MOYO, NAFSI, AKILI, MWILI na ROHO!!

soul

Mimi huwa Napata wakati mgumu sana. Nikiwa kanisani nawasikiliza walimu na wahubiri wakihubiri kuhusu mada ya MOYO, NAFSI, AKILI, MWILI na ROHO  huwa nabaki kwenye sintofahamu ya maswala hayo. Maneno hayo yanabeba maana zipi au maana ngapi?

Kila ninapowasikiliza wahubiri wakisisitiza hayo maeneo nabaki na maswali lukuki. Kwa mfano utasikia au utasoma maandiko yanasema, …..moyo huwa mdanganyifu….”, nimeliweka neno lako moyoni mwangu nisikutende dhambi….. au utasikia wapendwa wakisema, ‘…….hilo ni kanisa la kiroho…..” Niko rohoni….., huyu bwana yuko rohoni sana……., Haya ni mambo ya rohoni sana…., Mtu wa rohoni huwaelewa watu wa rohoni…., na wengine utawasikia wakisema kwamba, Mungu ni Roho nao wamwabuduo inawapasa kumwabudu katika roho. Sehemu nyingine utakutana na watu wakisema, …..Mungu aiweke pema peponi roho ya marehemu……nk, nk, nk.

Yote hayo hunifanya nipate maswali mengi bila kupata majibu. Maswali yafuatayo huwa yananiijia kwa sana kila siku na kupata majibu inakuwa ngumu:

1.      Moyo ni nini

2.      Moyo unakaa wapi mwilini?

3.      Je, Neno la Mungu huwa tanaliweka Moyoni au Akilini?

4.      Mungu Baba, Mungu Mwana, na Roho Mt wanakaa ndani yetu? Wanakaa Sehemu gani? Wanakaa Moyoni, Rohoni, Mwilini, Akilini, Nafsini au Kichwani?  

5.      Je kuna aina ngapi za Moyo?

6.      Roho ya ni nini?

7.      Roho iko upande gani wa mwili?

8.      Nafsi ni nini?

9.      Nafsi inakaa wapi mwilini?

10.  Mwili ni nini na uko wapi?

11.  Mwanadamu ni nini?

12.  Akili ni nini na ziko wapi mwilini?

13.  Dhamira ni nini na inakaa wapi mwilini?

Hebu wapendwa nisaidieni kupambanua kulingana na uelewa wenu. Ninyi mwaelewaje?  

Mr. Milinga.

Advertisements

35 thoughts on “MOYO, NAFSI, AKILI, MWILI na ROHO!!

 1. Pia, juu ya kuzaliwa mara ya pili, 1 Petro 1:23, Kwa maana mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele.

  Tukiunganisha mstari huu na Yohana 6:63, Maneno hayo ni Roho, na tena ni Uzima. Kwahiyo mtu ni Roho, anapokuwa amezaliwa na Mungu, ni roho iliyo hai, roho ya Kristo (Rumi 8:9)

 2. Yohana 6:63
  Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu. maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.

  Yohana 3:6
  Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili, na kilichozaliwa na Roho ni roho

  Genesis 6:3(a)
  And the Lord said, my spirit shall not always strive with man, FOR THAT HE IS ALSO FLESH…..(emphasis is mine)

  Naomba kuendeleza ule mjadala wa msingi kwa kuangalia zaidi hiyo mistari hapo juu. Nilipochangia hapo mwanzoni nilisema kwamba kimsingi mtu ni roho. Mungu alipomwuumba mtu kwa sura na mfano wake pale Mwanzo 1:6-7 alikuwa amekamilisha kumwuumba huyo mtu. Lakini mtu huyu alikuwa katika hali ya yale maneno aliyoyasema Mungu, kama niliyonukuu hapo Yohana 6:63. Na hayo maneno ndiyo roho, na ndiyo yaliyotia uzima, au ndiyo uzima wa yule mtu.

  Ule uzima ninaousema ni kuwa na ushirika na Mungu pekee. Lakini pale alipouacha ushirika na Mungu alikufa, katika lile neno, sura na mfano wa Mungu ilisitishwa ndani yake, akawa (katika roho) na sura na mfano wa yule aliyemsikia na kumtii, yaani shetani (ndiyo maana katika Yohana 8:43a, Yesu anawambia wayahudi kwamba, “ninyi ni wa babaenu ibilisi). Shetani naye ni roho. Hivyo mtu huyu asiyemtii Mungu angali ni roho, lakini ni roho iliyokufa, kwakuwa haina ushirika na yule aliyeoumba, haifanani naye tena. (Tukumbuke kuwa katika mwili, Adam alikufa miaka mingi tu baada ya kufanya lile kosa la kutokumwamini Mungu)

  Lakini Mungu kwa wema wake aliendelea kuwasiliana na huyu mty, japo sasa ni kwa sauti ya nhe, yaani katika mwili. Na kama asemavyo Paul katika Warumi 8:6-8, mwili hauwezi kumtii Mungu, Mungu alighairi, alichoka hatimaye akaangamiza kile kizazi cha kwanza, Mwanzo 6.

  Lakini mpango wq Mungu ulikuwa ni hatimaye, utimilifu wa nyakati utakapokuja, kumrejesha mwanadamu katka mahusiano na Mungu. Ndiyo ambapo Yesu anasema sharti huyu mwanadamu AZALIWE NA MUNGU, azaliwe katika roho; sasa kilichozaliwa na Roho, si ndiyo roho? Mtu, anakuwa mzima tena katika Mungu. Yule asiyezaliwa mara ya pili anakuwa bado ni mfu katika Mungu.

  Nafikiri nimeliweka vizuri kwq uchache mno. Ni kwa sababu ya ugumu wa kuelewa maana ya roho kunakochanganya kabisa akili zetu za mwilini.

  Nimalize na mistari michache.

  2 Corinthians 5:17 (KJV)

  17. Therefore if any man be in Christ, he is a new creature, old things are passed away, behold, all things are become new.

  Mistari ya 16 na 18 inatoa context.

  1 Corinthians 6:16
  But he that is joined unto the Lord is one spirit.

  Yeye aliyeungwa na Bwana ni ROHO MOJA. Kwanza ni roho…., kisha ni mmoja na Mungu.

  Tafadhali, tuendelee kuchangia na kujifunza kati yetu.

  Mungu awabariki.

 3. Kaka Millinga
  Wakati somo likiendelea naomba tafakari na haya maandiko

  Ebra7.9 Tena yaweza kusemwa ya kuwa, kwa njia ya Ibrahimu, hata Lawi apokeaye sehemu ya kumi alitoa sehemu ya kumi;

  7.10 kwa maana alikuwa katika viuno vya baba yake, hapo Melkizedeki alipokutana naye.

  Nami nipate kufunuliwa neno la Mungu aliye hai,

  Ni vizuri kujifunza kwa kusikiliza mafundisho mengine

  Barikiwa,

  Mjoli Haule

 4. Lwembe,

  Usichanganyikiwe kiwango hicho!
  Unasema Baba, Mwana, RM ni fundisho la kipagani? Unaona katika makala yako jinsi unavyoongeza tamko “Mungu” maksudi upindishe swali la Milinga? Hizo ni hila za yule joka wa zamani.
  Unaposema ni ya kipagani licha ya kuwa yameandikwa ndani ya Biblia kwa idadi kubwa utaishia kusema kama biblia yako nayo ni ya kipagani. Kama una fundisho au tafsiri lililo wazi lisemeni!!! Au hakikisha unasema kipagani kwa kukosa maarifa.
  Ndio maana hata kwa swala nyingine unabahatisha mno pasipo chembechembe za kimaandiko, ukitumia AKILI zako zitokazo ubongoni.
  Lwembe, unaweza nukuu mahala ambapo uliwai kusoma mtu akiandika AKILI=Ubongo? Unapochangia, usipindishe hoja il ndipo ujibu. Unapofanya hivyo hakikisha unajibu kwa hoja yako mwenyewe.

  Mungu akuwezeshe.

 5. Wapendwa,

  Nimefuatilia michango ya wapenzi wengi hapa kwenye jukwaa letu la Injili.

  Michango mingi karibu yote imejengwa kwa hoja tena zenye uzito. Mchangiaji wa hapo juu bwana Ziragora ndiye amefunga kazi kwa maandiko aliyotoa.

  Hata hivyo, bado kunahitajika ufafanuzi wa kimantiki, semantikia,kisayansi, kiroho na kimaandiko.

  Wengi wa waliochangia mada wamejikita kote kote. Kwenye sayansi, maandiko, mantiki, semantikia na kiroho.

  Lakini ukichunguza kwa ukweli kabisa tena kwa lugha nyepesi utagundua mambo makuu yafuatayo:

  1. ROHO, MOYO, NAFSI, = MWANADAMU.

  Hii ikimaanisha kwamba maneno hayo hutumia ama na maandiko au wahubiri lakini wakimaanisha jambo moja tu, nalo ni BINADAMU.

  Kwa mfano, maandiko yasemapo , …….roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa…… utagundua kwamba inamzungumzia BINADAMU.

  MWANADAMU = roho + Nafsi+Moyo.

  Ifahamike kwamba kuna wakati watu husema neno MOYO huku wakimaanisha AKILI au UBONGO. Kwa mfano ukisema, …..nilikuwa nawaza moyoni……. ukweli wa kisayansi kabisa ni kwamba ulikuwa unawza akilini mwako kichwani mwako na wala siyo moyoni kwa maana ya kiungo kinachosukuma damu mwilini

  Sehemu ya pili ya maana ya MOYO: Ni kwamba kuna kipindi watu husema MOYO huku wakimaanisha UBONGO. Kwa mfano watu wanaposema kwamba …..Neno la Mungu nimeliweka MOYONI….. Ukweli ni kwamba kimantiki ameliweka UBONGONI au AKILINI. Hii ni kwa sababu UBONGO wa mwanadamu ndio unaotunza kumbukumbu zote za maandishi, maneno, hotuba, mawazo, fikra, nk.

  UBONGO wa mwanadamu ni kama DVD au VCD au FLASHDISK au KOMPYUTA.

  Maandiko yanasema, ……Mfundishe mtoto njia impasayo naye hataiacha hata atakapokuwa mzeee…….. Ukitafakari hapa ni kwamba kila kitu mtoto anachofundishwa kinaandikwa au kutunzwa kwenye UBONGO wake. Kwa hiyo kila kitu anachokiona, anachoambiwa, anachogusa, anachosikia, anachohisi, anachokula, nk kumbukumbu (memory) zake zimehifadhiwa UBONGONI.

  UBONGO ndicho chombo pekee kinachotunza NENO LA MUNGU kama unavyoweza kutunza maandishi yako, picha, nyimbo, sauti kwenye kompyuta, ndivyo hata UBONGO unavyoweza kutunza kila kitu kinachosemwa, kinachoandikwa duniani.

