Naomba mniombee kwenye maeneo yafuatayo!!

maombiiBwana Asifiwe,

Naomba mniombee kwenye maeneo yafuatayo maana yananitatiza sana na peke yangu siwezi

1.Roho inaniuma sana na mara zote ikiuma ni msiba,naomba mniombee usitokee katika ukoo wetu na roho iache kuuma mana tangu mwaka jana mwezi wa 9 nilipata miscarriage ndo ilianzia hapo hadi leo inauma mara kwa mara na inansumbua sina raha.

2.Nipate mume atokaye kwa Mungu, nina miaka 26 na sina mchumba wala mume.Wananiacha kwa sababu zisizo za msingi na mimi siezi kukaa nao muda mrefu najikuta tu nawachoka bila sababu.Mimi si mvumilivu kabisa naomba Mungu anipe uvumilivu

3.Nipate kazi Tanesco nimefanya interview ya mwisho majibu yanatoka wiki hii

4.Niokoke na nisismame kwenye wokovu niachane na tamaa na mambo ya kidunia

5.Dada yangu akipata mimba inatoka kabla ya kujifungua au anazaa njiti na mtoto anafariki, Mungu amsaidie apate mimba na ajifungue salama.

Asanteni sana na Mungu awabariki

–Debora

Advertisements

10 thoughts on “Naomba mniombee kwenye maeneo yafuatayo!!

 1. Kwa Debora na wengine wengi humu mlioleta maombi. Jambo la msingi na la kwanza ambalo binafsi nimelishuhudia maishani mwangu, kwanza kuamua KUOKOKA na kuachana na maisha ya dhambi. Kumbukeni hasa kwa mtu anaye shiriki zinaa na mtu yeyote maana yake ameunganishwa na mtu huyo. Sasa fikiria umezini na wanaume watatu au zaidi na kila mmoja ana mapepo yake, kwa kushiriki nao maana yake na wewe umepokea sehemu ya upako wao (mapepo). Lazima tu hali yako itakuwa mbaya. Ndio maana mwanamke/mwanamme malaya lazima atakuwa na lundo la dhambi zingine zkiambatana nae na ni kazi sana kuacha zinaa hasa unapokuwa umetembea na wanaume/wanawake wengi.

  Sasa basi matokeo ya roho nyingine ni kama hayo ambayo waweza kuwa unayapitia (sio lazima iwe hiyo lakini). Hapo cha msingi ikatae hiyo dhambi ya zinaa (2Timotheo 2:22), mgeukie YESU kwa toba ya kweli mkabidhi njia zako na dumu katika maisha ya utakatifu kwa kupenda kusali na kusoma neno la MUNGU (2Timotheo 3:16-17). Ila pia chukua hatua hii tafuta kanisa la kiroho kweli kweli lenye mchungaji aliyedhamiria kuwapeleka watu mbinguni na sio wababaishaji ambao mungu wao ni matumbo yao!

  Hayo mambo mengine ambayo umeomba maombi hapa pamoja na watu wengine, MUNGU wetu anaweza kufanya kulingana na imani zetu. Ila kama sehemu yangu, nakuombea wewe Debora pamoja na wahitaji kwamba BWANA wangu YESU KRISTO awape majibu sawasawa na mahitaji ya mioyo yenu kulingana na kipimo cha imani kilichomo ndani yenu. Pokeeni kwa Jina la YESU!

 2. Yesu asifiwe mm nahtaji maombi katika mahusiano, nlkuwa na mchumba lakin ghafla naomba maombi yenu ili mungu atusuluhishe kwa neema na nguvu zake na tufunge ndoa

 3. Mungu akubariki sana dada kwa kutambua kuwa yy ni ndiye jibu!!!cha msingi tu tafuta kanisa la kipentecoste
  lililo jiran na ww kisha onana ma mchungaji kwa mazungumzo zaidi

 4. Tumsifu Yesu KRISTO Dada Debora, pole kwa magumu yanayokupata,, lakin 2mshukuru MUNGU umejua tatizo lako, kuokoka, Neema hii iko Juu yako n vile tu hujaikubali sawasawa, KUMPA YESU MAISHA ayaongoze ndiko kuna Amani mambo mengine ni mbwembwe tu, mpate Yesu upate yote,, Uwe mfuasi wa YESU na sio Mshabiki, ndipo utatoshelezwa ktk kila jambo. UNAJUA M2 HAWEZI KUTULIA MPAKA AMETULIA KTK MOYO WA YESU, n maombi yangu usimame ktk wokovu, Amina.

 5. Dada katika yote uliyoomba hapa ni moja tu ndilo la maana sana kwa sababu ndio ufunguo wa kufungua hayo mengine uuliyoomba. Yaani namba nne (4) kuokoka. Nenda katika kanisa linalofundisha habari za kuokoka watakusaidia. Bila kuokoka amani hutapata kamwe kwa sababu Yesualisema amani nawapeni, na si kama ulimwengu utoavyo. Maana yake kama unakosa amani moyoni ni kwamba mwenye amani yake kaichukua wewe huna ndiposa hutakuwa na amani mpaka umepatana naye kwa njia ya kuokoka. Fikiri sana hilo!!!

 6. Bwana Yesu apewe sifa…ninaomba mniombee nipate kazi nzuri itokayo kwa Bwana nimehangaika kutafuta kazi na kutuma maombi sehemu nyingi lakini sijafanikiwa pia naomba mniombee Mungu anipe imani thabiti nimtegemee yeye ktk kila jambo na aniondolee nguvu zote ambazo ni kinyume na maagano yake na mikosi na balaa visipate nafasi juu yangu na hatimaye nisimame katika neno lake…

 7. Usijal Mungu wetu ni mwema na atakusaidia kadiri ya kiwango cha imani ulichonacho nasi tupo pamoja na wewe katka maombi

 8. Ninakuombea dada yangu ukapokee muujiza wako sawa sawa na mapenzi ya Mungu, Mungu akakuponye, akakuondolee hiyo shida inayokupata katika jina la Yesu Kristo wa Nazareth aliye hai, Ukapate mume atokaye kwa Mungu,Misiba ikatoweke katikati ya ukoo wako,dada yako asizae njiti tena, ukapate ajira TANESCO katika jina la Yesu Kristo aliye hai.Wewe shetani mlaaniwa huna mamlaka na dada huyu ninaenda kuvunja mikataba ya kuzimu katika jina la Yesu Kristo wa Nazareth aliye hai,Mungu ninakusihi ukamsimamishe imara katika wokovu wake.Amen

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s