Msiogope vitisho vya wanatheolojia!!

theologists

Shalom.
Napenda kuwatia moyo wenye nia ya kutaka kujifunza ili kufikilia utimilifu kuwa wasiogepe vitisho vyovyote vinavyotolewa na WANATHEOLOJIA Bali wajisikie vizuri kuuliza maswali yanayojenga. Theolojia haikuanzishwa na Bwana Yesu bali ni mpango wa mwanadamu wa kuwatawala binadamu wenzake.Ndio maana hakuna Mtume hata MMOJA alikwenda kusoma theolojia baada ya Kuitwa na Bwana Yesu.

Mafarisayo,Masadukayo na Waandishi leo ni Wanatheolojia. Kazi kubwa waliyonayo hawa wanatheolojia ni KUWATISHA watu na KULIFANYA NENO LA MUNGU LISEME KILE WANACHOTAKA WAO.Soma MARKO 7:1-15. Theolojia ni MAPOKEO YA WANADAMU TU (MARKO 7:8…”Ninyi mwaicha amri ya Mungu,na kuyashika mapokeo ya wanadamu.” Bwana Yesu hakuwahi kuogopa kitisho chochote hata Herode alipomtishia ( LUKA 13 :31-32) Mitume wenyewe walifuata nyayo za Bwana Yesu za kutomuogopa mtu yeyote,wao walimuogopa Mungu tu ( MATENDO 4:1-22, 5:17-33) Siku zote hata ukitafuta Andiko la Kutendea uovu utapata na utapewa kulingana na haja ya Moyo wako. Na hii ni Kibiblia kabisa kwa sababu ‘Waisraeli waliambiwa wawape wake zao talaka kutokana na ugumu wa mioyo yao’ Ukitafuta Andiko la kukuhalalishia mungu mwenye nafsi tatu utalipata tena, utayapata Maandiko mengi na utaona uko sahihi kabisa hutahitaji kumsikiliza yeyote.

Kumbuka mpendwa;
1.Kama Mungu amekunyima ufunuo wa Neno lake hata ujitahidi vipi hutafanikiwa kamwe (MARKO 4;10-12, LUKA 10 :21-24)
2.Neno la Mungu halifasiriwi apendavyo mtu ( 2PETRO 1:20)
3.Kuna injili ya namna nyingine inayohubiriwa hapa Duniani (WAGALATIA 1:6-7)
4.Uwe mwangalifu (WAGALATIA 1:8-9)

KUANDIKWA NA KUTAFSIRIWA KWA BIBLIA.
-Bila shaka Wakristo wa kweli wanajua kuwa BIBLIA iliandikwa na watu Walioongozwa na ROHO MTAKATIFU, kwa maneno mengine Mwandishi wa BIBLIA ni ROHO MTAKATIFU.
-Waliotafsiri BIBLIA wapo katika makundi mawili;
(A) Kundi la kwanza ni la wale waliotafsiri BIBLIA wakioongozwa na ROHO MTAKATIFU
(B) Kundi la Pili ni la wale waliotafsiri BIBLIA wakiongozwa na roho wa Ibilisi

Ndio maana wamebadili maana ya asili ya maneno ili kukidhi haja za mioyo yao kama vile Mafundisho ya nafsi tatu za Mungu. Najua kusema hivi kwa mwanatheolojia ni ‘kukufuru’ kukuu sana.Ubarikwe ndugu Lwembe kwa kuwasaidia Wasomi kuwa Biblia Ya Kwanza ni ya Kiebrania na wala si ya Kiyunani. Lugha ya Kiswahili imechukua tafsiri ya BIBLIA kutoka Lugha ya Kiingereza, Wakristo wa kweli daima watapinga mafundisho ya Baraza la Nikea (Mafundiso ya mashetani) WAKRISTO WA KWELI hawakosoi BIBLIA bali pia HAWATAKUBALI KUPOTOSHWA KWA NENO LA MUNGU kwa kuingizwa kwa tafsiri za Mafundisho ya mashetani (1TIMOTHEO 4:1-6). MUNGU alitupa mamlaka ya kujaribu roho zote ili tusilishwe au kunyweshwa sumu ( Kitu ambacho si Neno la Mungu),soma 1YOHANA 4:1-3

Kwa kuwa niIilionekana kana kwamba napendelea BIBLIA YA “HOLY BIBLE-KING JAMES VERSION” kurekebisha tafsiri ya Biblia ya Kiswahili.Nitatumia tafsiri zingine ili mwongo aonekane.
Kuna tofauti kubwa kati ya neno “unity”-umoja na “one” mmoja kama ilivyotumika katika Biblia ya Kiingereza (one) na Biblia ya Kiswahili ikatafsiri ‘umoja’ Bila shaka neno ‘umoja’ na neno ‘mmoja’ ni maneno mawli tofati kabisa kimaana.

THE HOLY BIBLE-NEW INTERNATIONAL VERSION ( JOHN 17:22 ” I have given them the glory that you gave me,that they may be one as we are one”Je,neno ‘umoja’ linapatikana katika mstari huu? Kama shida ni lugha ya Kiingereza hilo ni tatizo la mtu binafsi. Hata sentensi hii kwa Kiswahilili si sahihi 1Yohana 5:8 ‘….na watatu hawa ni umoja’.1 YOHANA 5:8 inasomeka hivi Kwa Kiingereza ;

THE NEW TESTAMENT…WITH PSALM AND PROVERBS (THE GIDEONS INTERNATIONAL) … 1JOHN 5:7 “For there are three who bear witness in heaven:the Father, the Word, and the Holy Spirit; and these three are one” Je,neno ‘umoja’ linapatikana katika mstari huu? Tafakari tena mwisho wa huu mstari……”and these three are one”

Roho wa Mungu mwenye nafsi tatu akikukolea hutaamini Ufunuo Halisi wa ROHO MTAKATIFU mpaka BWANA YESU akuondolee hiyo roho. KARIBIA KILA KILA DHEHEBU LEO LINA BIBLIA YAKE TOFAUTI NA LINGINE.WENGINE WANA TAFSIRI TOFAUTI TOFAUTI YA BIBLIA YENYE VITABU 66 NA WENGINE WANA BIBLIA YENYE VITABU 77 !!! SWALI;KWANINI KILA DHEHEBU LINATAFSIRI BIBLIA KIVYAKE?
****INATEGEMEA NI JICHO GANI UNALOTUMIA KUSOMA BIBLIA****
Amina.

–Pendeli Simion

Advertisements

101 thoughts on “Msiogope vitisho vya wanatheolojia!!

 1. Afadhali Ziragora umeiona hiyo.

  Watu wanavimba kupinga vitu ambavyo havipo, ila vinawaogopesha kwa sababu tu ya ujinga wao wenyewe.

 2. Pendael,

  Ukipendelea confusion hutaewa chochote. Theolojia siyo injili. Ni shule tu.

 3. Tumaini Nelson,
  THEOLOJIA NI INJILI CHOTARA ( Hybrid Gospel)
  KILA DHEHEBU LINA CHUO CHAKE CHA BIBLIA,HEBU TUAMBIE DHEHEBU MOJA LINALOFUNDISHA THEOLOJIA YA KWELI.
  INJILI YA THEOLOJIA NI INJILI YA USHUNGI WA JOGOO. INJILI YA THEOLOJIA HAIJARUTUBISHWA HIVYO HAINA UHAI,NDIO MAANA WANAOSIKILIZA HUFA KIROHO WAKINGOJEA KUFA KIMWILI.MIMI SITISHIWI NA WANATHEOLOJIA NA MAFUNDISHO YA DHEHEBU LOLOTE.MADHEHEBU NDIO WALIOANZISHA VYUO VYA THEOLOJIA LEO HII WAMEONGEZA VITIVO MBALIMBALI KWA AJILI YA MATUMBO YAO. UDHEHEBU KWA MUNGU NI UKAHABA (UFUNUO 17:3-5). Majina ya MADHEHEBU ni Majina ya MAKUFURU.Madhebu ndio chimbuko la Mafundisho potofu.

 4. Sungura,

  Toka mwanzo, niligundua mapema sana kwamba HUIJUI maana ya Theology, na pia HAUKO tayari kujifunza!!! Kauli yako hii inalithibitisha jambo hilo kwa uwazi kabisa:
  “”Kwanza nimesema karibu mara mbili kuwa wanatheolojia huwa hawa- interpret maandiko bali hu-translate maandiko. Lakini nashangaa bado unanilazimisha kuwa nilisema huwa wana-interpret maandiko. Huo ni uzembe wa kufuatilia mambo Lwembe.””

  Unajua kuna wakati katika mada ya “Kiingilio kwenye semina” nilikushangaa sana pale ulipolazimisha kwamba kimsamiati, neno “Kiingilio” lina maana sawa na neno “Changizo”! Nakuona hata hapa ndicho unachojaribu kukifanya, kuwatia “ujinga wapendwa wengi tu, na unafanikiwa! Kimsingi HASARA ni yenu, maana mwisho wa siku Mungu alisema anakupa roho ya kuuamini uongo wako, na ndio ninachokiona!!!

  Unapokazana kuniambia kuwa “” wanatheolojia huwa hawa- interpret maandiko bali hu-translate maandiko”, hii inaonesha kuwa hata maana ya maneno hayo mawili huijui pia. Nimekuonesha maana halisi ya neno Theology, kwamba ni scientific, involving the STUDY of the NATURE of God and religious beliefs ambazo zinatengeneza Theories kuhusu Mungu, hizo zinazokuwa SYSTEMATICALLY DEVELOPED na kuishia kukupa kitu kamili kama UTATU MTAKATIFU wa Mungu, hii ndio Theologia kaka!!! UTATU si Translation bali ni Interpretation, ndio maana hakuna rejea za kiMaandiko za jambo hilo, jaribu kuwa makini, nenda polepole, hauoni kwamba huyo ni mungu aliyetengenezwa na wanatheolojia huko maabara?!

  Huyu ni mungu wa maabara ambaye umeambiwa huna uwezo wa kumfahamu, kwahiyo uchunguzi wetu huishia hapo kwa kuogopa kumkufuru, hence producing a mixture of fear and frustration which climax in deep ignorance abt the very god! Thats the spirit of bondage. Just as the fears which hide in our subconscious are psychiatric, so is the spirit of bondage!

  Neno la Mungu halieleweki kwa Teolojia, wala hakuna teolojia inayoweza kumjengea mtu imani.Teolojia huzalisha “Students” lakini Neno la Mungu huzalisha “disciples”, ndio hao kondoo!

  Unaposoma “Mafarisayo”, hawa walikuwa ni watu wa dini, wasomi wazuri wa theolojia yao, hiyo iliyowapa kuyafasiri Maandiko, ndio maana Kristo alikuwa akipambana nao kila wakati. Kayafa alikuwa ni msomi hata akawa kuhani mkuu, kuhusu dhambi ya matendo ya mwili, usingeweza kumshtaki kwa lolote lile maana alikuwa safi kulingana na Torati; bali alikuwa na ufahamu mdogo sana kuhusu Mungu chini hata ya yule mwanamke wa Kisamaria aliye kutana na Kristo pale kisimani; huyu anatupandoo ya maji na kutimua mbia kwa furaha, na huyu analirarua joho lake la ukuhani, kinyume na maelekezo ya Mungu, na akaishia kumsulubisha Mungu huyo huyo anayedhania anamwabudu!

  Kuhusu Oral Roberts, ndio ninamfahamu, a great Pentecostal theological preacher! Ukiniambia ametembea na Mungu, hilo ni sawa, bali ktk kiwango kipi? Jaribu kulipima hili, kwamba alikuwa na Neno lisilo kamili, kwahiyo kimsingi kwa Injili aliyoihubiri ameyazuia makundi ya Kipentekoste hapo alipoyatoa Sodoma, kama ilivyokuwa kwa Lutu, hakuvuka aende kwa nduguye Ibrahimu bali akaenda huko pembeni alikoishia ktk aibu, kama ambavyo Upentekoste unavyoingia ktk aibu leo hii ya kumkubali kila anayenena kwa lugha, kwamba amejazwa RM!! Alishindwa kukivuka kikwazo cha Thelojia akajikwaa. Yeye alilisimamia fundisho la “Kunena kwa lugha ni Ishara ya Kujazwa RM” akiongozwa na Theolojia, huku akijua fika kwamba hilo si Neno la Mungu! Kazi zetu zinapimwa kwa Neno na si kwa kuheshimiana kwetu!

  Ni sawa na wewe, kwa ignorance, unang’ang’aniza theology ituongoze, kwamba ktk Biblia kuna maneno ya Mungu, watu na ya shetani, hii inaonesha ni kwa kiwango gani hujui hata Biblia ni nini, zaidi ya uongo uliokaririshwa, Mungu hulilinda Neno lake, na hajawahi kumwachia mwanatheolojia yeyote yule kazi hiyo. Elimu ya kumpambanua Mungu haiwezi kumbadili RM, hapa ndipo walipojikabidhi ktk mikono ya uharibifu!

  Tazama unavyoshindwa kuelewa, umedanganywa kwamba Paul kwa kusema kwamba “hapa ni mimi na si Bwana” basi hayo ni maneno yake, hilo ndilo jiwe la kujikwaa mlilowekewa, maana mwisho wa siku mnabaki weupe, kama mlivyo, mnajivuruga ovyo; “All Scripture is given by Inspiration” mpaka hayo mnayojidhanisha kwamba ni maneno ya Paul; anasema “Nifuateni mimi…”, je, hili ni neno dogo???

  Watazame Wasabato, wanaonekana ni wajuzi wa Maandiko, lakini wakaishia ktk aibu, wakiisha kumpokea yule roho wa Mpinga Kristo, yule ktk Ufu 6:2, wakidhania ni Kristo, akawatengenezea Teolojia iliyowaongoza kutengeneza mbawa ili waruke wakamlaki Kristo hewani!! Liliposhindikana jambo hilo, yule roho wa dini akawaletea fix nyingine, kwamba eti kumbe Kristo alikuwa haji bali aliingia “patakatifu” kwa kazi maalum ya kutuombea! Unawaona, walijaribu kuyafungua Maandiko yaliyofungwa na Mungu wakaishia aibuni! Neno la Mungu hufikiwa kwa UFUNUO tu, vinginevyo tutaishia ktk Ibada pori za akili kama ya Kaini isiyo na Ufunuo!!!

  Kumbuka HAKUNA anayeweza kumsaidia Mungu ktk lolote lile, tena fahamu kwamba, Mungu ni Neno lake; hivyo kutembea na Mungu ni kuongozwa kwa Neno lake na si Teolojia!!!

  Gbu!

 5. Hahahahaha……!, Christina,
  Theolojia kipeo chake ni kukuvisha majani ya miti, kisha inakusimamisha kwenye balcony uwasalimie mashabiki wako wanaokuchungulia tokea huko chini!!

 6. Mama Ck kama una nguvu ya Mungu ndani yako sidhani mambo haya ni complex kiasi cha kusema hila za shetani zinahitaji nguvu za ziada kuzishinda!unless othrwise uwe unatembea peke yako!Neno la Mungu linapokuwa kwa wingi ndani yako huwa ni silaha tosha ya kumtambua adui na kumshinda kirahisi.Na pia Roho wa Mungu aliye ndani yako ni rahisi kugundua roho nyingine.1Yohana 4:6.Kwahiyo sidhani kuna haja ya kutishana sana bali kuna haya ya watu walijue Neno na hiyo ndiyo itakuwa dira ya mwamini.Barikiwa

 7. Pendaeli naomba ufahamu kuwa sipo kishabiki bali nachoangalia ni ile kweli inayozungumzwa huku dira yetu ikiwa ni neno la Mungu.Pendaeli Mimi nadhani wewe ndiyo unayejichanganya kwa kuipinga moja kwa moja theologia kwa kutahadharisha kuwa ni kitu kibaya wakati si kweli!mwanatheologia wa kweli aliye na Roho Mtakifu atatenda sawasawa na maelekezo ya mwalimu wa kweli Roho Mtakatifu.Yohana 14:26.Lakini sambamba na hilo tuliye ndani ya kristo mambo ya siri za Mungu hayatupigi chenga maana Roho Mtakatifu aliyendani yetu huyachunguza mafumbo yote huwa ni rahisi kuitambua kweli yote 1kornto 2:10-16.Lakini Pendaeli Yesu hakusema manabii wote ni wa uongo bali alisema utawatambua kwa matunda yao Matayo 7:15-23.Vivyo hivyo wanatheologia feki tutawatambua kwa matunda yao!Pendael niseme Mambo ya ufalme wa Mungu ni rahisi sana kuyatambua unapokuwa na nguvu ya Mungu ndani yako!alichozungumza ndugu yangu Sungura hakina shaka maana kipo wazi na ameeleza pande zote!lakini wewe umeng’ang’ania upande mmoja wa ubaya na kukataaa.

 8. Pendael,

  Hapo juu kuna kitu umesema, kwamba ” we are not asked to prove it but we are asked to believe it”

  Ukasema kuwa hatutakiwi kuthibitisha kitu bali kuamini tu!
  Huu ni uongo, na unatokana na kutojua maana ya imani.

  It’s just the opposite Pendael!

  Huwezi kuamini kitu ambacho hujakithibitisha.

  Look here:

  Kusikia ndiko huzaa imani, na ili huko kusikia kuzae imani lazima ukielewe ulichokisikia, huwezi kuamini tu hewani.

  Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo(note neno Hakika)

  Huwezi kutarajia bila kuwa na hakika(uthibitisho) ya kuwepo kwa unachokitarajia.
  Kinatakiwa kiwe kimethibitishwa kwanza kwamba kipo ndipo ukitarajie. Tunatarajia kuwa Yesu atarudi coz we are sure(uthibitisho) that he is there, and coz he first said( proved) that he is coming back,

  Ni bayana ya mambo yasiyoonekana(note neno Bayana)

  Bayana is a proof( uthibitisho) ya kitu kisichoonekana kwa macho ya nyama lakini kipo.

  Isingewezekana hicho kitu kikawa bayana(halisi, dhahiri) kama hakipo.

  Maana yake ni hii:

  Neno HAKIKA na BAYANA yanaongelea ulimwengu wa roho, na neno YATARAJIWAYO na YASIYOONEKANA yanaongelea ulimwengu wa mwili.

  Kitu kinachounganisha hizo limwengu mbili kinaitwa IMANI.

  Kwa hiyo ili uamini lazima unachokitarajia uwe umekithibitisha katika ulimwengu wa roho. Yaani uwe umehakikisha kwamba kipo. Maana katika ulimwengu wa roho kila kitu ni halisi/dhahiri.

  Kwamba uwe umekibayanisha (uwe umekithibitisha) ktk ulimwengu wa roho. Yaani katika ukimwengu wa roho unacho tayari.
  Lakini ktika ulimwengu wa mwili utakuwa unakitarajia, yaani hujakiona kwa macho ya nyama.

  “Amin amin nawaambia, mambo myaombayo mkiwa ktk kusali aminini ya kwamba MMEYAPOKEA nayo YATAKUWA ya kwenu- Mark 11:24”

  Kuna nyakati mbili tofauti hapo:
  MMEYAPOKEA hiyo ni katika ulimwengu wa roho!
  YATAKUWA ya kwenu, hiyo ni katika ulimwengu wa mwil

  Vinginevyo ingesema, mmeyapokea nayo Yamekuwa ya kwenu.

  Kwa hiyo ni lazima uthibitishe kwanza ndipo uamini. Huwezi amini kitu ambacho hujathibitisha kuwa kipo.

  Kwa hiyo anayeaminiwa hapa siyo kile kitu kitarajiwacho, bali ni yule aliyeahidi, yaani Mungu!

 9. MICHANGO YANGU IKO WAZI SANA!!!

  Tunachotakiwa ni kumruhusu Roho Mtakatifu kuitafakari kwa sababu
  kimsingi yeye ndiye anayeandika kwa kunitumia mimi.Leo nitarudia
  kwa kuweka wazi vipengele vichache kwa faida yetu sote

  Kwanza kabisa hakuna comment yangu inayopingana na THEOLOJIA
  Kama ambavyo Tumaini anasema Mungu ana njia nyingi za kutufundisha.Mimi siku zote nimetaka sana Tuyajue MAPUNGUFU
  ya THEOLOJIA na siyo kujua tu maana yake na faida zake.Katika nyakati hizi za hatari tunatakiwa kuangalia UNDANI wa mambo kwa
  muongozo wa Roho Mtakatifu.

  Makala ninazoongozwa kuandika zimekaa KIMAFUNDISHO ZAIDI na
  kama anavyosema Tumaini ni mafundisho yenye MAFUNUO YA
  ROHO MTAKATIFU na mara nyingi yanaambatana na UNABII.Sikiliza
  hii kwa makini.Yesu alipokuja alikutana na wanatheolojia wa madhehebu na siyo kanisa.Alikutana na wanatheolojia wa mikusanyiko
  ya watu wanaoongozwa na MAPOKEO NA TARATIBU ZAO,hawa ndiyo
  Mararisayo na masadukayo(dini zilizokufa).Bibilia inaeleza wazi kwamba
  kuna dini zilizo hai na dini zilizo kufa.Neno Dini kwa bahati mbaya
  limeunganishwa sana na suala la madhehebu.Ni lazima tuijue tofauti
  kati ya kanisa na dhehebu.Kanisa ni mwili wa kristo yaani mikusanyiko
  ya watu ambao wamezaliwa mara ya pili na wanaoongozwa na
  Roho Mtakatifu na siyo mapokeo na taratibu za kibinadamu walizojiwekea.Soma Mathayo 15:7-9 uone kile ambacho Yesu anasema
  kuhusu madhehebu.Yesu ALITAKA KUHAKIKISHA KWAMBA KAMA
  MAKANISA YANAITRODUCE THEOLOJIA BASI IFUNDISHWE KWA
  MUONGOZO WA ROHO MTAKATIFU na hili linawezekana kabisa
  japo shetani na wajumbe wake wamevuruga huu mpango kwa
  kiasi kikubwa.Manabii wa uongo wameanzisha vyuo vingi vya theolojia
  na wanajipenyeza sana ndani ya vyuo vya theolojia vilivyoanzishwa
  na wateule!!Wengi hujipenyeza kama waalimu na wafadhili
  Matokeo yake kumekuwa na mafundisho mengi yaliyo kufa
  na hii ni zaidi ya hatari.Ndiyo maana ndani ya mikusanyiko ya
  watu waliookoka NAKO KUNA MAPOKEO YAO!!!

  Mungu halazimiki kumpitisha kila mteule wake katika vyuo vya theolojia.Lakini pia wengine ni lazima awapitishe huko.Mtumishi
  kama mwalimu Mwakasege hajapitishwa katika mfumo huu wa
  kusoma theolojia lakini namna ambavyo Roho wa Mungu anamuongoza
  kufundisha Neno la Mungu ni ya ajabu na kutisha mno!Wale wanaofuatilia mafundisho yake na hata wapinzani wake wanakiri
  kwamba anafundisha MAFANUO YA ELIMU YA NENO LA MUNGU
  na siyo tu elimu ya neno la Mungu kama ilivyo katika vyuo
  vingi vya theolojia!Binafsi wanafahamu waalimu wachache walio katika
  vyuo vya theolojia vinavyomilikiwa na wateule wa Mungu,na waalimu
  hawa wanajitahidi sana kufuata mafundisho ya Roho Mtakatifu
  katika mitaala yao.Changamoto kubwa ya vyuo vingi vya theolojia
  havina watu ambao wana huduma ya ualimu bali wengi wanaofundisha
  wana karama ya ualimu na zaidi sana ni waanjilisti!!!Kanisa la Kristo
  halijawahi kupungukiwa zile huduma tano na wateule wenye huduma
  ya ualimu kama Mwakasege wako wengi isipokuwa HAWAJITAMBUI
  KIROHO kwa sababu wachungaji wengi hawako katika mkao wa kulea
  hizi huduma.Manabii wengi wa uongo wameonekana kama dhahabu
  safi za kukimbiliwa kwa sababu TUMESHINDWA KUWALEA NA KUWAPA
  NAFASI MANABII WA UKWELI WALIO NDANI YA MIKUSANYIKO YETU.
  Manabii wa uongo wameyatumia sana mapungufu tuliyo nayo ili
  kutugawa na kutuangamiza.CHACHU kidogo katika mafundisho potofu
  ya neno la Mungu imechachua donge zima!!