  UBONGO ndio kifaa pekee MUNGU alichokiweka kwa mwanadamu ambapo kikiharibika tu, BINADAMU anabakia kama kompyuta iliyoliwa na virusi.

  Kwa hiyo unaposema NENO LA MUNGU umelieka MOYONI kimaantiki ni kwamba umelisikia, umelikamata na umelisave UBONGONI au AKILINI.

  JE, AKILI NI NINI?

  Ukweli ulivyo ni kwamba AKILI ni NGUVU ya kumwezesha BINADAMU kukumbuka kile kilichotunzwa ndani ya UBONGO Wake. Kwa mfano ukifundishwa jambo lolote shuleni na wakakuletea Mtihani na ukaufaulu sana, wewe inasemekana kwamba una AKILI sana. Hii maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba kutokana na chembechembe za UBONGO wako zilivyo na nguvu kubwa (GB, MB, High capacity) uliweza kukumbuka kila kitu ulichofundishwa au ulichosoma na kwa muda mfupi uliweza kujibu kila swali bila kukosea.

  Kwa hiyo, akili ni UWEZO, NGUVU, (Powe and Ability) kukumbuka na kueleza yale yote yaliyotunzwa ndani ya UBONGO.

  Utakuwa umewahi kujiuliza BINADAMU walitoka wapi? Bila shaka wengi hutoa majibu mengi. Maandiko yako wazi kwamba Mungu alimuumba BINADAMU kutoka kwenye mavumbi na akapewa pumzi ya uhai.

  Lakini ukizidi kuchunguza maandiko na sayansi utakubaliana na mimi kwamba BINADAMU wanazaliwa kutoka matumboni mwa mama zetu. Utakubaliana na mimi kwamba kwa sasa Mungu hafanyi kazi ya kuumba tena. Aliumba mara moja na wala haumbi watu tena kila siku.

  Ukijiuliza BINADAMU anatoka tumboni mwa mama yake , je aliingiaje tumboni mwa mama yake? Utagundua kwamba aliingia baada ya mbegu na yai la kike kuungana.

  Je, Kabla ya yai la kike na mbegu ya kiume kuungana huyu BINADAMU alikuwa wapi? Utapata majibu meeeengi sana hasa kutoka kwa Wapendwa…… .

  Ukichunguza zaidi maandiko ndipo utaelewa kwamba BINADAMU ameumbwa kutokana na udongo kamili. Hapo ulipo wewe umetokana na udongo kabisa. Kisayansi ukichunuza madini yaliyomo kwenye UDONGO utayakuta mwilini mwa mwanadamu. Vyakula tunavyokula ndivyo hutengeneza protini na vinasaba vinavyoungana na kuunda kiumbe tumboni mwa mama. Ukila karanga, mihogo, maharage, majani, matunda, chumvi, nyama, nk hivyo ndivyo huenda kujitengeneza kwenye kizazi chako na kuunda ‘mbegu” au “yai” na hivyo vikiweza kukutana kama ilivyo Negative+Positive unapata UMEME, basi utakuta unapata BINADAMU baada ya -Ve force inapokutana na +Ve force kutoka kwa mwanaume na mwanamke. Hivyo, ndivyo uumbaji unavyofanyika.

  KWA HIYO KWA UFUPI:
  Ni kwamba MOYO, NAFSI, ROHO ni maneno yatumikayo mara nyingi yakimaanisha BINADAMU mwenyewe kwa upande mmoja na kwa upande mwingine
  MOYO, ROHO na NAFSI hutumika kumaanisha AKILI, FIKRA, MAWAZO na UBONGO wa BINADAMU.

  Kwa hiyo, ni juu yako kuelewa au kubaini kila mara usikiapo mtu akitumia maneno hayo ROHO YANGU, MOYO WANGU, NAFSI YANGU kujua haraka ana maanisha nini?.. Kwa hiyi vyote hivyo huwa ni kitu kimoja.

  HAKUNA SEHEMU HATA KIDOGO NDANI YA BINADAMU AMBAYO UKIMPASUA BINADAMU UTAKUTANA NA KITU KINAITWA …..NAFSI au ROHO. UTAKACHOKIONA PEKE YAKE NI .”…MOYO na UBONGO…..”

  MOYO na UBONGO ndivyo pekee vinavyomtia UHAI na NGUVU Binadamu.

  Somo litaendeleeeeaaaa……………………..

 6. Ndugu Milinga,

  Utuvumilie tukugeukie tu kwani ulisema utafika. Pokea hii nayo ili ufikapo uamue mwenyewe.

  Naomba tutafakari haya maandiko matakatifu:

  “Marko 12:30 nawe mpende Bwana Mungu wako kwa MOYO WAKO WOTE, na kwa ROHO YAKO YOTE, na kwa AKILI ZAKO ZOTE, na kwa NGUVU ZAKO ZOTE

  Mambo ya Walawi 17:11 Kwa kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu; nami nimewapa ninyi hiyo damu juu ya madhabahu, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu; kwani ni hiyo damu ifanyayo upatanisho kwa sababu ya nafsi.

  Mwanzo 2:7 Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.”

  Mimi naona Biblia iko wazi inaposema juu ya MOYO, ROHO, AKILI na NGUVU.
  Pia Uhai wa mwili uko ndani ya damu.
  Damu inaitumikia nafsi na hata kujulikana kuwa ndiyo nafsi yenyewe.
  Huo uhai apatikanayo ndani ya damu ndiwo unamfanya mtu awe nafsi iliyo hai. Ina maana damu inaweza kuwa hai au inayokufa.

  Hebu tuangalie hili andiko:
  “Wagalatia 2:20 Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na UHAI nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa NAFSI yake kwa ajili yangu.”

  Kristo alitoa nini haswa kwa ajili yetu? Kwani Biblia hapa inasema alitoa nafsi yake. Hiyo aliyoitoa tunawezasema ni Hisia, hiari, akili au moyo au roho yake? Hatujue kama alitoa damu yake ili atukomboe? Hivi huwezi disconnect nafsi na damu(uhai).

  Biblia inasema:”Waefeso 2:13 Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa DAMU yake Kristo.”

  Jumlisha, uone kama hutaona kama hiyo nafsi Kristo aliyoitoa kwetu ndio damu yake!!!

  Hivi hatuna haja ya kubahatisha tukitafuta sana nafsi ni nini wakati Biblia inatuonyesha wazi. Nafsi ni uhai unaokaa ndani ya damu. Ule uhai unasababisha viungo vingine vinavyojumuika na akili, hisia, hiari… viweze tumika kabisa.

  Ubarikiwe.

 7. Ndugu Millinga,
  Kwa leo nitakupa jibu la swali lako linalosema NAFSI NI NINI?
  kwa mijibu wa NENO lililofunuliwa NAFSI imegawanyika sehemu mbili. 1. NAFSI YA ROHO 2. NAFSI YA MWILI. Kwa ujumla NAFSI inaundwa na vitu vinne ambavyo ni HISIA, HIARI, AKILI NA MATAMANIO YA MOYO. Ukiwa na NAFSI YA ROHO ina maana kuwa una hisia za Mungu ambazo zinakuongoza kuwa na hisia za utakatifu wa Mungu ambazo hazikutoi nje ya NENO la MUNGU, Pia una Hiari moja tu ambayo inahiari kufanya mambo ya ufalme wa Mungu peke yake, pia una AKILI ya Mungu inayofikiri na kuamua mambo yote sawasawa na NENO la Mungu, pia una Matamanio ya Moyo / Moyo wako unatamani mambo ya ufalme wa Mungu yaani TUNDA LA ROHO MTAKATIFU – Galatia 5:22 wakati wote liwe ndani yako. SHIKA NENO!
  Ukiwa na NAFSI ya mwili maana yake una hisia zinazohisi mambo yaliyokinyume na ufalme wa Mungu, Unahiari mambo yaliyo kinyume na ufalme wa Mungu, pia una AKILI ambayo maamuzi yako yanaongozwa / yanabase kwenye kanuni za elimu uliyofundishwa, mila na desturi ulizofundishwa na maamuzi yako siku zote hayazingatii NENO linasema nini. Mfano NENO linasema “HAKUNA LISILOWEZEKANA KWA MUNGU” lakini elimu zingine tulizofundishwa zinaonyesha kushindwa maeneo fulanifulani. Kwa hiyo NAFSI ya mwili ina akili inayoona kushindwa shindwa maeneo fulanifulani lakini NAFSI ya ROHO/ MUNGU ina akili inayoona kushinda kila eneo. Kwa kumalizia naomba uelewe kuwa NAFSI ndio eneo linalobeba eneo kubwa la maisha yako. Kama mtu akiibiwa NAFSI yake basi ujue ameibiwa AKILI, HIARI, HISIA na MATAMANIO ya Moyo. Hivyo ni hatari sana kuibiwa NAFSI. Wachawi wanapokutafuta kukufanyia chochote kibaya wanaingia kwenye nafsi yako kwanza ili waweze kukuweza. Pokea huo ufahamu na ukiwa na maswali zaidi kuhusu NAFSI unakaribishwa. SHIKA NENO!- TENDA NENO!

 8. Ndugu Lwembe,

  Unapoleta uliyoyazungmuzia katika mada ingine ni kwani uliona hayakupokelewa. Lwembe, nakuomba uwe ukiliondoa polepole lile lililoitikiwa kiisha uendelee na mambo mengine.

  Ila nafsi si ndani ya moyo. Ni ndani ya damu. Pengine ukisema moyo ndiyo injini inayofanya nafsi iendelee kuwa na uhai, utakuwa uko sahihi. Lwembe huoni kama hapa kuna utofauti mdogo tu. Neno la Mungu linasema, “damu ya Abeli ililia katika ardhi.” Ndiyo hiyo nafsi yake iliyokuwa ikimuumiza Mungu kwani uhai uko katika nafsi. Nafsi ikichafuka na moyo kama injini inafikia kiwango cha kusimama wala isiendelee sambaza mwilini damu(iliyo hai) inayojumuika kuvipa viungo vingine chakula cha kuvuvia nguvu sememu zingine zinazotengeneza akili, kunusa, kuonja, kuona, kusikia …. Sasa hii moyo, unapoiongelea kifilosofia unakuta imepewa kwa kuchomekwa hayo mamlaka yote kwani kama moyo haitumike vile viungo vyote havitatumika.

  Kwa mfano kiziwi ana moyo(wa mwili na wa kiroho) kama ya watu wengine, lakini kwa sababu sehemu iliyo ndani ya ubongo wake inayojumuika na kusikia haitumike vizuri, yule mtu hawezi sikia; halikadhalika kipofu, ….

