Nabii Eliya au “Adam wa Pili” afariki dunia.

mchungajiKwa mujibu wa vyanzo mbali mbali vya habari ni kwamba Kiongozi wa kanisa la Pool of Siloam la jijini Dar es Salaam maarufu kama Nabii Munuo au Adam wa Pili amefariki dunia (amelala). Nabii Eliya kizazi cha nne alilala juzi mchana na taratibu za mazishi zinaendelea. SG inawapa pole washirika wote wa makanisa ya Siloamu na kila aliyeguswa na msiba huu.

Jina la Bwana libarikiwe.

Advertisements

55 thoughts on “Nabii Eliya au “Adam wa Pili” afariki dunia.

 1. asante sana kwa ufafanuzi huo !

  lakini kwanini watu wanakua wepesi sana kumuacha Mungu wa kweli na kukimbilia kushika mafundisho ambayo hata wao wanaweza kuyajaribu usahihi wake ?

  Uchawi, Ulozi , Kipaji au kazi ya Shetani ?

 2. Samson Mwasakafyuka.
  Baada ya kufariki kwa nabii huyu wa uongo, marehemu Nduminamfoo Munuo’ eliya adamu wa pili mungu wa majeshi’, aliyeachiwa Mikoba ya kuliongoza Sinagogi hilo anaitwa “Miaka 1000 ya kutawala na kristo”.
  Kama unavyojua hawa jamaa ni hodari kwa kujitungia/ kujibunia majina, hivyo ndivyo jamaa anavyojiita na anavyoitwa na wafuasi wake.
  Pia huyu jamaa ambaye ni msomi kutoka chuo kikuu cha Harvad cha Marekani, kwa kutumia ujanja/elimu yake amemtangaza rasmi Munuo kuwa ndiye ‘yesu
  kristo’ , jiwe kuu la pembeni na kwamba wanadamu wote wametoka viunoni mwake.
  Hivi ndivyo Wanasiloam Wanavyozidi kuzama JEHANAMU.

 3. POLENI SAANA WANA SILOAM. MUHIMU MKAJUA KUWA HUYO ALIKUWA NA NABII WA UONGO. NA Ukengeufu una nguvu kuliko sumaku inavyovuta chuma. Kazi ni kwenu wana siloam, ukweli mshaambiwa sana, nimaombi yangu neema ya Mungu iwazukie mjua/muone na kulielewa kwa uwaazi hilo shimo la kuzimu muliloingia.

 4. Mpandaji ni Mungu na muvunaji ni Mungu kumbe nabii Uyu alifaliki. Polelisana kanisa Tanzania na jamaa .aliyedani yu mungu kalala

 5. Thamani,
  Sikiliza, kwa vile wewe uliwauliza na majibu yake yakakuelea, ukitupa na majibu waliyokupa ya maswali hayo uliyoyaorodhesha, utakuwa ni mkweli kuliko ninavyokusoma!

  Tukisema tukusanyane wote tunaoitilia shaka huduma hiyo tuje huko, mtashangaa nayi mkihamishiwa huko kwenye viwanja vya Biafra kama walivyohamishwa kanisa la Glory of Christ kutoka Ubungo kwenda Kawe pale askofu wao alipoahidi kuwaleta akina Amina Chifupa waliofariki na kuzikwa, wengi kwa hila hiyo hawajarudi makanisani kwao mpaka leo!!!

  Gbu!

 6. Thamani,Kwa utafiti wa haraka,JINA LAKO linaonesha wewe nawe ni mmoja wa Wafuasi wa NABII HUYU WA UONGO (MUNUO) na Si eti ulikwenda tu kusali. Hebu wewe tujibu hayo Maswali kwa sababu inaonesha wewe una majibu.

 7. Tatizo jambo linapokuwa jipya huwa linasumbua watu as washazoea yale ya zamani,sasa katika manabii huyu Eliya kaja na mapya yote ,na huwezi linganisha mambo ya Musa na ya Yohana or Paulo or Yohana ,Yesu,nk.Kila anayetumwa huwa anakuwa na agizo alilopewa na Mungu,Na Ni Mungu ndiye anayemuamuru afanye hivyo.Naombeni kwanza muwaulize wahusika maana ya Mambo yafuatayo.
  1:Kwa nini Adamu wa pili Mungu wa majeshi?
  2.Shetani aliuwawa kivip?
  3.Maana ya neno Biblia
  4.Maana ya damu ya Haki kweli na hukumu
  5.Majira za kiungu
  I hope ukijua hayo hutapata tabu kuhusu hili kanisa.MImi niliwahi kupata huduma hapo na sikuona kama kuna tatizo.Niliuliza hayou maswali na walinifafanulia vizuri nikawaelewa.
  Mmebarikiwa.