  CK LWEMBE na PANDAELI wanachokifanya ni kuweka wazi MAPUNGUFU YA THEOLOJIA, ndicho ambacho Roho Mtakatifu
  ananionyesha.Mtumishi STEVE SUNGURA anajaribu kuweka wazi
  maana ya theolojia na kazi zinazofanywa na wanatheolojia wanaoongozwa na Roho Mtakatifu.Wote hawa kila mmoja anafanya
  vizuri katika kile anachokieleza lakini kinacho wafanya wapishane
  ni kule kila mmoja kutomuelewa mwenzake.Wakati fulani nilipoona
  mvutano umekuwa na muelekeo wenye sura mbaya,mtumishi CK
  LWEMBE akaniambia kuwa “Wote ni watu wazuri na wanampenda
  Yesu” kwahiyo nisishangazwe sana na kile ninachokiona.Kazi yangu
  mimi ambaye Yesu ananitumia kama chombo tu, ni KUTAKA
  WATEULE TUYATAZAME MAPUNGUFU YA THEOLOJIA KWA NIA
  YA KUUJENGA MWILI WA KRISTO.Nilikuwa nafuatilia undani wa theolojia katika mtandao mmoja nikakuta wataalamu wengi walio
  ndani ya kanisa na kwenye madhehebu WANAKIRI KWAMBA
  THEOLOJIA inafundishwa na wanadamu zaidi kuliko kufundishwa
  na Roho Mtakatifu.Watu kama mtume Paulo wangekuwa wanafundisha
  katika vyuo vya theolojia wangetufaa sana.Kwa sababu WANGETUTOFAUTISHIA KATI YA MAFUNDISHO YAO BINAFSI NA YALE
  YA ROHO MTAKATIFU.Hapa naomba niseme jambo kwa uwazi sana.
  Hakuna Maandiko ndani ya Biblia ambayo HAYAJAHAKIKISHWA
  NA KUHIDHINISHWA NA MUNGU.Paulo anasema hivi ” Lakini watu wengine NAWAAMBIA MIMI, WALA SI BWANA, ya kwamba iwapo ndugu
  mmoja ana mke asiyeamini na mke huyo anakubali kukaa naye ASIMWACHE”-1 WAKORINTHO 7:12.Hapa Paulo alijiondoa kwenye unafiki
  wa kunena au kufundisha na kusema ameongozwa na Mungu hata hivyo Mungu alihakikisha ili fundisho linatufikia kwa kurekodiwa ndani
  ya Biblia kwa sababu pamoja na kwamba yalikuwa ni matamanio
  au mapenzi ya Paulo lakini lilikuwa ndani ya moyo wa Mungu.Wakati
  mwingine mawazo yetu yanaweza kuwa ndani ya ratiba ya Mungu.
  Roho Mtakatifu asingeruhusu Paulo awaeleze wateule mambo
  yaliyo kufa ambayo yangewaangamiza.Tunahitaji hekima na mafunuo
  ya Roho wa Kristo kuielewa Biblia.

  Maaskari wa Yesu wanafuatilia kwa karibu kila kinachoendelea
  ndani ya hii Blog ili kutafuta namna iliyo hai ya kuujenga mwili
  wa KRISTO.

  UNABII KWA WATEULE WOTE WANAOJITAMBUA NA WALE WANAO
  WEKA BIDII KATIKA KUUTAFUTA UNYENYEKEVU WA YESU.

  Wapotoshaji japo wamejipanga lakini Yesu alishawatangulia ndiyo
  maana MUNGU anasema katika Yeremia 20:11 “……..Kwa sababu
  HAWAKUTENDA KWA AKILI,wataona aibu ya milele, ambayo
  haitasahaulika kamwe” .Wanaofundisha Maarifa ya Yesu kama
  nabii na mwalimu Mwakasege ni mashujaa wenye kutisha mno.
  Yesu anasema upotoshaji utaendelea kufichuliwa na kuwekwa
  wazi ili wateule wasiendelee KUANGAMIZWA(LUKA 12:2).

  2TIMOTHEO 3:9 Inaeleza wazi kwamba wajumbe wa shetani
  “……hawataendelea sana, maana UPUMBAVU wao utakuwa
  DHAHIRI kwa watu wote……..”

 10. Hahahaaaa, uwiiiii!

  Pendael unamwambia Tumain kuwa mchango wake hauna hata nukuu ya biblia! Kweli nimecheka!

  Sikia, umekariri maandiko pasipo kuwa na maarifa ya kilichosemwa kwenye hayo maandiko .

  Una bidii nyingi ta kukarii maandiko lakini u mjinga vya kutosha tu juu ya kile kilichosemwa kwenye hayo maandiko.
  Sasa wewe ndo umefanana kabisa na wanatheolojia ambao wamejaa mistari ya biblia lakini nuru ya hiyo mistari haimo ndani yao, hujijui tu!

  Hauna tofauti na yule kijana aliyemuuliza Yesu kuwa afanyeje ilo kurithi ufalme wa Mungu, akaambiwahabari ya kujua torati imesemaje,akajibu kuwa hayo anayajua tangu utoto wake. Lakini cha ajabu yalikuwa hayajamsaidia, maana alikuwa amyakariri tu kichwani bila kuyafanya yawe nuru kwake.

  Shetani hatishwi na wingi wa mistari kichwani mwako. Anatishwa na mstari mmoja tu unaoujua umemaanisha nini!

  Kujua kwako mistari ambayo unanukuu kumekusadia nini sasa, mbona bado u kipofu mkubwa tu wa kujua siri ya Kristo!!

  Hata hapo juu umenukuu mistari ya kitabu cha Timothy ya kutosha tu. Lakini nakuona jinsi usivyojua alikuwa anabiwa nani na kwa nini. Nakuona unajitwangia tu kama unavyofikiri katka huko kutokujua kwako.

  Hakuna aliyekuwa anajua mistari kama mafarisayo. Lakini shetani alikuwa amewakalia vichwani pamooja na singi wa hiyo mistari.

  Wewe kariri mistari mingiii bila kuwa na maatifa ya hiyo mistari moyoni mwako kisha nenda kakemee pepo kwa kumnukulia hiyo mistari uone kitakachokutokea!

  Yawezekana hata wewe unaijua mistari tangu utoto wako lakini hujawahi kuijua siri ya kuurithi ufalme wa Mungu iliyo kwenye hiyo mistari.

  Bado unahitaji mtu wa kukufundisha mambo ya msingi ya maneno ya Mungu.

  Usikariri maandiko ya kunukuu unaposema jambo, ELEWA maandiko ili ujue kuongea jambo kiusahihi!

  Take care
  (sijaedit)

 11. Tumaini Nelson
  Tarehe 01/12/2014 at 9:02 PM , Ulichaingia UKIMSIFU SANA SUNGURA.
  MBONA MCHANGO WAKO HAUNA HATA NUKUU MOJA YA BIBLIA?
  Epuka USHABIKI kwani HAUKUSADII KITU.

 12. WANATHEOLOJIA NA YEYOTE ANAYEHUSIKA,
  AONAVYO NAFSINI MWAKE NDIVYO ALIVYO…..( MITHALI 23:7)
  Unaweza kumtumikia IBILISI ukifikiri UNAMTUMIKIA MUNGU (MATHAYO 7:21-23)
  TATIZO SI KUTUMIKA, BALI UNAYEMTUIKIA NA ANAYEKUTUMIA NI NANI?
  Imani chanzo chake ni kusikia NENO LA KRISTO (WARUMI 10: 17),Hivyo;
  -Imani haichunguzi kitu bali HUAMINI TU.
  -IMANI haithibitishwi na SAYANSI au UTAFITI WA KISAYANSI (Scientific Research)
  -Unachosomea CHUONI KAMA TEOLOJIA si IMANI bali ni ujuzi wa mwanadamu na MAPOKEO YAKE.
  WAKRISTO, Hatukuambiwa kuthibitisha CHOCHOTE bali Tumeambiwa TUAMINI (We’re not asked to prove anything.We’re asked to believe it)
  WATU WA KIZAZI HIKI NI wajeuri ,hufuata akili zao zisizofaa,wenye husuda, WENYE KUMCHUKIA MUNGU nk.
  TEOLOJIA UMEJEGWA JUU YA MSINGI HUU.
  WARUMI 1: 28-32 “28 Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.
  29 Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya,
  30 wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao,
  31 wasio na ufahamu, wenye kuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema;
  32 ambao wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti, wanatenda hayo, wala si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao.”
  1TIMOTHEO 4:1-7 “1 Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;
  2 kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;
  3 wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.
  4 Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani;
  5 kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba.
  6 Uwakumbushe ndugu mambo hayo, nawe utakuwa mtumishi mwema wa Kristo Yesu, na mzoevu wa maneno ya imani, na mafundisho mazuri yale uliyoyafuata.
  7 Bali hadithi za kizee, zisizokuwa za dini, uzikatae; nawe ujizoeze kupata utauwa.”
  2TIMOTHEO 3:1-9 “1 Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari.
  2 Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi,
  3 wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema,
  4 wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu;
  5 wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao.
  6 Kwa maana katika hao wamo wale wajiingizao katika nyumba za watu, na kuchukua mateka wanawake wajinga wenye mizigo ya dhambi, waliochukuliwa na tamaa za namna nyingi;
  7 wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli.
  8 Na kama vile Yane na Yambre walivyopingana na Musa, vivyo hivyo na hawa wanapingana na ile kweli; ni watu walioharibika akili zao, wamekataliwa kwa mambo ya imani.
  9 Lakini hawataendelea sana; maana upumbavu wao utakuwa dhahiri kwa watu wote, kama vile na upumbavu wa hao ulivyokuwa dhahiri.”
  **** UPUMBAVU WA WANATHEOLOJIA NA WAPINGA NENO ( WAPINGA KRISTO) UPO DHAHIRI ****

 13. Ujuwe mimi nashangaa sana mtu anapokataa kutumia ufahamu wake ktk kujifunza mambo ya Mungu!Nimemfuatilia sana ndugu yangu Sungura,amejaribu kuweka vitu bayana!ila napomtazama Pendael, Ck Lwembe naona ni watu wanaotetea misimamo ya kile dini zao zimewafundisha kushika!hata namna Pendael alivyopresent mada hii amekuja na mtazamo wa dini yake na si mtazamo wa maandiko yanavyosema.anajaribu kulazimisha kile dini yake inachoamini.Jambo lingine ni pale kulazimisha namna Mungu anavyongea na watu kwa njia moja tu!yaani Mafunuo tu!kama Mama Ck anavyofanya.Mungu anajia nyingi za kuwasiliana nasi!Kwa kusoma na kujifunza Neno lake!mafunuo,ndoto,unabii n.k.Sasa unapomwekea Mungu kanuni moja tu!mfano sehemu unapotakiwa ujibidishe kusoma na kujifunza wewe unasubiri mafunuo kila wakati hapo ndipo unapobaki kama ulivyo!badala ya kusonga mbele wewe unakuwa mchanga kila siku.kwakweli tunatakiwa tusimwekee Mungu mipaka ktk kumtafuta na kumjua.

 14. wapendwa
  CK LWEMBE na PANDAELI

  Endeleeni kutupa changamoto zilizo hai,IVUENI THEOLOJIA
  NGUO ZOTE ibaki uchi kabisa!Tunataka tuuone utupu wake.
  Tunachohitaji hapa ni KUYAJUA MAPUNGUFU au UOZO
  uliofichika ndani ya theolojia ili tuufanyie kazi.

  Jiachieni kwa uhuru wote msijibanebane,Yesu anataka amalize
  hii biashara.Wateule wanaojitambua kiroho waameachana na biashara
  ya kucheka na nyani ili wasije wakavuna mabua.

  Mtumishi Pandaeli kandamiza zaidi usiache kitu,tunahitaji mtaji
  wa kuingia nao KWENYE ULIMWENGU WA ROHO.

  Hii vita kati ya wateule na uzao wa nyoka inaelekea pazuri
  naona kila kukicha mashetani wanazidi kuchanganyikiwa.Neno la
  Mungu limekuwa ni RADI inayoteketeza hila na kazi zao zote.

  1 SAMWELI 2:9-10
  “Yesu atailinda miguu ya watakatifu wake bali waovu watanyamazishwa gizani…….Washindanao na Bwana watapondwa
  kabisa.Toka mbinguni yeye atawapigia RADI…..”

  UTAMU WA YESU UNAONGEZEKA………Najisikia raha mpaka
  kwenye mifupa!

 15. Pendael,

  Wewe umenisema mimi kwa mafumbo( unafiki), lakini mimi nakutaja jina lako maana sipendi unafiki.

  Kama unadhani una Mungu ndani yako na mimi nina shetani basi tumia hiyo nafasi kunilaani, halafu uone hiyo laana kama itafanya kazi.

  Usudhani tunafanya burudani hapa, binafsi niko serious kutumika na ninawajibika kwa kile ninachokisema.

  Tumepewa uwezo tofautitofauti wa kuyaelewa mambo, kwa hiyo sikushangai unachosema, maana huo ndio uwezo wako wa kuelewa.

  Tia bidii kujifunza uwezo wako wa kuelewa utaongezeka. Lakini kama unafanya kama ulivyokuwa unafanya mwaka jana na juzi, utavuna mavuno yaleyale.

  Kuna mambo yanapatikana kwa bidii ya kujifunza wala si kwa ufunuo, na kuna mambo yanapatikana kwa ufunuo. Usilazimishe ufunuliwe wakati kumbe unatakiwa kutia bidii ya kujifunza.

  Ona hapa; 1Cor 7:12 – To the rest I say- I, not the Lord – if a brothet has a wife who is not a believer and she is happy to live with him, he should not divorce her. Yameenda mpaka mstari wa 16.

  Hebu niambie hayo maneno ni ya Paul au ya Bwana?

  Umesema mimi ni uzao wa nyoka kwa sababu ya reasoning juu ya maandiko. Wow, thank u so very much.

  Lakini sikia, watu wanaofikiri sawasawa walipoambiwa habari za Yesu hawakukomea tu kusikia na kukubali, bali walienda kuyachunguza maandiko ili wajiridhishe kama waliyoambiwa yako hivyo yalivyo ndipo waweke hitimisho.( hao ni watu wa Beroya) asomae na afaham.

  Kama wewe huwezi kureason unachoambiwa,basi ni mfu au hujielewi ila upo tu.

  Siyo tu ku-reason, tumeagizwa mpaka kuzijaribu roho, ili kujiridhisha kama zatokana na Mungu. Kama wewe ni wa kuambiwa tu fanya hivi na unafanya mara moja, basi sishangai kwa nini fikra yako iko hivyo.

  Huwezi ukaja kwangu ukaniambia toa laki tano utavuna mara mia halafu ukategemea nitanyanyuka ghafla na kufanya hivyo. Lazima nita-reason.

  Kukataa kuchunguza ni kukataa kujifunza, na watu wenye tabia hiyo ndio mnaotekwa kirahisi sana na manabii wa uongo . Coz u believe everything bila kufanya kama waberoya walivyofanya.

  In fact, mwanatheolojia aliyekamilika hawezi kudanganywa na nabii wa uongo, a.k.a Kibwetele kwa urahisi.

  Leo makanisa mengi washirika ni maskini sana pamoja na wingi wa utoaji wanaofanya.

  Nafikiri umeelewa, kama bado sema tuendelee!

  Reason before u jump into conclusion!

 16. Shalom.
  Wapendwa.
  Duniani Kuna Uzao wa aina MBILI.
  1.UZAO WA MUNGU (Mwanzo 6:1-2, Yohana Mtakatifu 1:12)
  2.UZAO WA NYOKA.(Mwanzo 3:15, Mathayo 3:7 )
  UZAO WA MUNGU hupenda kudumu na NENO na UZAO WA NYOKA hupenda kuishi KWA MAPOKEO NA HATA KUYATETEA KWA JUHUDI.
  UZAO WA MUNGU huishi kwa ” IMEANDIKWA…. na, BWANA ASEMA HIVI” na UZAO WA NYOKA huishi kwa ” Ati! Hivi ndivyo….. na, Hili naamini na hili siamini”
  UZAO WA MUNGU HULA NENO LISILOGHOSHIWA (NENO LA MUNGU) na UZAO WA NYOKA HULA MAPOKEO YA WANADAMU NA KANUNI ZA IMANI ( Dogma and creeds).
  UZAO WA MUNGU Hula kutoka kwenye MTI WA UZIMA (BWANA YESU KRISTO) na UZAO WA NYOKA hula kutoka kwenye MTI WA UJUZI WA MEMA NA MABAYA ( SHETANI)
  WANATHEOLOJIA hula katika MTI WA UJUZI WA MEMA NA MABAYA (WANAFUNDISHA UONGO NA UKWELI)
  Tangu lini CHEMCHEMI ikatoa MAJI MATAMU NA MACHUNGU?
  UZAO WA NYOKA HUPENDA KUHOJI BIBLIA,yaani ni watu wa hoja ‘ REASONINGS’
  Mtu anaposema Kwenye BIBLIA kuna MAENO YA MUNGU na ya WANADAMU hana tofauti NA MPAGANI asIyeamini BIBLIA.
  HUYU MTU ALIWAHI KUJUA NENO LA MUNGU NI NINI?
  LABDA hiyo BIBLIA yenye MANENO ya MUNGU NA WANADAMU ni ya KATOLIKI yenye VITABU 72.
  Paulo ANAYEZINGIZIWA kuwa ana MANENO YAKE katika Biblia anaandikia:
  1 WAKORINTHO 14 : 37-38, ” Mtu akijiona kuwa ni nabii au mtu wa rohoni, na ayatambue hayo ninayowaandikia , ya kwamba ni maagizo ya Bwana. Lakini mtu akiwa ni mjinga, na awe mijnga”
  Kusema Paulo ana Maneno yake Kwenye BIBLIA HUO SI UJINGA?
  WAGALATIA 1:8-9 ” Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe.Kama tulivyotangulia kusema, na sasa nasema tena mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo mliyoipokea na alaaniwe”
  Hawa WANATHEOLOJIA wanaosema BIBLIA INA MANENO YA MUNGU NA YA WANADAMU SI WAMELAANIWA?
  SOMA ( MITHALI 30: 5-6, LUKA 10:16, 1 WAKORINTHO 3: 10-15,WAEFESO 2:20, UFUNUO 22:18-19)
  Haya ndio MATOKEO YA THEOLOJIA na KIBURI CHA WANATHEOLOJIA ” Nilisema kwenye biblia kuna maneno ya Mungu na ya watu. Na hivyo ndivyo ilivyo.” ELIMU INAYOSEMA HIVI NI YA IBILISI NA YA MANABII WA UONGO. HUBADILISHA NENO MOJA TU kwenye BIBLIA NA SI SENTENSI KAMA NYOKA ALIVYOONGEZA “ha” ikawa ” hamtakufa” badala ya “mtakufa”! MWANZO 2:16-17, 3:1-7)
  >>>> UNAPOZUNGUMZIA NENO LA MUNGU UWE MAKINI NA KAULI UNAZOTUMIA KWA SABABU MUNGU SI BABU WA KIHINDI<<<
  TAKE CARE!!!!!!

 17. Mtumishi Lwitiko

  Bila shaka wewe ndiye Lwitiko katule!
  Ni maombi yangu kwa Mungu wangu kama ungepata neema
  ya kutupa mchango wako katika mada hii kama ulivyoitikisa
  dunia ya vipofu na viziwi wa kiroho katika mada inayosema
  TANZANIA INASUMBULIWA NA MALANGO!

  Kama ambavyo uliingia katika maombi na Mungu akakuonyesha
  kwenye ULIMWENGU WA ROHO chanzo
  cha umasikini wa Tanzania kuwa ni uhusiano wake mbaya na Taifa la Israeli kama LANGO lililoficha
  MUDA na BARAKA za mataifa yote duniani(ISAYA 60:1-22), ndivyo
  tunavyopaswa kuingia kwenye ulimwengu wa roho kwa ajili ya kuangalia kweli yote kuhusu THEOLOJIA.Bila shaka watu ambao
  wanautambua ulimwengu wa roho wanaona na kujua yote
  yanayoendelea kuhusu THEOLOJIA na changamoto zake.Ndani
  ya ulimwengu wa roho, Mungu huwa anaonyesha mwisho wa jambo
  mwanzoni mwake ili walinzi(waombaji) wapate kusimamia na kuhakikisha
  hilo analowaonyesha lanatimia(soma ISAYA 62:6-7).

  Ninamshukuru Mungu aliye hai kwa kujibu maombi ya wateule
  wa Tanzania akiwemo Mwalimu Mwakasege na huduma ya MANA.
  Kwa sasa kama ulivyoonyeshwa kwa njia ya maono, Tanzania imesogea
  karibu sana na Taifa la Israeli kwenye ulimwengu wa roho na Mungu
  ameshaanza kuipeleka Tanzania mahali pazuri mno!BILA SHAKA
  MATAIFA MENGINE WATAANZA KUTUTAFUTA MUDA SI MREFU
  ILI KUUSTAAJABU BARAKA ZA MUNGU JUU YA TANZANIA.Wachawi
  na waganga(manabii wa uongo) wakiwa chini ya uongozi wa PAPA
  wa roman catholic HAWAWEZI TENA KUZUIA HILI LISITIMIE!!!

  Pongezi za dhati ziwaendee watumishi Sungura, John Paul na Obri
  pamoja na wengineo ambao wamebobea katika kulichambua neno
  la Mungu na kuyajua sana Maandiko kuliko tunavyoweza kuwadhania!
  katika mada ya malango walikupa changamoto CHANYA ambayo
  ndiyo iliyoleta ushindi wa jumla kwa wateule wote.

  Maaskari wa Yesu wamejikita kwenye ulimwengu wa roho
  ili KUHAKIKISHA SUALA LA WANATHEOLOJIA NA CHANGAMOTO
  ZAO LINAKAA KATIKA MSTARI ULIOONYOOKA.MUNGU WETU NI
  HEKIMA YA MOTO ULAO.

 18. Lwembe,

  Kuna wakati niliwahi kukwambia kuwa kwa harakaharaka unaonekana u mtu mwenye uwezo mkubwa wa kufikiri, lakini libapofika suala linalohitaji akili kubwa kulichambua ndipo huwa nakuona u mtu mwenye fikra nyepesi sana.

  Kwanza nimesema karibu mara mbili kuwa wanatheolojia huwa hawa- interpret maandiko bali hu-translate maandiko. Lakini nashangaa bado unanilazimisha kuwa nilisema huwa wana-interpret maandiko. Huo ni uzembe wa kufuatilia mambo Lwembe.

  Nilisema kwenye biblia kuna maneno ya Mungu na ya watu. Na hivyo ndivyo ilivyo.

  Kuna wakati Paul anasema ” hapo ni mimi siyo Bwana”, hilo ni neno la mtu (Paul mtume).
  Na kama hujui, ni hivi zamani hawakuwa na maneno ya Mungu yameandikwa kwenye kitabu kimoja. Kila maneno au kitabu kilichoandikwa na mtumishi au nabii fulani kilikuwa kinajitegemea. Eg; Chuo cha nabii Isaya hakikuwa kimeunganishwa na chuo cha nabii Yeremia au Ezekiel.

  Hivyo vitabu vya manabii pamoja na vitabu vya torati, na vile vya injili na nyaraka za akina Paul zimekuja kukusanywa baadae na kuunganishwa pamoja, ndipo huo muunganiko (compilation) ukaitwa Biblia.

  Sasa huwezi ukaniambia kuwa neno ‘ Mathayo mtakatifu, au waraka wa Paul kwa Wakorintho, au neno ufunuo wa Yohana, n.k” ni maneno ya Mungu na si ya wanadamu.

  Inaposema biblia kuwa ‘kila neno lenye pumzi ya Mungu’ haikuwa inasema kuwa kila andiko/ neno la kwenye biblia lilisemwa na Mungu.

  Halafu unaponibishia kwa habari ya Luka, huo nao ndo nauona ni uvivu wa kufuatilia mambo au uwezo mdogo wa kufikiri. Hayo yako wazi kwenye sura ya kwanza ya Luka :1-4.

  By the way, hakuna mahali biblia imesema kuwa dini ni kitu kibaya, huwa nashangaa tu wakati mwingi nikiwaona watu wanaponda dini kwa ujumla, wakati hata wao wanadini.

  Tatizo linatakiwa liwe kile ambacho dini yako inakufundisha!

  Lwembe nasisitiza kuwa, kama kuna imani potofu, basi kuna imani sahihi, kama kuna injili ya uongo, basi kuna injili ya kweli, kama kuna manabii wa uongo basi kuna manabii wa kweli, na ndivyo hivyo kama kuna Theolojia ya/ wanathelojia wa uongo, basi na kinyume chake ni sahihi.

  Kama wanatheolojia wote ni watumishi wa shetani, au watu waongo, basi acha kutumia kazi zao, ikiwemo biblia.

  Kama si wao, ulitakiwa uwe na kila kitabu kikijitegemea.

  Achana na methali ya samaki mmoja akioza wote wameoza!

  Wekeni sawa mnachotaka hasa kusema!

  Take care!

 19. Sungura,

  Hakuna Theology ya ‘Kweli’ na ya ‘Uongo’, iko yenyewe tu moja kama ilivyo, kutegemeana na unaipata kutoka “school of thought” ipi; yaani who got you first before God could get you!

  Tafsiri ya neno Theology ni hii hapa:
  “”THEOLOGY:- The study of the nature of God and religious belief. (a theology degree.)
  • religious beliefs and theory when systematically developed: (in Christian theology, God comes to be conceived as Father and Son and the Holy Ghost
  [ count noun ] 😦 a willingness to tolerate new theologies.)””

  Sasa msichokielewa hapa ni nini? Religious Beliefs and theory zikiisha kuwa SYSTEMATICALLY DEVELOPED, ndio unapata TEOLOJIA!! Hamuoni kwamba hili jambo la Elimu? Elimu inatokana na ‘Ujuzi wa Mema na Mabaya’, zao la ule Mti walioonywa kuuhusu kule Edeni; kama Nyoka alivyolifafanua Neno la Mungu kwa Eva, ndicho kinachoendelea leo hii kwa hila!

  Ku Translate na ku Interpret ni mambo mawili tofauti ndg yangu, usiyang’ang’anize yawe moja. Mchango wangu wa kwanza ulilenga kuliweka wazi jambo hili ambalo kwa hila limechanganywa na kuwa moja, jinsi ambayo naona nawe ni mmoja wa waathirika wa hila hiyo! Ku Translate ni suala la Ujuzi wa Lugha, halina katazo, tena nikakuambia kuwa hilo ni jambo jema ambalo Mungu hulisimamia, nikakupa na mfano wa tukio la siku ya Pentekoste! Kuyatafsiri Maandiko kutoka lugha moja kwenda nyingine SI jambo la Teolojia kama ulivyodanganywa, rudi kwenye hiyo tafsiri ya neno Theology uone kama kuna sehemu yoyote inayohusika na lugha, HAKUNA.