  Mimi nataka turudilie mada kwa urefu zaidi jinsi ilivyoletwa na mwenye mada:

  1. Moyo ni nini
  KAMA KIUNGO CHA MWILI, NI NYAMA INAYOSAMBAZA DAMU MWILINI.
  KWA MANTIKI YA FILOSOFIA NA MITHALI, MTU ANAWEZA TUMIA HILO NENO PAHALI PA NAFSI NA ROHO.
  2. Moyo unakaa wapi mwilini?
  KWA KUWA SWALI NI WAPI MWILINI, HATUTAENDA MBALI, INA MAANA NI MOYO WA NYAMA UNAOPATIKANA NDANI YA KIFUA KWA UPANDE WA KUSHOTO.
  3. Je, Neno la Mungu huwa tanaliweka Moyoni au Akilini?
  KWA MANTIKI YA MSINjI NENO LA MUNGU LINAWEKWA AKILINI.
  KWA MANTIKI INGINE NENO LA MUNGU LINAWEKA NDANI YA MOYO NA ROHO KWANI HIYO MANTIKI NI YA KIROHO.
  4. Mungu Baba, Mungu Mwana, na Roho Mt wanakaa ndani yetu? Wanakaa Sehemu gani? Wanakaa Moyoni, Rohoni, Mwilini, Akilini, Nafsini au Kichwani?

  KUKAA KWA MUNGU NDANI YA MTU KUNADHIHIRISHWA NA RM ANAYEWAKILISHA BABA, MWANA NA RM. AKIWA ROHO ANAKAA ROHONI.

  5. Je kuna aina ngapi za Moyo?
  MBILI: YA NYAMA NA YA KIROHO (FILOSOFIA)
  6. Roho ya ni nini?
  NI HIYO PICHA YA MUNGU ALIYOMWEKEA MWANAADAMU KWA MHURI ILI AMTOFAUTISHE NA WANYAMA.
  7. Roho iko upande gani wa mwili?
  ROHO NI ROHO, HAIONEKANI. TUNACHOKIFAHAMU NI KWAMBA ROHO INASHINDANA NA MWILI. HIVI KWA KUWA ROHO HAIGUSIKI INAWEZASHINDANA NA MWILI IKIWA NDANI AO NJE YA MWILI.
  8. Nafsi ni nini?
  NAFSI NI UWEZA WA UHAI.
  9. Nafsi inakaa wapi mwilini?
  INAKAA NDANI YA DAMU
  10. Mwili ni nini na uko wapi?
  MWILI WA KUHARIBIKA NI ULE WA NYAMA UNOUONA.
  MWILI WA ROHO NI HOYO PICHA YA ROHO ITAKAYOENDELEA WAKATI MWILI WA KUHARIBIKA UTAKAPOTOWEKA.
  11. Mwanadamu ni nini?
  NI KIUMBE CHOTE KINACHO MIZIZI KWA ADAMU, MTU WA KWANZA.
  12. Akili ni nini na ziko wapi mwilini?
  AKILI ZIKO NDANI YA UBONGO? NA HUO UBONGO UNAISHI KWA DAMU. NA HIYO DAMU INASAMBAZWA NA MOYO. HIVI KWA MANTIKI YA FILOSOFIA UKISEMA AKILI ZIKO MOYONI UTAKUWA UKO SAHIHI KABISA.
  13. Dhamira ni nini na inakaa wapi mwilini?
  DHAMIRA INAKAA ROHONI. NI KATIKA DHAMIRA NDIPO RM ANAOPERATE ZAIDI. NAFSI INAWEZA JIPANDA SAWA SAWA ILI IUTII MWILI LAKINI DHAMIRA INAENDELEA LETA KIPINGAMIZI.

  Mada inaendelea, tusaidiane tu, nimesema jinsi roho yangu imeniambia niseme.

  Mungu awabariki.

 9. Ziragora,

  Nakuona umezoea mijadala yenye mizaha na kejeli aya Bwana mimi sipo huko. Naomba ujue kuwa;

  1.Hakuna hoja yako niliyokwepa
  2.Sijadhihaki wala kuhukumu mawazo ya Petrus, bali kwa uelewa wangu sijaelewa alichokiandika,
  3.Kumbe hapa unashindana hebu hona hoja zako , umesema…….”…..Mimi sina tabia ya jithahida za kukwama ndani ya upinzani”…….”…Kwa kufupisha, basi ukiona nuru iko, uniige….”. Pole sana.

  Rafiki kama upo makini na michango yangu hakuna sehemu yoyote niliyosema kuwa 100% nipo right kwani najua elimu ya Mungu ni pana na hivyo siwezi kuwa rigid. Ninachoomba tuwe na mjadala unao jenga. kwani wewe unadhani upo sahihi 100%???

  Rafiki utafiti nilifanya na ninaendelea kufanya ushauri wangu kwako fanya utafiti wa kutosha.

  Kwa mfano, nkirejea hoja zako ulizosema kuwa nimezikwepa;;;; Ikiwa umekubali kuwa Kuna Moyo miwili (2) wa nyama na dhahania, sasa unadhani kuwa moyo huo unakaa wapi kama hakuna utu wa dhahania?

  Maneno niliyosema tuyafanyie utafiti binafsi najua kuwa kuna ya kimwili/kawaida na dhahania/kiroho.

  Barikiwa

  **** Tufunguliwe Akili,Tuelewe na Maandiko*********

 10. Mjema,

  Mimi sina tabia ya jithahida za kukwama ndani ya upinzani. Jambo lililo jema ni elimu na siyo upinzani. Sione kwa nini Ndugu Petrus adhihakiwe. Aliyoyasema ni yake, sione kwa nini umeyanukuu kwa kuniandikia ukikwepa niliyokuandikia. Yeye Petrus iko sahihi kulingani na jinsi alivyosema amefanya utafiri wake. Nami nimefanya utafiti. Sasa nawe kama ulikuwa ukijadili pasipo utafiti nenda kabisa ukaufanye, itakusaidia sana.

  Ninachoona ni kwamba unaanza bahatisha katika unachikiita “jua” kisichoambatana na mada hii. Hiyo no makucha uliyoyaficha sasa unaona umeishiwa hoja unaanza yachomoa.

  Nakutakia utafiti mwema.

  Asante.

 11. Ndg Ziragora, Mjema & Siyi,

  Kwa faida ya ufahamu tukiisha kuujua haswa moyo, kwamba ndio makazi ya nafsi, hiyo inayowajibika kwa Mungu, tunaweza kulitazama zaidi jambo hili ktk msingi aliouleta ndg Petrus, alipoyarejea Maandiko ktk Gal 5:16-17 na kutamatisha kwamba maelezo hayo inapewa nafsi na si mwili wala roho. Basi ninanukuu sehemu ya maelezo niliyoyatoa ktk mada ya “Mungu Baba, Mwana na RM” kwani naona hii ndiyo sehemu yake haswa!

  Kwamba ktk 1The 5:23 ndio tunaona kwa uwazi kabisa jambo la jinsi yetu kwamba tu Nafsi, Roho na Mwili; “Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi NAFSI zenu na ROHO zenu na MIILI yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama …”

  Hapa tunaona kwamba mtu ana components tatu ambazo ni mwili + nafsi +roho. Hizo components 3 kila moja ina sifa bainishi tofauti.
  Mwa 1:27 “Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba”, nasi twafahamu kwamba “Mungu ni Roho” Yn 4:24; hivyo ni dhahiri kwamba huyo aliyeumbwa kwa mfano na sura yake, atakuwa ni roho pia. Kwahiyo tunaposema “mtu”, ninaamini huyu ndiye halisi, ambaye ni roho.

  “Mwili” ni mavumbi; Mwa 2:5 “… wala hapana mtu wa kuilima ardhi…”
  Roho haiwezi kulima, hivyo, “7BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi…” Sasa ni LAZIMA tuelewe kwamba hapa Mungu haumbi mtu wa pili, bali amechukua kutoka alichokiumba tayari, ule udongo, ndio ” akamfanya mtu…” pia huyu anayekuwa formed hapa si wa ” mfano na sura” ya Mungu!
  Baada ya kuufinyanga huo udongo, ” akampulizia puani pumzi ya uhai…”Uhai wote watoka kwa Mungu, hata uhai wa hilo dongo pia! “Pumzi ya mwanadamu (the spirit of man) ni taa ya BWANA; Hupeleleza yote yaliyomo ndani yake.” (‭Mit ‭20‬:‭27‬)‬‬‬‬‬‬; hii ndio roho ya mwanadamu, Zek 12:1 “… Haya ndiyo asemayo BWANA, azitandaye mbingu, auwekaye msingi wa dunia, aiumbaye roho ya mwanadamu ndani yake [‘aiumbaye…’ – formeth the spirit of man…].

  Mpaka umbali huu, hili ‘dongo’ kwa kutiwa uhai, limekuwa activated na hivyo sasa linaweza kufikiwa na dunia kimwili kupitia hisi tano- ‘Kuona, Kusikia, Kuonja, Kugusa na Kunusa’; na kiroho kupitia hisi tano nyingine za kiroho ndizo zile: ‘Kuwaza, Dhamiri, Kupenda, Mantiki na Kumbukumbu.’ Basi ktk stage hii hili ‘dongo’ liko sawa na mnyama, lina intelligence, kumbukumbu nk kama tu Biblia inavyolifunua jambo hili kupitia Nyoka, Mwa 3:1 “Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu.” Nyoka alikuwa ‘subtle’! Subtle = crafty; cunning; making use of clever and indirect methods to achieve something. Alikuwa ana uwezo mpaka wa kuongea, kama unavyomuona akiongea na Hawa akiudhihirisha huo werevu alionao! Sasa ukumbuke kwamba huyu nyoka wa leo si yule aliyekuwako kule Edeni, huyu wa leo ni badiliko lililomtokea baada ya kulaaniwa, akiwa ameshushwa kutoka ktk order ya “beast” mpaka kuwa “reptile” yule mwenye kutambaa!

  Tukiendelea mbele na lile ‘dongo’ letu, likiisha kuwa activated, iwapo Mungu angeishia hapo, basi Maandiko yangejivuruga kwani hicho kingekuwa ni kiumbe kipya na hivyo kulitangua lile Neno la kwamba alimaliza uumbaji ktk siku ya sita! Lakini tunasoma, “… mtu akawa nafsi hai.” Basi tunapaswa tujiulize yule mtu wa mfano wa Mungu yu wapi? “Je! Si zaidi sana hao wakaao katika nyumba za udongo, ambazo misingi yao i katika mchanga, hao waliosetwa mbele ya nondo?” (‭Ayu ‭4‬:‭19‬) Huyu akaaye ktk nyumba ya udongo ni yule mtu wa Mwa 1:27 huyu ndiye hiyo Nafsi hai akiisha kuingia humo ktk hilo dongo kuliendesha!!! Na Nafsini mwake, ndimo imo ‘imani’ ambayo kwayo yeye huwasiliana na Mungu tangu huko Edeni aliko wekwa baada ya kuumbwa!

