nyumba hiyo wanaaishi mke na mume (hawajafunga ndoa) na kijana mwingine.

Yatatu; niliota nipo katika sherehe ambayo tumekula  na tayar sherehe imeisha  na tunaanza kukusanya vitu,nikiwa nafungua betri iliyotusaidia kutoa mwanga mara ikanipiga shoti ya umeme mara nikaacha kidogo ,hapo baba mwenye nyumba alikuwa anaoga mara akafungua mlango wa bafu nakuniagiza nimchukulie maji yamtoto wake maji yakuoga lakin sikutekeleza,Hapo mkewe alikuwa ananiogopa sana na hakutaka nimuone ktk ndoto hiyo.Hapo alipofungua mlango wa bafu mwanaume alikuwa uchi upande mmoja yaan upande wa kulia kipindi mlango wa bafu uko wazi mwanamke alijificha nyuma ya mlango huo hivo hakutaka nimuone kabisa katika ndoto hiyo.

Note:katika ndoto zote nimewaota mke na mume wakiwa pamoja, Wala hawakushangazwa na vitendo vyao mbele yangu mfano kitendo chakuwa uchi

Tafadhali nahitaji msaada ili nichukuwe tahadhali mapema,

Natanguliza shukrani

–SO

Advertisements

16 thoughts on “Msaada wa kutafsiriwa ndoto zifuatazo!!

 1. Salamu Kwako Mtumishi Wa Mungu Alie Hai, Nashukuru Kwa uduma Pia Mungu Alie Kukabizi. Nina Itaji Musaada Wakipekee Kuhusu Maisha Yangu Yakiroho.Unitumie Adresse Ambayo Naweza Tumia Kwaku Wasiliana Nawewe. Ninaishi RDCongo pa GOMA.

 2. My brother recommended I might like this web site. He was
  once totally right. This put up truly made my day.
  You cann’t believe simply how much time I had spent for this information!
  Thank you!

 3. hapo ni nafsi yako imehamishwa katika ulimwengu wa roho…..ni mchezo wa shetani huo…sababu anapoikamata nasfi nakuitumikisha ameshika akili ya mtu huyo utashi na hisia ivyo mara nyingi sana utakuta unaota upo mabondeni, jangwani, sehemu ambayo ni usiku daima, kwenye bahari, visiwani au sehemu ambayo inaelea angani….angalia na uwe makini uhusiano wako na mungu. kama ujaokoka chukua hatua…wakristo tunafananishwa na wanaisrael kwenye biblia katika safari ya kwenda kaanani kuishi nchi ya ahadi mara nyingi walipomkosea mungu walichukuliwa kwenda utumwani na leo hii mkristo unapomkosea mungu nafsi yako inachukuliwa na adui yetu ibilisi shetani kwenda kutumikishwa katika ulimwengu wa roho…zaburi 142:7..”Uitoe nafsi yangu kifungoni. Nipate kulishukuru jina lako. Wenye haki watanizunguka, Kwa kuwa Wewe unanikirimu”………..ayubu 33:28 “Yeye ameikomboa nafsi yangu isiende shimoni, Na uhai wangu utautazama mwanga………….zaburi 6:3 “Na nafsi yangu imefadhaika sana; Na Wewe, Bwana, hata lini? 4 Bwana urudi, uniopoe nafsi yangu, Uniokoe kwa ajili ya fadhili zako. 5 Maana mautini hapana kumbukumbu lako; Katika kuzimu ni nani atakayekushukuru?”……………………zaburi 7:1-5 “1 Bwana, Mungu wangu, nimekukimbilia Wewe, Uniokoe na wote wanaonifuatia, uniponye. 2 Asije akaipapura nafsi yangu kama simba, Akiivunja-vunja pasipokuwa na wa kuponya. 3 Bwana, Mungu wangu, ikiwa nimetenda haya, Ikiwa mna uovu mikononi mwangu, 4 Ikiwa nimemlipa mabaya Yeye aliyekaa kwangu salama; (Hasha! Nimemponya yeye Aliyekuwa mtesi wangu bila sababu;) 5 Basi adui na anifuatie, Na kuikamata nafsi yangu; Naam, aukanyage uzima wangu, Na kuulaza utukufu wangu mavumbini…………………………………………….kupitia mistari hiyo utapata picha kwamba wakristo wa leo kuchukuliwa utumwani kama ilivyokuwa kwa wanaisrael ni nafsi ya mtu inapoamishwa katika ulimwengu wa roho