  Lakini ktk Interpretating ndio unaweza kuona cross-reference inayokupeleka kwenye neno la asili, kilugha, ktk kukidhi haja ya kulipambanua jambo, kupata ile context ili kusimamisha uelewa unaolifafanua Andiko fulani na hivyo ku develop theory husika, ambayo ndiyo Teolojia!

  Kikwazo kingine kinachokukabili ni kujiondoa kutoka ktk Uongo wa Kiteolojia unaoiondoa Nguvu ya Mungu iliyohifadhiwa ktk Biblia, hapo ulipoaminishwa kwamba “Biblia ina maeno ya watu, Shetani na ya Mungu”; ninaamini kwa hili, you simply sealed yourself out of the pure understanding of the scriptures!

  Angalia jinsi Teolojia inavyopingana na kile Mungu anachokisema:
  Biblia: 2Tim 3:16 ” All scripture is given by inspiration of God”
  Teolojia: “”Luka hakuwa miongoni mwa mitume, lakini aliamua kufanya utafiti wa mambo yaliyokuwa yakisimuliwa nae akayaandika kitaalam, wala hasemi kwamba alifunuliwa kufamya hivyo, bali anasema aliamua. Luka 1:
  Huyo kama si mwanatheolojia ni nani?””

  Unaona unavyotolewa kwenye reli kirahisi? Yakiisha kujaa moyoni mambo ya jinsi hii ni lazima uishie nje ya kambi! Kristo anasema, “Maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.” Basi iwapo Biblia ina maneno ya watu na ya Shetani na Mungu, itakulazimu uyatofautishe hayo kwanza, uyapate ya Kristo, ili kumpata huyo Roho! Yaani uyatofautishe hayo ili uyajue yaliyo Scripture uyahifadhi moyoni mwako, na ktk hila hiyo ndio unaishia kuyahifadhi hayo yenye kufisha yanayokuongoza kuyakataa yaliyo kweli!

  Nitaendelea Sungura, tuna mengi ya kuyatazama…!

 20. Kwa kweli katika michango Mungu humu hoja za kaka sungura zimesimama na inavutia sana kusoma hoja za ndugu. Zinaelekeza kwa kiwango cha utoshelevu sana. Mungu akubariki kaka

 21. Tumain,

  Heri iwe kwako ndg yangu kwa kupewa macho ya kuona ukweli tunaosema ktk mada hii!

  Mimi naheshimu kazi kubwa ya wasomi hawa (wanatheolojia), wametusaidia kuwa na kumbukumbu ya neno la Mungu katika mikono yetu.

  Kinyume cha hapo tulitakiwa tuwe naneno la Mungu kwa njia ya Fasihi simulizi. Sasa sijui nani angeamini mwenzake anasema kweli pale abapoamua kusema neno alilosimuliwa.

  Lazima tujue kuwa palipopandwa mbegu njema muovu nae hujipenyeza usiku wa manane na kupanda magugu, lakini kamwe magugu hayawezi kuzipoteza mbegu njema.

  Mtu anapinga wanatheolojia kwa kusifia toleo la Biblia la King James kana kwamba lenyewe liliandikwa na Roho mt., wakati liliandikwa na haohao wanatheolojia anaowaponda!

  Hicho kama si kiburi, basi ni upungufu mkubwa sana wa kufikiri.

  Hawa rafiki zangu nafikiri wana hoja nzuri wanayotaka kuongea kuhusu Theolojia, wamekosa kutengeneza mtindo mzuri wa kuijadili hoja hiyo.

  Mungu awape neema waweze kujadili kwa usahihi kitu walichonacho mioyoni mwao.

  Ubarikiwe!

 22. Lwembe,

  Kweki mnafiki hana rafiki. Wewe ni mnafiki rafiki yangu.

  Nilikuwa nimekungoja tu maana nilijua utakuja kwa hii kona. Katka komenti zako za kwanza ya tar.12/11/2014, naona ulikuwa hujafanya maamuzi ya upande gani unasimama ktk hii mada.

  Nilikushangaa msimamo wako kwenye hizo komenti, lakini nikasema acha nisubiri, hatimae umefika.

  Inawezekana wakati mwingine huwa unajisikia raha ukinipinga tu hata kama unachonipinga nacho hakina nguvu sana.

  Uliwahi kunipinga sehemu fulani niliposema kuwa biblia imeandikwa kwa lugha mbili kwa asili, yaani Kiebrania na Kiyunani. Wewe ukasema biblia imeandikwa kwa lugha moja tu ya Kiebrania kwa asili. Niliamua kukunyamazia tu nikajua umeandika bila kufanya utafiti wa kutosha.

  Haya, katika hili sasa:

  Kwanza nakushangaa unaponambia kuwa niliongelea suala la Translation na Interpretation kwa hila, sijui ni hilaipi hiyo.

  Kimsingi wanayheolojia makini hawafanyi interpretation ya maandiko kwenye biblia, bali wanafanya translation ya maandiko.

  Paul hakuwahi kuunganisha barua zake alizokuwa anatuma kwa watu na makudanyiko mbalimbali, kazi hiyo ilifanywa baadae ma wanatheolojia ambao walitafiti na kuziweka pamoja. Leo mtu mmoja aliyeshiba mikate anasema watu hao hawafai.

  Luka hakuwa miongoni mwa mitume, lakini aliamua kufanya utafiti wa mambo yaliyokuwa yakisimuliwa nae akayaandika kitaalam, wala hasemi kwamba alifunuliwa kufamya hivyo, bali anasema aliamua. Luka 1:
  Huyo kama si mwanatheolojia ni nani?

  Nimekushangaa sama kwa ufahamu ambao mimi hudhani unao, kuojadili Theolojia na wanatheolojia kwa ujumla, na kuhitimisha kuwa kitu kibaya.

  Ulipoanza kule mwanzo ulijaribu ku-balance kuwa wanatheolojia ni wasomi wanaofanya utafiti wa facts na kuulinganisha na ukweli wa biblia, ukajaribu kutofautisha wanatheolojia wa namna hiyo na wale wanatheolojia wa dini na madhehebu.

  Lakini baadae umebadilika na kuhitimisha kuwa theolojia na wanatheolojia haeafai, wanafundisha mafundisho ya wanadamu. Huo ni uandishi uchwara ndg Lwembe, na hapo ndipo nikakuona wewe ni mnafiki.

  Linganisha komenti zako utakubali mwenyewe kuwa umekuwa mnafiki!
  Yesu alisema jinsi ilivyoshida kwa wenye kutegemea mali kuuona ufalme wa Mungu.
  Lakini watu wengi baadae wakahitimisha kuwa Yesu alisema matajiri hawawezi kuuona ufalme wa Mungu.

  Ni sawa na mtu mwenye kuhitimisha kuwa Theolojia ni mbaya, wakati yeye mwenyewe ana kazi nyingi sana za wanatheolojia zinazomsadia kumjua Mungu.

  Biblia unayotumia ni kazi ya wanatheolojia. Kumbuka haikuwa imeandikwa ikiwa na namba za mistari(verses), bali hizo namba zilikuja kuwekwa na wanatheojia, na leo zinasaidia watu kusoma na kuishika biblia kwa urahisi.

  Hiyo KJV unayoipongeza ni kazi ya wanatheolojia, ndo walioi-compile baada ya utafiti.

  Lwembe watu kufundishana habari za Mungu haikuwa jwenye mfumo wa chuo kama leo ilivyo, bali walifundishwa miguuni pa watu, na hiyo kwa maana halisi ya chuo ilikuwa ni chuo tosha.

  Timothy anaambiwa na Paul ashike vema mambo ambayo alifundishwa na bibi yake Loyce. Kwa nini haijasema mambo aliyofundishwa na Roho mt.!

  Kitendo cha Timoth kukaa miguuni pa bibi yake akifundishwa ni chuo tosha.

  Mnatakiwa kutofautisha jati ya wanatheolojia wa dini fulani au dhehebu fulani na wanatheolojia wa kweli. Mungu hafanyi kazi kwenye kanuni ya samaki mmoja akioza wote wameoza.

  Halafu mnapopinga Theolojia ya kweli mnaipinga against what, Roho mt.au?
  Ni sawa na kumwambia mtu asitumie akili bali atumie Roho mt.

  Akili na Roho havitakiwi kuingiliana, yako mambo ambayo si ya kutumia akili bali Roho, eg; usitegemee akili kusema neno la maarifa. Lakini yako mambo si ya kutumia/ kutegemea Roho, eg; huhitaji sauti ya Roho kujua kuwa unatakiwa kuoga, ni akili tu ya kawaida.

  Kadhalika Theolojia na Roho, kila kimoja kina mahali pake.
  Mtu ambaye anaacha kuongozwa na Roho na kuanza kutegemea Theolojia(yaani tafiti za wanatheolojia), huyo hajui afanyacho, na ni mwanatheolojia wa uongo.

  Lakini usianze kufunga na kuomba ili biblia ijiandike yenyewe katika lugha ya kwenu, watafute wanatheolojia wa kweli watafanya hiyo kazi.

  Usifunge kwa ajili ya kutaka kujua biblia iliandikwa kwa lugha fani kwa asili, waulize wanatheolojia watakwambia kuwa Agano la kale liliandikwa Kiebrania na jipya liliandikwa Kiyunani.

  Lwembe sijui wewe unaongelea Theolojia ipi!

  Mnamjua mwanatheolojia Oral Roberts alivyotembea na Mungu, unamjua mwanafunzi wake Benson Idahosa alivyotembea na Mungu, unamjua mtu anaitwa Katherine Kuhman alivyotembea na Mungu, unamjua mtu anaitwa T.L. Osborn alivyotembea na Mungu?

  Mimi hiyo ndo Theolojia na wanatheolojia ninaoongelea, hawaligoshi neno la Mungu.

  Lwembe wewe unaongelea Theolojia ipi rafiki yangu? Hata injili ziko nyingi usipoelewa ni injili ipi unayosimama nayo unaweza kuchanganyikiwa.

  Asilimia kubwa ya manabii wa uongo ni watu ambao wamekwepa shule na kujifanya kuwa wao wanaenda kwa ufunuo tu. Hivyo huwadanganya watu kuwa wanaongozwa na Roho mt.

  Nakazia;

  Tofautisheni wanatheolojia wa uongo na wanatheolojia, kama mnavyotofautisha manabii wa uongo na manabii.

  Take care!

 23. Ubarikiwe ndg Lwembe.
  Hii ni nyundo kwa WANATHEOLOJIA.
  Katika (YOHANA MTAKATIFU 3:1-15) NIKODEMO alikuwa mwanatheolojia kuwashinda hawa wanaoongea WASICHOKIFAHAMU, Lakini NIKODEMO alishindwa “test” ya “KUZALIWA MARA YA PILI”.
  BWANA YESU KRISTO anamthibitishia NIKODEMO kuwa “ELIMU YAKE YA TEOLOJIA” haimkusadia kitu ( YOHANA MTAKATIFU 3:10 ‘Yesu akajibu, akamwambia, Je! Wewe u mwalimu wa Israeli, na mambo haya huyafahamu?”)
  Kama Theolojia inasaidia mbona;
  -WANATHEOLOJIA wanaunga mkono WANAWAKE KUHUBIRI mimbarani na kuongoza wanaume? 1 WAKORINTHO 14:34-38, 1TIMOTHEO 2:8-15
  -Wanatheolojia HUWAPINGA MITUME (mfano; KAKOBE hufundisha kuwa MITUME walifundisha kinyume cha MAAGIZO YA YESU- kuhusu Ubatizo) ? LUKA 10:16, WAEFESO 2:20, WAGALATIA 1:8-9
  -WANATHEOLOJIA wanapinga UBATIZO KATIKA JINA LA YESU KRISTO? (MATENDO 2:38-39, 8:14-16, 10:48, 19:1-5)
  *Wengine hubatiza WATOTO!
  -WANATHEOLOJIA hutetea MADHEHEBU wakati BWANA YESU na MITUME wake pamoja na WAKRISTO wa BIBLIA hawajawahi kuwa na DHEHEBU?
  * MADHEHEBU NI UKAHABA (UFUNUO 17:3-5)
  Haya ni mambo MACHACHE sana yaliyomo kwenye TEOLOJIA.
  ***KAMA UNA ROHO MTAKATIFU UTAITIKIA NENO LA MUNGU KWA AMINA***

 24. Sungura,

  Kwanza nikushukuru kwa jibu zuri, rahisi na lenye kueleweka, pia lenye kuonesha kiwango kikubwa cha ufahamu ulicho nacho kuhusu mambo haya, asante sana!

  Nilikuuliza swali hilo kutokana na nilivyokuona ukitumia hila kujadili jambo ambalo liko wazi saana, Translating na Interpreting ni mambo mawili tofauti, moja ni la lugha na jingine ni la ufunuo! Kwahiyo kuyafanya ni jambo moja, hiyo ni hila!

  Teologia ni mfumo wa elimu, ile hekima ya kibinadamu, unaojaribu kumpambanua Mungu au Uungu, kupitia tafiti na kwa kusoma Biblia kwa nia hiyo. Teologia HUFUNDISHWA vyuoni. Pia hutoa fursa ya kuzikagua “Kweli za Dini” zilizozalishwa na makundi mengine ya Teolojia, ndio kama huo mfano ulionipa ktk jibu lako, ambao unaonesha dhahiri kwamba kuna TOFAUTI za KIUFAFANUZI wa Maandiko; i.e. ule Ujuzi wa Kuifasiri Biblia yaani INTERPRETING – ktk maana ya kuyatolea UFAFANUZI Maandiko kulingana jinsi huyo mkufunzi wa Maandiko anavyoyadhania au fikiria na hivyo kuyapa maana hiyo, ambayo ndizo hizo “Kweli za Dini” zinazopokelewa na wanafunzi wa vyuo vya Teologia na kisha kulishwa waumini!

  Ni ktk msukumo huu ndio unaweza kuona kufanikiwa kwa fundisho la kuwainua wanateolojia kuwa juu ya waumini, kwa kuwaaminisha kwamba hawana uwezo wa kulielewa Neno la Mungu bila ya msaada wao! Kutokana na fundisho hili, waumini huwategemea kwa asilimia 100 wanateolojia wao.

  Kwahiyo bila ya ufahamu waumini huingizwa ktk kuwategemea watu badala ya Mungu, na hivyo kuingizwa ktk laana ya kumtegemea mtu bila ufahamu, (Yer 17:5); sasa hapa si waumini tu, bali hata hao wanaofuzu hayo masomo, na kuyabeba mafundisho ya hizo “Kweli za Dini” zilizoasisiwa na wakufunzi wao, wakiziamini kwamba ndilo Neno la Mungu na hivyo kuwahubiri watu mambo hayo!

  “Kweli za Dini” ni hekima ya kibinadamu isiyoweza kukufikisha Uweponi mwa Mungu. Mungu ndiye Amini na kila mtu na awe muongo kwetu, Rm 3:4

  Kwahiyo vyuo vya Teolojia huzalisha manabii wa uongo, licha ya upako wanaoonekana kuwa nao, kwani wanayafasiri Maandiko kinyume cha matakwa ya Mungu, 2Pet 1:20 “Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu.”

  Pia vyuo vya Teolojia si kwamba leo hii ndio vimekuwepo, hasha! Teolojia ilianza huko mbinguni, ndio iliyomsababisha Lusifa kuasi; na ndio iliyomfanya Hawa kula tunda, ikifanikiwa kumfikia mchanga wa Injili, huchipua hapo na kuwa mbuyu!

  Watazame akina Kora jangwani, walimfasiri Mungu ktk jinsi waliyoiona ni sahihi kwao mpaka wakapotea, yaani waliamini wako sahihi mpaka nchi ilipokifunua kinywa chake na kuwameza! Teolojia hukufanya kuwa sugu, ikiyaziba masikio yako ya kiroho kwa sementi!!!

  Mtazame Elisha, nabii wa Kweli. Alipofika ktk chuo cha Teolojia huko Betheli, aliwakuta hapo wanachuo mahiri, hata wakamtabiria kwamba bwana wake Elia atamuondoka, 2 Fal 2:3 “Basi wana wa manabii, waliokuwako Betheli, wakatoka kuonana na Elisha, wakamwambia, Je! Unajua ya kuwa BWANA atamwondoa bwana wako leo, asiwe mkubwa wako?” Unaona, wanao uwezo wa kuyakamata mambo ktk anga za chini, kama huko kuondoka kwa Elia! Wengine hawa hapa wa chuo cha Yeriko aliokutana nao baada ya Elia kuondoka, “15Na hao wana wa manabii, waliokuwako Yeriko wakimkabili, walipomwona, walisema, Roho ya Eliya inakaa juu ya Elisha.” Hivyo vyuo vya Kale vilikuwa na afadhali kuliko hivi vya leo ambavyo wanafunzi wake ni mbumbumbu wa Neno la Mungu hata inatisha, hawana hata uwezo wa kuitambua Kweli ya Maandiko zaidi ya hizo “kweli za dini” zinazowashikilia!

  Hahahaha…! wale wanachuo wa Yeriko wakajitosa kwenda kumtafuta Elia, masikini upeo wao wa kuona ni macho ya kimwili tu hivyo wakajua lazima ameangukia sehemu huko milimani!! Na wale wa Betheli nao alipofika wakatayarisha chakula kwa ajili ya watu tena ilikuwa ni wakati wa NJAA ya Neno la Mungu kama ilivyo leo hii. Wakawa wamechuma matango mwitu mazuri yenye kupendeza machoni na masikioni kama Injili mwitu zilizojaa leo hii. Lakini walipokitazama chungu wakakiona KIFO ndani yake, wakaangua kilio, HAWANA uwezo wa kukikabili kifo! Inachukua UFUNUO kuyaelewa Maandiko hayo yaliyo Uzima, ni nabii wa Kweli pekee ambaye anaweza kukabiliana na Kifo, haleluyaaa, Elisha alikuwepo akakifukuza kifo watu wakayala matango mwitu! Soma 2 Wafalme.

  Paulo, baada ya kuingizwa kt Ufalme, humo ambamo Ufunuo ndio chakula cha kila siku, hiyo Teolojia aliyoisoma chini ya mwalimu mashuhuri Gamaliel, anasema ni sawa na mavi anapoifananisha na mambo anayokutana nayo upande huu wa Ufalme!

  Sungura, Mungu si masikini, mkononi mwake kuna masikini, matajiri wasomi mbumbumbu nk Hebu fikiria ni nani kati ya wanafunzi wake, wale 11 waliobaki, ambaye angeweza kujitosa akauombe mwili wake uliokuwa pale msalabani? HAKUNA mwanateolojia hata mmoja aliyemsaidia Mungu kuyakusanya Maandiko hata kuwa kitabu kama mlivyodanganywa! King James alikuwa kasisi wa wapi? Huyo hapo kama Kornelio, sadaka yake ndio hii KJV tuliyonayo!!!!

  Watazame wale Mamajusi, walijuaje kuzaliwa kwa Mfalme hata wakasafiri safari yote ile, tena wakiongozwa na nyota!? Biblia yao ilikuwa hizo anga! Kwa kuzisoma anga wao waliyatambua mambo ya Mungu, aliwafunulia hayo.

  Walipokaribia Yerusalemu, ule mji wa Teolojia, pale makao makuu ya dini, wakavutwa na umaarufu wake, wakaiacha namna iliyowaongoza wakatafuta elimu, kama ambavyo nasi leo hii tunavyolikataa Neno lililodhahiri na kung’ang’ania mafundisho yetu! Matokeo ya jambo lao hilo wakaleta msiba mkubwa juu ya watu wa nchi kama ambavyo nasi yatatufika kwa ujinga!!

  Walipotoka Yerusalemu waliikuta nyota waliyoiacha na ikawaongoza tena! Mungu hana ushirika na Teolojia!

  Suala la ku Translate Biblia limevamiwa na kutekwa na Wanateolojia ili kulinda na kuendeleza maslahi yao ktk jamii, ndipo kwa hila wamelijumuisha ktk Interpretation zao zinazosimamia mafundisho waliyoyazalisha; hili ndilo chimbuko la hizo versions nyingi za Biblia zinazoendelea kuzalishwa. Bali suala la lugha ktk maana ya kutafsiri, hilo ni kipawa cha lugha, kama ilivyokuwa siku ya Pentekoste, inapobidi basi Mungu hawezi kuwa mbali!

  Athari za Teolojia ni nyingi saana, ngoja nijirejeshe ktk msingi wa mada halafu tuone kwa uhakika hasara yake ikoje kwa washirika tuliojazwa uongo wao!

  Mt 15:9 “Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu.”

  Gbu!

 25. Daaaah!Bonge Laa Mada!Pongezi kwako Pendaeli kwa kuja na mada hii ambayo nimesoma dot,to dot!kwa ujumla wachangiaji wote mmefunguka ipasavyo!ila niseme ukweli Sungura umenifurahisha saaaanaaa kwa kuusema ukweli mtupu pongezi kwako Kamanda wa Yesu a.k.a mzee wa makavu!!daaah!nimeipendaaa!kwakweli nimejifunza meng saana hapaa kwenyi hi maada!ila niseme tu watu tukubali kujifunza na ktk kujifunza huku au kosoma ndipo Roho Mtakatifu atakapokuelekeza,fundisha na kukutia kwenye kweli yote!Binafsi nimejifunza mengi saaana.daaaaah!nimejifunza kwa kweli!Nawapenda woote!

 26. Samileander,

  Kwanza ieleweke kuwa kitendo cha wewe kuchambua haya mambo unayochambua hapa ndiyo Theolojia yenyewe.
  Ndio maana wakati wote mimu nakushangaa sana unapoponda Theolojia wakati wewe mwenyewe unachokufanya hapa ni Theolojia.

  Ningekuelewa vema kama ungekuwa unaponda wanatheolojia wa uongo, lakini wewe ati unaponda wanatheolojia kwa ujumla, hiyo siyo sawa.

  Ni ukweli usiopingika kuwa matoleo ta biblia tulizonazo ni kazi ya wanatheolojia. Na kama tunaamini kuwa maandiko ya kwenye biblia ni kazi ya Roho mt.basi tukubali kuwa Roho aliwatumia/ anawatumia wanatheolojia.

  Suala la kuwepo kwa wanatheolojia wa uongo ni sawa tu na suala la kuwepo kwa manabii wa uongo.

  Umeongelea 1Sam 13:1

  Nakupongeza kwa utafiti huo. Hiyo ndo kazi ya mwanatheolojia.

  Lakini ulitakiwa uzame zaidi kwenye utafiti wako, ubgegubdua kuwa biblia ya Kiswahili haijafanya makosa katika hilo andiko.

  Historia inaonesha kuwa kuna mkanganyiko mkubwa tu juu ya hilo andiko kwa sababu inaaminika kuna manuscripts zilipotea hivyo kuleta mkanganyiko wa kipi hasa kilikuwa kinasemwa hapo. Yaani je ni umri ambao Saul alikuwa nao wakati anaanza kutawala, au inaongelea tukio fulani lililotokea baada ya Saul kuwa ametawala mwaka mmoja au miwili.

  Lakini kuna matoleo mengine wameweka (….) kabisa kuonyesha kuwa kuna hesabu ya miaka fulani hapo haijulikani vizuri.
  Ndio maana ya Kiswahili imesema miaka kadha wa kadha.

  Tafiti bado zinafanyika ili zipatikane hizo manuscripts ijulikane kama kinachoongelewa hapo ni umri wa Saul alipoanza kutawa au kama ni idadi ya miaka aliyotawala.

  Lakini kama ni idadi ya miaka aliyotawala Paul anatuambia ni miaka arobaini( matendo 13:21)

  Halafu kumbuka jambo hili kuwa biblia ya Kiswahili ilipatikana kwa usimamizi wa wakoloni, ambapo walitumia tu watu wanaojua lugha. Hivyo waislam pia walishiriki ktk hilo zoezi maana hili eneo letu mwanzo lilikuwa chini ya utawala wa waarabu.

  Bila wanatheolojia, basi neno la Mungu tungekuwa nalo kila mtu kichwani mwake, maana lingepatikana kwa njia ya Fasihi simulizi.

  Maana kazi ya uandishi wa neno la Mungu haikufanywa/ haifanywi na Roho mtakatifu bali ilifanywa/inafanywa na watu(wanatheolojia in particular)

  As far as Roho mtakatifu yupo. Wanatheolojia wa uongo hawataweza kulipoteza kanisa kwa kutoa matoleo yenye hila ndani yake.

  Kuna waislam miaka ya karibuni hapa walijaribu kutoa toleo la Kiswahili lenye hila, lakini lilinaswa.

  Kumbuka wanatheolojia hawa-interpret maandiko( hawatoi maana ya maandiko)bali wana- translate(wanayaandika maandiko kutoka lugha moja kwenda nyingine)

  Let us appreciate true Theologians please!!

 27. SHETANI ALIJARIBU KUTOKOMEZA BIBLIA LAKINI ALISHINDWA, WAFARANSA KUKUSANYA NA KUCHOMA BIBLIA KWA MIAKA MITATU, HAKUKUSAIDIA KITU.

  SHETANI ANATAKA KUHAKIKISHA UNA BIBLIA MKONONI LAKINI ALIPUNGUZE NENO HILO MPAKA UBAKI NA MAKARATASI MATUPU.

