Pamoja na kuwepo tishio la Ebola, Mwinjilisti Morris Cerullo anakuja Africa!

morrisc

Bado kuna taarifa nyingi kwenye vyombo vya habari kuhusu tishio la kihistoria la ugonjwa wa Ebola, lakini haitamzuia mwinjilisti wa kimataifa Morris Cerullo kuja Afrika kwa siku 11 kuomba kwa ajili ya bara hili na kukutana na watumishi wa Mungu.  Mwinjilisti Cerullo mwenye umri wa miaka 83 amekuwa akimtumikia Mungu kwa zaidi ya miaka 68 katika nchi mbali mbali zaidi sana Afrika. Mwezi huu atatembeleaAccra, Ghana; Abidjan, Ivory Coast; Lagos, Nigeria; Kigali, Rwanda; Bujumbura, Burundi; Nakuru, Kenya;  na Juba, South Sudan.

Advertisements

4 thoughts on “Pamoja na kuwepo tishio la Ebola, Mwinjilisti Morris Cerullo anakuja Africa!

 1. Nampenda sana Mtu huyo wa Mungu Dr.Moric Curulo,Tukiwatumia vizuri watumishi wa Mungu Bwana Yesu atatuinua juu.

 2. WAKATI UNABII WA CERULLO NA MWALIMU MWAKASEGE
  KUHUSU UCHUMI UMETIMIA………
  Dunia nzima sasa imefunikwa na MIALE YA MOTO WA MAARIFA ya Yesu
  sawa na HABAKUKI 2:14.Toka Mungu amewaita watumishi wake Mwalimu
  Mwakasege na nabii Cerullo,Yesu amewatumia kwa viwango vya kutisha
  mno katika kuisambaza miale ya moto wa maarifa ya Roho Mtakatifu yaani
  ROHO/MACHO SABA YA MUNGU.

  Mungu akikumbuke kizazi cha Mwinjilisti wa kimataifa Morris Cerullo
  kwa namna ambavyo alimtumia kuilea na kuweka chachu ya maarifa ya Yesu ndani ya huduma ya NABII NA MWALIMU C.MWAKASEGE.Bila shaka
  Mwalimu Mwakasege alijifunza na bado anaendelea kujifunza mengi kutoka
  kwa nabii Cerullo ambaye mpaka sasa amemtumikia Yesu kwa zaidi ya miaka 60!

  Namshukuru sana Mungu aliye hai kwa kuendelea kumuinua mtumishi
  wake mwalimu Mwakasege katika unyenyekevu wote,amempa huduma
  iliyofunikwa na utiisho na maarifa ya kutisha.Jambo zito ambalo nimejifunza
  kwa Cerullo na Mwakasege ni namna ambavyo wananyenyekea sana
  chini ya mkono hodari wa Bwana!Kila ninapofuatilia mafundisho wanayoongozwa kufundisha huwa NAJIKUTA NABUBUJIKA NA KUMRUDISHIA MUNGU UTUKUFU.Nilikuwa namuuliza Mungu kwenye mawazo kwamba ni kwanini Yesu ambaye anaishi ndani ya moyo wa Cerullo
  ameamua kuzitembelea nchi za GHANA,IVORY COST,RWANDA,BURUNDI,KENYA NA SOUTH SUDAN.Mungu amtie nguvu
  mwalimu wa kimataifa,Cerullo aweze kutimiza kusudi lake katika nchi hizi.

  Ni kweli kwamba hizi nchi ziko katika KIPINDI CHA MPITO KIROHO lakini
  nahitaji kujua zaidi kile ambacho Yesu anataka kupanda na kujenga.Ndipo
  sasa Roho Mtakatifu aliponipa ujumbe unaotoka katika YEREMIA 1:10 ya kwamba Mungu amemtuma nabii Morris Cerullo katika hizi nchi ili awashirikishe wateule wa hizo nchi SIRI ZA NAMNA YA KUNG’OA, KUBOMOA,KUHARIBU NA KUANGAMIZA NGOME ZA MANABII WA UONGO katika nchi zao ILI WAPANDE NA KUJENGA NGOME YA YESU.Na hichi ndicho ambacho Mwalimu Mwakasege na watumishi wengine wa Mungu aliye hai wanakifanya hapa TANZANIA.Ndiyo maana ngome za manabii wa uongo hapa Tanzania zinaendelea kuanguka na kusambaratika
  kila kukicha na mvua kamili za miale ya moto zimeshaanza kunyesha.