 4. Ndg SO hakuna mstari ktk biblia unaoonyesha kuwa kuna ndoto anazoleta shetani ila iko mistari mingi inayoonyesha kuwa Mungu alinena na watu katika ndoto.
  La pili ndoto huwa hatukemei ila tunazipokea kwa shukrani mbele za Mungu kwa sababu Mungu anahitaji sana mioyo yenye shukrani. Maana Mungu hufunua siri za ulimwengu wa roho kwa wanadamu ili kuwatoa katika maangamizi, ndiyo maana ni vizuri kupokea kwa moyo wa shukrani.
  Kwa maneno mengine kukemea ndoto ni kumkemea aliyeleta ndoto ambaye ni Mungu na hapo ufahamu ukimkemea Mungu huwezi kuwa salama katika dunia hii.
  Tatu, unaposema ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi fikiri sana juu ya aliyetengeneza ufahamu wako, yeye ndiye anayetumia ufahamu wako ili kukufikishia ujumbe wake. Lakini inakuwaje unaota yale uliyosikia, kuyaona, kuyawaza, unayoyafanya nk? Hayo yote anayaleta ukilala ili kukuondolea kiburi. Katika Danieli mfalme Nebukadrezza aliota jinsi anavyojitukuza mbele za Mungu na Mungu akamjulisha katika ndoto, na alipokosa kusikia akamfukuzia porini akala majani kama ng’ombe. Hivyo ndoto haziji sababu ya kazi za mchana ila ni kitu halisi.
  Nne hatufungi na kuomba ili kusambaratisha kazi za adui ambazo Mungu amezifunua katika ndoto la!, ila umnyenyekee Mungu aliyeyafunua hayo. Na wala hatufungi na kuomba ili Mungu aseme na wewe kwa lugha nyepesi anaweza au asiweze kwa sababu lugha ya Mungu (ndoto) ni ya mafumbo huwa haongei kwa uwazi ni mara chache sana mfano nilisema mwanzo miti ni watu, mti ni Yesu, bahari ni uovu, kupanda mlima ni majaribu, kutembea kwenye utelezi na majaribu, mbwa ni roho ya uzinzi, ng’ombe ni matambiko, mbuzi ni mizimu nk. nk. Kwahiyo lugha yake si ya moja kwa moja si nyepesi. Pia je umesikia alichosema Mungu katika ndoto zako? Kama hutasikia alichosema matokeo yake yako katika vitabu vifuiatavyo, asomaye na afahamu. Kutoka 15:26 atatia maradhi…..; Kumbukumbu 28:15 – 69 laana kibao. Mwisho ndg SO tunaongea na wewe je UMEOKOKA? maana pasipo kuokoka haya tunayoongea ni kazi bure yanapeperushwa na upepo tu maana upepo una nguvu sana kuliko unavyodhani!! UBARIKIWE.

 5. Pole mama Mangesho, lakini kutembea sana katika madhehebu si ndio kwamba utasaidika la!, wala sio kuomba sana, au kufunga sana hata ukilia sana huwezi kujiosha mwenyewe. Mbona mtumishi Kakobe huwa anaomba sala ya maneno matatu na wagonjwa wanapokea uponyaji? Mungu katika Malaki 3:11 anasema “nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye”, anakula nini? mali zako na kwa nini? na baadaye atakula afya yako. Dawa yake, kama nilivyomshauri ndg SO, hayo matatizo yako anayeyaweza ni Ukimpata Nabii wa Bwana, yeye analo jibu la matatizo yako maana anasikilizwa na Bwana. Kwa kawaida manabii huwa wamejenga urafiki na Mungu, unateseka bure.

 6. Nashukuru kwa ushauri mwema.Lakini cha ajabu ndoto nyingine huwa zinakuwa kama zilivyo mfano nilipoota tunapikia ndan mama mwenye nyumba alianza kupikia ndan kama nilivoota,Ni mimi SO.