 8. Shalom, Nimekutana na dada ambaye anaabudu Siloam nimesikitishwa na uongo wa Hutu marehemu Munuo kwamba alimuuwa shwtani. Hii ni cult na INA mizizi ktk ulimwengu wa kichawi ndio maana wanaoingia hili kanisa ni vigumu kutoka. Nashauri tuendelea kuangusha hii ngome ya mapepo! Eti wanasema Yesu ni kifo. Yaani funny doctrine! Huyu dada nimweleza kweli ya Neno LA Mungu na akasema anataka nimtembelee nabii wao. Nimemwambia siwezi kukaa kwenye viti vya wenye mizaha Bali kwa kuwa aliguswa na kweli akaandika mafundisho najua Roho mtakatifu atashughulika naye. Kwa sababu Neno Lima nguvu ya kuvunja vunja maagano. Amina

 9. Mimi niliwahi kusali kanisa la Siloam na ni mmoja ya watu waliokamatwa akili na kuwaamini kabisa. Kwa sababu Mungu amenibariki kwa kazi nzuri yenye kipato kizuri na ninaishi mkoani nikatokea kuwa karibu sana na wachungaji wa hili kanisa maana mara kwa mara nilikuwa nawasupport kwenye huduma na safari zao. Ila nilipowafahamu vizuri hawa watumishi roho yangu ikaanza kusita maana wengi wao maisha yao na mienendo yao haikunibariki mbaya zaidi kuna wakati mmoja wao alikuwa ananidanganya ili niwe namsaidia kifedha. kuna wakati nilipatwa na matatizo katika kuniombea wakafanya maombi ya kuita nafsi maombi yale kusema kweli badala ya kutoka na amani yalinifanya nijisikie vibaya zaidi. Wenyewe wakawa wanasisitiza inabidi uamini tu, ila namshukuru Mungu kuanzia wakati huo nikawa na mashaka nao mambo mengi tu yaliendelea lkn kuna wakati nikatafuta mtumishi wa sehemu nyingine ambaye alikuwa ananihudumia toka zamani kabla sijaingia Siloam yule mtumishi akaniambia huko unakoabudu sipo huyo mtumishi alishakamatwa na shetani na Mungu ataenda kufanya jambo juu yake. Ndipo nilipotoka huko na ilinibidi nitoke kiakili kuepusha vita toka kwao maana kwa imani ya Siloam mtu ukitoka Siloam UTAKUFA na wengi wanashindwa kutoka hata kama hawana amani sababu ya vitisho vingi wanavyopewa mimi nilikataa hiyo roho na kusema ” sitakufa nitaishi ili niyasimulie matendo makuu ya bwana”. Baada ya miezi kadhaa nikasikia kuwa Nabii Eliya amekufa nikakumbuka maneno aliyoniambia yule mchungaji kuwa Mungu atafanya jambo. Nakumbuka kabisa nabii Eliya mwenyewe alisema manabii wa kizazi cha kwanza waliuwawa, wa kizazi cha pili na cha tatu hivyo hivyo yeye Nabii wa kizazi cha nne hatakufa maana Mungu ameshuka mwenyewe na Mungu hawezi kufa hivyo hata yeye hatakufa. Nawaombea wote waliobaki huko maana nina ndugu zangu na marafiki ambao bado wanaabudu huko MUNGU awafunue na kuwakomboa kama Alivyonitoa mimi ili waweze kujua Kweli na Kweli iwaweke huru.

 10. Shetani kuuawa halikubaliani na neno linavyosema hivyo ni utapeli wa wachumia tumbo tu. Na kwa kuwa walishalishwa sumu ya uongo na baba wa huo ndio maana leo hii wanajaribu kuhada watu kuwa Munuo alifufuka wakati walimzika mapinga. HAWA NI MATAPELI WAONGO KAMA ALIVYO BABA YAO SHETANI. KAMA NABII WAO ALIDIRIKI KUSEMA YESU HAKUMALIZA KAZI NA HAKUFANYA VIZURI SANA NDIO MAANA AKAUWAWA KUNANINI HAPO. MUNGU WAO NI SHETANI SIO HUYU TUNAYEMWABUDU.

 11. Japo yawezekana, nasema pengine yawezekana kwamba kuna ukweli mahali fulani kwenye imani hii, lakini katika MAMBO MAGUMU KUYAAMINI KATIKA IMANI HII YA SILOAM NI HILI LA KUSEMA NABII ELIYA (MUNUO) ALIMUUA SHETANI na sasa Universe ni “SATAN FREE”! Dah, basi tuu yaani. Mambo mengine jamaniii…! Sidhani kama ni akili kamili ya binadamu inayoweza kuliamini jambo hili

 12. shetani ni muongo na baba wa uongo, kila dhambi ni uasi. uongo,uzinzi, uuaji, nk. kama shetani keshauwawa mbona bado dhambi ipo duniani

 13. Emmauel Kaaya, roho ya UKENGEUFU ina nguvu sana inawapoteza WATU WENGI sana isipokuwa haiwezi KUWADANGANYA WATEULE. Munuo ni mmojawapo wa MANABII WA UONGO.Hebu angalia hawa jamaa wa SILOAM wamedanganywa Kwa maneno ambayo hata wao hawaelewi.Hebu Ona jinsi roho hii ya UKENGEUFU ilivyo na NGUVU,Munuo aliwadanganya Wafuasi wake kuwa eti 2008 ALIMWUA Shetani! Pia Munuo aliwaambia kuwa wafuasi wake kuwa yeye ni Adamu Wa Pili.Kama si KUPOFUSHWA MACHO ni nini?Hawa jamaa Wa Siloamu Wameng’ang’ania kutetea UONGO WA IBILISI.Tusichoke kuwaambia Ukweli wa Neno la Mungu yawezekana Yupo mteule akasikia.