  RADI YA MIALE YA MOTO ULAO INAENDELEA KUTEKETEZA KAZI
  ZA MANABII WA UONGO(1 SAMWELI 2:9-10).

  Semina ya mwaka huu 2014 iliyofanywa na Mwalimu Mwakasege pale
  jangwani IMELETA UKOMBOZI WA KUTISHA KWA WATEULE katika
  ULIMWENGU WA ROHO!Kanisa ni lazima lipambane kwa juhudi na maarifa
  ya Yesu ili kuangamizi ROHO ZA MIUNGU(roho za mizimu).Hizi ni roho
  ambazo zinaendelea kuwatesa sana wateule ambao wanaabudu katika
  huduma(madanguro) za manabii wa uongo.Somo hili halifundishwi katika
  makanisa ya wateule na manabii wa uongo wameutumia udhaifu huo
  kuwavuta wateule katika huduma zao.

  Kinachofanyika ni kwamba wateule walio wengi wamefungwa na roho za
  mizimu sasa wanapokimbilia kwa manabii wa uongo ndiyo wanaenda kuweka maagano yaliyo imara na mizimu bila ya wao kujua!Manabii wa uongo ni wachawi na waganga ambao wanashirikiana na roho za kuzimu
  ambazo ndiyo vitendea kazi vyao.Wao walishakataliwa kwa kumkufuru
  Roho Mtakatifu tangu wakiwa tumboni mwa mama zao.Nilikuwa naongea na nabii fulani wa uongo akaniambia kuwa pamoja na kwamba wanatamka
  jina la Yesu lakini tafsiri ya yale wanayoyatamka na hata kuyafundisha,
  INARATIBIWA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO.Kwahiyo katika ulimwengu
  wa mwili anaweza kutamka neno la kawaida lakini tafsiri yake katika ulimwengu wa roho ni matusi mazito!

  INAENDELEA……………..hakikisha hauikosi,hila zote za ngome za manabii wa
  uongo zinawekwa hadharani.

 3. Mungu aliye hai aendelee kumbariki kwa viwango vya kutisha,mtumishi
  wake,Mwalimu na Mwinjilisti MORRIS CERULLO!Huyu ni mmoja kati ya watumishi ambao wamefanyika baraka kwa bara la Africa.Ni maombi yangu
  kwa Mungu kwamba wakati Morris Cerullo atakapomaliza utumishi wake
  katika uzee mwema,Yesu ainue mtumishi mwingine mwenye maono makubwa kutoka katika kizazi chake.Atapomaliza vizuri utumishi wake wa kazi kubwa na ngumu anayoendelea kuifanya,ule UROJOUROJO wa mbinguni unamsubiri kwa hamu!

  KWA FAIDA YA WATU WOTE WENYE NIA NJEMA!
  Mwalimu na nabii Morris Cerullo ni baba wa kiroho wa Mwalimu Mwakasege
  hasa katika kumkuza kihuduma.Mwalimu,mtume,nabii,mwinjilisti na mchungaji Christopher Mwakasege alimpokea Yesu au alizaliwa mara ya pili
  katika mkutano wa injili wa Shujaa wa imani mzee wetu,marehemu Moses
  Kulola.Kwahiyo Moses Kulola ni baba wa kiroho wa Mwalimu Mwakasege
  kwa kumzaa na Morris Cerullo ni baba wa kiroho katika kumkuza kihuduma
  na hii ni kwasababu huduma ya Mwakasege na Cerullo zinafanana.Mungu alimtumia Cerullo wa Marekani kuikuza na kuweka msukumo wa ajabu ndani ya huduma ya Mwakasege wa Tanzania kwa muongozo wa ROHO MTAKATIFU.