  Shetani huweza kuufikia mwili na roho yake ili kuishawishi nafsi iondoke ktk imani, huko ndiko kuvutana kwa mwili na roho yake ile spirit of man vikiishawishi nafsi iondoke ktk imani. Katika Anguko Shetani alifanikiwa kupandikiza “Mashaka” katika Nafsi na hivyo humo kukawa na “Imani” na “Mashaka”, huu ndio “Utu” wa ndani, au yule ‘Inner man’ ambaye ukimlisha Neno la Mungu lililo Kamilifu, huyo hukua ktk kimo, ile Imani, hata kumfanania Kristo na kulitiisha dongo na roho yake; na iwapo utamlisha mambo ya dini, hicho ndio chakula kipenzi cha “Mashaka”, ndipo huyo hukua ktk kimo akijiongeza ktk Kutokuamini, na mwishowe huchukua Chapa ya Mnyama, Imani ikiisha kufa na hivyo huyo mtu kubakia kuwa sawa na mnyama hapo Utu wake wa ndani unapofikia kufanana na ule wa Nje!

  Gbu all!

 12. Milinga,

  Majibu ya maswali uliyoyauliza, naona wapendwa wamejitahidi sana! Unajua inapofika ktk suala la “moyo”, ni gumu na la msingi sana haswa unapoitafakari Nafsi. Kila ninaposoma kuhusu awazacho mtu, sijaona ikizungumziwa akili au kichwa, mara zote inakuwa “moyo”! Labda kadiri tunavyolitazama hili twaweza kufika mahali tukajua na jinsi ya “kuulinda”!

  Ktk kuendelea, ngoja nijaribu kuyajibu yale maswali kama hivi:
  1. Moyo ni pump inayoisukuma damu ili kuizungusha mwilini, na pia humo mna ki compartment kidogo sana ambacho hakina mishipa ya damu.

  2. Moyo uko kifuani, katikati.

  3. Neno la Mungu tunaweza kuliweka Moyoni, iwapo nafsi zetu zina shauku au kiu ya Mungu, na likiwekwa humo huijenga imani kamilifu; na vilevile tunaweza kuliweka Akilini likatusaidia kuwa watu wema wa dini, likitujengea ile intellectual faith!

  4. Jambo la Mungu Baba, Mungu Mwana na RMt kukaa ndani yetu, hili halipo, kwa sababu hayo ni mafundisho ya kipagani, Baba, Mwana na RM ni dispensations za Mungu mmoja, na dispensation inayohusu Mungu kukaa ndani yetu, ni baada ya sisi kuwa tumekombolewa kwa Damu ya Kristo, hapo tunapobatizwa kwa Jina la Bwana Yesu Kristo ili kupata Ondoleo la dhambi zetu, nasi kuanzia hapo kuwa ni mali yake, ndiposa yeye huja kukaa ndani yetu ktk ile nafsi yetu na kutuongoza kama ambavyo yule Adam alivyowekwa ndani ya lile dongo kuliongoza, ndivyo ambavyo humtokea huyo anayemilikiwa na Kristo.

  5. Moyo wenye kukidhi hayo niliyoyaelezea hapo juu kuuhusu, ni wa aina moja tu; inaposemwa moyo wa nyama au wa mawe, hizo ni semi ktk maana ya wepesi au ugumu wa kupitisha mawasiliano ili kuifikia nafsi iliyomo humo ndani. Ni kama wale wadudu ambao hujitengenezea gamba gumu kisha wao kutulia humo ndani wakikata mawasiliano na dunia, cocooning! Naye Ibilisi ni hodari wa ujenzi huo hata kuizuia nafsi kupokea Neno la Mungu!

  6. Roho inaweza kuwa ya mtu au mnyama au ya Mungu au Kristo, inategemea unaongelea nini. Iwapo unamuongelea mtu, basi hiyo ndio ile “spirit of man.” Hii inatambulika au kufikiwa kwa hisi tano: Kuwaza, Dhamiri, Kupenda, Mantiki na Kumbukumbu.

  7. Roho iko ndani ya mwili.

  8. Nafsi ndio mtu mwenyewe, yule wa Mwa 1:27!

  9. Nafsi inakaa ktk ile compartment ndogo isiyo na damu ktk moyo. Compartment hii iko ktk moyo wa binadamu pekee, wanyama hawanayo, na pia HAWANA nafsi!

  10. Mwili ndio huo unaokufanya uonekane na kutambulika kama Milinga na jamii yote ya viumbe. Huo unaouvisha nguo ndio unaitwa mwili, nao unatambulika kwa zile hisi tano: kuona, kunusa, kuonja, kugusa na kusikia. Mwili huu hukaa juu ya sayari ya dunia, ktk nchi kavu.

  11. Mwanadamu ni mwili, roho na nafsi – yaani yule mtu wa Mwa 1:27 ndani ya huyo wa Mwa 2:7; na baada ya hapo ndio huo uzao wa dunia nzima unaotambulika kwa jina la Adamu akiwa ndiye baba yetu, ingawa yeye si “baba wa wote”!

  12. Akili (sio ubongo!) ni uwezo wa kufikiri, ambayo ni hisi ya roho, hivyo zinakaa rohoni.

  13. Dhamira ndio inayoongoza utendaji wa akili unaojidhihirisha ktk matendo ya mwili ktk zile hisi tano, hivyo dhamira ni moja ya hisi za roho.

  Gbu!

 13. Wapendwa,

  Niko nafuatilia michango yenu wote. Pamoja na changamoto za mada hii, naendelea kubarikiwa sana. Nitarejea tena kutoa dukuduku zangu ambazo bado hazijanitoka kichawani.

  Naomba msichoke kuendelea na mjadala huu mkali maana mimi bado nina maswali kibao

 14. Petrus Georgiy,

  Karibu Rafiki; Uenda vyanzo ulivyosoma vipo sahihi lakini jinsi ulivyoelezea yaani mimi ndo umenichanganya kweli. Sijui wenzangu ili nimejaribu kusoma mchango wako mara kadhaa ili mmmh! ndo kwanza inaifanya mada kuwa ngumu zaidi ya mwanzo.

  Ok, noja nione mrejesho wa wenzangu uenda watakuelewa ili na mimi nipate hapo. Karibu usichoke.

  *********Wakafunguliwa Akili….Wakaelewa na Maandiko*************

 15. Ziragora;

  Hebu angalia picha iliyosadifiwa hapo juu kabisa mwa post hii halafu Kabla ya kuendelea hebu tufanye utafiti kwa kuangalia tofauti ya maneno yafuatayo:

  1.Roho: Spirit Vs Soul
  2.Akili : Brain Vs Mind
  3.Moyo: Physical Heart vs Spiritual Heart
  4.N.K

  Kisha tuje vizuri. Mimi nafanya utafiti. Take a Pause.Relax.

  Nakutakia Ibada Njema ya siku ya Kwanza/Jua.

  *********Wakafunguliwa Akili….Wakaelewa na Maandiko*************

 16. Bwana yesu asifiwe kweli swali hilo limetatiza watu wengi sana lakini namshukuru mungu aliachia neema ya kulifuatilia tangia nikiwa sekondari lakini kupitia maandishi mbalimbali niliyosoma haya ndio majibu na vilevile ieleweke biblia kabla ya kufika ktk kiswahili ilipitia kiebrania>kiyunani>kiiingereza>kiswahili…..sasa hapo utaona neno ruach>pneuma>spirit>nafsi…..na nephesh>psuche(psych)>soul>roho

  Nafsi katika biblia ndio inaelezewa kama utu wa ndani (waefeso 3:14). na nafsi si roho kama wengine wanavyofikiri galatia 5:16-26 ” 16 Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. 17 Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.
  ktk mstari huu unaona mtume paulo anaelezea kutofuata mwili lakini twende kwa roho. moja kwa moja utabaini kinachoambiwa hapo si mwili wala roho hivyo ni nafsi na hapo utagundua nafsi ndio ina maamuzi ya nini cha kufuata UTASHI (ni uwezo wa mtu kufanya maamuzi kwa hiari). vile vile unapozungumzia moyo moja kwa moja moyo unahusisha HISIA (emotion) kwa hiyo moyo kama kiungo tu tunasema kinausika ktk interpreate hisia na muda mwingine mawazo sababu si moyo huu wanyama unabeba hisia na mawazo ila utu wa ndani ambao ni nafsi….(kama moyo ungekua unachukua mawazo ya mtu kumbuka kwamba siku hizi kuna matibabu ya kubadilisha moyo kwa njia ya operation kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine hivyo basi tungetarajia alie badilishiwa moyo na mfumo wa hisia mawazo kubadilika kabisa?) kwa hiyo moyo wa nyama ni kama kifaa kinachosaidia interpreate hisia kutoka katika nafsi ya mtu.kuhusu AKILI vilevile ni sehemu ya nafsi ya mwanadamu na hiyo inafasiliwa ubongo ivyo kwa ujumla nasfi ya mwanadamu ina sehemu kuu tatu (1) utashi (2) hisia (3) akili.
  (Ndio maana nafsi ya mtu inapokamatwa na nguvu za giza ina maana mtu huyo hana akili zake hisia zake wala utashi kama ni baba huruma juu ya watoto wake wa kuzaa na mama inakwisha sababu ya nyumba ndogo iliofanya ushirikina kumkamata baba huyo)

  Roho nayo inamegawanyika katika sehemu kuu tatu (1)dhamiri(2)utambuzi (3)ushirika
  Unapozungumzia dhamiri hii ni sehemu ambayo mungu alipomuumba mwanadamu aliiweka katika roho kusudi kwa asili awezejua hili ni baya na hili ni jema na ndio inayomshitaki mwanadamu pale anapofanya baya aijalishi kama alikutana na injili ktk maisha yake
  utambuzi (intuition) hii ni sehemu inahusika na mwanadamu kutambua mazingira pasipo akili za nafsi wala za kimazingira.
  Ushirika hii vilevile ni sehemu ya roho ambapo ndipo inaposaidia ushirika na mungu katika ulimwengu wa roho
  (Ndio maana mtu aliekufa kiroho hana tena ushirika na mungu wala tena dhamiri ya kumshitaki hili ni baya na hili ni zuri

  Kwa maelezo zaidi tafuta vitabu hivi illustrated encyclopedia na Maadili kwa kizazi kipya cha askofu gamanywa…weka ufahamu wako huru John F paul na introducing psychology by nigel benson

 17. Ndugu yangu Mjema,

  Na wewe Mungu akubariki sana.
  Usishangae ukiona penginne kuna wengine wanaojadili kwa style nyingine, kwa upole zaidi. Hiyo nayo inamfanya Mungu asieleweke kirahisi. Hata namna alivyotutolea vipaji siyo sawasawa.

  Kuna wanafunzi wanaofanya mtihani wa kiserkali, mara wanapomaliza mtihani wanaanza piga filimbi eti wamefaulu wakijitolea wao wenyewe % 80. Lakini wakati wa kutangaza matukio ya mtihani, vyeti hawana. Ndio maana hakuna mpumbavu kama mtu anaejiita mwenyewe bingwa.