 14. jamani hizi imani nyingine zinawadiscourage watu hata kumfahamu KRISTO , sasa siloam mnatumia neno la Mungu lipi linalosema marehemu Munuo atakuwa adam wa pili na kuwa ni mungu wa majeshi…nina video za hilo tukio la mazishi yake kwa kweli jamani watu wa Mungu tunapotea kwa kukosa maarifa, hii imani ya siloam imenichanganya sana , ni mojawapo ya roho kengeufu,,, nawashauri waumini wa hili kanisa wajitazame mara mbili mbili …

 15. Mkamilifiu nd Matunda Eliya hivi wewe ni Eliya wa ngapi maana inabidi mpatiwe no. Kwa njinsi kila muumini wenu amebeba hilo jina. Jamani naona tunampigia mbuzi music na hawezi kucheza. Wanaotekwa ni wale ambao hawalijui Neno.. Nasikia ninyi sio wanadamu Loo kweli Mungu anapata shida na watu aliowaumba. Yesu mwenyewe alipouvaa mwili aliitwa mwana wa Adamu sasa hawa waTz wameibuka na imani yao inayopindisha Neno eti ni mafunuo. Jamaa alianza vizuri lakini mafunuo yalipozidi ibilisi akapata mwanya akatengeneza makao humo ndani ili mafunuo yaende vizuri. Mbeba mafunuo hufunuliwa peke yake tu na akiyatoa haulizwi , huwezi kumchallenge, wala kubisha . Neno lake ni final kazi ni moja tu KUTII. Mafunuo yanyewe yanapotosha vibaya sana :- alishamuua shetani; Yesu amesharudi; tunatawala miaka 1000 ya amani; hakuna kufa; omba ukijiunganisha na sanduku la agano ; pia unganisha na madhabahu ya siloam ambayo wanaiona ni takatifu ili ujibiwe maombi yako; mapepo yanaamuriwa yamuingie anayeomba maana ana nguvu za kukabiliana nayo kuliko aliyepagawa ni dhaifu; Nafsi zinaitwa zijidhihirishe wakati wa maombi; huo no unajimu. Wakristo husaidiwa na Roho Mt. Kuingia ndani hivyo. Mtu anafiriki kujiita AD2 Mungu wa Majeshi!!! Hivi ninyi hamsomi neno au anawasomea na kuwatafsiria? Hamjui Mungu ana wivu mkali sana?!!Haya bro. Matunda hebu soma Wagalatia 4: 9-11. Paulo anapinga kurudia mafundisho manyonge ya kushika siku , miezi, nyakati. na miaka. Tena anachelea isiwe labda amejitaabisha bure kwa ajili yenu. Sasa nikuulize hayo mafunui yana uzima gani ktk maisha ya rohonj? Soma pia Wakolosai 2: 8- 23. Hebu tulia kwenye mustari wa 18. 20,- 23. Sasa ninakuwachia hapo. Mimi nimeganda kwa Yesu aliyenikomboa na kuniokoa yeye alipewa Uungu wote naye ni yote ktk yote. Hakuna cha Eliya au mtume au nabii au malaika anayeweza kunipeleka mbibguni. Isaya 35:8…. umenihakikishia nikiifuata njia ya uhakika yaani Yesu Ktisto nitafika mbinguni hata nikiwa mjinga sintapotea. Mimi nitaendelea kukuombea Mungu akutoe hapo maana inaonyesha sururu ya kukung’oa hapo haiwezi ni nguvu kubwa ya Mungu mwenyewe tu Usinuiombee nife kama munavyofanya kwa sababu sintakufa bado naishi nizidi kuhubiri na kumshufia Yesu aokoe wengi. God Bless u.

 16. Mkamilifu bwana Matunda Mungu akubariki sana kwa ufshamu ulioupata huko. Kumbuka Eliya Mtishib Nabii wa kweli alikimbilia mlimani akaogopa kuuawa na malikia jezebel. Akamwambia Mungu ni yeye tu aliyebaki wengine wamefyekwa na Jezebel. Mungu akamwambia anao watu wengi wapata elfu 7ambao hajamwabudu mungu baali.. Hivyo unaposema ni kanisa la Siloamu pekee lenye ufahamu utashangaa idadi ya watu kati ya billion 7 wenye msimamo wa Mungu baba wa Bwana wetu Yesu Kristo. Isaya 35:8-….Na hapo patakuwa na njia. Waliokombolewa ndio watapita njia ile . Wesio safi hawatapita njia ile bali walio safi na wajapokuwa wajinga hawatapotea njia ile…….. Ninachongojea ni Yesu Kristo arudi kunichukua ka ilivyoandikwa kwa Wathesalonike ingawa kwako wewe tayari Yesu amesharudi . Hatuwasemi vibaya ila tunajaribu kuwazibua ufahamu wenu uliotekwa urudi. Lakini sasa inaonekana tunangonga zege keli sana. Nakuasa ukumbuke ni Yesu tu atakeyekupeleka mbinguni ukimpa nafasi ya kwanza sio Eliya wa zamani , wala roho ya yule a Eliya iliyoinhia ndani ya Yohana Mbatizaji , wala Eliya wenu…. hao hawawezi kukupeleka mbinguni . hata ukiwa mkamilifu bila Yesu ni bure. Ninawapenda wanaSiloamu YESU TU NDIO YOTE KTK YOTE. Historia muliyoigundua nyakati na majira na siku etc zoote hizo hazina uzima. Ndio maana Paulo anasema ktk Wagalatia 4: 9 :11 nd Matunda pia soma kwa makini sa Wakosai 2 : 8-24 Mungu awabariki sana.