  Mwaka 1985 pale Kenyata Conference jijini Nairobi,nabii Morris cerullo alitoa tafsiri ya ndoto iliyokuwa inahusiana na utumishi wa mwalimu Mwakasege!Kijana Mwakasege wakati huo,alijikuta anapata msukumo wa
  ndani wa kwenda kwenye semina ambayo iliandaliwa na Cerullo pamoja na wenzake pale kenyata Conference,Nairobi.Mwakasege alikuwa amepanga
  kutafuta nafasi(appointment) ya kuonana na Cerullo ana kwa ana ili aweze
  kumtegulia kitendawili cha ndoto ambayo Mungu alikuwa akimsesha kuhusu utumishi wake.Hata hivyo hakupata hiyo nafasi na badala yake Mungu akaamua kumtumia Cerullo akiwa madhabahuni kuelezea mstari wa Bibilia ambao Mwakasege alipewa katika ndoto!Ilikuwa ni jambo la ajabu
  kwasababu somo ambalo Cerullo alikuwa anafundisha lilikuwa alihusiani kabisa na huo mstari!Na hii ilitokea baada ya Mwakasege kuachilia sadaka ambayo Roho Mtakatifu alimuongoza kutoa!Nabii Morris Cerullo alisimama
  gafla na kunyoosha kidole chake kuelekea pale alipokuwa Mwakasege alafu akasema “Hivi ndivyo Bwana anavyosema……….”.Cerullo alikuwa hamjui Mwakasege lakini Mungu alikuwa ndani ya Cerullo alimuona na akaamua kumueleza maana ya ule mstari aliyompa kwenye ndoto!

  SIRI YA AJABU NA YA KUTISHA MNO!!
  Watumishi wenye huduma ya ualimu kama ilivyokuwa kwa Mtume Paulo
  na Yesu katika mwili wa kibinadamu,huwa wana huduma zote tano na wanaweza kuzitumia kwa wakati mmoja.Musa pia alikuwa mwalimu na nabii kihuduma na Mungu aliwaambia wazi kina Haruni na Miriamu kwamba Musa
  ni zaidi ya nabii(Hesabu 12:6-8).Mtu mwenye huduma ya ualimu ni zaidi ya nabii!Kuna tofauti kati ya huduma ya ualimu na karama ya ualimu.Huduma ya ualimu huambatana na huduma zote tano kama zilivyotajwa katika Waefeso 4:11.
  Ukitaka kuliona hili kwa uwazi fuatilia huduma ya Paulo,Yesu,Morris Cerullo.
  Mwakasege na wengineo wenye huduma ya ualimu duniani kote.Watu wenye huduma ya ualimu wanaojitambua kiroho huwa wana kiwango cha kutisha cha unyenyekevu wa Yesu ndani yao.Kila jambo huwa wanafanya
  kwa kuomba kibali cha Yesu.NI WATUMISHI AMBAO WANAJITAMBULISHA
  KULINGANA NA VILE WANAVYOONGOZWA KUJITAMBULISHA.WENGI HAWAJIITI MANABII SIYO TU KWASABABU WAO NI ZAIDI YA MANABII BALI
  MUNGU HUWATAMBULISHA JINSI APENDAVYO YEYE.Watumishi wenye huduma ya ualimu wanatembea na ROHO YA MAARIFA kwa viwango vya kutisha kwa kadiri walivyokubali kunyenyekea mbele za Mungu.Hii aina maana kwa kwamba huduma ya ualimu ni bora kuliko huduma zingine bali
  huduma ya ualimu ni huduma iliyoficha siri nzito mno ndiyo maana Mungu
  alipokuja duniani alijifunua kama MWALIMU(RABI).Hili jambo linahitaji unyenyekevu kulielewa.Kuna tofauti ya mtu anaetembea na huduma moja
  au mbili na yule anaetembea na huduma zote tano.Sikiliza,mtu yeyote aliyezaliwa mara ya pili anatembea na ROHO YA UNABII-Roho Mtakatifu(Ufunuo 19:10).Lakini hii haina maana kwamba kila aliyeokoka ni nabii kihuduma.Huduma ya kinabii ndani ya kanisa imevamiwa na wajumbe wa
  shetani kwasababu wateule hatuweki bidii kutafuta maarifa ya Yesu na badala yake tunajaribu kuweka bidii ya kufuata injili ya mafanikio yanayotokana na miujiza ya shetani!Wajumbe wa ibilisi wanaendelea kueneza mafundisho ya mashetani na kuwafanya wateule wengi waendelee kuwameza MASIKINI KWA SIRI na Yesu ameamua kuingilia kati ili kuwakomboa kwa moto wa maarifa yake(Habakuki 3:12-14).