  (NEW VERSIONS ZITAKUJA KUFANYA WAKRISTO WA BAADAE WASIKUTE RADHA HALISI YA BIBLIA)

  LAKINI NENO LA MUNGU LITATIMIA TU,JAPO JESUIT WALITEGA BARUTI KUTAKA KUUA WABUNGE WOTE WA UINGEREZA WABADILISHE UONGOZI WA NCHI HIYO ULIOKUWA UMEHIFADHI COPY ZA KING JAMES BIBLES WALIKWAMA. KUWAFANYA WAINGEREZA MPAKA LEO WASHEREHEKEE SHEREHE ZA BONFIRE KUTOKANA NA KUSHINDWA KWA JESUIT JUU YA KUTAKA KUONDOA KING JAMES BIBLE. ZIBAKI VERSIONS WANAZOTAKA, NENO LA MUNGU

  HALITAPOTEA ILA WASIOLILA LILE HALISI/WAKILA CHACHU/MVINYO WATAPATA NJAA.

  WANATHEOLOJIA WA BIBLE SOCIETY OF TANZANIA NAO WAMESHINDWA KUTUJIBU KWA NINI,

  FUNGU LA SAMWELI NI TOFAUTI KABISA KATIKA BIBLIA YA KIINGEREZA NA YAO.

  1 SAMWELI 13:1
  “SAULI ALIKUWA NA MIAKA KADHA WA KADHA HAPO ALIPOANZA KUTAWALA; NAYE AKATAWALA MIAKA KADHA WA KADHA JUU YA ISRAELI.”

  KIINGEREZA IMETUFUNDISHA HIVI;
  1 SAMUEL 13:1
  “SAUL REIGNED ONE YEAR; AND WHEN HE HAD REIGNED TWO YEARS OVER ISRAEL’”
  KING JAMES VERSION

  KATIKA DANIEL 8:9 NENO EAST WAO WAMETUAMBIA MAGHARIBI, BADALA YA MASHARIKI

  DANIEL 8:9
  “AND OUT OF ONE OF THEM CAME FORTH A LITTLE HORN, WHICH EXCEEDING GREAT, TOWARD THE SOUTH, AND TOWARD THE EAST, AND TOWARD THE PLEASANT LAND.”

  DANIEL 8:9
  “NA KATIKA MOJA YA PEMBE HIZO ILITOKEA PEMBE NDOGO, ILIYOKUWA SANA, UPANDE WA KUSINI, NA UPANDE WA MAGHARIBI, NA UPANDE WA NCHI YA UZURI.”

  BAADHI YA MANENO PIA WALIOYAONDOA, KUTOKA WAINJILI KATIKA BIBLIA ZA KISASA NI ILE RADHA YA MANENO KAMA;

  MARKO 2:17 “KUTUBU”
  MATHAYO 16:20 “WAITWAO NI WENGI BALI WATEULE NI WACHACHE”
  MATHAYO 25:13 “ATAKAPOKUJA MWANA WA ADAMU”
  MARKO 10:21 “JITWIKE MSALABA WAKO KISHA UNIFUATE”

  WANATEOLOJIA WANAWAPA SHIDA WAHUBIRI WA SIKU HIZI HASA PALE WAHUBIRI WANAPOWAAMBIA WAUMINI WAPYA FUNGUENI MAHALI FULANI HALAFU MANENO HAYO HAYAPATIKANI, MNAPOTEZA IMANI YA WAUMINI WAPYA KWA NENO LA BIBLIA.

  MASADUKAYO NA MAFARISAYO WALIKUWA WALIMU/ WANATHEOLOJIA WALIOBOBEA KATIKA KUSOMEA VYUO VYA DINI, WAKAJIKWEZA HATA KUONGEZA TARATIBU ZAIDI YA 613 ZILIZOWAPA MZIGO MKUBWA WATU WA MUNGU.

  YESU ALIWAFUNDISHA MITUME KUPITIA MIKATE WALIYOISAHAU ENEO LA TUKIO, KUWA WAJILINDE NA CHACHU YA MAFARISAYO,ISIJE INGIZWA KWENYE MIKATE. LAKINI WANAFUNZI WALIDHANI CHACHU JUU YA MKATE WA KAWAIDA KUMBE NI CHACHU JUU YA NENO, YAANI MAFUNDISHO (MAPANDIKIZI YA WANATEOLOJIA WA KIPINDI HICHO KWA MKATE/NENO ALILOWAHUBIRIA YESU.)
  FUNDISHO DOGO TOFAUTI NA MUNGU ALIVYOSEMA LAWEZA CHACHUA BIBLIA NZIMA.

  TUJILINDE NA WANATHEOLOJIA WANAOTIA CHACHU KATIKA MKATE HUU WA PEKEE KANISA LA YESU LILILOACHIWA.

  MATHAYO 16:12
  “NDIPO WALIPOFAHAMU YA KUWA HAKUWAAMBIA KUJILINDA NA CHACHU YA MKATE, BALI NA MAFUNDISHO YA MAFARISAYO NA MASADUKAYO.”

  TUJILINDE NA CHACHU YA WANATEOLOJIA KWENYE MKATE TULIOACHIWA NA YESU/NENO LAKE.

 28. KUJIFUNZA KWA UNYENYEKEVU NI ZAIDI YA FAIDA!!!

  YESU anasema katika MITHALI 8:10,19 “Pokea mafundisho yangu
  wala si FEDHA, na MAARIFA kuliko DHAHABU safi…..Matunda yangu
  hupita dhahabu,naam, dhahabu safi na FAIDA yangu HUPITA FEDHA
  ILIYO TEULE”

  Kwa muongozo wa Roho Mtakatifu nimepata neema ya kuunganisha
  maelezo ya SAMILEANDER 21/11/2014 at 3:06 pm , PANDAELI
  SIMON 20/11/2014 at 11:13 pm na SUNGURA 28/11/2014 at 4:14 am and 4:34 am. NIKAPATA HITIMISHO LA AJABU
  NA KUTISHA kama ifuatavyo;

  1.Tunapojadili mada nyeti kama hii kwa kiburi ,ubinafsi na kujitafutia umaarufu
  tutakwama na kuwakwamisha wengine wanaotufuatilia kwa karibu.
  Lengo ni kujifunza ili kuujenga mwili wa Kristo.

  2.Mtumishi CK LWEMBE anajadili akiwa katika hali ya umakini,chanya
  na utulivu mkubwa.Haonyeshi kuolewa na ujinga wa kishabiki au kujitia
  ujuaji bali anazungumza kile anachokijua ili kusaidia na kusaidika.Kwa ufahamu wa kawaida ni vigumu kuijua rangi ya Lwembe.

  3.Mada haiongelei tu maana ya THEOLOJIA LAKINI ZAIDI SANA
  IMEKAZIA KATIKA MUELEKEO NA HATIMA YAKE.Mada imefocus
  zaidi katika kutatua changamoto za wanatheolojia.Mada inatutaka
  tukubaliane na Roho Matakatifu ambaye ndiye mwandishi wa Bibilia.

  4.Je! Theolojia imefaulu kuleta UMOJA WA KANISA LA KRISTO?Ule
  umoja wa wateule wanaoongozwa na BIBILIA TAKATIFU(maandiko
  matakatifu) ambayo iliandikwa na Roho Mtakatifu upo au umekufa?
  Je! Mungu alishayajibu maombi ya Yesu(YOHANA 17:6-26) kuhusu
  umoja wa watu wote waliozaliwa mara ya pili ambao wanaunganishwa
  na Neno la Mungu(Bibilia)?

  5.Maelezo ya SAMILEANDER na PANDAELI SIMON yanaonyesha
  wazi kwamba tunahitaji MAARIFA YA YESU ili kujenga na kuimarisha
  umoja wa wateule wa Mungu kwasababu wanatheolojia wa uongo
  ambao mtumishi SUNGURA amewaeleza WAMEFANIKIWA KWA KIWANGO KIKUBWA kuusambaratisha umoja wa wateule kwa KUCHAKACHUA maandiko matakatifu.Maajenti wa shetani waliowekwa
  wazi na SUNGURA wamejikita ndani ya Elimu kuhusu Mungu ili kuyapotosha maandiko ya Mungu.Lengo ni kuukata vipande vipande
  mwili wa Kristo.

  6.THEOLOJIA ni mpango wa Mungu lakini kwa kiasi kikubwa umegeuzwa kuwa mpango wa shetani na maajenti wa shetani.Wapo
  wengi ambao wamesoma Theolojia kwa bidii sana lakini haya MAPUNGUFU haya hawayatambui.Bila shaka wateule wanao soma na
  walio soma Theolojia ya maajenti wa shetani WAMEKUWA MZIGO
  USIOBEBEKA NDANI YA KANISA LA KRISTO.Ni mpaka pale watakapo
  jitambua kiroho ndipo watafanyika faida kubwa kwa kanisa maana watakuwa wameyajua mema na mabaya.

  7.Kwa sasa kwa kuwa Bibilia nyingi zina kupunguzwa kwa maandiko
  na hawa wataalamu wetu.Muongozo wa Roho Mtakatifu ni kwamba
  tunatakiwa kusoma version mbalimbali za Bibilia ili kupata kitu kamili.
  Hivyo ndivyo waalimu makini kama kina MWAKASEGE wanavyoongozwa
  kufanya.SAMILEANDER ameeleza kuhusu hili tena kwa mfano halisi
  wa namna uandishi na tafsiri ya MATHAYO 20:22,23 katika Bibilia za
  kiswahili ulivyo tofauti na Bibilia za kiingereza kama vile NEW KING
  JAMES VERSION.Mimi niliyonayo ni RED LETTER EDITION.

  8.YEREMIA 17:5 inasema ” ……..Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye
  mwanadamu kuwa kinga yake na moyoni mwake amemuacha BWANA”
  Na MITHALI 3:5-6 inasema “Mtumaini BWANA kwa MOYO WAKO WOTE
  wala USIZITEGEMEE AKILI ZAKO MWENYEWE.Katika njia zako zote
  mkiri yeye, naye atayanyosha MAPITO YAKO”.Tukiunganisha na 1 YOHANA 2:20,27 ndipo tunapopata JIBU KWAMBA PAMOJA NA MAPITO(changamoto) tulizo nazo kuhusu THEOLOJIA bado ROHO
  MTAKATIFU ndiye anayepaswa kutufundisha HABARI ZA MAMBO YOTE
  kuhusu mapungufu ya Theolojia na KUTUELEKEZA NINI CHA KUFANYA.
  MALUMBANO YANAWAPA NAFASI MAAJENTI WA SHETANI KUENDELEA KUTUGAWA.Maombi ya Yesu kuhusu UMOJA WA WATEULE YALISHAJIBIWA kwa Mungu kutupa hekima,maarifa na fedha
  za KUULINDA UMOJA WA KANISA LAKE(MUHUBIRI 7:12,HABAKUKI 2:14).

  9.Tuepeke kupokea ‘MAFUNDISHO YA FEDHA NA DHAHABU SAFI’
  na badala yake tupokee mafundisho ya Roho Mtakatifu ambayo
  ni zaidi ya fedha na dhahabu.Ndani ya neno la Mungu kuna fedha
  na dhahabu zinazotupa maisha marefu yenye afya na amani ya Kristo
  (TAFAKARI SANA HAGAI 2:5-9).

  HITIMISHO
  UTUKUFU wa mwisho wa wateule wanaojitambua ndani ya neno
  la Mungu utakuwa mkuu kuliko ule walioanza nao.Huu ni unabii wako
  kwa ajili yako na vizazi vyako.Ni unabii wa kanisa na Taifa la TANZANIA.

  Mungu akubariki sana mteule popote ulipo.

  MACHO YA MIOYO YETU NA YATIWE NURU NA TUTEMBEE NA ROHO
  YA HEKIMA NA UFUNUO(WAEFESO 1:17-19).

 29. Lwembe,

  Jibu ni kwamba, kama ambavyo aliyeokoka hawezi kufanya ibado kwa wasabato wala kwa wakatoliki, hata suala la chuo cha Theology haiwezekani.

  Lakuni pia kwa maana ya kibiblia ya mkristo, lazima awe amezaliwa mara ya pili!

 30. Wapendwa.
  Shalom.
  Nimeipenda sana hii Kutoka SG ” DON’T TRY TO BE SEEN , GOD MAY BE HIDING YOU ON PURPOSE”.
  ***Hii ni siri kuu, Mungu akikuficha jambo HATA UJITAHIDI VIPI,HUTAIPATA NG’O.***
  AMINA.

 31. Sungura,

  Katika jambo hili la Teolojia na umaarufu wake, kabla ya kuendelea ktk majadiliano haya, napenda nikuulize jambo moja, Je, mchungaji wa Kipentekoste, anaweza kupelekwa kusoma Teolojia ktk chuo cha Kikatoliki au Kisabato? Tukichukulia kwamba wote ni Wakristo!

  Gbu!

 32. Pendael,

  Hata usipate shida, wewe endelea tu na business zako.
  Nilishajua uwezo wako wa kufikiri pamoja na mlengo wako wa kuyaona mambo.

  Hata siwezi kuhangaika na wewe.

  Pengine nikushukuru kwa kutuletea mada, japo uliileta ukiwa unataka kusimamisha mtazamo fulani wa kwako ambao ni finyu sana.

  Wengine kazi yetu hapa ni kujaribu kunyosha kile ambacho kimepinda(kama huo mtazamo wako), ili kusudi watu wa Mungu wa hili kanisa la SG na mtandao kwa ujumla wasipotoshwe.

  Hivyo tunatumia kile cha kweli tunachokijua kuhakikisha hili linafanyika kikamilifu. Kikija kitu tusichokijua mimi binafsi hicho humwachia Roho mt.na wale wanaokijua kiusahihi washughulike nacho.

  Kwa wale waungwana wa hapa SG ambao tumezoeana kama hao akina Lwembe, Ziragora,Siyi, Seleli, Mjema, Millinga, n.k, huwa hatuogopi kulazimishana kuwa nataka unijibu hoja fulani.

  Kwa hiyo wewe kama si miongoni mwa hao wenye utamaduni wa hapa wala usipate shida, acha tu usijibu nilichokuta kunijibu. Hata hunipi shida yoyote.

  Lakini ukisema kisicho sahihi lazima nitakujibu moja kwa moja tena kwa kukutaja na jina lako.

  Uwe na amani!

 33. Samileander,

  Nikupongeze kwa kuonesha umuhimu wa shule. Japokuwa anawaambia watu wengine wajiepushe na Theolojia huku wew mwenyewe ukiwa unaongea Theolojia.

  Ni sawa na mtu anayewaambia watu wajiepushe na wakristo huku yeye mwenyewe akiwa mkristo. Kumbe alitakiwa kuwaambia watu wajiepushe na wakristo wa uongo.

  Huwezi ukawa nabii halafu ukawa unaambia watu wajiepushe na manabii. Maana yake unawaambia wakuepuke na wewe mwenyewe. Kumbe ulipaswa kuwaambia wajiepushe na manabii wa uongo.

  Ndio maana mwanzoni nilimtaka mleta mada atuambie nini maana ya Theolojia. Ingemsadia yeye mwenyewe kwanza na kuwasaidia wengine wasiojua uhusika wao ktk Theolojia.

  Ni sawa na kuwatangazia watanzania kuwa wajiepushe na siasa. Bila kujua kuwa kumbe unawaambia wasiende kupiga kura kuchagua viongozi, unawaambia wasigombee nafasi za uongozi, wasiwasikilize viongozi wa nchi, n.k. Maana hayo yote ndio yanayofanywa katika siasa au hayote ndio siasa imebeba.

  Kumbe ulipaswa kuwaambia wajiepushe na siasa zisizofaa, siasa chafu, siasa za uongo, siasa za uchochezi, n.k.

  Kuna watu wameingia kwa nia mbaya, wanatumia vibaya kitu kinachoitwa Elimu kuhusu asili ya Mungu (Theolojia). Wao ni maajenti wa shetani, wanajaribu kupindisha mambo mazuri kwa kupitia kitu kizuri kinachoitwa Theolojia.

  Kwa hiyo kwa lugha sahihi hao wamaitwa wanatheolojia wa uongo.

  Ni sawa na watu wanaojaribu kumtumikia shetani kwa kutumia kitu kizuri kinachoitwa unabii. Wanachofanya ni kutumia loophole zilizo kwenye hii huduma ya kinabii kufanya mambo yao.

  Watu kama hawa wanatakiwa kushughulikiwa na watu wa kweli(manabii wa kweli) walio kwenye hii huduma ya unabii, sio kuwashugulikia kwa kuwatangazia watu wajiepushe na unabii.

  Wanatheolojia wa uongo wanashughulikiwa na wanatheolojia wa kweli. Watu wanaojua nini kizuri kilichoko kwenye theolojia. Maana mwanatheolojia wa kweli lazima awe amejawa na Roho mtakatifu, ndipo aweze kumjifunza Mungu sawasawa.

  How do u know kuna maneno yaliyonyofolewa kwenye maandiko ya biblia na wanatheolojia wa uongo kama wewe si mwanatheolojia wa kweli?

  How do u know kuwa kuna upungufu uliofanywa na wanatheoloji wa uongo katika matoleo fulani ya biblia kama wewe si mwanatheolojia wa kweli?

  Samileander umeyajua hayo yote uliyosema hapa kwa sababu umeamua kufuatilia kwa kujifunza, umeamua kusoma maandishi, ndipo ukagundua ala kumbe kuna maneno yameachwa kwenye gili toleo la biblia!

  Hujayajua hayo kwa kufanya maombi marefu.

  Daniel aligundua ukomo wa miaka ya Israel kukaa utumwani Babel kwa kusoma vitabu, ndipo akiwa anasoma akakutana na unabii wa Yeremia.

  Kwa wasiojua, tafsiri za kwanza kabisa za biblia ya Kiswahili zilifanywa na wakoloni, na waliwatumia hata waislam walikuwa wanajua Kiingereza na Kiswahili kufanya hiyo tafsiri.

  Ndio maana kuna mpaka maneno shehe, iddi, haramu, msikiti, n.k.
  Na uwepo wa maneno haya umetumika vibaya sana na waislam wanaofanya midahalo ya kupinga ukristo.

  Utakuta wanakubana kuwa Yesu aliigia kwenye sinagogi, na sinagogi maana yake ni msikiti, na mtu anayeingia msikitini ni mwislam, lwa hiyo Yesu alimuwa mwislamu. Halafu mpendwa unabaki unag’aa macho tu.

  Sasa hatuwezi kuyajua haya kwa kufanya naombi, bali ni kwa kusoma maandishi, na historia. Na huko ndilo kunaitwa kujifunza elimu kuhusu Mungu, yaani Theolojia.

  Acha niweke koma hapa.
  Haija-editiwa.

 34. Sungura,
  Huwezi kunilazimisha nikujibu.Kama wewe ni mtu mzima akili yako ikusaidie!!

 35. HIVI MWANATELOJIA ALIYEBADILI TAFSIRI HII HAPA CHINI ALIDHANI KUWA ATATUFICHA WANAOMWABUDU DIANA NA JUPITER LEO KWA KUONDOA.

  ACTS 19:35

  AND WHEN THE TOWNCLERK HAD APPEASED THE PEOPLE, HE SAID, YE MEN OF EPHESUS, WHAT MAN IS THERE THAT KNOWETH NOT HOW THAT THE CITY OF THE EPHESIANS IS A WORSHIPPER OF THE GREAT GODDESS DIANA, AND OF THE IMAGE WHICH FELL DOWN FROM JUPITER?

  – KING JAMES BIBLE “AUTHORIZED VERSION”, CAMBRIDGE EDITION

  KUJA KISWAHILI KUWA HIVI;

  MATENDO 19:35
  “NA KARANI WA MJI ALIPOKWISHA KUWATULIZA WATU, AKASEMA, ENYI WANAUME WA EFESO, NI MTU GANI ASIYEJUA YA KUWA MJI WA EFESO NI MTUNZAJI WA HEKALU LA ARTEMI, ALIYE MKUU, NA WAKITU KILE KILICHOANGUKA KUTOKA MBINGUNI.”

  HUYU MWANATEOLOJIA ANAYEANDIKA KITU KILICHOANGUKA TOKA JUU ALIDHANI ATAWAFICHA WATU JUU YA IBADA KWA JUPITER HII LEO KATIKA MAKANISA.

  PIA TUNAJUA ARTEMI NI KWA WAGIRIKI,DIANA NI KWA WARUMI,

  KWA NINI JUPITER NA DIANA WAFICHWE KATIKA BIBLIA ZA SIKU HIZI ZA KISWAHILI.

  WANATEOLOJIA WANAOFASIRI BIBLIA KAMWE HAWATAFICHA UKWELI KWA KTOA FASIRI ZAO KWA UFISADI.

 36. RADHA HALISI YA MAFUNGU HAYA KADILI YANAVYOSOMEKA KATIKA KING JAMES VERSION, YENYE RADHA YA BIBLIA ZETU ZA KISWAHILI ZA ZAMANI.
  ZIKITAJA NENO UBATIZO KATIKA

  MATHAYO 20:22,23 ZIMEKWENDA WAPI KATIKA BIBLIA ZA KISASA.

  KADILI YA HAPO AWALI MAFUNGU YA KIINGEREZA YA KING JAMES VERSION
  YAKO HIVI,YAKITUPA RADHA. ILE YA BIBLIA ZA KISWAHILI TULIZOTUMIA AWALI
  SIO ZA WANATEOLOJIA WA LEO AMBAO NENO UBATIZO HAWAJUI WALITAFSIRIJE/SIJUI WAMEFANYA MAKUSUDI KWA AJILI YA KUUNGANISHA MAWAZO YA MAKANISA?

  KJV
  22BUT JESUS ANSWERED AND SAID, YE KNOW NOT WHAT YE ASK. ARE YE ABLE TO DRINK OF THE CUP THAT I SHALL DRINK OF, AND TO BE BAPTIZED WITH THE BAPTISM THAT I AM BAPTIZED WITH? THEY SAY UNTO HIM, WE ARE ABLE.

  23AND HE SAITH UNTO THEM, YE SHALL DRINK INDEED OF MY CUP, AND BE BAPTIZED WITH THE BAPTISM THAT I AM BAPTIZED WITH: BUT TO SIT ON MY RIGHT HAND, AND ON MY LEFT, IS NOT MINE TO GIVE, BUT IT SHALL BE GIVEN TO THEM FOR WHOM IT IS PREPARED OF MY FATHER.

 37. WALE WANAOTUMIA BIBLIA ZA KIINGEREZA PIA KUWENI MAKINI NA WANATEOLOJIA WANAOBADILISHA BIBLIA WAKIPINGANA NA MAFUNDISHO YA ROHO WA MUNGU.

  NENO NEW VERSION, NEW EDITION,REVISED VERSION YAMETUMIKA KUBADILI MAANDIKO MATAKATIFU.

  LAKINI HAWATAWEZA MAANA WAFARANSA WALICHOMA BIBLIA MIAKA MITATU LAKINI HAWAKUWEZA. NENO L MUNGU LITATIMIA NA ROHO WAKE AKITUHAKIKISHIA KWELI YA YALE MUNGU ALIYOSEMA.

  IDADI YA MANENO ILIYOONDOLEWA NA WATU WAJIITAO WAJUZI WA INJILI KWA KUSOMEA

  1.NEW AMERICAN STANDARD IMEONDOA MANENO 909
  2.REVISED VERSION IMEONDOA 788
  3.NEW WORLD TRANSLATION IMEONDOA MANENO 767
  4.NIV IMEONDOA MANENO 695
  5.GOOD NEWS IMEONDOA MANENO 614
  6.AMPLIFIED IMEONDOA MANENO 484
  7.DOUAY(JESUIT BIBLE) IMEONDOA MANENO 421
  8.OLD JEHOVAH’S WITNESSES IMEONDOA MANENO 120
  9.NKJ IGNORED THE TEXTUS
  10.RECEPTICUS IMEONDOA MANENO 1200 TIMES

  HII INAATHIRI HATA WALE WATAKAOTAFSIRI KUTOKA KIINGEREZA KWENDA KISWAHILI

  MFANO.WAPO WATU KATI YETU BADO WANAISIFIA BIBLIA YA JEHOVA WITNESS
  AMBAYO KWA MFANO MDOGO TU.

  IMEONDOA: MARKO 16:9-20

  TEOLOJIA IMEONDOA UMOJA AMBAO WATU WANAOTAKA KUMJUA YESU WANGEUPATA, KWA KULETA FASIRI NDANI YA MAKANISA.

  TUKIJADILI HAPO TUKIWA NA BAADHI YA WATU WALIO KATIKA MPANGO WA OIKUMENE DIALOGUE WENYE MPANGO WA KUWEKA NEUTRAL MSIMAMO WA KIBIBLIA, WAKIUNGA MKONO KAZI YA SHETANI KUPITIA

  KJV
  22BUT JESUS ANSWERED AND SAID, YE KNOW NOT WHAT YE ASK. ARE YE ABLE TO DRINK OF THE CUP THAT I SHALL DRINK OF, AND TO BE BAPTIZED WITH THE BAPTISM THAT I AM BAPTIZED WITH? THEY SAY UNTO HIM, WE ARE ABLE.

  23AND HE SAITH UNTO THEM, YE SHALL DRINK INDEED OF MY CUP, AND BE BAPTIZED WITH THE BAPTISM THAT I AM BAPTIZED WITH: BUT TO SIT ON MY RIGHT HAND, AND ON MY LEFT, IS NOT MINE TO GIVE, BUT IT SHALL BE GIVEN TO THEM FOR WHOM IT IS PREPARED OF MY FATHER.

  KAMA BIBLIA ZETU ZA KISWAHILI ZILISEMA UBATIZO NIBATIZWAO MIMI NANYI MTABATIZWA.