 7. jamani ninaomba msaada nateswa na kupoteza pesa vifaa vinaharibika kila mara natoa pesa nyingi kutengeneza lakini haviponi ndio kwanza vinaharibika zaidi nafanya kazi napata pesa lakini zinateketea. sinaamani kabisa. ninasali ninaamka kila siku saa nane kuvunja roho za kupoteza na kuibiwa lakini bado naendelea kuteseka nifanyeje mimi.

  magari nanne yamesimama, mashine za copy ofc, macomputer, sina hata redio nyumbani nisaidieni nimefunga nimechoka nalia usiku na mchana. huyu Yesu yuko kinywani kwangu kila wakati lakini bado nateswa nioneeni huruma nitalia mpaka lini?

  naomba ushauri kila j.mosi nafunga na kukesha ikiomba na kumlilia Mungu lakini wapi nimeomba staili zote nimetembea makanisa yote sipati jibu aomba ushauri

  sina mail nitumie ujumbe wa meseji kwenye 0778 877 877 tumia hiyo mail ni ya rafiki yangu

 8. ninatanguliza shukrani na ninawaombea mungu awatie nguvu ktk huduma yenu nzuri izidi kukua na kustawi…swali langu ambalo nahitaji kusaidiwa ni kwamba ndevu zangu zinapoota kuna baadhi ya sehemu ni kama kumenyolewa sasa ninashangaa nikinyoa zinaota lakina hali hiyo inajirudia na wakati hapo nyuma haikuwa hivi wala sio kawaida kabisa…ninawaomba mniombee pia naomba kujua ni kwanini

 9. Ndugu SO mimi sijui ila ninakupa pole kwani zinasumbua ndoto za namna hiyo. Mimi ninakushauri ufunge na kuomba Bwana Yesu Aweke wazi kwako maana ya ndoto hizo. Zinafanana na zinaelekea kuwa na ujumbe mmoja tena unaokuhusu. 1Yohana3:8 Bwana Mungu Akuepushe na kinachoonyeshwa katika ndoto hizo katika Jina la Yesu. Amen

 10. Fanya maombi ya kushindana kwamda wa wiki utapata maana ya ndoto za kako. kama hauna nijulishe nikutumie. nicheck kwenye fb by the same name

 11. Ndugu yangu, kuna ndoto za shetani, za Mungu na pia ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi pia kulingana na maelezo uliyotoa ndoto hizo zinaashiria kuna mambo mabaya yanaweza kukupata hivyo ulipaswa kuamka saa hiyo hiyo kukemea bila kupoteza muda kwani kila jambo linapotokea hapa duniani ujue limeanzia ktk ulimwengu wa roho usipuuze ingia ktk maombi ya kufunga na kuomba ili usambaratishe kazi za shetani. Ubarikiwe.