  Sitakuruhusu kugeuza mada ili niingie katika ukubwa wa Mungu. Biblia inasema kama matendo ya Mungu yanapita fahamu zote za binadamu. Sasa ukisema matendo yake ya uumbaji, kuelewa aliumbaje na ikoje ni rahisi sana utakuwa umehakikisha matendo ya Mungu yako chini ya kiwango cha fahamu zako.
  Hivi Mjema, hata kwa mfano uliyouleta wa mwanafunzi, yule yule mwanafunzi akiandika 1+1 =10 utasemaje?

  Sasa nataka niende polepole kwani nakuona unashikilia Neno la Mungu kama filosofia unayotengeneza mwenyewe katika akili zako ukidhani umeeleweka. Ukisema kitu, uwe mtulivu, uache walioambiwa ndiwo wahakikishe wameelewa. Kwani filosofia ya kichwani mwako utaiona tu rahisi na hiyo ni kawaida kabisa.

  -Kwa ujumla unasema mtu ana at once miili miwili, roho mbili, nafsi mbili, mioyo miwili. Aina moja ya kimwili na aina nyingine ya kiroho. Kwa filosofia hii mtu anaweza kuwa at once na roho ya kimwili pia roho ya kiroho. Unaposoma hili shairi, “Wagalatia 5:17 Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.”, je ni mwili upi unaoshindana na roho ipi?
  Je mtu anapookoka anabaki na hizo aina mbili za mwili, roho, nafsi, moyo?
  -Tutafakari vizuri zaidi. Mtu alipotiwa pumzi ya uhai, Mungu alifanya tendo la kumpulizia pumzi hiyo katika pua. na wewe unahakikisha kama ni hiyo hiyo pumzi wanyama wanayo bila tofauti. Kwa nini Mungu hakufanya sawasawa kwa wanyama? Notice: Mhubiri hakuhakikisha kama katika hiyo lugha yake hizo roho ni sawasawa. Alisema kwa maneno ya kifo, mtu na mnyama ni sawasawa.
  -Umesema pia kama mtu kuwa mfano wa Mungu ni utashi wa Mungu unaojumuika, unaweza tuambia kawa ule utashi wa Mungu unakaa wapi, ndani ao nje ya mtu ili tufahamu zaidi utofauti ulio kati ya mtu na mnyama?
  -Ninachofahamu, na baadhi ya wachangiaji wanachokifahamu, mtu ana roho ya kizalikio, hiyo roho inaweza kuwa imevuviwa uzima wa milele au inapata mauti ya milele. Mtu hana Roho ingine tofauti na ile moja. Sasa anapookoka ile roho inavuviwa na RM ndipo inasemwa kama mwili wa mtu umekuwa hekalu la Mungu/RM. Lakini ni ile ile roho wala siyo kwamba mtu alikuwa tayari na roho mbili. Mwili nao ni mmoja, na nafsi ni moja, huu wa mauti. Kwani imeandikwa kilichozaliwa kwa mwili ni mwili. Na kuzaliwa kwa roho ni kugeuzwa kikwelikweli. Hii ina maana, roho inayoshindana na mwili wa mauti inapewa nguvu za ushindi zinazoshurtisha mwili kutii roho.
  -Moyo ni tofauti, katika tu filosofia ya mwanadamu au tuseme lugha yake, licha ya kujua kama moyo ni sehemu ya mwili, hii sehemu, kulingana na jinsi ndio injini ya uhai wa mtu, imepewa mamlaka au characteristcs ya vile inavyotunza kwa kuvisukumia damu. Ndio maana ndimo mara na mara kwa lugha ya filosofia ndiyo ina hisia, akili, sensation, … licha ya kuwa ni sehemu zingine za mwili zinazofanya hiyo kazi.
  Hivi kuna moyo wa nyama na huo ndiwo moyo wa kawaida na mwingine wa fillosofia. Ni huwo wa filosofia unaoweza geuzwa kutokana na jinsi RM amekaa ndani ya mwili akitengeneza kila sehemu ya mwili itii roho iliyovuviwa na RM.
  -Kwa kufupisha, basi ukiona nuru iko, uniige.

  Mungu akubariki.

 18. 1. JIBU JUU YA BINADAMU

  “MIKONO YAKO IMENIUMBA NA KUNIFINYANGA; NAWE UTAGEUKA NA KUNIANGAMIZA?
  KUMBUKA, NAKUSIHI ULIVYONIFINYANGA KAMA VILE UDONGO; NAWE, JE! UTANIRUDISHA UVUMBINI TENA? JE! WEWE HUKUNIMIMINA KAMA MAZIWA, NA KUNIGANDISHA MFANO WA JININI? UMENIVIKA NGOZI NA NYAMA NA KUNIUNGA PAMOJA KWA MIFUPA NA MISHIPA. UMENIJAZI UHAI NA UPENDELEO, NA MAANGALIZI YAKO YAMEILINDA ROHO YANGU.”
  AYUBU 10:8-12

  “AKAMPULIZIA PUANI PUMZI YA UHAI; MTU AKAWA NAFSI HAI.”
  MWANZO 2:7

  2. ROHO

  ROHO HUKATA AU KUZIMA,

  ROHO NI NDIYO PUMZI, NI KAMA TAA INAYOWAKA

  “PUMZI YA MWANADAMU NI TAA YA BWANA; HUPELELEZA YOTE YALIYOMO NDANI YAKE”
  MITHALI 20:27

  “ROHO YANGU IMEZIMIKA, SIKU ZANGU ZIMEKOMA, KABURI TAYARI KUNIPOKEA”
  AYUBU 17:1

  “KWAKE HUYO ATAKAYE KUZIMA ROHO INAPASA ATENDEWE MEMA NA RAFIKI.”
  AYUBU 6:14

  JE! NI MARA NGAPI TAA YAO WAOVU HUZIMISHWA?
  AYUBU 21:17

 19. Ziragora;

  Ubarikiwe Mtu wa Mungu.Mtumishi sijakukataza kuiita hii mada ni ngumu au tata. uo ni uzoefu wako na wala sitakukataza kamwe. kwani hata darasani unaweza kusema 1+1=2 ila sio wanafunzi wote wataliona hilo hesabu kuwa ni rahisi la hata kidogo.

  Nafuruhai kujibu kwa kifupi ni ishara kuwa Nuru inakuzukia.

  Hoja yako bado ni ili ya Mhubiri 3:19- kama ifuatavyo:

  1.Imeandikwa wapi kama mnyama amepulizwa pumzi ya uhai katika pua lake?

  Jibu; Mhubiri 3:19-inasema kama vile pumzi imtokavyo mnaya ndiyo na mwanadamu. Na Biblia inasema kuwa Pumzi hiyo (ya Mwanadamu) Umrudia aliyeitoa.
  Ikiwa mtoa pumzi kwa wanadamu ni Mungu unadhani iyo ya wanyama inatoka kwa nani.

  Unachotakiwa kuelewa ni kwamba- Wanyama na viuombe wengine waliumbwa kwa neno la Mungu… Mungu akasema na iwe…. ikawa… Mungu akaumba…….n.k. Ni wazi kuwa iyo pumzi ya wanyama pia ilitoka kwa Mungu hata kama haijasema kuwa alipuliziwa puani kama ilivyokuwa kwa mwanadamu.

  Kwa mujibu wa Waebrania Neno la Mungu ni hai- au lina uhai- kama iliyo punzi yake ya uhai!!!!! Firiki nje ya Box ndipo utaelewa dhana hii.

  Kwa maana ya pumzi ya Uhai sisi na wanyama hatuzidiani- tupo droo rafiki. Utofauti wetu ni utashi unaoenda sambamba na kuncha Mungu.

  Mnyama akiwa na roho kama ya mutu, na Mungu akiwa Roho, je mnyama naye amefanywa kwa mfano wa Mungu?

  Jibu: La hasha. wanyama hawajaumbwa kwa sura na mfano wa Mungu.

  Roho/Pumzi ya Mungu ya Uhai sio kigezo sahihi cha kusema kuwa ndicho kitufanyacho kuwa na mfano wa Mungu. Viumbe wote hai wana Pumzi ya Uhai ya Mungu- kwa kuwa viliumbwa kwa Neno la Mungu ambalo ni hai.

  Sifa za mwanadamu kuwa na sura na mfano wa Mungu ni Utashi na Tabia tuliopemdelewa na Mungu ili Tuwe Watawala wa Viumbe Wengine- Kumbuka mara baada ya kuasi hatukupoteza pumzi ya uhai/roho bali tulipoteza Utashi na Tabia ya Mungu. Pumzi/Roho bado tunayo hadi pale inapomrudia yeye aliyeitoa yaani tunapo lala mauti.

  Je mnyama naye ana asili mbili, za Mwili na za Roho?

  Jibu: Hapana.-Wanyawa hawana asili mbili. Hawana Asili ya Roho. Kumbuka wanyama hawajaasi na wala kafara ya Yesu aiwahusu. wao wamefutata tu mkumbo wa matokeo ya dhambi za wanadamu. Yaani wameadapt anguko letu ili kutoaribu kabisa mfumo wa maisha-ecosystem aliyoikusudia Mungu kwetu kwani bila hiyo hakuna maisha na ndio maana mwanadamu aliumbwa wa mwisho-wanyama na mimea wanamuandalia mwanadamu mazingira ya kuishi.

  Barikiwa.

  **** Tufunguliwe Akili,Tuelewe na Maandiko*********

 20. Ndugu Mjema,

  Ahasante sana kwa jithihada zako za kulifahamu neno la Mungu. Nasi sote tunasonga mbele kwa neema ya Mungu.

  Lakini usilifanye swala hili kuwa rahisi sana. Kwani usidhani ni vigumu kwangu kusema “Ndugu Mjema umesikilika wala hakuna swali tena”. Elewa kwamba wanaopingana ndiwo hawallifikii lengo. Sasa hapa hatupingane, ni kuelimishana tu. Hence kwa kila hoja sherti uwe umejengwa na umejenga wengine. Siyo kwamba kuna anaejenga wengine tu pasipo yeye kujengwa.

  katika hoja yako unasema kama mnyama na mtu wana pumzi(roho) ile ile moja tu.
  Sasa kunajitokeza maswali:
  -Imeandikwa wapi kama mnyama amepulizwa pumzi ya uhai katika pua lake?
  -Mnyama akiwa na roho kama ya mutu, na Mungu akiwa Roho, je mnyama naye amefanywa kwa mfano wa Mungu.
  -Je mnyama naye ana asili mbili, za Mwili na za Roho?

  Kwa maswali ulioita homework, pengine umeweka chumvi nyingi. Hayo ni maswali ya kila leo. Ni kama unavyoweza uliza mtu “Yesu anaposema mkono wako wa kuume unapokukosesha ni heri uuongoe ina maana watu waanze jikata mikono?”

  Telemsha mambo, nimenena kwa kifupi ili nieleweke zaidi.

  Ubarikiwe .