  HIZI MATHAYO 20:22,23 MANENO YANAYOHUSU UBATIZO WANATEOLOJIA WAMEZIACHA WAPI KATIKA BIBLIA ZA KISWAHILI ZA SASA TOFAUTI NA ZA ZAMANI,

  MPANGO WA UMOJA WA MAKANISA NI KUONDOA MAMBO YOTE YANAYOLETA TOFAUTI YA IMANI, KAMA UBATIZO.
  NA MENGINE MENGI.

  HAWAJUI KUWA UMOJA WAKANISA UNAKUJA KWA KUTUMIA BIBLIA, YESU AKIWA MWALIMU,

  TUWENI KAMA WABEROYA TUSIPOKEE DOCTRINE ZINAZOTUNGWA KWA WELEVU WA WANATEOLOJIA.

  “WATU HAWA WALIKUWA WAUNGWA KULIKO WALE WA THESALONIKE, KWA KUWA WALILIPOKEA LILE NENO KWA UELEKEVU WA MOYO, WAKAYACHUNGUZA MAANDIKO KILA SIKU, WAONE KWAMBA MAMBO HAYO NDIVYO YALIVYO”
  MATENDO 17:11

  HATA VITA IFANYWE VIPI JUU YA NENO, DAIMA LITASIMAMA

 38. Samileander,

  Biblia nyingi kama s zote kuhusiana na Kutoka 20:17 zimesema OX au BULL.
  Ox ni ng’pmbe dume aliyehasia au Naksai kwa Kisw. Na bull ni ng’ombe dume ambaye hajahasiwa.

  Sasa unapolalama hapa kuwa mashahidi wa Yehova wamebadili tafsiri ni uongo wa wazi.

  Na tabia hii inasababishwa na kutojifunza kwa kufanya utafiti wa kutosha.
  Na tabia ya kutojifunza ni matokeo ya uvivu kwa kujiaminisha kuwa Roho atosha.

  Lakini ni matokeo ya kusoma source moja tu tena ya Kiswahili ambacho kimetafsiriwa kutoka lugha nyingine.

  Biblia kiasili iliandikwa katika lugha mbili; Kiebrania kwa agano la kale, na Kiyunani kwa agano jipya. So, ni vizuri kufanya utafiti toka huko kabla ya kulisema jambo hapa.

  Twendeni shule!

 39. Pendael,

  Kwa nini unapita pembeni? Mimi ndo nilikuuliza nini maana ya Theolojia, wala usiwe na sababu ya kuongea kwa mafumbo.

  Kama ukikuwa unajua maana yake ila hukutaka kujibu kwa sababu zako ungesema. Lakibi mpaka sasa nakuona bado hujui unachokisema.

  Fundisho la utatu haliko kwenye biblia na wala halijawahi kuwekwa. Kama wewe ulishawahi kusoma neno utatu mtakatifu tuoneshe.

  Kwa hiyo unalaumu watu kwa lawama isiyo haki. Na hata wewe unaposema kuwa bibilia iliandikwa na Roho mtakatifu, ni kujaribu kuwaingiza watu kulekule kama waliowafanya watu waamini neno utatu, maana hakuna huo mstari kwamba biblia iluandikwa na Roho mt.

  Na kiukweli kabisa ni uongo kusema kila neno lililo kwenye biblia lilisemwa na Mungu achilia mbali kuandikwa.

  Pia maelezo ya Lwembe kwa sehemu kubwa yako tofauti na mtazamo wako. Kaeleza kazi waliyo/wanayo-fanya wanatheolojia, lakini kasema shida na upungufu uko wapu kuhusiana nacqanagheolojia.

  Lakini wewe kazi yako imekuwa ni kutukana na kuponda Gheolojia katika ujumla wake kwa sababu ambazo hazina substance ya maana sana.

  Na mwisho, tunapojadili hapa hufika wakati mtu akakuuliza jambo, huwa ni muhimu kujibu, au kusema hutajibu kwa sababu fulani.

 40. Wapendwa;
  Shalom.
  Namshukuru Mungu Kuwa SG waliifanya Hii kuwa MADA japo ilikuwa ni mchango wangu kuhusu YESU,MUNGU NA ROHO MTAKATIFU na kwamba YESU NI MUNGU MKUU, NDIYE BABA,MWANA NA NDIYE ROHO MTAKATIFU. YEYE NI YOTE KATIKA YOTE NDANI YA YOTE,ALFA NA OMEGA.
  Wapo wachangiaji AMBAO kazi yao siku zote ni kuonesha umashuhuri kuwa WAO WANAJUA KILA KITU.
  Yupo muhubiri aliwahi kusema “Ukifika mahali unaona unajua kila kitu ndipo hujui kitu” na pia akasema “Mtilie shaka mtu anayejua kila kitu”
  Katika MADA hii mmeweza kuwaona watu ambao kazi yao ni kujionesha kuwa wao ndio WATAALAM na ndio pekee wanaojua kila kitu.
  Pia WAPO wale ambao Wamekuwa WANYOFU kwa kuliunga mkono NENO LA MUNGU.
  MASWALI YA UBISHI NILIYAEPUKA KIMAKSUDI KUTOKANA NA NIA YA WAULIZA MASWALI.
  Kwa mfano.
  Sikutaka kueleza maana ya teolojia kwa sababu naielewa vizuri na MADA hii imejikita kuonesha MAHALI TEOLOJIA ilipofikia na ukitaka kujua NIA YA WALE waliokuwa WANAULIZA MAANA YA TEOLOJIA NDIO WALE WALE WALIOKUBALI MAELEZO YA NDG LWEMBE BILA UBISHI WOWOTE.
  Swali, HAWA Waliouliza MAANA YA teolojia walikuwa hawajui maana ya teolojia au walitaka kubishana au kutafuta umaarufu?
  Maelezo yangu ya AWALI YALIWAONESHA WATU WA AINA MBILI waliohusika katika suala zima la Kufasiri Maandiko Matakatifu. (REJEA MAELEZO HAPO JUU)
  ” KUANDIKWA NA KUTAFSIRIWA KWA BIBLIA.
  -Bila shaka Wakristo wa kweli wanajua kuwa BIBLIA iliandikwa na watu Walioongozwa na ROHO MTAKATIFU, kwa maneno mengine Mwandishi wa BIBLIA ni ROHO MTAKATIFU.
  -Waliotafsiri BIBLIA wapo katika makundi mawili;
  (A) Kundi la kwanza ni la wale waliotafsiri BIBLIA wakioongozwa na ROHO MTAKATIFU
  (B) Kundi la Pili ni la wale waliotafsiri BIBLIA wakiongozwa na roho wa Ibilisi
  Ndio maana wamebadili maana ya asili ya maneno ili kukidhi haja za mioyo yao kama vile Mafundisho ya nafsi tatu za Mungu.”
  HIVYO SI WAFASIRI WOTE WALIOONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU.
  Hakika MUNGU ameahidi KUMTETEA Mtu atakayemtetea. HIVYO NASHAWISHIKA KUSEMA WOTE WALIOWEKA UMAARUFU KANDO NA KULITETEA NENO LA MUNGU HAWATAKOSA THAWABU.
  Pia wale waliojitokeza kulipiga vita NENO siku moja WATAKUTA NENO LIKIWAPIGA VITA.
  SI WAKATI WA KUBISHANA NA MTU AWAYE YOTE.
  MITHALI 27:22 ” Hata ukimtwanga mpumbavu kwa mchi kinuni pamoja na ngano;
  Upumbavu wake hautamtoka”.
  AMINA.

 41. Hahahahaaaaa…..uwuwiiiii!
  Simaleander!

  Nakushukuru sana kwa hii coment yako, maana imenifanya nicheke, halafu nikasirike, kisha nihuzunike.

  Kumbe wewe ni mburula kabisa pamoja na hao rafiki zako.
  Nilidhani tunahangaika na watu wenye ufahamu lakini hawaelewi tu, kumbe tunahangaika na mburula kabisa.

  Tafadhali rudi darasani ukasome ujue hata lugha angalao. Maana haihitaji kwenda kusona Theologia kujua kilichosemwa kwenye Kutoka 20: 17.

  Hata mtu asiye na elimu ya Mungu ila ana elimu ya kawaida tu akisoma lazima aelewe.

  Unachotaka kutudanganya tuwakasirikie mashahidi wa Yehova kiko wazi mno.
  Maana biblia imesema hivyohivyo kama ambavyo biblia yao umesema imesema.

  Hakuna biblia ambayo mimi nimesoma imesema …wala ng’ombe wake, bali nyingi zimetumia neno “Ox na bull”

  Ox siyo ng’ombe tu, ni ng’ombe dume aliyehasiwa au “maksai” kwa Kisw. Bull ni ng’ombe dume.

  Jiongezeni kiufahamu ili msiendelee kutupotezea muda na kutusumbua hapa, kwa sababu ya uvivu wenu wa kujifunza.

  Nendeni shule mkaondolewe ujinga katika vichwa vyenu, Mungu hafanyagi kazi na wajinga.

  Huna hata aibu mwanaume mzima unaleta jambo ambalo hujalifanyia uchunguzi hata chembe, halafu unalalama utadhani una hoja ya maana kumbe upuuzi tu.

  Hapo mlipo mnajiaminisha kuwa mna sifa za kuwa walimu, lakini kwaanza ndo mnahitaji maziwa. Na hii inatokana na uvivu wenu wa kujifunza.

  Mtu unasomaga biblia ya Kisw tuu, tena Kisw chenyewe ni kile cha zamani cha Kimvita, halafu unasimama mbele ya wanaume kuleta hoja ya kisomi, si ni aibu ya mwaka hiyo!

  Sina budi kuwapuuza kwa kweli!

 42. WAPENDWA WANATEOLOJIA WENGINE WAMELETA MAMBO YASIYOPENDEZA HATA WAPAGANI KUANZA KUUSHANGAA UKRISTO. NDIO WANAOLETA TAFSIRI BINAFSI ZA MAANDIKO.

  MIFANO YA KAZI ZA KUHARIBU ZA WANATHEOLOJIA.

  BIBLIA YA MASHAHIDI WA JEHOVA HUSEMA HIVI JUU YA AMRI YA KUMI.
  USIITAMANI NYUMBA YA JIRANI YAKO, USIMTAMANI MKE WA JIRANI YAKO; WALA MTUMWA WAKE, WALA MJAKAZI WAKE WALA NG’OMBE DUME WAKE, WALA PUNDA WAKE, WALA CHOCHOTE ALICHO NACHO JIRANI YAKO.” KUTOKA 20:17

  FASIRI YA HAPO JUU YASEMA TUSITAMANI NG’OMBE DUME, VP JIKE?

  FANANISHA NA HILI HAPA CHINI; AMBALO HUTAJA NGOMBE KWA UJUMLA.
  “USIITAMANI NYUMBA YA JIRANI YAKO, USIMTAMANI MKE WA JIRANI YAKO; WALA MTUMWA WAKE, WALA MJAKAZI WAKE WALA NG’OMBE WAKE, WALA PUNDA WAKE, WALA CHOCHOTE ALICHO NACHO JIRANI YAKO.” KUTOKA 20:17

  NENO LA MUNGU SI MALI YA WAFASIRI WA BIBLIA NA WANATEOLOJIA, HATA KAMA WANAFASIR, KAZI YA MUNGU HAIFANYWI KWA UZEMBE, HATA BILA WANATEOLOJIA NENO LA MUNGU LITAHUBIRIWA ULIMWENGU WOTE.

  BIBLIA ILIYOANDALIWA NA VIONGOZI WA KANISA KUBWA NCHINI TANZANIA LINALOAMINI IBADA KWA WAFU

  WANATEOLOJIA WALIVYOBADILI;

  LIMEBADILISHWA “…WALA MTU AWAOMBAYE MAHOKA,MIZIMU.” KUMB 18:11

  “ASIONEKANE KWAKO MTU AMPITISHAYE MWANAWE AU BINTI YAKE KATI YA MOTO, WALA MTU ATAZAMAYE NYAKATI MBAYA, WALA MWENYE KUBASHIRI, WALA MSIHIRI, WALA MTU ALOGAYE KWA KUPIGA MAFUNDO, WALA MTU APANDISHAYE PEPO, WALA MCHAWI, WALA MTU AWAOMBAYE WAFU.” KUMBUKUMBU LA TORATI 18:10-11

  MUNGU HAKUWATUMA KUHARIBU NENO, WALA SHUKRANI YA INJILI HAIENDI KWA BINADAMU, MUNGU NDIO HULISHA WATU WAKE MKATE USIOTIWA CHACHU.

  LISILOTOKA KWA BABA ROHO ATAWAAMBIA

 43. Samileander,

  Sidhani kama mtu mtaweza kumdanganya hapa, labda yule aliyekwishs danganyika tayari.

  Theology siyo kinyume cha kuongozwa na Roho mtakatifu, na kuongozwa na Roho mt.siyo kinyume cha Theologia.

  Kwa nini kama Theology inawakela mnatumia matunda yake, huko kama siyo kupungukiwa ufahamu ni nini?

  Biblia hiyo unayosoma kakikuwa kitabu cha kujisomea jwa maana ya kufanya study. Maandishi yake hayakuwa na mistari(verse), bali ilikuwa imeandikwa kama riwaya.

  Ni wanatheologia waliweka hiyo mistari ili watu tuweze kufanya rejea kwa urahisi.

  Bila shaka nawe biblia yako ina vitabu 66, sasa sijui kwa nini unatumia hiyo biblia wakati unajua kuna baadhi ya vitabu kama Wamakabayo, Judith viliondolewa.

  Wanatheolojia wamekutafsiria biblia katika lugha ya mama yako, ulitakiwa lazima ujue Kiyunani ili kulisoma agano jipya, na ujue Kiebrania ili kulisoma agano la kale.

  Inawezekana kuna jambo mnataka kuwasilisha, lakini kwa sababu ya kukosa ufahamu wa kutosha mmeshindwa jinsi ya kuliwasilisha, matokeo yake mnaongea nonsense za kutosha tu!

  Kwa nini mnafurahia matunda yao kama ni watu wasiofaa.

  Yesu hakuwahi kuwalaumu mafarisayo na masadukayo kwa sababu ya udarisayo na usadukayo wso. Bali aliwalaumu kwa sababu waliacha mambo ya adili na kukomaa naepesi.

  Hivyo akawataka washike yote.

  Wewe ambaye wanatheolojia wamekuletea biblia mpaka mlangoni kwako, leo unaanza kuwaona hawafai!

  Hizo huwa ni tabia za mtu aliyeshiba, bila kujua alichoshiba kimetengenezwa na nani!

  Mnatukana mambo msiyoyajua, kaeni chini mjifunze mpate maarifa!

 44. Wapendwa wateule
  Namshukuru sana Mungu kwa kuwa anaendelea kunifundisha mengi
  hapa na toka nimeanza kutembelea hii blog nimepandishwa viwango
  kwa kujifunza nini maana ya werevu na upumbavu.Lakini pia kuna mengi
  mazuri na mabaya ambayo nilikuwa siyajui kuhusu THEOLOJIA.Roho Mtakatifu ni mwalimu wa ajabu sana anaweza hata akakufundisha jambo
  ambalo limo moyoni mwa mtu ambalo bado hajalinena!!!KWA SABABU
  UPUMBAVU WA MUNGU UNA HEKIMA ZAIDI YA MWANADAMU, NA
  UDHAIFU WA MUNGU UNA NGUVU ZAIDI YA WANADAMU(1WAKORINTHO 1:25).

  NAOMBA KUONGEA NA YAKOBO(ISRAELI)
  Hebu wewe Yakobo kaa kitako nikuulize jambo ambalo pengine hujawahi
  kujiuliza!Ni kwanini Esau alikuuzia uzaliwa wake wa kwanza tena kwa chakula? Ina maana huo uzaliwa wa kwanza kwa haki ulikuwa wake au wako? Ndiyo! Nauliza hivyo kwasababu MUNGU AMESEMA NIMEMPENDA
  YAKOBO NA ESAU NIMEMCHUKIA! Kwani wewe Yakobo ni bora mbele za
  Mungu kuliko ndugu yako Esau? Ni kwanini Mungu alihakikisha anakupa
  mtihani ili ukifaulu akuite ISRAELI?Wewe Yakobo unajua ni kwanini Roho
  Mtakatifu alikuongoza kuinama mpaka nchi mara saba mbele za GAIDI Esau
  na kama haitoshi ukamwambia kuwa kuuona uso wake ni kama kuuona
  USO WA MUNGU!!? Hongera sana Yakobo lakini nakuomba utafakari sana
  haya maswali.Lugha na mafumbo ya Mungu hufumbuliwa na watu wanaoongozwa na Roho wa Kristo na siyo watu wanao tawaliwa na roho
  ya shetani.

  NI KWANINI NIMEULIZA HAYA MASWALI
  Ni kwa sababu naona pamoja na kwamba Esau alijikataa na kisha akakataliwa kwasababu ya unabii ambao Mungu alimpa mama yake
  tangu akiwa mjamzito(MWANZO 25:21-23), bado Esau analeta usumbufu
  kwa kutumia kiburi cha shetani ili amkoseshe Yakobo!Hata hivyo hekima
  ya shetani ni zaidi ya upumbavu.Hila na mitego ya watu wenye kiburi
  imegeuka kuwa majivu.Wateule wameshaelewa NI KWA KIASI GANI
  THEOLOJIA AMBAYO NI MPANGO WA MUNGU IMEGEUZWA KUWA MPANGO WA SHETANI.

  JAMBO LA MSINGI inabidi tujipange ili kuhakikisha THEOLOGIA ile ambayo
  Mungu alikuwa ameikusudia inarudi.Asante sana mtumishi LWEMBE,SUNGURA na wengine kwa upendo wenu wa kunipa Mtaji wa ajabu wa kuendelea kulitazama hili suala kwa UNDANI ZAIDI huku nikiwa nimemshika mkono Roho Mtakatifu.Yesu anasema katika MITHALI 8:12
  “Mimi, Hekima, nimefanya werevu kuwa kao langu.Natafuta maarifa na busara” na katika MITHALI 8:14 anasema “Shauri ni langu, na maarifa yaliyo sahihi.Mimi ni ufahamu, mimi nina nguvu”.Yesu anacho maanisha
  hapa ni kwamba TUNAWEZA TUKAWA NA UFAHAMU,MAARIFA NA BUSARA KATIKA JAMBO FULANI LAKINI KUMBE SIYO UTAJIRI SAHIHI!
  Tunaweza tukawa werevu lakini kumbe ni werevu usio sahihi!Tunaweza
  tukajiona tuna nguvu kumbe sisi ni wadhaifu.ANACHOSEMA YESU HAPA
  NI KWAMBA NI LAZIMA TUTOFAUTISHE KATI YA MAARIFA YA MUNGU(Maarifa yaliyo hai) na MAARIFA YA SHETANI(Maarifa yaliyo kufa).

  NI LAZIMA TUPATE MAARIFA SAHIHI KUHUSU THEOLOJIA.MITHALI 8:1-36
  YESU ANAJITAMBULISHA NA KUONGEA MAMBO YA KUTISHA KUHUSU
  THEOLOJIA AMBAYO HAINA MUONGOZO WA ROHO MTAKATIFU!!
  MSTARI WA 35 na 36 ANASEMA KWA KUWA HAINA UZIMA NDANI
  YAKE,HAINA KIBALI MBELE ZAKE NA IMEHARIBU NAFSI ZA WATEULE
  WENGI.

  NI MUHIMU TUKAJUA HILI!
  Mteule anayeongozwa na Roho Mtakatifu kusoma THEOLOJIA anaweza
  kuwa na mafunuo mengi zaidi katika Bibilia.Ni nafasi ambayo hata mimi naitamani sana lakini Mungu hajanipitisha katika mfumo huo.Wana theolojia
  wanaongozwa na Roho Mtakatifu wanaweza kuwa na wigo mpana zaidi
  wa kuelezea matukio yaliyo ndani ya Bibilia na hata kulichambua Neno la
  Mungu.Hata hivyo jambo linalonishangaza ni kuwa kuna wateule ambao
  hawajasoma theolojia kama Mwalimu Mwakasege wana uwezo wa kutisha
  katika kuelezea matukio na kuchambua Neno la Mungu!
  Si ajabu nikiambiwa kuwa hata mtumishi kama Lwembe hajasoma THEOLOJIA!pamoja na kwamba anatoa maelezo ya kina kuhusu undani
  wa theolojia.Ndiyo maana 1WAKORINTHO 12:11 inasema “LAKINI KAZI HIZI
  ZOTE HUZITENDA ROHO HUYO MMOJA,YEYE YULE,AKIMGAWIA KILA
  MTU PEKE YAKE KAMA APENDAVYO YEYE”

  MSIMAMO WANGU KAMA ASKARI WA YESU
  Sipambani katika ulimwengu wa damu na nyama bali napigana vita
  katika ulimwengu wa roho(WAEFESO 6:12).

  NI NANI MWENYE UJASIRI WA KUPAMBANA NA YESU USO KWA USO?
  Hekima na Maarifa ya moto ulao yataendelea kutamalaki.Yesu anawatafuta wateule wake.

 45. Mrs. Christina,

  Unapoteza muda, zama za ujinga wa mambo kama ya kwako zilishapita zamani sana.

  Zama za kuongea maluelue ili kuwatisha watu wadhani uko rohoni sana, na mwisho wake kuwafanya mateka wa kiufahamu kwa jina la imani.

  Hebu jitathmini mwenyewe, umeongea nini sasa, au unadhani mambo ya Mungu ni mambo yasiyo-make sense?

  Uwanja ambao shetani hupenda kupigia jaramba kwa bidii sana unaitwa UJINGA. Na ujinga huondolewa kwa kujifunza maarifa.
  Na Mungu huwa hamtumii mtu mjinga, ukiona mjinga anatumiwa na Mungu chunguza vizuri, unaweza ukakuta siyo Mungu anayefanya kazi ndani ya huyo mtu.

  Mungu ni superinelligent, hivyo hawezi kutumia mtu ambaye ni superignorant. Labda kama anataka kutimiza suala la kijinga tena kwa mtu mjinga. Kama alivyotumia pepo kumdanganya Ahab.

  Kumbe bado mpo watu ambao hudhani kuwa kuongea mambo yasiyoeleweka ndio kuaminiwa kuwa mnatumiwa na Mungu!

  Tena afadhali yasieleweke kwa maana ya kwamba yako juu mno kiufahamu, lakini yasiyoeleweka kwa vile yako shagalabagala, ni ya kilopokaji zaidi, na hayana ukweli wowote wa Mungu ndani yake. Ni maneno holelaholela!

  Na hizi guts za kuandika hivi sidhani kama ni za mwanamke, nafikiri hata jina lako ni la uongo!

  Hata kupoteza muda kukwambia huu ukweli ni kujinyenyekesha kukubwa sana.

  Pole sana!

 46. WASOMI WA SHERIA NA WALIMU WA DINI HAWAKUWEZA MBELE YA ROHO ALIYESEMA NA STEFANO. TUOMBE KUFUNDISHWA NA ROHO MTAKATIFU.

  “LAKINI BAADHI YA WATU WA SINAGOGI LA MAHURU, NA LA WAKIRENE, NA LA WAISKANDERIA, NA LA WALE WA KILIKIA NA ASIA, WAKAONDOKA NA KUJADILIANA NA STEFANO; LAKINI HAWAKUWEZA KUSHINDANA NA HIYO HEKIMA NA HUYO ROHO ALIYESEMA NAE.” MATENDO 6:9,10

  KUSOMEA DINI, HAKUNA FAIDA KAMA ROHO HAKUKUMBUSHI KUNENA ULIYOJIFUNZA KATIKA NENO LA MUNGU, NAWE UKAOGOPA.

  TEOLOJIA HUJENGA MATABAKA KUWAWEKA WENGINE MABWANA WA KUTAFUNA INJILI WENGINE WAPOKEE MIDOMONI,

  KANISA LA RUMI LILIHARIBU UKRISTO KWA KUSEMA KARAMA YA KUFUNUA MAANDIKO NA KUFASIRI NI KWA WALE WALIOSOMEA TEOLOJIA, KISHA KUWANYIMA WATU KUSOMA BIBLIA NA KWALISHA YASIYOFAA. mPAKA WATU WALIPOANZA KUSOMA WNYEWE WAKAJUA UKWELI.

 47. NI LAZIMA TUSHINDANE NA MUNGU NA WANADAMU NA TUWASHINDE(MWANZO 32:24-28).

  Wapendwa wateule
  Hii mada ni nyeti sana inajenga uelewa mpana hasa katika nyakati hizi
  za hatari.Ni vyema tunapopata kibali kwa Bwana tukaelimishana kwa
  upendo na lengo hapa ni kujenga hasa katika kuhakikisha kanisa haliyumbishwi na MAPOTOVU.Kama Mungu aliye hai aishivyo,hizi ni nyakati
  ambazo shetani na wajumbe wake kokote walipo duniani wataendelea
  kuaibika,kufedheheka na kuangamia.Unabii wa Yesu katika LUKA 12:2 kwamba “…..HAKUNA NENO LILILOSITIRIKA AMBALO HALITAFUNULIWA
  WALA LILILOFICHWA AMBALO HALITAJULIKANA” umetimia na zaidi ya
  kutimia!Machozi ya Roho Mtakatifu ndani ya wateule yanalikomboa
  kanisa.