 12. Ndugu SO kwanza hongera sana kwakuwa Mungu anakupenda anaposema na wewe katika ndoto maana yawezekana anakukemea, anakuonya nk (Ufunuo 3:19). Kabla ya kuomba msaada wowote unatakiwa ujue ndoto ni nini na zinatoka wapi na nani anaweza kufasiri ndoto.
  Kwanza ndoto ni lugha ya kinabii, ni ya Mungu mwenyewe katika kuzungumza na wanadamu. (Soma Ayubu 33:14 – 20). Kwasababu Mungu hana mwili huwezi kumuona na hata Kama ungemuona biblia inasema mwanadamu hatamwona Mungu akaishi na hakuna aliyewahi kumuona Mungu wakati wowote.
  Ukisoma katika kitabu cha Hesabu 12:6 anasema Yeye husema na manabii wake katika maono na katika ndoto. Ndoto kila mtu anaota awe mpagani anamjua Mungu au hamjui analewa au la Mungu anasema naye kwa sababu Yeye ni Mungu wa wote wenye mwili. Kama lugha hiyo ni lugha ya kinabii maana yake Mungu hutia roho ya unabii kwa mtu ili atabiri kupitia ndoto anazoota juu ya yale ambayo Mungu anataka kumjuza mtu.
  Anachosema Mungu katika Ayubu 33 ni kwamba Mungu hunena na mtu katika ndoto ingawa mtu atasema “si ndoto tu” yaani Mungu anaona umepuuza hujali. Biblia ya kiingereza inasema “For God speaketh once, yea twice, [yet man] perceiveth it not. {33:15} In a dream, in a vision of the night, when deep sleep falleth upon men, in slumberings upon the bed; {33:16} Then he openeth the ears of men, and sealeth their instruction” yaani mtu hatii ufahamu. Kwahiyo ndoto ni lugha mahsusi na rahisi ya Mungu kumfikia mwanadamu kwakuwa kama akinena kwa sauti ni rahisi Mwanadamu kusema huyo ni pepo anayesema naye na hapo atakuwa amemkufuru Mungu dhambi isiyosamehewa.
  Kwahiyo basi ujue ndoto zote zinatoka kwa Mungu bila kujali kama ni mbaya ( unaua, unazini, unatukana nk.) au nzuri; huyo ni Mungu anasema na wewe. Unachotakiwa ni kutia ufahamu (to perceive) hivi Mungu ananitaka nifanye nini katika hili analosema na mimi?
  Nimeongea ndoto ni nini (asikudanganye mtu akikuambia zinatokana na shughuli nyingi za mchana), nani anazileta, maana yake hakuna ndoto ya shetani wala ya kwako mwenyewe maana hujawahi kujiumba. Kwahiyo iko nguvu iliyo nje ya fahamu zako inayoleta ndoto zako.
  Nani anaweza kufasiri ndoto yako? Kwanza ufahamu ndoto ni lugha ya mafumbo anayotumia Mungu maana Mungu si mtu, au mtu rahisi kama wengi wanavyomdhania. Mkumbuke Yule jamaa aliyepewa talanta moja, wakati wa kutoa hesabu alisema hivi! “Nalijua ya kuwa wewe U Mtu mgumu sana, wavuna usipopanda, wakusanya usipotawanya, hivyo nikaogopa nikafukia talanta uliyonipa hii hapa ichukue!” Huyo ndiye Mungu, hivyo hawezi kijirahisisha kwa wanadamu, hata Rais ambaye ni mwanadamu hajirahisishi, si zaidi sana Mungu?
  Ukisoma katika Biblia utaona kwamba ni watu wachache sana waliofanya kazi ya kutafsiri ndoto. Mf. Daniel 1:17 huyo Danieli alikuwa na ujuzi katika maono na ndoto na si wenzie. Danieli 2:26-28 Soma mlango wote wa pili ili kupata picha nzuri. Anasema sio wachawi, wanajimu au waganga wanaoweza kutafsiri ile ndoto ila wababeli walipata akili wakampigia kura wakasema Danieli 2:11 wale wenye vikao na miungu isiyokaa na wanadamu ndio wanaweza kufasiri ndoto. Mizimu inakaa na wanadamu kwahiyo siyo!! Mwanzo 40:1-23 Yusufu alitafsiri ndoto za wafungwa wenzie wengine na Mwanzo 41:1,7, 14-40 wote walishindwa soma kwa makini mstari wa 38 na 39 utaelewa. 1Samweli 9:15-20 Samweli alikuwa mwonaji wa Israeli yaani mfasiri wa ndoto na mafunuo. Kwahiyo basi kwa leo si wanaojua na kukariri sana neno wanaoweza kufasiri ndoto, wala wajuzi, wala waombaji sana wala wenye ujuzi mwingi wa kunena ila Ayubu anasema IKO ROHO NDANI YA MWANADAMU AMBAYO INANENA ili kumjulisha mtu yampasayo. Ushauri wangu kwako tafuta nabii aliyepewa karama ya kufasili ndoto ili akuongoze yakupasayo kufanya juu ya hayo aliyoongea Mungu na wewe. Kumbuka hayo maongezi yako na Mungu ni siri yenu wewe na Mungu ndiyo maana ameongea kwa mafumbo ili hatimaye ukimpata mfasiri awe amekupa hekima. Mf ukiota umeona miti maana yake umeona watu wa dunia hii ila ukifukuzwa na hatari ukapanda juu ya mti au ukakimbilia chini yake ujue umekimbilia kwa yeye mti wa uzima (Yesu). Sio kwamba ndio ninaweza kufasiri ndoto la hasha ila ninakupa changamoto ya mafumbo ya Mungu wetu aliye hai . Ubarikiwe sana SO.

 13. Kama kuna kuibiwa NAFSI,basi matunda 9 nafsi yako imeibiwa na kufungiwa kuzimu. Tazama hata jina umebadilishiwa.uko mtupo hata kwa mashauri unayoyatoa.

  Ndg mleta hoja nakushauri mpe Yesu Kristo maisha yako ayatawale,Acha uovu
  Angalia neno la ufunuo …..

  “Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake; ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi, Kol 1:13-14

 14. Pole kwa ndoto hizo. Binfsi nina amini zina maana kubwa sana. Unahitaji kusimama kiroho. Yaonyesha unajishirikisha na mambo yasiompendeza mungu tena Inaonyesha unachofanya ni kutokukataa. Ni kama unaonyeshwa ubaya wa ufanyacho ili ubadili tabia. Njia utakayoweza kufanya Mara uzindukapo kwenye ndoto, usingoje sana amka na uombe na kukemea wakati huo huo. Maana ya jambo hilo litadhihirika katika macho ya mwili siku hiyo na utapata kuwa huru.kwani wakati mwingine ukiwa kwenye ndoto unashindwa kukemea.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s