 17. @ matunda 9, HIYO NI YA KWENU, LABDA NI TAREHE ALIYOZALIWA MUNUO KASHEHEREKEENI. HII NCHI IMETOA UHURU WA KUABUDU HIVYO UTUMIE NI UHURU WAKO KIKATIBA.

  ILA UONGO HUMU SII SEHEMU YAKE UNAJUA HII WEB INAITWA STRICTLY GOSPEL SIO SEHEMU YA MAFUNUO YA MASHETANI.

  MWISHO NINAKUKUMBUSHA KUWA UHURU HUU UNAISHIA PALE YESU ANAPORUDI AU UNAPOONDOKA HAPA DUNIANI KAMA ALIVYOONDOKA NABII WENU. BAADA YA HAPO HUKUMU.

 18. How is it done? This is my first contribution. Kindly do it for me and correct the misspelled words. May the good God continue to bless you even more abundantly. Amen.

 19. TUNAMSHUKURU MUNGU WA MJUMBE WA MAPENZI YA MUNGU KWA KITUO KIKUBWA CHA UFAHAMU WA NENO LA UFUNUO ALIPOLIFIKISHA KANISA. KANISA TUNATUBU KWA AJILI YA YOTE, VYOTE NA WOTE KWA AJILI YA WALIOKOSA UFAHAMU WA NENO LA UFUNUO. UNAJUA HATA YESU ALIPOFUFUKA WALE WAKUU WA MAKUHANI WALIWAHONGA FEDHA WALE WALINZI WALIOKUWA WANALINDA KABURI ILI WASEME KWAMBA YESU HAJAFUFUKA BALI WANAFUNZI WAKE WAMEMWIBA. NA MPAKA LEO WAPO WAYAHUDI WANAOAMINI HIVYO. KWAHIYO HATA SISI KANISA LA SILOAM HATUSHANGAI KWA WOTE MNAOSEMA UOVU JUU YA MJUMBE WA MAPENZI YA MUNGU BALI TUNATUBU KWAKUWA TUNAFAHAMU MUNGU ALIYEFUNULIWA KWETU KUPITIA JUMBE WA MAPENZI YA MUNGU NI MUNGU WA KWELI HATA MKIJITAHIDI KUPINGA UKWELI KWA KUTUMIA UONGO AU MANENO BADO KWELI ITABAKI PALEPALE KWAKUWA NENO LA MUNGU HALIWEZI KUPINGWA NA YEYOTE. NYIE TULIENI KIDOGO TU MTAONA MAMBO YANAYOKUJA HALAFU MTAJIJIBU WENYEWE.
  SHIKA NENO!
  MWISHO KANISA LA SILOAMU TUNAWAKARIBISHA WOTE KWENYE SHEREHE KUBWA YA KUZALIWA KWA BWANA YESU AMBAYO ITAKUWA TAREHE 28 ADARI,3 (2/12/2014). HII INAMAANISHA KWAMBA X-MAS AMESHAFUTWA KWAKUWA DINI NA MADHEHEBU WALITUDANGANYA KUWA NDIO SIKU YA KUZALIWA BWANA YESU KUMBE ILIKUWA NI SIKU YA FREEMASON/SHETANI KUABUDIWA. TUNAMSHUKURU MUNGU WA ELIYA KWA UFAHAMU HUU AMBAO UNAPATIKANA NDANI YA KANISA LA SILOAM PEKE YAKE KWA DAMU YA HAKI KWELI NA HUKUMU.

 20. Mungu wa kweli wanaomsisitizia ni kwa sababu mungu wao ni wa mashakamashaka. mungu alitafuta mbinu ya kuwafanya wajione wao ni bora. Mengine yote ni madhehehebu na dini. Siei ni Walokole watakatifu kama JEHOVA MUNGU wetu alivyo mamtakatifu. Wao eti ni wakamilifu wameksmilisha na mungu wao. Mambo ya wazi ambayo inashangaza hawaywoni ni..
  1. Shetani aliuwawa na eliya wao.
  2.Yesu amesharudi yuko hapa duniani.
  3.Hawafungi na kuomba c
  bcoz bwana akiwepoo nao hawana haja kugunga
  4. Wawafi kwani wanatawala na Bwana miaka elfu moja.
  Loo nimechoka kabisa kusikia hivyo vituko. Tuendelee kuwaombea . Tusiwakebehe ili na sisi tusiingie ktk mitego. Ndugu zetu wameghafilika tuwarejeshe kwa upenndo.