  Kama ambavyo nilisema na ninarudia tena kusema kwamba THEOLOGIA
  ni mpango wa Mungu lakini imeshageuzwa kwa asilimia kubwa kuwa mpango wa shetani ambaye anawatumia watumishi wake na hata watumishi wa Mungu kusambaza mapotovu.Duniani kuna watu wa aina mbili tu.Watu wema na watu wabaya(MITHALI 16:4) na watu wabaya(wasio haki) wamewazunguka watu wenye haki(Habakuki 1:4).Lengo la Mbwamwitu ni kutaka kuwageuza kondoo wananane nao.Kuna sababu kwanini Mtumishi Pandaeli amesema TUSIOGOPE VITISHO VYA WANA THEOLOGIA.Bila shaka Mungu ana sababu za kuliweka hili mezani.Kwahiyo
  tunatakiwa kuwa makini jinsi tunavyoliendea ili LENGO LA MUNGU KATIKA
  MADA HII LITIMIE.Infact hakuna anayeweza kulizuia maana naona limeshatimia.Wote wanaojaribu kushindana na Mungu wanaendelea kupondwa na RADI YA MIALE YA MOTO WA MAARIFA YA MUNGU kutoka
  mbinguni.Nawaona wanagalagala chini kama Esau na kizazi chake.Unyenyekevu wa Yakobo(Israeli) ulikisambaratisha kizazi chote cha
  Esau na huyo Esau mwenyewe alipigwa kofi la unyenyekevu walipokutana
  na Yakobo uso kwa uso.Haijalishi mbwamwitu waliokuzunguka ni wangapi
  kama vile Esau alivyomkabili Yakobo na watu mia nne,MTEULE SIMAMA NDANI YA UNYENYEKEVU WA YESU UTAUONA MKONO WA BWANA.
  Lengo hapa ni wateule wajue MAZURI NA MAPUNGUFU YA THEOLOJIA
  Ili wale walio na dhamiri njema wasimame katika NURU YA YESU.

  Maelezo ya mtumishi Lwembe na rtuo yamenipa PICHA KUBWA MNO
  na hivi karibuni dunia ya wajinga na wapumbavu wenye roho za kisasi na
  mauaji na walioshiba KIBURI CHA SHETANI, wakae mkao wa KUKABILIANA
  NA MOTO WA YESU USO KWA USO,MACHO KWA MACHO NA PUMZI KWA
  PUMZI.Dar-es-salaam imeshaanza kulipuka.Namuona Yesu anamnyanyua
  mtumishi wake na kusimama pamoja nae katika KUANGAMIZA MISINGI
  YOTE YA GIZA.

  Shetani na majeshi yake wanaogopa kuja duniani!Wataanzia wapi na huo
  ujasiri wataupata wapi wakati MOTO WA UNYENYEKEVU WA YESU UMETANDA KILA MAHALI(LUKA 12:49).Pamoja na upotoshaji ambao umekuwa mwingi KUSUDI LA MUNGU TANZANIA LINATIMIA MAPEMA
  HUKU MWAMWITU WAKISHUHUDIA KWA MACHO YAO.Manabii wa uongo
  wataendelea kuzikwa “kishujaa”!!!Hakuna mteule wa Mungu aliye mwaminifu atakaye kufa.Tukivipiga vile vita vizuri vya imani hakika tutahamishwa tu na kwenda kula RAHA na akina Mtume Paulo.

  Roho Mtakatifu anaendele kufichua mbinu na hila zote za watu wabaya
  na utafiti wanaoufanya ndani ya mitandao ya mitandao mbalimbali ya kijamii.MTEULE UWE MAKINI NA KILA MAFUNDISHO UNAYOYAPATA.SALAMU ZANGU ZIWAFIKIE MANABII WOTE WA UONGO
  AMBAO KWA HIYARI YAO WENYEWE WALIAMUA KUVUA NGUO ZAO NA KUNIONYESHA MAUNGO YAO.SIRI ZENU MLIZONIPA ZIMESHAIKOMBOA
  TANZANIA.

  HUU NI UTIISHO WA BWANA YESU AMBAO UNAWATANGULIA WATEULE KILA MAHALI(KUTOKA 23:27).

  ……….ZIMEBAKI SEKUNDE CHACHE………….

 48. Samileader,

  Theolojia ni nini?

  Na ulishawahi kujua ni lini vitabu vya Agano jipya vilianza kuwekwa pamoja na kuwa sehemu ya biblia?

  Ivi aliyetafsiri biblia kutoka Kiingereza kuja Kiswahili alikuwa ni nani, Roho mt.au nani?

  Hebu twende sawa hapo, ili sasa tushugulike facts, halafu nini ni nini!

  Nakungoja!

 49. Mrs. Christina,

  Nilikuwa nimekusubiri kwa muda, maana nilijua si muda mrefu utajifunua wewe ni nani.

  Ulijitahidi kujifichaficha ili ukwepe kupewa kinachokustahili kulingana na msimamo wako, ila sasa umeamua kujiweka wazi!

  Kuna kitu kingine bado unakificha, ila nacho joto likikuzidi utakifunua tu.

  Hongera kwa kuonyesha sasa uko upande gani!

  Nondo zitakufuata muda si mrefu!

 50. WANATEOLOJIA WENGI WANAWAFUNDISHA WATU VILE WANAVYOFIKIRI SIO NENO LISEMAVYO/ROHO ALIVOWAAMBIA WASEME, NA ROHO HUSEMA KUTEGEMEA KAMA UMELIHIFADHI NENO LA MUNGU YEYE AKUTUMIA KUFUNDISHA/KUHUTUBU.

  “MTU AWAYE YOTE AKIFUNDISHA ELIMU NYINGINE, WALA HAYAKUBALI MANENO YENYE UZIMA YA BWANA WETU YESU KRISTO, WALA MAFUNDISHO YAPATANAYO NA UTAUWA, AMEJIVUNA; WALA HAFAHAMU NENO LOLOTE; BALI WAZIMU WA KUWAZIA HABARI ZA MASWALI, NA MASHINDANO YA MANENO, AMBAYO KATIKA HAYO HUTOKA HUSUDA, NA UGOMVI, NA MATUKANO, NA SHUKU MBAYA.”

  1 TIMOTHEO 6:3-4

 51. MAMBO YANAENDELEA KUWA MATAMU ZAIDI!!!

  Naona upendo wa Kristo unatutafuna na inavyoeleke utatumeza kabisa!
  Kama kuna mtu dhalimu ambaye nimewahi kukutana naye ndani ya wokovu ni Yesu! Na udhalimu wa Yesu unaitwa UNYEYEKEVU WA KWELI(2WAKORINTHO 12:11-16).Unyeyekevu ‘upumbavu’ wa mtume Paulo ndiyo ilikuwa HILA iliyomfanikisha katika kuokoa roho zilizokuwa zinapotea.

  Sikiliza wapendwa,Mimi ninachotamani katika maisha yangu yote ni kuishi
  ndani ya UDHAIFU na UPUMBAVU wa Mungu(1WAKORINTHO 1:25).Udhaifu na upumbavu wa Mungu unaitwa UNYENYEKEVU WA YESU(WAFILIPI 2:3-8).Hata hivyo si rahisi kuishi ndani ya unyenyekevu wa Yesu,ni mpaka nikubali KUCHAPWA VIBOKO VYA MOTO WA ROHO MTAKATIFU.GHARAMA ya kuchapwa viboko vya moto wa Roho Mtakatifu
  ni kutokwa machozi na damu ya Yesu iliyomwagika pale msalabani(LUKA 22:41-44,MATHAYO 26:36-44).Roho yangu i radhi lakini mwili ni dhaifu kwahiyo nahitaji msaada wa nguvu ya Roho Mtakatifu.

  Mimi bado niko katika ngazi ya kuzaliwa mara ya pili.Hata hivyo kwa nguvu za Mungu ninaweka bidii mchana na usiku ili niingie katika ngazi inayofuata
  inayoitwa Unyenyekevu wa Yesu ili badala ya kuwa na kiburi kama cha Kaini,niwe mwanafunzi wa Yesu tena mwanafunzi kweli kweli(YOHANA 8:31-32).Nataka niifahamu KWELI ili hiyo kweli iniweke HURU.

  Ninaendele kujifunza mambo mengi hapa.Kwa macho ya rohoni naiona
  THEOLOJIA ikivuliwa nguo zote na kuachwa uchi kabisa.Tunapoongozwa
  na Roho Mtakatifu kunena au kufundisha jambo ina maana Roho Mtakatifu
  ndiye anayefundisha au kunena na siyo sisi.Kwahiyo hata kama kuna mtu
  ana maswali ya kuuliza inabidi amuulize Roho Mtakatifu na kama anataka
  kujenga hoja inabidi ajipange kukabiliana na Roho Mtakatifu.Mungu anazungumza lugha ngumu hapa lakini tukikubali kuitafakari itatuweka mahali pazuri sana.

  NI LAZIMA TUFIKE KATIKA NGAZI YA KUSHINDANA NA MUNGU NA WANADAMU NA TUWASHINDE!!(MWANZO 32:24-28).Ukikubali kuishi ndani
  ya unyenyekevu wa Yesu uwe na uhakika utamshinda Mungu na wanadamu!Mungu tusaidie una maana gani unaposema kwamba tunweza
  kushindana na wewe na kukushinda?

 52. Mrs. Christina,

  Kwenye vyuo huwa hawafundishwi elimu ya Theolojia, ispokuwa huwa wanafundishwa Theolojia!

  Pia, kitu unachokiita utulivu ktk comments, ni jambo la kihali(conditional). Kuna wakati maneno makali hutumika na wakati mwingine maneno ya unyenyekevu, lakini ukali wa maneno si lazima kuwa maana yake ni jaziba.

  Hata Yesu kuna wakati mwingi tu alitumia maneno makali na magumu.

  Binafsi hata Pendael sijaona kama ametumia maneno makali kiasi cha kunifanya nidhani ana jaziba.

  Lakini pia kiukweli, kwa habari ya watu kutumia neno la Mungu kutapeli, kati ya wanatheolojia wa uongo na waongo wanaojificha katika kufunuliwa, nafikiri wenye kudai wameongozwa na Roho wanaongoza kwa utapeli wa kutumia biblia.

  Tunamtazamo hasi tu kuhusu Theolojia bila kujua hasa kwa undani Theolojia maana yake nini!

 53. rtuo,

  Watu wabishi na wagumu wa kuelewa kwa kuwa hudhani wanajua kama alivyo Pendael, nawapenda sana kwenye mijadala hii.

  Mimi huwa siwaachi mpaka nihakikishe wameufahamu ukweli au wamekimbia.

  Pendael sintamwacha, mpaka nihakikishe akili yake imetia akili. Maana anayatukana mambo asiyonayo ufahamy wa kutosha.

  Watu wenye kujidai kuwa wao hawafundishwi na watu wengine ispokuwa hufundishwa na Roho mt. ndo mara nyingi hutengeneza imani potofu zenye madhara ya haraka ya kiroho na kimwili kwa wanaowafuata.

  Imani za watu kama Kibwetelele, hata hiyo imani ya Pool of siloam.

  In fact, hata uislam ulianzishwa na mkristo aliyekengeuka tu kuanza mafunuo akidai anaongozwa na Roho, wakampuuza na matokeo yake ndo hayo.
  Maana sehemu uislam ulikoshamiri ukisoma historia utagundua ni maeneo ambayo Mtume Paul alihubiri sana injili kabla ya hapo.

  Pendael kwenye comment ya Lwembe ameona hi ho tu cha mwisho angalao kidogo kinamfariji, japo na chenyewe content yake ya msingi si hiyo ambayo Pendael amekusema nayo.

  Ila pia najua comment ya Lwembe kwa sehemu kubwa imemvunja moyo Pendael kwa sababu alitegemea kuwa Lwembe angemsapoti kwa 100% lakini ikawa tofauti.

  Pendael hajui maana ya Theology, ispokuwa aliwahi tu kumsikia mwinjilisti wa kanisani kwao ambaye alishindwa kwenda shule, akisema kwenda shule ni kumzuia Roho mt.kukuongoza!

  Kuna watumishi wengi tu waliwahi kuwa na huu mtazamo, lakini mbio zao zikaishia sakafuni!

 54. KUSOMA TEOLOJIA HAKUTAKUSAIDIA KAMA HUJAPEWA ZAWADI YA UALIMU,KUHUTUBU NA ROHO MTAKATIFU

  “NAYE AMEMTILIA MOYONI MWAKE ILI APATE KUFUNDISHA, YEYE, NA OHOLIABU MWANA WA AHIMASAKI, WA KABILA YA DANI.”

  KUTOKA 35:34

 55. “NINAZO AKILI KULIKO WAKUFUNZI WANGU WOTE, MAANA SHUHUDA ZAKO NDIZO NIZIFIKIRIZO” ZABURI 119:99

  MSIWAOGOPE WANATEOLOJIA

 56. SASA TUNAELEKEA PAZURI!!
  Comments za watu zinaonyesha kuvaa hekima ya Yesu.Comments za watumishi
  rtuo,Harris,Sungura,Samileander na Lwembe zinaleta matumaini ya kujenga.Hata hivyo bila ya kuwa mnafiki comments za rtuo na Lwembe
  zimebeba UTULIVU WA KUTOSHA.

  Kwako Mtumishi Pandaeli,
  Suala la vyuo vya THEOLOJIA kupotosha neno la Mungu liko wazi sana
  kwasababu si wengi wanaompa Roho Mtakatifu(mwalimu) nafasi yake.
  Hili ni jaribu kwa wateule wote waliodhamiria kumuishi Mungu katika ROHO
  na KWELI.Maandiko matakatifu kwa kiasi kikubwa yamegeuzwa kuwa biashara haramu.Mlango wa kutokea katika hili jaribu ni kutafuta unyenyekevu wa kweli yaani maarifa na hekima ya Mungu katika kuliendea
  jambo hili na kama Yesu akitupa kibali cha kunena au kulifundisha tuwaweke wengine
  huru kweli kweli.Na hili litawezekana kama tukikubali kuendelea kuwa wanafunzi wa Yesu(soma Yohana 8:31,36).ELIMU YA THEOLOJIA kufundishwa vyuoni ni mpango wa Mungu lakini walio wengi wamegeuza
  umekuwa mpango wa shetani.Siwezi kuingia katika mtego wa kuwa na jazba katika hili wakati ninao mlango wa kutokea na kuwaeleza wateule kweli isiyopingika kwa upendo kabisa.

 57. Sokia,

  Hapawezi pakawa na wanafunzi pasipo mwalimu, hapawezi pakawa na wanafunzi na mwalimu pasipo kuwepo shule.

  Yohana alikuwa na wanafunzi, kw hiyo aliwafundisha, na hiyo ilikuwa ni shule/ chuo.

  Halikadhalika Yesu alikuwa na wanafunziwengi tu, nae alikuwa ni mwalimu aliyefundisha. Kwa hiyo waliokuwa wanafunzi wake walikuwa shuleni/ chuoni.

  Pendael yeye anataka aone mahali imeandikwa kuwa kulimuwa na majengo na mabweni ndo ajue kuwa wanafunzi wa Yesu walikuwa chuoni.

  Samileander, unaelewa maana ya hayo maneno kwamba watafundishwa na Mungu au unajisemea tu kwa vile imeandikwa?

  Hebu lifikirie agizo la Yesu kwa mitume… Enendeni ulimwenguni mwote mkawafanye mataifa kuwa wanafunzi wangu,…… MKIWAFUNDISHA kuyashika yote niliyowaamuru/ waagiza.
  Kama kazi ya kufundisha ni ya Mungu, mbona sasa anawaagiza hawa jamaa wakafundishe?

  Siyo vizuri kurukia tu kineno kimoja bila kujua maana yake hasa kw kufanya ufuatiliaji wa maneno mengine!

  Ukiwa hivyo unaweza ukafunua biblia ukakuta inasema ..” Yuda akajiua” halafu nawe ukaamini kuwa mambo yakikuzidia waweza kujiua maana kuna mfano wa mtu kujiua kwenye biblia!.

  Usomaji wa namna hiyo ni hatari sana!

 58. rtuo,
  Mbona uko “OP”?
  Unaniambia “Hivi unafikiri wahubiri wakubwa ambao walipakwa mafuta kama evangelist Dr Billy Graham walipita katika vyuo vya theology ”
  HILO LINA UHUSIANO GANI NA BIBLIA?TUMFUATE YEYE?
  SALA YA TOBA UNAYODAI NI SAHIHI UMEIPATA WAPI KWENYE BIBLIA? UKIAMBIWA NI TUNGO ZA WANADAMU WASIOONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU UNAKASIRIKA!!
  JIBU MASWALI KAMA ELIMU INASAIDIA KUMJUA MUNGU!
  HASIRA ZENU WANATHEOLOJIA NI PALE UNAPOAMBIWA TU THIBITISHA JAMBO HILO KIMAANDIKO,NDIPO HUANZA JAZBA.HILO HALISAIDII.
  Halafu umeniambia natumia Maneno makali na mipasho-HAYO NI MAONI YAKO.Yawezekana maswali ni magumu kiasi cha kutafuta mbinu ya kukimbia.

  HEBU SOMA HII ILIYOANDIKWA NA LWEMBE HAPO JUU ‘COMMENT’ YA MWISHO.
  ” Kwa kifupi tofauti ya Kanisa na Dhehebu ni moja tu, Msingi vilipojengewa; Kanisa limejengwa juu ya Msingi wa mitume na manabii, na Dhehebu limejengwa juu ya msingi wa Teolojia!”
  AMEN.

 59. @ kaka sungura naona ni vigumu pendael kusaidika. Kwanza ni mbishi, anauliza maswali ya kibishi. Maswali ya kibishi kujibika ni ngumu kidogo. Huwezi ukajifunza na ukaelewa kwa maswali ya namna hiyo

 60. Pandael,

  Ngoja tukwambie ukweli kwa upendo, kwamba unachokifanya hapa ni ujinga na hata hujajiandaa kujifunza.

  Maswali unayouliza ni ya kitoto sana, lakini hapo wew unajiona uko rohoni kuliko wengine.

  Kama umesoma vizuri comment ya Lwembe, ulitakiwa uwe umesaidika. Lakini nakuona hata huwezi kuielewa maana inawezekana kabisa imeupita mbali ufahamu wako.

  Lakin pia rtuo kakwambia vizuri kuwa kuna Theologia ya uongo na Theologia ya kweli.
  Just kama ambavyo kuna manabii wa uongo na manabii wa kweli!

  Kwanza hata sijui ni kitu gani hasa unataka ku-communicate katika hii mada.

  Ni mtoto tu ndiye anaweza kuuliza swali kuwa Yesu alianzisha chuo gani.
  Ni sawa na kuuliza Yesu aliuanzisha lini ukristo.

  Kama unalenga kujifunza kweli soma vizuri mchango wa Lwembe na wa rtuo kwa sehemu.

  Vinginevyo kama hutaki kujifunza utazidi kutusumbua kwa mambo ya kitoto.

  Ila jua hatutakuacha utudanganye!

 61. “IMEANDIKWA KATIKA MANABII, NA WOTE WATAKUWA WAMEFUNDISHWA NA MUNGU. BASI KILA ALIYESIKIA NA KUJIFUNZA KWA BABA HUJA KWANGU”
  YOHANA 6:45

 62. “IMEANDIKWA KATIKA MANABII, NA WOTE WATAKUWA WAMEFUNDISHWA NA MUNGU. BASI KILA ALIYESIKIA NA KUJIFUNZA KWA BABA HUJA KWANGU.”
  YOHANA 6:45

 63. Harafu unapotetea hoja yako punguza kutumia maneno makali na mipasho ya hapa na pale. Haikusaidii sana@ pendael

 64. Hivi unafikiri wahubiri wakubwa ambao walipakwa mafuta kama evangelist Dr Billy Graham walipita katika vyuo vya theology wewe mtazamo wako ni kuwa theology ni false kwasababu umezama huko. Hivi unafikiri vyuo vya uchungaji Hata vya makanisa ya pentecostal wale wachungaji wanafundishwa mini hasa. Somo biblia yako uone kulikuwa na vyuo vya manabii. Kwa vile wakati wa Yesu hakukuwa na hivi vyuo hoja yako bado iko poor. Ni sawa sawa na kuuliza sala ya toba ipo wapi katika biblia. Hakuna mahali tunaona kuna sala ya toba lakini tunaona tunaitumia wakati huo. Hii ina maana kuna mambo ni kweli hayakuwepo wakati wa Yesu lakini bado tunapokea mafunio ya ki Mungu na kuyatendea kazi. Hata akina Paulo walikuwa wanafundisha wanafunzi habari za ufalme wa Mungu na elimu ihusuyo ufalme wa mbinguni. Walitoa wapi hiyo elimu. Roho mtakatifu aliwafunulia nao wakawafundisha watu. Hata Yesu biblia inasema kuna wakati mafarisayo walijiuliza amepataje huyu kujua elimu ambayo hakusoma. Biblia inatumia neno elimu. Kina petro hawakuwa na elimu ya kujifunza Roho mtakatifu aliwafunulia na kuweka elimu ya Kimungu juu yao. Daniel pia alikuwa na elimu ya ki Mungu pia tena ya kusomea. Kwahiyo Roho mtakatifu anapoweka ufunuo wa ki Mungu ndani yako na akakufundisha hiyo elimu na wewe ukawafundisha watu hiyo doctrine sio vibaya. Kuna watu walifunuliwa na kupokea elimu ya ki Mungu imhusuyo Mungu wakawafundisha wengine. Doctrine hiyo ndio inaitwa theology. Uenda huelewi maana ya neno theology. Theology ni doctrine au fundisho au mafundisho yanayohusiana na elimu ya Mungu. Kuna elimu ya kidunia na kuna elimu ya ki Mungu. Theology isipofundishwa chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu inaleta uharibifu na kuingiza mambo au mafundisho ya kutunga au ya upotoshaji. Lakini ikifundishwa chini ya uongozi wa Roho na kuendana na biblia haina tatizo kabisa.

 65. WAPENDWA,
  Hebu tutafakari,
  1.Kama teolojia inaongozwa na ROHO MTAKATIFU mbona kila dhehebu linafundisha kivyake?
  2.Mbona wanatheolojia wakimaliza VYUO na wengine humaliza mpaka miaka saba huja na Mafundisho Ya Mpinga kristo? Mfano;
  a. Ubatizo wa watoto wadogo.
  b.Kipaimara
  c.Ibada za Kuombea wafu.
  d.Kuwafanya wanawake kuwa WAHUBIRI,MASHEMASI au WAZEE WA KANISA.
  e.Huwabatiza watu KWA JINA LA BABA NA MWANA NA ROHO MTAKATIFU kinyume na MITUME ambao walibatiza Kwa JINA YESU KRISTO ( MATENDO 2:38, 8:14-17, 10:48, 19:1-5,)
  f.Madai kuwa MITUME walifundisha kinyume Cha Bwana Yesu.
  g.Petro alikuwa papa wa kwanza wa dhehebu la Katoliki.
  nk.
  3.Wengi hutuambia kuwa YESU alisoma,mbona hawatuambii alisoma wapi mpaka darasa la ngapi?
  4.Mbona katika Maagizo Ya Bwana Yesu hakuna hata AGIZO MOJA kwa KANISA kuhusu kujenga Vyuo,hospitali au Shule? Bwana Yesu hakujua umuhimu wa elimu?
  5.Hawa MITUME wa YESU walisoma Chuo gani Cha BIBLIA?
  6.Dhehebu gani linafundisha teolojia kwa usahih?
  Haya ni baadhi tu ya mambo Ya kutafakari.
  Ahsante.

 66. rtuo,
  Hebu nipe mfano wa Chuo cha teolojia alichokianzisha Yesu.
  Pia nithibitishie CHUO hata kimoja kinachofundisha TRUE DOCTRINES.
  Inonekana hiyo mada hukuisoma vizuri NA KAMA UMEISOMA VIZURI hebu jitahidi kujibu maswali mengine si hilo moja tu ambalo kwanza huna nukuu ya BIBLIA zaidi ya kutumia tungo za watu.

 67. Harris,
  Sijaona umejibu maswali zaidi ya kujitetea sana.
  JIBU MASWALI KWA MTIRIRIKO KAMA ELIMU YAKO IMEKUSAIDIA KULIKO KUTOA MAELEZO YASIYO NA TIJA AMBAYO HUKUULIZWA.
  JIBU MASWALI,ACHA HADITHI.

 68. Ukiacha neno theology kuna maneno mengine yanatumika unapoongelea theology kwa upana wake. Maneno hayo ni kama vile christology, pheumatology ambayo ni doctrine of the holy spirit, angelogy ambayo ni the doctrine of angels, ecclesiology ambayo ni the doctrine of the church na eschatology ambayo ni the doctrine of the last things as it relate with second return of christ .

 69. Pandael neno theology maana yake kwa ufupi ni ” the doctrine about God. Kuna false theologians na true theologians. Any doctrine which is contrary to what the bible say that doctrine is false. Every doctrine which is allign itself with what the scripture say it is the good doctrine. A doctrine cannot be considered biblical until it takes into account all that the bible has to say about it

 70. Ametumia neno theology pasipo kujua maana Yake kwa undani. Pendael upo mis guided rudi kwanza katafute maana ya theology. Umeandika vitu vizuri ila kutojua maana ya neno moja ambalo ulitaka libebe mada yako imefanya mada yako yote iwe crack.