 21. Ziragora,

  Ubarikiwe. Karibu tena. Ninachotaka kusema ni kuwa ili haya mambo yawe rahisi kueleweka turejee Yohana 3- “…kilichozaliwa kwa mwili ni mwili na kilichozaliwa kwa roho ni roho…” na akakazia “…maana akuna atakayeingia mbinguni bila kuzaliwa mara ya pili….yaani kwa roho. Mwanadamu anapande MBILIi!!

  Mada hii itaeleweka kama tukimtazama kwa makini mambo yafuatayo;

  1.Mwanadamu kama matokeo ya adamu kuasi- biblia inasema “… ADAMU wa kwanza..” Mwanzo sura ya 1, 2,3. wakoritho inasema mwanadamu wa Asili

  2.Mwanadamu kama matokeo ya Neema ya Yesu-Kuzaliwa Upya/Mara ya Pili-Biblia Inamwita ” ..ADAMU wa Pili..”Yesu katika maisha ya Mtu. 1Kor 15:45.

  3.Biblia Inasema mtu akiipokea neema ya “Adanu wa Pili..” anakuwa kiumbe kipya..na yakae yamepita.!

  4.Pia kama nilivyoeleza kwny michango ya nyuma biblia inasema…” Mungu ni Roho na Ili ibada zetu ziwe halisi lazima tumwabudu katika roho na kweli..”

  Hivyo basi kwa mtiririko huo hapo juu wa mambo manne naweza kusema;

  1.Mtu ambaye hajampokea Yesu ana upande mmoja tu- Mwanadamu wa Asili- UMWILI- Na huyu ana, MOYO,ROHO,NAFSI,MWILI ambavyo ni hivyo tunavyovijua na kila mtu, hata asiyemjua Mungu anavijua/soma/gusa n.k

  2.Mtu alyeipokea Neema ya Yesu KIKAMILIFU katika maisha yake- ana pande mbili.

  a)Uhasili wake katika UMWILI/ NYAMA na DAMU ambapo ana MOYO,ROHO,NAFSI= MWILI + PUMZI YA MUNGU. Hivi pote kwa mujibu wa Yohana 3-havitaurithi ufalme wa Mungu. Na Ndio maana wafia dini/wacha Mungu hawaoni shida kuvipoteza kwa ajili ya Yesu.

  b)Ubinadamu wa Pili/Utu upya ya Kiumbe kipya-Utu wa Roho ambao biblia inasema tuendende kwao-Galatia-Huu unatokana na kuzaliwa mara ya pili/Kwa Roho na Maji.sasa hapa napo biblia imetumia maneno yale yale: MOYO,ROHO,NAFSI n.k ili kujenga picha tu lakini haimaanishi kuwa ni vile tunavyovijua,gusa/osha n.k. Biblia inasema ni huyu pekee atakaye ingia mbinguni. Akimaanisha kuwa-Hatutaingia mbinguni na MOYO,ROHO,NAFSI na MWILI huu tuujuao bali ule wa dhahania/Kiroho ambapo tunao katika mahusiano yetu na Mungu.!!!!!!!

  Yaani kwa kifupi, Mwanadamu anayetokana na Neema ya Adamu wa Pili-Ambaye yupo kiroho ktk mahusiano na MUNGU naye ana MOYO, ROHO, NAFSI,AKILI na MWILI wa kiroho. ambavyo ndivyo vitampa stahiki ya kumwona na Kusihi na Mungu.

  Swali la Mhubiri3:19- lipo wazi. Roho ya mwanadamu na mnyama zote wanapokufa umrudia Mungu.!! na ndiyo maana mhubiri anasema hatuna cha kunzidi mnyama.

  Kumbuka Mungu alipoumba- Kabla ya Kumpulizia Adamu Pumzi ya Uhai na kuwa Nafsi hai alikuwaje?????

  Jibu ni Rahisi: Kinyume cha kuwa Nafsi Hai ni nini? Alikuwa Nafsi Mfu- kwa hiyo Pumzi ya Mungu au Roho inapomtoka Mtu anakuwa Nafsi Mfu.

  Kazi ya Nyumbani (Home Work) Ifanye kwa Uaminifu itakusaidia:

  1.Anaposema nitatoa moyo wa jiwe ulio ndani yetu na kutupa moyo wa nyama-anamaanisha nini-ni kweli kuwa moyo tulionao unaweza kuwa jiwe?

  2.Katika Zaburi 51-Daudi anapoomba “..Uifanye upya Roho iliyotulia ndani yangu…” alikuwa ana Roho yaani alikuwa amekufa?

  3.Biblia inaposema ktika Rom13- “….Iweni na akili mkeshe katika sala…” Je ni kweli kuwa hatuna akili hii unayosema inapimika na wanasanyansi tunapokosa maombi au?

  Karibu.

 22. Wapendwa,

  Mmefika mbali kabisa. Mungu awabariki kwa michango yenu.

  Kutofautiana ndani ya hoja zetu ndiko kunaonyesha ukubwa wa Mungu. Mungu wetu ni wa ajabu kabisa.

  Mimi nafikiri kilicho kigumu kusikia haswa ni roho na moyo. Vingine nafikiri vinaweza eleweka tu kwani vinauhusiano fulani fulani na mwili.

  Kwa upande mwingine kuna aina ya moyo inayoeleweka kirahisi, hiyo ya nyama.

  Mwili, nafsi,akili ni maneno inayoeleweka hata pasipo kuyashikilia kiroho.

  Mjema, unaposema kama hiyo pumzi Mungu aliyompulizia mtu ndani ya pua ndiyo roho, pia iliifanya moyo wa nyama kuwa injini inayotumika, na wakati mtu anapokata roho hiyo pumzi humrudilia Mungu, nakuta sielewi. Sielewi kwani moyo wa wanyama nao unatumika na wanyama nao huwa wanakufa(kukata roho), Sijue sasa ile pumzi wanayoikosa wanyama wakati ya kufa nayo humrudilia Mungu!

  Tusaidiane kuielewa hii mistari ya Biblia:

  “Mhubiri 3:19 Kwa maana linalowatukia wanadamu linawatukia wanyama; jambo moja lawatukia; anavyokufa huyu ndivyo anavyokufa huyu; naam, wote wanayo pumzi moja; wala mwanadamu hana kitu cha kumpita mnyama; kwa maana yote ni ubatili.20 Wote huendea mahali pamoja; wote hutoka katika mavumbi; na hata mavumbini hurudi tena.
  21 Ni nani ajuaye kama roho ya binadamu huenda juu, na kama roho ya mnyama huenda chini?
  22 Hivyo nikaona ya kwamba hakuna jema kupita mwanadamu kuzifurahia kazi zake; kwa sababu hili ni fungu lake; kwa maana ni nani atakayemrudisha tena ili ayaone yatakayomfuata baadaye.”

  Mimi ninachoona ni kwamba, roho yenyewe ndiyo haswa inatofautisha wanyama na binadamu kwani ndipo Mhubiri anajiswali tu kama zote mbili huenda mahala moja au la. Kwa sehemu, akili tu kwa tofauti iliyo kati ya wanyama na binadamu, lakini hata sayansa au namna sisi wenyewe tunavyoona, akili za wanyama nazo zipo, lakini kwa kiwango tofauti tofauti na binadamu. Binadamu nawo hawana akili sawa sawa.

  Alimradi, lugha ya Biblia ifikapo kwa mwanadamu inaongea kama Biblia na wala si kama binadamu. ndio maana tunapata confusion kati ya Roho, nafsi, na moyo. Lakini Biblia ifikapo mahala inapojifunza juu ya utofauti kati ya mnyama na binadamu inaiweka ndani ya lugha nyepesi, hiyo tunayoiona katika msitari michache ya Biblia niliyoweka pale.

  -Mwili haina maelezo mengine inajulikana ni sawasawa tu hata kwa wanyama.
  -Nafsi ni uhai unaodhihirika katika damu, ni sawa sawa kwa wanyama na kwa watu. Nafsi ya mtu haiwezi ishi milele tangu mwanadamu aliasi. Inakufa tu!!!!
  -Akili zinapimwa hata kisayanza, mtu anawezapoteza akili zake na bado anaitwa mtu. Lakini akipoteza uhai (nafsi) anaitwa maiti.
  -Moyo wa nyama ni sehemu ya mwili nawo unakufa pamoja na mwili wake. Wa kiroho ndiyo roho mwenyewe, tusipime vitofautisha kiroho, haiwezikani.
  -Pumzi inayoifanya moyo kutumika siyo roho kwa lugha ya kiroho kwani nadhani wanyama hawana roho kwa lugha ya kiroho.
  -Roho ni hiyo picha ya Mungu iliyo ndani ya mwanadamu, wala hakuna mtu anayeweza ipiga picha tena ili afahamu ilipo ndani ya mtu. Roho kwa lugha ya kimwili ndio moyo, lakini kwa lugha ya Biblia ni hiyo picha ya Mungu iliyobandikwa kiupekee kwa mtu, kwani kila mtu ana roho yake licha ya kuwa yote imetoka kwa Mungu. Kuwa na roho ndiko kunamfanya mtu awe ameumbwa kwa mfano wa Mungu. Ndipo Mhubiri anatafakari juu ya roho ya Mnyama na ya mtu. Kumbe kwa lugha nyingine mnyama naye ana roho, je sasa hiyo ni roho kama ya mtu au la?

  Tusaidiane jamani, mambo haya siyo mepesi.

  Mbarikiwe.

 23. Chemo;

  Mwanadamu sio Roho- Mungu ndiye Roho. Mwanadamu ni wa kimwili Ila Mausiano yake na Mungu-Ibada, ndiyo yanapaswa yawe ya Roho-Na hii inatokana na uzoefu wa kuzaliwa upya kama ifuatavyo;

  ” …kilicho zaliwa kwa mwili ni mwili na kilichozaliwa kwa roho ni roho…” hivyo basi kwa kuwa wote tumezaliwa kwa Mwili ili tuupate uzima wa milele lazima twende hatua ya pili- kuzaliwa kwa Roho-Mara ya Pili. Na hivyo kuzaliwa huko kunatufanya tuwe na uanadamu wa pili unaotokana na adamu wa pili-Yesu. Biblia ina sema tunakuwa viumbe/watu wapya-yaani katika mahusiano yetu na Mungu katika ulimwengu wa roho.

  Hivyo mwanadamu ana uzoefu wa pande mbili; 1.kimwili na 2.kiroho na hizi mbili zina moyo, roho. akili na nafsi tofauti. Rejea mchango wangu wa tarehe 14/11/2014 at 8:13 PM kwa ufafanuzi zaidi na tupeane changamoto.

 24. samileander,

  Jaribu kuichukulia biblia kwa Ujumla wake. Usitake kutuchekesha kuwa Roho ya Mungu inakaa kwenye pua.!!