 21. Problem kubwa ni ufahamu wa wenzetu umeshatekwa. It cmz ile style yao ya kuomba kwa kumfuatilizia kiongozi ni njia ya initiation yaani kuwaingiza kimpango kwenye CULT yao. Unjanja huo kama Mungu hakuingilia kati ungeleta kumpigia magoti na kumabudu. Kumtoa mwana siloam pale inahitajika nguvu ya ki Mungu tu. Hawaoni na hawasikii. Kwao ni eliya mungu wao wa majeshi. Sio ajabu wataweka utaratibu wa kumtembelea kaburini mara kwa mara. Hawajielewi. Hata wachungaji wameshakuwa hypnotised. Hasa huyo 1000yrs ya amani ; lmagine alishawishiwa achwne Degree Certificate zake eti ndio amtumikie mungu wao vizuri. Arrogance yote na majivuno ya ku downlook others walio nje ya cult yao inatokana na kutekwa ufahamu. Sasa wako kama mazuzu . Kubweteka kwa kitoto. Kweli tuwahurumie. Ila tukazane na maombi. Mungu atafa mwenyewe na kuwaponya wenzetu.

 22. Pia naomba mtu yeyote anayesali siloamu anisaidie kujua haya.Adamu wa pili ni Yesu au huyo aliyefariki juzi?nataka nijue Maneno ya Yesu ya ENENDENI DUNIANI KOTE MKAYAFANYE MATAIFA YOTE KUWA WANAFUNZI WANGU yana maana gani ikiwa bwana Munuo anataja kuwa ndiye aliyekuja kufanya kazi iliyomshinda Yesu?nasikia cover la Biblia alilichana na kuamuru waumini wote wafanye ivyo kwa sababu tu ni jeusi na neno Biblia ni la kutunga.je!ni kweli jina analotumia ndo hasa lilitakwa na Mungu?nasema hiv kwa sababu lugha ya kiswhili siyo iliyoleta maneno ya Bibliani sasa kutooa si makosa?pia maandishi yote hayakuwa kwenye karatasi bali kwenye ngozi za wanyama je,siloamu wanatumia magombo ya ngozi za wanyama?nasubiri msaada wa majibu.

 23. niombe tu neno moja.mnapotaja kiumbe kilichojiita au kinachojiita ama kitakachojiita mungu,zingatia msitumie herufi kubwa M.mfano huyu ajenti wa shetani aliyekatiliwa mbali yafaa aitwe mungu wa majeshi na si Mungu wa majeshi.

 24. Wanalaaana hawa ndugu Edwin. Wamemkufuru Roho Mtakatifu hapo kuna nini kimebaki. Wanasubiri jehanam, nakiongozi wao amekwisha tangulia.

 25. Yaani Wanadamu wakishagonga dona na dagaa, zikawakaa vema sana tumboni,kisha wakalala na wakaanza kuota-ota/ona-ona/funuliwa-funuliwa, watasumbua kweli hapa mujini Duniani aisee dah!

  So, kiumbe tu cha kawaida chimwanadamu tu kama sisi sote, kinakwenda ”Main Office” kama siye wote hata Obama hadi Malkia Eliza wa Uk, pia kinachoweza ugua na kutandikwa dengue, ebola kama kawaida tu maana ni wanadamu tu wote, icho chiuuumbeee ichoooo ndio Adam wa 2? ndio kikatwe pumzi ya Oxygen kisha Mbingu ya Mungu Mkuu anayeliheshimu Neno lake, atikisike na kupanda kufanya maaajabu ktk anga/mwezi na jua kwa chiuuumbe tu hicho,?????????/!!!!!!!!! aisee hadi inauuziiii sana na kutia majabza ya kweli, sasa nina muelewa Bwana Yesu kwanini alibetua meza zao na kubilingisha kureeee makomamanga hata kupeperusha njiwa wao, namueelewa sana sasa.

  Namuelewa sana Kamanda wa ukweli Paul aliyekata networks na kujaa ghadhabu safi hata kuwaambia Wagalatia kua nani amewagonga ulozi hatari? namuelewa kwanini ali MANUFACTURE na ku SUPPLY in advance LAANA kwa kiiiiiila kiumbe-Mwanadamu na hata Malaika-akijichanganya tu akaleta za kuleta-gombo tofauti na lile alihubiri na kuwajenga, basi anyukwe Laana, namuelewa kwanini alijaa hewa hata kuwaambie wengine wale wachague, awaendee na mkwaju au vipi, nadhani sasa nimeelewa hayo maandiko kupitia jinga-jinga issues kama izi.

  Press on,
  Edwin.

 26. MARKO 13:21
  na wakati huo mtu akiwaambia Tazama Kristo yupo hapa au kule msisadiki kwa maana wataondoka makriso wa uongo na manabii wa uongo watatoa ishara na maajabu wapate kuwadanganya yakin hata hao wateule

 27. kaanzisha imani chafu yeye alijiita Adamu wa pili Mungu wa majeshi ivi kweeli kabisa kama binadamu mungu kakupa ubungo ili uutumie unakubaliana na uzushi wa namna hiyo?.mimi nilisali kwake kama miezi mitatu nikawa nishajua sio imani sahihi ya Yesu kristo ni upotoshaji tu huo