 71. Hata Mimi nilitaka kumuuliza maana ya thelogy . ametumia neno asilolijua matokeo yake amekuwa misguided na baadhi ya wapendwa wakimshangilia

 72. ……….naendelea,

  Lakini, Teologia, kimsingi ni mfumo kamili wa elimu unaojaribu kumpambanua Mungu au Uungu, kupitia tafiti na kusoma kwa nia ya kujifunza, huku ukiyafuatilia matukio na maelekezo mbali mbali kama yalivyorekodiwa ktk Biblia, ukijaribu na kuyaoanisha na historia za tamaduni husika ili kuipata maana kamili ya jambo, na pia kuyalinganisha na hayo yanayojiwakilisha kama “Kweli za Dini” kutoka tafakari tofauti zinazotokana na elimu hiyo hiyo!! Nayo Teologia hufundishwa ktk vyuo vikuu, seminari au shule za dini.

  “Kweli za Dini” ni mafundisho yanayojiwakilisha kama Neno la Mungu ambayo yameasisiwa na wakufunzi watafiti ktk fani hiyo ya Teologia, na kwa sehemu kubwa ni INTERPRETATION ya Maandiko kulingana na jinsi ya msukumo wa dhana wanayotaka kuijenga ili kuwa Fundisho kamili linalohusiana na Mungu!

  Teologia imegawanyika ktk makundi mengi sana kulingana na migawanyiko ya imani, yaani madhehebu. Nayo tafsiri rahisi ya Dhehebu ktk ulinganishi na Kanisa ambalo ni Mwili wa Kristo ni kwamba, “Dhehebu ni jamii ya watu waliokubaliana ktk mfumo wa ibada ulio bora zaidi kuliko mingine”, ndio kusema kila Dhehebu hujihesabia kuwa na Ibada iliyo bora kuliko madhehebu mengine. Ndipo Wanateologia hutambulika kwa migawanyiko hiyo. Nafasi wanazozishikilia ktk makundi yao ni za kitume, na wakati wao mwingi hutumika ktk tafiti hizo na kuunda mafundisho ambayo huwa ndiyo msingi wa madhehebu yao!

  Na ktk jitihada za kuzilinda himaya zao, ktk migawanyiko hiyo, madhehebu mengi sasa hivi yanaanzisha vyuo vyao, yakiacha matumizi ya vile vyuo huru vya Biblia vilivyokuwa vikihudumia Uprotestant ktk ujumla wao, ili kufundisha zaidi Doctrines za madhehebu yao. Navyo vyuo hivyo ni incubators zenye kuzalisha wasomi wa kimadhehebu, Biblia ikiwa si kiongozi tena, bali Doctrines zilizozalishwa na hao wakufunzi wasomi walioyatafsiri Maandiko kutengeneza hizo ‘Kweli za Dini’ ambazo kimsingi huonekana ni za ki Ungu kabisa!

  Kwahiyo, mhitimu wa vyuo hivyo, anakuwa amejengwa ktk u tayari wa kuitetea na kuitangaza dhana aliyofuzu, yaani kwa kifupi hupewa “Theme” ambayo humuongoza, akiamini kabisa kwamba ni Neno la Mungu! Cha kusikitisha zaidi ni kwamba huyo hugeuka kuwa mtumwa mwaminifu wa “Fundisho” hilo, nao uwezo wa kufikiri na kuyachambua Maandiko ili kujifunza humuondoka kabisa; hebu fikiria, kwamba kwa nguvu kabisa anakwambia:
  “”Divai aliyoitengeneza Yesu ni karibu mapipa saba! Divai hii haikuwa kileo au pombe maana aliudhihirisha utukufu wake. Ingekuwa amewapa watu kileo, ingekuwa aibu kwake badala ya utukufu. Ilikuwa ni divai mpya au divai tamu yaani juisi ya zabibu, tofauti na divai iliyochanganyika au kuchachuka ambayo ni pombe angalia Mithali 9:4-6; 23:29-30; Yoeli 3:17-18). Hatupaswi kunywa mvinyo au divai iliyochanganyika ambayo ni kileo.””
  Hizi ndizo “Kweli za Dini”!!!!

  Kweli ya Maandiko hii hapa:
  Lk 7:33-34 ” … Yohana Mbatizaji alikuja, hali mkate wala hanywi divai, nanyi mwasema, Ana pepo. Mwana wa Adamu amekuja, anakula na kunywa; nanyi mwasema, Tazama, mlafi huyu, na mnywaji wa divai…”
  Hebu jiulizeni, kunywa au kutokunywa juisi, kunaweza kuinua masimango dhidi ya muhusika kweli?

  Kwa kifupi tofauti ya Kanisa na Dhehebu ni moja tu, Msingi vilipojengewa; Kanisa limejengwa juu ya Msingi wa mitume na manabii, na Dhehebu limejengwa juu ya msingi wa Teolojia!

  Gbu all!

 73. Dada Christina,

  Usisikitike sana, jitahidi uwaelewe, wote ni watu wazuri, wanampenda Kristo!

  Hoja ni nzuri kweli, lakini mtazamo wa mleta hoja na wa wachangiaji licha ya kuonekana wanazungumzia jambo moja, ukweli ni kwamba wanazungumzia mambo mawili yaliyo tofauti kwa kiwango kikubwa ingawa yanaonekana kuwa moja!

  Hoja inazungumzia Wanatheolojia, lakini wachangiaji wengi inaonekana HAWAJUI sawa sawa maana ya Theology, kwahiyo kwa mazoea, mambo yote yanayohusiana na dini au Neno la Mungu wao huyachukulia kuwa ktk fungu hilo la Theolojia na ndio sababu ya mkanganyiko unaouona hapa!

  Kuna wasomi wa Kikristo (Christian scholars) ambao ni wataalamu wa lugha, hawa waliutumia utaalamu wao ktk kazi ya kuyafasiri Maandiko kutoka lugha moja kwenda nyingine, yaani ku TRANSLATE. Basi ktk kuendelea kwa fani hii, licha ya kuwa imesaidia Biblia kutafsiriwa ktk lugha nyingi sana, kumekuwako na hitilafu ktk hili, ninaamini ndilo lililomfanya Mfalme James awakusanye wasomi wakristo ktk jitihada ya kupata tafsiri iliyo sahihi ya Maandiko ktk maana ya lugha, ndiyo hiyo Biblia ya KJV tuliyonayo leo hii, pamoja na versions nyingine mbali mbali zilizotafsiriwa ktk jitihada ya kweli ya jambo hili; Ni jambo la baraka sana kwamba tunazo Biblia ktk lugha mbali mbali licha ya mapungufu ya hapa na pale! Ieleweke kwamba hapa nazungumzia jitihada za kisomi na si za kidini; maana kipawa cha kuombea wagonjwa hakiwezi kukupa Biblia ktk lugha ya Kingoni!!!

  Kwahiyo, jitihada za kisomi ktk kuyachambua Maandiko zimekuwepo na zinaendelea, na kwa leo, jitihada hizi zinapatikana ktk Vyuo vya Biblia independent, hivyo ambavyo vimejikita ktk Utafiti wa Maandiko. Jitihada thabiti, ambazo zimetuletea pamoja na Kamusi za Biblia, Concordances, Biblia za lugha mbali mbali na zenye commentaries na Cross refences, ili kutusaidia wasomaji kufuatilia jambo kwa urahisi, na mambo mengine mazuri kemkem! Na ifahamike pia kwamba jitihada hizo kwa sehemu ni BIASHARA, ndio sababu kazi zao ni interdenominational!!! Na katika mtazamo wa jumla kundi hili linajumuishwa na kujulikana kama WANATHEOLOGIA kutokana na evolvement ya taasisi hiyo hapo ilipohamia ktk vyuo!

  Jambo la msingi ktk taasisi hii likiwa ni Translation ya Maandiko na si Interpretation!

  nitaendelea….

 74. TUFUNDISHWE NA MUNGU KUPITIA ROHO MTAKATIFU, UNAWEZA UKASOMA TEOLOJIA MIAKA SABA LAKINI USIFUNDISHWE NA ROHO MTAKATIFU.

  EZEKIEL 11:5
  “ROHO YA BWANA IKANIANGUKIA, NAYE AKANIAMBIA, NENA, BWANA ASEMA HIVI;..”

  2 SAMWELI 23:2
  “ROHO YA BWANA ILINENA NDANI YANGU NA NENO LAKE LIKAWA ULIMINI MWANGU”

  YOHANA 14:26
  “LAKINI HUYO MSAIDIZI, HUYO ROHO MTAKATIFU, AMBAYE BABA ATAMPELEKA KWA JINA LANGU, ATAWAFUNDISHA YOTE, NA KUWAKUMBUSHA YOTE NILIYOWAAMBIA.”

 75. Kinachoendelea hapa kinasikitisha mno!!!

  Hoja iliyowekwa mezani ni nzuri sana na inapanua uelewa.Yawezekana
  mamilioni ya watu duniani wanafuatilia kwa karibu kuliko tunavyodhani.Hivi hapa
  mnajenga au mnabomoa? Mijadala ya kiroho inatakiwa itawaliwe na UPENDO WA KRISTO yaani hekima na maarifa ya Mungu aliye hai.WARUMI 5:5 inasema “……pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu
  na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi”

  Kwa staili hii ya MALUMBANO YA KIMWILI YALIYOJAA HEKIMA YA KIBINADAMU NA KUJIHESABIA HAKI,huo upendo wa kristo miongoni mwetu uko wapi? Hakuna aliye bora zaidi ya Mwalimu na msaidizi wetu,
  Roho Mtakatifu.Yeye ndiye anayetufundisha habari za mambo yote.Naomba kutoa angalizo la upendo,Huu ni mtandao kwa watu wote
  waliozaliwa mara ya pili na wasiozaliwa mara ya pili,Upendo wa Kristo unawavuta wote,huu si mtandao wa wana SG peke yao!Walioanzisha hii blog bila shaka walisukumwa na upendo wa Yesu ili INJILI YA AMANI iwafikie watu wengi zaidi.

  Sisi sote ni wanafunzi wa Yesu naomba tumpe nafasi Mungu aliyehai ambaye jina lake ni Yesu na sasa amejifunua kwetu kama Roho Mtakatifu
  atufundishe(YOHANA 17:6).Lengo hapa ni kujifunza ili tukue kiroho na siyo
  mashindano ya nani zaidi au nani mwerevu na nani mjinga.YULE ALIYE MJINGA YUKO MAHALI PAZURI ZAIDI KULIKO YULE ANAYEJIFANYA MWEREVU!Maana wote kama tunafahamu basi ni kwa sehemu na hatujajua jinsi itupasavyo kujua(1 WAKORINTHO 8:2-3,1WAKORINTHO
  13:9).MTU YEYOTE ANAYEDHANI AMESIMAMA BASI AANGALIE ASIANGUKE.Ni lazima tujue ni kwanini tunachangia au kuleta MADA, au ni kwanini hatuchangii.Wakati mwingine ni vyema tukakaa pembeni ili tujifunze zaidi.KWELI HAIWEZI CHANGAMANA NA UONGO.Mwalimu wa wale waliosoma THEOLOGIA na wale ambao hawajapita katika mfumo huo
  anatakiwa kuwa ROHO MTAKATIFU na si vinginevyo.

  HATA MPUMBAVU AKINYAMAZA HUHESABIWA KUWA MWENYE HEKIMA!

 76. Pendael,

  Nilikwambia kuwa watu wenye maneno mengi kama wewe……

  Naona tayari umeanza kujipambanua sasa. Ulidhani wewe ndiye mwenye kujua kuliko wengine wote hapa. Lakini nikakwambia kuwa unaponda Theology wakati wewe unachokifanya na kukisema ni Theology.

  Ndipo kwa makusudi nikaamua kukuyliza kuwa Theology ni nini?
  Hujajibu hilo swali badala yake unafoka na kugomba tu.

  Kwa nini unapata shida ya kuniita mwongo, wakati una nafasi ya kuthibitisha uongo wangu hapa kila mtu akauona?

  Sikia, usijaribu kuja kwenye ulingo kama huu ukidhani kuwa wewe ndo unajua kuljko wote, utaishia kuaibika.
  Na ninakuona umebakiza hatua chache sana uaibike usipokuwa mwangalifu.

  Na mimi tabia yangu ni hii; sitakuacha utudanganye juu ya mambo ambayi tunajua usahihi wake, nitakomaa na wewe mpaka uujue usahihi wa jambo uliloliparamia au mpaka uamue kunyamaza kabisa.

  Lakini kuniambia kuwa hutaki kujibizana na mimi haitasaidia. Lazima ujibu maana umeamua mwenyewe kuja SG, mahali tunaposemezana kwa hoja.

  Hapa siyo kwenye ibada ya mhubiri kusimama madhabahuni na kusema anavyotaka bila kuulizwa swali.

  Kuna ushauri mzuri Ziragora kakupa, ni vema ukazingatia ili ufanye homework yako.

  Vitisho vyako havisaidii, jibu hoja!

 77. Pendael,

  Umeleta mada, kiisha unafokea wachangiaji pasipo kuwa sahihi.
  Pengine hukuweka vizuri mada yako ili watu wakuelewe kama jinsi unajielewa.
  Kwani katika mijadala kama hii, kiinachojitokeza ni matusi tu.
  Inatakiwa utulie uweke kwa maneno machache yenye kueleweka ni nani unaeita theologian. Kwa mfano unaposema wanateoteolojia ndiwo waliotafsiri Biblia vibaya mimi sielewi. Kweli ni wanateolojia ndiwo wanatafsiri Biblia, sasa zote ni mbaya? na kama kuna nzuri zilitafsiriwa na wanani? Usipoweka wazi neno hutaeleweka. Kwani ukiwa mtu mzima naamini huwezi foka kwa bure kama hujihesabie haki na hiyo haki ndiyo unapigania. Sasa kama una haki hebu iweke wazi, usiwe wa kulaumu tu lakini weka wazi namna unawaita waliotafsiri Biblia vizuri na wenye walitafsiri vibaya.
  Pia kwangu kulingana na jinsi nasikia tafsiri ya theologian, ni kusema anajifunza kindani Neno la Mungu (au Mungu mwenyewe kwani Neno la Mungu ni Mungu). Kinachotusumbua ni kwani unajaribu kuitumia Biblia ukifahamu ilitafsiriwa, pili hata hapa wewe mwenyewe, kulingana na mantiki ya “theologian”, kiwango unayotelemsha wino inakuweka katika kundi la wanateolojia, wala sijue kama uko sahihi au la. Kwani jamani, tuwe wa kufikiri kama watu, si na wewe unaandika hii yote ili uelewe na ueleweshe wengine kuhusu Mungu? Sasa huone kama kwa mtindo huo uko theologian? Inatakiwa kabisa uambie vizuri watu ni nani unaeita theologian, aliejifunzia wapi na anae degree gani ili tuone kwa pamoja anachokifanya tofauti ya wengine wanaojifunza Neno la Mungu.

  Asante.

 78. Sungura.
  Usiwe mwwongo kiasi hicho.UWE MWANGALIFU unaporudia kitu ambacho mtu mwingine amesema.
  SINA MUDA WA KUJIBIZANA NA WEWE.

 79. Pendael,

  Nilitangulia kusema kuwa watu wenye maneno mengi kama wew huwa hawako mbali na uongo.

  Unaniambia kuwa wewe unamtumia Roho mt.wala hutumii akili.
  Lakini hakuna mahali biblia inatuambia tumtumie Roho mt. Yeye ndiye anatutumia sisi.

  Acha ujinga, tumia akili yako kufikiri lakini mtegemee Roho. Mt katika kutoa kwako hukumu.
  Kama hutaki kufikiri kwa kujidanganya Roho mt ndo anafikiri kwa niaba yako, utaendelea kuongea maneno mengi yasiyo na tija.

  Kuna tofauti ya kutosha kati ya kutegemea akili na kutumia akili. Kama unadhani akili hazina kazi jichome sindano ya ukichaa kisha nenda kahubiri, uone watu wangapi watakuelewa.

  Naona unajaribu kukwepa kibarua kwa kusema maneno mengiii!

  Jibu maswali niliyokuuliza tafadhali. Likiwemo ” what is Theology”?

  Mbona unakwepa?

  Mind u, huongei na mtu mjinga!

 80. Harris,
  Kwanza nashukuru kwa kujitahidi kuwa mnyofu.
  Mbona haujajibu maswali yangu mengine? REJEA HAYO MASWALI.Ingependeza kama ungejibu moja baada ya lingine.
  Pia naomba unapojibu ujitahidi kuweka NUKUU ZA BIBLIA.
  Ahsante.

 81. Sungura,
  Mojawapo ya dalili ya kwamba HUJAOKOLEWA NA BWANA YESU ni kuwa na kiburi na majivuno ambayo mwisho wake ni Jehanamu.
  Unasema “Sijawahi kuwa na wewe kwenye hii mijadala ili kujua uwezo wako wa kufikiri. Lakini nikuonavyo wewe si mtu makini sana kiufahamu, huoneshi kama unajitegemea kiufahamu, ila ni mtu mwenye kudaka mapokeo na kuyameza, na baadae kutaka kuwacheulia wengine yaleyale uliyomeza wewe”
  Ni kweli kuwa kazi yenu ninyi wanafalsafa ni kupima watu uwezo wa kufikiri. MAPOKEO YA DHEHEBU LAKO YAMEKULOGA RAFIKI HUONI UKWELI MPAKA HIYO ROHO YA DHEHEBU IKUTOKE.
  BWANA YESU HUWAPIMA WATU KWA NENO si kwa kufikiri.Ninyi huwapima watu uwezo wa kufikiri!!!! NI KAMA KASKAZINI NA KUSINI HAZIKUTANI KAMWE.
  HILI LINAONESHWA WAZI KUWA KAZI YENU KUBWA NI KUTUMIA AKILI NA ROHO MTAKATIFU mmemuweka kando. .
  Ni Kweli kuwa Mimi sijtegemei kiufahahamu BALI NAMTEGEMEA BWANA YESU (Mithali 3:5 ” Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe) Hili usilitupe LITAKUSAIDIA SANA.
  Nimeona roho ya nafsi tatu BADO IMEKUSHIKILIA,ETI UNANIULIZA “Unaonaje nami nikakuuliza Timotheo alifundishwa na Yesu au na Roho mtakatifu?”
  KWELI HUU NI UPOFU WA NIKEA NDIO UNAOKUTESA.HUJUI YA KUWA YESU NI ROHO MTAKATIFU?
  KWA NUKUU ZA MAANDIKO HEBU REJEA MCHANGO NILIOUTOA NA ALIOUTOA LWEMBE NA WENGINE WANOAMINI MUNGU MWENYE NAFSI MOJA KWENYE ILE MADA YA DADA JANNETH MMARI.
  Maelezo yako mengi HAYANA USHAHIDI WA BIBLIA NA MIMI NILIKUTAKA UNITHIBITISHIE KIMAANDIKO, MATOKEO YAKE UMETUMIA MAARIFA ULIYOFUNDISHWA. NAOMBA MAANDIKO SI MAPOKEO.
  INAONEKANA WEWE MAPOKEO HUYAJUI VIZURI.KAMA WEWE NI MSABATO HUJUI UNA MAPOKEO YA NIKEA KAMA HABARI YA NAFSI TATU nk?
  KAMA LUKA HAJAKUANDIKIA WEWE HIYO INJILI MBONA UNAISOMA?AU MAFUNDISHO YA DHEHEBU LAKO NDIO WALE WASEMAO ” HAYO NI MAFUNDISHO YA PAULO, HAYO NI MAFUNDISHO YA WAKORINTHO,….nk)
  Paulo alikwenda Damaskas kusoma!!!HUYO MWALIMU WAKO KAKUDANGAANYA.POLE RAFIKI.
  KABLA YA KUBISHA MAMBO USIYOYAFAHAMU,PUNGUZA JAZBA ILI UWEZE KUPATA CHA KUJIBU.
  Ahsante.

 82. hizi nyakati za mwisho kweli kazi ipo, baadaye hata kwenda makanisani tutasema ni mapokeo maana yesu alienda kwenye sinagogi na sio kanisani.!!! kazi mnayo wazee!!

 83. Pendael
  Wakati wa Yesu. Walifundishwa moja kwa moja. Theology Imekuja baada ya miaka mingi kupita. Ikiwa na lengo LA ku-maintain integrity ya neno La mungu.wakati haya yote yanafanyika hatuwepo na mambo mengi yamebadilika.hata mfumo wa uandishi, na uelewa wa watu kuhusu dunia tunayoishi umebadilika sana.
  Theology inawezesha ujumbe uliopokelewa miaka 2000 iliyopita usiwe distorted na maendeleo yetu ya sayansi na technolojia.

 84. Pendael,

  Sijawahi kuwa na wewe kwenye hii mijadala ili kujua uwezo wako wa kufikiri. Lakini nikuonavyo wewe si mtu makini sana kiufahamu, huoneshi kama unajitegemea kiufahamu, ila ni mtu mwenye kudaka mapokeo na kuyameza, na baadae kutaka kuwacheulia wengine yaleyale uliyomeza wewe.

  Unaniuliza Paul alisoma chuo gani cha Biblia. Nakuona hata huelewi maana ya chuo.
  Unaonaje nami nikakuuliza Timotheo alifundishwa na Yesu au na Roho mtakatifu?

  Sikia, kuna kitu kinaitwa Formal and Informal Education.

  Formal Educatio ni hii elimu ya kwenda darasani, mnasoma kwa kufuata silabasi, mnafanya mitihani, n.k. ( Elimu rasmi)

  Informal Education ni kinyume cha formal, lakini mwisho wa siku mtu anatakiwa atoke na maarifa yaleyale.

  Hata ktk ufarisayo Paul hakwenda chuo kwa maana ya mfumo kama wa leo, lakini alifundishwa na mwalimu mmoja anaitwa Gamaliel

  Paul anapokutana na Yesu, anaenda kwenye mtaa unaoitwa Mnyoofu, anakutana na Anania, anaponywa upofu, baada ya hapo alikaa kwa muda na wabafunzi walikuwa huko Damaskas.

  Baadae baada ya kuwa amekaa nao kwa muda ndipo anapoanza kidogokidogo kumhubiri kristo.

  Jiulize kwa nini hakuanza kuhubiri baada tu ya kukutana na Yesu, au baada tu ya kujazwa Roho mt.?

  Kuhusu Luka iko wazi sana, ila naona mahali lilipoandikwa hilo jambo wewe hupasoma kwa makengeza hivyo huwa hupaoni.

  Kwanza elewa Luka hakuwa anakuandikia wewe wal mimi hi hicho kitabu, bali alikuwa anamwandikia mtu mmoja anaitwa Theofil, ili kumpa uhakika wa mambo ambayo huyo mkuu alikuwa ameyafundishwa kumhusu Yesu.

  Sasa ili Luka aupate ukweli halisi ilimbidi afanye utafiti na kuyafuatilia mambo hayo kwa umakini mkubwa ili aweze kuandika kitu ambacho ni thabiti.

  Wewe kama husoma biblia kwa makengeza shauri yako.

  Lakini pia ni kudanganya kusema kuwa maandishi yote kwenye biblia watu waliandika kwa ufunuo wa Roho.
  Yako mengine yameandikwa kwa watu kuona yakitokea, mengine kwa kuyasikia kwa masikio yao, mengine kwa kusimuliwa, na mengine kwa kufunuliwa na Roho. Na yote hayo bado ni neno la Mungu lililo imara.

  Ngoja niweke koma nikungoje!

 85. Pendael, wasalaam!

  Sikia rafiki, usitake tufanye mjadala kama watu wa kijiweni. Tarehe 4/11/2014 nilikuuliza maswali mawili.
  Please hebu yajibu bwana, usijifanye kuwa hujayaona.

  Nikiri kwamba kuna maswali uliniuliza kwenye mada ya utatu, cha ajabu sikuwa nimeyaona ispokuwa jana ndo nkayaona.

  Naenda huko kukujibu, wala usipate shida.

  Nijibu sasa na wewe hayo maswali yangu mawili ili twende sawa.

 86. Pia Pendael Simon ningeomba ufaham kuwa mengi niliyoorotdhesha hap sikuweka reference kwakuwa nina imani ni general knowledge isiyohitaji mpka kuwepo reference.
  Pia unatakiwa ujiulize ikiwa wayahudi walimwona Yesu kuwa ni Mwema: Na sifa zake zilienea. Na angali waona mambo mengi aliyoyafanya lakini kwanini walimsulubisha. Tena kwanini walipiga kelele wakisema bora jambazi baraba atolewe na Yesu asulubiwe.
  Katika hali ya kawaida bila kutoa majibu ya juu juu kama vile shetani n.k. Kwanini Yesu?
  Kwanini HAruni akubaliane na wayahudi wakatengeneza ndama washaba wakakiabudu. Wakati wanajua Musa amekwenda mlimani.? Kitu gani kiliwabadilisha. Walikuwa wanajua nini kuhusu ndama wa shaba kuwa ni Mungu? watu wa kale wanatofauti gani na sisi wa leo?
  Kwanini Dunia imejaa uovu kama Mungu yupo?
  Kwanini Mungu hayamteketeza shetani kama yupo?

 87. kweli @Pendaeli simon hujitambui?
  Hoja yangu iko wazi hivyo lakini bado inakukwamisha.
  Elimu ina faida ya ku-meet changamoto za kila siku katika maisha yawe ya kidunia naya kiroho. Mtu asiye na Elimu utakuta ame-cram bibilia baadhi ya mistari kisha anajitamkia yeye mwenyewe kuwa ana-roho wa Mungu. Kwakuwa akikemea mapepo wanatoka!!
  Lakini hawezi kabisa kutoa majibu ya maswali magumu yanayoendana na Ukristo wa kileo.