  Niachafikiri mimi ni kuwa Ayubu alikuwa katika wakati mgumu na hivyo kwa kuwa alikuwa akiiona mauti mbele yake aliiona kama Roho yake kama inataka kutoka. Na ndio maana leo tulio wengi ukutaka kujua kama mtu anekata roho unakimbilia puani. Haina maana kuwa ndipo hasa roho inapokaa.

  Rejea mchango wangu wa tarehe 14/11/2014 at 8:13 PM tipeane changamoto.

 25. Sungura;

  jaribu kufikiri zaidi. binafsi naona upo utufauti kati ya Moyo,Akili na Nafsi. Jaribu kupitia mchango wangu hapo juu tarehe 14/11/2014 at 8:13 PM kisha tupeane changamoto.

 26. Wandugu,

  Neno la Mungu lazima tulishike kwa akili zetu au miyo yetu au nafsi zetu.

  Kwamba mtu anaweza akalikariri neno kwa akili bila maisha yake kubadilika, hiyo ni kweli.
  Lakini ni kwa sababu akili ikilishika neno lazima kuna maamuzi yafanyike katika dhamira / utashi ndipo matokeo ktk maisha ya huyo mtu yaonekane.

  Maamuzi katika dhamira/ utashi wa huyo mtu yakiwa ni kukubali kile neno linasema basi maisha yake yatamwelekea Mungu, yasipokubali basi huyo mtu ataendelea kuishi kinyume na neno.

  Biblia inaposema moyoni mwangu nimeliweka neno lako…., maana yake ni akilini mwangu au nafsini mwangu, ambamo ndani yake kuna nia.

 27. JIBU LA SWALI NAMBA SABA NI HILI:
  “KWA KUWA UHAI WANGU UKALI MZIMA NDANI YANGU, NA ROHO YA MUNGU I KATIKA PUA YANGU” AYUBU 27:3

 28. Milinga,

  Maswali mengine ni mepesi sana ndugu. Kwa mfano swali kwamba mwili ni nini nauko wapi!

  Anyway, moyo, akili, nafsi almost ni kitu kimoja.
  Neno la Mungu linatakiwa kukaa alilini mwetu, na ndoo sehemu ambapo kuna utashi.

  Mwanadamu ni mwili nafsi na roho. Nafsi na roho vyote vinakaa mwilini. Bila mwili, nafsi na roho hiviwezi kuwepo duniani.

  Kitu ambacho utaicha akili ibebe ndicho kitakachokwenda kuathiri roho yako.
  Ndio maana shetani huwa anashambulia akili ya mtu maana anajua akiiweza hiyo ndo ameweza kuiathiri roho ya huyo mtu.

  Akili/moyo/ nafsi ikiwa na Mungu basi roho lazima ifuate huo utashi wa nafsi.

  Kwa hiyo roho ni uhai ulio kwenye nafsi unaomfanya mtu awe nafsi hai!

  Tunachoweza kusaidiwa na mjadala huu ni kujua hasa adui hushughulika na nini anapotushambulia.
  Na hicho kinachoshambuliwa na adui ndo tunatakiwa kukilinda zaidi.

  Ngoja niweke koma!

 29. Moyo, ni kiungo cha mwili, kinakaa kifuani. Kazi ya moyo ni kuratibu mtiririko wa damu katika mwili wote. Pia moyo unatajwa mara nyingi katika Biblia, siyo kama kiungo tena, bali kama mahali pasiposhikika ambapo nafsi inafanya makao. Neno la Mungu linaingia ndani ya mtu kwa kusikia, kupitia akilini, na hatimaye, kwa kutafakari lile neno, yaani kujenga taswira ya hili neno katika maisha ya huyo anayelisikia, neno huingia ndani ya moyo, na kukaa huko, Kwa hakika, neno la Mungu limeandikwa kwaajili ya moyo wa mtu. Utakubaliana na mimi kwamba, mtu anaweza kukariri Biblia lakini isimbadilishe au isilete matokeo yanayotarajiwa, yaliyoahidiwa katika Biblia. Lakini, moyo wa mtu ukiguswa na neno lile, unabadilishwa kabisa, na mabadiliko yale yanakuwa ndiyo maisha ya huyo msikiaji. Nimeongea kwa kifupi sana. Nitachangia zaidi nikipata fursa.

 30. Mtu ni roho, anaishi kwenye mwili, ana nafsi. Mwili ni huu unaouona kwa macho, unashikika kwa jinsi ya mwili. Mwili ulifanywa na Mungu kwa mavumbi ya nchi, kwaajili ya mtu aliyeumbwa na Mungu kuisha na kuwasiliana na mazingira yenye asili ya kushikika (Mwanzo 2:7). Katika mwili kuna viungo, na viungo vya mwili vinamwezesha mwenye mwili kuweza kuyakabili mazingira ya mwilini. Kisha nafsi, ina akili, dhamiri, maamuzi, utashi, hisia na mhemuko. Yaani vitu visivyoshikika. Katika huo mstari wa Mwanzo 2:7, nafsi inaingia kwenye mwili kupitia pumzi ya Mungu. Na hatimaye roho tunaweza kuifahamu kwa vile neno linavyosema. Yaani, Mwanzo 1:26-27, Mungu anapomuumba mtu. Mungu anajiongeza kwa neno lile na kuumba huyu mtu. Huyu mtu aliyeumbwa hapa ndiye roho, yaani kwamba yupo tayari (being). Kwahiyo, MTU ni roho, napata ugumu kuelezea zaidi juu ya roho, maana sasa akili ya mwilini, yenye kuzoea kutambua mazingira ya mwilini, inakomea hapo, haiweze kupambanua mambo yaliyo tofauti na asili yake, lakini. KUWA (being) kwake yule mtu ndio udhihirisho wa roho. Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu ni mmoja (1Yohana 5:7). Katika hali ya kutafakari neno hili, ni muhimu kuvuka fikra za kimwili, zinazoishia kwenye kushika, kunusa, kuhisi, kuonja na kusikia na kuona, na kuingia kwenye elimu ya roho, yaani neno la Mungu. Maswali mengine yoooote, yanabakia kwenye mwili. Pia kuthibitisha zaidi juu ya roho, nafsi na mwili 1Thesalonike 5:23.

  Na haya yote tunayoyatafakari hayatakuwa na mashiko isipokuwa kwa kufunuliwa na Roho Mtakatifu, yaani haya maandiko tuliyoyasoma ni lazima tufunuliwe na Roho Mtakatifu.

  Amina

 31. Mr Milinga;

  1.Kabla sijaanza kujibu maswali uliyouliza napenda kukukumbusha kuwa usichanganye moyo,roho,akili za kimwili-zinazoshikika naza kiroho-kisizoshikika (zilizokatika ulimwengu wa Dahania/Roho)

  Umaweza kuwa bado hujanielewa, Fikiri hivi: Yesu alimwambia Nikodemu ” kilichozaliwa kwa Mwili ni Mwili na Kilichozaliwa kwa Roho ni Roho” na Hakuna hatakayeingia mbinguni bila kuzaliwa mara ya pili-kiroho. Yohana 3:6 Tena akamwambia kuzaliwa huko uwezikukuona bali utaonaviashiria ktk matendo kuwa uyu mtu amezaliwa mara ya pili.kama vile upepo uzivyouona ila unajuakuwa kuna upepo kwa kuona viashiria vyake.

  Maana ya mfano huo ni kwamba, Roho,Moyo,akili ni vitu vya dhahania-visivyoshikika,gusika,nusika. Huwezi kuvihakikisha uwepo wake kisayansi-maabara kwamba leo ukipasuliwa basi tutaviona.

  2.Pia Yesu aliwaambia wanafunzi wake kuwa uzoefu huo wa kuzaliwa upya Watampenda Mungu- kwa moyo wao wote, Roho yote, Akili yote …. na jirani kama Nafsi yake….. Marko 12:30

  Bila shaka hivi ni viungo vya dhahania ambavyo hapo hasa ndipo uhusiano, mawasiliano yetu na Mungu ndipo yalipo hasa.

  3.Pia Yesu alisema, ..Mungu ni Roho na waabudua halisi …umwabudu katika Roho… sio kimwili. Yaani kwa maneno mengine MUNGU wetu ni wa DHAHANIA-ashikiki/anusiki na Uhusiano wetu nae niwa dhahania.??!!!!!! Yohana4:24

  Mungu upokea Ibada zetu kupitia hivi viungo vyetu vya dhahania ambapo hasa ndipo uhusiano na mawasiliano yetu ufanyika. Mungu awezi kupokea Ibada kwa viungo vya kimwili kwa mwili huu ni wakufatu na hauna/hauwezi kumpatia Mungu ibada anayotaka tumpe.

  4.Pia Paulo anasema; Mtu akiwa ndani ya Yesu amekuwa KIUMBE KIPYA..yakala…tazama ni mapya. 2Kor5:17

  Hivyo basi,kwa ufupi haya zote hizi zinaweza kufupishwa hivi: kwa kuwa anasema imetupasa kuzaliwa mara ya pili, na kuzaliwa huko kunatufanya kuwa viumbe wapya. Hii ni katika dhana ya dhahania-kiroho na sio kimwili huu wa kufa.

  Hivyo basi, Dhana ya Moyo,Roho,Akili inayotumika hapa imaweza kubainishwa kwa kupiga picha viuongo hivi katika hali ya Kimwili ILI KUELEWA DHANA IYO YA KIDHANANIA-KIROHO kama ifuatavyo;

  1.Moyo-ni kiungo muhimu katika mwili kinachosukuma damu mwili mzima-biblia inasema damu ndio uhai wa mwili. Hivyo moyo ndio Injini ya mwili ambapo pasipo huo hakuna uhai.Mwanzo 9:3-4

  2.Roho-Pumzi ya Mungu ya Uhai-Kitabu cha mwanzo kinasema-Mungu akampulizia huyo mtu pumzi ya Uhai……… leo hii punzi hiyo inapotutuka tunasema mtu huyo amekata Roho-ambayo ndiyo hiyo pumzi inayo mrudia MUNGU. Mwanzo 2:7

  3.Akili-kiuongo kinachotumika kufanya maamuzi yote yanaoongoza maisha ya mwanadamu.

  Baada ya ufafanuzi huu unaotujengea msingi napenda nijibu maswali yako kama Ifuatavyo;

  1. Moyo ni nini

  Jibu-Kiungo cha dhahania ambapo uhai/uhusiano wetu na Mungu aliye Roho ufanyika na mwanadamu aliyezaliwa mara ya pili na kuwa MTU/KIUMBE kipya.

  2. Moyo unakaa wapi mwilini?

  Jibu: Moyo haukai mwilini. Upo ndani ya mtu/kiumbe kipya aayetokana na kuzaliwa upya

  3. Je, Neno la Mungu huwa tanaliweka Moyoni au Akilini?

  Jibu: Zaburi 119:11-Neno la Mungu uwekwa Moyoni- na Kama ilvyo damu Vs moyo wa kawaida- Neno ili linapowekwa katika moyo huo wa dhanania- usambazwa mwili mzima-(wa dhahania) na hivyo kupelekea uhai wa kiroho/uzima na ukuaji wa kiroho. Na hii ndio ile dhana kuwa usiposoma neno la Mungu unakufa kiroho.