 28. Huyo munuo mimi nimesali kanisani kwake alikua nabii wa uongo hana Roho mtakatifu ni mjumbe wa freemason.Actually freemasoons katika harakati zao za kuitawala dunia sasa wanajiingiza ktk kanisa na huyu jamaa ndo kazi aliyotumwa kufanya mwenye masikio asikie Roho wa mungu anachosema.Atakaetaka kuiponya roho yake ajiondoe siloam afuate imani za kweli zinazomwamini yesu kuwa ndo mwanzo na mwisho na ndio bwana wa mabwana na mwokozi wa wanadamu

 29. WAAMBIENI UKWELI NDUGU ZETU HAWA, WAFARIJINI LAKINI WAPEWE KWELI YA INJILI.

  “WALA MSISHIRIKIANE NA MATENDO YASIOZAA YA GIZA, BALI MYAKEMEE;”
  WAEFESO 5:11

 30. wahubil wengi dunian wanajifanya miungu watu wanatazama matumbo yao huku wakiwa hawana mpango wa kusaidia masikin na wajane tumukumbuke mose kolola tuige mfano wake.

 31. Mhh mwenye macho na aone mwenye sikio na asikie……….Kila roho mnayopotosha hapa duniani mtalipia. Acheni kudanganya watu wakati ukweli mnaujua.

 32. SASA MLIYEMWITA ADAMU WA PILI KAONDOKA KABLA YA UTAWALA WAKE WA MIAKA 1000 KUISHA, SASA NANI ANAENDELEA KUTAWALA. MUNGU HUWA HAKATISHI SAFARI JAMANI AKIIANZA LAZIMA, LAZIMA, LAZIMA AIMALIZE, YESU ALIPOIANZA KAZI YA UKOMBOZI ALIIMALIZA KWA GHARAMA KUBWA. MUNGU MWENYEWE ALISHUKA SASA AMEONDOKA, HUO NI UONGO MWEPESI SANA.

  ELIA NA WALIOKUWA NA ROHO YA KWELI YA ELIA HAWAKUOZEA KWENYE MAKABURI WALIYOZIKWA KAMA WATU WENGINE KASOME ULETE HOJA, MUSA ALIZIKWA NA MUNGU MWENYEWE, HATUJUI KABURI LAKE LILIFANANAJE, ELIA ALIPAA, YESU ALILALA SIKU TATU AKAFUFU NAYE AKAPAA NA YUKO MKONO WA KUUME WA MUNGU BABA AKITUOMBEA. HUYU ALIKUWA MWEREVU TU KAMA NYOKA (mwanzo 3:1) NA NDIO MAANA ALIJAZA WANAWAKE KANISANI.

  MPAKA ANAONDOKA SIJAWAHI SIKIA UNABII ALIOTOA NA UKATIMIA, WAKATI KAMA TAIFA TU MAJANGA MENGI YAMETOKEA WAKATI WA UHAI WAKE, KIMATAIFA PIA. PILI UTABIRI WA KIFO CHAKE ALIUTOA MUDA MCHACHE KABAL YA KUKATA ROHO, ALISHAJUA KUWA KWA TETENAS HII ASINGE PONA NDIO MAANA MUDA MCHACHE KABLA HAJAFARIKI ALIWAAMBIA WASAIDIZI WAKE. HAYA NI YA KAWAIDA KABISA, KUAGA NA KUACHA WOSIA NI JAMBO LA KAWAIDA KABISA. , NILIULIZA KAMA KUNA GAZETI YA NEEMA KUBWA LILILOMNUKUU NABII KATIKA HOTUBA ZAKE AKISEMA JUU YA KUFA KWAKE, HAKUNA. MUNGU HUTANGAZA MWISHO KABLA YA MWANZO. UMUNGU WAMAJESHI WAKE UKOWAPI SASA KAMA NAYEYE AMEISHIA KUFANYA YA KAWAIDA KAMA WENGI, AMEKUFA NA TETENAS KAMA WANAVYOKUFA WATU WENGINE.

  WAMEANZA KUZUSHA KUWA WAKATI WANASHUSHA MWILI UPINDE WA MVUA ULIZUNGUKA JUA, THIS IS NORMAL JAMANI RUDINI SHULE MTACHEZEWA SANA NA HAWA MATAPELI HII KITU JINA LAKE NI “SUNDOGS”. HII HUTOKEA PIA KWENYE MWEZI. SASA HALI YA HEWA YA JANA ILIKUWA NA MAWINGU YA MVUA, A FAVOURABLE CONDITION YA SUNDOGS KUONEKANA. SOMA HAPA http://www.komonews.com/weather/faq/4308372.html. NINAWAPENDA NA NINAJISIKIA VIBAYA KUONA MNAANGAMIA ILHALI TUNAWATAZAMA.

 33. huyu jamaa alijifanya yeye ni Mungu,, akajenga misingi yakuabudiwa,,,,na watu wa siloamu kwa ujinga wamemfata,, sasa icho kiti ni cha moto,, huyo eliya amefyekelewa mbali,, tambueni yuko Mungu Yehova ambae hachakachuliwi ,,,wala Neno lake halighoshiwi.