  Na hii inatokana na mkanganyiko mkubwa uliopo kwenye bibilia:
  mfano:
  Hatma ya kuanguka kwa mwanadamu, na kwanini Yesu aje duniani?
  Kwanini Adam na Eva wakiwa hawajui jema wala baya:Mungu aruhusu wajaribiwe wakati ni kama watoto wadogo? Je wewe ukiwa na mtoto wako utampa Gobole achezee?
  Kwanini Shetani aliingia Bustanini (Eden)?
  Nyoka aliyekuwa mwerevu Bustanini akalaaniwa ni nyoka wa kawaida anayetembea kwa tumbo au nini maana yake?
  Kwanini bibilia kwenye Ayubu inasema Shetani alikwenda mbinguni wakati alishafukuzwa?
  Kwanini Mikali binti sauli anadaiwa hakuzaa na wakati huo huo kitabu kingine kinasema alikuwa na watoto?
  Kwanini Eva hakujiona yu uchi mpaka alipompa adam tunda na wote wakajiona wako uchi?
  Kitabu cha UFunuo: na nini maana ya 666? Je waliosema papa john ni anti christ mbona makufa siku nyingi??
  Je Gharika ya wakati wa Nuhu ilinyesha dunia yote ama ni maeneo ya pale tu?
  Je mbingu ya Yesu ni ya phyisical body ama spiritual world . Kama ni physical ni kwanini basi Yesu aende mbinguni na mwili huu unaodaiwa kufa?
  Mungu kuwajaalia wasiosoma baadhi ya vipawa haimaanishi wao ni bora katika kufundisha wengine Bibilia. Bali namna Mungu anavyotuangalia anatubariki pamoja na udhaifu wetu.

  Mtu aliyesoma Theology anaweza ku-articulate maana na mazingira ambamo Bibilia iliandikwa. Pia akaweza kutoa jibu la lengo kuu la Mpango wa Mungu katika wokovu wa mwanadamu . Pia changamoto za Ukristo katika Ulimwengu wa leo
  Mfano:

  Kuna changamoto za baadhi ya maandiko kupishana ama kutofautiana maelezo. NA wakati huohuo watu wanasema Bibilia ni neno la kweli la Mungu.Hii ipo hadi kwenye Injili na Old testment.Mtu ambaye ni Novice hawezi akatoa majibu ya maswali haya maswali magumu.
  NA hii imepelekea most Christians kuhamia kwenye atheisms na agnoistic kwasababu wanaona kuwa Bibilia ni mapokeo ya wanadamu na wanahisi hakuna Mungu. Kama inavyodhaniwa.
  Pia kupitia hoja kama zako zimepelekea wale waliowaamini manabii mbalimbali waanze kuona shaka baada ya majengo yao kuua watu.

  Kuna Christians walikuwa wanaogopa baadhi ya maendelo ya kisayansi kama kumtengeneza mtu kwa chupa wakiamini wanasayansi wafanyao hayo wanashindana na Mungu: theology inasaidia kumuunganisha mtu kuulewa Ukristo katika dunia ya kisasa.
  Elimu ya theology ndio inawafanya hata wasiosoma waendelee kuwa na Imani walionyao. Laiti Dunia nzima ingekuwa wasomi wote wanakataa dini? Asiyesoma asingeweza kusimama katika hili.
  Kwani katika mazingira ya kawaida watu wakijua umesoma wanaongeza Imani kwako kwa kuamini kile usemacho kuliko kwa yule mtu asiyesoma. Ikiwa ninakuja na Ugonjwa unaniambia ni pepo nisimeze Dawa nitapona na mwisho nakufa. Wakati ningeenda kwa Daktari nikatibiwa malaria ningepona.Je iweje watu ama wachungaji maarufu walikuwa wanakwenda kutibiwa hata kufanyiwa baadhi ya operation mahospitalini ikiwa wao walikuwa wanawaombea wengine wakapona?

  Sasa Swala la kupuuza Theology kwa kutaka mtu yoyote aamini kila kilichoandikwa kwenye bibilia ndivyo kilivyo, kimepelekea wengi kuangamia.Na mwishowe wsio amini wanakebehi kuwa hakuna Mungu. Kule nchini Korea kuna mtu alijiingiza kwenye simba kwa kigezo cha imani kuwa Mungu alimlinda Daniel kwenye tundu la simba na mwishowe jamaa akararuriwa.

  Ndio maana inabidi ujue Theology. Watu wengi wanakimbilia Miujiza.NA kusema hapa ndio pana Mungu. Lakini Yesu ameshasema watakuja manabii watasema walitoa pepo kwa jina langu nitawaambia siwajui nyinyi.Je Ukishakuwa na nguvu ya kutoa mapepo unaamini una roho wa Mungu sio?

  Nalazimika kuamini kuwa lengo la hoja yako lilitakiwa pengine liseme: Kukremu bibilia sio sawa na kuiishi Bibilia, Kwani bibilia sio kitabu cha historia bali ni neno la mungu.
  Pia ufahamu tu kuwa Kiburi cha watu hakitegemei theology, tena wale waliosoma theology wanakuwa na matumaini kwa Mungu zaidi kuliko wasiosoma. Kwani ni rahisi kwa yeye kudumu kiimani: kwakuwa inamsaidia kumwelewa Mungu na mpango wake wa wokovu katika hali zote.
  Ikitokea mtu mwenye theology amekubishia ama kukukosoa: Hutakiwi kuchukulia kuwa anakiburi nenda kwenye hoja yake kwanza.
  Unachotakiwa kufanya ni kujifunza namna ya kum-approach ili apate kile usemacho kwa usahihi.

  Yesu kristo Ni Msomi, Mwali mwema, na mwanafalsafa vilevile.
  Nakumbuka kuna mahali watu walisema ..Amepataje huyu(Yesu) kuwa na Elimu ambayo hakusoma. Kimsingi Yesu alikuwa msomi na ndio maana walimwita mwalimu.
  Asingeweza kwenda mbele kufundisha lile gombo la nabii isaya linaloanza na neno Roho ya bwana yu juu yangu” .Alikuwa anafundisha .
  Yesu alisoma dini ya kiyahudi vizuri. Mitume wake walikuwa wanapata darasa kwa Yesu mwenyewe ni msomi. kitendo cha Yesu kukaa na mitume wake miaka mitatu inamaana aliwapika miaka mitatu na elimu ya Roho na ufalme wa Mungu akiwapa na mifano kabla hajawaachia. Dunia ya kwetu degree inasomwa miaka mitatu.
  Historia ya Bibilia ilikuwa simulizi mpaka guttenburg machine ilipochapa Bibilia ya kwanza miaka hiyo.Mambo mengi yatakuwa yalipotea ama kubadilika.Haya yaliyoachapwa ni yale ambayo hayakuweza kusahahulika kirahisi na yenye ushahidi wa kutosha.

  Pia yapo mambo mengi yesu aliyafanya lakini hayakuandikwa. Hiyo kuamini tu kuwa yesu kafanya yale machache yaliyopo kwenye Bibilia huu utakuwa ni udhaifu wako wa kupambanua.

  conclusion yako ya kukosoa wenye theology inakufanya uwe na kiburi cha kuamini unajua kla kitu kuliko wenye Theology. NA mwisho unatenda dhambi ya majivuno kwa kuwaona hawa wenye theology hawana Mungu.
  Bibilia inasema usitamani mali ya mwenzako: na wewe usitamani Elimu ya mwenzako kwa kumuonea wivu.Acha wenye theology waendelee kuwepo na wewe kaisome. Itakusaidia……..

 88. WANATHEOLOJIA,
  NILITANGULIA KUSEMA AWALI ;na nukuu,……………………….
  “KUANDIKWA NA KUTAFSIRIWA KWA BIBLIA.
  -Bila shaka Wakristo wa kweli wanajua kuwa BIBLIA iliandikwa na watu Walioongozwa na ROHO MTAKATIFU, kwa maneno mengine Mwandishi wa BIBLIA ni ROHO MTAKATIFU.
  -Waliotafsiri BIBLIA wapo katika makundi mawili;
  (A) Kundi la kwanza ni la wale waliotafsiri BIBLIA wakioongozwa na ROHO MTAKATIFU
  (B) Kundi la Pili ni la wale waliotafsiri BIBLIA wakiongozwa na roho wa Ibilisi.
  Ndio maana wamebadili maana ya asili ya maneno ili kukidhi haja za mioyo yao kama vile Mafundisho ya nafsi tatu za Mungu. Najua kusema hivi kwa mwanatheolojia ni ‘kukufuru’ kukuu sana”……………Mwisho wa kunukuu.
  HAYO MMEYASOMA VIZURI AU UNACHANGIA UKIWA NA CHUKI BINAFSI NA HASIRA YA KUHARIBIWA BIASHARA YAKO?
  MADA HII NAJUA KAMA NILIVVOTANGULIA KUSEMA IITAWAUDHI SANA LAKINI MUNGU AZIREHEMU NAFSI ZENU.
  HEBU KUWENI WAVUMILIVU VINGINEVYO ONESHENI RANGI ZENU MJULIKANE VIZURI.
  1.TETEA MAANDIKO SI MAFUNDISHO YA KANUNI ZA IMANI NA MAPOKEO YA WAZEE (MAFUNDISHO YA DHEHEBU LAKO)
  2.IKIWA ASILI YAKO NI YA MBINGUNI HUTAKWENDA KUSOMEA CHUONI.
  KWA MFANO;
  HIVI, JOGOO ANASOMEA KUWIKA?
  3.USITEE VYETI ULINAVYO BALI TETEA KILE BIBLIA INACHOSEMA.
  4.HUWEZI KUMTAFITI MUNGU KWA AKILI YAKO (ISAYA 55:8-9)
  Ubongo wako tu ni kama punje ya KARANGA.
  5.MUNGU ANAANGALIA WATU WANYONGE WENYE MIOYO ILIYOPONDEKA,WATETEMEKAO WASIKIAPO NENO LA MUNGU (ISAYA 66:2)
  MUNGU HAWEZI KUSIKILIZA WATU WENYE KIBURI CHA UZIMA WANAOJUA KILA KITU. NA SIKU ZOTE UKIMUONA MTU ANAYEJUA KILA KITU MITILIE MASHAKA ( Mfano: Ziragora na rafiki yake Sungura)
  Je,mnaanza kujisifu wenyewe…..kwa barua zenye sifa? 2 WAKORINTHO 3:1…
  6.ROHO MTAKATIFU PEKE YAKE NDIYE MFASIRI WA NENO LA MUNGU NA NDIYE ANAJUA MAFUMBO ALIYOYASEM MUNGU NA SI WANATHEOLOJIA? 1 WAKORINTHO 2:10-16
  MASWALI:
  1.Je, theolojia ni chanzo cha maarifa?
  2.Ambao hawajasoma hawajui KIle Mungu anachosema?
  3.WANAFUNZI WA YESU PAMOJA NA YESU WALIKUWA DHEHEBU GANI?
  4.Kuna tofauti gani kati ya KANISA NA DHEHEBU?
  5.Wanafunzi wa YESU au MITUME walifundisha tu kile YESU KRISTO alichowaamuru?
  6.Yesu Kristo, Petro, Yohana na mitume wengine walikuwa na elimu ya darasa la ngapi?
  7.BIblia imezungumza popote habari ya WAKRISTO kusoma teolojia?
  KUMBUKA ;
  -KUNA KUADHIRIKA HUKUMUNI MOJA YA SIKU HIZI.THEOLOJIA YAKO HAITAKUSADIA KITU.
  -MUNGU HATISHIWI NA VYETI VYAKO VYA LLD,LLB,PhD…..nk.
  HAYO HAYAKUPI MAJALIWA YA KUMUONA MUNGU HATA KIDOGO.
  -NIKODEMO MWENYEWE ELIMU YAKE HAIKUMSAIDIA BALI YESU KRISTO ALIYE UFUNUO HALISI ALIMSAIDIA NA NIKODEMO AKALIPATA ( YOHANA MTAKATIFU 3:1-15)
  KWA NINI MSIWE KAMA NIKODEMO ILI MPEWE UFUNUO NA BWANA YESU?
  -MBINGUNI HATUENDI KWA KUWA NA THEOLOJIA BALI KWA KUWA NA ROHO WA KRISTO.
  -MUNGU NA AYAPAKE MACHO YENU DAWA (MPATE UFUNUO WA NENO LA KWELI) ILI roho wa Laodikia awatoke (UFUNUO 3:14-22)
  **TILIA SHAKA MASHAKA YAKO NA SI NENO LA MUNGU.***
  *****KILA NENO LA MUNGU LIWE AMINI NA LA MWANADAMU LIWE UONGO (WARUMI 3:4)*******

 89. Shalom.
  SG,
  Mungu awabariki kwa kazi nzuri mnayoifanya.Mmenifurahisha kwa jinsi MILIVYOOIWEKA HIYO PICHA HAPO JUU kwa kweli imesadifu. Mpaka LENSI YA KUSOMEA MAANDIKO!!!! Ni zaidi ya “research”.
  KWELI WANATHEOLOJIA WANAPATA SHIDA SANA.
  MAREKEBISHO; Jina langu ni PENDAEL SIMON na si kama linavyoonekana hapo juu.
  Bwana Yesu Kristo awabariki.

 90. Harris,
  Inaonekana wewe nia MWANATHEOLOJIA MCHANGA bado teolojia haijakukolea.
  Unafurahisha unaposema kuwa “Ndio maana theology na Elimu ni muhimu sana. Wako manabii wanatoa utabiri hautimii wako wale walioaka kwenda ulaya bila viza, na wote wanasema wamesom bibilia”
  Japo sentensi yako imekanganyika lakini,hebu nikuulize mwanatheolojia:
  1.Unafikiri MANABII WA UONGO NA MAKRISTO WA UONGO ni watu waliokosa Elimu na Teolojia?
  (NIKUSAIDIE REJEA:MATHAYO 24:24)
  2.Umesema YESU KRISTO alikwenda shule.HEBU TUSAIDIE NA UTUTHIBITISHIE;
  (a) YESU KRISTO alisoma shule gani?
  (b)YESU KRISTO alihitimu elimu ya darasa la ngapi?
  Pia umeniandikia kuwa “Haiwezekani wewe ukatae theology na kutumia hisia zako. Lazima uelewe hata kumkaribisha huyo roho wa Mungu katika moyo wako bado inahitajika uelewe neno la mungu na theology”
  3.Je,YESU KRISTO alisema kumkairibisha Roho wa Mungu mpaka uwe na theolojia kama unavyodai wewe?
  Pia umesema kwa maneno yako mwenyewe;
  “Ninaimani wewe huna na nikikuuliza swali kwenye bibilia hutaweza kujibu na pengine utanitisha kuwa Mungu anakasirika, ili nisiulize, lakini ukweli utabaki palepale huwezi kujua Bibilia kama hujasoma”
  SOMA HIYO MADA VIZURI UJUE KUWA WENYE VITISHO NI WATU KAMA WEWE (Harris),WANATHEOLOJIA.
  4.HUONI KUWA HICHO NI KIBURI CHA TEOLOJIA (Kiburi cha uzima)?
  5.Unajua kuwa si kila SWALI aliloulizwa BWANA YESU alilijibu?
  6.PETRO NA YOHANA walikwenda shule gani?
  7.Hawa manabii MUSA,ISAYA,ELIYA,SAMWELI,ELISHA,YOELI,YEREMIA,EZEKIELI,MALAKI,……Walikwenda chuo gani?
  8.Unasisitiza pia kuwa ili kumjua MUNGU LAZIMA WATU waende SHULE.
  Je, kazi ya ROHO MTAKATIFU ni nini?
  Vilevile umesema YESU alifundisha kwa mifano,Ni kweli kuwa YESU alifundisha Kwa MAFUMBO.
  9.Unajua kwamba anayeyajua MAFUMBO hayo ni ROHO MTAKATIFU PEKE YAKE NA SI WANATHEOLOJIA? 1 WAKORINTHO 2:10-16
  MAANDIKO HAYA YATAKUSAIDIA SANA UKIWEKA ELIMU YAKO KANDO.
  10.JE,WEWE UMEBATIZWA KWA JINA LA YESU KRISTO KAMA BIBLIA INAVYOSEMA,(MATENDO 2:38…….”Petro akawaambia,Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo,mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu”)
  ANGALIZO: USIJE UKAMCHAMBUA PETRO KULINGANA NA TEOLOJIA.
  KUMBUKA RAFIKI:
  YESU KRISTO KAMWE MAHALI POPOTE HAKUWAAGIZA WANAFUNZI WAKE KWENDA KUJENGA VYUO VYA BIBLIA,SHULE WALA HOSPITALI.
  VYUO VYA BIBLIA,SHULE NA HOSPITALI NI MIRADI YA WATU “WANAODAI” KUWA NI ‘WAKRISTO’ KWA AJILI YA ‘mungu tumbo’.
  NDIO MAANA KILA DHEHEBU LINAJENGA CHUO CHAKE CHA BIBLIA ILI KUFUNDISHA MAPOKEO YAO NA KANUNI ZA IMANI TOFATI NA LINGINE (MFANO:WALUTHERI,WAANGLIKANA,WAPENTEKOSTE…nk),
  PIA KILA DHEHEBU LINAJENGA HOSPITALI NA SHULE KUWEKEZA KATIKA MIRADI YAO.WAKIJARIBU KUHUSIANISHA NA BIBLIA NA UONGO.
  HAYO YANAYOFANYWA NA KILA DHEHEBU NDIO YESU KRISTO ALIAGIZA?
  SOMA KWA MAKINI WALICHOAGIZWA WAKRISTO (MATHAYO 28:18-20, MARKO 16;15-18….nk.).
  *****KUMBUKA PENYE SWALI KUNA JIBU. PIA ELEWA KUWA HATUTAFUTI UMAARUFU BALI TUNAHUBIRI NENO LA MUNGU LINALOLETA UZIMA WA MILELE*****

 91. Sungura,
  Nimefuatilia Mada zako pamoja na michango yako nikagundua kuwa wewe ni MWANATHEOJIA KWELIKWELI!
  Pole kwa kukugusa,ikiwezekana MUNGU akuponye.
  Tarehe 30/10/2014 at 3:45 AM
  Katika mada iliyohusu nafsi tatu,nilikuandikia hivi;
  “Kabla sijakujibu baadhi ya maswali yako,naomba uniambie tofauti kati ya UKRISTO na UDHEHEBU”.
  Mpaka sasa hujaweza kunipa jibu.NAOMBA UNIPE JIBU RAFIKI.
  Lakini cha kuchekesha katika mada hii UMEULIZA MAASWALI HALAFU UNAJIJIBU MWENYEWE.
  Unachanyanya mambo yasiyochanyika .Elimu ya Dunia na MAMBO YA UFALME WA MBINGUNI.
  Hebu nisaidie kwa sababu umekiri kuwa mimi siielewi Teolojia;
  Umesema Wanafunzi(MITUME) wa YESU walifundishwa na BWANA YESU,hIyo ni KWELI KABISA.
  1.Wewe umefundishwana nani?
  2.Paulo unayemsingizia kuwa mwanatheolojia mwenzako alisoma Chuo gani Cha BIBLIA?
  3.Ni WAPI KWENYE BIBLIA LUKA alioneshwa kuwa alikwenda kufanya “research”?
  4.Petro unayemzungumzia una historia yake ya teolojia?
  Hayo maswali yanakutosha kwa sasa.
  ****USITANGULIZE UMAARUFU WAKO WALA MASLAHI YAKO BALI TANGULIZA UMAARUFU NA MASLAHI YA BWANA YESU KRISTO******

 92. Shalom.
  Siyi & Yusha,
  Ubarikiwe kwa moyo mnyenyekevu,na hasa SIYI kwa kuona Kuwa wanatheolojia wengi ndio WANAOFUNDISHA UKENGEUFU kuhusu MAANDIKO MATAKATIFU.
  Lengo la WAKRISTO wa kweli ni kuitikia KILA NENO LA MUNGU KWA AMINA na si kuonesha Umaarufu.
  Ubarikiwe.

 93. Pendael hata hajui maana ya Theology, anatembea tu kwenye maneno ya jinsi watu wanavyoisema theology.

  Wale mitume kukaa na Yesu miaka mitatu, hicho kilikuwa chuo tosha, na haikutokea kwa bahati mbaya. Alihakikisha akili zao kiufahamu wa kujua mission ya Yesu zimekaa sawa ndipo akaamua kuondoka.

  Petro anawajibu wayahudi kuwa waamue wenyewe cha kufanya, lakini yeye na wenzake hawaweza kuacha kuyanena waliyoyasikia kwa masikio yao Yesu akiyasema na kuyashuhudia lwa macho yao Yesu akiyatenda.

  Tena soma historia ujue Paul alikaa miaka mingapi akijifunza baada ya kuokoka, kabla hajaanza huduma yake.

  Luka aliyeandika litabu cha Luka na cha Matendo ya mitume hakuwa mwanafunzi wa Yesu, wala hakuandika mambo ya kufunuliwa na Roho, bali alifanya research na kufuatilia kutaka kujua yalikuwaje mambo hayo.

  Ikambidi awatafute wale walioyashuhudia wamsimulie, ndipo walipomsimulia naye akaandika.
  Alitafuta kusikia kutoka kwenye original source.

  Ninyi mnajifanya kuwa hamhitaji kusoma theology, ndio mnajifanya kuwa mnaenda kwa ufunuo. Nanatumia sana hicho kivuli cha kwenda kwa ufunuo pekee ili mnaposema mambo yasiyo tuogope tusiwahoji ili mtudanganye.

  Nendeni shule mkajifunze, whether ni formal or informal school.

  Kwa mfano kuna ubaya gani kwenda kujifunza Yesu aliongea lugha ngapi?

  Kuna ubaya gani kwenda kujifunza kama alichotengeneza Yesu pale Kana ya Galilaya ilikuwa na kilevi?

  Chuoni unaenda kujifunza msingi wa mambo wala siyo liturjia.
  Naongelea vyuo vya kweli.

 94. Pendael simon umegusa mada ngumu sana, na umeshindwa kuimaliza.MAmbo mengi Yesu kasema kimifano. Elimuya theology inahitajika, sio tu kujisifu una roho wa Mungu. LAiti huyo roho angekuwa na alama kila mtu anamwona nisingekubishia lakini hata manabii wa uongo wanajisifia kuwa wanayo roho wa Mungu anayewafunulia.

  Ndio maana theology na Elimu ni muhimu sana. Wako manabii wanatoa utabiri hautimii wako wale walioaka kwenda ulaya bila viza, na wote wanasema wamesom bibilia.
  YEsu kristo mwenyewe alikwenda shule. Haiwezekani wewe ukatae theology na kutumia hisia zako. Lazima uelewe hata kumkaribisha huyo roho wa Mungu katika moyo wako bado inahitajika uelewe neno la mungu na theology.
  Mambo mengi Yesu alisema kwa mifano kiasi kwamba yanahitaji Elimu kuelewa, sio tu kila mtu kwakuwa anajua kusoma na kuandika anajiiita mchungaji. Hawa wachungaji na manabii ndio wanaovuruga jamii world wide. Kwa mafunuo yao ya uongo, huku wakipondea makanisa mengine na kujiinua nafsi zao kuwa wao wana Yesu na roho wa Mungu.
  Theology ni Muhimu sana mkuu.
  Ninaimani wewe huna na nikikuuliza swali kwenye bibilia hutaweza kujibu na pengine utanitisha kuwa Mungu anakasirika, ili nisiulize, lakini ukweli utabaki palepale huwezi kujua Bibilia kama hujasoma. Na theology ni muhimu pia.

 95. Pendael,

  Hebu tuambie ile versions zote za Biblia ulizipataje. RM akazitelemsha kwako? Tuambie wala usiseme mambo usiyoyafahamu.
  Waandishi hawakushutumiwa kuwa wanao ujuzi wa kuandika Neno la Mungu lakini ni kwani walishindwa litimiza. Ninapongoja umjibu Ndugu Sungura, fahamu kuwa theologian ni huduma wala siyo wokovu. Lakini wako wanateolojia waliyookoka. Wawe wameokoka au la wana nafasi yao, yaani wanatutengenezea vitabu wakivutwa na RM hata wao pasipo kufahamu.
  Nafikiri umesema mitume wakiishachaguliwa na Yesu hawakuingia ndani ya teolojia kwani hujafahamu teolojia ni nini na nani ndiye mwanateolojia wa kwanza. Hebu tuambie, Yesu alipomaliza chagua wanafunzi, aliwatupilia ao aliwafunza? na kwa nini aliwaita wanafunzi, hakuwaita walokole, wakristo, nabii, …?
  Ina maana walikuwa ndani ya shule.

  Hee, hapa kuko watu specialists kushutumu wengine!!! Kabla uandike omba Mungu, hapa ni kanisani.

  Ubarikiwe.

 96. Pendeleli,
  Uko sahihi mtumishi. Hicho ni kizungumkuti ambacho wengi wetu tumeingia bila kujua!! Na teolojia ndiyo mwasisi wa cults nyingi sana katika madhehbu ya Kikristo. Najua hoja yako ina utata fulani kwa tulio wengi wetu! Tutakubishia weee!! Jambo la kutia moyo ni kwamba, wengine tutabisha kwa lengo la kujifunza, lakini tutabisha kifedhuli tu!!
  Mungu atusaidie sote. Amina
  Siyi

 97. Pendael,

  Watu wenye maneno mengi hivi kama wewe mara nyingi huwa hawako mbali na uongo.

  Ili twende sawa nataka unijibu tu haya maswali mawili:

  1. What is Theology?

  2. Nini tafsiri ya Kiswahili ya hii tungo “that they may be one as we are one”?

  Ninakuona unavyopinga kitu ambacho wewe mwenyewe unakifanya. Na unasema uongo yawezekana bila kujua.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s