  Wakati mwalimu Mwakasege ni nabii wa Mungu aliye hai ambaye amepewa
  maono kwa ajili ya watanzania(wateule) wanaoishi mahali popote duniani.Mwinjilisti Morris Cerullo ni nabii wa Mungu aliye hai aliyepewa maono kwa ajili ya wateule wote duniani hasa waafrika.Nchi hizo za Afrika ambazo ameongozwa na Mungu kuzitembelea kihuduma ni nchi ambazo
  ZIKO KATIKA KIPINDI CHA MPITO KIROHO.Mungu anawatafuta wateule
  wake ambao wamo ndani ya hizo nchi kwa gharama ya machozi,jasho na damu ya Yesu!!Wateule wa Yesu ndiyo watu matajiri kuliko wote duniani
  lakini kwasababu ya vita kati ya uzao wa Yesu na uzao wa shetani,watu wa Mungu wamejikuta kwenye changanoto nzito za kielimu,kiafya,kiroho na kiuchumi ingawa kiuhalisia hizi zote ni changamoto za kiroho.Mungu amekuwa akiinua watumishi mbalimbali ili kulisimamisha kusudi lake ndani
  ya bara la Afrika.UFUNDISHAJI NA STAILI YA MWAKASEGE INAFANANA SANA NA YA CERULLO JAPO MUNGU HUJIFUNUA KWA HEKIMA NA MAARIFA TOFAUTI.FUATILIA CD ZA CERULLO UTABAINI HILI.

  UNABII ULIOANDIKWA NDANI YA KITABU CHA HABAKUKI UMETIMIA!!!

  Nabii Morris Cerullo na Nabii Mwakasege wametabiri mafanikio ya kiuchumi
  au tuseme ukombozi wa kiuchumi kwa wateule wa Mungu.Mwaka huu 2014,Mwinjilisti Cerullo alitoa unabii kuhusu mafanikio makubwa ya kiuchumi kwa wateule wa Mungu popote pale walipo duniani.Miaka miwili
  iliyopita Mwalimu Mwakasege alitoa unabii kuhusu hatima kubwa na ya kutisha ya Taifa la Tanzania na uchumi wa wateule watanzania ambao wanaishi nje na ndani ya Tanzania.

  Unabii wa watumishi hawa unapatikana katika mstari wa Habakuki 2:14 unaosema “KWA MAANA DUNIA ITAJAZWA NA MAARIFA YA UTUKUFU WA
  BWANA,KAMA MAJI YAIFUNIKAVYO BAHARI”.Unabii huu unaweza kuelezewa zaidi na Danieli 12:4 “…….WAKATI WA MWISHO,WENGI WATAENDA MBIO HUKO NA HUKO, NA MAARIFA YATAONGEZEKA”.
  Maarifa ya Mungu yameongezeka na wakati huo huo maarifa ya shetani pia
  yameongezeka lakini kulingana na Habakuki 2:14, maarifa ya shetani yamemezwa na maarifa ya Mungu kwa wale wenye macho ya rohoni wameshaliona hili.Kulingana na Hosea 4:6 ni kwamba MAARIFA YA YESU
  ndiyo yanayoleta ukombozi kwa watu wa Mungu.Kwahiyo huu ndiyo wakati
  wa watu wa Mungu waliokataa kuolewa na shetani, KUWA HODARI NA KUTENDA MAMBO MAKUU.Danieli 11:32 inasema “…….LAKINI WATU WAMJUAO MUNGU WAO WATAKUWA HODARI, NA KUTENDA MAMBO MAKUU”.Pamoja na unabii huu kutimia, wateule ambao watamtumikia Mungu kwa ulegevu na kukataa kuingia ndani ya unyenyekevu wa Yesu
  WATAENDELEA KUANGAMIA!Wakati wenzao wanakula wao wataishia kutazama tu maana hata nafasi ya kunawa hawatapewa!!

  HII NI SUMU KALI INAYOKATA MATUMBO YA WAJUMBE WA SHETANI
  POPOTE PALE WALIPO DUNIANI.UJUMBE HUU NI MOTO ULAO.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s