 34. The pool of siloam church ndipo yupo Mungu wa kweli na Mungu ameoneka leo kwa uhalisi kabisa.kanisa litasimama/limesimama milele yote.watu na wanadamu wanashangaa siloam hawaielewi ss tumewaacha kazi zetu hazichunguziki kwa damu moja ya haki kweli na hukumu tunamtukuza Mungu wa eliya na shukurani na toba ya kweli msingi wa kanisa umesimama kwaajili yote wasio na ufahamu.Amen

 35. ukweri ni kwamba nyie msemao mabaya juu ya huyu eliya msitaabike na maneno ya ajabu yasiyo na utukufu kwa mungu simama kaulize vizuri huko Siloam niyapi aliyo Fanya kama nice mabaya mnahaki ya kusema mabaya kama nimema unahakiya kusema mema. sioni sababu ya nyie kusema vibaya wakati hamjashuhudia je? uliza vizuri upate jibu …. ila mungu yupo kwenye haki tu sio uovu mungu atusamehee kwa kunena mabaya

 36. Shalom
  Mhh! hii ni hatari!!!! Lakini salama
  Utakufa ktk umri timilifu
  Labda umri wake ulishafikia umri wa kibiblia jamani aliotuhadi mungu wetu na baba yetu aliye wa pekee na hakuna mwiingine wa kumfananisha naye
  Barikiwa.

 37. Roho ya kusambaratisha makanisa,yote imesambaratika,MUNGU amewapa muda wa kutubu viongozi na wafuasi wa siloamu.Lakini hamkutaka sasa UNABII unatimia,(MITHALI 11:2) KIJAPO KIBURI NDIPO IJAPO AIBU.TENA SOMA,(UFUNUO 2:21-25)NAMI NIMEMPA MUDA ILI ATUBU,WALA HATAKI KUUTUBIA UZINZI WAKE.TAZAMA NITAMTUPA JUU YA KITANDA,NA HAO WAZINIO PAMOJA NAYE WAPATE DHIKI KUBWA,WASIPOTUBIA MATENDO YAKE:NAMI NITAWAUA WATOTO WAKE KWA MAUTI,NA MAKANISA YOTE YATAJUA MIMI NDIYE ACHUNGUZAYE VIUNO NA MIOYO,NAMI NITAMPA KILA MMOJA WENU KWA KADRI YA MATENDO YAKE,LAKINI NAWAAMBIA NINYI MLIOKO THIATIRA,WOWOTE WASIO NA MAFUNDISHO HAYO,….MLICHO NACHO KISHIKENI SANA,NA KUYATUNZA MATENDO YANGU MPAKA MWISHO,NITAMPA MAMLAKA JUU YA MATAIFA.

 38. Hakuaga, hili la kuaga mnatunga baada ya yeye kuondoka ilikuendelea kulifariji kundi kuwa alikuwa nabii wa kweli. Yote aliyokuwa anasema mlikuwa mnayaandika katika gazeti lenu. Ninayasoma magazeti yenu hili halijawahi kuwepo. Hivyo mnaendeleza utapeli wa marehemu, nanyi mtahukumiwa msipo badilika. Anayebisha aniambie gazeti la lini lilisema utabiri wa kifo chake kama sio uzushi unaoibuka tu baada ya kumuombea ikashindikana kupona. WATU WANGU WANAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA. Mnafanyia kazi tumbo wala sio Mungu. Mmewatapeli watu, lakini hamuwezi kumtapeli Mungu.

 39. Mungu awainulieni mtu atakayewafikisha kwenye hatma zenu na si vinginevyo. Mambo yote yatapita lakini Neno la Mungu litasimama milele na milele. Yesu ni yule yule jana leo na hata msilele Hakuna atakayesimama kwa kusema Yeye ni Adam wa pili Biblia inamtambulisha Yesu Kristko kuwa yeye ni Adam wa pili na kwa tulioliamini jina lake tumekuwa ndugu zake. Watumishi wa Mungu tunapotumiwa na Mungu tusijichukulie Utukufu kwani Utukufu ni wa Mungu pekee yake. Nyenyekea chini ya mkono wa Mungu ulio hodari yeye atakukweza kwa wakati wake. Siloam simameni imara msiyumbishwe jamani

 40. pole sana sana wafiwa, ninachotaka kuwaambia tu ni kwamba yale mazuri aliyoyaacha mtumishi wa Mungu huyu myaendeleze. Lakini kama kuna mambo ambayo hayako kwenye maandiko matakatifu yaani biblia hayo ni upotevu achaneni nayo songeni mbele katika kweli ya neno la Mungu tu na si vinginevyo. msikubali mtu kuwatoa katika mstari wa Imani yenu

 41. Hakiazi 12 kaandika hivi:

  “Damu nyingine zote za magonjwa,umasikini,aibu,hukumu,kafara,damu za ufisadi,damu za watu na wanadamu,damu za kuku ndege na wanyama,damu za maagano ya giza ZOTe ZIMeFUTWA na MUnGU wa Majeshi”

  Nimeshindwa kuelewa hapo mwishoni kwamba damu zooote zimefutwa na Mungu wa Majeshi?

  Mungu wa Majeshi yupi? maana hata huyu Nabii nimesoma mahali alikuwa anaitwa Mungu wa Majeshi.

  Naomba msada hapo!

 42. Hata wapagani huaga ndg zao wanapotaka kufa, labda aliumwa ugonjwa aliojua hatapona…sioni cha ajabu hapo!

 43. KWELI ITABAKI KUWA KWELI UONGO HAUGEUKI KUWA KWELI!!!!!! NA SIKU ZOTE TRUTH SHALL PREVAIL. Huwezi kumtenganisha Mungu na Neno lake (BIBLE) then utoke salaama.