  Tena hata Mr.Mabinza anayekupinga kuhusu umuhimu wa fundisho hili ana moto anao malizia nao kila siku kuwa “ufahamu ni cheme ya Uhai” yaani kama ilivyo “damu ni chembe ya Uhai” vivyo kulielewa Neno-Ufahamu ni chembe ya uhai=damu ukaa moyoni.

  Ukiweka Neno la Mungu akilini-tena hiyo ya kimwili-Ubongoni- itakuwa ni sawa na Yesu alivyosema-Itakuwa ni sawa na mbegu iliyoanguka njiani ambapo ndege/shetani uiondoa na kuila na haitazaa kamwe/Hakuna uhai. Mtu aliyezaliwa mara ya pili/kiumbe kipya uuweka ukweli Moyo.

  Ushahidi mwingine ni pale anaposema ………..linda moyo kuliko yote……hapo ndipo zitokazo chemchem za uzima. Mithali 4:23 Hebu jiulize- chem chem za uzima wa kawaida utoka wapi? jibu-damu ndio uzima na ni moyo utoa chem chem hizo.

  Mtu anayeweka neno la Mungu kwenye akili-kumbu kumbu za Ubongo- hakai akaliishi/akatenda Neno-anaiishia kulijua tu ila kamwe hanauzoefu/ushuhuda nalo ila anayeweka moyoni-uo wa dhanania daima litakuwa chem chem.

  4. Mungu Baba, Mungu Mwana, na Roho Mt wanakaa ndani yetu? Wanakaa Sehemu gani? Wanakaa Moyoni, Rohoni, Mwilini, Akilini, Nafsini au Kichwani?

  Jibu: NDIYO-Mungu Baba, Mungu Mwana, na Roho Mt wanakaa NDANI yetu. Katika uo mwili wa kiroho/dhahania unaofanyika mtu anapo kuwa kiumbe kipya.

  Mungu anakaa moyoni-kama nilivyosema awali hapa ndipo Ikulu- mausiano yote kati yetu na Mungu aliye Roho ufanyika. !!

  5. Je kuna aina ngapi za Moyo?

  Jibu:Mbili (2). Moyo wa kawaidia unaosukuma damu ya mwili huu wa kufa na moyo wa dhahania-wa kiumbe kipya kinachofanya mausiano na Mungu katika ulimwengu wa Roho.

  6. Roho ya ni nini?

  Uwepo wa Mungu/RM moyoni mwetu-zingatia nimesema Roho-ya kimwili ni pumzi ya Mungu ambayo tumezoea kusema “amekata Roho” ikimaanisha pumzi ya Mungu imetutoka.

  RM-ambaye Yesu amesema ndiyo msaidizi-Yeye ndiye Pumzi ya Mungu maishani. Yaani, pale mtu anapozaliwa mara ya pili Mungu utupatia Uhai huo yaani RM ambaye yeye ndiye utupa Nguvu ya kuwa mashaidi wake kama Roho ya kawaida utolewa na Mungu kama zawadi ambapo utufanya sisi kuwa nafsi hai.

  Mtunga zaburi anasema…… ” na Roho yako usiniondolee…” au “Uifanye upya Roho yako…” Zab 51:10-11

  Na kwa sababu huyo ndiye uwepo wa Mungu ndani Yetu, tunaweza tu kutembea ktk ulimwengu wake akiwepo yeye tu.

  7. Roho iko upande gani wa mwili?

  Jibu:Nimeshasema ni pumzi ya Mungu na kwa kuwa Mungu ni Roho- hata iyo roho tunayoijua ktk maana ya kawaida haishikiki.

  ZINGATIA: sambamba na jibu Na.6 hapo juu- Ni MUNGU pekee anayetoa zawadi ya RM kama vile ni Yeye pekee anayetoa PUMZI YA UHAI-wanadamu wamejaribu kuiunda Roho ila hadi leo zero zero. Tena wengine wanasema walijaribu kumfungia mtu kweye eneo lisilo na upenyo wa hali yeyote ili waione Roho lakini wapi hadi kesho hawawezi.

  Roho haisikiki/gusiki/kamatiki kwa hali yeyote ile kwani aliye na Neno la siri/PassWord katika hili ni Mungu pekee kama alivyo RM.

  8. Nafsi ni nini?

  Jibu: wakati wa uumbaji Mungu alisema; Mungu akampulizia hao mavumbi ya ardhi pumzi mtu akwawa nafsi hai;Mwanzo 2:7; yaani kwa kifupi

  A:Maaa ya Kawaidia-Kiwmili

  Nafsi =Mavumbi ya Ardhi aliyofinyanga Mungu (Mwili wa Nyama) + Pumzi ya Mungu(Roho)

  *******ukitenga nisha hakuna uhai

  B:Maana ya Kiroho-dhahania

  Nafsi= Mwili wa Kiroho/kiumbe kipya/Utu upya + Roho Mtakatifu

  9. Nafsi inakaa wapi mwilini?

  Jibu: Nafsi haikai mwilini- Ni matokeo ya Jumla ya Mwili na Pumzi ya Mungu. Nafsi ni kubwa zaidi ya Mwili, wanamahesabu wanasema. Mwili ni Subset ya Nafsi.!!!!

  10. Mwili ni nini na uko wapi?

  Jibu:
  Mwanzo 2:6-7
  1.Maana ya Kawaida: Ni muunganiko wa viungo mbali mbali ambao ni matokeo ya uwepo wa mzunguko wa damu na uhai wa ubongo.

  2.Kiroho/dhahania- Muunganiko wa viungo vya dhahania vinavyotokana na uwepo wa RM maishani mwa mtu aliyezaliwa upya/kiumbe kipya

  11. Mwanadamu ni nini?

  Jibu:

  Maana ya kawaida: Mtoto wa Adamu yaaani Neno lenyewe ni matokeo ya Maneno mawili, Mwana wa Adamu kwa kifupi tunasema-Mwanadamu- Kiumbe cha Mungu cheye utashi kuliko viumbe wengine kwenye sayari dunia.

  Maanda ya Kiroho: Biblia Inasema Adamu wa Pili ni Yesu, hivyo ni wale wote wanaoumbwa upya kwa uzoefu wa Neema ya Yesu maishani.

  12. Akili ni nini na ziko wapi mwilini?

  Jibu:

  1. Kawaida: Utashi unaotokana na mchakato wa Ubongo kufanya maamuzi/ufumbuzi wa jambo linalomkabili.

  2:Kiroho:tashi unaotokana na mchakato wa RM kufanya maamuzi/ufumbuzi wa jambo linalomkabili mtu aliyezaliwa upya.

  13. Dhamira ni nini na inakaa wapi mwilini

  Jibu: Nia ya moyo. Kusudio la Moyo.

  Ni uelewa wangu. Nakubali kukosolewa.

  Asanteni.Karibuni

  ” Yesu…akawafunulia akili zao wapate kuelewa na Maandiko…” Luka 24:45

 32. Ndugu Milinga,

  Pengine unataka kweli ufahamu kisayansa baada ya haya maneno kuzungmuziwa ndani ya mada nyingine.

  Nami ningelipenda viwekwe kwanza pembeni yaliyo kwa watu na kwa wanyama ili maswali yapunguzwe. Kwa mfano mwili, nafsi na moyo kama nyama. Ndipo tutaelewa zaidi kwamba Biblia ina lugha yake tofauti na lugha za binadamu.

  Mda ukituruhusu tutaendelea.

  God bless you!

 33. M.r Milinga

  Umeuliza swali zuri sana, naona Mabinza ameanza kuwa mvivu .Anasema kufahamu hayo mambo hakutufanyi kumshinda shetani sio kweli.Kufahamu haya yote ni Muhimu katika Ushindi wetu. Milinga nakuunga mkono sana tu. Na rafiki yetu Mabinza Hasisahau manene yafuatayo:

  1. Linda moyo kuliko yote uyalinadayo maana humo ndipo zitokapo chemchem za uzima. Kumbe uzima upo katika kulinda moyo. sasa mabinza jiulize utalindaje kitu usichokijua?

  2.Moyoni mwako nimeliweka neno lako nisije nikakutenda dhambi- kumbe kushinda dhambi siri ni kuweka neno lake huko.sasa mabinza usipojua ulipo huo moyo uoni kuwa umaweza kuliweka pasipo.Watu uweka maneno ya Mungu sehemu tofauti na hii ni mbinu ya shetani ili kama alivyosema Yesu ili Neno hilo lisizae matunda, moja-20, moja-50, moja-100.

  3.Vita vyetu sio vya damu na nyama……bali…. katika ulimwengu wa roho…… swali ni lile lile tusipojua ulipo moyo uoni kuwa tunaweza kupigana kimwili na kukosa shabaha

  Mabinza-acha uvivu, leta unachokijua kwani hapa hasa ndipo mwanzo wa ushindi ulipo.

  Mimi nakuja.

 34. Mr. Milinga,

  Lakini usinielewe vibaya rafiki yangu,

  Kwa maoni yangu sioni sababu ya mawsali hayo, na siamini kama kweli yanakuchanganya, maana Biblia si kitabu cha Sayansi! Sababu nyingine inayonifanya nione kama mawsali hayo yote hayana maana ni kwasababu, hata ikitokea ukajulishwa kwa ufasaha sana maana ya mambo hayo uliyoyauliza, kujua huko hakutakufanya wewe binafsi au jamaa yetu yeyote, KUTODANGANYWA na shetani, kuupata uzima wa milele au ufalme wa Mungu!

  Biblia inahimiza watu waijue kweli, na hiyo kweli ni Neno la Mungu. Kuijua kweli kunamfanya mtu kuwa huru kwelikweli, anakuwa katika mwanga wa kutodanganywa na shetani na akidanganywa hatadanganyika tena kabisa! Na hilo ndilo lengo kuu la Biblia, watu waifilie toba, yaani waponywe. Inatupasa kwenda ulimwenguni kote kusema Injili, kutekeleza lengo la Biblia ambalo ndilo Neno la Mungu tu na si vinginevyo. Maswali hayo mimi nayaona siyo Injili, kwanini kupoteza Muda?

  Au, Sasa kwa vipi kujua maana ya maulizo hayo kunaweza kukafanya mtu aokolewe na Bwana Yesu Kristo? Au umeyaleta ili tufurahi na kujipunguzi Stress pamoja? Labda, lakini mimi binafsi naona kama haina maana kujadili maswali hayo, au acha nisikie wengine wakisemacho ili nijue pengine nimeelewa isivyo, ili tujifunze pamoja ikibidi!

  “Ufahamu ni chembe ya Uhai!”

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s