Ujumbe wa mwezi November na Mwamfupe Anyisile

imagesShalom wapendwa katika Kristo Bwana. Awali ya yote niwape pole na hongera kwa kazi ya Mungu kila mmoja kwa sehemu aliyoitiwa kwayo.

Ashukuriwe sana Jehova kwa kuwa hapana miongoni mwetu asiyependa kuwa mwana wa Mungu ama lah yupo basi na ionekane kazi ya uinjilisho wetu juu ya nafsi na roho yake! Ndugu zangu! Ikiwa ninalo la kujisifu basi ni katika Kristo ama si hivyo ninalo jipya gani mwanadamu mimi pasipo neema ya Mungu? Maana ikiwa nitajisifu katika niliyo nayo katika mwili huu wa uharibifu basi ninayo ziada kwa shetani.

Lakini kama nalijisifu katika Kristo, basi nalijisifu katika utumwa wa viungo vyangu katika gereza la INJILI nalo ni lile lenye fahari ile iliyo mbali na fahari ya dunia! Maana; niseme nini basi? Kwa kuwa pasipo YESU kuimiliki kawaida ya kuishi kwangu ili nisipate kuwa mwamuzi katika yale niyapendayo. Je mimi niseme niko hai tu kwa sababu ya kule kutembea kwangu?

Lah! Hasha mimi ni mfu tu. Lakini sasa ni hai naam; wa roho na mwili pia kwa kuwa ile sheria ya Mungu imeshinda vita ya mwili wangu wa kujisifu katika kiburi cha uzima. Na sasa si mimi katika ujana huu ingali nimo katika ujana huu naam; tena si mimi katika dunia hii ingali nimo katika dunia hii! Maana kwa neema ya Mungu siishi kwa faida za mwili ili roho yangu ipate hasara bali naishi kwa hasara za mwili ili roho yangu ipate faida!

Maana nimeyachagua magumu kuwa sehemu ya kuishi kwangu na mepesi nimeyatupilia mbali ili ubinadamu wangu uadhibiwe pamoja na KRISTO. Tena ujapo kufa ufe pamoja na KRISTO na ujapofufuliwa ufufuliwe pamoja na KRISTO! Kwa maana yale matamu ya dunia nimeyahesabu kuwa machungu na yale machungu ya rohoni nimeyafanya kuwa ndiyo matamu kwangu ili sheria ya Mungu ipate kutawala pamoja na mimi.

Lile nilitamanilo mbali na Mungu likifanywa kuwa haramu na lile nisilopenda pamoja na Mungu likifanywa kuwa halali kwangu! Ndugu zangu pamoja na KRISTO Yesu; katika ninyi kama kunaye apendaye kujivuna basi na ajivune katika yale yenye hasara kwa Utu wa nje bali yenye faida kwa Utu wa ndani. Kwa maana kunayo hatima njema na hakika ya Peponi kwa yeyote asiyejitenga na NDIYO ama HAPANA ya Mungu.

Naliwashirikisha haya ninyi waombao pamoja nami  mmeyachagua maisha ya dhiki duniani ili kujihakikishia maisha ya raha Mbinguni tusipoiacha njia ya KWELI na UZIMA wa MILELE

Aaamen, Mbarikiwe sana!

-Mwamfupe Anyisile

Advertisements

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s