 44. POLENI SANA,
  NDUGU HAKIKAKAZI 2, ACHA KUINGIZA UONGO KWA WATU, TUNACHOJUA KWENDANA NA TAARIFA NI KUWA MUNUO AMEKUFA/AMELALA. ACHA HABARI ZA KUTWALIWA. NDO MAANA WANAANDAA MAZISHI YAKE, WALOTWALIWA KAMA ELIYA, HENOKO, HAKUKUWA NA MAZISHI.

  “KAMA VILE MAJI KUPWA KATIKA BAHARI, NA MTO KUPuNGUKA NA KUKATIKA;NI VIVYO MWANADAMU HULALA CHINI, ASIINUKE; HATA WAKATI WA MBINGU KUTOKUWAKO TENA, HAWATAAMKA WALA KUAMSHWA USINGIZINI.”
  AYUBU 14:10-12

  “MSISTAAJABIE MANENO HAYO; KWA MAANA SAA YAJA, AMBAYO WATU WOTE WALIOMO MAKABURINI WATAISIKIA SAUTI YAKE. NAO WATATOKA; WALE WALIOFANYA MEMA KWA UFUFUO WA UZIMA, NA WALE WALIOTENDA MABAYA KWA UFUFUO WA HUKUMU.”
  YOHANA 5:28,29

  1.MAFUNDISHO YA MIAKA ELFU KUWA NDIO SASA
  2.MAFUNDISHO YA KUTOKUFA
  3. NA KUWA SHETANI ALIUWAWA YAONDOLEWE PIA KWA SALAMA YA WAUMINI WALIOBAKI.

  TUJUE KUWA SHETANI AMELETA KIFO,BASI UHIFADHINI UHAI WENU MBAVUNI PA YESU.

 45. It is the matter of time. Hakikazi 12, baada ya tukio mlikaa kimya mkapanga cha kusema kabla ya kutangaza. Mtatunga sana lakini punde si punde ukweli utakuwa hadharani. Jisalimisheni kwa Yesu huko ndiko kweli ilipo.

 46. Wafiwa,
  Poleni sana,
  Ninafahamu kwamba huu ni wakati mgumu saana kwenu kama familia; lakini ni wakati pia wa kuyatafakari maisha, haswa UHUSIANO wetu na Mungu katika Kristo aliye Adamu wa Pili kwa jinsi mwili, kule kuumbwa, bali aliye Uzima wetu, na Mfariji wetu ktk nyakati hizi ngumu kama mnayoipitia leo hii, ambayo ninaamini itakuwa a TURNING POINT ktk mahusiano yenu na Mungu!

  Ninawaombeeni faraja ktk Kristo, awakusanye ktk Yeye hapo anapowafungua kutoka ktk vifungo vya dhiki na kuwaingiza ktk Kweli yake!

  Gbu!

 47. Hakika alikuwa mjumbe wa mapenzi ya Mungu.Jina la Bwana litaetndelea kutukuzwa Siloam na kwenye madhabahu zote zinazomuabudu Mungu katika roho na kweli.Hongera baba kwa ushindi.

 48. Amen.
  Mjumbe wa mapenzi ya Mungu wa Majeshi ametwaliwa na Bwana.
  Awali aliwaita makuhani wote wa njia kuu nchi yote ya Gosheni na watenda neno na wakamilifu akawaambia maagizo muhimu kuhusu kazi ya kanisa na kazi za kuzikamilisha kupitia Agizo. kwamba kila mtenda neno ni Agizo la Eliya. Mjumbe aliwaaambia kwamba yeye amemaliza kazi aliyoagizwa na Mungu wa Majeshi ya kujenga msingi wa kanisa la mwisho. na kwamba majira imefika yeye anatwaliwa na Bwana.Na baadaye akatwaliwa.

  Tunamtukuza Mungu kwa kutuinua kituo cha ushindi kwa kanisa..

  Tunainua shukurani kwa kazi njema za Mungu wa Majeshi kwa kanisa kizazi cha Nne.

  Kwa hiyo kila jambo jema na kazi njema zimesimamishwa kwa Damu moja, ya haki kweli na Hukumu.
  Damu nyingine zote za magonjwa,umasikini,aibu,hukumu,kafara,damu za ufisadi,damu za watu na wanadamu,damu za kuku ndege na wanyama,damu za maagano ya giza ZOTe ZIMeFUTWA na MUnGU wa Majeshi.

 49. Haleluyah, hatuwezi kufurahi kwa mtu kuondoka ktk dunia hii ila ninachojua kuondoka kwa nabii Eliya MTU aliyejitukuza na kuchukua nafasi ya juu kwamba yeye ni ADAM Wa pili, bwana Wa majeshi, nabii Wa kizazi cha NNE yaani kizazi cha Yesu kimepita basi huh ndio mwisho Wa upotofu na hakika zipo roho zitakazopona kwasababu MTU huyu ameondoka. Hata kama ameacha mrithi Wa kuendeleza hu upotofu bado hataweza kudumu na ninaamini hii ngome ndio imeanguka na kwa jina la Yesu haitainuka tena. Amen.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s